sw_tn/gen/19/01.md

44 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Malaika wawili
Mwanzo 18 unasema ya kwamba wanamume wawili waliondoka kwenda Sodoma. Hapa tunajifunza ya kwamba ni kweli walikuwa malaika.
# langoni mwa Sodoma
"malango wa mji wa Sodoma." Mji ulikuwa na kuta ukiuzunguka, na watu iliwabidi kupitia malango ili kuingia. Hii ilikuwa sehemu muhimu sana katika mji. Watu muhimu mara kwa mara walitumia muda wao pale.
# akainama uso wake chini ardhini
Aliweka goti lake juu ya ardhi na kisha kugusa ardhi kwa kipaji cha uso wake na pua.
# Bwana zangu
Huu ulikuwa usemi wa heshima Lutu alitumia kwa malaika.
# nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu
"Tafadhali njooni na mkae ndani ya nyumba ya mtumishi wenu"
# nyumba ya mtumishi wenu
Lutu anajitambulisha kama mtumishi ili kuonyesha heshima kwao.
# muoshe miguu yenu
Watu walipenda kuosha miguu yao baada ya kusafiri.
# muamke asubuhi
"muamke mapema"
# usiku tutalala
Malaika wawili waliposema hivi, walikuwa wakimaanisha wao wenyewe, na sio Lutu. Wao wawili walipanga kukaa usiku pale mjini.
# mjini
Hili ni eneo la wazi, lililo nje katika mji.
# wakaondoka pamoja nae
"waligeuka na kuondoka pamoja naye"