sw_tn/gen/33/01.md

24 lines
702 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# tazama
Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari juu ya sehemu mpya ya simulizi ya kushangaza.
# watu mia nne
"wanamume 400"
# Yakobo akawagawanya watoto ... wajakazi wawili wakike
Hii haimaanishi Yakobo aliwagawanya watoto wake sawa sawa ili kwamba kila mwanamke awe na idadi sawa ya watoto pamoja nao. Yakobo aliwagawa watoto ili kila mmoja aondoke na mama yake.
# watumishi wa kike
"watumishi wa kike wake zake". Hii ina maana ya Bilha na Zilpa"
# Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao
Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Yakobo aliondoka peke yake mbele ya wenzake.
# Akasujudu
Hapa neno "sujudu" lina maana ya kuinama chini kuonyesha kwa unyenyekevu heshima na taadhima kwa mtu.