sw_tn/isa/01/05.md

24 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.
# Kwa nini bado mnapigwa? Kwa nini mnaasi zaidi na zaidi?
Isaya anatumia maswali haya kuwakaripia watu wa Yuda. Maswali haya yanaweza kutafsiriwa kama kauli. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unaendelea kufanya mambo ambayo Yahwe anatakiwa kukuadhibu. Unaendelea kuasi dhidi yake"
# mnapigwa
Hapa neno "mnapigwa" ina maana ya watu ambao huishi Yuda na kwa hiyo ni katika wingi.
# Kichwa kizima kimeugua, moyo wote ni dhaifu
Sitiari hii inalinganisha taifa la Israeli na mtu ambaye amepigwa. "Wewe ni kama mtu ambaye kichwa chake kimejeruhiwa na ambaye moyo wake ni dhaifu" au "Wewe ni kama mtu ambaye akili na moyo wake wote ni mgonjwa"
# Hakuna sehemu iliyodhuriwa
Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kila sehemu ya kwako imejeruhiwa" au "mtu amejeruhi kila sehemu ya kwako"
# vilikuwa havijafunikwa, safishwa, kufungwa bendeji, wala kutibiwa kwa mafuta
Sitiari hii inalinganisha adhabu ambayo Mungu amewapa Israeli na vidonda halisi. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu aliyefunga, safisha, kufunga bendeji, au kuwatibu kwa mafuta"