sw_tn/gen/09/05.md

52 lines
1.8 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake.
# Lakini kwa ajili ya damu yenu
Hii inatofautisha damu ya mwanadamu na damu ya wanyama
# kwa ajili ya damu yenu
Inaonyesha ya kwamba damu imemwagwa, au imemwagika, au mwagikia. "iwapo yeyote atasababisha damu yako kumwagika" au "iwapo yeyote atamwaga damu yako" au "iwapo yeyote atakuua"
# uhai
Hii ina maana ya uhai wa mwili.
# nitataka malipo
Malipo haya yana maana kifo kwa yule muuaji, sio fedha. "Nitataka yeyote atakayekuua kulipa"
# Kutoka katika mkono
Hapa neno "mkono" lina maana ya yule mtu anayehusika na jambo kutendeka.
# Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka
"Nitataka mnyama yeyote atakayetoa uhai wako kulipa"
# Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.
"Nitataka mtut yeyote atakayetoa uhai wa mtu mwingine kulipa"
# Kutoka katika mkono
Msemo huu una maana ya mtu katika hali ya ukaribu sana. "Kutoka kwa mtu huyo kabisa"
# ndugu
Hapa "ndugu" inatumika kama kumbukumbu ya jumla kwa jamaa, kama wanajumuiya wa kabila moja, ukoo au kikundi cha watu.
# Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa
Kumwaga kwa damu ni sitiari kwa ajili ya kuua mtu. Hii ina maanisha kama mtu atamuua mtu, mtu mwingine anapaswa kumuua muuaji. japokuwa, "damu" ina umuhimu sana katika kipengele hichi na inapaswa kutumiwa katika tafsiri ikiwezekana.
# kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu
"kwa sababu Mungu aliumba watu wafanane na yeye" au "kwa sababu niliumba watu katika mfano wangu"
# zaeni na kuongezeka
Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu na familia yake kuzaa wanadamu wengine kama wao wenyewe, ili kusudi waweze kuwa wengi zaidi. Neno "kuongezeka" linafafanua jinsi ya wao "kuzaa"