sw_tn/isa/10/33.md

44 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Tazama
HIi inaweza kutafsiriwa kama "Angalia" au "'Sikiliza" au "Zingatia kwa makini kile ninachotaka kukuambia".
# Yahwe wa majeshi
Yahwe wa majeshi ya Israeli
# atapogoa matawi ... na Lebanoni katika ufahari wake utaanguka
Isaya anazungumzia jeshi la Ashuru kana kwamba lilikuwa miti mirefu katika Lebanoni. Mungu ataangamiza jeshi kama watu wanvyokata chini miti mikubwa ya Lebanoni. Hii inasisitiza ya kwamba ingawa jeshi lina nguvu, Mungu ana uwezo wa kuliangamiza.
# atapogoa matawi
"atakata matawi makubwa ya miti". Ataangamiza jeshi la Ashuru kama wanamume wenye nguvu wanavyokata matawi makubwa ya miti"
# kwa kishindo cha kutisha
Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "kishindo" inaelezwa kama kitenzi "kupiga kelele". "na matawi yataanguka chini katika ardhi na kutoa sauti ya kutisha" au "na matawi yataanguka katika ardhii kwa sauti kubwa sana"
# miti mirefu zaidi itakatwa chini
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'atakata chini miti mirefu zaidi"
# miti mirefu zaidi
Hii ni sitiari kwa ajili ya "wanajeshi wenye nguvu zaidi"
# wenye kiburi watashushwa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "atawashusha chini watu wenye kiburi"
# wenye kiburi
mjivuno
# vichaka vya msitu
"vichaka vinene katika msitu". Hii inawezekana kuwa sitiari kwa wale watu ambao hawajulikani"
# Lebanoni katika ufahari wake utaanguka
"misitu ya Lebanoni haitakuwa mikubwa tena". Hii inaweza kuwa sitiari kwa ajili ya jeshi la Ashuru. "Yahwe atawashinda jeshi la Ashuru, kama jinsi lilivyo na nguvu"