sw_tn/gen/48/21.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# atakuwa nanyi ... atawarudisha ... baba zenu
Hapa "nanyi" na "zenu" ni wingi na ina maana ya watu wote wa Israeli.
# atakuwa nanyi
Hii ni lahaja yenye maana ya Mungu atasaidia na kubariki watu wa Israeli. "Mungu atakusaidia" au "Mungu atakubariki"
# atawarudisha
Hapa "atawarudisha" inaweza kutafsiriwa kama "kuchukua"
# nchi ya baba zenu
"nchi ya mababu zenu"
# Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima
Maana zinawezekana kuwa 1) Yusufu kuwa na heshima na mamlaka zaidi kuliko ndugu zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa juu yao kiuhalisia wa kimwili. "Kwako, ambaye ni mkubwa kuliko ndugu zako, ninakupa mteremko wa mlima" au 2) Yakobo ana maanisha anatoa nchi zaidi kwa Yusufu kuliko anavyotoa kwa ndugu wa Yusufu. "Kwako, ninakupa kilima kimoja zaidi ya nayowapatia ndugu zako. Ninakupatia mteremko wa mlima"
# Kwako wewe
Hapa "wewe" ni umoja na ina maana ya Yusufu.
# mteremko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu
Hapa "upanga" na "upinde" ina maana ya kupigana vitani. "sehemu ya nchi niliyopigania na kuchukua kutoka kwa Waamori"