sw_ulb_rev/27-DAN.usfm

739 lines
64 KiB
Plaintext

\id DAN
\ide UTF-8
\h Danieli
\toc1 Danieli
\toc2 Danieli
\toc3 dan
\mt Danieli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja Yerusalemu na kuuzunguka mji ili kuzuia mahitaji yake yote.
\v 2 Bwana alimpa Nebukadneza ushindi dhidi ya Yehoyakimu mfalme wa Yuda, na alimpatia vitu vitakatifu kutoka nyumba ya Mungu. Alivipeleka vitu hivyo mpaka katika nchi ya Babeli, kwa nyumba ya mungu wake, na aliviweka vitu vitakatifu katika hazina ya mungu wake.
\s5
\v 3 Mfalme akamwambia Ashipenazi, afisa wake mkuu, awalete baadhi ya watu wa Israeli, wa familia ya kifalme na za kiungwana -
\v 4 vijana wasio na hila, wenye mwonekano wa kuvutia, wenye ujuzi katika hekima yote, wenye kujawa na ufahamu na weledi, na wenye sifa za kutumika katika ikulu ya mfalme. Alitakiwa kuwafundisha maandiko na lugha ya Babeli.
\v 5 Mfalme aliwatengea kwa ajili yao fungu kutoka katika chakula chake kizuri kwa kila siku na katika divai aliyokunywa. Vijana hawa walitakiwa kufunzwa kwa miaka mitatu, na baada ya hapo, wangeweza kumtumikia mfalme.
\s5
\v 6 Miongoni mwao walikuwa ni Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria, baadhi ya watu wa Yuda.
\v 7 Afisa mkuu aliwapa majina: Danieli alimwita Belteshaza, Hanania alimwita Shadraka, Mishaeli alimwita Meshaki, na Azaria alimwita Abedinego.
\s5
\v 8 Lakini Danieli alinuia katika akili yake kuwa asingejitia ujanisi mwenyewe kwa chakula kizuri cha mfalme wala kwa divai ambayo alikunywa.
\v 9 Basi, aliomba ruhusa kutoka kwa afisa mkuu ili kwamba asije akajitia uchafu yeye mwenyewe. Hivyo, Mungu alimpa Danieli kibali na huruma kupitia katika heshima ambayo afisa mkuu alikuwa nayo kwake.
\v 10 Afisa mkuu alimwambia Danieli, "Ninamwogopa bwana wangu mfalme. Ameagiza aina ya chakula na vinywaji mnavyotakiwa kutumia. Kwa nini awaone ninyi mkiwa mnaonekana vibaya kuliko vijana wengine wa umri wenu? Mfalme aweza kukitwaa kichwa changu kwa sababu yenu.
\s5
\v 11 Kisha Daniel akamwambia msimamizi ambaye afisa mkuu alikuwa amemweka juu ya Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria.
\v 12 Alisema, "Tafadhari tujaribuni, sisi watumishi wako kwa siku kumi. Tupatieni tu mboga mboga za kula na maji ya kunywa.
\v 13 Kisha ulinganishe mwonekano wetu na mwonekano wa vijana wanaokula vyakula vya mfalme, na mtutendee, sisi watu wako kulingana na kile unachokiona." '
\s5
\v 14 Hivyo msimamizi alikubaliana naye kufanya hivi, na aliwajaribu kwa siku kumi.
\v 15 Katika mwisho wa siku kumi mwonekano wao ulikuwa ni wenye afya nzuri kuliko wa wale vijana waliokula vyakula vya kifalme.
\v 16 Basi, msimamizi aliliondoa fungu lao la chakula na vivywaji vyao na walipewa mboga mboga tu.
\s5
\v 17 Na kuhusu vijana hawa nne Mungu aliwapa uelewa na ufahamu katika maandiko yote na hekima, na Danieli aliweza kupambanua aina zote za maono na ndoto.
\v 18 Katika mwisho wa muda uliokuwa umepangwa na mfalme kuwaleta ndani, afisa mkuu aliwaleta mbele ya Nebukadneza.
\s5
\v 19 Mfalme aliongea nao, na miongoni mwa kundi lote hapo hapakuwa na wa kuwalinganisha na akina Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria. Walisimama mbele ya mfalme, wakiwa tayari kumtumikia.
\v 20 Katika kila swali la hekima na ufahamu ambalo mfalme aliwauliza, aliwakuta wakiwa na uwezo mara kumi kuliko waganga wote na wale waliojidai kusema na wafu, waliokuwa katika ufalme wake wote.
\v 21 Danieli alikuwa hapo mpaka mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza, alikuwa na ndoto. Akili yake ilisumbuka, na hakuweza kulala.
\v 2 Ndipo mfalme alipowaita waganga na wale wenye kuongea na wafu. Lakini pia aliwaita wachawi na watu wenye hekima. Aliwataka wamwambie juu ya ndoto zake. Basi walikuja na kusimama mbele za mfalme.
\s5
\v 3 Mfalme akawambia, "Nilikuwa na ndoto, na akili yangu ina mashaka nataka kujua ndoto hiyo nini maana yake."
\v 4 Kisha watu wenye hekima wakamwambia mfalme katika Kiaramaiki, " Mfalme, aishi milele! Twambie sisi ndoto, watumishi wako, nasi tutaifunua maana yake."
\s5
\v 5 Mfalme akawajibu watu wenye hekima, " Jambo hili limeshamalizika. Kama hamtaweza kuiweka wazi ndoto kwangu na kuitafsiri, miili yenu itakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vichuguu vya uchafu.
\v 6 Lakini kama mtaniambia ndoto na maana yake, mtapokea zawadi kutoka kwangu, thawabu, na heshima kubwa. Basi niambie ndoto na maana yake."
\s5
\v 7 Wakamjibu tena na kusema, "Mfalme na atuambie, watumishi wake, ndoto nasi tukwambia maana yake."
\v 8 Mfalme akawajibu, " Ninajua kwa hakika mnahitaji muda zaidi kwasababu mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili.
\v 9 Lakini kama hamtaweza kuniambia ndoto, kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu. Mmeamua kuandaa uongo na maneno ya kudanganya ambayo mmekubaliana kwa pamoja kuniambia mpaka pale nitakapobadili akili zangu. Basi, niambieni ndoto, na kisha nitajua kuwa mnaweza kuitafsiri kwa ajili yangu."
\s5
\v 10 Watu wenye hekima wakamjibu mfalme, " Hakuna mtu katika dunia anayeweza kutimiza matakwa ya mfalme. Hakuna mfalme yoyote mkuu na mwenye nguvu ambaye alishataka jambo kama hilo kutoka kwa wachawi, wala wenye kuongea na wafu, wala mwenye hekima.
\v 11 Kile anachokitaka mfalme ni kigumu, na hakuna yeyote awezaye kumwambia mfalme isipokuwa miungu, ambayo haishi miongoni mwa watu."
\s5
\v 12 Jambo hili lilimfanya mfalme akasirike na kughadhabika sana, na alitoa amri kuwaangamiza wale wote waliojulikana kuwa ni wenye hekima zao katika Babeli.
\v 13 Hivyo, amri ilitoka kwamba wale wote waliojulikana kwa hekima yao ni lazima wauawe. Na kwa sababu ya amri hii, walimtafuta Daniel na rafiki zake ili kwamba wauawe.
\s5
\v 14 Ndipo Daniel alipomjibu kwa busara na umakini, Arioki, kamanda wa walinzi wa mfalme, ambaye alikuwa amekuja kuwaua wale wote waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.
\v 15 Danieli alimwuliza kamanda wa mfalme, " Kwanini amri ya mfalme ni ya haraka hivyo?" Hivyo, Arioki akamwambia Danieli kile kilichotokea.
\v 16 Ndipo Danieli aliingia ndani na akaomba ahadi ya muda wa kuonana na mfalme ili kwamba aweze kuwasilisha tafsiri kwa mfalme.
\s5
\v 17 Kisha Danieli aliingia ndani ya nyumba na aliwaelezea Hanania, Mishaeli, na Azaria, kile kilichotokea.
\v 18 Aliwasihi kutafuta rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusiana na siri hii ili kwamba yeye na wao wasije wakauawa pamoja na watu wengine waliosalia waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.
\s5
\v 19 Usiku ule siri ilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Kisha Danieli akamtukuza Mungu wa mbinguni
\v 20 na kusema, "Litukuzwa jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na nguvu ni zake.
\s5
\v 21 Anabadili wakati na majira; anaondoa wafalme na kuweka wafalme katika viti vyao vya enzi. Anawapa hekima wenye hekima na ufahamu kwa wenye weledi.
\v 22 Hufunua vitu vya chini na vilifichika kwa sababu anajua kile kilicho gizani, naye anaishi pamoja na mwanga.
\s5
\v 23 Mungu wa baba zetu, ninakushukuru na kukutukuza wewe kwa ajili ya hekima na nguvu uliyonipa. Sasa umeyafanya yawe wazi kwetu yale tuliyokuomba; umetujulisha mambo yamhusuyo mfalme."
\s5
\v 24 Ndipo Danieli alienda kumwona Arioki ( yule ambaye mfalme alimchagua kuua kila mtu aliyekuwa na hekima katika Babeli). Alimwendea na kumwambia, "Usiwauwe watu wenye hekima katika Babeli. Nipeleke kwa mfalme na nitamwonesha mfalme tafsiri ya ndoto yake."
\s5
\v 25 Kisha Arioki kwa haraka alimleta Danieli mbele za mfalme na kusema, " Nimempata miongoni wa watu wa mateka wa Yuda mtu ambaye atafunua maana ya ndoto ya mfalme."
\v 26 Mfalme akamwambia Danieli (ambaye alikuwa akiitwa Beliteshaza), "Je unaweza kunimbia ndoto niliyoiona na maana yake?"
\s5
\v 27 Danieli alimjibu mfalme na kusema, "Siri ambayo mfalme ameiomba haiwezi kufunuliwa na watu wenye hekima, wala wale wenye kuongea na wafu, wala wachawi, na wala wataalamu wa nyota.
\v 28 Isipokuwa kuna Mungu ambaye anaishi mbinguni, ambaye hufunua siri, na amekwisha kukujulisha wewe, mfalme Nebukadneza, kile kitakachotokea katika siku zijazo. Hizi ndizo Ndoto na maono ya akili zako uliyoyaona wakati ulipokuwa umelala kitandani mwako.
\s5
\v 29 Na kwako Wewe, mfalme, mawazo yako kitandani mwako yalikuwa ni juu ya mambo yajayo, na yule afichuaye siri ameifanya ijulikane kwako kuhusu kile kilicho karibu kutokea.
\v 30 Na kuhusu mimi, siri hii haikufunuliwa kwangu kwa sababu ya hekima yoyote niliyo nayo zaidi ya mtu yoyote anayeishi. Siri hii imefunliwa kwangu ili kwamba wewe, mfalme, uweze kufahamu maana, na ili kwamba ujuwe mawazo yaliyo ndani mwako.
\s5
\v 31 Mfalme, uliangalia juu na ukaona sanamu kubwa. Sanamu hii ambayo ilikuwa yenye nguvu na yenye kung'aa, ilisimama mbele yako. Mng'ao wake ulikuwa unatisha.
\v 32 Kichwa cha sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi. Matiti yake na mikono ilikuwa ya fedha. Sehemu ya katikati na mapaja yake yalikuwa yametengenezwa kwa shaba,
\v 33 na miguu yake ilikuwa imetengenezwa kwa chuma. Miguu yake ilikuwa ilitengenezwa kwa sehemu chuma na sehemu kwa udongo.
\s5
\v 34 Ulitazama juu, na jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na liliipiga sanamu katika miguu yake ya chuma na udongo, na ponda ponda.
\v 35 Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo huyapeperushia mbali na hakuna alama inayoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanammu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
\s5
\v 36 Hii ndiyo ilikuwa ndotoyako. Na sasa tutamwambia mfalme maana yake.
\v 37 Wewe, mfalme, ni mfalme wa wafalme kwa wale ambao Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, nguvu, uweza na heshima.
\v 38 Amevitia mkononi mwako sehemu ambazo binadamu huishi. Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako, na amekufanya wewe utawale juu yao wote. Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu.
\s5
\v 39 Baada yako, ufalme mwingine utainuka ambao ni mdogo kwako, na hata ufalme wa tatu wa shaba utatawala juu ya dunia yote.
\s5
\v 40 Kutakuwa na ufalme wa tatu, wenye nguvu kama chuma, kwa kuwa chuma huvunja vipande vipande vitu vingine na kuponda ponda kila kitu. Itaviharibu vitu hivi vyote na kuvisaga.
\s5
\v 41 Kama vile ulivyoona, miguu na vidole vilikuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo na kwa sehemu vimefanywa kwa chuma, hivyo utakuwa ni ufalme uliogawanyika; baadhi ya nguvu za chuma zitakuwa ndani yake, kama tu ulivyoona kuwa chuma kimechanganyikana na udongo laini.
\v 42 Kama vile vidole vya miguuni vilivyokuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa chuma na kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo, ndivyo ufalme utakuwa kwa sehemu una nguvu na kwa sehemu utakuwa dhaifu.
\v 43 Kama ulivyoona chuma kimechanganywa na udongo laini, na hivyo na watu watakuwa wamechanganyikana; hawakaa kwa pamoja, kama vile chuma kisivyoweza kushikamana na udongo
\s5
\v 44 Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao hautaweza kuangushwa, wala kushindwa na watu wengine. Utazivunja falme zingine vipande vipande na kuzikomesha zote, nao utadumu milele.
\v 45 Kama tu ulivyoona, jiwe lilichongwa kutoka katika mlima, lakini si kwa mikono ya wanadamu. Lilivunja vunja chuma, shaba, udongo, fedha, na dhahabu katika vipande vipande. Mungu mkuu amekujulisha wewe, mfalme, kile kitakachotokea baada ya haya. Ndoto ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.
\s5
\v 46 Mfalme Nebukadneza alianguka kifudifudi mbele ya Daniel na alimweshimu; aliamuru kwamba sadaka zitolewe na manukato yatolewe kwake.
\v 47 Mfalme alimwambia Danieli, " Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme, na ambaye hufunua mafumbo, kwa kuwa umekuwa ukiweza kufumbua mafumbo haya."
\s5
\v 48 Ndipo mfalme alimfanya Danieli kuwa wa kuheshiwa sana na alimpa zawadi nyingi nzuri. Alimfanya kuwa mtawala juu ya jimbo lote la Babeli. Danieli akawa liwali mkuu juu watu wenye hekima wa Babeli.
\v 49 Danieli alipeleka ombi kwa mfalme, na mfalme aliwateua Shadraka, Meshaki na Abedinego kuwa watawala juu ya jimbo la Babeli. Lakini Danieli alisalia katika ikulu ya mfalme.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu ambayo ilikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita. Aliiweka katika uwanda wa Dura katika jimbo la Babeli.
\v 2 Kisha Nebukadneza alituma ujumbe wa kuwaita pamoja magavana wote wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na na washauiri, wahazini, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wakuu wa majimbo ili waje kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu aliyokuwa ameiweka.
\s5
\v 3 Ndipo magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka. Walisimama mbele yake.
\v 4 Kisha mtangazaji alipiga kelele, "Enyi watu, mataifa, na lugha mmeamriwa
\v 5 kwamba mtakaposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, ni sharti kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameiweka.
\s5
\v 6 Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto."
\v 7 Basi watu walilposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, watu wote, mataifa na lugha walianguka na kuisujudia wao wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.
\s5
\v 8 Wakati huu baadhi ya Walkadayo walikuja na kuleta mashitaka kinyume na Wayahudi.
\v 9 Walimwambia mfalme Nebukadneza, "mfalme aishi milele!
\v 10 Ewe mfalme, umeweka amri kwamba kila mtu aisikiye sauti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari, na aina zote za muziki, lazima kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu.
\s5
\v 11 Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru linalowaka moto.
\v 12 Sasa kuna baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu masuala ya jimbo la Babeli; majina yao ni Shadraka, Meshaki, na Abednego. Mfalme, hawa watu hawakutii wewe. Hawataiabudu, kuitumikia wala kuisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka."
\s5
\v 13 Ndipo Nebukadneza alijawa na hasira na ghadhabu, aliagiza kwamba Shadraka, Meshaki na Abednego waletwe kwake. Hivyo, waliwalete hawa watu mbele ya mfalme.
\v 14 Nebukadneza aliwaambia, "Je mmejipanga katika akili zenu, enyi Shadraka, Meshaki na Abedinego, kwamba hamtaiabudu miungu yangu wala kuisujudia wenyewe sanamu ile ya dhahabu ambayo nimeiweka?
\s5
\v 15 Basi sasa kama mko tayari - mtakaposikia sauti pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinumbi na zumari, aina zote za muziki - kuanguka chini na kuisujudia wenyewe sanamu ile ambayo nimeitengeneza, mambo yote yatakuwa mazuri. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa mara katika tanuru la moto. Ni mungu gani atakayeweza kuwaokoa katika mikono yangu?"
\s5
\v 16 Shadraka, Meshaki, na Abednego wakamjibu mfalme, "Nebukadneza, hatuhitaji kukujibu wewe katika jambo hili.
\v 17 Kama kuna jibu, ni kwamba Mungu wetu ambaye tunamtumikia anaweza kutuhifadhi sisi salama katika katika tanuru la moto, na atatuokoa sisi katika mkono wako, mfalme.
\v 18 Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme, kwamba hatutaiabudu miungu yako, na wala hatutaisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu uliyoiweka.
\s5
\v 19 Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.
\v 20 Kisha aliwaamuru baadhi ya watu wenye nguvu katika jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika tanuru liwakalo moto.
\s5
\v 21 Walifungwa akali wakiwa wamevaa nguo zao, kanzu, kilemba, na mavazi mengine, na walitupa katika tanuru liwakalo moto.
\v 22 Kwasababu ya agizo la mfalme lilifuatwa na tanuru lilikuwa na joto sana, miali ya moto iliwaua watu waliowatupa Shadraka, Meshaki, na Abedinego.
\v 23 Hawa wanaume watatu, Shadraka, Meshaki, na Abednego, waliangukia katika tanuru liwakalo moto wakali wamefungwa.
\s5
\v 24 Kisha Nebukadneza mfalme alishangazwa na alisimam haraka. Aliwauliza washauri wake, "Je hatukutupa watu watatu wakiwa wamefungwa katika moto?" Nao walimjibu mfalme, "Hakika mfalme."
\v 25 Alisema, "Lakini ninaona watu wanne ambao hawajafungwa wakizunguka katika moto, na hawajaumizwa. Mng'ao wa mtu wa nne ni kama mwana wa miungu."
\s5
\v 26 Ndipo Nebukadneza aliposogea karibu na mlango wa tanuru liwakalo moto na akaaita, "Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni nje! Njooni hapa! Ndipo Shadraka, Meshaki na Abednego walitoka nje ya moto.
\v 27 Magavana wa majimbo, magavana wengine, na washauri wa mfalme waliokuwa wamekusanyika kwa pamoja waliwaona watu hawa. Moto haukuunguza miili yao; nywele katika vichwa vyao hazikuungua; mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa; na hawakuwa na harufu ya moto.
\s5
\v 28 Nebukadneza alisema, "Na tumsifu Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego, ambaye amemtuma mjumbe wake na amewapa ujumbe watumishi wake. Walimtumaini yeye wakati walipoikana amri yangu, na waliitoa miili yao badala ya kuabudu au kusujudia mungu mwingine isipokuwa Mungu wao.
\s5
\v 29 Hivyo basi ninaagiza kwamba watu wote, taifa au lugha ambayo itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego lazima wakatwe vipande, na ya kwamba nyumba zao lazima zifanywe kuwa vichuguu vya uchafu kwasababu hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama hivi."
\v 30 Ndipo mfalme aliwapandisha cheo Shadraka, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi: "Na amani yenu na iongezeke.
\v 2 Imeonekana vizuri kwangu kuwaambia juu ya ishara na maajabu ambayo Mungu Mkuu Aliye juu amenifanyia.
\v 3 Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi."
\s5
\v 4 Mimi, Nebukadneza, nilikuwa ninaishi kwa furaha katika nyumba yangu, na nilikuwa nikifurahia mafanikio katika ikulu yangu.
\v 5 Lakini ndoto niliyoiota ilifanya niogope. Nilipokuwa nimejilaza pale, taswira niliyoiona na maono katika akili yangu yalinitaabisha.
\v 6 Basi nilitoa agizo la kuwaleta mbele yangu watu wote wa Babeli waliokuwa na hekima ili kwamba waweze kunitafsiria ndoto.
\s5
\v 7 Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria.
\v 8 Bali mwishoni Danieli aliingia ndani - yeye ambaye huitwa Belteshaza jina la mungu wangu, na ambaye ndani yake kuna roho ya miungu mitakatifu - na nilimwambia juu ya ndoto.
\v 9 "Belteshaza, mkuu wa wachawi, ninajua kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako na ya kwamba hakuna siri iliyo ngumu kwako. Niambie kile nilichokiona katika ndoto yangu na nini maana yake.
\s5
\v 10 Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana.
\v 11 Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote.
\v 12 Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliisha katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo.
\s5
\v 13 Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni.
\v 14 Alipiga kelele na kusema, 'Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake.
\s5
\v 15 Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini.
\v 16 Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.
\s5
\v 17 Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.'
\v 18 Mimi, Mfalme Nebukadneza nilipata ndoto hii. Sasa, wewe Belteshaza, niambie tafsiri yake, kwasababu hakuna mtu mwenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunitafsiria. Lakini wewe unaweza kufanya hivyo, kwa kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako."
\s5
\v 19 Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, " Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake." Belteshaza akajibu, " Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.
\s5
\v 20 Mti ule uliouona - uliokua na ukawa na wenye nguvu, na ambao sehemu yake ya juu ilifika hata mbinguni, na ambao waweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote -
\v 21 ambao majani yake ni mazuri, na matunda yake yalikuwa ni mengi, ili kwamba ndani yake kulikuwa na chakula cha wote, na chini yake wanyama wa mwituni walipata kivuli, na ndani yake ndege wa angani waliishi -
\v 22 huu mti ni wewe, mfalme, wewe uliyekua na kuwa na nguvu. Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia.
\s5
\v 23 Ewe mfalme, ulimwona mjumbe akishuka kutoka mbinguni na akisema, "Ukateni mti na uteketezeni, lakni kiacheni kisiki cha mizizi yake katika nchi, kifungeni kwa ukanda wa chuma na shaba, katikati ya mche mororo katika shamba. Na kilowanishwe na umande kutoka mbinguni. Kiache kiishi katika wanyama wa mwituni katika mashamba mpaka ipite miaka saba.'
\s5
\v 24 Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme.
\v 25 Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu, na utaishi pamoja na wanyama wa mwituni huko mashambani. Utafanywa uwe unakula majani kama ng'ombe, na utalowanishwa na umande wa kutoka mbinguni, miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba yeye humpa falme hizo mtu yeyote amtakaye.
\s5
\v 26 Kama ilivyoamriwa kwamba kukiacha kisiki cha mizizi ya mti, kwa njia hii ufalme wako utarudishiwa katika kipindi ambacho utajifunza kwamba mbingu inatawala.
\v 27 Hivyo basi, mfalme, ushauri wangu na ukubalike kwako. Acha kutenda dhambi na utende haki. Geuka uache uovu wako wa kuonesha huruma kwa walionewa, na itakuwa kwamba mafanikio yako yataongezwa."
\s5
\v 28 Vitu hivi vyote vilitokea kwa mfalme Nebukadneza.
\v 29 Baada ya miezi wa kumi na miwili alipokuwa akitembea juu ya dari la ikulu ya kifalme katika Babeli,
\v 30 na alisema, " Je hii si Babeli kuu, ambayo nimeijenga kwa ajili ya makao yangu ya kifalme, kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?"
\s5
\v 31 Wakati maneno yakali katika midomo ya mfalme, sauti ilisikika kutoka mbinguni: "Mfalme Nebukadneza, imetangazwa kwako kwamba ufalme huu umeondolewa kutoka kwako.
\v 32 Utafukuziwa mbali kutoka miongoni mwa watu, na makao yao yatakuwa pamoja na wanyama wa mwitu katika mashamba. Utafanywa kulamajani kama ng'ombe. Miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na humpa falme mtu yeyote amtakaye."
\s5
\v 33 Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
\s5
\v 34 Na katika mwisho wa siku, mimi, Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, utimamu wa akili nilirudishiwa. "Nilimsifu Mungu Aliye Juu sana, na nilimheshimu na kumtukuza yeye aishiye milele. Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.
\s5
\v 35 Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure; hufanya lolote limpendezalo miongoni mwa jeshi la mbinguni na wakazi wa dunia. Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia au kumpa changamoto. Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, "Mbona umefanya hivi?"
\s5
\v 36 Kwa wakati ule ule utimamu wa akili zangu uliponirudia, utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na watu wenye heshima walitafuta msaada wangu. Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi.
\v 37 Sasa basi, mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za adili. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Mfalme Belshaza alifanya sherehe kubwa kwa kwa ajili ya wakuu wake wa kuheshimiwa wapatao elfu moja, na alikunywa divai mbele yao wote watu elfu moja.
\v 2 Wakati Belshaza alipokuwa akionja divai, alitoa agizo la kuleta vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu au kwa fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka katika hekalu huko Yerusalemu, ambavyo yeye, na wakuu wake, na wake zake, na masuria waliweza kuvinywea.
\s5
\v 3 Watumishi walivileta vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mfalme na wakuu wake, na wake zake na masuria walivinywea.
\v 4 Walikunywa divai na kuzisifu sanamu zao zilizotengenezwa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.
\s5
\v 5 Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa lipu katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.
\v 6 Ndipo uso wa mfalme ulibadilika na mawazo yake yalimwogopesha; miguu yake haikuweza kumfanya asimame, na magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja.
\s5
\v 7 Mfalme alitoa agizo kwa kupiga kelele, waletwe ndani wale ambao hudai wanaweza kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wataalamu wa nyota. Mfalme akawaambia wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli, "Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme."
\s5
\v 8 Ndipo watu wote wa mfalme walikuwa wakijulikana kwa hekima yao waliingia ndani, lakini hawakuweza kuyasoma maandishi wala kueleza maana yake kwa mfalme.
\v 9 Kisha mfalme Belshaza alishitushwa sana na mwonekano wa uso wake ulibadilika. Wakuu wake nao walishangazwa sana.
\s5
\v 10 Ndipo sasa malkia alikuja katika nyumba ya sherehe kwasababu ya kile ambacho mfalme na wakuu wake walikuwa wamekisema. Malkia akasema, "Mfalme na aishi milele! Usiache mawazo yako yakakusumbua. Usiruhusu mwonekano wa uso wako ubadilike.
\s5
\v 11 Kuna mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu watakatifu dani yake. Katika siku za baba yako, mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake. Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme, alimfanya kuwa mkuu wa waganga, pamoja na mkuu wa wale wanazungumza na wafu, na wa wenye hekima, na wa wataalamu wa nyota.
\v 12 Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa."
\s5
\v 13 Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamwambia, "Wewe ni yule Danieli, mmoja kati ya watu wa mateka wa Yuda, ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda.
\v 14 Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.
\s5
\v 15 Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.
\v 16 Nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo. Sasa kama utaweza kusoma maandishi na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako, na utakuwa mtawala wa tatu mwenye mamlaka katika ufalme."
\s5
\v 17 Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, "Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana.
\v 18 Na juu yako, Ewe mfalme, Mungu Aliye juu sana alimpa Nebukadneza baba yako ufalme, ukuu, heshima na enzi.
\v 19 Na kwasababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.
\s5
\v 20 Lakini wakati moyo ulipokuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwasababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.
\v 21 Aliondolewa katika ubinadamu, alikuwa na akili za mnyama, na aliishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.
\s5
\v 22 Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote.
\v 23 Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilitengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe - sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wa kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote.
\v 24 Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.
\s5
\v 25 Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa: 'Mene, Mene, Tekeli na Peresin.'
\v 26 Maana yake ni: 'Mene,' 'Mungu ameuhesabu ufalme wako na ameukomesha.'
\v 27 'Tekeli' 'umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.'
\v 28 'Peresi' 'ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.'"
\s5
\v 29 Ndipo Belshaza alitoa agizo, na walimvalisha Danieli mavazi ya zambarau. Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni, na mfalme alitoa tamko juu ya Danieli kuwa atakuwa mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu katika ufalme.
\v 30 Usiku ule Belshaza, mfalme wa Babeli aliuawa,
\v 31 na Dario Mwajemi aliuchukua ufalme alipokuwa na miaka ipatayo sitini na miwili.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ilimpendeza Dario kuchagua juu ya ufalme magavana wa majimbo 120 ambao wangetawala juu ya ufalme wote.
\v 2 Juu yao kulikuwa na watawala wakuu watatu, na Daniel alikuwa mmoja wao. Hawa watawala waliwekwa ili waweze kuwasimamia magavana wa majimbo, ili kwamba mfalme asipate hasara.
\v 3 Danieli alipambanuliwa juu ya watawala wakuu na juu ya magavana wa majimbo kwasababu alikuwa na roho isiyo ya kawaida. Mfalme alikuwa akipanga kumweka juu ya ufalme wote.
\s5
\v 4 Basi watawala wakuu wengine na magavana wa majimbo walitafuta makosa katika kazi ambazo Danieli alizifanya kwa ufalme, lakini hawakuweza kuona ufisadi au kushindwa katika majukumu yake kwasababu alikuwa mwaminifu. Hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake.
\v 5 Kisha watu hawa wakasema, "Hatukuweza kupata sababu yoyote ya kumshitaki huyu Danieli isipokuwa tukitafuta kitu fulani dhidi yake kuhusiana na sheria za Mungu wake.'"
\s5
\v 6 Ndipo watawala hawa na magavana walileta mpango mbele ya mfalme. Walimwambia, "Mfalme Dario, uishi milele!
\v 7 Watawala wote wakuu wa ufalme, magavana wa mikoa, na magavana wa majimbo, washauri, na magavana wameshauriana kwa pamoja na kuamua kuwa wewe, mfalme, unapaswa kupitisha amri na kuitekeleza, ili kwamba mtu yeyote anayefanya dua kwa mungu yeyote au mtu kwa siku thelathini, isipokuwa wewe mfalme, mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba.
\s5
\v 8 Sasa mfalme, litoe agizo na utie saini nyaraka ili kwamba isije ikabadilika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi, hivyo haiweze ikabatilishwa.
\v 9 Basi, mfalme Dario alitia saini nyaraka kwa kuifanya amri kuwa sheria.
\s5
\v 10 Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kusainiwa kuwa sheria, alienda ndani ya nyumba yake (madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu), na alipiga magoti yake, kama alivyokuwa akifanya mara tatu kwa siku, na aliomba na kushukuru mbele ya Mungu wake, kama alivyofanya hapo kabla.
\v 11 Kisha watu hawa walikuwa wameunda hila kwa pamoja walimwona Danieli akiomba na kutafuta msaada kutoka kwa Mungu.
\s5
\v 12 Ndipo walipomwendea mfalme na kuongea naye kuhusiana na amri yake: "Je haukuweka amri kwamba mtu yeyote akayefanya maombi kwa mungu mwingine au kwa binadamu ndani ya siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, mfalme, lazima mtu huyo atupwe katika tundu la simba? Mfalme akajibu, "Jambo hili ni la hakika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi; ambazo haziwezi zikabatilishwa."
\s5
\v 13 Kisha wakamjibu mfalme, " Mtu yule Daniel, ambaye ni mmoja wa watu wa mateka kutoka Yuda, hakutii wewe, mfalme wala maagizo yako uliyoyasaini. Yeye humwomba Mungu wake mara tatu kwa siku."
\v 14 Mfalme aliposikia haya, alisikitishwa sana, alitumia akili jinsi ya kumwokoa kutoka katika utawala huu. Alisumbuka sana mpaka wakati wa kuzama kwa jua akijaribu kumwokoa Danieli.
\s5
\v 15 Kisha watu hawa waliokuwa wamepanga njama walikusanyika kwa pamoja na mfalme, na wakamwambia, "Ujue mfalme kwamba ni sheria ya Wamedi na Waajemi kwamba hakuna amri au sanamu ambayo mfalme anaipitisha yaweza kubadilishwa."
\s5
\v 16 Ndipo mfalme alitoa agizo, na walimleta ndani Danieli, na kisha wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, "Mungu wako, ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.''
\s5
\v 17 Jiwe lililetwa katika mlango wa tundu, na mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli.
\v 18 Basi mfalme alienda kwenye ikulu yake na usiku ule alikuwa na mfungo. Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake, nao usingizi ulimkimbia.
\s5
\v 19 Kisha katika mapambazuko mfalme aliamka na kwa haraka alienda kwenye tundu la simba.
\v 20 Na alipokaribia kwenye tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya huzuni, akimwambia Danieli, "Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je Mungu wako ambaye anamtumkia daima ameweza kukuokoa kutoka katika simba?
\s5
\v 21 Ndipo Danieli akamwambia mfalme, "Mfalme, uishi milele!
\v 22 Mungu wangu amemtuma mjumbe na amevifunga vinywa vya simba, na hazijaweza kunidhuru. Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote mbele yake na pia mbele yako, ewe mfalme, na sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru."
\s5
\v 23 Basi mfalme alikuwa na furaha sana. Alitoa agizo kwamba wanatakiwa wamtoe Danieli nje ya tundu. Hivyo Danieli aliondolewa kutoka katika tundu. Hakuna dhara lolote lililoonekana kwake, kwa kuwa alikuwa amemtumainia Mungu wake.
\s5
\v 24 Mfalme alitoa agizo, waletwe wale watu waliomshitaki Danieli na kisha akawatupa wao katika tundu la simba - wao, na watoto wao, na wake zao. Kabla hawajafika sakafuni, simba waliwararua na kuvunjavunja mifupa yao vipande vipande.
\v 25 Kisha mfalme Dario aliandika ujumbe kwa watu wote, mataifa na lugha ambazo ziliishi katika dunia yote: "Amani na iongezeke kwenu.
\s5
\v 26 Ninaagiza kwamba katika utawala wote wa ufalme wangu watu watetemeka na kumcha mbele ya Mungu wa Danieli, kwa kuwa ni Mungu aliye hai na huishi milele, na ufalme wake hauwezi kuharibiwa; utawala wake utakuwepo hadi mwisho.
\v 27 Yeye anatuhifadhi salama na kutuokoa, na anafanya ishara na maajabu mbinguni na duniani; amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba."
\s5
\v 28 Na hivyo basi, Danieli alifanikiwa katika utawala wa Dario na katika utawala wa Koreshi Mwajemi.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana:
\v 2 Danieli alieleza, "Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu.
\v 3 Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.
\s5
\v 4 Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, lakini alikuwa na mabawa ya tai. Nilipokuwa natazama, mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu. Na alipewa akili za kibinadamu.
\v 5 Na kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu, na alikuwa ameinama, alikuwa na mbavu tatu katikati ya meno yake katika mdomo wake. Aliambiwa, 'Inuka na umeze watu wangi.'
\s5
\v 6 Baada ya hili, niliangalia tena. Kulikuwa na mnyama mwingine ambaye alionekana kama chui. Mgongoni mwake alikuwa na mabawa manne kama mabawa ya ndege, na alikuwa na vichwa vinne. Alipewa mamlaka ya kutawala.
\v 7 Baada haya, niliona usiku katika ndoto yangu mnyama wa nne, mwenye kuogofya, na kutisha na mwenye nguvu. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; aliteketeza, na kuvunja vunja katika vipande, na kusaga saga katika miguuni pake kile kilichosalia. Alikuwa ni wa tofauti na wanyama wengine, na alikuwa na pembe kumi.
\s5
\v 8 Na wakati nilipokuwa natafakari juu ya pembe, nilitazama na niliona pembe nyingine ndogo ilichipuka katikati ya pembe zingine. Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa. Niliona katika pembe hii macho kama macho ya mtu na mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa.
\s5
\v 9 Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto.
\s5
\v 10 Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na mamilioni ya watu walimtumikia, na wengine mia moja milioni walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.
\s5
\v 11 Niliendelea kuangalia kwasababu ya maneno ya kiburi yaliyosemwa na pembe. Nilitazama wakati mnyama anauliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto.
\v 12 Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda.
\s5
\v 13 Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake.
\v 14 Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.
\s5
\v 15 Na kwangu mimi, Danieli, roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua.
\v 16 Nilimsogelea mmoja wa hawa walikuwa wamesimama hapo na nikamwomba anioneshe maana ya mambo haya.
\s5
\v 17 Hawa wanyama nne wakubwa ni wafalme wanne ambao watatoa katika nchi.
\v 18 Lakini watu watakatifu wa Mungu aliyejuu wataupokea ufalme na wataumiliki milele na milele.'
\s5
\v 19 Ndipo nilipotaka kujua zaidi juu ya mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti sana na wengine na alikuwa wa kutisha pamoja na meno yake ya chuma na makucha ya shaba; alimeza, na alivunja vipande vipande, na alisaga saga kwa miguu yake kile kilichokuwa kimesalia.
\v 20 Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliokuwa unajisifu kwa mambo makubwa na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine.
\s5
\v 21 Na nilipotazama, pembe hii iliinua vita dhidi ya watu watakatifu na ilikuwa inawawashinda mpaka pale
\v 22 Mzee wa Siku alipokuja, na watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana. Ndipo wakati ulipowadia ambapo watu watakatifu waliupokea ufalme.
\s5
\v 23 Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande.
\v 24 Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu.
\s5
\v 25 Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana na atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka.
\v 26 Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa.
\s5
\v 27 Ufalme na utawala, ukubwa wa falme chini ya mbingu yote, watapewa watu walio wa watu watakatifu wa Yeye Aliye juu Sana. Ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zingine zote zitamtumikia na kumtii yeye.'
\v 28 Na huu ndio mwisho wa mambo. Na kuhusu mimi, Danieli, mawazo yangu yanihuzunisha sana mimi na mwonekano wa uso wangu ulibadilika. Lakini mambo haya niliyahifadhi mimi mwenyewe."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, mimi Danieli niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata).
\v 2 Nilipokuwa nikiangalia katika ndoto, niliona kwamba nilikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu. Niliona katika ndoto kuwa nilikuwa karibu na mfereji wa Ulai.
\s5
\v 3 Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine.
\v 4 Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana.
\s5
\v 5 Na nilipokuwa natafakari juu ya haya, niliona beberu akitoka magharibi, na kuvuka katika uso wa dunia yote, akikimbia kwa kasi kana kwamba hakuonekana kama aligusa ardhini. Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake.
\v 6 Alienda mpaka kwa kondoo aliyekuwa na pembe mbili, nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji na mbuzi alikimbia kumwelekea kondoo dume kwa hasira kali.
\s5
\v 7 Niliiona mbuzi ikija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira na kondoo, alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake.
\v 8 Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.
\s5
\v 9 Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri.
\v 10 Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa.
\s5
\v 11 Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.
\v 12 Kwasababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo.
\s5
\v 13 Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, " Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa?
\v 14 Aliniambia, " Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2, 300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa."
\s5
\v 15 Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. na hapo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu.
\v 16 Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, "Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono."
\v 17 Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, niliogopa na nilisujudia hadi chini. Aliniambia,"Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho."
\s5
\v 18 Alipokuwa anaongea na mimi, nilipata usiingizi mzito nikiwa nimelala kifudifudi. Kisha alinishika na kunisimamisha.
\v 19 Akaniambia, "Tazama, nitakuonyesha kile kitachotokea baadaye katika kipindi cha ghadhabu, kwasababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa.
\s5
\v 20 Na kuhusu kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi.
\v 21 Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki. Pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
\s5
\v 22 Na kuhusu pembe iliyovunjika, ambayo katika nafasi yake pembe zingine nne zilichipuka - hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu kubwa.
\v 23 Katika siku zijazo za falme hizo, wakati ambapo wahalifu watakuwa wamefikia kikomo chao, mfalme mwenye uso katili, na yeye mwenye akili sana, atainuka.
\s5
\v 24 Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu.
\v 25 Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwasababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu.
\s5
\v 26 Maono kuhusu jioni na asubuhi ulizoambiwa ni ya kweli. Lakini uyafunge maono haya, kwa kuwa yanahusu siku nyingi za wakati ujao.
\s5
\v 27 Ndipo mimi, Danieli nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa. Kisha nikainuka na nikaenda kufanya kazi za mfalme. Lakini nilikuwa nimetishwa sana na maono, na hapakuwa na mtu yeyote aliyeweza kuyaelewa.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Dario mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi. Alikuwa na Ahasuero ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.
\v 2 Sasa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario, mimi Danieli, nilikuwa najisomea vitabu vilivyo na neno la Yahweh, neno ambalo lilikuwa limemjia Yeremia nabii. Niligundua kwamba kungekuwa na miaka sabini hadi mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.
\s5
\v 3 Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.
\v 4 Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, "Tafadhali, Bwana, wewe ni Mungu mkuu na mwenye kuheshimiwa, wewe hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda wewe na kuzishika amri zako.
\s5
\v 5 Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya. Tumeenenda kwa uovu na tumeasi, tumegeuka upande kinyume na amri na maagizo yako.
\v 6 Hatujawasikiliza watumishi wako manabii walizungumza na wafalme wetu, viongozi wetu, baba zetu, na kwa watu wote wa nchi kwa jina lako.
\s5
\v 7 Kwako Bwana, kuna uadilifu. Hata hivyo, kwetu kuna aibu katika nyuso zetu, kwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalem, na kwa Israeli yote. Hii ni pamoja na wale walio karibu na wale walio mbali katika nchi zote ambazo kwazo uliwatawanya. Hii ni kwasababu ya udanganyifu mkubwa tulioufanya kinyume chako.
\v 8 Kwetu sisi, Yahweh, kuna fedheha katika nyuso, na kwa wafalme wetu, na kwa viongozi wetu, na kwa baba zetu, kwasababu tumekutenda dhambi wewe.
\s5
\v 9 Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha, kwa kuwa tumemwasi yeye.
\v 10 Hatujaitii sauti ya Yahweh Mungu wetu kwa kutembea katika sheria zake alizotupatia kupitia watumishi wake manabii.
\v 11 Israeli wote wameiasi sheria yako na kugeukia upande, kwa kukataa kuitii sauti yako. Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, zimemwagwa juu yetu kwa kuwa tummetenda dhambi.
\s5
\v 12 Yahweh ameyathibitisha maneno ambayo aliyasema kinyume na sisi na kinyume na viongozi wetu juu yetu, kwa kuleta juu yetu janga kubwa. Kwa kuwa chini ya mbingu yote haijawahi kufanyika kitu chochote ambacho kinaweza kulinganishwa na kile kilichofanyika huko Yerusalemu.
\v 13 Kama ilivyoandikwa kwenye sheria ya Musa, baa hili lote limetupata, ingawa bado hatujaomba rehema kutoka kwa Yahweh Mungu wetu kwa kugeuka na kuacha maovu yetu na kuufuata ukweli wako.
\v 14 Hivyo basi, Yahweh ameyaweka tayari maafa na ameyaleta juu yetu, kwa kuwa Yahweh Mungu wetu ni mwenye haki katika matendo yote anayoyafanya, ingawa bado hatujaitii sauti yake.
\s5
\v 15 Basi sasa, Bwana Mungu wetu, uliwatoa watu wako katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu, na umejifanyia jina maarufu kwa ajli yako mwenyewe, hata siku hii ya leo. Lakini bado tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila. Kwasababu ya matendo yako yote ya haki,
\v 16 Bwana, iache hasira na ghadhabu yako iwe mbali na mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Hii ni kwasababu ya dhambi zetu, na kwasababu ya uovu wa baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamekuwa kitu cha kudharauliwa na wote wanaotuzunguka.
\s5
\v 17 Basi sasa, Mungu wetu, sikiliza sala za mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema; kwa ajili yako, Bwana ufanye uso wako ung'ae katika sehemu yako takatifu iliyoachwa ukiwa.
\v 18 Mungu wangu, fungua masikio yako na usikie; fumbua macho yako na uone. Tumeharibiwa; utazame mji unaoitwa kwa jina lako. Hatukuombi msaada wako kwasababu ya haki yetu, ila kwasababu ya rehema zako kuu.
\v 19 Bwana, sikiliza! Bwana, samehe! Bwana, tuangalie na ufanye jambo! Kwa ajili yako mwenyewe, usichelewe, Mungu wangu, kwa kuwa mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako."
\s5
\v 20 Nilipokuwa ninaongea kwa kuomba na kuungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuwasilisha maombi yangu mbele ya Yahweh Mungu wangu kwa niaba ya mlima mtakatifu wa Mungu.
\v 21 Nilipokuwa ninaomba, mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika ndoto hapo awali, alipaa kwa kasi kushuka kuja nilipo, ilikuwa ni wakati wa sadaka ya jioni.
\s5
\v 22 Alinipa ufahamu na aliniambia, "Danieli, nimekuja sasa ili nikupe utambuzi na ufahamu.
\v 23 Ulipoanza kuomba rehema, amri ilitolewa na nimekuja kukueleza jibu, kwa kuwa unapendwa sana. Hivyo basi, tafakari neno hili na uufahamu ufunuo.
\s5
\v 24 Miaka sabini na saba zimeamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu kukomesha hatia na kumaliza dhambi, na kuleta haki ya milele, na kutimiza maono na unabii, na kupaweka wakfu mahali patakatifu sana.
\v 25 Ujue na kufahamu kuwa tangu kupitishwa kwa amri ya kurudi na kuijenga upya Yerusalemu mpaka ujio wa mpakwa mafuta (atakayekuwa kiongozi), kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili. Yerusalemu itajengwa pamoja na mitaa yake na handaki, licha ya kuwepo kwa nyakati za shida
\s5
\v 26 Baada ya miaka ya majuma sitini na mbili, mtiwa mafuta ataharibiwa na atakuwa hana kitu chochote. Jeshi la kiongozi ajaye litauangamiza mji na mahali patakatifu. Mwisho wake utatatokea kwa gharika, na kutakuwa na vita hata mwisho. Uharibifu umekwisha amriwa.
\s5
\v 27 Atalithibitisha agano pamoja na watu wengi kwa miaka saba. Katikati ya miaka saba atakomesha dhabihu na sadaka. Baada ya chukizo la uharibifu atatokea mtu atakayeleta ukiwa. Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ujumbe ulifunuliwa kwa Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza. Ujumbe huu ulikuwa ni wa kwelil. Ulihusu vita kuu. Danieli aliufahamu ujumbe alipopata ufumbuzi kutoka katika maono.
\s5
\v 2 Katika siku hizo, mimi Danieli, nilikuwa katika maombolezo kwa wiki tatu.
\v 3 Sikula chakula kizuri, sikula nyama, sikunywa divai, na sikujipaka mafuta mwenyewe mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzima.
\s5
\v 4 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa niko karibu na mto mkubwa (ambao ni Tigrisi),
\v 5 Nilitazama juu na nikamwona mtu aliyevaa kitani, akiwa na mkanda kiunoni mwake uliotengenezwa kwa dhahabu safi kutoka Ufazi.
\v 6 Mwili wake ulikuwa kama kito, na sura yake ilikuwa kama radi. Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi, na mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa. Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu.
\s5
\v 7 Mimi, Danieli peke yangu niliyaona maono, na watu niliokuwa na pamoja hawakuyaona maono. Lakini, jambo kuu la kuogofya liliwaijia juu yao, na walikimbia na kujificha wao wenyewe.
\v 8 Hivyo niliachwa peke yangu na niliyaona maono haya ajabu. Hakuna nguvu iliyobakia ndani yangu; mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu, na hazikubakia nguvu ndani yangu.
\v 9 Kisha nikasikia maneno yake, na nilipoyasikia, nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito.
\s5
\v 10 Mkono ulinigusa, na ilinifanya nitetemeke katika magoti yangu na viganja vya mikono yangu.
\v 11 Malaika aliniambia, "Danieli, mtu aliyetunzwa sana, yafahamu maneno ninayokwambia wewe. Simama wima, kwa kuwa nimeshakutuma." Na alipomaliza kuniambia ujumbe huu, nilisimama nikiwa natetemeka.
\s5
\v 12 Kisha aliniambia, "Usiogope, Danieli. Tangu siku ya kwanza ulipoiweka akili yako kutaka kufahamu na kujinyenyekeza mwenyewe mbele ya Mungu, maneno yako yalisikiwa, na nimekuja kwasababu ya maneno yako.
\v 13 Mwana wa mfalme wa ufalme wa Uajemi alinizuia, na niliwekwa huko na mfalme wa Uajemi kwa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja kati ya wakuu alikuja kunisaidia.
\s5
\v 14 Sasa nimekuja kukusaidia ili ufahamu kile kitakachotokea kwa watu wako katika siku za mwisho. Kwa kuwa maono ni kwa ajili siku ambazo hazijatokea bado.
\v 15 Na alipokuwa akali akiniambia maneno haya, niligeuza uso wangu na kuuelekeza chini na sikuwa na uwezo wa kuzungumza.
\s5
\v 16 Yeye aliyekuwa kama wana wa mtu alinigusa mdomo wangu na nifumbua kinywa changu na nilimwambia huyo aliyekuwa amesimam mbele yangu: "Bwana wangu, niko katika masumbuko makali kwasababu ya maono; sina nguvu ndani yangu iliyosalia.
\v 17 Mimi ni mtumishi wako. Je ninawezaje kuongea na Bwana wangu? Kwa kuwa sasa sina nguvu, na hakuna pumzi iliyosalia ndani yangu."
\s5
\v 18 Tena yule mwenye mwonekano wa mtu alinigusa na kunitia nguvu.
\v 19 Alisema, "Usiogope, mtu ulithaminiwa sana. Amani na iwe kwako! Uwe mwenye nguvu, uwe na nguvu!" Na alipokuwa anaongea na mimi, nilipata nguvu. Nilimwambia, "Bwana wangu na aseme, kwa kuwa umenitia nguvu."
\s5
\v 20 Aliniambia, "Je unajua ni kwanini nimekuja kwako? Nitarudi hivi karibuni kupigana na mkuu wa Uajemi. Na nitakapoenda, mkuu wa Ugiriki atakuja.
\v 21 Lakini nitakwambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Ukweli. Hakuna yeyote anayejionesha kuwa na nguvu pamoja nami dhidi yao, isipokuwa Mikaeli mkuu wenu."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Dario Mmedi, mimi mwenyewe nilikuja kumwezesha na kumlinda Mikaeli.
\v 2 Na sasa nitakufunulia ukweli. Wafalme watatu watainuka katika Uajemi, na mfalme wa nne atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Na wakati atakapopata nguvu kupitia utajiri wake, atamwamsha kila mtu kinyume na ufalme wa Ugiriki.
\s5
\v 3 Mfalme wenye nguvu atainuka ambaye atatawala ufalme mkubwa, na ataenenda kufuatana na matakwa yake mwenyewe.
\v 4 Na atakapokuwa ameinuka, ufalme wake utavunjika na utagawanyika katika pepo nne za mbinguni, lakini hawatakuwa wazao wake mwenyewe, na si kwa nguvu zake kwa wakati alipokuwa akitawala. Kwa kuwa ufalme wake utang'olewa kwa ajili ya wengine tofauti na wazawa wake.
\s5
\v 5 Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mwenye nguvu kuliko yeye na atautawala ufalme wake kwa nguvu kubwa.
\v 6 Baada ya miaka michache, wakati muda utakapokuwa sawa, watafanya mwungano. Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao. Lakini hataweza kuzitunza nguvu za mkono wake, wala mfalme hatasimama wala mkono wake. Ataachwa na wale waliomleta, na baba yake, na yeye aliyemwunga mkono katika nyakati hizo.
\s5
\v 7 Lakini tawi kutoka katika mizizi yake litachipuka katika nafasi yake. Atalishambulia jeshi na kuingia ngome ya mfalme wa Kaskazini. Atapigana nao, na atawashinda.
\v 8 Ataichukua miungu yao mpaka Misri pamoa na sanamu zao za chuma na vyombo vyao vya fedha na vya dhahabu vyenye thamani. Kwa miaka mingi atakaa mbali na mfalme wa Kaskazini.
\v 9 Kisha mfalme wa Kaskazini atauvamia ufalme wa mfalme wa Kusini, lakini atajitoa na kwenda katika nchi yake mwenyewe.
\s5
\v 10 Wana wake watajiweka tayari na kuunganisha jeshi kubwa. Litaendelea kukua na litagharikisha kila kitu, litapita katikati hadi kwenye ngome yake.
\s5
\v 11 Ndipo mfalme wa Kusini atakasirika, na ataenda na kupigana naye, mfalme wa Kaskazini. Mfalme wa Kaskazini atainua jeshi kubwa, bali jeshi litatiwa katika mkono wake.
\v 12 Jeshi litachukuliwa, na moyo wa mfalme wa Kusini utainuliwa juu, na atawafanya makumi maelfu kuanguka, lakini hataweza kuwa mshindi.
\s5
\v 13 Kisha mfalme wa Kaskazini atainua jeshi jingine, kubwa kuliko la kwanza. Baada ya miaka kadhaa, mfalme wa Kaskazini atakuja na jeshi kubwa likiwa na vifaa vingi.
\s5
\v 14 Katika siku hizo wengi watainuka kinyume na mfalmea wa Kusini. Wana wa vurugu miongoni mwa watu wake watasimama wao wenyewe ili kuyatimiliza maono, lakini watajikwaa.
\s5
\v 15 Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima, na kuuteka mji wenye ngome. Majeshi ya Kusini hayataweza kusimama, hata wanajeshi wake bora. Hawatakuwa na nguvu za kusimama.
\v 16 Badala yake, yeye ajaye ataenenda kwa kufuata tamaa zake kinyume chake; hakuna yeyote atakayesimama katika njia yake. Atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi wake.
\s5
\v 17 Mfalme wa Kaskazini atauelekeza uso wake ili kuja kwa nguvu za ufalme wake wote, na kutakuwa na makubaliano atakayoyafanya na mfalme wa Kusini. Atampatia katika ndoa binti wa wanawake ili kuuharibu ufalme wa Kusini. Lakini mpango huo hautafanikiwa wala kumsaidia.
\v 18 Baada ya hayo, mfalme atafuatilia nchi za pwani na ataziteka nchi nyingi. Lakini amiri jeshi atakikomesha kiburi chake na atakisababisha kiburi chake kiishe.
\v 19 Kisha atafuatilia miji yenye ngome katika nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka; na hatapatikana tena.
\s5
\v 20 Kisha mtu mwingine atainuka katika nafasi ambaye atamfanya mtoza ushuru apite kwa ajili ya ufahari wa ufalme. Lakini katika siku zijazo atakatiliwa mbali, lakini si kwa hasira wala si katika vita.
\v 21 Katika nafasi atainuka mtu wa kudharauliwa ambaye watu hawatampa heshima ya nguvu ya kifalme; atakuja bila kukusudiwa na atautwaa ufalme kwa ulaghai.
\v 22 Mbele yake, kila jeshi litafutiliwa mbali kama gharika. Jeshi na kiongozi wa agano wataangamizwa wote kwa pamoja.
\s5
\v 23 Tangu katika kipindi kile ambacho makubaliano yalifanywa pamoja naye, ataenenda kwa kwa hila; atakuwa mwenye nguvu akiwa na watu wachache tu.
\v 24 Kwa ghafla ataingia katika sehemu tajiri sana za jimbo, na atafanya kile ambacho si baba yake wala baba wa baba yake alishakifanya. Atagawanya mateka, nyara, na mali zake miongoni mwa wafuasi wake. Atapanga mpango wa kuiangusha ngome, lakini ni kwa muda tu.
\s5
\v 25 Ataamsha nguvu zake na moyo wake kinyume na mfalme wa Kusini kwa jeshi kubwa. Mfalme wa Kusini atapigana vita akiwa na jeshi kubwa lenye nguvu, lakini hataweza kusimama kwa kuwa wengine watafanya njama dhidi yake.
\v 26 Hata wale wanaokula chakula chake kizuri watajaribu kumwangamiza. Jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika, na wengi wao watauawa.
\v 27 Wafalme wote hawa wawili, wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake, watakaa katika meza moja na kudanganyana, lakini haitakuwa na maana yoyote. Kwa kuwa mwisho utatokea katika kipindi ambacho kimeshapangwa.
\s5
\v 28 Kisha mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake akiwa na utajiri mkubwa, na moyo wake ukipinga vikali agano takatifu. Atatenda na kisha atarudi katika nchi yake mwenyewe.
\s5
\v 29 Katika muda uloamriwa atarudi na kuushambulia ufalme wa Kusini. Lakini katika kipindi hiki hakitakuwa kama awali.
\v 30 Kwa kuwa meli kutoka Kitimu zitamshambulia, naye ataogopa na kurudi nyuma. Atakuwa mwenye hasira dhidi ya agano takatifu, na atawaonyesha mema wale watakaoliacha agano takatifu.
\s5
\v 31 Majeshi yake yatainuka na kukufuru sehemu takatifu katika ngome. Wataziondoa sadaka za kawaida za kuteketezwa, na watasimamisha chukizo la uharibifu litakalosababisha ukiwa.
\v 32 Na kwa wale walioenenda kwa ouvu kinyume na agano, atawadanganya na kuwatia uovu. Bali watu wale wanaomjua Mungu wao watakuwa jasiri na watachukua hatua.
\s5
\v 33 Watu wenye hekima miongobi mwa watu watawafanya watu waelewe. Lakini watajikwaa kwa upanga na kwa miali ya moto; watatiwa mateka na kunyang'anywa kwa siku.
\v 34 Katika siku za kujikwaa kwao, watasaidiwa kwa msaada kidogo. Watu wengi watajiunga nao wenyewe katika unafiki.
\v 35 Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa ili kujisafisha kutokee kwao, na kujiosha, na kujitakasa, mpaka wakati wa mwisho. Kwa kuwa wakati ulioamriwa haujaja bado.
\s5
\v 36 Mfalme atafanya kutokana na matakwa yake. Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa kuliko kila mungu. Kinyume cha Mungu wa miungu, atasema vitu vibaya, kwa kuwa atafanikiwa mpaka pale ghadhabu itakapokuwa imekamilika. Kwa ajili kile kilichoamriwa kitakapokuwa kimefanyika.
\v 37 Hatazijali miungu ya baba zake wala mungu anayependwa na wanawake. Wala hatamjali mungu mwingine yeyote. Kwa kuwa zaidi ya mtu yeyote atajifanya mwenyewe kuwa mkuu.
\s5
\v 38 Atamheshimu mungu wa ngome badala ya haya. Ni mungu ambaye baba zake hawakumkubali ambaye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa mawe ya thamani na zawadi zenye kuthaminiwa.
\v 39 Atazishambulia ngome imara sana kwa msaada wa mungu mgeni. Atampa heshima kubwa yeyote anayemkubali. Atawafanya kuwa watawala juu ya watu wengi, na ataigawanya nchi kama thawabu.
\s5
\v 40 Kwa wakati wa mwisho mfalme wa Kusini atamshambulia. Mfalme wa Kaskazini atamvamia kwa ukali wa magari na wapanda farasi, na meli nyingi. Naye ataenda kinyume cha nchi, kuwagharikisha, na kupita katikati.
\v 41 Naye ataingia katika nchi ya uzuri, makumi elfu ya Waisraeli wataanguka. Lakini watu hawa watatoroka kutoka katika mkono wake: Waedomu, Wamoabu, na mabaki ya watu wa Amoni.
\s5
\v 42 Naye ataunyosha mkono katika nchi; nchi ya Misri haitaokolewa.
\v 43 Atakuwa na mamlaka juu ya hazina za dhahabu na za fedha, na juu ya utajiri wote wa Misri; watu wa Libya na Ethiopia watakuwa chini katika nyayo za miguu yake.
\s5
\v 44 Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamwogopesha, naye atatoka akiwa mwenye hasira nyingi kuwa ili kuwaharibu kabisa na kuwahifadhi kwa ajli ya uharibifu.
\v 45 Naye ataisimamisha hema ya makao yake ya kifalme kati ya bahari na milima ya uzuri wa utakatifu. Ataufikia mwisho wake, na hapatakuwa na msaidizi wa kumsadia.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Katika kipindi hicho, Mikaeli, jemedari mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwa na wakati wa mateso ambao haujawahi kutokea tangu mwanzo wa taifa lolote mpaka kipindi hicho. Katika muda huo watu wako wataokolewa, yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu.
\v 2 Na wengi wa wale waliolala katika mavumbi ya dunia watainuka. baadhi kwa uzima wa milele na baadhi kwa ajili ya fedheha na matwezo ya milele.
\s5
\v 3 Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele.
\v 4 Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya; kihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa chapa mpaka nyakati za mwisho. Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.
\s5
\v 5 Kisha mimi, Danieli, nilitazama, na kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama. Mmoja alisimama katika upande huu wa ukingo wa mto, na mwingine alisimama katika ukingo wa upande mwingine wa mto.
\v 6 Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani, yeye aliyekuwa juu ya mkondo wa mto, "Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?"
\s5
\v 7 Nilimsikia mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu katika mkondo wa mto, aliinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni na kuapa kwa yeye aishiye milele kwamba itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati. Na wakati nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimeshaharibiwa, mambo haya yote yatakuwa yamemalizika.
\s5
\v 8 Nilisikia, lakini sikufahamu. Basi nikamwuliza, "Bwana wangu, mambo haya yote yatakuwa na matokeo gani?"
\v 9 Alisema, "Nenda zako Danieli, kwa kuwa maneno yamefungwa na kutiwa chapa mpaka wakati wa mwisho.
\s5
\v 10 Watu wengi watakuwa wametakaswa, wameoshwa, na kusafishwa, lakini waovu wataenenda katika uovu.
\v 11 Katika muda ule ambapo sadaka ya kawaida ya kuteketezwa itakapokuwa imeondolewa na chukizo la uharibifu liliosababisha ukiwa limesimamishwa, kutakuwa na siku zipatazo 1, 290.
\s5
\v 12 Ana heri mtu yule anayengojea mpaka mwisho wa siku 1, 335.
\v 13 Unapaswa uondoke uende njia yako hata mwisho, na kisha utapumzika. Utainuka katika sehemu uliyopewa, mwishoni mwa siku."