sw_tn/isa/27/09.md

24 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kwa hiyo kwa njia hii
Maana zaweza kuwa 1) "hii" ina maana ya Yahwe kuwatuma watu uhamishoni kama Isaya alivyosema katika mstari uliopita au 2) "hii" ina maana ya matendo ambay Isaya atayataja katiika sehemu inayofuata ya mstari wa 9.
# udhalimu wa Yakobo utalipiwa kosa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataondoa dhambi kutoka kwa Waisraeli" au "Yahwe atasamehe dhambi ya Waisraeli"
# udhalimu wa Yakobo ... kuondolewa kwa dhambi yake
Hapa "Yakobo" inawakilisha uzao wa Yakobo. "udhalimu wa Waisraeli ... kuondolewa kwa dhambi zao"
# kwa maana hii itakuwa
Hapa "hii" ina maana ya matendo ambayo Isaya atafafanua katika sehemu inayofuata ya mstari wa 9.
# tunda kamili
Hii inazungumzia matokeo ya matendo kana kwamba ilikuwa tunda ambalo huota juu ya mti au mzabibu. "tokeo"
# atafanya mawe yote ya madhabahu kama chokaa na kupondwa vipande vipande, na hakuna nguzo za Ashera au ubani wa madhabahu utabaki ukisimama
Hapa "atafanya" ina maana ya Yakobo ambaye anawakilisha vizazi vyake. "Wataangamiza kabisa madhabahu yote ambayo wanatoa sadaka kwa miungu ya uongo, na watatoa sanamu zote za Ashera na madhabahu ambayo wanachoma ubani kwa miungu ya uongo"