sw_tn/deu/32/15.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli.
# Yeshuruni
Musa anazungumzia Waisraeli kana kwamba walikuwa mnyama aliyelishwa vizuri ambaye mmiliki wake alimuita Yeshuruni. Unaweza kuongeza maandishi yanayosema, "Jina la "Yeshuruni" ina maana ya "mnyoofu". Kama lugha yako haiwezi kuzungumza juu ya Waisraeli kama Yeshuruni, unaweza kuwasema Waisraeli kama watu wengi.
# akakua kwa unene na kupiga mateke
Yeshuruni, mnyama aliyelishwa vizuri ambaye hupiga mateke badala ya kuwa mpole ni sitiari ya Waisraeli, ambao waliasi ingawa Mungu aliwatunza.
# ulikua kwa unene, ulikua mnene sana, na ulikuwa umekula ujazo wako
Musa anawakaripia Waisraeli kwa kuzungumza ndani ya wimbo kwa Yeshuruni. "ukawa mnene, ukwa mnene zaidi, na ukawa mnene kadri uwezavyo kuwa"
# Mwamba wa wokovu wake
Hii ina maana Yahwe ana nguvu kama mwamba na anaweza kuwalinda watu wake.
# Mwamba
Hii ni jina stahiki ambalo Musa anampatia Yahwe, ambaye, kama mwamba, ana nguvu na anaweza kuwalinda watu wake.
# Walimfanya Yahwe apatwe wivu
Waisraeli walimfanya Yahwe awe na wivu.