sw_ulb_rev/19-PSA.usfm

5040 lines
236 KiB
Plaintext

\id PSA
\ide UTF-8
\h Zaburi
\toc1 Zaburi
\toc2 Zaburi
\toc3 psa
\mt Zaburi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha.
\v 2 Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku.
\s5
\v 3 Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa.
\s5
\v 4 Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
\v 5 Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
\s5
\v 6 Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa nini mataifa wanafanya dhoruba, kwa nini watu wanafanya njama ambazo zitafeli?
\v 2 Wafalme wa nchi kwa pamoja hushikilia misimamo yao na watawala kwa pamoja hufanya njama kinyume na Yahwe na kinyume na Masihi, wakisema,
\v 3 "Ngoja tuzikate pingu walizo tufingia sisi na kuzitupa pingu zao."
\s5
\v 4 Yeye aketie katika mbingu atacheka kwa dharau mbele yao; Bwana atawadhihaki wao.
\v 5 Kisha ataongea nao katika hasira yake na kuwaogofya kwa gadhabu yake, akisema,
\s5
\v 6 "Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu."
\v 7 Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, "wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako.
\s5
\v 8 Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako.
\v 9 Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande."
\s5
\v 10 Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe.
\v 11 Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka.
\s5
\v 12 Mumbusu mwana vinginevyo atawakasirikia, na mtakufa pale pale hasira yake ikiwaka. Ni jinsi gani wamebarikiwa wale wote watafutao usalama ndani yake.
\s5
\c 3
\p Zaburi ya Daudi, wakati alipo mkimbia mtoto wake Absalom.
\v 1 Yahewh, maadui zangu wako wangapi! Ni wengi wamekuja kinyume na mimi.
\v 2 Ni wengi wanaonisema, "Hakuna msaada wowote kutoka kwa Mungu kwa ajili yake." Selah
\s5
\v 3 Bali wewe, Yahweh, u ngao yangu pande zote, utukufu wangu, na uniinuaye kichwa changu.
\v 4 Nampazia Yahweh sauti yangu, na yeye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.
\s5
\v 5 Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda.
\v 6 Sitaogopa kusanyiko la watu ambao wamejipanga kinyume na mimi pande zote.
\s5
\v 7 Inuka, Yahweh! Uniokoe, Mungu wangu! Kwa kuwa utawapiga maadui zangu wote kwenye taya zao; utayavunja meno ya waovu.
\v 8 Wokovu unatoka kwa Yahweh. Baraka zako ziwe juu ya watu wako.
\s5
\c 4
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Unijibu nikuitapo, Mungu wa haki yangu; uniokoe niwapo katika hatari. Unihurumie na usikie maombi yangu.
\s5
\v 2 Ninyi watu, mpaka lini mtaiabisha heshima yangu? Mpaka lini mtaendelea kupenda kile kisicho stahili na kutafuta uongo?
\v 3 Lakini mjue ya kuwa Yahweh huchagua watu wa kimungu kwa ajili yake. Nitakapo mwita Yahwe atasikia.
\s5
\v 4 Tetemekeni na kuogopa, lakini msitende dhambi! Tafakarini mioyoni mwenu kwenye vitanda vyenu na muwe kimya.
\v 5 Toeni matoleo ya haki na muweke imani yenu katika Yahweh.
\s5
\v 6 Wengi husema, "Ni nani atakaye tuonyesha chochote kilicho kizuri?" Yahweh, utuangazie nuru ya uso wako.
\v 7 Umeupa moyo wangu furaha kuu kuliko wao wanapozidishiwa nafaka na divai mpaya.
\v 8 Ni amani kuwa nitajilaza na kusinzia, kwako pekee, Yahweh, nifanye kuwa salama kabisa.
\s5
\c 5
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwa vyombo vya upepo. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Sikiliza nikuitapo, Yahweh; tazama kuugua kwangu.
\v 2 Sikiliza sauti yangu nikuitapo, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa kuwa ni kwako Bwana naomba.
\v 3 Yahweh; sikia kilio changu asubuhi; na asubuhi nitaleta dua yangu kwako na kungoja kwa matarajio.
\s5
\v 4 Hakika wewe ni Mungu usiye kubaliana na uovu; watu waovu hawawezi kuwa wageni wako.
\v 5 Wenye kiburi hawata simama katika uwepo wako; wewe unawachukia wote wanaofanya maovu.
\v 6 Nawe utawaharibu waongo; Yahweh huwadharau vurugu na watu wadanganyifu.
\s5
\v 7 Lakini kwangu mimi, kwa sababu ya ukuu na uaminifu wa agano lako, nitakuja nyumbani mwako; na kwa heshima nitakuinamia mbele ya hekalu lako takatifu.
\v 8 Oh Bwana, uniongoze katika haki yako kwa sababu ya adui zangu; usawazishe njia yako mbele yangu.
\s5
\v 9 Kwa kuwa midomoni mwao hamna ukweli; utu wao wa ndani ni mwovu; makoo yao ni kaburi lililo wazi; husifu kinafiki kwa ulimi wao.
\v 10 Mungu, wafanye kuwa na hatia; mipango yao iwe kuanguka kwao! Kwa ajili ya makosa yao mengi uwatoe nje, kwa kuwa wamekuasi wewe.
\s5
\v 11 Bali wale wanao kukimbilia wafurahi; uwafanye wapige kelele kwa shangwe siku zote kwa sababu unawapigania; uwafanye wenye furaha ndani yako, wale walipendao jina lako.
\v 12 Kwa maana utawabariki wenye haki, Yahweh; utawazunguka kwa neema kama ngao.
\s5
\c 6
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi, weka kwenye mtindo wa Sheminith. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahweh, usinikemee ukiwa na hasira au usiniadhibu katika gadhabu yako.
\v 2 Unihurumie, Yahwe, kwa maana ni dhaifu; uniponye, Yahweh, kwa kuwa mifupa yangu ina tikisika.
\s5
\v 3 Moyo wangu pia umesumbuka sana. Lakini wewe, Yahweh, mpaka lini hali hii itaendelea?
\v 4 Rudi, Yahweh! uniokoe. Uniokoe kwa sababu ya uaminifu wa agano lako!
\v 5 kwa kuwa kifoni hakuna kumbukumbu lako. Kuzimuni ni nani atakaye kushukuru?
\s5
\v 6 Nimechoshwa na kuugua kwangu. Ninalowanisha kitanda changu kwa machozi usiku kucha; ninaosha kiti changu kwa machozi.
\v 7 Macho yangu yanafifia kwa kulia sana; yanazidi kuwa dhaifu kwa sababu ya adaui zangu.
\s5
\v 8 Ondokeni kwangu, nyote mtendao maovu; kwa kuwa Yahweh amesikia sauti ya kilio changu.
\v 9 Yahweh amesikia malalamiko yangu kwa ajili ya huruma; Yahweh ameyapokea maombi yangu.
\v 10 Maadui zangu wote wataaibishwa na kuteswa sana. Watarudi nyuma na ghafra kufedheheshwa.
\s5
\c 7
\p Utungo wa muziki wa daudi, ambao alimwimbia Yahwe kuhusu maneno ya Cush Mbenjamini
\v 1 Yahweh Mungu wangu, kwako napata kimbilio! Uninusuru na hao wote wanikimbizao, na uniokoe.
\v 2 Vinginevyo, watanipura kama simba, na kunitawanya viapande vipande na asiwepo mtu wa kuweza kunirudisha katika usalama.
\s5
\v 3 Yawheh Mungu wangu, Sijawahi kufanya kile maadui zangu wanacho sema nilifanya; sina hatia katika mikono yangu.
\v 4 Sijawahi kumkosea mtu yeyote aliye na amani na mimi, au kumdhuru kipumbavu yeyote aliye kinyume na mimi.
\s5
\v 5 Ikiwa sisemi ukweli basi umruhusu adui yangu kuyaingilia maisha yangu na kuyaharibu; na umuache aukanyage mwili wangu ulio hai kwenye aridhi na kuuacha umelala kwa aibu mavumbini. Selah
\s5
\v 6 Inuka, Yahweh, katika hasira yako; simama kinyume na hasira kali ya adui zangu; amka kwa ajili yangu na ubebe amri zako ambazo wewe umeamuru kwa ajili yao.
\v 7 Mataifa yote yamekuzunguka; uwatawale kutoka mbinguni.
\s5
\v 8 Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu.
\v 9 Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu.
\s5
\v 10 Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki.
\v 11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anaye chukizwa na waovu kila siku.
\s5
\v 12 Ikiwa kuna mtu hatubu, Mungu atanoa upanga wake na ata andaa upinde wake kwa ajili ya vita.
\v 13 Ana jiandaa kutumia siraha kupambana naye; anatengeneza mishale yake kuwa ya moto.
\s5
\v 14 Fikiria kuhusu huyo ambaye ana ujauzito wa maovu, mwenye mimba ya mipango ya uharibifu, anaye zaa sumu ya uharibifu.
\v 15 Yeye huchimba shimo na kuliacha wazi kisha baadaye hudumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
\v 16 Mipango yake mwenyewe ya uharibifu hugeukia kichwa chake mwenyewe, kwa kuwa vurugu zake mwenyewe humshukia kichwani pake.
\s5
\v 17 Kwa haki yako Mungu nitakushukuru; nitaimba sifa kwa Mungu aliye juu.
\s5
\c 8
\p Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa gittith. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote, wewe ufunuaye utukufu wako juu mbinguni.
\v 2 Kutoka katika midomo ya watoto na vichanga umeumba sifa kwa sababu ya utukufu wako, ili kuwanyamazisha maadui wote na walipa kisasi wote.
\s5
\v 3 Ninapozitazama mbingu, ambazo vidole vyako vimeumba, mwezi na nyota, ambazo umeziweka kila mmoja katika nafasi yake,
\v 4 Binadamu ni nani hata umtazame, na watu hata uwajali wao?
\v 5 Umewaumba chini kidogo kuliko viumbe vya mbinguni na umewazunguka na utukufu na heshima.
\s5
\v 6 Umemfanya binadamu kutawala kazi ya mikono yako; umeviweka vitu vyote chini ya miguu yake:
\v 7 kondoo na ng'ombe wote, na hata wanyama wa porini,
\v 8 ndege wa angani, na samaki wa baharini, na vyote vipitavyo katika mikondo ya bahari.
\s5
\v 9 Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote!
\s5
\c 9
\p Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa Muth Labben. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nitamshukuru Yahweh kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako makuu.
\v 2 Nitafurahi na kushangilia katika wewe; nitaliimbia jina lako, Wewe uliye juu.
\s5
\v 3 Maadui zangu wanaponirudia, hujikwaa na kuangamia mbele zako.
\v 4 Kwa kuwa umenitetea kwa haki; unakaa kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki!
\s5
\v 5 Uliwakemea mataifa; umewaharibu waovu; na kuwa futilia mbali jina lao milele na milele.
\v 6 Maadui wamebomoka kama magofu ulipo pindua miji yao. Kumbukumbu yao yote imepotea.
\s5
\v 7 Bali Yahweh anadumu milele; ameweka kiti chake cha enzi kwa ajili ya haki.
\v 8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki, na atatekeleza hukumu kwa ajili ya mataifa kwa haki.
\s5
\v 9 Yahweh pia atakuwa ngome kwake aliye onewa, na ngome wakati wa shida.
\v 10 Wale wakujuao jina lako wanaamini katika Wewe, kwa ajili yako, Yahweh, usiwaache wale wakutafutao.
\s5
\v 11 Mwibieni sifa Yahweh, anaye tawala katika Sayuni; waambieni mataifa yale aliyo yatenda.
\v 12 Kwa kuwa Mungu alipizae kisasi cha damu hukumbuka; naye hasahau kilio cha anayeonewa.
\s5
\v 13 Unihurumie, Yahweh; tazama vile ninavyo onewa na wale wanao nichukia, wewe ambaye unaweza kunikwapua katika lango la kifo.
\v 14 Oh, ili niweze kutangaza sifa zako. Katika lango la binti sayuni nitaufurahia wokovu wako!
\s5
\v 15 Mataifa yamedidimia chini katika shimo ambalo walilolitengeneza; miguu yao imenaswa kwenye nyavu walioificha wenyewe.
\v 16 Yahweh amejidhihilisha; na kutekeleza hukumu; waovu wameangamia kwa matendo yao wenyewe. Selah
\s5
\v 17 Waovu wamekataliwa na kupelekwa kuzimu, mataifa yote yanayo msahau Mungu.
\v 18 Kwa kuwa mhitaji hata sahauliwa siku zote, wala matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
\s5
\v 19 Inuka, Yahweh, usimruhusu mtu kutushinda; mataifa na wahukumiwe mbele zako.
\v 20 Bwana, waogopeshe; mataifa waweze kutambua kuwa ni wanadamu tu. Selah
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kwa nini, Yahweh, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?
\v 2 Kwa sababu ya majivuno yao, watu waovu waawakimbiza wanyonge; Basi tafadhari uwafanye waovu kunaswa kwa mipango yao wenyewe walioipanga.
\v 3 Kwa kuwa mtu mwovu hujivuna kwa tamaa yake ya ndani; yeye hufurahisha tamaa na kumtusi Yahweh.
\s5
\v 4 Mtu mwovu ameinua uso wake; naye hamtafuti Mungu. Yeye hamfikilii Mungu kamwe kwa kuwa hamjali kabisa Mungu.
\v 5 Yeye yuko salama wakati wote, amri zako za haki ziko juu sana kwake; naye huwadharau adui zake wote.
\s5
\v 6 Yeye husema moyoni mwake, "Siwezi kamwe kushindwa; katika kizazi chote sitakutana na shida."
\v 7 Mdomoni mwake kumejaa kulaani na udanganyifu, maneno yenye sumu; ulimi wake unajeruhi na kuharibu.
\s5
\v 8 Yeye husubilia kwenye shambulio karibu na kijiji; mahali pa siri huwauwa watu wasio na hatia; macho yake huwatazama wasionahatia.
\v 9 Hujibanza mahari pa siri kama simba katika kichaka; yeye hulala akisubiri kumkamata mnyonge. Humkamata pale anapokwisha mweka mtegoni mwake.
\v 10 Wanyonge wake hugandamizwa chini na kupigwa; wao huangukia katika mtego imara.
\s5
\v 11 Yeye husema katika moyo wake, "Mungu amesahau; huficha uso wake; hawezi kujishughulisha kutazama."
\v 12 Inuka, Yahweh! Inua mkono wako, Mungu! Usiwasahau wanyonge.
\s5
\v 13 Kwa nini mtu mwovu anamkataa Mungu na kusema moyoni mwake, "Hautanipata katika hatia?"
\v 14 Umeona, maana mara zote unaangalia mtu aletaye madhara na jeuri. Mtu asiye na msaada hukuachia nafsi yake; maana wewe huwaokoa yatima.
\s5
\v 15 vunja mkono wa mwovu lo na mtu mwovu. Umuajibishe kwa matendo yake maovu, ambayo kwayo alifikiri hautayagundua.
\v 16 Yahweh ni mfalme milele daima; mataifa yanaondolewa katika aridhi yake.
\s5
\v 17 Yahweh, umesikia uhitaji wa wanyonge; nawe umeitia nguvu mioyo yao, wewe unasikia maombi;
\v 18 Unawatetea yatima na wanyonge ili kusudi pasiwepo na mtu katika dunia hii atakaye leta hofu tena.
\s5
\c 11
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi.
\v 1 Ni kwako Yahweh ninapata usalama; ni kwa namna gani utasema na mimi, "Ruka kama ndege hadi mlimani"?
\v 2 Tazama! Waovu wana andaa pinde zao. Wana tayarisha gizani mishale yao kwenye kamba ili kufyatua mioyo ya wenye haki.
\s5
\v 3 Ikiwa misingi imeharibiwa, mwenye haki atafanya nini?
\v 4 Yahweh yuko katika hekalu takatifu; macho yake yanatazama, yakiuchunguza ubinadamu.
\s5
\v 5 Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine.
\v 6 Yeye huwanyeshea waovu makaa ya mawe na moto wa jehanamu; upepo uunguzao utakuwa ni sehemu yao kutoka katika kikombe chake!
\v 7 Kwa kuwa Yahweh ni mwenye haki, Naye hupenda haki; wenye haki watauona uso wake.
\s5
\c 12
\p Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye Sheminith. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Msaada, Yahweh, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; nao waaminifu wametokomea.
\s5
\v 2 Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu.
\v 3 Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa.
\v 4 Hawa ni wale ambao wamesema, "Kwa ndimi zetu tutashinda. Wakati midomo yetu itakapo ongea, ni nani atakaye kuwa mtawala juu yetu?"
\s5
\v 5 "Kwa sababu ya vurugu zilizopo kinyume na maskini, na kwa sababu ya kuugua kwao wahitaji, Nitainuka," asema Yahwe. "Nitawaletea usalama wanao hitaji."
\s5
\v 6 Maneno ya Yahwe ni masafi, kama fedha iliyo safishwa katika tanuru duniani, iliyo ng'arishwa mara saba zaidi.
\v 7 Wewe ni Yahwe! Unaye watunza. Una wahifadhi wacha Mungu kutoka katika hiki kizazi cha waovu na hata milele.
\v 8 Waovu hutembea kila pande pale uovu unapoinuliwa kati ya wanadamu.
\s5
\c 13
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone?
\v 2 Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida?
\s5
\v 3 Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti.
\v 4 Usimuache adui yangu aseme, "Nimemshinda huyu," ili kwamba asiweze kusema, "Nimemtawala adui yangu;" la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini.
\s5
\v 5 Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako.
\v 6 Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.
\s5
\c 14
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Mpumbavu husema moyoni mwake, "Hakuna Mungu." Wamepotoka nakufanya uovu haramu; hakuna hata mmoja atendaye dhambi.
\s5
\v 2 Yahwe anatazama chini kwa wanadamu kutoka mbinguni aone kama kuna yeyote anayeelewa, amtafutaye Mungu.
\v 3 Wote wamegeukia njia nyingine. Kwa pamoja wamepotoka. Hakuna yeyote atendaye mema, hakuna, hata mmoja.
\s5
\v 4 Je, hawajui lolote, wale wafanyao uovu, wale wanao kula watu wangu kama vile wanakula mkate, lakini hao hawamuiti Yahwe?
\s5
\v 5 Wao wana tetemeka kwa hofu. Kwa kuwa Mungu yuko pamoja na kusanyiko la wenye haki!
\v 6 Ninyi mnataka kumfedhehesha mtu maskini japo kuwa Yahwe ni kimbilio lake.
\s5
\v 7 Oh, kwamba wokovu wa Israeli ungetokea Sayuni! Wakati Yahwe akiwarudisha watu wake kutoka utumwani, ndipo Yakobo atashangilia na Israeli itakuwa na furaha!
\s5
\c 15
\p
\v 1 Zaburi ya Daudi. Yahwe, ni nani atabaki hemani mwako? Ni nani atakaye ishi kwenye mlima wako mtakatifu?
\v 2 Yeyote anaye tembea bila lawama, yeye hufanya kilicho haki na huongea ukweli kutoka moyoni mwake.
\s5
\v 3 Yeye huwa hakashfu kwa ulimi wake, hawadhuru wengine, na hamtusi jirani yake.
\s5
\v 4 Mtu asiye na maana hudharauliwa machoni pake, bali yeye huwaheshimu wale wanao mhofu Yahwe. Yeye huapa kwa hasara yake mwenyewe na habadilishi ahadi yake.
\v 5 Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.
\s5
\c 16
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Unilinde, Mungu, kwa kuwa nakimbilia kwako kwa ajili ya usalama.
\v 2 Nami ninasema kwa Yahwe, "Wewe ni Bwana wangu; wema wangu ni bure pasipo wewe.
\v 3 Kama kwa watakatifu walioko duniani, ndio walio bora; furaha yangu yote iko kwao.
\s5
\v 4 Taabu yao itaongezeka, wale watafutao miungu mingine. Sitamimina sadaka ya damu kwa miungu yao. Wala kuyainua majina yao kwa midomo yao.
\s5
\v 5 Yahwe, wewe ni sehemu ya chaguo langu na kikombe changu. Unaishikilia kesho yangu.
\v 6 Mistari iliyo pimwa imelelazwa mahari pa kufurahisha kwa ajili yangu; hakika urithi ufurahishao ni wangu.
\s5
\v 7 Nitakubariki Yahwe, wewe unishauliye; hata wakati wa usiku akili zangu za nielekeza.
\v 8 Nimemuweka Yahwe mbele yangu kila wakati, ili nisitikisike kutoka mkono wake wa kuume.
\s5
\v 9 Kwa hiyo moyo wangu unafuraha, utukufu wangu washangilia. Hakika nitaishi katika usalama.
\v 10 Kwa kuwa hautaiacha roho yangu kuzimuni. Wewe hautamuacha mwaminifu wako kuliona shimo.
\s5
\v 11 Wewe hunifundisha njia ya maisha; furaha tele inakaa katika uwepo wako; furaha inakaa katika mkono wako wa kuume milele!"
\s5
\c 17
\p
\v 1 Maombi ya Daudi. Sikia ombi langu kwa ajili ya haki, Yawhe; uusikilize mwito wangu wa msaada. Uyasikilize maombi yangu yatokayo katika midomo isiyo na udanganyifu.
\v 2 Uthibitisho wangu na uje kutoka uweponi mwako; macho yako na yaone kile kilicho sahihi!
\s5
\v 3 Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria.
\s5
\v 4 Kama kwa matendo ya binadamu, ni katika neno la midomo yako ya kuwa nimejiepusha na njia za wahalifu.
\v 5 Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza.
\s5
\v 6 Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea.
\v 7 Onyesha uaminifu wa agano lako katika namna ya ajabu, wewe uokoaye kwa mkono wa haki yako wale wanao kukimbilia wewe kutoka kwa adui zao.
\s5
\v 8 Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako
\v 9 kutoka katika uwepo wa waovu ambao wananitusi, adui zangu wanizungukao.
\v 10 Wao hawana huruma kwa yeyote; midomo yao huongea kwa majivuno.
\s5
\v 11 Wao wame zizunguka hatua zangu. Wamekaza macho yao wanishambulie mpaka ardhini.
\v 12 Wao ni kama mfano wa hasira ya simba mawindoni. Ni kama simba kijana anapotokea mafichoni.
\s5
\v 13 Inuka, Yahwe! Uwashambulie! Uwaangushe chini kwenye nyuso zao! Uyaokoe maisha yangu kutokana na waovu kwa upanga wako!
\v 14 Uniokoe kutoka kwa watu hawa kwa mkono wako, Yahwe, kutoka kwa watu wa dunia hii ambao utajiri wao ni maisha haya pekee! Wewe utayajaza matumbo ya wale uwathaminio na utajiri; watakuwa na watoto wengi na wataacha utajiri wao kwa watoto wao.
\s5
\v 15 Bali mimi, nitauona uso wako katika haki; Nitashuhudiwa, pale nitakapo amka, na macho yako.
\s5
\c 18
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi, mtumishi wa Yahwe, alipomwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu katika ile siku ambayo Yahwe alimuokoa kutoka katika mkono wa adui zake wote na kutoka katika mkono wa Sauli. Yeye aliimba:
\v 1 Nakupenda, Yahwe, nguvu yangu.
\s5
\v 2 Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, yeye ambaye aniwekae kweye usalama; yeye ni Mungu wangu, mwamba wangu; ninapata kimbilio kwake. Yeye ni ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
\v 3 Nitamuita Yahwe kwa sababu anastahili kusifiwa, na nitaokolewa kutoka kwa adui zangu.
\s5
\v 4 Kamba za mauti zilinizunguka, na mafuriko yakimbiayo yalinielemea.
\v 5 Kamba za kuzimu zilinizunguka; mitego ya mauti ilininasa.
\s5
\v 6 dhiki yangu nilimuita Yahwe; Niliita msaada kwa Mungu. Naye alisikia sauti yangu kutoka hekaluni mwake; kuita kwangu msaada kulienda mpaka uweponi mwake; na kuingia masikioni pake.
\s5
\v 7 Kisha nchi ikatikisika na kutetemeka; misingi ya milima pia ilitetemeka na kutikiswa kwa sababu Mungu alikuwa amekasirika.
\v 8 Moshi ulifuka kutoka kwenye pua zake, na moto mkali ulitokea mdomoni mwake. Makaa yaliwashwa kwa moto huo.
\s5
\v 9 Yeye alizifunua mbingu na alishuka chini, na giza nene lilikuwa chini ya miguu yake.
\v 10 Alipanda kwenye kerubi na akaruka; alinyiririka kwenye mabawa ya upepo.
\s5
\v 11 Yahwe alilifanya giza kuwa hema likimzunguka yeye, wingu la mvua zito katika mbingu.
\v 12 Mawe ya barafu na makaa ya moto yalianguka kutoka katika mwangaza kabla yake.
\s5
\v 13 Yahwe aliongea katika mbingu! Sauti ya aliye juu ilisikika.
\v 14 Yeye aliifyatua mishale yake na kuwatawanya adui zake; na radi nyingi zenye mwanga alizitawanya katika maeneo tofauti tofauti.
\s5
\v 15 Ndipo mifereji ya maji ilitokea; misingi ya dunia ikadhihirishwa kwa mlio wa pigo lako, Yahwe kwa sauti ya pumzi ya pua zako.
\s5
\v 16 Yeye alishuka chini kutokea juu; akanishikilia mimi! Akanivuta nje ya maji yafurikayo.
\v 17 Aliniokoa kutoka kwa maadui zangu wenye nguvu, kutoka kwa wale ambao walinichukia mimi, kwa kuwa walikuwa na nguvu sana kuliko mimi.
\s5
\v 18 Wao walikuja kinyume na mimi katika siku ile ya dhiki yangu lakini Mungu alikuwa msaada wangu!
\v 19 Yeye aliniweka huru katika eneo pana la wazi; yeye aliniokoa kwa sababu alipenezwa nami.
\s5
\v 20 Yahwe amenitunuku mimi kwa sababu ya haki yangu; yeye amenirejesha mimi kwa sababu mikono yangu ilikuwa misafi.
\v 21 Kwa kuwa nimezitunza njia za Yahwe na sijafanya uovu wa kumgeuka Mungu wangu.
\s5
\v 22 Kwa kuwa amri zake zote za haki zimekuwa mbele yangu; kama asemavyo, sijaenda kinyume nazo.
\v 23 Pia nimekuwa sina hatia mbele zake, na nimejiweka mwenyewe mbali na dhambi.
\v 24 Hivyo Yahwe amenirejesha kwa sababu ya haki yangu, na kwa sababu mikono yangu ilikuwa safi mbele ya macho yake.
\s5
\v 25 Kwa yeyote aliye mwaminifu, jionyeshe wenyewe kuwa mwaminifu; kwa mtu asiye na lawama, jionyeshe mwenyewe kuwa usiye na lawama.
\v 26 Kwa yeyote aliye msafi, jionyeshe mwenyewe safi; bali ni mjanja kwa yeyote aliye geuzwa.
\s5
\v 27 Kwa kuwa wewe huwaokoa watu walio taabishwa, lakini wewe huwashusha chini wale wenye majivuno, yaani macho yaliyo jinua!
\v 28 Kwa kuwa wewe huipa mwanga taa yangu; Yahwe Mungu wangu hutia mwanga giza langu.
\v 29 Kwa kuwa kwa kupitia wewe ninaweza kuruka juu ya kiwazo kilichowekwa; kupitia Mungu ninaweza kuruka juu ya ukuta.
\s5
\v 30 Kama kwa Mungu: njia yake ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi! Yeye ni ngao kwa yeyote anaye kimbilia katika yeye.
\v 31 Kwa kuwa nani ni Mungu ispokuwa Yahwe? Nani ndiye mwamba ispokuwa Mungu wetu?
\v 32 Ni Mungu anitiaye nguvu ndani yangu kama vile mkanda, ambaye humweka mtu mwenye lawama katika njia yake.
\s5
\v 33 Yeye hunifanya miguu yangu kuwa myepesi kama mbawala na kuniweka mahali pa juu!
\v 34 Yeye hufunza viganja vyangu kwa ajili ya vita na mikono yangu kupiga upinde wa shaba.
\s5
\v 35 Wewe umenipa mimi ngao ya wokovu. Mkono wako wa kuume umenisaidia, na neema yako imenifanya kuwa mkubwa.
\v 36 Wewe umetengeneza nafasi pana kwa ajili ya miguu yangu ili miguu yangu isiteleze.
\s5
\v 37 Ninawashawishi adui zangu na kuwakamata; nami sikurudi nyuma mpaka walipo haribiwa.
\v 38 Niliwashambulia hata hawakuweza kuamka; nao wameangukia chini ya miguu yangu.
\v 39 Kwa kuwa unanitia nguvu kama mshipi kwa ajili ya vita; wewe unawaweka chini yangu wale ambao wanainuka kinyume na mimi.
\s5
\v 40 Wewe ulinipa visogo vya maadui zangu; niliwaagamiza wale walio nichukia.
\v 41 Wao waliita msaada lakini hakuna aliye wasaidia; walimuita Yahwe, lakini hakuwaitikia.
\v 42 Niliwapiga wao katika vipande vidogo vidogo kama vile vumbi mbele ya upepo; niliwatupa nje kama udongo mtaani.
\s5
\v 43 Wewe uliniokoa mimi kutoka katika migogoro ya watu. wewe umenifanya kichwa juu ya mataifa. Watu ambao sikuwahi kuwafahamu huntumikia.
\v 44 Pindi tu waliposikia kuhusu mimi, wao walinitii; wageni walilazimishwa kunisujudu.
\v 45 Wageni walitoka kwenye ngome yao wakitetemeka.
\s5
\v 46 Yahwe anaishi; mwamba wangu usifiwe. Ainuliwe Mungu wa wokovu wangu.
\v 47 Yeye ni Mungu ambaye hutelekeza visasi kwa ajili yangu, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.
\s5
\v 48 Nimewekwa huru kutoka kwa adui zangu! wewe uliniinua juu ya wale walioinuka kunyume na mimi! Wewe uliniokoa kutoka kwa watu wenye vurugu.
\v 49 Kwa hiyo nitakushukuru wewe, Yahwe, kati ya mataifa; Nitaliimbia sifa jina lako!
\s5
\v 50 Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na yeye huonyesha uaminifu wa agano lake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na ukoo wake milele.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane!
\v 2 Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa.
\v 3 Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki.
\s5
\v 4 Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao.
\v 5 Jua liko kama mfano wa bwana harusi akitokea chumbani kwake na kama mtu shujaa ambaye hushangila pale anapokimbia mbio zake.
\v 6 Jua huchomoza kutokea upeo wa macho na likikatisha winguni kwenda jingine; hakuna chochote kinacho epuka joto lake.
\s5
\v 7 Sheria ya Yahwe ni kamilifu, huokoa roho; ushuhuda wa Yahwe ni wa kuaminika, ukifanya hekima nyepesi.
\v 8 Maelekezo ya Yahwe ni ya hakika, yakiufanya moyo kuwa na furaha; amri ya Yahwe ni safi, ikileta mwanga kwenye macho yetu.
\s5
\v 9 Hofu ya Yahwe ni safi, inadumu milele; amri za haki ya Yahwe ni za kweli na zote ni za hakika!
\v 10 Nazo zina thamani kuliko dhahabu, nazo ni tamu kuliko asali na matone ya asali kutoka sega la asali (sega la nyuki).
\s5
\v 11 Ndiyo, kupitia hizo mtumishi wako anaonywa; na katika kuziamini kuna thawabu.
\v 12 Ni nani ambaye aweza kuyatambua makosa yake yote mwenyewe? Unitakase makosa yaliyo fichika.
\s5
\v 13 Pia umuepushe mtumishi wako na dhambi za majivuno; usiziruhusu kunitawala. Ndipo nitakuwa mkamilifu, na mimi sitakuwa na hatia ya makosa mengi.
\v 14 Maneno ya midomo yangu na mawazo ya moyo wangu nayakubalike machoni pako, ewe Yahwe, mwamba wangu na mkombozi wangu.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde
\v 2 na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni.
\s5
\v 3 Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa.
\v 4 Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.
\s5
\v 5 Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki.
\v 6 Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye.
\s5
\v 7 Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu.
\v 8 Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima!
\s5
\v 9 Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mfalme anashangilia katika uweza wako, Yahwe! Ni kwa namna kuu anashangilia katika wokovu uliouleta!
\v 2 Wewe umempa yeye matamanio ya moyo wake na hauja mkatalia maombi midomo yake.
\s5
\v 3 Kwa kuwa wewe unamletea baraka nyingi; wewe uliweka katika kichwa chake taji ya dhahabu iliyo safi kabisa.
\v 4 Yeye alikuomba wewe maisha; ukampatia maisha; wewe ulimpatia maisha malefu milele na milele.
\s5
\v 5 Yeye utukufu wake ni mkuu kwa sababu ya ushindi wako; wewe umemuwekea mapambo na enzi.
\v 6 Kwa kuwa unampatia yeye baraka za kudumu; unamfurahisha kwa furaha ya uwepo wako.
\s5
\v 7 Kwa kuwa Mfalme humwamini Yahwe; kwa kupitia uaminifu wa agano la aliye juu zaidi yeye hataondolewa.
\v 8 Mkono wako utawakamata adui zangu wote wote; mkono wako wa kuume utawakamata wale wote wanao kuchukia.
\s5
\v 9 Wakati wa hasira yako, wewe utawachoma kama katika tanuru la moto. Yahwe atawamaliza wao katika hasira yake, na moto utawateketeza upesi wao.
\v 10 Wewe utawaangamiza watoto wao duniani na ukoo wao kutoka katika mrorongo wa wanadamu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa walikusudia kukufanyia mambo maovu wewe; wao walitunga njama ambayo kwayo hawawezi kufanikiwa!
\v 12 Kwa kuwa wewe utawarudisha nyuma; wewe utafyatua upinde wako mbele yao.
\s5
\v 13 Uninuliwe, Yahwe, katika uweza wako; tutaimba na kusifu nguvu zako.
\s5
\c 22
\p Kwa kiongozi wa muziki; "aina ya muziki wa deer." Zaburi ya Daudi.
\v 1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali na wokovu wangu na mbali na maneno yangu yenye uchungu?
\v 2 Mungu wangu, ninalia mchana kutwa, lakini haunijibu, na wakati wa usiku sinyamazi!
\s5
\v 3 Bado wewe ni mtakatifu; wewe umekaa kama mfalme pamoja na sifa za Israeli.
\v 4 Mababu zetu walikuamini wewe, na wewe uliwaokoa wao.
\v 5 Walikulilia wewe nao waka okolewa. Wao walikuamini wewe na hawakuvunjwa moyo.
\s5
\v 6 Bali mimi ni funza na sio mtu, nisiye faa kwa ubinadamu na hudharauliwa na watu.
\v 7 Wale wote wanionao hunisuta; hunidhihaki; hunitikisia vichwa vyao.
\v 8 Wao husema, "Yeye anamwamini Yahwe; mwache Yahwe amuokoe. Mwache amuokoe yeye, kwa kuwa yeye anampendeza sana Yeye."
\s5
\v 9 Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.
\v 10 Nimekwisha tupwa kwako wewe tokea tumboni; wewe ni Mungu wangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!
\s5
\v 11 Usiwe mbali na mimi, kwa kuwa shida ikaribu; hayupo hata mmoja wa kusaidia.
\v 12 Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
\v 13 Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
\s5
\v 14 Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
\v 15 Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
\s5
\v 16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
\v 17 Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
\s5
\v 18 Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
\v 19 Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
\s5
\v 20 Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
\v 21 Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
\s5
\v 22 Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.
\v 23 Ninyi mnao mwogopa Yahwe, msifuni yeye! Ninyi nyote kizazi cha Yakobo, muheshimuni yeye! Simameni katika hofu yake, ninyi nyote kizazi cha Israeli!
\s5
\v 24 Kwa kuwa haja dharau au kuchukia mateso ya aliye taabishwa; Yahwe hajamficha uso wake yeye; pindi wale walio taabishwa walipo mlilia yeye, yeye alisikia.
\v 25 Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
\s5
\v 26 Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
\v 27 Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
\s5
\v 28 Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa.
\v 29 Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe.
\s5
\v 30 Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana.
\v 31 Wao watakuja na kuzungumza kuhusu haki yake; wao watawaambia watu ambao bado hawaja zaliwa yale ambayo Yahwe ameyafanya!
\s5
\c 23
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahwe ni mchungaji wangu; sita pungukiwa na kitu.
\v 2 Yeye hunilaza katika majani mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu.
\s5
\v 3 Yeye huurejesha uhai wangu; huniongoza katika njia iliyo sahihi kwa ajili ya jina lake.
\s5
\v 4 Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji.
\s5
\v 5 Wewe waandaa meza mbele yangu katika uwepo wa maadui zangu; umenipaka mafuta kichwa changu na kikombe changu kinafurika.
\s5
\v 6 Hakika wema na uaminifu wa agano vitaniandama siku zote za maisha yangu; nami nitaishi katika nyumba ya Yahwe milele!
\s5
\c 24
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake.
\v 2 Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito.
\s5
\v 3 Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake?
\v 4 Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya.
\s5
\v 5 Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake.
\v 6 Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.
\s5
\v 7 Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia!
\v 8 Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe, mwenye nguvu na uweza; Yahwe, mwenye uweza katika vita.
\s5
\v 9 Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia!
\v 10 Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe wa majeshi, yeye ni Mfalme wa utukufu.
\s5
\c 25
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Kwako, Yahwe, nayainua maisha yangu!
\v 2 Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu.
\v 3 Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
\s5
\v 4 Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
\v 5 Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.
\s5
\v 6 Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote.
\v 7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe!
\s5
\v 8 Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi.
\v 9 Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
\s5
\v 10 Njia zote za Yahwe ni za upendo wa kudumu na niaminifu kwa wote wanao tunza agano na maagizo ya amri zake.
\v 11 Kwa ajili ya jina lako, Yahwe, unisamehe dhambi zangu, kwa kuwa ni nyingi mno.
\s5
\v 12 Ni nani ambaye anamuogopa Yahwe? Bwana atamfundisha yeye katika njia ambayo anapaswa kuichagua.
\v 13 Maisha yake yataenenda katika uzuri; na uzao wake utairithi nchi.
\s5
\v 14 Urafiki wa Yahwe ni kwa ajili ya wale wanao mheshimu yeye, naye hulifanya agano lake lijulikane kwao.
\v 15 Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
\v 16 Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
\s5
\v 17 Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
\v 18 Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
\v 19 Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.
\s5
\v 20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe; usiniache niaibishwe, Kwa kuwa kwako nakimbilia usalama!
\v 21 Uadilifu na unyofu vinihifadhi, kwa kuwa nina kutumainia wewe.
\s5
\v 22 Mungu, uiokoe Israeli, na shida yake yote!
\s5
\c 26
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Unihukumu mimi, Yahwe, kwa kuwa nimeenenda katika uadilifu; nimeamini katika Yahwe bila kusita.
\v 2 Unichunguze, Yahwe, na unijaribu; uujaribu usafi wa sehemu zangu za ndani na moyoni mwangu!
\v 3 Kwa maana uaminifu wa agano lako uko mbele ya macho yangu, na mwenendo wangu ni katika uaminifu wako.
\s5
\v 4 Mimi sichangamani na watu waovu, wala sichangamani na watu wanafiki.
\v 5 Ninachukia waovu, na siishi na waovu.
\s5
\v 6 Ninaosha mikono yangu kounesha sina hatia, na kuikaribia madhabahu yako, Yahwe,
\v 7 kuimba wimbo wa sauti ya sifa na kutoa taarifa ya matendo yako yote ya ajabu.
\v 8 Yahwe, ninaipenda nyumba ninayoishi, mahali ambapo utukufu wako unaishi!
\s5
\v 9 Usiniangamize pamoja na wenye dhambi, au maisha yangu na watu wenye kiu ya kumwaga damu,
\v 10 ambao katika mikono yao kuna njama, na ambao mkono wa kuume umejaa rushwa.
\s5
\v 11 Lakini kwangu mimi, nitaenenda katika uadilifu; uniokoe na unihurumie.
\v 12 Miguu yangu husimama sehemu salama; katika kusanyiko la watu nitambariki Yahwe!
\s5
\c 27
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahwe ni nuru yangu na wokovu wangu; nimuogope nani? Yahwe ni salama ya maisha yangu; ni mhofu nani?
\s5
\v 2 Wakati waovu waliponijia kunila mwili wangu, wapinzani wangu na adui zangu walijikwaa na wakaanguka.
\v 3 Ingawa jeshi hujipanga kupigana na mimi, moyo wangu hautaogopa; japo vita vijapo inuka kupigana nami hata hapo nitabaki kuwa jasiri.
\s5
\v 4 Kitu kimoja nimekiomba kwa Yahwe, nami nitakitafuta hicho: kwamba niweze kukaa katika nyumba ya Yahwe siku zote za maisha yangu, kuutazama uzuri wa Yahwe na kutafakari hekaruni mwake.
\s5
\v 5 Kwa kuwa katika siku ya shida atanificha nyumbani mwake; atanificha katika mfuniko wa hema lake. Yeye ataniinua juu ya mwamba!
\v 6 Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya maadui wote wanizungukao, nami nitatoa sadaka ya furaha hemani mwake! Nitaimba na kutunga nyimbo kwa Yahwe!
\s5
\v 7 Sikia, sauti yangu nikuitapo, Yahwe! Unihurumie, na unijibu!
\v 8 Moyo wangu huongea kuhusu wewe, "Utafute uso wake!" Nami nautafuta uso wako, Yahwe!
\s5
\v 9 Usiufiche uso wako mbali na mimi; usinikasirikie mimi mtumishi wako! Wewe umekuwa msaada wangu; usiniache wala kunitelekeza, Mungu wa wokovu wangu!
\v 10 Hata kama baba yangu na mama yangu wakiniacha, Yahwe utanitunza kwako.
\s5
\v 11 Unifundishe njia yako, Yahwe! Kwa sababu ya adui zangu uniongoze katika njia salama.
\v 12 Usiwaache adui zangu wanifanyie watamanivyo, kwa sababu mashahidi wa uongo wameinuka kinyume namimi, nao wanapumua vurugu!
\s5
\v 13 Kitu gani kingeweza kunitokea kama nisingeamini kuwa nitauona uzuri wa Yahwe katika nchi ya walio hai?
\v 14 Umngoje Yahwe; uwe imara, na moyo wako uwe jasiri! Umngoje Yahwe!
\s5
\c 28
\p Zaburi ya Daudi. Kwako,
\v 1 Yahwe, ninalia; mwamba wangu, usinipuuze. Ikiwa haunijibu, nitaungana na wale waendao chini kaburini.
\v 2 Sikia kilio cha kusihi kwangu pale niitapo msaada kutoka kwako, niinuapo mikono yangu mbele ya mahali patakatifu zaidi!
\s5
\v 3 Usiniburute pamoja na waovu, wale wafanyao uovu, waongeao amani na majirani zao lakini mioyoni mwao mna uovu.
\v 4 Uwape kulingana na sitahili ya matendo yao na uwalipe kulingana na madai ya maovu yao, uwalipe kwa ajili ya kazi ya mikono yao na uwape kile wanachostahili.
\v 5 Kwa sababu hawayaelewi matendo ya Yahwe wala kazi ya mikono yake, atawakanyaga kanyaga chini na hata wajenga tena wao.
\s5
\v 6 Abarikiwe Yahwe kwa sababu yeye amesikia sauti ya kusihi kwangu!
\v 7 Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba.
\v 8 Yahwe ni nguvu ya watu wake, naye ni mkombozi salama wa wapakwa mafuta wake.
\s5
\v 9 Uwaokoe watu wako na uwabariki warithi wako. Uwe mchungaji wao na uwabebe milele.
\s5
\c 29
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Mpeni sifa Yahwe, enyi wana wa Mungu! Mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu.
\v 2 Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili. Mpigieni magoti Yahwe katika mapambo ya utakatifu.
\s5
\v 3 Sauti ya Yahwe imesikika zaidi ya maji; Mungu wa radi ya utukufu, radi yaYahwe i juu ya maji mengi.
\v 4 Sauti ya Yahwe ina nguvu; sauti ya Yahwe ni kuu.
\v 5 Sauti ya Yahwe huivunja mierezi; Yahwe huivunja vipande vipande mierezi ya Lebanon.
\s5
\v 6 Yeye huifanya Lebanoni kuruka kama ndama wa ng'ombe na Sirioni kama mwana wa nyati.
\v 7 Sauti ya Yahwe hutoa miale ya moto.
\v 8 Sauti ya Yahwe hutetemesha Jangwa; Yahwe hutetemesha jangwa la Kadeshi.
\s5
\v 9 Sauti ya Yahwe huufanya miti mikubwa kutikisika na huipukutisha misitu. Kila mmoja katika hekalu lake husema, "Utukufu!"
\v 10 Yahwe hukaa kama mfalme juu ya mafuriko; Yahwe hukaa kama mfalme milele.
\s5
\v 11 Yahwe huwatia nguvu watu wake; Yahwe huwa bariki watu wake na amani.
\s5
\c 30
\p Zaburi; wimbo wakati wa kuweka wakifu hekalu. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nitakutukuza wewe, Yahwe, kwa kuwa umeniinua na haujawaruhusu maadui zangu juu yangu.
\v 2 Yahwe Mungu wangu, nilikulilia wewe kwa ajili ya msaada, nawe ukaniponya.
\v 3 Yahwe, wewe umeitoa roho yangu kuzimuni; nawe umeniweka hai mbali na kaburi.
\s5
\v 4 Mwimbieni sifa Yahwe, ninyi waaminifu wake! Mshukuruni Bwana mkumbukapo utakatifu wake.
\v 5 Kwa kuwa hasira yake ni ya muda tu; bali neema yake yadumu milele. Kilio huja usiku, bali furaha huja asubuhi.
\s5
\v 6 Kwa ujasiri nilisema, "Sitatikiswa kamwe."
\v 7 Yahwe, kwa neema yako uliniweka mimi kama mlima imara; lakini ulipouficha uso wako, nilisumbuka.
\v 8 Nilikulilia wewe, Yahwe, na kuomba msaada kwa Bwana wangu!
\s5
\v 9 Kuna faida gani katika kifo changu, kama nitaenda kaburini? Je, mavumbi yatakusifu wewe? Yatatangaza uaminifu wako?
\v 10 Sikia, Yahwe, na unihurumie! Yahwe, uwe msaidizi wangu.
\s5
\v 11 Wewe umegeuza kuomboleza kwangu kuwa kucheza; wewe umeyaondoa mavazi yangu ya magunia na kunivisha furaha.
\v 12 Hivyo sasa utukufu wangu utakuimbia sifa wewe na hautanyamaza; Yahwe Mungu wangu, nitakushukuru wewe milele!
\s5
\c 31
\p
\v 1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. In wewe, Yahwe, nakimbilia usalama; usiniache niaibishwe. Katika haki yako uniokoe.
\v 2 Unisikie; uniokoe haraka; uwe mwamba wangu wa usalama, ngome ya kuniokoa.
\s5
\v 3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu; kwa hiyo kwa ajili ya jina lako, uniongoze na unielekeze.
\v 4 Unitoe katika mtego ambao wameuficha kwa ajili yangu, kwa kuwa wewe ni usalama wangu.
\s5
\v 5 Mikononi mwako naikabidhi roho yangu; nawe utaniokoa, Yahwe, mwenye kuaminika.
\v 6 Ninawachukia wale wanaotumikia miungu isiyo na maana, bali ninaamini katika Yahwe.
\v 7 Nitafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano lako, kwa kuwa uliyaona mateso yangu; wewe uliijua dhiki ya moyo wangu.
\s5
\v 8 Wewe haujaniweka kwenye mkono wa maadui zangu. Nawe umeiweka miguu yangu mahali pa wazi papana.
\v 9 Uniurumie, Yahwe, kwa maana niko katika dhiki; macho yangu yanafifia kwa huzuni pamoja na moyo wangu na mwili wangu.
\s5
\v 10 Kwa kuwa maisha yangu yamechoshwa kwa huzuni na miaka yangu kwa kuugua kwangu. Nimekuwa dhaifu kwa sababu ya dhambi zangu, na mifupa yangu inachakaa.
\v 11 Kwa sababu ya maadui zangu wote, watu wananibeza; majirani zangu wanaishangaa hali yangu, na wale wanao nifahamu wanashtuka. Wale wanionao mitaani hunikimbia.
\s5
\v 12 Nimesahaulika kama mtu aliye kufa ambaye hakuna mtu anaye mfikiria. Niko kama chungu kilicho pasuka.
\v 13 Kwa maana nimesikia minong'ono ya wengi, habari za kutisha kutoka pande zote kwa pamoja wamepanga njama kinyume na mimi. Wao wanapanga njama ya kuniua.
\s5
\v 14 Bali mimi ninakuamini wewe, Yahwe; Ninasema, "Wewe ni Mungu wangu."
\v 15 Hatima yangu iko mikononi mwako. Uniokoe mikononi mwa maadui zangu na wale wanao nifukuzia.
\v 16 Nuru ya uso wako imuangazie mtumishi wako; uniokoe katika uaminifu wa agano lako.
\s5
\v 17 Usiniache niaibishwe, Yahwe; kwa maana ninakuita wewe! Waovu waaibishwe! Na wanyamaze kimya kuzimuni.
\v 18 Na inyamazishwe midomo midanganyifu ambayo husema maneno mabaya kuhusu watu wenye haki huku wakiwa na kiburi na dharau.
\s5
\v 19 Uzuri wako ni wa namna gani nao umeuhifadhii kwa ajili ya wale wanao kuheshimu sana, ambao wewe huufanya kwa ajili ya wale ambao hukimbilia kwako kwa ajili ya usalama mbele ya watoto wote wa wanadamu!
\v 20 Katika makao ya uwepo wako, wewe huwaficha mbali na njama za watu. Wewe huwaficha mahali salama na ndimi zenye vurugu.
\s5
\v 21 Atukuzwe Yahwe, kwa maana yeye alinionesha maajabu ya uaminifu wa agano lake mahali nilipoishi.
\v 22 Ingawa kwa haraka zangu nilisema, "Nimeondolewa machoni pako," bali wewe ulisikia kusihi kwangu nilipokulilia wewe.
\s5
\v 23 Enyi wafuasi waaminifu, mpendeni Yahwe, Yahwe huwalinda waaminifu, lakini huwalipa wakaidi ipasavyo.
\v 24 Iweni imara na jasiri, ninyi nyote mnao mwamini Mungu kuwasaidia.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Zaburi ya Daudi. Zaburi. Amebarikiwa mtu yule aliyesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimesitiriwa.
\v 2 Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe hamuhesabii hatia na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu.
\s5
\v 3 Nilipokaa kimya, mifupa yangu ilidhohofika huku nikiugua muda wote.
\v 4 Mchana na usiku mkono wako ulinielemea. nguvu zangu zilikauka wakati wa kiangazi. Selah
\s5
\v 5 Ndipo nilipotambua makosa yangu kwako, nami sifichi tena uovu wangu. Nilisema, "Nitakiri makosa yangu kwa Yahwe," nawe ulinisamehe hatia ya dhambi zangu. Selah
\v 6 Kwa sababu ya haya, wale wote ambao ni wa kimungu wanapaswa kukuomba wakati wa shida kubwa. Nayo mafuriko yajapo, hayatawapata watu hao.
\s5
\v 7 Wewe u mahali pangu pa kujifichia, nawe utanilinda matatizoni. Wewe utanizunguka pamoja na nyimbo zaushindi. Selah
\v 8 Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia upasayo kuiendea. Nitakuelekeza huku macho yangu yakikutazama.
\s5
\v 9 Msiwe kama farasi au kama nyumbu, ambao hawana uelewa; ni kwa hatamu na lijamu tu unaweza kuwapeleka popote utakapo wao waende.
\v 10 Waovu wanahuzuni nyingi, bali uaminifu wa agano la Yahwe utamzunguka yule anaye mwamini yeye.
\s5
\v 11 Furahini katika Yahwe, na mshangilie, ninyi wenye haki; pigeni kelele za shangwe, ninyi nyote wenye haki mioyoni mwenu.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Furahini katika Yahwe, ninyi wenye haki; kusifu kwa wenye haki kwa faa sana.
\v 2 Mshukuruni Bwana kwa kinubi; mwimbieni sifa kwa kinubi chenye nyuzi kumi.
\v 3 Mwimbieni yeye wimbo mpaya; pigeni kwa ustadi na muimbe kwa furaha.
\s5
\v 4 Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki.
\v 5 Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe.
\v 6 Kwa neno la Yahwe mbingu ziliumbwa, na nyota zote ziliumbwa kwa pumzi ya mdomo wake.
\s5
\v 7 Yeye huyakusanya maji ya baharini kama rundo; naye huiweka bahari katika ghala.
\v 8 Basi ulimwengu wote umwogope Yahwe; wenyeji wote wa ulimwengu wamuhofu yeye.
\v 9 Kwa maana yeye alisema, na ikafanyika; aliamuru, na ikasimama mahali pake.
\s5
\v 10 Yahwe huvunja muungano wa mataifa; naye huishinda mipango ya wanadamu.
\v 11 Mipango ya Yahwe husimama milele, mipango ya moyo wake ni kwa ajili ya vizazi vyote.
\v 12 Limebarikiwa taifa ambalo Mungu wao ni Yahwe, watu ambao yeye amewachagua kama warithi wake.
\s5
\v 13 Yahwe anatazama kutoka mbinguni; yeye huona watu wote.
\v 14 Kutokea mahali ambapo yeye anaishi, huwatazama wote waishio juu ya nchi.
\v 15 Yeye anaye iumba mioyo yao na kuyaona matendo yao yote.
\s5
\v 16 Hakuna mfalme anayeokolewa na jeshi kubwa; shujaa haokolewi na nguvu zake nyingi.
\v 17 Farasi sio salama kwa ajili ya ushindi; ijapokuwa nguvu zake ni nyingi, hawezi kuokoa.
\s5
\v 18 Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu
\v 19 kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa.
\s5
\v 20 Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
\v 21 Mioyo yetu hufurahia ndani yake, kwa kuwa tunaamini katika jina lake takatifu.
\s5
\v 22 Yahwe, agano lako takatifu, liwe pamoja nasi tuwekapo tumaini letu katika wewe.
\s5
\c 34
\p Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje.
\v 1 Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu.
\s5
\v 2 Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi.
\v 3 Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake.
\s5
\v 4 Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.
\v 5 Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
\v 6 Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
\s5
\v 7 Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
\v 8 Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
\v 9 Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
\s5
\v 10 Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
\v 11 Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
\s5
\v 12 Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
\v 13 Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
\v 14 Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
\s5
\v 15 Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.
\v 16 Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani.
\v 17 Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
\s5
\v 18 Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
\v 19 Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
\v 20 Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
\s5
\v 21 Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.
\v 22 Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.
\s5
\c 35
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahwe, uwashughulikie wale wanao nishughulikia mimi; upigane nao wanao pigana nami.
\v 2 Uikamate ngao yako ndogo na ngao kubwa; inuka unisaidie.
\v 3 Uutumie mkuki wako na shoka lako la vita kwa wale wanao nifukuzia; uuambie moyo wangu, "Mimi ni wokovu wako."
\s5
\v 4 Waaibishwe na kudharauliwa wale wanaoutafuta uhai wangu. Warudishwe nyuma na wafedheheshwe wanao panga kunidhuru.
\v 5 Wao wawe makapi mbele ya upepo, malaika wakiwafutilia mbali.
\v 6 Njia yao na iwe giza na utelezi, malaika wa Yahwe wakiwafukuzia.
\s5
\v 7 Wamenitegea mtego bila sababu; bila sababu wamechimba shimo kwa ajili ya uhai wangu.
\v 8 Uharibifu na uwapate wao kwa kushitukiza. Mtego ambao wameutega na uwanase wao. Na wadumbukie humo, ili kwamba waangamizwe.
\s5
\v 9 Bali mimi nitakuwa nafuraha ndani ya Yahwe na ndani ya wokovu wake.
\v 10 Mifupa yangu yote itasema, "Yahwe, ni nani kama wewe, uokoaye walio onewa mkononi mwa walio na nguvu kuwazidi wao na masikini na wahitaji mkononi mwa wale wanaojaribu kuwaibia?"
\s5
\v 11 Mashahidi wa uongo wamesimama; wananishitakia uongo.
\v 12 Kwa ajili ya wema wananilipa mabaya. Nina huzuni nyingi.
\s5
\v 13 Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
\v 14 Nilienenda katika huzuni kana kwamba walikuwa ni ndugu zangu; niliinama chini nikiomboleza kana kwamba ni kwa ajili ya mama yangu.
\s5
\v 15 Bali mimi nilipokuwa mashakani, walifurahi sana na kukutanika pamoja; walikutanika pamoja kinyume na mimi, nami nilishangazwa nao. Walinirarua bila kuacha.
\v 16 Kwa dharau kabisa walinidhihaki; walinisagia meno yao.
\s5
\v 17 Bwana, mpaka lini utaendelea kutazama? uiokoe roho yangu na mashambulizi yao ya maagamizi uyaokoe maisha yangu na simba.
\v 18 Nami nitakushukuru wewe katika kusanyiko kubwa; nitakusifu kati ya watu wengi.
\s5
\v 19 Usiwaache maadui zangu wadanganyifu kufurahi juu yangu; usiwaache waendelee na mipango yao ya uovu.
\v 20 Kwa maana hawaongei amani, bali wanabuni maneno ya uongo kwa wale wanaoishi kwa amani katika ardhi yetu.
\s5
\v 21 Midomo yao inapaza sauti ikinishtaki; wakisema, Aha, Aha, macho yetu yameona."
\v 22 Yahwe wewe umeona, usikae kimya; Bwana, usiwe mbali nami.
\v 23 Inuka mwenyewe na usimame kunitetea; Mungu wangu na Bwana wangu, unitetee.
\s5
\v 24 Kwa sabababu ya haki yako, Yahwe Mungu wangu, unitetee; usiwaache wafurahi kwa ajili yangu.
\v 25 Usiwaache waseme mioyoni mwao, "Aha, tumepata tulicho kihitaji." Usiwaache waseme, tumemmeza."
\v 26 Uwaaibishe na kuwa fendhehesha wale wanaotaka kunidhuru. Wale wote wanao ni dhihaki wafunikwe kwa aibu na kudharauliwa.
\s5
\v 27 Nao wote wanao tamani kudhihirishwa kwangu washangilie na wafurahi; siku zote waseme, "Usifiwe Yahwe, yeye ajifurahishaye katika mafanikio ya mtumishi wake.
\v 28 Kisha nitatangaza matendo yako ya haki na kukusifu wewe wakati wote.
\s5
\c 36
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi ya mtumishi wa Yahwe.
\v 1 Dhambi hunena kama unabii katika moyo wa mwovu; machoni mwake hamna hofu ya Mungu.
\v 2 Kwa maana yeye hujifariji mwenyewe, akifikiria kuwa dhambi zake hazitagundulika na kuchukiwa.
\s5
\v 3 Maneno yake ni yenye dhambi na udanganyifu; hataki kuwa mwenye hekima na kutenda mema.
\v 4 Alalapo kitandani, hupanga namna ya kutenda dhambi; yeye hukaa nje kwenye nja ya uovu; yeye hakatai uovu.
\s5
\v 5 Uaminifu wa agano lako, Yahwe, unafika mbinguni; uaminifu wako unafika mawinguni.
\v 6 Haki yako ni kama milima ya Mungu; hukumu yako ni kama kina kirefu. Yahwe, wewe huwahifadhi wote wanadamu na wanyama.
\s5
\v 7 Ni jinsi gani uaminifu wa aganao lako ni wa thamani, Mungu! Watu hukimbilia usalama chini ya uvuli wa mbawa zako.
\v 8 Nao watatoshelezwa tele na utajiri wa chakula nyumbani mwako; utawafanya wanywe kutoka katika mto wa baraka zako za thamani.
\v 9 Kwa kuwa mna chemichemi ya uzima; na katika mwanga wako tutaiona nuru.
\s5
\v 10 Uupanue uaminifu wa agano lako kikamilifu kwa wale wanao kujua wewe, ulinzi wako uwe juu ya wanyoofu wa moyo.
\v 11 Usiuache mguu wa mwenye kiburi unisogelee. Usiiache mkono wa mwovu unitoweshe.
\v 12 Kule wafanyao maovu wameanguka; wameharibiwa hawawezi kuinuka.
\s5
\c 37
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Usikereshwe na wafanyao maovu; usiwaonee wivu wale watendao yasiyo haki.
\v 2 Kwa kuwa muda mfupi watakauka kama nyasi na kukauka kama vile mimea ya kijani ikaukavyo wakati wa kiangazi.
\s5
\v 3 Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani.
\v 4 Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
\s5
\v 5 Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako.
\v 6 Yeye ataidhihilisha haki yako kama mchana na usafi wako kama mwangaza wa mchana.
\s5
\v 7 Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.
\s5
\v 8 Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
\v 9 Watendao maovu watafutiliwa mbali, bali wale wamngojao Yahwe watairithi nchi.
\v 10 Katika muda mfupi mtu mwovu atatoweka; wewe utatazama mahali pake, wala hautamuona.
\s5
\v 11 Lakini wapole watairithi nchi nao watafurahia katika mafanikio makubwa.
\v 12 Mtu mwovu hupanga njama kinyume na mwenye haki na kumsagia meno.
\v 13 Bwana humcheka, kwa maana anaona siku yake inakuja.
\s5
\v 14 Waovu wametoa nje panga zao na wametayarisha pinde zao ili kuwaangamiza wanyonge na wahitaji, na kuwaua wenye haki.
\v 15 Panga zao zitawaua wenyewe, na pinde zao zitavunjika.
\s5
\v 16 Ni bora kuwa mwenye haki maskini kuliko tajiri mwenye mali nyingi.
\v 17 Kwa maana mikono ya watu waovu itavunjika, bali Yahwe huwasaidia watu wenye haki.
\s5
\v 18 Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele.
\v 19 Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
\s5
\v 20 Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
\v 21 Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
\s5
\v 22 Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
\v 23 Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
\v 24 Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
\s5
\v 25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
\v 26 Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
\v 27 Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
\s5
\v 28 Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli.
\v 29 Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
\v 30 Mdomo wa mwenye haki huongea hekima na huongeza haki.
\s5
\v 31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; miguu yake haitelezi.
\v 32 Mtu mwovu humvizia mwenye haki na kutafuta kumuua.
\v 33 Yahwe hatamuacha yeye kwenye mkono wa mtu mwovu wala kumlaumu atakapohukumiwa.
\s5
\v 34 Umngoje Yahwe na uishike njia yake, naye atakuinua uimiliki nchi. Atakapo waondosha waovu wewe utaona.
\s5
\v 35 Nimewaona waovu na mtu wa kutisha akienea kama mti wa kijani katika udongo wa asili.
\v 36 Lakini nilipopita tana mara nyingine, hakuwepo pale. nilimtafuta, lakini sikumpata.
\s5
\v 37 Uwachunguze watu waadilifu, na uwatambue wenye haki; kuna hatima nzuri kwa ajili ya mtu wa amani.
\v 38 Mwenye dhambi wataharibiwa kabisa; hatima ya mtu mwovu ni kuondoshwa.
\s5
\v 39 Wokovu wa haki unatoka kwa Yahwe; yeye huwalinda wao nyakati za shida.
\v 40 Yahwe huwasaidia na kuwaokoa. Yeye huwaokoa dhidi ya watu waovu na kuwanusuru wao kwa sababu wao wamemkimbilia yeye kwa ajili ya usalama.
\s5
\c 38
\p Zaburi ya Daudi, kuirejeza katika kumbukumbu.
\v 1 Yahwe, usinikemee katika hasira yako; usiniadhibu katika ghadhabu yako.
\v 2 Kwa kuwa mishale yako hunichoma, na mkono wako huniangusha chini.
\s5
\v 3 Mwili wangu wote unaumwa kwa sababu ya hasira yako; kwa sababu ya dhambi zangu mifupa yangu haina afya.
\v 4 Kwa maana maovu yangu yamenielemea; yamekuwa mzigo mzito kwangu.
\s5
\v 5 Vidonda vyangu vimeoza na vinanuka kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
\v 6 Nimepindika na kuwa mnyonge kila siku; ninaenenda katika maombolezo siku zote.
\s5
\v 7 Kwa maana ndani yangu, ninaungua; hakuna afya katika mwili wangu.
\v 8 Nimedhohofika na kulemewa sana; ninaugua kwa sababu ya dhiki yangu.
\s5
\v 9 Bwana, wewe unaielewa shauku ya ndani kabisa ya moyo wangu, na kuugua kwangu hakujifichika kwako.
\v 10 Moyo wangu unapwita pwita, nguvu zangu zinaniisha, macho yangu yanafifia.
\s5
\v 11 Marafiki na ndugu zangu wamenitenga kwa sababu ya hali; majirani zangu hukaa mbali nami.
\v 12 Wale wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego kwa ajili yangu. Wao ambao hutafuta kunidhuru huongea maneno ya uharibifu na husema maneno ya uongo siku nzima.
\s5
\v 13 Lakini, niko kama mtu kiziwi na sisikii lolote; niko kama mtu bubu ambaye hasemi lolote.
\v 14 Niko kama mtu asiye sikia na mbaye hawezi kujibu.
\s5
\v 15 Hakika ninakungoja wewe, Yahwe; wewe utanijibu, Bwana Mungu wangu.
\v 16 Ninasema hivi ili kwamba maadui zangu wasije wakafurahia juu yangu. Ikiwa mguu wangu utateleza, watanifanyia mambo mabaya.
\s5
\v 17 Kwa kuwa niko karibu mashakani, na niko katika maumivu ya mara kwa mara.
\v 18 Ninatubu makosa yangu; ninahuzunika kwa dhambi zangu.
\s5
\v 19 Lakini maadui zangu ni wengi; wale wanichukiao ni wengi.
\v 20 Wao wananilipa mabaya kwa mema; wanavurumiza shutuma kwangu ingawa nimefuata lililo jema.
\s5
\v 21 Usinitelekeze, Yahwe, Mungu wangu, usikae mbali nami.
\v 22 Njoo haraka unisaidie, Bwana, wokovu wangu.
\s5
\c 39
\p Kwa kiongozi wa muziki, kwa ajili ya Jeduthun. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Niliamua, "Nitakuwa mwangalifu kwa kile nisemacho ili kwamba nisitende dhambi kwa ulimi wangu. Nitaufumba mdomo wangu niwapo uweponi mwa mtu mwovu."
\s5
\v 2 Nilikaa kimya; Nilizuia maneno yangu hata kuongea lolote zuri, na maumivu yangu yalizidi sana.
\v 3 Moyo wangu ukawaka moto; nilipoyatafakari mambo haya, yaliniunguza kama moto. Ndipo mwishowe niliongea.
\s5
\v 4 Yahwe, unijulishe ni lini utakuwa mwisho wa maisha yangu na kiwango cha siku zangu. Unioneshe jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.
\v 5 Tazama, wewe umezifanya siku zangu kama upana wa kiganja changu tu, sikuzangu za kuishi ni kama si kitu mbele zako. Hakika kila mtu ana pumzi moja. Selah
\s5
\v 6 Hakika kila mtu hutembea kama kivuli. Hakika kila mmoja hufanya haraka kuhusu kukusaya utajiri ingawa hawajui ni nani atazipokea.
\v 7 Sasa, Bwana, ninasubiri kwa ajili ya nini? Wewe ni tumaini langu pekee.
\s5
\v 8 Uniokoe na dhambi zangu; usinifanye laumu ya wabumbavu.
\v 9 Niko kimya na siwezi kufungua mdomo wangu, kwa sababu ni wewe ndiwe umefanya hivyo.
\s5
\v 10 Acha kunijeruhi; nimezidiwa na pigo la mkono wako.
\v 11 Wewe unapowaadhibu watu kwa ajili ya dhambi, huvila kama nondo vitu vyao wavitamanivyo; hakika watu si kitu bali mvuke. Serah
\s5
\v 12 Sikia maombi yangu, Yahwe, na unisikilize; usikie kilio changu! Usiwe kiziwi kwangu, kwa maana niko kama mgeni pamoja nawe, kimbilio langu la usalama kama mababu zangu walivyokuwa.
\v 13 Geuzia furaha yako kwangu ili kwamba niweze kutabasamu kabla sijafa.
\s5
\c 40
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nalimungoja Yahwe kwa uvumilivu; alinisikia na kusika kilio changu.
\v 2 Yeye akanitoa nje ya shimo la kutisha, nje ya matope, naye aliiweka miguu yangu juu ya mwamba na kuzifanya hatua zangu salama.
\s5
\v 3 Yeye ameweka wimbo mpya mdomoni mwangu, sifa kwa Mungu. Wengi watauona na kumheshimu yeye na kumwamini Yahwe.
\v 4 Amebarikiwa mtu yule ambaye humfanya Yahwe tumaini lake naye hathamini majivuno wala wale wanaokengeuka kwa uongo.
\s5
\v 5 Yahwe Mungu wangu, matendo ya ajabu ambayo wewe umeyafanya, ni mengi, na mawazo yako yatuhusuyo sisi hayahesabiki; Ikiwa ningetangaza na kuyazungumza kwao, ni mengi sana hayahesabiki.
\v 6 Wewe haufurahishwi katika sadaka au matoleo, bali wewe umeyafungua masikio yangu; wala haukuhitaji sadaka ya kuteketeza au sadaka ya dhambi.
\s5
\v 7 Ndipo nilisema mimi, "Tazama, nimekuja; imeandikwa kuhusu mimi katika kitabu cha hati.
\v 8 Ninafurahia kuyafanya mapenzi yako, Mungu wangu; sheria zako ziko moyoni mwangu."
\v 9 Katika kusanyiko kubwa nimetangaza habari njema ya haki yako; Yahwe, wewe unajua sikuizuia midomo yangu.
\s5
\v 10 Sikuficha haki yako moyoni mwangu; nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako; sijaficha uaminifu wa agano lako au uaminifu wako kwenye kusanyiko kubwa.
\v 11 Usiache kunitendea kwa rehema, Yahwe; Uaminifu wa agano lako na uaminifu wako unihifadhi siku zote.
\s5
\v 12 Mabaya yasiyo hesabika yamenizunguka; Maovu yangu yamenipata nami siwezi kuona chochote; nayo ni mengi kuliko nywele za kichwa changu, na moyo wangu umeniangusha.
\v 13 Yahwe, tafadhari uniokoe; njoo haraka unisaidie Yahwe.
\s5
\v 14 Waaibike na wafedheheke kabisa wanaufuatilia uhai wangu wauondoe. Warudishwe nyuma na wadharaulike, wale wanaofurahia kuniumiza.
\v 15 Waogopeshwe kwa sababu ya aibu yao, wale waniambiao, "Aha, aha!"
\s5
\v 16 Bali wale wote wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; na kila mmoja apendaye wokovu wako aseme daima, "Asifiwe Yahwe."
\v 17 Mimi ni maskini na muhitaji; lakini Bwana hunifikiria. Wewe ni msaada wangu nawe huja kuniokoa; usichelewe, Mungu wangu.
\s5
\c 41
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Amebarikiwa mtu yule amkumbukaye mnyonge; katika siku ya taabu, Yahwe atamuokoa.
\v 2 Yahwe atamuhifadhi na kumuweka hai, naye atabarikiwa duniani; Yahwe hata mrudisha kwenye mapenzi ya adui zake.
\v 3 Awapo kwenye kitanda cha mateso Yahwe atamsaidia; nawe utakifanya kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha uponyaji.
\s5
\v 4 Nami nilisema, "Yahwe unihurumie! Uniponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe."
\v 5 Adui zangu huongea maovu dhidi yangu, wakisema, 'Atakufa lini na jina lake lipotee?'
\v 6 Adui yangu ajapo kuniona, huongea mambo yasiyo na maana; moyo wake hukusanya maafa yangu kwa ajili yake mwenyewe; na aondokapo kwangu, yeye huwaambia watu wengine kuhusu hayo.
\s5
\v 7 Wale wote wanaonichukia kwa pamoja hunon'gona dhidi yangu; nao wanafarijika kwa ajili ya maumivu yangu.
\v 8 Wakisema, "Gonjwa baya limemshikilia yeye haswa; na sasa kuwa amelala kitandani, hatainuka kamwe."
\v 9 Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.
\s5
\v 10 Bali wewe, Yahwe, unihurumie na uniinue ili kwamba niwalipizie kisasi.
\v 11 Na hivi nitajua kuwa unafurahishwa nami, kwa kuwa adui yangu hatafurahia kunishinda.
\v 12 Kwangu mimi, wewe unanisaidia katika uadilifu wangu na utaniweka mbele ya uso wako milele.
\s5
\v 13 Yahwe, Mungu wa Israeli asifiwe milele na milele. Amen na Amen. Kitabu ya Pili
\s5
\c 42
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah
\v 1 Kama ayala ayatamanivyo maji ya mto. ndivyo hivyo ninakiu yako, Mungu.
\v 2 Ninakiu yako Mungu, Mungu uliye hai, ni lini nitaonekana mbele zako?
\s5
\v 3 Machozi yangu yamekuwa ni chakula changu mchana na usiku, wakati maadui zangu siku zote wanasema, "Yuko wapi Mungu wako?"
\v 4 Mambo haya niayakumbuka ninapoumimina roho yangu: nilipoenda na umati wa watu na kuwaongoza kwenye nyumba ya Mungu kwa sauti ya shangwe na kusifu, ni wengi tulisherekea.
\s5
\v 5 Roho yangu, kwa nini unainama? Kwa nini unahuzuni ndani yangu? Mtumaini Mungu, Kwa kuwa kwa mara nyingine nitamsifu yeye ambaye ni wokovu wangu.
\v 6 Mungu wangu, roho yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo ninakukumbuka toka nchi ya Yordani, toka kwenye vilele vitatu vya mlima Hermoni, na toka mlima wa Mizari.
\s5
\v 7 Kina huita kina kwenye kelele za maporomoko ya maji yako; mawimbi na mafuriko yako yote yako juu yangu.
\v 8 Wakati wa mchana Yahwe ataamuru uaminifu wa agano lake; na usiku wimbo wake utakuwa nami, ombi kwa Mungu wa uhai wangu.
\s5
\v 9 Nami nitasema kwa Mungu wangu, mwamba wangu, "Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninaenenda katika maombolezo kwa sababu ya ukandamizaji wa adui yangu?"
\v 10 Kama upanga mifupani pangu, maadui zangu wananikemea, siku zote wakiniambia, "Yuko wapi Mungu wako?"
\s5
\v 11 Roho yangu, kwa nini umeinama chini? Kwa nini unahuzuni ndani yangu? Mtumaini Mungu kwa kuwa nitamsifu tena yeye aliye wokovu wangu na Mungu wangu.
\s5
\c 43
\p
\v 1 Mungu, uniletee haki, na unitetee dhidi ya taifa lisilo la kimungu.
\v 2 Kwa kuwa wewe ni Mungu wa nguvu zangu. Kwa nini umenikataa? Kwa nini ninaenenda katika maombolezo kwa sababu ya ukandamizaji wa adui yangu?
\s5
\v 3 Oh, tuma nuru yako na kweli yako ziniongoze. Ziniletee mlima wako mtakatifu na makao yako.
\v 4 Kisha nitakwenda madhabahuni mwa Mungu, kwa Mungu wangu aliye furaha yangu kuu. Nami nitakusifu wewe kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu.
\s5
\v 5 Roho yangu, kwa nini umeinama? Kwa nini unahuzuni ndani yangu? Kwa kuwa nitamsifu tena yeye ambaye ni wokovu wangu na Mungu wangu.
\s5
\c 44
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya mwana wa Korah.....
\v 1 Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametuambia kazi uliyofanya katika siku zao, siku za kale.
\v 2 Uliwafukuza mataifa kwa mkono wako, lakini ukawafanya watu wetu kuishi humo; wewe uliwataabisha mataifa, lakini ukawaeneza watu wetu katika nchi.
\s5
\v 3 Kwa maana hawakupata umiliki wa nchi kwa upanga wao, wala mkono wao wenyewe haukuwaokoa; bali mkono wako wakuume, mkono wako, na nuru ya uso wako, na kwa sababu uliwaridhia.
\v 4 Mungu, wewe ni Mfalme wangu, amuru ushindi kwa ajili ya Yakobo.
\s5
\v 5 Kwa uweza wako tutawaangusha chini maadui zetu; kwa jina lako tutatembea juu yao, wale wanao inuka dhidi yetu.
\v 6 Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
\s5
\v 7 Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
\v 8 Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah
\s5
\v 9 Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.
\v 10 Umetufanya kuwakimbia maadui zetu; na wale watuchukiao huchukua vitu vyetu vya thamani kwa ajili yao wenyewe.
\v 11 Umetufanya kama kondoo aliyeandaliwa kwa ajili ya chakula na umetutawanya kati ya mataifa.
\s5
\v 12 Wewe unawauza watu wako bure; kwa kufanya hivyo haukupata faida.
\v 13 Wewe umetufanya kukemewa na majirani zetu, kuchekwa, na kudhihakiwa na wale wanao tuzunguka.
\v 14 Umetufaya kituko kati ya mataifa,.......................................................
\s5
\v 15 Siku zote fedheha yangu iko mbele yangu, na aibu ya uso wangu imenifunika
\v 16 kwa sababu ya sauti yake iliyo kemea na kutukana, kwa sababu ya adui na kisasi.
\v 17 Yote haya yametupata sisi; bado hatukukusahau wewe wala kulikosea agano lako.
\s5
\v 18 Mioyo yetu haikukengeuka; hatua zetu hazikuiacha njia yako.
\v 19 Bali wewe umetuadhibu vikali katika mahali pa mbweha na kutufunika na uvuli wa mauti.
\v 20 Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kueneza mikono yetu kwa Mungu mgeni,
\v 21 Mungu asingeligundua hili? Kwa maana yeye anazijua siri za moyo.
\v 22 Hakika, kwa ajili ya jina lako tutauawa siku zote; tunahesabiwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.
\s5
\v 23 Bwana, amka, kwa nini unalala? Inuka, usitutupe moja kwa moja.
\v 24 Kwa nini unaficha uso wako na kusahau mateso yetu na kukandamizwa kwetu?
\s5
\v 25 Kwa maana tumeyeyushwa kwenye mavumbi; miili yetu imeshikamana na ardhi.
\v 26 Inuka utusaidie na utuokoe kwa ajili ya uaminifu wa agano lako.
\s5
\c 45
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Shoshanim. Zaburi ya wana wa Korah....... Wimbo wa upendo.
\v 1 Moyo wangu unafurika kwa neno zuri; nitasoma kwa sauti maneno niliyo yaandika kuhusu mfalme; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mwenye ustadi.
\v 2 Wewe u mzuri sana kuliko mwanadamu yeyote; neema imemiminwa midomoni mwako; Kwa hiyo tunajua ya kuwa Mungu amekubariki milele.
\s5
\v 3 Weka upanga wako upande wako, wewe uliye mwenye nguvu, katika utukufu wako na enzi yako.
\v 4 Katika enzi yako enenda katika ushindi kwa sababu ya uaminifu, upole, na haki; mkono wako wa kuume utakufundisha mambo ya kutisha.
\s5
\v 5 Mishale yako ni mkali; watu huanguka chini yako; mishale yako imo ndani ya mioyo ya adui za mfalme.
\v 6 Kiti chako cha enzi, Mungu ni cha milele na milele; na fimbo ya haki ni fimbo ya utawala wako.
\v 7 Umeipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekupaka mafuta ya furaha kuliko wenzako.
\s5
\v 8 Mavazi yako yote hunukia manemane, udi, na mdalasini; kukoka katika majumba ya pembe vyombo vya muziki wa nyuzi vimekufurahisha.
\v 9 Binti za wafalme ni kati ya wake zako waheshimiwa; na mkono wako wa kuume amesimama malikia aliye vaa mavazi ya dhahabu ya Ofiri.
\s5
\v 10 Sikiliza, mwanangu, tafakari na utege sikio lako; uwasahahu watu wako na watu wa nyumba ya baba yako.
\v 11 Hivyo mfalme atautamani uzuri wako; yeye ni Bwana wako; umstahi.
\s5
\v 12 Binti wa Tiro atakuwepo akiwa na zawadi; matajiri kati wa watu watajipendekeza kwako.
\v 13 Binti mfalme katika jumba la kifahari ana utukufu wote; mavazi yake yametengenezwa kwa dhahabu.
\s5
\v 14 Naye ataongozwa kwa mfalme akiwa katika mavazi ya dhahabu; mabikra, wenzake wanoumfuata, wataletwa kwako mafalme.
\v 15 Wao wataongozwa kwa furaha na shangwe; wataingia mahali pa mfalme.
\s5
\v 16 Katika mahali pa baba zako watoto wako watakuwepo, ambao wewe utawafanya kuwa wakuu katika nchi yote.
\v 17 Nami nitalifanya jina lako kukumbukwa katika uzao wote; kwa hiyo watu watakushukuru milele na milele.
\s5
\c 46
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya mwana wa Korah; seti kwenye Alamoth. Wimbo.
\v 1 Mungu kwetu ni kimbilio la usalama na nguvu, upatikanao tele wakati wa mateso.
\v 2 Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu,
\v 3 hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. Selah
\s5
\v 4 Kuna mto, mikondo yake huufanya mji wa Mungu kufurahi, mahali patakatifu pa hema ya Aliye Juu.
\v 5 Mungu yuko katikati yake; naye hatasogezwa; Mungu atamsaidia, naye atafanya hivyo asubuhi na mapema.
\s5
\v 6 Mataifa yalikasirika na falme zikataharuki; yeye alipaza sauti yake, na nchi ikayeyuka.
\v 7 Yahwe wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Selah
\s5
\v 8 Njoni, mtazame matendo ya Yahwe, uharibifu alioufanya juu ya nchi.
\v 9 Anaisitisha vita kwenye nchi; yeye anauvunja upinde na kuikata vipande vipande mishale; anazichoma ngao.
\s5
\v 10 Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi.
\v 11 Mungu wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Serah
\s5
\c 47
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah.
\v 1 Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi.
\v 2 Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote.
\s5
\v 3 Yeye anawatiisha chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu.
\v 4 Yeye huchagua urithi kwa ajili yetu, utukufu wa Yakobo ambaye alimpenda. Serah
\v 5 Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu.
\s5
\v 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
\v 7 Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa.
\s5
\v 8 Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi.
\v 9 Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Ibrahimu; kwa kuwa ngao za duniani ni za Mungu; yeye ameinuliwa juu sana.
\s5
\c 48
\p Wimbo; zaburi ya wana wa Korah.
\v 1 Yahwe ndiye aliye mkuu na mwenyekusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu kwenye mlima wake mtakatifu.
\v 2 Ni mzuri katika mwinuko wake, furaha ya nchi yote, ni mlima Sayuni, kwenye upande wa kaskazini, mji wa Mfalme mkuu.
\v 3 Mungu amejifunua mwenyewe katika jumba lake la kifahari kama kimbilio la usalama.
\s5
\v 4 Maana, tazama, wafalme walikusanyika wenyewe; wote pamoja walipita.
\v 5 Nao waliuona, wakashangaa; walifadhaika, na wakaharakisha kuondoka.
\v 6 Pale pale tetemeko liliwashikilia, maumivu makali kama mwanamke anaye zaa.
\s5
\v 7 Kwa upepo wa mashariki wewe huivunja meli ya Tarshishi.
\v 8 Kama tulivyo sikia, vivyo hivyo tumeona katika mji wa Yahwe wa majeshi, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atautunza milele. Selah
\s5
\v 9 Tumeutafakari uaminifu wa agano lako, Mungu, katikati ya hekalu lako.
\v 10 Kama lilivyo jina lako, Mungu, hivyo ndivyo zilivyo sifa zako mpaka miisho ya dunia; mkono wako wa kuume umejaa haki.
\s5
\v 11 Milma Sayuni na ufurahi, nao wana wa Yuda washangilie kwa sababu ya amri ya haki yako.
\s5
\v 12 Tembeeni katika Mlima Sayuni, muuzungukie mji,
\v 13 mzitazame kwa makini nguzo zake, na mtazame majumba yake ya kifahari ili kwamba muweze kuwasimulia kizazi kijacho.
\s5
\v 14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; naye atakuwa kiongozi wetu mpaka kufa.
\s5
\c 49
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah.
\v 1 Sikieni hili, ninyi watu wote; tegeni masikio, ninyi wenyeji wa dunia,
\v 2 wote walio chini na walio juu, tajiri na masikini wote pamoja.
\s5
\v 3 Mdomo wangu utazungumza hekima na tafakari ya moyo wangu itakuwa ya uelewa.
\v 4 Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
\v 5 Kwa nini nilazimike kuziogopa siku za uovu, wakati uovu umenizunguka kwenye visigino vyangu?
\s5
\v 6 Kwa nini niwaogope wale wanao amini katika mali zao na kujivuna kuhusu utajiri wao?
\v 7 Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
\v 8 Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
\s5
\v 9 Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
\v 10 Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
\s5
\v 11 Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
\s5
\v 12 Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
\v 13 Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa,.................
\s5
\v 14 Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao.
\v 15 Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. Selah
\s5
\v 16 Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.
\v 17 Maana atakapo kufa hataondoka na chochote; utukufu wake hautamfuata yeye.
\s5
\v 18 Yeye huifurahisha nafsi yake awapo hai na watu hukusifu wewe uishipo maisha yako mwenyewe-
\v 19 naye atakwenda kwenye ukoo wa baba zake naye kamwe hataiona nuru tena.
\v 20 Yule ambaye ana mali lakini hana ufahamu ni kama wanyama, ambao wataangamia.
\s5
\c 50
\p Zaburi ya Asafu.
\v 1 Mungu, Mwenye nguvu, Yahwe, amenena naye aliita nchi toka mawio ya jua mpaka machweo yake.
\v 2 Tokea Sayuni, Mungu ameangaza, ukamilifu wa uzuri.
\s5
\v 3 Mungu wetu huja naye hakai kimya; mbele yake moto hula, na kuna dhoruba kubwa karibu naye.
\v 4 Yeye huziita mbingu zilizo juu na nchi ili kwamba aweze kuwahukumu watu wake:
\v 5 Kwa pamoja kusanyikeni waaminifu wangu kwangu, wale waliofanya nami agano kwa sadaka."
\s5
\v 6 Mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye jaji. Serah
\s5
\v 7 Sikilizeni, watu wangu, nami nitazungumza; mimi ni Mungu, Mungu wenu.
\v 8 Sitawakaripia ninyi kwa ajili ya sadaka zenu; sadaka zenu za kuteketeza ziko nami siku zote.
\s5
\v 9 Sitachukua ng'ombe katika nyumba yenu, wala beberu katika mazizi yenu.
\v 10 Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, nao ng'ombe kwenye milima elfu ni wangu.
\v 11 Ninawajua ndege wa mlimani, na wanyama pori katika shamba ni wangu.
\s5
\v 12 Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi; maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.
\v 13 Je! sitakula nyama ya ngombe na kunywa damu ya mbuzi?
\s5
\v 14 Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu.
\v 15 Mniite katika siku ya shida; nami nitawaokoa
\s5
\v 16 Lakini kwa waovu Mungu anasema, "Inawahusu nini kuitangaza hali yangu, kwamba ninyi mmeliweka agano langu mdomoni mwenu,
\v 17 wakati ninyi mnayachukia maelekezo na mnayatupa maneno yangu?
\s5
\v 18 Mumuanapo mwizi, ninyi hukubaliana naye; ninyi na mnashirikiana na wale wafanyao uasherati.
\v 19 Mwautoa mdomo wenu kwa mabaya, huelezea udanganyifu.
\v 20 Mnakaa na kuongea dhidi ya ndugu yenu; na kukashfu mwana wa mama yenu.
\s5
\v 21 Mmefanya mambo haya, lakini nimekaa kimya, hivyo mlidhani kuwa ni mtu flani nilliye kama ninyi mlivyo. Lakini nitawakaripia ninyi na kuwafunua, mbele ya macho yenu, mambo yote miliyofanya.
\v 22 Mlitilie maanani hili, ninyi mnao msahau Mungu, vinginevyo nitawakata ninyi vipande vipande, na hatakuwepo yeyote wakuja kuwasaidia!
\s5
\v 23 Yule atoaye sadaka ya shukurani hunitukuza, na yeyote apangaye njia zake katika namna iliyo sahihi nitamuonesha wokovu wa Mungu."
\s5
\c 51
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; wakati nabii Nathani amekuja kwake baada ya kusikia kuwa alilala na Bathsheba.
\v 1 Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu.
\v 2 Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu.
\s5
\v 3 Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
\v 4 Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.
\s5
\v 5 Tazama, nilizaliwa katika uovu; pindi tu mama yangu aliponibeba mimba, nilikuwa katika dhambi. Tazama, wewe unahitaji uaminifu ndani ya moyo wangu;
\v 6 katika moyo wangu wewe utanifanya niijue hekima.
\s5
\v 7 Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
\v 8 Unifanye kusikia furaha na shangwe ili kwamba mifupa ulioivunja ifurahi.
\v 9 Uufiche uso wako mbali na dhambi zangu na uyafute maovu yangu yote.
\s5
\v 10 Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.
\v 11 Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu.
\s5
\v 12 Unirudishie furaha ya wokovu wako, na unihifadhi mimi kwa roho ya utayari.
\v 13 Ndipo nitawafundisha wakosaji jia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
\s5
\v 14 Unisamehe kwa ajili ya umwagaji damu, Mungu wa wokovu wangu, nami nitapiga kelele za shangwe ya haki yako.
\v 15 Ee Bwana, uifungue midomo yangu, na mdomo wangu itazieleza sifa zako.
\v 16 Kwa maana wewe haufurahishwi katika sadaka, vinginevyo ningekutolea sadaka; wewe hauwi radhi katika sadaka ya kuteketezwa.
\s5
\v 17 Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.
\v 18 Uitendee mema Sayuni katika nia yako nzuri; uzijenge tena kuta za Yerusalem.
\v 19 Kisha wewe utafurahia sadaka yenye haki, katika sadaka za kuteketeza; ndipo watu wetu watatoa ng'ombe kwenye madhabahu yako.
\s5
\c 52
\p Kwa kiongozi wa muziki. Maschil ya Daudi; wakati Doegi Mwedomi alipokuja na kumwambia Sauli, na kumwambia yeye, "Daudi amekuja kwenye nyumba ya Ahimeleki."
\v 1 Kwa nini wewe unajivunia kufanya uovu, wewe mtu mwenye nguvu? Uaminifu wa agano la Mungu huja kila siku.
\v 2 Ulimi wako hupanga uharibifu kama wembe mkali, na kufanya udanganyifu.
\s5
\v 3 Wewe unapenda uovu kuliko wema na udanganifu kuliko kuongea haki. Selah
\s5
\v 4 Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu.
\v 5 Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. Selah
\s5
\v 6 Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema,
\v 7 "Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine."
\s5
\v 8 Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele.
\v 9 Nitakushukuru wewe daima kwa uliyo tenda. Nitalisubiri jina lako, kwa sababu ni zuri, uweponi mwa wantu wako wa kimungu.
\s5
\c 53
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Mahalath. Maschil ya Daudi.
\v 1 Mpumbavu husema moyoni mwake, "Hakuna Mungu." Wamepotoka na kufanya machukizo; hakuna mmoja atendaye mema.
\v 2 Toka mbinguni Mungu hutazama chini kwa wanadamu kuona kama kuna yeyote mweye akili, amtafutaye yeye.
\v 3 Wote wamekengeuka. Kwa pamoja wamepotoka. Hakuna atendaye mema, hata mmoja.
\s5
\v 4 Je, wale wanao fanya uovu hawana uelewa - wale walao watu wangu kana kwamba wanakula mkate na hawamuiti Mungu?
\v 5 Wao walikuwa katika hofu kuu, ingawa hakuna sababu ya kuogopa ilikuwepo hapo; maana Mungu ataitawanya mifupa ya yeyote atakaye kusanyika dhidi yako; watu kama hao wataaibishwa kwa sababu Mungu amewakataa wao.
\s5
\v 6 Oh, kwamba wokovu wa Israel ungepatikana Sayuni! Wakati Mungu atakapowaleta watu wake kutoka kifungoni, ndipo Yakobo atashangilia na Israeli itafurahi!
\s5
\c 54
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschil ya Daudi; wakati Ziphites alipokuja na kumwambia Sauli, "Hivi Daudi hakujificha pamoja nasi?"
\v 1 Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu.
\v 2 Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu.
\v 3 Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. Selah
\s5
\v 4 Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye.
\v 5 Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu!
\s5
\v 6 Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
\v 7 Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.
\s5
\c 55
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschili ya Daudi.
\v 1 Uyategee sikio maombi yangu, Mungu; nawe usijifiche mbali na kusihi kwangu.
\v 2 Unitazame kwa makini na unijibu; Sina pumziko katika shida zangu
\v 3 kwa sababu ya sauti ya adui zangu, kwa sababu ya ukandamizaji wa waovu; maana wananiletea matatizo na kunitesa wakiwa na hasira.
\s5
\v 4 Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
\v 5 Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
\s5
\v 6 Nikasema, "Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
\v 7 Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
\s5
\v 8 Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani."
\v 9 Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
\s5
\v 10 Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
\v 11 Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.
\s5
\v 12 Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione.
\v 13 Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu.
\v 14 Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
\s5
\v 15 Kifo na kiwapate ghafla; na washuke wakiwa hai kuzimuni, maana ndiko waishiko waovu, hapo hapo kati yao.
\s5
\v 16 Lakini kwangu mimi, nitamwita Mungu, na Yahwe ataniokoa.
\v 17 Wakati wa jioni, asubuhi na mchana ninalalamika na kuomboleza; yeye atasikia sauti yangu.
\v 18 Kwa usalama kabisa atayaokoa maisha yangu na vita dhidi yangu, kwa maana wale waliopigana nami walikuwa ni wengi.
\s5
\v 19 Mungu, yule unayetawala milele, atawasikia na kuwaaibisha wao. Selah Hawabadiliki, na hawamhofu Mungu.
\s5
\v 20 Rafiki yangu ameinua mikono yake dhidi ya wale waliokuwa na amani naye; Hakuheshimu agano alilokuwa nalo.
\v 21 Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi, lakini moyo wake ulikuwa adui; maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, lakini yalikuwa ni panga zilizochomolewa.
\s5
\v 22 Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
\v 23 Bali wewe, Mungu, utawaleta waovu chini kwenye shimo la uharibifu; watu wenye kiu ya kumwaga damu na waongo hawataishi hata nusu ya maisha kama wengine, lakini mimi nitakuamini wewe.
\s5
\c 56
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Jonath elem rehokim. Zaburi ya daudi. Zaburi; wakati Wafilisti walipomchukua katika Gath.
\v 1 Uwe na huruma nami, Mungu, kwa maana watu wananishambulia! Muda wote wale wanao pigana nami hunikaribia zaidi ili wanishambulie.
\v 2 Adui zangu hunikanyaga muda wote; maana ni wengi ambao kwa kiburi hupigana dhidi yangu.
\s5
\v 3 Wakati nina woga, nitaweka imani yangu katika wewe.
\v 4 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu - nimeweka imani yangu katika Mungu; sitaogopa; mtu wa kawaida atanifanya nini?
\s5
\v 5 Muda wote wanayageuza maneno yangu; mawazo yao yote yako kinyume na mimi kwa ajili ya uovu.
\v 6 Wanajikusanya kwa pamoja, wanajificha wenyewe, na kuzifuatilia hatua zangu, wakisubiri kuniua.
\s5
\v 7 Usiwaache waikimbie adhabu yako kwa ajili ya uovu wao. Uwaangushe watu chini katika hasira yako, Mungu.
\v 8 Wewe unahesabu kutangatanga kwangu na kuweka machozi yangu kwenye chupa yako; je, hayako kitabuni mwako?
\s5
\v 9 Ndipo maadui zangu watakimbia katika siku ile nikuitapo wewe; hili najua, kwamba Mungu yupo kwa ajili yangu.
\v 10 Katika Mungu ambaye neno lake ninalisifu, katika Yahwe ambaye neno lake ninalisifu,
\v 11 katika Mungu ninaamini, sitaogopa. Yeyote atanifanya nini?
\s5
\v 12 Wajibu wa kutimiza viapo vyangu kwako uko juu yangu, Mungu; nitatoa sadaka ya shukurani.
\v 13 Kwa kuwa umeokoa uhai wangu na mauti; umezuia miguu yangu isianguke, ili kwamba niweze kutembea mbele ya Mungu katika nuru ya uhai.
\s5
\c 57
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi; wakati alipo mkimbia Sauli, pangoni.
\v 1 Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
\s5
\v 2 Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu.
\v 3 Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. Selah Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake.
\s5
\v 4 Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga.
\v 5 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu, utukufu wako uwe juu ya nchi yote.
\s5
\v 6 Wao walisambaza nje wavu kwa ajili ya miguu yangu; nilikuwa na shida sana. Walichimba shimo mbele yangu. Wao wenyewe wameangukia katikati ya shimo! Selah
\s5
\v 7 Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa.
\v 8 Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
\s5
\v 9 Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa.
\v 10 Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni.
\v 11 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.
\s5
\c 58
\p Kwa kiongiozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi.
\v 1 Je, ninyi watawala mnaongea haki? Mnahukumu kwa haki, ninyi watu?
\v 2 Hapana, mnafanya uovu mioyoni mwenu; munaeneza vurugu nchi yote kwa mikono yenu.
\s5
\v 3 Waovu huenenda katika upotovu hata walipokuwa tumboni; wao wanaenenda katika upotovu tangu kuzaliwa, wakiongea uongo.
\v 4 Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake,
\v 5 ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
\s5
\v 6 Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe.
\v 7 Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha.
\v 8 Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua.
\s5
\v 9 Kabla ya vyungu vyenu kupata joto la kuungua kwa miiba, yeye ataviondosha kwa upepo mkali, miiba ya kijani yote na ile inayoungua.
\v 10 Mwenye haki atafurahia atakapoona kisasi cha Mungu; ataiosha miguu yake kwenye damu ya waovu,
\v 11 hivyo watu watasema, "Hakika kuna tuzo kwa ajili ya mtu wenye haki; hakika kuna Mungu ahukumuye ulimwengu."
\s5
\c 59
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi; wakati Sauli alituma, waliilinda nyumba ili kumuua Daudi.
\v 1 Uniokoe dhidi ya adui zangu, Mungu wangu; uniweke mahali pa juu mbali na wale wanaoinuka dhidi yangu.
\v 2 Uniweke salama mbali na wafanyao kazi ya uovu, na uniokoe dhidi ya watu wenye kiu ya damu.
\s5
\v 3 Maana, tazama, wanasubiria uvamizini waniue. Wafanya maovu wenye nguvu hujikusanya wenyewe pamoja dhidi yangu, lakini sio kwa sababu ya makosa yangu au dhambi yangu, Yahwe.
\v 4 Wao wanajiandaa kunikimbiza ingawa sina kosa; amka unisaidie na unitazame.
\s5
\v 5 Ewe, Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, inika uwaadhibu mataifa yote; usiwe na huruma kwa mhalifu mwovu yeyote. Selah
\s5
\v 6 Wao wanarudi jioni, wanabweka kama mbwa na kuuzungukia mji.
\v 7 Tazama, wanapiga kelele mbaya kwa midomo yao; panga ziko kwenye midomo yao, maana wanasema, "Ni nani anaye tusikia?"
\s5
\v 8 Lakini wewe, Yahwe, utawacheka; wewe huwadhihaki mataifa yote.
\v 9 Mungu, nguvu yangu, nitakuwa msikivu kwako; wewe ni mnara wangu mrefu.
\s5
\v 10 Mungu atakutana nami akiwa na uaminifu wa agano lake; Mungu atanifanya nione shauku yangu juu ya adui zangu.
\v 11 Usiwaue, hivyo watu watasahau. Uwatawanye kwa nguvu zako na uwaangushe, Bwana ngao yetu.
\s5
\v 12 Kwa ajili ya dhambi za midomo yao na maneno ya midomo yao, wakamatwe katika majivuno yao, na kwa laana na uongo ambao wao huelezea.
\v 13 Uwamalize katika gadhabu yako, uwamalize ili kwamba wasiwepo tena; wajue kuwa Mungu anatawala katika Yakobo na mwisho wa nchi. Selah
\s5
\v 14 Wakati wa jioni wao hurudi, wakibweka kama mbwa wakiuzungukia mji.
\v 15 Wanatangatanga wakitafuta chakula na wanabweka kama mbwa kama hawajatosheka.
\s5
\v 16 Lakini nitaimba kuhusu nguvu zako, na asubuhi nitaimba kuhusu upendo wako imara! maana umekuwa mnara wangu mrefu na kimbilio la usalama katika siku ya taabu.
\v 17 Kwako, nguvu yangu, nitaimba sifa; kwa kuwa Mungu ni mnara wangu mrefu, Mungu wa uaminifu wa agano.
\s5
\c 60
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Shushan Eduth. Zaburi ya Daudi, kwa ajili ya kufundisha. Wakati alipopigana na Aram Naharaim pamoja na Aram Zobah, na Joab walirudi na kuwaua Wendomi elfu kumi na mbili katika bonde la chumvi.
\v 1 Mungu, wewe umetutupa; umeuvunja ulinzi wetu; wewe umekuwa hasirani; utuwezeshe tena.
\s5
\v 2 Wewe umeifanya nchi kutetemeka; umeipasua pasua; uiponye nyufa zake, maana zinatikisika.
\v 3 Wewe umewafanya watu wako kuona mambo magumu; umetufanya tunywe mvinyo wenye kutufanya kupepesuka.
\s5
\v 4 Kwa wale wanao kuheshimu wewe, wewe umeweka bandera ionekane dhidi ya wale wabebao upinde. Selah
\v 5 Ili kwamba wale uwapendao waweze kuokolewa, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu.
\s5
\v 6 Mungu ameongea katika utakatifu wake, "Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na kuligawa bonde la Sukothi.
\v 7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu na Ephraimu pia ni kofia yangu ya chuma; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
\s5
\v 8 Moabu ni bakuli langu la kunawia; juu ya Edomu nitatupa kiatu changu; nitapiga kelele za ushindi kwa sababu ya Filisti."
\v 9 Ni nani atakaye nileta kwenye mji imara? Ni nani ataniongoza kwenda Edomu?
\s5
\v 10 Lakini wewe, Mungu, je, haukutukataa? Wewe hauendi vitani pamoja na jeshi letu.
\v 11 Utusaidie dhidi ya adui yetu, maana msaada wa mwanadamu ni bure.
\v 12 Kwa msaada wa Mungu tutashinda; yeye atawakanyaga chini adui zetu.
\s5
\c 61
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye chombo cha nyuzi. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Sikia kulia kwangu, shughulikia maombi yangu.
\v 2 Kutokea mwisho wa nchi nitakuita wewe wakati moyo wangu umeelemewa; uniongoze kwenye mwamba ulio juu kuliko mimi.
\v 3 Maana wewe umekuwa kimbilio langu la usalama, nguzo imara dhidi ya adui.
\s5
\v 4 Uniache niishi hemani mwako milele! Nipate kimbilio salama chini ya makazi ya mbawa zako. Selah
\v 5 Kwa kuwa wewe, Mungu, umesikia viapo vyangu, wewe umenipa mimi urithi wa wale wanao liheshimu jina lako.
\s5
\v 6 Wewe utaongeza maisha ya mfalme; miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
\v 7 Yeye atabakia mbele ya Mungu milele.
\s5
\v 8 Nitaliimbia sifa jina lako milele ili kwamba niweze kufanya viapo vyangu kila siku.
\s5
\c 62
\p Kwa kiongozi wa muziki; Baada ya namna ya Jeduthun. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; wokovu wangu watoka kwake.
\v 2 Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa kamwe.
\s5
\v 3 Mpaka lini, ninyi nyote, mtamshambulia mtu, ili kwamba mumpindue yeye kama ukuta ulio inama au kama fensi isiyo imara?
\v 4 Wanashauliana naye ili tu kumshusha chini kutoka kwenye nafasi yake heshimiwa; wao wanapenda kuongea uongo; wanambariki yeye kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wana mlaani yeye. Selah
\s5
\v 5 Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; kwa maana matumaini yangu yako kwake.
\v 6 Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa.
\s5
\v 7 Na Mungu ni wokovu wangu na utukufu wangu; mwamba wa nguvu yangu na kimbilio langu salama liko katika Mungu.
\v 8 Mwaminini Mungu wakati wote, ninyi watu; mimina moyo wako mbele zake; Mungu ni kimbilio salama kwa ajili yetu. Selah
\s5
\v 9 Hakika watu wenye msimamo mdogo ni ubatili, na watu wenye msimamo mkubwa ni waongo; wao watakuwa wepesi kwenye mzani; uzito wao pamoja ni wepesi kuliko kitu chochote.
\v 10 Usiamini katika ukandamizaji au wizi; usitumainie utajiri, maana hawatazaa matunda; usiuweke moyo wako kwenye hivyo.
\s5
\v 11 Mungu ameongea mara moja, mara mbili nimesikia hili: nguvu ni za Mungu.
\v 12 Pia kwako, Bwana, ni uaminifu wa agano, maana humlipa kila mtu kwa kile alichokifanya.
\s5
\c 63
\p Zaburi ya Daudi, wakati yeye alipokuwa katika jangwa la Yuda.
\v 1 Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji.
\v 2 Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako.
\s5
\v 3 Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe.
\v 4 Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu.
\s5
\v 5 Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe,
\v 6 nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
\s5
\v 7 Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.
\v 8 Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia.
\s5
\v 9 Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi;
\v 10 watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha.
\s5
\v 11 Bali mfalme atashangilia katika Mungu; yeyote anaye apa kupitia yeye atajivunia yeye, lakini vinywa ya wale wasemao uongo watanyamazishwa.
\s5
\c 64
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Sikia sauti yangu, Mungu, usikilize malalamiko yangu; unilinde dhidi ya hofu ya adui zangu.
\v 2 Unifiche dhidi ya mipango ya siri ya wafanyao maovu, unifiche dhidi ya watendao vurugu ya udhalimu.
\s5
\v 3 Wao wamenoa ndimi zao kama panga; wamelenga mishale yao, maneno machungu,
\v 4 ili kwamba waweze kupiga kutoka mahali pa siri kwenda kwa mtu asiye na hatia; wampige yeye kwa ghafla nao wasihofu lolote.
\s5
\v 5 Wao wanahamasishana wenyewe katika kupanga uovu; wanashauriana pamoja wao binafsi ili kuweka mitego; nao husema, "Ni nani atakayetuona?"
\v 6 Wanabuni mipango ya dhambi; "Tumemaliza," wanasema, "ni mpango makini." Mawazo ya ndani na mioyo ya watu ni ya kina.
\s5
\v 7 Lakini Mungu atawapiga wao; ghafla watajeruhiwa kwa mishale yake.
\v 8 Watafanywa kuwa mashakani, kwa kuwa ndimi zao wenyewe ziko kinyume nao; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao.
\v 9 Watu wote wataogopa na kutangaza matendo ya Mungu. Kwa hekima watafikiria kuhusu kile yeye ametenda.
\s5
\v 10 Wenye haki watakuwa na furaha kuhusu Yahwe nao watakimbilia kwake; wote wenye haki moyoni watajivuna katika yeye.
\s5
\c 65
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi. Wimbo wa Daudi.
\v 1 Kwako wewe, Mungu katika Sayuni, sifa zetu za kungoja; viapo vyetu vitaletwa kwako.
\v 2 Wewe usikiaye maombi yetu, miili yote itakuja kwako.
\v 3 Maovu yanatutawala sisi; kama yalivyo makosa yetu, wewe utayasamehe.
\s5
\v 4 Amebarikiwa mtu yule ambaye wewe huchagua kumsogeza karibu yako ili kwamba aishi hekaluni mwako. Tutatoshelezwa kwa uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu.
\s5
\v 5 Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari.
\s5
\v 6 Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza.
\v 7 Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu.
\s5
\v 8 Wale wanaoishi sehemu za mwisho kabisa wa nchi wanaogopa ushahidi wa matendo yako; wewe hufanya mashariki na magharibi kushangilia.
\v 9 Wewe huja kuisaidia nchi; unainyeshea inchi; wewe unaiimarisha nchi vizuri; mto wa Mungu umejaa maji; wewe humpa mwanadamu nafaka unapokuwa umekwisha iandaa nchi.
\s5
\v 10 Wewe huyajaza matuta maji ya kutosha; wapasawazisha palipoinuka; wailainisha nchi kwa manyunyu ya mvua; waibariki mimea kati yao.
\v 11 Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mvumo wa mapito yako hudondosha unono katika nchi.
\v 12 Majani ya nyikani hudondosha umande, na vilima vimevikwa furaha.
\s5
\v 13 Malisho yamevishwa mifugo; mabonde pia yamefunikwa na nafaka; yanapiga kelele za shangwe, nayo yanaimba.
\s5
\c 66
\p Kwa kiongozi wa muziki. Wimbo, Zaburi.
\v 1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, nchi yote;
\v 2 Imbeni utukufu wa jina lake; mzitukuze sifa zake.
\s5
\v 3 Mwambieni Mugu, "Matendo yako yanatisha kama nini! Kwa ukuu wa nguvu zako maadui zako watajisalimisha kwako.
\v 4 Nchi yote watakuabudu wewe na watakuimbia wewe; wataliimbia jina lako." Selah
\s5
\v 5 Njoni na mtazame kazi za Mungu; yeye anatisha katika matendo yake awatendeayo wanadamu.
\v 6 Aligeuza bahari kuwa nchi kavu; wao walitembea kwa mguu juu ya mto; huko tulishangilia katika yeye.
\v 7 Yeye anatawala milele kwa nguvu zake; macho yake yanachunguza mataifa; waasi wasijivune. Selah
\s5
\v 8 Mtukuzeni Mungu, enyi watu wa mataifa yote, sauti ya sifa zake isikike.
\v 9 Yeye atuwekaye hai, naye hairuhusu miguu yetu iteleze.
\s5
\v 10 Kwa maana wewe, Mungu, umetupima sisi, wewe umetupima kama inavyopimwa fedha.
\v 11 Wewe ulituingiza sisi kwenye wavu; uliweka mzigo mzito viunoni mwetu.
\v 12 Wewe uliwafanya watu wasafiri juu ya vichwa vyetu; tulipita motoni na majini, lakini ukatuleta mahali pa wazi palipo salama.
\s5
\v 13 Nitaingia nyumbani mwako nikiwa na sadaka ya kuteketezwa; nitakulipa viapo vyangu
\v 14 ambavyo midomo yangu iliahidi na kinywa changu kiliongea nilipokuwa katika dhiki.
\v 15 Nitakutolea sadaka ya kuteketezwa ya wanyama wanene pamoja na harufu nzuri ya kondoo waume; Nitatoa ng'ombe na mbuzi. Selah
\s5
\v 16 Njoni, msikie, ninyi nyote mnao mwabudu Mungu, nami nitatangaza yale yeye aliyoitendea roho yangu.
\v 17 Nilimlilia kwa kinywa changu, naye alipendezwa na ulimi wangu.
\v 18 Kama ningelikuwa na dhambi ndani ya moyo wangu, Bwana asingenisikiliza.
\s5
\v 19 Lakini Mungu hakika amesikia; amesikia sautiya kuomba kwangu.
\v 20 Atukuzwe Mungu, ambaye hakuyakataa maombi yangu wala kuweka uaminifu wa agano lake mbali nami.
\s5
\c 67
\p Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo.
\v 1 Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah
\v 2 ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote.
\s5
\v 3 Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
\v 4 Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
\s5
\v 5 Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
\v 6 Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
\s5
\v 7 Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.
\s5
\c 68
\p Kwa kiongozi wa muziki; Zaburi ya Daudi, wimbo.
\v 1 Mungu ainuke, maadui zake watawanyike; pia wale wamchukiao wakimbie mbele zake.
\v 2 Kama moshi uondoshwavyo, hivyo uwaondoshe wao; kama nta iyeyukavo mbele ya moto, hivyo waovu waangamizwe uweponi mwa Mungu.
\v 3 Bali wenye haki wafurahi; washangilie mbele za Mungu; washangilie na kufurahi.
\s5
\v 4 Mwimbieni Mungu! Lisifuni jina lake! Msifuni yule aendeshaye farasi kwenye tambarare ya bonde la Mto Yordani! Yahwe ni jina lake! Shangilieni mbele zake!
\v 5 Baba wa yatima, na mwamuzi wa wajane, ni Mungu anayeishi mahali patakatifu.
\v 6 Mungu huwaweka wakiwa katika familia; yeye huwafungua wafungwa kwa kuimba bali waasi huishi katika ardhi kavu.
\s5
\v 7 Mungu, wewe ulipoenda mbele ya watu wako, ulipotembea kupitia jangwani, Selah
\v 8 nchi ilitetemeka; mbingu pia zilidondosha mvua katika uwepo wa Mungu, uweponi mwa Mungu wakati alipokuja Sinai, uweponi mwa Mungu, Mungu wa Israeli.
\s5
\v 9 Wewe, Mungu, ulituma mvua nyingi; uliuimarisha urithi wako wakati ulipokuwa umechoka.
\v 10 Watu wako waliishi humo; Wewe, Mungu, uliutoa kwa wema wako kwa maskini.
\s5
\v 11 Bwana alitoa amri, na wale walio zitangaza walikuwa ni jeshi kuu.
\v 12 Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia, na wanawake wakisubiri nyumbani kuvigawana wao na familia zao vilivyotekwa nyara.
\v 13 Njiwa walio vikwa fedha wakiwa na mabawa ya njano ya dhahabu. Wakati baadhi ya watu wakikaa kati ya mifugo ya kondoo, kwa nini umefanya haya?
\s5
\v 14 Mwenyezi Mungu aliwatawanya Wafalme huko, ilikuwa kama vile wakati wa theluji juu ya Mlima Salmoni.
\v 15 Mlima mkubwa ni milima wa mji wa Bashani; mlima mrefu ni mlima wa mji wa Bashani.
\v 16 Ewe mlima mrefu wa nchi, kwa nini unatazama kwa jicho la husuda, kwenye mlima ambao Mungu ameutaka kwa ajili ya mahali ambapo yeye ataishi? Hakika, Yahwe ataishi humo milele.
\s5
\v 17 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu juu ya maelfu; Bwana yu kati yao katika mahari patakatifu, kama katika Sinai.
\v 18 Wewe umepaa juu; uliwaongoza mateka; umepokea zawadi kutoka kati ya watu, hata kutoka kwa wale waliopigana dhidi yako, ili kwamba wewe, Yahwe Mungu, uweze kuishi huko.
\s5
\v 19 Abarikiwe Bwana, atubebeaye mizigo yetu, Mungu ambaye ni wokovu wetu. Selah
\v 20 Mungu wetu ni Mungu aokoaye; Yahwe Bwana ni yule awezaye kutuokoa sisi dhidi ya kifo.
\v 21 Lakini Bwana atapiga vichwa vya adui zake, mpaka kwenye ngozi ya kichwa yenye nywele ya wale watembeao katika makosa dhidi yake.
\s5
\v 22 Bwana alisema, "Nitawarudisha adui zangu kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka katika kina cha bahari
\v 23 ili kwamba upate kuwaangamiza adui zako, ukichovya mguu wako katika damu, na ili kwamba ndimi za mbwa wako zipate mlo wao kutoka kwa adui zenu."
\s5
\v 24 Mungu, wameona maandamano yako, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, kwenye mahali patakatifu.
\v 25 Waimbaji walitangulia, walifuatiwa na wapiga muziki, na katikati walikuwa wanawali wakicheza ngoma.
\s5
\v 26 Mtukuzeni Mungu katika kusanyiko; msifuni Yahwe, ninyi ukoo wa kweli wa Israeli.
\v 27 Kuna Benjamini kwanza, kabila dogo, kisha viongozi wa Yuda na watu wao, viongozi wa Zabuloni na viongozi wa Naftali.
\s5
\v 28 Mungu wenu, Israeli, ameamuru nguvu zenu; uzifunue kwetu nguvu zako, Mungu, kama ulivyo zifunua wakati uliopita.
\v 29 Uzifunue nguvu zako kwetu toka katika hekalu la Yerusalemu, ambako wafalme huleta zawadi kwako.
\s5
\v 30 Pigeni kelele katika vita dhidi ya wanyama wa porini katika mianzi, dhidi ya watu, lile kundi la mafahari na ndama. Wafedhehesheni na kuwalazimisha wawaletee zawadi; watawanyeni watu wapendao kupigana vita.
\v 31 Wakuu watatoka katika Misri; Ethiopia itafanya haraka kuufikisha mkono wake kwa Mungu.
\s5
\v 32 Mwimbieni Mungu, enyi falme za nchi; Selah mwimbieni sifa Yahwe.
\v 33 Kwake yeye apitaye juu ya mbingu za mbingu, zilizokuwepo tangu zama za kale; tazama, yeye hupiga kelele kwa nguvu
\s5
\v 34 Tangazeni kuwa Mungu ni mwenye nguvu; enzi yake iko juu ya Israeli, na nguvu zake ziko angani.
\v 35 Mungu, mahali pako patakatifu panatisha; Mungu wa Israeli, yeye huwapa watu wake nguvu na uweza. Atukuzwe Mungu.
\s5
\c 69
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Shoshannim. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Uniokoe, Mungu; maana maji yameweka uhai wangu hatarini.
\v 2 Ninazama kwenye kina cha matope, pasipo na hahari pa kusimama; nimekuja kwenye kina kirefu cha maji, ambako mafuriko yananifunika.
\s5
\v 3 Nimechoka sana kwa kulia kwangu; koo langu ni kavu; macho yangu yanafifia wakati namngoja Mungu wangu.
\v 4 Wale wanichukiao bila sababu wako zaidi ya nywele za kichwa changu; wale ambao wangeweza kuniua, wakiwa adui zangu kwa sababu zisizo sahihi, ni wengi mno; wanalazimisha nirudishe kile ambacho sijaiba.
\s5
\v 5 Mungu, wewe unaujua ujinga wangu, na dhambi zangu hazifichiki kwako.
\v 6 Usiwaache wale wanao kungoja wewe waaibishwe kwa sababu yangu, Bwana Yahwe wa majeshi; usiwaache wale wanaokutafuta wewe wadharauliwe kwa sababu yangu, Mungu wa Israeli.
\s5
\v 7 Kwa ajili yako nimestahimili lawama; aibu imeufunika uso wangu.
\v 8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, nisiye fahamika wala kuaminika kwa watoto wa mama yangu.
\v 9 Kwa maana bidii ya nyumba yako imenila, na laumu zao wanao kulaumu wewe zimeniangukia mimi.
\s5
\v 10 Wakati nilipolia na kutokula chakula, walinitukana.
\v 11 Nilipoteneneza mavazi ya gunia, nikawa kituko kwao.
\v 12 Wale wakaao katika lango la mji huniseng'enya; mimi ni wimbo wa walevi.
\s5
\v 13 Lakini kwangu mimi, maombi yangu ni kwako, Yahwe, wakati ambao wewe utayapokea; unijibu katika uaminifu wa wokovu wako.
\v 14 Unitoe matopeni, na usiniache nizame; uniondoe mbali na wale wanaonichukia na uniokoe katika kina cha maji.
\v 15 Usiache mafuliko ya maji yanielemee, wala kina kisinimeze. Usiache mdomo wa shimo unimeze.
\s5
\v 16 Unijibu, Yahwe, maana uaminifu wa agano lako ni mwema; kwa maana rehema zako kwangu ni nyingi, unigeukie.
\v 17 Usiufiche uso wako mbali na mtumishi wako, maana niko katika dhiki; unijibu haraka.
\s5
\v 18 Uje kwangu na unikomboe. Kwa sababu ya adui zangu, uwe fidia yangu.
\v 19 Wewe wajua kulaumiwa kwangu, kuaibishwa kwangu, na kudharauliwa kwangu; wapinzani wangu wote wako mbele yako.
\s5
\v 20 Lawama imevunja moyo wangu; nimejawa na huzuni kubwa; nilitafuta mtu wa kunihurumia, lakini hakuwepo; nilitafuta wafariji, lakini sikupata.
\v 21 Walinipa sumu kwa ajili ya chakula changu; katika kiu yangu walinipa siki ninywe.
\s5
\v 22 Meza yao mbele yao na iwe mtego; wafikiripo wako kwenye usalama, iwe kitanzi.
\v 23 Macho yao na yatiwe giza ili kwamba wasiweze kuona; uvifanye viuno vyao kutetemeka daima.
\s5
\v 24 Wamwagie gadhabu yako, ukali wa hasira yako uwafikie wao.
\v 25 Sehemu yao na iwe ukiwa; mtu yeyote asiishi katika hema yao.
\s5
\v 26 Kwa kuwa walimtesa yule uliyempa adhabu. Mara kwa mara walihesabu maumivu ya wale walioumizwa.
\v 27 Wakiwashtaki kuwa wamefanya uovu juu ya uovu; usiwaache waje kwenye ushindi wa haki yako.
\s5
\v 28 Uwafute kwenye Kitabu cha Uzima na wasiandikwe pamoja na wenyehaki.
\v 29 Lakini mimi ni maskini na mwenye huzuni; uruhusu wokovu wako, Mungu, uniweke juu sana.
\s5
\v 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na nitamtukuza yeye kwa shukrani.
\v 31 Nitamsifu Yahwe zaidi kuliko ng'ombe au ndama aliye na mapembe na kwato.
\s5
\v 32 Wanyenyekevu wameona na kufurahi; ninyi mnao matafuta Mungu, mioyo yenu itiwe nguvu.
\v 33 Maana Yahwe husikia wenye uhitaji naye hawadharau wafungwa wake.
\s5
\v 34 Mbingu na nchi zimsifu yeye, bahari na vyote vitembeavyo majini.
\v 35 Kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na ataujenga tena mji wa Yuda; watu wataishi huko na kupata umiliki wao.
\v 36 Ukoo wa watumishi wake watairithi; nao walipendao jina lake wataishi humo.
\s5
\c 70
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; kuleta kumbukumbu.
\v 1 Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi.
\v 2 Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu.
\v 3 Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, "Aha, aha."
\s5
\v 4 Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, "Mungu asifiwe."
\v 5 Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.
\s5
\c 71
\p
\v 1 Katika wewe, Yahwe, napatakimbilio salama; usiniache niaibishwe.
\v 2 Uniokoe na kunifanya salama katika haki yako; geuzia sikio lako kwangu.
\v 3 Uwe kwagu mwamba kwa ajili ya kimbilio salama ambako naweza kwenda siku zote; wewe umeamuru kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
\s5
\v 4 Uniokoe mimi, Mungu wangu, kutoka katika mkono wa asiye haki na katili.
\v 5 Maana wewe ni tumaini langu, Bwana Yahwe. Nimekuamini wewe siku zote tangu nilipokuwa mtoto.
\s5
\v 6 Nimekuwa nikisaidiwa na wewe tangu tumboni; wewe ndiye yule uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; sifa zangu zitakuhusu wewe siku zote.
\v 7 Mimi ni mfano bora kwa watu wangu; wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
\s5
\v 8 Mama yangu atajawa na sifa zako, siku zote akikuheshimu.
\v 9 Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
\s5
\v 10 Maana adui zangu wanazungumza kuhusu mimi; wale wanao fatilia uhai wangu wanapanga njama pamoja.
\v 11 Wao husema, "Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye."
\s5
\v 12 Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
\v 13 Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
\s5
\v 14 Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
\v 15 Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
\v 16 Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
\s5
\v 17 Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.
\v 18 Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
\s5
\v 19 Pia haki yako, Mungu, iko juu sana; wewe ambaye umefanya mambo makuu, Mungu, ni nani aliye kama wewe?
\v 20 Wewe ambaye umetuonesha sisi mateso mengi utatuhuisha tena na utatupandisha tena juu kutoka kwenye kina cha nchi.
\s5
\v 21 Uiongeze heshima yangu; rudi tena na unifariji.
\v 22 Nami pia nitakushukuru kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako, Mungu wangu; kwako nitaimba sifa kwa kinubi, Mtakatifu wa Israel.
\s5
\v 23 Midomo yangu itapiga kelele kwa sababu ya furaha wakati nikikuimbia sifa, hata kwa roho yangu, ambayo wewe umeikomboa.
\v 24 Ulimi wangu pia utaongea kuhusu haki yangu mchana kutwa; maana wameaibishwa na kuvurugwa, wale waliotafuta kuniumiza.
\s5
\c 72
\p Zaburi ya Sulemani.
\v 1 Mpe mfalme amri ya haki yako, Mungu, haki yako kwa wana wa mfalme.
\v 2 Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa.
\v 3 Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki.
\s5
\v 4 Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa.
\v 5 Na wakuheshimu wewe wakati wa jua, na kwa kipindi cha kudumu kwa mwezi katika vizazi vyote.
\s5
\v 6 Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
\v 7 Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka.
\s5
\v 8 Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.
\v 9 Na wote waishio jangwani wainame mbele zake; adui zake na walambe mavumbi.
\v 10 Wafalme wa Tashishi na visiwa walete kodi; wafalme wa Sheba na Seba watoe zawadi.
\s5
\v 11 Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
\v 12 Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
\s5
\v 13 Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
\v 14 Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
\s5
\v 15 Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
\v 16 Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
\s5
\v 17 Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.
\s5
\v 18 Yahwe Mungu, Mungu wa Israel, atukuzwe, ambaye pekee hufanya mambo ya ajabu.
\v 19 Jina lake tukufu litukuzawe milele, nayo nchi yote ijazwe na utukufu wake. Amina, Amina.
\v 20 Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamemalizika. Kutatu cha tatu
\s5
\c 73
\p Zaburi ya Asafu.
\v 1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale walio na moyo safi.
\v 2 Lakini kwangu mimi, kidogo tu miguu yangu iteleze; miguu yangu karibu iteleze kutoka kwangu
\v 3 kwa sababu niliwaonea wivu wenye kiburi nilipoona mafanikio ya waovu.
\s5
\v 4 Kwa maana hawana maumivu hadi kufa kwao, lakini wana nguvu na wameshiba.
\v 5 Wako huru dhidi ya mizigo ya watu wengine; nao hawateswi kama watu wengine.
\s5
\v 6 Kiburi kinawapamba kama mkufu kwenye shingo zao; jeuri huwavika kama vazi.
\v 7 Katika upofu wa jinsi hii dhambi huja; mawazo maovu hupita mioyoni mwao.
\s5
\v 8 Wao hudhihaki na kuongea kwa namna ya uovu; kwa kiburi chao hutishia mateso.
\v 9 Wameweka vinywa vyao dhidi ya mbingu, na ndimi zao hutanga tanga duniani.
\s5
\v 10 Kwa hiyo watu wake huwageukia na maji yaliyojaa hukaushwa.
\v 11 Nao husema, "Mungu anajuaje? Yako maarifa kwake yeye aliye juu?"
\v 12 Fahamu: watu hawa ni waovu; mara zote hawajali, wakifanyika matajiri na matajiri.
\s5
\v 13 Hakika nimeutunza moyo wangu bure na nimenawa mikono yangu pasipo kukosa.
\v 14 Maana mchana kutwa nimeteswa na kuadhibiwa kila asubuhi.
\v 15 Kama ningesema, "Ningesema mambo haya," kumbe nigewasaliti kizazi hiki cha watoto wenu.
\s5
\v 16 Ingawa nilijaribu kuyaelewa mambo haya, yalikuwa ni magumu sana kwangu.
\v 17 Ndipo nilipoingia patakatifu pa Mungu na kuelewa hatma yao.
\s5
\v 18 Hakika wewe huwaweka penye utelezi; huwaangusha mpaka palipoharibika.
\v 19 Jinsi gani wamekuwa ukiwa kwa muda mfupi! Wamefika mwisho nao wamemaliza kwa utisho.
\v 20 Wao ni kama ndoto wakati wa mtu kuamka; Bwana, utakapo inuka, utazidharau ndoto zao.
\s5
\v 21 Maana moyo wangu ulipata uchungu, nami nilijeruhiwa sana.
\v 22 Nilikuwa mjinga na sijui neno; nilikuwa kama mnyama tu mbele yako.
\s5
\v 23 Lakini mimi nipo pamoja nawe daima; umenishika mkono wa kuume.
\v 24 Utaniongoza kwa shauri lako na baadaye utanipokea katika utukufu.
\s5
\v 25 Ni nani niliye naye mbinguni isipokuwa wewe? Hakuna nimtamaniye duniani isipokuwa wewe.
\v 26 Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.
\s5
\v 27 Wale walio mbali nawe wataangamia; utawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
\v 28 Lakini mimi, linipasalo kufanya ni kumkaribia Mungu. Nimemfanya Bwana Yahwe kimbilio langu. Nami nitayatangaza matendo yako yote.
\s5
\c 74
\p Zaburi ya Asafu.
\v 1 Mungu, kwa nini umetukataa milele? Kwa nini hasira yako inawaka dhidi ya kondoo wa malisho yako?
\v 2 Wafikilie watu wako, ambao uliwanunua siku nyingi zilizopita, kabila ambalo wewe umelikomboa liwe urithi wako, na Milima Sayuni, mahali uishipo.
\s5
\v 3 Uje utazame uharibifu kamili, uharibifu ambao umefanywa na adui mahali patakatifu.
\v 4 Washindani wako walivamia katikati ya mahali pako maalumu; walipandisha bendera zao za vita.
\v 5 Walipakatakata kwa shoka kama katika msitu mnene.
\v 6 Walipaharibu na kuvunja sanaa zilizonakshiwa zote; walizivunja kwa shoka na nyundo.
\s5
\v 7 Walipachoma patakatifu pako; walipanajisi mahari unapoishi, wakigongagonga kwenye ardhi.
\v 8 Walisema mioyoni mwao, "Tutawaharibu wote." Walichoma sehemu zako zote za kukutania katika nchi.
\s5
\v 9 Sisi hatuoni tena ishara; hakuna tena nabii, na hakuna yeyote miongoni mwetu ajuaye haya yatadumu kwa muda gani.
\v 10 Mpaka lini, Mungu, adui atakurushia wewe matusi? Je, atalitukana jina lako milele?
\v 11 Kwa nini umerudisha nyuma mkono wako, mkono wako wa kuume? Utoe mkono wako kwenye mavazi yako na uwaangamize.
\s5
\v 12 Lakini Mungu amekuwa mfalme wangu tangu enzi, akileta wokovu tuniani.
\v 13 Wewe uliigawa bahari; ulishambulia vichwa vya majitu ya kutisha baharini majini.
\s5
\v 14 Wewe ulishambulia vichwa vya lewiathani; na kumfanya awe chakula cha viumbe hai jangwani.
\v 15 Ulizifungulia chemchem na vijito; uliikausha mito itiririkayo.
\s5
\v 16 Mchana ni wako, na usiku ni wako pia; uliweka jua na mwezi mahari pake.
\v 17 Umeiweka mipaka ya nchi; umeumba majira ya joto na majira ya baridi.
\s5
\v 18 Kumbula vile adui alivyo vurumisha matusi kwako, Yahwe, na kwamba watu wapumbavu wamelitukana jina lako.
\v 19 Usimtoe njiwa afe kwa mnyama wa porini. Usiusahau milele uhai wa watu wako walio onewa.
\s5
\v 20 Kumbuka agano lako, maana majimbo ya giza ya nchi yamejaa maeneo ya vurugu.
\v 21 Usiwaache walioonewa warudishwe kwa aibu; uwaache maskini na walioonewa walisifu jina lako.
\s5
\v 22 Inuka Mungu, itetee heshima yako; kumbuka wajinga wanavyokutukana machana kutwa.
\v 23 Usisahau sauti ya adui zako au kelele za wale wanaoendelea kukuchafua.
\s5
\c 75
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Asafu, wimbo.
\v 1 Tunatoa shukrani kwako, Mungu; tunatoa shukrani, maana wewe unaufunua uwepo wako; watu huzungumza kuhusu kazi zako za ajabu.
\v 2 Kwa wakati maalum nitahukumu kwa haki.
\v 3 Ingawa nchi na wenyeji wote watatikisika katika hofu, ninaifanyia nchi nguzo za kutosha. Selah
\s5
\v 4 Nilisema kwa wenye kiburi, "Msiwe wenye kiburi," na kwa waovu, "Msiinue mapembe.
\v 5 Msiinue mapembe yenu kwenye marefu; wala msizungumze kwa shingo ya kiburi."
\v 6 Sio kutoka mashariki au magharibi, na wala sio kutoka jangwani ambako kuinuliwa kunakuja.
\s5
\v 7 Bali Mungu ni muhumkumu; humshusha huyu na kumuinua huyu.
\v 8 Kwa kuwa Yahwe kashikilia mkononi mwake kikombe cha mvinyo wenye povu, ambao umechanganywa na vilolezo, naye huimimina. Hakika waovu wote wa duniani watakunywa mvinyo hadi tone la mwisho.
\s5
\v 9 Bali mimi nitaendelea kusema yale ambayo umeyatenda; nami nitamwimbia sifa Mungu wa Yakobo.
\v 10 Yeye husema, "Nitayakata mapembe yote ya waovu, lakini mapembe ya wenye haki yatainuliwa."
\s5
\c 76
\p Kwa kiongozi wa muziki, kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi ya Asafu, wimbo.
\v 1 Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
\v 2 Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
\v 3 Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. Selah
\s5
\v 4 Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
\v 5 Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.
\s5
\v 6 Kwa kukemea kwako, ewe Mungu wa Yakobo, wote gari na farasi walilala mauti.
\v 7 Wewe, ndiyo wewe, ni wa kuogopwa; ni nani awezaye kusimama mbele yako wakati ukiwa na hasira?
\s5
\v 8 Kutoka mbinguni wewe uliifanya hukumu yako isikike; nchi iliogopa na ikaa kimya
\v 9 wakati wewe, Mungu, ulipoinuka kutekeleza hukumu na kuwaokoa wote wa nchi walio onewa. Selah
\s5
\v 10 Hakika hukumu ya hasira yako dhidi ya binadamu itakuletea wewe sifa; wewe hujifunga mwenyewe hasira yako iliyo baki.
\s5
\v 11 Wekeni nadhiri kwa Yahwe Mungu wenu na kuzihifadhi. Nao wote wamzungukao yeye mleteeni zawadi yeye ambaye ni wa kuogopwa.
\v 12 Yeye huzikata roho za wakuu; huogopwa na wafalme wa nchi.
\s5
\c 77
\p Kwa kiongozi wa muziki; baada ya manner ya Jeduthun. Zaburi ya Asafu.
\v 1 Nitampazia Mungu sauti yangu, nitamuita Mungu kwa sauti yangu, na Mungu wangu atanisikia.
\s5
\v 2 Katika siku ya taabu nilimtafuta Bwana; usiku niliinua mikono yangu, nayo haikuchoka. Moyo wangu ulikataa kufarijiwa.
\v 3 Ningali nikiugua nilielekeza mawazo yangu kwa Mungu. Nilimfikiria Mungu nilipokuwa dhaifu. Selah
\s5
\v 4 Uliyafanya macho yangu yasisinzie; nilisumbuka sana kuongea.
\v 5 Nilifikiri kuhusu siku za kale, kuhusu mambo yaliyopita muda mrefu.
\s5
\v 6 Wakati wa usiku niliukumbuka wimbo niliouimba mara moja. Nilifikiria kwa makini na kujaribu kuelewa kile kilichokuwa kimetokea.
\v 7 Je, Mungu atanikataa milele? Je, hatanionesha tena huruma?
\s5
\v 8 Je, uaminifu wa agano lake ulikuwa umetoweka milele? Je, ahadi yake imeshindwa milele?
\v 9 Je, Mungu amesahau kuwa mwenye neema? Je, hasira yake imeifunga huruma yake? Selah
\s5
\v 10 Nilisema, "Hii ni huzuni yangu: mabadiliko ya mkono wa kuume wa Aliye Juu dhidi yetu."
\s5
\v 11 Lakini nitayakumbuka matendo yako, Yahwe; nitafikiri kuhusu matendo yako makuu yaliyopita.
\v 12 Nitayatafakari matendo yako yote nami nitayaishi.
\s5
\v 13 Njia yako, Mungu, ni takatifu; ni mungu gani wa kulinganishwa na Mungu wetu aliye mkuu?
\v 14 Wewe ni Mungu utendaye maajabu; wewe umeonesha nguvu zako kati ya mataifa.
\v 15 Uliwapa watu wako ushindi kwa uweza wako mkuu - ukoo wa Yakobo na Yusufu. Selah
\s5
\v 16 Maji yalikuona wewe, Mungu; maji yalikuona wewe, nayo yakaogopa; vina vya maji vilitetemeka.
\v 17 Mawingu yalitiririsha maji chini; anga zito lilitoa sauti; mishale yako ilipita kati.
\s5
\v 18 Sauti yako kama ya radi ilisikika katika upepo; radi iliwasha dunia; nchi iliogopa na kutetemeka.
\v 19 Njia yako ilipita baharini na mapito yako katika maji mengi, lakini alama za miguu yako hazikuonekana.
\v 20 Uliwaongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Musa na Haruni.
\s5
\c 78
\p Zaburi ya Asafu.
\v 1 Watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu.
\v 2 Nitafungua kinywa changu katika mifano; nitaimba kuhusu mambo yaliyofichika yahusuyo yaliyopita.
\s5
\v 3 Haya ni mambo ambayo tumeyasikia na kujifunza mambo ambayo mababu zetu wametuambia sisi. Hatutawaficha uzao wao.
\v 4 Tutawaambia kizazi kijacho kuhusu sifa anazostahili Yahwe kwa matendo yake, nguvu zake, na maajabu ambayo ameyafanya.
\s5
\v 5 Kwa kuwa yeye alianzisha agano la amri katika Yakobo na sheria maalumu katika Israeli. Yeye aliamuru mababu zetu kuwa walipaswa kuzifundisha kwa watoto wao.
\v 6 Aliamuru hivi ili kwamba kizazi kijacho kiweze kuzijua amri zake, ili wawafundishe wana ambao bado hawajazaliwa.
\s5
\v 7 Kisha wangeweka tumaini lao katika Mungu na kutokusahau matendo yake bali wazishike amri zake.
\v 8 Ndipo wasingekuwa kama mababu zao, ambao walikuwa wakaidi na wenye uasi, kizazi ambacho mioyo yao haikuwa kamilifu, na ambao roho zao hazikuwa na nia thabiti na aminifu kwa Mungu.
\s5
\v 9 Waefraimu walikuwa na silaha na upinde, lakini walikimbia siku ya vita.
\v 10 Hawakutunza agano na Mungu, na walikataa kutii sheria yake.
\v 11 Walisahau matendo yake, mambo ya ajabu ambayo yeye amewaonesha wao.
\s5
\v 12 Walisahau mambo ya ajabu aliyofayafanya machoni pa mababu zao katika nchi ya Misri, katika ardhi ya Soani.
\v 13 Aliigawa bahari na akawaongoza katikati ya bahari; aliyafanya maji yasimame kama kuta.
\v 14 Wakati wa mchana aliwaongoza kwa wingu na usiku wote kwa nuru ya moto.
\s5
\v 15 Alipasua miamba jangwani, na aliwapa maji mengi, ya kutosha kujaza vina virefu vya bahari.
\v 16 Alifanya maporomoko ya maji kutiririka tokea mwambani na aliyafanya maji yatiririke kama mito.
\s5
\v 17 Lakini bado waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi dhidi ya Aliye Juu katika jangwa.
\v 18 Walimjaribu Mungu mioyoni mwao kwa kuomba chakula cha kuwatosheleza hamu zao.
\s5
\v 19 Waliongea dhidi ya Mungu; walisema, "Kweli Mungu anaweza kuweka meza ya chakula kwa ajili yetu jangwani?
\v 20 Tazama, wakati alipoupiga mwamba, maji yalibubujika, mito ikafurika. Lakini anaweza kutoa mkate tena? Ataweza kuleta nyama kwa watu wake?"
\s5
\v 21 Yahwe aliposikia haya, alikasirika; moto wake uliwaka dhidi ya Yakobo, hasira yake ikamshambulia Israeli,
\v 22 kwa sababu hawakumwamini Mungu na hawakuamini katika wokovu wake.
\s5
\v 23 Lakini yeye bado aliziamuru mbingu juu na kufungua milango ya mbingu.
\v 24 Aliwanyeshea mana ili wale, na aliwapa nafaka kutoka mbinguni.
\v 25 Watu walikula mikate ya malaika. Aliwatumia chakula kingi.
\s5
\v 26 Alisababisha upepo wa mashariki kupiga mawinguni, na kwa uweza wake aliuongoza upepo wa kusini.
\v 27 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, na ndege kama wingi wa mchanga wa baharini.
\v 28 Walianguka katikati ya kambi yao, na maeneo yote karibu na hema zao.
\s5
\v 29 Hivyo walikula na walishiba. Maana aliwapa kile walichokitamani sana.
\v 30 Lakini walikuwa bado hawajatosheka; chakula chao kilikuwa bado kinywani mwao.
\s5
\v 31 Ndipo hasira ya Mungu iliwashambulia na kuwaua wenye nguvu kati yao. Aliwaangusha chini vijana wa Israeli.
\v 32 Licha ya hili, waliendelea kutenda dhambi na hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.
\s5
\v 33 Hivyo Mungu alizikatisha siku zao; miaka yao ilijawa na hofu.
\v 34 Wakati wowote Mungu alipowataabisha, nao waligeuka na kumtafuta yeye kwa bidii.
\s5
\v 35 Walikumbuka kuwa Mungu alikuwa mwamba wao na kuwa Mungu Aliye Juu Sana alikuwa mwokozi wao.
\v 36 Lakini walimsifia tu kwa vinywa vyao na kumdanganya kwa maneno yao.
\v 37 Maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, na hawakuwa waaminifu kwa agano lake.
\s5
\v 38 Lakini yeye, kwa kuwa alikuwa alikuwa na huruma, aliwasamehe uovu wao na hakuwaangamiza. Ndiyo, wakati mwingi aliizuia hasira yake na hakuionesha ghadhabu yake yote.
\s5
\v 39 Alikumbuka kuwa waliumbwa kwa mwili, upepo ambao hupita nao haurudi.
\v 40 Mara ngapi wameasi dhidi yake jangwani na kumuhuzunisha nyikani!
\v 41 Tena na tena walimjaribu Mungu na wakamtilia mashaka Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 42 Hawakufikiria kuhusu uweza wake, jinsi alivyo waokoa dhidi ya adui
\v 43 alipofanya ishara za kutisha katika Misri na maajabu yake katika konde la Soani.
\s5
\v 44 Aligeuza mito ya Wamisri kuwa damu ili wasipate kunywa kutoka katika vijito vyao.
\v 45 Alituma makundi ya inzi yaliyowavamia na vyura ambao walisambaa katika nchi yao.
\v 46 Aliwapa mazao yao panzi na kazi yao nzige.
\s5
\v 47 Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na miti ya mikuyu kwa mvua ya mawe zaidi.
\v 48 Aliinyeshea mifugo yao mvua ya mawe na alirusha radi ya umeme ikapiga mifugo yao. Ukali wa hasira yake ulielekea dhidi yao.
\v 49 Alituma gadhabu, uchungu na taabu kama wakala aletaye maafa.
\s5
\v 50 Aliifanyia njia hasira yake; hakuwakinga dhidi ya kifo bali aliwakabidhi kwa pigo.
\v 51 Aliwaua wazaliwa wote wa kwanza katika Misri, wazaliwa wa kwanza wa nguvu zao katika mahema ya Hamu.
\s5
\v 52 Aliwaongoza nje watu wake mwenyewe kama kondoo na aliwaelekeza kupitia jangwani kama kundi.
\v 53 Aliwaongoza salama na pasipo na woga, lakini bahari iliwaelemea adui zao.
\s5
\v 54 Kisha aliwaleta mpaka wa nchi yake takatifu, kwenye mlima huu ambao aliutwaa kwa mkono wake wa kuume.
\v 55 Aliwafukuza mataifa mbele yao na akawapa urithi wao. Aliwakalisha makabila ya Israeli katika mahema yao.
\s5
\v 56 Lakini bado walimjaribu na walimkaidi Mungu Aliye Juu na hawakushika amri zake takatifu.
\v 57 Hawakuwa waaminifu na walienenda katika hila kama baba zao; walikuwa sio wa kutegemewa kama upinde mbovu.
\s5
\v 58 Kwa maana walimkasirisha kwa mahali pao pa juu na walimgadhabisha hata akawa na hasira ya wivu kwa miungu yao.
\v 59 Mungu aliposikia hili, alikasirika na alimkataa kabisa Israeli.
\s5
\v 60 Alipaacha patakatifu pa Shilo, na hema alikoishi kati ya watu.
\v 61 Aliruhusu nguvu zake kutekwa na kuutoa utukufu wake mkononi mwa adui.
\s5
\v 62 Aliukabidhi upanga watu wake, na aliukasirikia urithi wake.
\v 63 Moto uliwavamia vijana wao wa kiume, na vijana wao wa kike hawakuwa na nyimbo za harusi.
\s5
\v 64 Makuhani wao waliangushwa kwa upanga, na wajane wao hawakulia.
\v 65 Kisha Bwana aliamshwa kama aliyetoka usingizini, kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo.
\v 66 Aliwarudisha adui zake nyuma; aliwaweka kwenye aibu ya milele.
\s5
\v 67 Aliikataa hema ya Yusufu, na hakulichagua kabila la Efraimu.
\v 68 Alilichagua kabila la Yuda na Mlima Sayuni aliyoupenda.
\v 69 Alipajenga patakatifu pake kama mbinguni, na kama nchi aliyoiimarisha milele.
\s5
\v 70 Alimchagua Daudi, mtumishi wake, alimchukua kutoka zizi la kondoo.
\v 71 Alimtoa kutoka katika kufuata kondoo pamoja na wana wao, na kumweka kuwa mchungaji wa Yakobo, watu wake, na Israeli, urithi wake.
\v 72 Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo wake, naye aliwaongoza kwa ujuzi wa mikono yake.
\s5
\c 79
\p
\v 1 Zaburi ya Asafu. Mungu, Mataifa ya kigeni yameingia kwenye urithi wako; wamelinajisi hekalu lako takatifu; wameigeuza Yerusalemu kuwa chungu cha magofu.
\v 2 Wamezitoa maiti za watumishi wako ziwe chakula cha ndege wa angani, miili ya watakatifu wako iwe chakula cha wanyama wa nchi.
\v 3 Wamemwaga damu zao kama maji sehemu zote za Yesrusalemu, na hakuwepo wa kuwazika.
\s5
\v 4 Sisi tumekuwa aibu kwa majirani zetu, tukidhihakiwa na kuzomewa na wale wanaotuzunguka.
\v 5 Mpaka lini Yahwe? Utabaki kuwa na hasira milele? Ni kwa muda gani hasira yako ya wivu itawaka kama moto?
\s5
\v 6 Mwaga hasira yako juu ya mataifa ambayo hayakujui wewe na ufalme ambao hauliiti jina lako.
\v 7 Kwa maana walimvamia Yakobo na waliharibu kijiji chake.
\s5
\v 8 Usiendelee kukumbuka dhambi za baba zetu dhidi yetu; matendo yako ya huruma yaje kwetu, maana tuko chini.
\v 9 Utusaidie, Mungu wa wokovu wetu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako; utuokoe na usamehe dhambi zetu kwa ajili ya jina lako.
\s5
\v 10 Kwa nini mataifa yalazimike kusema, "Mungu wao yuko wapi?" Damu ya watumishi wako ambayo ilimwagwa na ilipize kisasi juu ya mataifa mbele ya macho yako.
\v 11 Kilio cha wafungwa na kije mbele zako; kwa uweza wa nguvu zako uwaweke ai wana wa mauti.
\s5
\v 12 Uwalipize majirani zetu vifuani mwao mara saba zaidi ya walivyo kutukana wewe, Bwana.
\v 13 Hivyo sisi watu wako na kondoo wa malisho yako tutakushukuru milele. Tutazisimulia sifa zako kwa vizazi vyote.
\s5
\c 80
\p Kwa kiongozi wa muziki, seti kwenye mtindo wa Shoshannim Eduth. Zaburi ya Asafu.
\v 1 Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie!
\v 2 Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe.
\v 3 Mungu, uturejeshe sisi; uangaze uso wako juu yetu, nasi tutaokolewa.
\s5
\v 4 Yahwe Mungu wa majeshi, mpaka lini utawakasirikia watu wako wanapoomba?
\v 5 Umewalisha wa mkate wa machozi na umewapa machozi ili wanywe katika kiasi kikubwa.
\v 6 Umetufanya kitu kwa ajili ya majirani zetu kubishania, na maadui zetu hucheka kuhusu sisi kati yao.
\s5
\v 7 Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; nasi tutaokolewa.
\v 8 Wewe ulileta mzabibu kutoka Misri; ukawafukuza mataifa na ukaupanda.
\s5
\v 9 Uliisafisha ardhi kwa ajil yake; nao ulipata mzizi na kuijaza nchi.
\v 10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, mierezi ya Mungu kwa matawi yake.
\v 11 Ilieneza matawi yake mbali kama bahari na mashina yake mpaka kwenye Mto Euphrates.
\s5
\v 12 Kwa nini umezibomoa kuta zake hata wapitao karibu huyachuma matunda yake.
\v 13 Ngurue wa msituni wanauharibu, na wanyama wa kondeni wanaula.
\s5
\v 14 Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu.
\v 15 Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue.
\v 16 Yamekatwa na kuchomwa; yameangamia kwa sababu ya kukemea kwako.
\s5
\v 17 Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe.
\v 18 Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.
\s5
\v 19 Yahwe, Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; utuangazie nuru ya uso wako, nasi tutaokolewa.
\s5
\c 81
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye mtindo wa Gittith.
\v 1 Mwimbieni Mungu aliye nguvu yetu kwa sauti; pigeni kelele za furaha kwa Mungu wa Yakobo.
\v 2 Imbeni wimbo na pigeni matari, kinubi chenye sauti nzuri pamoja na kinanda.
\v 3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, katika siku ya mbalamwezi, mwanzoni mwa sikukuu.
\s5
\v 4 Kwa kuwa ni agizo kwa Israeli, amri iliyotolewa na Mungu wa Yakobo.
\v 5 Aliitoa kama maelekezo kwa Yusufu alipoenda katika nchi ya Misri, ambako nilisikia sauti ambayo sikuweza kuitambua:
\s5
\v 6 "Niliutua mzigo kutoka mabegani mwake; mikono yake ilipumzishwa kubeba kikapu.
\v 7 Katika dhiki yako uliniita, nami nikakusaidia; nilikujibu kutoka katika wingu jeusi la radi. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. Selah
\s5
\v 8 Sikilizeni, watu wangu, nami nitawaonya, Israeli, kama tu ugalinisikiliza!
\v 9 Lazima kati yenu kusiwepo na mungu wa kigeni; haupaswi kumwabudu mungu wa kigeni.
\v 10 Mimi ni Yahwe niliyekutoa katika nchi ya Misri, fungua sana kinywa chako, nami nitakijaza.
\s5
\v 11 Lakini watu wangu hawakusikiliza maneno yangu; Israeli hawakunitii.
\v 12 Nikawaacha waende katika katika njia yao wenyewe ya ukaidi ili kwamba waweze kufanya kinachoonekana sahihi kwao.
\s5
\v 13 Oh, laiti watu wangu wangenisikiliza mimi; oh, watu wangu wangelitembea katika njia yangu.
\v 14 Kisha ningewatiisha adui zao haraka na kugeuzia mkono wangu dhidi ya watesi wao.
\s5
\v 15 Wale wanaomchukia Yahwe katika hofu na waanguke chini mbele zake! Wawe wanyonge milele.
\v 16 Ningewalisha Israeli kwa ngano bora; Ningewatosheleza kwa asali itokayo mwambani."
\s5
\c 82
\p Zaburi ya Asafu.
\v 1 Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.
\v 2 Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah
\s5
\v 3 Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.
\v 4 Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.
\s5
\v 5 Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.
\s5
\v 6 Mimi nilisema, "Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.
\v 7 Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu."
\s5
\v 8 Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.
\s5
\c 83
\p Wimbo. Zaburi ya Asafu.
\v 1 Ee Mungu, usikae kimya! usitupuuze na kustarehe, Ee Mungu.
\v 2 Tazama, adui zako wanafanya vurugu, na wale wakuchukiao wameinua vichwa vyao.
\s5
\v 3 Wanafanya hila juu ya watu wako na kwa pamoja kupanga njama dhidi ya wale uwalindao. Wamesema,
\v 4 "Njoni na tuwaangamize wao kama taifa. Kisha jina la Israeli halitakumbukwa."
\v 5 Wamepanga njama pamoja wakiwa na mkakati mmoja; wamefanya muungano dhidi yako.
\s5
\v 6 Hii inajumuisha hema za Edomu na Waishmaeli, na watu wa Moabu na Wahagari, ambao wamepanga njama pamoja nao
\v 7 Gebal, Amoni, Amaleki; pia inajumuisha Filisti na wenyeji wa Tiro.
\s5
\v 8 Ashuri pia ameshirikina nao; wanawasaidia wana wa Lutu. Serah
\s5
\v 9 Ufanye kwao kama ulivyofanya kwa Midiani, kama ulivyofanya kwa Sisera na kwa Yabini kwenye Mto Kishoni.
\v 10 Waliangamizwa kule Endori na wakawa kama mbolea juu ya chi.
\s5
\v 11 Uvifanye vyeo vyao kama Oreb na Zeeb, na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
\v 12 Wao walisema, natujimilikishe malisho ya Mungu."
\s5
\v 13 Ee Mungu wangu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi mbele ya upepo,
\v 14 Kama moto uteketezao msitu, na kama miali ya moto iwakayo milimani.
\v 15 Uwafuatie kwa tufani yako, na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
\s5
\v 16 Uwajaze nyuso zao kwa aibu ili kwamba waweze kulitafuta jina lako, Yahwe.
\v 17 Nao waaibishwe na kufadhaishwa milele; waangamizwe katika aibu.
\s5
\v 18 Kisha watajua kwamba ni wewe pekee, Yahwe, Uliye Juu ya nchi yote.
\s5
\c 84
\p Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye mtindo wa Gittith. Zaburi ya wana wa Kora.
\v 1 Ni jinsi gani maskani yako yapendeza, Ewe Yahwe wa Majeshi!
\v 2 Ninashauku ya kuingia nyumbani mwa Yahwe, nimechoka sana kwa sababu ninatamani sana kuwa nyumani mwako. Moyo wangu na mwili wangu wote wakuita wewe Mungu uliye hai.
\s5
\v 3 Hata Shomoro naye amepata nyumba yake na mbayuwayu amejipatia kiota kwa ajili yake mwenyewe mahali awezapo aweza kuweka makinda yake karibu na madhabahu yako, Ee Yahwe wa majeshi, Mfalme wangu, na Mungu wangu.
\v 4 Wamebarikiwa wale ambao huishi katika nyumba yako; nao hukusifu wewe siku zote. Selah
\s5
\v 5 Amebarikiwa mtu yule ambaye nguvu zake ziko katika wewe, katika moyo wake mna njia kuu ziendazo mpaka Sayuni.
\v 6 Wanapopita katika bonde la machozi, hupata chemchem ya maji kwa ajili ya kunywa. Mvua ya vuli hulivika baraka.
\s5
\v 7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu; kila mmoja wao katika sayuni huonekana mbele ya Mungu.
\v 8 Yahwe Mungu wa majeshi, sikia maombi yangu; Mungu wa Yakobo, usikilize nisemacho! Selah
\v 9 Ee Mungu, uiangalie ngao yetu; uwaangalie wapakwa mafuta wako.
\v 10 Kwa maana siku moja katika nyumba yako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine. Ni bora niwe mlinzi wa mlango katika nyumba ya Mungu wangu, kuliko kuishi katika mahema ya waovu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa Yahwe Mungu ni jua letu na ngao yetu; Yahwe atatoa neema na utukufu; hazuii zuri lolote kwa wale ambao hutembea katika uadilifu.
\v 12 Yahwe wa majeshi, amebarikiwa mtu yule anaye kutumainia wewe.
\s5
\c 85
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Kora.
\v 1 Yahwe, wewe umeonesha fadhilia kwenye nchi yako; umeurejesha ustawi wa Yakobo.
\v 2 Umesamehe dhambi ya watu wako; umezisitiri dhambi zao zote. Selah
\s5
\v 3 Umeondoa ghadhabu yako yote; umeiacha hasira yako kali.
\v 4 Uturejeshe sisi, Ee Mungu wa wokovu wetu, na uikomeshe chuki yako juu yetu.
\v 5 Je! Utaendelea kuwa na hasira juu yetu milele? utadumisha hasira kizazi chote kijacho?
\s5
\v 6 Je, hautatuhuisha tena? Kisha watu wako watafurahia katika wewe.
\v 7 Utuoneshe sisi uaminifu wa agano lako, Yahwe, utupe sisi wokovu wako.
\s5
\v 8 Nitasikiliza yale Yahwe Mungu asemayo, maana yeye atafanya amani pamoja na watu wake, wafuasi wake waminifu. Lakini lazima wasirudi tena katika njia za kipumbavu.
\v 9 Hakika wokovu wake u karibu na wale wanao mwabudu yeye; kisha utukufu utabaki katika nchi yetu.
\s5
\v 10 Uaminifu wa agano na uaminifu vimekutana pamoja; haki na amani vimebusiana.
\v 11 Uaminifu unatoa chemchem kutoka ardhini, na haki hutazama chini kutoka mawinguni.
\s5
\v 12 Ndiyo, Yahwe atatoa baraka zake njema, na nchi itatoa mazao yake.
\v 13 Haki itaenda mbele zake na kufanya njia kwa ajili ya nyayo zake.
\s5
\c 86
\p Maombi ya Daudi.
\v 1 Sikia, Ee Yahwe, na unijibu, kwa kuwa ni maskini na mnyonge.
\v 2 Unilinde, maana mimi ni mwaminifu; Mungu wangu, umuokoe mtumishi wako anayekuamini.
\s5
\v 3 Unihurumie, Bwana, maana ninakulilia wewe mchana kutwa.
\v 4 Umfurahishe mtumishi wako, maana ni kwako, Bwana, ninaomba.
\s5
\v 5 Wewe, Bwana, ni mwema, na uko tayari kusamehe, na huonesha huruma kubwa kwa wale wanao kulilia wewe.
\v 6 Yahwe, sikiliza maombi yangu; sikia sauti ya ombi langu.
\v 7 Katika siku ya shida ninakuita wewe, kwa maana utanijibu.
\s5
\v 8 Katikati ya miungu hakuna wa kufananishwa na wewe, Bwana. Hakuna matendo kama matendo yako.
\v 9 Mataifa yote ambayo umeyafanya yatakuja kwako na kusujudu mbele zako, Bwana. nao wataliheshimu jina lako.
\s5
\v 10 Kwa kuwa wewe ni mkuu na utendaye mambo ya ajabu; wewe pekee ndiwe Mungu.
\v 11 Unifundishe njia zako, Yahwe. Kisha nitatembea katika kweli yako. Unifanye kukuheshimu wewe.
\v 12 Bwana Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wangu wote; nitalitukuza jina lako milele.
\s5
\v 13 Kwa maana uaminifu wa agano lako ni mkuu kwangu; wewe umeokoa uhai wangu kutoka chini kuzimuni.
\v 14 Ee Mungu, wenye kiburi wameinuka dhidi yangu. Kundi la watu wenye vurugu wanautafuta uhai wangu. Nao hawakuheshimu wewe.
\s5
\v 15 Lakini wewe, Bwana, ni mwenye huruma na neema, hukasiliki haraka, na mwingi katika uaminifu wa agano lako na kweli.
\v 16 Unigeukie na unihurumie; mpe nguvu zako mtumishi wako; umuokoe mwana wa mjakazi wako.
\v 17 Unioneshe ishara ya fadhila zako. Kisha wale wanichukiao wataziona na kuaibishwa kwa sababu yako; Yahwe, umenisaidia na kunifariji.
\s5
\c 87
\p Zaburi ya wana wa Kora; wimbo.
\v 1 Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;
\v 2 Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.
\v 3 Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah
\s5
\v 4 Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'"
\s5
\v 5 Itasemwa juu ya Sayuni, "Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.
\v 6 Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, "Huyu alizaliwa humo." Selah
\s5
\v 7 Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, "chemchem zangu zimo kwako."
\s5
\c 88
\p Wimbo, Zaburi ya wana wa Kora; kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye mtindo wa Mahalath Leannoth. Zaburi ya Heman mu Ezrahite.
\v 1 Yahwe, Mungu wa wokovu wangu, ninalia mchana na usiku mbele zako.
\v 2 Sikiliza maombi yangu; utazame kulia kwangu.
\s5
\v 3 Maana nimejawa taabu, na uhai wangu umefika kuzimuni.
\v 4 Watu hunichukulia kama wale waendao chini shimoni; mimi ni mtu asiye na nguvu.
\s5
\v 5 Nimetelekezwa miongoni mwa wafu; niko kama mfu alalaye katika kaburi, wao ambao wewe huwajari tena kwa sababu wametengwa mbali na nguvu zako.
\v 6 Wewe umeniweka katika sehemu ya chini kabisa ya shimo, sehemu yenye giza na kilindini.
\s5
\v 7 Gadhabu yako yanielemea, na mawimbi yako yote yanatua juu yangu. Selah
\s5
\v 8 Kwa sababu yako, wale wanijuao wote hunikwepa. Umenifanya wakutisha machoni pao. Nimefungwa na siwezi kutoroka.
\s5
\v 9 Macho yangu yamefifia kutokana na shida; kila siku nakuita wewe, Yahwe; ninakunyoshea wewe mikono yangu.
\v 10 Je! utafanya miujiza kwa ajili ya wafu? Wale waliokufa watafufuka na kukusifu wewe? Selah
\s5
\v 11 Uaminifu wa agano lako utatangazwa kaburini? au uaminifu wako mahali pa wafu?
\v 12 Matendo yako ya ajabu yatajulikana gizani? au haki yako katika mahali pa usahaulifu?
\s5
\v 13 Lakini ninakulilia wewe, Yahwe; wakati wa asubuhi maombi yangu huja kwako.
\v 14 Yahwe, kwa nini unanikataa? Kwa nini unauficha uso wako mbali nami?
\s5
\v 15 Nimekuwa nikiteswa kila siku na hatihati ya kifo tangu ujana wangu. Nimeteseka dhidi ya hofu yako kuu; ninakata tamaa.
\v 16 Matendo yako ya hasira yamepita juu yangu, na matendo yako ya kutisha yameniangamiza.
\s5
\v 17 Siku zote yananizingira mimi kama maji; yote yamenizunguka mimi.
\v 18 Wewe umemuondoa kwangu kila rafiki na anijuaye. Na sasa anijuaye pekee ni giza.
\s5
\c 89
\p Zaburi ya Ethan Muezrahite.
\v 1 Nitimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele. Nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo.
\v 2 Maana nimesema, "Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni."
\s5
\v 3 "Nimefanya agano na wateule wangu, nimeapa kiapo kwa Daudi mtumishi wangu.
\v 4 Nitauimarisha uzao wako milele, na nitauimarisha utawala wako vizazi vyote." Selah
\s5
\v 5 Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
\v 6 Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
\s5
\v 7 Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
\v 8 Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
\s5
\v 9 Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
\v 10 Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
\s5
\v 11 Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
\v 12 Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
\s5
\v 13 una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
\v 14 Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
\s5
\v 15 Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
\v 16 Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
\s5
\v 17 Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
\v 18 Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 19 Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, "Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
\v 20 Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
\v 21 Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
\v 22 Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
\v 23 Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
\s5
\v 24 Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
\v 25 Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
\v 26 Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
\s5
\v 27 Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.
\v 28 Nitaongeza uaminifu wa agano langu kwake milele; na agano langu pamoja naye litakuwa salama.
\v 29 Nitaufanya uzao wake kudumu milele na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu zilizo juu.
\s5
\v 30 Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
\v 31 na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
\v 32 ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
\s5
\v 33 Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
\v 34 Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
\s5
\v 35 Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
\v 36 uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
\v 37 Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni." Selah
\s5
\v 38 Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
\v 39 Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
\v 40 Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
\s5
\v 41 Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
\v 42 Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
\v 43 Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
\s5
\v 44 Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.
\v 45 Umefupisha siku za ujana wake. Umemfunika kwa aibu. Selah
\s5
\v 46 Mpaka lini, Yahwe? utajificha, milele? Mpaka lini hasira yako itawaka kama moto?
\v 47 Oh, fikiria jinsi muda wangu ulivyo mfupi, na ni kwa ajili gani umewaumba wana wote wa wanadamu wasio na manufaa!
\v 48 Ni nani aweza kuishi na asife, au atakaye iokoa nafsi yake dhidi ya mkono wa kuzimu? Selah
\s5
\v 49 Bwana, yako wapi matendo yako ya zamani ya uaminifu wa agano ambayo ulimwapia Daudi katika kweli yako?
\v 50 Kumbuka, Bwana, watumishi wako walivyodhihakiwa na vile nilivyo vumilia moyoni mwangu matusi mengi dhidi ya mataifa.
\v 51 Maadui zako wanavurumiza matusi, Yahwe; wanadhihaki nyayo za mpakwa mafuta wako.
\s5
\v 52 Atukuzwe Yahwe milele. Amina na Amina. Kitabu cha Nne
\s5
\c 90
\p Maombi ya Musa mtu wa Mungu.
\v 1 Bwana, wewe umekuwa kimbilio letu vizazi vyote.
\v 2 Kabla milima haijaumbwa, wala haujaumba nchi na dunia, tangu milele na milele, wewe ni Mungu.
\s5
\v 3 Humrudisha mtu mavumbini, na kusema, "Rudi, ewe uzao wa mwanadmu.
\v 4 Kwa maana miaka elfu machoni pako ni kama jana ipitapo, na kama saa wakati wa usiku.
\s5
\v 5 Huwafagia kama vile kwa mafuliko nao hulala; na wakati wa asubuhi wako kama majani yameayo.
\v 6 Asubuhi yachipuka na kumea; jioni yakatika na kukauka.
\s5
\v 7 Hakika, tumeangamizwa kwa hasira yako, na gadhabu yako inatuogopesha sana.
\v 8 Umeudhihirisha uovu wetu mbele zako, na dhambi zetu zilizofichika katika nuru ya uwepo wako.
\s5
\v 9 Uhai wetu unatoweka chini ya gadhabu yako; Miaka yetu inapita haraka kama pumzi.
\v 10 Miaka yetu ni sabini, au themanini tukiwa na afya; lakini hata hivyo miaka yetu mizuri imetiwa alama ya taabu na huzuni. Ndiyo, inapita haraka, kisha tunatoweka.
\s5
\v 11 Ni nani ajuaye kiwango cha hasira yako, na ghadhabu yako ambayo iko sawa na hofu yako?
\v 12 Hivyo utufundishe sisi kuyafikiria maisha yetu ili kwamba tuweze kuishi kwa hekima.
\v 13 Ugeuke, Ee Yahwe! Mpaka lini itakuwa hivi? Uwahurumie watumishi wako.
\s5
\v 14 Ututosheleze sisi wakati wa asubuhi kwa uaminifu wa agano lako ili kwamba tuweze kufurahi na kushangilia siku zote za maisha yetu.
\v 15 Utufurahishe kwa uwiano sawa na zile siku ulizo tutesa na kwa ile miaka tuliyopitia taabu.
\v 16 Watumishi wako na waione kazi yako, na watoto wetu wauone ukuu enzi yako.
\s5
\v 17 Na neema ya Bwana Mungu wetu iwe yetu; fanikisha kazi za mikono yetu; hakika, fanikisha kazi ya mikono yetu.
\s5
\c 91
\p
\v 1 Yeye aishiye katika makazi ya Aliye Juu atakaa katika uvuli wa mwenyezi.
\v 2 Nami nitasema kuhusu Yahwe, "Yeye ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye niaamini katika yeye."
\s5
\v 3 Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti.
\v 4 Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
\s5
\v 5 Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
\v 6 wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
\v 7 Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
\s5
\v 8 Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
\v 9 Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
\s5
\v 10 Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
\v 11 Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.
\s5
\v 12 Nao watakuinua juu kwa mikono yao ili usiweze kujigonga mguu wako kwenye jiwe.
\v 13 Utawaangamiza simba na nyoka chini ya miguu yako; utawakanyaga wana-simba na nyoka.
\s5
\v 14 Kwa sababu amejitoa kwangu, nitamuokoa. Nitamlinda kwa sababu yeye ni mwaminifu kwangu.
\v 15 Aniitapo, nitamjibu. Katika shida nitakuwa naye; nitampatia ushindi na nitamuheshimu.
\v 16 Nitamtosheleza kwa maisha malefu na kumuonesha wokovu wangu.
\s5
\c 92
\p Zaburi, wimbo kwa ajili ya siku ya Sabato.
\v 1 Ni jambo jema kumshukuru Yahwe na kuliimbia sifa jina lako, Uliye Juu,
\v 2 kutangaza uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi na uaminifu wako kila usiku,
\v 3 kwa kinubi cha nyuzi kumi na kwa tuni ya kinubi.
\s5
\v 4 Kwa kuwa wewe, Yahwe, matendo yako yamenifurahisha. Nitaimba kwa furaha kwa sababu ya matendo ya mikono yako.
\v 5 Ni jinsi gani matendo yako ni makuu, Yahwe! mawazo yako ni ya kina.
\s5
\v 6 Mtu mpumbavu hawezi kuyajua, wala mjinga kuyaelewa haya:
\v 7 Wasio haki watakapochipuka kama nyasi, na hata watendao uovu watakapo stawi, bado wataangamizwa kwenye uharibifu wa milele.
\s5
\v 8 Lakini wewe, Yahwe, utatawala milele.
\v 9 Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa.
\s5
\v 10 Wewe umeyainua mapembe yangu kama mapembe ya Nyati wa porini; nimepakwa mafuta safi.
\v 11 Macho yangu yameona kuanguka kwa adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya maadui zangu waovu.
\s5
\v 12 Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni.
\v 13 Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe; wakistawi katika nyua za Mungu wetu.
\s5
\v 14 Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya,
\v 15 kutangaza kuwa Yahwe ni wa haki. Yeye ni mwamba wangu, na hakuna udhalimu ndani yake.
\s5
\c 93
\p
\v 1 Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa.
\v 2 Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote.
\s5
\v 3 Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo.
\v 4 Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu.
\s5
\v 5 Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.
\s5
\c 94
\p
\v 1 Yahwe, Ee Mungu ulipaye kisasi, Mungu ulipaye kisasi, utuangazie sisi.
\v 2 Inuka, muhukumu wa nchi, uwape wenye majivuno kile wanachosahili.
\s5
\v 3 Mpaka lini waovu, Yahwe, mpaka lini waovu watafurahia?
\v 4 Wanamwaga maneno yao ya kiburi; wote watendao uovu wanajivuna.
\s5
\v 5 Wanawaangamiza watu wako, Yahwe; wanalitesa taifa ambao ni milki yako.
\v 6 Wanamuua mjane na mgeni aishiye nchini mwao, na wanamuua yatima.
\v 7 Nao husema, "Yahwe hawezi kuona, Mungu wa Yakobo hayagundui haya."
\s5
\v 8 Tambueni, ninyi watu wajinga! Enyi wapumbavu, mtajifunza lini?
\v 9 Yeye aliye liumba sikio, hasikii? Yeye aliye litengeneza jicho, haoni?
\s5
\v 10 Yeye awaadhibuye mataifa, hayuko sahihi? Yeye ndiye ampaye maarifa mwanadamu.
\v 11 Yahwe anayajua mawazo ya wanadamu, kuwa ni mvuke.
\s5
\v 12 Amebarikiwa yule ambaye umuongozaye, Yahwe, yule ambaye wewe humfundisha kutoka katika sheria yako.
\v 13 Wewe humpa pumziko wakati wa shida mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa kwa ajili ya waovu.
\s5
\v 14 Maana Yahwe hatawaacha watu wake wala kutelekeza warithi wake.
\v 15 Kwa kuwa tena hukumu itakuwa ya haki; na wote walio wanyoofu wa moyo wataifuata.
\v 16 Ni nani atainuka kunitetea dhidi ya watendao uovu? Ni nani atasimama dhidi ya waovu kwa ajili yangu?
\s5
\v 17 Kama Yahwe asingelikuwa msaada wangu, haraka ningekuwa nimelala mahali pa ukimya.
\v 18 Niliposema, mguu wangu unateleza," Uaminifu wa agano lako, Yahwe, uliniinua.
\v 19 Wasiwasi uwapo mwingi ndani yangu, faraja yako hunifurahisha.
\s5
\v 20 Kiti cha uharibifu chaweza kushirikiana nawe, kitungacho madhara kwa njia ya sheria?
\v 21 Wao kwa pamoja hupanga njama kuwaua wenye haki na kuwahukumu adhabu ya kifo wenye haki.
\s5
\v 22 Lakini Yahwe amekuwa mnara wangu mrefu, na Mungu wangu amekuwa mwamba wa kimbilio langu.
\v 23 Yeye atawarudishia uovu wao wenyewe na atawaangamiza katika uovu wao wenyewe. Yahwe Mungu wetu atawaangamiza.
\s5
\c 95
\p
\v 1 Oh njoni, tumwimbie Yahwe; na tumwimbie kwa shangwe mwamba wa wokovu wetu.
\v 2 Tuingie uweponi mwake kwa shukrani; tumwimbie yeye kwa zaburi ya sifa.
\v 3 Kwa maana Yahwe ni Mungu mkuu na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
\s5
\v 4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia; navyo vilele vya milima ni vyake.
\v 5 Bahari ni yake, maana aliiumba, na mikono yake ilitengeneza nchi kavu.
\s5
\v 6 Oh njoni, tumwabudu na tupige magoti; tupige magoti mbele za Yahwe, muumbaji wetu:
\v 7 Kwa maana yeye ni Mungu wetu, na sisi tu watu wa malisho yake na kondoo wa mkono wake. Ni heri leo mngesikia sauti yake!
\s5
\v 8 Msiifanye migumu mioyo yenu, kama vile huko Meriba, au kama ile siku ya Masa jangwani,
\v 9 ambako baba zenu walinijaribu na kunipima, japo walikuwa wameyaona matendo yangu.
\s5
\v 10 Kwa miaka arobaini nilikasirishwa na kizazi hicho na kusema, 'Hawa ni watu ambao mioyo yao imepotoka; hawazijui njia zangu.'
\v 11 Hivyo katika hasira yangu niliapa kwamba wasingeingia kamwe mahali pa pumziko."
\s5
\c 96
\p
\v 1 Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote.
\v 2 Mwimbieni Yahwe, tukuzeni jina lake; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
\s5
\v 3 Tangazeni utukufu wake kati ya mataifa, matendo yake ya ajabu kati ya mataifa.
\v 4 Maana Yahwe ni mkuu na wakusifiwa sana. Ni wakuhofiwa kuliko miungu mingine.
\s5
\v 5 Maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, bali ni Yahwe aliye zifanya mbingu.
\v 6 Heshima na adhama ziko mbele zake. Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
\s5
\v 7 Mpeni Yahwe sifa, enyi ukoo wa watu, mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu.
\v 8 Mpeni Yahwe utukufu ambao unastahili jina lake. Leteni matoleo na muingie nyuani mwake.
\s5
\v 9 Mpigieni magoti Yahwe mkiwa mmevaa mavazi ambayo yanaheshimu utakatifu wake. Nchi yote tetemekeni mbele zake.
\v 10 Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala." Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
\s5
\v 11 Mbingu na zifurahi, na nchi ishangilie; bahari na ivume na vyote viijazavyo vipige kelele kwa shangwe.
\v 12 Mashamba yashangilie na vyote vilivyomo. Kisha miti ya mstuni ipige kelele kwa furaha
\v 13 mbele za Yahwe, maana yeye anakuja. Anakuja kuihukumu nchi. Naye atauhukumu ulumwengu kwa haki na mataifa kwa uaminifu wake.
\s5
\c 97
\p
\v 1 Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi.
\v 2 Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
\s5
\v 3 Moto huenda mbele zake nao huwateketeza adui zake pande zote.
\v 4 Taa yake huangaza ulimwengu; nchi huona na kutetemeka.
\v 5 Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote.
\s5
\v 6 Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake.
\v 7 Wale wote waabuduo sanamu za kuchonga wataaibishwa, wale wanao jivuna katika sanamu zisizo na maana mpigieni yeye magoti, enyi miungu wote!
\v 8 Sayuni ilisikia na kufurahi, na miji ya Yuda ilishangilia kwa sababu ya amri zako za haki, Yahwe.
\s5
\v 9 Kwa kuwa wewe, Yahwe, ndiye uliye juu sana, juu ya nchi yote. Umetukuka sana juu ya miungu yote.
\v 10 Ninyi ambao mnampenda Yahwe, chukieni uovu! Yeye hulinda uhai wa watakatifu wake, naye huwatoa mikononi mwa waovu.
\v 11 Nuru imepandwa kwa ajili ya wenye haki na furaha kwa ajili ya wanyoofu wa moyo.
\s5
\v 12 Furahini katika Yahwe, enyi wenye haki; na mpeni shukurani mkumbukapo utakatifu wake.
\s5
\c 98
\p Zaburi.
\v 1 Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi.
\v 2 Yahwe ameufanya wokovu wake ujulikane; ameidhihirisha haki yake kwa mataifa yote.
\s5
\v 3 Hukumbuka uaminifu wa agano lake na uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia itauona ushindi wa Mungu wetu.
\v 4 Mshangilieni Yahwe, nchi yote; pazeni sauti kwa wimbo, imbeni kwa furaha, na imbeni sifa.
\s5
\v 5 Mwimbieni Yahwe sifa kwa kinubi, kwa kinubi na wimbo wenye muiki wa kupendeza.
\v 6 Kwa panda na sauti ya baragumu, fanyeni kelele za shangwe mbele ya Mfalme, Yahwe.
\s5
\v 7 Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake!
\v 8 Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha.
\v 9 Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.
\s5
\c 99
\p
\v 1 Yahwe anatawala; mataifa na yatetemeke. Ameketi juu ya makerubi; nchi inatetemeka.
\v 2 Yahwe ni mkuu katika Sayuni; naye ametukuka juu ya mataifa yote.
\v 3 Nao walisifu jina lako kuu na lenye kutisha; yeye ni mtakatifu.
\s5
\v 4 Mfalme ana nguvu, naye hupenda haki. Wewe umeimarisha haki; umetenda haki na hukumu katika Yakobo.
\v 5 Msifuni Yahwe Mungu wetu na sujuduni miguuni pake. Yeye ni mtakatifu.
\s5
\v 6 Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, na Samweli alikuwa miongoni mwa wale walio muomba Yeye. Walimuomba Yahwe, naye akawajibu.
\v 7 Alizungumza nao toka nguzo ya wingu. Walizishika amri zake takatifu na sheria ambazo aliwapatia.
\s5
\v 8 Wewe uliwajibu, Yahwe Mungu wetu. Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe, lakini uliye adhibu matendo yao ya dhambi.
\v 9 Msifuni Yahwe Mungu wetu, na mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, maana Yahwe Mungu wetu ni Mtakatifu.
\s5
\c 100
\p Zaburi ya shukrani.
\v 1 Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote.
\v 2 Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha.
\s5
\v 3 Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.
\s5
\v 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.
\v 5 Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.
\s5
\c 101
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nitaimba uaminifu wa agano lako na hukumu; kwako, Ee Yahwe, Nitakuimbia sifa.
\s5
\v 2 Nitatembea katika njia ya uadilifu. Oh, ni lini utakuja kwangu? Nitatembea kwa uadilifu ndani ya nyumba yangu.
\v 3 Sitaweka matendo maovu mbele ya macho yangu; ninachukia uovu usio na maana; hauta shikamana nami.
\s5
\v 4 Watu waliopotoka wataniacha mimi; mimi sichangamani na uovu.
\v 5 Nitamwangamiza yeyote amsengenyaye jirani yake kwa siri. Sitamvumilia yeyote mwenye kiburi.
\v 6 Nitawachagua walio waaminifu katika nchi wakae upande wangu. Wale watembeao katika njia ya uhadilifu watanitumikia.
\s5
\v 7 Watu wadanganyifu hawatabaki ndani ya nyumba yangu; waongo hawatakaribishwa mbele ya macho yangu.
\v 8 Asubuhi hata asubuhi nitawaangamiza waovu wote kutoka nchini; nitawaondoa watendao maovu wote katika mji wa Yahwe.
\s5
\c 102
\p Maombi ya aliyeteswa wakati yeye alipolemewa na kumwaga maombolezo yake mbele ya Yahwe.
\v 1 Sikia maombi yangu, Ee Yahwe; sikia kulia kwangu kwako.
\v 2 Usiufiche uso wako mbali nami wakati wa shida. Unisikilize. Nikuitapo, unijibu upesi.
\s5
\v 3 Kwa maana siku zangu zinapita kama moshi, na mifupa yangu kama moto.
\v 4 Moyo wangu umeumizwa na niko kama majani yaliyo kauka. Ninasahau kula chakula chochote.
\s5
\v 5 Kwa muendelezo wa kuugua kwangu, nimekonda sana.
\v 6 Niko kama mwali wa jangwani; nimekuwa kama bundi magofuni.
\s5
\v 7 Ninalala macho kama shomoro faraghani, pekeyake juu ya paa.
\v 8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; wale wanao nidhihaki hutumia jina langu katika laana.
\s5
\v 9 Ninakula majivu kama mkate na kuchanganya kinywaji changu kwa machozi.
\v 10 Kwa sababu ya hasira yako kali, umeniinua juu kunitupa chini.
\s5
\v 11 Siku zangu ni kama kivuli kanachofifia, na ninanyauka kama majani.
\v 12 Lakini wewe, Yahwe, unaishi milele, na kumbukumbu lako ni kwa vizazi vyote.
\s5
\v 13 Wewe utasimama na kuirehemu Sayuni. Sasa ni wakati wa mkurehemu yeye. Wakati ulio teuliwa umefika.
\v 14 Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake pendwa na kuyaonea huruma mavumbi ya magofu yake.
\v 15 Mataifa wataliheshimu jina lako, Yahwe, na wafalme wote wa nchi watauheshimu utukufu wako.
\v 16 Yahwe ataijenga tena Sayuni na ataonekana katika utukufu wake.
\s5
\v 17 Wakati huo, atajibu maombi ya fukara; hatayakataa maombi yao.
\v 18 Hii itaandikwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na watu ambao bado hawajazaliwa watamsifu Yahwe.
\s5
\v 19 Maana ametazama chini toka mahali pa juu patakatifu;
\v 20 Toka mbinguni Yahwe ameiangalia nchi, ili kusikia kuugua kwa wafungwa, kuwafungua waliohukumiwa kufa.
\s5
\v 21 Kisha watu watalitangaza jina la Yahwe katika Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu
\v 22 pindi mataifa na falme watakapokusanyika pamoja kumtumikia Yahwe.
\s5
\v 23 Amechukua nguvu zangu katikati ya siku zangu za kuishi, amezifupisha siku zangu.
\v 24 Nilisema, "Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; wewe uko hapa hata kizazi chote.
\s5
\v 25 Tangu zama za kale wewe uliiweka nchi mahali pake; mbingu ni kazi ya mikono yako.
\v 26 Mbingu na nchi zitaangamia lakini wewe utabaki; zitachakaa kama mavazi; utaziondoa kama watu waondoavyo mavazi yaliyo chakaa, nazo hazitaonekana tena.
\v 27 Lakini wewe ni yuleyule, na miaka yako haitakuwa na mwisho.
\s5
\v 28 Watoto wa watumishi wako wataendelea kuishi, na uzao wao utaishi katika uwepo wako.
\s5
\c 103
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, na vyote vilivyomo ndani yangu, nitalisifu jina lake takatifu.
\v 2 Maishani mwangu mwote nitamsifu Yahwe, na kukumbuka matendo yake yote mazuri.
\s5
\v 3 Yeye husamehe dhambi zako zote; huponya magonjwa yako yote.
\v 4 Huukomboa uhai wako dhidi ya uharubifu; hukuvika taji kwa uaminifu wa agano lake na hutenda kwa rehema.
\v 5 Huyatosheleza maisha yako kwa mambo mema ili kwamba ujana wako ufanywe upya kama tai.
\s5
\v 6 Yahwe hutenda yaliyo haki naye hutenda hukumu ya haki kwa ajili ya wote walio onewa.
\v 7 Alimjulisha Musa njia zake, matendo yake kwa uzao wa Israeli.
\v 8 Yahwe ni wa huruma na neema; ni mvumilivu; ana agano kuu la uaminifu.
\s5
\v 9 Hataadhibu siku zote; hakasiriki siku zote.
\v 10 Hatushughulikii sisi kama dhambi zetu zinavyostahili au kutulipa kulingana na uhitaji wa dhambi zetu.
\s5
\v 11 Kama mbingu zilivyo juu zaidi ya nchi, ndivyo ulivyo ukuu wa uaminifu wa agano lake kwao wale wanaomcha yeye.
\v 12 Kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi, hivi ndivyo ameondoa hatia zetu za dhambi zetu mbali nasi.
\v 13 Kama vile baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Yahwe alivyo na huruma kwao wamchao.
\s5
\v 14 Maana anajua tulivyo umbwa; anajua kuwa tu mavumbi.
\v 15 Kama ilivyo kwa mwanadamu, siku zake ni kama majani; hustawi kama ua katika shamba.
\v 16 Upepo hulipiga, nalo hutoweka, na hakuna hata mmoja awezaye kuelezea mahali lilipokua.
\s5
\v 17 Lakini agano la uaminifu wa Yahwe uko kwa wale wamchao yeye milele hata milele. Haki yake ni endelevu kwa uzao wao.
\v 18 Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maagizo yake.
\v 19 Yahwe ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake watawala juu ya kila mtu.
\s5
\v 20 Msifuni Yahwe, enyi malaika zake, ninyi hodari wenye nguvu na mtendao neno lake, na kutii sauti ya neno lake.
\v 21 Msifuni Yahwe, enyi jeshi la malaika wote, ninyi ni watumishi mfanyao mapenzi yake.
\v 22 Msifuni Yahwe, viumbe wake wote, mahali popote atawalapo. Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote.
\s5
\c 104
\p
\v 1 Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, Ewe Yahwe Mungu wangu, wewe ni mkubwa sana; umevikwa kwa utukufu na enzi.
\v 2 Unajifunika mwenyewe kwa nuru kama kwa mavazi; umetandaza mbingu kama pazia za hema.
\v 3 Umeweka mawinguni mihimili ya vyumba vyako; huyafanya mawingu gari lako; hutembea juu ya mbawa za upepo.
\s5
\v 4 Yeye huufanya upepo kuwa wajumbe wake, miale ya moto kuwa watumishi wake.
\v 5 Aliiweka misingi ya nchi, nayo haitahamishwa kamwe.
\s5
\v 6 Wewe uliifunika nchi kwa maji kama kwa mavazi; maji yalifunika milima.
\v 7 Kukemea kwako kulifanya maji kupungua; kwa sauti ya radi yako yakaondoka kasi.
\s5
\v 8 Milima iliinuka, na mabonde yakaenea mahali ambapo wewe ulikwisha pachagua kwa ajili yao.
\v 9 Umeweka mipaka kwa ajili yao ambao hayawezi kuupita; hayawezi kuifunika nchi tena.
\s5
\v 10 Yeye alifanya chemchemi kutiririsha maji mabondeni; mito kutiririka katikati ya milima.
\v 11 Inasambaza maji kwa ajili ya wanyama wote wa shambani; punda wa porini hukata kiu yao.
\v 12 Kandokando ya mito ndege hujenga viota vyao; huimba kati ya matawi.
\s5
\v 13 Humwagilia milima kutoka katika chumba chake cha maji mawinguni. Nchi imejazwa kwa matunda ya kazi yake.
\v 14 Huzifanya nyasi kukua kwa ajili ya mifugo na mimea kwa ajili ya binadamu kulima ili kwamba mwanadamu aweze kuzalisha chakula toka nchini.
\v 15 Hutengeneza mvinyo kumfurahisha mwanadamu, mafuta yakumfanya uso wake ung'ae, na chakula kwa ajili ya kuimarisha uhai wake.
\s5
\v 16 Miti ya Yahwe hupata mvua nyingi; Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
\v 17 Hapo ndege hutengeneza viota vyao. Na korongo, misunobari ni nyuma yake.
\v 18 Mbuzi mwitu huishi kwenye milima mrefu; na urefu wa milima ni kimilio la wibari.
\s5
\v 19 Aliuchagua mwezi kuweka alama ya majira; jua latambua kuchwa kwake.
\v 20 Wewe hufanya giza la usiku ambapo wanyama wote wa msituni hutoka nje.
\s5
\v 21 Wana simba huunguruma kwa ajili ya mawindo na hutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.
\v 22 Jua linapochomoza, huenda zao na kujilaza mapangoni mwao.
\s5
\v 23 Wakati huo huo, watu hutoka nje kuelekea kazi zao na utumishi wake mpaka jioni.
\v 24 Yahwe, ni jinsi gani kazi zako zilivyo nyingi na za aina mbalimbali! Kwa hekima ulizifanya zote; nchi inafurika kwa kazi zako.
\s5
\v 25 Kule kuna bahari, yenye kina kirefu na pana, ikiwa na viume vingi visivyo hesabika, vyote vidogo na vikubwa.
\v 26 Meli husafili humo, na ndimo alimo Lewiathani uliye muumba acheze baharini.
\s5
\v 27 Hawa wote hukutazama wewe uwape chakula kwa wakati.
\v 28 Unapowapa chakula, hukusanyika; ufunguapo mkono wako, wanatosheka.
\s5
\v 29 Unapouficha uso wako, wanateseka; ukiiondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.
\v 30 Unapotuma Roho yako, wanaumbwa, nawe unaifanya upya nchi.
\s5
\v 31 Utukufu wa Yahwe na udumu milele; Yahwe na aufurahie uumbaji wake.
\v 32 Yeye hutazama nchi, nayo hutikisika; huigusa milima, nayo hutoa moshi.
\s5
\v 33 Nitamwimbia Yahwe maisha yangu yote; nitamwimbia sifa Mungu wangu nigali ninaishi.
\v 34 Mawazo yangu na yawe matamu kwake; nitafurahia katika Yahwe.
\s5
\v 35 Wenye dhambi na waondoshwe katika nchi, na waovu wasiwepo tena. Ninamsifu Yahwe maisha yangu yote. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 105
\p
\v 1 Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa.
\v 2 Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau.
\v 3 Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi.
\s5
\v 4 Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote.
\v 5 Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda,
\v 6 miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake.
\s5
\v 7 Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote.
\v 8 Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu.
\s5
\v 9 Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka.
\v 10 Hiki ndicho alicho mthibitishia Yakobo kama agano na kama agano la milele kwa Israeli.
\v 11 Alisema, "Nitakupa wewe ardhi ya Kanaani kama sehemu yako ya urithi."
\s5
\v 12 Alisema hili wakati tu walipokuwa wachache katika hesabu, yaani wachahe sana, nao walikuwa wageni katika nchi.
\v 13 Walienda taifa hadi taifa na kutoka ufalme moja kwenda mwingine.
\s5
\v 14 Hakuruhusu yeyote kuwaonea; aliwakemea wafalme kwa ajili yao.
\v 15 Alisema, "Msiwaguze wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu."
\s5
\v 16 Aliita njaa katika nchi; akaondoa upatikanaji wa mkate wote.
\v 17 Akatuma mtu mbele yao; Yusufu aliuzwa kama mtumishi.
\s5
\v 18 Miguu yake ilifungwa kwa pingu; alivishwa mnyororo wa chuma shingoni mwake,
\v 19 mpaka wakati wa maneno yake ulipotimia, nalo neno la Yahwe lilimjaribu.
\s5
\v 20 Mfalme alituma watumishi kumfungua; mtawala wa watu alimuweka huru.
\v 21 Alimuweka kuwa msimamizi wa nyumba yake kama mtawala wa mali zake zote
\v 22 kuwaelekeza wakuu kama alivyopenda na kuwafundisha viongozi wake hekima.
\v 23 Kisha Israeli iliingia Misri, na Yakobo aliishi kwa muda katika nchi ya Hamu.
\s5
\v 24 Yahwe aliwajalia watu wake wazae sana, na aliwafanya wenye nguvu kuliko adui zao.
\v 25 Alisababisha adui zao wawachukie watu wake, na kuwatendea visivyo watumishi wake.
\v 26 Alimtuma Musa, mtumishi wake, na Haruni, ambaye alikwisha mchagua.
\v 27 Walifanya ishara zake kati ya Wamisri na maajabu yake katika ya nchi ya Hamu.
\s5
\v 28 Alituma giza na likaifanya nchi hiyo kuwa giza, lakini watu wake hawakutii amri zake.
\v 29 Aligeuza maji kuwa damu na aliua samaki wao.
\v 30 Nchi yao ilijaa vyura, hata katika vyumba vya watawala wao.
\s5
\v 31 Alisema, na makundi ya inzi na chawa wakaja mjini mwote.
\v 32 Aliigeuza mvua yao kuwa mvua ya mawe, pamoja na miali ya moto juu ya ardhi yao.
\v 33 Aliiharibu mizabibu yao na mitini yao; akaivunja miti ya mji wao.
\s5
\v 34 Alisema, na nzige wakaja, nzige wengi sana.
\v 35 Nzige walikula mboga zao zote za majani katika nchi yao. Walikula mazao yote ardhini.
\v 36 Aliua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi yao, malimbuko ya nguvu zao.
\s5
\v 37 Aliwatoa nje Waisraeli wakiwa na fedha na dhahabu; hakuna mmoja wa kabila lake aliyejikwaa njiani.
\v 38 Misri ilifurahi walipoondoka, maana Wamisri waliwaogopa.
\v 39 Alitandaza wingu liwafunike na alifanya moto uwaangazie wakati wa usiku.
\s5
\v 40 Waisraeli waliomba chakula, naye aliwaletea kware na aliwatosheleza kwa mkate kutoka mbiguni.
\v 41 Aliugawa mwamba, maji yalimwagika kutoka humo; yalitiririka katika jangwa kama mto.
\v 42 Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu aliyoifanya kwa Ibrahimu mtumishi wake.
\s5
\v 43 Aliwaongoza watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za ushindi.
\v 44 Aliwapa nchi za mataifa; walichukua milki ya mali za watu
\v 45 ili waweze kushika amri zake na kutii sheria zake. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 106
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 2 Ni nani awezaye kuyahesabu mataendo makuu ya yahwe au kutangaza katika ukamilifu sifa zote za matendo yake ya kuaminika.
\s5
\v 3 Wamebarikiwa wale watendao yaliyo mema na matendo yao yaliyo haki siku zote.
\v 4 Ukumbuke, Ee Yahwe, unapowaonesha watu wako neema; unisaidie unapowaokoa.
\v 5 Ndipo nitaona mafanikio ya wateule wako, wakifurahia katika furaha ya taifa lako, na utukufu pamoja na urithi wako.
\s5
\v 6 Tumefanya dhambi kama babu zetu, tumekosea, na kufanya uovu.
\v 7 Baba zetu hawakuyatambua matendo yako ya ajabu katika Misri; walipuuzia matendo yako mengi ya uaminifu wa agano; waliasi penye bahari, bahari ya Shamu.
\s5
\v 8 Hata hivyo, yeye aliwaokoa kwa ajili ya jina lake ili kwamba aweze kuzifunua nguvu zake.
\v 9 Aliikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka. Kisha akawaongoza vilindini, kana kwamba ni jangwani.
\s5
\v 10 Aliwaokoa kutoka mkononi mwa wale waliowachukia, na aliwaokoa kutoka mkononi mwa adui.
\v 11 Lakini maji yaliwafunika washindani wao; hakuna hata mmoja aliye okolewa.
\v 12 Ndipo waliyaamini maneno yake, nao waliimba sifa zake.
\s5
\v 13 Lakini walisahau haraka kile alichofanya; hawakuyasubiri maelekezo yake.
\v 14 Walikuwa na tamaa isiyotoshelezwa jangwani, wakamjaribu Mungu nyikani.
\v 15 Aliwapa ombi lao, lakini alituma gonjwa ambalo lilishambulia miili yao.
\s5
\v 16 Katika kambi wakawa na wivu juu Musa na Haruni, kuhani mtakatifu wa Yahwe.
\v 17 Nchi ilifunguka na ilimmeza Dathani na iliwafunika wafuasi wa Abiramu.
\v 18 Moto uliwaka kati yao; moto uliwaangamiza waovu.
\s5
\v 19 Walitengeneza ndama huko Horebu na kuabudu sanamu ya kuyeyuka.
\v 20 Wakaubadili utukufu wa Mungu kuwa mfano wa ng'ombe alaye majani.
\v 21 Walimsahau Mungu wokozi wao, aliyefanya mambo makuu katika Misri.
\s5
\v 22 Alifanya matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu na matendo makuu penye Bahari ya Shamu.
\v 23 Mungu angetangaza uharibifu wao, kama sio Musa, mteule wake, aliingilia kati kugeuza hasira yake dhidi ya kuwaangamiza.
\s5
\v 24 Kisha waliidharau nchi yenye matunda; hawakuiamini ahadi yake,
\v 25 bali walilalamiaka katika mahema yao, na hawakumtii Yahwe.
\s5
\v 26 Kwa hiyo aliinua mkono wake na kuapa kwao kuwa atawaacha wafe jangwani,
\v 27 akitawanya uzao wao kati ya mataifa, na kuwatawanya katika nchi za kigeni.
\s5
\v 28 Waliabudu Baal ya Poeri na walizila dhabihu zilizotolewa kwa wafu.
\v 29 Walimkasirisha kwa matendo yao, na pigo la gonjwa baya liliwashambulia kati yao.
\s5
\v 30 Ndipo Finehasi aliinuka kuingilia kati, na pigo likakoma.
\v 31 Ilihesabika kwake kama tendo la haki kwa vizazi vyote hata milele.
\s5
\v 32 Pia walimkasirisha Yahwe penye maji ya Meriba, na Musa aliteseka kwa ajili yao.
\v 33 Walimghadhabisha Musa naye akaongea haraka.
\v 34 Hawakuyaharibu mataifa kama Yahwe alivyowaamuru,
\v 35 bali walichangamana na mataifa na walijifunza njia zao
\v 36 nao waliabudu sanamu, nazo zikawa mtego kwao.
\s5
\v 37 Waliwatoa wana wao na binti zao kwa mapepo.
\v 38 Walimwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana na binti zao, ambao waliwatoa kama dhabihu kwa sanamu za Kanaani, waliinajisi nchi kwa damu.
\v 39 Walinajisiwa kwa matendo yao; katika matendo yao walikuwa kama malaya.
\s5
\v 40 Hivyo Yahwe aliwakasilikia watu wake, akawadharau watu wake mwenyewe.
\v 41 Akawaruhusu mataifa, na wale walio wachukia wakawatawala.
\s5
\v 42 Maadui zao wakawaonea, wakatiishwa chini ya mamlaka yao.
\v 43 Mara nyingi alienda kuwasaidia, lakini waliendelea kuasi nao walishushwa chini kwa dhambi zao wenyewe.
\s5
\v 44 Hata hivyo, aliiangalia dhiki yao aliposikia kilio chao kwa ajili ya msaada.
\v 45 Alikumbuka agano lake pamoja nao na alijirudi kwa sababu ya upendo wake thabiti.
\v 46 Aliwafanya wote waliowateka wawahurumie.
\s5
\v 47 Utuokoe, Ee Yahwe, Mungu wetu. Utukusanye kutoka kati ya mataifa ili kwamba tuweze kulishukuru jina lako takatifu na utukufu katika sifa zako. Yahwe,
\v 48 Mungu wa Israeli, na asifiwe toka milele na milele. watu wote walisema, "Amen." Msifuni Yahwe. Kitabu cha tano.
\s5
\c 107
\p
\v 1 Mshukuruni Yahwe, maana ni mwema, na uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 2 Waseme hivi waliokombolewa na Yahwe, wale aliowaokoa toka mkononi mwa adui.
\v 3 Yeye amewakusanya kutoka nchi za kigeni, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.
\s5
\v 4 Walitanga-tanga janwani katika njia ya nyika hawakuona mji wa kuishi.
\v 5 Kwa sababu walikuwa na njaa na kiu, walikata tamaa kutokana na uchovu.
\v 6 Kisha walimuita Yahwe katika shida yao, naye aliwaokoa toka katika dhiki yao.
\v 7 Aliwaongoza kupitia njia ya moja kwa moja waweze kwenda mjini kuishi humo.
\s5
\v 8 Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliowatendea wanadamu!
\v 9 Maana hutosheleza shauku za walio na kiu, na hamu ya wale wenye njaa yeye huwashibisha kwa mambo mema.
\v 10 Baadhi walikaa katika giza na uvuli wa mauti, walifungwa katika mateso na minyororo.
\s5
\v 11 Hii ni kwa sababu walikuwa wameliasi neno la Mungu na walikataa maelekezo ya Aliye Juu.
\v 12 Aliinyenyekesha mioyo yao kupitia magumu; walipata mashaka na hakukuwa na mmoja wa kuwasaidia.
\v 13 Kisha wakamwita Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
\s5
\v 14 Aliwatoa gizani na kwenye uvuli wa mauti na kuvunja vifungo vyao.
\v 15 Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyoyatenda kwa wanadamu!
\v 16 Kwa maana amevunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma.
\s5
\v 17 Walikuwa wapumbavu katika njia zao za uasi na kuteswa kwa sababu ya dhambi zao.
\v 18 Walipoteza hamu yao ya kula chakula chochote, na waliyakaribia malango ya kifo.
\v 19 Kisha walimlilia Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
\s5
\v 20 Alituma neno lake na likawaponya, na akawaokoa kutoka katika uharibifu wao.
\v 21 Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyoyatenda kwa wanadamu!
\v 22 Na watoe dhabihu ya shukrani na kutangaza matendo yake kwa kuimba.
\s5
\v 23 Baadhi husafiri baharini katika meli na kufanya biashara juu ya bahari.
\v 24 Hawa huona matendo ya Yahwe na maajabu yake baharini.
\s5
\v 25 Kwa maana aliamuru na alivumisha upepo wa dhoruba ambao uliyainua juu mawimbi ya baharini.
\v 26 Walipanda juu mawinguni na kushuka vilindini. Nafsi zao ziliyeyuka katika dhiki.
\v 27 Waliyumba-yumba na kupepesuka kama walevi na hawakujua la kufanya.
\s5
\v 28 Kisha walimlilia Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
\v 29 Aliituliza dhoruba, na mawimbi yakatulia.
\v 30 Ndipo walifurahia kwa sababu bahari ilikuwa shwali, na aliwaleta kwenye bandari waliyoitamani.
\s5
\v 31 Oh, ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyowatendea wanadamu!
\v 32 Wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu na wamsifu yeye katika baraza la viongozi.
\s5
\v 33 Aligeuza mito ikwa jangwa, chemchem ya maji ikawa nchi kame,
\v 34 na nchi ya matunda mengi ikawa nchi isiyozaa kwa sababu ya uovu wa watu wake.
\v 35 Aligeuza jangwa likawa ziwa la maji na nchi kame ikawa chemchem ya maji.
\s5
\v 36 Aliwakalisha huko wenye njaa, nao walijenga mji na kuishi humo.
\v 37 Walijenga mji ili kupanda mimea shambani, kupanda mizabibu, na kuleta humo mazao tele.
\v 38 Yeye huwabariki wameongezeka sana katika hesabu. Haachi mifugo yao ipungue katika hesabu.
\s5
\v 39 Kisha wakapungua na kudhilika kwa dhiki na mateso.
\v 40 Akawamwagia viongozi dharau na akawafanya wazunguke katika jangwa, mahali pasipo na njia.
\s5
\v 41 Lakini aliwalinda wahitaji dhidi ya mateso na kujali kwa ajili ya familia yake kama kundi la kondoo.
\v 42 Wenye haki wataona hili na kufurahi, na uovu wote utaona na kufunga kinya chake.
\v 43 Yeyote mwenye hekima anapaswa kuyaangalia haya na kutafakari juu ya matendo ya uaminifu wa agano la Yahwe.
\s5
\c 108
\p Wimbo, Zaburi ya Daudi.
\v 1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti; nitaimba, naam, nitaimba sifa pia kwa moyo mkuu.
\v 2 Amka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
\s5
\v 3 Nitakushukuru wewe, Yahwe, kati ya watu; nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
\v 4 Kwa maana uaminifu wa agano lako ni mkuu juu ya mbingu; na uaminifu wako wafika mawinguni.
\s5
\v 5 Ee Mungu, uinuliwe, juu ya mbingu, na utukufu wako utukuke juu ya nchi.
\v 6 Ili kwamba wale uwapendao waokolewe, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu.
\s5
\v 7 Mungu ameongea katika utakatifu wake; "Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na nitalipima bonde la Sukothi.
\v 8 Gileadi ni yangu, na manase ni yangu; Ephraimu ni nguvu ya kichwa changu; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
\s5
\v 9 Moabu ni bakuli langu la kunawia; nitatupa kiatu changu juu ya Edomu; nitapaza sauti katika ushindi kwa ajili ya Filisti.
\v 10 Ni nani atakaye nipeleka kwenye mji imara? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?"
\s5
\v 11 Ee Mungu, sio wewe uliyetukataa? Hauendi vitani na jeshi letu.
\v 12 Utupe msaada dhidi ya adui yetu, maana msaada wa wanadamu ni bure.
\v 13 Tutashinda kwa msaada wa Mungu; atawakanyaga kwa adui zetu.
\s5
\c 109
\p Kwa kiongozi wa muziki.
\v 1 Zaburi ya Daudi. Mungu ninaye msifu, usinyamaze kimya.
\v 2 Kwa maana waovu na wadanganyifu wananishambulia; wanazungumza uongo dhidi yangu.
\v 3 Wananizunguka na kusema mambo ya chuki, na wananishambulia bila sababu.
\s5
\v 4 Wananilipa kashfa badala ya upendo, lakini mimi ninawaombea.
\v 5 Wananilipa uovu badala ya mema, na wanachukia upendo wangu.
\s5
\v 6 Teua mtu mwovu aliye adui zaidi kama watu hawa; teua mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
\v 7 Na atakapohukumiwa, aonekane na hatia; maombi yake yachukuliwe kuwa ni dhambi.
\s5
\v 8 Siku zake na ziwe chahe; mamlaka yake na yachukuliwe na mtu mwingine.
\v 9 Watoto wake wawe yatima, na mke wake awe mjane.
\v 10 Watoto wake wenye kutanga tanga na kuombaomba, wakiondoka katika nyumba zao zilizo haribika na kuomba chakula au pesa kwa wapita njia.
\s5
\v 11 Mdai na achukue vitu vyake vyote amilikivyo; wageni wateke mapato ya kazi yake.
\v 12 Asiwepo mtu yeyote wa kumfanyia wema; mtu yeyote asiwahurumie yatima wake.
\v 13 Watoto wake waangamizwe; majina yao na yafutwe katika kizazi kijacho.
\s5
\v 14 Uovu wa baba zake utajwe kwa Yahwe; na dhambi ya mama yake isisahaulike.
\v 15 Hatia zao na ziwe mbele ya Yahwe siku zote; Yahwe na aiondoe kumbukumbu yao duniani.
\v 16 Yahwe na afanye hivi kwa sababu mtu huyu kamwe hakusumbuka kuonesha uaminifu wa agano wowote, lakini badala yake aliwasumbua wanyonge, wahitaji, na kuwaua walio vunjika moyo.
\s5
\v 17 Alipenda kulaani; na imrudie juu yake. Alichukia kubariki; baraka zozote na zisije kwake.
\v 18 Alijivika kulaani kana kwamba ni vazi lake, na laana yake iliingia ndani yake kama maji, na kama mafuta mifupani mwake.
\s5
\v 19 Laana zake na ziwe kwake kama vazi avaalo kujifunika mwenyewe, na kama mkanda avaao kila siku.
\v 20 Na haya yawe malipo ya mshitaki wangu kutoka kwa Yahwe, ya wale wasemao mambo maovu juu yangu.
\s5
\v 21 Yahwe Bwana wangu, unishughulikie kwa wema kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni mwema, uniokoe.
\v 22 Kwa maana ni mnyonge na muhitaji, na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
\v 23 Ninatoweka kama kivuli cha jioni; ninapeperushwa kama nzige.
\s5
\v 24 Magoti yangu ni dhaifu kutokana na kufunga; ninakuwa mwembamba na mifupa.
\v 25 Nimedharauliwa na washitaki wangu; wanionapo; hutikisa vichwa vyao.
\s5
\v 26 Nisaidie, Yahwe Mungu wangu; uniokoe kwa uaminifu wa agano lako.
\v 27 Nao wajue kuwa wewe umefanya haya, kwamba wewe, Yahwe, umetenda haya.
\s5
\v 28 Ingawa wananilaani, tafadhali unibariki; wanishambuliapo, waaibishwe, lakini mtumishi wako afurahi.
\v 29 Washitaki wangu na wavishwe kwa aibu; wavae aibu yao kama vazi.
\s5
\v 30 Kwa kinywa changu ninatoa shukrani kuu kwa Yahwe; nitamsifu yeye katikati ya kusanyiko.
\v 31 Maana nitasimama mkono wa kuume wa mhitaji, ili nimuokoe dhidi ya wale wanao muhukumu.
\s5
\c 110
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahwe humwambia bwana wangu, "Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako."
\s5
\v 2 Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako.
\v 3 Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande.
\s5
\v 4 Yahwe ameapa, na hatabadilika: "Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki."
\s5
\v 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme.
\v 6 Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi.
\s5
\v 7 Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu.
\s5
\c 111
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano.
\v 2 Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio.
\v 3 Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele.
\s5
\v 4 Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema.
\v 5 Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake.
\v 6 Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa.
\s5
\v 7 Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika.
\v 8 Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri.
\v 9 Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha.
\s5
\v 10 Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.
\s5
\c 112
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake.
\v 2 Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa.
\s5
\v 3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali; na haki yake itadumu milele.
\v 4 Nuru huangazia gizani kwa ajili ya mtu mcha Mungu; yeye ni wa fadhili, huruma, na haki.
\v 5 Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu.
\s5
\v 6 Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele.
\v 7 Haogopi habari mbaya; ni jasiri, akimtumainia Yahwe.
\s5
\v 8 Moyo wake ni mtulivu, hana woga, mpaka aonapo ushindi dhidi ya watesi wake.
\v 9 Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima.
\s5
\v 10 Mtu mwovu ataona haya na kukasirika; atasaga meno yake na kuyeyuka; tamaa ya wasio haki itapotea.
\s5
\c 113
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe.
\v 2 Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele.
\s5
\v 3 Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe.
\v 4 Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni.
\s5
\v 5 Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu,
\v 6 atazamaye chini angani na duniani?
\s5
\v 7 Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani,
\v 8 ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
\s5
\v 9 Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!
\s5
\c 114
\p
\v 1 Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni,
\v 2 Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli.
\s5
\v 3 Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma.
\v 4 Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo.
\s5
\v 5 Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma?
\v 6 Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo?
\v 7 Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo.
\s5
\v 8 Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.
\s5
\c 115
\p
\v 1 Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu, bali kwa jina lako ulete heshima, kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na uaminifu wako.
\v 2 Kwa nini mataifa yalazimike kusema, "Yuko wapi Mungu wako?"
\s5
\v 3 Mungu wetu aliye mbinguni; hufanya chochote apendacho.
\v 4 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
\s5
\v 5 Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
\v 6 zina masikio, lakini hazisikii; zina pua lakini hazinusi.
\s5
\v 7 Sanamu hizo zina mikono, lakini hazishiki; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala haziongei kutoka viywani mwao.
\v 8 Wale wanao zitengeneza wanafanana nazo, vile vile yeyote anaye amini katika hizo.
\s5
\v 9 Israeli, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
\v 10 Nyumba ya Haruni, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
\v 11 Ninyi mnao mheshumu Yahwe, mwamini yeye; yeye ni msaada wenu na ngao yenu.
\s5
\v 12 Yahwe hutukumbuka sisi na atatubariki; ataibariki familia ya Israeli; atabariki familia ya Haruni.
\v 13 Atawabariki wale wanao muheshimu yeye, wote vijana na wazee.
\v 14 Yahwe na awaongeze ninyi zaidi na zaidi, ninyi pamoja na watoto wenu.
\s5
\v 15 Yahwe na awabariki, aliyeziumba mbingu na nchi.
\v 16 Mbingu ni za Yahwe; lakini nchi amewapa wanadamu.
\s5
\v 17 Wafu hawamsifu Yahwe, wala wote washukao chini kwenye ukimya;
\v 18 bali tutamtukuza Yahwe sasa na hata milele. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 116
\p
\v 1 Nampenda Yahwe kwa kuwa anasikia sauti yangu na kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
\v 2 Kwa sababu alinisikiliza, nitamuita yeye ningali ninaishi.
\s5
\v 3 Kamba za mauti zilinizunguka, na mitego ya kuzimu ilinikabili; niliona dhiki na huzuni.
\v 4 Kisha niliita kwa jina la Yahwe: "Tafadhali Yahwe, uiokoe nafsi yangu."
\s5
\v 5 Yahwe ni mwenye neema na haki; Mungu wetu ni mwenye huruma.
\v 6 Yahwe huwalinda wasio na hila; nilishushwa chini akaniokoa.
\s5
\v 7 Nafsi yangu inaweza kurudi mahali pake pa kupumzika, kwa kuwa Yahwe amekuwa mwema kwangu.
\v 8 Kwa maana uliokoa uhai wangu dhidi ya kifo, mcho yangu dhidi ya machozi, na miguu yangu dhidi ya kujikwaa.
\s5
\v 9 Nitamtumikia Yahwe katika nchi ya walio hai.
\v 10 Nilimwamini yeye, hata niliposema, "nimeteswa sana."
\v 11 Kwa haraka nilisema, "Watu wote ni waongo."
\s5
\v 12 Nimlipeje Yahwe kwa wema wake wote kwangu?
\v 13 Nitakiinua kikombe cha wokovu, na kuliitia jina la Yahwe.
\v 14 Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote.
\v 15 Mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pa Mungu.
\s5
\v 16 Ee Yahwe, hakika, mimi ni mtumishi wako; mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umefungua vifungo vyangu.
\v 17 Nitakutolea dhabihu ya shukrani na nitaliitia jina la Yahwe.
\s5
\v 18 Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote,
\v 19 katika nyua za nyumba ya Yahwe, katikati yako, Yerusalemu. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 117
\p
\v 1 Msifuni Yahwe, enyi mataifa yote; enyi watu mhimidini yeye.
\v 2 Kwa kuwa uaminifu wa agano lake ni mkuu kwetu, na uaminifu wa Yahwe wadumu milele. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 118
\p
\v 1 Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 2 Israeli na aseme, "Uaminifu wa agano lake wadumu milele."
\s5
\v 3 Nyumba ya Haruni na iseme, "Uaminifu wa agano lake wadumu milele."
\v 4 Wafuasi waaminifu wa Yahwe na waseme, "Uaminifu wa agano lake wadumu milele."
\s5
\v 5 Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe; Yahwe alinijibu na kuniweka huru.
\v 6 Yahwe yuko pamoja nami; sitaogopa; mwanadamu atanifanya nini? Yahwe yuko upande wangu kama msaidizi;
\v 7 nitawatazama kwa ushindi wale walio nichukia.
\s5
\v 8 Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu.
\v 9 Ni bora kukimbilia katika Yahwe kuliko kuamini katika wakuu.
\s5
\v 10 Mataifa yote walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
\v 11 Walinizunguka; naam, walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
\v 12 Walinizunguka kama nyuki; walitoweka haraka kama moto kati ya miiba; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
\s5
\v 13 Walinishambulia ili waniangushe, lakini Yahwe alinisaidia.
\v 14 Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu, na ndiye anaye niokoa.
\s5
\v 15 Kelele za ushindi zimesikika katika maskani ya wenye haki; mkono wa kuume wa Mungu umeshinda.
\v 16 Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda.
\s5
\v 17 Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe.
\v 18 Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife.
\s5
\v 19 Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe.
\v 20 Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo.
\v 21 Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu.
\s5
\v 22 Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi.
\v 23 Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu.
\s5
\v 24 Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.
\v 25 Tafadhali, Yahwe, utupe ushindi! Tafadhali, Yahwe, utupe mafanikio!
\s5
\v 26 Amebarikiwa yule ajaye katika jina la Yahwe; tunakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe.
\v 27 Yahwe ni Mungu, na ametupa sisi nuru; ifungeni dhabihu kwa kamba pembeni mwa madhabahu.
\v 28 Wewe ni Mungu wangu, nami nitakushukuru; wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe.
\s5
\v 29 Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema; kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\c 119
\p ALEPH.
\v 1 Wamebarikiwa wale ambao njia zao hazina lawama, waenendao katika sheria ya Yahwe.
\v 2 Wamebarikiwa wale wazishikao amri zake thabiti, wamtafutao kwa moyo wao wote.
\s5
\v 3 Hawatendi makosa; wanaenenda katika njia zake.
\v 4 Wewe umetuamuru kuyashika maagizo yako ili tuyachunguze kwa umakini.
\s5
\v 5 Oh, ningependa njia zangu ziwe thabiti nizitii amri zako!
\v 6 Ndipo sitaaibika nizifikiripo amri zako zote.
\s5
\v 7 Nitakushukuru wewe kwa unyofu wangu wa moyo nijifunzapo amri za haki yako.
\v 8 Nitazitii amri zako; usiniache peke yangu. BETH.
\s5
\v 9 Ni jinsi gani kijana aweza kuendelea kuishi katika njia yake ya utakatifu? Ni kwa kulitii neno lako.
\v 10 Kwa moyo wangu wote ninakutafuta wewe; Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
\s5
\v 11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisije nikakutenda dhambi.
\v 12 Umetukuka, Yahwe; unifundishe amri zako.
\s5
\v 13 Kwa kinywa changu nimetangaza amri ya haki yako yote ambayo umeifunua.
\v 14 Ninafurahi katika njia ya amri za agano lako zaidi kuliko katika utajiri.
\s5
\v 15 Nitayatafakari maagizo yako na kuzitilia maanani njia zako.
\v 16 Ninafurahia katika amri zako; sitalisahau neno lako. GIMEL.
\s5
\v 17 Uwe mwema kwa mtumishi wako ili niweze kuishi na kulishika neno lako.
\v 18 Ufungue macho yangu ili niweze kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
\s5
\v 19 Mimi ni mgeni katika nchi; usizifiche amri zako mbali nami.
\v 20 Moyo wangu unauma kwa kutamani sana kuzijua amri zako za haki wakati wote.
\s5
\v 21 Wewe huwakemea wenye kiburi, waliolaaniwa, wanao tanga-tanga mbali na amri zako.
\v 22 Uniokoe dhidi ya aibu na udhalilishaji, maana nimezitii amri za agano lako.
\s5
\v 23 Ingawa watawala wanapanga njama na kunikashfu, mtumishi wako huzitafakali amri zako.
\v 24 Amri za agano lako ni furaha yangu, na washauri wangu. DALETH.
\s5
\v 25 Uhai wangu unashikamana na mavumbi! nipe uhai kwa neno lako.
\v 26 Nilikuambia mapito yangu, na ulinijibu; nifundishe sheria zako.
\s5
\v 27 Unifahamishe njia ya maagizo yako, ili niweze kutafakari juu ya mafundisho yako ya ajabu.
\v 28 Nimelemewa na huzuni! Nitie nguvu kwa neno lako.
\s5
\v 29 Uiondoe kwangu njia ya udanganyifu; kwa wema wako unifundishe sheria yako.
\v 30 Nimechagua njia ya uaminifu; siku zote nimeweka amri za haki yako mbele yangu.
\s5
\v 31 Ninashikamana na amri za agano lako; Yahwe, usiniache niaibike.
\v 32 Nitakimbia katika njia ya amri zako, kwa sababu wausukuma moyo wangu kufanya hivyo. HE
\s5
\v 33 Unifundishe, Yahwe, njia za sheria yako, nami nitazishika hadi mwisho.
\v 34 Unipe uelewa, nami nitazishika sheria zako; nitazitii kwa moyo wangu wote.
\s5
\v 35 Uniongoze katika njia ya amri zako, maana ninafurahi kuenenda katika hizo.
\v 36 Uelekeze moyo wangu kuzielekea amari za agano lako na uniweke mbali na matendo yasiyo haki tena.
\s5
\v 37 Uyageuze macho yangu dhidi ya kutazama mambo yasiyofaa; unihuishe katika njia zako.
\v 38 Umtendee mtumishi wako ahadi ambayo uliifanya kwa wale wanaokuheshimu wewe.
\s5
\v 39 Uniondolee shutumu niiogopayo, maana hukumu zako za haki ni njema.
\v 40 Tazama, nimeyatamani maagizo yako; unihuishe katika haki yako. VAV.
\s5
\v 41 Ee Yahwe, unipe upendo wako usiokwisha na wokovu wako kulingana na ahadi yako;
\v 42 ndipo nitakuwa na jibu kwa ajili ya yule anayenidhihaki.
\s5
\v 43 Usiliondoe neno la kweli mdomoni mwangu, maana nimesubiri kwa ajili ya amri zako za haki.
\v 44 Nitazitii sheria zako siku zote, milele na milele.
\s5
\v 45 Nitaenenda salama, maana ninayatafuta maagizo yako.
\v 46 Nitazinena amri zako thabiti mbele ya wafalme nami sitaaibika.
\s5
\v 47 Ninafurahia katika amri zako, nizipendazo sana.
\v 48 Nitaziinulia mikono yangu amri zako, nizipendazo; nitazitafakari sheria zako. ZAYIN.
\s5
\v 49 Kumbuka ahadi yako kwa mtumishi wako kwa sababu umenipa tumaini.
\v 50 Hii ni faraja yangu katika mateso: kuwa ahadi yako imeniweka hai.
\s5
\v 51 Wenye kiburi wamenicheka, lakini sijaiacha sheria yako.
\v 52 Nimezitafakari amri zako za haki tangu zamani, Yahwe, nami ninajifariji mwenyewe.
\s5
\v 53 Hasira kali imenishikilia kwa sababu ya waovu wanaoikataa sheria yako.
\v 54 Sheria zako zimekuwa nyimbo zangu katika nyumba ninayoishi kwa muda.
\s5
\v 55 Ninalifikiria jina lako wakati wa usiku, Yahwe, na kuzishika sheria zako.
\v 56 Hili limekuwa zoezi langu kwa sababu nimeyatii maagizo yako. HETH.
\s5
\v 57 Yahwe ni sehemu yangu; nimeamua kuyatii maneno yake.
\v 58 Kwa bidii ninaomba neema yako kwa moyo wangu wote; unihurumie, kama neno lako lilivyo ahidi.
\s5
\v 59 Nilizichunguza njia zangu na kugeuzia miguu yangu kwenye amri za agano lako.
\v 60 Naharakisha na sichelewi kuzishika amri zako.
\s5
\v 61 Kamba za waovu zimenifunga; nami sijaisahau sheria yako.
\v 62 Katikati ya usiku ninaamka kukushukuru wewe kwa sababu ya amri za haki yako.
\s5
\v 63 Ninaurafiki na wale wanao kuabudu wewe, wale wote watiio maagizo yako.
\v 64 Yahwe, nchi, imejaa uaminifu wa agano lako; unifundishe sheria zako. TETH.
\s5
\v 65 Wewe umemtendea mema mtumishi wako, Yahwe, sawasawa na neno lako.
\v 66 Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako.
\s5
\v 67 Kabla sijateswa nilipotea, lakini sasa nimelitii neno lako.
\v 68 Wewe ni mwema, na ndiye yule utendaye mema; unifundishe sheria zako.
\s5
\v 69 Wenye kiburi wamenichafua kwa uongo, lakini niliyashika maagizo yako kwa moyo wangu wote.
\v 70 Mioyo yao ni migumu, lakini ninafurahia katika sheria yako.
\s5
\v 71 Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako.
\v 72 Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. YOD.
\s5
\v 73 Mikono yako imeniumba na kunitengeneza; unipe uelewa ili niweze kujifunza amri zako.
\v 74 Wale wanao kucha wewe watafurahi wanionapo kwa sababu ninapata tumaini katika neno lako.
\s5
\v 75 Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa.
\v 76 Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.
\s5
\v 77 Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu.
\v 78 Wenye kiburi na waaibishwe, maana wamenitukana; bali mimi nitayatafakari maagizo yako.
\s5
\v 79 Wale wote wanao kucha wewe na wanigeukie, wale wazijuao amri za agano lako.
\v 80 Moyo wangu uwe mkamilifu pamoja na heshima kwa sheria zako ili nisiaibike. KAPH.
\s5
\v 81 Ninazimia kwa kutamani sana kuwa wewe unaweza kuniokoa! Ninamatumaini katika neno lako.
\v 82 Macho yangu yanatamani sana kuiona ahadi yako; ni lini utanifariji mimi?
\s5
\v 83 Kwa maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; sisahau sheria zako.
\v 84 Ni kwa muda gani gani mtumishi wako atalazimika kuyavumilia haya; ni lini utawahukumu wale wanaonitesa?
\s5
\v 85 Wenye kiburi wamenichimbia shimo, wasiotii sheria yako.
\v 86 Amri zako zote ni za kuaminika; wale watu walinitesa bila ya haki; unisaidie.
\s5
\v 87 karibu kunifanya nifikie mwisho juu ya nchi hii, lakini siyakatai maagizo yako.
\v 88 Kwa upendo wako thabiti, uniweke hai, ili niweze kuzitii amri zako. LAMEDH.
\s5
\v 89 Yahwe, neno lako linasimama milele; neno lako limefanywa imara mbinguni.
\v 90 Uaminifu wako wadumu kwa ajili ya vizazi vyote; umeiimarisha nchi, nayo inadumu.
\s5
\v 91 Vitu yote yaliendelea mpaka leo hii, kama vile ulivyosema katika amri zako za haki, maana vitu vyote ni watumishi wako.
\v 92 Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningeangamia katika mateso yangu.
\s5
\v 93 Sitayasahau kamwe maagizo yako, maana kupitia hayo umeniweka hai.
\v 94 Mimi ni wako, kwa maana ninayatafuta maagizo yao.
\s5
\v 95 Waovu hujiandaa kuniangamiza, lakini nitatafuta kuzielewa amri za agano lako.
\v 96 Nimeona kuwa kila kitu kina mipaka, lakini amri zako ni pana, zaidi ya mipaka. MEM.
\s5
\v 97 Oh ni jinsi gani naipenda sheria yako! Ni tafakari yangu mchana kutwa.
\v 98 Amri zako hunifanya mwenye hekima kuliko adui zangu, maana amri zako siku zote ziko pamoja nami.
\s5
\v 99 Ninauelewa zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa maana ninazitafakari amri za agano lako.
\v 100 Ninaelewa kuliko wale wanaonizidi umri; hii ni kwa sababu nimeyashika maagizo yako.
\s5
\v 101 Nimeiepusha miguu yangu na kila njia ya uovu ili niweze kulitii neno lako.
\v 102 Sijaenda kinyume na amri zako za haki, kwa maana wewe umenifundisha.
\s5
\v 103 Ni jinsi gani maneno yako ni matamu kwenye majaribu yangu, naam, matamu kuliko asali kinywani mwangu!
\v 104 Kupitia maagizo yako ninapata utambuzi; kwa hiyo kila njia isiyo ya kweli.
\s5
\v 105 Neno lako ni taa ya mguu miguu yangu na mwanga wa njia yangu.
\v 106 Nimeapa na nimethibitisha, kuwa nitazitii amri za haki yako.
\s5
\v 107 Nimeteswa sana; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika neno lako.
\v 108 Yahwe, tafadhali pokea dhabihu yangu ya hiari ya kinywa changu, na unifundishe amri zako za haki.
\s5
\v 109 Uhai wangu ziku zote uko mkononi mwangu, lakini bado sisahau sheria yako.
\v 110 Waovu wamenitegea mtego, lakini sijapotea mbali na maagizo yako.
\s5
\v 111 Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu.
\v 112 Moyo wangu umewekwa kuzitii sheria zako milele mpaka mwisho kabisa. SAMEKH.
\s5
\v 113 Ninawachukia watu wa kusita-sita, lakini naipenda sheria yako.
\v 114 Wewe ni ficho langu na ngao yangu; nalingoja neno lako.
\s5
\v 115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu, ili niweze kuzitii amri za Mungu wangu.
\v 116 Uniwezeshe kwa neno lako ili niweze kuishi na nisiaibike na matumaini yangu.
\s5
\v 117 Unisaidie, nami nitakuwa salama; siki zote nitazitafakari sheria zako.
\v 118 Wewe huwakataa wale wote wapoteao mbali na sheria zako, maana watu hao ni wadanganyifu na si wakuaminika.
\s5
\v 119 Wewe huwaondoa waovu wa nchi kama takataka; kwa hiyo ninazipenda amri zako thabiti.
\v 120 Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako. AYIN.
\s5
\v 121 Ninafanya kilicho sahihi na haki; usiniache kwa watesi wangu.
\v 122 Uwe mdhamini wa ustawi wa mtumishi wako; usiwaache wenye kiburi wanionee.
\s5
\v 123 Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
\v 124 Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
\s5
\v 125 Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako.
\v 126 Ni wakati wa Yahwe kutenda, kwa maana watu wamevunja sheria yako.
\s5
\v 127 Hakika ninazipenda amri zako kuliko dhahabu, naam, kuliko dhahabu safi.
\v 128 Hivyo ninayafuata maagizo yako yote kwa makini, na ninachukia kila njia ya uongo. PE.
\s5
\v 129 Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii.
\v 130 Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
\s5
\v 131 Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
\v 132 Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako.
\s5
\v 133 Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale.
\v 134 Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako.
\s5
\v 135 Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.
\v 136 Mito ya machozi yatiririka kutoka machoni pangu kwa sababu watu hawaitii sheria yako. TSADHE.
\s5
\v 137 Wewe ni mwenye haki, Yahwe, na amri zako ni haki.
\v 138 Umezipa amri za agano lako haki na uaminifu.
\s5
\v 139 Hasira imeniangamiza kwa sababu adui zangu husahau maneno yako.
\v 140 Neno lako limepimwa sana, naye mtumishi wako analipenda.
\s5
\v 141 Sina umuhimu na ninadharauliwa, lakini bado siyasahau maagizo yako.
\v 142 Hukumu yako ni ya haki milele, na sheria yako ni ya kuaminika.
\s5
\v 143 Japo dhiki na taabu vimenipata, amri zako bado ni furaha yangu.
\v 144 Amri za agano lako ni za haki milele; unipe uelewa ili niweze kuishi. QOPH.
\s5
\v 145 Nililia kwa moyo wangu wote, "Unijibu, Yahwe, nitazishika sheria zako.
\v 146 Ninakuita wewe; uniokoe, nami nitazitii amri za agano lako."
\s5
\v 147 NInaamka asubuhi kabla jua halijachomoza na kulia kwa ajili ya msaada.
\v 148 Ninatumaini katika maneno yako. Macho yangu yako wazi usiku kucha ili niweze kutafakari juu ya neno lako.
\s5
\v 149 Sikia sauti yangu katika uaminifu wa agano lako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika amri zako za haki.
\v 150 Wale wanaonitesa wananikaribia, lakini wako mbali na sheria yako.
\s5
\v 151 Wewe uko karibu, Yahwe, na amri zako ni za kuaminika.
\v 152 Muda mrefu uliopita nilijifunza kutoka katika amri za agano lako ulizoziweka katika mahali pa milele. RESH.
\s5
\v 153 Uyatazame mateso yangu na unisaidie, maana siisahau sheria yako.
\v 154 Unitetee na kunikomboa; unihifadhi, kama ulivyo ahidi katika neno lako.
\s5
\v 155 Wokovu uko mbali na waovu, maana hawazipendi amri zako.
\v 156 Matendo yako ya huruma ni makuu, Yahwe; uniweke hai; kama ufanyavyo siku zote.
\s5
\v 157 Watesi wangu na adui zangu ni wengi, lakini bado sijaenda mbali na amri za agano lako.
\v 158 Nimewaona wasaliti wakitia kinyaa kwa sababu hawalishiki neno lako.
\s5
\v 159 Tazama jinsi niyapendavyo maagizo yako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika uaminifu wa agano lako.
\v 160 Kiini cha neno lako ni kweli; kila mmoja mwenye amri za haki hudumu milele. SHIN.
\s5
\v 161 Wakuu hunitesa bila sababu; moyo wangu hutetemeka, ukiogopa kutolitii neno lako.
\v 162 Ninalifurahia neno lako kama apataye nyara nyingi.
\s5
\v 163 Ninachukia na kudharau uongo, lakini naipenda sheria yako.
\v 164 Mara saba kwa siku ninakusifu wewe kwa sababu ya amri zako za haki.
\s5
\v 165 Wana amani nyingi, waipendao sheria yako; hakuna cha kuwatia mashakani.
\v 166 Naungoja wokovu wako, Yahwe, na ninatii amri zako.
\s5
\v 167 Ninazishika amri zako thabiti, na ninazipenda sana.
\v 168 Ninayashika maagizo yako na amri zako thabiti, kwa maana unajua kila kitu nifanyacho. TAV.
\s5
\v 169 Sikia kilio changu, Yahwe; unipe uelewa wa neno lako.
\v 170 Maombi yangu yaje mbele zako; unisaidie, kama ulivyoahidi katika neno lako.
\s5
\v 171 Midomo yangu na imwage sifa, maana wewe unanifundisha sheria zako.
\v 172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
\s5
\v 173 Mkono wako unisaidie, maana nimechagua maagizo yako.
\v 174 Ninautamani wokovu wako, Yahwe, na sheria yako ni furaha yangu.
\s5
\v 175 Naomba niishi na nikusifu wewe, na amri zako za haki zinisaidie.
\v 176 Nimetanga-tanga kama kondoo aliyepotea; mtafute mtumishi wako, kwa maana sijazisahau amri zako.
\s5
\c 120
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe, naye akanijibu.
\v 2 Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao.
\s5
\v 3 Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu?
\v 4 Atawaadhibu kwa mishale ya shujaa iliyo nolewa kwa makaa ya moto ya mretemu.
\s5
\v 5 Ole wangu mimi kwa sababu ninaishi kwa muda Mesheki; huko nyuma niliishi kati ya maskani ya Kedari.
\v 6 Kwa muda mrefu sana niliisha na wale waichukiao amani.
\v 7 Nipo kwa ajili ya amani, lakini ninenapo, wao wako kwa ajili ya vita.
\s5
\c 121
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi?
\v 2 Msaada wangu unatoka kwa Yahwe, aliyezifanya mbingu na nchi.
\s5
\v 3 Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia.
\v 4 Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe.
\s5
\v 5 Yahwe ni mlinzi wako; Yahwe ni uvuli mkono wako wa kuume.
\v 6 Jua halitakudhuru wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
\s5
\v 7 Yahwe atakulinda na madhara yote, na ataulinda uhai wako.
\v 8 Yahwe atakulinda katika yote ufanyayo sasa na hata milele.
\s5
\c 122
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi.
\v 1 Nilifurahi waliponiambia, "Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe."
\v 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako!
\v 3 Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini!
\s5
\v 4 Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe.
\v 5 Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
\s5
\v 6 Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! "Wote wakupendao wawe na amani.
\v 7 Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako."
\s5
\v 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, "Amani iwe ndani yenu."
\v 9 Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.
\s5
\c 123
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
\v 2 Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia.
\s5
\v 3 Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana.
\v 4 Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.
\s5
\c 124
\p Wimbo wa kwenda kuabudu; wa Daudi.
\v 1 "Kama Yahwe asingekuwa upande wetu," Israeli na aseme sasa,
\v 2 "Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu,
\v 3 basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu.
\s5
\v 4 Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia.
\v 5 Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha."
\s5
\v 6 Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao.
\v 7 Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka.
\s5
\v 8 Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.
\s5
\c 125
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele.
\v 2 Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele.
\v 3 Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea.
\s5
\v 4 Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao.
\v 5 Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.
\s5
\c 126
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.
\s5
\v 2 Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, "Yahwe amewatendea mambo makuu."
\v 3 Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo!
\s5
\v 4 Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini.
\v 5 Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.
\v 6 Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.
\s5
\c 127
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Solomoni.
\v 1 Yahwe asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure. Yahwe asipoulinda mji, aulindaye afanya kazi bure.
\v 2 Ni kazi bure kwa wewe unayeamka mapema, na kulala kwa kuchelewa, au kula mkate kwa kuufanyia kazi ngumu, maana Yahwe huwapa chakula awapendao hata wawapo usingizini.
\s5
\v 3 Tazama, wana ni urithi kutoka kwa Yahwe, uzao wa tumbo ni thawabu kutoka kwake.
\v 4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani.
\v 5 Ni namna gani alivyo barikiwa mtu ambaye amelijaza podo lake hivyo. Hata aibishwa pindi atakapo kabiliana na adui zake katika lango.
\s5
\c 128
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake.
\v 2 Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa.
\s5
\v 3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako.
\v 4 Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa.
\v 5 Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.
\v 6 Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.
\s5
\c 129
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 "Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia," Israeli na iseme.
\v 2 "Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda.
\v 3 Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu.
\s5
\v 4 Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu."
\v 5 Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni.
\s5
\v 6 Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua,
\v 7 ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.
\v 8 Wale wapitao karibu wasiseme, "Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe."
\s5
\c 130
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe.
\v 2 Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
\s5
\v 3 Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama?
\v 4 Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa.
\s5
\v 5 Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia.
\v 6 Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi.
\s5
\v 7 Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe.
\v 8 Ni
yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.
\s5
\c 131
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu; wa Daudi.
\v 1 Yahwe, moyo wangu haujivuni wala macho yangu hayana kuburi. Sina matarajio makubwa kwa ajili yangu mwenyewe wala kujihofia kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wangu.
\s5
\v 2 Hakika nimejituliza na kuinyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa na mama yake, nafsi yangu ndani yangu iko kama mtoto aliye achishwa.
\v 3 Israeli, umtumainie Yahwe sasa na hata milele.
\s5
\c 132
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Yahwe, kwa ajili ya Daudi kumbuka mateso yake yote.
\v 2 Kumbuka ndiye aliye mwapia Yahwe, aliweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.
\s5
\v 3 Alisema, sitaingia nyumbani mwangu wala sitaenda kitandani mwangu,
\v 4 sitayapa macho yangu usingizi wala kope zangu kupumzika
\v 5 mpaka nitakapopata mahali kwa ajili ya Yahwe, na maskani kwa ajili ya Shujaa wa Yakobo."
\s5
\v 6 Tazama tulisikia kuhusu hilo katika Efrata; tuliipata katika konde la Yearimu.
\v 7 Tutaingia katika maskani ya Mungu; tutasujudu miguuni pake.
\v 8 Inuka, Ee Yahwe, uje mahali pako pa kupumzika, wewe na sanduku la nguvu zako!
\s5
\v 9 Makuhani wako na wavikwe uadilifu; waaminifu wako washangilie.
\v 10 Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi, usimuache mfalme wako uliye mpaka mafuta.
\s5
\v 11 Yahwe alimwapia Daudi kiapo cha uhakika, kiapo cha uhakika ambacho hatakivunja: "Nitamuweka mmoja wa wazawa wako kwenye kiti chako cha enzi.
\v 12 Kama wana wako watalishika agano langu na sheria ambazo nitawafundisha, watoto wao pia watakaa kwenye kiti chako cha enzi milele."
\s5
\v 13 Hakika Yahwe ameichagua Sayuni, ameitamani kwa ajili ya makao yake.
\v 14 "Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele. Nitaishi hapa, kwa kuwa ninapatamani.
\s5
\v 15 Nitapabariki sana kwa mahitaji. Nitawatosheleza maskini wake kwa mkate.
\v 16 Nitawavisha makuhani wake kwa wokovu, waaminifu wake watashangilia kwa furaha.
\s5
\v 17 Hapo nitachipusha pembe kwa ajili ya Daudi na kuweka taa juu kwa ajili ya mpakwa mafuta wangu.
\v 18 Nitawavisha adui kwa aibu, bali juu yake taji yake itang'aa."
\s5
\c 133
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi.
\v 1 Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja!
\s5
\v 2 Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
\v 3 Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.
\s5
\c 134
\p Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
\v 1 Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku.
\v 2 Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.
\s5
\v 3 Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.
\s5
\c 135
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Lisifuni jina la Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe,
\v 2 ninyi msimamao katika nyumba ya Yahwe, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
\s5
\v 3 Msifuni Yahwe, kwa kuwa ni mwema; liimbieni sifa jina lake, maana ni vizuri kufanya hivyo.
\v 4 Kwa kuwa Yahwe amemchagua Yakobo kwa ajili yake mwenyewe, Israeli kama urithi wake.
\s5
\v 5 Najua ya kuwa Yahwe ni mkuu, na kwamba Bwana wetu yuko juu ya miungu yote.
\v 6 Chochote Yahwe apendacho, hufanya mbinguni, duniani, katika bahari na katika vilindi vyote.
\s5
\v 7 Hushusha mawingu kutoka mbali, akifanya mianga ya radi kuongozana na mvua na kuleta upepo toka katika ghala yake.
\s5
\v 8 Aliua mzaliwa wa kwanza wa Misri, wote wanadamu na wanyama.
\v 9 Alituma ishara na maajabu kati yako Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
\s5
\v 10 Aliwashambulia mataifa mengi na aliua wafalme wenye nguvu,
\v 11 Sihoni mfalme wa Waamori na Ogu mfalme wa Bashani na falme zote za Kanaani.
\s5
\v 12 Alitupatia sisi nchi yao kama urithi, urithi wa Israeli watu wake.
\v 13 Jina lako, Yahwe, inadumu milele; Yahwe, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
\s5
\v 14 Kwa kuwa Bwana huwatetea watu wake na anahuruma juu ya watumishi wake.
\v 15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
\v 16 Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
\v 17 zina masikio, lakini hazisikii, wala vinywani mwao hamna pumzi.
\v 18 Wale wazitengenezao wanafanana nazo, vilevile kila anaye zitumainia.
\s5
\v 19 Enyi kizazi cha Israeli, mtukuzeni Yahwe; kizazi cha Haruni, mtukuzeni Yahwe.
\v 20 Kizazi cha Lawi, mtukuzeni Yahwe.
\v 21 Atukuzwe Yahwe katika Sayuni, yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 136
\p
\v 1 Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 2 Oh, Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 3 Oh, mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 4 Mshukuruni yeye ambaye peke yake hufanya maajabu makuu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 5 Yeye aliyezifanya mbingu kwa hekima zake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 6 Mshukuruni yeye alitetandaza nchi juu ya maji, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 8 Mshukuruni yeye alipaye jua kutawala mchana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 9 Mwezi na nyota vitawale usiku, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 10 Mshukuruni yeye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 11 Akawatoa Waisraeli kati yao, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 12 Kwa mkono hodari na mkono ulio nyooshwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 13 Mshukuruni yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 14 Na kuwapitisha Waisraeli katikati yake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 15 Lakini akamtupa Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 16 Mshukuruni yeye aliye waongoza watu wake jangwani, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wa milele.
\v 17 Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
\s5
\v 18 Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 19 Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 20 Na Ogu, mfalme wa Bashani, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 21 Mshukuruni yeye aliyewapa nchi yao kama urithi, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 22 Urithi wa Israel mtumishi wake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 23 Yeye aliyetukumbuka na kutusaidia katika unyonge wetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\v 24 Mshukuruni yeye ambaye ametupa ushindi juu ya aui zetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 25 Yeye awapaye chakula viumbe hai wote, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\v 26 Oh, mshukuruni Mungu wa mbinguni, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
\s5
\c 137
\p
\v 1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni.
\v 2 Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon.
\s5
\v 3 Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, "Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni."
\v 4 Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni?
\s5
\v 5 Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
\v 6 Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu.
\s5
\v 7 Kumbuka, Ee Yahwe, kile walichofanya Waedomu siku ya anguko la Yerusalemu. Walisema, "Ibomoeni, ibomoeni mpaka chini kwenye misingi yake."
\s5
\v 8 Binti za Babeli, hivi karibuni wataharibiwa- mtu na abalikiwe, yeyote atakaye walipizia yale mliotufanyia sisi.
\v 9 Mtu na abarikiwe, yeyote achukuaye na kusambaratisha watoto wenu juu ya jiwe.
\s5
\c 138
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote; mbele ya miungu nitakuimbia sifa.
\v 2 Nitasujundu mbele ya hekalu lako takatifu na kulishukuru jina lako kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na kwa uaminifu wako. Umelifanya muhimu zaidi neno lako na jina lako kuliko kitu chochote.
\s5
\v 3 Siku ile niliyo kuita, ulinijibu; ulinitia moyo na kuitia nguvu nafsi yangu.
\v 4 Wafalme wote wa nchi watakushukuru wewe, Yahwe, maana watasikia maneno kutoka kinywani mwako.
\s5
\v 5 Hakika, wataimba kuhusu matendo ya Yahwe, kwa kuwa utukufu wa Yahwe ni mkuu.
\v 6 Maana ingawa Yahwe yuko juu, lakini anawajali wanyenyekevu, lakini hawatambui wenye majivuno.
\s5
\v 7 Nijapopita katikati ya hatari, wewe utauhifadhi uhai wangu; utanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa.
\v 8 Yahwe yuko pamoja nami hadi mwisho; uaminifu wa agano lako, Yahwe, wadumu milele. Usiwaache wale ambao mikono yako imewaumba.
\s5
\c 139
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi.
\v 1 Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua.
\v 2 Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana.
\s5
\v 3 Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote.
\v 4 Kabla hakujawa na neno kwenye ulimi wangu, wewe unalijua kabisa, Yahwe.
\v 5 Nyuma yangu na mbele yangu unanizunguka na kuniwekea mkono wako.
\v 6 Maarifa hayo ni mengi yananizidi mimi; yako juu sana, nami siwezi kuyafikia.
\s5
\v 7 Niende wapi mbali na roho yako? Niende wapi niukimbie uwepo wako?
\v 8 Kama nikipaa mbinguni, uko huko; kama nikifanya kitanda changu Kuzimuni, tazama, uko huko.
\s5
\v 9 Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari,
\v 10 hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika.
\s5
\v 11 Kama nikisema, "Hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo itakuwa usiku,"
\v 12 Hata giza lisingweza kuwa giza kwako. Usiku ungeng'aa kama mchana, maana giza na nuru kwako vinafanana.
\s5
\v 13 Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu.
\v 14 Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana.
\s5
\v 15 Mifupa yangu haikusitirika kwako nilipoumbwa kwa siri, nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi.
\v 16 Uliniona ndani ya tumbo; siku zote zilizo pangwa kwangu ziliandikwa kitabuni mwako hata kabla ya siku ya kwanza kutokea.
\s5
\v 17 Ni jinsi gani mawazo yako ni ya thamani kwangu, Mungu! Njinsi ilivyo kubwa jumla zake!
\v 18 Kama nikijaribu kuyahesabu ni mengi kuliko mchanga. Niamkapo bado niko na wewe.
\s5
\v 19 Ee Mungu, kama ungewaua waovu; ondokeni kwangu enyi watu wenye vurugu.
\v 20 Wanakuasi wewe na kutenda udanganyifu; adui zako wananena uongo.
\s5
\v 21 Je, siwachukii hao, wale wakuchukiao Yahwe? Je, siwadharau wale wanao inuka dhidi yako?
\v 22 Nawachukia kabisa; wamekuwa adui zangu.
\s5
\v 23 Ee Mungu, unichunguze na kuujua moyo wangu; unijaribu na uyajue mawazo yangu.
\v 24 Uone kama kuna njia ya uovu ndani yangu, na uniongoze katika njia ya milele.
\s5
\c 140
\p Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
\v 1 Yahwe, uniokoe dhidi ya waovu; unikinge dhidi ya watu wenye vurugu.
\v 2 Wao wanapanga uovu mioyoni mwao; wanasababisha mapigano kila siku.
\v 3 Ndimi zao zinajeruhi kama nyoka; sumu ya fira imo midomoni mwao. Selah
\s5
\v 4 Ee Yahwe, unilinde dhidi ya mikono ya waovu; unikinge na vurugu za watu wanaopanga kuniangusha.
\v 5 Wenye majivuno wameweka mtego kwa ajili yangu; wameeneza nyavu; wameweka kitanzi kwa ajili yangu. Selah
\s5
\v 6 Nilimwambia Yahwe, "Wewe ni Mungu wangu; usikie kilio changu unihurumie."
\v 7 Ee Yahwe, Bwana wangu, wewe ni mwenye nguvu uwezaye kuniokoa; hunifunika ngao kichwa changu siku ya vita.
\v 8 Ee Yahwe, usiyatimize matakwa ya waovu; usiruhusu njama zao kufanikiwa. Selah
\s5
\v 9 Wale wanao nizunguka huinua vichwa vyao; madhara ya midomo yao wenyewe na yawafunike.
\v 10 Makaa ya moto na yawaangukie; uwatupe motoni, kwenye shimo refu, wasiweze kuinuka tena.
\v 11 Watu wenye ndimi na wasifanywe salama juu ya nchi; na uovu umuwinde kumpiga mtu mwenye vurugu mpaka afe.
\s5
\v 12 Ninajua kuwa Yahwe atahukumu kwa haki walioteswa, na kuwa atawapa haki wahitaji.
\v 13 Hakika watu wenye haki watalishukuru jina lako; watu wanyoofu wataishi uweponi mwako.
\s5
\c 141
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Ee Yahwe, ninakulilia wewe; uje upesi kwangu. Unisikilize nikuitapo.
\v 2 Maombi yangu na yawe kama uvumba mbele zako; mikono yangu iliyoinuliwa na iwe kama dhabihu ya jioni.
\s5
\v 3 Ee Yahwe, uweke mlinzi kinywani mwangu; mngojezi malangoni pa midomo yangu.
\v 4 Usiruhusu tamaa ya moyo wangu kutamani uovu wowote wala kushiriki katika matendo ya dhambi na watu waishio maovuni. Nisile vyakula vyao vya anasa.
\s5
\v 5 Mwenye haki na anipige; nao utakuwa ni wema kwangu. Anirudi; itakuwa kama mafuta kichwani pangu; kichwa changu na kisikatae kupokea. Lakini maombi yangu siku zote yatakuwa dhidi ya matendo yao mauvu.
\v 6 Viongozi wao watatupwa chini toka juu mlimani; watayasikia maneno yangu kuwa ni matamu.
\v 7 Watalazimika kusema, "Kama vile jembe moja livunjapo ardhi, hivyo mifupa yetu imesambaratishwa kinywani pa kuzimu."
\s5
\v 8 Hakika macho yangu yanakutazama wewe, Yahwe, Bwana; katika wewe napata kimbilio; usiiache nafsi yangu.
\v 9 Unilinde dhidi ya mitego waliyoiweka kwa ajili yangu, na matanzi yao watendao maovu.
\v 10 Waovu na waangukie kwenye nyavu zao wenywe pindi mimi nitorokapo.
\s5
\c 142
\p Zaburi ya Daudi, alipokuwa pangoni; maombi.
\v 1 Kwa sauti yangu namlilia Yahwe anisaidie; kwa sauti yangu naomba kwa ajili ya neema ya Yahwe.
\v 2 Namwaga malalamiko yangu mbele zake; ninamwambia shida zangu.
\s5
\v 3 Roho yangu inapokuwa dhaifu ndani yangu, wewe unajua mapito yangu. Kwenye njia niipitayo wamenifichia mtego.
\v 4 Natazama kulia kwangu na sioni yeyote anayenijali. Sina pa kukimbilia; hakuna anayejali kuhusu uhai wangu.
\v 5 Nilikuita wewe, Yahwe; nikasema, "Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.
\s5
\v 6 Sikia kuita kwangu, maana nimeshushwa chini sana; uniokoe dhidi ya watesi wangu, maana wana nguvu kuliko mimi.
\v 7 Uitoe nafsi yangu kifungoni ili niweze kulishukuru jina lako. Wenye haki watakusanyika karibu nami kwa sababu umekuwa mwema kwangu."
\s5
\c 143
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Ee Yahwe, usikie maombi yangu; sikia kuomba kwangu. Kwa sababu ya uaminifu wa agano lako na haki yako, unijibu!
\v 2 Usimuhukumu mtumishi wako, kwa kuwa machoni pako hamna aliye haki.
\s5
\v 3 Adui ameifuatia nafsi yangu; amenisukuma hadi chini; amenifanya niishi gizani kama wale ambao wamekwisha kufa siku nyingi zilizopita.
\v 4 Na roho yangu inazidiwa ndani yangu; moyo wangu unakata tamaa.
\s5
\v 5 Nakumbuka siku za zamani zilizopita; nayatafakari matendo yako yote; nawaza juu ya utimilifu wako.
\v 6 Nakunyoshea mikono yangu katika maombi; nafsi yangu inakuonea kiu katika nchi kavu. Selah
\s5
\v 7 Unijibu upesi, Yahwe, kwa sababu roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, vinginevyo nitakuwa kama wale waendao chini shimoni.
\v 8 Unifanye kusikia uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi, maana ninakuamini wewe. Unionyeshe njia niipasayo kutembea kwayo, kwa maana nakuinulia wewe nafsi yangu.
\s5
\v 9 Uniokoe dhidi ya adui zangu, Yahwe; nakimbilia kwako ili nijifiche.
\v 10 Unifundishe kufanya mapenzi yako, maana wewe ni Mungu wangu. Roho wako mwema na aniongoze mimi katika nchi ya unyoofu.
\s5
\v 11 Ee Yahwe, kwa ajili ya jina lako, unihifadhi hai; katika haki yako uitoe nafsi yangu taabuni.
\v 12 Katika uaminifu wa agano lako uwaondoshe maadui zangu na uwaangamize maadui wa uhai wangu, maana mimi ni mtumishi wako.
\s5
\c 144
\p Zaburi ya Daudi.
\v 1 Atukuzwe Yahwe, mwamba wangu, anifundishaye mikono yangu vita na vidole vyangu kupigana.
\v 2 Wewe ni uaminifu wa agano langu na ngome yangu, mnara wangu mrefu na uniokoaye, ngao yangu na yule ambaye katika yeye napata kimbilio, uyatiishaye mataifa chini yangu.
\s5
\v 3 Ee Yahwe, mtu ni kitu gani hata umtazame au mwana wa mtu hata umfikirie?
\v 4 Mtu ni kama pumzi, siku zake ni kama uvuli upitao.
\s5
\v 5 Ee Yahwe uziinamishe mbingu na ushuke chini, uiguse milima na uifanye kutoa moshi.
\v 6 Utume umeme uwatawanye adui zangu; upige mishale yako na uwavuruge.
\s5
\v 7 Nyosha mkono wako toka juu; uniokoe kutoka katika maji mengi, na kutoka katika mkono wa wageni.
\v 8 vinywa vyao hunena uongo, na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
\s5
\v 9 Nitakuimbia wimbo mpya, Mungu; kwa kinanda cha nyuzi kumi nitakuimbia sifa wewe,
\v 10 uwapaye wafalme wokovu, uliye muokoa Daudi mtumishi wako dhidi ya upanga wa uovu.
\v 11 Uniokoe na unitoe mkononi mwa wageni. Midomo yao huongea uongo, na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
\s5
\v 12 Wana wetu na wawe kama mimea ikuayo kwa ukumbwa timilifu katika ujana wao na binti zetu kama nguzo za pembeni, zilizonakishiwa kwa kupamba jumba la kifahari.
\v 13 Ghala zetu na zijae akiba ya kila aina ya mazao, na kondoo wetu wazae elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
\s5
\v 14 Kisha ng'ombe wetu watakuwa na nddama wengi. Hakuna atakayevunja kuta zetu; hakutakuwa na uhamisho wala kilio mitaani mwetu.
\v 15 Wamebarikiwa watu wenye baraka hizo; furaha ina watu ambao Mungu wao ni Yahwe.
\s5
\c 145
\p Zaburi ya sifa. Ya Daudi.
\v 1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu, Mfalme; nitalihimidi jina lako milele na milele.
\v 2 Kila siku nitakuhimidi; nitalisifu jina lako milele na milele.
\v 3 Yahwe ndiye mkuu na wakusifiwa sana; ukuu wake hauchunguziki.
\s5
\v 4 Kizazi kimoja kitayasifu matendo yako kwa kizazi kijacho na kitatangaza matendo yako makuu.
\v 5 Nitaitafakari fahari ya utukufu wa adhama yako na matendo yako ajabu.
\s5
\v 6 Watanena juu ya nguvu ya kazi zako za kutisha, nami nitatangaza ukuu wako.
\v 7 Nao watatangaza wingi wa wema wako, na wataimba kuhusu haki yako.
\s5
\v 8 Yahwe ni wa neema na huruma, si mwepesi wa hasira na mwingi katika uaminifu wa agano lake.
\v 9 Yahwe ni mwema kwa wote; huruma zake zi juu ya kazi zake zote.
\s5
\v 10 Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
\v 11 Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako.
\v 12 Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
\s5
\v 13 Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
\s5
\v 14 Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.
\v 15 Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.
\v 16 Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai.
\s5
\v 17 Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo.
\v 18 Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.
\v 19 Hutimiza haja za wale wanao mheshimu yeye; husikia kilio chao na kuwaokoa.
\s5
\v 20 Yahwe huwalinda wale wampendao, lakini atawaangamiza waovu wote.
\v 21 Kinywa changu kitazinena sifa za Yahwe; wanadamu wote na walitukuze jina lake takatifu milele na milele.
\s5
\c 146
\p
\v 1 Msifu Yahwe. Msifu Yahwe, ee nafsi yangu.
\v 2 Ninamsifu Mungu maisha yangu yote; nitamuimbia sifa Mungu wangu ni ngali ni hai.
\s5
\v 3 Msiweke imani katika wakuu au wanadamu, ambaye katika yeye hamna wokovu.
\v 4 Wakati uhai wa pumzi ya mtu unapokoma, hurudi aridhini; siku hiyo mipango yake hufikia mwisho.
\s5
\v 5 Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake.
\v 6 Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele.
\s5
\v 7 Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa;
\v 8 Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki.
\s5
\v 9 Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki.
\v 10 Yahwe atatawala milele, Mungu wako, Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 147
\p
\v 1 Msifuni Yahwe, kwa maana ni vyema kumwimbia sifa Mungu wetu, ni kuzuri, kusifu kwa faa sana.
\s5
\v 2 Yahwe huijenga tena Yerusalemu, huwakusanya pamoja watu wa Israeli waliotawanyika.
\v 3 Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
\s5
\v 4 Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote.
\v 5 Ukuu ni wa Bwana wetu na nguvu zake ni za kutisha, ufahamu wake hauwezi kupimika.
\s5
\v 6 Yahwe huwainua wanyonge, huwashusha chini wenye jeuri.
\v 7 Mwimbieni Yahwe kwa shukurani, mwimbieni sifa Mungu wetu kwa kinubi.
\s5
\v 8 Huzifunika mbingu kwa mawingu na huiandaa mvua kwa ajili ya nchi, akizifanya nyasi kukua juu ya milima.
\v 9 Huwapa wanyama chakula na wana kunguru waliapo.
\s5
\v 10 Hapati furaha katika nguvu ya farasi, wala haridhii miguu imara ya mwanadamu.
\v 11 Yahwe huridhia katika wale wanao muheshimu yeye, watumainio katika uaminifu wa agano lake.
\s5
\v 12 Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni.
\v 13 Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
\v 14 Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
\s5
\v 15 Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.
\v 16 Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
\s5
\v 17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo, ni nani awezaye kuhimili baridi aitumayo?
\v 18 Hutuma amri zake na kuziyeyusha, huvumisha upepo wake na hutiririsha maji.
\s5
\v 19 Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
\v 20 Hajafanya hivyo kwa taifa linginelo lolote, na kama ilivyo amri zake, hawazijui. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 148
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe, ninyi mlio katika mbingu; msifuni yeye, ninyi mlio juu.
\v 2 Msifuni yeye, enyi malaika wake wote; msifuni yeye, majeshi ya malaika wake wote.
\s5
\v 3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi; msifuni yeye, nyota zote zing'aazo.
\v 4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu zaidi na maji yaliyo juu ya anga.
\s5
\v 5 Na vilisifu jina la Yahwe, maana aliamuru, navyo vikaumbwa.
\v 6 Pia ameviimrisha milele na milele; naye alitoa amri ambayo haitabadilika.
\s5
\v 7 Msifuni yeye kutoka nchi, ninyi viumbe wa baharini na viumbe vyote katika kina cha bahari,
\v 8 moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba ukitimiza neno lake.
\s5
\v 9 Msifuni yeye, enyi milima na vilima, miti ya matunda na mierezi yote,
\v 10 wanyama pori na wanyama wafugwao, viumbe vitambaavyo na ndege.
\s5
\v 11 Msifuni Yahwe, wafalme wa nchi na mataifa yote, wakuu na watawala wote wa nchi,
\v 12 wote vijana wa kiume na vijana wa kike, wazee na watoto.
\s5
\v 13 Na walisifu jina la Yahwe, kwa kuwa jina lake pekee limetukuka na utukufu wake umeongezwa juu ya nchi na mbingu.
\v 14 Naye ameyainua mapembe ya watu wake kwa ajili ya sifa kutoka kwa waaminifu wake wote, Waisraeli, watu wa karibu naye. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 149
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu.
\s5
\v 2 Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao.
\v 3 Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi.
\s5
\v 4 Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu.
\v 5 Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao.
\s5
\v 6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao
\v 7 kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu.
\s5
\v 8 Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa.
\v 9 Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.
\s5
\c 150
\p
\v 1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake.
\v 2 Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
\s5
\v 3 Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi.
\v 4 Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi.
\v 5 Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana.
\s5
\v 6 Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.