sw_tn/gen/42/37.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Mweke mikononi mwangu
Hili ni ombi la Rubeni kumchukua Benyamini pamoja naye na kumtunza katika safari hiyo. "Niweke kama msimamizi juu yake" au "Niache nimtunze"
# Mwanangu hatashuka pamoja nanyi
Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" walipokuwa wakizungumzia safari ya Kaanani kuelekea Misri. "Mwanangu, Benyamini, hatakwenda nawe hadi Misri"
# pamoja nanyi
Hapa "nanyi" ni wingi na ina maana ya wana wa yakobo wakubwa.
# Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki
Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "Kwa maana mke wangu, Raheli, alikuwa na watoto wawili pekee. Yusufu amekufa na Benyamini amebaki mwenyewe tu"
# katika njia mnayoiendea
"utakapokuwa ukisafiri kwenda Misri na kurudi" au "utakapokuwa mbali". Hapa "njia" ina maana ya kusafiri.
# ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni
"mtakapozishusha ... kuzimu" ni njia ya kusema watamsababisha afariki na kushuka kuzimu. Anatumia neno "chini" kwa sababu iliaminika kuzimi ni sehemu chini ya ardhi. "basi mtanisababisha, mtu mzee, kufariki na huzuni"
# mvi zangu
Hii ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "mimi, mtu mzee"