sw_ulb_rev/44-JHN.usfm

1649 lines
102 KiB
Plaintext

\id JHN
\ide UTF-8
\h Yohana
\toc1 Yohana
\toc2 Yohana
\toc3 jhn
\mt Yohana
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.
\v 2 Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu.
\v 3 Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika.
\s5
\v 4 Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote.
\v 5 Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha.
\s5
\v 6 Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana.
\v 7 Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.
\v 8 Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru
\s5
\v 9 Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja
\s5
\v 10 Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua.
\v 11 Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea.
\s5
\v 12 Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu,
\v 13 Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe.
\s5
\v 14 Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.
\v 15 Yohana alishuhudia kuhusu yeye, na alipaza sauti akisema, "Huyu ndiye ambaye nilisema habari zake nikisema, "Yule ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu amekuwako kabla yangu."
\s5
\v 16 Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa.
\v 17 Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo.
\v 18 Hakuna mwanadamu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mtu pekee ambaye ni Mungu, aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane.
\s5
\v 19 Na huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati makuhani na walawi waliotumwa kwake na Wayahudi kumwuliza, "Wewe ni nani?"
\v 20 Bila kusitasita na hakukana, bali alijibu, "Mimi sio Kristo."
\v 21 Hivyo wakamuuliza, "kwa hiyo wewe ni nani sasa?" Wewe ni Eliya? Akasema, "Mimi siye." Wakasema, Wewe ni nabii? Akajibu," Hapana."
\s5
\v 22 Kisha wakamwambia, "Wewe ni nani, ili kwamba tuwape jibu waliotutuma"? Wajishuhudiaje wewe mwenyewe?"
\v 23 Akasema, "Mimi ni sauti yake aliaye nyikani: 'Inyosheni njia ya Bwana,' kama nabii Isaya alivyosema."
\s5
\v 24 Basi kulikuwa na watu wametumwa pale kutoka kwa Mafarisayo. Wakamuuliza na kusema,
\v 25 "Kwa nini unabatiza basi kama wewe sio Kristo wala Eliya wala nabii?"
\s5
\v 26 Yohana aliwajibu akisema, "Ninabatiza kwa maji. Hata hivyo, miongoni mwenu anasimama mtu msiyemtambua.
\v 27 Huyu ndiye ajaye baada yangu. Mimi sisitahili kulegeza kamba za viatu vyake."
\v 28 Mambo haya yalitendeka huko Bethania, ng'ambo ya Yordani, mahali ambapo Yohana alikuwa akibatiza.
\s5
\v 29 Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, " Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!
\v 30 huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, "Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.'
\v 31 Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, kwamba nilikuja nikibatiza kwa maji."
\s5
\v 32 Yohana alishuhudia, "Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa hua, na ilibaki juu yake.
\v 33 Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, 'yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.'
\v 34 Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu."
\s5
\v 35 Tena siku iliyofuata Yohana alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili,
\v 36 walimwona Yesu akitembea na Yohana akasema, "Tazama, Mwana kondoo wa Mungu!"
\s5
\v 37 Wanafunzi wawili walimsikia Yohana akisema haya wakamfuata Yesu.
\v 38 Tena Yesu aligeuka na kuwaona wanafunzi wale wakimfuata, na akawambia, "Mnataka nini?" Wakajibu, "Rabbi, (maana yake 'mwalimu,' unaishi wapi?"
\v 39 Akawambia, "Njooni na mwone."Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi; walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.
\s5
\v 40 Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro.
\v 41 Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, "Tumempata Masihi" (ambayo inatafsiriwa Kristo).
\v 42 Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, "Wewe ni Simoni mwana wa Yohana" utaitwa Kefa," (maana yake 'Petro').
\s5
\v 43 Siku iliyofuata wakati Yesu alipotaka kuondoka kwenda Galilaya, alimpata Filipo na akamwambia, "Nifuate mimi."
\v 44 Filipo alikuwa ni mwenyeji wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro.
\v 45 Filipo alimpata Nathanaeli na kumwambia, Tumempata yule ambaye Musa aliandika habari zake katika sheria na Manabii. Yesu mwana wa Yusufu, kutoka Nazareti.
\s5
\v 46 Nathanaeli akamwambia, "Je kitu chema chaweza kutokea Nazareti?" Filipo akamwambia, Njoo na uone."
\v 47 Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake na akasema, "Tazama, Mwisraeli kweli kweli asiye na udanganyifu ndani yake!"
\v 48 Nathanaeli akamwambia, "Umenifahamuje mimi?" Yesu akajibu na akamwambia, "Kabla Filipo hajakuita ulipokuwa chini ya mtini, nalikuona."
\s5
\v 49 Nathanaeli akajibu, "Rabi wewe u Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli"!
\v 50 Yesu akajibu akamwambia, Kwa sababu nilikuambia 'nilikuona chini ya mtini' je waamini? utaona matendo makubwa kuliko haya."
\v 51 Yesu akasema, "Amini amini nawambieni mtaziona mbingu zikifunguka, na kuwaona malaika wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya siku tatu, kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya na mama yake Yesu alikuwa huko.
\v 2 Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa katika arusi.
\s5
\v 3 Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, "Hawana divai."
\v 4 Yesu akajibu, "Mwanamke hiyo inanihusu nini mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia."
\v 5 Mama yake akawambia watumishi, "Chochote atakachowambia fanyeni."
\s5
\v 6 Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu.
\v 7 Yesu akawambia, "Ijazeni maji mitungi ya mawe." Wakajaza hadi juu.
\v 8 Kisha akawambia wale watumishi, "Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza." Wakafanya kama walivyoagizwa.
\s5
\v 9 Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na
\v 10 kumwambia, "Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa"
\s5
\v 11 Muujiza huu wa Kana ya Galilaya, ulikuwa ndio mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini.
\s5
\v 12 Baada ya hii, Yesu, mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake walienda katika mji wa Kapernaum na wakaa huko kwa siku chache.
\s5
\v 13 Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.
\v 14 Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu.
\s5
\v 15 Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.
\v 16 Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, "Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko."
\s5
\v 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, "Wivu wa nyumba yako utanila."
\v 18 Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?"
\v 19 Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu."
\s5
\v 20 Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, "Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?"
\v 21 Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.
\v 22 Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.
\s5
\v 23 Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka, wakati wa sikukuu watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya.
\v 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote.
\v 25 Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Basi kulikuwa na Farisayo ambaye jina lake Nikodemo, mmoja wa wajumbe wa baraza la Wayahudi.
\v 2 Mtu huyu alimwendea Bwana Yesu usiku na akamwambia, "Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu kutoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kutenda ishara hizi zote Mungu asipokuwa pamoja naye."
\s5
\v 3 Yesu akamjibu, "Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili."
\v 4 Nikodemo akasema," Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?"
\s5
\v 5 Yesu akajibu, "Amini, amini mtu sipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
\s5
\v 7 Usishangae kwa sababu nilikuwambia, 'ni lazima kuzaliwa mara ya pili.'
\v 8 Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho.
\s5
\v 9 Nikodemo akajibu, kwa kusema, "Mambo haya yawezekanaje?"
\v 10 Yesu akamjibu, "Wewe u mwalimu wa Israeli, hata hauyajui mambo haya?
\v 11 Amini, amini, nakuambia, kile tunachokifahamu twakishuhudia kwa kile tulichokiona. Lakini hampokei ushuhuda wetu.
\s5
\v 12 Kama nimewambia mambo ya hapa duniani na hamuamini, mtawezaje kuamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni?
\v 13 Maana hakuna aliyepanda juu kutoka mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka, Mwana wa Adamu.
\s5
\v 14 Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe,
\v 15 ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele.
\s5
\v 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele.
\v 17 Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
\v 18 Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ameshahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
\s5
\v 19 Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu.
\v 20 kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi.
\v 21 Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.
\s5
\v 22 Baada ya haya, Yesu pamoja na wanafunzi walienda katika nchi ya Yudea. Huko alitumia muda pamoja nao na alikuwa akibatiza.
\v 23 Sasa Yohana pia alikuwa akibatiza huko Ainea karibu na Salim maana kulikuwa na maji mengi pale. Watu walikuwa wakija kwake na kubatizwa,
\v 24 kwa kuwa Yohana alikuwa hajatupwa gerezani.
\s5
\v 25 Kisha palitokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi kuhusu sikukuuu za utakaso.
\v 26 Wakaenda kwa Yohana wakamwambia, "Rabi, yeye uliyekuwa naye ng'ambo ya Mto Yorodani, yeye uliyeshuhudia habari zake, tazama, anabatiza na wote wanaenda wanamfuata."
\s5
\v 27 Yohana akajibu mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa kama amepewa kutoka mbinguni.
\v 28 Ninyi wenyewe mwashuhudia kuwa nalisema kuwa, 'mimi sio Kristo', badala yake nilisema, 'nimetumwa mbele yake.'
\s5
\v 29 Yeye aliye na bibi arusi ni bwana harusi. Sasa rafiki wa bwana arusi, asimamaye na kusikiliza hufurahia sana kwa sababu ya sauti ya bwana arusi. Hii sasa ni furaha yangu iliyotimilika.
\v 30 Anapaswa kuzidi, nami napaswa kupungua.
\s5
\v 31 Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote.
\v 32 Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake.
\v 33 Yeye aliye pokea ushuhuda wake amehakikisha kuwa Mungu ni mkweli.
\s5
\v 34 Kwa sababu yeye aliyetumwa na Mungu huongea maneno ya Mungu. Kwa kuwa hampi Roho kwa kipimo.
\v 35 Baba humpenda Mwana na amempa vitu vyote mikononi mwake.
\v 36 Yeye amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini kwa yeye asiye mtii Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hushikamana juu yake.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Basi Yesu alipofahamu kuwa Mafarisayo wamesikia kuwa Yesu alikuwa anafuasa na kuwabatiza zaidi ya Yohana,
\v 2 (ingawa Yesu mwenyewe alikuwa habatizi ila wanafunzi wake),
\v 3 alitoka Judea na akaenda Galilaya.
\s5
\v 4 Hivyo ilikuwa muhimu kupitia Samaria.
\v 5 Na akafika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari, karibu na eneo ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.
\s5
\v 6 Na kisima cha Yakobo kilikuwa hapo. Yesu alikuwa amechoka kwa ajili ya safari na akakaa karibu na kisima. Ilikuwa muda wa mchana.
\v 7 Mwanamke Msamaria alikuja kuteka maji, na Yesu akamwambia, "Nipe maji ninywe."
\v 8 Kwa sababu wanafunzi wake walikuwa wameenda zao mjini kununua chakula.
\s5
\v 9 Yule mwanamke akamwambia, "Inakuaje wewe Myahudi, kuniomba mimi mwanamke Msamaria, kitu cha kunywa?" Kwa sababu Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.
\v 10 Yesu akamjibu, "Kama ungelijua karama ya Mungu, na yule anayekuambia 'Nipe maji, ' ungelimwomba, na angelikupa maji ya uzima."
\s5
\v 11 Mwanamke akajibu, "Bwana hauna ndoo ya kuchotea, na kisima ni kirefu. Utayapata wapi Maji ya Uzima.?
\v 12 Je wewe ni mkuu, kuliko baba yetu Yakobo, ambaye alitupa kisima hiki, na yeye mwenyewe na watoto wake pamoja na mifugo yake wakanywa maji ya kisima hiki?"
\s5
\v 13 Yesu akajibu, "Yeyote anywae maji haya atapata kiu tena,
\v 14 lakini yeye atakaye kunywa maji nitakayompa hatapata kiu tena. Badala yake maji nitakayompa yatakuwa chemchemi inayobubujika hata milele."
\s5
\v 15 Yule mwanamke akamwambia, "Bwana, nayaomba maji hayo ili nisipate kiu, na nisihangaike kuja hapa kuchota maji."
\v 16 Yesu akamwambia, "Nenda kamwite mumeo, kisha urudi."
\s5
\v 17 Mwanamke akamwambia, "Sina mume." Yesu akajibu, "Umesema vyema, 'Sina mume;'
\v 18 kwa maana umekuwa na wanaume watano, na mmoja ambaye unaye sasa sio mume wako. Katika hili umesema kweli!"
\s5
\v 19 Mwanamke akamwambia, "Bwana naona yakuwa wewe ni nabii.
\v 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi mwasema ya kuwa Yerusalemu ndiyo sehemu ambayo watu wanapaswa kuabudu."
\s5
\v 21 Yesu akamjibu, "Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu au Yerusalemu.
\v 22 Ninyi watu mwaabudu kile msichokijua, lakini sisi twaabudu tunachokijua, kwa sababu wokovu watoka kwa Wayahudi."
\s5
\v 23 Hatahivyo, wakati unakuja, na sasa upo hapa, wakati waabuduo kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli, kwa sababu Baba anawatafuta watu wa namna hiyo kuwa watu wake wanao mwabudu.
\v 24 Mungu ni Roho, na wale wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu kwa roho na kweli."
\s5
\v 25 Mwanamke akamwambia, "Ninajua kuwa Masihi anakuja, (aitwaye Kristo). Huyo atakapokuja atatwambia yote."
\v 26 Yesu akamwambia, "Mimi unayesema nami ndiye."
\s5
\v 27 Wakati huo huo wanafunzi wake wakarudi. Nao walishangaa kwa nini alikuwa akizungumza na mwanamke, lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza, "Unataka nini?" au "Kwa nini unazungumza naye.?"
\s5
\v 28 Hivyo mwanamke akauacha mtungi wake na akaenda mjini na akawambia watu,
\v 29 "Njooni mwone mtu aliyeniambia mambo yangu yote niliyoyatenda, je yawezekana akawa ndiye Kristo?"
\v 30 Wakatoka mjini wakaja kwake.
\s5
\v 31 Wakati wa mchana wanafunzi wake walimsihi wakisema, "Rabi kula chakula."
\v 32 lakini yeye aliwambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi."
\v 33 Wanafunzi wakaambizana, hakuna aliyemletea kitu chochotekula,"Je walileta?"
\s5
\v 34 Yesu akawambia, "Chakula changu ni kufanya mapenzi yake yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake.
\v 35 Je, hamsemi, 'Bado miezi mitano na mavuno yatakuwa tayari?' Ninawambieni tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno!
\v 36 Yeye avunaye hupokea mishahara na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.
\s5
\v 37 Kwa kuwa msemo huu ni wa kweli, 'Mmoja apanda na mwingine avuna.'
\v 38 Niliwatuma kuvuna ambacho hamkukihangaikia, Wengine wamefanya kazi na ninyi mmeingia katika furaha ya kazi yao."
\s5
\v 39 Wasamaria wengi katika mji ule walimwani kwa sababu ya taarifa ya yule mwanamke aliyekuwa akishuhudia, "Aliyeniambia mambo yote niliyoyafanya."
\v 40 Hivyo Wasamaria walipokuja walimsihi akae pamoja nao na akakaa kwao kwa siku mbili.
\s5
\v 41 Na wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.
\v 42 Wakamwambia yule mwanamke, "Tunaamini sio tu kwa maneno yako, kwa sababu sisi wenyewe tumesikia, na sasa twafahamu kuwa hakika yeye ni mwokozi wa ulimwengu."
\s5
\v 43 Baada ya siku hizo mbili, akaondoka na kuelekea Galilaya.
\v 44 Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe.
\v 45 Alipokuja kutoka Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.
\s5
\v 46 Alikuja tena Kana ya Galilaya huko alikoyabadilisha maji kuwa divai. Palikuwa na ofisa ambaye mwana wake alikuwa ni mgonjwa huko Kapernaumu.
\v 47 Aliposikia kuwa Yesu alitoka Judea na kwenda Galilaya, alienda kwa Yesu na kumsihi atelemke amponye mwanawe, ambaye alikuwa karibu kufa.
\s5
\v 48 Ndipo Yesu akamwambia, "Ninyi msipoona ishara na maajabu hamwezi kuamini.
\v 49 Kiongozi akasema, " Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa."
\v 50 Yesu akamwambia, "Nenda mwanao ni mzima." Yule mtu akaamini neno alilolisema Yesu na akaenda zake.
\s5
\v 51 Alipokuwa akishuka, watumishi wake walimpokea na kumwambia mwana wake alikuwa mzima.
\v 52 Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, "Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha."
\s5
\v 53 Ndipo baba yake akatambua kuwa ni muda ule ule Yesu aliosema, "Mwana wako ni mzima." Hivyo yeye na familia yake wakaamini.
\v 54 Hii ilikuwa ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipotoka Yudea kwenda Galilaya.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Baada ya hapo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.
\v 2 Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiebrania Bethzatha, nalo lina matao matano.
\v 3 Idadi kubwa ya wagonjwa ilikuwemo, vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika matao hayo. {Zingatia: Maneno ya mstari wa 3 hayaonekani katika nakala nzuri za kale. "Wakisubiri maji kutibuliwa.") Kwa hakikia wakati fulani malaika alishuka ndani ya Bwana na kuyatibua maji.
\v 4 Kwahiyo, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani ya baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.
\s5
\v 5 Na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane alikuwa ndani ya matao.
\v 6 Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu Yesu alimwambia, "Je unataka kuwa mzima?"
\s5
\v 7 Yule mgonjwa akamjibu, "Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapojaribu kuingia mtu mwingine hunitangulia."
\v 8 Yesu akamwambia, "Inuka na uchukue godoro lako na uende."
\s5
\v 9 Mara yule mtu akaponywa, akachukua kintanda chake na akaenda. Na siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
\s5
\v 10 Hivyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, "Leo ni siku ya Sabato, na hauruhusiwi kubeba godoro lako."
\v 11 Akajibu, yeye aliyeniponya ndiye aliyeniambia, "Chukua godoro lako na uende."
\s5
\v 12 Wakauliza, "Ni nani aliyekuambia 'Chukua godoro lako na uende?'''
\v 13 Ingawa, yule aliyeponywa hakumjua, kwa sababu Yesu alikuwa ameondoka kwa siri. Kwa kuwa kulikuwa na watu wengi katika sehemu hiyo.
\s5
\v 14 Baada ya hapo Yesu alimkuta yule mtu hekaluni na akamwambia, "Tazama, umepona! "Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi."
\v 15 Yule mtu akaenda na kuwataarifu Wayahudi kuwa Yesu ndiye aliyemponya.
\s5
\v 16 Hivyo, kwa sababu ya mambo hayo Wayahudi walimtesa Yesu, kwa sababu alifanya mambo haya siku ya Sabato.
\v 17 Yesu akawambia, "Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami nafanya kazi."
\v 18 Kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kumtafuta ili wamuue sio tu kwa sababu ya kuivunja Sabato, bali kwa kumwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.
\s5
\v 19 Yesu akawajibu, "Amini, amini, Mwana hawezi kufanya kitu chochote isipokuwa kile ambacho amemwona Baba yake anakifanya, kwa kuwa chochote Baba akifanyacho ndicho na Mwana atakachofanya.
\v 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, na amwonyesha kila kitu anachokifanya na atamwonyesha mambo makubwa kuliko haya ili kwamba mzidi kushangaa."
\s5
\v 21 Kwa kuwa kama vile ambavyo Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, halikadhalika Mwana pia humpa yeyote ampendaye.
\v 22 Kwa kuwa Baba hamhukumu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote
\v 23 ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.
\s5
\v 24 Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.
\s5
\v 25 Amini, amini, nawambia wakati unakuja na sasa upo ambao wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wote watakao sikia wataishi.
\s5
\v 26 Kwa kuwa kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake mwenyewe,
\v 27 kadhalika amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake, na Baba amempa Mwana mamlaka ili kwamba ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.
\s5
\v 28 Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
\v 29 nao watatoka nje: kwa waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
\s5
\v 30 Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\v 31 Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
\v 32 Kuna mwingine anayeshuhudia kuhusu mimi na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
\s5
\v 33 Mmetuma kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
\v 34 Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
\v 35 Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
\s5
\v 36 Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
\v 37 Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
\v 38 Hamna neno lake likikaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
\s5
\v 39 Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
\v 40 hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
\s5
\v 41 Sipokei sifa kutoka kwa watu,
\v 42 lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.
\s5
\v 43 Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.
\v 44 Je mnawezaje kuamini ninyi ambao mnapokea sifa kutoka kwa kila mmoja wenu lakini hamtafuti sifa itokayo kwa Mungu wa pekee?
\s5
\v 45 Msidhani mimi nitawashitaki mbele za Baba. Anayewashitaki ninyi ni Musa, ambaye ninyi mmeweka matumaini yenu kwake.
\v 46 Kama mngekuwa mnamwamini Musa, mngeniamini mimi kwa sababu aliandika kuhusu habari zangu.
\v 47 Kama hamuamini maandiko yake, mtawezaje kuamini maneno yangu.?
\s5
\c 6
\p
\v 1 Baada ya mambo haya, Yesu alienda pande za Bahari ya Galilaya, pia huitwa Bahari ya Tiberia.
\v 2 Mkutano mkubwa ulikuwa ukimfuata kwa sababu waliona ishara alizozifanya kwa waliokuwa wagonjwa.
\v 3 Yesu alipanda juu hadi upande wa juu wa mlima na akakaa huko na wanafunzi wake
\s5
\v 4 (Na Pasaka, Sikukuu ya Wayahudi ilikuwa imekaribia).
\v 5 Yesu alipoinua macho yake juu na kuona umati mkubwa unakuja kwake, akamwambia Filipo, "Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula"?
\v 6 (Lakini Yesu aliyasema haya kwa Filipo kwa kumjaribu kwa kuwa yeye mwenyewe alijua atakachofanya).
\s5
\v 7 Filipo akamjibu, "Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo."
\v 8 Andrea, mmoja wa wanafunzi wake ndugu yake Simoni Petro akamwambia
\v 9 Yesu, "Kuna mvulana hapa ana mikate mitano na samaki wawili, lakini hii yafaa nini kwa watu wengi namna hii?"
\s5
\v 10 Yesu akawambia, "Waketisheni watu chini" (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini.
\v 11 Kisha Yesu akachukua ile mikate mitano akashukuru akawawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile wavyohitaji.
\v 12 Watu waliposhiba, aliwambia wanafunzi wake, "Vikusanyeni vipande vya mabaki, vilivyobaki ili kwamba kisipotee chochote."
\s5
\v 13 Basi wakakusanya na kujaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri- vipande vilivyosazwa na wale waliokula.
\v 14 Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, "Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni."
\v 15 Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao, alijitenga, tena na akaenda mlimani yeye peke yake.
\s5
\v 16 Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake walishuka kwenda ziwani.
\v 17 Wakapanda kwenye mtumbwi na walikuwa wakivuka kuelekea Kapernaumu. (Giza lilikuwa limeingia na Yesu alikuwa bado hajaja kwao).
\v 18 Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukivuma, na bahari ilikuwa ikendelea kuchafuka.
\s5
\v 19 Tena wanafunzi wake walipokuwa wamepiga makasia kama ishirini na matano au thelathini, wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari kuukaribia mtumbwi, na wakaogopa.
\v 20 Lakini akawambia, "Ni mimi! Msiogope."
\v 21 Tena walikuwa tayari kumbeba kwenye mtumbwi, na mara mtumbwi ulifika kwenye nchi mahali walipokuwa wakienda.
\s5
\v 22 Siku iliyofuata, mkutano uliokuwa umesimama upande wa bahari waliona kuwa hakuna mtumbwi mwingine isipokuwa ule ambayo Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaupanda lakini wanafunzi wake walikuwa wameenda zao wenyewe.
\v 23 (Ingawa, kulikuwa na baadhi ya mitumbwi iliyotoka Tiberia karibu na mahali walipokula mikate baada ya Bwana kutoa shukrani).
\s5
\v 24 Wakati makutano walipotambua kuwa sio Yesu wala wanafunzi wake walikuwa kule, wao wenyewe walipanda ndani ya mitumbwi wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.
\v 25 Baada ya kumpata upande mwingine wa ziwa wakamuuliza, "Rabbi ulikuja lini huku?"
\s5
\v 26 Yesu akawajibu, akawambia, Amini, amini, mnanitafuta mimi, sio kwa sababu mliziona ishara, bali kwa sababu mlikula mikate na kushiba.
\v 27 Acheni kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali mkifanyie kazi chakula kidumucho hata milele kile ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa kuwa Mungu Baba ameweka muhuri juu yake."
\s5
\v 28 Kisha wakamwambia, "Ni nini tunapaswa kufanya ili kuzifanya kazi za Mungu?"
\v 29 Yesu akajibu, "Hii ndiyo kazi ya Mungu: kwamba mmwamini yeye aliyemtuma."
\s5
\v 30 Basi wakamwambia, "Ni ishara zipi utakazofanya, kwamba tunaweza kuziona na kukuamini? Utafanya nini?
\v 31 Baba zetu walikula manna jangwani, kama ilivyo andikwa, "Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale."
\s5
\v 32 Kisha Yesu akawajibu, "Amini, amini, sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni.
\v 33 Kwa kuwa mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupatia uzima ulimwengu.
\v 34 Basi wakamwambia, "Bwana tupatie huu mkate wakati wote."
\s5
\v 35 Yesu akawambia, "Mimi ndiye mkate wa uzima, yeye ajaye kwangu hatapata njaa na yeye aniaminiye hatahisi kiu kamwe."
\v 36 Ingawa niliwaambia kwamba, mmeniona, na bado hamuamini.
\v 37 Wote ambao Baba anaonipa watakuja kwangu, na yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kabisa.
\s5
\v 38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni, sio kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\v 39 Na haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali nitawafufua siku ya mwisho.
\v 40 Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
\s5
\v 41 Kisha wayahudi wakamnung`unikia kumhusu yeye kwa sababu alisema, "Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni."
\v 42 Wakasema, "Huyu siyo Yesu mwana wa Yusuph, ambaye baba yake na mama yake tunamfahamu? Imekuwaje sasa anasema, 'Nimeshuka kutoka mbinguni`?"
\s5
\v 43 Yesu akajibu, akawambia, "Msinung'unikiane miongoni mwenu wenyewe.
\v 44 Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.
\v 45 Kwa kuwa imeandikwa katika manabii, 'Watafundishwa na Mungu.' Kila aliyesikia na amejifunza kutoka kwa Baba, huja kwangu.
\s5
\v 46 Sio kwamba kuna mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu- amemwona Baba.
\v 47 Amini, amini yeye aaminiye anao uzima wa milele.
\s5
\v 48 Mimi ni mkate wa uzima.
\v 49 mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa.
\s5
\v 50 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife.
\v 51 Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu."
\s5
\v 52 Wayahudi wakakasirika wenyewe kwa wenyewe na wakaanza kubishana wakisema, "Mtu huyu anawezaje kutupa mwili wake tuule?"
\v 53 Kisha Yesu akawambia, "Amini, amini, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamta kuwa na uzima ndani yenu.
\s5
\v 54 Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.
\v 55 Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
\v 56 Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake.
\s5
\v 57 Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, na yeye pia ataishi kwa sababu yangu.
\v 58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele.
\v 59 Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.
\s5
\v 60 Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, "Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?"
\v 61 Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza?
\s5
\v 62 Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla?
\v 63 Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima.
\s5
\v 64 Bado kuna watu kati yenu wasioamini." kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti.
\v 65 Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba."
\s5
\v 66 Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena.
\v 67 Yesu akawambia wale kumi na wawili, "Je na ninyi mnataka kuondoka?"
\v 68 Simoni Petro akamjibu, "Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,
\v 69 na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu."
\s5
\v 70 Yesu akawambia, "Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni ibilisi?
\v 71 Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
\v 2 Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
\s5
\v 3 Ndipo ndugu zake walipomwambia, "Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
\v 4 Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu."
\s5
\v 5 Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
\v 6 Ndipo Yesu alipowaambia, "Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
\v 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
\s5
\v 8 Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado."
\v 9 Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
\s5
\v 10 Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
\v 11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, "Yuko wapi?"
\s5
\v 12 Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, "Ni mtu mwema." Wengine walisema, "Hapana, huwapotosha makutano."
\v 13 Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
\s5
\v 14 Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
\v 15 Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, "Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe."
\v 16 Yesu akawajibu na kuwaambia, "Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
\s5
\v 17 Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
\v 18 Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
\s5
\v 19 Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
\v 20 Makutano wakajibu, "Una pepo. Nani anataka kukuua?"
\s5
\v 21 Yesu akajibu na akawaambia, "Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
\v 22 Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahili mtu.
\s5
\v 23 Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
\v 24 Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa haki.
\s5
\v 25 Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, "Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
\v 26 Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
\v 27 Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka."
\s5
\v 28 Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, "Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
\v 29 Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma."
\s5
\v 30 Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\v 31 Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, "Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?"
\v 32 Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.
\s5
\v 33 Ndipo Yesu aliposema, "Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.
\v 34 Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja."
\s5
\v 35 Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, "Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa Waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
\v 36 Ni neno gani hili alilolisema, 'Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja'?"
\s5
\v 37 Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, "Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
\v 38 Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima."
\s5
\v 39 Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
\s5
\v 40 Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, "Kweli huyu ni nabii."
\v 41 Wengine walisema, "Huyu ni Kristo." Lakini wengine walisema, "nini, Kristo aweza kutoka Galilaya?
\v 42 Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?
\s5
\v 43 Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.
\v 44 Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake.
\s5
\v 45 Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, "Kwa nini hamjamleta?"
\v 46 Maofisa wakajibu, "Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla."
\s5
\v 47 Ndipo Mafarisayo walipowajibu, "Na nyinyi pia mmepotoshwa?
\v 48 Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?
\v 49 Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa."
\s5
\v 50 Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),
\v 51 "Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?"
\v 52 Walijibu na kumwambia, "Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya."
\s5
\v 53 (Zingatia: Baadhi ya maneno ya Yohana 7: 53 - 8: 11 hayamo katika nakala bora za kale). Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.
\s5
\c 8
\p
\v 1 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Yesu alienda mlima wa Mizeituni.
\v 2 Mapema asubuhi akaja tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; akakaa na kuwafundisha.
\v 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha kuzini. Wakamweka katikati.
\s5
\v 4 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Ndipo wakamwambia Yesu, "Mwalimu, mwanamke huyu amekamatwa katika uzinzi, katika kitendo kabisa.
\v 5 Sasa, katika sheria, Musa ametuamuru kuwaponda mawe watu kama hawa, unasemaje juu yake?
\v 6 Walisema haya ili kumtega ili kwamba wapate jambo la kumshitaki, lakini Yesu akainama chini akaandika katika ardhi kwa kidole chake.
\s5
\v 7 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Walipoendelea kumwuliza, alisimama na kuwaambia, "Yeye asiyekuwa na dhambi miongoni mwenu, awe wa kwanza kumponda mawe."
\v 8 Akainama tena chini, akaandika katika ardhi kwa kidole chake.
\s5
\v 9 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Waliposikia hayo, waliondoka mmoja baada ya mwingine, kuanzia aliye mzee. Mwishowe Yesu aliachwa peke yake, pamoja na mwanamke aliyekuwa katikati yao.
\v 10 Yesu alisimama na kumwambia, "Mwanamke, waliokushitaki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?"
\v 11 Akasema, "Hakuna hata mmoja Bwana." Yesu akasema, "Hata mimi sikuhukumu. Nenda njia yako; kuanzia sasa na kuendelea usitende dhambi tena."
\s5
\v 12 Tena Yesu akazungumza na watu akisema, "Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeye anifuataye hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya uzima."
\v 13 Mafarisayo wakamwambia, "Unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako siyo wa kweli."
\s5
\v 14 Yesu alijibu akawaambia, "Hata kama nitajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli. Ninajua mahali nilikotoka na kule ninakoenda, lakini ninyi hamjui mahali ninapotoka au kule ninakoenda.
\v 15 Nyinyi mnahukumu kimwili; mimi simhukumu yeyote.
\v 16 Mimi hata nikihukumu, hukumu yangu ni kweli kwa sababu siko peke yangu, bali niko pamoja na baba aliyenituma.
\s5
\v 17 Ndiyo, na katika sheria yenu imeandikwa kwamba ushuhuda wa watu wawili ni kweli.
\v 18 Mimi ndiye ninayejishuhudia, na Baba aliyenituma ananishuhudia."
\s5
\v 19 Wakamwambia, "Baba yako yuko wapi?" Yesu akajibu, "mimi hamnijui wala Baba yangu hammjui; mngelikuwa mnanijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia."
\v 20 Alisema maneno haya akiwa karibu na hazina alipokuwa akifundisha hekaluni, na hakuna hata mmoja aliyemkamata kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\s5
\v 21 Basi akawaambia tena, "Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja."
\v 22 Wayahudi wakasema, "Atajiua mwenyewe, yeye ambaye alisema, 'kule niendako hamuwezi kuja'?"
\s5
\v 23 Yesu akawaambia, "Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa Ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu.
\v 24 Kwa hiyo, naliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu".
\s5
\v 25 Kwa hiyo wakamwambia, "Wewe ni nani?" Yesu akawaambia, Yale niliyowaambia tangu mwanzo.
\v 26 Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa Ulimwengu."
\v 27 Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba.
\s5
\v 28 Yesu akasema, "Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya.
\v 29 Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza."
\v 30 Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi walimwamini.
\s5
\v 31 Yesu akasema kwa wale Wayahudi waliomwamini, "Ikiwa mtakaa katika neno langu, ndipo mtakuwa wanafunzi wangu kweli,
\v 32 nanyi mtaijua kweli, na kweli itawaweka huru."
\v 33 Walimjibu, "Sisi ni uzao wa Ibrahimu na kamwe hatujawahi kwa chini ya utumwa wa yeyote; utasemaje, "Tutawekwa huru?"
\s5
\v 34 Yesu aliwajibu, "Amini, amini, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
\v 35 Mtumwa hakai nyumbani wakati wote; mwana hudumu siku zote.
\v 36 Kwa hiyo, ikiwa Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kabisa."
\s5
\v 37 Ninajua kwamba ninyi ni uzao wa Ibrahimu; mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.
\v 38 Ninasema mambo ambayo nimeyaona pamoja na Baba yangu, na ninyi vile vile mnafanya mambo ambayo mliyasikia kutoka kwa baba yenu."
\s5
\v 39 Walijibu na kumwambia, "Baba yetu ni Abrahamu." Yesu akawaambia, Kama mngelikuwa watoto wa Ibrahimu, mngefanya kazi za Ibrahimu.
\v 40 Hata sasa mnatafuta kuniua, mtu aliyewaambia ukweli kwamba nilisikia kutoka kwa Mungu. Abrahamu hakufanya hivi.
\v 41 Mnafanya kazi za baba yenu." Wakamwambia, "Hatukuzaliwa katika uzinzi, tunaye Baba mmoja, Mungu."
\s5
\v 42 Yesu akawaambia, "Ikiwa Mungu ni Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nimetoka kwa Mungu; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye alinituma.
\v 43 Kwa nini hamyaelewi maneno yangu? Kwa sababu hamuwezi kuvumilia kuyasikia maneno yangu.
\v 44 Ninyi ni wa baba yenu, shetani, na mnataka kuzitenda tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.
\s5
\v 45 Hata sasa, kwa sababu ninasema iliyo kweli, hamniamini.
\v 46 Ni nani kati yenu anayenishuhudia kuwa nina dhambi? ikiwa ninasema iliyo kweli, kwa nini hamniamini?
\v 47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; ninyi hamyasikii kwa sababu ninyi si wa Mungu."
\s5
\v 48 Wayahudi wakamjibu na kumwambia, hatujasema kweli kuwa wewe ni Msamaria na una pepo?"
\v 49 Yesu akajibu, sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.
\s5
\v 50 Sitafuti utukufu wangu; kuna mmoja atafutaye na kuhukumu.
\v 51 Amini, amini, nawaambia, iwapo yeyote atalishika neno langu, hataona mauti kamwe."
\s5
\v 52 Wayahudi wakamwambia, "Sasa tumejua kuwa una pepo. Abrahamu na mabii walikufa; lakini unasema, 'Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti'.
\v 53 Wewe si mkuu kuliko baba yetu Abrahamu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?"
\s5
\v 54 Yesu akajibu, "Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu.
\v 55 Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, 'simjui,' nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika.
\v 56 Baba yenu Abrahamu alishangilia atakavyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi."
\s5
\v 57 Wayahudi wakamwambia,"Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?"
\v 58 Yesu akawaambia, "Amini, amini, nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, MIMI NIKO."
\v 59 Ndipo waliokota mawe wapate kumpiga, lakini Yesu alijificha na akatoka nje ya hekalu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Wakati, kama Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu kipofu tangu kuzaliwa kwake.
\v 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, "Rabi, nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?"
\s5
\v 3 Yesu akawajibu, "Siyo huyu mtu wala wazazi wake waliotenda dhambi, bali kazi za Mungu zipate kufunuliwa kupitia kwake.
\v 4 Tunapaswa kufanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana. Usiku waja wakati ambapo hakuna atakayeweza kufanya kazi.
\v 5 Wakati niwapo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu."
\s5
\v 6 Baada ya Yesu kusema maneno haya, alitema kwenye ardhi, alifanya tope kwa mate, na akampaka yule mtu machoni na lile tope.
\v 7 Akamwambia, nenda kaoge katika kisima cha Siloam (Inayotafsiriwa kama 'aliyetumwa')." Kwa hiyo huyo mtu alienda, akanawa, na akarudi, anaona.
\s5
\v 8 Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji walisema, Je! huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?" wengine walisema, "Ni yeye."
\v 9 Na wengine walisema, "Hapana, bali anafanana naye." Lakini alikuwa akisema, "Ni mimi."
\s5
\v 10 Wakamwambia, "Sasa macho yako yalifunguliwaje?"
\v 11 Alijibu, mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, 'Nenda Siloam ukanawe.' Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena."
\v 12 Wakamwambia, "Yuko wapi?" Alijibu, "Sijui."
\s5
\v 13 Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.
\v 14 Nayo ilikuwa siku ya Sabato wakati Yesu alipotengeneza tope na kuyafumbua macho yake.
\v 15 Ndipo tena Mafarisayo wakamwuliza alipataje kuona. Aliwaambia, "Aliweka tope katika macho yangu, nikanawa, na sasa naweza kuona."
\s5
\v 16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, "Mtu huyu hajatoka kwa Mungu kwa sababu haishiki Sabato." Wengine walisema, "Inawezekanaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?" Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati yao.
\v 17 Ndipo walipomwuliza yule kipofu tena, "Unasemaje juu yake kwa sababu aliyafungua macho yako?" Kipofu akasema, "Ni nabii."
\v 18 Hata wakati huu Wayahudi hawakumwamini kwamba alikuwa kipofu naye amepata kuona mpaka walipowaita wazazi wake yeye aliyepata kuona.
\s5
\v 19 Waliwauliza wazazi, Je, huyu ni mtoto wenu mnayesema alizaliwa kipofu? amewezaje sasa kuona?"
\v 20 Hivyo wazazi wake wakamjibu, "Tunajua kuwa huyu ni mtoto wetu na kwamba alizaliwa kipofu.
\v 21 Jinsi gani sasa anaona, hatujui, na yeye aliyemfumbua macho yake, hatumjui. Mwulizeni yeye. Ni mtu mzima. Anaweza kujieleza mwenyewe."
\s5
\v 22 Wazazi wake walisema mambo haya, kwa sababu waliwaogopa Wayahudi. Kwa vile Wayahudi walikuwa wamekubaliana tayari kuwa, ikiwa yeyote atakiri kuwa Yesu ni Kristo, atatengwa na Sinagogi.
\v 23 Kwa sababu hii, wazazi wake walisema, "Ni mtu mzima, mwulizeni yeye."
\s5
\v 24 Kwa hiyo kwa mara ya pili, walimwita yule mtu aliyewahi kuwa kipofu na kumwambia, "Mpe Mungu utukufu. Tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi."
\v 25 Ndipo yule mtu alijibu, "Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui. Kitu kimoja ninachokijua: nilikuwa kipofu, na sasa ninaona."
\s5
\v 26 Ndipo walipomwambia, "Amekufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?"
\v 27 Alijibu, "Nimekwishawaambia tayari, na nyinyi hamkusikiliza! Kwa nini mnataka kusikia tena? Nanyi hamtaki kuwa wanafunzi wake pia, sivyo?
\v 28 Walimtukana na kusema, "Wewe ni mwanafunzi wake, lakini sisi ni wanafunzi wa Musa.
\v 29 Tunajua kwamba Mungu alizungumza na Musa, lakini kwa huyu mtu, hatujui kule atokako."
\s5
\v 30 Yule mtu akajibu na kuwaambia, "Kwa nini, hili ni jambo la kushangaza, kwamba hamjui anakotoka, na bado ameyafumbua macho yangu.
\v 31 Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.
\s5
\v 32 Tangu kuanza kwa Ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
\v 33 Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote."
\v 34 Walijibu na kumwambia, "Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?" Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
\s5
\v 35 Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, "Unamwamini Mwana wa Mtu?"
\v 36 Alijibu na kusema, "Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?"
\v 37 Yesu akamwambia, "Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye."
\v 38 Yule mtu akasema, "Bwana, Naamini." Ndipo akamsujudia.
\s5
\v 39 Yesu akasema, "Kwa hukumu nimekuja katika Ulimwengu huu ili kwamba wale wasioona wapate kuona na wale wanaoona wawe vipofu."
\v 40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye wakasikia maneno hayo na kumwuliza, "Na sisi pia ni vipofu?"
\v 41 Yesu akawaambia, "Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, 'Tunaona,' dhambi yenu inakaa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
\v 2 Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
\s5
\v 3 Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje.
\v 4 Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.
\s5
\v 5 Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni."
\v 6 Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
\s5
\v 7 Yesu akasema nao tena, "Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
\v 8 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
\s5
\v 9 Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
\v 10 Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
\s5
\v 11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
\v 12 Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
\v 13 Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
\s5
\v 14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
\v 15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
\v 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
\s5
\v 17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
\v 18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba."
\s5
\v 19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
\v 20 Wengi wao wakasema, "Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?"
\v 21 Wengine wakasema, "Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?"
\s5
\v 22 Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
\v 23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
\v 24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, "Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
\s5
\v 25 Yesu akawajibu, "Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
\v 26 Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
\s5
\v 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
\v 28 Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
\s5
\v 29 Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
\v 30 Mimi na Baba tu mmoja."
\v 31 Wakabeba mawe ili wamponde tena.
\s5
\v 32 Yesu akawajibu, "Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?"
\v 33 Wayahudi wakamjibu, "Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu."
\s5
\v 34 Yesu akawajibu, "Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, "Ninyi ni miungu"'?"
\v 35 Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
\v 36 mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'?
\s5
\v 37 "Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
\v 38 Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba."
\v 39 Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.
\s5
\v 40 Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.
\v 41 Watu wengi wakaja kwa Yesu. Waliendelea kusema, "Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli."
\v 42 Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Alitokea Bethania, kijiji cha Mariamu na dada yake Martha.
\v 2 Alikuwa ni Mariamu yule yule aliyempaka Bwana Marhamu na kumfuta miguu yake kwa nywele zake, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa ni mgonjwa.
\s5
\v 3 Ndipo dada hawa walituma ujumbe kwa Yesu na kusema, "Bwana, angalia yule umpendaye anaumwa."
\v 4 Yesu aliposikia alisema, "Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo Ugonjwa."
\s5
\v 5 Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.
\v 6 Aliposikia kuwa Lazaro ni mgonjwa, Yesu alikaa siku mbili zaidi mahali alipokuwa.
\v 7 Ndipo baada ya hili aliwaambia wanafunzi wake, "Twendeni Uyahudi tena."
\s5
\v 8 Wanafunzi wakamwambia, "Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukuponda mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?"
\v 9 Yesu akawajibu, "Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana.
\s5
\v 10 Hata hivyo, ikiwa atatembea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haiko ndani yake."
\v 11 Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini."
\s5
\v 12 Ndipo wanafunzi wakamwambia, "Bwana, kama amelala, ataamka.
\v 13 Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
\v 14 Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, "Lazaro amekufa.
\s5
\v 15 Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake."
\v 16 Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, "Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu."
\s5
\v 17 Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.
\v 18 Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita arobaini na tano hivi.
\v 19 Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.
\v 20 Ndipo Martha aliposikia kuwa Yesu anakuja, alienda kukutana naye, lakini Mariamu aliendelea kukaa nyumbani.
\s5
\v 21 Ndipo Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa.
\v 22 Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia."
\v 23 Yesu akamwambia, kaka yako atafufuka tena."
\s5
\v 24 Martha akamwambia, najua kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho."
\v 25 Yesu akamwambia, "Mimi ni ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;
\v 26 na yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa. Unaamini hili?"
\s5
\v 27 Akamwambia, "Ndiyo, Bwana naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye katika ulimwengu."
\v 28 Alipokwisha kusema hili, alienda zake na kumwita dada yake Mariamu faraghani. Akasema, "Mwalimu yuko hapa na anakuita."
\v 29 Mariamu aliposikia haya, aliinuka kwa haraka na kwenda kwa Yesu.
\s5
\v 30 Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.
\v 31 Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.
\v 32 Ndipo Mariamu, alipofika pale Yesu alipokuwa alimuona na, alianguka chini ya miguu yake na kumwambia, "Bwana, kama ungelikuwa hapa, ndugu yangu asingelikufa."
\s5
\v 33 Yesu alipomuona analia, na Wayahudi waliokuja pamoja naye walikuwa wakilia pia, aliomboleza katika roho na kufadhaika;
\v 34 akasema, "Mmemlaza wapi? wakamwambia, Bwana, njoo utazame."
\v 35 Yesu akalia.
\s5
\v 36 Ndipo Wayahudi wakasema, "Angalia alivyompenda Lazaro!"
\v 37 Lakini wengine kati yao wakasema, "Siyo huyu, mtu aliyeyafumbua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya huyu mtu asife?"
\s5
\v 38 Ndipo Yesu, hali akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.
\v 39 Yesu akasema, "Liondoweni jiwe." Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, "Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne."
\v 40 Yesu akamwambia, "Mimi sikukuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?"
\s5
\v 41 Kwa hiyo wakaliondoa jiwe. Yesu akainua macho yake juu na kusema, "Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikiliza.
\v 42 Nilijua kwamba unanisikia mara zote, lakini ni kwa sababu ya kusanyiko ambalo limesimama kunizunguka kwamba nimesema haya, ili kwamba wapate kuamini kuwa wewe umenituma."
\s5
\v 43 Baada ya kusema haya, alilia kwa sauti kubwa, "Lazaro, toka nje!"
\v 44 Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa." Yesu akawaambia, "Mfungueni mkamwache aende."
\s5
\v 45 Ndipo Wayahudi wengi waliokuja kwa Mariamu na kuona Yesu alichofanya, walimwamini;
\v 46 lakini baadhi yao walienda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo aliyoyafanya Yesu.
\s5
\v 47 Ndipo wakuu wa Makuhani na Mafarisayo wakakusanyika pamoja katika baraza na kusema, "Tutafanya nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi.
\v 48 Ikiwa tutamwacha hivi peke yake, wote watamwamini; Warumi watakuja na kuchukua vyote mahali petu na taifa letu."
\s5
\v 49 Hata hivyo, mtu mmoja kati yao, Kayafa, aliyekuwa kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, " Hamjui chochote kabisa.
\v 50 Hamfikirii kwamba yafaa kwa ajili yenu kwamba mtu mmoja yapasa kufa kwa ajili ya watu kuliko taifa lote kuangamia."
\s5
\v 51 Haya hakuyasema kwa sababu yake mwenyewe, badala yake, kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa;
\v 52 na si kwa taifa peke yake, bali Yesu apate vile vile kuwakusanya watoto wa Mungu ambao wametawanyika sehemu mbali mbali.
\v 53 Kwa hiyo kuanzia siku hiyo na kuendelea wakapanga namna ya kumwua Yesu.
\s5
\v 54 Yesu hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bali aliondoka hapo na kwenda nchi iliyo karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Hapo alikaa na wanafunzi.
\v 55 Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, na wengi wakapanda kwenda Yerusalemu nje ya mji kabla ya Pasaka ili wapate kujitakasa wenyewe.
\s5
\v 56 Walikuwa wakimtafuta Yesu, na kuzungumza kila mmoja walipokuwa wamesimama hekaluni, "Mnafikiri nini? Kwamba hatakuja katika sikukuu?"
\v 57 Wakati huu wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba ikiwa mmoja atajua Yesu alipo, anapaswa kutoa taarifa ili kwamba wapate kumkamata.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu.
\v 2 Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu.
\v 3 Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.
\s5
\v 4 Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi wake, ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
\v 5 "Kwanini manukato haya yasingeuzwa kwa dinari mia tatu na wakapewa maskini?"
\v 6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 7 Yesu alisema, "Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
\v 8 Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote."
\s5
\v 9 Basi umati mkubwa wa Wayahudi walipata kujua ya kuwa Yesu yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila wamwone na Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka katika wafu.
\v 10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri ili wamue Lazaro;
\v 11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walienda zao na wakamwamini Yesu.
\s5
\v 12 Na siku ya pili yake umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
\v 13 walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, "Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli."
\s5
\v 14 Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,
\v 15 "Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda."
\s5
\v 16 Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.
\s5
\v 17 Basi lile kundi la watu waliokuwepo pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, wakashuhudia kwa wengine.
\v 18 Na ilikuwa kwa sababu hii pia kwamba kundi la watu walikwenda kumlaki kwasababu walisikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.
\v 19 Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, "Tazama, sasa hamwezi kufanya lolote; tazama, ulimwengu umekwenda kwake."
\s5
\v 20 Sasa baadhi ya Wayunani walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakienda kuabudu kwenye sikukuu.
\v 21 Hawa walimwendea Filipo, ambaye alitoka Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, "Bwana, sisi tunatamani kumwona Yesu."
\v 22 Filipo akaenda akamwambia Andrea; Andrea na Filipo wakaenda na kumwambia Yesu.
\s5
\v 23 Yesu akawajibu akasema, "Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
\v 24 Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi.
\s5
\v 25 Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele.
\v 26 Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.
\s5
\v 27 Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? 'Baba, uniokoe katika saa hii'? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii.
\v 28 Baba, ulitukuze jina lako." Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, "Nimelitukuza nami nitalitukuza tena."
\v 29 Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, "Malaika amesema naye."
\s5
\v 30 Yesu akajibu na kusema, "Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.
\v 31 Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje.
\s5
\v 32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu."
\v 33 Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.
\s5
\v 34 Mkutano wakamjibu, "Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, 'Mwana Adamu lazima ainuliwe juu'? Huyu Mwana wa Mtu ni nani?"
\v 35 Basi Yesu akawaambia, "Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako.
\v 36 Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru." Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.
\s5
\v 37 Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini
\v 38 ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: "Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?"
\s5
\v 39 Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,
\v 40 "Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya."
\s5
\v 41 Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.
\v 42 Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakatengwa na sinagogi.
\v 43 Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
\s5
\v 44 Yesu akapaza sauti na kusema, "Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi,
\v 45 naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma.
\s5
\v 46 Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
\v 47 Ikiwa mtu yeyote atayasikia maneno yangu lakini asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.
\s5
\v 48 Yeye anikataye mimi na asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
\v 49 Maana mimi sikunena kwa nafsi yangu tu. Bali ni Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
\v 50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi - kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sasa kabla ya sikukuu ya pasaka, kwa sababu Yesu alifahamu kuwa saa yake imefika ambayo atatoka katika dunia hii kwenda kwa baba, akiwa amewapenda watu wake ambao walikuwa duniani, aliwapenda upeo.
\v 2 Na ibilisi alikuwa amewekwa tayari katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.
\s5
\v 3 Yesu alifahamu kuwa baba ameweka vitu vyote katika mikono yake na kwamba ametoka kwa Mungu na alikuwa anakwenda tena kwa Mungu.
\v 4 Aliamka chakulani na akatandika chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.
\v 5 Kisha akatia maji katika bakuli na akaanza kuwaosha miguu wanafunzi wake na kuwafuta na taulo ambayo alijifunga yeye mwenyewe.
\s5
\v 6 Akaja kwa Simoni Petro, na Petro akamwambia, "Bwana, Unataka kuniosha miguu yangu?"
\v 7 Yesu akajibu na kumwambia, "Nifanyalo hulijui sasa, lakini utaelewa baadaye."
\v 8 Petro akamwambia, "Hutaniosha miguu yangu kamwe." Yesu akamjibu, "Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami."
\v 9 Simoni Petro akamwambia, "Bwana, usinioshe miguu yangu tuu, bali pia na mikono na kichwa changu."
\s5
\v 10 Yesu akamwambia, "Yeyote ambaye amekwisha kuoga haitaji kuoga isipokuwa miguu yake, na amekuwa safi mwili wake wote; ninyi mmekuwa safi, lakini si nyote."
\v 11 Kwa kuwa Yesu alijua yule atakaye msaliti; hii ndiyo sababu alisema, si nyote mmekuwa safi."
\s5
\v 12 Wakati Yesu alipokuwa amewaosha miguu yao na akiisha chukua vazi lake na kukaa tena, aliwaambia, "Je Mnaelewa kile ambacho nimewafanyia?
\v 13 Mnaniita mimi "Mwalimu" na Bwana hii mnasema kweli, maana ndivyo nilivyo.
\v 14 Ikiwa mimi Bwana na mwalimu, nimewaosha miguu yenu, ninyi pia imewapasa kuwaosha wenzenu miguu.
\v 15 Kwa kuwa nimewapa mfano ili kwamba ninyi pia mfanye kama mimi nilivyo fanya kwenu.
\s5
\v 16 Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa ni mkuu kuliko yule aliye mtuma.
\v 17 Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda.
\v 18 Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: 'Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.'
\s5
\v 19 Ninawambia hili sasa kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, muweze kuamini kuwa mimi NDIYE.
\v 20 "Amini, amini, nawambia, anipokeaye mimi humpokea ambaye nina mtuma, na yule anipokeaye mimi humpokea yule aliye nituma mimi."
\s5
\v 21 Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, "Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti."
\v 22 Wanafunzi wake wakatazamana, wakishangaa ni kwa ajili ya nani alizungumza.
\s5
\v 23 Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.
\v 24 Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, "Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza."
\v 25 Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, "Bwana, ni nani?"
\s5
\v 26 Kisha Yesu alijibu, "Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia." Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.
\v 27 Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, "Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka."
\s5
\v 28 Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.
\v 29 Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, "Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu," au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.
\v 30 Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje harak; na ilikuwa usiku.
\s5
\v 31 Wakati Yuda alipokuwa ameondoka, Yesu alisema, "Sasa mwana wa Adam ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa katika yeye.
\v 32 Mungu atamtukuza katika yeye mwenyewe, na atamtukuza haraka.
\v 33 Watoto wadogo, niko pamoja nanyi kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama nilivyowambia Wayahudi, 'Niendako, hamuwezi kuja.' sasa nawambia ninyi, pia.
\s5
\v 34 Ninawapa amri mpya, kwamba mpendane; kama mimi nilivyo wapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pia imewapasa kupendana ninyi kwa ninyi.
\v 35 Kwa ajili ya hili watu watatambua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu, ikiwa mna upendo kwa kila mmoja na mwingine."
\s5
\v 36 Simoni Petro alimwambia, "Bwana, unakwenda wapi?" Yesu akajibu, "Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye."
\v 37 Petro akamwambia, "Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako."
\v 38 Yesu akajibu, "Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu."
\s5
\c 14
\p
\v 1 "Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
\v 2 Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi ya kukaa; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.
\v 3 Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo.
\s5
\v 4 Mnajua njia mahali ninakoenda."
\v 5 Tomaso alimwambia Yesu, "Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia?
\v 6 Yesu alimwambia, " Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
\v 7 Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye."
\s5
\v 8 Philipo alimwambia Yesu, "Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha."
\v 9 Yesu akamwambia, "Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba'?
\s5
\v 10 Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.
\v 11 Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa.
\s5
\v 12 Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.
\v 13 Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
\v 14 Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.
\s5
\v 15 Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.
\v 16 Na nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele,
\v 17 Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
\s5
\v 18 Sitawaacha peke yenu; Nitarudi kwenu.
\v 19 Kwa muda kitambo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.
\v 20 Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu.
\s5
\v 21 Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye mmoja ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na Nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake."
\v 22 Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, "Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?
\s5
\v 23 Yesu alijibu akamwambia, "Kama yeyote danipendaye, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.
\v 24 Yeyote ambaye hanipendi mimi, hashiki maneno yangu. Neno ambalo mnasikia siyo langu bali la Baba ambaye alinituma.
\s5
\v 25 Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.
\v 26 Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.
\v 27 Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.
\s5
\v 28 Mlisikia vile nilivyowaambia, 'Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.' Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.
\v 29 Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.
\v 30 Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,
\v 31 lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Mimi ni mzabibu wa huu kweli, na baba yangu ni mkulima wa mzabibu.
\v 2 Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi.
\s5
\v 3 Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.
\v 4 Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu.
\s5
\v 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
\v 6 Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.
\v 7 Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.
\s5
\v 8 Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.
\v 9 Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.
\s5
\v 10 Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.
\v 11 Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.
\s5
\v 12 Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi.
\v 13 Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.
\s5
\v 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.
\v 15 Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba.
\s5
\v 16 Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
\v 17 Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.
\s5
\v 18 Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
\v 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao; Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.
\s5
\v 20 Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, 'Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.' Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, wangelishika la kwenu pia.
\v 21 Watawatendeeni mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.
\v 22 Kama nisingekuja na kuwaambia waambia, wasingalikuwa wamefanya dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
\s5
\v 23 Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.
\v 24 Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.
\v 25 Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: 'Wananichukia mimi bila sababu.'
\s5
\v 26 Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.
\v 27 Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nimewaambia mambo haya ili msiweze kukwazwa.
\v 2 Watawatoa nje ya masinagogi; hakika saa inakuja ambayo kila atakayewaua atafikiri kuwa anafanya kazi njema kwa ajili ya Mungu.
\s5
\v 3 Watawatendea mambo haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi.
\v 4 Nimewaambia mambo haya ili kwamba wakati ukifika wa haya kutokea, mnaweza kuyakumbuka na jinsi nilivyowaambia muweze wao. Sikuwaambia kuhusu mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
\s5
\v 5 Japokuwa, sasa naenda kwa yule aliyenituma; lakini hakuna kati yenu anayeniuliza, "Unaenda wapi?"
\v 6 Kwa sababu nimesema maneno haya kwenu, huzuni imejaa mioyoni mwenu.
\v 7 Hata hivyo, nawaambia ukweli: ni vyema kwenu nikiondoka; kwa maana nisipoondoka, mfariji hatakuja kwen; lakini nikienda ntamtuma kwenu.
\s5
\v 8 Akija, huyo mfariji ataubitisha ulimwengu kuhusiana na dhambi, kuhusiana na haki na kuhusiana na hukumu.
\v 9 Kuhusiana na dhambi, kwa sababu hawakuniamini mimi,
\v 10 kuhusiana na haki, kwa sababu naenda kwa baba, na hamtaniona tena;
\v 11 na kuhusiana na hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa.
\s5
\v 12 Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa.
\v 13 Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atayadhihirisha kwenu mambo yatakayokuja.
\v 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa sababu atayachukua mambo yangu na atayatangaza kwenu.
\s5
\v 15 Vitu vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; kwa hiyo, nimesema kwamba Roho atachukua mambo yangu na atayadhihirisha kwenu.
\v 16 Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi tena, mtaniona."
\s5
\v 17 Baadhi ya wanafunzi wake wakaambizana, "Ni nini anachotuambia, "muda mfupi, na hamtaniona tena,' na, kisha, mda mfupi mtaniona,' na, 'kwa sababu naenda kwa Baba?"
\v 18 Kwa hiyo wakasema, "Ni kitu gani anachosema, 'Bado mda mfupi'? Hatujui asemavyo."
\s5
\v 19 Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, "Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, 'Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona'?
\v 20 Amin, amin, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
\v 21 Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
\s5
\v 22 Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu.
\v 23 Siku hiyo hamtaniuliza maswali. Amin, Amin, nawaambia, Mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu.
\v 24 Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu ikamilike.
\s5
\v 25 Nimezungumza na ninyi kwa lugha isiyoeleweka, lakini saa inakuja ambapo sitazungumza kwa lugha isiyoeleweka lakini badala yake nitawaambia waziwazi kuhusu Baba.
\s5
\v 26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitaomba kwa Baba kwa ajili yenu;
\v 27 Kwa kuwa Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na kwa sababu mmeniamini kuwa nimetoka kwa Baba.
\v 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni; tena, naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba".
\s5
\v 29 Wanafunzi wake wakamwambia, "Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo.
\v 30 Sasa, tunajua kwamba unajua mambo yote, na hauhitaji mtu yoyote akuulize maswali. Kwa sababu hii tunaamini kuwa unatoka kwa Mungu.
\v 31 Yesu akawajibu, "Sasa mmeamini?"
\s5
\v 32 Tazama, saa inakuja, ndiyo na hakika imefika, ambapo mtatawanyika kila mmoja na kwa wa kwao mtaniacha mwenyewe. Lakini siko peke yangu kwa sababu Baba yupo nami.
\v 33 Nawaambia mambo haya ili kwamba ndani yangu muwe na amani. Duniani mna matatizo, lakini jipeni moyo, nimeushinda ulimwengu.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yesu aliyasema mambo haya; kisha akainua macho yake kuelelea mbinguni na akasema, "Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe -
\v 2 kama vile ulivyompatia mamlaka juu ya vyote vyenye mwili ili awape uzima wa milele wale wote uliompatia.
\s5
\v 3 Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo.
\v 4 Nilikutukuza hapa duniani, na kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye.
\v 5 Sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja na wewe mwenyewe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ya ulimwengu kuumbwa.
\s5
\v 6 Nililifunua jina lako kwa watu ulionipa hapa duniani. Walikuwa watu wako; lakini ulinikabidhi mimi. nao wamelishika neno lako.
\v 7 Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,
\v 8 kwa maneno yale uliyonipatia mimi-- Nimekwisha wapatia wao maneno hayo. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\s5
\v 9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.
\v 10 Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.
\v 11 Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa sisi ili wao nao wawe na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo na umoja.
\s5
\v 12 Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.
\v 13 Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
\v 14 Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
\s5
\v 15 Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
\v 16 Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
\v 17 Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
\s5
\v 18 Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
\v 19 Kwa ajili yao mimi mwenyewe ninajitoa kwako ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli.
\s5
\v 20 Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao
\v 21 ili kwamba wao nao wawe na umoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\s5
\v 22 Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa na umoja, kama vile sisi tulivyo umoja -
\v 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.
\s5
\v 24 Baba, kile ulichonipa mimi - Natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.
\s5
\v 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua wewe, lakini mimi nakujua wewe; na wanajua kwamba ulinituma.
\v 26 Nililifanya jina lako lijulikane kwao, na nitalifanya lijulikane ili kwamba lile pendo ambalo kwalo ulinipenda mimi liweze kuwa ndani yao, na mimi niweze kuwa ndani yao."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.
\v 2 Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake.
\v 3 Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.
\s5
\v 4 Naye Yesu, hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, "Ni nani mnayemtafuta?"
\v 5 Nao wakamjibu, "Yesu Mnazareth." Yesu akawaambia, "Mimi ndiye" Naye Yuda aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.
\s5
\v 6 Kwa hiyo alipowaambia, "Mimi ndiye" walirudi kinyume na kuanguka chini.
\v 7 Halafu akawauliza tena, "Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena "Yesu mnazareth."
\s5
\v 8 Yesu akawajibu, "Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende."
\v 9 Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; "Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja."
\s5
\v 10 Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
\v 11 Yesu akamwambia Petro, "Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?"
\s5
\v 12 Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
\v 13 Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.
\v 14 Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
\s5
\v 15 Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;
\v 16 lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
\s5
\v 17 Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, "Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?" Naye akasema, "Mimi siye."
\v 18 Na wale watumishi na wakuu walikuwa wakisimama mahali pale; wamekoka moto wa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.
\s5
\v 19 Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
\v 20 Yesu akamjbu, "Nimeuambia waziwazi ulimwengu; Mimi nilifundisha mara kwa mara kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.
\v 21 Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.
\s5
\v 22 Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa wakuu aliyekuwa amesimama akampiga Yesu kwa mkono wake na kisha akasema, "Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?"
\v 23 Naye Yesu akamjibu, "Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?
\v 24 Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.
\s5
\v 25 Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. "Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?" Akakana akisema "Mimi siye."
\v 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, "Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?"
\v 27 Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.
\s5
\v 28 Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
\v 29 Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. "Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?"
\v 30 Wakamjibu na kumwambia, "Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako."
\s5
\v 31 Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu." Nao Wayahudi wakamwambia, "Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote."
\v 32 Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
\s5
\v 33 Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?"
\v 34 Yesu akamjibu, "Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?"
\v 35 Naye Pilato akamjibu, "Mimi si Myahudi, au sivyo?" Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
\s5
\v 36 Yesu akajibu; "Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa" Basi
\v 37 Pilato akamwambia, "Je, wewe basi u mfalme?" Yesu akajibu, "wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
\s5
\v 38 Pilato akamwambia, "Kweli ni nini?" Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia "Siona katika lolote mtu huyu.
\v 39 Ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi."
\v 40 Kisha walipiga kelele wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba." Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Basi Pilato alimchukua Yesu na kumchapa.
\v 2 Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.
\v 3 Wakamjia na kusema, "Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao.
\s5
\v 4 Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, "Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake."
\v 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, "Tazameni mtu huyu hapa!"
\v 6 Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, "Msulubishe, msulubishe." Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake."
\s5
\v 7 Wayahudi wakamjibu Pilato, "Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu."
\v 8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
\v 9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, "Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
\s5
\v 10 Kisha Pilato akamwambia, "Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?"
\v 11 Yesu akamjibu, "Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa."
\s5
\v 12 Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, "Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cah kaisari."
\v 13 Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.
\s5
\v 14 Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni mfalme wenu huyu hapa!"
\v 15 Wakapiga kelele, "Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!" Pilato akawaambia, "Je, nimsulubishe mfalme wenu?" Naye Kuhani mkuu akajibu, "Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari."
\v 16 Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulibiwe.
\s5
\v 17 Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.
\v 18 Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao.
\s5
\v 19 Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI.
\v 20 Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.
\s5
\v 21 Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, "Usiandike, 'Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi."
\v 22 Naye Pilato akawajibu, "Niliyoandika nimeandika."
\s5
\v 23 Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
\v 24 Kisha wakasemezana wao kwa wao, "Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani." Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura."
\s5
\v 25 Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
\v 26 Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, "Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!"
\v 27 Kisha akamwambia yule mwanfunzi, "Tazama, huyu hapa mama yako. "Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
\s5
\v 28 Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, "Naona kiu."
\v 29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
\v 30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, "Imekwisha." Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
\s5
\v 31 Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
\v 32 Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
\v 33 Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.
\s5
\v 34 Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu.
\v 35 Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini.
\s5
\v 36 Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, "Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa."
\v 37 Tena andiko lingine husema, "Watamtazama yeye waliyemchoma"
\s5
\v 38 Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.
\v 39 Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja.
\s5
\v 40 Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika.
\v 41 Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo.
\v 42 Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
\v 2 Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, "wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza."
\s5
\v 3 Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini.
\v 4 Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza.
\v 5 Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani.
\s5
\v 6 Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale
\v 7 na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake.
\s5
\v 8 Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini.
\v 9 Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu.
\v 10 Kisha wanafunzi wakaenda tena nyumbani kwao.
\s5
\v 11 Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama kaburini akilia, alivyokuwa akiendelea kulia alisimama kisha akatazama kaburini.
\v 12 Akaona malaika wawili wenye sura nyeupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala.
\v 13 Nao wakamwambia, "Mwanamke, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka."
\s5
\v 14 Alipokwisha sema hayo, aligeuka na kumwona Yesu akiwa amesimama. Lakini hakutambua kama huyo alikuwa Yesu.
\v 15 Naye Yesu akamwambia, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Naye huku akidhani kuwa ni mtunza bustani akamwambia, "Bwana, kama ni wewe uliyemchukua, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."
\s5
\v 16 Yesu akamwambia, "Mariamu." Naye akageuka mwenyewe na kumwambia kwa Kiaramu, "Raboni," yaani hii ni kusema, "Mwalimu."
\v 17 Yesu akamwambia, "Usiniguse, kwani bado sijapaa kwenda kwa baba; bali uende kwa ndugu zangu ukawaambie kuwa nitapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."
\v 18 Mariamu Magdalena akaja kuwaambia wanafunzi, "Nimemwona Bwana," na kwamba amemwambia mambo haya.
\s5
\v 19 Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, "Amani iwe kwenu."
\v 20 Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi.
\s5
\v 21 Kisha Yesu akawaambia tena, "Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi."
\v 22 Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
\v 23 Yeyote mmsameheye dhambi, wamesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa."
\s5
\v 24 Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja.
\v 25 Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, "Tumemwona Bwana." Naye akawambia, "Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini."
\s5
\v 26 Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. na akasema, "Amani na iwe nanyi."
\v 27 Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye."
\s5
\v 28 Naye Thomaso akajibu na kumwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu."
\v 29 Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona."
\s5
\v 30 Kisha Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi, ambazo hazijawahi kuandikwa katika kitabu hiki;
\v 31 bali hizi zimeandikwa ili kwamba muweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu, na kwamba muaminipo muwe na uzima katika jina lake.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika Bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe:
\v 2 Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu.
\v 3 Simon Petro akawaambia, "Mimi naenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Sisi, pia tutaenda nawe." Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.
\s5
\v 4 Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu.
\v 5 Kisha Yesu akawambia, "Vijana, mna chochote cha kula?" Nao wakamjibu, "Hapana."
\v 6 Akawambia, "Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi." Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa cha samaki.
\s5
\v 7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, "Ni Bwana." Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini.
\v 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki.
\v 9 Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.
\s5
\v 10 Yesu akawambia, "Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi."
\v 11 Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.
\s5
\v 12 Yesu akawaambia, "Njoni mpate kifungua kinywa." Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, "Wewe ni nani?" Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.
\v 13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki.
\v 14 Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.
\s5
\v 15 Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, "Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?" Petro akajibu, "Ndiyo, Bwana; "Wewe wajua kuwa mimi nakupenda." Yesu akamwambia, "Lisha wanakondoo wangu."
\v 16 Akamwambia mara ya pili, "Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?" Petro akamwambia, "Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. "Yesu akamwambia, "Chunga kondoo wangu."
\s5
\v 17 Akamwambia tena mara ya tatu, "Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?" Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, "Je Wewe wanipenda?" Naye akamwambia, "Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda." Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
\v 18 Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda."
\s5
\v 19 Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, "Nifuate."
\s5
\v 20 Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, "Bwana, ni nani atakayekusaliti?"
\v 21 Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, "Bwana, Huyu mtu atafanya nini?"
\s5
\v 22 Yesu akamjibu, "Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?" Nifuate."
\v 23 Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, "Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?"
\s5
\v 24 Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
\v 25 Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.