sw_ulb_rev/67-REV.usfm

839 lines
62 KiB
Plaintext

\id REV
\ide UTF-8
\h Ufunuo
\toc1 Ufunuo
\toc2 Ufunuo
\toc3 rev
\mt Ufunuo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana.
\v 2 Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo.
\v 3 Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia.
\s5
\v 4 Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
\v 5 na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mtawala wa wafalme wa dunia hii. Kwake yeye atupendaye na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake,
\v 6 ametufanya kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba yake - kwake kuwa utukufu na nguvu milele daima. Amina.
\s5
\v 7 Tazama, anakuja na mawingu; kila jicho litamwona, pamoja na wote waliomchoma. Na kabila zote za dunia wataomboleza kwake. Ndiyo, Amina.
\v 8 "Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu, "Yeye aliyepo, na aliyekuwepo, na ambaye anakuja, Mwenye nguvu."
\s5
\v 9 Mimi, Yohana - ndugu yenu na mmoja anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu; nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patimo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda kuhusu Yesu.
\v 10 Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana. Nilisikia nyuma yangu sauti ya juu kama ya tarumbeta,
\v 11 ikisema, "andika katika kitabu unayo yaona, na uyatume kwa makanisa saba, kwenda Efeso, kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia."
\s5
\v 12 Nikageuka kuona ni sauti ya nani aliyekuwa akiongea nami, na nilipogeuka niliona kinara cha dhahabu cha taa saba.
\v 13 Katikati ya kinara cha taa alikuwemo mmoja kama Mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu iliyofika chini ya miguu yake, na mkanda wa dhababu kuzunguka kifua chake.
\s5
\v 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji, na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto.
\v 15 Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi.
\v 16 Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kutoka kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa uking'aa kama mwanga mkali wa jua.
\s5
\v 17 Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, "Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho,
\v 18 na ambaye ninaishi. Nalikuwa nimekufa, lakini tazama, ninaishi milele! Na ninazo funguo za mauti na kuzimu.
\s5
\v 19 Kwa hiyo, yaandike uliyoyaona, yaliyopo sasa, na yale yatakayotokea baada ya haya.
\v 20 Kwa maana iliyojificha kuhusu nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na kile kinara cha dhahabu cha taa saba: nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na kinara cha taa saba ni yale makanisa saba."
\s5
\c 2
\p
\v 1 "Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, "
\v 2 '"Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.
\s5
\v 3 Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado.
\v 4 Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza.
\v 5 Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.
\s5
\v 6 Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia.
\v 7 Kama una sikio, sikiliza yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.'
\s5
\v 8 "Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: 'Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena:
\v 9 '"Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).
\s5
\v 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima.
\v 11 Kama una sikio, sikiliza Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.'
\s5
\v 12 "Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: 'Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
\v 13 '"Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.
\s5
\v 14 Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu na kuzini.
\v 15 Katika hali iyo hiyo, hata wewe unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.
\s5
\v 16 Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu.
\v 17 Kama una sikio, sikiliza Roho anachowaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu ya jiwe, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.'
\s5
\v 18 "Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: "Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana:
\v 19 '"Najua ambacho umefanya - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.
\s5
\v 20 Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita mwenyewe nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.
\v 21 Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.
\s5
\v 22 Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu kwa alichofanya.
\v 23 Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na tamaa. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.
\s5
\v 24 Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, 'sitaweka juu yenu mzigo wowote.'
\v 25 Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.
\s5
\v 26 Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa.
\v 27 'Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.'
\v 28 Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi.
\v 29 Ukiwa na sikio, sikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.'
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa malaika wa kanisa la Sardi andika: 'Maneno ya yule anayeshikilia zile roho saba za Mungu na nyota saba. "Najua ambacho umefanya. Una sifa ya kuwa hai, lakini u-mfu.
\v 2 Amka na kuimarisha yaliyosalia, lakini yako karibu kufa, kwa sababu sikuyaona matendo yako yamekamilika machoni pa Mungu wangu.
\s5
\v 3 Kwa hiyo, kumbuka, yale uliyoyapokea na kusikia. Yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwivi, na hutajua saa ipi nitakayokuja juu yako.
\v 4 Lakini kuna majina machache ya watu katika Sardi ambao hawakuchafua nguo zao. Watatembea pamoja nami, wamevaa nguo nyeupe, kwa sababu wanastahili.
\s5
\v 5 Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe, na kamwe sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, na nitalitaja jina lake mbele ya Baba yangu, na mbele ya malaika.
\v 6 Ukiwa na sikio, sikiliza Roho ayaambiavyo makanisa."
\s5
\v 7 "Kwa malaika wa kanisa la Philadefia andika: Maneno ya aliye mtakatifu na kweli - aliye na funguo za Daudi, hufungua na hakuna afungaye, hufunga na hakuna awezaye kufungua.
\v 8 Najua ambacho umetenda. Tazama, nimekuwekea mbele yako mlango uliofunguliwa ambao hakuna awezaye kuufunga. Najua unazo nguvu kidogo, lakini umelitii neno langu na hujalikana jina langu.
\s5
\v 9 Angalia! Wote walio wa sinagogi la shetani, wale wasemao wao ni Wayahudi na kumbe siyo, badala yake wanadanganya. Nitawafanya waje na kusujudu mbele ya miguu yako, na watajua ya kuwa nilikupenda.
\v 10 Kwa kuwa umetunza amri yangu kwa uvumilivu wa uthabiti, nitakulinda pia katika saa yako ya kujaribiwa ambayo inakuja katika ulimwengu wote, kuwajaribu wale wote wanaoishi katika nchi.
\v 11 Naja upesi. Shikilia sana kile ulichonacho ili asiwepo mtu wa kuitwaa taji yako.
\s5
\v 12 Nitamfanya yeye ashindaye kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka nje kamwe. Nitaliandika kwake jina la Mungu wangu, jina la mji wa Mungu wangu (Yerusalemu mpya, ushukao chini toka mbinguni kwa Mungu wangu), na jina langu jipya.
\v 13 Yeye aliye na sikio, na asikie ambacho Roho anasema kwa makanisa.'
\s5
\v 14 "Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika: 'Maneno yake aliye Amina, wakutegemewa na shahidi mwaminifu, mtawala juu ya uumbaji wa Mungu.
\v 15 Najua ambacho umefanya, na kwamba wewe si baridi wala moto, natamani kwamba ungekuwa wa baridi au moto!
\v 16 Hivyo, kwa sababu wewe ni vuguvugu, si moto wala baridi, nitakutapika utoke kinywani mwangu.
\s5
\v 17 Kwa kuwa unasema, "Mimi ni tajiri, nimekuwa na mali nyingi, na sihitaji chochote." Lakini hujui kwamba wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi.
\v 18 Sikiliza ushauri kwangu: Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri, na nguo nyeupe za kumetameta ili ujivike mwenyewe na usioneshe aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka katika macho yako upate kuona.
\s5
\v 19 Kila nimpendaye, namwelekeza na kuwafundisha namna iwapasavyo kuishi; kwa hiyo, kuwa mkweli na kutubu.
\v 20 Tazama nasimama katika mlango na kubisha. Yeyote asikiaye sauti yangu na kufungua mlango, nitakuja na kuingia nyumbani kwake, na kula chakula naye na yeye pamoja nami.
\s5
\v 21 Yeye ashindaye, nitampa haki ya kukaa chini pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na kukaa chini pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi.
\v 22 Yeye aliye na sikio, na asikilize ambacho Roho ayaambia makanisa."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Baada ya mambo haya nilitazama, nikaona kuwa mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni. Ile sauti ya kwanza, ikizungumza nami kama tarumbeta, ikisema, "Njoo hapa, nitakuonesha yatakayotokea baada ya mambo haya."
\v 2 Mara moja nilikuwa katika Roho, niliona kulikuwa na kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mtu amekikalia.
\v 3 Mmoja aliyekuwa amekikalia alionekana kama jiwe la yaspi na akiki. Kulikuwa na upinde wa mvua umekizunguka kiti cha enzi. Upinde wa mvua ulionekana kama zumaridi.
\s5
\v 4 Kukizunguka kiti cha enzi kulikuwa na viti vya enzi vingine ishirini na vinne, na waliokaa kwenye viti vya enzi walikuwa wazee ishirini na wanne, wamevikwa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao.
\v 5 Kutoka katika kiti cha enzi kulitoka miale ya radi, muungurumo na radi. Taa saba zilikuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi, taa ambazo ni roho saba za Mungu.
\s5
\v 6 Tena mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na bahari, iliyowazi kama kioo. Wote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa na wenye uhai wanne, waliojaa macho mbele na nyuma.
\s5
\v 7 Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, kiumbe wa pili mwenye uhai alikuwa kama ndama, kiumbe wa tatu mwenye uhai alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na yule mwenye uhai wa nne alikuwa kama tai apaaye.
\v 8 Viumbe wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita, wamejaa macho juu na chini yake. Usiku na mchana hawakomi kusema, "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, mtawala juu ya wote, aliyekuwepo, na aliyepo na atakayekuja."
\s5
\v 9 Kila wakati viumbe wenye uhai walipotoa utukufu, heshima, na kushukuru mbele za aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele na daima,
\v 10 wazee ishirini na wanne walisujudu wenyewe mbele yake aliyekikalia kiti cha enzi. Waliinama chini kwake aishiye milele na daima na kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema,
\v 11 "Wastahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Kwa kuwa uliviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako, vilikuwepo na viliumbwa."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyekuwa amekaa katika kiti cha enzi, gombo lililoandikwa mbele na nyuma, na lilikuwa limetiwa mihuri saba.
\v 2 Nilimwona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kubwa, "Nani astahiliye kulifungua gombo na kuzivunja mihuri yake?"
\s5
\v 3 Hakuna mtu mbinguni au duniani au chini ya dunia aliyeweza kulifungua gombo au kulisoma.
\v 4 Nililia kwa uchungu kwa kuwa hakupatikana yeyote aliyestahili kulifungua gombo au kulisoma.
\v 5 Lakini mmoja wa wazee akaniambia, "Usilie. Tazama! Simba wa kabila ya Yuda, shina la Daudi, ameshinda, na anaweza kulifungua gombo na mihuri yake saba."
\s5
\v 6 Kati ya kiti cha enzi na wenye uhai wanne na miongoni mwa wazee, niliona mwanakondoo amesimama, akionekana kama aliye uawa. Alikuwa na pembe saba na macho saba - hizi ni roho saba za Mungu zilizotumwa duniani kote.
\v 7 Akaenda akalichukua gombo kutoka katika mkono wa kuume wa yule aliye kaa katika kiti cha enzi.
\s5
\v 8 Alipolichukua gombo, wenye uhai wanne na wazee ishirini na wanne wakainama hadi nchi mbele ya mwanakondoo. Kila mmoja alikuwa na kinubi na bakuli ya dhahabu iliyojaa uvumba ambayo ni maombi ya waamini.
\s5
\v 9 Waliimba wimbo mpya: "Unastahili kulitwaa gombo na kuzifungua muhuri zake. Kwa kuwa ulichinjwa, na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu wa kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
\v 10 Ukawafanya ufalme na makuhani kwa ajili ya kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala juu ya nchi."
\s5
\v 11 Kisha nilitazama na nikasikia sauti ya malaika wengi kuzunguka kiti cha enzi - idadi yao ilikuwa 200, 000, 000 na wenye uhai na wazee.
\v 12 Wakasema kwa sauti kuu, "Astahili mwanakondoo ambaye amechinjwa kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na sifa."
\s5
\v 13 Nikasikia kila kilichoumbwa kilichokuwa mbinguni na duniani na chini ya nchi na juu ya bahari, kila kitu ndani yake kikisema, "Kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na kwa mwanakondoo, kuwe sifa, heshima, utukufu na nguvu ya kutawala milele na milele."
\v 14 Wenye uhai wanne wakasema, "Amina!" na wazee wakainama chini na kuabudu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Nikatazama wakati mwanakondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema kwa sauti iliyofanana na radi, "Njoo!"
\v 2 Nikatazama na palikuwa na farasi mweupe! Aliyempanda alikuwa na bakuli, na akapewa taji. Alitokea kama mshindi ashindaye ili ashinde.
\s5
\v 3 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri wa pili, nikasikia mwenye uhai wa pili akisema, "Njoo!"
\v 4 Kisha farasi mwingine akatokea - mwekundu kama moto. Aliye mpanda alipewa ruhusa ya kuondoa amani duniani, ili kwamba watu wachinjane. Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa.
\s5
\v 5 Wakati mwanakondoo alipofungua ule muhuri wa tatu, nikasikia mwenye uhai wa tatu akisema, "Njoo!" Nikaona farasi mweusi, na aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
\v 6 Nikasikia sauti iliyoonekana kuwa ya mmoja wa wale wenye uhai ikisema, "kibaba cha ngano kwa dinari moja na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiyadhuru mafuta na divai."
\s5
\v 7 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya nne, nilisikia sauti ya mwenye uhai wa nne ikisema, "Njoo!"
\v 8 Kisha nikaona farasi wa kijivu. Aliye mpanda aliitwa jina lake mauti, na kuzimu ilikuwa ikimfuata. Walipewa mamlaka juu ya robo ya nchi, kuua kwa upanga, kwa njaa na kwa ugonjwa, na kwa wanyama wa mwitu katika nchi.
\s5
\v 9 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya tano, niliona chini ya madhabahu roho za wale waliokuwa wameuawa kwa sababu ya neno la Mungu na kutokana na ushuhuda walioushika kwa uthabiti.
\v 10 Wakalia kwa sauti kuu, "mpaka lini, Mtawala wa vyote, mtakatifu na mkweli, utahukumu wakaao juu ya nchi, na kulipiza kisasi damu yetu?"
\v 11 Kisha kila mmoja alipewa kanzu nyeupe na wakaambiwa kuwa wanapaswa kusubiri kidogo hata itakapotimia hesabu kamili ya watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume itakapotimia ambao watauawa, kama vile ambavyo wao waliuawa.
\s5
\v 12 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya sita, nilitazama na palikuwa na tetemeko kuu. Jua likawa jeusi kama gunia la singa, na mwezi mzima ukawa kama damu.
\v 13 Nyota za mbinguni zikaanguka katika nchi, kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga.
\v 14 Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa. Kila mlima na kisiwa vilihamishwa mahali pake.
\s5
\v 15 Kisha wafalme wa nchi na watu maarufu na majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mmoja aliye mtumwa na huru, wakajificha katika mapango na katika miamba ya milima.
\v 16 Wakaiambia milima na miamba, "Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo.
\v 17 Kwa kuwa siku kuu ya gadhabu yao imewadia, na ni nani awezaye kusimama?"
\s5
\c 7
\p
\v 1 Baada ya haya niliona malaika wanne wamesimama kwenye kona nne za dunia, wamezuia pepo nne za nchi kwa nguvu ili kwamba pasiwe na upepo unaovuma katika nchi, juu ya bahari au dhidi ya mti wowote.
\v 2 Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari:
\v 3 "Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu."
\s5
\v 4 Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144, 000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel:
\v 5 12, 000 kutoka katika kabila ya Yuda walitiwa muhuri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Rubeni, 12, 000 kutoka katika kabila ya Gadi.
\v 6 12, 000 kutoka katika kabila ya Asheri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Naftali, 12, 000 kutoka katika kabila ya Manase.
\s5
\v 7 12, 000 kutoka kabila ya Simioni, 12, 000 kutoka kabila ya Lawi, 12, 000 kutoka kabila ya Isakari,
\v 8 12, 000 kutoka kabila ya Zebuloni, 12, 000 kutoka kabila ya Yusufu, na 12, 000 kutoka kabila ya Benyamini walitiwa muhuri.
\s5
\v 9 Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao,
\v 10 na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: "Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!"
\s5
\v 11 Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu,
\v 12 wakisema, "Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!"
\s5
\v 13 Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, "hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi?
\v 14 Nikamwambia, "Bwana mkubwa, unajua wewe," na akaniambia, "Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.
\s5
\v 15 Kwa sababu hii, wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanamwabudu yeye usiku na mchana katika hekalu lake. Yeye aliye keti juu ya kiti cha enzi atasambaza hema yake juu yao.
\v 16 Hawataona njaa tena, wala kiu tena. Jua halitawachoma, wala joto la kuunguza.
\v 17 Kwa kuwa Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, na atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima, na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati Mwanakondoo alipofungua muhuri ya saba, kukawa na ukimya mbinguni takribani nusu saa.
\v 2 Kisha nikaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, na wakapewa tarumbeta saba.
\s5
\v 3 Malaika mwingine akaja, ameshikilia bakuli ya dhahabu yenye uvumba, amesimama madhabahuni. Akapewa uvumba mwingi ili kwamba autoe pamoja na maombi ya waamini wote katika madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi.
\v 4 Moshi wa ule uvumba, pamoja na maombi ya waamini, ukapanda juu mbele za Mungu kutoka mkononi mwa malaika.
\v 5 Malaika akatwaa bakuli la uvumba na akalijaza moto kutoka kwenye madhabahu. Kisha akalitupa chini juu ya nchi, na kukatokea sauti za radi, miale ya radi na tetemeko la nchi.
\s5
\v 6 Wale malaika saba ambao walikuwa na tarumbeta saba wakawa tayari kuzipiga.
\v 7 Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, na kukatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyikana na damu. Vikatupwa chini katika nchi ili kwamba theluthi yake iungue, theluthi ya miti ikaungua na nyasi zote za kijani zikaungua.
\s5
\v 8 Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake, na kitu kama mlima mkubwa uliokuwa unaungua kwa moto ukatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu,
\v 9 theluthi ya viumbe hai katika bahari vikafa, na theluthi ya meli zikaharibiwa.
\s5
\v 10 Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ikimulika kama kurunzi, juu ya theluthi ya mito na chemichemi za maji.
\v 11 Jina la nyota ni pakanga. Theluthi ya maji ikawa pakanga, na watu wengi wakafa kutokana na maji yaliyokuwa machungu.
\s5
\v 12 Malaika wa nne alipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua ikapigwa, pamoja na theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota. Kwa hiyo theluthi ya vyote ikageuka kuwa giza; theluthi ya mchana na theluthi ya usiku havikuwa na mwanga.
\s5
\v 13 Nilitazama, na nikasikia tai aliye kuwa anaruka katikati ya anga, akiita kwa sauti kuu, "Ole, ole, ole, kwa wale wakaao katika nchi, kwa sababu ya mlipuko wa tarumbeta iliyosalia ambayo imekaribia kupigwa na malaika watatu."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha malaika wa tano alipiga tarumbeta yake. Niliona nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka kwenye dunia. Nyota ilipewa ufunguo wa shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho.
\v 2 Alifungua shimo lisilo na kikomo, na moshi ukapanda juu kwa safu kutoka ndani ya shimo kama moshi kutoka katika tanuru kubwa. Jua na anga vilibadilika vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka shimoni.
\s5
\v 3 Ndani ya moshi nzige walitoka kuja juu ya dunia, nao walipewa nguvu kama ile ya nge juu ya dunia.
\v 4 Waliambiwa kutokudhuru majani katika nchi au mmea wowote wa kijani au mti, isipokuwa tu watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu katika paji za nyuso zao.
\s5
\v 5 Hawakupewa ruhusa ya kuwaua hao watu, bali kuwatesa tu kwa miezi mitano. Uchungu wao ulikuwa kama ule wa kuumwa na nge amwumapo mtu.
\v 6 Katika siku hizo watu watatafuta kifo, lakini hawatakipata. Watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.
\s5
\v 7 Nzige walifanana na farasi walioandaliwa kwa vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji ya dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
\v 8 Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba.
\v 9 Walikuwa na vifua kama vifua vya chuma na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari mengi ya vita na farasi wakimbiao kwenda vitani.
\s5
\v 10 Walikuwa na mikia inayouma kama nge; katika mikia yao walikuwa na nguvu ya kudhuru watu kwa miezi mitano.
\v 11 Walikuwa naye kama mfalme juu yao malaika wa shimo lisilokuwa na mwisho. Jina lake katika Kiebrania ni Abadoni, na katika Kiyunani ana jina Apolioni.
\v 12 Ole ya kwanza imepita. Angalia! Baada ya hili kuna maafa mawili yaja.
\s5
\v 13 Malaika wa sita alipiga tarumbeta yake, na nikasikia sauti ikitoka katika pembe ya madhabahu ya dhahabu ambayo iko mbele za Mungu.
\v 14 Sauti ilimwambia malaika wa sita aliyekuwa na tarumbeta, "Waachie malaika wanne ambao wamefungwa katika mto mkubwa Efrata."
\v 15 Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa kwa saa hiyo maalumu, siku hiyo, mwezi huo, na mwaka huo, waliachiwa wawaue theluthi ya wanadamu.
\s5
\v 16 Idadi ya maaskari waliokuwa juu ya farasi ilikuwa 200, 000, 000. Nilisikia idadi yao.
\v 17 Hivi ndivyo nilivyoona farasi katika maono yangu na wale waliopanda juu yao: Vifua vyao vilikuwa vyekundu kama moto, bluu iliyoiva na njano isiyoiva. Vichwa vya farasi vilifanana na vichwa vya simba, na midomoni mwao ulitoka moto, moshi na salfa.
\s5
\v 18 Theluthi ya wanadamu waliuawa na haya mapigo matatu: moto, moshi, na salfa iliyotoka katika midomo yao.
\v 19 Kwa kuwa nguvu ya farasi ilikuwa katika midomo yao na katika mikia yao—kwa kuwa mikia yao ilikuwa kama nyoka, na walikuwa na vichwa ambavyo walitumia kuwatia majeraha wanadamu.
\s5
\v 20 Watu waliobaki, wale ambao walikuwa hawajauawa na mapigo haya, hawakutubia matendo yao waliyokuwa wamefanya, wala hawakuacha kuabudu mapepo na miungu ya dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti—vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia au kutembea.
\v 21 Wala hawakutubia uuaji wao, uchawi wao, uasherati wao au njia zao za wizi.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kisha nikaona malaika mwingine mkuu akishuka chini kutoka mbinguni. Alikuwa amefungwa katika wingu, na kulikuwa na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake ulikuwa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto.
\v 2 Alishikilia gombo dogo katika mkono wake lililokuwa limefunuliwa, naye aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari na mguu wake wa kushoto juu ya nchi kavu.
\s5
\v 3 Kisha alipaza sauti ya juu kama simba aungurumapo, na wakati alipopaza sauti radi saba ziliunguruma.
\v 4 Wakati radi saba zilipounguruma, nilikuwa nakaribia kuandika, lakini nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Tunza iwe siri kile ambacho radi saba zimesema. Usiiandike."
\s5
\v 5 Kisha malaika niliyemwona amesimama juu ya bahari na nchi kavu, aliinua mkono wake juu mbinguni
\v 6 na kuapa kwa yule aishiye milele na milele —aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo, na bahari na vyote vilivyomo: "Hakutakuwepo kuchelewa tena.
\v 7 Lakini katika siku ile, wakati malaika wa saba atakapokaribia kupiga tarumbeta yake, ndipo siri ya Mungu itakuwa imetimizwa, kama alivyotangaza kwa watumishi wake manabii."
\s5
\v 8 Sauti niliyosikia kutoka mbinguni iliniambia tena: "Nenda, chukua gombo dogo lililofunuliwa ambalo kiko katika mkono wa malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu."
\v 9 Kisha nilikwenda kwa malaika na kumwambia anipe gombo dogo. Aliniambia, "Chukua gombo na ule. Litalifanya tumbo lako liwe na uchungu, lakini katika mdomo wako litakuwa tamu kama asali."
\s5
\v 10 Nilichukua gombo dogo kutoka mkononi mwa malaika na kulila. Lilikuwa kitamu kama asali katika mdomo wangu, lakini baada ya kula, tumbo langu lilikuwa na uchungu.
\v 11 Kisha baadhi ya sauti ziliniambia, "Unapaswa kutabiri tena kuhusu watu wengi, mataifa, lugha, na wafalme."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Nilipewa mwanzi wa kutumia kama fimbo ya kupimia. Niliambiwa, "Ondoka na ukapime hekalu la Mungu na madhabahu, na wale wanaoabudu ndani yake.
\v 2 Lakini usipime eneo la ua wa nje ya hekalu, kwa kuwa wamepewa watu wa Mataifa. Wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
\s5
\v 3 Nitawapa mashahidi wangu wawili mamlaka ya kutabiri kwa muda wa siku 1, 260, wakiwa wamevaa magunia."
\v 4 Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili ambavyo vimesimama mbele ya Bwana wa dunia.
\v 5 Kama mtu yeyote ataamua kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao. Yeyote anayetaka kuwadhuru lazima auawe kwa njia hii.
\s5
\v 6 Hawa mashahidi wana uwezo wa kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe wakati wanatabiri. Wana nguvu ya kubadili maji kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo wakati wowote wakitaka.
\v 7 Wakati watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama anayetoka kwenye shimo lisilo na mwisho atafanya vita dhidi yao. Atawashinda na kuwaua.
\s5
\v 8 Miili yao italala katika mtaa wa mji mkuu (ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri) ambapo Bwana wao alisulubiwa.
\v 9 Kwa siku tatu na nusu baadhi kutoka katika jamaa za watu, kabila, lugha na kila taifa watatazama miili yao na hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi.
\s5
\v 10 Wale wanaoishi katika nchi watafurahi kwa ajili yao na kushangilia, hata kutumiana zawadi kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nchi.
\v 11 Lakini baada ya siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia nao watasimama kwa miguu yao. Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona.
\v 12 Kisha watasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, "Njoni huku!" Nao watakwenda juu mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakitazama.
\s5
\v 13 Katika saa hiyo kutakuwepo na tetemeko kuu la ardhi na moja ya kumi ya mji itaanguka. Watu elfu saba watauawa katika tetemeko na watakaobaki hai wataogopeshwa na kumpa utukufu Mungu wa mbinguni.
\v 14 Ole ya pili imepita. Angalia! Ole ya tatu inakuja upesi.
\s5
\v 15 Kisha malaika wa saba alipiga tarumbeta yake, na sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema, "Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake. Atatawala milele na milele."
\s5
\v 16 Kisha wazee ishirini na wanne waliokuwa wameketi kwenye viti vya enzi mbele ya Mungu walianguka wenyewe chini kwenye ardhi, nyuso zao zimeinama chini, nao walimwabudu Mungu.
\v 17 Walisema, "Twatoa shukrani zetu kwako, Bwana Mungu, mtawala juu ya vyote, ambaye upo na ambaye ulikuwepo, kwa sababu umetwaa nguvu yako kuu na kuanza kutawala.
\s5
\v 18 Mataifa walikasirika, lakini gadhabu yako imekuja. Wakati umefika kwa wafu kuhukumiwa na wewe kuwazawadia watumishi wako manabii, waamini na wale walio na hofu ya jina lako, wote wawili wasiofaa kitu na wenye nguvu. Na wakati wako umefika wa kuwaharibu wale ambao wamekuwa wakiiharibu dunia."
\s5
\v 19 Kisha hekalu la Mungu mbinguni lilifunuliwa na sanduku la agano lake lilionekana ndani ya hekalu lake. Kulikuwa na miali ya mwanga, kelele, ngurumo za radi, tetemeko la ardhi na mawe ya mvua.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ishara kuu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyefunikwa na jua, na akiwa na mwezi chini ya miguu yake; na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa juu ya kichwa chake.
\v 2 Alikuwa na mimba na alikuwa analia kwa ajili ya maumivu ya kuzaa—katika uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 3 Na ishara nyingine ilionekana mbinguni: Tazama! Kulikuwa na joka mwekundu mkubwa ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kulikuwa na taji saba kwenye vichwa vyake.
\v 4 Mkia wake ulikokota theluthi moja ya nyota mbinguni na kuzitupa chini duniani. Joka alisimama mbele ya mwanamke aliyekuwa anakaribia kuzaa, ili kwamba wakati anazaa, apate kummeza mtoto wake.
\s5
\v 5 Alimzaa mwana, mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Mtoto wake alinyakuliwa juu kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi,
\v 6 na mwanamke alikimbilia nyikani, mahali ambapo Mungu alikuwa ameandaa eneo kwa ajili yake, ili aweze kuhudumiwa kwa siku 1, 260.
\s5
\v 7 Sasa kulikuwa na vita mbinguni. Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka; naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana nao.
\v 8 Lakini joka hakuwa na nguvu za kutosha kushinda. Kwa hiyo haikuwepo tena nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika zake.
\v 9 Joka mkubwa—yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani ambaye hudanganya - dunia nzima akatupwa chini katika dunia, na malaika zake wakatupwa chini pamoja naye.
\s5
\v 10 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni: "Sasa wokovu umekuja, nguvu—na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini—ambaye aliwashitaki mbele za Mungu wetu mchana na usiku.
\s5
\v 11 Walimshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao, kwa maana hawakupenda sana maisha yao, hata kufa.
\v 12 Kwa hiyo, shangilieni, ninyi mbingu, na wote mnaokaa ndani yake. Lakini ole wa nchi na bahari kwa sababu mwovu ameshuka kwenu. Amejawa na hasira kali, kwa sababu anajua kwamba ana muda mchache tu.
\s5
\v 13 Wakati joka alipotambua kuwa ametupwa chini kwenye nchi, alimfuata mwanamke ambaye alikuwa amezaa mtoto wa kiume.
\v 14 Lakini mwanamke alipewa mabawa mawili ya tai mkubwa, ili kwamba aweze kuruka hadi kwenye eneo lililoandaliwa kwa ajili yake kule jangwani, eneo ambalo angeweza kutunzwa, kwa wakati, nyakati na nusu wakati-mahali asipoweza kupafikia huyo nyoka.
\s5
\v 15 Nyoka alimwaga maji kutoka mdomoni mwake kama mto, ili afanye gharika ya kumgharikisha.
\v 16 Lakini ardhi ilimsaidia mwanamke. Ilifunua kinywa chake na kuumeza mto alioutema joka kutoka kinywani mwake.
\v 17 Kisha joka akamkasirikia mwanamke naye aliondoka na kufanya vita na uzao wake wote—wale wanaotii amri za Mungu na kushikilia ushuhuda kuhusu Yesu.
\v 18 Kisha joka alisimama juu ya mchanga ufukwe wa bahari.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu.
\v 2 Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, na katika kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.
\s5
\v 3 Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama.
\v 4 Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, "Nani kama mnyama? na "Nani atapigana naye?"
\s5
\v 5 Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili.
\v 6 Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.
\s5
\v 7 Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa.
\v 8 Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.
\s5
\v 9 Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize.
\v 10 Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.
\s5
\v 11 Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka.
\v 12 Alionyesha mamlaka yote katika mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wakimuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.
\s5
\v 13 Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu,
\v 14 na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.
\s5
\v 15 Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe.
\v 16 Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso.
\v 17 Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.
\s5
\v 18 Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Nilitazama na nikaona Mwana Kondoo amesimama mbele yangu juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa 144, 000 wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
\v 2 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisikika kama ngurumo za maji mengi na sauti kubwa ya radi. Sauti niliyoisikia ni kama wapiga vinubi wapigao vinubi vyao.
\s5
\v 3 Wakiimba wimbo mpya mbele za kiti cha enzi na mbele za wenye uhai wanne na wazee. Hakuna hata mwenye uwezo wa kujifunza huo wimbo isipokuwa kwa 144, 000 ambao wamekombolewa kutoka duniani.
\v 4 Hawa ni wale ambao hawakujichafua wenyewe kwa wanawake, maana walijitunza wenyewe dhidi ya matendo ya zinaa. Ni hawa ambao walimfuata Mwana Kondoo popote alipoenda. Hawa walikombolewa kutoka kwa wanadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo.
\v 5 Hakuna uongo uliopatikana katika vinywa vyao; hawalaumiwi.
\s5
\v 6 Nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, ambaye mwenye ujumbe wa mbinguni wa habari njema kwa kuwatangazia wenye kuishi duniani kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu.
\v 7 Akawaita kwa sauti kuu, "Mwogopeni Mungu na mpeni utukufu. Kwa maana muda wa hukumu umekaribia. Mwabuduni yeye, yeye aliyeumba mbingu, na dunia, na bahari, na chemchemi za maji."
\s5
\v 8 Malaika mwingine - malaika wa pili - akafuata akisema, "Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu, ambaye uliwanywesha mataifa divai ya ukahaba, divai ambayo ilileta ghadhabu juu yake."
\s5
\v 9 Malaika mwingine - malaika wa tatu - aliwafuata, akasema kwa sauti kuu, "Yeyote atakayemwabudu huyo mnyama na sanamu yake, na kupokea alama katika paji lake la uso au mkononi,
\v 10 yeye pia atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu, divai ambayo imeandaliwa na kumwagwa bila kuchanganywa katika kikombe cha hasira yake. Mtu atakayekunywa atateswa kwa moto na moto wa kiberiti mbele za malaika zake watakatifu na mbele za Mwana Kondoo.
\s5
\v 11 Na moshi wa maumivu yao ukaenda milele na milele, na hawakuwa na mapumziko mchana au usiku - hao waabuduo mnyama na sanamu yake, na kila mtu aliyepokea alama ya jina lake.
\v 12 Huu ni wito wa subira na uvumilivu kwa waamini, wale ambao hutii amri za Mungu na imani katika Yesu."
\s5
\v 13 Nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Andika haya: Heri wafu wafao katika Bwana." "Ndiyo," asema Roho, "ili waweze kupumzika kutoka kwenye kazi zao, maana matendo yao yatawafuata."
\s5
\v 14 Nilitazama na nikaona kulikuwa na wingu jeupe, na aliyeketi kwenye wingu ni mmoja aliyekuwa na mfano wa Mwana wa Mtu. Alikuwa na taji ya dhahabu katika kichwa chake na mundu mkali katika mkono wake.
\v 15 Malaika mwingine tena alikuja kutoka kwenye hekalu na aliita kwa sauti kuu kwenda kwa yule aliyekaa katika wingu: "Chukua mundu wako na uanze kuvuna. Kwa kuwa muda wa mavuno umeshawadia, maana mavuno yaliyo katika dunia yameshaiva."
\v 16 Tena yule aliyekuwa kwenye wingu aliupitisha mundu wake juu ya dunia, na dunia ikavunwa.
\s5
\v 17 Na malaika mwingine akaja kutoka kwenye hekalu la mbinguni; naye alikuwa na mundu mkali.
\v 18 Na bado malaika mwingine akaja kutoka kwenye madhabahu, na malaika aliyekuwa na mamlaka juu ya moto. Akamwita kwa sauti kuu malaika ambaye alikuwa na mundu mkali, "Chukua mundu mkali na uyakusanye matawi ya mzabibu kutoka kwenye mzabibu wa nchi, kwa kuwa zabibu sasa zimeiva."
\s5
\v 19 Malaika alipeleka mundu wake katika dunia na alikusanya mavuno ya zabibu ya dunia na alirusha katika pipa kubwa la divai ya ghadhabu ya Mungu.
\v 20 Chujio la divai lilipondwapondwa nje ya mji na damu ikamwagika kutoka katika hicho kimo cha hatamu ya farasi, kwa stadia 1, 600.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Tena nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na yenye kushangaza; Kulikuwa na malaika saba wenye mapigo saba, ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho (katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika).
\s5
\v 2 Niliona kile kilichotokea kuwa bahari ya bilauri iliyochanganywa na moto, na ikasimama pembeni mwa bahari ambapo wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake, na juu ya namba inayowakilisha jina lake. Walikuwa wameshikilia vinubi walivyopewa na Mungu.
\s5
\v 3 Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo: "Kazi zako ni kubwa na zenye kushangaza, Bwana Mungu, utawalaye vyote. Mwaminifu na njia zako ni za kweli, Mfalme wa mataifa.
\v 4 Nani atashindwa kukuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu mbele zako kwa sababu u mwema na matendo yako yamejulikana."
\s5
\v 5 Baada ya mambo hayo nilitazama, na sehemu takatifu sana, ambapo palikuwa na hema ya ushuhuda, iliyofungukia mbinguni.
\v 6 Kutoka mahali patakatifu sana wakaja malaika saba wenye mapigo saba, wamevaa mavazi safi, kitani yenye kung'aa na mshipi wa dhahabu kuzunguka vifua vyao.
\s5
\v 7 Mmoja wa wale wenye uhai wanne akatoa kwa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu mwenye kuishi milele na milele.
\v 8 Mahali patakatifu sana kulijawa moshi kutoka kwenye utukufu wa Mungu na kutoka kwenye uwezo wake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nikasikia sauti kubwa ikiita kutoka kwenye sehemu ya patakatifu na ikasema kwa wale malaika saba, "Nenda na ukamwage juu ya dunia mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu."
\s5
\v 2 Malaika wa kwanza alienda na kumwaga bakuli lake katika dunia; majeraha mabaya na yenye maumivu makali yalikuja kwa watu wenye alama ya mnyama, kwa wale ambao waliabudu sanamu yake.
\s5
\v 3 Malaika wa pili alimwaga bakuli lake katika bahari; ikawa kama damu ya mtu aliyekufa, na kila kiumbe hai katika bahari kilikufa.
\s5
\v 4 Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na katika chemichemi za maji; zikawa damu.
\v 5 Nikasikia malaika wa maji akisema, "Wewe ni mwaminifu - mmoja uliyepo na uliyekuwako, Mtakatifu - kwa sababu umezileta hukumu hizi.
\v 6 Kwa sababu walimwaga damu za waamini na manabii, umewapa wao kunywa damu; ndicho wanachostahili."
\v 7 Nikasikia madhabahu ikijibu, "Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki."
\s5
\v 8 Malaika wa nne akamwaga kutoka kwenye bakuli lake juu ya jua, na likapewa ruhusa kuunguza watu kwa moto.
\v 9 Waliunguzwa kwa joto lenye kutisha, na wakalikufuru neno la Mungu, mwenye nguvu juu ya mapigo yote. Hawakutubu wala kumpa yeye utukufu.
\s5
\v 10 Malaika wa tano akamwaga kutoka kwenye bakuli lake katika kiti cha enzi cha mnyama, na giza likaufunika ufalme wake. Walisaga meno katika maumivu makali.
\v 11 Wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na majeraha yao, na bado waliendelea kutokutubu kwa kile walichotenda.
\s5
\v 12 Malaika wa sita alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika mto mkubwa, Frati, na maji yake yakakauka ili kuweza kuandaa njia kwa wafalme watakaokuja kutoka mashariki.
\v 13 Nikaona roho tatu chafu zilizoonekana kama chura watokao nje ya mdomo wa yule joka, yule mnyama, na yule nabii wa uongo.
\v 14 Ni roho za pepo zitendazo ishara na miujiza. Walikuwa wakienda kwa wafalme wa dunia yote ili kuweza kuwakusanya pamoja kwa vita katika siku kuu ya Mungu, mwenye kutawala juu ya vyote.
\s5
\v 15 ("Tazama! Ninakuja kama mwizi! Heri yule adumuye katika kukesha, atunzaye mavazi yake ili asiweze kwenda nje uchi na kuiona aibu yake.")
\v 16 Waliwaleta pamoja katika sehemu iliyoitwa katika kiebrania Amagedoni.
\s5
\v 17 Malaika wa saba alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika anga. Kisha sauti kuu ikasikika kutoka pakatifu na kutoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, "Imekwisha!"
\v 18 Kulikuwa na miale ya mwanga wa radi, ngurumo, vishindo vya radi, na tetemeko la kutisha - tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea duniani tangu wanadamu wamekuwepo duniani, hivyo ni tetemeko kubwa zaidi.
\v 19 Mji mkuu uligawanyika katika sehemu tatu, na miji ya mataifa ikaanguka. Kisha Mungu akamkumbusha Babeli mkuu, na akaupa mji huo kikombe kilichokuwa kimejaa divai kutoka kwenye ghadhabu yake iliyo kali.
\s5
\v 20 Kila kisiwa kikapotea na milima haikuonekana tena.
\v 21 Mvua kubwa ya mawe, ikiwa na uzito wa talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya watu, na wakamlaani Mungu kwa mapigo ya mvua ya mawe kwa sababu lile pigo lilikuwa baya sana.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, "Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi,
\v 2 ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa."
\s5
\v 3 Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
\v 4 Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake.
\v 5 Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: "BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI."
\s5
\v 6 Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu.
\v 7 Lakini malaika akaniambia, "Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).
\s5
\v 8 Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja.
\s5
\v 9 Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake.
\v 10 Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.
\s5
\v 11 Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na anaenda kwenye uharibifu.
\s5
\v 12 Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama.
\v 13 Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama.
\v 14 Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na katika yeye tuliitwa, tulichaguliwa, waaminifu."
\s5
\v 15 Malaika akaniambia, "Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.
\s5
\v 16 Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto.
\v 17 Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.
\s5
\v 18 Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya vitu hivi nilimwona malaika mwingine akishuka chini kutoka mbinguni. Yeye alikuwa na mamlaka kuu, na nchi iliangazwa kwa utukufu wake.
\v 2 Alilia kwa sauti kuu, akisema, "Umeanguka, umeanguka, ule mji mkuu Babeli! Umekuwa sehemu yakaapo mapepo, na sehemu ikaapo kila roho chafu, na sehemu akaapo kila mchafu na ndege achukizaye.
\v 3 Kwa kuwa mataifa yote yamekunywa mvinyo ya tamaa ya uasherati wake ambayo humletea ghadhabu. Wafalme wa nchi wamezini naye. Wafanyabiashara wa nchi wamekuwa matajiri kwa nguvu ya maisha yake ya anasa."
\s5
\v 4 Kisha nilisikia sauti nyingine kutoka mbinguni iikisema, "Tokeni kwake watu wangu, ili msije mkashiriki katika dhambi zake, na ili msije mkapokea mapigo yake yoyote.
\v 5 Dhambi zake zimerundikana juu kama mbingu, na Mungu ameyakumbuka matendo yake maovu.
\v 6 Mlipeni kama alivyowalipa wengine, na mkamlipe mara mbili kwa jinsi alivyotenda; katika kikombe alichokichanganya, mchanganyishieni mara mbili kwa ajili yake.
\s5
\v 7 Kama alivyojitukuza yeye mwenyewe, na aliishi kwa anasa, mpeni mateso mengi na huzuni. Kwa kuwa husema moyoni mwake, 'Nimekaa kama malkia; wala siyo mjane, na wala sitaona maombolezo.'
\v 8 Kwa hiyo ndani ya siku moja mapigo yake yatamlemea: kifo, maombolezo, na njaa. Atateketezwa kwa moto, kwa kuwa Bwana Mungu ni mwenye nguvu, na ni mhukumu wake."
\s5
\v 9 Wafalme wa nchi waliozini na kuchanganyikiwa pamoja naye watalia na kumwombolezea watakapouona moshi wa kuungua kwake.
\v 10 Watasimama mbali naye, kwa hofu ya maumivu yake wakisema, "Ole, ole kwa mji mkuu, Babeli, mji wenye nguvu! Kwa saa moja hukumu yako imekuja."
\s5
\v 11 Wafanyabiashara wa nchi lieni na kuomboleza kwa ajili yake, kwa kuwa hakuna hata mmoja anunuaye bidhaa zake tena -
\v 12 bidhaa za dhahabu, fedha, mawe ya thamani, lulu, kitani nzuri, zambarau, hariri, nyekundu, aina zote za miti ya harufu nzuri, kila chombo cha pembe za ndovu, kila chombo kilichotengenezwa kwa miti ya thamani, shaba, chuma, jiwe,
\v 13 mdalasini, viungo, uvumba, manemane, ubani, mvinyo, mafuta, unga mzuri, ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na watumwa, na roho za watu.
\s5
\v 14 Matunda uliyoyatamani kwa nguvu zako yameondoka kutoka kwako. Anasa zako zote na mapambo yametoweka, hayatapatikana tena.
\s5
\v 15 Wafanyabiashara wa vitu hivi waliopata utajiri kwa mapenzi yake watasimama mbali kutoka kwake kwa sababu ya hofu ya maumivu yake, wakilia na sauti ya maombolezo.
\v 16 Wakisema, "Ole, ole mji ule mkuu uliovikwa kitani nzuri, zambarau, na nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani na lulu!"
\v 17 Ndani ya saa moja utajiri wote huo ulitoweka. Kila nahodha wa meli, kila baharia, na wote wanamaji, na wote wafanyao kazi baharini, walisimama mbali.
\s5
\v 18 Walilia walipouona moshi wa kuungua kwake. Walisema, "Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa?"
\v 19 Walitupa mavumbi juu ya vichwa vyao, na walilia, wakitokwa machozi na kuomboleza, "Ole, ole mji mkubwa mahali wote waliokuwa na meli zao baharini walikuwa matajiri kutokana na mali zake. Ndani ya saa moja umeangamizwa."
\v 20 "Furahini juu yake, mbingu, ninyi waumini, mitume, na manabii, kwa maana Mungu ameleta hukumu yenu juu yake!"
\s5
\v 21 Malaika mwenye nguvu aliinua jiwe kama jiwe kuu la kusagia na alilitupa baharini, akisema, "Kwa njia hii, Babeli, ule mji mkuu, utatupwa chini kwa ukatili na hautaonekana tena.
\v 22 Sauti ya vinanda, wanamuziki, wacheza filimbi, na tarumbeta hawatasikika tena kwenu. Wala fundi wa aina yoyote hataonekana kwenu. Wala sauti ya kinu haitasikika tena kwenu.
\s5
\v 23 Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako. Sauti ya bwana harusi na bibi harusi hazitasikiwa tena ndani yako, maana wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, na wa mataifa, wamedanganywa kwa uchawi wako.
\v 24 Ndani yake damu ya manabii na waamini ilionekana, na damu ya wote waliouawa juu ya nchi."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Baada ya mambo haya nilisikia sauti kama ya mlio mkubwa wa kundi kubwa la watu mbinguni ikisema, "Haleluya. Wokovu, utukufu, na nguvu ni vya Mungu wetu.
\v 2 Hukumu zake ni kweli na za haki, kwa kuwa amemhukumu kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uzinzi wake. Amefanya kisasi kwa damu ya watumishi wake, ambayo aliimwaga yeye mwenyewe."
\s5
\v 3 Kwa mara ya pili walisema, "Haleluya! Moshi hutoka kwake milele na milele."
\v 4 Wale wazee ishirini na wanne na viumbe hai wanne wakasujudu na kumwabudu Mungu akaaye kwenye kiti cha enzi. Walikuwa wakisema, "Amina. Haleluya!"
\s5
\v 5 Ndipo sauti ilitoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, "Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha yeye, wote wasio na umuhimu na wenye nguvu."
\s5
\v 6 Ndipo nilisikia sauti kama sauti ya kundi kubwa la watu, kama sauti ya ngurumo ya maji mengi, na kama ngurumo ya radi, ikisema, "Haleluya! Bwana ni Mungu wetu, mtawala juu ya wote, hutawala.
\s5
\v 7 Na tushangilie na kufurahi na kumpa utukufu kwa sababu harusi na sherehe ya Mwana Kondoo imekuja, na bibi harusi yuko tayari."
\v 8 Aliruhusiwa kuvalishwa kitani safi na yenye kung'aa (kitani safi ni matendo ya haki ya waumini).
\s5
\v 9 Malaika akasema nami, "Yaandike haya: Wamebarikiwa walioalikwa kwenye sherehe ya harusi ya Mwana kondoo." Vilevile akaniambia, "Haya ni maneno ya kweli ya Mungu."
\v 10 Nilisujudu mbele ya miguu yake nikamwabudu, lakini akaniambia, "Usifanye hivi! Mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako mwenye kuushika ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu, kwa kuwa ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii."
\s5
\v 11 Kisha niliona mbingu zimefunguka, na tazama kulikuwa na farasi mweupe! Na yule aliyekuwa amempanda anaitwa Mwaminifu na wa Kweli. Huhukumu kwa haki na kufanya vita.
\v 12 Macho yake ni kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake ana taji nyingi. Ana jina lililoandikwa juu yake asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe.
\v 13 Amevaa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aliitwa Neno la Mungu.
\s5
\v 14 Majeshi ya mbinguni yalikuwa yakimfuata juu ya farasi weupe, walivalishwa kitani nzuri, nyeupe na safi.
\v 15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao huyaangamiza mataifa, naye atawatawala kwa fimbo ya chuma. Naye hukanyaga vyombo vya mvinyo kwa hasira kali ya Mungu, hutawala juu ya wote.
\v 16 Naye ameandikwa juu ya vazi lake na katika paja lake jina, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
\s5
\v 17 Niliona malaika amesimama katika jua. Aliwaita kwa sauti kuu ndege wote warukao juu, "Njoni, kusanyikeni pamoja kwenye chakula kikuu cha Mungu.
\v 18 Njoni mle nyama ya wafalme, nyama ya majemedari, nyama ya watu wakubwa, nyama ya farasi na wapanda farasi, na nyama ya watu wote, walio huru na watumwa, wasio na umuhimu na wenye nguvu."
\s5
\v 19 Nilimwona mnyama na wafalme wa nchi pamoja na majeshi yao. Walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kufanya vita na mmoja aliyepanda farasi na jeshi lake.
\v 20 Mnyama alikamatwa na nabii wake wa uongo aliyezifanya ishara katika uwepo wake. Kwa ishara hizi aliwadanganya wale walioipokea chapa ya mnyama na walioisujudia sanamu yake. Wote wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.
\s5
\v 21 Wale waliobaki waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa mmoja aliyepanda juu ya farasi. Ndege wote walikula mizoga ya miili yao.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kisha niliona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
\v 2 Alimshika yule joka, nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi au Shetani, na kumfunga miaka elfu.
\v 3 Alimtupa kwenye shimo lisilo na mwisho, akalifunga na kulitia mhuri juu yake. Hii ilikuwa hivyo ili kwamba asiwadanganye mataifa tena mpaka miaka elfu itakapoisha. Baada ya hapo, ataachiwa huru kwa muda mchache.
\s5
\v 4 Kisha niliona viti vya enzi. Waliokuwa wamevikalia ni wale ambao walikuwa wamepewa mamlaka ya kuhukumu. Vilevile niliona nafsi za wale ambao walikuwa wamekatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda kuhusu Yesu na kwa neno la Mungu. Walikuwa hawajamwabudu mnyama au sanamu yake, na walikataa kupokea alama juu ya paji za nyuso zao au mkono. Walikuja uzimani, na wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu.
\s5
\v 5 Wafu waliobaki hawakuja uzimani mpaka miaka elfu ilipokuwa imeisha. Huu ndio ufufuo wa kwanza.
\v 6 Mbarikiwa na mtakatifu ni mtu yeyote ambaye achukua nafasi katika ufufuo wa kwanza! Mauti ya pili haina nguvu juu ya watu kama hawa. Patakuwa na makuhani wa Mungu na wa Kristo na watatawala na yeye kwa miaka elfu.
\s5
\v 7 Wakati miaka elfu itakapofikia mwisho, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
\v 8 Atakwenda nje kuwadanganya mataifa katika kona nne za dunia -Gogu na Magogu - kuwaleta pamoja kwa ajili ya vita. Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari.
\s5
\v 9 Walikwenda juu kwenye tambarare ya nchi nao walizunguka kambi ya waumini, mji upendwao. Lakini moto ulikuja kutoka mbinguni na kuwaangamiza.
\v 10 Shetani, ambaye aliwadanganya, alitupwa ndani ya ziwa liwakalo kiberiti, ambamo mnyama na nabii wa uongo walikuwa wameshatupwa. Watateswa mchana na usiku milele na milele.
\s5
\v 11 Kisha niliona kiti cha enzi kikubwa cheupe na yule ambaye alikaa juu yake. Dunia na mbingu zilikimbia mbali kutoka katika uwepo wake, lakini hapakuwako nafasi ya wao kwenda.
\v 12 Niliwaona waliokufa - hodari na wasio wa muhimu wamesimama katika kiti cha enzi, na vitabu vilifunuliwa. Kisha kitabu kingine kilifunguliwa - Kitabu cha Uzima. Wafu walihukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya vitabu, matokeo ya kile walichokifanya.
\s5
\v 13 Bahari iliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake. Kifo na kuzimu viliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake, na wafu walihukumiwa kulingana na walichofanya.
\v 14 Kifo na kuzimu zilitupwa ndani ya ziwa la moto. Hii ni mauti ya pili - ziwa la moto.
\v 15 Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa ndani ya Kitabu cha Uzima, alitupwa ndani ya ziwa la moto.*
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimekwishapita, na bahari haikuwepo tena.
\v 2 Niliona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ambao ulikuja chini kutoka mbinguni kwa Mungu, ulioandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
\s5
\v 3 Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, "Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao.
\v 4 Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
\s5
\v 5 Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, "Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya." Alisema, "Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli."
\v 6 Aliniambia, "Mambo haya yalikwisha kupita! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aonaye kiu nitampatia kinywaji bila gharama kutoka katika chemchemi za maji ya uzima.
\s5
\v 7 Yeye ashindaye atayarithi mambo haya, na nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
\v 8 Lakini kama ilivyo kwa waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao itakuwa katika ziwa la moto wa kiberiti uunguzao. Hiyo ndiyo mauti ya pili."
\s5
\v 9 Mmoja wa malaika saba alikuja kwangu, mmoja ambaye alikuwa na mabakuli saba yaliyojaa mapigo saba ya mwisho na alisema, "Njoo hapa. Nitakuonesha bibi harusi, mke wa mwana kondoo."
\v 10 Kisha alinichukua mbali katika Roho kwenye mlima mkubwa na mrefu na alinionesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu.
\s5
\v 11 Yerusalemu ulikuwa na utukufu wa Mungu, na uzuri wake ulikuwa kama kito cha thamani, kama jiwe la kioo safi la yaspi.
\v 12 Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na miwili, pamoja na malaika kumi na wawili milangoni. Juu ya milango palikuwa pameandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli.
\v 13 Upande wa mashariki palikuwa na milango mitatu, upande wa kusini milango mitatu, upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa magharibi milango mitatu.
\s5
\v 14 Kuta za mji zilikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake palikuwa na majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo.
\v 15 Mmoja aliyeongea nami alikuwa na kipimo cha fimbo iliyotengenezwa kwa dhahabu kwa ajili ya kupima mji, milango yake na kuta zake.
\s5
\v 16 Mji uliwekwa ndani ya mraba; urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Alipima mji kwa kipimio cha fimbo, stadia 12, 000 kwa urefu (urefu wake, upana, na kimo vilifanana).
\v 17 Vilevile alipima ukuta wake, unene wake ulikuwa dhiraa 144 kwa vipimo vya kibinadamu (ambavyo pia ni vipimo vya malaika).
\s5
\v 18 Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi na mji wenye dhahabu safi, kama kioo safi.
\v 19 Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa na kila aina ya jiwe la thamani. La kwanza lilikuwa yaspi, la pili lilikuwa yakuti samawi, la tatu lilikuwa kalkedon, la nne zumaridi,
\v 20 la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolitho, la nane zabarajadi, la tisa yakuti ya manjano, la kumi krisopraso, la kumi na moja hiakintho, la kumi na mbili amethisto.
\s5
\v 21 Milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili, kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja. Mitaa ya mji ilikuwa dhahabu safi, ikionekana kama kioo safi.
\v 22 Sikuona hekalu lolote ndani ya mji, kwa kuwa Bwana Mungu, ambaye anatawala juu ya vyote, na Mwana Kondoo ni hekalu lake.
\s5
\v 23 Mji haukuhitaji jua au mwezi ili kungaza juu yake kwa sababu utukufu wa Mungu uliangaza juu yake, na taa yake ni Mwana Kondoo.
\v 24 Mataifa watatembea kwa mwanga wa mji huo. Wafalme wa dunia wataleta fahari zao ndani yake.
\v 25 Milango yake haitafungwa wakati wa mchana, na hapatakuwa na usiku pale.
\s5
\v 26 Wataleta fahari na heshima ya mataifa ndani yake,
\v 27 na hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake. Wala yeyote ambaye afanyaye jambo lolote la aibu au udanganyifu hataingia, bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uzima, maji yalikuwa ya mng'ao kama wa bilauri. Yalikuwa yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo
\v 2 Kupitia katikati ya mtaa wa mji. Katika kila pembe ya mto palikuwa na mti wa uzima, unaozaa aina kumi na mbili za matunda, na huzaa matunda kila mwezi. Majani ya mti ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
\s5
\v 3 Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwemo ndani ya mji, na watumishi wake watamtumikia.
\v 4 Watamuona uso wake, na jina lake litakuwa juu ya vipaji vya nyuso zao.
\v 5 Hapatakuwa na usiku tena; wala hapatakuwa na hitaji la mwanga wa taa au jua kwa sababu Bwana Mungu ataangaza juu yao. Nao watatawala milele na milele.
\s5
\v 6 Malaika akaniambia, "Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana Mungu wa roho za manabii alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake kitakachotokea hivi karibuni."
\v 7 "Tazama! Ninakuja upesi! Amebarikiwa yeye anayeyatii maneno ya unabii wa kitabu hiki."
\s5
\v 8 Mimi, Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Nilipoyasikia na kuyaona, nilianguka chini mwenyewe mbele ya miguu ya malaika kumwabudu, malaika aliyenionesha mambo haya.
\v 9 Akaniambia, "Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi mwenzako, pamoja na ndugu zako manabii, pamoja na wale wanaotii maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!"
\s5
\v 10 Akaniambia, "Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, maana wakati umekaribia.
\v 11 Asiye mwenye haki, aendelee kutokuwa mwenye haki. Ambaye ni mchafu kimaadili, na aendelee kuwa mchafu kimaadili. Mwenye haki, na aendelee kuwa mwenye haki. Aliye mtakatifu, na aendelee kuwa mtakatifu."
\s5
\v 12 "Tazama! Naja upesi. Ujira wangu uko pamoja nami, kumlipa kila mmoja kulingana na alichokifanya.
\v 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
\s5
\v 14 Wamebarikiwa wale waoshao mavazi yao ili kwamba wapate haki ya kula kutoka katika mti wa uzima na kuuingia mji kupitia malangoni.
\v 15 Nje kuna mbwa, wachawi, wazinzi, wauwaji, waabudu sanamu, na kila apendaye na ashuhudiaye ushahidi wa uongo.
\s5
\v 16 Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia kuhusu mambo haya kwa makanisa. Mimi ni mzizi wa uzao wa Daudi, Nyota ya Asubuhi ing'aayo."
\s5
\v 17 Roho na Bibi harusi asema, "Njoo!" Na yeye asikiaye aseme, "Njoo!" Yeyote aliye na kiu, na aje, na yeyote anayetamani, na apate maji ya uzima bure.
\s5
\v 18 Namshuhudia kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Kama yeyote ataongeza katika hayo, Mungu atamuongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
\v 19 Kama mtu yeyote atayaondoa maneno ya kitabu hiki cha unabii, Mungu ataondoa sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo habari zake zimeandikwa ndani ya kitabu hiki.
\s5
\v 20 Yeye ashuhudiaye mambo haya asema, "Ndiyo! Naja upesi." Amina! Njoo, Bwana Yesu!
\v 21 Neema ya Bwana Yesu iwe na kila mtu. Amina.