sw_tn/gen/49/05.md

24 lines
883 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Simoni na Lawi ni ndugu
Hii haimaanishi tu ya kwamba wao ni ndugu kwa kuzaliwa. yakobo anasisitiza ya kwamba walishirikiana pamoja kuwaua watu wa Shekemu.
# Panga zao ni silaha za vurugu
"Wanatumia panga zao kudhuru na kuua watu"
# Ee nafsi yangu ... moyo wangu
Yakobo anatumia maneno "nafsi" na "moyo" kujitambulisha na kusema ya kwamba watu wengine, na labda Mungu pia, wanamheshimu sana ya kwamba hatamani kujiunga na wale wanaopanga kufanya uovu.
# usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao
Misemo hii miwili ina maana moja. Yakobo anaunganisha kuweka msisitizo ya kwamba hataki kushirikiana katika mipango yao miovu. "hakika sitajiunga nao kufanya mipango yoyote"
# kuwakata visigino ng'ombe.
Hii ina maana ya Simoni na Lawi kulemaza ng'ombe kwa starehe tu.
# kuwakata visigino
Hii ina maana ya kukata visigino vya miguu ya wanyama ili isiweze kutembea.