sw_ulb_rev/51-PHP.usfm

194 lines
13 KiB
Plaintext

\id PHP
\ide UTF-8
\h Wafilipi
\toc1 Wafilipi
\toc2 Wafilipi
\toc3 php
\mt Wafilipi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu, Kwa wale walitengwa katika Kristo wanaoishi Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi.
\v 2 Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka ninyi nyote.
\v 4 Mara zote katika kila ombi langu kwa ajili yenu ninyi nyote, huwa na furahi ninapowaombea.
\v 5 Nina shukrani nyingi kwa sababu ya ushirika wenu katika injili tangu siku ya kwanza mpaka leo.
\v 6 Nina hakika kuwa yeye aliyeanzisha kazi njema ndani yenu ataendelea kuikamilisha mpaka siku ya Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 7 Ni sawa kwangu kujisikia hivi juu yenu ninyi nyote kwa sababu nimewaweka moyoni wangu. Maana ninyi mmekuwa washirika wenza katika neema katika kifungo changu na katika utetezi na uthibitishaji wangu wa injili.
\v 8 Mungu ni shahidi wangu, jinsi nilivyo na shauku juu ya yenu nyote katika undani wa pendo la Kristo Yesu.
\s5
\v 9 Na ninaomba kwamba: upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote.
\v 10 Ninaomba kwa ajili ya hili ili muwe na uwezo wa kupima na kuchagua mambo yaliyo bora sana. Pia ninawaombea ili muwe safi pasipokuwa na hatia yoyote katika siku ya Kristo.
\v 11 Na pia ili mjazwe na tunda la haki lipatikanalo katika Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
\s5
\v 12 Sasa ndugu zangu, nataka mjue kuwa, mambo yaliyotokea kwangu yameifanya injili iendelee sana.
\v 13 Ndiyo maana vifungo vyangu katika Kristo, vimejulikana kwa walinzi wa ikulu yote na kwa kila mtu pia.
\v 14 Na ndugu wengi katika Bwana, kwa sababu ya vifungo vyangu, wameshawishika na kuthubutu kulihubiri Neno pasipo hofu.
\s5
\v 15 Baadhi kweli hata humtangaza Kristo kwa fitina na ugomvi, na pia wengine kwa nia njema.
\v 16 Wale wanaomtangaza Kristo kwa upendo wanajua kuwa nimewekwa hapa kwa ajili ya utetezi wa injili.
\v 17 Bali wengine wanamtangaza Kristo kwa ubinafsi na nia mbaya. Hudhani kuwa wanasababisha matatizo kwangu katika minyororo yangu.
\s5
\v 18 Kwa hiyo? Sijali, aidha njia ikiwa ni kwa hila au kwa kweli, Kristo anatangazwa, na katika hili ninafurahia! Ndiyo, nitafurahia.
\v 19 kwa kuwa ninajua ya kuwa hili litaleta kufunguliwa kwangu. Jambo hili litatokea kwa sababu ya maombi yenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo.
\s5
\v 20 Kulingana na matarajio yangu ya uhakika na kweli ni kwamba, sitaona aibu. Badala yake, kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, natarajia kuwa Kristo atainuliwa katika mwili wangu, ikiwa katika uzima au katika kifo.
\v 21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.
\s5
\v 22 Lakini, kama kuishi katika mwili huzaa tunda katika kazi yangu, kwa hiyo sijui ni lipi la kuchagua.
\v 23 Maana ninasukumwa sana na mawazo haya mawili. Nina hamu ya kuuacha mwili na kuwa pamoja na Kristo, kitu ambacho ni cha thamani sana sana.
\v 24 Ingawa, kubaki katika mwili huu ni jambo la muhimu sana kwa ajili yenu.
\s5
\v 25 Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili, ninajua nitabaki na kuendelea kuwa pamoja nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo na furaha ya imani yenu.
\v 26 Na hii italeta furaha yenu kubwa katika Kristo Yesu, kwasababu yangu itaongezeka, kwa sababu ya uwepo wangu tena pamoja nanyi.
\v 27 Mnatakiwa kuishi maisha yenu katika mwenendo mzuri uipasayo injili ya Kristo. fanyeni hivyo ili nikija kuwaona au nisipokuja, nisikie kuwa mmesimama imara katika roho moja. natamani kusikia kuwa mna roho moja, mkiishindania imani ya injili kwa pamoja.
\s5
\v 28 na msitishwe na kitu chochote kinachofanywa na maadui zenu. Hii kwao ni ishara ya uharibifu. Bali kwenu ni ishara ya wokovu kutoka kwa Mungu.
\v 29 kwa maana ninyi mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa pia katika Yeye.
\v 30 kwa maana mna mgogoro uleule kama mliouona kwangu na mnasikia kwamba ninao hata sasa.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ikiwa kuna kutiwa moyo katika Kristo. Ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake. Ikiwa kuna ushirika wa Roho. Ikiwa kuna rehema na huruma.
\v 2 Ikamilisheni furaha yangu kwa kunia mamoja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja.
\s5
\v 3 Msifanye kwa ubinafsi na majivuno. Isipokuwa kwa unyenyekevu mkiwaona wengine kuwa bora zaidi yenu.
\v 4 Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.
\s5
\v 5 Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu.
\v 6 Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho.
\v 7 Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu.
\v 8 Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba.
\s5
\v 9 Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina.
\v 10 Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi.
\v 11 Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
\s5
\v 12 Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka.
\v 13 Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye.
\s5
\v 14 Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano.
\v 15 Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu.
\v 16 Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
\s5
\v 17 Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote.
\v 18 Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami.
\s5
\v 19 Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu.
\v 20 Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu.
\v 21 Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo.
\s5
\v 22 Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili.
\v 23 Kwa hiyo ninatumaini kumtuma haraka pindi tu nitakapofahamu nini kitatokea kwangu.
\v 24 Lakini nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja hivi karibuni.
\s5
\v 25 Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 26 Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.
\v 27 Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
\s5
\v 28 Kwa hiyo ninamrejesha kweny haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi.
\v 29 Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye.
\v 30 Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwa mko mbali nami.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.
\v 2 Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.
\v 3 Kwa kuwa sisi nndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.
\s5
\v 4 Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
\v 5 Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.
\s5
\v 6 Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa. Kwa tuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria.
\v 7 Lakini katika mambo yote niliyoyaona kuwa ya faida kwangu mimi, niliyahesabu kama takataka kwa sababu ya kumfahamu Kristo.
\s5
\v 8 Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo
\v 9 na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.
\v 10 Sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,
\v 11 angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu.
\s5
\v 12 Siyo kweli kwamba tayari nimeishayapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.
\v 13 Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.
\v 14 Najitahidi kufikia lengo kusudi ili nipate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.
\s5
\v 15 Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunuao hiilo kwenu.
\v 16 Hata hivyo, hatua ifikia na tuenende katika mtindo huo.
\s5
\v 17 Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.
\v 18 Wengi wanaoishi niwale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi -wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
\v 19 Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
\s5
\v 20 Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 21 Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.
\v 2 Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.
\v 3 Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
\s5
\v 4 katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.
\v 5 Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.
\v 6 Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.
\v 7 Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
\s5
\v 8 Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.
\v 9 Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.
\s5
\v 10 Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
\v 11 Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
\v 12 Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji.
\v 13 Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
\s5
\v 14 Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.
\v 15 Ninyi wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.
\v 16 Hata nilipokuwa Thesaslonika, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 17 Simaanishi kwamba natafuta msaada. Bali nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu.
\s5
\v 18 Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.
\v 19 Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
\v 20 Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina.
\s5
\v 21 Salamu zangu zimfikie kila muumini katika Kristo Yesu. Wapendwa nilio nao hapa wanawasalimieni.
\v 22 Pia waumini wote hapa wanawasalimieni, hususani wale wa familia ya Kaisari.
\v 23 Na sasa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu.