sw_tn/isa/19/01.md

32 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Tazama
"Angalia" au "Sikiliza". Neno hili linaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadaye.
# Yahwe anaendesha juu ya wingu jepesi
Yahwe anaonekana kupigwa picha hapa akiendesha juu ya wingu kana kwamba alikuwa akiendesha katika kibandawazi.
# sanamu za Misri zinatetemeka mbele zake
Sanamu zinaelezwa kama kuwa na hisia za uoga Yahwe anapokaribia. "sanamu za Misri zinatetemeka kwa uoga mbele za Yahwe"
# na mioyo ya Wamisri zinayeyuka ndani mwao
Moyo kuyeyuka kunawakilisha kupoteza ujasiri wake. "na Wamisri hawana ujasiri tena"
# mwanamume dhidi ya jirani yake
Maneno "atapigana" inaeleweka kutoka kwa msemo uliopita. "mwanamume atapigana dhidi ya jirani yake"
# mji utakuwa dhidi ya mji
Neno "mji" unawakilisha watu wa mji. "watu wa mji mmoja watapigana dhidi ya watu wa mji mwingine" au "watu kutoka miji tofauti watapigana dhidi yao wenyewe"
# ufalme dhidi ya ufalme
Manebo "utakuwa" au "utapigana" inaeleweka kutoka kwa misemo ya nyuma. "ufalme utakuwa dhidi ya ufalme" au "ufalme utapigana dhidi ya ufalme"
# ufalme dhidi ya ufalme
Neno "ufalme" una maana ya ufalme mdogo ndani ya Misri. Pia inaweza kuitwa mkoa. Inawakilisha watu wa ufalme huo au mkoa. "watu wa mkoa mwingine watakuwa dhidi ya watu wa mko mwingine" au "watu kutoka mikoa tofauti watapigana dhidi yao wenyewe"