sw_ulb_rev/55-1TI.usfm

223 lines
14 KiB
Plaintext

\id 1TI
\ide UTF-8
\h 1Timotheo
\toc1 1Timotheo
\toc2 1Timotheo
\toc3 1ti
\mt 1Timotheo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, Mtume wa Kristo Yesu, kulingana na amri ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliye ujasiri wetu,
\v 2 kwa Timotheo mwanangu wa kweli katika imani: Neema, rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\v 3 Kama nilivyokusihi nilipoondoka kwenda Makedonia, ubaki Efeso ili kwamba uweze kuwaamru watu fulani wasifundishe mafundisho tofauti.
\v 4 Pia wasisikilize hadithi na orodha za nasaba zisizo na mwisho. Haya husababisha mabishano zaidi kuliko kuwasaidia kuendeleza mpango wa Mungu wa imani.
\s5
\v 5 Basi lengo la agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi, katika dhamiri nzuri na katika imani ya kweli.
\v 6 Baadhi ya watu wamelikosa lengo wakayaacha mafundisho haya na kugeukia mazungumzo ya kipumbavu.
\v 7 Wanataka kuwa waalimu wa sheria, lakini hawafahamu wanachosema au wanachosisitiza.
\v 8 lakini tunajua kwamba sheria ni njema kama mtu ataitumia kwa usahihi.
\s5
\v 9 Tunajua kuwa, sheria haikutungwa kwa ajili ya mtu mwenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, watu wasio wataua na wenye dhambi, na ambao hawana Mungu na waovu. Imetungwa kwa ajili ya wauao baba na mama zao, kwa ajili ya wauaji,
\v 10 kwa ajili ya waasherati, kwa ajili ya watu wazinzi, kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kuwafanya watumwa, kwa ajili ya waongo, kwa ajili ya mashahidi wa uongo, na yeyote aliye kinyume na maelekezo ya uaminifu.
\v 11 Malekezo haya yanatokana na injili yenye utukufu ya Mungu mwenye kubarakiwa ambayo kwayo nimeaminiwa.
\s5
\v 12 Ninamshukuru Yesu Kristo Bwana wetu. Alinitia nguvu, kwa kuwa alinihesabu mimi kuwa mwaminifu, na akaniweka katika huduma.
\v 13 Nilikuwa mtu wa kukufuru, mtesaji na mtu wa vurugu. Lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda kwa ujinga kwa kutoamini.
\v 14 Lakini neema ya Mungu wetu imejaa imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.
\s5
\v 15 Ujumbe huu ni wa kuaminika na unastahili kupokelewa na wote, ya kuwa Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi. Mimi ni mbaya zaidi ya wote.
\v 16 Lakini kwa sababu hii mimi nilipewa rehema ili kwamba ndani yangu mimi, awali ya yote, Kristo Yesu adhihirishe uvumilivu wote. Alifanya hivyo kama kielelezo kwa wote watakaomtumaini Yeye kwa ajili ya uzima wa milele.
\v 17 Na sasa kwa Mfalme asiye na ukomo, asiyekufa, asiyeonekana, Mungu pekee, iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
\s5
\v 18 Ninaliweka agizo hili mbele yako Timotheo, mtoto wangu. Nafanya hivi kulingana na unabii uliotolewa hapo kwanza kukuhusu wewe, ili kwamba uhusike katika vita njema.
\v 19 Fanya hivyo ili kwamba uwe na imani na dhamiri njema. Baadhi ya watu wameyakataa haya wakaangamiza imani.
\v 20 Kama vile Himeneyo na Alekizanda ambao nimempa shetani ili wafundishwe wasikufuru.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo awali ya yote, nahitaji maombi, na dua, na maombezi, na shukrani vifanyike kwa ajili ya watu wote,
\v 2 kwa ajili ya wafalme na wote ambao wako kwenye mamlaka, ili kwamba tuweze kuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na heshima.
\v 3 Hili ni jema na lenye kukubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu.
\v 4 Yeye hutamani kuwa watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli.
\s5
\v 5 Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu.
\v 6 Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka.
\v 7 Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. Nasema kweli. Sisemi uongo. Mimi ni mwalimu watu Mataifa katika imani na kweli.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.
\v 9 Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.
\v 10 Pia nataka wavae mavazi yanayowastahili wanawake wanaokiri uchaji kwa kupitia matendo mema.
\s5
\v 11 Mwanamke na ajifunze katika hali ya utulivu na kwa utii wote.
\v 12 Simruhusu mwanamke kufundisha, au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume bali aishi katika hali ya ukimya.
\s5
\v 13 Kwa kuwa Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva.
\v 14 Adamu hakudanganywa, lakini mwanamke alidanganywa kabisa katika uasi.
\v 15 Hata hivyo, ataokolewa kwa kupitia kuzaa watoto, kama wataendelea katika imani na upendo na katika utakaso na akili njema.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema.
\v 2 Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi,, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe uwezo wa kufundisha.
\v 3 Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha.
\s5
\v 4 Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote.
\v 5 Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu?
\s5
\v 6 Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu.
\v 7 Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu.
\s5
\v 8 Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa.
\v 9 Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa.
\v 10 Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama.
\s5
\v 11 Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote.
\v 12 Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao.
\v 13 Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
\s5
\v 14 Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni.
\v 15 Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli.
\s5
\v 16 Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: "Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa
\v 2 katika uongo na unafiki. Dhamiri zao zitabadilishwa.
\s5
\v 3 Watawazuia kuoa na kupokea vyakula ambavyo Mungu aliviumba vitumiwe kwa shukrani miongoni mwao waaminio na wenye kuijua kweli.
\v 4 Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu amekiumba ni chema. Hakuna ambacho tunapokea kwa shukrani kinastahili kukataliwa.
\v 5 Kwa sababu kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi.
\s5
\v 6 Kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu, utakuwa mtumishi mzuri wa Yesu Kristo. Kwa sababu umestawishwa kwa maneno ya imani na kwa mafundisho mazuri ambayo umeyafuata.
\v 7 Lakini zikatae hadithi za kidunia ambazo zinapendwa na wanawake wazee. Badala yake, jifunze mwenyewe katika utaua.
\v 8 Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.
\s5
\v 9 Ujumbe huu ni wakuaminiwa na unastahili kukubaliwa kabisa.
\v 10 Kwa kuwa ni kwa sababu hii tunataabika na kufanya kazi kwa bidii sana. Kwa kuwa tunao ujasiri katika Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, lakini hasa kwa waaminio.
\s5
\v 11 Uyaseme na kuyafundisha mambo haya.
\v 12 Mtu yeyote asiudharau ujana wako. Badala yake, uwe mfano kwa wote waaminio, katika usemi, mwenendo, upendo, uaminifu, na usafi.
\v 13 Mpaka nitakapokuja, dumu katika kusoma, katika kuonya, na katika kufundisha.
\s5
\v 14 Usiipuuze karama iliyomo ndani yako, ambayo ulipewa kupitia unabii, kwa kuwekewa mikono na wazee.
\v 15 Uyajali mambo haya. Ishi katika hayo ili kukua kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Zingatia sana mwenendo wako na mafundisho.
\v 16 Dumu katika mambo haya. Maana kwa kufanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.
\v 2 Uwatiye moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote.
\s5
\v 3 Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli.
\v 4 Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.
\s5
\v 5 Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
\v 6 Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai.
\s5
\v 7 Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.
\v 8 Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini.
\s5
\v 9 Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.
\v 10 Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
\s5
\v 11 Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili dhidi ya Kristo, wanataka kuolewa.
\v 12 Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.
\v 13 Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
\s5
\v 14 Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.
\v 15 Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.
\v 16 Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.
\s5
\v 17 Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu.
\v 18 Kwa kuwa maandiko yanasema, "Usimfumbe ng'ombe kinywa apulapo nafaka," na "Mfanya kazi anastahili mshahara wake."
\s5
\v 19 Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu.
\v 20 Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.
\s5
\v 21 Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uzitunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
\v 22 Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe usafi.
\s5
\v 23 Hakupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.
\v 24 Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.
\v 25 Vivyo hivyo, baadhi ya kazi njema hujulikana kwa uwazi, lakini hata zingine hazitafichika.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote, wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe.
\v 2 Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.
\s5
\v 3 Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa.
\v 4 Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya,
\v 5 na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiri"
\s5
\v 6 Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
\v 7 Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani.
\v 8 Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.
\s5
\v 9 Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.
\v 10 Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.
\s5
\v 11 Lakini wewe mtu wa Mungu, yakimbie mambo hayo. Fuata haki, utauwa, uaminifu, upendo, usitahimilivu, na upole.
\v 12 Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema.
\s5
\v 13 Nakupa amri hii mbele za Mungu, anayesababisha vitu vyote kuishi, na mbele ya Yesu Kristo, aliyenena iliyo kweli kwa Pontio Pilato:
\v 14 itunze amri kwa ukamilifu, pasipo mashaka, hadi ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 15 Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza.
\v 16 Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiriwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina.
\s5
\v 17 Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie.
\v 18 Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa.
\v 19 Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.
\s5
\v 20 Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yenye kujipinga ambayo kwa kwa uongo huitwamaarifa.
\v 21 Baadhi ya watu huyatangaza mambo haya, na hivyo wameikosa imani. Neema na iwe pamoja nawe.