forked from WA-Catalog/sw_tn
40 lines
1.2 KiB
Markdown
40 lines
1.2 KiB
Markdown
|
# Sasa
|
||
|
|
||
|
Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya kuonyesha mapumziko kwa simulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.
|
||
|
|
||
|
# Weka mkono wako chini ya paja langu
|
||
|
|
||
|
Abrahamu alikuwa akitaka kumuliza mtumishi wake kuapa kufanya jambo. Kuweka mkono chini ya paja la Abrahamu ingeonyesha ya kwamba hakika angefanya kile alichotaka kuapa kukifanya.
|
||
|
|
||
|
# nitakufanya uape
|
||
|
|
||
|
Hii inaweza kuelezwa kama amri. "apa"
|
||
|
|
||
|
# uape kwa Yahwe
|
||
|
|
||
|
Msemo "uape kwa" una maana ya kutumia jina la kitu au mtu kama msingi au nguvu ambayo kiapo kinafanywa. "niahidi mimi pamoja na Yahwe kama shahidi wako"
|
||
|
|
||
|
# Mungu wa Mbingu na Mungu wa nchi
|
||
|
|
||
|
"Mungu wa mbingu na nchi". Maneno "mbingu" na "nchi" yanatumika pamoja kumaanisha kila kitu ambacho Mungu aliumba. "Mungu wakila kitu mbinguni na nchini"
|
||
|
|
||
|
# mbingu
|
||
|
|
||
|
Hii ina maana ya sehemu ambayo Mungu anaishi.
|
||
|
|
||
|
# kutoka kwa mabinti wa Wakanaani
|
||
|
|
||
|
"kutoka kwa wanawake wa Kanaani" au "kutoka kwa Wakaanani". Hii ina maana ya wanawake wa Kanaani.
|
||
|
|
||
|
# miongoni mwao wale nikaao kati yao
|
||
|
|
||
|
"miongoni mwao wale namoishi" Hapa "nikaapo" ina maana ya Abrahamu na familia yake yote na watumishi. "miongoni mwao tunapoishi"
|
||
|
|
||
|
# Lakini utakwenda
|
||
|
|
||
|
Hii inaweza kuelezwa kama amri. "Apa ya kwamba utakwenda" au "Lakini ondoka"
|
||
|
|
||
|
# ndugu zangu
|
||
|
|
||
|
"familia yangu"
|