sw_tn/gen/17/09.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# nawe
Mungu anatumia msemo huu kutambulisha kile Abramu alichokuwa akielekea kufanya kama sehemu ya agano la Mungu na yeye.
# ulishike agano langu
"fuata agano langu" au "heshimu agano langu" au "tii agano langu"
# Hili ndilo agano langu
"Hili ni hitaji la agano langu" au "Hii ni sehemu ya agano langu". Sentensi hii inatambulisha sehemu ya agano ambayo Abramu ilimpasa afanye.
# Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unapaswa kutahiri kila mwanamume miongoni mwako"
# Kila mwanaume
Hii ina maana ya wanadamu wa kiume
# Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele
Baadhi ya jamii inaweza kutumia lugha nyepesi zaidi kama "Unatakiwa kutairiwa." Iwapo tafsiri yako ya "fanya tohara" inajumlisha neno la govi la ngozi ya mbele, hauhitaji kurudia.Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unatakiwa kuwatahiri wanamume wote miongoni mwenu"
# ishara ya agano
"ishara inayoonyesha ya kwamba agano lipo"
# ishara
Maana zaweza kuwa 1) "ishara" au 2) "ishara". Maana ya kwanza inaonyesha kulikuwa na ishara moja, na maana ya pili inaonyesha kulikuwa na ishara zaidi ya moja. Hapa neno "ishara" ina maana ya ukumbusho kuhusu jambo ambalo Mungu aliahidi.