sw_ulb_rev/57-TIT.usfm

108 lines
6.0 KiB
Plaintext

\id TIT
\ide UTF-8
\h Tito
\toc1 Tito
\toc2 Tito
\toc3 tit
\mt Tito
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli iletayo utauwa.
\v 2 Wapo katika tumaini la uzima wa milele ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele.
\v 3 Kwa wakati muafaka, alilifunua neno lake katika ujumbe alionipa mimi kuhubiri. Ilinipasa kufanya hivi kwa amri ya Mungu mwokozi wetu.
\s5
\v 4 Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani yetu. Neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu.
\v 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, kwamba uyatengeneze mambo yote yaliyokuwa hayajakamilika na kuweka wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza.
\s5
\v 6 Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasioshuhudiwa mabaya au wasio na nidhamu.
\v 7 Ni muhimu kwa mwangalizi, kama msimamizi wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu wa kelele au asiye jizuia. Lazima asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi, asiwe mtu wa kusababisha ugomvi, na asiwe mwenye tamaa.
\s5
\v 8 Badala yake: awe mtu mkaribishaji, apendaye wema. Lazima awe mtu mwenye akili timamu, mwenye haki, mcha Mungu, anayejitawala mwenyewe.
\v 9 Awezaye kusimamia mafundisho ya kweli yaliyofundishwa, ili aweze kuwatia moyo kwa mafundisho mazuri na awezaye kuwarekebisha wote wanaompinga.
\s5
\v 10 Kwa kuwa kuna waasi wengi, hasa wale wa tohara. Maneno yao ni ya upuuzi. Wanadanganya na kuwaongoza watu katika upotovu.
\v 11 Ni lazima kuwazuia watu kama hao. Wanafundisha yale wasiyopaswa kwa faida za aibu na kuharibu familia zote.
\s5
\v 12 Mmoja wao, mtu mwenye busara, alisema, "Wakrete wana uongo usio na mwisho, wabaya na wanyama wa hatari, wavivu na walafi."
\v 13 Haya maelezo ni ya kweli, kwa hiyo uwazuie kwa nguvu ili kwamba waweze kusema kweli katika imani.
\s5
\v 14 Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli.
\s5
\v 15 Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Lakini kwa wote walio wachafu na wasioamini, hakuna kilicho kisafi. Kwa kuwa mawazo yao na dhamira zao zimechafuliwa.
\v 16 Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni waovu na wasiotii. Hawakuthibitishwa kwa tendo lolote jema.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Lakini wewe yaseme yale yanayoendana na maelekezo ya kuaminika.
\v 2 Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu.
\s5
\v 3 Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe.
\v 4 Wanapaswa kufundisha yaliyo mazuri ili kuwaandaa wasichana kwa busara kuwapenda waume zao na watoto wao.
\v 5 Wanapaswa kuwafundisha kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na watii kwa waume zao wenyewe. Inawalazimu kufanya mambo haya ili kwamba neno la Mungu lisitukanwe.
\s5
\v 6 katika namna iyo hiyo, watieni moyo vijana wa kiume wawe na busara.
\v 7 Katika njia zote jiwekeni wenyewe kuwa mfano katika kazi nzuri; na mfundishapo, onesheni uadilifu na heshima.
\v 8 Ongeeni ujumbe wenye afya na usio na dosari, ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe kwa sababu hana baya la kusema juu yetu.
\s5
\v 9 Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu. Wanapaswa kuwafurahisha na sio kubishana nao.
\v 10 Hawapaswi kuiba. Badala yake, wanapaswa kuonesha imani yote nzuri ili kwamba katika njia zote wayapambe mafundisho yetu kumhusu Mungu mwokozi wetu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa watu wote.
\v 12 Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia. Inatufundisha kuishi kwa busara, kwa haki, na katika njia za kimungu kwa wakati huu.
\v 13 Wakati tunatarajia kupokea tumaini letu lenye baraka, mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 14 Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili kutukomboa kutoka katika uasi na kutufanya wasafi, kwa ajili yake, watu maalumu walio na hamu ya kufanya kazi nzuri.
\s5
\v 15 Yaseme na kuyasisitiza mambo haya. Kemea kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Uwakumbushe kuwanyenyekea viongozi na mamlaka, kuwatii na kuwa tayari katika kila kazi njema.
\v 2 Wakumbushe kutokumtendea mtu yeyote ubaya, waepuke majibizano, wawape nafasi watu wengine katika kufanya maamuzi, na kuonesha unyenyekevu kwa watu wote.
\s5
\v 3 Kwa kuwa sisi pia tulikuwa na mawazo potofu na wakaidi. Tulikuwa upotevuni na tulifanywa watumwa kwa tamaa nyingi na starehe. Tuliishi katika wivu na uovu. Tulichukiza na kuchukiana.
\s5
\v 4 Lakini wakati huruma ya Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana,
\v 5 haikuwa kwa matendo yetu ya haki tuliyofanya, bali alituokoa kwa neema yake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na katika kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu.
\s5
\v 6 Mungu alimwaga Roho Mtakatifu kwa wingi juu yetu kupitia Yesu Kristo mwokozi wetu.
\v 7 Alifanya hivi ili kwamba, tukiwa tumehesabiwa haki kwa neema yake, tuwe washirika katika uhakika wa maisha ya milele.
\s5
\v 8 Huu ni ujumbe wa kuaminika. Ninawataka myanene kwa ujasiri mambo haya, ili kwamba wale wanaomwamini Mungu wawe na dhamira juu ya kazi nzuri ambayo aliiweka mbele yao. Mambo haya ni mazuri na yanafaida kwa ajili ya watu wote.
\s5
\v 9 Lakini jiepusheni na mijadala ya kipumbavu, nasaba, mashindano, na migongano kuhusu sheria. Mambo hayo hayana maana wala faida.
\v 10 Mkataeni yeyote anayesababisha migawanyiko kati yenu. Baada ya onyo moja ama mawili,
\v 11 jueni kwamba mtu wa jinsi hiyo ameiacha njia iliyo sahihi na anatenda dhambi na kujihukumu mwenyewe.
\s5
\v 12 Nitakapomtuma kwako Artemi au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi.
\v 13 Harakisha na umtume Zena mtaalamu katika sheria, na Apolo, pasipo kupungukiwa na kitu.
\s5
\v 14 Watu wetu lazima wajifunze kujishughulisha katika kazi nzuri ambazo zinagusa mahitaji muhimu ili kwamba wasije wakawa wasiozaa matunda.
\s5
\v 15 Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu wale watupendao katika imani. Neema iwe nanyi nyote.