sw_ulb_rev/42-MRK.usfm

1256 lines
78 KiB
Plaintext

\id MRK
\ide UTF-8
\h Marko
\toc1 Marko
\toc2 Marko
\toc3 mrk
\mt Marko
\s5
\c 1
\p
\v 1 Huu ni mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
\v 2 Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, "Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako.
\v 3 Sauti ya mtu aitaye nyikani, "Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake".
\s5
\v 4 Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi.
\v 5 Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao.
\v 6 Yohana alikuwa anavaa vazi la manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini.
\s5
\v 7 Alihubiri na kusema, "Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake.
\v 8 Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu."
\s5
\v 9 Ilitokea katika siku hizo kwamba Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, na alibatizwa na Yohana katika mto Yordani.
\v 10 Wakati Yesu alipoinuka kutoka majini, aliona mbingu zimegawanyika wazi na Roho akishuka chini juu yake kama njiwa.
\v 11 Na sauti ilitoka mbinguni, "Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe."
\s5
\v 12 Kisha mara moja Roho akamlazimisha kwenda nyikani.
\v 13 Alikuwako nyikani siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walimhudumia.
\s5
\v 14 Sasa baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alikuja Galilaya akitangaza injili ya Mungu,
\v 15 akisema, "Muda umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini katika injili".
\s5
\v 16 Na akipita kando ya bahari ya Galilaya, alimwona Simoni na Andrea ndugu wa Simoni wakitupa nyavu zao katika bahari, kwa kuwa walikuwa wavuvi.
\v 17 Yesu aliwaambia, "Njoni, nifuateni, na nitawafanya wavuvi wa watu."
\v 18 Na mara moja waliacha nyavu na wakamfuata.
\s5
\v 19 Wakati Yesu alipotembea umbali kidogo, alimwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; walikuwa kwenye mtumbwi wakitengeneza nyavu.
\v 20 Mara aliwaita na wao walimwacha baba yao Zebedayo ndani ya mtumbwi na watumishi waliokodiwa, wakamfuata.
\s5
\v 21 Na walipofika Kaperinaumu, siku ya Sabato, Yesu aliingia kwenye sinagogi na kufundisha.
\v 22 Walilishangaa fundisho lake, kwa vile alikuwa akiwafundisha kama mtu ambaye ana mamlaka na siyo kama waandishi.
\s5
\v 23 Wakati huo huo kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mchafu, na alipiga kelele,
\v 24 akisema, "Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani. Wewe ni Mtakatifu pekee wa Mungu!"
\v 25 Yesu alimkemea pepo na kusema, "Nyamaza na utoke ndani yake!"
\v 26 Na roho mchafu alimwangusha chini na akatoka kwake wakati akilia kwa sauti ya juu.
\s5
\v 27 Na watu wote walishangaa, hivyo wakaulizana kila mmoja, "Hii ni nini? Fundisho jipya lenye mamlaka? Hata huamuru pepo wachafu nao wanamtii!"
\v 28 Na habari kuhusu yeye mara moja zikasambaa kila mahali ndani ya mkoa wote wa Galilaya.
\s5
\v 29 Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.
\v 30 Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake.
\v 31 Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia.
\s5
\v 32 Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, au waliopagawa na pepo.
\v 33 Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango.
\v 34 Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa pepo wengi, bali hakuruhusu pepo kuongea kwa sababu walimjua.
\s5
\v 35 Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.
\v 36 Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta.
\v 37 Walimpata na wakamwambia, "Kila mmoja anakutafuta"
\s5
\v 38 Aliwaambia, "Twendeni mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa."
\v 39 Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea pepo.
\s5
\v 40 Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimsihi; alipiga magoti na alimwambia, "Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi."
\v 41 Akisukumwa na huruma, Yesu alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, "Ninataka. Uwe msafi."
\v 42 Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa safi.
\s5
\v 43 Yesu akamwonya vikali na akamwambia aende mara moja,
\v 44 Alimwambia, "Hakikisha hausemi neno kwa yeyote, lakini nenda, ujionyeshe kwa kuhani, na utoe dhabihu kwa ajili ya utakaso ambayo Musa aliagiza, kama ushuhuda kwao."
\s5
\v 45 Lakini alikwenda na kuanza kumwambia kila mmoja na kueneza neno zaidi hata Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru. Hivyo alikaa mahali pa faragha na watu walikuja kwake kutoka kila mahali.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Aliporudi Kaperinaumu baada ya siku chache, ilisikika kwamba alikuwa nyumbani.
\v 2 Watu wengi sana walikuwa wamekusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya pale mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.
\s5
\v 3 Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.
\v 4 Wakati waliposhindwa kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu ya mahali pale alipokuwa. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
\s5
\v 5 Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, "mwanangu, dhambi zako zimesamehewa."
\v 6 Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,
\v 7 "Anawezaje mtu huyu kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
\s5
\v 8 Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, "Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
\v 9 Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama, chukua kitanda chako, na utembee?'
\s5
\v 10 Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,
\v 11 "Nakuambia wewe, inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako."
\v 12 Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alikwenda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote walishangaa na walimpa Mungu utukufu, na wakasema "Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili."
\s5
\v 13 Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.
\v 14 Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, "Nifuate." Alisimama na kumfuata.
\s5
\v 15 Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.
\v 16 Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, "Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?"
\s5
\v 17 Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, "Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi."
\s5
\v 18 Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, "Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
\v 19 Yesu aliwaambia, "Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga."
\s5
\v 20 Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.
\v 21 Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitabanduka kutoka katika hilo, kipya kubanduka kutoka katika kikuukuu, na kutakuwepo mpasuko mbaya.
\s5
\v 22 Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya."
\s5
\v 23 Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.
\v 24 Na Mafarisayo walimwambia, "Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?"
\s5
\v 25 Aliwaambia, "Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?
\v 26 Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani—na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?"
\s5
\v 27 Yesu alisema, "Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.
\v 28 Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, hata kwa Sabato."
\s5
\c 3
\p
\v 1 Na tena aliingia ndani ya sinagogi na mle palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza.
\v 2 Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili kwamba wamshitaki.
\s5
\v 3 Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, " Inuka na usimame katikati ya umati huu."
\v 4 Kisha akawaambia watu, "Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?" Lakini walibaki kimya.
\s5
\v 5 Akawaangalia kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, "Nyoosha mkono wako". Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.
\v 6 Mafarisayo wakaenda nje na mara wakafanya njama pamoja na Maherode dhidi yake ili kumuua.
\s5
\v 7 Kisha Yesu, pamoja na wanafunzi wake, walienda baharini, na umati mkubwa wa watu uliwafuata ukitokea Galilaya na Uyahudi
\v 8 na kutoka Yerusalemu na kutoka Idumaya na mbele ya Yorodani na jirani ya Tiro na Sidoni, umati mkubwa, uliposikia kila kitu alichokuwa anakifanya, walikuja kwake.
\s5
\v 9 Na aliwaambia wanafunzi wake kuandaa mtubwi mdongo kwa ajili yake kwa sababu ya umati, ili kwamba wasije wakamsonga.
\v 10 Kwa kuwa aliponya wengi, ili kila mtu aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumfikia ili amguse.
\s5
\v 11 Popote roho wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia, na walisema, "Wewe ni Mwana wa Mungu".
\v 12 Aliwaamuru kwa msisitizo wasifanye ajulikane.
\s5
\v 13 Alienda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakaenda kwake.
\v 14 Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri,
\v 15 na kuwa na mamlaka ya kutoa mapepo.
\v 16 Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro,
\s5
\v 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,
\v 18 na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
\v 19 na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.
\s5
\v 20 Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakaja pamoja tena, hata wasiweze kula hata mkate.
\v 21 Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, " Amerukwa na akili".
\v 22 Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, " Amepagawa na Beelzebuli," na, " Kwa mtawala wa mapepo anatoa mapepo".
\s5
\v 23 Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, " Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani?
\v 24 Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
\v 25 Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
\s5
\v 26 Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake.
\v 27 Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga mwenye nguvu kwanza, na kisha kukusanya kilichomo nyumbani.
\s5
\v 28 Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,
\v 29 lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele".
\v 30 Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, "Ana roho chafu".
\s5
\v 31 Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita.
\v 32 Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, "mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe".
\s5
\v 33 Aliwajibu, "Ni nani mama yangu na ndugu zangu?"
\v 34 Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, "Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!
\v 35 Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu".
\s5
\c 4
\p
\v 1 Tena alianza kufundisha kandokando ya bahari. Na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka, akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kukaa. Umati wote walikuwa pembeni mwa bahari ufukweni.
\v 2 Na akawafundisha mambo mengi kwa mifano, na akasema kwao kwa mafundisho yake.
\s5
\v 3 Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda.
\v 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila.
\v 5 Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Mara zikanyauka, kwa sababu hazikuwa na udongo wakutosha.
\s5
\v 6 Lakini jua lilipochomoza, zilinyauka, na kwa sababu hazikuwa na mzizi, zilikauka.
\v 7 Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yeyote.
\s5
\v 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka, zingine zilizaa mara thelathini zaidi, na zingine sitini, na zingine mia".
\v 9 Na akasema, "Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!"
\s5
\v 10 Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mifano.
\v 11 Akasema kwao, "Kwenu mmepewa siri za ufalme wa Mungu. Lakini kwa walio nje kila kitu ni mifano,
\v 12 ili wakitazama, ndiyo hutazama, lakini hawaoni, na kwa hiyo wanaposikia ndiyo husikia, lakini hawaelewi, amasivyo wangegeuka na Mungu angeliwasamehe."
\s5
\v 13 Na akasema kwao, "Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?.
\v 14 Mpanzi alipanda neno.
\v 15 Baadhi ni wale walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao.
\s5
\v 16 Na baadhi ni wale waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa haraka wanalipokea kwa furaha.
\v 17 Na hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda mfupi. Halafu tabu na masumbufu vinapokuja kwa sababu ya neno, mara hujikwaa.
\s5
\v 18 Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno,
\v 19 lakini masumbufu ya dunia, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda.
\v 20 Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia moja."
\s5
\v 21 Yesu akawaambia, " Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango.
\v 22 Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitawekwa wazi.
\v 23 Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!"
\s5
\v 24 Akawaambia, " Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu.
\v 25 Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kutoka kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo."
\s5
\v 26 Na akasema, "Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo.
\v 27 Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea.
\v 28 Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa.
\v 29 Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia."
\s5
\v 30 Na akasema, "tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?.
\v 31 Ni kama mbegu ya haradali, ambapo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani.
\v 32 Hata, wakati imepandwa, inakuana kuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa mbinguni huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake."
\s5
\v 33 Kwa mifano mingi alifundisha na alisema neno kwao, kwa kadiri walivyoweza kuelewa,
\v 34 na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, akawaelezea kila kitu wanafunzi wake.
\s5
\v 35 Katika siku hiyo, wakati wa jioni ulipowadia, akasema kwao, "Twendeni upande wa pili".
\v 36 Hivyo wakauacha umati, wakamchukua Yesu, wakati huo tayari alikuwa ndani ya mtumbwi. Mitumbwi mingine ilikuwa pamoja naye.
\v 37 Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa.
\s5
\v 38 Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, "Mwalimu, haujali sisi tunakufa?"
\v 39 Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, "'Iwe shwari, amani". Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa.
\s5
\v 40 Na akasema kwao, "Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?"
\v 41 Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakasemezana wao kwa wao, " Huyu ni nani tena, kwa sababu hata upepo na bahari vya mtii?".
\s5
\c 5
\p
\v 1 Walikuja mpaka upande mwingine wa bahari, katika mkoa wa Gerasi
\v 2 Na ghafla wakati Yesu alipokuwa akitoka nje ya mtumbwi, mtu mwenye roho chafu alikuja kwake kutoka makaburini.
\s5
\v 3 Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia zaidi, hakuna hata kwa minyororo.
\v 4 Alikuwa amefungwa nyakati nyingi kwa pingu na minyororo. Aliikata minyororo na pingu zake zilivunjwa. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
\s5
\v 5 Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata yeye mwenyewe kwa mawe makali.
\v 6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alikimbilia kwake na kuinama mbele yake.
\s5
\v 7 Alilia kwa sauti kuu, "Wataka nikufanyie nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Ninakusihi kwa Mungu mwenyewe, usinitese."
\v 8 Kwa kuwa alikuwa amemwambia, "Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu."
\s5
\v 9 Naye alimwuliza, "Jina lako ni nani?" Naye alimjibu, "Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi."
\v 10 Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.
\s5
\v 11 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likilishwa juu ya kilima,
\v 12 nao walimsihi, wakisema, "Tutume kwa nguruwe; tuingie ndani yao."
\v 13 Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.
\s5
\v 14 Na wale waliokuwa wakiwalisha nguruwe walikimbia na kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na katika nchi. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.
\v 15 Ndipo walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyepagawa na pepo—aliyekuwa na Jeshi—amekaa chini, amevikwa, na akiwa katika akili yake timamu, nao waliogopa.
\s5
\v 16 Wale waliokuwa wameona kilichotokea kwa mtu aliyekuwa amepagawa na pepo waliwaambia kilichotokea kwake na pia kuhusu nguruwe.
\v 17 Nao walianza kumsihi aondoke katika mkoa wao.
\s5
\v 18 Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.
\v 19 Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, "Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alikufanyia Bwana, na rehema aliyokupa."
\v 20 Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.
\s5
\v 21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari.
\v 22 Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.
\v 23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, " Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili kwamba aweze kupata afya na kuishi."
\v 24 Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati mkubwa ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka.
\s5
\v 25 Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa imetoka kwa miaka kumi na miwili.
\v 26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakusaidika kwa chochote, lakini badala yake alizidi kuwa na hali mbaya.
\v 27 Alisikia habari kuhusu Yesu. Hivyo alikuja nyuma yake wakati alipokuwa akitembea ndani ya umati, naye aliligusa vazi lake.
\s5
\v 28 Kwa kuwa alisema, "Kama nikiyagusa mavazi yake tu, nitakuwa mzima."
\v 29 Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba aliponywa kutoka kwenye mateso yake.
\s5
\v 30 Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Na aligeuka huku na huku katika umati wa watu na kuuliza, "Ni nani aliyeligusa vazi langu?"
\v 31 Wanafunzi wake walimwambia, "Unaona umati huu umekusonga ukikuzunguka, nawe wasema, 'Ni nani aliyenigusa?'"
\v 32 Lakini Yesu alitazama huku na huku kuona ambaye aliyekuwa amefanya hili.
\s5
\v 33 Mwanamke, akijua kilichotokea kwake, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote.
\v 34 Alisema kwake, "Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe kutoka kwenye ugonjwa wako."
\s5
\v 35 Alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakisema, "Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?"
\s5
\v 36 Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, "Usiogope. Amini tu."
\v 37 Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo.
\v 38 Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu, kulia kwingi na kuomboleza.
\s5
\v 39 Alipoingia nyumbani, aliwaambia, "Kwa nini mmesikitika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala."
\v 40 Walimcheka, lakini yeye, aliwatoa wote nje, alimchukua baba wa mtoto na mama na wale waliokuwa pamoja naye, na aliingia ndani alimokuwa mtoto.
\s5
\v 41 Aliuchukua mkono wa mtoto na alimwambia, "Talitha koum," ambayo ni kusema, "Binti mdogo, nakuambia, amka."
\v 42 Ghafla mtoto aliamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa.
\v 43 Aliwaamuru kwa nguvu kwamba hakuna yeyote anapaswa kujua kuhusu hili. Na aliwaambia wampatie yule binti chakula.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao, na wanafunzi wake wakamfuata.
\v 2 Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikia na wakashangazwa. Wakasema, "Amepata wapi mafundisho haya?" "Ni hekima gani hii aliyopewa?" "Anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?"
\v 3 "Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?" Na hawakufurahishwa na Yesu.
\s5
\v 4 Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na miongoni mwa ndugu zake na nyumbani mwake."
\v 5 Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya.
\v 6 Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.
\s5
\v 7 Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,
\v 8 na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni;
\v 9 lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili.
\s5
\v 10 Na akawaambia, "Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.
\v 11 Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao."
\s5
\v 12 Nao wakaenda wakitangaza watu watubu na kuacha dhambi zao.
\v 13 Waliwafukuza pepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.
\s5
\v 14 Mfalme Herode aliposikia hayo, kwa kuwa jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Baadhi walisema, "Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake."
\v 15 Baadhi yao wakasema, "Huyu ni Eliya," Bado wengine wakasema, "Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani."
\s5
\v 16 Lakini Herode aliposikia haya akasema, "Yohana, niliyemkata kichwa amefufuliwa."
\v 17 Maana Herode mwenyewe aliagiza Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake Filipo) kwa sababu yeye alikuwa amemuoa.
\s5
\v 18 Kwa maana Yohana alimwambia Herode, "Si halali kumuoa mke wa kaka yako."
\v 19 Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuua, lakini hakuweza,
\v 20 maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza alihuzunika sana, lakini alifurahi kumsikiliza.
\s5
\v 21 Hata ilipofika wakati mwafaka ikiwa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake karamu, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.
\v 22 Ndipo binti wa Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, "Niombe chochote unachotaka nami nitakupa."
\s5
\v 23 Akamwapia na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu."
\v 24 Akatoka nje akamuuliza mama yake, "Niombe nini?" Akasema, "Kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\v 25 Na mara moja akaingia kwa mfalme akaanza kusema, "Nataka unipatie ndani ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\s5
\v 26 Mfalme alisikitishwa sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake.
\v 27 Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa akiwa kifungoni.
\v 28 Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake.
\v 29 Na wanafunzi wake waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini.
\s5
\v 30 Na mitume, walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.
\v 31 Naye akawaambia, "Njooni wenyewe mahali pa faragha na tupumzike kwa muda." Watu wengi walikuwa wanakuja na kuondoka, hata hawakupata nafasi ya kula.
\v 32 Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha peke yao.
\s5
\v 33 Lakini waliwaona wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa miguu kutoka miji yote, nao wakafika kabla yao.
\v 34 Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.
\s5
\v 35 Muda ulipoendelea sana, wanafunzi wakamjia wakamwambia,"Hapa ni mahali pa faragha na muda umeendelea.
\v 36 Uwaage waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula."
\s5
\v 37 Lakini akawajibu akisema, "Wapeni ninyi chakula." Wakamwambia, "Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?"
\v 38 Akawambia," Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie." walipopata wakamwambia, "Mikate mitano na samaki wawili."
\s5
\v 39 Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi.
\v 40 Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.
\v 41 Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akaibariki kisha akawapa wanafunzi waweke mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili kwa watu wote.
\s5
\v 42 Walikula wote hadi wakatosheka.
\v 43 Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki.
\v 44 Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate.
\s5
\v 45 Mara akawaambia wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.
\v 46 Walipokuwa wamekwisha kuondoka, akaenda mlimani kuomba.
\v 47 Kulipokuwa jioni, na mashua yao wakati huo ikiwa katikati ya bahari, naye alikuwa peke yake nchi kavu.
\s5
\v 48 Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
\v 49 Lakini walipomwona anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu hata wakapiga kelele.
\v 50 kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara akasema nao akawaambia, "Muwe wajasiri! ni mimi! Msiwe na hofu."
\s5
\v 51 Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa kabisa.
\v 52 Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa na uelewa mdogo.
\s5
\v 53 Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.
\v 54 Walipotoka nje ya mashua, mara wakamtambua.
\v 55 Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta wagonjwa kwa machela, kila waliposikia anakuja.
\s5
\v 56 Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na wakamsihi awaruhusu kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Mafarisayo na baadhi ya waandishi ambao walikuwa wametokea Yerusalemu walikusanyika kumzunguka yeye.
\s5
\v 2 Na waliona kuwa baadhi ya wanafunzi wake walikula mkate kwa mikono najisi; ambayo haikuoshwa.
\v 3 (kwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali mpaka wameosha mikono yao vizuri; wanashikilia utamaduni wa wazee. Wakati
\v 4 Mafarisayo wanaporudi kutoka mahali pa soko, hawali mpaka wameoga kwanza. Na kuna sheria zingine ambazo wanazifuata kabisa, ikiwa ni pamoja na kuosha vikombe, masufuria, vyombo vya shaba, na hata viti vinavyotumika wakati wa chakula.)
\s5
\v 5 Mafarisayo na waandishi walimuuliza Yesu, " Kwa nini wanafunzi wako hawaishi kulingana na tamaduni za wazee, kwani wanakula mkate pasipo kunawa mikono?"
\s5
\v 6 Lakini yeye aliwaambia, "Isaya alitabiri vizuri kuhusu ninyi wanafiki, aliandika, 'Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na mimi.
\v 7 Wananifanyia ibaada zisizo na maana, wakifundisha sheria za wanadamu kama mapokeo yao.'
\s5
\v 8 Mmeiacha sheria ya Mungu na kushikilia kwa wepesi tamaduni za wanadamu."
\v 9 Na akasema kwao, "Mmeikataa amri ya Mungu kwa urahisi ili kwamba mtunze tamaduni zenu!
\v 10 Kwa kuwa Musa alisema, 'mheshimu baba yako na mama yako,' na 'Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa.'
\s5
\v 11 Lakini mnasema, 'kama mtu akisema kwa baba yake au mama, "Msaada wowote ambao mngepokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu,"' (hiyo ni kusema kwamba, 'imetolewa kwa Mungu')
\v 12 hivyo haumruhusu kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake.
\v 13 Mnaifanya amri ya Mungu kuwa bure kwa kuleta tamaduni zenu. Na mambo mengi ya jinsi hiyo mnayoyafanya."
\s5
\v 14 Aliwaita makutano tena na kuwaambia, "Mnisikilize mimi, ninyi nyote, na mnielewe.
\v 15 Hakuna chochote kutoka nje ya mtu ambacho chaweza kumchafua mtu kiingiapo kwake. Bali ni kile kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho.
\v 16 (Zingatia: mstari huu, "kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia, na asikie" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 17 Yesu alipowaacha makutano na kuingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu mfano huo.
\v 18 Yesu akasema, "Na ninyi pia bado hamjaelewa? Hamuoni kwamba chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua,
\v 19 kwa sababu hakiwezi kwenda kwenye moyo wake, lakini kinaingia katika tumbo lake na kisha kinapita kwenda chooni." Kwa maelezo haya Yesu alivifanya vyakula vyote kuwa safi.
\s5
\v 20 Alisema, "Ni kile ambacho kinamtoka mtu ndicho kimchafuacho.
\v 21 Kwa kuwa hutoka ndani ya mtu, nje ya moyo, hutoka mawazo maovu, zinaa, wizi, mauaji,
\v 22 uasherati, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, kujamiiana, wivu, kashfa, majivuno, ujinga.
\v 23 Maovu haya yote yanatoka ndani, ndiyo yale yamchafuayo mtu."
\s5
\v 24 Aliamka kutoka pale na kuondoka kwenda katika mkoa wa Tiro na Sidoni. Aliingia ndani na hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa hapo, lakini haikuwezekana kumficha.
\v 25 Lakini ghafla mwanamke, ambaye mtoto wake mdogo alikuwa na roho mchafu, alisikia habari zake, akaja, na akaanguka miguuni pake.
\v 26 Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoeniki. Alimsihi yeye amfukuze pepo kutoka kwa binti yake.
\s5
\v 27 Yesu akamwambia mwanamke, "Waache watoto walishwe kwanza, kwa kuwa sio sawa kuuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa."
\v 28 Lakini mwanamke akamjibu na kusema, "Ndiyo Bwana, hata mbwa chini ya meza hula mabaki ya chakula cha watoto."
\s5
\v 29 Akamwambia, "Kwa kuwa umesema hivi, uko huru kwenda. Pepo ameshamtoka binti yako."
\v 30 Mwanamke alirudi nyumbani kwake na akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo alikuwa amemtoka.
\s5
\v 31 Yesu alitoka tena nje ya mkoa wa Tiro na kupitia Sidoni kuelekea Bahari ya Galilaya mpaka kanda ya Dikapolisi.
\v 32 Na wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, walimsihi Yesu aweke mikono juu yake.
\s5
\v 33 Alimtoa nje ya kusanyiko kwa siri, na akaweka vidole vyake kwenye masikio yake, na baada ya kutema mate, aligusa ulimi wake.
\v 34 Alitazama juu mbinguni, akahema na kumwambia, "Efata," hiyo ni kusema "funguka!"
\v 35 Na muda ule ule masikio yakafunguka, na kilichokuwa kimezuia ulimi kiliharibiwa na akaweza kuongea vizuri.
\s5
\v 36 Na aliwaamuru wasimwambie mtu yeyote. Lakini kadri alivyowaamuru, ndivyo walivyotangaza habari hizo kwa wingi.
\v 37 Hakika walishangazwa, na kusema, "Amefanya kila kitu vizuri. Hata amewafanya viziwi kusikia na mabubu kuongea."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,
\v 2 "Ninauhurumia umati huu, wameendelea kuwa nami kwa siku tatu na hawana chakula.
\v 3 Nikiwatawanya warudi majumbani kwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana."
\v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, "Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwashibisha watu hawa katika eneo hili lililoachwa?"
\s5
\v 5 Akawauliza, "mna vipande vingapi vya mikate?" Wakasema, "Saba".
\v 6 Aliuamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.
\s5
\v 7 Pia walikuwa na samaki wadogo wachache, na baada ya kushukuru, aliwaamuru wanafunzi wake wawagawie hivi pia.
\v 8 Walikula na wakatosheka. Na walikusanya vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba.
\v 9 Walikaribia watu elfu nne. Na aliwaacha waende.
\v 10 Mara aliingia kwenye mashua na wanafunzi wake, na wakaenda katika ukanda ya Dalmanuta.
\s5
\v 11 Kisha Mafarisayo walitoka nje na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, kwa kumjaribu.
\v 12 Akatafakari kwa kina moyoni mwake akasema, "Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki."
\v 13 Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.
\s5
\v 14 Wakati huo wanafunzi walisahau kuchukua mikate. Hawakuwa na mikate zaidi ya kipande kimoja kilichokuwa kwenye mashua.
\v 15 Aliwaonya na kusema, "Muwe macho na mjilinde dhidi ya chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.
\s5
\v 16 Wanafunzi wakasemezana wao kwa wao, "Ni kwa sababu hatuna mikate."
\v 17 Yesu alilitambua hili, na akawaambia, "Kwa nini mnasemezana kuhusu kutokuwa na mikate? Hamjajua bado? Hamuelewi? Mioyo yenu imekuwa miepesi?
\s5
\v 18 Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?
\v 19 Nilipoigawanya mikate mitano kwa watu elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?" Wakamjibu, "kumi na mbili."
\s5
\v 20 "Na nilipoigawanya mikate saba kwa watu elfu nne, mlichukua vikapu vingapi?"
\v 21 Wakasema, "Saba." Akawaambia, "Bado hamuelewi?"
\s5
\v 22 Wakaja Bethsaida. Watu hao walimleta kwa Yesu mtu kipofu na wakamsihi Yesu amguse.
\v 23 Yesu akamshika kwa mkono yule kipofu, na kumwongoza nje ya kijiji. Alipotema mate juu ya macho yake na kunyosha mikono yake juu yake, alimuuliza, "Unaona chochote?"
\s5
\v 24 Alitazama juu na kusema, "Naona watu wanaonekana kama miti inatembea."
\v 25 Ndipo akanyosha tena mikono yake juu ya macho yake, mtu yule akafungua macho yake, aliona tena, na akaona kila kitu vizuri.
\v 26 Yesu alimwacha aende nyumbani na akamwambia, "Usiingie mjini."
\s5
\v 27 Yesu aliondoka na wanafunzi wake kwenda vijiji vya Kaiseria ya Filipi. Wakiwa njiani aliwauliza wanafunzi, "Watu wanasema mimi ni nani?"
\v 28 Wakamjibu wakasema, "Yohana mbatizaji. Wengine wanasema, 'Eliya' na wengine, 'Mmoja wa Manabii."
\s5
\v 29 Akawauliza, "Lakini ninyi mnasema mimi ni nani?" Petro kamwambia, "Wewe ni Kristo."
\v 30 Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye.
\s5
\v 31 Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na viongozi na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.
\v 32 Alisema haya kwa uwazi. Ndipo Petro akamchukua pembeni na akaanza kumkemea.
\s5
\v 33 Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na akamkemea Petro na kusema, "Pita nyuma yangu Shetani! Hujali mambo ya Mungu, isipokuwa mambo ya watu."
\v 34 Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, "Kama kuna mtu anataka kunifuata, ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake, na anifuate.
\s5
\v 35 Kwa kuwa yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, atayaokoa.
\v 36 Inamfaidia nini mtu, kupata ulimwengu wote, na kisha kupata hasara ya maisha yake?
\v 37 Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake?
\s5
\v 38 Yeyote anioneaye aibu na maneno yangu katika kizazi hiki cha wazinzi na kizazi cha wenye dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea aibu atakapokuja katika ufalme wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Na alisema kwao, "Hakika nasema kwenu, baadhi yenu kuna watu waliosimama hapa hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu."
\v 2 Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye mlimani, pekee yao. Ndipo alianza kubadilika mbele yao.
\v 3 Mavazi yake yakaanza kung'aa sana, meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani.
\s5
\v 4 Ndipo Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu.
\v 5 Petro alijibu akamwambia Yesu, "Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya."
\v 6 (Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana.)
\s5
\v 7 Wingu lilitokea na kuwafunika. Ndipo sauti ikatoka mawinguni ikisema, " Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye."
\v 8 Ghafla, walipokuwa wakitazama, hawakumuona yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu.
\s5
\v 9 Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.
\v 10 Ndipo waliyatunza mambo wao wenyewe. Lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake "kufufuliwa kutoka kwa wafu"
\s5
\v 11 Walimwuliza Yesu,"Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?"
\v 12 Akawaambia, "hakika Eliya atakuja kwanza kuokoa vitu vyote. Kwa nini imeandikwa Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi na achukiwe?
\v 13 Lakini nasema kwenu Eliya alikwisha kuja, na walimfanya kama walivyopenda, kama vile maandiko yasemavyo kuhusu yeye."
\s5
\v 14 Na waliporudi kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na Masadukayo walikuwa wanabishana nao.
\v 15 Na mara walipomwona, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia.
\v 16 Aliwauliza wanafunzi wake, "Mnabishana nao juu ya nini?"
\s5
\v 17 Mmoja wao katika kundi alimjibu, "Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu ambayo humfanya asiweze kuongea,
\v 18 na humsababishia kutetemeka na kumwangusha chini, na kutoka povu mdomoni na kusaga meno na kukakamaa. Niliwaomba wanafunzi wako kumtoa pepo, lakini hawakuweza.
\v 19 Aliwajibu, "Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi kwa muda gani? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni kwangu."
\s5
\v 20 Walimleta mtoto wake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.
\v 21 Yesu alimwuliza baba yake, "Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?" Baba alisema, " Tangu utoto.
\v 22 Mara nyingine huanguka katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie."
\s5
\v 23 Yesu alimwambia, "Kama uko tayari? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye."
\v 24 Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, " Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu."
\v 25 Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, "wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru mwache, usiingie kwake tena."
\s5
\v 26 Alilia kwa nguvu na kumhangaisha mtoto na roho alimtoka. Mtoto alionekana kama amekufa, Ndipo wengi walisema, "Amekufa,"
\v 27 Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mtoto alisimama.
\s5
\v 28 Wakati Yesu alipoingia ndani, wanafunzi wake walimwuliza faragha, "Kwa nini hatukuweza kumtoa?"
\v 29 Aliwaambia, " kwa namna hii hatoki isipokuwa kwa maombi."
\s5
\v 30 Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,
\v 31 kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, "Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena."
\v 32 Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza.
\s5
\v 33 Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani"?
\v 34 Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
\v 35 Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, "Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote."
\s5
\v 36 Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema,
\v 37 "Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma."
\s5
\v 38 Yohana alimwambia, "Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati."
\v 39 Lakini Yesu alisema, "Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
\s5
\v 40 Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
\v 41 Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
\s5
\v 42 Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.
\v 43 Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto "usiozimika".
\v 44 (Zingatia: Mstari hii, "Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika." haumo katika nakala za kale).
\s5
\v 45 Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili.
\v 46 (Zingatia: Mstari huu, "Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 47 Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu.
\v 48 Mahali palipo na funza wasiokufa, na moto usiozimika.
\s5
\v 49 Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto.
\v 50 Chumvi ni nzuri, kama chumvi ikipoteza ladha yake, utaifanyaje iwe na ladha yake tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe, na muwe na amani kwa kila mmoja."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.
\v 2 Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, "Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?"
\v 3 Yesu akawajibu, "Musa aliwaamuru nini?"
\v 4 Wakasema, "Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke."
\s5
\v 5 "Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii," Yesu aliwaambia.
\v 6 "Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.'
\s5
\v 7 Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,
\v 8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
\v 9 Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."
\s5
\v 10 Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.
\v 11 Akawaambia, "Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.
\v 12 Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi."
\s5
\v 13 Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
\v 14 Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, "Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
\s5
\v 15 Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 16 Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.
\s5
\v 17 Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima ya milele?"
\v 18 Na Yesu akasema, "Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.
\v 19 Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'."
\s5
\v 20 Mtu yule akasema, "Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana."
\v 21 Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, "Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. Ndipo uje unifuate."
\v 22 Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondoka akiwa mwenye huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
\s5
\v 23 Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, "Ni jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 24 Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, "Watoto, ni jinsi gani ilivyo vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 25 Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 26 Walishangazwa sana na wakasemezana, "Hivyo nani ataokoka"
\v 27 Yesu akawaangalia na kusema, " Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana."
\v 28 "Petro akaanza kuzungumza naye, "Angalia tumeacha vyote na tumekufuata."
\s5
\v 29 Yesu akasema, "Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
\v 30 ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.
\v 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."
\s5
\v 32 Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaambia ambacho kitamtokea hivi karibuni:
\v 33 "Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
\v 34 Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka."
\s5
\v 35 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, "Mwalimu, tunakuhitaji utufanyie chochote tukuombacho."
\v 36 Aliwaambia, "Mnataka niwatendee nini?"
\v 37 Wakasema, "Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto."
\s5
\v 38 Lakini Yesu aliwajibu, "Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?"
\v 39 Wakamwambia, "Tunaweza" Yesu akawaambia, "Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.
\v 40 Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa."
\s5
\v 41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.
\v 42 Yesu akawaita kwake na kusema, "Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala, na watu wao mashuhuri huwaonyesha mamlaka juu yao."
\s5
\v 43 Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,
\v 44 na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.
\v 45 Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi."
\s5
\v 46 Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
\v 47 Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
\v 48 Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
\s5
\v 49 Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, "Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita."
\v 50 Akalitupa pembeni koti lake, akakimbia zaidi, na kuja kwa Yesu.
\s5
\v 51 Yesu akamjibu na kusema, "Unataka nikufanyie nini?" Yule mwanaume kipofu akamjibu, "Mwalimu, ninataka kuona."
\v 52 Yesu akamwambia, "Nenda. Imani yako imekuponya." Hapo hapo macho yake yakaona; na akamfuata Yesu barabarani.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Wakati huo walipokuja Yerusalemu, walipokaribia Besthfage na Bethania, katika Mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake
\v 2 na aliwaambia, "Nendeni katika kijiji kinachokabiliana nasi. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu.
\v 3 Na kama yeyote akiwaambia, 'Kwa nini mnafanya hivi'?, mnapaswa kusema, 'Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa'."
\s5
\v 4 Walikwenda na kumkuta mwanapunda amefungwa nje mlangoni kwenye mtaa ulio wazi, nao walimfungua.
\v 5 Na baadhi ya watu walikuwa wamesimama pale na waliwaambia, "Mnafanya nini, kumfungua mwanapunda huyo?"
\v 6 Waliwaambia kama Yesu alivyowaambia, na watu wakawaacha waende.
\s5
\v 7 Wanafunzi wawili walimleta mwanapunda kwa Yesu na walitandika mavazi yao juu yake ili Yesu aweze kumpanda.
\v 8 Watu wengi wakatandika mavazi yao barabarani, na wengine wakatandika matawi waliyoyakata kutoka mashambani.
\v 9 Wale waliokwenda mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, "Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.
\v 10 Ubarikiwe ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Hosana kwa aliye juu"
\s5
\v 11 Ndipo Yesu aliingia Yerusalemu na alikwenda hekaluni na alitazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alikwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili.
\v 12 Siku iliyofuata, wakati walipokuwa wakirudi kutoka Bethania, alikuwa na njaa.
\s5
\v 13 Na akaona mti wa mtini uliokuwa na majani kwa mbali, alikwenda kutazama kama angeweza kupata chochote juu yake. Na wakati alipokwenda kwa huo, hakupata chochote isipokuwa majani, kwa kuwa haikuwa majira ya mtini.
\v 14 Aliuambia, "Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena". Na wanafunzi wake wakasikia.
\s5
\v 15 Walikuja Yerusalemu, naye aliingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Alizipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
\v 16 Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa.
\s5
\v 17 Aliwafundisha na akasema, "Je haikuandikwa, 'nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote'? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi".
\v 18 Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwua. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake.
\v 19 Na kila wakati jioni ilipofika, waliondoka mjini.
\s5
\v 20 Walipokuwa wakitembea asubuhi, waliuona mti wa mtini umekauka mpaka kwenye mizizi yake.
\v 21 Petro alikumbuka na kusema, "Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka".
\s5
\v 22 Yesu aliwajibu, "Muwe na imani katika Mungu.
\v 23 Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya.
\s5
\v 24 Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu.
\v 25 Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.
\v 26 (Zingatia: Mstari huu, "Lakini msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatasamehe dhambi zenu" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 27 Walikuja Yerusalemu tena. Na Yesu alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu, waandishi na wazee walikuja kwake.
\v 28 Walimwambia, "Kwa mamlaka gani unafanya mambo haya?" Na ni nani aliyekupa mamlaka kuyafanya haya?"
\s5
\v 29 Yesu aliwaambia, "Nitawauliza swali moja. Niambieni na mimi nitawaambia kwa mamlaka gani ninayafanya mambo haya.
\v 30 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au ulitoka kwa wanadamu? Nijibuni."
\s5
\v 31 Walijadiliana miongoni mwao na kushindana na kusema, "Kama tukisema, 'Kutoka mbinguni,' atasema, 'Kwa nini basi hamkumwamini?'
\v 32 Lakini kama tukisema, 'Kutoka kwa wanadamu,'..." Waliwaogopa watu, kwa kuwa wote walishikilia kwamba Yohana alikuwa Nabii.
\v 33 Ndipo walimjibu Yesu na kusema, "Hatujui. Ndipo Yesu akawaambia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nayafanya mambo haya.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, "Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.
\v 2 Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.
\v 3 Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.
\s5
\v 4 Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu.
\v 5 Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua.
\s5
\v 6 Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, "Watamheshimu mwanangu".
\v 7 Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, "Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu."
\s5
\v 8 Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.
\v 9 Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.
\s5
\v 10 Hamjapata kusoma andiko hili? "Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.
\v 11 Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu."
\v 12 Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.
\s5
\v 13 Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.
\v 14 Walipofika, wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?
\v 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, "Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama."
\s5
\v 16 Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, "Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, "Ya Kaisari."
\v 17 Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu." Wakamstaajabia.
\s5
\v 18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
\v 19 "Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
\s5
\v 20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
\v 21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
\v 22 Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa.
\v 23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake."
\s5
\v 24 Yesu aliwaambia, "Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?"
\v 25 Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
\s5
\v 26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?'
\v 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka."
\s5
\v 28 Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, "Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?"
\v 29 Yesu alimjibu, "Iliyo ya muhimu ni hii, "Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
\v 30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.'
\v 31 Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi."
\s5
\v 32 Mwandishi akasema, "Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.
\v 33 Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza."
\v 34 Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, "Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu." Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.
\s5
\v 35 Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, "Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
\v 36 Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.'
\v 37 Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?" Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
\s5
\v 38 Katika mafundisho yake Yesu alisema, "Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko
\v 39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu.
\v 40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu."
\s5
\v 41 Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.
\v 42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.
\s5
\v 43 Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, "Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.
\v 44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, "Mwalimu, tazama mawe haya yakushangaza na majengo!"
\v 2 Akamwambia, Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini".
\s5
\v 3 Naye alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni nyuma ya hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri,
\v 4 "Tuambie, mambo haya yatakuwa lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?"
\s5
\v 5 Yesu alianza kuwaambia, "Kuweni makini kwamba mtu yoyote asiwapotoshe.
\v 6 Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, 'Mimi ndiye', na watawapotosha wengi.
\s5
\v 7 Mtakaposikia vita na tetesi za vita, msiogope; mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho bado.
\v 8 Taifa litainuka kinyume na taifa jingine, na ufalme kinyume na ufalme. Patakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali, na njaa. Huu ni mwanzo wa utungu.
\s5
\v 9 Iweni macho. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapingwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao.
\v 10 Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.
\s5
\v 11 Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Ndani ya muda huo, mtapewa nini cha kusema; hamtakuwa ninyi mtakaoongea, bali Roho Mtakatifu.
\v 12 Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa, baba na mtoto wake. Watoto watasimama kinyume cha baba zao na kuwasababisha kuuawa.
\v 13 Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.
\s5
\v 14 Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama pale lisipotakiwa kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yuda wakimbilie milimani,
\v 15 naye aliyeko juu ya nyumba asishuke chini ya nyumba, au kuchukua chochote kilichoko nje,
\v 16 na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.
\s5
\v 17 Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo!
\v 18 Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi.
\v 19 Kwani patakuwa na mateso makubwa, ambayo hayajawahi kutokea, tangu Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka sasa, hapana, wala haitatokea tena.
\v 20 Mpaka Bwana atakapopunguza siku, hakuna mwili utakaookoka, lakini kwa ajili ya wateule, atakaowachagua, atapunguza namba za siku.
\s5
\v 21 Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yuko hapa!' au 'Tazama, yuko pale!' msiamini.
\v 22 Kwani Wakristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule.
\v 23 Iweni macho! Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.
\s5
\v 24 Lakini baada ya mateso ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake,
\v 25 nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika.
\v 26 Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu.
\v 27 Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
\s5
\v 28 Kwa mtini jifunzeni. Kama tawi liwezavyo kutoa na kuweka haraka majani yake, ndipo mtajua kwamba kiangazi kiko karibu.
\v 29 Ndivyo ilivyo, mtakapoona mambo haya yakitokea, jueni kwamba yuko karibu, na malango.
\s5
\v 30 Kweli, nawambieni, hiki kizazi hakitapita mbali kabla mambo haya hayajatokea.
\v 31 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\v 32 Lakini kuhusu siku hiyo au saa, hakuna ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
\s5
\v 33 Iweni macho, Tazama, kwa sababu hamjui ni muda gani yatatokea. (Zingatia: Mstari huu, "Muwe waangalifu, Tazameni na ombeni kwa sababu..." haumo kwenye nakala za kale).
\v 34 Ni kama mtu anayeenda safarini: akaacha nyumba yake, na kumweka mtumwa wake kuwa mtawala wa nyumba, kila mmoja na kazi yake. Na kumwamuru mlinzi kukaa macho.
\s5
\v 35 Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi.
\v 36 Kama akija ghafla, asikukute umelala.
\v 37 Kile nikisemacho kwako nakisema kwa kila mtu: Kesheni"!
\s5
\c 14
\p
\v 1 Ilikuwa siku mbili tu baada ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta namna ya kumkamata Yesu kwa hila na kumuua.
\v 2 Kwa kuwa walisema, "Sio wakati huu wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia."
\s5
\v 3 Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake.
\v 4 Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Waliambiana wao kwa wao wakisema, "Ni nini sababu ya upotevu huu?
\v 5 Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini." Nao walimkemea.
\s5
\v 6 Lakini Yesu alisema, "Mwacheni peke yake. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu.
\v 7 Siku zote maskini mnao, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote.
\v 8 Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.
\v 9 Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.
\s5
\v 10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa wakuu wa makuhani ili kwamba apate kumkabidhi kwao.
\v 11 Wakati wakuu wa Makuhani waliposikia hivyo, walifurahi na wakaahidi kumpa fedha. Alianza kutafuta nafasi ya kumkabidhi kwao.
\s5
\v 12 Katika siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu, wakati walipotoa mwanakondoo wa pasaka, wanafunzi wake walimwambia, "Unataka twende wapi tukaandae ili upate kula mlo wa Pasaka?"
\v 13 Aliwatuma wanafuzi wake wawili na kuwaambia, "Nendeni mjini, na mwanamume ambaye amebeba mtungi ataonana nanyi. Mfuateni.
\v 14 Nyumba atakayoingia, mfuateni na mmwambie mwenye nyumba hiyo, 'Mwalimu asema, "Kiko wapi chumba cha wageni mahali nitakapokula Pasaka na wanafunzi wangu?"
\s5
\v 15 Atawaonesha chumba cha juu kikubwa chenye samani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale."
\v 16 Wanafunzi waliondoka wakaenda mjini; walikuta kila kitu kama alivyokuwa amewaambia, na wakaandaa mlo wa Pasaka.
\s5
\v 17 Wakati ilipokuwa jioni, alikuja na wale Kumi na wawili.
\v 18 Na walipokuwa wakiikaribia meza na kula, Yesu alisema, "Kweli nawaambia, mmoja kati yenu anayekula pamoja nami atanisaliti."
\v 19 Wote walisikitika, na mmoja baada ya mwingine walimwambia, "Hakika siyo mimi?"
\s5
\v 20 Yesu alijibu na kuwaambia, "Ni mmoja wa Kumi na wawili kati yenu, mmoja ambaye sasa anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.
\v 21 Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake. Lakini ole wake mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa! Ingekuwa vizuri zaidi kwake kama mtu yule asingezaliwa."
\s5
\v 22 Na walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, akaubariki, na kuumega. Aliwapa akisema, "Chukueni. Huu ni mwili wangu."
\v 23 Alichukua kikombe, akashukuru, na akawapatia, na wote wakakinywea.
\v 24 Aliwaambia, "Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi.
\v 25 Kweli nawaambia, sitakunywa tena katika zao hili la mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 26 Walipokwisha kuimba wimbo, walikwenda nje katika Mlima wa Mizeituni.
\v 27 Yesu aliwaaambia, "Ninyi nyote mtajitenga mbali kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, 'Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.'
\s5
\v 28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia mbele yenu Galilaya."
\v 29 Petro alimwambia, "Hata kama wote watakuacha, mimi sitakuacha."
\s5
\v 30 Yesu alimwambia, "Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu."
\v 31 Lakini Petro alisema, "Hata itanilazimu kufa pamoja nawe, sitakukana." Wote walitoa ahadi ile ile.
\s5
\v 32 Walikuja kwenye eneo lililoitwa Gethsemane, na Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa wakati nasali."
\v 33 Aliwachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye, akaanza kuhuzunika na kutaabika sana.
\v 34 Aliwaambia, "Nafsi yangu ina huzuni sana, hata kufa. Bakini hapa na mkeshe."
\s5
\v 35 Yesu alienda mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba, kama ingewezekana, kwamba saa hii ingemwepuka.
\v 36 Alisema, "Aba, Baba, Mambo yote kwako yanawezekana. Niondolee kikombe hiki. Lakini siyo kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako."
\s5
\v 37 Alirudi na kuwakuta wamelala, na akamwambia Petro, "Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?
\v 38 Kesheni na muombe kwamba msije mkaingia katika majaribu. Hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
\v 39 Alienda tena na kuomba, na alitumia maneno yaleyale.
\s5
\v 40 Alikuja tena akawakuta wamelala, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito na hawakujua nini cha kumwambia.
\v 41 Alikuja mara ya tatu na kuwaambia, "Bado mmelala na kupumzika? Yatosha! Saa imefika. Tazama! Mwana wa Adamu atasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
\v 42 Amkeni, twendeni. Tazama, yule anayenisaliti yuko karibu."
\s5
\v 43 Mara tu alipokuwa bado anaongea, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, alifika, na kundi kubwa kutoka kwa wakuu wa makuhani, waandishi na wazee wenye mapanga na marungu.
\v 44 Wakati huo msaliti wake alikuwa amewapa ishara, akisema, Yule nitakayembusu, ndiye. Mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi."
\v 45 Wakati Yuda alipofika, moja kwa moja alienda kwa Yesu na kusema, "Mwalimu!" Na akambusu.
\v 46 Kisha wakumtia chini ya ulinzi na kumkamata.
\s5
\v 47 Lakini mmoja kati yao aliyesimama karibu naye alichomoa upanga wake akampiga mtumishi wa kuhani mkuu na kumkata sikio.
\v 48 Yesu aliwaambia, "Mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama mnyang'anyi?
\v 49 Wakati kila siku nilikuwa nanyi na nikifundisha hekaluni, hamkunikamata. Lakini hili limefanyika ili maandiko yatimie.
\v 50 Na wale wote waliokuwa na Yesu walimwacha na kukimbia.
\s5
\v 51 Kijana mmoja alimfuata, aliyekuwa amevaa shuka tu aliyokuwa amejifunika kumzunguka; walimkamata lakini
\v 52 aliwaponyoka akaiacha shuka pale akakimbia uchi.
\s5
\v 53 Walimwongoza Yesu kwa kuhani mkuu. Pale walikusanyika pamoja naye makuhani wakuu wote, wazee, na waandishi.
\v 54 Petro naye alimfuata Yesu kwa mbali, kuelekea kwenye ua wa kuhani mkuu. Aliketi pamoja na walinzi, waliokuwa karibu na moto wakiota ili kupata joto.
\s5
\v 55 Wakati huo makuhani wakuu wote na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua. Lakini hawakuupata.
\v 56 Kwa kuwa watu wengi walileta ushuhuda wa uongo dhidi yake, lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\s5
\v 57 Baadhi walisimama na kuleta ushahidi wa uongo dhidi yake; wakisema,
\v 58 "Tulimsikia akisema, 'Nitaliharibu hekalu hili lililotengenezwa kwa mikono, na ndani siku tatu nitajenga lingine lisilotengenezwa kwa mikono.'"
\v 59 Lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\s5
\v 60 Kuhani mkuu alisimama katikati yao na akamwuliza Yesu, "Je, huna jibu? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?"
\v 61 Lakini alikaa kimya na hakujibu chochote. Mara Kuhani mkuu alimwuliza tena, "Je wewe ni Kristo, mwana wa Mbarikiwa?"
\v 62 Yesu alisema, "Mimi ndiye. Na utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa nguvu akija na mawingu ya mbinguni."
\s5
\v 63 Kuhani mkuu alirarua mavazi yake na kusema, "Je, bado tunahitaji mashahidi?
\v 64 Mmesikia kufuru. Uamuzi wenu ni upi?" Na wote walimhukumu kama mmoja aliyestahili kifo.
\v 65 Baadhi wakaanza kumtemea mate na kumfunika uso na kumpiga na kumwambia, "Tabiri!" Maafisa walimchukua na kumpiga.
\s5
\v 66 Na Petro alipokuwa bado yuko chini uani, mtumishi mmoja wa wasichana wa kuhani mkuu alikuja kwake.
\v 67 Alimwona Petro alipokuwa amesimama akiota moto, na alimtazama kwa kumkaribia. Kisha alisema, "Nawe pia ulikuwa na Mnazareti, Yesu".
\v 68 Lakini alikataa, akisema, "Sijui wala sielewi kuhusu kile unachosema!" Kisha alitoka akaenda nje uani. (Zingatia; Mstari huu, "Na jogoo akawika" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 69 Lakini mtumishi wa kike pale, alimwona na alianza kuwaambia tena wale ambao walikuwa wamesimama pale, "Mtu huyu ni mmoja wao!"
\v 70 Lakini alikana tena. Baadaye kidogo wale waliokuwa wamesimama pale walikuwa wakimwambia Petro, "Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya."
\s5
\v 71 Lakini alianza kujiweka mwenyewe chini ya laana na kuapa, "Simjui mtu huyu mnayemsema."
\v 72 Kisha jogoo aliwika mara ya pili. Kisha Petro alikumbuka maneno ambayo Yesu aliyokuwa amemwambia: "Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu." Na alianguka chini na kulia.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Asubuhi na mapema wakuu wa makuhani walikutana pamoja na wazee na waandishi na baraza zima la wazee. Kisha wakamfunga Yesu wakampeleka kwa Pilato. Pilato akamwuliza, "wewe ni Mfalme wa Wayahudi?"
\v 2 "Akamjibu, "Wewe umesema hivyo."
\v 3 Wakuu wa makuhani wakaeleza mashitaka mengi juu ya Yesu.
\s5
\v 4 Pilato akamwuliza tena, "Hujibu chochote? Huoni jinsi wanavyokushtaki kwa mambo mengi?
\v 5 Lakini Yesu hakumjibu Pilato, na hiyo ilimshangaza.
\s5
\v 6 Kwa kawaida wakati wa sikukuu humfungulia mfungwa mmoja, mfungwa waliyemwomba.
\v 7 Kulikuwapo wahalifu gerezani, miongoni mwa wauaji kati ya walioasi wanaotumikia makosa yao. Alikuwepo mtu mmoja aitwaye Baraba.
\v 8 Umati ulikuja kwa Pilato, na kumwomba afanye kama alivyofanya huko nyuma.
\s5
\v 9 Pilato akawajibu na kusema, "Mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?"
\v 10 Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake.
\v 11 Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba afunguliwe Baraba badala yake.
\s5
\v 12 Pilato akawajibu tena na kusema, "Nimfanye nini Mfalme wa Wayahudi?
\v 13 Wakapiga kelele tena, "Msulibishe!"
\s5
\v 14 Pilato akasema, "Amefanya jambo gani baya?" Lakini wakazidi kupiga kelele zaidi na zaidi "Msulibishe."
\v 15 Pilato akitaka kuwaridhisha umati, akawafungulia Baraba. Akampiga Yesu mijeledi kisha akamtoa ili asulibiwe.
\s5
\v 16 Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ule ulio ndani ya kambi) na walikusanyika pamoja kikosi cha askari.
\v 17 Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.
\v 18 Wakaanza kumdhihaki na kusema, "Salam, Mfalme wa Wayahudi!"
\s5
\v 19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.
\v 20 Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulibisha.
\v 21 Wakamlazimisha mpita njia kumsaidia, aliyekuwa anaingia mjini kutoka shamba. Aitwaye Simoni Mkirene (baba yake Iskanda na Rufo); wakamlazimisha kubeba msalaba wa Yesu.
\s5
\v 22 Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa).
\v 23 Wakampa mvinyo iliyochanganywa na manemane, lakini hakunywa.
\v 24 Wakamsulibisha na wakagawana mavazi yake, wakayapigia kura kuamua kipande atakachopata kila askari.
\s5
\v 25 Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.
\v 26 Wakaweka juu yake ubao ulioandikwa shitaka, "Mfalme wa Wayahudi."
\v 27 Walimsubisha pamoja na majambazi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine kushoto kwake.
\v 28 (Zingatia: Mstari huu, "Na maandiko yakatimia yaliyonena" haumo katika nakala za kale).
\s5
\v 29 Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, "Aha! wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,
\v 30 jiokoe mwenyewe na ushuke chini toka msalabani!"
\s5
\v 31 Kwa namna ile ile wakuu wa makuhani walimdhihaki wakisemezana, pamoja na waandishi na kusema, "Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe.
\v 32 Kristo Mfalme wa Israel, shuka chini sasa toka msalabani, ili tuweze kuona na kuamini." Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimdhihaki.
\s5
\v 33 Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.
\v 34 Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lama sabaktani?" ikiwa na maana "Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?"
\v 35 Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, "Tazama, anamwita Eliya."
\s5
\v 36 Mtu mmoja akakimbia, akajaza siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, "Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini."
\v 37 Kisha Yesu akalia kwa sauti kubwa na akafa.
\v 38 Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini.
\s5
\v 39 Ofisa mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, "Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu."
\v 40 Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome.
\v 41 Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.
\s5
\v 42 Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,
\v 43 Yusufu wa Arimathaya alikuja pale. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza anayeheshimiwa mtu anayeutarajia Ufalme wa Mungu. Kwa ujasiri akaenda kwa Pilato, na kuuomba mwili wa Yesu.
\v 44 Pilato akashangazwa kwamba Yesu tayari amekufa; akamwita yule afisa akamwuliza kama Yesu amekufa.
\s5
\v 45 Alipopata uhakika kwa afisa kwamba amekufa, alimruhusu Yusufu kuuchukua mwili.
\v 46 Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.
\v 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yose waliona sehemu alipozikwa Yesu.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake na Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu kwa ajili ya maziko.
\v 2 Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza.
\s5
\v 3 Wakisemezana wao kwa wao, "Nani ataliviringisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?"
\v 4 Wakati walipotazama, walimuona mtu amekwisha kulivingirisha jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana.
\s5
\v 5 Wakaingia kwenye kaburi na wakamwona kijana amevaa joho jeupe, ameketi upande wa kulia, na wakashangazwa.
\v 6 Akawaambia, "Msiogope. Mnamtafuta Yesu, wa Nazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayupo hapa. Tazama mahali pale walipokuwa wamemweka.
\v 7 Nendeni, mkawaambie wanafunzi wake na Petro ya kuwa amewatangulia kuelekea Galilaya. Huko mtamwona, kama alivyokua amewaambia."
\s5
\v 8 Wakaondoka na kukimbia kutoka kwenye kaburi; walitetemeka na walishangazwa. Hawakusema chochote kwa mtu yeyote sababu waliogopa sana.
\s5
\v 9 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba.
\v 10 Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakihuzunika na kutoa machozi.
\v 11 Walisikia kwamba ni mzima na ameonekana naye, lakini hawakumwamini.
\s5
\v 12 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Baada ya hayo, akajitokeza katika namna tofauti kwa watu wengine wawili, wakati walipokuwa wakitembea kutoka katika nchi.
\v 13 Walienda na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini.
\s5
\v 14 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wameegama katika meza, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
\v 15 Akawaambia, " Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote.
\v 16 Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa.
\s5
\v 17 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya.
\v 18 Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kufisha hakitawadhuru. Wataweka mikono kwa wagonjwa, nao watakuwa wazima".
\s5
\v 19 Baada ya Bwana kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
\v 20 Wanafunzi wakaondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana akifanya kazi nao na kulithibitisha neno kwa miujiza na ishara zikifuatana nao.