sw_tn/isa/26/19.md

32 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Wafu wako wataishi
Hii inawezwa kuandikwa upya ili kwamba kivumishi kidogo "wafu" kinaelezwa kama kitenzi "wamekufa". "Watu wako ambao wamekufa wataishi tena"
# Wafu wako
Maana zaweza kuwa 1) "wako" ina maana ya Yahwe au 2) "Wako" ina maana ya watu wa Israeli. Iwapo utachagua chaguo la pili unaweza kutafsiri kama "Wafu wetu"
# Inukeni
Hii inazungumzia watu waliokufa kurudi katika uhai kana kwamba walikuwa wakiamka kutoka usingizini.
# nyie mnaoishi katika vumbi
Hii ni njia ya upole ya kumaanisha wale waliokufa. "wale ambao wamekufa na kuzikwa"
# kwa maana umande wako ni umande wa mwanga
Yahwe kuwa mwema kwa watu wake na kuwaleta katika uhai inazungumziwa kana kwamba ilikuwa umande ambao unasababisha mimea kuishi.
# kwa maana umande wako
Maana zaweza kuwa 1) "wako" ina maana ya Yahwe na huu ni umande ambao Yahwe hutoa au 2) "wako" ina maana ya watu wa Israeli na huu ni umande wanaopata kutoka kwa Yahwe.
# umande wa mwanga
Maana zaweza kuwa 1) "mwanga" ina maana ya nguvu ya Yahwe kufanya watu waliokufa kuishi tena. "umande kutoka kwa Yahwe" au 2) "mwanga" ina maana ya kipindi cha asubuhi ambapo umande upo juu ya mimea. "umande wa asubuhi"
# dunia italeta mbele wafu wake
"dunia itazaa wale waliokufa". Yahwe kusababisha watu waliokufa kuja katika uzima inazungumziwa kana kwamba dunia ingeweza kuzaa wale waliokufa. "na Yahwe atasababisha wale ambao wamekufa kuinuka kutoka katika dunia"