sw_ulb_rev/20-PRO.usfm

1867 lines
84 KiB
Plaintext

\id PRO
\ide UTF-8
\h Mithali
\toc1 Mithali
\toc2 Mithali
\toc3 pro
\mt Mithali
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
\v 2 Mithali hizi zinafundisha hekima na maarifa, kufundisha maneno ya busara,
\v 3 ili mpate maarifa kwa ajili ya kuishi kwa kutenda wema, haki na adili.
\s5
\v 4 Mithali hizi zinatoa hekima kwa wale ambao hawakufunzwa, na kuwapa vijana maarifa na hadhari.
\v 5 Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao na watu wenye ufahamu wapate mwongozo,
\v 6 kwa kuelewa mithali, misemo, vitendawili na maneno ya wenye busara.
\s5
\v 7 Hofu ya Yehova ni chanzo cha maarifa- wapumbavu hudharau hekima na nidhamu.
\v 8 Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;
\v 9 zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako.
\s5
\v 10 Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi katika dhambi zao, kataa kuwafuata.
\v 11 Kama watasema, " haya tufuatae, tuvizie ili kufanya mauaji, tujifiche ili tuwashambulie watu wasio na hatia, pasipo sababu.
\s5
\v 12 Haya tuwameza wakiwa hai, kama kuzimu inavyowachukua wenye afya, na kuwa kama wale waangukao kwenye shimoni.
\v 13 Tutapata vitu vyote vya thamani; tutazijaza nyumba zetu vile tunavyoiba kwa wengine.
\v 14 Weka vitu vyako kwetu; tutakuwa na mfuko moja kwa pamoja."
\s5
\v 15 Mwanangu, usitembee katika njia moja pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa katika mapito yao;
\v 16 miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu.
\v 17 Kwa kuwa haina maana kumtegea ndege mtego wakati ndege anaona.
\s5
\v 18 Watu hawa huvizia kujiua wenyewe--wanatega mtego kwa ajili yao wenyewe.
\v 19 Ndivyo zilivyo njia za kila ambaye hupata utajiri kwa udhalimu; mapato ya udhalimu huondoa uhai wa wenye utajiri.
\s5
\v 20 Hekima inalia kwa sauti mtaani, inapaza sauti katika viwanja;
\v 21 katika mitaa inalia kwa sauti kuu, kwenye maingilio ya milango ya mji inasema "
\v 22 Mpaka lini enyi wajinga mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini enyi wenye dhihaka mtapenda dhihaka, na hadi lini enyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
\s5
\v 23 Zingatia karipio langu; nitatoa mawazo yangu kwa ajili yenu; nitawafahamisha maneno yangu.
\v 24 Nimeita, nanyi mkakataa kusikiliza; nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyezingatia.
\v 25 Lakini mumedharau mafundisho yangu yote na wala hamkuzingatia maelekezo yangu.
\s5
\v 26 Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu-
\v 27 hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata.
\s5
\v 28 Halafu wataniita, nami sitawajibu; wataniita katika hali ya kukata tamaa lakini hawataniona.
\v 29 Kwa sababu wamechukia maarifa na hawakuchagua kuwa na hofu ya Yehova,
\v 30 hawakufuata mafundisho yangu na wakayadharau masahihisho yangu yote.
\s5
\v 31 Watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa kwa matunda ya hila zao wenyewe.
\v 32 kwa maana wajinga hufa wanaporudi nyuma, na kutojali kwa wapumbavu kutawaangamiza.
\v 33 Bali kila anisikilizaye ataishi kwa usalama na atapumzika salama pasipo hofu ya maafa.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Mwanangu, kama ukiyapokea maneno yangu na kuzitunza amri zangu,
\v 2 usikilize hekima na utaelekeza moyo wako katika ufahamu.
\s5
\v 3 kama utalilia ufahamu na kupaza sauti yako kwa ajili ya ufahamu,
\v 4 kama utautafuta kama fedha na kupekua ufahamu kama unatafuta hazina iliyojificha,
\v 5 ndipo utakapofahamu hofu ya Yehova na utapata maarifa ya Mungu.
\s5
\v 6 Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu.
\v 7 Yeye huhifadhi sauti ya hekima kwa wale wampendezao, yeye ni ngao kwa wale waendao katika uadilifu,
\v 8 huongoza katika njia za haki na atalinda njia ya waaminifu kwake.
\s5
\v 9 Ndipo utakapoelewa wema, haki, usawa na kila njia njema.
\v 10 Maana hekima itaingia moyoni mwako na maarifa yataipendeza nafsi yako.
\s5
\v 11 Busara itakulinda, ufahamu utakuongoza.
\v 12 Vitakuokoa kutoka katika njia ya uovu, kutoka kwa wale waongeao mambo potovu.
\v 13 Ambao huziacha njia za wema na kutembea katika njia za giza.
\s5
\v 14 Hufurahia wanapotenda maovu na hupendezwa katika upotovu.
\v 15 Hufuata njia za udanganyifu na kwa kutumia ghilba huficha mapito yao.
\s5
\v 16 Busara na hekima zitakuokoa kutoka kwa mwanamke malaya, kutoka kwa mwanamke anayetafuta visa na mwenye maneno ya kubembeleza.
\v 17 Yeye humwacha mwenzi wa ujana wake na kusahau agano la Mungu wake.
\s5
\v 18 Maana nyumba yake huinama na kufa na mapito yake yatakupeleka kwa wale walioko kaburini.
\v 19 Wote waiendeao njia yake hawatarudi tena na wala hawataziona njia za uzima.
\s5
\v 20 kwa hiyo utatembea katika njia ya watu wema na kufuata njia za wale watendao mema.
\v 21 Kwa wale watendao mema watafanya makazi yao katika nchi, na wale wenye uadilifu watadumu katika nchi.
\v 22 Lakini waovu wataondolewa katika nchi na wale wasioamini wataondolewa katika nchi.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Mwanangu, usizisahau amri zangu na uyatunze mafundisho yangu katika moyo wako,
\v 2 maana ziatakuongezea siku zako na miaka ya maisha yako na amani.
\s5
\v 3 Usiache utiifu wa agano na uaminifu viondoke kwako, vifunge katika shingo yako, viandike katika vibao vya moyo wako.
\v 4 Ndipo utapata kibali na heshima mbele Mungu na wanadamu.
\s5
\v 5 Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe,
\v 6 katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako.
\s5
\v 7 Usiwe mwenye busara machoni pako mwenyewe; mche Yehova na jiepushe na uovu.
\v 8 Itakuponya mwili wako na kukuburudisha mwili wako.
\s5
\v 9 Mheshimu Yehova kwa utajiri wako na kwa malimbuko ya mazao kwa kila unachozalisha,
\v 10 na ndipo ghala zako zitajaa na mapipa makubwa yatafurika kwa divai mpya.
\s5
\v 11 Mwanangu, usidharau kuadibishwa na Yohova na wala usichukie karipio lake,
\v 12 maana Yehova huwaadibisha wale wapendao, kama baba anavyoshughulika kwa mtoto wake ampendezaye.
\s5
\v 13 Yeye apataye hekima anafuraha, naye hupata ufahamu.
\v 14 Kwani katika hekima unapata manufaa kuliko ukibadilisha kwa fedha na faida yake inafaa zaidi kuliko dhahabu.
\s5
\v 15 Hekima inathamani zaidi kuliko kito, na hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na hekima.
\v 16 Yeye anasiku nyingi katika mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto ni utajiri na heshima.
\s5
\v 17 Njia zake ni njia za ukarimu na mapito yake ni amani.
\v 18 Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomshikilia, wale wanaomshikilia wanafuraha.
\s5
\v 19 Kwa hekima Yehova aliweka msingi wa dunia, kwa ufahamu aliziimarisha mbingu.
\v 20 Kwa maarifa yake vina vilipasuka na mawingu kudondosha umande wake.
\s5
\v 21 Mwanangu, zingatia hukumu ya kweli na ufahamu, na wala usiache kuvitazama.
\v 22 Vitakuwa uzima wa nafsi yako na urembo wa hisani wa kuvaa shingoni mwako.
\s5
\v 23 Ndipo utatembea katika njia yako kwa usalama na mguu wako hautajikwaa;
\v 24 ulalapo hutaogopa; utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu.
\s5
\v 25 Usitishwe na hofu ya ghafula au uharibifu uliosababishwa na waovu unapotokea,
\v 26 kwa maana Yehova utakuwa upande wako na ataulinda mguu wako usinaswe kwenye mtego.
\s5
\v 27 Usizuie mema kwa wale wanaoyastahili, wakati utendaji upo ndani ya mamlaka yako.
\v 28 Jirani yako usimwambie, "Nenda, na uje tena, na kesho nitakupa," wakati pesa unazo.
\s5
\v 29 Usiweke mpango wa kumdhuru jirani yako- anayeishi jirani nawe na yeye anakuamini.
\v 30 Usishindane na mtu pasipo sababu, ikiwa hajafanya chochote kukudhuru.
\s5
\v 31 Usimhusudu mtu jeuri au kuchagua njia zake zozote.
\v 32 Maana mtu mjanja ni chukizo kwa Yehova, bali humleta mtu mwaminifu kwenye tumaini lake.
\s5
\v 33 Laana ya Yehova ipo katika nyumba ya watu waovu, bali huibariki maskani ya watu wenye haki.
\v 34 Yeye huwadhihaki wenye dhihaka, bali huwapa hisani watu wanyenyekevu.
\s5
\v 35 Watu wenye busara huirithi heshima, bali wapumbavu huinuliwa kwa fedheha yao wenyewe.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Wanangu, sikilizeni, fundisho la baba, na zingatieni ili mjue maana ya ufahamu.
\v 2 Mimi ninawapa mafundisho mazuri; msiyaache mafundisho yangu.
\s5
\v 3 Mimi nilikuwa mwana kwa baba yangu, mpole na mtoto pekee kwa mama yangu,
\v 4 baba alinifundisha akiniambia, "Moyo wako uzingatie sana maneno yangu; shika amri zangu nawe uishi.
\s5
\v 5 Jipatie hekima na ufahamu; usisahau na kuyakataa maneno ya kinywa changu;
\v 6 usiiache hekima nayo itakulinda; ipenda nayo itakuhifadhi salama.
\s5
\v 7 Hekima ni kitu cha muhimu sana, hivyo jipatie hekima na tumia namna zote kuweza kupata ufahamu.
\v 8 Tunza hekima nayo itakutukuza; ikumbatie nayo itakuheshimu.
\v 9 Hekima itaweka kilemba cha heshima juu ya kichwa chako; itakupa taji zuri.
\s5
\v 10 Mwanangu, sikiliza, na kuzingatia maneno yangu, nawe utapata miaka mingi ya maisha yako.
\v 11 Ninakuelekeza katika njia ya hekima, nimekuongoza katika mapito yaliyonyooka.
\v 12 Unapotembea, hakuna atakayesimama katika njia yako na kama ukikimbia hutajikwaa.
\s5
\v 13 Shika mwongozo wala usiuache, utakuongoza, maana ni uzima wako.
\v 14 Usifuate njia ya waovu wala usiende katika njia ya watendao uovu.
\v 15 Jiepushe nayo, usipite katika njia hiyo; geuka na upite njia nyingine.
\s5
\v 16 Maana hawawezi kulala mpaka wafanye ubaya na hupotewa na usingizi hadi wasababishe mtu kujikwaa.
\v 17 Maana wao hula mkate wa uovu na hunywa divai ya vurugu.
\s5
\v 18 Bali njia ya mwenye kutenda haki ni kama mwanga ung'aao, huangaza zaidi na zaidi hadi mchana inapowasili kwa ukamilifu.
\v 19 Njia ya waovu ni kama giza - hawajui ni kitu gani huwa wanajikwaa juu yake.
\s5
\v 20 Mwanangu, zingatia maneno yangu; sikiliza kauli zangu.
\v 21 Usiziache zikaondoka machoni pako; uzitunze katika moyo wako.
\s5
\v 22 Maana maneno yangu ni uzima kwa wenye kuyapata na afya katika mwili wao.
\v 23 Ulinde salama moyo wako na uukinge kwa bidii zote; kwa kuwa katika moyo hububujika chemichemi za uzima.
\s5
\v 24 Jiepushe na kauli za udanganyifu na ujiepushe na mazungumzo ya ufisadi.
\v 25 Macho yako yatazame mbele kwa unyoofu na kwa uthabiti tazama mbele sawasawa.
\s5
\v 26 Usawazishe pito la mguu wako; na njia zako zote zitakuwa salama.
\v 27 Usigeuke upande wa kulia au kushoto; ondoa mguu wako mbali na uovu.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Mwanangu, zingatia hekima yangu; sikiliza kwa makini ufahamu wangu,
\v 2 ili ujifunze busara na midomo yako iweze kuhifadhi maarifa.
\s5
\v 3 Maana midomo ya malaya hutiririsha asali na kinywa chake ni laini kuliko mafuta,
\v 4 lakini mwishoni anakuwa mchungu kama mnyoo, hukata kama upunga mkali.
\s5
\v 5 Miguu yake huelekea mauti; hatua zake huelekea njia yote ya kuzimu.
\v 6 Hafikirii njia ya uzima. Hatua za miguu yake hupotea, maana hajui anakwenda wapi.
\s5
\v 7 Sasa, wanangu, nisikilizeni; wala msiache kusikiliza maneno ya kinywa changu.
\v 8 Lindeni njia yenu mbali naye wala msiende karibu na mlango wa nyumba yake.
\s5
\v 9 Kwa njia hiyo hamtawapa wengine heshima yenu au miaka ya uzima wenu kwa mtu mkatiri;
\v 10 wageni usije kufanya karamu kwa utajiri wenu; kazi mliyoifanya haitaenda katika nyumba ya wageni.
\s5
\v 11 Mwishoni mwa maisha yenu mtajuta ambapo nyama na mwili wenu vitaangamia.
\v 12 Nanyi mtasema, " Namna gani nilichukia fundisho na moyo wangu ulidharau sahihisho!
\s5
\v 13 Sikuweza kuwatii walimu wangu au kuwasikiliza walionielekeza.
\v 14 Nilikuwa nimeharibika kabisa katikati ya kusanyiko, miongoni mwa makutano ya watu."
\s5
\v 15 Munywe maji kutoka kwenye birika lenu mwenyewe na munywe maji yanatiririka kutoka kwenye kisima chenu.
\v 16 Je inapaswa chemichemi yenu ifurike popote na mifereji yenu ya maji itiririke katika njia kuu?
\v 17 Yawe yenu wenyewe peke yenu wala si kwa wageni.
\s5
\v 18 Chemichemi yako ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
\v 19 Maana ni ayala apendezaye na kulungu mwenye uzuri. Matiti yake na yakujaze furaha muda wote; daima na utekwe na upendo wake.
\s5
\v 20 Mwanangu, kwa nini uwe mateka wa malaya, kwa nini uyakumbatie matiti ya mwanamke mgeni?
\v 21 Yehova huona kila kitu afanyacho mtu na huangalia mapito yake yote.
\s5
\v 22 Mtu mwovu atatekwa na makosa yake mwenyewe; kamba za dhambi yake zitamnasa kwa nguvu.
\v 23 Atakufa kwa kukosa maonyo; atapotelea mbali kwa upumbavu wake wingi.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Mwanangu, kama utaweka pesa zako kuwa dhamana kwa mkopo wa jirani yako; kama ukitoa ahadi yako katika mkopo wa mtu usiyemjua,
\v 2 basi umejiwekea mtego mwenyewe na umenaswa kwa maneno ya kinywa chako.
\s5
\v 3 Mwanagu, ukinaswa kwa maneno yako mwenyewe, fanya haya ili kujiokoa, kwa kuwa umeangukia kwenye mikono ya jirani yako; nenda unyenyekee na ufanye shauri mbele ya jirani yako.
\s5
\v 4 Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia.
\v 5 Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.
\s5
\v 6 Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara.
\v 7 Hana akida, afisa au mtawala,
\v 8 lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
\s5
\v 9 Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?"
\v 10 Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo" -
\v 11 ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
\s5
\v 12 Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
\v 13 akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
\s5
\v 14 Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
\v 15 Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
\s5
\v 16 Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
\s5
\v 17 Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
\v 18 moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,
\v 19 shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
\s5
\v 20 Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
\v 21 Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
\s5
\v 22 utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
\v 23 Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
\s5
\v 24 Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
\v 25 Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.
\s5
\v 26 Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote.
\v 27 Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake?
\s5
\v 28 Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake?
\v 29 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu.
\s5
\v 30 Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa.
\v 31 Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake.
\s5
\v 32 Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe.
\v 33 Anasitahili aibu na majeraha na fedheha yake haiwezi kuondolewa.
\s5
\v 34 Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake.
\v 35 Ujapompa zawadi nyingi, hatakubali mbadala wa kusuruhishwa wala kulipwa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.
\v 2 Uzilinde amri zangu ili uishi na uyatunzetu mafundisho yangu kama mboni ya jicho.
\v 3 Uyafunge katika vidole vyako; uyaandike katika kibao cha moyo wako.
\s5
\v 4 Mwambie hekima, "wewe ni dada yangu," na ufahamu mwite jamaa yako,
\v 5 ili ujitunze mwenyewe dhidi ya mwanake haramu, dhidi ya mwanamke mgeni mwenye maneno laini.
\s5
\v 6 Nilikuwa naangalia kwenye wavu wa dirisha la nyumba yangu.
\v 7 Nikawatazama watu mwenye ukosefu wa uzoefu, na miongoni mwa watu vijana nikamwona kijana asiye na akili.
\s5
\v 8 Kijana huyo alishuka mtaani kwenye kona karibu na yule mwanamke, akaenda kwenye nyumba yake.
\v 9 Ilikuwa katika utusiutusi wa siku muda wa jioni, wakati wa usiku na giza.
\s5
\v 10 Akakutana na yule mwanake, amevaa kama kahaba, katika moyo wa udanyanyifu.
\v 11 Alikuwa na kelele na upotovu; miguu yake haikutulia kwenye masikani.
\v 12 Alielekea mitaani, kisha sehemu ya sokoni, na katika kila upande alisubiri kwa kuviza.
\s5
\v 13 Basi akamshika na kumbusu, kwa uso wa nguvu akamwambia,
\v 14 leo nimetoa sadaka yangu ya amani, nimelipa nadhili yangu,
\v 15 hivyo nilikuja kukutana nawe, kuutafuta uso wako kwa hamu, na sasa nimekupata.
\s5
\v 16 Nimeweka matandiko juu ya kitanda changu, kitani za rangi kutoka Misri.
\v 17 Kitanda changu nimenyunyizia manemane, udi na mdalasini.
\v 18 Njoo, tunywe tujishibishe kwa upendo wetu hata asubuhi; tupate furaha kuu kwa matendo ya mahaba.
\s5
\v 19 Maana mume wangu hayupo nyumbani kwake; amekwenda safari ya mbali.
\v 20 Alichukua mkoba wa fedha; atarudi siku ya mwezi mpevu.
\v 21 katika maneno yake mengi akamshinda; na kwa midomo yake laini anampotosha.
\s5
\v 22 Ghafula alimfuata kama maksai anayekwenda kwa mchinjaji, kama ayala aliyekamatwa kwa nguvu,
\v 23 mpaka mshale upasue ini lake. Alikuwa kama ndege anayekimbili kwenye mtego. Hakujua kuwa itamgharimu maisha yake.
\s5
\v 24 Na sasa, wanangu, nisikilizeni; zingatieni maneno ya kinywa changu.
\v 25 Moyo wako usiyageukie mapito yake; usipotoshwe katika mapito yake.
\s5
\v 26 Amesababisha watu wengi kuanguka kwa kuwajeruhi; ameua watu wengi.
\v 27 Nyumba yake ipo juu ya barabara ya kwenda kuzimu; huelekea chini kwenye vyumba vya mauti.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Je hekima haiti? Je ufahamu hapazi sauti yake?
\v 2 Juu ya kilima kando ya barabara, kwenye njia panda, hekima anasimama.
\v 3 Kando ya njia ya kuingilia mjini, karibu na milango ya mji, anaita kwa sauti.
\s5
\v 4 Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu.
\v 5 Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu.
\s5
\v 6 Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki.
\v 7 Maana kinywa changu hunena uaminifu na midomo yangu huchukia uovu.
\s5
\v 8 Maneno ya kinywa changu yote ni haki; hakuna kilichogeuzwa wala kupotoshwa.
\v 9 Maneno yangu yote yamenyooka kwa yule mwenye kuelewa; maneno yangu ni haki kwa wale wanaotafuta maarifa.
\s5
\v 10 Chagua fundisho langu badala ya fedha na maarifa kuliko dhahabu safi.
\v 11 Maana mimi, hekima ni bora kuliko vito; hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na mimi.
\s5
\v 12 Mimi, hekima, naishi kwa utaratibu, na ninamiliki maarifa na busara.
\v 13 Hofu ya Mungu ni kuchukia uovu- nachukia majivuno na kiburi, njia ya uovu, na kauli iliyopotoka- hivyo ninavichukia.
\s5
\v 14 Ninaushauri mzuri na hekima sahihi; mimi ni busara; nguvu zipo kwangu.
\v 15 Kwa njia yangu wafalme hutawala- pia na waungwana, na wote ambao hutawala kwa haki.
\v 16 Kwa njia yangu wafalme hutawala na waungwana na wote wanaotawala kwa haki.
\s5
\v 17 Nawapenda wale wanaonipenda, na wale wanaonitafuta kwa bidii, wataniona.
\v 18 Kwangu kunautajiri na heshima, utajiri wa kudumu na haki.
\s5
\v 19 Tunda langu ni bora kuliko dhahabu, bora hata kuliko dhahabu safi.
\v 20 Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki,
\v 21 katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
\s5
\v 22 Yehova aliniumba tokea mwanzo- mwazoni mwa matendo yake ya nyakati za kale.
\v 23 Tokea enzi za kale niliwekwa katika nafasi- tokea kwanza, tokea mwanzo wa dunia.
\s5
\v 24 Kabla ya bahari, mimi nilizaliwa- kabla ya kuwepo chemchemi zenye maji tele.
\v 25 Kabla ya milima na vilima kuwekwa, mimi nilizaliwa.
\s5
\v 26 Nilizaliwa kabla ya Yehova hajaiumba dunia wala makonde, hata mavumbi ya kwanza katika dunia.
\v 27 Nilikuwepo alipoziimarisha mbingu, wakati alipochora mstari katika sura ya kilindi.
\s5
\v 28 Nilikuwepo alipoimarisha anga la juu na wakati wa kutengeneza kina cha chemchemi.
\v 29 Nilikuwepo alipotengeneza mipaka ya bahari, ili maji yasisambae kuvuka pale alipoyaamuru, na wakati anaamuru misingi ya dunia sehemu ya kukaa.
\s5
\v 30 Nilikuwa kando yake, kama fundistadi mkuu, na mimi nilikuwa furaha yake siku kwa siku, nikifurahi mbele zake daima.
\v 31 Nilikuwa nikifurahi katika dunia yake yote na furaha yangu ilikuwa kwa wana wa wanadamu.
\s5
\v 32 Na sasa, wanangu, nisikilizeni, maana wale wazishikao njia zangu watakuwa na furaha.
\v 33 Sikilizeni fundisho langu na mpate hekima; wala msilipuuze.
\v 34 Anisikilizaye atakuwa na furaha- kila siku akitazama katika malango yangu, akinisubiri pembeni mwa milango ya masikani yangu.
\s5
\v 35 Maana yeyote anionaye mimi, anapata uzima, naye atapata kibali kwa Yehova.
\v 36 Na yeyote asiyeniona mimi, hujiumiza mwenyewe, wote wanaonichukia hupenda mauti.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba.
\v 2 Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake.
\s5
\v 3 Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita:
\v 4 "Wale wasiofunzwa waje hapa!" anawaambia wale wasionaufahamu.
\s5
\v 5 Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya.
\v 6 Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
\s5
\v 7 Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara.
\v 8 Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda.
\v 9 Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu.
\s5
\v 10 Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.
\v 11 Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
\v 12 Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako.
\s5
\v 13 Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote.
\v 14 Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji.
\v 15 Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao.
\s5
\v 16 Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!" anawaambia wale wasio na akili. "
\v 17 Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza."
\v 18 Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Mithali za Sulemani. Mwana mwenye hekima humfurahisha baba yake lakini mwana mpumbavu huleta majonzi kwa mama yake.
\v 2 Hazina zilizolimbikizwa kwa uovu hakosa thamani, bali kwa kutenda haki hujilinda mbali na kifo.
\v 3 Yehova hawaachi wale watendao haki wapate njaa, bali hamu ya waovu huizuia.
\s5
\v 4 Mkono mlegevu humfanya mtu awe masikini, bali mkono wa mtu mwenye bidii hupata utajiri.
\v 5 Mwana mwenye busara hukusanya mazao wakati wa kiangazi, bali ni aibu kwake alalaye wakati wa mavuno.
\s5
\v 6 Zawadi kutoka kwa Mungu zipo juu ya kichwa cha wale watendao haki; bali kinywa cha uovu hufunikwa kwa jeuri.
\v 7 Mtu atendaye haki anatufurahisha tunapomkumbuka, bali jina la mwovu litaoza.
\s5
\v 8 Wale wenye akili hukubali maagiza, bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataangamia.
\v 9 Yeye anayetembea katika uadilifu hutembea katika usalama, bali yule anayepotosha njia zake, ataonekana.
\s5
\v 10 Yeye ambaye hukonyeza kwa jicho lake huleta majonzi, bali mpumbavu mwenye maneno mengi atatupwa chini.
\v 11 Kinywa cha mwenye kutenda haki ni kama chemchemi ya maji ya uzima, bali kinywa cha uovu hufunikwa kwa jeuri.
\s5
\v 12 Chuki huchochea mafarakano, bali upendo hufunika juu ya makwazo yote.
\v 13 Hekima inapatikana kwenye kinywa cha mtu mwenye ufahamu, bali fimbo ni kwa ajili ya mgongo wa yule asiye na akili.
\s5
\v 14 Watu wenye hekima hutunza maarifa, bali kinywa cha mpumbavu huleta uharibifu karibu.
\v 15 Mali ya mtu tajiri ni mji wake mwenye ngome; ufukara wa masikini ni uharibifu wao.
\s5
\v 16 Mshahara wa watenda haki huelekea kwenye uzima; manufaa ya waovu huelekea dhambini.
\v 17 Kuna njia kwenda kwenye uzima kwa yule anayefuata maongozo, bali anayekataa maonyo hupotea.
\s5
\v 18 Yeye afichaye chuki anamidomo ya uongo, na yeye anayesambaza kashfa ni mpumbavu.
\v 19 Katika maneno mengi, hapakosi uhalifu, bali aliyemwangalifu katika usemi wake ni mwenye busara.
\s5
\v 20 Ulimi wa yule atendaye haki ni fedha safi; kuna thamani ndogo katika moyo wa mbaya.
\v 21 Midomo ya yule atendaye haki huwastawisha wengi, bali wapumbavu hufa kwa sababu ya kukosa akili.
\s5
\v 22 Zawadi njema za Yehova huleta utajiri na haweki maumivu ndani yake.
\v 23 Uovu ni mchezo achezao mpumbavu, bali hekima ni furaha kwa mtu mwenye ufahamu.
\s5
\v 24 Hofu ya mwenye uovu humkumba ghafla, bali shauku ya mwenye haki itatimizwa.
\v 25 Waovu ni kama dhoruba inayopita, na hawapo tena, bali mwenye haki ni msingi unaodumu milele.
\s5
\v 26 Kama siki kwenye meno na moshi kwenye macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
\v 27 Hofu ya Yehova huongeza maisha, bali miaka ya waovu itakuwa mifupi.
\s5
\v 28 Matumaini ya wale watendao haki ndiyo furaha yao, bali miaka ya waovu itakuwa mifupi.
\v 29 Njia ya Yehova huwalinda wale wenye uadilifu, bali kwa waovu ni uhalibifu.
\v 30 Wale watendao haki hawataondolewa, bali waovu hawatabaki katika nchi.
\s5
\v 31 Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa.
\v 32 Midomo ya wale watendao mema huyajua yanayokubalika, bali kinywa cha waovu, huyajua yanayopotosha.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri.
\v 2 Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima.
\s5
\v 3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza.
\v 4 Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti.
\s5
\v 5 Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao.
\v 6 Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao.
\s5
\v 7 Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu.
\v 8 Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu.
\s5
\v 9 Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama.
\v 10 Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha.
\v 11 Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa.
\s5
\v 12 Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.
\v 13 Anayekwenda akizunguka kwa kukashifu hufunua siri, bali mtu mwaminifu hustiri jambo.
\s5
\v 14 Pasipokuwa na uongozi wenye busara, taifa huanguka, bali ushindi huja kwa kushauriana washauri wengi.
\s5
\v 15 Anayemdhamini mkopo wa mgeni ataumia kwa usumbufu, bali anayechukia kutoa rehani kwa namna ya ahadi yupo salama.
\v 16 Mwanamke mwenye rehema hupata heshima, bali watu wakorofi hufumbata utajiri.
\s5
\v 17 Mtu mkarimu hufaidika mwenyewe, bali mkatili hujiumiza mwenyewe.
\v 18 Mtu mwovu husema uongo kupata mishahara yake, bali yeye apandaye haki anavuna mishahara ya kweli.
\s5
\v 19 Mtu mwaminifu atendaye haki ataishi, bali yeye atendaye uovu atakufa.
\v 20 Yehova anawachukia wenye ukaidi mioyoni, bali anawapenda wale ambao njia zao hazina makosa.
\s5
\v 21 Uwe na uhakika juu ya hili- watu waovu hawatakosa adhabu, bali uzao wa wale watendao haki watawekwa salama.
\v 22 Kama pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe ndiyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.
\s5
\v 23 Shauku ya wale watendao haki ni matokeo mema, bali watu waovu wanaweza kutumainia ghadhabu tu.
\v 24 Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini.
\s5
\v 25 Mtu mkarimu atafanikiwa na yule awapaye maji wengine atapata maji yake mwenyewe.
\v 26 Watu wanamlaani mtu ambaye hukataa kuuza nafaka, bali zawadi njema hufunika kichwa chake ambaye huuza nafaka.
\s5
\v 27 Yule ambaye hutafuta mema kwa bidii pia anatafuta kibali, bali yule atafutaye ubaya atapata ubaya.
\v 28 Wale wanaotumaini utajiri wataanguka, bali kama jani, wale watendao haki watasitawi.
\s5
\v 29 Yule ambaye analeta taabu kwenye kaya yake ataurithi upepo na mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye moyo wa hekima.
\s5
\v 30 Wale watendao haki watakuwa kama mti wa uzima, lakini vurugu huondoa uzima.
\v 31 Tazama! Ikiwa wale watendao haki hupokea wanachositahili, je si zaidi kwa waovu na wenye dhambi!
\s5
\c 12
\p
\v 1 Anayependa mafundisho hupenda maarifa, bali yule anayechukia maonyo ni mpumbavu.
\v 2 Yehova humpa fadhila mtu mwema, bali mtu ambaye hufanya mipango ya ufisada atahukumiwa.
\s5
\v 3 Mtu hawezi kuimarishwa kwa uovu, bali wale watendao haki hawawezi kung'olewa.
\v 4 Mke mwema ni taji ya mume wake, bali yule aletaye aibu ni kama ugonjwa unaoozesha mifupa yake.
\s5
\v 5 Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu.
\v 6 Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
\s5
\v 7 Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.
\v 8 Mtu husifiwa kwa kadri ya hekima yake, bali yule anayechagua ukaidi hudharauliwa.
\s5
\v 9 Bora kuwa na cheo duni- kuwa mtumishi tu- kuliko kujisifu kuhusu ukuu wako bila kuwa na chakula.
\v 10 Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.
\s5
\v 11 Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.
\v 12 Watu waovu hutamani wanavyoiba watu wabaya kutoka kwa wengine, bali tunda la wale watendao haki hutoka kwao mwenyewe.
\s5
\v 13 Mtu mbaya hunaswa kwa maongezi yake mabaya, bali wale watendao haki hujinasua katika taabu.
\v 14 Mtu hushiba vitu vyema kutokana na tunda la maneno yake, kama vile kazi ya mikono yake inavyompa thawabu.
\s5
\v 15 Njia ya mpumbavu ni sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu wa hekima husikiliza ushauri.
\v 16 Mpumbavu huonyesha hasira yake papo hapo, bali asiyejali tusi ni mwenye busara.
\s5
\v 17 Asemaye ukweli huongea ilivyo haki, bali shahidi wa uongo huongea uongo.
\v 18 Maneno yake asemaye kwa pupa ni kama kurusha upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
\s5
\v 19 Midomo yenye kweli itadumu milele, bali ulimi wa uongo ni kwa kitambo kidogo tu.
\v 20 Kuna udanganyifu katika mioyo ya wale wanaopanga kutenda uovu, bali furaha hutoka kwa washauri wa amani.
\s5
\v 21 Hakuna ugonjwa utakaowajia wale watendao haki, bali watu waovu watajazwa matatizo.
\v 22 Yehova anachukia midomo ya uongo, bali wale ambao huishi kwa uaminifu ndiyo furaha yake.
\s5
\v 23 Mtu mwenye busara anasitiri maarifa yake, bali moyo wa wapumbavu hupiga yowe za kipumbavu.
\v 24 Mkono wa mwenye bidii utatawala, bali watu wavivu watawekwa katika kazi za kulazimishwa.
\s5
\v 25 Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.
\v 26 Mwenye haki ni kiongozi kwa rafiki yake, bali njia ya waovu huwaongoza katika kupotea.
\s5
\v 27 Watu wavivu hawawezi kubanika mawindo yao wenyewe, bali mtu wenye bidii atapata mali zenye thamani.
\v 28 Wale ambao wanatembea katika njia ya haki wanapata uzima na katika mapito hayo hakuna kifo.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya baba yake, bali mwenye dhihaka hatasikiliza karipio.
\v 2 Mtu hufurahia vitu vizuri kutokana na matunda ya kinywa chake, bali hamu ya wadanganyifu ni jeuri.
\s5
\v 3 Yeye anayelinda kinywa chake huyalinda maisha, bali anayefumbua sana midomo yake atajiangamiza mwenyewe.
\v 4 Hamu ya watu wavivu ni uchu lakini hawapati kitu, bali hamu ya watu wenye bidii hutoshelezwa sana.
\s5
\v 5 Atendaye haki huchukia uongo, bali mtu mwovu hukinzana mwenyewe, na kufanya ya kuaibisha.
\v 6 Wenye haki huwalinda wale ambao ni wakamilifu katika mapito yao, bali uovu huwaangusha wale watendao dhambi.
\s5
\v 7 Kuna mtu ambaye hujitajirisha mwenyewe, lakini hana chochote na kuna mtu ambaye hutoa kila kitu, bado ni tajiri kweli.
\v 8 Mtu tajiri anaweza kufidia maisha yake kwa mali zake, bali mtu masikini hatapokea kitisho cha aina hiyo.
\s5
\v 9 Mwanga wa mtu atendaye haki hufurahia, bali taa ya waovu itazimika.
\v 10 Kiburi huzaa mafarakano, bali kwa wale wasikiao shauri jema kuna hekima.
\s5
\v 11 Penye majivuno mengi utajiri hufifia, bali yeye apataye pesa kwa kufanya kazi kwa mkono wake pesa zake zitaongezeka.
\v 12 Tumaini linapoachwa, huvunja moyo, bali kukamilishwa kwa shauku ni mti wa uzima.
\s5
\v 13 Yule ambaye anadharau fundisho bado atakuwa chini ya utawala wake, bali yeye ambaye anaheshimu amri atapewa thawabu.
\v 14 Mafundisho ya mtu mwenye hekima ni chemchemi ya uzima, yanakuondoa kutoka kwenye mitego ya mauti.
\s5
\v 15 Busara njema huleta fadhila, bali njia ya wadanganyifu haina mwisho.
\v 16 Watu wenye busara hutenda kwa maarifa kwa kila uamuzi, bali mpumbavu huonyesha upuuzi wake.
\s5
\v 17 Mjumbe mbaya huangukia kwenye shida, bali balozi mwaminifu huleta upatanisho.
\v 18 Yeye ambaye hupuuza kurudiwa atapata umasikini na aibu, bali heshima itamjia yeye ambaye hujifunza kutokana na masahihisho.
\s5
\v 19 Shauku iliyotambuliwa ni tamu kwa hamu, bali wapumbavu huchukia kuacha uovu.
\v 20 Tembea pamoja na watu wenye hekima nawe utakuwa na hekima, bali rafiki wa wapumbavu atateseka.
\s5
\v 21 Maafa huwakimbilia wenye dhambi, bali wale watendao haki hupewa thawabu kwa mema.
\v 22 Mtu mwema huacha urithi kwa wajukuu wake, bali mali ya mwenye dhambi huwekwa akiba kwa yule atendaye haki.
\s5
\v 23 Shamba la masikini lisilolimwa linaweza huzalisha chakula kingi, bali huchukuliwa kwa udhalimu.
\v 24 Yeye ambaye hamrudi mwanawe humchukia, bali yule anayempenda mwanawe humjali kwa kumwadibisha.
\s5
\v 25 Yeye atendaye haki hula hadi kutosheleza hamu yake bali tumbo la mwovu linanjaa daima.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Mwanamke mwenye busara huijenga nyumba yake, bali mwanamke mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
\v 2 Yeye aendaye kwa uaminifu humcha Yehova, bali mkaidi humdharau katika njia zake.
\s5
\v 3 Katika kinywa cha mpumbavu hutoka chipukizi la kiburi chake, bali midomo ya wenye busara itawalinda.
\v 4 Pale pasipo na mifugo hori la kulishia ni safi, bali mazao mengi huweza kupatikana kwa nguvu za maksai.
\s5
\v 5 Shahidi mwaminifu hasemi uongo, bali shahidi wa uongo hupumua uongo.
\v 6 Mwenye dharau hutafuta hekima na hakuna hata, bali maarifa huja kwa urahisi kwa mwenye ufahamu.
\s5
\v 7 Nenda mbali kutoka kwa mtu mpumbavu, maana hutapata maarifa kwenye midomo yake.
\v 8 Hekima ya mtu mwenye busara ni kuifahamu njia yake mwenyewe, bali upuuzi wa wapumbavu ni udanganyifu.
\s5
\v 9 Wapumbavu hudharau wakati sadaka ya hatia inapotolewa, bali miongoni mwao waaminifu hushiriki fadhila.
\v 10 Moyo unayajua machungu yake mwenyewe na hakuna mgeni anayeshiriki furaha yake.
\s5
\v 11 Nyumba ya waovu itaangamizwa, bali hema ya watu waaminifu itasitawi.
\v 12 Kuna njia ambayo huonekana sawa kwa mtu, lakini mwisho wake huelekea mauti tu.
\s5
\v 13 Moyo unaweza kucheka lakini bado ukawa katika maumivu na furaha inaweza kukoma ikawa huzuni.
\v 14 Yule asiyemwaminifu atapata anachostahili kwa njia zake, bali mtu mwema atapata kilicho chake.
\s5
\v 15 Yeye ambaye hakufundishwa huamini kila kitu, bali mtu mwenye hekima huzifikiria hatua zake.
\v 16 Mtu mwenye hekima huogopa na kutoka kwenye ubaya, bali mpumbavu huliacha onyo kwa ujasiri.
\s5
\v 17 Yeye ambaye anakuwa na hasira kwa haraka hufanya mambo ya kipumbavu, na mtu anayefanya hila mbaya huchukiwa.
\v 18 Wajinga hurithi upumbavu, lakini watu wenye hekima wamezingirwa kwa maarifa.
\s5
\v 19 Hao ambao ni waovu watainama mbele yao walio wema na wale wenye uovu watasujudu kwenye malango ya wenye haki.
\v 20 Mtu masikini huchukiwa hata na marafiki zake, bali watu matajiri wanamarafiki wengi.
\s5
\v 21 Yeye ambaye huonyesha dharau kwa jirani yake anafanya dhambi, bali yule ambaye huonyesha fadhila kwa masikini anafuraha.
\v 22 Je wale wanaofanya njama mbaya hawapotei? Bali wale wenye mpango wa kutenda mema watapokea agano la uaminifu na udhamini
\s5
\v 23 Katika kazi zote ngumu huja faida, bali palipo na maongezi tu, huelekea kwenye umasikini.
\v 24 Taji ya watu wenye busara ni utajiri wao, bali upuuzi wa wapumbavu huwaletea upuu zaidi.
\s5
\v 25 Shahidi mkweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo hupumua uongo.
\s5
\v 26 Mtu anapokuwa na hofu ya Yehova, pia anakuwa na matumaini zaidi ndani yake; vitu hivi vitakuwa kama sehemu imara ya ulinzi kwa watoto wa mtu huyu.
\v 27 Kumcha Yehova ni chemchemi ya uzima, ili kwamba mtu aweze kujiepusha kutoka katika mitego ya mauti.
\s5
\v 28 Utukufu wa mfalme upo katika idadi kubwa ya watu wake, bali pasipo watu mfalme huangamia.
\v 29 Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
\s5
\v 30 Moyo wenye raha ni uzima wa mwili, bali husuda huozesha mifupa.
\v 31 Anayemkandamiza masikini humlaani Muumba wake, bali anayeonyesha fadhila kwa wahitaji humtukuza yeye.
\s5
\v 32 Mtu mwovu huangushwa chini kwa matendo yake mabaya, bali mtu mwenye haki anakimbilio hata katika kifo.
\v 33 Hekima hukaa katika moyo wa ufahamu, bali hata miongoni mwa wapumbavu hujiachilia mwenyewe kwa kujulikana
\s5
\v 34 Kutenda haki huliinua taifa, bali dhambi ni chukizo kwa watu wowote.
\v 35 Fadhila ya mfalme ni kwa mtumishi mwenye kutenda kwa hekima, bali hasira yake ni kwa yule atendaye kwa kuaibisha.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
\v 2 Ulimi wa watu mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha wapumbavu humwaga upuuzi.
\s5
\v 3 Macho ya Yehova yapo kila mahali, yakiwatazama juu ya waovu na wema.
\v 4 Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.
\s5
\v 5 Mpumbavu hudharau marudi ya baba yake, bali yeye anayejifunza kutokana na masahihisho ni mwenye hekima.
\v 6 Katika nyumba ya wale watendao haki kuna hazina kubwa, bali mapato ya watu waovu huwapa taabu.
\s5
\v 7 Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
\v 8 Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake.
\s5
\v 9 Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki.
\v 10 Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa.
\s5
\v 11 Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu?
\v 12 Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima.
\s5
\v 13 Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.
\v 14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi.
\s5
\v 15 Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima.
\v 16 Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia.
\s5
\v 17 Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
\v 18 Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.
\s5
\v 19 Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
\v 20 Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
\s5
\v 21 Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
\v 22 Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
\s5
\v 23 Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
\v 24 Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu.
\s5
\v 25 Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
\v 26 Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
\s5
\v 27 Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
\v 28 Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
\s5
\v 29 Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
\v 30 Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
\s5
\v 31 Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.
\v 32 Yeye anayekataa karipio hujidharau mwenyewe, bali yule asikilizaye masahihisho hujipatia ufahamu.
\s5
\v 33 Kumcha Yehova hufundisha hekima na unyenyekevu huja kabla ya heshima.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Mipango ya moyo ni ya mtu, bali Yehova hutoa jawabu kutoka kwenye ulimi wake.
\v 2 Njia zote za mtu ni safi kwenye macho yake mwenyewe, bali Yehova huipima mioyo.
\s5
\v 3 Kabidhi kwa Yehova kazi zako zote na mipango yako itafanikiwa.
\v 4 Yehova alifanya kila kitu kwa kusudi lake, hata waovu kwa ajili ya siku ya taabu.
\s5
\v 5 Yehova anamchukia kila mtu mwenye moyo wa majivuno, ingawa wanasimama imara, hawakosi kupata adhabu.
\v 6 Kwa agano la uaminifu na udhamini uovu husafishwa na kwa kumcha Yehova watu hujitenga na ubaya.
\s5
\v 7 Njia za mtu zinapompendeza Yehova, huwafanya hata adui zake huyo mtu wawe na amani naye.
\v 8 Bora kitu kidogo pamoja na haki, kuliko mapato makubwa pamoja na udhalimu.
\s5
\v 9 Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.
\v 10 Mshauri yupo katika midimo ya mfalme, katika hukumu kinywa chake hakisemi kwa udanganyifu.
\s5
\v 11 Vipimo vya kweli hutoka kwa Yehova; uzito wote kwenye gunia ni kazi yake.
\v 12 Wafalme wanapofanya mambo maovu, hicho ni kitu cha kudharauliwa, kwa maana utawala huimarishwa kwa kutenda haki.
\s5
\v 13 Mfalme hufurahia midomo ambayo husema haki na anampenda mwenye kusema waziwazi.
\v 14 Hasira ya mfalme ni mjumbe wa mauti lakini mtu mwenye busara atajaribu kutuliza hasira yake.
\s5
\v 15 Katika nuru ya uso wa mfalme ni uzima na fadhila yake ni kama wingu linaloleta mvua ya masika.
\v 16 Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu. Kuchagua kupata ufahamu ni zaidi kuliko fedha.
\s5
\v 17 Njia kuu ya watu waadilifu hujitenga na ubaya; mwenye kuyahifadhi maisha yake huilinda njia yake.
\v 18 Kiburi hutangulia kabla ya uharibifu na moyo wa kujivuna kabla ya maangamizi.
\s5
\v 19 Ni bora kunyenyekea miongoni mwa watu masikini kuliko kugawana ngawira pamoja watu wenye kiburi.
\v 20 Mwenye kutafakari yaliyofundishwa hupata kilicho chema na wenye kumtumaini Yehova watafurahi.
\s5
\v 21 Mwenye hekima moyoni anaitwa ufuhamu na utamu wa hotuba huongeza uwezo wa kufundisha.
\v 22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake ambaye nayo, bali adhabu ya wapumbavu ni upumbavu wao.
\s5
\v 23 Moyo wa mtu mwenye hekima hutoa busara katika kinywa chake na huongeza ushawishi katika midomo yake.
\v 24 Maneno yenye kufaa ni sega la asali -matamu kwenye nafsi na huponya mifupa.
\s5
\v 25 Kuna njia ambayo huonekana sawa kwa mtu, bali mwisho wake ni njia ya mauti.
\v 26 Hamu ya kibarua humfanyia kazi; njaa yake humsihi kuendelea.
\s5
\v 27 Mtu duni huchimba madhara na usemi wake ni kama moto unaounguza.
\v 28 Mtu mkaidi huchochea mafarakano na umbeya huwafarakanisha marafiki.
\s5
\v 29 Mtu wa vurugu humdanganya jirani yake na kumwongoza kwenye mapito ambayo si mema.
\v 30 Yule anayekonyeza kwa jicho anapanga njama za mambo ya ukaidi; wenye kuandama midomo yao watapitisha mabaya.
\s5
\v 31 Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa kuishi katika njia ya haki.
\v 32 Ni bora kukawia kuwa na hasira kuliko kuwa shujaa na mwenye kutawala roho yake ni imara zaidi kuliko yule anayeuteka mji.
\s5
\v 33 Kura hurushwa kwenye mkunjo, bali maamuzi hutoka kwa Yehova.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Ni bora kuwa na utulivu pamoja chembe za mkate kuliko nyumba yenye sherehe nyingi pamoja na ugomvi.
\v 2 Mtumishi mwenye busara atatawala juu ya mwana atendaye kwa aibu na atashiriki urithi kama mmoja wa ndugu.
\s5
\v 3 Kalibu ni kwa fedha na tanuu ni kwa dhahabu, bali Yehova huisafisha mioyo.
\v 4 Mtu atendaye mabaya huwasikiliza wale wanaosema maovu; muongo anausikivu kwa wale wanaosema mambo mabaya.
\s5
\v 5 Mwenye kumdhihaki masikini humtukana Muumba wake na anayefurahia msiba hatakosa adhabu.
\v 6 Wajukuu ni taji ya wazee na wazazi huleta heshima kwa watoto wao.
\s5
\v 7 Hotuba ya ushawishi haifai kwa mpumbavu; kidogo zaidi midomo ya uongo inafaa kwa ufalme.
\v 8 Rushwa ni kama jiwe la kiini macho kwa yule ambaye atoaye; yeye anayeiacha, hufanikiwa.
\s5
\v 9 Anayesamehe kosa hutafuta upendo, bali yeye anayerudia jambo huwatenganisha marafiki wa karibu.
\v 10 Karipio hupenya ndani ya mtu mwenye ufahamu kuliko mapigo mamia kwenda kwa mpumbavu.
\s5
\v 11 Mtu mbaya hutafuta uasi tu, hivyo mjumbe katiri atatumwa dhidi yake.
\v 12 Ni bora kukutana na dubu aliyeporwa watoto wake kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
\s5
\v 13 Mtu anaporudisha mabaya badala ya mema, mabaya hayatatoka katika nyumba yake.
\v 14 Mwanzo wa mafarakano ni kama mtu anayefungulia maji kila mahali, hivyo ondoka kwenye mabishano kabla ya kutokea.
\s5
\v 15 Yeye ambaye huwaachilia watu waovu au kuwalaumu wale wanaotenda haki - watu hawa wote ni chukizo kwa Yehova.
\v 16 Kwa nini mpumbavu alipe fedha kwa kujifunza hekima, wakati hana uwezo wa kujifunza?
\s5
\v 17 Rafiki hupenda kwa nyakati zote na ndugu amezaliwa kwa ajili ya nyakati za taabu.
\v 18 Mtu asiyekuwa na akili hufanya ahadi zenye mashariti na kuanza kuwajibika kwa madeni ya jirani yake.
\s5
\v 19 Apendaye mafarakano anapenda dhambi; ambaye hutengeneza kizingiti kirefu sana kwenye mlango wake husababisha kuvunjia kwa mifupa.
\v 20 Mtu mwenye moyo wa udanganyifu hapati chochote ambacho ni chema; na mwenye ulimi wa ukaidi huanguka kwenye janga.
\s5
\v 21 Mzazi wa mpumbavu huleta majonzi kwake mwenyewe; baba wa mpumbavu hana furaha.
\v 22 Moyo mchangamfu ni dawa njema, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
\s5
\v 23 Mtu mwovu hukubali rushwa ya siri ili kupotosha njia za haki.
\v 24 Mwenye ufahamu huelekeza uso wake kwenye hekima, bali macho ya mpumbavu huelekea ncha za dunia.
\s5
\v 25 Mwana mpumbavu ni huzuni kwa baba yake na uchungu kwa mwanamke aliyemzaa.
\v 26 Pia, si vizuri kumwadhibu mwenye kutenda haki; wala si vema kuwachapa mjeledi watu waadilifu wenye ukamilifu.
\s5
\v 27 Mwenye maarifa hutumia maneno machache na mwenye ufahamu ni mtulivu.
\v 28 Hata mpumbavu hudhaniwa kuwa na busara kama akikaa kimya; wakati anapokaa amefunga kinywa chake, anafikiriwa kuwa na akili.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yule ambaye hujitenga hutafuta matakwa yake mwenyewe na hupingana na hukumu zote za kweli.
\v 2 Mpumbavu hapati raha katika ufahamu, lakini hufunua kile kilichopo katika moyo wake.
\s5
\v 3 Mtu mwovu anapokuja, dharau huja pamoja naye- sambamba na aibu na shutuma.
\v 4 Maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina kirefu; chemchemi ya hekima ni mkondo unaotiririka.
\s5
\v 5 Si vema kuwa na upendeleo kwa mwovu, wala haifai kukana haki kwa wale watendao mema.
\v 6 Midomo ya mpumbavu huletea mafarakano na kinywa chake hukaribisha mapigo.
\s5
\v 7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na hujinasa mwenye kwa midomo yake.
\v 8 Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu na hushuka katika sehema za ndani sana kwenye mwili.
\s5
\v 9 Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.
\v 10 Jina la Yehova ni mnara imara; atendaye haki hukimbilia na kuwa salama.
\s5
\v 11 Mali ya tajiri ni mji wake imara na katika fikira zake ni kama ukuta mrefu.
\v 12 Moyo wa mtu huwa na kiburi kabla ya anguko lake, bali unyenyekevu hutangulia kabla ya heshima.
\s5
\v 13 Anayejibu kabla ya kusikiliza- ni upuuzi na aibu yake.
\v 14 Roho ya mtu itajinusuru na madhara, bali roho iliyopondeka nani anaweza kuivumilia?
\s5
\v 15 Moyo wa mwenye akili hujipatia maarifa na usikivu wa mwenye busara huitafuta.
\v 16 Zawadi ya mtu inaweza kufungua njia na kumleta mbele ya mtu muhimu.
\s5
\v 17 Wa kwanza kujitetea katika shitaka lake huonekana kuwa na haki hadi mpinzani wake aje na kumuuliza maswali.
\v 18 Kupiga kura kunamaliza mabishano na kuwatawanya wapinzani imara.
\s5
\v 19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kushawishiwa kuliko mji wenye nguvu, na kugombana ni kama makomeo ya ngome.
\v 20 Tumbo la mtu litashiba kutoka kwenye tunda la kinywa chake; atatoshelezwa kwa mavuno ya midomo yake.
\s5
\v 21 Uzima na kifo hutawaliwa kwa ulimi, na wale wenye kuupenda ulimi watakula tunda lake.
\v 22 Yeye apataye mke anapata kitu chema na kupokea fadhila kutoka kwa Yehova.
\s5
\v 23 Mtu masikini huomba rehema, lakini mtu tajiri hujibu kwa ukali.
\v 24 Anayejidai kwa marafiki wengi watamleta katika uharibifu, bali yupo rafiki ambaye huwa karibu kuliko ndugu.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Bora mtu masikini ambaye huenenda katika uadilifu wake kuliko mwenye ukaidi katika maneno yake na ni mpumbavu.
\v 2 Tena, si vizuri kuwa na hamu bila maarifa na mwenye kukimbia haraka sana hukosea njia.
\s5
\v 3 Upuuzi wa mtu unaharibu maisha yake na moyo wake hughadhabika dhidi ya Yehova.
\v 4 Utajiri huongeza marafiki wengi, bali mtu masikini hutengwa na rafiki zake.
\s5
\v 5 Shahidi wa uongo hatakosa adhabu na mwenye kupumua uongo hataokoka.
\v 6 Wengi wataomba fadhila kutoka kwa mtu mkarimu na kila mtu ni rafiki wa yule anayetoa zawadi.
\s5
\v 7 Mtu masikini huchukiwa na ndugu zake wote; je marafiki wengi kiasi gani hujitenga kutoka kwake! Anawaita, lakini wameondoka.
\v 8 Anayepata hekima huyapenda maisha yake mwenyewe; yeye atunzaye ufahamu atapata kilicho chema.
\s5
\v 9 Shahidi wa uongo hatakosa kuadhibiwa, bali mwenye kupumua uongo ataangamia.
\v 10 Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa- wala kwa mtumwa kutawala juu ya wafalme.
\s5
\v 11 Busara humfanya mtu achelewe kukasirika na utukufu wake ni kusamehe kosa.
\v 12 Ghadhabu ya mfalme ni kama muungurumo wa simba kijana, bali fadhila yake ni kama umande kwenye majani.
\s5
\v 13 Mwana mpumbavu ni uharibifu kwa baba yake na mke mgomvi ni maji yanayochuruzika daima.
\v 14 Nyumba na utajiri ni urithi kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Yehova.
\s5
\v 15 Uvivu unamtupa mtu kwenye usingizi mzito, bali asiyetamani kufanya kazi atakwenda njaa.
\v 16 Yeye anayetii amri huyaongoza maisha yake, bali mtu asiyefikiri juu ya njia zake atakufa.
\s5
\v 17 Mwenye ukarimu kwa masikini humkopesha Yehova na atalipwa kwa kile alichofanya.
\v 18 Mrudi mwanao wakati kuna matumaini na usiwe na shauku ya kumweka katika mauti.
\s5
\v 19 Mtu mwenye hasira kali lazima alipe adhabu; kama ukimwokoa, utafanya hivyo mara mbili.
\v 20 Sikiliza ushauri na ukubali maelekezo, ili uweze kuwa na hekima mwishoni mwa maisha yako.
\s5
\v 21 Moyoni mwa mtu kuna mipango mingi, bali kusudi la Yehova ndilo litakalo simama.
\v 22 Shauku ya mtu ni uaminifu na mtu masikini ni bora kuliko muongo.
\s5
\v 23 Kumheshimu Yehova huwaelekeza watu kwenye uzima; mwenye nayo atashibishwa na hatadhurika kwa madhara.
\v 24 Mtu goigoi huuzika mkono wake ndani ya dishi; hataurudisha juu ya kinywa chake.
\s5
\v 25 Kama utampiga mwenye mzaha, wajinga watakuwa na hekima; mwelekeze mwenye ufahamu, naye atapata maarifa.
\s5
\v 26 Anayempora baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana anayeleta aibu na shutuma.
\v 27 Mwanangu, kama utaacha kusikiliza maelekezo, utapotea kutoka kwenye maneno ya maarifa.
\s5
\v 28 Shahidi mpotofu huidhihaki haki na kinywa cha waovu humeza uovu.
\v 29 Hukumu ipo tayari kwa wenye dhihaka na mjeledi kwa migongo ya wapumbavu.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Divai ni dhihaka na kinywaji kikali ni mgomvi; anayepotea kwa kunywa hana busara.
\v 2 Kumwogopa mfalme ni kama kumwogopa simba kijana aungurumaye, yeyote anayemkasirisha hutoa fidia ya maish yake.
\s5
\v 3 Ni heshima kwa mtu yeyote kujiepusha na mafarakano, bali kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano.
\v 4 Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
\s5
\v 5 Makusudi ndani ya moyo wa mtu ni kama maji yenye kina, bali mtu mwenye ufahamu huyateka.
\v 6 Mara nyingi mtu husema yeye ni mwaminifu, lakini ni nani awezaye kumpata yule mwaminifu?
\s5
\v 7 Mtu atendaye haki hutembea katika uaminifu wake na wana wake wanaofuata baada yake wanafuraha.
\v 8 Mfalme anayeketi kwenye kiti cha hukumu akifanya kazi za kuhukumu hupembua kwa macho yake mabaya yote yaliyoko mbele yake.
\s5
\v 9 Nani anayeweza kusema, "Nimeuweka safi moyo wangu; nipo huru na dhambi zangu"?
\v 10 Mizani tofauti na vipimo visivyosawa - Yehova huvichukia vyote.
\s5
\v 11 Hata kijana hujulikana kwa matendo yake, kwa mwenendo wake kama ni safi na uadilifu.
\v 12 Masikio yanayosikia na macho yanayoona- Yehova aliyafanya yote.
\s5
\v 13 Usipende usingizi au utakuwa masikini; fumbua macho yako na utakuwa na vyakula tele.
\v 14 "Mbaya! Mbaya!" anasema mnunuzi, lakini akiondoka anajisifu.
\s5
\v 15 Ipo dhahabu na mawe ya thamani, lakini midomo yenye maarifa ni kito cha thamani.
\v 16 Chukua vazi kama mmiliki wake ataweka fedha kama dhamana kwa deni la mgeni, na lichukue kama anaweka dhamana kwa uzinifu.
\s5
\v 17 Mkate uliopatikana kwa ulaghai unaladha tamu, lakini baadaye kinywa chake kitajaa kokoto.
\v 18 Mipango huimarishwa kwa ushauri na kwa mwongozo wa busara utapigana vita.
\s5
\v 19 Mmbea hufunua siri na kwa hiyo hupaswi kushirikiana na watu ambao huongea sana.
\v 20 Kama mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itapulizwa katikati ya giza.
\s5
\v 21 Urithi uliopatikana mwanzoni kwa haraka utakuwa na mema kidogo mwishoni.
\v 22 Usiseme " Mimi nitakulipiza kwa kosa hili" Msubiri Yehova na yeye atakuokoa.
\s5
\v 23 Yehova huchukia mizani isiyo sawa na vipimo vya udanganyifu si vizuri.
\v 24 Hatua za mtu huongozwa na Yehova; namna gani basi ataifahamu njia yake?
\s5
\v 25 Ni mtego kwa mtu kusema kwa pupa, " Kitu hiki ni kitakatifu" na kuanza kufikiri juu yake kwamba kina maana gani baada ya kufanya kiapo.
\v 26 Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu na huligeuza juu yao gurudumu la kupuria.
\s5
\v 27 Roho ya mtu ni taa ya Yehova, hutafiti sehemu zake zote za ndani kabisa.
\v 28 Agano la uaminifu na udhamini humhifadhi mfalme; kiti chake cha enzi hufanywa thabiti kwa upendo.
\s5
\v 29 Utukufu wa watu vijana ni nguvu zao na fahari ya watu wazee ni mvi zao.
\v 30 Mapigo yanayoleta kidonda huusafisha ubaya na vichapo hufanya sehemu za ndani kabisa kuwa safi.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Moyo wa mfalme ni mfereji wa maji katika mkono wa Yehova; anaugeuza popote anakopenda.
\v 2 Kila njia ya mtu ni sawa katika macho yake mwenyewe, lakini ni Yehova anayeipima mioyo.
\s5
\v 3 Kutenda haki na adili hukubaliwa zaidi na Yehova kuliko sadaka.
\v 4 Macho ya kiburi na moyo wa majivuno- taa ya waovu- ni dhambi.
\s5
\v 5 Mipango ya mwenye juhudi huelekea kwenye mafanikio tu, bali kila mtu anayetenda kwa haraka huelekea umasikini.
\v 6 Kujipatia utajiri kwa ulimi wa uongo ni mvuke unaopita upesi na mtego ambao unafisha.
\s5
\v 7 Vurugu ya waovu itawaburuta mbali, maana wanakataa kutenda haki.
\v 8 Njia ya mwenye hatia ni ukatiri, bali mwenye usafi hutenda yaliyo ya haki.
\s5
\v 9 Bora kuishi kwenye kona ya juu darini kuliko katika nyumba pamoja na mke mgonvi.
\v 10 Hamu ya mwovu ni uchu wa mabaya; jirani yake haoni ukarimu katika macho yake.
\s5
\v 11 Mwenye dhihaka anapoadhibiwa mjinga hupata busara, na mtu mwenye busara anapofundishwa, anaongeza maarifa.
\v 12 Atendaye haki huilinda nyumba ya mwovu; huwashusha waovu kwenye uharibifu.
\s5
\v 13 Anayeziba masikio yake kwenye kilio cha masikini, pia atalia, lakini hatajibiwa.
\v 14 Zawadi ya siri hutuliza hasira na zawadi ya kificho hutuliza ghadhabu kuu.
\s5
\v 15 Haki ikitendeka, huleta furaha kwa mwenye kutenda wema, lakini huleta hofu kubwa kwa watenda mabaya.
\v 16 Yule anayezurura kutoka kwenye njia ya ufahamu, atapumzika kwenye kusanyiko la wafu.
\s5
\v 17 Anayependa raha atakuwa masikini; anayependa divai na mafuta hawezi kuwa tajiri.
\v 18 Mtu mbaya ni fidia kwa yule atendaye haki, na mdanganyifu ni fidia kwa waaminifu.
\s5
\v 19 Bora kuishi jangwani kuliko kuishi pamoja na mwanamke ambaye huchochea sana ugomvi na malalamiko.
\v 20 Hazina yenye thamani na mafuta vipo nyumbani kwa mwenye busara, bali mtu mpumbavu huviharibu.
\s5
\v 21 Mtu atendaye haki na mwema -huyu mtu hupata uzima, haki na heshima.
\v 22 Mtu mwenye busara huupima mji wa mashujaa, na huiangusha ngome wanayoitumaini.
\s5
\v 23 Anayelinda kinywa chake na ulimi wake hujilinda mwenyewe na taabu.
\v 24 Mtu mwenye kiburi na maringo- " Dhihaka" ndilo jina lake - hutenda kwa majivuno na kujidai.
\s5
\v 25 Shauku ya mtu mvivu itamuua, maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
\v 26 Kwa siku nzima hupatwa na uchu na uchu zaidi, lakini atendaye haki hutoa na wala hazuii.
\s5
\v 27 Sadaka ya mwovu ni chukizo; huwa ni chukizo zaidi anapoileta kwa nia mbaya.
\v 28 Shahidi wa uongo ataangamia, bali anayesikiliza ataongea kwa muda wote.
\s5
\v 29 Mtu mwovu huufanya uso wake kuwa mgumu, bali mtu mwadilifu ni thabiti juu ya njia zake.
\s5
\v 30 Hakuna hekima, hakuna ufahamu, na hakuna shauri linaloweza kusimama kinyume na Yehova.
\v 31 Farasi hutayarishwa kwa siku ya mapigano, lakini ushindi hupatikana kwa Yehova.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Jina jema huchaguliwa dhidi ya utajiri mwingi na fadhila ni bora kuliko fedha na dhahabu.
\v 2 Watu matajiri na masikini wanafanana katika hili - Yehova ni muumba wao wote.
\s5
\v 3 Mtu mwenye hekima huiona taabu na kujificha mwenyewe, bali mjinga huendelea mbele na huumia kwa ajili yake.
\v 4 Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Yehova ni utajiri, heshima na uzima.
\s5
\v 5 Miiba na mitego hulala katika njia ya wakaidi; yeye anayelinda maisha yake atakuwa mbali navyo.
\v 6 Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.
\s5
\v 7 Watu matajiri huwatawala watu masikini na mwenye kukopa ni mtumwa wa yule anayekopesha.
\v 8 Yule anayepanda udhalimu atavuna taabu na fimbo ya hasira yake itanyauka.
\s5
\v 9 Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa, maana anashiriki mkate wake pamoja na masikini.
\v 10 Mfukuze mbali mwenye dhihaka, na ugomvi utaondoka, mashindano na matukano yatakoma.
\s5
\v 11 Anayependa moyo safi na mwenye maneno ya neema, atakuwa rafiki yake mfalme.
\v 12 Macho ya Yehova huyaangalia maarifa, bali huyapindua maneno ya wadanganyifu.
\s5
\v 13 Mtu mvivu husema, " Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia."
\v 14 Kinywa cha malaya ni shimo lenye kina kirefu; hasira ya Yehova huchochewa dhidi ya yule anayetumbukia ndani yake.
\s5
\v 15 Upumbavu umefungwa katika moyo wa mtoto, lakini marudi ya fimbo huutoa.
\v 16 Anayewanyanyasa watu masikini ili kuongeza mali yake, au kuwapa matajiri, atakuwa masikini.
\s5
\v 17 Tega sikio lako na usikilize maneno ya wenye busara na utumia moyo wako katika maarifa yangu,
\v 18 maana itakuwa furaha kwako kama utayaweka ndani yako, kama yote yatakuwa katika midomo yako.
\v 19 Basi tumaini lako liwe kwa Yehova, ninayafundisha kwako leo- hata kwako.
\s5
\v 20 Sijakuandikia wewe misemo thelathini ya mafundisho na maarifa,
\v 21 kwa kukufundisha kweli katika maneno haya yenye uaminifu, ili uwe na majibu yenye kutegemewa kwa waliokutuma?
\s5
\v 22 Usimwibie masikini kwa sababu ni masikini, au kumponda kwenye lango,
\v 23 maana Yehova ataitetea kesi yao, na atawaibia uzima wale waliowaibia masikini.
\s5
\v 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye kutawaliwa na hasira na wala usiambatane pamoja na mwenye hasira kali,
\v 25 au utajifunza njia zake na utakuwa chambo kwa nafsi yako.
\s5
\v 26 Usiwe miongoni mwao wapigao mikono, mwenye kuahidi madeni.
\v 27 Kama umekosa njia za kulipa, nini kitaweza kuzuia mtu kuchukua kitanda chako chini yako?
\s5
\v 28 Usiondoe jiwe la mpaka la wahenga ambalo baba zako wameweka.
\v 29 Je umemwona mtu aliyeuwawa kwenye kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme; hatasimama mbele ya watu wa kawaida.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Unapoketi kula pamoja na mtawala, angalia kwa uangalifu kilichopo mbele yako,
\v 2 na kama ni mtu unayependa kula chakula sana weka kisu kooni.
\v 3 Usitamani vinono vyake maana ni chakula cha uongo.
\s5
\v 4 Usifanye kazi sana ili kupata mali; uwe na busara ya kutosha ili ujue wakati wa kuacha.
\v 5 Je utaruhusu macho yako yaangaze juu yake? Itaondoka, maana itawaa mabawa kama tai na kuruka angani.
\s5
\v 6 Usile chakula cha yule mwenye jicho baya- na usiwe na shauku ya vinono vyake,
\v 7 maana ni mtu mwenye kuhesabu gharama ya chakula. "Kula na kunywa!" anakuambia, lakini moyo wake haupo pamoja nawe.
\v 8 Utatapika kiasi kidogo ulichokula na utakuwa umepoteza sifa zako njema.
\s5
\v 9 Usiongee katika usikivu wa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako.
\v 10 Usihamishe jiwe la mpaka wa kale au kunyang'anya mashamba ya yatima,
\v 11 maana Mkombozi wao ni imara na atatetea kesi yao dhidi yako.
\s5
\v 12 Elekeza moyo wako katika mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.
\s5
\v 13 Usizuie kuadilisha mtoto, maana ukimchapa kwa fimbo, hatakufa.
\v 14 Ni wewe unayepaswa kumchapa kwa fimbo na kuikoa nafsi yake kuzimu.
\s5
\v 15 Mwanangu, kama moyo wako una busara, basi moyo wangu utafurahi pia;
\v 16 sehemu zangu ndani kabisa zitafurahi sana midomo yako inaponena haki.
\s5
\v 17 Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote.
\v 18 Hakika tumaini lako halitaondolewa na siku zako za hapo baadaye.
\s5
\v 19 Sikia- wewe! - mwanangu, na uwe mwenye busara na uelekeze moyo wako katika njia.
\v 20 Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi,
\v 21 maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara.
\s5
\v 22 Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.
\v 23 Inunue kweli, lakini usiiuze; nunua hekima, nidhamu, na ufahamu.
\s5
\v 24 Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia.
\v 25 Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.
\s5
\v 26 Mwanangu, nipe moyo wako na macho yako yachunguze njia zangu.
\v 27 Maana malaya ni shimo refu, na mke wa mume mwingine ni kisima chembamba.
\v 28 Anavizia kama mnyang'anyi na huongeza idadi ya wadanganyifu miongoni mwa wanadamu.
\s5
\v 29 Nani mwenye taabu? Nani mwenye huzuni? Nani mwenye mapigano? Nani mwenye malalamiko? Nani mwenye majeraha bila sababu? Nani mwenye macho mekundu?
\v 30 Ni wale ambao huzengea kwenye mvinyo, wale wanaojaribu kuchanganya mvinyo.
\s5
\v 31 Usiutazame mvinyo ukiwa mwekundu, wakati unametameta kwenye kikombe na kutelemka kwa uraini.
\v 32 Mwisho wake unauma kama nyoka na sumu yake kama kifutu.
\v 33 Macho yako yataona vitu vigeni na moyo wako utatamka vitu vya ukaidi.
\s5
\v 34 Utakuwa kama anayelala kwenye bahari au anayelala juu ya mlingoti. "
\v 35 Wamenipiga," utasema, " lakini sikuumia. Wamenichapa, lakini sikuwa na hisia. Nitaamka lini? Nitatafuta kinywaji kingine."
\s5
\c 24
\p
\v 1 Usiwe na husuda kwa wenye ubaya, wala usitamani kuambatana nao,
\v 2 kwa sababu mioyo yao inapanga njama za vurugu na midomo ya huongea juu ya madhara.
\s5
\v 3 Kwa hekima nyumba hujengwa na kwa ufahamu huimarishwa.
\v 4 Kwa maarifa vyumba hujazwa vitu vyote vya thamani na utajiri wa kupendeza.
\s5
\v 5 Shujaa wa hekima ni imara, na mtu wa maarifa huongeza nguvu zake;
\v 6 maana kwa uongozi wa busara unaweza kufanya vita na kwa washauri wengi kuna ushindi.
\s5
\v 7 Hekima ipo juu sana kwa mpumbavu; hafumbui kinywa chake kwenye mlango.
\s5
\v 8 Kuna yule mwenye kupanga kufanya mabaya- watu wanamwita bwana wa njama.
\v 9 Mipango ya mpumbavu ni dhambi na watu humchukia mwenye dhihaka.
\s5
\v 10 Kama utakuwa dhaifu na mwenye kuogopa siku ya taabu, basi nguvu zako ni haba.
\s5
\v 11 Waokoe wanaochukuliwa kwenda kwenye mauti na uwashikilie wale wanaopepesuka kwenda kwa mchinjaji.
\v 12 Kama utasema, "Tazama, hatujui chochote juu ya hili," je yule anayepima mioyo hajui unachosema? Na yule anayelinda maisha yako, je hajui? Je Mungu hatampa kila mmoja kile anachostahili?
\s5
\v 13 Mwanangu, kula asali kwa kuwa ni nzuri, kwa sababu matone ya sega la asali ni matamu unapoonja.
\v 14 Hekima ndiyo ilivyo katika nafsi yako - kama utaitafuta, tumaini lako halitabatilika na kutakuwa na tumaini.
\s5
\v 15 Usisubiri kwa kuvizia kama waovu ambao hushambulia nyumba ya mwenye haki. Usiiharibu nyumba yake!
\v 16 Maana mwenye haki huanguka mara saba na kuinuka tena, lakini waovu huangushwa kwa maafa.
\s5
\v 17 Usisherekee wakati adui yako anapoanguka na wala moyo wako usifurahi anapojikwaa,
\v 18 au Yehova ataona na kutoridhika na kuondoa ghadhabu juu yake.
\s5
\v 19 Usifadhaike kwa sababu ya watenda mabaya, na wala usiwahusudu watu waovu,
\v 20 maana mtu mbaya hana matumaini na taa ya watu waovu itazimika.
\s5
\v 21 Mwanangu; mche Yehova, na umwogope mfalme, usishirikiane na watu wenye kuasi dhidi yao,
\v 22 maana kwa ghafula msiba wao utakuja na ni nani ajuaye ukubwa wa uharibifu utakao kuja kutoka kwa hao wote?
\s5
\v 23 Haya ni maneno ya wenye busara pia. Upendeleo katika kuhukumu kesi kwa sheria si vizuri.
\s5
\v 24 Anayemwambia mwenye hatia, " Wewe upo sawa," atalaaniwa na watu na mataifa yatamchukia.
\v 25 Bali wenye kuwakemea waovu watakuwa na furaha na zawadi za wema zitakuja kwao.
\s5
\v 26 Anayetoa jibu la kweli hutoa busu kwenye midomo.
\v 27 Andaa kazi yako ya nje, na tayarisha kila kitu kwa ajili yako mwenyewe shambani; baada ya hapo, jenga nyumba yako.
\s5
\v 28 Usitoe ushahidi dhidi ya jirani yako bila sababu na usidanganye kwa midomo yako.
\v 29 Usiseme, " Mimi nitamtendea kile alichonitendea; nitalipiza kwa kile alichofanya."
\s5
\v 30 Nilikwenda jirani na shamba la mtu mvivu, nikapita kwenye shamba la mzabibu la mtu asiye na akili.
\v 31 Miiba imeota kila sehemu, ardhi ilikuwa imefunikwa kwa upupu, na ukuta wake wa mawe ulikuwa umebomoka.
\s5
\v 32 Kisha nikaliona na kufikiria juu yake; nikatazama na kupokea mafundisho.
\v 33 Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kupumzika kwa kukunja mikono kidogo-
\v 34 na umasikini huja kwa kutembea juu yako, na mahitaji yako kama askari mwenye silaha.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Hizi tena ni mithali za Sulemani, zilinakiliwa na watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda.
\v 2 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali utukufu wa wafalme kutafiti juu ya jambo.
\v 3 Kama mbingu ni kwa kimo na dunia ni kwa kina, ndivyo hivyo moyo wa wafalme hauchunguziki.
\s5
\v 4 Ondoa takataka kutoka kwenye fedha na mfua vyuma anaweza kutumia fedha katika ufundi wake.
\v 5 Pamoja na hayo, waondoe watu waovu mbele ya mfalme na kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa kutenda haki.
\s5
\v 6 Usijitukuze mwenyewe mbele ya mfalme na usisimame katika sehemu iliyoteuliwa kwa watu wakuu.
\s5
\v 7 Ni bora yeye akuambie, "Njoo hapa" kuliko wewe kujiaibisha mbele ya mkuu.
\v 8 Usiharakishe kufanya kuhukumu, kwa kile ulichokishuhudia. Maana utafanya nini mwishoni, wakati jirani yako atakapokuaibisha?
\s5
\v 9 Jitetee kesi yako kati ya jirani yako na wewe na usifunue siri ya mtu mwingine,
\v 10 au vinginevyo anayekusikia ataleta aibu juu yako na taarifa mbaya juu yako haiwezi kunyamazishwa.
\s5
\v 11 Kunena maneno yenye kuchaguliwa vizuri, ni kama nakshi za dhahabu iliyoungwa kwenye fedha.
\v 12 Kama pete ya dhahabu au kito kilichotengenezwa kwa dhahabu safi ndivyo lilivyo karipio la busara kwenye sikio linalosikia.
\s5
\v 13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wenye kumtuma; huyahifadhi maisha ya mabwana wake.
\v 14 Kama mawingu na upepo bila mvua ndivyo alivyo mwenye kujisifu kuhusu zawadi asiyoitoa.
\s5
\v 15 Kwa uvumilivu mtawala anaweza kushawishiwa na ulimi raini unaweza kuvunja mfupa.
\s5
\v 16 Kama utapata asali, kula ya kutosha- vingenevyo, ukila nyingi sana, utaitapika.
\v 17 Usiweke mguu wako kwenye nyumba ya jirani yako mara nyingi, anaweza kuchoshwa nawe na kukuchukia.
\s5
\v 18 Mtu anayetoa ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake ni kama rungu lililotumiwa katika vita, au upanga, au mshale mkali.
\v 19 Kumtumaini mtu asiye mwaminifu wakati wa taabu ni kama jino bovu au mguu unaoteleza.
\s5
\v 20 Kama mtu anayevua nguo katika hali ya baridi, au kama siki iliyotiwa kwenye magadi, ndivyo alivyo anayeimba wimbo kwa mwenye moyo mzito.
\s5
\v 21 Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale na kama ana kiu, mpe maji ya kunywa,
\v 22 maana utamwekea mkaa juu ya kichwa chake na Yehova atakupa thawabu.
\s5
\v 23 Ni hakika upepo wa kaskazini huleta mvua, ndivyo mtu anayesema siri hufanya sura zikasirike.
\v 24 Ni bora kuishi kwenye pembe ya darini kuliko kuchangia nyumba pamoja na mwanamke mgomvi.
\s5
\v 25 Kama maji ya baridi kwa mwenye kiu, ndivyo ilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali.
\v 26 Kama chemchemi iliyochafuliwa au kisima kilichoharibiwa ndivyo alivyo mtu mwema ambaye huyumbayumba mbele ya watu waovu.
\s5
\v 27 Si vema kula asali nyingi mno; hivyo ni kama kutafuta heshima baada heshima.
\v 28 Mtu bila kujitawala ni kama mji ulibomolewa na usiokuwa na kuta.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima.
\v 2 Kama shorowanda hurukaruka na kumeza wadudu wakati wa kuruka, ndivyo ilivyo laana isiyostahili haishuki.
\s5
\v 3 Mjeledi ni kwa ajili ya farasi, hatamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu.
\v 4 Usimjibu mpumbavu na kujiunga katika upumbavu wake, au utakuwa kama yeye.
\s5
\v 5 Mjibu mpumbavu na jiunge katika upumbavu wake, ili asiweze kuwa na busara katika macho yake mwenyewe.
\v 6 Anayetuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu huikata miguu yake mwenyewe na kunywa vurugu.
\s5
\v 7 Miguu ya kiwete inayoning'ia chini ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
\v 8 Kujaribisha jiwe kwenye kombeo ni sawa na kumpa heshima mpumbavu.
\s5
\v 9 Mwiba unaochoma kwenye mkono wa mlevi ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
\v 10 Mpiga mishale anayejeruhi kila mtu ni kama mtu anayemwajiri mpumbavu au kila mtu anayepita karibu yake.
\s5
\v 11 Kama mbwa anavyorudia matapishi yake, ndivyo alivyo mpumbavu anayerudia upuuzi wake.
\v 12 Je unamwona mtu mwenye busara katika macho yake mwenyewe? Mpumbavu anamatumaini zaidi kuliko yeye.
\s5
\v 13 Mtu mvivu husema " Kuna simba kwenye barabara! Kuna simba katikati ya njia kuu!"
\v 14 Kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba zake, ndivyo alivyo mtu mvivu kwenye kitanda chake.
\s5
\v 15 Mtu mvivu hutia mkono wake kwenye sufuria na bado hana nguvu kuunyanyua kwenda kwenye kinywa chake.
\v 16 Mtu mvivu ni mwenye hekima kwenye macho yake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu.
\s5
\v 17 Kama mtu anayeshikilia masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitajia anayepata hasira kwenye ugomvi ambao si wake.
\s5
\v 18 Kama mtu mwendawazimu anayetupa mishale,
\v 19 ndivyo alivyo ambaye humdanganya jirani yake na kusema, " Je sikuwa naongea utani?"
\s5
\v 20 Kwa kukosa kuni, moto huzimika; na pale pasipo na mmbea ugomvi hukoma.
\v 21 Mkaa ni kwa kuwasha makaa na kuni kwa ajili ya moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuwasha ugomvi.
\s5
\v 22 Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu; nazo zinashuka chini kwenye sehemu za ndani ya mwili.
\v 23 Kioo kinachofunika chombo cha udongo ni kama midomo inayoungua na moyo mbaya.
\s5
\v 24 Yule ambaye huwachukia wengine huficha hisia zake kwa midomo na hufunika uongo ndani yake mwenyewe.
\v 25 Ataongea kwa huruma, lakini usimwamini, maana kuna machukizo saba kwenye moyo wake.
\v 26 Ingawa chuki zake zimefunikwa kwa udanganyifu, uovu wake utakuwa wazi katika kusanyiko.
\s5
\v 27 Anayechimba shimo atatumbukia ndani yake na jiwe litamsaga yule anayelisukuma.
\v 28 Ulimi wa uongo huchukia watu unaowajeruhi na kinywa cha uongo husogeza karibu uharibifu.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Usijisifu kwa ajili ya kesho, maana hujui siku italeta nini.
\v 2 Mtu mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe, mgeni na wala si midomo yako mwenyewe.
\s5
\v 3 Fikiria uzito wa jiwe na uzito wa mchanga- uchokozi wa mpumbavu ni mzito zaidi kuliko hivyo vyote.
\v 4 Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
\s5
\v 5 Ni bora karipio la wazi kuliko upendo uliofichwa.
\v 6 Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
\s5
\v 7 Mtu aliyekula na kushiba hulikataa hata sega la asali, bali kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu ni kitamu.
\v 8 Ndege anayezurura kutoka kwenye kiota chake ni kama mtu anayepotea sehemu ambayo anaishi.
\s5
\v 9 Pafumu na manukato huufanya moyo ufurahi, lakini utamu wa rafiki ni bora kuliko ushauri wake.
\v 10 Usimwache rafiki yako na rafiki wa baba yako, na usiende kwenye nyumba ya ndugu yako katika siku ya msiba wako. Ni bora rafiki ambaye yupo karibu kuliko ndugu ambaye yupo mbali.
\s5
\v 11 Mwanangu, uwe na busara, moyo wangu ufurahi; kisha nitamjibu yule anayenidhihaki.
\v 12 Mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini mjinga huendelea mbele na kuteseka kwa ajili ya taabu.
\s5
\v 13 vazi kama mwenyewe anaweka pesa kama dhamana kwa deni la mgeni; lichukue kama anaweka dhamana kwa malaya.
\v 14 Anayempa jirani yake baraka kwa sauti ya juu mapema asubuhi, baraka hiyo itafikiriwa kuwa laana!
\s5
\v 15 Mke mgomvi ni kama siku ya manyunyu ya mvua ya daima;
\v 16 kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kujaribu kushika mafuta kwa mkono wako wa kulia.
\s5
\v 17 Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.
\v 18 Yule anayeutunza mtini atakula matunda yake, na yule mwenye kumlinda bwana wake ataheshimiwa.
\s5
\v 19 Kama maji yanavyoakisi taswira ya sura ya mtu, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwaksi mtu.
\v 20 Kama kuzimu na Uharibifu havitosheki, ndivyo yalivyo macho ya mtu hayawezi kutosheka.
\s5
\v 21 Kalibu ni kwa fedha na tanuru ni kwa dhahabu; na mtu hujaribiwa anaposifiwa.
\v 22 Hata kama utamponda mpumbavu kwa mchI- pamoja na nafaka- bado upumbavu wake hautatoka.
\s5
\v 23 Hakikisha unajua hali ya makundi yako na ujishughulishe juu ya makundi yako,
\v 24 maana utajiri haudumu daima. Je taji hudumu kwa vizazi vyote?
\v 25 Majani huondoka na ukuaji mpya huonekana na milima ya chakula cha mifugo hukusanywa ndani.
\s5
\v 26 Wanakondoo watakupatia mavazi yako na mbuzi watakupatia gharama ya shamba.
\v 27 Kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula chako- chakula kwa kaya yako- na chakula kwa watumishi wako wasichana.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Waovu hukimbia wakati hakuna mtu anayewafukuza, bali wale watendao haki ni thabiti kama simba kijana.
\v 2 Kwa sababu ya uhalifu wa nchi, kuna wakuu wengi, bali kwa mtu mwenye ufahamu na maarifa, itadumu kwa muda mrefu.
\s5
\v 3 Mtu masikini mwenye kukandamiza watu wengine masikini ni kama mvua inayopiga ambayo haisazi chakula.
\v 4 Wale wanaokataa sheria huwatukuza watu waovu, bali wale wenye kuitunza sheria hupigana dhidi yao.
\s5
\v 5 Watu wabaya hawafahamu haki, bali wale wanaomtafuta Yehova wanafahamu kila kitu.
\v 6 Ni bora mtu masikini ambaye anatembea katika uadilifu, kuliko mtu tajiri ambaye ni mdanganyifu katika njia zake.
\s5
\v 7 Yeye anayetunza sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali mwenye ushirika na walafi humwaibisha baba yake.
\v 8 Anayepata mafanikio kwa kutoza riba kubwa anakusanya utajiri wake kwa ajili ya mwingine ambaye atakuwa na huruma kwa watu masikini.
\s5
\v 9 Kama mtu atageuzia mbali sikio lake kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
\v 10 Yeye anayempotosha mwenye uadilifu katika njia ya uovu ataangukia kwenye shimo lake mwenyewe, bali wakamilifu watapata urithi mwema.
\s5
\v 11 Mtu tajiri anaweza kuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu masikini mwenye ufahamu atamtafuta.
\v 12 Kunapokuwa na ushindi kwa wenye kutenda haki, kunafuraha kuu, bali wanapoinuka waovu, watu hujificha wenyewe.
\s5
\v 13 Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali mwenye kutubu na kuziacha ataonyeshwa rehema.
\v 14 Anafuraha ambaye huishi kwa unyenyekevu, bali anayeufanya moyo wake ataanguka katika taabu.
\s5
\v 15 Kama simba anayeunguruma au dubu anayeshabulia ni kama mtawala mwovu juu ya watu masikini.
\v 16 Mtawala anayekosa ufahamu ni mkandamizaji katili, bali mwenye kuchukia aibu atadumu katika siku zake.
\s5
\v 17 Kama mtu anahatia kwa sababu amemwaga damu ya mtu, atakuwa mkimbizi hadi kifo na hakuna atakayemsaidia.
\v 18 Mwenye kuenenda kwa ukaminifu atakuwa salama, bali mwenye njia ya udanganyifu ataanguka ghafla.
\s5
\v 19 Anayefanya kazi kwenye shamba lake atapata chakula kingi, bali afuataye shughuli za upuuzi atapata umasikini mkubwa.
\v 20 Mtu mwaminifu atapata baraka nyingi bali apataye utajiri wa haraka hawezi kukosa adhabu.
\s5
\v 21 Siyo vema kuonyesha upendeleo, lakini kwa kipande cha mkate mtu atafanya ubaya.
\v 22 Mtu mchoyo huharakisha kwenye utajiri, lakini hajui ni umasikini gani utakuja juu yake.
\s5
\v 23 Anayemkaripia mtu baadaye atapata fadhila zaidi kutoka kwake kuliko mwenye kumsifia sana kwa ulimi wake.
\v 24 Yule anayemwibia baba yake na mama yake na kusema, " Hiyo siyo dhambi," ni mshirika wa mwenye kuharibu.
\s5
\v 25 Mtu mwenye tamaa huchochea mafarakano, bali anayemtumaini Yehova atafanikiwa.
\v 26 Yule anayeutumaini moyo wake mwenyewe ni mpumbavu, bali anayekwenda kwa hekima atajilinda mbali na hatari.
\s5
\v 27 Mwenye kuwapa masikini hatapungukiwa kitu, bali anayewafumbia macho atapokea laana nyingi.
\v 28 Watu waovu wanapoinuka, watu hujificha wenyewe, lakini watu waovu wataangamia, wale watendao haki wataongezeka.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Mtu aliyepokea makaripio mengi lakini anashupaza shingo yake atavunjika ndani ya muda mfupi na hata pona.
\v 2 Watenda mema wanapoongezeka, watu wanafurahi, bali wakati mtu mwovu anapotawala, watu huugua.
\s5
\v 3 Mwenye kupenda hekima baba yake anafurahi, bali anayeshikamana na makahaba huuharibu utajiri wake.
\v 4 Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
\s5
\v 5 Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
\v 6 Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
\s5
\v 7 Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
\v 8 Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.
\s5
\v 9 Mtu mwenye busara anapojadiliana na mpumbavu, hughadhabika na kucheka, hakutakuwa na utulivu.
\v 10 Mkatili humchukia mwenye ukamilifu na hutafuta maisha ya mwenye haki.
\s5
\v 11 Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
\v 12 Kama matawala atazinagatia uongo, maafisa wake wote watakuwa waovu.
\s5
\v 13 Mtu masikini na mkandamizaji wanafanana, maana Yehova huyapa nuru macho yao wote.
\v 14 Kama mfalme atamhukumu masikini kwa uaminifu, kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.
\s5
\v 15 Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
\v 16 Watu waovu wanapotawala, uovu huongezeka, bali wenye kutenda haki wataona anguko la watu waovu.
\s5
\v 17 Mwadibishe mwanao naye atakupa pumziko; ataleta furaha katika maisha yako.
\v 18 Pasipo na maono ya kinabii watu huenda bila utaratibu, bali mwenye kuitunza sheria amebarikiwa.
\s5
\v 19 Mtumwa hawezi kurekebishwa kwa maneno, maana ingawa anaelewa, hakuna mwitikio.
\v 20 Je unamwona mtu mwenye haraka katika maneno yake? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
\s5
\v 21 Mwenye kumdekeza mtumwa wake tangu ujana, mwisho wake itakuwa taabu.
\v 22 Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi na bwana mwenye hasira sana hutenda dhambi nyingi.
\s5
\v 23 Kiburi cha mtu humshusha chini, bali mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima.
\v 24 Anayeshirikiana na mwizi huyachukia maisha yake mwenyewe; husikia laana na wala hasemi chochote.
\s5
\v 25 Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.
\v 26 Wengi huutafuta uso wa mtawala, bali kutoka kwa Yehova huja haki kwa ajili yake.
\s5
\v 27 Mtu dhalimu ni chukizo kwa wenye kutenda haki, bali mwenye njia ya haki ni chukizo kwa watu waovu.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Maneno ya Aguri mwana wa Yake - mausia: Mtu huyu alimwambia Ithieli, kwa Ithiel na Ukali:
\v 2 Hakika nipo kama mnyama kuliko mwanadamu na sina ufahamu wa wanadamu.
\v 3 Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya Mtakatifu.
\s5
\v 4 Je ni nani amekwenda juu mbinguni na kurudi chini? Je ni nani aliyekusanya upepo kwenye mikono yake? Je ni nani aliyekusanya maji kwenye kanzu? Je ni nani aliyeziimarisha ncha za dunia yote? Jina lake ni nani, na jina la mtoto wake ni nani? Hakika unajua!
\s5
\v 5 Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
\v 6 Usiyaongezee maneno haya, au atakukemea, na utathibitishwa kuwa mwongo.
\s5
\v 7 Vitu viwili ninakuomba, usivikatalie kwangu kabla sijafa:
\v 8 Majivuno na uongo viweke mbali nami. Usinipe umasikini wala utajiri, nipe tu chakula ninachohitaji.
\v 9 Maana nikipata vingi zaidi, nitakukana wewe na kusema, " Yehova ni nani?" Au kama nitakuwa masikini, nitaiba na kukufuru jina la Mungu wangu.
\s5
\v 10 Usimkashifu mtumwa mbele ya bwana wake, au atakulaani na utapata hatia.
\s5
\v 11 Kizazi ambacho kinachomlaa baba yao na hakimbariki mama yao,
\v 12 kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
\s5
\v 13 Hicho ni kizazi- jinsi gani macho yao yanakiburi na kope zao zimeinuka juu! -
\v 14 kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
\s5
\v 15 Ruba anamabinti wawili, " Toa na Toa" wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, "Inatosha":
\v 16 Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, "Inatosha."
\v 17 Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.
\s5
\v 18 Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu:
\v 19 njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
\s5
\v 20 Hii ni njia ya mzinzi- anakula na kufuta kinywa chake na kusema, "sijafanya ubaya wowote."
\s5
\v 21 Chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka na vinne haiwezi kuvivumilia:
\v 22 mtumwa anapokuwa mfalme; mpumbavu anaposhiba vyakula;
\v 23 mwanamke anayechukiwa anapoolewa; kijakazi anapochukua nafasi ya mkuu wake.
\s5
\v 24 Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara:
\v 25 mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
\v 26 Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba.
\s5
\v 27 Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio.
\v 28 Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.
\s5
\v 29 Kuna vitu vitatu ambavyo ni fahari katika mwendo na vinne ambavyo ni fahari katika namna ya kutembea:
\v 30 simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama- wala hajiepushi na kitu chochote;
\v 31 jogoo anayetembea kwa mikogo; mbuzi; na mfalme ambaye askari wapo kando yake.
\s5
\v 32 Kama umekuwa mpumbavu, jitukuze mwenyewe, au kama umekuwa ukisimamia vibaya- weka mkono wako juu ya kinywa chako.
\v 33 Kama kusuka maziwa hufanya siagi na pua ya mtu hutoa damu kama imepigwa, basi matendo yanayofanywa kwa hasira huzalisha mafarakano.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Maneno ya mfalme Lemueli - mausia aliyofundishwa na mama yake.
\v 2 Mwanangu nini? Na ni nini mwana wa tumbo langu? Na ni nini mwana wa nadhiri zangu?
\v 3 Nguvu zako usiwape wanawake; au wenye kuharibu wafalme njia zako.
\s5
\v 4 Lemueli, kunywa divai, siyo kwa ajili ya wafalme, wala kwa watawala kuuliza, " kileo kikali kiko wapi?"
\v 5 Kwa sababu kama watakunywa, watasahau sheria ni nini, na kupotosha haki za wote walioonewa.
\s5
\v 6 Wape kileo kikali watu wanaopotea na mvinyo kwa wale wenye kutaabika kwa uchungu.
\v 7 Atakunywa na kusahau umasikini wake na hataikumbuka taabu yake.
\s5
\v 8 Ongea kwa ajili yao wasioweza kuongea, kwa madai ya wote wanaopotea.
\v 9 Ongea na uhukumu kwa vipimo vya haki na utetee dai la masikini na watu wahitaji.
\s5
\v 10 Mke hodari ni nani anaweza kumpata? Thamani yake ni zaidi kuliko vito.
\v 11 Moyo wa mume wake humwamini, na hatakuwa masikini.
\v 12 Humtendea mambo mema na wala si mabaya siku zote za maisha yake.
\s5
\v 13 Huchagua sufu na kitani, na hufanya kazi yake ya mikono kwa furaha.
\v 14 Yupo kama meli za wafanyabiashara; huleta chakula chake kutoka mbali.
\v 15 Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike.
\s5
\v 16 Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu.
\v 17 Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake.
\s5
\v 18 Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi.
\v 19 Mikono yake huiweka kwenye mpini wa kisokotea nyuzi na hushikilia kisokotea nyuzi.
\s5
\v 20 Mkono wake huwafikia watu masikini; mikono yake huwafikia watu wahitaji.
\v 21 Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu.
\s5
\v 22 Hutengeneza matandiko ya kitanda chake, na huvaa nguo za kitani ya dhambarau safi.
\v 23 Mume wake anajulikana malangoni, anapoketi na wazee wa nchi.
\s5
\v 24 Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara.
\v 25 Amevaa nguvu na heshima, na wakati ujao huucheka.
\s5
\v 26 Anafumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake.
\v 27 Huangalia njia za nyumba yake na hawezi kula mkate wa uvivu.
\s5
\v 28 Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema,
\v 29 "Wanawake wengi wamefanya vizuri, lakini wewe umewapita wote."
\s5
\v 30 Madaha ni udanganyifu, uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Yehova, atasifiwa.
\v 31 Mpeni tunda la mikono yake na kazi zake zimsifu katika malango.