sw_tn/isa/02/04.md

40 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.
# Atawahukumu
"Yahwe atawahukumu"
# atatoa maamuzi
"atatatua ugomvi"
# watatwanga panga zao katika majembe, na mikuki yao katika ndoano za kupogolea
Watu wa mataiufa watageuza silaha zao za vita kuwa vifaa kwa ajili ya ukulima.
# panga ... mikuki ... upanga
Maneno haya ni maana sawa ya silaha za aina yoyote.
# majembe ... ndoano za kupogolea
Maneno haya ni maana sawa ya vifaa vya aina yoyote ambavyo watu hutumia katika shughuli za amani.
# watatwanga panga zao katika majembe
"watafanya panga zao kuwa vifaa kwa ajili ya kuoanda mbegu". Jembe ni ubapa ambao watu hutumia kuchimba katika ardhi iuli waweze kupanda mbegu pale.
# na mikuki yao katika ndoano za kupogolea
"watatwanga mikuki yao kuwa ndoano za kupogolea" au "watafanya mikuki yao kuwa vifaa kwa kutunza mimea". Ndoano ya kupogolea ni kisu ambacho watu hutumia kukata matawi ambayo hayahitajiki kutoka kwa mimea.
# taifa halitainua panga lake dhidi ya taifa
"hakuna taifa litainua panga lake dhidi ya taifa lingine". Panga ni mfano wa maneno kwa ajili ya vita. "taifa moja halipigana vita dhidi ya taifa lingine"
# wala hatafanya maandalizi kwa ajili ya vita
"wala hawatafanya maandalizi kupigana vitani". Mwandishi anatarajia msomaji kuamiini ya kwamba wale wanaopigana vita hufanya maandalizi kabla ya kupigana na kwamba baadhi wanaofanya maandalizi hawapigani.