sw_ulb_rev/50-EPH.usfm

297 lines
18 KiB
Plaintext

\id EPH
\ide UTF-8
\h Waefeso
\toc1 Waefeso
\toc2 Waefeso
\toc3 eph
\mt Waefeso
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kwa waliotengwa kwa ajili ya Mungu walioko Efeso na ambao ni waaminifu katika Kristo Yesu.
\v 2 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa. Ni yeye aliyetubariki kwa kila baraka za kiroho, katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo.
\v 4 Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake.
\s5
\v 5 Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani.
\v 6 Matokeo yake ni kwamba Mungu anatukuzwa kwa neema ya utukufu wake. Hiki ndicho alichotupatia bure kwa njia ya mpendwa wake.
\s5
\v 7 Kwa kuwa katika mpendwa wake, tunaukombozi kupitia damu yake, msamaha wa dhambi. Tunalo hili kwa sababu ya utajiri wa neema yake.
\v 8 Alifanya neema hii kuwa nyingi kwa ajili yetu katika hekima na ufahamu.
\s5
\v 9 Mungu alifanya ijulikane kwetu ile kweli iliyofichika ya mpango, kutokana na hamu iliyodhihirishwa ndani ya Kristo.
\v 10 Wakati nyakati zimetimia kwa utimilifu wa mpango wake, Mungu ataviweka pamoja kila kitu cha mbinguni na cha juu ya nchi ndani ya Kristo.
\s5
\v 11 Katika Kristo tulikuwa tumechaguliwa na kukusudiwa kabla ya wakati. Hii ilikuwa ni kutokana na mpango wa anayefanya vitu vyote kwa kusudi la mapenzi yake.
\v 12 Mungu alifanya hivyo ili kwamba tuweze kuwapo kwa sifa ya utukufu wake. Tulikuwa wa kwanza kuwa na ujasiri ndani ya Kristo.
\s5
\v 13 Ilikuwa kwa njia ya Kristo kwamba mlisikia neno la kweli, injili ya wokovu wenu kwa njia ya Kristo. Ilikuwa katika yeye pia kwamba mmeamini na kutiwa mhuri na Roho Mtakatifu aliye ahidiwa.
\v 14 Roho ndiyo dhamana ya urithi wetu mpaka umiliki utakapopatikana. Hii ilikuwa ni kwa sifa ya utukufu wake.
\s5
\v 15 Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake.
\v 16 Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu.
\s5
\v 17 Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake.
\v 18 Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.
\s5
\v 19 Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake.
\v 20 Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu.
\v 21 Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia.
\s5
\v 22 Mungu amevitiisha vitu vyote chini ya miguu ya Kristo. Amemfanya yeye kichwa juu ya vitu vyote katika kanisa.
\v 23 Ni kanisa kwamba ndilo mwili wake, ukamilifu wake ambaye hujaza vitu vyote katika njia zote.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
\v 2 Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi.
\v 3 Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
\s5
\v 4 Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
\v 5 Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa.
\v 6 Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
\v 7 Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu.
\s5
\v 8 Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.
\v 9 Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.
\v 10 Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
\s5
\v 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa "msio na tohara" kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
\v 12 Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
\s5
\v 13 Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
\v 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
\v 15 Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
\v 16 Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.
\s5
\v 17 Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani kwao wale waliokuwa karibu.
\v 18 Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.
\s5
\v 19 Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
\v 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
\v 21 Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
\v 22 Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa sababu ya hii mimi, Paulo, ni mfungwa wa Yesu Kristo kwa ajili yenu Mataifa.
\v 2 Na amini ya kwamba mmesikia juu ya kazi ya neema ya Mungu aliyo nipa kwa ajili yenu.
\s5
\v 3 Nawaandikieni kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu. Huu ni ukweli uliyofichika ambao niliandika kwa kifupi kwenye barua nyingine.
\v 4 Usomapo kuhusu haya, utaweza kutambua busara yangu katika ukweli huu uliofichika kuhusu Kristo.
\v 5 Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa wana wa watu. Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho kwa Mitume waliotengwa na Manabii.
\s5
\v 6 Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili.
\v 7 Na kwa hili nimefanyika mtumishi kwa zawadi ya neema ya Mungu iliyotolewa kwangu kupitia utendaji wa nguvu yake.
\s5
\v 8 Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote katika wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo.
\v 9 inanipasa kuwaangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote.
\s5
\v 10 Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu.
\v 11 Haya yangetokea kupitia mpango wa milele ambao aliukamilisha ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\v 12 Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake.
\v 13 Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwasababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu.
\s5
\v 14 Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba.
\v 15 ambaye kwa yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina.
\v 16 Ninaomba kwamba apate kuwanemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu.
\s5
\v 17 Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani.
\v 18 Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo.
\v 19 Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu.
\s5
\v 20 Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu,
\v 21 kwake yeye kuwe utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita.
\v 2 Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo.
\v 3 Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
\s5
\v 4 Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu.
\v 5 Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
\v 6 na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.
\s5
\v 7 Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo.
\v 8 Ni kama maandiko yasemavyo: "Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu."
\s5
\v 9 Ni nini maana ya, "Alipaa," isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia?
\v 10 Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote.
\s5
\v 11 Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu.
\v 12 Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo.
\v 13 Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.
\s5
\v 14 Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka.
\v 15 Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo.
\v 16 Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
\s5
\v 17 Kwa hiyo, nasema hili, na nawasihi katika Bwana: Msitembee tena kama watu wa mataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao.
\v 18 Wametiwa giza katika mawazo yao. Wamefukuzwa kutoka katika uzima wa Mungu kwa ujinga ulio ndani yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
\v 19 Hawajisikii aibu. Wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu, katika kila aina ya uchoyo.
\s5
\v 20 Lakini, hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo.
\v 21 Nadhani kwamba mmesikia kuhusu yeye. Nadhani kwamba mmekuwa mkifundishwa katika yeye, kama tu ukweli ulivyo ndani ya Yesu.
\v 22 Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu.
\s5
\v 23 Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu.
\v 24 Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.
\s5
\v 25 Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. "Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake," kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake.
\v 26 Mwe na hasira, lakini msitende dhambi." Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.
\v 27 Msimpe Ibilisi nafasi.
\s5
\v 28 Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.
\v 29 Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.
\v 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
\s5
\v 31 Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi.
\v 32 Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.
\v 2 Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
\s5
\v 3 Zinaa au uchafu wowote na tamaa mbaya lazima visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
\v 4 wala machukizo yasitajwe, mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
\s5
\v 5 Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo nimwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
\v 6 Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
\v 7 Hivyo usishiriki pamoja nao.
\s5
\v 8 Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.
\v 9 Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
\v 10 Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.
\v 11 Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.
\v 12 Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.
\s5
\v 13 Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,
\v 14 kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, "Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako."
\s5
\v 15 Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
\v 16 Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
\v 17 Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.
\s5
\v 18 Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.
\v 19 Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.
\v 20 Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.
\v 21 Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.
\s5
\v 22 Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana.
\v 23 Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.
\v 24 Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.
\s5
\v 25 Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
\v 26 Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
\v 27 Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
\s5
\v 28 Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
\v 29 Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
\v 30 Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.
\s5
\v 31 "Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja".
\v 32 huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.
\v 33 Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
\v 2 "Mheshimu baba yako na mama yako" (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
\v 3 "ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi."
\s5
\v 4 Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
\s5
\v 5 Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
\v 6 Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
\v 7 watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
\v 8 mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.
\s5
\v 9 Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
\s5
\v 10 Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
\v 11 Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.
\s5
\v 12 kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu.
\v 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
\s5
\v 14 Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani.
\v 15 Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
\v 16 Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu.
\s5
\v 17 Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
\v 18 pamoja na maombi na dua. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.
\s5
\v 19 Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
\v 20 Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema.
\s5
\v 21 Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.
\v 22 Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.
\s5
\v 23 Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
\v 24 Neema na iwe pamoja na wote wanampenda Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo kufa.