sw_tn/isa/50/10.md

20 lines
1016 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Mtumishi anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# Ni nani miongoni mwenu anamwogopa Yahwe? Ni nani anayetii sauti ya mtumishi wake? Ni nani anayetembea katika giza zito bila nuru? Anatakiwa ... Mungu wake.
Mtumishi anatumia maswali haya kuwatambua wale ambao anazugumza nao. "Kama mtu miongoni mwenu anamwogopa Yahwe na kutii sauti ya mtumishi wake, lakini anatembea katika giza zito bila nuru, basi anatakiwa ... Mungu wake"
# anayetii sauti ya mtumishi wake
Hapa neno "sauti" linawakilisha kile mtumishiu anachosema. "kumtii mtumishi wake"
# anayetembea katika giza zito bila nuru
Mtumishi anazungumzia watu ambao wanateseka na kuhisi kutojiweza kana kwamba walikuwa wakitembea katika sehemu ya giza sana. "anateseka na anajihisi kutojiweza"
# tumaini katika jina la Yahwe na mtegemee Mungu wake
Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Hapa neno "jina" linawakilisha Yahwe mwenyewe. Kumtumaini Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kumuegemea yeye. "mtumaini Yahwe, Mungu wake"