sw_ulb_rev/24-JER.usfm

2616 lines
215 KiB
Plaintext

\id JER
\ide UTF-8
\h Yeremia
\toc1 Yeremia
\toc2 Yeremia
\toc3 jer
\mt Yeremia
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ndilo neno la Yeremia mwana wa Hilikia; yeye alikuwa mmoja wa makuhani kule Anatothi katika nchi ya Benjamini.
\v 2 Neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wake.
\v 3 Lakini pia lilimjia katika wakati wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa Zedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipochukuliwa kuwa watumwa.
\s5
\v 4 Neno la BWANA lilinijia, likisema,
\v 5 "kabla sijakuumba tumboni, Nilikuchagua; kabla hujazailiwa toka tumboni Nilikutenga; Nilikufanya kuwa nabii kwa mataifa."
\v 6 "Ahaa, BWANA!" Nilisema, "mimi sijui kusema, kwa kuwa mimi ni mtoto."
\s5
\v 7 Lakini BWANA akaniambia, "Usiseme, 'mimi ni mtoto.' Utaenda kila mahali ninapokutuma, na utasema kila kitu ninachokuamuru!
\v 8 Usiwaogpe hao, kwa kuwa Mimi niko pamoja na wewe kukuokoa- asema BWANA."
\s5
\v 9 Kisha BWANA akanyosh mkono wake, akagusa kinywa changu, na akaniambia, "Nimeweka maneno yangu kinywani mwako.
\v 10 Nimekuchagua leo juu ya mataifa na juu ya mataifa, ili kung'oa na kuvunja, kuharibu na kutupa, kujenga na kupanda."
\s5
\v 11 Neno la BWANA lilinijia, likisema, "Yeremia, unaona nini?" Nikasema, "Ninaona tawi la mlozi."
\v 12 BWANA akaniambia, "umeona vyema, kwa kuwa ninaliangalia neno langu ili nilitimize."
\s5
\v 13 Neno la BWANA likaniji mara ya pili likisema, "Unaona nini? "Nikasema, "Ninaona chungu kikichemuka, ambacho mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini,"
\v 14 BWANA akaniambia, "Janga litatokea kaskazini juu ya wote wanaoishi katika nchi hii.
\s5
\v 15 Kwa kuwa ninayaita makabila yote ya falme za kaskazini, asema BWANA. Yatakuja, na kila mmoja atasimika enzi yake katika malango ya Yerusalemu, dhidi ya kuta zote zinazoizunguka, na dhidi ya miji ya Yuda.
\v 16 Nitatamka hukumu dhidi yao juu ya uovu wao wa kuniacha, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kwa kuabudu kile walichotengeneza kwa mikono yao.
\s5
\v 17 Jiandae! Simama ukawaambie kila kitu ninachokuamuru. Usifdhaike mbele zao nisije nikakufadhaisha wewe mbele zao!
\v 18 Tazama! Leo nimekufanya kuwa mji ulio na ngome, kuwa ngome ya chuma, na ukata wa shaba dhidi ya nchi yote - dhidi ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wote wa nchi.
\v 19 Watapigana na wewe, lakinai hawatakushinda, kwa kuwa nitakuwa pamoja na wewe ili kukuokoa- asema BWANA."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Neno la BWANA lilinijia likisema,
\v 2 "Nenda ukanene katika masikio ya Yerusalemu. Useme; BWANA asema hivi: Ninakumbuka agano la uaminifu la ujana wako, upendo wako wakati tulipokuwa tumechumbiana, ulipokuwa ukinihitaji kule jangwani, katika ile nchi iliyokuwa haijapandwa.
\v 3 Israeli alikuwa ametengwa kwa BWANA, malimbuko yake ya mavuno yake! Wote waliokula malimbuko yake walikuwa na hatia! majanga yaliwajia--asema BWANA.'"
\s5
\v 4 Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli.
\v 5 BWANA anasema hivi, "Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu?
\v 6 Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?
\s5
\v 7 Lakini nilwaleta katika nchi ya Kameli, ili mle matunda yake na vitu vingine vyema! Lakini mlipokuja, mliitia unajisi nchi yangu, mliufany urithi wangu kuwa chukizo!
\v 8 Hata makuhani hawakusema, 'BWANA yuko wapi?' na watalamu wa sheria hawakunijali mimi! wachungaji wametenda dhambi dhidi yangu. Manabii wamemtolea Baali unabii na kuvitafuta vitu ambvyo havina faida.
\s5
\v 9 Kwa hiyo nitaendelea kuwashitaki - hili ni neno la BWANA - na nitawashitiki watoto wa watoto wenu.
\v 10 Kwa kuvuka kwenda hadi pwani ya Kitimu na kutazama. Tuma wajumbe kwenda Kedari na tafuta uone kama kama iliwahi kutokea hapo awali vitu kama hivi.
\v 11 Je, taifa limebadilisha miungu, hata kama haikuwa miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia.
\s5
\v 12 Sitajabuni, enyi mbingu kwa sababu ya hili! Tetemekeni na kuogopa -asema BWANA.
\v 13 Kwa kuwa watu wangu wametenda maovu mawili dhidi yangu: Wameziacha chemichemi za maji ya uhai kwa kuchimba mabarika kwa ajili yao, mabarika yanayovuja yasiyoweza kutunza maji!
\s5
\v 14 Je, Israeli ni mtumwa? Kwani hakuzaliwa nyumbani? Kwa nini sasa amekuwa nyara?
\v 15 Wanasimba wameunguruma dhidi yake. Wamepiga kelele sana na kuifanya kuwa ukiwa. Miji yake imeharibiwa na kubaki bila watu.
\v 16 Pia watu wa Nufu na Tahapanesi watakinyoa kichwa chako.
\v 17 Je, hamkufanya haya kwa ajili yenu mlipomwacha BWANA, wakati Mungu wenu, alipokuwa akiwaongoza njiani?
\s5
\v 18 Kwa hiyo, kwa nini kutafuta msaada Misri na kunywa maji ya Shihori? Kwa nini kutafuta msaada Ashuru na kunywa maji ya Mto Frati?
\v 19 Uovu wako unakukemea, na maasi yako yatakuadhibu. Kwa hiyo yafikiri hayo; tambua kuwa ni uovu na uchungu kwenu ninyi kuniacha mimi, BWANA Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 20 Kwa kuwa niliivunja nira yenu mliyokuwa nayo wakati wa kale; Nilivichana vifungo vyako kutoka kwako. Lakini bado ulisema, 'Sitamtumikia!' tangu ulipopiga magoti katika kila kilima kuusogelea kila mti wenye majani mabichhi, enyi makahaba.
\v 21 Lakini mimi mwenyewe niliwapanda kama mzabibu niliouchagua, mbegu iliyokamilika. Lakini tazama jinsi ulivyobadilika mbele yangu, na kuwa mzabibu usiofaa na mzabibu pori!
\v 22 Kwa kuwa hata kama utajisafisha mwenyewe mtoni na kuoga kwa sabuni kali, bado dhambi yako ni madoa mbele yangu - asema BWANA Mungu.
\s5
\v 23 Wawezaje kusema, 'Mimi sijanajisika! Mimi sjaenda kwa Mabaal?' Tazama tabia zako zilivyokuwa bondeni! Tambua kile ulichofanya, wewe ngamia mwepesi! akimbiaye katika njia yake!
\v 24 Wewe ni punda wa mwitu, aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo usiofaa katika tamaa ya kuishi! Ni nani awezaye kumgeuza anapotafuta dume la kumpanda? Na punda dume amtafutaye hajichoshi mwenyewe. Huenda kwake wakati wa mwezi wa kupandwa.
\v 25 Lazima uizuie miguu yako isikose kiatu na koo lako kuwa na kiu! Lakini umesema, 'Hakuna matumaini! Hapana! Nawapenda wageni nami huwatafuta!'
\s5
\v 26 Kama aibu ya mwizi ilivyo anapokuwa amekamatwa, ndivyo aibu ya Israeli itakavyokuwa - wao, wafalme wao, malikia wao, makuhani na manabii wao!
\v 27 Hawa ndio wale waiambiayo miti, 'Ninyi ndio baba zangu,' na mawe, 'Ninyi ndio mlinizaa.' Kwa kuwa migongo yao hunitazama na siyo nyuso zao. Hata hivyo, wakati wa shida husema, 'Amka utuokoe!'
\v 28 Lakini iko wapi ile miungu mliyojitengenezea? Acha hao wainuke kama wanaweza kuwaokoa wakati wa shida, kwa kuwa hizo sanamu zenu zina idadi sawa na miji yenu, katika Yuda.
\s5
\v 29 Kwa hiyo kwa nini kunituhumu kwa kufanya makosa? Ninyi nyote mmeniasi - asema BWANA wa majeshi.
\v 30 Nimewadhibu watu wenu bure. Wala hawakutaka kurudiwa. Upanga wako umewaangamiza manabii wenu kama kama simba aangamizaye!
\v 31 Enyi watu wa kizazi hiki! Sikilizeni neno langu, neno la BWANA! Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza nene? Kwa nini watu wangu husema, 'Acha tuzungukezunguke, hatutakuja kwako tena'?
\s5
\v 32 Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wngu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
\v 33 Jinsi mlivyotengeneza njia zenu vizuri ili kutafuta mapenzi. Hata mmewafundisha njia zenu wanawake waovu.
\v 34 Damu ambayo ilikuwa ndio uhai wa watu wasio na hatia, imeonekana katika mavazi yenu. Hawa watu hawajawahi kuonekana katika matendo maovu.
\s5
\v 35 Pamoja na mambo haya yote, wewe unaeendelea kusema kuwa hauna hatia. Kwa hakika hasira ya BWANA itageuka kutoka kwangu. 'Lakini tazama! Utahukumiwa kwa sababu, 'Sikutenda dhambi.'
\v 36 Kwa nini mnatangatanga kwa urahisi katika njia zenu? Pia Misri itawahuzunisha sana, kama ilivyokuwa kwa Ashuru.
\v 37 Mtaondoka hapo mkiwa mmehuzunika sana, mkiwa mmeweka mikono vichwani mwenu, kwa kuwa BWANA amemkutaa yule mliyemtumainia, kwa hiyo hamtapata msaada toka kwao,"
\s5
\c 3
\p
\v 1 Wanaema, 'Mwanamume akimfukuza mke wake, naye akaondoka kwake na kuwa mke wa mwanamume mwingine. Je, anaweza kumrudia tena? Je huyo si najisi kabisa?' Huyo mwanamke ndiyo hii nchi! Mmetenda kama kama Kahaba aliye na wapenzi wengi, na sasa mnapenda kurudi kwangu tena? - asema BWANA wa majeshi.
\v 2 Inua macho yako uvitazame vielele tasa! Je kuna mahali ambapo hukufanya ukahaba? Pembeni mwa barabara ulikaa ukisubiri wapenzi wako, kama vile Mwarabu jangwani. Uneiharibu nchi kwa ukahaba na uovu wako.
\s5
\v 3 Kwa hiyo chemichemi za mvua zilizuiliwa na mvua za vuli hazikunyesha. Lakini uso wako una kiburi, kama uso wa mwanamke kahaba. Unakataa kuona aibu.
\v 4 Na sasa hutaniita mimi: 'Baba yangu, hata marafiki zangu wa tangu ujanani! Je, atakuwa na hasira dhidi yangu milele?
\v 5 Je, utaendelea kuwa na hasira zako?' Tazama! Umesema kuwa utatenda maovu, na kweli umetenda hivyo. kwa hiyo endelea kufanya hivyo!"
\s5
\v 6 Kisha BWANA akanena nami katika siku za mfalme Yosia, "Je, unaona jinsi Israeli alivyoniasi? Yeye anaenda kwenye kila kilima na katika kila mti wenye majani mabichi, na kule anafanya kama mwanamke kahaba.
\v 7 Nikisema, 'Baada ya kuwa amefanya mambo haya yote, atanirudia,' lakini hakurudi. Kisha dada yake Yuda ambaye ni mwasi pia aliona alichokifanya.
\s5
\v 8 Kwa hiyo nami nikaona kuwa kwa sababu amefanya uzinzi huu wote. Huyo Israeli aliyeasi! Nilimfukuza na kumpatia talaka ya ndoa. Lakini dada yake Yuda mwenye hiana hakuwa na hofu, na yeye akaenda kuafanya kama mwanamke kahaba!
\v 9 Hukusikitika kuwa ameinajisi nchi, kwa hiyo wakatengeneza sanamu za mti na za jiwe.
\v 10 Kisha baada ya haya yote, wala Yuda dada yake muasi hakurudi kwangu na moyo wake wote, bali alikuja na uongo! -asema BWANA wa majeshi,"
\s5
\v 11 Kisha BWANA akanena na mimi, "Israeli muasi amekuwa mwenye haki zaidi kuliko Yuda muasi!
\v 12 Nenda ukaseme maneno haya huko kaskazini. Uwaambie, 'Rudi wewe Israeli uliyeasi! - asema BWANA - sitakuwa na hasira dhidi yako. Kwa kuwa mimi ni mwaminifu - asema BWANA - sitakuwa na hasira milele.
\s5
\v 13 Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako mgeni chini ya kila mti wenye majani mabichi! wala hukuisikiliza sauti yangu! - asema BWANA.
\v 14 Rudini, enyi watu waasi! - asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni!
\v 15 Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu.
\s5
\v 16 Ndipo itakapotokea kuwa utaongezeka na kuzaa matunda katika nchi hiyo siku hizo-asema BWANA. Hawataweza kusema kuwa, "Sanduku la agano la BWANA! Jambo hili hawatalikumbuka tena katika mioyo yao, kwa kuwa hawataliwaza tena wala kulijali tena. Usemi huu hawatausema tena.'
\s5
\v 17 Katiak wakati huo watasema juu ya Yerusalemu, 'Hii ndiyo enzi ya BWANA,' na mataifa mengine yote yatakusanyika Yerusalemu katika jna la BWANA. Hawataishi katika taabu ya uovu wa mioyo yao.
\v 18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaishi na nyumba ya Israeli. Watarudi pamoja kutoka katika nchi ya kaskazini katika nchi niliyowapa mababu wao kuwa urithi.
\s5
\v 19 Lakini mimi, Nilisema, 'Jinsi nipendavyo kukuheshimu kama mwanangu na kukupa nchi ipendezayo, kuwa urithi mzuri kuliko ulio katika taifa lolote!' Nami nikasema, ''mtaniita baba yangu''.'Nami nitasema kwamba hamtageuka na kuacha kunifuata.
\v 20 Lakini kama mwanamke aliyemwasi mume wake, mmenisaliti, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA."
\s5
\v 21 Sauti ilisikika juu ya nyanda, kilio na kusihi kwa watu wa Israeli! kwa kuwa wamezibadili njia; wamemsahau BWANA, Mungu wao.
\v 22 "Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!" "Tazama! tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu!
\s5
\v 23 Uongo hutoka kwenye vilima, kutoka kwenye milima mingi. Kwa hakika wokovu wa Israeli unapatikana kwa BWANA, Mungu wetu.
\v 24 Lakini miungu ya aibu imeramba kazi ambayo mababu zetu waliifanya - makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao!
\v 25 Na tulale chini kwa aibu. Aibu yetu na itufunike, kwa kuwa tumefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wetu! Sisi wenyewe na mababu zetu, kutoka wakati wa ujana wetu hadi leo, hatujaisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wetu!"
\s5
\c 4
\p
\v 1 "Kama utarudi, Israeli- asema BWANA - ikawa kwangu kwamba umerudi. Kama utaondoa hayo mambo yachukizayo mbele yangu na ukaacha kunikimbia mimi tena,
\v 2 na ukaapa hivi, 'kama BWANA aishivyo katika kweli, na haki, na katika hukumu.' mataifa yataniomba baraka, na yatanisifu mimi.
\v 3 Kwa kuwa BWANA asema hivi kwa kila mmoja katika Yuda na Yerusalemu; 'Limeni shamba zenu na msipande katika miiba.
\s5
\v 4 Mtahiriwe kwa BWANA na kuondoa govi za mioyo yenu, ninyi wanaume wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, vinginevyo hasira yangu itawaka kama moto na kuteketeteza, na hakutakuwa na mtu wa kuizima. Hii itatokea kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
\v 5 Waambie Yuda na Yerusalemu isikie. Waambie, "pigeni baragumu katika nchi." Tangazeni, "Kusanyeni pamoja. Twendeni kwenye miji ya Maboma."
\v 6 Inueni ishara za bendera na zielekezeni Sayuni, na kimbilieni usalama! Msibaki, kwa kuwa ninaleta majanga kutokea kaskazini na anguko kubwa.
\s5
\v 7 Simba anakuja kutokea kwenye kichaka chake na yeye atakayeyaharaibu mataifa ameanza kuja. Anaondoka kwenye eneo lake ili aache hofu katika nchi yenu, kuibadili miji yenu kuwa uharibifu, ambapo hakuna hata mmoja atakayeishi. Kwa sababu hii vaeni magunia, lieni na kuomboleza.
\v 8 Kwa kuwa nguvu ya hasira ya BWANA haijaondoka kwetu.
\s5
\v 9 Ndipo itakapotokea katika siku hiyo - asema BWANA - mioyo ya mfalme na wakuu itakufa. Makuhani watasitaajabu na manabii watashangaa.'"
\v 10 Kwa hiyo nikasema, "Ahaa! BWANA. Kwa hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kuwaambia, 'Kutakuwa na amani kwenu.'Wakati upanga unawaangukia dhidi ya maisha yao."
\s5
\v 11 Wakati huo itasemwa juu ya mji huu na Yerusalemu kuwa, "Upepo uwakao kutoka katika nyanda za jangwani utachukua njia yake kuelekea kwa binti ya watu wangu. Hautapepetwa wala kuwatakasa.
\v 12 Upepo ulio na nguvu sana utakaokuja kwa amri yangu, na sasa nitapitisha hukumu dhidi yao.
\s5
\v 13 Tazama anavamia kama wingu, na magari yake ni kama dhoruba. Farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu kwa kuwa tutaharibiwa!
\v 14 Itakaseni mioyo yenu kutoka uovu wenu, Yerusalemu, ili kwamba muokolewe. Mawazo yako mabaya yatafikiri juu ya kutenda dhambi mpaka lini?
\v 15 Kwa kuwa kuna sauti iletayo habari kutoka Dani, na janga lijalo linasikika kutoka vilele vya milima ya Efraimu.
\s5
\v 16 Yafanyeni mataifa kulifikiria hili: Tazama, na uwatangazie Yerusalemu kuwa wale watekaji wanakuja kutoka katika nchi ya mbali ili kupiga kelel za vita juu ya miji ya Yuda.
\v 17 Watakuwa kama walinzi wa shamba liliolimwa dhidi yake pande zote, kwa kuwa amekuwa mpinzani wangu - asema BWANA -
\v 18 tabia na matendo yako yamesababisha haya yatokee kwako. Hii itakuwa adhabu yako. Jinsi itakavyokuwa vibaya kwako! itakupiga moyo wako.
\s5
\v 19 Moyo wangu! Moyo wangu! Niko katika maumivu ya moyo. Moyo wangu umefadhaika ndani yangu. Siwezi kunyamaza kwa kuwa nasikia sauti za pembe, sauti za vita.
\v 20 Anguko baada ya anguko limetangazwa, kwa nchi yote imeharibika mara. Wanaharibu masikani yangu na hema yangu ghafula.
\s5
\v 21 Vita hivi vitaendelea mpaka lini? Ni mpaka lini nitasikiliza sauti za pembe?
\v 22 Kwa kuwa upumbavu wa watu wangu - hawanijui mimi. Ni watu wajinga wasio na ufahamu. Wanaufahamu wa mambo maovu, tena hawajui kutenda mema.
\s5
\v 23 Niliiona nchi, na kuiona! ilikuwa ukiwa na utupu. Kwa kuwa hapakuwa na taa za mbinguni.
\v 24 Nilitazama katka miliima. Tazama, ilikuwa inatetemeka, na vilima vyote vilikuwa vinatikisika.
\v 25 Nilitazama. Tazama, hapakuwa na mtu, na ndege wote wa angani walikuwa wamekimbia.
\v 26 Nikaangalia. Tazama, mashamba yalikuwa jangwa na miji imeangushwa mbele za BWANA, mbele ya hasira yake."
\s5
\v 27 Hiki ndicho BWANA asemacho, "Nchi yote itakuwa uharibifu, lakini sitawaharibu wote kabisa.
\v 28 Kwa sababu hii nchi itaomboleza, na mbingu juu zitatiwa giza. Kwa kuwa nimesema haya na kuyakusudia; sitarudi nyuma; Sitaacha kuyatekeleza.
\v 29 Kila mji utakimbia kutoka katka kelele za wapandafarasi na wenye pinde; Watakimbilia msituni, Kila mji utapanda hadi mahali pa miamba. Miji itatelekezwa, kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuishi katika miji hiyo.
\s5
\v 30 Sasa umeharibiwa, utafanya nini? Japokuwa unavaa mavazi mekundu, unajipamba na mapambo ya dhahabu, na kuyafanya macho yako yaonekane makubwa na kupakwa wanja, wale wanaume waliokutamani sasa wanakukataa. Badala yake wanajaribu kukuua.
\v 31 Kwa hiyo nasikia sauti ya maumivu, yenye utungu kama ya mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti wa Sayuni. Atwetaye kupata pumzi. Ananyosha mikono yake na kusema, 'Ole wangu mimi! ninazimia kwa sababu ya wauaji hawa.'"
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kimbieni mkapite katika mitaa ya Yerusalemu, Tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja anayetenda kwa haki na kufanya kwa uaminifu, basi nitaisamehe Yerusalemu.
\v 2 Hata kama wanasema, 'Kama BWANA aishivyo,' wanaapa uongo."
\v 3 BWANA, macho yako hayatazami uaminifu? Unawapiga watu, lakini hawasikii maumivu. Umewaangsmiza kabisa, lakini bado wanakataa kuwa waadilifu. Wanafanya nyuso zao kuwa ngumu kama mwamba. kwa kuwa wanakataa kutubu.
\s5
\v 4 Kwa hiyo nilisema, "Hakika hawa ni watu masikini, Ni wapumbavu, Kwa kuwa hawazijui njia za BWANA, wala maagizo ya Mungu wao.
\v 5 Nitaenda kwa watu wa muhimu na kutangaza ujumbe wa Mungu kwao, kwa kuwa angalau wanazijua njia za BWANA, maagizo ya Mungu wao. Lakini wote wanavunja nira yao pamoja; wote wanaivunja ile minyororo inayowafunga kwa ajili ya Mungu.
\v 6 Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawavamia. Mbweha kutoka Arabaha atawaangamiza. Chui ataivunja miji yao. Mtu yeyota anayeenda nje ya mji wake atavunjwavunjwa. Kwa kuwa maovu yao yameongezeka. Matendo yao ya uasi hayana ukomo.
\s5
\v 7 Kwa nini niwasamehe hawa watu? Wana wenu wameniacha na wamefanya viapo na wale ambao si miungu. Niliwalisha vya kutosha, lakini wamefanya uasherati na kuchukua alama za nyumba ya uzinzi.
\v 8 Walikuwa farasi wanaotafuta kupandwa. Walitembea huku na huku wakitafutwa kupandwa. Kila mwanamume alimkaribia mke wa jirani yake.
\v 9 Kwa hiyo kwa nini nisiwaadhibu - asema BWANA - na kwa nini nisijilipizie kisasi juu ya taifa kama hili?
\s5
\v 10 Nenda hadi kwenye kuta za shamba lake la mizabibu na zihariibuni. Lakini wao msiwaharibu kabisa. Ondoeni matawi kwa sababu hayatoki kwa BWANA.
\v 11 Kwa sababu nyumba ya Yuda na Israeli wamenisaliti kabisa - asema BWANA -
\v 12 na wamenikataa. Wanasema, ''Yeye si halisi. Maovu hayawezi kutupata, wala hatutaona upanga wala njaa.
\v 13 Kwa kuwa manabii wamekuwa si kitu kama upepo na hakuna mtu mwiingine wa kunena ujumbe wa BWANA kwetu. Vitisho vyao na viwjie wao wenyewe."'
\s5
\v 14 Kwa hiyo BWANA, Mungu wa majeshi asema hivi, tazama nataka kuweka maneno yangu katika kinywa chako. Yatakuwa kama moto na watu hawa watakuwa kama kuni! Kwa kuwa utawaramba.
\v 15 Tazama nataka kuleta taifa dhidi yenu kutoka mbali, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA - ni taifa linalodumu, taifa la kale! Ni taifa ambalo lugha yake hamuijui, wala hamtaelewa wasemacho.
\s5
\v 16 Podo lao ni kaburi wazi. Wote ni wanajeshi.
\v 17 Kwa hiyo mavuno yako yataliwa, wana wako na binti zako pia, na chakula chako. Watakula kondoo wako na ng'ombe wako, watakula matunda ya zabibu zako na ya mitiini. Wataiangusha chini miji yenu na boma zake ambazo mnazitumainia.
\s5
\v 18 Lakini hata katika siku hizo - asema BWANA - sikusudii kuwaharibu kabisa.
\v 19 Itatokea kwenu, ninyi Yuda na Israeli, mkisema, 'Kwa nini BWANA, Mungu wetu ametufanyia haya yote?' kwamba wewe Yeremia, utawaambia, 'Kama vile mlivyomwacha BWANA na kuabudu miungu mingine katika nchi yenu, vivyo hivyo mtawatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.'
\s5
\v 20 Waambia haya watu wa nyumba ya Yakobo na yasikike katika Yuda. Waambie,
\v 21 'Sikilizeni hili, eny watu wapumbavu! Sanamu hazina matakwa; zina masikio lakini haziwawezi kusikia.
\v 22 Je, hamnihofu mimi - asema BWANA - au kutetemeka mbele ya uso wangu? Nimeweka mpaka wa mchanga kwenye bahari, ambao ni agizo la kudumu ambalo halibomoki - hata kama bahari ina kupwa na kujaa, bado hauwenzi kubomoka. Hata kama mawimbi yake yanaunguruma, hayawezi kuvuka.
\s5
\v 23 Lakini hawa watu wana mioyo ya usumbufu. Hugeuka kuwa wapinzani na kuondoka.
\v 24 Kwa kuwa hawasemi mioyoni mwao, "basi na tumche BWANA, Mungu wetu, yeye aletaye mvua za awali na mvua za vuli - kwa wakati wake, ambaye hutuzna majuma ya mavuno kwa ajili yetu."
\v 25 uovu wako umezuia haya yasitokee. Dhambi zako zimeyazuia mambo mema yasitokee.
\s5
\v 26 Kwa watu waovu wamo kati ya watu wangu. Wanatazama kama mtu anayenyatia ili kukamata ndege; wanaweka mitego na kukamata watu;
\v 27 Kama tundu la mtego lijaavyo ndege, nyumba zao zimejaa uongo. Kwa hiyo wanakua na kutajirika.
\v 28 Wamenenepa; wanang'aa na kupendeza. Wamepitiliza hata mipika ya maovu. Wala hawajali sababu ya kuwepo kwa watu na wala uwepo wa yatima. Wanafanikiwa hata kama hawatoi hukumu ya haki kwa yatima.
\v 29 Kwa nini nisiwadhibu kwa sababu ya haya - asema BWANA - sitajilipizia kisasi juu ya taifa la namna hii?
\s5
\v 30 Jambo la ajabu na la kuchukiza limetokea katika nchi hii.
\v 31 Mananbii wanatabiri kwa uongo, na makuhani wanatwala kwa msaada wa wa hao. Watu wangu wanapenda mambo ya hivyo, lakini mwisho kitatokea nini?
\s5
\c 6
\p
\v 1 Tafuteni mahali salama, enyi watu wa Benjamini, kwa kuondoka Yerusalemu. Pigeni tarumbeta zaTekoa. Simamisheni ishara juu ya Beth- Hakeremu, kwa uovu unaonekana ukitokea kaskazinni; pigo kubwa linakuja.
\v 2 Binti za Sayuni, warembo na mwororo, wataangamizwa.
\v 3 Wachungaji na kondoo wao watawaendea; wataweka hema zao zikiwazunguka pande zote; kila mtu atachunga kwa mkono wake.
\s5
\v 4 Jitakaseni wenyewe kwa miungu kwa ajili ya vita. Twendeni tukamvamie wakati wa adhuhuri. Ni vibaya sana kwamba mchana unatoweka na vivuli vya jioni vinakuja.
\v 5 Lakini tumvamieni usiku na na tuharibu ngome zake.
\s5
\v 6 Kwa kuwa BWANA wa majeshi asema hivi: Kateni miti yake, na tengenezeni vifusi vya kuitekea Yerualemu. Huu ndio mji sahihi kuuteka, Kwa sababu umejaa ukandamizaji.
\v 7 Kama vile kisima kitoavyo maji, vivyo hivyo mji huu uzaavyo uovu. Uaribifu na jeuri vimesikika kwake. Mateso na tauni viko mbele yangu daima.
\v 8 Uadhibiswhe, ee Yerusalemu, vingenevyo nitaondoka kwako na kukufanya ukiwa, na nchi isiyokaliwa na watu.
\s5
\v 9 BWANA wa majeshi asema hivi, "Hakika wataokota mabaki ya Isreli waliobaki kama zabibu. Nyosha mkono wako ili uchume zabibu.
\v 10 Nitamwambia nani na kumwonya nani ili wasikilize? Tazama! Masikio yao hayakutahariwa; hayawezi kutilia manani! Tazama! Neno la BWANA limekuja kuwarudi, lakini hawalitaki."
\s5
\v 11 Lakini nimejazwa na hasira za BWANA. Nimechoka kuizuia. Aliniambia, "Imwage mbele ya watoto mitaani na katika makundi ya vijana. Kwa kuwa kila mume atachukuliwa pamoja na mke wake; na kila mzee mwenye miaka mingi.
\v 12 Nyumba zao watapewa watu wengine, kwa kuwa nitawavamia wakazi wa nchi kwa mkono wangu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 13 BWANA amesema hayo kutoka kwa mdogo hadi kwa mkubwa, kila mmoja anatamani mapato ya udanganyifu. Kuanzia kuhani hadi nabii, Kila mmoja anafanya hila.
\v 14 Lakini wameponya vidonda vya watu wangu kwa juu juu tu. Wanasema, 'Amani! Amani! na kumbe amani haipo.
\v 15 Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hasha, hawakuona aibu! Hawakuwa na aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoj na wale watakaoanguka wakati nitakpowaadhibu. Wataangushwa chini," asema BWANA.
\s5
\v 16 BWANA asema hivi, `Simama kwenye njia panda utazame; uliza nzile njia za zamani, 'Je, hii tabia njema iko wapi?' Kisha endelea nayo na tafuta mahali pa kupumzika. Lakini watu wanasema, 'Hatutaenda.'
\v 17 Niliweka walinzi juu yenu ili wasikilize tarumbeta. Lakini walisema, 'Hatutasikiliza.'
\v 18 Kwa hiyo, sikilizeni, enyi mataifa! Tazameni, enyi mashahidi, muone kile kitakachowapata.
\v 19 Sikia, wewe dunia! Tazama, niko tayari kuleta janga kwa watu hawa - matunda ya fikra zao. Hawakusikiliza neno langu wala sheria zangu, badala yake walizikataa.
\s5
\v 20 Huu ubani kutoka sheba unaopanda una maana gani kwangu? Au huu uudi kutoka nchi ya mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki kwangu wala dhabihu zenu.
\v 21 Kwa hiyo BWANA asema hivi, 'Tazama, 'Niko tayari kuweka kikwazo dhidi ya watu hawa. Watajikwaa juu yake - baba na watoto wao kwa pamoja watajikwaa. Wakazi na jirani zao pia watapotea.'
\v 22 BWANA asema hivi, 'Tazama watu wanakuja toka nchi ya kaskazini. Kwa kuwa taifa kubwa limechochewa kutoka nchi ya mbali.
\s5
\v 23 Watachukua pinde na mishale yao. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama muungurumo wa bahari, na wapanda farasi katika mfumo wa wanaume wa vita, enyi binti wa Sayuni,"'
\v 24 Tumesikia habai zao. Mikono yetu inalegea kwa dhiki. Na maumivu yametukamata kama utungu wa mwanamke anayezaa.
\s5
\v 25 Usiende nje mashambani, na usitembee barabarani, kwa kuwa upanga wa adui na hofu vimekaribia.
\v 26 Binti za watu wangu, jivikeni magunia na kugaagaa kwenye majivu ya maombolezo ya mwana pekee. Ombolezeni kwa huzuni kuu, kwa kuwa anayewaangamiza anakuja kwetu ghafula juu yetu.
\s5
\v 27 "Nimekufanya wewe, Yeremia, kuwajaribu watu wangu kama mtu anayepima fedha, kwa hiyo utachunguza na kupima njia zao.
\v 28 Wao ni watu wasumbufu miongoni mwa watu, wanaoenda huko na kule wakisingizia wengine. Wote ni shaba na chuma, wakitenda kwa dhuluma.
\v 29 Mifuo inafukuta kwa moto unaoziunguza; risasi inaunguzwa na moto. Risasi tu ndiyo inayotoka kati yake, lakini haifai kitu kwa sababu uovu haujaondolewa.
\v 30 Wataitwa taka za fedha, kwa sababu BWANA amewakataa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Yermia,
\v 2 Simama katika lango la nyumba ya BWANA na utangaze ujumbe huu! Sikiilizeni neno la BWANA, ninyi nyote watu wa Yuda, ninyi mnaoingia katika malango haya kumwabudu BWANA.
\s5
\v 3 BWANA wsa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Tengenezeni njia zenu na kufanya mema, nami nitawaacha muishi hapa.
\v 4 Msitumainie maneno ya uongo mkisema, "Hekalu la BWANA!, Hekalu la BWANA! Hekalu la BWANA!"
\s5
\v 5 Bali kama mtazitengeneza njia zenu na kufanya mema, kama mtatoa hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake
\v 6 -kama hamtanyonya anayekaa katika nchi, yatima, mjane, na kama hamtamwaga damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa, na kama hataenda kwa miungu mingine kwa ajili ya maumivu yenu
\v 7 -ndipo nitakapowaacha mkae mahali hapa, katika nchi ambayo niliwapia mababu zenu toka zamani na hata milele.
\s5
\v 8 Tazama! Mnatumainia maneno ya uongo ambayo hayawasaidii.
\v 9 Je, mnaiba. mnaua, manafanya uzinzi? na mnaapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kwenda kwa miungu mingine ambao hamkuwajua?
\v 10 Je, mnakuja na kusimama mbele yangu katika nyumba hii ambapo jina langu linatangazwa na kusema, "Tumeokoka." hivyo mnaweza kufanya machukizo yote haya?
\v 11 Je, hii ndiyo nyumba inayobeba jina langu, pango la wanyang'anyi mbele ya macho yenu? Lakini tazama, Nimeiona - BWANA asema.'
\s5
\v 12 Kwa hiyo uende mahali pangu kule Shiloh, Kule ambako mwanzoni niliruhusu jina langu kukaa, na tazama kile nilichofanya pale kwa sababu ya maovu ya watu wangu Israeli.
\v 13 Kwa hiyo sasa, kwa sababu ya matendo yako haya yote - asema BWANA - Nilikuambia mara kadhaa, lakini hukusikiliza. Nilikuita, lakini hukuitika.
\v 14 Kwa hiyo kile nilichofanya Shilo, ndicho ambacho pia nitakachofanya kwa nyumba yangu hii inayoitwa kwa jina langu, nyumba amabyo ninyi mmeitumainia, mahali hapa ambapo niliwapa ninyi na mababu zenu.
\v 15 Kwa kuwa nitawafukuza mtoke kwangu kama vile nilivyowafukuza ndugu zenu wote, uzao wote wa Efraimu.'
\s5
\v 16 Na wewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa, na usiinue maombolezo ya kilio au kuomba sala kwa niaba yao, na usinishi, kwa kuwa sitakusikiliza.
\v 17 Kwani huoni kile wanachofanya katika miji ya Yuda na katika mitaa ya Yerusalemu?
\v 18 Watoto wanakusanya kuni na baba zao huwasha moto! Wanawake hukanda unga ili kuoka mikate kwa ajili ya malikia wa mbinguni na kumimina sadaka ya vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha mimi.
\s5
\v 19 Ni kweli wananikasirisha mimi? - asema BWANA - Je, si wao wanaojikasirisha, ili kwamba aibu iwe juu yao?
\v 20 Kwa hiyo BWANA, Mungu asema hivi, 'Tazama, hasira na ghahdabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, kwa watu wote na wanyama, juu ya miti katika mashamba na mazao ya ardhi, Itawaka nayo haitazimishwa.
\s5
\v 21 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Jiongezeeni sadaka za kuteketezwa katika dhabihu zenu na nyama zake.
\v 22 Kwani wakati nilipowatoa mababu zenu kutoka nchi ya Misri, Sikuhitaji chochote kutoka kwao. Sikuwapa amri juu ya maswala ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu.
\v 23 Niliwapa amri hii tu, "Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Kwa hiyo muishi katika njia ambazo ninawaamuru, ili mambo yenu yawe mazuri."
\s5
\v 24 Lakini hawkunisikiliza wala kuzingatia. Walishi kwa kufuata mipango yao ya uasi ya mioyo ya maovu, kwa hiyo walirudi nyuma badala ya kuendelea mbele.
\v 25 Tangu siku ambayo mababu zenu walitoka katika nchi ya Misri mpaka leo, Nimetuma watumishi wangu, manabii wangu, kwenu. Niliendelea kuwatuma.
\v 26 Lakini hawakuwasikiliza. Hawakuzingatia. Badala yake walishupaza shingo zao. Walikuwa waovu zaidi ya mababu zao.
\s5
\v 27 Kwa hiyo yatangaze maneno haya yote kwao, japo hawatakusikiliza. Yatangaze mambo haya kwao, lakini hawatakujibu.
\v 28 Waambie kuwa hili ni taifa ambalo haliisikilizi sauti ya BWANA, Mungu wake na lisilopokea mafundisho. Ukweli uneharibiwa na kukatwa kutoka kwenye vinywa vyao.
\s5
\v 29 Zikate nywele zako na kujinyoa, na kuzitupa. Imba wimbo wa maombolezo katika maeneo yaliyo wazi. Kwa kuwa BWANA amekikataa na kukitupa kizazi hiki cha hasira yake.
\v 30 Kwa kuwa wana wa Yuda wamefanya maovu mbele ya macho yangu - asema BWANA - wameweka machukizo yao katika nyumba ambayo jina langu hunenwa, ili kulinajisi.
\s5
\v 31 Kisha wamejenga mahali palipoinuka pa Tofethi ambapo pako kwenye bonde la Ben Hinomu. Walifanya hivi ili kuwachoma wana na binti zao kwenye moto - kitu ambacho mimi sikuamuru, wala kuweka jambo hilo katika akili zangu.
\v 32 Kwa hiyo, tazama siku zinakuja - asema BWANA - ambapo hapataitwa tena Tofethi au bonde la Ben Hinomu. Litakuwa bonde la machinjio; watazika maiti hapo Tofethi mpaka eneo lote lienee.
\s5
\v 33 Mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa duniani, na hakutakuwa na mtu wa kuwafukuza.
\v 34 Nitazikomesha katika miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalaemu sauti za kuiniuliwa na vicheko, Sauti ya bwana arusi na ya bibi arusi; kwa kuwa nchi hiyo itakuwa ukiwa."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati huo - BWANA asema - wataleta kutoka makaburini mifupa ya wafalme wa Yuda na wakuu wake, mifupa ya makuhani na ya manabii na mifupa ya wakazi wa Yerusalemu.
\v 2 Kisha wataitandaza nje mchana kweupe na mbalamwezi na nyota zote za angani; hivi vitu katika anga vimenifuata na kunitumikia, na kwamba vimetembea na kutafuta, na kwamba vimeniabudu. Mifupa haitakusanywa na kuzikwa tena. Itakuwa kama mavi juu ya uso wa dunia.
\v 3 Na katika kila eneo lililobaki ambalo nimewafukuza, Watachagua mauti badala ya uzima kwa ajili yao, wote ambao watasalia kutokana na taifa hili ovu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 4 Kwa hiyo uwaambie, 'BWANA asema hivi: Je, kuna mtu anyeanguka na hasimami? Je, kuna mtu anayepotea na hawezi kujaribu kurudi?
\v 5 Kwa nini hawa watu, Yerusalemu, wamegeukia uasi daima? Wanashikilia uongo na wanakataa kutubu.
\s5
\v 6 Nilikaa kwa uangalifu na nikasikiliza, lakini hawakuongea kilicho sahihi; hakuna aliyetubia uovu wake, hakuna asemaye, "Nimefanya nini?" Kila mmoja wao huenda kule anakotaka, kama farasi aendaye kasi vitani.
\v 7 Hata koikoi angani hujua wakati sahihi; na njiwa, na mbayuayu, n a korongo. Huhama kwa wakati sahihi, lakini watu wangu hawayajui maagizo ya BWANA.
\s5
\v 8 Kwa nini mnasema, "Sisi tuna hekima! na sheria ya BWANA tunayoi?" Hakika, Tazama! Kalamu yenye uongo ya mwandishi imefanya uongo.
\v 9 Wenye hekima wataaibishwa. Wameyeyuka na na kunaswa. Tazama! wanakataa neno la BWANA, kwa hiyo hekima yao ni kwa ajili ya matumizi gani?
\v 10 Kwa wake zao nitawapa wengine, na mashamba yao kwa wale watakaowamiliki, kwa kuwa kuanzia kijana hadi mkuu, kwa pamoja ni wachoyo! Kuanzia nabii hadi kuhani, wote wanasema uongo.
\s5
\v 11 Kwa kuwa wametibu jeraha ya binti za watu wangu kwa juu juu. Walijisemea, "Amani, Amani," na kumbe hapakuwa na amani.
\v 12 Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hawakuaibika. Hawakuwa na utu. Kwa hiyo wataanguka wakati wa adhabu, pamoja na wale walioanguka. Watatupwa chini, asema BWANA.
\v 13 Nitawaondoa kabisa - asema BWANA - hapatakuwa na zabibu kwenye mizabibu yao, wala tini katika mitini yao. kwa kuwa jani litanyauka, na kile nilichowapatia kitaisha.
\s5
\v 14 Kwa nini tunakaa hapa? Njoni pamoja; twendeni kwenye hiyo miji yenye maboma, na tutakaa kimya kule katika kifo. Kwa kuwa BWANA, Mungu wetu atatunyamazisha. Atatufanya tunywe sumu, kwa kuwa tumemtenda dhambi.
\v 15 Tunatumainia amani, lakini hakutakuwa na jema. Tunatumainia wakati wa uponyaji, lakini tazama kutakuwa na hofu.
\s5
\v 16 Mkoromo wa farasi wake umesikika kutoka Dani. Dunia nzima inatikisika kwa sababu ya sauti ya kukaribia kwa farasi wake wenye nguvu. Kwa kuwa watakuja kuiangamiza nchi na utajiri wake, mji na wote wakaao nadani yake.
\v 17 Hebu tazama, ninawatuma nyoka kati yenu, fira ambao hawawezi kuzuiliwa kwa uganga. Watawauma - asema BWANA,."
\s5
\v 18 Huzuni yangu haina ukomo, na moyo wangu unaugua.
\v 19 Tazama! sauti ya maumivu ya binti wa watu wangu kutoka mbali! Je, BWANA hayumo Sayuni? Je, mfalme wake hayumo ndani yake? Kwa nini sasa wananichukiza kwa vitu vya kuchongwa na sanamu za kigeni zilizo batili?
\s5
\v 20 Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha. Lakini sisi hatujaokoka.
\v 21 Nimeumia kwa sababu ya maumivu ya binti wa watu wangu. Ninaomboleza kwa sababu ya mambo ya kushangaza ambayo yametokea kwake; Nimeyeyuka.
\v 22 Je, kule Gileadi hakuan dawa? Je, huko hayuko mponyaji? Kwa nini uponyaji wa binti wa watu wangu hautokei?
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.
\v 2 Kama mtu anganipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
\v 3 asema BWANA, "Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwiingine. Hawanijui mimi."
\s5
\v 4 Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. kwa kuwa kila ndugu ni mwongo,
\v 5 kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanamume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhofisha ili kusema uongo.
\v 6 Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema BWANA."
\s5
\v 7 Kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, "Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
\v 8 Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubri.
\v 9 Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema BWANA na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
\s5
\v 10 Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anAyeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
\v 11 Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
\v 12 Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha BWANA kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.
\s5
\v 13 BWANA asema, "Ni kwa sababu wameziacha sheria zake ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuta.
\v 14 Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.
\s5
\v 15 Kwa hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.
\v 16 Ndipo nitakapowasambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.'"
\s5
\v 17 BWANA wa majeshi asema hivi, "Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
\v 18 Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
\s5
\v 19 Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, 'Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walIpoangusha nyumba zetu.'
\v 20 Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la BWANA; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
\s5
\v 21 Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
\v 22 Uyatangaze haya, 'Asema BWANA - mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.'"
\s5
\v 23 BWANA asema hivi, "Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
\v 24 Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busra na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni BWANA, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema BWANA.
\s5
\v 25 Tazama, siku zaja - asema BWANA wakati nitakapowaadhibu wote ambao hawajatahiriwa ambao wako hivyo hivyo katika miili yao.
\v 26 Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 "Sikilizeni neno ambalo BWANA anawaambieni, enyi nyumba ya Israeli.
\v 2 BWANA asema hivi, 'msijifunze njia za mataifa, na msishangazwe na ishara za mbinguni, kwa kuwa mataifa hushangazwa na haya.
\s5
\v 3 Kwa kuwa desturi za watu ni ubatili. Kwa kuwa mtu mmoja hukata mti msituni; kazi ya mikono ya mtu na shoka.
\v 4 Kisha huzipamba kwa fedha na dhahabu. Huikaza kwa misumari na nyundo ili isitikisike.
\v 5 Sanamu hizi ni mfano wa sanamu za kutishia ndege katika shamba la matango, kwa kuwa haziwezi kusema chochote. Hubebwa, kwa kuwa haziwezi hata kusogea hatua moja. Usiwaogope, Kwani hawawezi kutenda maovu wala mema."
\s5
\v 6 Hakuna aliye kama wewe, BWANA. Wewe ni mkuu, na jina lako lina nguvu.
\v 7 Ni nani asiyekuwa na hofu juu yako, wafalme wa mataifa? Kwa kuwa hiki ndicho unachostahili, kwa kuwa hakuna wa kuwa kama wewe kati ya wote wenye hekima katika mataifa yote au katika hali yao ya enzi.
\s5
\v 8 Wote wako sawa, ni kama wanyama na wapumbavu, wanafunzi wa samamu ambazo si chochote isipokuwa miti tu.
\v 9 Wanaleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi iliyotengenezwa na sonara, ni kazi ya ustadi. Mavazi yao ni ya rangi ya samawi na urujuani. Watu wao stadi waliyafanya haya yote.
\v 10 Lakini BWANA ni Mungu wa kweli. Yeye ni Mungu aliye hai na mfalme wa milele. Matetemeko yako katika hasira yake, na mataifa hayawezi kuvumilia hasira yake.
\s5
\v 11 Utawaambia hivi, "Miungu ambayo haikuumba mbingu na nchi itaangamia katika dunia hii na chini ya mbingu."
\v 12 Aliyeiumba dunia kwa nguvu zake aliumba nchi kavu kwa hekima zake na kuzitandaza mbingu kwa fahamu zake.
\v 13 Sauti yake ndiyo itengenezayo muungurumo wa maji mbinguni, naye huzileta mbingu katika mwisho wa dunia. Hutengeneza radi kwa ajili ya mvua na kutuma upepo kutoka katika hazina yake.
\s5
\v 14 Kila mtu amekuwa mjinga, hawana maarifa. Kila mfua chuma ameaibishwa kwa sanamu zake. Maana sanamu yake ya kuyeyushwa ni uongo; hakuna pumzi ndani yake.
\v 15 Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu; zitapotea wakati wa hukumu.
\v 16 Lakini Mungu ni fungu la Yakobo, si kama hawa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; BWANA wa majeshi ndiye jina lake.
\s5
\v 17 Kusanya vitu vyako na uiache nchi, wewe ambaye umekuwa ukiishi katika mazingiwa haya.
\v 18 Kwa kuwa BWANA asema hivi, "Tazama, Ni tayari kuwatupa wakazi wa nchi nje wakati huu. Nitawasababishia huzuni, na itakuwa hivyo."
\s5
\v 19 Ole wangu! Kwa sababu ya mifupa yangu iliyovunjika, Jeraha zangu zimeumia. Kwa hiyo nilisema. "Hakika haya ni maumivu, lakini lazima nivumilie."
\v 20 Hema yangu imeharibiwa, na kamba za hema yangu zote zimekatwa. Wamewachukua watoto wangu wote, Kwa hiyo hawaishi tena. Hakuna tena mtu wa kuitandaza hema yangu au wa kuziinua pazia za hema yangu.
\s5
\v 21 Kwa kuwa wachungaji wamekuwa wapumbavu. Hawamtafuti BWANA. Kwa hiyo hawana mafanikio; Kondoo wao wote wamesambaa.
\v 22 Taarifa imewadia, "Tazama! inakuja, tetemeko kubwa linakuja kutoka katika nchi ya kaskazini kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, na maficho ya mbweha.
\s5
\v 23 Ninajua, BWANA, kwamba njia ya mtu haiji kutoka kwake. Wala hakuna mtu atembeaye anayeongoza hatua zake mwenyewe.
\v 24 Ee BWANA, unirudi, kwa hukumu za haki, si kwa hasira zako vinginevyo utaniangamiza.
\v 25 Mwaga hasira zako kwa mataifa ambao hawakujui na katika familia ambazo hawakuiti kwa jina lako. Kwa kuwa wamemla Yakobo na kumwangamiza kabisa na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Hili ndilo neno lililojia Yeremia kutoka kwa Bwana, akasema,
\v 2 "Sikiliza maneno ya agano hili, uwaambie kila mtu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
\s5
\v 3 Uwaambie, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: na alaaniwe yeyote asiyesikiliza maneno ya agano hili.
\v 4 Hili ndilo agano nililowaamuru baba zenu walishike siku nilipowatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka tanuru ya chuma. Nikawaambia, "Sikilizeni sauti yangu na mfanye mambo yote kama nilivyowaamuru, kwa kuwa mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu."
\v 5 Nisikilizeni ili nipate kukitimiza kiapo nilichoapa kwa baba zenu, kiapo kwamba nitawapa nchi iliyojaa maziwa na asali kama ilivyo leo.'" Kisha mimi Yeremia nikajibu na kusema, "Ndio, Bwana!"
\s5
\v 6 Bwana akaniambia, "Hubiri habari hizi yote katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu. Sema, "Sikilizeni maneno ya agano hili na mkayafanye.
\v 7 Kwa maana nimewaagiza wazee wenu tangu siku ile niliyowaleta kutoka nchi ya Misri hadi wakati huu wa sasa, nimewaonya mara kwa mara na kusema, "Sikilizeni sauti yangu.'"
\v 8 Lakini hawakusikiliza au wala kutega masikio yao. Kila mtu amekuwa akitembea katika ukaidi wa moyo wake mbaya. Kwa hiyo nilileta laana zote katika agano hili nililoamuru kuja juu yao. Lakini watu bado hawakuitii."
\s5
\v 9 Kisha Bwana akaniambia, "Njama imeonekana kati ya watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
\v 10 Wameugeukia uovu wa mababu zao wa mwanzo, ambao walikataa kusikiliza neno langu, ambao badala yake walifuata miungu mingine ili kuabudu. Waisraeli na nyumba ya Yuda walivunja agano langu nililoweka na baba zao.
\s5
\v 11 Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Tazameni, nitawaletea majanga juu yao, majanga ambayo hawataweza kuyaepuka. Ndipo wataniita, lakini sitawasikiliza.
\v 12 Miji ya Yuda na wenyeji wa Yerusalemu watakwenda na kuiita miungu ambayo walitoa sadaka, lakini hakika hawatawaokoa wakati wa majanga yao.
\v 13 Kwa kuwa idadi ya miungu yako ewe Yuda imeongezeka sawa na idadi ya miji yako. Na umefanya idadi ya madhabahu ya aibu huko Yerusalemu, madhabahu ya kufukiza uvumba kwa Baali, sawa na idadi ya njia zake.
\s5
\v 14 Kwa hiyo wewe mwenyewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa. Lazima usiomboleze au kuomba kwa niaba yao. Kwa maana siwezi kusikiliza wakati wananiita katika majanga yao.
\v 15 Mpendwa wangu anafanya nini nyumbani kwangu, ikiwa amekuwa na nia mbaya? Nyama za sadaka yako hazitakusaidia. Unafurahi kwa sababu ya matendo yako mabaya.
\v 16 Katika siku za nyuma Bwana alikuita mti wa mzeituni wenye majani, mzuri wenye matunda mazuri. Lakini atawasha moto juu yake ambayo itaonekana kama sauti ya dhoruba; matawi yake yatavunjika.
\s5
\v 17 Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekua amekusudia maafa juu yako, kwa sababu ya matendo mabaya ambayo nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamefanya-wamenikasirisha kwa kumtolea Baali sadaka.'"
\s5
\v 18 Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nakayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao.
\v 19 Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, "Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena.
\v 20 Lakini Bwana wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.
\s5
\v 21 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya watu wa Anathothi, wanaotafuta uhai wako, "wanasema, 'Usifanye unabii kwa jina la Bwana, usije utakufa kwa mkono wetu.'
\v 22 Kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, nitawaadhibu. Vijana wao wenye nguvu watakufa kwa upanga. Wana wao na binti zao watakufa kwa njaa.
\v 23 Hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa maana nitaleta maafa dhidi ya watu wa Anathothi, mwaka wa adhabu yao.'"
\s5
\c 12
\p
\v 1 Wewe ni mwenye haki, Bwana, wakati wowote ninapoleta mashitaka kwako. Lazima nikuambie sababu yangu ya kulalamika: Kwa nini njia za waovu hufanikiwa? Watu wote wasiokuwa na imani wanafanikiwa.
\v 2 Wewe uliwapanda nao wakawa na mizizi. Wanaendelea kuzaa matunda. Wewe upo karibu nao katika vinywa vyao, lakini mbali na mioyo yao.
\s5
\v 3 Lakini wewe mwenyewe unanijua, Bwana. Umeona mimi na kuchunguza moyo wangu. Waondoe kama kondoo wa kuchinjwa. Ukakaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
\v 4 Je! Nchi itakauka kwa muda gani, na mimea katika kila shamba itaota kwa sababu ya uovu wa wenyeji wake? Wanyama na ndege wameondolewa. Hakika, watu wanasema, "Mungu hajui nini kitatokea kwetu."
\s5
\v 5 Bwana akasema, "Kweli, wewe, Yeremia, umetembea na askari wa miguu na wamechoka, unawezaje kushindana dhidi ya farasi? Ikiwa unashuka chini ya nchi iliyo salama, utafanyaje katika misitu karibu na Yordani?
\v 6 Kwa maana hata ndugu zako na familia ya baba yako wamekudharau na kukukemea kwa sauti kubwa. Usiwaamini, hata kama wanasema mambo mazuri kwako.
\s5
\v 7 Nimeiacha nyumba yangu; Nimeacha urithi wangu. Nimewatia watu wangu wapendwa mikononi mwa adui zake.
\v 8 Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba katika tundu; yeye hujiweka juu yangu kwa sauti yake mwenyewe, hivyo nimemchukia.
\v 9 Malipo yangu ya thamani ni fisi, na ndege wenye madoadoa karibu na kichwa chake. Nenda, ukakusanye viumbe vyote vilivyomo katika mashamba, na uwalete ili wale.
\s5
\v 10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu. Wameipoteza sehemu yangu yote ya ardhi; Waligeuza sehemu yangu nzuri kuwa jangwa, ukiwa.
\v 11 Wamemfanya kuwa ukiwa. Ninaomboleza kwa ajili yake; yeye ni ukiwa. Nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa maana hakuna mtu aliyeweka haya moyoni mwake.
\s5
\v 12 Waangamizi wamekuja juu ya maeneo yote yaliyo wazi jangwani, kwa maana upanga wa Bwana unakula kutoka upande mmoja wa nchi hadi mwingine. Hakuna usalama katika nchi kwa kiumbe chochote kilicho hai.
\v 13 Walipanda ngano lakini mavuno ya miiba. Wao wamechoka kutokana na kazi lakini hawajapata chochote. Basi muaibike kwa faida yenu kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana."
\s5
\v 14 Bwana asema hivi dhidi ya majirani zangu wote, waovu wanaopiga milki niliyowarithisha watu wangu Israeli, "Tazama, mimi ndimi ambaye nitawafukuza kutoka nchi yao wenyewe, nami nitaifuta nyumba ya Yuda kutoka kati yao.
\v 15 Ndipo baada ya kuangamiza mataifa hayo, itatokea kwamba nitakuwa na huruma juu yao na kuwaleta tena; Nitawarudi-kila mtu kwa urithi wake na nchi yake.
\s5
\v 16 Kisha itakuwa ikiwa mataifa hayo yatajifunza kwa makini njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu 'Kama Bwana anaishivyo!' vile vile kama walivyowafundishwa watu wangu kuapa kwa Baali, basi watajengwa katikati ya watu wangu.
\v 17 Lakini kama hakuna yeyote anayesikiliza, basi nitaling'oa taifa hilo. Kwa hakika litang'olewa na kuharibiwa-hili ndilo tamko la Bwana."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Bwana aliniambia hivi, "Nenda ukape nguo ya kitani na kuiweka karibu na kiuno chako, lakini usiiweke kwenye maji kwanza."
\v 2 Kwa hiyo nilinunua vazi kama vile Bwana alivyoagiza, na nikafunga karibu na kiuno changu.
\v 3 Ndipo neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema,
\v 4 "Twaa vazi lako ulilolinunua lililo karibu na kiuno chako, uinuke, ukasafiri mpaka Frati. Ukaifiche huko katika mwamba wa jabali.
\s5
\v 5 Basi nikaenda na kuificha katika Frati kama vile Bwana alivyoniamuru.
\v 6 Baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, "Simama, urudi Frati. Ukaichukue nguo ambayo nilikuambia ufiche."
\v 7 Kwa hiyo nikarudi Frati na kuchimba na kuchukua nguo mahali pale nilipoificha. Lakini tazama! Nguo hiyo ilikuwa imeharibika; haikuwa nzuri kabisa.
\s5
\v 8 Ndipo neno la Bwana likanijia tena, kusema,
\v 9 "Bwana asema hivi, Nitakiangamiza kiburi cha Yuda na Yerusalemu.
\v 10 Watu hawa waovu wanaokataa kusikia neno langu, ambao huenda katika ugumu wa mioyo yao, ambao hufuata miungu mingine ili kuabudu na kuinama-watakuwa kama hii nguo isiyofaa kwa lolote.
\v 11 Kwa maana kama vile vazi lililofungwa kwenye viuno vya mtu, ndivyo nimefainya nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda zimefungwa kwangu- hili ndilo tamko la Bwana-wawe watu wangu, ili kunifanya jina, sifa, na heshima. Lakini hawakunisikiliza.
\s5
\v 12 Basi uwaambie neno hili, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi Kila chupa itajazwa divai.' Watakuambia, 'Je, hatujui kwamba kila chupa itajazwa divai?'
\v 13 Basi uwaambie,' Bwana asema hivi: Tazama, nitawajaza kila mkaaji wa nchi hii ulevi, na wafalme wanaokaa kiti cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.
\v 14 Ndipo nitawagonganisha kila mtu na mwenzake baba na watoto wao pamoja; hili ndilo tamko la Bwana-sitawahurumia au kuwa na huruma, wala sitawarehemu kutoka kwenye uharibifu.
\s5
\v 15 Sikilizeni na makini. Msiwe na kiburi, kwa kuwa Bwana amesema.
\v 16 Mtukuze Bwana, Mungu wako, kabla ya hajaleta giza, na kabla ya kuifanya miguu yako kuwa na mashaka juu ya milima wakati wa jioni. Kwa maana unatarajia mwanga, lakini ataugeuza kuwa mahali pa giza, na kuwa giza nene.
\v 17 Kwa hiyo ikiwa husikilizi, nitaomboleza peke yangu kwa sababu ya kiburi chako. Hakika macho yangu yatalia na kutoa machozi, kwa sababu kundi la Bwana limechukuliwa mateka.
\s5
\v 18 "Mwambieni mfalme na mama wa malkia, 'Jinyenyekezeni, na kukaa chini, kwa maana taji juu ya kichwa chako, kiburi chako na utukufu wako, umeanguka.'
\v 19 Miji ya Negebu itafungwa, bila mtu wa kufungua. Yuda watachukuliwa mateka, wote uhamishoni.
\s5
\v 20 Inua macho yako na angalia wale wanaokuja kutoka kaskazini. Je, ni kundi gani alilokupa, kundi ambalo lilikuwa zuri sana kwako?
\v 21 Je, unasema nini wakati Mungu anawaweka wale ambao uliwafundisha kuwa marafiki? Je, huu si mwanzo wa maumivu ya utungu ambayo yatakuchukua kama mwanamke aliye katika kuzaa?
\s5
\v 22 Kisha unaweza kusema moyoni mwako, 'Kwa nini mambo haya yanatokea kwangu?' Itakuwa kwa uovu wa maovu yako ambapo marinda yako yamefunuliwa na umeumizwa.
\v 23 Je, watu wa Kushi hubadilisha rangi yao ya ngozi, au chui hubadilisha madoa yake? Ikiwa ndivyo, basi wewe mwenyewe, ingawa unazoea uovu, utaweza kufanya mema.
\v 24 Kwa hiyo nitawaangamiza kama makapi ambayo yanaangamia katika upepo wa jangwa.
\s5
\v 25 Hii ndiyo niliyokupa, sehemu ambayo nimekuagiza kwako-hili ndilo tamko la Bwana - kwa sababu umenisahau na kuamini katika udanganyifu.
\v 26 Kwa hiyo mimi mwenyewe nitaondoa nguo zako, na sehemu zako za siri zitaonekana.
\v 27 Uzinzi na ubembe wako, aibu ya tabia yako ya uasherati kwenye milima na katika mashamba! Nitayafanya yaonekane, mambo haya ya machukizo! Ole wako, Yerusalemu! Hutaki kuwa safi. Je! Hili litaendelea kwa muda gani?"
\s5
\c 14
\p
\v 1 Neno la Bwana lilimjia Yeremia kuhusu ukame,
\v 2 "Wayahudi waomboleze; basi milango yake ianguke. Wao wanaomboleza kwa ajili ya ardhi; Kilio chao kwa Yerusalemu kimepaa juu.
\v 3 Wenye nguvu huwatuma watumishi wao kwa ajili ya maji. Wanapoingia kwenye visima, hawawezi kupata maji. Wote wanarudi hawajafanikiwa; Wao hufunika vichwa vyao na aibu.
\s5
\v 4 Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
\v 5 Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
\v 6 Punda mwitu husimama kwenye mabonde yaliyo wazi na hupiga upepo kama mbweha. Macho yao yanashindwa kufanya kazi, kwa maana hakuna mimea.
\s5
\v 7 Hata ingawa maovu yetu yanatushuhudia, Bwana, tenda kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu matendo yetu yasiyo na imani yamezidi; tumekutenda dhambi.
\v 8 Matumaini ya Israeli, yule anayemwokoa wakati wa dhiki, kwa nini utakuwa kama mgeni katika nchi, kama mtu akaaye nchi ya kigeni ambaye hujinyoosha na kutumia hutumia usiku mmoja tu?
\v 9 Kwa nini utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kama shujaa ambaye hawezi kuokoa mtu yeyote? Kwa maana wewe u katikati yetu, Bwana! Jina lako limetangazwa juu yetu. Usiondoke
\s5
\v 10 Bwana awaambia hivi watu hawa "Kwa kuwa wanapenda kutanga tanga, hawakuzuia miguu yao kufanya hivyo." Bwana hafurahi nao. Sasa anawakumbusha uovu wao na ameadhibu dhambi zao.
\v 11 Bwana akaniambia, Usiombe kwa ajili ya watu hawa.
\v 12 Maana ikiwa wanafunga, sitasikiliza kulia kwao; na wanapotoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga, sitawafurahia. Kwa maana nitawaangamiza kwa upanga, njaa, na tauni.
\s5
\v 13 Ndipo nikasema, "Ee Bwana, Bwana! Angalia! mabii wanawaambia watu, 'Huwezi kuona upanga; hakutakuwa na njaa kwako, kwa kuwa nitakupa usalama wa kweli mahali hapa.'"
\v 14 Bwana akaniambia, 'manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwafukuza, wala sikuwapa amri au kusema nao. Lakini maono ya udanganyifu na ya maana, uchawi wa udanganyifu unaotokana na akili zao ndicho wanachowahubiria."
\s5
\v 15 Kwa hiyo Bwana asema hivi, "Kwa habari ya manabii wakihubiri kwa jina langu, ambao mimi siwakutuma; wale wanaosema kuwa hakutakuwa na upanga wala njaa katika nchi hii mabii hawa wataangamia kwa upanga na njaa.
\v 16 Na watu waliopewa utabiri watafukuzwa nje ya barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga; kwa kuwa hakuna mtu wa kuwazikas-wao, na wake zao, na wana wao, wala binti zao; kwa maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
\s5
\v 17 Sema neno hili kwao 'Acha macho yangu yatokwe machozi, usiku na mchana. wala yasikome, kwa kuwa kutakuwa na kuanguka kwa bikira, binti ya watu wangu - jeraha kubwa lisilotibika.
\v 18 Ikiwa nitatoka kwenye shamba basi angalia! kuna wale waliouawa kwa upanga. Na kama nitakuja mjini, basi, tazama! kuna wale walio na ugonjwa wa njaa. Hata nabii na kuhani wote wanatembea juu ya nchi bila maarifa.'"
\s5
\v 19 Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu.
\v 20 Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.
\s5
\v 21 Usitukatae! Kwa ajili ya jina lako, usikifedheheshe kiti chako cha enzi cha utukufu. Kumbuka na usivunje agano lako na sisi.
\v 22 Je, kuna miongoni mwa sanamu za mataifa yeyote zinazoweza kuifanya mbingu kutoa mvua? Je, si wewe, Bwana Mungu wetu, ambaye hufanya jambo hili? Tunatumaini kwako, kwa kuwa umefanya mambo haya yote.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Kisha Bwana akaniambia, "Hata kama Musa au Samweli walisimama mbele yangu, bado sitawafikiria watu hawa. Watoe mbele yangu, ili waweze kuondoka.
\v 2 Ikiwa watakuambia, 'Tunapaswa kwenda wapi?' Kisha uwaambie, 'Bwana asema hivi Wale wanaotakiwa kufa wanapaswa kufa; wale waliotayarishwa kwa upanga wanapaswa kwenda kwa upanga. Wale waliopelekwa kwa njaa wanapaswa kwenda kwa njaa; na wale waliopelekwa uhamisho wanapaswa kuhamishwa.'
\s5
\v 3 Kwa kuwa nitawapa kwa makundi manne-hili ndilo tamko la Bwana-upanga wa kuua wengine, mbwa wararue, ndege wa angani na mnyama mkali wale na kuangamiza.
\v 4 Nitawafanyia jambo lenye kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu Manase mwana wa Hezekia, mfalme wa Yuda, alifanya huko Yerusalemu.
\s5
\v 5 Kwa maana ni nani atakayewahurumia, Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Nani atakayegeuka kuuliza kuhusu ustawi wako?
\v 6 Umeniacha-hili ndilo tamko la Bwana-umerudi nyuma. Kwa hiyo nitawapiga kwa mkono wangu na kukuangamiza. Nimechoka kuwahurumia.
\v 7 Kwa hiyo nitawapepea kwa kipepeo katika milango ya nchi. Nitawafukuza. Nitawaangamiza watu wangu kwani hawakurudi na kuziacha njia zao.
\s5
\v 8 Nitawafanya wajane wao kuwa zaidi ya mchanga wa bahari. Dhidi ya mama wa vijana nitamtuma mwangamizi mchana. Nitafanya mshtuko na hofu ghafla kuanguka juu yao.
\v 9 Mama aliyezaa watoto saba ataharibika. Atashuka. Jua lake limekuchwa wakati bado ni siku. Yeye atakuwa na aibu na kufedheheka, kwa kuwa nitawatoa wale waliosalia kwa upanga mbele ya maadui zao-hili ndilo tamko la Bwana."
\s5
\v 10 Ole wangu, mama yangu! Kwa maana umenizaa, mimi ambaye ni mtu wa kushindana na hoja katika nchi yote. Sijakopesha, wala hakuna mtu aliyenikopesha, lakini wote wananilaani.
\v 11 Bwana akasema "Je sitakuokoa kwa manufaa? Kwa hakika nitawafanya maadui wako waombe msaada wakati wa msiba na dhiki.
\v 12 Je, mtu anaweza kusaga chuma? Hasa chuma kutoka kaskazini iliyochanganywa na shaba?
\s5
\v 13 Nitawapa adui zako utajiri wako na hazina yako kama nyara za bure. Nitafanya hili kwa sababu ya dhambi zako zote zilizofanywa ndani ya mipaka yako yote.
\v 14 Ndipo nitakufanya utumikie adui zako katika nchi ambayo huijui, maana moto utawaka, ukawaka katika ghadhabu yangu juu yako."
\s5
\v 15 Wewe mwenyewe wajua, Bwana! Unikumbuke na kunisaidia. Ukanilipie kisasi kwa ajili ya wanaonifuata. Katika uvumilivu wako usiniondoe. Utambue kwamba nimekuwa na aibu kwa ajili yako. Maneno yako yamepatikana, na nikayala.
\v 16 Maneno yako yalikuwa furaha kwangu, furaha yangu kwa moyo wangu; kwa maana jina lako linatangazwa juu yangu, Bwana, Mungu wa majeshi.
\s5
\v 17 Sikuketi katika mkutano wa wale waliosherehekea au waliofurahi. Nimeketi kwa faragha kwa sababu ya mkono wako wenye nguvu, kwa maana umenijaza na hasira.
\v 18 Kwa nini maumivu yangu yanaendelea na jeraha langu halitibiki, linakataa kuponywa? Je, utakuwa kama maji ya udanganyifu kwangu, maji yanayokauka?
\s5
\v 19 Kwa hiyo Bwana asema hivi, "Yeremia, Ikiwa utatubu, nitakurejesha, nawe utasimama mbele yangu na kunitumikia. Kwa maana ukitenganisha mambo ya kipumbavu kwa vitu vya thamani, utakuwa kama kinywa changu. Watu watakuja kwako, lakini wewe mwenyewe usirudi kwao.
\v 20 Nitakufanya kama ukuta wa shaba usioweza kuingilika kwa watu hawa, nao watapigana vita dhidi yako. Lakini hawatakushinda, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe ili kuokoa na kukuponya-hili ndilo tamko la Bwana-
\v 21 kwa maana nitakuokoa mikononi mwa waovu na kukukomboa katika mkono wa mshindani."
\s5
\c 16
\p
\v 1 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 2 "Usiwe na mke, wala usiwe na wana au binti hapa.
\v 3 Kwa kuwa Bwana asema hivi kwa wana na binti ambao wamezaliwa hapa, kwa mama waliowabeba, na kwa baba waliowafanya wazaliwe katika nchi hii,
\v 4 'Watakufa vifo vya magonjwa. Hawataliliwa wala kuzikwa. Watakuwa kama samadi juu ya nchi. Kwa maana wataangamizwa kwa upanga na njaa, na miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.'
\s5
\v 5 Maana Bwana asema hivi, 'Usiingie nyumba yoyote yenye kuomboleza. Usiende kuwaombolezea, wala usihuzunike kwa ajili ya watu hawa. Kwa maana nimeondoa amani yangu, uaminifu wa agano, na huruma, kutoka kwa watu hawa! Ndivyo asemavyo Bwana;
\v 6 kwa hiyo wakuu na wadogo watakufa katika nchi hii. Wala hawatazikwa, wala hakuna yeyote atakayeomboleza kwa ajili yao. Hakuna mtu atakayejikata-kata au kunyoa vichwa vyao kwa ajili yao.
\s5
\v 7 Hakuna mtu anayepaswa kugawa chakula chochote wakati wa kuomboleza ili kuwafariji kwa sababu ya vifo, na hawatawapa kikombe cha faraja kwa baba yake au mama yake ili kuwafariji.
\v 8 Usiende kwenye nyumba ya karamu ili ukae pamoja nao ili kula au kunywa.
\v 9 Kwa maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, mbele yako, siku zako na mahali hapa, nitakomesha sauti ya furaha na sherehe, sauti ya bwana na bibi arusi. '
\s5
\v 10 Kisha itatokea kwamba utawaambia watu hawa maneno haya yote, na watakuambia, 'Mbona Bwana amesema maafa yote haya juu yetu? Uovu wetu ni uovu gani na dhambi yetu tuliyomtendea Bwana, Mungu wetu?'
\v 11 Basi uwaambie, 'hii ndiyo ahadi ya Bwana; Kwa sababu baba zenu waliniacha, nao wakafuata miungu mingine, wakaiabudu na kuisujudia. Waliniacha na hawakuishika sheria yangu.
\s5
\v 12 Lakini ninyi wenyewe mmeleta uovu zaidi kuliko baba zenu, kwa maana, kila mtu anaenda kwa ukaidi wa moyo wake mbaya; hakuna mtu anayenisikiliza.
\v 13 Kwa hiyo nitawafukuza kutoka nchi hii mpaka nchi msiyoijua, wewe wala baba zako, nanyi mtaiabudu miungu mingine huko mchana na usiku, kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu.'
\s5
\v 14 Kwa hiyo tazama! Siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo hawatasema tena, 'Kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.'
\v 15 Kwa maana, kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi aliyowaangamiza, nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
\s5
\v 16 Angalia! hili ni tamko la Bwana-Nitatuma wavuvi wengi-kwa hiyo watawavua watu. Baada ya hayo nitatuma wawindaji wengi ili waweze kuwinda kati ya milima na vilima vyote, na katika miamba ya mwamba.
\v 17 Kwa kuwa macho yangu yapo juu ya njia zao zote; hawawezi kujificha mbele yangu. Uovu wao hauwezi kufichika mbele ya macho yangu.
\v 18 Nami kwanza nitawalipa mara mbili uovu na dhambi zao kwa kuwa wameichafua nchi yangu sanamu za machukizo, na kwa kujaza urithi wangu na sanamu zao za machukizo.
\s5
\v 19 Ee Bwana, wewe ndiwe ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama wangu siku ya shida. Mataifa yatakujia kwako kutoka mwisho wa dunia na kusema, 'Hakika baba zetu walirithi udanganyifu. Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao. Je!
\v 20 Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe? Lakini wao sio miungu.
\v 21 Kwa hiyo tazama! Nitawafanya wajue wakati huu, nitawafanya watambue mkono wangu na nguvu zangu, kwa hiyo watajua kwamba Yahweh ni jina langu."
\s5
\c 17
\p
\v 1 "Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi. Imechongwa kwenye kibao cha mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zako.
\v 2 Watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na miti yao ya Ashera kwa miti ya majani kwenye milima mirefu.
\s5
\v 3 Mlima wangu katika nchi ya wazi na mali yako yote pamoja na hazina zako zote, nitakupa kama nyara kwa wengine. Hiyo ndiyo thamani ya maeneo yako ya juu na dhambi iliyo katika maeneo yako yote.
\v 4 Utapoteza urithi niliokupa. Nitakutumikisha kwa adui zako katika nchi ambayo hujui, kwa maana umewasha moto katika ghadhabu yangu, ambao utakawaka milele."
\s5
\v 5 Bwana asema, "Mtu anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa; amfanyaye mwanadamu kuwa nguvu yake na kugeuza moyo wake mbali na Bwana.
\v 6 Kwa maana atakuwa kama msitu mdogo katika Araba na hawezi kuona kitu kizuri kikija. Atakaa katika maeneo ya mawe jangwani, nchi isiyokuwa na wakazi.
\s5
\v 7 Lakini mtu anayemtegemea Bwana amebarikiwa, kwa kuwa Bwana ndiye tumaini lake.
\v 8 Kwa maana atakuwa kama mmea karibu na maji kando ya mto; mizizi yake itaenea. Hawezi kuona joto likija, kwa kuwa majani yake yatakuwa mabichi. Kisha mwaka wa ukame hawezi kuwa na wasiwasi, wala hataacha kuzalisha matunda.
\s5
\v 9 Moyo ni mdanganyifu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Una mgonjwa; ni nani anayeweza kuelewa?
\v 10 Mimi ni Bwana, ninayechunguza akili, ambaye hujaribu viuno. Ninampa kila mtu kulingana na njia zake, kulingana na matunda ya matendo yake.
\v 11 kama Kware akusanyaye mayai asiyotaga. Mtu anaweza kuwa tajiri kwa udhalimu, lakini wakati nusu ya siku zake ukipita, utajiri huo utamuacha, na mwishowe atakuwa mpumbavu."
\s5
\v 12 "Mahali pa hekalu letu ni kiti cha enzi cha utukufu, kilichoinuliwa tangu mwanzo.
\v 13 Bwana ni tumaini la Israeli. Wote ambao wanakuacha watakuwa na aibu. Wale walio katika nchi ambao wanageuka kutoka kwako watauliwa. Kwa maana wamwacha Bwana, chemchemi ya maji yaliyo hai.
\v 14 Niponye, Bwana, na mimi nitaponywa! Niokoe mimi, nami nitaokolewa. Kwa maana wewe ndio wimbo wangu wa sifa.
\s5
\v 15 Tazama, wananiambia, 'Neno la Bwana liko wapi? Hebu lije!'
\v 16 Mimi sikuwahi kuacha kuwa mchungaji nyuma yako. Sikuitamani siku ya maafa. Unajua yaliyotoka mdomoni mwangu. Yalifanyika mbele ya uwepo wako.
\s5
\v 17 Usiwe sababu ya hofu kwangu. Wewe ni kimbilio langu siku ya msiba.
\v 18 Waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi. Wataogopa, lakini usiache nifadhaike. Tuma siku ya maafa dhidi yao na kuwaangamiza maradufu."
\s5
\v 19 Bwana akaniambia hivi,: "Nenda ukasimame katika lango la watu ambako wafalme wa Yuda wanaingia na kutoka, basi katika malango mengine yote ya Yerusalemu.
\v 20 Uwaambie, 'Sikieni neno la Bwana, wafalme wa Yuda, na ninyi watu wote wa Yuda, na kila mtu wa Yerusalemu atakayeingia kwa njia ya malango haya.
\s5
\v 21 Bwana asema hivi: "Jihadharini kwa ajili ya maisha yenu na msichukue mzigo siku ya sabato ili muilete katika malango ya Yerusalemu.
\v 22 Wala msilete mzigo nje ya nyumba zenu siku ya sabato. Msifanye kazi yoyote, lakini muitenge siku ya Sabato, kama nilivyowaagiza wazee wako kufanya.'"
\v 23 Hawakusikiliza wala kutaega masikio yao, lakini walifanya shingo zao kuwa ngumu ili wasinisikilize wala kukubali maonyo.
\s5
\v 24 Itatokea kwamba ikiwa mtanisikiliza kweli-hili ndilo tamko la Bwana-na msilete mzigo kwenye malango ya jiji hili siku ya sabato lakini badala yake mkatenga siku ya sabato kwa Bwana na msifanye kazi yoyote juu yake -
\v 25 basi wafalme, wakuu, na wale wanaokaa kiti cha Daudi wataingia malango ya mji huu kwa magari na farasi, wao na viongozi wao, watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu. Na mji huu utakaa milele.
\s5
\v 26 Watakuja kutoka miji ya Yuda na kutoka pande zote za Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na visiwa vya chini, kutoka milimani na kutoka kaskazini, wakileta sadaka za kuteketezwa, dhabihu, sadaka za nafaka na ubani, sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana.
\v 27 Lakini ikiwa hamtasikiliza-kutakasa siku ya Sabato, kutochukua mizigo nzito, wala msiingie milango ya Yerusalemu siku ya sabato, nitawasha moto katika malango yake, nao utaangamiza majumba kuteketeza ngome za Yerusalemu, na hauwezi kuzimika.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Neno la Bwana lilimjia Yeremia, kusema,
\v 2 "Simama, uende kwa nyumba ya mfinyanzi; kwa maana nitakusikilizisha neno langu huko.
\v 3 Basi, nikaenda nyumbani kwa mfinyanzi, na tazama! Mfinyanzi alikuwa akifanya kazi kwenye gurudumu la mfinyanzi.
\v 4 Lakini chombo cha udongo ambacho alikuwa akikifinyanga kiliharibika mkononi mwake, kwa hiyo alibadili mawazo yake na akafanya kitu kingine ambacho kilionekana kuwa kizuri machoni pake.
\s5
\v 5 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 6 "Je, siwezi kuwa kama huyu mfinyanzi kwenu, nyumba ya Israeli? Angalia! Kama udongo katika mkono wa mfinyanzi-ndivyo ulivyo mkononi mwangu, nyumba ya Israeli.
\v 7 Kwa wakati mmoja, ninaweza kutangaza jambo fulani juu ya taifa au ufalme, kwamba nitaufukuza, kuuvunja, au kuuharibu.
\v 8 Lakini kama taifa ambalo nimefanya tamko hilo linageuka na kuacha maovu yake, basi nitaghairi nisitende maafa niliyokuwa nimepanga.
\s5
\v 9 Wakati mwingine, ninaweza kutangaza jambo fulani kuhusu taifa au ufalme, kwamba nitaujenga au kuupanda.
\v 10 Lakini ikiwa watafanya mabaya machoni pangu kwa kutosikiliza sauti yangu, basi nitaghairi mema ambayo nilikuwa nimewaambia nitawafanyia.
\s5
\v 11 Basi sasa, waambie watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, ukisema, 'Bwana asema hivi: Tazameni, nitawaangamiza. Mimi ni karibu kufinyanga mabaya dhidi yenu. Tubuni, kila mtu kutoka njia yake mbaya, hivyo njia zako na matendo yako yatakuletea mema.'
\v 12 Lakini watasema, 'Hili halina maana. Tutafanya kulingana na mipango yetu wenyewe. Kila mmoja wetu atafanya mabaya kwa kuufuata uchupavu wa moyo wake.'
\s5
\v 13 Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Uliza watu wa mataifa, ambao wamewahi kusikia habari kama hii? Bikira wa Israeli amefanya kitendo cha kutisha.
\v 14 Je, theluji ya Lebanoni imetoka milima yenye miamba juu ya pande zake? Je, mito ya mlima inayotoka mbali iliharibiwa, mito hiyo ya baridi?
\s5
\v 15 Hata hivyo watu wangu wamesahau. Wamefanya sadaka kwa sanamu zisizo na maana na wamefanya mashaka katika njia zao; wameacha njia za kale za kutembea katika njia ndogo.
\v 16 Nchi yao itakuwa ya hofu, kitu cha kuzomewa milele. Kila mtu atakayepita karibu naye atashuhudia na kutingisha kichwa chake.
\v 17 Nitawaangamiza mbele ya adui zao kama upepo wa mashariki. Nitawageuzia kisogo, wala sio uso wangu, siku ya msiba wao.'"
\s5
\v 18 Basi watu wakasema, "Njoni, tufanye njama dhidi ya Yeremia, maana sheria haitapotea kabisa kwa makuhani, wala ushauri kutoka kwa wenye hekima, au maneno ya manabii. Njoo, mshambulie kwa maneno yetu na tusisikilize tena chochote anachosema."
\v 19 Sikiliza, Ee Bwana! Na kusikiliza sauti ya adui yangu.
\v 20 Je, maafa kutoka kwao itakuwa malipo yangu kwa kuwa mema kwao? Kwa maana wamenichimbia shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele yako ili niseme mema kwa ajili yao na kugeuza ghadhabu yako isiwapate.
\s5
\v 21 Basi uwape watoto wao njaa, na uwatie mikononi mwa wale wanaotumia upanga. Basi, waache wanawake wao wafiwe na kuwa wajane, na watu wao watauawa, na vijana wao wauawe kwa upanga wa vita.
\v 22 Kelele ya kusikitisha isikiwe kutoka katika nyumba zao, kama utakapoleta washambuliaji ghafla juu yao. Kwa kuwa wamechimba shimo kunikamata na wameficha mitego katika miguu yangu.
\v 23 Lakini wewe, Bwana, unajua mipango yao yote dhidi yangu ya kuniua. Usisamehe uovu na dhambi zao. Usiondoe dhambi zao mbali nawe. Badala yake, waache waangamizwe mbele yako. Tenda juu yao wakati wa ghadhabu yako.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Bwana akasema hivi, "Nenda ukanunue chupa ya udongo wakati ukiwa na wazee wa watu na makuhani.
\v 2 Kisha uende mpaka bonde la Ben Hinomu wakati wa kuingia kwenye mlango uliovunjika wa mfinyanzi, na huko utangaza maneno nitakayokuambia.
\v 3 Ukisema, 'Sikilizeni neno la Bwana, wafalme wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu! Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Tazameni, na nitaletea msiba juu ya mahali hapa, na masikio ya kila mtu anayesikia yatawaka.
\s5
\v 4 Nitafanya hivyo kwa sababu wameniacha na kudharau mahali hapa. Katika mahali hapa wanatoa sadaka kwa miungu mingine ambayo hawakuijua. Wao, baba zao, na wafalme wa Yuda pia wamejaza mahali damu isiyo na hatia.
\v 5 Walimjengea Baali mahali pa juu na kuwachoma watoto wao kwa moto kama sadaka za kuteketezwa kwake-kitu ambacho sijawaamuru au kutaja, wala hakuingia ndani ya akili yangu.
\s5
\v 6 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, bonde la Ben Hinomu, kwa kuwa litakuwa bonde la machinjo.
\v 7 Katika mahali hapa nitatamgua mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya wapate kuuawa kwa upanga mbele ya adui zao na kwa mkono wa wale wanaotafuta maisha yao. Ndipo nitawapa miili yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.
\v 8 Ndipo nitaifanya mji huu kuwa uharibifu na kitu cha kuzomewa, kila mtu anayepita atashangaa na kuzomea kwa sababu mateso yake yote.
\v 9 Nitawafanya wale nyama ya wana wao na binti zao; kila mtu atakula mwili wa jirani yake katika dhiki na katika uchungu ambao umeletwa kwao na maadui zao na wale wanaotaka maisha yao.'"
\s5
\v 10 Kisha utavunja chupa ya udongo mbele ya watu ambao walikwenda pamoja nawe.
\v 11 Uwaambie,'Bwana wa majeshi asema hivi: nitafanya jambo hili kwa watu hawa na mji huu- hii ndiyo ahadi ya Bwana, kama vile Yeremia alivyovunja chupa ya udongo ili isiweze kutengenezwa tena. Watu watazika wafu huko Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
\s5
\v 12 Hivyo ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na wenyeji wake nitakapofanya jiji hili kama Tofethi, hili ndio tamko la Bwana;
\v 13 kwa hiyo nyumba za Yerusalemu na wafalme wa Yuda watakuwa kama Tofethi, nyumba zote zilizo juu ya watu waovu wanaoabudu nyota zote za mbinguni na kumwaga sadaka za kinywaji kwa miungu mingine.'"
\s5
\v 14 Ndipo Yeremia akatoka Tofethi, ambako Bwana amemtuma ahubiri. Akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote,
\v 15 "Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazameni, nitawaletea mji huu na miji yake yote maafa yote niliyonena dhidi yake, kwa kuwa walifanya shingo zao kuwa ngumu na kukataa kusikiliza maneno yangu.'"
\s5
\c 20
\p
\v 1 Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, alikuwa msimamizi mkuu, akamsikia Yeremia akihubiri maneno haya mbele ya nyumba ya Bwana.
\v 2 Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini ndani ya nyumba ya Bwana.
\s5
\v 3 Ikawa siku ya pili Pashuri akamtoa Yeremia nje ya makabati. Yeremia akamwambia, "Bwana hakukuita Pashuri, lakini wewe ni Magor-Misabibu.
\v 4 Kwa maana Bwana asema hivi, 'Tazama, nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wewe na wapendwa wako wote; kwa maana wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona. Nitawatia Yuda mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atawafanya kuwa mateka huko Babeli au kuwaangamiza kwa upanga.
\s5
\v 5 Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli.
\v 6 Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.'"
\s5
\v 7 "Umenidanganya, Bwana. Kwa hakika nimedanganyika. Wewe ulinikamata na kunishinda. Nimekuwa kitu cha kuchekesha. Watu wananidharau kila siku, siku zote.
\v 8 Kwa maana wakati wowote nimenena, nimeita na kutangaza, 'Vurugu na uharibifu.' Na neno la Bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwangu kila siku.
\v 9 Nami nikisema, 'Sitafikiria juu ya Bwana tena. Sitatangaza tena jina lake.' Ni kama moto moyoni mwangu, uliofanyika ndani ya mifupa yangu. Kwa hiyo ninajitahidi kustahimili lakini siwezi.
\s5
\v 10 Nimesikia habari za ugaidi kutoka kwa watu wengi pande zote. 'Mshitaki! Lazima tumshitaki' Wale walio karibu nami kuangalia kama nitaanguka. 'Labda anaweza kudanganywa. Ikiwa ndivyo, tunaweza kumshinda na kujilipiza kisasi kwake.'
\v 11 Lakini Bwana yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu, hivyo wale wanaonifuata watajikwaa. Hawatanishinda. Watakuwa na aibu sana, kwa sababu hawatafanikiwa. Watakuwa na aibu ya kudumu, haitasahauliwa kamwe.
\s5
\v 12 Lakini wewe, Bwana wa majeshi, wewe unayemtazama wenye haki na ambaye huona akili na moyo. Hebu nipate kuona kisasi chako juu yao kwa maana nimekuletea shitaka langu kwako.
\v 13 Mwimbieni Bwana! Msifuni Bwana! Kwa kuwa ameokoa maisha ya wale waliokandamizwa kutoka kwenye mikono ya waovu.
\s5
\v 14 Na ilaaniwe siku niliyozaliwa. Usiruhusu siku ambayo mama yangu alinizaa ibarikiwe.
\v 15 Na alaaniwe mtu aliyemwambia baba yangu akisema, 'Amezaliwa mtoto wa kiume,' na kusababisha furaha kubwa.
\s5
\v 16 Mtu huyo atakuwa kama miji ambayo Bwana aliiangamiza bila huruma. Na asikie wito wa msaada asubuhi na sauti ya vita wakati wa mchana.
\v 17 Hiyo itatokea, kwa kuwa Bwana hakuniua tumboni au kumfanya mama yangu kaburi langu, tumbo la ujauzito milele.
\v 18 Kwa nini nilitoka tumboni ili kuona matatizo na uchungu, ili siku zangu zijazwe na aibu?"
\s5
\c 21
\p
\v 1 Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana kwa Yeremia wakati mfalme Sedekia alimtuma Pashuri mwana wa Malkiya na Sefania mwana wa Maaseya, kuhani. Wakamwambia,
\v 2 "Pata ushauri kutoka kwa Bwana kwa ajili yetu, kwa kuwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita. Labda Bwana atafanya miujiza kwetu, kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya aondoke kwetu."
\s5
\v 3 Basi Yeremia akawaambia, "Hivi ndivyo mtakavyomwambia Sedekia
\v 4 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, niageuza nyuma vyombo vya vita vilivyo mkononi mwenu, ambavyo mnapigana dhidi ya mfalme wa Babeli na Wakaldayo wanaokufunga kutoka nje ya kuta! Kwa maana nitawakusanya katikati ya jiji hili.
\v 5 Nami nitapigana nanyi kwa mkono ulioinuka na mkono wenye nguvu, na ukali, ghadhabu, na hasira kubwa.
\s5
\v 6 Kwa maana nitawaangamiza wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama, watakufa kwa tauni kali.
\v 7 Baada ya hayo- hii ndiyo ahadi ya Bwana-Sedekia mfalme wa Yuda, watumishi wake, watu, na kila mtu aishiye katika mji huu baada ya tauni, upanga na njaa, nitawatia wote mkononi mwa Nebukadreza mfalme wa Babeli, na mikononi mwa adui zao, na katika mkono wa wale wanaotaka uhai wao. Ndipo atawaua kwa makali ya upanga. Hatawahurumia, hatawaokoa, au kuwa na rehema.'
\s5
\v 8 Basi uwaambie watu hawa, 'Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti.
\v 9 Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake.
\v 10 Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.'
\s5
\v 11 Kuhusu nyumba ya mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Bwana.
\v 12 Nyumba ya Daudi, Bwana asema, "Hukumuni kwa haki asubuhi. Umuokoe yule aliyeibiwa kwa mkono wa mwenye kuonea, au ghadhabu yangu itatoka kama moto na kuchoma, na hakuna mtu anayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yako mabaya.
\s5
\v 13 Angalia, mwenyeji wa bonde na mwamba wa nchi ya wazi! Mimi niko juu yako, - hii ndiyo ahadi ya Bwana- Mimi ni juu ya mtu yeyote anayesema, 'Ni nani atashuka kutupiga?' au 'Ni nani atakayeingia kwenye nyumba zetu?'
\v 14 Nitawaadhibu kutokana na matunda ya matendo yako-hili ndilo tamko la Bwana- na nitawasha moto katika misitu, na utateketeza kila kitu.'"
\s5
\c 22
\p
\v 1 Bwana asema hivi, "Nenda kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda, utangaze neno hili huko.
\v 2 Ukaseme, 'Ewe Mfalme wa Yuda, wewe aliyeketi kiti cha Daudi, usikilize neno la Bwana. Nisikilizeni, enyi watumishi wake, na ninyi, watu wake mnaokuja kwa malango haya.
\v 3 Bwana asema hivi, "Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa.
\s5
\v 4 Kwa kuwa mkifanya mambo hayo, basi wafalme wanaoketi kiti cha Daudi wataingia milango ya nyumba hii wakiendesha gari na farasi, yeye, watumishi wake, na watu wake!
\v 5 Lakini ikiwa hamsikilizi maneno haya kutoka kwangu ambayo nimeyasema-hili ndilo tamko la Bwana-basi nyumba hii ya kifalme itaharibiwa.'"
\s5
\v 6 Kwa maana Bwana asema hivi juu ya nyumba ya mfalme wa Yuda, "Wewe uko kama Gileadi, au kama kilele cha Lebanoni kwangu. Hata hivyo nitakugeuza kuwa jangwa, katika miji isiyo na wenyeji.
\v 7 Kwa kuwa nimewaagiza waharibifu kuja juu yenu! Watu wenye silaha zao watakata mierezi yako iliyo bora na kuiacha kuanguka kwenye moto.
\s5
\v 8 Kisha mataifa mengi yatapita kwenye mji huu. Kila mtu atamwambia yule anayefuata, "Mbona Bwana amefanya hivi kwa jiji hili kuu?"
\v 9 Na mwingine atajibu, "Kwa sababu waliiacha agano la Bwana, Mungu wao, wakainama kwa miungu mingine, wakaiabudu."
\s5
\v 10 Usilie kwa ajili ya aliyekufa. Usiomboleze kwa ajili yake. Lakini mlilie mtu yeyote anayeingia kifungoni, kwa maana hatarudi tena kuiona nchi aliyozaliwa.'
\s5
\v 11 Maana Bwana asema hivi juu ya Yehoahazi, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyekuwa mfalme badala ya Yosia babaye, 'ametoka mahali hapa, wala hatarudi.
\v 12 Atakufa huko mahali ambapo walimchukua mateka, na hataiona tena nchi hii.'
\s5
\v 13 Ole mtu yeyote anayejenga nyumba yake kwa uovu na vyumba vyake vya juu katika udhalimu; ambao wengine hufanya kazi, lakini hawalipwi.
\v 14 Ole mtu yeyote atakayesema, 'Nitajenga nyumba ndefu na vyumba vya juu vipana, na hujenga madirisha mapana, na kuta zenye mwerezi, na huipaka rangi nyekundu.'
\s5
\v 15 Je, hii ndiyo inakufanya uwe mfalme mzuri, kwamba unataka kuwa na mbao za mwerezi? Je baba yako hakula na kunywa, lakini lakini alifanya hukumu na haki? Kisha mambo yakawa mazuri kwa ajili yake.
\v 16 Alihukumu maneno ya masikini na mhitaji. Ilikuwa vizuri. Je, huku siko kunijua mimi? - hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 17 Lakini hakuna kitu machoni na moyoni mwako isipokuwa wasiwasi kwa faida yako isiyo ya haki na kwa kumwaga damu isiyo na hatia, kwa ukandamizaji kuwatendea jeuri wengine.
\v 18 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Hawatamwomboleza wakisema 'ole, ndugu yangu! au 'Ole, dada yangu!' Hawataomboleza kwa kusema 'Ole, bwana! ' au 'ole, utukufu!'
\v 19 Atazikwa maziko ya punda, ataburuzwa mbali na kutupwa nje ya milango ya Yerusalemu.
\s5
\v 20 Panda milima ya Lebanoni piga kelele. Paza sauti yako Bashani. Piga kelele kutoka kwenye milima ya Abarimu, kwa maana marafiki zako wote wataharibiwa.
\v 21 Nilinena nawe wakati ulioko salama, lakini ukasema, 'Sitasikia.' Hii ilikuwa desturi yako tangu ujana wako, kwani hukusikiliza sauti yangu.
\s5
\v 22 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na marafiki zako watakwenda kufungwa. Hakika wewe utakuwa na aibu na kufadhaika kwa matendo yako yote mabaya.
\v 23 Wewe mfalme, wewe ambaye huishi katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni, wewe aliyefanya kiota kati ya mierezi, utakuwa na hali ya kuhurumiwa utakapopata utungu kama wakati wa kuzaa."
\s5
\v 24 "Kama mimi niishivyo-hili ndilo tamko la Bwana-hata kama wewe, Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ulikuwa alama ya mkono wangu wa kulia, ningekuangusha.
\v 25 Kwa kuwa nimewatia mikono ya wale wanaotaka uhai wenu na kwenye mkono wa wale ambao mnawaogopa, hata mkononi mwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Wakaldayo.
\v 26 Nitawatupa wewe na mama yako aliyekuzaa katika nchi nyingine, nchi ambayo hujazaliwa, na huko utakufa.
\s5
\v 27 Na kuhusu eneo hili ambalo watataka kurudi, hawatarudi hapa.
\v 28 Je! Hiki ni chombo kilichodharauliwa na kilichopasuka? Je, Konia ni chombo kilichodharauliwa? Kwa nini wamemtupa yeye na wazao wake, kumpeleka katika nchi wasiyoijua?
\s5
\v 29 Ee Ardhi, Ardhi, Ardhi! Sikieni neno la Bwana!
\v 30 Bwana asema hivi, 'Andika juu ya mtu huyu Konia Yeye hatakuwa na mtoto. Hatafanikiwa wakati wa siku zake, wala hakuna hata mmoja kati ya uzao wake atakayefanikiwa au kuketi tena kwenye kiti cha Daudi na kutawala juu ya Yuda.'"
\s5
\c 23
\p
\v 1 "Ole wao wachungaji ambao huangamiza na kuwatawanya kondoo wa malisho yangu-hii ndiyo ahadi ya Bwana."
\v 2 Kwa hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi juu ya wachungaji ambao wanawachunga watu wake, "Ninyi mnawatawanya kundi langu na kuwafukuza. Hamuwajali hata kidogo. Tambueni hili! Mimi nitawalipiza uovu wa matendo yenu-hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 3 Mimi mwenyewe nitakusanya mabaki ya kondoo wangu kutoka nchi zote nilizowafukuza, nami nitawarejesha kwenye eneo la malisho, ambako watazaa na kuongezeka.
\v 4 Ndipo nitawainua wachungaji juu yao ambao watawachunga hivyo hawataogopa tena au kupotezwa. Hakuna hata mmoja atakayepotea-hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 5 Angalia, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-nitakapomuinulia Daudi tawi la haki. Atatawala kama mfalme; atatenda kwa busara na kusababisha hukumu na haki katika nchi.
\v 6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli wataishi kwa usalama. Na jina lake atakayeitwa Bwana ni haki yetu.
\s5
\v 7 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-hawatasema tena, 'Kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.'
\v 8 Badala yake watasema, 'Kama Bwana aishivyo, ambaye aliwaleta na ambaye aliwaongoza wana wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote walizofukuzwa.' Nao watakaa katika nchi yao wenyewe."
\s5
\v 9 Kuhusu manabii, moyo wangu umevunjika ndani yangu, na mifupa yangu yote imetetemeka. Nimekuwa kama mlevi, kama mtu ambaye ameshindwa na divai, kwa sababu ya Bwana na maneno yake matakatifu.
\v 10 Kwa maana nchi imejaa wazinzi. Kwa sababu ya hayo nchi imeuka. Milima katika jangwa imekauka. Njia hizi za manabii ni mbaya; nguvu zao hazitumiwi kwa namna sahihi.
\s5
\v 11 Kwa maana manabii na makuhani wote wamekufuru. Nimeona uovu wao ndani ya nyumba yangu! - hili ndilo tamko la Bwana;
\v 12 kwa hiyo njia yao itakuwa kama mahali pa kupumzika katika giza. Watasukumwa chini. Wao wataanguka ndani yake. Kwa maana nitawatuma mabaya juu yao katika mwaka wa adhabu yao; hili ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 13 kwa maana nimeona uchungu kati ya manabii huko Samaria. Walitabiri kwa Baali na wakawaongoza watu wangu Israeli kwenye njia sahihi.
\v 14 Na miongoni mwa manabii huko Yerusalemu nimeona mambo ya kutisha: wanafanya uzinzi na huenda kwa udanganyifu. Wanaimarisha mikono ya waovu; hakuna mtu anarejea na kuacha uovu wake. Wote wamekuwa kama Sodoma kwangu na wenyeji wake kama Gomora!"
\v 15 Kwa hiyo, Bwana wa majeshi asema hivi juu ya manabii, "Tazameni, nitawafanya wale magugu na kunywa maji yenye sumu, kwa maana kufuru imetoka kwa manabii wa Yerusalemu na kuingia katika nchi yote."
\s5
\v 16 Bwana wa majeshi asema hivi, "Usisikilize maneno ya manabii wanaokuhubiri. Wamekudanganya! Wanatangaza maono kutoka kwenye mawazo yao wenyewe, si kwa kinywa cha Bwana.
\v 17 Wanasema daima kwa wale wanaonidharau mimi, 'Bwana asema kutakuwa na amani kwako.' Na kila mtu anayetembea katika ukaidi wa moyo wake anasema, 'mabaya hayatakuja kwenu.'
\v 18 Lakini nani amesimama katika mkutano wa baraza la Bwana? Ni nani anayeona na kusikia neno lake? Ni nani anayezingatia maneno yake na kusikiliza?
\s5
\v 19 Tazama, kuna dhoruba inayotoka kwa Bwana! Hasira yake inatoka, na dhoruba inazunguka. Inazunguka vichwa vya waovu.
\v 20 Hasira za Bwana hazitarejea mpaka zitakapotimiza nia ya moyo wake. Katika siku za mwisho, utaelewa.
\s5
\v 21 Sikuwatuma manabii hawa. Wao tu walionekana. Sikuwahubiri jambo lolote kwao, lakini bado wanatabiri.
\v 22 Kwa kuwa kama walisimama katika mkutano wangu wa baraza, wangeweza kuwasababisha watu wangu kusikia neno langu; wangewafanya wapate kuacha maneno yao mabaya na mazoea mabaya.
\s5
\v 23 Mimi ni Mungu aliye karibu-hili ni tamko la Bwana-mimi sio Mungu aliye mbali?
\v 24 Je, kuna mtu yeyote anayejificha mahali penye siri ili nisiweze kumwona? -Hili ndilo tamko la Bwana-Je mbingu na nchi hazikujawa nami? -hili Ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 25 Nimesikia yale waliyosema manabii, wale waliokuwa wanatabiri uongo kwa jina langu. Wakisema, 'Nilikuwa na ndoto!
\v 26 Nilikuwa na ndoto!' Je, hii itaendelea mpaka lini, manabii wanaotabiri uongo kutoka kwa akili zao, na wanasema nini kutokana na udanganyifu mioyoni mwao?
\v 27 Wana mpango wa kuwafanya watu wangu kusahau jina langu kwa ndoto ambazo wanazoripoti, kila mmoja kwa jirani yake, kama vile babu zao walivyosahau jina langu kwa ajili ya jina la Baali.
\s5
\v 28 Nabii aliye na ndoto, aseme ndoto hiyo. Lakini yule ambaye nimemwambia kitu fulani, basi aseme neno langu kwa kweli. Je, majani yanahusiana na nafaka? - hili ni tamko la Bwana-
\v 29 Na neno langu si kama moto? -Hili ni tamko la Bwana-na kama mwamba wenye kupiga nyundo?
\v 30 Tazameni, ninapingana na nabii-hii ndiyo ahadi ya Bwana-yeyote anayeiba maneno kutoka kwa mtu mwingine na anasema yanatoka kwangu.
\s5
\v 31 Tazama, ninapingana na manabii-hili ndilo tamko la Bwana-ambao hutumia lugha zao kutabiri maneno.
\v 32 Tazameni, ninapingana na manabii wanaoota ndoto-hii ndiyo ahadi ya Bwana-na kisha kuwahubiri na kwa njia hii kuwadanganya watu wangu kwa udanganyifu wao na kujivunia. Mimi ni juu yao, kwa kuwa sikuwatuma wala kuwapa amri. Kwa hivyo hawatawasaidia watu hawa - hili ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 33 Watu hawa au nabii au kuhani wakakuuliza, 'Je, ni nini tamko la Bwana?' basi lazima uwaambie, 'Ni tamko gani? Kwa maana nimekuacha wewe-hili ndilo tamko la Bwana.
\v 34 Kwa habari ya manabii, makuhani, na watu wanaosema, 'Hili ndilo tamko la Bwana,' nitamuadhibu mtu huyo na nyumba yake.
\s5
\v 35 Endelea kusema, kila mtu kwa jirani yake na kila mtu kwa ndugu yake, 'Bwana alijibu nini?' na 'Bwana alitangaza nini?'
\v 36 Lakini usizungumze tena juu ya tamko la Bwana, kwa kuwa kila tamko kutoka kwa kila mtu limekuwa ujumbe wake mwenyewe, na umepotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana wa majeshi, Mungu wetu.
\s5
\v 37 Utamuuliza nabii hivi, 'Bwana alikujibu nini? Je, Bwana alisema nini? Kisha unasema tamko kutoka kwa Bwana;
\v 38 lakini Bwana asema hivi, Sema hivi, "Hili ni tamko la Bwana" ingawa nimekuagiza na kusema, "Usiseme: Hili ni tamko kutoka kwa Bwana."
\v 39 Kwa hiyo, angalia, nitawachukua na kukutupa mbali na mimi, pamoja na jiji ambalo nilikupa wewe na baba zako.
\v 40 Ndipo nitaweka aibu ya milele na fedheha juu yenu ambayo haitasahauliwa.'"
\s5
\c 24
\p
\v 1 Bwana alinionyeshea kitu. Tazama, vikapu viwili vya tini viliwekwa mbele ya hekalu la Bwana. (Maono haya yalitokea baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, maofisa wa Yuda, mafundi na wafua vyuma kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.)
\v 2 Kikapu kimoja cha tini kilikuwa nzuri sana, kama tini za kwanza zilizoiva, lakini kikapu kingine cha tini zilizokuwa mbaya sana zisizoweza kuliwa.
\v 3 Bwana akaniambia, "Unaona nini Yeremia?" Nikasema, "Tini. Tini ambazo ni nzuri sana na tini ambazo ni mbaya sana haziwezi kuliwa."
\s5
\v 4 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 5 "Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: nitawaangalia mateka wa Yuda kwa manufaa yao, kama vile tini hizi nzuri, nilipowatoa mateka kutoka hapa mpaka nchi ya Wakaldayo.
\v 6 Nitaweka macho yangu kwao wapate mema na kuwarejeshea nchi hii. Nitawajenga, wala sitawaangamiza.
\v 7 Nitawapanda, wala sitawang'oa. Ndipo nitawapa moyo wa kunijua; kwa kuwa mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu na mimi nitakuwa Mungu wao, hivyo watanirudia kwa moyo wao yote.
\s5
\v 8 Lakini kama vile tini mbaya ambazo ni hazifai kuliwa - asema Bwana - nitatenda hivi kwa Sedekia, mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wake, na pamoja na wengine wa Yerusalemu ambao wanabaki katika nchi hii au kwenda kukaa katika nchi ya Misri.
\v 9 Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha, wapate maafa, mbele ya falme zote duniani, aibu na somo kwa mithali, matusi, na laana mahali pote nitakapowafukuza.
\v 10 Nitatuma upanga, njaa, na tauni dhidi yao watapotelea mbali kutoka kwenye nchi niliyowapa wao na baba zao."
\s5
\c 25
\p
\v 1 Hili ndilo neno ambalo lilimjia Yeremia juu ya watu wote wa Yuda. Ikawa mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Huo ndio mwaka wa kwanza wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
\v 2 Yeremia nabii aliwahubiria watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu.
\s5
\v 3 Akasema, "Kwa miaka ishirini na mitatu, tangu mwaka wa kumi na tatu wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda mpaka leo, maneno ya Bwana yamekuja kwangu. Nimewahubiria ninyi. Nilikuwa na nia ya kutangaza, lakini hamkunisikiliza.
\v 4 Bwana akawapeleka watumishi wake wote manabii kwako. Walikuwa na nia ya kwenda, lakini hukusikiliza wala kutega masikio.
\s5
\v 5 Manabaii hawa walisema, 'Kila mtu auache uovu wake na udhalimu wa matendo yake na kurudi kwenye nchi ambayo Yahwe aliitoa wakati wa zamanai kwa ajili ya babu zenu na ninyi, kama zawadi ya kudumu.
\v 6 Kwa hiyo msiifuate miungu mingine ili kuiabudu au kuiinamia chini, na msimkasirishe kwa kazi ya mikono yenu ili kwamba awaumize.
\s5
\v 7 Lakini hamkunisikiliza-hili ndilo tamko la Bwana-kwa hiyo umenikasirisha kwa kazi ya mikono yako ili kujidhuru nafsi zemu.
\v 8 Basi, Bwana wa majeshi asema hivi, 'Kwa kuwa hukusikiliza maneno yangu,
\v 9 tazama, nitaagiza amri ya kukusanya watu wote wa kaskazini- asema Bwana- na Nebukadreza, mtumishi wangu, mfalme wa Babeli, na kuwaleta juu ya nchi hii na wenyeji wake, na juu ya mataifa yote yaliyo karibu nawe. Kwa maana nitawaangamiza. Nitawageuza kuwa na hofu, kuwa kitu cha kuzomewa na ukiwa wa daima.
\s5
\v 10 Sauti ya furaha na sherehe-sauti ya bwana arusi na bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa-nitafanya mambo yote haya kutoweka kutoka kwa mataifa haya.
\v 11 Ndipo nchi hii yote itakuwa ukiwa na hofu, na mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.
\s5
\v 12 Kisha miaka sabini itakapokamilika, nitamuadhibu mfalme wa Babeli na taifa hilo, nchi ya Wakaldayo-hili ndilo tamko la Bwana-kwa uovu wao na kuifanya kuwa ukiwa milele.
\v 13 Nami nitaleta juu ya nchi hiyo maneno yote niliyosema, na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hiki ambacho Yeremia ametabiri juu ya mataifa yote.
\v 14 Kwa maana pia mataifa mengi na wafalme wakuu watapata watumwa kutoka mataifa haya. Nitawalipa kwa matendo yao na kazi za mikono yao.'"
\s5
\v 15 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Chukua kikombe hiki cha divai ya ghadhabu kutoka mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote niliyokutuma.
\v 16 Kwa maana watakunywa na kisha watalewa na kufanya wazimu mbele ya upanga ambao nitaupeleka kati yao."
\s5
\v 17 Basi, nikakichukua kikombe mkononi mwa Bwana, nikawanywesha mataifa yote ambayo Bwana alinituma:
\v 18 Yerusalemu, miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, na kuwafanya kuwa ukiwa na kitu cha kutisha, na kuwa kitu cha kuzomewa na laana, kama ilivyo hata leo..
\s5
\v 19 Mataifa mengine pia walipaswa kunywa: Farao mfalme wa Misri na watumishi wake; maafisa wake na watu wake wote;
\v 20 watu wote wa urithi wa mchanganyiko na wafalme wote wa nchi ya Uzi; na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;
\v 21 Edomu na Moabu na wana wa Amoni.
\s5
\v 22 Wafalme wa Tiro na Sidoni, wafalme wa pwani ng'ambo ya pili ya bahari,
\v 23 Dedani, Tema, na Busi pamoja na wale wanyoao nywele zao upande wa pili wa vichwa vyao, pia walipaswa kukinywa.
\s5
\v 24 Watu hawa pia walitakiwa kukinywa; wafalme wote wa Uarabuni na wafalme wote wa watu wa asili mchanganyiko wanaoishi nyikani;
\v 25 wafalme wote wa Zimri, wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi;
\v 26 wafalme wote wa kaskazini, wale wa karibu na wale wa mbali—kila mmoja na ndugu zake na falme zote za ulimwengu ambazo ziko chini ya uso wa dunia. Hatimaye mfalme wa Babeli atakunywa baada yao wote.
\s5
\v 27 Bwana akaniambia, "Basi, uwaambie, 'Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi kunywa na kulewa, kisha tapika, uanguke, wala usisimame mbele ya upanga nitakaoutuma kati yenu.'
\v 28 Kisha itatokea kwamba ikiwa wanakataa kuchukua kikombe mkononi mwako ili kunywa, utawaambia, 'Bwana wa majeshi asema hii lazima mnywe.
\v 29 Kwa maana, tazama, nitaleta janga juu ya mji ulioitwa kwa jina langu, je ninyi mtaachiliwa msiadhibiwe? Hutakuwa huru, kwa maana nitaita upanga juu ya wenyeji wote wa nchi! - ndilo tamko la Bwana wa majeshi.'
\s5
\v 30 Basi wewe mwenyewe, Yeremia, tabiri kwao maneno haya yote. Uwaambie, 'Bwana atanguruma kutoka juu, naye atapaza sauti yake toka makao yake matakatifu, na radi kutoka mahali pake patakatifu; naye atapiga kelele kama wale wakanyagao zabibu dhidi ya wote wanaoishi duniani.
\v 31 Kelele huja mpaka mwisho wa nchi, kwa sababu mgogoro kutoka kwa Bwana utaleta mashtaka dhidi ya mataifa. Ataleta haki kwa wote wenye mwili. Yeye atawatia waovu katika upanga-hili ndi'o tamko la Bwana.'
\s5
\v 32 Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, taabu itatokea toka kwa taifa hadi taifa, na dhoruba kubwa itatokea toka pande za mwisho za dunia.
\v 33 Kisha wale waliouawa na Bwana watakuja kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine; hawataomboleza, kukusanyika, au kuzikwa. Watakuwa kama samadi chini.
\s5
\v 34 Pigeni Yowe, wachungaji, na pigeni kelele ya kuomba msaada! Gaagaa katika ardhi, enyi mlio hodari katika kundi. Kwa kuwa siku yako ya kuuawa na kutawanywa imekuja. Utaanguka kama kondoo waliochaguliwa.
\v 35 Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia. Hakuna kutoroka kwa watu walio hodari katika kundi.
\v 36 Kuna mlio wa wasiwasi wa wachungaji na milio ya kulalama kwa watu walio hodari katika kundi, kwa kuwa Yahweh anayaharibu malisho yao.
\s5
\v 37 Kwa hiyo, malisho ya amani yataharibiwa kwa sababu ya hasira ya Bwana.
\v 38 Kama simba, ameacha shimo lake, kwa kuwa ardhi yao itakuwa kitu cha kushangaza kwa sababu ya hasira ya muonevu, kwa sababu ya ghadhabu yake kali'"
\s5
\c 26
\p
\v 1 Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, neno likaja kutoka kwa Yeremia, likisema,
\v 2 "Yahwe anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote!
\v 3 Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
\s5
\v 4 Kwa hiyo lazima useme kwao, 'Yahwe anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu—
\v 5 kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! —
\v 6 kisha nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote juu ya dunia.
\s5
\v 7 Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahwe.
\v 8 Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza aliyokuwa Yahwe alimwwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, "Hakika utakufa!
\v 9 Kwa nini umetabiri katika jina la Yahwe na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?" Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya nyumba ya Yeremia.
\s5
\v 10 Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe.
\v 11 Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, "Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!"
\v 12 Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, "Yeremia amenituma kutabiri juu ya nyumb hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.
\s5
\v 13 Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikilizeni sauti ya Yahwe Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu.
\v 14 Mimi mwenyewe—niangalieni! —niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu.
\v 15 Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahwe amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu."
\s5
\v 16 Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, "Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahwe Mungu wetu."
\v 17 Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu.
\s5
\v 18 Wakasema, "Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, 'Yahwe wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilichoota vichaka.' Hezekia mfalme wa Yuda na Yunda wote walimuua?
\v 19 Hakumwogopa Yahwe na kuutaka radhi uso wa Yahwe ili kwamba Yahwe angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?"
\s5
\v 20 Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahwe—Uria mwan wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia.
\v 21 Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri
\s5
\v 22 Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria.
\v 23 Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
\v 24 Lakini mkno wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikonono mwa watu ili auawe.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema "Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema "Sedekia", kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake).
\v 2 Hiki ndicho Yahwe alisema kwangu, "Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako.
\v 3 Kisha akawatuma kwenda kw mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
\v 4 Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ' Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo utakavyosema kwa mabwana zenu,
\s5
\v 5 Mimi mwenyewe niliiumba dunia kwa nguvu zangu kuu na mkono wangu ulioinuka. Pia niliwaumba watu na wanyama juu ya dunia, na nikawatoa kwa yeyote aliyesahihi katika macho yangu.
\v 6 Kwa hiyo sasa, Mimi mwenyewe naziweka nchi hizi zote kwenye mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu. Pia, ninavikabidhi kwake viumbe hai vyote katika mashamba ili vimtumikie.
\v 7 Kwa maana mataifa yote watamtumikia yeye, wanaye, na wajukuu zake hadi muda wa nchi yake ufike. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamtiisha.
\s5
\v 8 Kwa hiyo taifa na ufalme ambo haumtumikii Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na ule usioweka shingo yake chini ya nira ya Nebukadreza mfalme wa Babeli—nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa, na pigo—hili ni tangazo la Yahwe—hadi nitakapokuwa nimewateketeza kwa mkono wake.
\s5
\v 9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, wabashiri wenu, waonaji wenu, ndoto zenu, watambuzi wenu, ambao wamekuw wakisema kwenu na kusema, ' Msimtumikie mfalme wa Babeli.'
\v 10 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu ili kuwapeleka mbali na nchi zenu, kwa maana nitawapeleka mbali, na mtakufa.
\v 11 Lakini taifa ambalo wataweka shingo zao chini ya nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitawaruhusu kupumzika katika nchi yao—hili ni tangazo la Yahwe—na watailima na kufanya nyumba zao humo.""
\s5
\v 12 Kwa hiyo nilisema kwa Sedekia mfalme wa Yuda na kumpa ujumbe huu, "Ziwekeni shingo zenu chini ya nira ya mfalme wa Babeli na mtumikieni yeye na watu wake, na mtaishi.
\v 13 Kwa nini mfe—wewe na watu wako—kwa upanga, njaa, na pigo, kama vile nilivyotangaza kuhusu taifa ambalo watapuuza kumtumikia mfalme wa Babeli?
\s5
\v 14 Msisikilize maneno ya manabii wanaozungumza kwenu na kusema, 'Msimtumikie mfalme wa Babeli', kwa maana wanatabiri uongo kwenu.
\v 15 'Kwa maana mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana wanatabiri uongo katika jina langu ili kwamba niwafukeze inje na muangamie, ninyi nyote na manabii wanaotabiri kwenu."'
\s5
\v 16 Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, "Yahwe anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, 'Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahwe vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!' Wanatabiri uongo kwenu.
\v 17 Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe?
\v 18 Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamwombe Yahwe wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.
\s5
\v 19 Yahwe wa majeshi anasema hivi kuhusu zile nguzo, bahari, na kitako, na vyombo vyote vilivyosalia katika mji huu—
\v 20 vyombo ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika utumwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
\s5
\v 21 Yahwe wa majeshsi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu vyombo vilivyosalia katika nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu,
\v 22 'Vitaletwa Babeli, na vitabaki huko hadi siku niyovipangia kutimia—hili ni tangazo la Yahwe—kisha nitavileta na kuvirudisha kataika sehemu hii."
\s5
\c 28
\p
\v 1 Ilitokea katika mwaka ule, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne na mwezi wa tano, Hanania mwana wa Azuri nabii, alikuwa wa Gibeoni, alisema kwangu katika nyumba ya Yahwe mbele za makuhani na watu wote. Alisema,
\v 2 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeivunja nira iliyowekwa na mfalme wa Babeli.
\s5
\v 3 Ndani ya miaka miwili nitavirudisha katika sehemu hii vyombo vyote vya nyumba ya Yahwe ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli livichukua kutoka sehemu hii na kuvisafirisha hadi Babeli.
\v 4 Kisha nitawarudisha katika sehemu hii Yekonia mwana wa Yehotakimu, mfalme wa Yuda, na mateka wote wa Yuda ambao walipelekwa Babeli—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli."
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yeremia nabii akasema kwa Hanania nabii mbele ya makuhani na kwa watu wote waliosimama katika nyumba ya Yahwe.
\v 6 Yeremia nabii akasema, "Yahwe afanye hivi! Yahwe ayathibitishe maneno ambayao ulitabiri na kuvirudisha katika sehemsu hii vyombo vya nyumb a ya Yahwe, na mateka wote kutoka Babeli.
\v 7 Vile vile, sikilizeni neno ambaloo ninalitangaza katika masikio yenu na katika masikio ya watu wote.
\s5
\v 8 Manabii ambao walikuwepo mbele yangu na na mbele yenu muda mrefu uliopita pia walitabiri kuhusu mataifa mengi na juu ya falme kuu, kuhusu vita, njaa, na mapigo.
\v 9 Kwa hiyo nabii anayetabiri kwamba kutakuwa na amani—kama neno lake litatimia, basi itajulikana kwamba yeye ni nabii kweli aliyetumwa na Yahwe."
\s5
\v 10 Lakini Hanania nabii akaichukua nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia na kuivunja.
\v 11 Kisha Hanania akanena mbele ya watu wote na kusema, "Yahwe anasema hivi: Kama hivi tu, ndani ya miaka miwili nitaivunja nira iliyowekwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo ya kila taifa." Kisha Yeremia nabii akaenda njia yake.
\s5
\v 12 Baada ya Hanania nabii kuivunja nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia nabii, neno la Yahwe likamjia Yeremia. likisema,
\v 13 Nenda na ukaseme kwa Hanania na useme, Yahwe anasema hivi: Uliivunja nira ya mbao, lakini badala yake nitafanya nira ya chuma.'
\v 14 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma shingoni mwa mataifa haya yote ili wamtumikea Nebukadreza mfalme wa Babeli, na watamtumikia. Pia nimempa wanyama wa mashambani awatawale."
\s5
\v 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia Hanania nabii, "Sikiliza Hanania! Yahwe hajakutuma, bali wewe mwenyewe umewasababisha watu hawa kuamini katika uongo.
\v 16 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kukutuma nje ya dunia. Mwaka huu utakufa."
\v 17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, Hanania nabii akafa.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Haya ni maneno katika waraka ambao Yeremia nabii alituma kutoka Yerusalemu kwa wazee waliosalia miongoni mwa mateka na makuhuni, manabii, na watu wote ambao Nebukadreza aliwapeleka utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli.
\v 2 Hii ilikuwa baada ya Yekonia mfalme, mama yake mfalme, na watumishi wakuu, viongozi wa Yuda na Yerusalemu, na wahunzi walikuwa wamepelekwa mbali na Yerusalemu.
\v 3 Aliutuma waraka huu kwa mkono wa Elasa mwana wa Shafani, Gemaria, mwana wa Hilkia, ambaye Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemtuma kwa Nebukadreza mfalme wa Babeli
\s5
\v 4 Waraka ulisema, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kwa mateka ambao niliwasababisha kuwa mateka kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
\v 5 'Jengeni nyumba na muishi ndani yake. Pandeni bustani na mle matunda yake.
\s5
\v 6 Chukueni wake na mzae wana na mabinti. Kisha Kisha chukueni wake kwa ajili ya wana wenu, na wapatieni waume binti zenu. Wazae wana na mabinti na waongezeke ili msiwe wachache sana.
\v 7 Itafuteni amani ya mji ambako nimewafanya kuwa watumwa, na mkauombee kwangu kwa niaba yake kwa kuwa kutakuwa na amani kwenu kama mji uko katika amani.'
\s5
\v 8 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Msiwaache manabii ambao wako katikati yenu na wabashiri wenu kuwadanganya, na msizisikilize ndoto ambazo ninyi wenyewe mnaota.
\v 9 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu katika jina langu. Mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe.'
\s5
\v 10 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Babeli atakapokuwa amewatawala kwa muda wa mika sabini, nitawasaidia ninyi na kulitimiza neno langu jema kwa ajili yenu ili kuwarudisha ninyi katika sehemu hii.
\v 11 Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho.
\s5
\v 12 Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza.
\v 13 Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.
\v 14 Kisha nitapatikana kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawarudisha watu wenu waliofungwa; nitawakusanya kutoka mataifa yote na sehehemu zote ambako nimewatawanya—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawarudisha kutoka sehemu ambako niliwasababisha kuwa mateka.
\s5
\v 15 Tangu mliposema kwamba Yahwe ameinua manabii kwa ajili yetu katika Babeli,
\v 16 Yahwe anasema hivi kwa mfalme aliyeketi katika kiti cha enzi cha Daudi na watu wote wakaao katika mji huo, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi utumwani—
\v 17 Yahwe wa majeshi anasema hivi, ''Ona, niko karibu kutuma upanga, njaa, na ugonjwa juu yao. Kwa maana nitawafanya kuwa kama tini mbovu ambazo ni mbaya sana hazifai kuliwa.
\s5
\v 18 Kisha nitawafuata kwa upanga, njaa, na tauni na kuwafanya kuwa kitu cha kushangaza kwa falme zote juu ya dunia—kitu cha kuogofya, kitu cha kulaaniwa na kuzomewa, na kitu cha aibu miongoni mwa mataifa yote ambako nilimtawanya.
\v 19 Hii ni kwa sababu hawakulisikiliza neno langu—hili ni tangazo la Yahwe—ambalo nililituma kwao kupitia watumishi wangu manabii. Niliwatuma tena na tena, lakini hamkusikiliza—hili ni tangazo la Yahwe. '
\s5
\v 20 Kwa hiyo ninyi wenyewe sikilizeni neno la Yahwe, ninyi mateka wote ambao amewatuma kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
\v 21 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya na Sedekia mwana wa Maaseya, watabirio uongo kwenu katika jina langu: Ona, niko karibu kuwaweka katika mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli. Atawaua mbele ya macho yenu.
\s5
\v 22 Kisha laana itatamkwa na wafungwa wote wa Yuda katika Babeli kuhusu watu hawa. Laana itasema: Yahwe awafanye kuwa kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka kwenye moto.
\v 23 Hili litatokea kwa sababu ya mambo ya aibu waliyofanya katika Israeli walipofanya uzinzi na wake za majarani zao na kutangaza maneno ya uongo katika jina langu, mambo ambayo sikuwaamuru wayaseme. Kwa maana mimi ndiye nijuaye; mimi ni shahidi—hili ni tangazo la Yahwe."'
\s5
\v 24 Kuhusu Shemaya Mnehelami, sema hivi:
\v 25 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwa sababu ulituma barua kwa jina lako kwa watu wote katika Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa Maaseya kuhani, na kwa makuhani wote, na ulisema,
\v 26 "Yahwe aliwafanya ninyi kuwa makuhani badala ya Yehoyada kuhani, ili muwe wasimamizi wa nyumba ya Yahwe. Ninyi ni viongozi wa watu wote wajitiao wazimu na kujifanya wenyewe manabii. Mtawaweka katika mkatale na minyororo.
\s5
\v 27 Kwa hiyo sasa, kwa nini hamkumkemea Yeremia wa Anathothi, ambaye hujifanya mwenyewe nabii juu yenu?
\v 28 Kwa maana ametutumia sisi katika Babeli, 'Itakuwa muda mrefu. Jengeni nyumba na muishi ndani yake, na pandeni busitani na mule matunda yake.""
\v 29 Sefania kuhani akaisoma barua hii mbele ya Yeremia nabii.
\s5
\v 30 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 31 "tuma neno kwa mateka wote na sema, 'Yahwe anasema hivi kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi wakati mimi sikumtuma, na amewaongoza kuamini uongo,
\v 32 kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kumwadhibu Shemaya Mnehelami na uzao wake. Hapatakuwa na mtu wa kukaa miongoni mwa watu hawa kwa ajili yake. Hataona mema nitakayofanya kwa ajili ya watu wangu—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana ametangaza uasi dhidi ya Yahwe.""
\s5
\c 30
\p
\v 1 Neno lilokuja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe likisema,
\v 2 "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema, 'Jiandikie mwenyewe katika baraua maneno yote niliyotangaza kwako katika barua.
\v 3 Maana ona, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapowarudisha mateka wa watu wangu Israeli na Yuda. Mimi, Yahwe, nimesema hili. Kwa maana nitawarudisha kwenye nchi ambayo niliwapa babu zao, na wataimiliki."'
\s5
\v 4 Haya ni maneno ambayo Yahwe anatangaza kuhusu Israeli na Yuda,
\v 5 "Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Tumesikia sauti ya kutetemesha ya hofu na wala siyo ya amani.
\s5
\v 6 Ulizeni na muone kama mwanaume anamwogopa mtoto. Mbona ninamwona kila mwanaume kijana ameshika mikono yake juu ya kiuno chake kama mwanamke anayejifungua mtoto? Kwa nini nyuso zao wote zimegeuka rangi?
\v 7 Ole! Kwa maana siku hiyo itakuwa kuu, isiyofanana na yoyote. Utakuwa wakati wa huzuni kwa Yakobo, lakini ataokolewa.
\s5
\v 8 Kwa maana itakuwa katika siku hiyo—hili ni tangazo la Yahwe wa majeshi—kwamba nitaivunja nira ya shingo zenu, na nitaisambaza minyororo yenu, kwa hiyo wageni hawatawafanya watumwa tena.
\v 9 Bali watamwabudu Yahwe Mungu wao na kumtumikia Daudi mfalme wao, ambaye nitamfanya mfalme juu yao.
\s5
\v 10 Kwa hiyo wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope—hili ni tangazo la Yahwe—na usikate tamaa, Israeli. Maana ona, niko karibu kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa,. Yakobo atarudi na kuwa katika amani; ataokolewa, na hapatakuwa na hofu zaidi.
\v 11 Kwa maana niko pamoja nawe—hili ni tangazo la Yahwe—ili kukuokoa. Kisha nitaleta mwisho kamili kwa mataifa yote ambako nimewatawanya. Bali sitaweka mwisho kwako, ingawa ninakuadhibu kwa haki na kwa hakika sitakuacha bila kukuadhibu.'
\s5
\v 12 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Jeraha lako si la kupona; kidonda chako kimeenea.
\v 13 Hakuna mtu wa kukutetea kesi yako; hakuna utetezi kwa ajili ya kidonda chako ili upone.
\s5
\v 14 Wapenzi wako wote wamekusahau. Hawatakuangalia, kwa maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui na nidhimu ya bwana mkatili kwa sababu ya uovu wako mwingi na dhambi zako zisizohesabika.
\v 15 Kwa nini unaita msaada kwa ajili ya jeraha lako? Maumivu yako hayaponyeki. kwa sambabu ya uovu wako mwingi, dhambi zako zisizohesabika, nimefanya mambo haya kwako.
\s5
\v 16 Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo.
\v 17 Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahwe—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayeujali Sayuni."
\s5
\v 18 Yahwe anasema hivi, "Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida.
\v 19 Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge.
\s5
\v 20 Kisha watu watakuwa kama ilivyokuwa mwanzo, na kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu wakati nitakapowaadhibu wote wanaowatesa kwa sasa.
\v 21 Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao nitakapomleta karibu na atakapanikaribia mimi. kama sitafanya hivyo, ni nani atakayethubutu kunisogelea? —hili ni tangazo la Yahwe.
\v 22 Kisha mtakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu.
\s5
\v 23 Ona, tufani ya Yahwe, ghadhabu yake, imekwenda nje. Ni tufani isiyokoma. Itazunguka juu ya vichwa vya watu waovu.
\v 24 Hasira ya Yahwe haitarudi mpaka itoke na kutimiza makusudi ya moyo wake. Katika siku za mwisho mtalielewa hili."
\s5
\c 31
\p
\v 1 "Katika wakati huo—hili ni tangazo la Yahwe—Nitakuwa Mungu wa familia zote za Israel, na watakuwa watu wangu."
\v 2 Yahwe anasema hivi, "Watu ambao wamenusurika na upanga wamepata kibali katika nyika; nitatoka nje kuwapa pumziko Israeli."
\v 3 Yahwe alionitokea zamani na kusema, "Nimekupenda wewe, Israeli, kwa upendo wa milele. Kwa hiyo nimekuvuta kwang kwa agano la uaminifu.
\s5
\v 4 Nitakujenga tena kwa hiyo utakuwa umejengwa, bikra wa Israeli..... na kwenda nje michezo ya furaha.
\v 5 Utapanda mizabibu tena juu ya milima Samaria; wakulima watatapanda na kuweka matunda kwa ajili ya matumizi mazuri.
\v 6 Kwa maana siku itakuja wakati walizi watakapotangaza katika milima ya Efraimu, 'Inuka, twndeni juu kwenye mlimaa wa Yahwe Mungu wetu.'
\s5
\v 7 Kwa maana Yahwe anasema hivi, Piga kelele za shangwe juu ya Yakobo! Pigeni za furaha kwa ajili ya watu wakuu wa mataifa! Sifa zisikike. Sema, ''Yahwe amewaokoa watu wake, masalia wa Israeli.'
\s5
\v 8 Ona, niko karibu kuwaletaa kutoka nchi za kusini. Nitawakusanya kutoka sehemu zaa mbali za dunia. Vipofu na wenye ulemavu watakuwa kati kati yao; wanawake wajawazito na wale waliokaribu kujifungua wataakuwa pamoja nao. Kusanyiko kubwa litarudi hapa.
\v 9 Watakuja kwa kuomboleza; nitawaongoza huku wakifanya maoambi yao. Nitawafanya wasafiri kataika mikondo ya maji katika bara bara ilinyoka. Hawatajikwaa juu yake, kwa maana nitakuwa baba kwa Israeli, na Afraimu atakuwa mzaliwa wanagau wwa kwanza
\s5
\v 10 Sikia neno la Yahwe, mataifa. Litangazeni pembezoni mwa visiwa mbali. Enyi mataifa lazima museme, 'Yule aliyemtawanya Israeli anamkusanya tena na kuwalinda kama mchungaji alindavyo kondoo.'
\v 11 Kwa maana Yahwe amemfidia Yakobo na kumkomboa kutoka mkono ambao ulikuwa na nguvu sana kwake.
\s5
\v 12 Kisha watakuja na kufurahia katika vilele vya Sayuni. Nyuso zao zitamelemeta kwa sababu ya wema wa Yahwe, juu ya nafaka na divai mpya, juu ya mafuta na malimbuko ya kwanza ya makundi na ng'ombe. Kwa maana maisha yao yatakuwa kama busitani iliyomwagiliwa, na hatatajisikia huzuni tena.
\s5
\v 13 Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamaoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
\v 14 Kisha nitayaloanaisha sana maisha ya makuhani. Watu wangu watajijaza wenyewe kwa wema—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 15 Yahwe anasema hivi: "Sauti imesikika katika Rama, kilio na maombolezo mengi. Ni Raheli akiomboleza kwa ajili watoto wake. Hataki kufarijiwa tena juu yao, kwa maana hawako hai tena."
\s5
\v 16 Yahwe anasema hivi, Zuia sauti yako usilie na macho yako yasitoe machizi; kwa maana kuna fidia kwa ajili ya mateso yako—hili ni tangazo la Yahwe—watoto wako watarudi kutoka nchi ya adui.
\v 17 Kuna matumaini kwa ajili ya siku zenu za baadaye—hili ni tangazo la Yahwe—uzao wako watarudi ndani ya mipaka yao."
\s5
\v 18 Kwa hakika nimemsikia Efraimu akilia, 'Uliniadhibu, nami nieadhibika kama ndama assiye na mafunzo. Nirudisha na nitarudishwa, kwa maana wewe ni Yahwe Mungu wangu.
\v 19 Kwa maana baada ya kurudi kwako, nilikuwa na huzuni; baada ya kufundiswa, nilijipiga kofi sshavu langu. Niliaibika ana dharirika, kwa maana nilizaliwa na hataia ya ujana wangu.'
\v 20 Efraimu siyo mtoto wangu wa thamani? Yeye si mpendwa wangu, mwanangu anipendezaye? Kwa maana kila ninaponena juu yake, bado nina mwita kipenzi cha akili yangu. Kwa namna hii moyo wangu unamtamani. Kwa hakika nitaakuwa na huruma ajuu yake—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 21 Jiwekee alama za bara bara kwa ajili yako mwenyewe. Weka matangaazo ya maelekezo kwa ajili yako mwenyewe. Iweke akili yako juu ya njia sahihi, njia unayopaswa kufuata. Rudii, bikra Israeli! Rudi kwenye hii miji yako.
\v 22 Utatanga tanga hadi lini, binti usiye mwaminifu? Kwa maana Yahwe ameumba kitu fulani kipya juu ya dunia—mwanamke anamzunguka mwanaume.
\s5
\v 23 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, '"Nitakapowarudisha watu katika nchi yao, watasema hivi katika anchi ya Yuda na miji yake, "Yahwe akubariki, wewe sehemu takatifu ambapo anaishi, ewe mlima mtakatifu.'
\v 24 Kwa maana Yuda na miji yake yote wataishi pamoja humo, kama vile watakavyoishi wakulima na wachungaji pamaoja na makundi yao.
\v 25 Kwa maana nitawapa majai ya kunywa waliochoaka, na nitamjaza kila anayeteseka na kiu."
\v 26 Baada ya haya niliamka, na nikagundua kwamba usingizi wangu ulikuwa unaburudisha.
\s5
\v 27 Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yaahwe—nitakapoipanda nyumba ua Israeli na Yuda pamoja na wazawa wa wanadamaau na wanyama.
\v 28 Zamani, niliwaweka katika uangalizi ili kuwang'oa na kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu, na kuwaletea madhara. Lakini katika siku zijazo, nitawaangalia, ili niwajenge na kuwapanda—hili ji tangazo la Yahwe.
\s5
\v 29 Katika siku hizo hakuna atakayesema tena, "Baba za watu wamekula zabibu kali, bali meno ya watoto ni butu.'
\v 30 Kwa maana kila mtu atakuwa katika uovu wake mwenyewe; kila alaye zabibu kalai, meno yake yataakuwa butu.
\s5
\v 31 Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapoanzisha aganao jipya pamaoja na nyumba aya Israeli na nyumba ya Yuda.
\v 32 Halitakuwa kama agano ambalo nilianzisha na baba zao nilipowatoa kwa mkono wao nje ya nchi ya Missiri. Hizo zzilikuwa siku ambapo walilivunja aaganao lanaahu, ingawa nilikuwa mme kwao—hili ni tangazo la Yahwe.
\s5
\v 33 Lakaini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahwe: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watau wangu.
\v 34 Kisha kila mtu hatamfundisha jiranai yake, wala mtu hatamfundisha ngugu yake akisema, 'Mjue Yahwe!' Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao."'
\s5
\v 35 Yahwe anasema hivi—Yahwe, yeye afanyaye jua kuangaza mchana na kuzipanga mwezi na nyota kuangaza usiku. Yeye ndiye aiwekaye bahari katika mwendo ili mawimbi yake yaungurume. Yahwe wa majeshi katika ajina lake.
\v 36 Anasema hivi, ikiwa tu mambo haya ya akudumu yakitoweka machoni panaagu—hili ni agizo la Yahwe—uzao wa Israeli hawatasimama mbaalai nami wasiwe taiafa."
\s5
\v 37 Yahwe anasema hivi, "Kama tu urefu wa mbingu unaweza kupimwa, na kama tu misingi ya dunia chini inaweza kugunduliwa, nitawakataa uzao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyofanya—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 38 "Angalia, siku zinakuja—hili ni tanagazo la Yahwe—ambapo mji utajengwa tena kwa ajili yanagu, kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye Lango la Pembeni.
\v 39 Kisha mistari ya kupimia itaenda nje hadi mbali, hadi kwenye kilima cha Garebu na kuzunguka Goa.
\v 40 Bonde lote la miili iliyokufa na majivu, na shamaba lenye matuta linalofika hadi Bonde la Kidroni mbali hadi kwenye kona ya Lango la Farasi upande wa mashariki, litateuliwa kwa ajili ya Yahwe. Mji hautang'olewa wala kupinduliwa tena, milele."
\s5
\c 32
\p
\v 1 Neno likaja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe katika mwaka wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza.
\v 2 Katika wakati huo, jeshsi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka Yerusalemu, na Nehemia nabii alikuwwa amefungwa katika uwanja wa walinzi katika nyumba ya mfalme wa Yuda.
\s5
\v 3 Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga na kusema, "Kwa nini unatabiri na kusema, 'Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kuweka mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, na atauteka.
\v 4 Sedekia mfalme wa Yuda hatapona kutoka kwenye mikono ya Wakaldayo, kwa maana hakika atatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli. Mdomo wake utazumzia kwenye mdomo wa mfalme, na macho yake yatayaona macho ya mfalme.
\v 5 Atampeleka Sedekia Babeli, na atabaki huko hadi nimuadhibu—hili ni tangazo la Yahwe. Ingawa unapigana dhidi ya Wakaldayo, hautafanikiwa."
\s5
\v 6 Yeremia akasema, "Neno la Yahwe likaja kwangu, likisema, Angalia, Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako anakuja kwako na atasema,
\v 7 "Linunue shamba langu ambalo liko katika Anathothi kwa ajili yako, kwa maana haki ya kununua ni yako.""
\s5
\v 8 Kisha, kama Yahwe alivyotangaza, Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu katika uwanja wa walinzi, na akasema kwangu, 'Linunue shamba langu kwa ajili yako ambalo liko Anathothi katika nchi ya Benyamini, kwa maana haki ya urithi ni ya kwako, na haki ya kulinunua ni yako. Linunue kwa ajili yako.' Kisha nilijua kuwa hili lilikuwa neno la Yahwe.
\v 9 Kwa hiyo nililinua shamba katika Anathothi kutoka kwa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na nilipima fedha kwa ajili yake, shekeli kumi na saba katika uzito.
\s5
\v 10 Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashadi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani.
\v 11 Kisha nikaichukua hati ya manunuzi ambayo ilikuwa imepigwa muhuri, kwa kuifuata amri na taratibu, na kama ilivyo ada.
\v 12 Ile barua nikampa Baruku mwana wa Neria wa Maaseya mbele ya Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mashahidi waliotia sahihi kwenye barua iliyopigwa muhuri, na mbele ya Wayahudi wote waliokaa katika uwanja wa walinzi.
\s5
\v 13 Kwa hiyo nikampa amri Baruku mbele yao. Nilisema,
\v 14 Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Chukua nyaraka hizi, vyote hati hii ya manunuzi iliyopigwa muhuri na nakala zisizopigwa muhuri za manunuzi, na uziweke katika chungu cha udongo ili vidumu kwa muda mrefu.
\v 15 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nyumba, mashamba, na mashamba ya mizabibu vitanunuliwa tena katika nchi hii.
\s5
\v 16 Baada ya kumpa Baruki mwana wa Neria ile hati ya manunuzi, nikaomba kwa Yahwe nikasema,
\v 17 Ole, Bwana Yahwe! Angalia! Wewe peke yako umezitengeneza mbingu na dunia kwa nguvu zako kuu na kwa mkono wako ulioinuka. Hakuna kitu ambacho ukisema kwako ni kigumu sana kukifanya.
\v 18 Wewe huonesha agano la uaminifu kwa maelfu na kumimina makosa ya wanadamu katika mapaja ya watoto wao baada yao. Wewe ni Mungu mkuu na mwenye nguvu.
\s5
\v 19 Wewe ni mkuu katika hekima na una nguvu katika matendo, kwa maana macho yako yanaona njia zote za watu, ili kumlipa kila mtu stahiki ya matendo yake.
\v 20 Ulifanya ishara na maajabu katika nchi ya Misiri. Hata leo hapa Israeli na kati ya wanadamu wengine wote, umelifanya jina lako kuwa maarufu.
\v 21 Kwa maana uliwanunua watu wako Israeli kwa ishira na maajabu, kwa mkono hodari, kwa mkono ulioinuka, na kwa hofu kuu.
\s5
\v 22 Kisha uliwapa nchi hii—ambayo uliapa kwa babu zao kwamba utawapa—nchi itiririkayo maziwa na asali.
\v 23 Hivyo walingia na kuimiliki. Lakini hawakuitii sauti yako wala kuishi kwa kuitii sheria yako. Hawakufanya chochote ulichowaamuru kufanya, kwa hiyo umeleta juu yao majanga haya yote.
\s5
\v 24 Angalia! Urefu wa maboma haya umefika hadi kwenye mji ili kuuteka. Kwa sababu ya upanga, njaa, na tauni, mji umetiwa kwenye mikono ya Wakaldayo wanaopigana dhidi yake. Kwa maana ulichosema kitatokea sasa kinatokea, na ona, unatazama.
\v 25 Kisha wewe mwenyewe uliniambia, "Nunua shamba kwa fedha kwa ajili yako na mashahidi wameshuhudia, ingawa mji huu unatiwa mikononi mwa Wakaldayo.""
\s5
\v 26 Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 27 "Angalia! Mimi ni Yahwe, Mungu wa wanadamu wote. Kuna kitu cho chote kigumu sana kwangu kukifanya?
\v 28 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi, 'Ona, niko karibu kuutia mji huu kwenye mikono ya Wakaldayo na Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Atauteka.
\s5
\v 29 Wakaldayo wanaopigana dhidi ya mji huu watakuja na kuwasha moto kwenye mji huu na kuunguza, pamoja na nyumba juu ya paa la watu waliomwabudu Baali na kumimina dhabihu kwa miungu wengine ili kunikasirisha.
\v 30 Kwa maana watu wa Israeli na Yuda hakika wamekuwa watu wanaofanya maovu mbele ya macho yangu tangu ujana wao. Watu wa Israeli hakika wameniudhi kwa matendo ya mikono yao—hili ni tangazo la Yahwe.
\s5
\v 31 Yahwe anatangaza kwamba mji huu umekuwa sababu ya hasira yangu na ghadhabu yangu tangu siku walipoujenga. Umekuwa hivyo hata leo. Kwa hiyo nitaundoa mbele ya uso wangu
\v 32 kwa sababu ya uovu wote wa watu wa Israeli na Yuda, mambo waliyofanya ili kunichukiza—wao, wafalme wao, wana wa wafalme, makuhani, manabii, na kila mtu katika Yuda na wakaaji wa Yerusalemu.
\s5
\v 33 Wamenigeuzia migongo yao badala ya nyuso zao, ingawa niliwafundisha kwa furaha. Nilijitahidi kuwafundisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyenisikiliza ili kupokea marekebisho.
\v 34 Walisimamisha sanamu zao za ajabu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu, ili kunitia unajisi.
\v 35 Wakazijenga sehemu za juu katika Bonde la Beni Hinomu ili kuwatia katika moto wana wao na binti zao kwa ajili ya Moleki. Mimi sikuwaagiza. Sikuweka akilini mwangu kamwe kwamba watafanya mambo maovu na kwa hiyo kuwasabisha Yuda watende dhambi.
\s5
\v 36 Kwa hiyo sasa, Mimi, Yahwe, Mungu wa Israeli, kuhusu mji huu ninasema hivi, 'mji ambao mnasema, 'Umetiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli kwa upanga, njaa, na pigo.'
\v 37 Ona, niko karibu kuwakusanya kutoka kila nchi nilikowapeleka katika hasira yangu, ghadhabu, hasira kuu. Niko karibu kuwarudisha kwenye sehemu hii na kuwawezesha kuishi katika usalama.
\s5
\v 38 Kisha watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
\v 39 Nitawapa moyo mmjoa na na njia moja ya kuniheshimu kila siku ili kwamba yawepo mema kwa ajili yao na uzao wao baada yao.
\v 40 Kisha nitafanya pamoja nao agano la milele, ili nisiache kufanya mema kwa ajili yao. nitajiwekea heshima katika mioyo yao, ili kwamba wasiniache.
\s5
\v 41 Kisha nitajifurahisha katika kufanya mema kwao. Kwa uaminifu nitawapanda katika anchi hii kwa moyo wangu wote na maisha yangu yoye.
\v 42 Kwa amaana Yahwe anasema hivi, 'Kama tu nilivyoyaleta majanga haya makubwa yote juu ya watu hawa, hivyo hivyo nitaleta juu yao mambo mema niliyosema kwamba nitafanya kwa ajili yao.
\s5
\v 43 Basi mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, ambayo mnaisema, "Hii ni nchi iliyoharibiwa, isiyo na mwanadamu wala mnyama. Imetiwa mikononi mwa Wakaldayo"
\v 44 Watanunua mashamba kwa fedha na kuandika katika barua zilizopigwa muhuri. Watawakusanya mashahidi katika nchi ya Benyamini, wote kuzunguka Yerusalemu na miji ya Yuda katika miji ya nchi yenye vilima, na katika nchi tambarare, na katika miji ya Negebu. Kwa maana nitawarejesha wafungwa wao—hili ni tangazo la Yahwe."'
\s5
\c 33
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia mara ya pili, alipokuwa bado amefungwa ndani ya uwanja wa walinzi, likisema,
\v 2 Yahwe muumbaji, anasema hivi—Yahwe, aumbaye ili athibitishishe—Yahwe ndilo jina lake,
\v 3 'Niite, na nitakuitika, nitakuelezea mambo makuu, siri ambazo huzielewi.'
\s5
\v 4 Kwa maana Yahwe, Mungu wa Israel, anasema hivi kuhusu nyumba zilizo katika mji huu na nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa kwa sababu ya maboma na upanga,
\v 5 Wakaldayao wanakuja kupigana na kuzijaza nyumba kwa hizi kwa majeshi ya watu ambao wataua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, nitakapouficha mji huu uso wangu kwa sababu ya uovu wao wote.
\s5
\v 6 Lakini ona, niko karibu kuleta uponyaji na tiba, kwa maana nitawaponya na nitawapa wingi wa, amani na uamainifu.
\v 7 Kwa maana nitawarudhisha wafungwa wao wa Yuda na Israeli; nitawajenga tena kama ilivyokuw mwanzo.
\v 8 Kisha nitawatakasa uovu wote walioufanya dhidi yangu. Nitasamehe makosa yote waliyonitenda, na na njia zote walizo asi dhidi yangu.
\v 9 Kwa maana mji huu kwa ajili yangu utakuwa chombo cha furaha, nyimbo, sifa na heshima kwa mataiafa yote ya dunia ambao watasikia mambo yote mema ninayokwenda kufanya kwa ajili ya huu mji. Kisha wataogopa na kutetemeka kwa sababu ya mambo yote mema na amani nitayoupa mji huu.'
\s5
\v 10 Yahwe anasema hivi, 'Katika sehemu hii ambayo sasa mnaisema, "Imetengwa, sehemu isiyo na mwanadamu wala mnyama," katika mji huu wa Yuda, na katika mitaa ya Yerusalemu ambayo imetengwa bila mwanadamu wala mnyama, zitasikika tena
\v 11 sauti za furaha na sauti za shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti za wale wasemao, wanapoleta shukrani katika nyumba ya Yahwe, "Mshukuruni Yahwe wa majeshi, kwa maana Yahwe ni mwema, na upendo wake usioshindwa wadumu milele!" Kwa maana nitawafanaya tena wafungwa wa nchi kuwa walivyokuwa mwanzo,' asema Yahwe.
\s5
\v 12 Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika sehemu hii ya ukiwa, ambamo sasa hakuna mwanadamu wala mnyama—katika miji yake yote kutakuwepo tena malisho ambapo wachungaji wataweza kupumzisha makundi yao.
\v 13 Katika miji hii katika nchi ya vilima, nchi tambarare, na Negevu katika nchi ya Benyamini na kuzunguka Yerusalemu yote, na katika miji ya Yuda, makundi yatapata njia chini ya mkono wa yule anayewahesabu,' asema Yahwe.
\s5
\v 14 Angalia! Siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—ambapo nitafanya niliyoahidi kwa nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
\v 15 Katika siku hizo na katika wakati huo nitachipua shina la haki kwa ajili ya Daudi, na litafanaya hukumu na haki katika nchi.
\v 16 Katika siku hizo Yuda wataokolewa, na Yurusalemu utaishi katika usalama, kwa maana hivi ndivyo atakavyoitwa, "Yahwe ni haki ni haki yetu."
\s5
\v 17 Kwa maana Yahwe anasema hivi: 'Mwana kutoka ukoo wa Daudi hatakosa kuketi katika kiti cha nyumba ya Israeli,
\v 18 wala mtu kutoka ukuhani wa Kilawi hatakosa kutoa sadaka za kuteketezwa mbele zangu, kutoa sadaka za chakula, na kutoa sadaka za nafaka wakati wote."'
\s5
\v 19 Neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 20 "Yahwe anasema hivi: 'Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana na usiku ili kwamba siku isikawie wala usiku usikawie kuja kwa wakati wake,
\v 21 basi mtaweza u kulivunja agano langu na Daudi mtumishi wangu, ili kwamba aspate mwana wa kuketi juu ya kiti chake cha enzi, na gano langu na makuhuni wa Kilawi, watumishsi wangu.
\v 22 Kama vile majeshsi ya mbinguni yasivyoweza kuhesabika, na kama vile mchanga wa ufukwe wa bahari usivyoweza kupimwa, ndivyo nitakavyouongeza uzao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi watumikao mbele zangu."
\s5
\v 23 Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 24 Hamkuzingatia walichotangaza watu hawa waliposema, 'Zile Familia mbili ambazo Yahwe alizichagua, sasa amezikataa'? Kwa jinsi hii hii waliwapuuza watu wangu, wakisema kwamba si taifa tena katika macho yao.
\s5
\v 25 Mimi, Yahwe, nasema hivi, 'Kama sijalithibitisha agano la mchana na usiku, na kama sijaziweka sheria za mbingu na dunia,
\v 26 basi nitawakataa uzao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na nisilete mtu kutoka kati yao wa kutawala juu ya uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha wafubgwa wao na kuonesha huruma kwao."'
\s5
\c 34
\p
\v 1 Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe, wakati Nebukadreza mfalme wa Babeli, majeshi yake yote, pamoja na falme zote za dunia, maeneo yote yaliyo chini ya mamlaka yake, na watu wake wote walikuwa wanapigana vita dhidi ya Yerusalemu na miji yake yote, kusema:
\v 2 'Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nenda na uzungumze kwa Sedekia mfalme wa Yuda na useme kwake, 'Yahwe asema hivi: Angalia, niko karibu kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atauchoma moto.
\v 3 Hautapona kutoka mkono wake, kwa maana kwa hakika utakamatwa na kutiwa mkononi mwake. Macho yako yatayaangalia macho ya mfalme wa Babeli; atazungumza kwako moja kwa moja ukiwa unaenda Babeli.'
\s5
\v 4 Sedekia mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Yahwe! Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, 'Hautakufa kwa upanga.
\v 5 Utakufa katika amani. Kama kwenye mafukizo ya babu zako, wafalme waliokuwepo kabla yako, watauchoma mwili wako. Watasema, 'Ole, bwana!" Watakuomboleza. Sasa nimesema—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 6 Kwa hiyo Yeremia nabii akatangaza kwa Sedekia mfalme wa Yuda maneno haya yote katika Yerusalemu.
\v 7 Jeshi la mfalme wa Babeli likafanya dhidi ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda iliyobaki: Lakishi, na Azeka. Miji hii ya yuda ilisalia kama miji yenye maboma.
\s5
\v 8 Neno lilomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe baada ya mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote katika Yurusalemu, ili kuwatanagazia uhuru
\v 9 ya kwamba kila mtu lazima amwachie huru mtumwa wake wa Kiebrania, wote wa kiume na wa kike, kwa hiyo mtu alipaswa kutomtumikisha Myahudi, ambaye alikuwa ndugu yake.
\s5
\v 10 Kwa hiyo watu wote na viongozi wakaingia katika agano kwamba kila mtu amwachie huru mtumwa wake wa kiume na waikke ili asiwe mtumwa tena. Walitii na kuwaweka huru.
\v 11 Lakini baada ya hapo walibadili akili zao. Wakawarudisha watumwa ambao walikuwa wamewaachia huru. Wakawalazimisha kuwa wataumwa tena.
\s5
\v 12 Kwa hiyo neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 13 "Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Mimi mwenyewe nilifanya agano na babu zenu katika siku ambayo niliwatoa nje ya nchi ya Misiri, nje ya nyumba ya utumwa. Hapo ndipo niliposema,
\v 14 Katika mwisho wa mwaka wa saba, kila mtu lazima amwachie ndugu yake, Mwebrania mwenzake aliyejiuza mwenyewe kwako ili kukutumikia kwa miaka sita. Mwagize aende kwa uhuru." Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kutega masikio yao kwangu.
\s5
\v 15 Sasa ninyi wenyewe mlitubu na kuanza yaliyomema katika macho yangu. Mlitangaza uhuru, kila mtu kwa jirani yake, na mlifanya agano mbele zangu kwenye nyumba iitwayo kwa jina langu.
\v 16 Lakini tena mmegeuka na kulichafua jina langu; mmemsababisha kila mtu kumleta tena mtumwa wake wa kiume na wa kike, wale mliowachie kwenda walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa tena.'
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, 'Ninyi wenyewe hamkunisikiliza. Mlipaswa kuwa mmetangaza uhuru, kila mmoja wenu, kwa ndugu zenu na Waisraeli wenzenu. Kwa hiyo angalia! Niko karibu kutangaza uhuru kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—uhuru wa upanga, tauni, na njaa, kwa maana naenda kuwafanya kitu cha ajabu katika macho aya kila ufalme juu ya dunia.
\v 18 Kisha nitashughulika na watu waliolivuja agano langu, ambao hawakuyashika maneno ya agano ambalo walilithibitisha mbele zangu walipomkata ng'ombe dume katika vipande viwili na kutembea katika vipande vyake,
\v 19 na kisha viongozi wa Yuda na Yerusalemu, matowashi na makuhani, na watu wote wa nchi wakatembea katika vipande vya yule ng'ombe dume.
\s5
\v 20 Nitawatia katika mikono ya adui zao na katika mikono ya hao wanaoutafuta uhai wao. Miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama juu ya dunia.
\v 21 Kwa hiyo nitawatia Sedekia mfalme wa Yuda na viongozi wake kwenye mikono ya adui zao na kwenye miko ya wale wanaoutafuta uhai wao na katika mikono ya majeshi ya mfalme wa Babeli ambayo yameinuka dhidi yenu.
\v 22 Angalia, niko karibu kutoa amari—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawaleta tena kwenye mji huu ili wapigane dhidi yake, na kuunguza kwa moto. Kwa maana nitaigeuza miji ya Yuda kuwa sehemu za ukiwa ambamo hapatakuwa na wakaaji."
\s5
\c 35
\p
\v 1 Neno kutoka kwa Yahwe likamjia Yeremia katika siku za Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, kusema,
\v 2 "Nenda kwenye familia ya Warekabi na zungumza nao. Kisha uwalete kwenye nyumba yangu, mle ndani ya moyawapo ya vyumba, na uwape divai wanywe."
\s5
\v 3 Hivyo nilimchukua Yaazania mwana wa Yeremia mwana wa Habasinia na ndugu zake, wanawe wote, na familia yote ya Warekabi.
\v 4 Nikawapeleka wote kwenye nyumba ya Yahwe, katika vyumba vya wana wa Hanani mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu. Vyumba hivi vilikuwa karibu na chumba cha viongozi, ambacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya mwana wa Shalumu, mtunza lango.
\s5
\v 5 Kisha nikaleta mabakuli na vikombe vilivyojaa divai mbele ya Warekabi na kusema kwao, 'Kunyeni divai."
\v 6 Lakini walisema, "hatutakunywa divai yoyote, kwa maana babu yetu, Yonadabu mwana wa Rekabu, alituamuru, Msinywe divai yoyote, ninyi wala uzao wenu, milele.
\v 7 Pia, msijenge nyumba yoyote, kupanda mbegu zozote, wala kupanda shamba lolote la mizabibu; hivi siyo kwa ajili yenu. Kwa maana lazima muishi katika hema maisha yenu yote, ili kwamba muweze kuishsi siku nyingi katika nchi mnayoishi kama wageni.'
\s5
\v 8 Tumeitii sauti ya Yonadabu mwana wa Rekabu, babu yetu, katika yote aliyotuamuru, kutokunywa divai maisha yetu yote, sisi, wake zetu, wana wetu, na binti zetu.
\v 9 Hatutajenga nyumba kwa ajili ya kuishi ndani, na hatutakuwa na shamba la mizabu, konde, wala mbegu ya kumiliki sisi.
\v 10 Tumeishi katika hema na tumetii na kufanya yote aliyotuamuru Yonadabu babu yetu.
\v 11 Lakini Nebukadreza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi, tulisema, 'Njoo, lazima twende Yerusalemu ili tupone na mkono wa Wakaldayo na majeshi ya Waaramu. 'Kwa hiyo tunaishi Yerusalemu."
\s5
\v 12 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 13 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Nenda na useme kwa wanaume wa Yuda na wakaaji wa Yeruslemu, 'Hamtapokea maelekezo na kulisikiliza neno langu? —hili ni tangazo la Yahwe.
\v 14 Maneno ya Yonadabu mwana wa Rekabu aliyowapa wanawe kama amri. wasinywe divai yoyote, yameheshimiwa hadi leo. Wameitii amri ya babu yao. Lakini mimi, nimekuwa nikifanya matangazo kwenu bila kukoma, lakini hamnisikilizi.
\s5
\v 15 Niliwatuma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nilikuwa nawatuma bila kukom ili waseme, 'Kila mtu auache uovu wake na kutenda matendo mema; asiwepo mtu wa kuifuata miungu mingine tena na kuiabudu. Bdala yake, rudini kwenye nchi niliyowapa ninyi na babu zenu,' bado hamtanisikiliza wala kutega maskio yenu kwangu.
\v 16 Kwa maana uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu wamezishika amri za babu yao alizowapa, lakini watu hawa hupuuza kunisikiliza."
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Angalia, Ninaleta juu ya Yuda na juu ya kila mtu anayeishi Yerusalemu, majanga yote niyotamka dhidi yao kwa sababu niliwaambia, lakini hawakusikiliza; niliwaita, lakini hawakuitika."
\s5
\v 18 Yeremia akasema kwa familia ya Warekabi, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: mmezisikiliza amri za Yonadabu babu yenu na kuzishika zote—mmeyatii yote aliyowaamuru kufanya—
\v 19 kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Siku zote kutakuwa na mtu kutoka uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu kwa ajili ya kunitumikia."'
\s5
\c 36
\p
\v 1 Ilikuja tokea katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosiah mfalme wa Yuda, kwamba neno hili lilikuja kwa Yeremiah kutoka kwa Yahwe, na alisema,
\v 2 "Chukua kitabu kwa ajili yako na uandike juu yake maneno yote ambayo nimekwisha kukuambia kuhusiana na Israel na Yuda, na kila taifa. Fanya hivi kwa kila kitu nilichokuambia tokea siku za Yosia mpaka siku ile.
\v 3 Huenda watu wa Yuda watasikiliza majanga yote ambayo ninakusudia kuleta juu yao. Huenda kila mmoja ataacha njia zake mbaya, ili kwamba niweze kuwasamehe maovu yao na dhambi zao."
\s5
\v 4 Kisha Yeremia alimwita Baruku mwana wa Neria, na Baruku aliandika kwenye kitabu, kwa imla ya Yeremia, maneno yote ya Yahwe yalizunguzwa kwake.
\v 5 Kisha Yeremia alitoa amri kwa Baruku. Alisema, "Niko gerezani na siwezi kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 6 Kwa hiyo unapaswa uende na kusoma kutoka kwenye kitabu ulichoandika kwa imla yangu. Kwa siku ya kufunga, unapaswa usome maneno ya Yahwe kwenye masikio ya watu katika nyumba yake, na pia kwenye masikio ya Yuda yote waliokuja kutoka katika miji yao. Tangaza maneno haya kwao.
\s5
\v 7 Huenda maombi yao ya rehema yatakuja mbele ya Yahwe. Huenda kila mtu ataacha njia mbaya, kwani gathabu na hasira ya Yahwe imetangazwa dhidi ya watu kwa ukali."
\v 8 Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alifanya kila kitu ambacho Yeremia nabii alimwamuru yeye kufanya. Alisoma kwa sauti maneno ya Yahwe ndani mwa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 9 Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahwe.
\v 10 Baruku alisoma kwa sauti maneno ya Yeremia katika nyumba ya Yahwe, kutoka kwenye chumba cha Gamaria mwana wa Shafani mwandishi, katika ua wa juu, kwa mlango wa kuingilia wa nyumba ya Yahwe. Alifanya hivi kwa masikio ya watu wote.
\s5
\v 11 Basi Mikaya mwana wa Gemaria alisikia maneno yote ya Yahwe kwenye kitabu.
\v 12 Alienda chini kwenye nyumba ya mfalme, kwenye chumba cha katibu. Tazama, maafisa wote walikuwa wamekaa hapo: Elishama mwandishi, Delaiah mwana wa Shemaiah, Elnathan mwana wa Achbor, Gemaria mwana wa Shefani, na Sedekia mwana wa Hananiah, na maafisa wote.
\s5
\v 13 Kisha Mikaya alitoa taarifa ya maneno yote kwao ambayo alikuwa amesikia ambayo Baruku alisoma kwa sauti kwenye masikio ya watu.
\v 14 Kwa hiyo maafisa wote walimtuma Jehudi mwana wa Nethania mwana wa Shelemiah mwana wa Kushi, kwa Baruku. Jehudi alisema kwa Baruku, "Chukua kitabu katika mkono wako, kitabu ambacho ulikuwa unakisoma kwa masikio ya watu and kuja." Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alichukua kitabu katika mkono wake na alienda kwa maafisa.
\v 15 Kisha walisema naye,"Kaa chini na usome haya katika masikio yetu." Kwa hiyo Baruku akasoma kitabu.
\s5
\v 16 Ilitokea wakati waliposikia haya maneno yote, kila mtu alipatwa na hofu kwa mtu aliye karibu naye na kusema kwa Baruku, "Kwa hakika tunapaswa kutoa taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme."
\v 17 Kisha walimuuliza Baruku, "Tuambie, ulipataje kuandika maneno yote haya kwa imla ya Yeremia?"
\v 18 Baruku aliwaambia, "Alitoa imla ya maneno haya yote kwangu, na nikayaandika kwa wino kwenye kitabu hiki."
\v 19 Kisha maafisa walisema kwa Baruku, "Nenda, jifiche mwenyewe, na Yeremiah, pia. Usipatikane mtu yeyote kujua uko wapi."
\s5
\v 20 Kisha walienda kwa uwanja wa mfalme na wakatoa taarifa ya maneno haya kwake. Lakini kwanza walikihifadhi kitabu kwenye chumba cha katibu Elishama.
\v 21 Basi mfalme alimtuma Yehudi kuchukua kitabu. Yehudi alikichukua toka chumba cha Elishama katibu. Kisha alikisoma kwa sauti kwa mfalme na wote maafisa walikuwa wamesimama karibu naye.
\v 22 Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake.
\s5
\v 23 Ilitokea wakati Yehudi aliposoma kurusa tatu au nne, mfalme angeweza kuikata kwa kisu na kuitupa kwenye moto katika mkaa mpaka kitabu chote kiliteketea.
\v 24 Lakini wala mfalme wala yeyote wa mjakazi wake aliyesikia haya maneno yote aliogopa, wala hawakuchana nguo zao.
\s5
\v 25 Elnathani, Delaya, na Gemaria walikuwa wamemuomba mfalme asikichome kitabu, lakini hakuwasikiliza.
\v 26 Basi mfalme alimwamuru Yerameeli, ndugu, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kumfunga Baruku mwandishi na Yeremia nabii, lakini Yahwe alikuwa amewaficha.
\s5
\v 27 Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia baada ya mfalme kuwa amechoma kitabu na maneno ya Baruku yaliyokuwa yameandikwa kwa imla ya Yeremia, na alisema,
\v 28 "Rudi, chukua kitabu kingine kwa ajili yako, na uandike maneno haya yote ambayo yalikuwa kwenye kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikichoma.
\v 29 Kisha unapaswa kusema hivi kwa mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: 'Ulichoma hicho kitabu! Na ulisema: Kwanini umeandika juu yake, " Mfalme wa Babeli hakika atakuja na kuharibu nchi hii, kwa kuwa atawaangamiza wanaume wote na wanyama ndani yake?"
\s5
\v 30 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, Yehoyakimu mfalme wa Yuda: "Hakuna mzao wako atawahi kukaa kwenye kiti cha Daudi. Kama wewe, maiti yako itatupwa kwenye siku ya joto na usiku wa baridi.
\v 31 Kwa kuwa nitakuadhibu, wazao wako, na wajakazi wako kwa maovu yenu yote. Nitaleta kwenu, kwa wakazi wote wa Yerusalemu, na kwa kila mtu Yuda majanga ambayo nimewatishia ninyi, lakini kwa hamkuwa makini."
\s5
\v 32 Kwa hiyo Yeremia alichukua kitabu kingine na akampa Baruku mwana wa Neria mwandishi. Baruku aliandika juu yake kwa imla ya Yeremia maneno yote ambayo yalikuwa katika kitabu kilichochomwa moto na mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda. Zaidi, maneno mengi ya kufanana yaliongezwa kwenye kitabu hiki.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Sasa Sedekia mwana wa Yosia alitawala kama mfalme badala ya Yehoyachin mwana wa Yehoyakimu. Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa amemfanya Sedekia mfalme juu ya nchi ya Yuda.
\v 2 Lakini Sedekia, wajakazi wake, na watu wa nchi hawakusikiliza maneno ya Yahwe ambayo alitangaza kwa mkono wa Yeremia nabii.
\s5
\v 3 Kwa hiyo Mfalme Sedekia, Yehukali mwana wa Shelemia, na Zefania mwana wa Maaseia kuhani alituma ujumbe kwa Yeremia nabii. Walisema, "Omba kwa niaba kwa Yahwe Mungu wetu."
\v 4 Sasa Yeremia alikuwa anakuja na kwenda miongoni mwa watu, kwa kuwa alikuwa bado hajawekwa ndani ya gereza.
\v 5 Jeshi la Farao lilitoka Misri, na Wakaldayo waliozingira Yerusalem walisikia habari kuhusu wao na kuondoka Yerusalem.
\s5
\v 6 Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia nabii na kusema,
\v 7 "Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi: Hiki ndivyo utakavyosema kwa mfalme wa Yuda, kwa sababu amekutuma wewe kutafuta ushauri toka kwangu, 'Ona, jeshi la Farao, ambalo lilikuja kukusaidia, liko tayari kurudi Misri, kwenye nchi yao.
\v 8 Wakaldayo watarudi. Watapigana dhidi ya mji huu, kuuteka, na kuuchoma.'
\s5
\v 9 Yahwe asema hivi: Msidaganyane kwa kusema, "Hakika Wakaldayo wanatuacha sisi,' kwa kuwa hawatatuacha.
\v 10 Hata kama mmelishinda jeshi la Wakaldayo lote ambalo linapigana nanyi ili kwamba wanaume waliojeruhiwa walibakizwa katika mahema yao, wangeweza kunyanyuka na kuchoma mji huu."
\s5
\v 11 Basi ilikuwa wakati jeshi la Wakaldayo lilipoondoka Yerusalem wakati jeshi la Farao lilikuwa linakuja,
\v 12 kisha Yeremia alienda toka Yerusalem kwenda nchi ya Benjamini. Alitaka kumiliki njia ya nchi huko miongoni mwa watu wake.
\v 13 Kama alivyokuwa katika mlango wa Benjamini, mlinzi mkuu aliyekuwa hapo. Jina lake lilikuwa Yeria mwana wa Shelemia mwana wa Hanania. Alimshika kwa kumnyakua Yeremia nabii na kusema, " Mnatoka jangwani kwa Wakaldayo."
\s5
\v 14 Lakini Yeremia alisema, "Hiyo si kweli. Siendi jangwani kwa Wakaldayo." Lakini Yeria hakumsikiliza. Alimchukua Yeremia na kumleta kwa maafisa.
\v 15 Maafisa walikuwa wamemkasirikia Yeremia. Walimpiga na kumweka gerezani, ambayo ilikuwa nyumba ya Yonathani mwandishi, kwa kuwa waligeuza kuwa gereza.
\s5
\v 16 Kwa hiyo Yeremia alikuwa amewekwa kwenye kifungo cha chini, ambako alikuwa huko kwa siku nyingi.
\v 17 Kisha mfalme Sedekia alimtuma mtu mmoja aliyemleta kwenye ikulu. Kwenye nyumba yake, mfalme alimuuliza binafsi, "Kuna neno: Utatiwa kwenye mkono wa mfalme wa Babeli."
\s5
\v 18 Kisha Yeremia alisema kwa mfalme Sedekia, "Kwa namna gani nimekutenda dhambi, mjakazi wako, au watu hawa kwamba umeniweke mimi kwenye gereza?
\v 19 Wako wapi nabii wako, wale waliotabiri kwa ajili yako na kusema mfalme wa Babeli hatakuja dhidi yako au dhidi ya nchi hii?
\v 20 Lakini sasa sikiliza, bwana wangu mfalme! Acha ombi langu liwe mbele yako. Usinirudie mimi kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, au nitakufa huko."
\s5
\v 21 Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja walinzi.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, na Pashuri mwana wa Malkiya alisikia maneno ambayo Yeremia alikuwa akitanganza kwa wato wote. Alikuwa akisema,
\v 2 "Yahwe asema hivi: Yeyote anayeishi kwenye mji huu atauwawa kwa upanga, njaa, na pigo. Lakini yeyote ambaye aendae kwa Wakaldayo ataishi. Atatoroka pamoja na maisha yake mwenyewe, na kuishi.
\v 3 Yahwe asema hivi: Huu mji huu utapewa kwa mkono wa jeshi la mfalme wa Babeli, na ataukamata."
\s5
\v 4 Kwa hiyo maafisa walisema kwa mfalme, "Acha mtu huu afe, kwa kuwa kwa njia hii anadhofisha mikono ya wanaume wapiganaji waliobaki kwenye mji huu, na mikono ya watu wote. Anatanganza maneno haya, kwa kuwa huyu mtu hafanyi kwa usalama wa watu hawa, lakini kwa majanga."
\v 5 Basi mfalme Sedekia alisema, "Tazama, yuko mkononi mwako kwa kuwa hakuna mfalme awezae kumpinga."
\s5
\v 6 Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
\s5
\v 7 Sasa Ebed Meleki Mkushi alikuwa mmoja wa watowashi katika nyumba ya mfalme. Alisikia kwamba walikuwa wamemuweka Yeremia kwenye kisima. Sasa mfalme alikuwa ameketi kwa mlango wa Benjamini.
\v 8 Basi Ebed Meleki alienda toka nyumba ya mfalme na kuzungumza na mfalme.
\v 9 Alisema, "Bwana wangu mfalme, hawa wanaume wamefanya uovu kwa namna walivyomtendea Yeremia nabii. Walimtupa kwenye kisima kwa ajili ya kufa kutokana na njaa, tangu hakuna chakula zaidi katika mji."
\s5
\v 10 Kisha mfalme alitoa amri kwa Ebed Meleki Mkushi. Alisema, "Chukua amri ya watu thelasini kutoka hapa na mtoe Yeremia nabii nje ya kisima kabla hajafa."
\v 11 Basi Ebed Meleki alichukua amri ya watu hao na akaenda nyumba ya mfalme, kwenye ghala la nguo chini ya nyumba. Toka hapo alichukua vitambaa na nguo zilizochanika na kuyashusha chini kwa kamba kwa Yeremia ndani ya kisima.
\s5
\v 12 Ebed Meleki Mkushi alisema kwa Yeremia, "Weka matambara na nguo zilizoraruka chini ya mikono yako na juu ya kamba." Basi Yeremia alifanya hivyo.
\v 13 Kisha walimvuta Yeremia kwa kamba. Kwa njia hii walimtoa kutoka kisimani. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi.
\s5
\v 14 Kisha Mfalme Sedekia alituma neno na kumleta Yeremia nabii kwake, kwenye lango la tatu la nyumba ya Yahwe. Mfalme alisema kwa Yeremia, "Nataka nikuulize kitu. Usinizuilie jibu mimi."
\v 15 Yeremia alisema kwa Sedekia, "Kama nakujibu, hautaniuawa kwa hakika? Na kama nakupa ushauri, hautanisikiliza mimi."
\v 16 Lakini Mfalme Sedekia aliapa kwa Yeremia kwa siri na kusema, "Kama Yahwe aishivyo, yeye aliyetufanya sisi, Sitakuuwa au kukuweka kwenye mkono wa watu wale wanaotafuta maisha yako."
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yeremia alisema kwa Sedekia, "Yahwe, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama kwa kweli utatoka kwenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli basi utaishi, and mji huu hautachomwa. Wewe na familia yako mtaishi.
\v 18 Lakini kama hautaenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, basi mji huu utachukuliwa kwa mkono wa Wakaldayo. Watauchoma, na hautakwepa kutoka mkono wao."
\s5
\v 19 Mfalme Sedekia alisema kwa Yeremia, "Lakini ninaogopa watu wa Yuda waliotoka jangwani kwenda kwa Wakaldayo, kwa sababu nitapewa katika mkono wao, kwa kunifanyia vibaya."
\s5
\v 20 Yeremia alisema, "Hawatakutoa kwao. Tii ujumbe toka kwa Yahwe ambao ninakuambia, ili kusudi mambo yataenda vizuri kwako, na ili kusudi utaishi.
\v 21 Lakini kama unakataa kutoka, hivi ndivyo Yahwe amenionesha mimi.
\s5
\v 22 Tazama! Wanawake wote walioachwa kwenye nyumba yako, mfalme wa Yuda, ataletwa kwa maafisa wa mfalme wa Babeli. Hawa wanawake watasema kwako, "Umedaganywa na rafiki zako; wamekuharibu. Miguu yako sasa imezama kwenye matope, na rafiki zako watakimbia.'
\v 23 Kwa kuwa wake zenu wote na watoto wataletwa kwa Wakaldayo, na wewe mwenyewe hautatoroka nchi yao. Utashikwa na mkono wa mfalme wa Babeli, na mji huu utachomwa."
\s5
\v 24 Kisha Sedekia alisema kwa Yeremia, "Usimjulishe yeyote kuhusu maneno haya, ili kwamba usije kufa.
\v 25 Kama maafisa wanasikia kwamba nimeongea na wewe- kama wanakuja na kusema kwako, 'Tuambia umezungumza nini pamoja na mfalme. Usitufiche, au tutakuuwa. Na tuambie nini mfalme amesema kwako'-
\v 26 kisha unapaswa kusema nao, "Nilishawishiana pamoja na mfalme asirudi kwangu kwa nyumba ya Yonathan nitakufa humo."
\s5
\v 27 Kisha maafisa wote walikuja kwa Yeremia na kumuuliza, basi aliwajibu kama mfalme alivyomuelekeza. Basi waliacha kuongea pamoja naye, kwa sababu hawakusikia mazungumzo kati ya Yeremia na mfalme.
\v 28 Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi mpaka siku ile Yerusalem ilipotekwa.
\s5
\c 39
\p
\v 1 Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem na kuizingira.
\v 2 Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sekeia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa.
\v 3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sarsechimu, afisa muhimu. Nerga Sharezeri alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.
\s5
\v 4 Ilitokea kwamba wakati Sedekia, mfalme wa Yuda, na wanaume wapiganaji wake wote walipowaona, walikimbia. Walitoka nje usiku toka kwenye mji kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango la kati la kuta mbili. Mfalme alitoka nje katika mwelekeo wa Arabah.
\v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo walimfatilia na kumpata Sedekia kwenye tambarare za mto Yordani karibu na Yeriko. Kisha walimshika na kumleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Riblah kwenye nchi ya Hamath, ambapo Nebukadreza alipitisha sentensi juu yake.
\s5
\v 6 Mfalme wa Babeli alimchinja binti wa Sedekia mbele ya macho yake huko Ribla. Pia aliwachinja wanaume wote wa heshima wa Yuda.
\v 7 Kisha alingoa macho ya Sedekia na kumfunga mnyororo wa shaba ili kusudi kumpeleka Babeli.
\s5
\v 8 Kisha Wakaldayo walichoma nyumba ya mfalme na nyumba za watu. Pia walivunja kuta za Yerusalem.
\v 9 Nebukadreza, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliwachukua katika mateka watu wengine waliobaki katika mji. Hii ilijumuisha watu waliotoka jangwa kwenda Wakaldayo na watu wengine walioachwa katika mji.
\v 10 Lakini Nebukadreza nahodha wa walinzi wa mfalme aliwaruhusu watu maskini ambayo hawakuwa na chochote wao kubaki katika chi ya Yuda. Aliwapa mashamba ya mizabibu na maeneo katika siku ile.
\s5
\v 11 Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa amri kuhusu Yeremia kwa Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme. Alikuwa amesema,
\v 12 "Mchukue na umjali. Usimdhuru. Fanya kwa ajili yake chochote anachokuambia."
\v 13 Basi Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme, Nebushazbani mkuu wa matoashi, Nergali Sharezeri afisa mkuu, na wote maafisa wa muhimu wa mfalme wa Babeli walituma watu nje.
\v 14 Watu wao walimchukua Yeremia kutoka uwanja wa mlinzi na kumkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikami mwana wa Shafani, kumchua nyumbani, basi Yeremia alibaki miongoni mwa watu.
\s5
\v 15 Sasa neno la Yahwe lilikuwa limekuja kwa Yeremia wakati alipokuwa chini ya kifungo kwenye uwanja wa mlinzi, na alisema,
\v 16 "Zungumza kwa Ebedi Meleki Mkushi na sema, 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Ona, Nimekaribia kubeba maneno yangu dhidi ya mji huu kwa ajili ya janga na si kwa uzuri. Kwa kuwa yatakuwa kweli mbele yako katika siku hiyo.
\s5
\v 17 Lakini nitakuokoa katika siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe - na hautatiwa katika mkono wa wanaume ambayo unawaogopa.
\v 18 Kwa kuwa nitakuokoa hakika. Hautaanguka kwa upanga. Utatoroka pamoja na maisha yako, kwani unanitumaini - hili lilikuwa tamko la Yahwe."
\s5
\c 40
\p
\v 1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia toka kwa Yahwe baada ya Nebuzaradni, amri wa walinzi wa mfalme, amemtuma mbali kutoka Ramah. Huko ndiko Yeremia alikuwa amechukuliwa, na huko alikuwa amefungwa kwa minyororo. Alikuwa miongoni mwa mateka wote ya Yerusalem na Yuda ambayo walipaswa kuwa matekani Babeli.
\v 2 Mlinzi mkuu alimchukua Yeremia na kusema kwake, "Yahwe Mungu wako aliamrisha maafa haya dhidi ya eneo hili.
\s5
\v 3 Basi Yahwe alileta. Alifanya kama alivyoamrisha, kwani ninyi watu mmefanya dhambi dhidi yake na hamkutii sauti yake. Hii ni sababu ya jambo hili limetokea kwenu. Lakini sasa tazama!
\v 4 Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda."
\s5
\v 5 Wakati Yeremia hakujibu, Nebuzaradani alisema, "Nenda kwa Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka msimamizi wa miji ya Yuda. Baki pamoja naye miongoni mwa watu au nenda popote ni pazuri katika macho yako kwenda." Amri wa walinzi wa mfalme alimpa chakula na zawadi, na kisha akamtuma mbali.
\v 6 Basi Yeremia alienda kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpah. Alibaki pamoja naye miongoni mwa watu ambao walibaki nyuma katika nchi.
\s5
\v 7 Sasa baadhi ya amri wa wanawajeshi wa Yuda ambao walikuwa bado katika uwanja- wao na watu wao - walisikia kuwa mfalme wa Babeli alimfanya Gedalia mwana wa Ahikam, liwali juu ya nchi. Pia walisikia kuwa amemweka kusimamia wanaume, wanawake, na watoto ambao walikuwa watu maskini katika nchi, wale ambao hawakuwa wamechukuliwa mateka Babeli.
\v 8 Basi walienda kwa Gedalia huko Mizpa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana Nethania; Yonathan na Yonathani, wana wa Kareaa; Seraya mwana wa Tanhumethi; wana wa Efai Netophathite; na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
\s5
\v 9 Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, alichukua kiapo kwao na kwa watu wao, na kusema kwao, "Usiogope kuwatumikia maafisa wa Wakaldayo. Ishi katika nchi na kumtumkia mfalme wa Babeli, na itakuwa vizuri kwenu.
\v 10 Na tazama, Ninaishi Mizpa kukutana pamoja na Wakaldayo waliokuja kwetu. Basi vuna mvinyo, matunda ya kiangazi, na mafuta na viweke kwenye vyombo vyako. Uishi katika miji ambayo umechukua."
\s5
\v 11 Kisha Wayahudi wote katika Moabu, miongoni mwa watu wa Ammoni, na katika Edomu, na katika kila nchi ilisikiwa kwamba mfalme wa Babalei ameruhusu mabaki ya Yuda kubaki, kwamba alimteua Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani juu yao.
\v 12 Basi Wayahudi wote walirudi toka kila eneo ambako walikuwa wametawanyika. Walirudi kwenye nchi ya Yuda, kwa Gedalia huko Mizpa. Walivuna mvinyo na matunda ya kiangazi kwa wingi.
\s5
\v 13 Yonathan mwana wa Karea na amri wote wa jeshi katika uwanja walikuja kwa Gedalia huko Mizpa.
\v 14 Walisema kwake, "Haujui kuwa Baalis mfalme wa watu wa Ammoni amemtuma Ishmael mwana wa Nethania kukuua?" Lakini Gedalia mwana wa Ahikim hakuwaamini.
\s5
\v 15 Basi Yonathan mwana wa Karea alizungumza kwa siri kwa Gedalia huko Mizpa na kusema, "Niruhusu niende kumuua Ishmael mwana wa Nethania. Hakuna atakaye nituhumu. Kwanini asikuue wewe? Kwanini kuruhusu Yuda yote ambayo imekusanywa kwako kutawanyishwa na mabaki ya Yuda kuharibiwa?"
\v 16 Lakini Gedalia mwana wa Ahikam alisema kwa Yonathan mwana wa Karea, "Usifanye jambo hili, kwa kuwa unasema uongo kuhusu Ishmael."
\s5
\c 41
\p
\v 1 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmael mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja - wanaume kumi walikuwa pamoja naye - kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja hukp Mizpa.
\v 2 Lakini Ishmael mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, kwa upanga. Ishmael alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi.
\v 3 Kisha Ishmael aliwauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa huko.
\s5
\v 4 Kisha ilikuwa siku ya pili baada ya kumuua Gedila, lakini hakuna moja aliyejua.
\v 5 Wanaume baadhi walikuja toka Shechem, toka Shiloh, na toka Samaria-wanaume semanini ambayo walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 6 Basi Ishmael mwana wa Nethania alienda toka Mizpa kukutana nao kama walivyoenda, wakitembea na kulia. Kisha ilitokea kwamba kama alivyokutana nao, alisema nao, "Njoo kwa Gedalia mwana wa Ahikam!"
\v 7 Ilikuja kuwa kwamba wakati walipokuja katika mji, Ishmaeil mwana wa Nethania aliwauwa na kuwatupa kwenye shimo, yeye na wanaume ambao walikuwa pamoja naye.
\s5
\v 8 Lakini palikuwa na wanaume kumi miongoni mwao ambao walisema kwa Ishmael, " Usituue, kwa kuwa kuna riziki zetu kwenye shamba: ngano na shayiri, mafuta na asili" Kwa hiyo hakuwauwa pamoja na rafiki zao wengine.
\v 9 Kisima ambacho Ishmael alitupa miili yote ya waliokufa ambaye yeye na Gedalia waliwapiga, kilikuwa ni kilekile ambacho mfalme Asa alichimba wakati alipokuwa akivamiwa na mfalme Baasha wa Israel. Ishmael mwana wa Nethania alilijaza wale ambao walikuwa wameuawa.
\s5
\v 10 Badae Ishmael aliwashika watu wengine wote ambao walikuwa huko Mizpa, mabinti wa mfalme na watu wote ambao walikuwa wameachwa huko Mizpa ambayo Nebuzaradani mlinzi mkuu alikuwa amewakabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikam. Basi Ishmael mwana wa Nethania aliwashika na kuvuka kwa watu wa Ammon.
\s5
\v 11 Lakini Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi pamoja naye walisikia madhara yote ambayo Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amefanya.
\v 12 Basi waliwachukua wanaume wao na kwenda kupigana dhidi ya Ishmanel mwana wa Nethania. Walipigana naye huko kwenye kisima kuu cha Gibeoni.
\s5
\v 13 Kisha ilitokea kwamba wakati watu wote ambao walikuwa na Ishmael kuona Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi ambao walikuwa pamoja naye, walikuwa na furaha.
\v 14 Basi watu wote ambao Ishmael alikuwa amewashika huko Mizpa waligeuka na kwenda kwa Yonathani mwana wa Karea.
\s5
\v 15 Lakini Ishmael mwana wa Nethania alitoroka na wanaume wanane toka kwa Yonathani. Alienda kwa watu wa Ammon.
\v 16 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi pamoja naye walichukua toka Mizpa watu wote ambao walikuwa wameokolewa kutoka kwa Ishmael mwana wa Nethania. Hii ilikuwa baada ya Ishmael kuwa amemuuwa Gedalia mwana wa Ahikam. Yonathan na rafiki zake walichukua wanaume shujaa, wanaume wapiganaji, wanawake na watoto, na mtoashi ambaye alikuwa ameokolewa huko Gibeoni.
\s5
\v 17 Kisha walienda na kubaki kwa muda huko Geruthi Chimham, ambayo iko karibu Bethelemu. Walikuwa wakienda Misri
\v 18 kwa sababu ya Wakaldayo. Walikuwa wakiwaogopa kwani Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amemua Gedalia mwana wa Ahikam, ambaye mfamle wa Babeli amewekwa kwenye usimamizi wa nchi.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Kisha amri wote wa jeshi na Yonathan mwana wa Karea, Jezania mwana wa Hoshaia, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa walimkaribia Yeremia nabii.
\v 2 Walisema naye, "Acha maombi yetu yaje mbele yako. Omba kwa ajili yetu kwa Yahwe Mungu wako kwa ajili ya watu hawa ambao wanabaki kwani tuko wachache katika idadi, kama unavyoona.
\v 3 Muulize Yahwe Mungu wako atuambia sisi njia yakuendea na nini tufanye."
\s5
\v 4 Basi Yeremia nabii alisema nao, "Nimewasikia, Tazama, Nitaomba kwa Yahwe Mungu wenu kama mlivyoomba. Vyovyote Yahwe ananijibu, Nitawambia. Sitawaficha chochote ninyi."
\v 5 Walisema na Yeremia, "Na Yawhe awe shahidi mkweli na mwaminifu dhidi yenu, kama hatutafanya kila kitu ambacho Yahwe Mungu wenu anatuambia kufanya.
\v 6 Hata kama ni vizuri au vibaya, tutatii sauti ya Yahwe Mungu wetu, ambaye tunawatuma ninyi, ili kwamba iwe vizuri pamoja nasi wakati tunatii sauti ya Yahwe Mungu wetu."
\s5
\v 7 Basi ilitokea kwamba baada ya siku kumi, neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia.
\v 8 Kwa hiyo Yeremia alimwita Yonathan mwana wa Karea na amri wote jeshi pamoja naye, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa.
\v 9 Na alisema nao, "Yahwe, Mungu wa Israel, ambaye umenituma mimi ili niweze kuweka maombi yako mbele zake. Yahwe asema hivi,
\v 10 Kama mtarudi na kuishi katika nchi hii, basi nitawajenga na sitawararua chini; Nitapanda na sitawangoa, kwa kuwa nitageuza maafa ambayo nimeleta juu yako.
\s5
\v 11 Msimugope mfalme wa Babeli, ambaye mnamuogopa. Msimuogope-hili ni tamko la Yahwe kwani niko pamoja nanyi kuwahifadhi na kuwaokoa toka mkono wake.
\v 12 Kwa kuwa nitawapa rehema. Nitakuwa na huruma juu yenu, na nitawarudisha kwenye nchi yenu.
\s5
\v 13 Lakini tudhani kusema kwamba, "Hatutakaa katika nchi hii"- kama hamtasikiliza sauti yangu, sauti ya Yahwe Mungu wenu.
\v 14 Tudhani kwamba mnasema, "Hapana! Tutaenda kwenye nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita yoyote, ambayo hatutasikia sauti ya tarumbeta, na hatutaona njaa ya chakula. Tutaishi huko."
\s5
\v 15 Sasa sikiliza neno hili la Yahwe, wewe mabaki ya Yuda. Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Kama kweli mtatoka kwenda Misri, kwenda na kuishi huko,
\v 16 basi upanga ambao mnauogopa utawapita huko kwenye nchi ya Misri. Njaa ambayo mnawasiwasi nayo itawafatilia huko Misri. Na mtakufa huko.
\v 17 Basi itatokea kwamba wanaume wote waliondoka kwenda Misri kuishi huko watakufa kwa upanga, njaa, au pigo. Hapatakuwa na mwathirika wao, hakuna atakayetoroka maafa ambayo nitaleta juu yao.
\s5
\v 18 Kwa kuwa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama gadhabu yangu na hasira yangu imemwanga juu ya wakazi wa Yerusalem, kwa njia hiyo hasira yangu itamwangwa juu yenu kama mtaenda Misri. Mtakuwa sababu ya hasira na hofu, sababu la kuzungumza laana, na kitu kisichokuwa na heshima. Na hamtaona eneo hili tena."
\v 19 Basi Yeremia alisema, "Yahwe amezungumza kuhusu ninyi - mabaki ya Yuda. Msiende Misri! Unajua kwa hakika kwamba nimekuwa shahidi dhidi yenu leo.
\s5
\v 20 Kwa kuwa mmejidanganya vibaya wenyewe wakati mliponituma mimi kwenda kwa Yahwe Mungu wenu na kusema, 'Omba kwa Yahwe Mungu wetu kwa ajili yetu. Kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema, tuambie, na tutaibeba.'
\v 21 Kwa kuwa nimekwisha toa taarifa kwako leo, lakini hajusikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu au kwa chochote kuhusu ambacho alinituma mimi kwako.
\v 22 Basi sasa, utajua kwa hakika kwamba utakufa kwa upanga, njaa, na pigo katika eneo ambalo ulitamani kwenda kuishi."
\s5
\c 43
\p
\v 1 Ilitokea kwamba Yeremia alimaliza kuhubiri kwa watu wote maneno yote ya Yahwe Mungu wao kwamba Yahwe Mungu wao alimwambia kusema.
\v 2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yonathani mwana wa Karea, na watu wenye kiburi walisema kwa Yeremia, "Unasema uongo. Yahwe Mungu wetu hajakutuma wewe kusema, 'Usiende Misri kuishi huko.'
\v 3 Kwa kuwa Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu kututoa sisi kwenye mkono wa Wakaldayo, kwa kuwa wewe umesababisha kifo chetu na kutufanya sisi mateka huko Babeli."
\s5
\v 4 Basi Yonathani mwana wa Karea, wakuu wa jeshi, na watu wote walikataa kusikiliza sauti ya Yahwe kuishi kwenye nchi ya Yuda.
\v 5 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi wote waliwachukua mabaki wa Yuda ambao walikuwa wamerudi kutoka mataifa yote ambapo walikuwa wametawanyika kuishi katika nchi ya Yuda.
\v 6 Waliwachukua wanaume na wanawake, watoto na mabinti wa mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliruhusu kubaki pamoja na Gedali mwana wa Ahikam mwana wa Shafan. Pia walimchukua Yeremia nabii na Baruku mwana wa Neria.
\v 7 Walienda nchi ya Misri, kwa Tahpanhesi, kwa sababu hawakusikiliza sauti ya Yahwe.
\s5
\v 8 Basi neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema,
\v 9 "Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi.
\v 10 Kisha wakasema nao, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadreza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadreza ataweka banda lake juu yao.
\s5
\v 11 Kwa kuwa atakuja na kuvamia nchi ya Misri. Yeyote aliyeandikiwa kufa atakufa. Yeyote aliyeandikiwa mateka atachukuliwa mateka. Na yeyote aliyeandikiwa kwa upanga atakufa kwa upanga.
\v 12 Kisha nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri. Nebukadreza atawachoma na kuwashika. Atasafisha nchi ya Misri kama wachungaji wanavyosafisha wanyama waharibio nguo zao. Ataenda nje kutoka eneo hilo kwa ushindi.
\v 13 Atavunja nguzo za mawe huko Heliopolisi kwenye nchi ya Misri. Atachoma mahekalu ya miungu ya Misri."
\s5
\c 44
\p
\v 1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migdoli, Tahpanhesi, Memphis, na katika nchi ya Patrosi.
\v 2 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao.
\v 3 Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mengine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.
\s5
\v 4 Basi nirudie kuwatuma watumwa wangu wote manabii kwao. Niliwatuma wao kusema, 'Acha kufanya vitu hivi machukizo ambayo nachukia.
\v 5 Lakini hawakunisikiliza. Walikataa kuwa makini au kuyaacha maovu kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine.
\v 6 Basi hasira yangu na gadhabu yangu zilimwanga na kuwasha moto kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Basi waliharibiwa na kuteketezwa, kama katika siku ya leo."
\s5
\v 7 Basi sasa Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israel, asema hivi, "Kwanini unafanya maovu makubwa dhidi yenu? Kwanini mnasababisha ninyi wenyewe kujitenga kutoka miongoni mwa Yuda - wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao? Hakuna mabaki yenu yatabaki.
\v 8 Kwa maovu yenu mmenikosea pamoja na matendo ya mikono yenu, kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine kwenye nchi ya Misri, ambapo mmekwenda kuishi. Mmeenda huko ili kwamba mtaangamizwa, ili kwamba mtalaaniwa na mashutumu miongoni mwa mataifa yote ya duniani.
\s5
\v 9 Mmesahau maovu yaliyofanywa na mababu zenu na maouvu yaliyofanywa na wafalme wa Yuda na wake zao? Mmesahau uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu?
\v 10 Kwa siku hii, hawajanyenyekea bado. Hawashimu sheria yangu au maagizo niliyoweka mbele yao na mababu zao, wala hawatembei nazo."
\s5
\v 11 Kwa hiyo sasa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, "Ona, Nimekaribia kuweka uso wangu dhidi yenu kuleta maafa kwenu na kuiharibu Yuda yote.
\v 12 Kwa kuwa nitachukua mabaki wa Yuda ambaye ameanza safari kwenda nchi ya Misri kuishi huko. Nitafanya hivi ili kwamba wataangamia wote katika nchi ya Misri. Wataanguka kwa upanga na njaa. Kutoka wadogo kwa wakubwa wataangamia kwa upanga na njaa. Watakufa na watakuwa sababu ya kuaapa, kulaani, mashutumu, na kitu kibaya.
\s5
\v 13 Kwa kuwa nitawaadhibu watu wakazi wa nchi ya Misri kama nilivyoadhibu Yerusalem kwa upanga, njaa, na pigo.
\v 14 Hakuna mkimbizi au mwathirika wa mabaki ya Yuda ambaye wataenda kuishi huko kwenye nchi ya Misri watarudi kwenye nchi ya Yuda, hata kama wanataka kurudi na kuishi huko. Hakuna kati yao atarudi, ijapokuwa wachache ambayo watatoroka kutoka huko."
\s5
\v 15 Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia.
\v 16 Walisema, "Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahwe: Hatutakusikiliza.
\v 17 Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa Mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.
\s5
\v 18 Wakati tunajiepusha kutofanya mambo haya, si kutoa sadaka ya ubani kwa Malkia wa Mbinguni na si kumwanga kinywaji cha sadaka kwake, tulikuwa wote tunaumwa umaskini na tulikuwa tunakufa kwa upanga na njaa."
\v 19 Wanawake walisema, "Wakati tulipokuwa tunatengeneza ubani wa sadaka mbele ya Malkia wa Mbinguni na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulifanya hivi vitu pasipo waume wetu kujua."
\s5
\v 20 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote - kwa wanaume na wanawake, na watu wote waliomjibu yeye - alihubiri na kusema,
\v 21 "Je Yahwe hakukumbuka ubani ambao mliuchoma kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalem - wewe na mababu zenu, wafalme wenu na viongozi, na watu wa nchi? Kwa kuwa Yahwe anakumbuka hili kwenye akili; inakuja kwenye mawazo yake.
\s5
\v 22 Basi hawakuweza tena kuvumilia kwa sababu ya matendo yenu maovu, kwa sababu machukizo ambayo mlifanya. Basi nchi yenu imekuwa ukiwa, kutisha, na laana basi hapakuwa na mkazi tena kwa siku hii.
\v 23 Kwa sababu mlichoma ubani na kufanya dhambi dhidi ya Yahwe, na kwa sababu msingesikiliza sauti yake, sheria yake, amri zake, au maagizo ya agano lake, maafa haya dhidi yenu yemetokea kama kwa siku hii. "
\s5
\v 24 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote na wanawake wote, " Sikia neno la Yahwe, Yuda yote ambao wamo katika nchi ya Misri.
\v 25 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, Wewe na wake zako wote mmesema kwa vinywa vyenu na kubeba kwa mikono yenu kile mlichosema, " Hakika tutabeba viapo ambavyo tulifanya kumwabudu Malkia wa Mbinguni, kwanga kinywaji cha sadaka kwake." Sasa timiza viapo vyenu, vibebe."
\s5
\v 26 Basi, sikiliza neno la Yahwe, Yuda yote ambao mnaishi katika nchi ya Misri, 'Ona, Nimeapa kwa jina langu kuu-asema Yahwe. Jina langu halitaitwa kwa vinywa vya wanaume wowote wa Yuda kwenye nchi ya Misri, wewe ambaye sasa unasema, "Kama Bwana Yahwe aishivyo."
\v 27 Ona, Ninakutazama juu yako kwa ajili ya maafa na si kwa uzuri. Kila mtu wa Yuda katika nchi ya Misri ataangamia kwa upanga na njaa mpaka wote wameishia.
\v 28 Kisha waathirika wa upanga watarudi kutoka nchi ya Misri kwa nchi ya Yuda, peke idadi ndogo yao. Basi mabaki yote ya Yuda walioenda kwenye nchi ya Misri kuishi huko watajua ambao neno litakuwa kweli: yangu au yao.
\s5
\v 29 Hii itakuwa ishara kwa ajili yako - hili ni tamko la Yahwe - kwamba ninaweka dhidi yenu katika eneo hili, ili kwamba mtajua kwamba maneno yangu hakika yatawavamia pamoja na maafa.
\v 30 Yahwe asema hivi, 'Tazama, ninakaribia kumtoa Farao Hofra mfalme wa Misri kwenye mkono wa adui zake na kwenye mkono wa wale wanaotafuta kumuua. Itakuwa sawa kama wakati nilimpa Sedekia mfalme wa Yuda kwenye mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, adui wake aliyetafuta maisha yake.
\s5
\c 45
\p
\v 1 Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia - hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema,
\v 2 "Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku:
\v 3 Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu wa maumivu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.'
\s5
\v 4 Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: "Yahwe asema hivi: Ona, nilichojenga, sasa ninararua chini. Nilichopanda, sasa ninangoa. Hii ni kweli juu ya dunia.
\v 5 Lakini unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja kwa binadamu wote - hii ni tamko la Yahwe - lakini ninakupa maisha yangu kama nyara popote utakakoenda."
\s5
\c 46
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii juu ya mataifa.
\v 2 Juu ya Misri; "Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
\v 3 Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge vitani.
\v 4 Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
\s5
\v 5 Ninaona nini hapa? Wana woga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote - hili ni tamko la Yahwe -
\v 6 wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wana jikwaa kaskazini na kuanguaka kando ya mto Frati.
\s5
\v 7 Ni nani hawa wainukao kama Nile, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito?
\v 8 Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, 'nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake.
\v 9 Inukeni, farasi. Mwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
\s5
\v 10 Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahwe wa majeshi, naye atajilipizia kisasa juu ya adui zake. Upanga utararua na kujirishisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka kwa Bwana Yahwe wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
\s5
\v 11 Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliyebikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
\v 12 Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na maombolezo yako, maana askari anajikwaa juu ya askari; na wote wawili uanguka pamoja."
\s5
\v 13 Hili ndilo neno Yahwe alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
\v 14 Toa taarifa kwa Misri na isikiwe katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi, wekeni kituo na mwe imara, kwa maana upanga unakula wote kati yenu.
\s5
\v 15 Kwa nini Apisi mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini.
\v 16 Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anaanguka kinyume cha anayefuata. Wanasema, "Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuuache upanga huu unaotuuwa."
\v 17 Walitangaza pale, "Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, ameuacha wasaa wake mbali."
\s5
\v 18 Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahwe wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
\v 19 Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti mwishio Misri. Kwani Memfisi haitafaa, magofu. Hakuna atakayeishi huko.
\s5
\v 20 Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
\v 21 Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake. lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakatik wa kuadhibiwa kwao.
\v 22 Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa. maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
\s5
\v 23 Wataangusha misitu - japokuwa ni mingi sana - hili ni tamko la Yahwe. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasiohesabika.
\v 24 Binti Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini."
\s5
\v 25 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, "Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Farao mfalme wake, na wote wanaomtumaini.
\v 26 Nitawaweka katika mkono wa wanaoyaona maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo - asema Yahwe."
\s5
\v 27 Lakini, wewe Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitakurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, tafuta amani, na kuwa salama, na hapatakuwa na wa kumwogofya.
\v 28 Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope - asema Yahwe - kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu."
\s5
\c 47
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabi juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.
\v 2 "Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
\s5
\v 3 Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mwungurumo wa vibandawazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
\v 4 Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
\s5
\v 5 Maombolezo yatakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni, watu waliosalia bondeni watakuwa kimya. Ni kwa muda gani mtajiondoa katika maombolezo?
\v 6 Ole, upanga wa Yahwe! itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
\v 7 Wawezaje kuwa kimya, maana Yahwe amekuagiza. Amekuamuru kumpiga Ashikeloni na dhidi ya nchi ya pwani ya bahari.
\s5
\c 48
\p
\v 1 Juu ya Moabu, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Ole kwa Nebo, kwani umekuwa ukiwa. Kiriathaimu umetekwa na kuaibishwa. Ngome zake zimeangushwa na kuaibishwa.
\v 2 Heshima ya Moabu haipo tena. Adui zake katika Heshboni walipanga njama za kumwangamiza. Walisema, 'Njoni tumwangamize kama taifa. Madmena pia itaangamizwa - upanga utakutangulia.'
\s5
\v 3 Sikilizeni! Sauti ya mvumo inakuja kutoka Horonaimu.
\v 4 Moabu ameangamizwa. Vilio vya watoto wake vinasikika.
\v 5 Wanapanda kilima cha Luhithi wakilia, njia yote kuelekea Horonaimu, vilio vinasikika kutokana na maangamizi.
\s5
\v 6 Kimbieni! okeeni maisha yenu kama kichaka cha mreteni katika nyika.
\v 7 Maana kwa sababu ya tumaini lenu katika matendo na utajiri wenu, ninyi pia mtatekwa. Kisha Kemoshi atachukuliwa matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
\s5
\v 8 Maana mwaribu atafika kila mji; hakuna mji utakaookoka. Hivyo bonde litaangamia na tambarare itateketezwa, kama alivyosema Yahwe.
\v 9 Mpeni Moabu mabawa, maana ni lazima aruke mbali bila shaka. Miji yake itakuwa magofu, pasipo na mtu wa kuishi humo.
\v 10 Na alaaniwe kila aliye mvivu katika kufanya kazi ya Yahwe! Na alaaniwe kila auzuiaye upanga wake usimwage damu!
\s5
\v 11 Moabu amekuwa akijisikia salama tangu alipokuwa kijana. Yeye ni kama mvinyo wake ambao haujamiminwa kutoka mtungi kwenda mtungi mwingine. Hajaenda matekani. Hivyo radha yake ni njema kama mwanzo; radha yake haibadiliki.
\v 12 Hivyo tazama, siku zinakuja - asema Yahwe - nitakapompelekea watakao mchovya na kumwaga mitungi yake yote na kupasua mitungi yake.
\s5
\v 13 Kisha Moabu atamwaibikia Kemoshi kama ambavyo nyumba ya Israeli ilivyoiabikia Betheli, tumaini lao.
\v 14 Utawezaje kusema, 'Tu askari, wapiganaji wenye nguvu'?
\s5
\v 15 Moabu itaangamizwa na miji yake kushambuliwa. Kwa maana vijana wake wazuri wameshuka katika eneo la machinjo. Hili ni tamko la mfalme! Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\v 16 Maangazizo ya Moabu yanakaribia; maafa yanaharakisha.
\v 17 Ninyi nyote mlio karibu na Moabu, ombolezeni. Nanyi mjuao fahari yake, pigeni kelele hivi, 'Ole, fimbo yenye nguvu, fimbo yenye heshima, imevunjwa.'
\s5
\v 18 Shukeni kutoka mahali penu pa heshima na kuketi katika nchi kavu, ewe binti uishie Diboni. Maana aiangamizaye Moabu anakushambulia, atakayeziharibu ngome zako.
\v 19 Simameni njiani na kuangalia, enyi mwishio katika Aroeri. Waulizeni wanaokimbia na kutoroka. Sema, 'Nini kimetokea?'
\v 20 Moabu ameaibika, maana amevujwa. Lieni kwa sauti na uchungu; pigeni yowe kuomba msaada. Wambieni watu waliokando ya Mto Arinoni kwamba Moabu ameangamizwa.
\s5
\v 21 Basi maangamizi yamefika katika nchi ya kilima, huko Holoni, Yakza, na Mefathi,
\v 22 huko Diboni, Nebo, na Bethi Diblathaimu,
\v 23 huko Kiriatahaimu, Beth Gamul, na Bethi Meoni,
\v 24 huko Keriothi na Bozra, na katika miji yote iliyomo katika nchi ya Moabu - miji iliyoko mbali na karibu.
\v 25 Nguvu za Moabu zimekwisha; mkono wake umevunjwa - asema Yahwe.
\s5
\v 26 Mnywesheni, maana alitenda kwa kiburi kinyume changu, Yahwe. Basi Moabu anapiga makofi kwa machukizo kwa matapiko yake mwenyewe, hivyo amekuwa pia kitu cha kuchekesha.
\v 27 Maana Israeli hakuwa kitu cha kuchekesha kwako? Alionekana miongoni mwa wezi, kwamba ulitikisa kichwa chako kwake mara ulipoongea juu yake?
\s5
\v 28 Jitengeni na miji na kuweka kambi katika minuko, enyi watu wa Moabu. Kuwa kama njiwa anayeatamia juu ya mlango wa tundu katika miamba.
\v 29 Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu - majivuno yake, maringo, kiburi, utukufu binafsi na kujiinua moyoni.
\s5
\v 30 Hili ni tamko la Yahwe - mimi mwenyewe najua maneno yake ya ukaidi, yasiyosaidia chochote, kama matendo yake.
\v 31 Hivyo nitavumisha maombolezo kwa ajili ya Moabu, na nitapiga kelele katika uzuni kwa ajili ya Moabu. Nitaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir Hereshi.
\v 32 Nitalia zaidi kwa ajili yenu kuliko nilivyofanya kwa Yazeri, mzabibu wa Sibma! Matawi yako yalipita katika Bahari ya Chumvi na kufika hata Yazeri. Mwaribu ameshambulia matunda yenu ya kiangazi na mzabibu wenu.
\s5
\v 33 Hivyo sherehe na furaha vimeondolewa kutoka miti ya matunda na nchi ya Moabu. Nimekomesha mvinyo kutoka mashinikizo yao. Hawatakanyaga kwa kelele za furaha. Kelele yoyote haitakuwa kelele ya furaha.
\s5
\v 34 Kutoka kelele huko Heshiboni hata kufika Eleale, sauti yao inasikika hata Yahazi, kutoka Soari hata Horonaimu na Eglathi Shelishiya, hata maji ya Nimrimu yamekauka.
\v 35 Maana nitamkomesha kila mtu katika Moabu atoaye sadaka mahali pa juu na kuteketeza uvumba kwa miungu yake - asema Yahwe.
\s5
\v 36 Hivyo moyo wangu unamwombolezea Moabu kama zomari. Moyo wangu unaomboleza kama zomari kwa ajili ya watu wa Kir Heresi. Utajiri walioupata umekwisha.
\v 37 Maana kila kichwa kina upaa na kila kidevu kimenyolewa. Chale zipo katika kila mkono, na nguo za magunia katika viuno vyao.
\s5
\v 38 Maombolezo yapo kila mahali, juu ya kila paa la nyumba ya Moabu na katika masoko ya Moabu. Kwa maana nimeivunja Moabu kama chungu kisichotakiwa tena - asema Yahwe.
\v 39 Jinsi gani imeharibiwa! Jinsi wanavyopiga kelele katika maombolezo yao! Moabu ameigeuza kwa aibu! Hivyo Moabu atakuwa kitu cha kuchekwa na kitisho kwa wote wanaomzunguka."
\s5
\v 40 Maana Yahwe asema hivi, "Tazama, adui atakuja akiruka kama tai, akieneza mabawa yake juu ya Moabu.
\v 41 Keriothi umetekwa, na ngome zake zimekamatwa. Maana siku hiyo myoyo ya askari wa Moabu itakuwa kama mioyo ya wanawake katika uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 42 Hivyo Moabu utaharibiwa kama watu, kwa kuwa walijivuna kinyume changu, Yahwe.
\v 43 Hofu na shimo, na mtego vinakujia, watu wa Moabu - asema Yahwe.
\v 44 Kila akimbiaye kwa sababu ya hofu ataanguka shimoni, na kila atokaye shimoni atanaswa na mtego, maana nitayaleta haya juu yao katika mwaka wa kisasi changu dhidi yao - asema Yahwe.
\s5
\v 45 Wakimbiao watasimama katika kivuli cha Heshboni bila nguvu, maana moto utatoka Heshboni, miale kutoka katikati ya Sihoni. Utateketeza paji la uso wa Moabu na juu ya vichwa vya watu wenye majivuno.
\s5
\v 46 Ole wako, Moabu! watu wa Kemoshi wameangamizwa, Kwa maana wana wako wamechukuliwa kama mateka na binti zako matekani.
\v 47 Lakini nitazirejesha siku njema za Moabu katika siku zijazo - asema Yahwe." Hukumu ya Moabu inaishia hapa.
\s5
\c 49
\p
\v 1 Juu ya watu wa Amoni, Yahwe asema hivi, "Je Israeli hana watoto? Je hakuna mtu wa kurithi chochote katika Israeli? Kwa nini Moleki aikalie Gadi, na watu wake kukaa katika miji yake?
\v 2 Hivyo angalia, siku zinakuja - asema Yahwe - nitakapo sikizisha ishara ya vita juu ya Raba miongoni mwa watu wa Amoni, hivyo itakuwa rundo lililoachwa na binti zake watawasha moto. Maana Israeli atawamiliki wanaommiliki," asema Yahwe.
\s5
\v 3 Piga kelele kwa maombolezo, Heshboni, maana Ai utaangamizwa! Piga kelele, Binti za Raba! Vaeni nguo za magunia. Ombolezeni na kukimbia kwa kuchanganyikiwa, maana Moleki anakwenda matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
\v 4 Kwa nini mnajivunia nguvu zenu? Nguvu zenu zitakwisha, binti wasioamini, ninyi mnaotumaini utajiri wenu. Mwasema, "Nani atakayekuja kinyume changu?'
\s5
\v 5 Tazama, nitaleta kitisho juu yenu - hili ni tamko la Yahwe, Bwana wa majeshi - kitisho hiki kitatoka kwao wote wanaowazunguka. Kila mmoja wenu atatawanyika mbele yake. Hakutakuwa na wa kuwakusanya wanaotawanyika.
\v 6 Lakini baada ya haya nitarejesha mema ya watu wa Amoni - hili ni tamko la Yahwe."
\s5
\v 7 Juu ya Edomu, Yahwe wa majeshi asema hivi, Je hakuna tena hekima katika Temani? Je ushauri mwema umepotea kutoka kwa wenye ufahamu? Je hekima yao imeharibika?
\v 8 Kimbieni! Rudini nyuma! Bakini katika mashimo katika ardhi, wenyeji wa Dedani. Maana naleta maafa ya Esau juu yake wakati ninaomwadhibu.
\s5
\v 9 Ikiwa wavunaji wa zabibu walikuja kwako, je wasinge acha kidogo? Ikiwa wezi walikuja usiku, je wasingeiba kiasi walichotaka?
\v 10 Lakini nimempiga Esau kwa ukiwa. Nimefunua maficho yao. Hivyo hataweza kujificha mwenyewe. Watoto wake, ndugu zake, na jirani zake wameharibiwa, wamepotea.
\v 11 Acha nyuma yatima wako. Nitachukua uhai wao, na wajane wako wanaweza kuniamini."
\s5
\v 12 Maana Yahwe asema hivi, "Tazama, wasiostahili ni lazima wanywe sehemu ya kikombe. Je mnadhani mtaachwa bila kuhadhibiwa? Hapana, maana hakika mtakunywa.
\v 13 Maana nimekwisha apa kwangu mimi mwenyewe - asema Yahwe - Hiyo Bozra itakuwa hofu, aibu, magofu, na kitu cha laana. Miji yake yote itakuwa magofu daima.
\s5
\v 14 Nimesikia habari kutoka kwa Yahwe, na mjumbe ametumwa katika mataifa, 'Kusanyikeni na kumpiga. Jiandaeni kwa vita.'
\v 15 "Maana tazama, nimekufanya kuwa mdogo kulinganisha na mataifa mengine, yenye kudharauliwa na watu.
\s5
\v 16 Na kwa hofu yenu, kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wakaaji wa maeneo ya mwinuko, ninyi mliomiliki vilele vya vilima ili mfanye viota vyenu kama tai. Nitawashusha kutoka huko - asema Yahwe.
\s5
\v 17 Edomu atakuwa kitisho kwa kila aipitaye. Kila mtu atatetemeka na kutoa sauti kwa sababu ya maafa yake.
\v 18 Kama maangamizi ya Sodoma na Gomora na jirani zake," asema Yahwe, "hakuna atakayeishi pale; hakuna mtu atakayekaa huko.
\s5
\v 19 Tazama, nitapanda kama simba kutoka katika misitu ya Yordani hata eneo la malisho mabichi. Maana nitaharakisha kumfanya Edomu kumkimbia, nami nitamweka mwingine atakayekuwa amechaguliwa kwa usimamizi huo. Maana ni nani aliyekama mimi, ni nani atakayeniagiza kuja? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
\s5
\v 20 Hivyo sikiliza mipango ambayo Yahwe ameamua dhidi ya Edom, mipango aliyoifanya kinyume cha wakaao Temani. Bila shaka wataondolewa, hata kundi dogo kuliko yote. Nchi yao yenye malisho yao mabichi itageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
\s5
\v 21 Kwa kishindo cha kuanguka kwao nchi hutikisika. Sauti ya milio ya kukata tamaa inasikika katika Bahari ya Shamu.
\v 22 Tazama, mtu fulani atapiga kama tai, na kushuka chini kwa kasi na kueneza mabawa yake juu ya Bozra. Kisha katika siku hiyo, mioyo ya askari wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika kuzaa."
\s5
\v 23 Juu ya Dameski: "Hamathi na Arpadi zitaaibika, maana wamesikia habari ya madhara. Wanayeyuka! Wamesumbuka kama bahari, isiyotulia.
\v 24 Dameski umekuwa dhaifu sana. Unageuka kukimbia; hofu imeushika, Maangaiko na maumivu yameupata, kama uchungu wa mwanamke ajifunguaye.
\v 25 Watu wake wanasema, "Umekuwaje mji maarufu, mji ambao nimeufurahia, kabla haujaachwa?
\s5
\v 26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika mitaa yake na askari wake wote watateketea siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi."
\v 27 "Maana nitawasha moto katika kuta za Dameski, nami nitazivunja ngome za Beni Hadadi."
\s5
\v 28 Juu ya Kedari na falme za Hazori, Yahwe amwambia hivi Nebukadneza (Basi Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa akienda kuyashambulia maeneo haya): "Inuka na uipige Kedari na kuwaharibu wale watu wa mashariki.
\v 29 Jeshi lake litachukua hema zao na makundi yao, nguzo za hema yao, na vitu vyao vyote. Watachukua ngamia wao kutoka kwa watu wa Kedari na kuwambia, 'Hofu ipo pande zote!"
\s5
\v 30 Kimbia, Tangatanga mbali! Kaa katika maandaki ardhini, mkaao Hazori - asema Yahwe - maana Nebukadneza mfalme wa Babeli amepanga mpango kinyume chenu. Kimbieni! Geukeni!
\v 31 Simama! lishambulie taifa lililokatika amani, waishio salama," asema Yahwe. Hawana malango wala nguzo ndani yao, na watu wake wanakaa wenyewe.
\s5
\v 32 Maana farasi wao watakuwa mateka, na wingi wa mali zao utakuwa mateka wa vita. Kisha nitawatawanya katika kila upepo wanaonyoa pembe za nywele zao, nami nitaleta madhara juu yao kutoka kila upande - hili ni tamko ya Yahwe.
\v 33 Hazori utakuwa makao ya mbwea, nchi isiyofaa daima. Hakuna atakayeishi huko; hakuna mwanadamu atakayekaa huko."
\s5
\v 34 Hili ni neno la Yahwe lililomwijia Yeremia nabii kuhusu Elamu. Ilikuwa wakati wa mwanzo wa kutawala kwake Sedekia mfalme wa Yuda, naye akasema,
\v 35 "Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, ninakaribia kumvunja mpiga upinde wa Elamu, sehemu kuu ya nguvu zao.
\v 36 Maana nitaleta pepo nne kutoka katika pande nne za mbingu, nami nitawatawanya watu wa Elamu katika pepo hizo zote. Hakuta kuwa na taifa ambalo kwalo waliotawanywa kutoka Elamu hawatakwenda.
\s5
\v 37 Hivyo nitawavunjavunja Elamu mbele ya adui zao na mbele ya watafutao uhai wao. Maana nitaleta maangamizo dhidi yao, hasira ya gadhabu yangu - hili ni tamko la Yahwe - nami nitapeleka upanga nyuma yao hata nitakapowafuta wote.
\v 38 Kisha nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme na viongozi wao kutoka huko - asema Yahwe -
\v 39 na itakuwa siku zijazo kwamba nitarejesha mema ya Elamu - asema Yahwe."
\s5
\c 50
\p
\v 1 Hili ni neno alilolisema Yahwe juu ya Babeli, nchi ya Wakalidayo, kwa mkono wa Yeremia nabii,
\v 2 "Wajulishe mataifa ili wasikie. Toa ishara ili wasikie. Usiiache. Sema, 'Babeli imetwaliwa. Beli ameaibika. Merodaki amefadhaika. Sanamu zake zimeaibishwa; vinyago vyake vimefadhaika
\s5
\v 3 Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka.
\v 4 Katika siku hizo na wakati huo - hili ni tamko ya Yahwe - watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahwe Mungu wao.
\v 5 Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahwe katika agano la milele lisilosahaulikal
\s5
\v 6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea. Wachungaji wao wamewapoteza milimani; wamewageuza kutoka mlima hata mlima. Walikwenda, wakasahau mahali walipokuwa wanaishi.
\v 7 Kila awaendeaye anawararua. Washitaki wao walisema, 'Hatuna hatia, kwa sababu walimtenda dhambi Yahwe, nyumbani kwao halisi - Yahwe, tumaini la mababu zao.'
\s5
\v 8 Tokeni kati ya Babeli; tokeni katika nchi ya Wakalidayo; iweni kama wafanyavyo mabeberu mbele ya kundi lote.
\v 9 Maana tazama, ninaelekea kupeleka na kuinua kinyume cha Babeli kundi la mataifa makubwa kutoka kaskazini. Yatajipanga yenyewe kinyume chake. Kutoka hapo Babeli utatekwa. Mishale yao ni kama shujaa mzoefu asiyerudi mikono tupu.
\v 10 Ukaldayo itakuwa mateka. Wate waitekao wataridhika - asema Yahwe.
\s5
\v 11 Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu.
\v 12 Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, nyika, nchi kame, na jangwa.
\v 13 Kwa sababu ya hasira ya Yahwe, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na atatoa sauti kwa sababu ya majeraha yake.
\s5
\v 14 Jipangeni wenyewe kumzunguka Babeli kinyume chake. Kila apindaye upinde na ampige. Msizuie mshale wenu wowote, maana amemtenda dhambi Yahwe.
\v 15 Pigeni kelele za ushindi kinyume chake ninyi nyote mmzungukao. Amesalimu mamlaka yake; minara yake imeanguka. Kuta zake zimebomolewa, maana hiki ni kisasi cha Yahwe. Jilipizeni kisasi juu yake! Mtendeeni kama alivyoyatenda mataifa mengine.
\s5
\v 16 Waaribuni wote mkulima apandaye mbegu naye atumiaye mundu wakati wa mavuno katika Babeli. Haya kila mtu na arudi kwa watu wake kutoka upanga wa mtesaji; na wakimbilie katika nchi yao wenyewe.
\s5
\v 17 Israeli ni kondoo aliyetawanywa na kupelekwa na simba mbali. Kwanza mfalme wa Ashuru alimrarua; kisha baadaye, Nebukadneza mfalme wa Babeli akavunja mifupa yake.
\v 18 Kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
\s5
\v 19 Nitamrudisha Israeli katika nchi yake; atajilisha katika Karmeli na Bashani. Kisha atajishibisha katika nchi ya kilima ya Efraimu na Gileadi.
\v 20 Siku hizo na wakati huo, asema Yahwe, uovu utatafutwa katika Israeli, lakini hautaonekana. Nitauliza kuhusu dhambi za Yuda, lakini hazitaonekana, maana nitawasamehe mabaki niliowaacha."
\s5
\v 21 Inuka dhidi ya nchi ya Merathaimu, kinyume chake nao waishio Pekodi. Wapigeni kwa makali ya upanga na mwatenge kwa ajili ya maangamizo - asema Yahwe - fanyeni kila ninachowaamru.
\v 22 Sauti ya vita na maangamizi ya kustaajabisha yamo katika nchi.
\s5
\v 23 Jinsi gani nyundo ya mataifa yote imekatiliwa mbali na kuharibiwa. Jinsi Babeli amekuwa kitu cha kushangaza kati ya mataifa.
\v 24 Nimetega mtego dhidi yako. Umenaswa, Babeli, nawe haukutambua! Ulionekana na kukamatwa, tangu uliponidhihaki, Yahwe.
\s5
\v 25 Yahwe amefungua ghala lake la silaha na anachukua silaha kwa ajili ya kutekekeleza hasira yake. Kuna kazi kwa ajili ya Yahwe wa majeshi katika nchi ya Wakaldayo.
\v 26 Mshambulie kutokea mbali. Fungua maghala yake ya chakula na kumrundika kama marundo ya nafaka. Mtenge mbali na maangamizi. Usimbakizie masalia.
\s5
\v 27 Ua madume wake wote wa ng'ombe. Washushe sehemu ya machinjio. Ole wao, maana siku yao imefika - wakati wa kuadhibiwa kwao.
\v 28 Kuna sauti ya wale wanaokimbia, walionusurika, katika nchi ya Babeli. Hawa watatoa taarifa ya kisasi cha Yahwe Mungu wetu kwa Sayuni, kisasi kwa hekalu lake."
\s5
\v 29 Ita wapiga pinde dhidi ya Babeli - wale wote wapindao pinde zao. Piga kambi kinyume chake, na msimwache yeyote kutoroka. Mlipeni kwa kile alichofanya. Mfanyieni kwa kipimo alichotumia. Maana amemdharau Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
\v 30 Hivyo vijana wake wataanguka katika viwanja vya mji, na wapiganaji wake wote wataangamizwa siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe."
\s5
\v 31 Tazama, mimi ni kunyume chako, mwenye majivuno - hili ni tamko la Bwana Yahwe wa majeshi - maana siku yako imefika, mwenye kiburi, wakati nitakapokuadhibu.
\v 32 Hivyo wenye kiburi watajikwaa na kuanguka. Hakuna atakaye wainua. Nitawasha moto katika miji yao; utateketeza kila kitu kati yake.
\s5
\v 33 Yahwe wa majeshi asema hivi: watu wa Israeli wamenyanyaswa, pamoja na watu wa Yuda. Wate waliowateka bado wanawashikilia; wanakataa kuwaacha waondoke.
\v 34 Yeye awaokoaye ni mwenye nguvu. Yahwe wa majeshi ni jina lake. Kwa hakika atalitetea shitaka lao, ili kuleta pumziko katika nchi, na kuwapiga wakaao Babeli.
\s5
\v 35 Upanga u juu ya Wakalidayo - asema Yahwe - na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake.
\v 36 Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu.
\v 37 Upanga utakuwa juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.
\s5
\v 38 Ukame unakuja juu ya maji yake, hivyo yatakauka. Maana ni nchi ya miungu wasiofaa, na wanafanya kama watu waliofanywa punguani kwa miungu yao isiyosaidia.
\v 39 Hivyo wanyama wa jangwani wakaishi na mbwea wataishi huko, na watoto wa mbuni wataishi ndani yake. Kwa muda wote, hatakaliwa tena. Kutoka kizazi hata kizazi, hatakaliwa tena na watu.
\v 40 Kama vile Mungu alivyoziangamiza Sodoma na Gomora na majirani zake - asema Yahwe - hakuna atakayeishi huko; hakuna mtu atakayekaa ndani yake."
\s5
\v 41 "Tazama, watu wanakuja kutoka kaskazini, maana taifa kubwa na wafalme wengi wamemtikisa kutokea mbali.
\v 42 Watachukua pinde na mishale. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mngurumo wa bahari, na wamepanda farasi katika mpangilio kama watu wapiganao, dhidi yako, bindi Babeli.
\v 43 Mfalme wa Babeli amesikia habari yao na mikono yake imelegea kwa huzuni. Mashaka yamemshika kama mwanamke katika utungu.
\s5
\v 44 Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
\s5
\v 45 Sikilizeni mipango ambayo Yahwe ameamua juu ya Babeli, mipango aliyonayo dhidi ya nchi ya Wakaldayo. Kwa hakika wataondolewa, hata kundi dogo zaidi. Eneo lao la malisho litageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
\v 46 Kwa sauti ya kuangushwa kwa Babeli nchi inatikisika, na sauti ya mateso yao inasikiwa kati ya mataifa."
\s5
\c 51
\p
\v 1 Yahwe asema hivi: Tazama, ninakwenda kuleta upepo wa maangamizi dhidi ya Babeli na dhidi yao waishio ndani ya Leb Kamei.
\v 2 Nitawatuma Babeli wageni. Watamtawanya na wataifanya ukiwa nchi yake, maana watakuja kinyume chake kutoka pote siku ya madhara.
\s5
\v 3 Msiwaache wapiga mishale wakapinda pinde zao; msiwache wakavaa silaha zao. Msiwahifadhi vijana wake wa kiume; litengeni jeshi lake lote kwa maangamizi.
\v 4 Maana watu waliojeruhiwa wataanguka katika nchi ya Wakaldayo; waliouawa wataanguka katika mitaa yake.
\s5
\v 5 Maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, na Yahwe wa majeshi, japokuwa nchi yao imejaa na maasi yaliyotendwa kinyume cha Mmoja aliye Mtakatifu wa Israeli.
\v 6 Kimbieni kutoka Babeli; kila mtu na ajiokoe mwenyewe. Msiangamie katika maasi yake. Maana ni wakati wa kisasi cha Yahwe. Atamlipa kwa yote.
\s5
\v 7 Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Yahwe kilichoinywesha nchi yote; mataifa walikunywa mvinyo wake wakawa wendawazimu.
\v 8 Babeli utaanguka ghafla na kuangamizwa. Mwombolezeeni! mpeni dawa kwa maumivu yake; pengine aweza kupona.
\s5
\v 9 Tulinuia kumponya Babeli, lakini hajaponywa, haya na tumwache twende, katika nchi yetu. Maana hatia yake imefika juu mbinguni; imerundikwa kufika mawinguni.
\v 10 Yahwe ametamka kwamba sisi hatuna hatia. Njooni, teseme katika Sayuni matendo ya Yahwe Mungu wetu.'
\s5
\v 11 Noweni mishale na kuchukua ngao. Yahwe anaiimiza roho ya mfalme wa Umedi katika mpango wa kuiangamiza Babeli. Hii ni kwa kisasi cha Yahwe, kisasi kwa maangamizi ya hekalu lake.
\v 12 Inueni bendela juu ya kuta za Babeli; wekeni walinzi. Wekeni waangalizi; wekeni askari waviziao ili kumkamata kila akimbiliaye mjini, maana Yahwe atafanya kile alichokipanga. Atafanya alichokisema juu ya wakaao Babeli.
\s5
\v 13 Enyi mwishio kati ya chemchemi nyingi za maji, ninyi mlio na wingi wa hazina, mwisho wenu umefika. upindo wa maisha yenu umepunguzwa.
\v 14 Yahwe wa majeshi ameapa kwa maisha yake, 'nitakujaza na adui zako, kama pigo la nzige; watainua kelele za vita juu yako.'
\s5
\v 15 Ameifanya dunia kwa nguvu zake; akaiweka dunia mahali kwa hekima yake. Kwa ufahamu wake alizitanda mbingu.
\v 16 Anapovuma, kunakuwa na mvumo wa maji mbinguni, maana huleta umande kutoka miisho ya dunia. Hufanya radi kwa ajili ya mvua na kuituma na kuutuma upepo kutoka katika maghala ya nyumba zake.
\s5
\v 17 Kila mtu anakuwa kama mnyama asiye na akili; kila mfua chuma ameaibishwa na sanamu zake. Maana mwonekano wake unadanganya; maana hakuna uzima ndani yake.
\v 18 Hazifai, kazi ya wafanya mzaa; wataangamizwa wakati wa kuadhibiwa kwao.
\v 19 Lakini Mungu, urithi wa Yakobo, siyo kama hawa, maana yeye ndiye afanyaye vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; Yahwe wa majeshi ni jina lake.
\s5
\v 20 Wewe ni nyundo ya vita yao, silaha ya vita yangu. Kwa wewe nitawaponda mataifa na kuharibu falme.
\v 21 Kwa wewe nitaponda farasi na wawapandao; kwa wewe nitaponda vibandawazi na madereva wake.
\s5
\v 22 Kwa wewe nitawafutilia mbali mme na mke; kwa wewe nitafutilia mbali mzee na kijana. Kwa wewe nitafutilia mbali kijana wa kiume na wasichana bikra.
\v 23 Kwa wewe nitafutilia mbali wachungaji na makundi yao; kwa wewe nitawafutilia mbali wakulima na jozi zao za kulimia. kwa wewe nitawafutilia mbali watawala na maafsa.
\s5
\v 24 Maana mbele yako nitamlipa Babeli na wote wakaao Ukaldayo kwa maovu yote waliyoyafanya huko Sayuni - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 25 Tazama, mimi ni kinyume chako, ewe mlima, wewe unayewaharibu watu wengine - hili ni tamko la Yahwe - kuiharibu dunia yote. Nitakupiga na mikono yangu na kuvingirisha chini kutoka ukingo wa kilima. Kisha nitakufanya mlima ulioteketezwa kabisa kwa moto.
\v 26 Hivyo hawatachukua kwako jiwe lolote ili kujengea pembe ya nyumba au msingi; kwani utakuwa ukiwa wa milele - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 27 Inua bendela ya vita juu ya nchi. Piga tarumbeta katika mataifa. Yaite mataifa yamshambuliye: Ararati, Mini na Ashkenazi. Teua majemedari wa kumshambulia; leta farasi kama nzige warukao.
\v 28 Waandae mataifa kumshambulia: wafalme wa Umedi na magavana wao, maafsa wake wote na nchi yake yete.
\s5
\v 29 Maana nchi itatikisika na kudhoofika, kwa kuwa mipango ya Yahwe inaendelea juu ya Babeli, kuifanya nchi ya Babeli kuwa nchi isiyofaa mahali pasipo na mtu.
\s5
\v 30 Maaskari wameacha kupigana huko Babeli; wamekaa katika ngome zao. Nguvu zao zimeshindwa; wamekuwa wanawake - nyumba zake zipo motoni, makomeo ya malango yake yamevunjika.
\v 31 Mjumbe hukimbia ili amwambie mjumbe mwingine, na mtoa habari humwambia mtoa habari mwingine ili amwambie mfalme wa Babeli kwamba mji wake umetwaliwa kutoka mwisho hata mwisho.
\v 32 Hivyo vivuko katika mito vimekamatwa; adui anaunguza mafunjo ya bwawa, na wapiganaji wa Babeli wamechanganyikiwa.
\s5
\v 33 Maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria. Ni muda wa kumkanyaga. Ni kitambo kidogo wakati wa mavuno utakuja juu yake.
\s5
\v 34 Yerusalemu husema, 'Nebukadneza mfalme wa Babeli amenirarua. Amenikausha na amenifanya kuwa mtungi mtupu. Amenimeza kama joka. Alijishibisha kwa chakula changu chema. Amenitupa mbali.'
\v 35 Wenyeji wa Sayuni watasema, 'Gasia nilizofanyiwa na mwili wangu na ziwe kwa Babeli.' Yerusalem atasema, Damu yangu na iwe juu ya wakaao Ukaldayo.'
\s5
\v 36 Kwa hiyo Yahwe asema hivi: Tazama, nikotayari kulitetea shitaka lako na kuleta kisasi kwa ajili yako. Maana nitayakausha maji ya Babeli na kufanya vyanzo vyake kukauka.
\v 37 Babeli utakuwa rundo la magofu, pango la mbwea, sehemu itishayo, kitu cha kutoa sauti ya nyoka, pasipo na watu.
\s5
\v 38 Wababeli wataunguruma kwa pamoja kama wanasimba. Watanguruma kama watoto wa simba.
\v 39 wanapopashwa moto kwa hasira, nitawafanyia sherehe; nitawalewesha hata wafurahi, na kisha kulala usingizi usio na mwisho hata wasiamke - hili ni tamko la Yahwe -
\v 40 nitawapeleka chini kama wanakondoo kwa mchinjaji, kama kondoo dume pamoja na mbuzi majike.
\s5
\v 41 Jinsi Babeli ulivyotekwa! Hivyo fahari ya dunia yote imekamatwa. Jinsi Babeli ulivyofanyika sehemu yenye magofu kati ya mataifa.
\v 42 Bahari imekuja juu ya Babeli! Amefunikwa na mawimbi yavumayo.
\s5
\v 43 Miji yake imekuwa ukiwa, sehemu kame na nyika, nchi isiyo na watu, na hakuna mtu apitaye hapo.
\v 44 Hivyo nitamwadhibu Beli huko Babeli; nitakitoa kinywani mwake alichokimeza, na mataifa hawatamminikia tena pamoja na wazao wao. Kuta za Babeli zitaanguka.
\s5
\v 45 Tokeni kati yake, enyi watu wangu. Kila mmoja wenu aokowe maisha yake kutoka katika hasira ya gadhabu yangu.
\v 46 Msiache mioyo yenu ikaogopa au kuhofu habari iliyosikiwa nchini, maana habari itakuja siku moja. Baada yake mwaka unaofuata kutakuwa na habari, na ghasia zitakuwa nchini. Mtawala atakuwa kinyume cha mtawala.
\s5
\v 47 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja nitakapoadhibu sanamu za Babeli. Nchi yake yote itaaibika, na wote waliochinjwa wataanguka ndani yake.
\v 48 Kisha mbingu na nchi, na vyote vilivyomo ndani yake vitafurahi juu ya Babeli. Maana mwalibifu atamwijia kutoka kaskazini - hili ni tamko la Yahwe.
\v 49 "Kama Babeli alivyowafanya waliouawa wa Israeli kuanguka, hivyo waliouawa katika nchi yake wataanguka katika Babeli.
\s5
\v 50 Ondokeni!, manusura wa vita, Msikawiye. Mkumbukeni Yahwe tokea mbali; Yerusalemu na ikumbukwe.
\v 51 Tumeaibika, maana tumesikia matusi; dhihaka imefunika nyuso zetu, maana wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 52 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - nitakapoziadhibu sanamu zake, na waliojeruhiwa watanung'unika kwa maumivu katika nchi yake yote.
\v 53 Maana hata kama Babeli angepanda mbinguni au kujenga ngome zake ndefu, aharibuye kutoka kwangu angemwendea - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 54 Kelele ya maangamizi ilitoka Babeli, anguko kubwa kutoka nchi ya Wakaldayo.
\v 55 Maana Yahwe anaiharibu Babeli. Anaifanya kelele ya sauti yake kuisha. Adui zake wanaunguruma kama mawimbi ya maji mengi; kelele yao imekuwa na nguvu.
\v 56 Maana aharibuye amekuja kinyume chake - kinyume cha Babeli! - na shujaa wake wametekwa. Pinde zao zimevunjwa, maana Yahwe ni Mungu wa kisasi; atatekeleza kisasi hiki.
\s5
\v 57 Maana nitawafanya wana wafalme wake, wenye hekima wake, maofsa wake, na maaskari wake kulewa, nao watalala usingizi kwa usingizi usioisha na bila kuamka - hili ni tamko la mfalme: Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\v 58 Yahwe wa majeshi asema hivi: Ukuta mnene wa Babeli utaangushwa kabisa, na malango marefu yataunguzwa. Kisha watu wanaokuja kumsaidia watafanya kazi isiyofaa; kila mataifa wanachojaribu kikifanya kwa ajili yake kitateketezwa kwa moto."
\s5
\v 59 Hili ndilo neno Yeremia nabii alilomwamru Seraya mwana wa Neria mwana wa Makseya alipokwenda na Sedekia mfalme wa Yuda huko Babeli katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. Basi Seraya alikuwa afsa mwandamizi.
\v 60 Maana Yeremia alikuwa ameandika katika gombo kuhusu madhara yote yeliyokuwa yakienda kutendeka juu ya Babeli - maneno haya yote yaliyokuwa yameandikwa juu ya Babeli
\s5
\v 61 Yeremia akamwambia Seraya, "Unapokwenda Babeli, hakikisha unayasoma maneno haya yote.
\v 62 Nawe utasema, 'Yahwe, wewe! - wewe mwenyewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa. Hapatakuwa na wa kukaa, kwamba ni watu au wanyama. Patakuwa nchi isiyofaa daima.'
\s5
\v 63 Kisha mtakapomaliza kusoma gombo hili, funga jiwe kubwa juu yake na ulitupe katikati ya Frati.
\v 64 Sema, 'Babeli utazama kama hivi. Hautainuka kwa sababu ya mabaya ninayoyapeleka juu yake, nao wataanguka." Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.
\s5
\c 52
\p
\v 1 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna.
\v 2 Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu.
\v 3 Kwa hasira ya Yahwe, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
\s5
\v 4 Ikawa katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedeki, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem. Wakapiga kambi kuukabili, nao wakajenga ukuta wa kuusuria kuuzunguka.
\v 5 Hivyo mji ukausuriwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa mfalme Sedekia.
\s5
\v 6 Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.
\v 7 Kisha mji ukatobolewa, na wapiganaji wote wakakimbia nje ya mji wakati wa usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili, kwa bustani ya mfalme, japokuwa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Hivyo wakaenda kwa njia ya Araba.
\v 8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata Sedekia katika tambarare za bonde la Mto Yordani karibu na Yeriko. Jeshi lote lilikuwa limetawanyika mbali naye.
\s5
\v 9 Wakamkamata mfalme na kumleta hadi kwa mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, alipotoa hukumu juu yake.
\v 10 Mfalme wa Babeli akawachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na huko Ribla akawachinja viongozi wote wa Yuda.
\v 11 Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.
\s5
\v 12 Basi mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani akaja Yerusalemu. Alikuwa jemedari wa walinzi wa mfalme na mtumishi wa mfalme wa Babeli.
\v 13 Akaiteketeza nyumba ya Yahwe, kasiri, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo mhimu mjini alilichoma.
\v 14 Kama kwa kuta za kuuzunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli lililokuwa pamoja na jemedari wa mlinzi wakaviaribu.
\s5
\v 15 Kama kwa watu maskini sana, watu waliosalia walioachwa katika mji, waliokuwa wamemwendea mfalme wa Babeli, na baadhi ya watu wenye ujuzi - Nebuzaradan, jemedari wa askari walinzi, akawachukua baadhi yao uhamishoni.
\v 16 Lakini Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawaacha baadhi ya maskini sana wa nchi kuitunza mizabibu na mashamba.
\s5
\v 17 Lakini kwa nguzo za shaba lilizokuwa katika nyumba ya Yahwe, mishikio na bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakaivunja vipande wakaondoka navyo kurudi Babeli.
\v 18 Vyungu, makoleo, kinara cha taa, mabakuri, na vitu vyote vya shaba ambavyo makuhani walikuwa wakivitumia hekaluni - Wakaldayo wakavichukua vyote.
\v 19 Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.
\s5
\v 20 Nguzo mbili, bahari, na ng'ombe kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, vitu Selemani alivyokuwa amevifanya kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vikiwa na shaba nyingi sana isiyoweza kupimwa.
\v 21 Nguzo zilikuwa na urefu wa dhiraha kumi na nane kila moja, na mstari kuzunguka kila moja wenye urefu wa dhiraha kumi na mbili. Kila moja ilikuwa na unene wa vidole vinne na tundu.
\s5
\v 22 Kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Kichwa kilikuwa dhiraha tano urefu wake, kazi ya waya zinazokingamana na makomamanga kukizunguka. Chote kilitengenezwa kwa shaba. Na nguzo nyingine ilikuwa na makomamanga yake vilikuwa kama ya kwanza.
\v 23 Hivyo kulikuwa na makomamanga tisini na sita ubavuni mwa kila kichwa, na makomamanga mia moja juu ya nyaya zilizokingamana kukizunguka.
\s5
\v 24 Jemedari wa mlinzi akamchukua Seraya mfungwa, kuhani mkuu, pamoja na Sefania, kuhani wa pili, na wale mabawaba watatu.
\v 25 Kutoka mjini akamchukua mfungwa afsa aliyekuwa juu ya askari, na watu saba wa wale waliomshauri mfalme, waliokuwa wamesalia mjini. Akamchukua mfungwa afsa wa jeshi la mfalme aliyekuwa na wajibu wa kuwaingiza watu katika jeshi, pamoja na watu mashuhuri sitini kutoka katika nchi waliokuwamo mjini.
\s5
\v 26 Kisha Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawachukuwa na kuwaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.
\v 27 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaondoka katika nchi yake na kwenda uhamishoni.
\s5
\v 28 Hawa walikuwa watu Nebukadneza aliwaamisha: katika mwaka wa saba, Wayudea 3, 023.
\v 29 Katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza alichukuwa 832 kutoka Yerusalemu.
\v 30 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, jemedari wa walinzi wa mfalme, aliwahamisha Wayudea 745. Jumla ya watu walioamishwa walikuwa 4, 600.
\s5
\v 31 Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.
\s5
\v 32 Akaongea naye kwa upole na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.
\v 33 Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.
\v 34 Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.