sw_tn/isa/48/12.md

32 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# Yakobo, na Israeli
Zote hizi zina maana ya watu wa Israeli.
# Mimi ni wa kwanza, mimi pia ni wa mwisho
Msemo huu unasisitiza asili ya milele ya Yahwe. Maana zaweza kuwa 1) "Mimi ndiye niliyeanzisha vitu vyote, na mimi ndiye humaliza vitu vyote" au 2) "Mimi ndiye niliyekuwa nikiendelea kuishi, na mimi ndiye nitakayekuwa nikiendelea kuishi".
# mkono wangu umelaza msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezinyosha mbingu
Hapa "mkono" una maana ya Yahwe. "Nililaza msingi wa dunia, na nikatandaza mbingu"
# msingi wa dunia
Neno "msingi" kawaida ina maana ya umbo la mawe ambalo hutoa mhimili kwa jengo kutoka chini. Hapa inafafanua umbo ambalo ilidhaniwa kushikilia dunia katika nafasi yake.
# umezinyosha mbingu
Yahwe anazungumzia kuumba mbingu kana kwmaba zilikuwa kitambaa ambacho Yahwe alinyosha nje.
# ninapoziita, zinasimama juu pamoja
Kusimama pale Yahwe anapoita ni sitiari kwa kuwa tayari kumtii. Yahwe anazungumzia dunia na mbingu kana kwamba ziliweza kumsikia na kumtii.
# ninapoziita
Maana zaweza kuwa 1) "ninapoziita dunia na mbingu" au 2) "ninapoziita nyota na mbingu"