sw_tn/isa/02/07.md

20 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza na Yahwe katika mtindo wa shairi.
# Nchi yao imejaa fedha ... nchi yao pia imejaa farasi ... Nchi yao pia imejaa sanamu
Isaya anazungumza kana kwamba nchi ilikuwa chombo ambacho mtu ameweka fedha, farasi, na sanamu. Neno "nchi" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wenyewe, na maneno "imejaa" ni sitiari kwa ajili ya watu kumiliki vifaa hivi. "Wanamiliki fedha nyingi ... pia wanamiliki farasi nyingi ... Pia wanamiliki sanamu nyingi"
# ufundistadi wa mikono yao wenyewe, vitu ambavyo vidole vya wenyewe vimetengeneza
Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba hivi sio miungu ya kweli. Kama lugha yako haina maana ya jumla kwa kitu ambacho mtu ametengeneza, unaweza kuunganisha misemo hii miwili katika moja. "vitu ambavyo wao wenyewe umetengeneza"
# ufundistadi wa mikono yao wenyewe
Neno "mikono" ina maana sawa na watu wenyewe. "ufundistadi wao wenyewe" au "kazi yao wenyewe" au "vitu ambavyo wametengeneza kwa mikono yao"
# vitu ambavyo vidole vya wenyewe vimetengeneza
Neno "vidole" ina maana sawa na watu wenyewe. "vitu ambavyo wametengeneza kwa vidole vyao wenyewe"