sw_tn/hos/05/05.md

20 lines
896 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya jumla:
Mungu anazungumza juu ya Israeli.
# Kiburi cha Israeli kinawashuhudia
Hii inamaanisha kwamba tabia yao ya kiburi inaonesha kwamba wana makosa ya kutomtii Bwana.
# hiyo Israeli na Efraimu watajikwaa kwa hatia zao; na Yuda pia wataanguka pamoja nao
Falme mbili zitaacha kumtii Mungu kabisa kwa sababu ya kiburi chao na dhambi yao.
# Walikuwa wasio waaminifu kwa Bwana, kwa kuwa wamezaa watoto haramu
Hii yaweza kuwa na maana 1) Waisraeli walioa watu toka mataifa mengine na kuzaa watoto pamoja nao au 2) Wazazi wa Israeli hawakuwa waaminifu na waliwafundisha watoto wao kuabudu miungu.
# Sasa sherehe mpya za mwezi zitawaangamiza na mashamba yao.
Wana wa Israeli walipaswa kusherehekea kipindi cha mwezi moya. Maelezo haya yanaonesha kuwa mwezi mpya ni mnyama atakayewala watu na mazao yao. maana ya jumla ni kwamba Mungu atawaadhibu watu kwa kutokuwa waaminifu kwake.