sw_ulb_rev/41-MAT.usfm

1998 lines
126 KiB
Plaintext

\id MAT
\ide UTF-8
\h Mathayo
\toc1 Mathayo
\toc2 Mathayo
\toc3 mat
\mt Mathayo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
\v 2 Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.
\v 3 Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.
\s5
\v 4 Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.
\v 5 Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,
\v 6 Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.
\s5
\v 7 Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.
\v 8 Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.
\s5
\v 9 Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.
\v 10 Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.
\v 11 Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.
\s5
\v 12 Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.
\v 13 Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.
\v 14 Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.
\s5
\v 15 Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.
\v 16 Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.
\v 17 Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.
\s5
\v 18 Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
\v 19 Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.
\s5
\v 20 Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
\v 21 Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''
\s5
\v 22 Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,
\v 23 "Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli"-- maana yake, "Mungu pamoja nasi."
\s5
\v 24 Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.
\v 25 Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema,
\v 2 "Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu."
\v 3 Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.
\s5
\v 4 Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, "Kristo atazaliwa wapi?"
\v 5 Wakamwabia, "Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
\v 6 Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli."
\s5
\v 7 Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana.
\v 8 Akawatuma Bethelehem, akisema, "Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu."
\s5
\v 9 Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa.
\v 10 Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.
\s5
\v 11 Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane.
\v 12 Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.
\s5
\v 13 Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, "Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.
\v 14 Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri.
\v 15 Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, "Kutoka Misri nimemwita mwanangu."
\s5
\v 16 Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.
\s5
\v 17 Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia,
\v 18 "Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena."
\s5
\v 19 Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema,
\v 20 "Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa."
\v 21 Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.
\s5
\v 22 Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya
\v 23 na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema,
\v 2 "Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu."
\v 3 Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, "sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; 'wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake."'
\s5
\v 4 Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
\v 5 Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake.
\v 6 Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.
\s5
\v 7 Lakini alipowaona wengi wa mafarisayo na masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, ''Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
\v 8 Zaeni matunda yaipasayo toba.
\v 9 Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, 'Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.' Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.
\s5
\v 10 Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto.
\v 11 Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
\v 12 Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
\s5
\v 13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana.
\v 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, "Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?''
\v 15 Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu.
\s5
\v 16 Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake.
\v 17 Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, "Huyu ni mwanangu mpendwa. Ninaye pendezwa sana naye.''
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi.
\v 2 Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.
\v 3 Mjarabu akaja na akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate."
\v 4 Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, "Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.'''
\s5
\v 5 Kisha ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu,
\v 6 na kumwambia,'' kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, 'Ataamuru malaika wake waje wakudake,' na, 'watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe."
\s5
\v 7 Yesu akamwambia, ''Tena imeandikwa, 'Usimjaribu Bwana Mungu wako.'''
\v 8 Kisha, ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote.
\v 9 Akamwambia, "Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu."
\s5
\v 10 Kisha Yesu akamwambia, "Nenda zako utoke hapa, Shetani! Kwa maana imeandikwa, 'Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.'"
\v 11 Kisha ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.
\s5
\v 12 Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya.
\v 13 Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.
\s5
\v 14 Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya,
\v 15 "Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea Baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa!
\v 16 Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.''
\s5
\v 17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
\s5
\v 18 Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.
\v 19 Yesu akawaambia, "Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu."
\v 20 Mara moja waliziacha nyavu na walimfuata.
\s5
\v 21 Na Yesu alipokuwa akiendelea kutoka hapo aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita,
\v 22 na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.
\s5
\v 23 Yesu alienda karibia Galilaya yote, akifundisha katika Masinagogi yao, akihubiri injili ya ufalme, na akiponya kila aina ya maradhi na magonjwa miongoni mwa watu.
\v 24 Habari zake zilienea Siria yote, na watu wakawaleta kwake wale wote waliokuwa wakiugua, wakiwa na maradhi mbalimbali na maumivu, waliokuwa na mapepo, na wenye kifafa na waliopooza. Yesu aliwaponya.
\v 25 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.
\v 2 Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,
\v 3 "Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
\v 4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
\s5
\v 5 Heri wenye upole, maana watairithi nchi.
\v 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.
\v 7 Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema.
\v 8 Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.
\s5
\v 9 Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
\v 10 Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
\s5
\v 11 Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.
\v 12 Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.
\s5
\v 13 Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.
\v 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.
\s5
\v 15 Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.
\v 16 Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.
\s5
\v 17 Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza.
\v 18 Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.
\s5
\v 19 Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
\v 20 Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.
\s5
\v 21 Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, "usiue" na 'yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.'
\v 22 Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, 'Wewe ni mtu usiyefaa!' atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, 'Wewe mjinga!' atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.
\s5
\v 23 Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako,
\v 24 iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.
\s5
\v 25 Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.
\v 26 Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.
\s5
\v 27 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Usizini.'
\v 28 Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
\s5
\v 29 Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.
\v 30 Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.
\s5
\v 31 Imenenwa pia, yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.'
\v 32 Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.
\s5
\v 33 Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, 'Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.'
\v 34 Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu;
\v 35 wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Jerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.
\s5
\v 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
\v 37 Bali maneno yenu yawe, 'Ndiyo, ndiyo, Hapana, hapana.' Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
\s5
\v 38 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.'
\v 39 Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.
\s5
\v 40 Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia.
\v 41 Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.
\v 42 Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.
\s5
\v 43 Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.'
\v 44 Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,
\v 45 Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.
\s5
\v 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?
\v 47 Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?
\v 48 Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni.
\v 2 Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
\s5
\v 3 Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia,
\v 4 ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
\s5
\v 5 Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao.
\v 6 Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
\v 7 Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.
\v 9 Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako.
\v 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
\s5
\v 11 Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku.
\v 12 utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu.
\v 13 Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.'
\s5
\v 14 Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi.
\v 15 Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
\s5
\v 16 Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
\v 17 Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako.
\v 18 Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.
\s5
\v 19 Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.
\v 20 Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.
\v 21 Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.
\s5
\v 22 Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru.
\v 23 Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani!
\v 24 Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.
\s5
\v 25 Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
\v 26 Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?
\s5
\v 27 Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake?
\v 28 Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.
\v 29 Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.
\s5
\v 30 Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?
\v 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au "Je tutakunywa nini?" au "Je tutavaa nguo gani?"
\s5
\v 32 Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo.
\v 33 Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
\v 34 Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.
\v 2 Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.
\s5
\v 3 Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?
\v 4 Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?
\v 5 Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.
\s5
\v 6 Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.
\s5
\v 7 Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
\v 8 Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.
\v 9 Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe?
\v 10 Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
\s5
\v 11 Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?
\v 12 Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.
\s5
\v 13 Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo.
\v 14 Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.
\s5
\v 15 Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali.
\v 16 Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti?
\v 17 Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.
\s5
\v 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.
\v 19 Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.
\v 20 Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.
\s5
\v 21 Si kila mtu aniambiaye mimi, 'Bwana, Bwana,' ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
\v 22 Watu wengi wataniambia siku hiyo, 'Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?'
\v 23 Ndipo nitawaambia wazi, 'sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!'
\s5
\v 24 Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
\v 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
\s5
\v 26 Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
\v 27 Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika."
\s5
\v 28 Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake,
\v 29 kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.
\v 2 Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, "Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi".
\v 3 Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, "Niko tayari. Uwe msafi." Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.
\s5
\v 4 Yesu akamwambia, "Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao"
\s5
\v 5 Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza
\v 6 akisema, "Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha."
\v 7 Yesu akamwambia, "Nitakuja na kumponya".
\s5
\v 8 Jemedari akajibu na kumwambia, "Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa.
\v 9 Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu "Nenda' na huenda, na kwa mwingine 'Njoo' na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, 'Fanya hivi,' na yeye anafanya hivyo"
\v 10 Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, "Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.
\s5
\v 11 Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni.
\v 12 Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno."
\v 13 Yesu akamwambia Jemadari, "Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako". Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.
\s5
\v 14 Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa.
\v 15 Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. kisha akaamka akaanza kumhudumia.
\s5
\v 16 Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya.
\v 17 Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, "Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu"
\s5
\v 18 Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa Bahari ya Galilaya.
\v 19 Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, "Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda."
\v 20 Yesu akamwambia, "Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake."
\s5
\v 21 Mwanafunzi mwingine akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu."
\v 22 Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao."
\s5
\v 23 Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini.
\v 24 Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala.
\v 25 Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!"
\s5
\v 26 Yesu akawaambia, "kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?" Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu,
\v 27 wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, "Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?"
\s5
\v 28 Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.
\v 29 Tazama, walipaza sauti na kusema, "Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?"
\s5
\v 30 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa,
\v 31 pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. "Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe."
\v 32 Yesu akawaambia, "Nendeni!" Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.
\s5
\v 33 Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, hususani kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo.
\v 34 Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.
\v 2 Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. alipooiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, uwe na furaha, Dhambi zako zimesamehewa"
\s5
\v 3 Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, "Huyu mtu anakufuru"
\v 4 Yesu akatambua mawazo yao na kusema, "Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?
\v 5 Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?'
\v 6 Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi..." aliyasema haya kwa yule aliyepooza, "Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako"
\s5
\v 7 Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.
\v 8 Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.
\v 9 Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, "Nifuate mimi" Naye akasimama na kumfuata.
\s5
\v 10 Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake.
\v 11 Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi "Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?"
\s5
\v 12 Yesu aliposikia hayo, naye alisema " Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa.
\v 13 Inawapasa muende mkajifunze maana yake, "Ninapenda rehema na siyo dhabihu" Kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.
\s5
\v 14 Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, "Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?"
\v 15 Yesu akawaambia, Je wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.
\s5
\v 16 Hakuna mtu anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani, kiraka kitatatuliwa kutoka kwenye nguo na mpasuko mkubwa utatokea.
\s5
\v 17 Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika chombo cha mvinyo wa zamani, ikiwa watafanya, ngozi itachanika, mvinyo utatoweka na ngozi itaharibika. Badala yake, huweka mvinyo mpya katika ngozi mpya na vyote vitakuwa salama.
\s5
\v 18 Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, Naye akasema, " Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena.
\v 19 Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia.
\s5
\v 20 Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake.
\v 21 Kwa kuwa alisema, "Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji."
\v 22 Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. "Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone," Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji muda huo.
\s5
\v 23 Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.
\v 24 Naye akasema, "Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala. Lakini wao walicheka na kumkebehi.
\s5
\v 25 Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka.
\v 26 Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.
\s5
\v 27 Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, "Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi."
\v 28 Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, "Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?" Nao wakamwambia "Ndiyo, Bwana"
\s5
\v 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema "Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo"
\v 30 Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema "Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili."
\v 31 Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.
\s5
\v 32 Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, Tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu.
\v 33 Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema "Hii haijawahi kutokea katika Israel.
\v 34 Lakini mafarisayo walikuwa wakisema " Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo"
\s5
\v 35 Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.
\v 36 Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.
\s5
\v 37 Naye akawaambia wanafunzi wake. "Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache.
\v 38 Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maladhi na aina zote za magonjwa.
\s5
\v 2 Majina ya mitume kumi na wawili ni haya. La kwanza simeoni (ambaye pia anaitwa Petro), na Andrea kaka yake, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake:
\v 3 Philipo, na Bartelemayo, Thomaso, na Mathayo mtoza ushuru, Yakobo mwana wa Alfayo, na Tadeo,
\v 4 Simoni mkananayo, na Yuda iskariote, ambaye alimsaliti.
\s5
\v 5 Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema "Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya wasamalia.
\v 6 Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel.
\v 7 Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ufalme wa mbinguni umekaribia.'
\s5
\v 8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.
\v 9 Msichue dhahabu, almasi au shaba kwenye pochi zenu.
\v 10 Usichukue mkoba katika safari yenu, au nguo za ziada, viatu au fimbo, kwa kuwa mfanyakazi anastahili chakula chake.
\s5
\v 11 Mji wowote au kijiji mtakachoingia, tafuteni ambaye anastahili na mkae pale mpaka mtakapoondoka.
\v 12 Mtakapoingia katika nyumba salimieni,
\v 13 endapo nyumba inastahili, amani yenu ibaki pale, lakini kama nyumba haistahili, amani yenu iondoke pamoja nanyi.
\s5
\v 14 Na kwa wale wasiowapokea ninyi au kusikiliza maneno yenu, wakati mnaondoka kwenye nyumba au mji huo, jipanguseni mavumbi ya nyayo zenu mahali hapo.
\v 15 Kweli ninawaambia, itakuwa ya kustahimili zaidi miji ya Sodoma na Gomorah siku ya hukumu kuliko mji huo.
\s5
\v 16 Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.
\v 17 Muwe waangalifu na watu, watawapeleka kwenye mabaraza, na watawapiga kwenye masinagogi.
\v 18 Na mtaletwa mbele ya wakuu na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao na kwa mataifa.
\s5
\v 19 Pindi watakapowashutumu, msiwe na wasiwasi jinsi gani au nini cha kuongea, kwa kuwa kitu cha kusema mtapewa kwa wakati huo.
\v 20 Kwa kuwa sio ninyi mtakaoongea, lakini Roho wa Baba yenu ataongea ndani yenu.
\s5
\v 21 Ndugu atamwinukia ndugu yake kumwua, na baba kwa mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi, na kuwasababishia kifo.
\v 22 Nanyi mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini yeyote atakayevumilia mpaka mwisho mtu huyo ataokolewa.
\v 23 Pindi wanapowatesa katika mji huu, kimbilieni mji unaofuata, kwa kweli ninawaambia, hamtakuwa mmekwenda kwenye miji yote ya Israeli kabla ya mwana wa Adam hajarudi.
\s5
\v 24 Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya Bwana wake.
\v 25 Inatosha kwa mwanafunzi kwamba awe kama mwalimu wake, na mtumishi kama Bwana wake. Ikiwa wamemwita Bwana wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi watawakashifu wa nyumba yake!
\s5
\v 26 Hivyo basi msiwahofu wao, kwa kuwa hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililofichika ambalo halitajulikana.
\v 27 Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba.
\s5
\v 28 Msiwaogope wale ambao wanaua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho. Badala yake, mwogopeni yule ambaye awezaye kuangamiza mwili na roho kule kuzimu.
\v 29 Je kasuku wawili hawauzwi kwa senti ndogo? Hata hivyo hakuna anayeweza kuanguka chini bila Baba yenu kufahamu.
\v 30 Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa.
\v 31 Msiwe na hofu, kwa kuwa mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi.
\s5
\v 32 Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
\v 33 Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
\s5
\v 34 Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga.
\v 35 Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.
\v 36 Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake.
\s5
\v 37 Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili.
\v 38 Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili.
\v 39 Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata.
\s5
\v 40 Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi.
\v 41 Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki.
\s5
\v 42 Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
\v 2 na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
\v 3 na wakamuuliza, "Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?"
\s5
\v 4 Yesu akajibu na kusema kwao "Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.
\v 5 Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema.
\v 6 Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.
\s5
\v 7 Pindi watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, "Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa __tete likitikiswa na upepo?
\v 8 Lakini nini mlikwenda kuona__mtu aliyevaa mavazi mololo? Hakika, wale wavaao mavazi mololo hukaa katika nyumba za wafalme.
\s5
\v 9 Lakini mliondoka kuona nini-Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.
\v 10 Huyu ndiye aliyeandikiwa, 'Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.
\s5
\v 11 Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.
\v 12 Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.
\s5
\v 13 Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.
\v 14 Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.
\v 15 Aliye na masikio ya kusikia na asikie.
\s5
\v 16 Nikilinganishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana
\v 17 na kusema, 'Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.'
\s5
\v 18 Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, 'Ana pepo.'
\v 19 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''
\s5
\v 20 Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu,
\v 21 Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yangetendeka Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka hapa, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
\v 22 Lakini itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko kwako.
\s5
\v 23 Wewe, Kapernaum, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo.
\v 24 Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.
\s5
\v 25 Katika muda huo Yesu alisema, "Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.
\v 26 Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.
\v 27 Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.
\s5
\v 28 Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.
\v 29 Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu.
\v 30 Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.
\v 2 Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu "Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda siku yasiyo yuhusiwa siku ya Sabato''
\s5
\v 3 Lakini Yesu akawaambia, "Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao?
\v 4 Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate ya wonyesho, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa Makuhani?
\s5
\v 5 Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato Makuhani ndani ya hekalu huinajisi Sabato, lakini hawana hatia?
\v 6 Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa.
\s5
\v 7 Kama mngalijua hii ina maanisha nini; nataka rehema na siyo dhabihu; msingaliwahukumu wasio na hatia,
\v 8 Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato."
\s5
\v 9 Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao.
\v 10 Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. "Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?" ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi.
\s5
\v 11 Yesu akawaambia, "Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?
\v 12 Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo! Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.''
\s5
\v 13 Kisha Yesu akamwambia yule mtu," Nyoosha mkono wako" Akaunyoosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.
\v 14 Lakini Mafarisayo wakatoka njena wakapanga jinsi ya kumwangamiza walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua.
\s5
\v 15 Yesu alipoelewa hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaaponya wote.
\v 16 Aliwaagiza wasije wakamfanya afahamike kwa wengine,
\v 17 kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema,
\s5
\v 18 Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa Mataifa.
\s5
\v 19 Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani.
\v 20 Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda.
\v 21 Na Mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake.
\s5
\v 22 Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona.
\v 23 Makutano wote walishangaa na kusema,"Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?"
\s5
\v 24 Lakini pindi Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, "Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo.
\v 25 "Lakini Yesu alifahamu fikra zao na kuwaambia, "Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama.
\s5
\v 26 Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe.
\v 27 Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu huwatatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu.
\s5
\v 28 Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu.
\v 29 Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndiyo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba.
\v 30 Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya.
\s5
\v 31 Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.
\v 32 Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao
\s5
\v 33 Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake.
\v 34 Nyinyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni.
\v 35 Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu.
\s5
\v 36 Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.
\v 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa."
\s5
\v 38 Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema" Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako."
\v 39 Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, "Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.
\v 40 Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.
\s5
\v 41 Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Yona yuko hapa.
\s5
\v 42 Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Selemani yupo hapa.
\s5
\v 43 Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni
\v 44 Kisha husema, 'nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.' Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari.
\v 45 Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu.
\s5
\v 46 Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.
\v 47 Mtu mmoja akamwambia, "Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe".
\s5
\v 48 Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, "Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?"
\v 49 Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, "Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!
\v 50 Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu".
\s5
\c 13
\p
\v 1 Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.
\v 2 Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama kando ya bahari.
\s5
\v 3 Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, "Tazama, mpanzi alienda kupanda.
\v 4 Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.
\v 5 Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.
\v 6 Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.
\s5
\v 7 Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.
\v 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini
\v 9 Aliye na masikio na asikie.
\s5
\v 10 Wanafunzi walikuja na kumwambia Yesu, "Kwa nini unazungumza na makutano kwa mifano?"
\v 11 Yesu alijibu kuwaambia, "Mmepewa upendeleo wa kufahamu siri za ufalme wa mbinguni, bali kwao hawajapewa.
\v 12 Lakini yeyote aliyenacho, kwake yeye ataongezewa zaidi, na atapata faida kubwa. Ilasiye nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa.
.
\s5
\v 13 Hivyo naongea nao kwa mifano kwa sababu ingawa wanaona, wasione kweli. Na ingawa wanasikia wasisikie wala kufahamu.
\v 14 Unabii wa Isaya umetimia kwao, ule usemao, "Msikiapo msikie, lakini kwa namna yoyote hamtaelewa; wakati mwonapo muweze kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue.
\s5
\v 15 Na mioyo ya watu hawa imekuwa giza, ni vigumu kusikia, na wamefumba macho yao, ili wasiweze kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao, au kufahamu kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena, na ningewaponya.'
\s5
\v 16 Bali macho yenu yamebarikiwa, kwa kuwa yanaona, na masikio yenu kwa kuwa yanasikia.
\v 17 Hakika nawaambia manabii wengi na watu wenye haki walikuwa na hamu ya kuyaona mambo yale myaonayo, na hawakuweza kuyaona. Walitamani kusikia mambo yale mnayosikia, hawakuyasikia.
\s5
\v 18 . Sasa sikilizeni mfano wa mpanzi.
\v 19 Wakati yeyote asikiapo neno la ufalme na asilifahamu, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kupandwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.
\s5
\v 20 Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.
\v 21 Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.
\s5
\v 22 Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.
\v 23 Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.''
\s5
\v 24 Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, "Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake
\v 25 Lakini watu waliposinzia, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake.
\v 26 Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia.
\s5
\v 27 Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, 'Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu?
\v 28 Akawaambia, Adui ametenda hili.' Watumishi walimwambia, "Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?"
\s5
\v 29 Mwenye shamba akisema, 'Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano.
\v 30 Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, 'Kwanza yang'oeri magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.''''
\s5
\v 31 Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, "Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake.
\v 32 Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake."
\s5
\v 33 Akawaambia mfano mwingine tena."Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke.
\s5
\v 34 Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao.
\v 35 Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, "Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu".
\s5
\v 36 Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, "Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.''
\v 37 Yesu alijibu na kusema, "Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
\v 38 Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni ibilisi.
\v 39 Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.
\s5
\v 40 Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu.
\v 41 Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi.
\v 42 Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\v 43 Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na sikie.
\s5
\v 44 Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba.
\v 45 Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani.
\v 46 Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.
\s5
\v 47 Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina.
\v 48 Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali.
\s5
\v 49 Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki.
\v 50 Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno.
\s5
\v 51 Mmefahamu mambo yote haya? Wanafunzi walimjibu, ''Ndiyo.''
\v 52 Kisha Yesu akawambia, ''Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.''
\v 53 IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo.
\s5
\v 54 Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, "Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?
\v 55 Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda?
\v 56 Na dada zake tunao hapa petu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?".
\s5
\v 57 Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, "Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao.
\v 58 Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu..
\v 2 Akawaambia watumishi wake, "Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake."
\s5
\v 3 Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.
\v 4 Kwa kuwa Yohana alimwambia, "Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake."
\v 5 Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.
\s5
\v 6 Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.
\v 7 Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.
\s5
\v 8 Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, "Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\v 9 Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.
\s5
\v 10 Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani
\v 11 ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.
\v 12 Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.
\s5
\v 13 Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.
\v 14 Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao.
\s5
\v 15 Jioni ilipotimia, wanafunzi wakaja kwake na kusema, "Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao.
\s5
\v 16 Lakini Yesu akawaambia, ''Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula"
\v 17 Wakamwambia, ''Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu."''
\v 18 Yesu akasema, "Ileteni kwangu."
\s5
\v 19 Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini ya nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati.
\v 20 Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili.
\v 21 Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.
\s5
\v 22 Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.
\v 23 Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.
\v 24 Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mpisho.
\s5
\v 25 Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.
\v 26 Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, "Ni mzuka,'' na kupaaza sauti katika hali ya uoga.
\v 27 Yesu akawaambia mara moja, akisema, "Jipeni moyo! ni mimi! msiogope."
\s5
\v 28 Petro alimjibu kwa kusema, "Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.''
\v 29 Yesu akasema, "Njoo.'' Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.
\v 30 Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, "Bwana, niokoe!''
\s5
\v 31 Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, "Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?"
\v 32 Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulikoma kuvuma.
\v 33 Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, "Kweli wewe ni Mwana wa Mungu."
\s5
\v 34 Na walipokwisha kuvuka, walifika katika nchi ya Genesareti.
\v 35 Na watu katika eneo lile walipomtambua Yesu, walituma ujumbe kila sehemu za kando, na kuleta kila aliyekuwa mgonjwa.
\v 36 Walimsihi kwamba waweze kugusha pindo la vazi lake, na wengi walioligusa waliponywa.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,
\v 2 "Kwa nini wanafunzi wanayahalifu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.''
\v 3 Yesu akawajibu na kuwaambia, "Nanyi__kwa nini mnaihalifu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?
\s5
\v 4 Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.'
\v 5 Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '"Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,'''
\v 6 "Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
\s5
\v 7 Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,
\v 8 'Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
\v 9 Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu."'
\s5
\v 10 Ndipo akawaita makutano na kuwaambia," Sikilizeni na mfahamu__
\v 11 Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.''
\s5
\v 12 Ndipo wanafunzi wakamwendea na kusema na Yesu, "Je!, Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?"
\v 13 Yesu aliwajibu na kusema, "Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.
\v 14 Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni."
\s5
\v 15 Petro akajibu na kumwambia Yesu," Tuelezee mfano huu kwetu,
\v 16 Yesu akajibu, ''Nanyi pia bado hamuelewi?
\v 17 Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?.
\s5
\v 18 Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.
\v 19 Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.
\v 20 Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi."
\s5
\v 21 Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.
\v 22 Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, ''Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.''
\v 23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsihi, wakisema, ''Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.''
\s5
\v 24 Yesu aliwajibu na kusema, Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.''
\v 25 Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, ''Bwana nisaidie.''
\v 26 Alimjibu na kusema, "Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa,"
\s5
\v 27 Akasema, "Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao."
\v 28 Ndipo Yesu akajibu na akisema "Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo." Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.
\s5
\v 29 Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko.
\v 30 Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya.
\v 31 Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.
\s5
\v 32 Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, " Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani."
\v 33 Wanafunzi wake wakamwambia, "Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkuwbwa hivi?"
\v 34 Yesu akawaambia, "Mna mikate mingapi?" Wakasema, "Saba, na samaki wadogo wachache."
\v 35 Yesu akawaamuru umati uketi chini.
\s5
\v 36 Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.
\v 37 Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.
\v 38 Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.
\v 39 Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Mafarisayo na Masadukayo walimjia na kumjaribu Yesu awaonyeshe ishara inayotoka angani.
\v 2 Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kuwa "Ikiwa ni jioni mnasema kuwa hali ya hewa ni nzuri, kwa kuwa anga ni jekundu.
\s5
\v 3 Na asubuhi mnasema 'Hali ya hewa leo si nzuri kwa kuwa anga ni jekundu na mawingu yameifunika anga lote.' Mnajua kufasiri mwonekano wa anga, lakini hamwezi kufasiri ishara za nyakati.
\v 4 Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakuna ishara yoyote kitakachopewa, isipokuwa ile ya Yona. Kisha Yesu akawaacha na akaenda zake.
\s5
\v 5 Wanafunzi wakaja upande wa pili, lakini walikuwa wamesahau kuchukua mikate.
\v 6 Yesu akawaambia " Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo."
\v 7 Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. "Ni kwa sababu hatukuchukua mikate."
\v 8 Yesu alitambua hilo na kusema, "Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate?
\s5
\v 9 Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya?
\v 10 Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlikuchukua?
\s5
\v 11 Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo."
\v 12 Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
\s5
\v 13 Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, "Watu wanasema kuwa Mwana wa Mtu ni nani?"
\v 14 Wakasema," Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii.
\v 15 Akawaambia, ninyi mwasema mimi ni nani?
\v 16 Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, "Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai"
\s5
\v 17 Yesu akamjibu na kumwambia, "Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
\v 18 Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda.
\s5
\v 19 Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni."
\v 20 Kisha Yesu akawaamuru wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye alikuwa ni Kristo.
\s5
\v 21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.
\v 22 Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, kwa kusema, "Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako.
\v 23 Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, "Rudi nyuma yangu shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu."
\s5
\v 24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kama mtu yeyote akitaka kunifuata mimi, ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.
\v 25 Kwa kuwa anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na kwa yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
\v 26 Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?
\s5
\v 27 Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika wake. Naye atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.
\v 28 Kweli nawaambieni kuna baadhi yenu mliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.
\v 2 Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.
\s5
\v 3 Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.
\v 4 Petro akajibu na kumwambia Yesu, "Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya."
\s5
\v 5 Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye."
\v 6 Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.
\v 7 Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, "Inukeni wala msiogope."
\v 8 Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.
\s5
\v 9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, "Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu."
\v 10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, " Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?
\s5
\v 11 Yesu akawajibu na kusema, "Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.
\v 12 Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao."
\v 13 Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.
\s5
\v 14 Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,
\v 15 "Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.
\v 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
\s5
\v 17 Yesu akajibu akisema, "Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu."
\v 18 Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.
\s5
\v 19 Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, "Kwanini hatukuweza kumfukuza?"
\v 20 Yesu akawaambia, "Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.
\v 21 (Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 "Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga" hayaonekani katika nakala bora za kale).
\s5
\v 22 Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, "Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.
\v 23 Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka." Wanafunzi walihuzunika sana.
\s5
\v 24 Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, "Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?"
\v 25 Akasema, "Ndiyo" Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, " Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni?
\s5
\v 26 Na wakati Petro aliposema, "Kutoka kwa wageni" Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.
\v 27 Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, "Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?"
\v 2 Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao,
\v 3 na kusema, "Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
\s5
\v 4 Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.
\v 5 Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi.
\v 6 Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari.
\s5
\v 7 Ole kwa dunia kwa sababu ya wakati wa kukwazwa! kwa kuwa haina budi kwa nyakati hizo kuja, lakini ole kwake kwa mtu yule nyakati hizo zitakuja kwa ajili yake!
\v 8 kama mkono wako au mguu wako ukikusababishia kukwazika, ukate na uutupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe kuingia kwenye uzima ukiwa bila mkono au kilema, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote au miguu yote.
\s5
\v 9 Kama jicho lako likikukwaza, uling`oe na ulitupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe uingie kwenye uzima na jicho moja, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na macho yote.
\s5
\v 10 Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
\v 11 (Zingatia: Maneno yanayoonekana kama ya msitari wa 11, "Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichokuwa kimepotea" hayakuonekana katika nakala bora za kale).
\s5
\v 12 Mnafikiri nini? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je hatawaacha tisini na tisa ya mlimani na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea?
\v 13 Na akiisha kumpata, kweli nawaambieni, anamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
\v 14 Vivyo hivyo, siyo mapenzi ya Baba yenu wa mbinguni kuwa mmoja wa wadogo hawa aangamie.
\s5
\v 15 Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako.
\v 16 Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa.
\s5
\v 17 Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
\s5
\v 18 Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa.
\v 19 Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya.
\v 20 Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.
\s5
\v 21 Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, "Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?"
\v 22 Yesu akamwambia, "Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba.
\s5
\v 23 Kwa sababu hiyo ufalme wa mbinguni ni sawa na mfalme fulani aliyetaka kusahihisha hesabu kutoka kwa watumwa wake.
\v 24 Alipoanza kusahihisha hesabu, mtumwa moja akaletwa kwake ambaye alikuwa anamdai talanta elfu kumi.
\v 25 Kwa kuwa hakuwa na njia ya kulipa, bwana wake aliagiza auzwe, mke wake pamoja na watoto wake na kila kitu alichokuwa nacho, na malipo yafanyike.
\s5
\v 26 Hivyo mtumwa alianguka, akapiga magoti mbele yake, akisema, 'Bwana, uwe na uvumilivu pamoja nami, na nitakulipa kila kitu.'
\v 27 Hivyo bwana wa yule mtumwa, kwa kuwa alisukumwa sana na huruma, alimwachilia na kumsamehe deni hilo
\s5
\v 28 Lakini mtumwa yule alitoka na kumpata mmoja kati ya watumwa wenzake, aliyekuwa anamdai denari mia. Alimvuta, akamkaba kooni, na kumwambia, 'Nilipe kile ninachokudai.'
\v 29 Lakini yule mtumwa mwenzake alianguka na kumsihi sana, akisema, 'Uwe na uvumilivu nami, na nitakulipa.'
\s5
\v 30 Lakini mtumwa yule wa kwanza alikataa. Badala yake, alienda na kumtupa gerezani, mpaka atakapo mlipa kile anachomdai.
\v 31 Na walipoona watumwa wenzake kile kilichotokea. Walisikitishwa sana. Walikuja na kumwambia bwana wao kila kitu kilichotokea.
\s5
\v 32 Ndipo yule bwana wa mtumwa yule alimwita, na kumwambia, 'Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni langu lote kwa sababu ulinisihi sana.
\v 33 Je! Haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio, kama mimi nilivyokuhurumia wewe?
\s5
\v 34 Bwana wake alikasirika na kumkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa kiasi chote alichokuwa anadaiwa.
\v 35 Hivyo ndivyo Baba yangu wa Mbinguni atakavyowafanyia, kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwenu."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ilitokea wakati Yesu alipomaliza maneno hayo, akaondoka Galilaya, na akaenda mpakani mwa Yudea mbele ya mto Jordani.
\v 2 Umati mkubwa ukamfuata, na akawaponya huko.
\s5
\v 3 Mafarisayo wakamjia, wakamjaribu, wakamwambia, "Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?"
\v 4 Yesu akajibu na kusema, "Hamkusoma, kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke?
\s5
\v 5 Na tena akasema, 'Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?'
\v 6 Hivyo siyo wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, kile alichokiunganisha Mungu, mtu yeyote asikitenganishe."
\s5
\v 7 Wakamwambia, "Sasa kwa nini Musa alituamuru kutoa hati ya talaka na kumwacha?"
\v 8 Akawaambia, "Kwa ugumu wenu wa mioyo Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.
\v 9 Nawaambieni, kwamba yeyote atayemwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, na akamwoa mwingine, amezini. Na mwanaume atakayemwoa mke aliyeachwa amezini."
\s5
\v 10 Wanafunzi wakamwambia Yesu, "Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa."
\v 11 Lakini Yesu akawaambia, "Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea.
\v 12 Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vilevile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee."
\s5
\v 13 Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea.
\v 14 Bali Yesu akasema, "Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.
\v 15 Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.
\s5
\v 16 Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, "Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?"
\v 17 Yesu akamwambia, "Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu."
\s5
\v 18 Yule mtu akamwuliza, "Ni sheria zipi?" Yesu akasema, "Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,
\v 19 waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako."
\s5
\v 20 Mtu yule akamwambia, "Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini?
\v 21 "Yesu akamwambia, "Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate."
\v 22 Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na amemiliki mali nyingi.
\s5
\v 23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kweli nawaambieni, ni vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.
\v 24 Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 25 Wanafunzi waliposikia hivyo, wakashangaa sana na kusema, "Ni yupi basi atakayeokoka?"
\v 26 Yesu akawatazama na kusema, "Kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana."
\v 27 Kisha Petro akamjibu na kumwambia, "Tazama, tumeacha vyote na kukufuata wewe. Ni kitu gani tutakachopata?"
\s5
\v 28 Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, yeye aliyenifuata mimi, katika uzao mpya wakati Mwana wa Adam atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake, ninyi pia mtaketi juu ya viti kumi na viwili vya enzi, kuwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
\s5
\v 29 Kila mmoja wenu aliyeacha nyumba, kaka, dada, baba, mama, watoto, au shamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele.
\v 30 Lakini wengi walio wa kwanza sasa, watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu.
\v 2 Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.
\s5
\v 3 Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.
\v 4 Akawaambia, 'Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.' Hivyo wakaenda kufanya kazi.
\s5
\v 5 Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo.
\v 6 Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, 'kwanini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?
\v 7 Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, 'Nanyi ninyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.'
\s5
\v 8 Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, 'Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.'
\v 9 Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.
\v 10 Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu.
\s5
\v 11 Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba.
\v 12 Wakasema, 'Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.'
\s5
\v 13 Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, 'Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja?
\v 14 Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe.
\s5
\v 15 Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?
\v 16 Hivyo wa mwisho atakuwa kwanza na wa kwanza wa mwisho''
\s5
\v 17 Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,
\v 18 ''Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo
\v 19 na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulibisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.''
\s5
\v 20 Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake.
\v 21 Yesu akamwambia, "Unataka nini?" Akamwambia, ''Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.''
\s5
\v 22 Lakini Yesu akajibu na kusema, "Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?" wakamwambia, "Tunaweza."
\v 23 Akawaambia, "Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu."
\v 24 Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.
\s5
\v 25 Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, "Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao.
\v 26 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
\v 27 Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
\v 28 Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi."
\s5
\v 29 Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.
\v 30 Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, "Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie."
\v 31 Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, "Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie."
\s5
\v 32 Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
\v 33 Wakamwambia, "Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe."
\v 34 Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethfage, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,
\v 2 akiwaambia, "Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. wafungueni na kuwaleta kwangu.
\v 3 Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, `Bwana anawahitaji, ` na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao"
\s5
\v 4 Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,
\v 5 Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme, mwana punda mchanga.
\s5
\v 6 Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.
\v 7 Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.
\v 8 Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.
\s5
\v 9 Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema,"Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!"
\v 10 Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, "Huyu ni nani?
\v 11 "Umati ulijibu, "Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya."
\s5
\v 12 Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.
\v 13 Akawaambia, "Imeandikwa, `'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi, `lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang`anyi."
\v 14 kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.
\s5
\v 15 Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, "Hosana kwa Mwana wa Daudi," walishikwa na hasira.
\v 16 Wakamwambia, "Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?" Yesu akawaambia, "Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, 'Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?''
\v 17 Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.
\s5
\v 18 Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.
\v 19 Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, "Kusiwe na matunda kwako daima tena." Na mara hiyo mtini ule ukanyauka.
\s5
\v 20 Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, "Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?"
\v 21 Yesu akajibu na kuwaambia, "Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ` uchukuliwe na ukatupwe baharini, `na itafanyika.
\v 22 Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea."
\s5
\v 23 Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, "Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?"
\v 24 Yesu akajibu na kuwaambia, "Nami tena nitawauliza swali moja. kama mkiniambia, nami vilevile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
\s5
\v 25 Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?" Wakahojiana wenyewe, wakisema, tukisema, ulitoka mbinguni, `atatuambia, kwa nini hamkumwamini? `
\v 26 Lakini tukisema, `ulitoka kwa wanadamu, `tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii."
\v 27 Kisha wakamjibu Yesu na kusema, "Hatujui" Akawaambia pia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.
\s5
\v 28 Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, `Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu
\v 29 leo. `Mwana akajibu na kusema, `sitakwenda, ' Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda.
\v 30 Na Mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kilekile. Mwana huyu akajibu na kusema, `nitakwenda, bwana', lakini hakwenda.
\s5
\v 31 Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, "Mwana wa kwanza." Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia.
\v 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.
\s5
\v 33 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.
\v 34 Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.
\s5
\v 35 Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.
\v 36 Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile.
\v 37 Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, `'Watamheshimu mwanangu.'`
\s5
\v 38 Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, `'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.'
\v 39 `Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.
\s5
\v 40 Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?"
\v 41 Wakamwambia, "Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva."
\s5
\v 42 Yesu akawaambia, "Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?'
\s5
\v 43 Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.
\v 44 Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga."
\s5
\v 45 Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.
\v 46 Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,
\v 2 "Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.
\v 3 Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.
\s5
\v 4 Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. "Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi."
\s5
\v 5 Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.
\v 6 Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua.
\v 7 Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
\s5
\v 8 Kisha aliwaambia watumishi wake, "Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.
\v 9 Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi."
\v 10 Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.
\s5
\v 11 Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!
\v 12 Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote.
\s5
\v 13 Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, "Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\v 14 Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache."
\s5
\v 15 Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.
\v 16 Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, "Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.
\v 17 Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?"
\s5
\v 18 Yesu alifahamu uovu wao na akasema, "Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?
\v 19 Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi." Ndipo wakamletea dinari.
\s5
\v 20 Yesu akawauliza, "Sura na jina hili ni vya nani?"
\v 21 Wakamjibu, "Vya Kaisari." Ndipo Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu."
\v 22 Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.
\s5
\v 23 Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,
\v 24 wakisema, "Mwalimu, Musa alisema, Ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.
\s5
\v 25 Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.
\v 26 Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.
\v 27 Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.
\v 28 Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa."
\s5
\v 29 Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, "Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.
\v 30 Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.
\s5
\v 31 Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,
\v 32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
\v 33 Wakati kusanyiko waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.
\s5
\v 34 Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.
\v 35 Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.
\v 36 "Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?"
\s5
\v 37 Yesu akamjibu, "Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
\v 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.
\s5
\v 39 Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
\v 40 Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili."
\s5
\v 41 Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.
\v 42 Akisema, "J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?" Nao wakamjibu, "Ni mwana wa Daudi."
\s5
\v 43 Yesu akawajibu, "Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,
\v 44 'Bwana alimwambia Bwana wangu, "Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako."'?"
\s5
\v 45 Kama Daudi anamwita Kristo "Bwana," jinsi gani atakuwa mtoto wake?"
\v 46 Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema,
\v 2 "Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.
\v 3 Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.
\s5
\v 4 Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.
\v 5 Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.
\s5
\v 6 Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,
\v 7 na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa "Walimu" na watu.
\s5
\v 8 Lakini ninyi hampaswi kuitwa "Walimu," Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.
\v 9 Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.
\v 10 Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.
\s5
\v 11 Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.
\v 12 Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
\s5
\v 13 Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.
\v 14 (Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 "Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane").
\v 15 Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ngambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo.
\s5
\v 16 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao,, Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.
\v 17 Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?
\s5
\v 18 Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.
\v 19 Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?
\s5
\v 20 Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
\v 21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.
\v 22 Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.
\s5
\v 23 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.
\v 24 Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!
\s5
\v 25 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.
\v 26 Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.
\s5
\v 27 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila kitu kilicho kichafu.
\v 28 Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.
\s5
\v 29 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.
\v 30 Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.
\v 31 Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.
\s5
\v 32 Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.
\v 33 Enyi nyoka, wana wa vipiribao, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu?
\s5
\v 34 Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.
\v 35 Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.
\v 36 Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.
\s5
\v 37 Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, lakini haukukubali!
\v 38 Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.
\v 39 Nami nakuambia, Kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, 'Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana."'
\s5
\c 24
\p
\v 1 Yesu alitoka hekaluni na kwenda zake. Wanafunzi wake walimwendea na kumuonesha majengo ya hekalu.
\v 2 Laikni aliwajibu na kuwaambia, "Je, hamuyaoni mambo haya yote? Kweli nawaambia, hakuna jiwe litalobaki juu ya lingine bila kubomolewa."
\s5
\v 3 Na alipokaa katika Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, "Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?"
\v 4 Yesu aliwajibu na kuwaambia, "Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha.
\v 5 Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, 'Mimi ndiye Kristo', na watawapotosha wengi.
\s5
\v 6 Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado.
\v 7 Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali.
\v 8 Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 9 Ndipo watawatoa kwa ajili ya mateso na kuwaua. Mtachukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.
\v 10 Ndipo wengi watajikwaa na kusalitiana na watachukiana wenyewe kwa wenyewe.
\v 11 Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.
\s5
\v 12 Kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapoa.
\v 13 Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
\v 14 Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote. Na ndipo ule mwisho utafika.
\s5
\v 15 Kwa hiyo, mtakapoona chukizo la uharibifu, lililosemwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu [asomaye na afahamu],
\v 16 ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani.
\v 17 Na yule aliyeko juu ya paa la nyumba asiweze kuteremka chini kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya nyumba yake,
\v 18 naye aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.
\s5
\v 19 Lakini ole wao ambao wana mtoto na wale ambao wananyonyesha katika siku hizo!
\v 20 Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
\v 21 Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi sasa, na wala haitakuwapo tena.
\v 22 Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka. Lakini kwa sababu ya wateule, siku hizo zitafupishwa.
\s5
\v 23 Kisha ikiwa mtu yeyote atawaambia 'Tazama, Kristo yuko hapa! au, 'Kristo yuko kule' msiamini maneno hayo.
\v 24 Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo watakuja na kuonesha ishara kubwa na maajabu, kwa kusudi la kupotosha, kama ingewezekana hata na wateule.
\v 25 Tazameni, nimewatahadharisha kabla ya mambo hayo kutokea.
\s5
\v 26 Kwa hiyo, ikiwa watawaambia, ''Kristo yuko jangwani,' msiende huko jangwani. Au, 'Tazameni, yuko ndani ya nyumba,' msiamini maneno hayo.
\v 27 Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\v 28 Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.
\s5
\v 29 Lakini mara baada ya dhiki kuu ya siku zile, Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbinguni zitatikisika.
\s5
\v 30 Ndipo ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na makabila yote ya dunia wataomboleza. Watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu ya angani kwa nguvu na utukufu mkuu.
\v 31 Atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine.
\s5
\v 32 Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.
\v 33 Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango.
\s5
\v 34 Kweli nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.
\v 35 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\s5
\v 36 Lakini kuhusu siku ile na saa hakuna mtu ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, bali Baba peke yake.
\s5
\v 37 Kama vile ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\v 38 Kwa kuwa katika siku hizo kabla ya gharika watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa hadi siku ile ambayo Nuhu aliingia katika safina,
\v 39 na hawakujua kitu chochote hadi gharika ilipokuja na kuwasomba wote - ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\s5
\v 40 Ndipo watu wawili watakuwa shambani- mmoja atachukuliwa, na mmoja ataachwa nyuma.
\v 41 Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja - mmoja atachukuliwa, na mmoja atabaki.
\v 42 Kwa hiyo, kuweni macho kwa sababu hamjui ni siku gani ambayo atakuja Bwana wenu.
\s5
\v 43 Lakini mjue kwamba, ikiwa bwana mwenye nyumba angejua ni saa ipi ambayo mwizi angekuja, angekesha na asingeruhusu nyumba yake kuvamiwa.
\v 44 Kwa hiyo, pia mnapaswa kuwa tayari, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika saa msiyoitarajia.
\s5
\v 45 Hivyo ni nani aliye mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake amempa madaraka juu ya walio katika nyumba yake, ili awape chakula kwa wakati unaofaa?
\v 46 Amebarikiwa mtumishi huyo, ambaye bwana wake atamkuta akifanya hivyo wakati ajapo.
\v 47 Kweli nawaambia kwamba bwana atamweka juu ya kila kitu kilicho chake.
\s5
\v 48 Lakini kama mtumwa mwovu akisema moyoni mwake, 'Bwana wangu amekawia,'
\v 49 na akaanza kuwapiga watumishi wake, na akala na kulewa vileo,
\v 50 Bwana wa mtumwa huyo atakuja katika siku ambayo haitarajii, na katika saa ambayo haijui.
\v 51 Bwana wake atamkata vipande viwili na kumweka katika nafasi moja sawa na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi.
\v 2 Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu.
\v 3 Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote.
\v 4 Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.
\s5
\v 5 Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala.
\v 6 Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.'
\s5
\v 7 Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao.
\v 8 Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.'
\v 9 Lakini wale welevu waliwajibu na kuwaambia, 'Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.'
\s5
\v 10 Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa.
\v 11 Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.'
\v 12 Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.'
\v 13 Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.
\s5
\v 14 Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake.
\v 15 Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake.
\v 16 Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.
\s5
\v 17 Vilevile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili.
\v 18 Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.
\s5
\v 19 Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao.
\v 20 Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, 'Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.'
\v 21 Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
\s5
\v 22 Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, 'Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,'
\v 23 Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
\s5
\v 24 Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, 'Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia.
\v 25 Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.'
\s5
\v 26 Lakini bwana wake alijibu na kusema, 'Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.
\v 27 Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.
\s5
\v 28 Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi.
\v 29 Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa.
\v 30 Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.'
\s5
\v 31 Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu.
\v 32 Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi.
\v 33 Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto.
\s5
\v 34 Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, 'Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.
\v 35 Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;
\v 36 Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.'
\s5
\v 37 Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji?
\v 38 Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo?
\v 39 Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia?
\v 40 Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.'
\s5
\v 41 Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, 'Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake,
\v 42 kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji;
\v 43 Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.'
\s5
\v 44 Ndipo wao pia watamjibu na kusema, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia?
\v 45 Kisha atawajibu na kusema, 'Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.'
\v 46 Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele."
\s5
\c 26
\p
\v 1 Wakati Yesu alipomaliza kusema maneno yote hayo, aliwaambia wanafunzi wake,
\v 2 "Mnajua kwamba baada ya siku mbili kutakuwa na sikukuu ya pasaka, na mwana wa Adamu atatolewa ili asulibiwe."
\s5
\v 3 Baadaye wakuu wa makuhani na wazee wa watu walikutana pamoja katika makao ya Kuhani Mkuu, aliye kuwa anaitwa Kayafa.
\v 4 Kwa pamoja walipanga njama ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.
\v 5 Kwa kuwa walisema, "Isifanyike wakati wa sikukuu, kusudi isije ikazuka ghasia miongoni mwa watu."
\s5
\v 6 Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,
\v 7 alipokuwa amejinyoosha mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa amebeba mkebe wa alabasta iliyokuwa na mafuta yenye thamani kubwa, na aliyamimina juu ya kichwa chake.
\v 8 Lakini wanafunzi wake walipoona jambo hilo, walichukia na kusema, "Nini sababu ya hasara hii?
\v 9 Haya yangeweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa na kupewa maskini."
\s5
\v 10 Lakini Yesu, akiwa anajua hili, aliwaambia, "Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Kwa kuwa amefanya kitu kizuri kwangu.
\v 11 Masikini mnao siku zote, lakini hamtakuwa pamoja nami daima.
\s5
\v 12 Kwa sababu alipomimina mafuta haya juu ya mwili wangu, alifanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.
\v 13 Kweli nawaambieni, popote Injili hii itakapohubiriwa katika ulimwengu mzima, kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka."
\s5
\v 14 Ndipo mmoja wa wale Kumi na wawili, aliyeitwa Yuda Iskariote, alienda kwa wakuu wa makuhani
\v 15 na kusema, "Mtanipatia nini nikimsaliti?" Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.
\v 16 Tangu muda huo alitafuta nafasi ya kumsaliti.
\s5
\v 17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, "Wapi unataka tukuandalie ule chakula cha Pasaka?"
\v 18 Akawaambia, "Nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni, Mwalimu anasema, "Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.""
\v 19 Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza, na waliandaa chakula cha Pasaka.
\s5
\v 20 Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi Kumi na Wawili.
\v 21 Walipokuwa wanakula chakula, alisema, "Kweli nawaambia kwamba mmoja wenu atanisaliti."
\v 22 Walihuzunika sana, na kila mmoja alianza kumuuliza, "Je, hakika siyo mimi, Bwana?"
\s5
\v 23 Akawajibu, "Yule ambaye anachovya mkono wake pamoja nami katika bakuli ndiye atakaye nisaliti.
\v 24 Mwana wa Adamu ataondoka, kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu ambaye atamsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama asingezaliwa."
\v 25 Yuda, ambaye angemsaliti alisema, "Je!, Ni mimi Rabi?" Yesu akamwambia, "Umesema jambo hilo wewe mwenyewe."
\s5
\v 26 Walipokuwa wakila chakula, Yesu aliutwaa mkate, akaubariki, na kuumega. Akawapa wanafunzi wake akisema, "Chukueni, mle. Huu ni mwili wangu."
\s5
\v 27 Akatwaa kikombe na kushukuru, akawapa na kusema, "Kunyweni wote katika hiki.
\v 28 Kwa kuwa hii ni damu ya agano langu, inayomwagwa kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.
\v 29 Lakini nawaambieni, sitakunywa tena matunda ya mzabibu huu, hadi siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu."
\s5
\v 30 Walipokuwa wamemaliza kuimba wimbo, walitoka kwenda Mlima wa Mizeituni.
\v 31 Kisha Yesu aliwaambia, "Usiku huu ninyi nyote mtajikwaa kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika.
\v 32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya."
\s5
\v 33 Lakini Petro alimwambia, "Hata kama wote watakukataa kwa sababu ya mambo yatakayokupata, mimi sitakukataa."
\v 34 Yesu akamjibu, "kweli nakuambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
\v 35 Petro akamwambia, "hata kama ingenipasa kufa na wewe, sitakukana." Na wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
\s5
\v 36 Baadaye Yesu alienda nao mahali panapoitwa Gethsemane na aliwaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa wakati nikienda huko na kuomba."
\v 37 Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo na akaanza kuhuzunika na kusononeka.
\v 38 Kisha aliwaambia, "Roho yangu ina huzuni kubwa sana, hata kiasi cha kufa. Bakini hapa na mkeshe pamoja nami."
\s5
\v 39 Akenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, na kuomba. Akasema, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniepuke. Isiwe kama ninavyotaka mimi, bali kama utakavyo wewe."
\v 40 Akawaendea wanafunzi na akawakuta wamelala usingizi, na akamwambia Petro, "Kwa nini hamkuweza kukesha nami kwa saa moja?
\v 41 Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
\s5
\v 42 Akaenda zake mara ya pili na kuomba, akasema, "Baba yangu, kama jambo hili haliwezi kuepukika na ni lazima nikinywee kikombe hiki, mapenzi yako yatimizwe."
\v 43 Akarudi tena na kuwakuta wamelala usingizi, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito.
\v 44 Kisha akawaacha tena akaenda zake. Akaomba mara ya tatu akisema maneno yaleyale.
\s5
\v 45 Baadaye Yesu aliwaendea wanafunzi wake na kuwaambia, "Bado mmelala tu na kujipumzisha? Tazameni, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
\v 46 Amkeni, tuondoke. Tazama, yule anaye nisaliti amekaribia."
\s5
\v 47 Wakati alipokuwa bado anaongea, Yuda mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Kundi kubwa lilifika pamoja naye likitokea kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu. Walikuja na mapanga na marungu.
\v 48 Tena mtu aliyekusudia kumsaliti Yesu alikuwa amewapa ishara, akisema, "Yule nitakayembusu, ndiye yeye. Mkamateni."
\s5
\v 49 Mara hiyo alikuja kwa Yesu na kusema, "Salamu, Mwalimu!" Na akambusu.
\v 50 Yesu akamwambia, "Rafiki, lifanye lile ambalo limekuleta." Ndipo wakaja, na kumnyooshea mikono Yesu, na kumkamata.
\s5
\v 51 Tazama, mtu mmoja aliyekuwa pamoja na Yesu, alinyosha mkono wake, akachomoa upanga wake, na akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, na kumkata sikio lake.
\v 52 Ndipo Yesu akamwambia, rudisha upanga wako pale ulipoutoa, kwa kuwa wote watumiao upanga wataangamizwa kwa upanga.
\v 53 Mnadhani kuwa siwezi kumwita Baba yangu, naye akanitumia majeshi zaidi ya kumi na mawili ya malaika?
\v 54 Lakini basi jinsi gani maandiko yangeweza kutimizwa, hivi ndivyo inapasa kutokea?"
\s5
\v 55 Wakati huo Yesu akauambia umati, "Je! Mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi? Kila siku nilikaa hekaluni nikifundisha, na hamkunishika!
\v 56 Lakini yote haya yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie." Ndipo wanafunzi wake wakamwacha na kukimbia.
\s5
\v 57 Wale waliomkamata Yesu alimpeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, mahali ambapo waandishi na wazee walikuwa wamekusanyika pamoja.
\v 58 Lakini Petro alimfuata nyuma kwa mbali hadi katika ukumbi wa Kuhani Mkuu. Aliingia ndani na kukaa pamoja na walinzi aone kitakachotokea.
\s5
\v 59 Basi wakuu wa makuhani na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu, kusudi wapate kumuua.
\v 60 Ingawa walijitokeza mashahidi wengi, Lakini hawakupata sababu yoyote. Lakini baadaye mashahidi wawili walijitokeza mbele
\v 61 na kusema, " Mtu huyu alisema, ''Naweza kulivunja hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu."'
\s5
\v 62 Kuhani Mkuu alisimama na kumwuliza, "Hauwezi kujibu? Hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?"
\v 63 Lakini Yesu alikaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, "Kama Mungu aishivyo, nakuamuru utwambie, kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu."
\v 64 Yesu akamjibu, "Wewe mwenyewe umesema jambo hilo. Lakini nakuambia, toka sasa na kuendelea utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wenye Nguvu, na akija katika mawingu ya mbinguni."
\s5
\v 65 Ndipo Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake na kusema, "Amekufuru! Je, twahitaji tena ushahidi wa nini? Angalia, tayari mmesikia akikufuru.
\v 66 Je! Mnawaza nini? Wakajibu na kusema, "Anastahili kifo."
\s5
\v 67 Kisha walimtemea mate usoni na kumpiga ngumi, na kumchapa makofi kwa mikono yao,
\v 68 na kusema, "Tutabirie, wewe Kristo. Ni nani amekuchapa?"
\s5
\v 69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa nje katika ukumbi, na mtumishi wa kike alimwendea na kusema, "Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."
\v 70 Lakini alikana mbele yao wote, akisema, Sijui kitu unachosema."
\s5
\v 71 Alipoenda nje ya lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona na kuwaambia waliokuwepo hapo, "Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti."
\v 72 Akakana tena kwa kiapo, "Mimi simjui mtu huyu."
\s5
\v 73 Muda mfupi baadaye, wale waliokuwa wamesimama karibu, walimwendea na kusema na Petro, "Kwa hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa kuwa hata lafudhi yako inaonesha."
\v 74 Ndipo alianza kulaani na kuapa, "Mimi simfahamu mtu huyu," na mara hiyo jogoo akawika.
\v 75 Petro alikumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, "Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu."
\s5
\c 27
\p
\v 1 Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.
\v 2 Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.
\s5
\v 3 Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,
\v 4 na akasema, "Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia." Lakini wakajibu, "Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe."
\v 5 Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.
\s5
\v 6 Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, "Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu."
\v 7 Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
\v 8 Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, "Shamba la damu" hadi leo hii.
\s5
\v 9 Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, "Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,
\v 10 na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza."
\s5
\v 11 Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, "Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu alimjibu, "Wewe wasema hivyo."
\v 12 Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.
\v 13 Kisha Pilato alimwambia, "Hujayasikia mashitaka yote dhidi yako?"
\v 14 Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao.
\s5
\v 15 Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.
\v 16 Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.
\s5
\v 17 Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, "Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?" Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?"
\v 18 Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
\v 19 Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, "Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake."
\s5
\v 20 Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.
\v 21 Liwali aliwauliza, "Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?" Walisema, "Baraba."
\v 22 Pilato akawaambia, "Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?" Wote wakajibu, "Msulibishe"
\s5
\v 23 Naye akasema, "Kwa nini, ni kosa gani ametenda?" Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, "Msulibishe."
\v 24 Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, "Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe."
\s5
\v 25 Watu wote wakasema, "Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu."
\v 26 Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.
\s5
\v 27 Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika.
\v 28 Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.
\v 29 Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, "Salamu, Mfalme wa Wayahudi?"
\s5
\v 30 Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.
\v 31 Wakati walipokuwa wakimkejeri, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.
\s5
\v 32 Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.
\v 33 Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, "Eneo la fuvu la Kichwa."
\v 34 Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.
\s5
\v 35 Wakati walipokuwa wamemsulibisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.
\v 36 Na waliketi na kumwangalia.
\v 37 Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, "Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi."
\s5
\v 38 Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.
\v 39 Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao
\v 40 na kusema, "Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!"
\s5
\v 41 Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,
\v 42 "Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.
\s5
\v 43 Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'"
\v 44 Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.
\s5
\v 45 Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
\v 46 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, "Eloi, Eloi, lama thabakithan?" akimaanisha, "Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?"
\v 47 Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, "Anamwita Eliya."
\s5
\v 48 Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.
\v 49 Nao waliosalia wakasema, "Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa."
\v 50 Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.
\s5
\v 51 Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
\v 52 Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.
\v 53 Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.
\s5
\v 54 Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, "Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu."
\v 55 Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.
\v 56 Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo
\s5
\v 57 Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
\v 58 Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.
\s5
\v 59 Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na nguo ya sufi safi,
\v 60 na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
\v 61 Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.
\s5
\v 62 Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.
\v 63 Wakamwambia, "Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, 'Baada ya siku tatu atafufuka tena.'
\v 64 Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.' Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza."
\s5
\v 65 Pilato akawaambia, "Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo."
\v 66 Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi.
\v 2 Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.
\s5
\v 3 Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
\v 4 Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.
\s5
\v 5 Yule malaika akawafafanulia wale wananawake akisema, "msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulibiwa.
\v 6 Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala.
\v 7 Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, 'Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.' Tazama mimi nimewaambia."
\s5
\v 8 Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.
\v 9 Tazama Yesu akakutana nao na kusema, "Salamu."wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu.
\v 10 Kisha Yesu akawaambia, "msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.
\s5
\v 11 Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea.
\v 12 Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari
\v 13 na kuwaambia, "Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.'
\s5
\v 14 Kama taarifa hii itamfikia liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote."
\v 15 Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.
\s5
\v 16 Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza.
\v 17 Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka.
\s5
\v 18 Yesu akaja kwao akawambia akisema, "Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni.
\v 19 Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.
\s5
\v 20 Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.