sw_ulb_rev/61-1PE.usfm

209 lines
14 KiB
Plaintext

\id 1PE
\ide UTF-8
\h 1 Petro
\toc1 1 Petro
\toc2 1 Petro
\toc3 1pe
\mt 1 Petro
\s5
\c 1
\p
\v 1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wageni wa utawanyiko, kwa wateule, katika Ponto yote, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia,
\v 2 kutokana na ufahamu wa Mungu, Baba, kwa kutakaswa na Roho Mtakatifu, kwa utiifu wa Yesu Kristo, na kwa kunyunyuziwa damu yake. Neema iwe kwenu, na amani yenu iongezeke.
\s5
\v 3 Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na abarikiwe. Katika ukuu wa rehema yake, alitupa kuzaliwa upya kwa ujasiri wa urithi kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka katika wafu,
\v 4 kwa urithi usioangamia, hautakua na uchafu wala kupungua. Umehihifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu.
\v 5 Kwa uwezo wa Mungu mnalindwa kupitia imani kwa wokovu ambao upo tayari kufunuliwa katika nyakati za mwisho.
\s5
\v 6 Furahini katika hili, ingawaje sasa ni lazima kwenu kujisikia huzuni katika majaribu ya aina mbalimbali.
\v 7 Hii, ni kwa sababu imani yenu iweze kujaribiwa, imani ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ambayo inapotea katika moto ambao hujaribu imani yenu. Hii hutokea ili imani yenu ipate kuzaa sifa, utukufu, na heshima katika ufunuo wa Yesu Kristo.
\s5
\v 8 Hamjamuona yeye, lakini mnampenda. Hamumuoni sasa, lakini mnaamini katika yeye na mna furaha isiyoweza kuelezeka kwa furaha ambayo imejawa na utukufu.
\v 9 Sasa mnapokea wenyewe matokeo ya imani yenu, wokovu wa nafsi zenu.
\v 10 Manabii walitafuta na kuuliza kwa umakini kuhusu wokovu huu, kuhusu neema ambayo ingekuwa yenu.
\s5
\v 11 Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata.
\v 12 Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.
\s5
\v 13 Kwa hiyo fungeni viuno vya akili zenu. Muwe watulivu katika fikra zenu. Muwe na ujasiri mkamilifu katika neema ambayo italetwa kwenu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo.
\v 14 Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu.
\s5
\v 15 Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.
\v 16 Kwa kuwa imeandkwa, "Iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu."
\v 17 Na kama mkiita "Baba" yule ahukumuye kwa haki kulingana na kazi ya kila mtu, tumia muda wa safari yako katika unyenyekevu.
\s5
\v 18 Mnafahamu kwamba haikuwa kwa fedha au dhahabu - vitu vinavyoharibika- ambavyo mmekombolewa kutoka kwenye tabia zenu za ujinga ambazo mlijifunza kutoka kwa baba zenu.
\v 19 Lakini mmekombolewa kwa damu ya heshima ya Kristo, kama ya kondoo asiye na hila wala doa.
\s5
\v 20 Kristo alichaguliwa kabla ya misingi ya dunia, lakini sasa siku hizi za mwisho, amefunuliwa kwenu.
\v 21 Mnamwamini Mungu kupitia yeye, ambaye Mungu alimfufua toka kwa wafu na ambaye alimpa utukufu ili kwamba imani yenu na ujasiri uwe katika Mungu.
\s5
\v 22 Mmefanya nafsi zenu kuwa safi kwa utii wa ile kweli, kwa dhumuni la pendo la kidugu lililo na unyofu, hivyo pendaneni kwa bidii toka moyoni.
\v 23 Mmekwisha zaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, lakini kutoka katika mbegu isiyoharibika, kupitia uzima na neno la Mungu lililosalia.
\s5
\v 24 Kwa maana " miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
\v 25 lakini neno la Bwana hubakia milele." Huu ni ujumbe ambao ulitangazwa kama injili kwenu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo wekeni pembeni uovu wote, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa.
\v 2 Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwamba mweze kukua ndani ya wokovu,
\v 3 kama mmeonja kwamba Bwana ni mwema.
\s5
\v 4 Njoni kwake aliye jiwe hai linaloishi ambalo limekataliwa na watu, lakini hilo limechaguliwa na Mungu na ni la thamani kwake.
\v 5 Ninyi pia ni kama mawe yaliyo hai yanayojengwa juu kuwa nyumba ya kiroho, ili kuwa ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.
\s5
\v 6 Andiko husema hivi, "Tazama, nimeweka katika Sayuni jiwe la pembeni, kuu na lililochaguliwa na la thamani. Yeyote aaminiye katika yeye hataona aibu".
\s5
\v 7 Hivyo heshima ni yenu kwenu ninyi mnaoamini. Lakini, "jiwe lililokataliwa na wajenzi, hili limekuwa jiwe kuu la pembeni"-
\v 8 na, "jiwe la kujikwaa na mwamba wa kujikwaa."Wao hujikwaa, wanaolikataa neno, kwa lile ambalo pia walikuwa wameteuliwa kwalo.
\s5
\v 9 Lakini ninyi ni ukoo uliochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kutangaza matendo ya ajabu ya yule aliyewaita kutoka gizani kuja kwenye nuru yake ya ajabu.
\v 10 Ninyi kwanza hamkuwa watu, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Ninyi hamkupokea rehema, lakini sasa mmepokea rehema.
\s5
\v 11 Wapendwa, nimewaita kama wageni na wazurujaji kujinyima kutoka kwenye tamaa mbaya za dhambi, ambazo zinapigana vita na roho zenu.
\v 12 Mnapaswa kuwa na tabia njema kati ya mataifa, ili kwamba, kama watawasema kama kwamba mmefanya mambo maovu, wataziangalia kazi zenu njema na kumsifu Mungu katika siku ya kuja kwake.
\s5
\v 13 Tii kila mamlaka ya mwanadamu kwa ajili ya Bwana, ikiwa mfalme kama mkuu,
\v 14 ikiwa watawala waliotumwa kuwaadhibu watenda mabaya na kuwasifu wale wanaotenda mema.
\v 15 Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kufanya mema mwanyamazisha mazungumzo ya kipuuzi ya watu wapumbavu.
\v 16 Kama watu huru, msiutumie uhuru wenu kama kifuniko kwa maovu, bali muwe kama watumishi wa Mungu.
\v 17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mwogopeni Mungu. Mweshimuni mfalme.
\s5
\v 18 Watumwa, watiini bwana zenu kwa heshima yote, siyo tu bwana walio wazuri na wapole, lakini pia walio waovu.
\v 19 Kwa kuwa ni sifa kama yeyote atavumilia maumivu wakati anapoteseka pasipo haki kwa sababu ya dhamiri yake kwa Mungu.
\v 20 Ni faida gani iliyopo kama mwadumu kutenda dhambi kisha mwendelee kuadhibiwa? Lakini kama mmefanya mema na ndipo mteseke kwa kuhukumiwa, hii ni sifa njema kwa Mungu.
\s5
\v 21 Kwa hili mliitwa, kwa sababu Kristo pia aliteswa kwa ajili yenu, amewaachia mfano kwa ajili yenu kufuata nyayo zake.
\v 22 Yeye hakufanya dhambi, wala haukuonekana udanganyifu wowote kinywani mwake.
\v 23 Wakati yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteseka, hakutisha bali alijitoa mwenyewe kwake Yeye ahukumuye kwa haki.
\s5
\v 24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake kwenye mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena katika dhambi, na kwamba tuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa kwake ninyi mmepona.
\v 25 Wote mliokuwa mkitangatanga kama kondoo aliyepotea, lakini sasa mmerudi kwa mchungaji na mlinzi wa roho zenu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa njia hii, ninyi ambao ni wake mnapaswa kujitoa kwa waume zenu wenyewe, ili, hata kama baadhi yao hawajalitii neno, kupitia tabia za wake zao wanaweza kuvutwa pasipo neno,
\v 2 kwa sababu wao wenyewe watakuwa wameiona tabia yenu njema pamoja na heshima.
\s5
\v 3 Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.
\v 4 Lakini badala yake ifanyike kwa utu wa ndani wa moyo, na kuzidi katika uzuri wa unyenyekevu na utulivu wa moyo, ambao ni wa thamani mbele za Mungu.
\s5
\v 5 Kwa kuwa wanawake watakatifu walijipamba wenyewe kwa njia hii. Walikuwa na imani katika Mungu na waliwatii waume zao wenyewe.
\v 6 Kwa njia hii Sara alimtii Ibrahamu na kumwita yeye "bwana" wake. Ninyi sasa ni watoto wake kama mtafanya yaliyo mazuri na kama hamwogopi mabaya.
\s5
\v 7 Kwa njia hiyo hiyo, ninyi wanaume mnapaswa kuishi na wake zenu mkijua kuwa wao ni wenzi wa kike dhaifu, mkiwatambua wao kama wapokeaji wenzenu wa zawadi ya uzima. Fanyeni hivi ili kwamba maombi yenu yasizuiliwe.
\s5
\v 8 Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.
\v 9 Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.
\s5
\v 10 "Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.
\v 11 Na ageuke na kuacha mabaya na kufanya yaliyo mazuri. Atafute amani na kuifuata.
\v 12 Macho ya Bwana humwona mwenye haki na masikio yake husikia maombi yake. Lakini uso wa Bwana uko kinyume cha wale watendao uovu."
\s5
\v 13 Ni nani atakayewadhuru ninyi, ikiwa mwatamani lililo zuri?
\v 14 Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.
\s5
\v 15 Badala yake, mmuweke Kristo Bwana katika mioyo yenu kama mtakatifu. Kila mara muwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza ninyi kwa nini mna tumaini katika Mungu. Fanyeni hivi kwa upole na heshima.
\v 16 Muwe na dhamiri njema ili kwamba watu wanaotukana maisha yenu mema katika Kristo waweze kuaibika kwa sababu wanaongea kinyume dhidi yenu kama kwamba mlikuwa watenda maovu.
\v 17 Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.
\s5
\v 18 Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi. Yeye ambaye ni mwenye haki aliteseka kwa ajili yetu, ambao hatukuwa wenye haki, ili kwamba atulete sisi kwa Mungu. Alikufa katika mwili, lakini alifanywa mzima katika roho.
\v 19 Katika roho, alikwenda na kuzihubiri roho ambazo sasa ziko kifungoni.
\v 20 Hazikuwa tiifu wakati uvumilivu wa Mungu ulipokuwa unasubiri wakati wa Nuhu, siku za ujenzi wa safina, na Mungu aliokoa watu wachache—nafsi nane—kutoka katika maji.
\s5
\v 21 Hii ni alama ya ubatizo unaowaokoa ninyi sasa, siyo kama kuosha uchafu kutoka mwilini, lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo.
\v 22 Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu. Alikwenda mbinguni. Malaika, mamlaka, na nguvu lazima vimtii yeye.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni silaha za nia ile ile. Yeye aliyeteseka katika mwili ameondokana na dhambi.
\v 2 Mtu huyu haendelei tena kuishi katika tamaa za mwili, bali kwa mapenzi ya Mungu, kwa maisha yake yaliyosalia.
\s5
\v 3 Kwa kuwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo.
\v 4 Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu.
\v 5 Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu.
\v 6 Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho.
\s5
\v 7 Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu.
\v 8 Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.
\v 9 Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika.
\s5
\v 10 Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu.
\v 11 Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina.
\s5
\v 12 Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu.
\v 13 Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.
\v 14 Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.
\s5
\v 15 Lakini asiwepo yeyote mwenye kuteswa kama muuaji, mwizi, mtenda maovu, au ajishughulishaye na mambo ya wengine.
\v 16 Lakini ikiwa mtu anateswa kama Mkristo, asione aibu, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
\s5
\v 17 Kwa kuwa wakati umefika kwa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Na kama inaanzia kwetu, itakuwaje kwa wale wasioitii injili ya Mungu?
\v 18 Na kama "mwenye haki anaokolewa kupitia magumu, itakuwaje kwa mtu asiyehaki na mwenye dhambi?"
\v 19 Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, mimi, niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso ya Kristo, na ambaye vile vile ni mshirika katika utukufu utakaodhihirika.
\v 2 Kwa hiyo, ninawatia moyo ninyi wazee, lichungeni kundi la Mungu lililo miongoni mwenu. Liangalieni, sio kwa sababu mnapaswa, lakini kwa sababu mnatamani hivyo, kulingana na Mungu. Liaangalieni, sio kwa kupenda pesa za aibu, lakini kwa kupenda.
\v 3 Msijifanye mabwana juu ya watu waliyochini ya uangalizi wenu, lakini iweni mfano katika kundi.
\v 4 Pale Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu isiyopoteza uthamani wake.
\s5
\v 5 Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.
\v 6 Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.
\v 7 Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.
\s5
\v 8 Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.
\v 9 Simameni kinyume chake. Kuweni na nguvu katika imani yenu. Mkijua kwamba ndugu zenu walioko ulimwenguni wanapitia mateso kama hayo.
\s5
\v 10 Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.
\v 11 Enzi iwe kwake milele na milele. Amina.
\s5
\v 12 Namthamini Silwano kama ndugu mwaminifu, na nimewaandikia ninyi kwa ufupi kupitia kwake. Ninawatia moyo na ninashuhudia kwamba nilichokiandika ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni ndani yake.
\v 13 Waamini waliloko Babeli, waliochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu, na Marko mwanangu, anawasalimu.
\v 14 Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.