sw_ulb_rev/18-JOB.usfm

2028 lines
107 KiB
Plaintext

\id JOB
\ide UTF-8
\h Ayubu
\toc1 Ayubu
\toc2 Ayubu
\toc3 job
\mt Ayubu
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kulikuwa na mtu katika nchi ya Usi jina lake Ayubu; na Ayubu alikuwa mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na
\v 2 uovu. Wakazaliwa kwake watoto saba wa kiume na mabinti watatu.
\v 3 Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
\s5
\v 4 Kwa siku yake kila mtoto wa kiume, hufanya karamu katika nyumba yake. Wakatuma na kuwaita dada zao watatu waje kula na kunywa pamoja nao.
\v 5 Baada ya siku za karamu zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao na kuwatakasa. Aliamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa kila mtoto wake, kwa kusema, "Yawezekana kwamba wanangu wamefanya dhambi na kumkufuru Mungu mioyoni mwao." Siku zote Ayubu alifanya hivi.
\s5
\v 6 Kisha ilikuwa siku ambayo watoto wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia akaenda pamoja nao.
\v 7 BWANA akamuuliza Shetani, "Umetoka wapi wewe?" Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo."
\v 8 BWANA akamuuliza Shetani, "Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu."
\s5
\v 9 Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Je Ayubu amcha Mungu bila sababu?
\v 10 Wewe hukumwekea kinga pande zote, kuzunguka nyumba yake, na kuzunguka vitu vyote alivyo navyo kutoka kila upande? Wewe umebariki kazi za mikono yake, na mifugo yake imeongezeka katika nchi.
\v 11 Lakini sasa nyosha mkono wako na uguse yote hayo aliyonayo, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako."
\v 12 BWANA akamwambia Shetani, "Tazama, hayo yote aliyonayo yamo mkononi mwako. Isipokuwa juu yake yeye mwenyewe usinyoshe mkono wako." Kisha Shetani akatoka mbele za BWANA.
\s5
\v 13 Ilitokea siku moja, wana wake wa kiume na binti zake walipokuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
\v 14 Mjumbe akamfikia Ayubu na kusema, "Hao maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakichunga karibu nao.
\v 15 Waseba wakawaangukia na kutoweka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\s5
\v 16 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni na kuwateketeza kondoo na watumishi. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\v 17 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Wakaldayo walifanya vikundi vitatu, wakawashambulia ngamia, na kuondoka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\s5
\v 18 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Wana wako wa kiume na binti zako walikuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
\v 19 Upepo wenye nguvu ulitokea jangwani na ukapiga pembe nne za nyumba. Ikawaangukia vijana hao, na wakafa wote. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.
\s5
\v 20 Kisha Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akaanguka chini kifudifudi na kumwabudu Mungu.
\v 21 Akasema, "Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu ni uchi, nami nitakuwa uchi wakati nitakaporudi huko. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa. Jina la BWANA libarikiwe."
\v 22 Katika mambo hayo yote, Ayubu hakutenda dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa uovu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha kulikuwa na siku wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia alikwenda kati yao kujihudhulisha mbele za BWANA.
\v 2 BWANA akamuuliza Shetani, "umetoka wapi wewe?" Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo."
\s5
\v 3 BWANA akamuuliza Shetani, "Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliye mcha Mungu na kuepukana na uovu. Hata sasa anashikamana na utimilifu wake, japokuwa ulinichochea juu yake, nimwangamize pasipo sababu."
\s5
\v 4 Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Ngozi kwa ngozi, kweli; mtu atatoa vyote alivyo navyo kwaajili ya uhai wake.
\v 5 Lakini nyosha mkono wako sasa na uguse mifupa yake na nyama yake, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako."
\v 6 BWANA akamwambia Shetani, "Tazama, yumo mkononi mwako; ni uhai wake tu ambao lazima uutunze."
\s5
\v 7 Kisha Shetani akatoka mbele ya uso wa BWANA. Akampiga Ayubu na majipu mabaya toka wayo wa mguu hadi kichwani.
\v 8 Ayubu akachukua kipande cha kigae kujikunia, na akaketi chini majivuni.
\s5
\v 9 Kisha mkewe akamuuliza, "Je hata sasa wewe unashikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu na ufe.
\v 10 Lakini yeye akamwambia, "Wewe unaongea kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu waongeavyo. Je sisi tupate mema toka kwa Mungu na tusipate mabaya?" Katika mambo hayo yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.
\s5
\v 11 Sasa wakati rafiki zake watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya yaliyompata, kila mmoja wao akaja kutoka mahali pake: Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi. Wakatenga muda ili waende kuomboleza naye na kumfariji.
\s5
\v 12 Walipoinua macho yao wakiwa mbali, hawakuweza kumtambua. Wakapaza sauti zao na kulia; kila mmoja wao akararua joho lake na kurusha majivu hewani na juu ya kichwa chake.
\v 13 Kisha wakaketi chini pamoja naye kwa muda wa siku saba-mchana na usiku. Hakuna hata mmoja aliyesema naye neno, kwa kuwa waliona kuwa huzuni yake ilikuwa kuu mno.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Baada ya hayo, Ayubu akafunua kinywa chake na kuilani siku aliyozaliwa.
\v 2 Akasema,
\v 3 "Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
\s5
\v 4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu toka juu asiifikilie, wala mwanga usiiangazie.
\v 5 Ishikwe na giza na giza la mauti liwe lake. Wingu na likae juu yake; kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza kweli na kiitishe.
\s5
\v 6 Usiku huo, na ukamatwe na giza tororo. Usihesabiwe miongoni mwa siku za mwaka; na usiwekwe katika hesabu ya miezi.
\v 7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; na sauti ya shangwe isiwe ndani yake.
\s5
\v 8 Na wailani siku hiyo, hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathani.
\v 9 Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza. Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate; wala makope ya mapambazuko isiyaone,
\v 10 kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu, na kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.
\s5
\v 11 Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi? Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?
\v 12 kwanini magoti yake yalinipokea? Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?
\s5
\v 13 Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimya kimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko
\v 14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia, ambao walijijengea makaburi ambayo sasa ni magofu.
\s5
\v 15 Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha.
\v 16 Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.
\s5
\v 17 Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.
\v 18 Huko wafungwa kwa pamoja hupata amani; hawaisikii sauti ya msimamizi wa watumwa.
\v 19 Wote wadogo na watu maarufu wako huko; mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.
\s5
\v 20 Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai,
\v 21 ambao hutamani mauti lakini hawapati; ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika?
\v 22 Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi?
\s5
\v 23 Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa?
\v 24 Kwa kuwa kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji.
\s5
\v 25 Maana jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia.
\v 26 Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko; badala yake huja taabu."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
\v 2 Kama mtu yeyote akijaribu kuzungumza na wewe, je utakosa ustahimilivu? Lakini ni nani anaweza kujizuia asizungumze?
\v 3 Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
\s5
\v 4 Maneno yako yamemsaidia yeye mwanamme aliyekuwa anaanguka; wewe umeyaimarisha magoti dhaifu.
\v 5 Lakini sasa matatizo yamekuja kwako, na wewe umechoka; yanakugusa wewe, na wewe umetatizika.
\v 6 Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?
\s5
\v 7 Tafakari juu ya hili, tafadhari: ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa? Au ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali?
\v 8 Kutokana na vile nilivyoona, wale walimao uovu na kupanda taabu huvuna hayo.
\v 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea.
\s5
\v 10 Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.
\v 11 Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
\s5
\v 12 Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo.
\v 13 Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu..
\s5
\v 14 Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika.
\v 15 Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama.
\s5
\v 16 Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
\v 17 "Je binadamu anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu? Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko muumba wake?
\s5
\v 18 Tazama, kama Mungu hawaamini watumishi wake; kama hulaumu upumbavu wa malaika zake,
\v 19 je si zaidi sana ukweli huu kwa wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi, wale waliopondwa mbele ya nondo?
\s5
\v 20 Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa; wameangamia milele wala bila yeyote kuwatambua.
\v 21 Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Wanakufa; wanakufa bila hekima.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ita sasa; je kuna yeyote ambaye atakujibu? Utamrudia yupi katika watakatifu hao?
\v 2 Kwa kuwa hasira huua mtu mpumbavu; wivu huua mjinga.
\v 3 Nimemuona mtu mpumbavu akishika mzizi, lakini ghafla niliyalaani makazi yake.
\s5
\v 4 Watoto wake wako mbali na uzima; wameangamia langoni mwa mji. Hakuna yeyote atakaye waponya.
\v 5 Mwenye njaa hula mavuno yao; hata huyachukua katikati ya miiba. Wenye kiu huzihemea mali zao.
\s5
\v 6 Kwa kuwa magumu hayatoki udongoni; wala taabu haichipuki katika nchi.
\v 7 Badala yake, wanadamu huzaliwa kwaajili ya taabu, kama tu cheche za moto zirukavyo juu.
\s5
\v 8 Lakini kwa mimi, ningemrudia Mungu mwenyewe; kwake ningeaminisha kusudi langu -
\v 9 yeye afanyae makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu.
\v 10 Hutoa mvua juu ya nchi, na huyapeleka maji mashambani.
\s5
\v 11 Hufanya haya kwaajili ya kuwainua juu hao walio chini; huwapandisha sehemu salama hao waombolezao.
\v 12 Yeye huharibu mipango ya watu wenye hila, ili mikono yao isipate mafanikio.
\v 13 Yeye huwanasa watu wenye hekima katika matendo ya hila zao wenyewe; mipango ya watu waliogeuzwa huharibika haraka.
\s5
\v 14 Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, na hupapasa mchana kama vile ni usiku.
\v 15 Lakini yeye huokoa maskini kwa upanga wa vinywa vyao na mhitaji kwa mkono wa mtu mwenye nguvu.
\v 16 Hivyo mtu maskini ana matumaini, na udhalimu hufumba kinywa chake mwenyewe.
\s5
\v 17 Tazama, amebarikiwa mtu ambaye hutiwa adabu na Mungu; kwa sababu hiyo, usidharau uongozi wa Mwenyezi.
\v 18 Kwa kuwa yeye hujeruhi na kisha huuguza; yeye hutia jeraha na kisha mikono yake huponya.
\v 19 Yeye atakuokoa na mateso sita; kweli, katika mateso saba, hakuna uovu utakao kugusa.
\s5
\v 20 Wakati wa njaa atakukomboa na kifo, na kwa uwezo wa upanga wakati wa vita.
\v 21 Wewe utafichwa na mateso ya ulimi; na usitishike na uharibifu utakapokuja.
\v 22 Wewe utaufurahia uharibifu na njaa, na hutatishika na wanyama wakali wa nchi.
\s5
\v 23 Kwa kuwa wewe utakuwa na mapatano na mawe ya shambani mwako, na wanyama wa mwituni watakuwa na amani na wewe.
\v 24 Wewe utajua kwamba hema lako lina usalama; utatembelea zizi la kondoo wako na hutakosa kitu chochote.
\v 25 Pia utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, na vizazi vyako vitakuwa kama nyasi ardhini.
\s5
\v 26 Wewe utafika kaburini kwako mwenye umri kamili, kama vile rundo la mashuke ya nafaka liendavyo juu wakati wake.
\v 27 Tazama, tumelipeleleza jambo hili; ndivyo lilivyo; lisikie, na ulifahamu kwa ajili yako mwenyewe."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Oo, laiti maumivu yangu makubwa yangepimwa; laiti misiba yangu yote mikubwa ingewekwa kwenye mizani!
\v 3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa baharini. Kwa sababu hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
\s5
\v 4 Kwa kuwa mishale ya Mwenyezi ipo ndani yangu, moyo wangu umelewa sumu; Vitisho vya Mungu vimejipanga vyenyewe dhidi yangu.
\v 5 Je punda mwitu hulia akiwa na malisho? Au ng'ombe huwa dhaifu wakati wa njaa ambapo anachakula?
\v 6 Je inawezekana kitu kisicho na ladha kulika bila chumvi? Au kuna radha yoyote katika ute mweupe wa yai?
\s5
\v 7 Nakataa kuvigusa; kwangu mimi vinafanana na chakula kichukizacho.
\v 8 Oo, kama nigeweza kupata haja yangu; oo, kama Mungu angeridhia jambo nilitamanilo sana:
\v 9 kama Mungu ingempendeza kuniangamiza mara moja, kwamba angeulegeza mkono wake na kuyakatilia mbali maisha yangu!
\s5
\v 10 Hii ingeweza kuwa faraja yangu hata sasa - hata kama nafurahia sana maumivu yasiyopungua: kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
\v 11 Nguvu yangu ni ipi, hata nijaribu kusubiri? Mwisho wangu ni upi, utakao refusha maisha yangu?
\s5
\v 12 Je nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu umeumbwa kwa shaba nyeusi?
\v 13 Je si kweli kwamba sina msaada ndani yangu, na kwamba hekima imeondolewa mbali nami?
\s5
\v 14 Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake; hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi.
\v 15 Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani, mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu,
\v 16 ambayo imekuwa mieusi kwa sababu ya barafu juu yake, na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake.
\v 17 Wakati zikiyeyuka, hutoweka; kukiwa na joto, hutoweka mahali hapo.
\s5
\v 18 Misafara ambayo husafiri kwa njia yao hugeuka na maji; huzurura jangwani na kisha hupotea.
\v 19 Misafara kutoka Tema huitazama, wakati majeshi ya Sheba huitarajia.
\v 20 Wamevunjika moyo kwa sababu walitumaini kupata maji. Wakaenda huko, lakini walidanganywa.
\s5
\v 21 Kwa sasa ninyi rafiki si kitu kwangu; mmeona hali yangu ya kutisha nanyi mwaogopa.
\v 22 Je nilisema kwenu, 'Nipeni kitu furani?' Au, 'nitoleeni zawadi katika mali zenu?'
\v 23 Au, 'Niokoeni toka mkononi mwa mtesi wangu?' Au, 'Nitoleeni fidia kwa watesi wangu?'
\s5
\v 24 Nifundishe, nami nitaishika amani yangu; nifanye nifahamu wapi nilipokosea.
\v 25 Jinsi gani maneno ya kweli yanavyo umiza! Lakini hoja zenu, jee hasa zimenionya nini mimi?
\s5
\v 26 Je mnapanga kuyakemea maneno yangu, mnayachukulia maneno ya mtu mwenye kukata tamaa sawa na upepo?
\v 27 Hasa, mna piga kura kwa ajili ya yatima, na kupatana bei juu ya rafiki yenu kama bidhaa.
\s5
\v 28 Sasa, kwa sababu hiyo, tafadhari nitazame, kwa hakika sitasema uongo usoni penu.
\v 29 Rudini, nawasihi; lisiwepo neno la uonevu na nyinyi; Hasa, rudini, sababu zangu ni za haki.
\v 30 Je mna uovu ulimini mwangu? Je kinywa changu hakiwezi kungundua madhara?
\s5
\c 7
\p
\v 1 Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi? Je siku zake si kama siku za mwajiriwa?
\v 2 Kama mtumwa atamaniye sana kivuli cha jioni, kama mwajiriwa atafutaye ujira wake -
\v 3 hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku.
\s5
\v 4 Hapo nilalapo chini, najiuliza mwenyewe, 'Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?' Nimejawa na kujitupa huku na huko hadi mwanzo wa siku.
\v 5 Mwili wangu umevikwa minyoo na madonda yenye vumbi; maumivu katika ngozi yangu yamekuwa magumu na kisha hutoweka na huendelea tena.
\s5
\v 6 Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia; zinapita bila tumaini.
\v 7 Mungu, anakumbuka kwamba maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona mema tena.
\s5
\v 8 Jicho lake Mungu, huyo anionaye mimi, halitaniangalia tena; Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako.
\v 9 kama vile wingu liishavyo na kutoweka, hivyo wale waendao sheoli hawatarudi tena kabisa.
\v 10 Yeye hatarudi tena nyumbani kwake, wala mahali pake hapatamtambua tena.
\s5
\v 11 Kwa sababu hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitasema juu ya maumivu makubwa ya roho yangu; Nitanung'unika juu ya uchungu wa nafsi yangu.
\v 12 Je mimi ni bahari au kiumbe cha kutisha baharini hata ukaweka mlinzi juu yangu?
\s5
\v 13 Hapo nisemapo, 'kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu,'
\v 14 halafu unitishapo kwa ndoto na kunitisha kwa maono,
\v 15 ili nichague kunyongwa na kufa kuliko kulinda mifupa yangu hii.
\s5
\v 16 Ninayachukia kabisa maisha yangu; sitamani siku zote kuwa hai; usinisumbue maana siku zangu hazifai.
\v 17 Je mtu ni nini hata ukatia bidii kwake, na ukaweka akili yako kwake,
\v 18 na kumwangalia kila asubuhi, na kumjaribu kila mara?
\s5
\v 19 Je itachukuwa muda gani kabla hujaacha kuniangalia, wala kunisumbua muda wa kutosha kwaajili ya kumeza mate yangu?
\v 20 Hata kama nimefanya dhambi, itakusaidia nini, wewe ulindaye wanadamu? Kwa nini umenifanya shabaha yako, kiasi kwamba nimekuwa mzigo kwako?
\s5
\v 21 Kwa nini hunisamehi makosa yangu na kuniondolea uovu wangu? kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; na wewe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwako."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Kisha Bildadi huyo Mshuhi akajibu na kusema,
\v 2 "hata lini wewe utasema mambo haya? Kwa muda gani maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo wenye nguvu?
\v 3 Je Mungu hupotosha hukumu? Je Mwenyezi hupotosha haki?
\s5
\v 4 Watoto wako wametenda dhambi dhidi yake; tunalifahamu hili, kwa kuwa amewatia mkononi kwa makosa yao.
\v 5 Lakini wewe unaonaje ukimtafuta Mungu kwa bidii na kufikisha haja yako kwa huyo Mwenyezi.
\s5
\v 6 Ukiwa wewe ni msafi na mkamilifu, hakika angeamka mwenyewe kwa niaba yako na kukurudisha kwenye makazi ya haki yako.
\v 7 Japokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, hata hivyo hali yako ya mwisho itaongezeka sana.
\s5
\v 8 Tafadhari uwaulize vizazi vya zamani, na utie bidii katika hayo mababu zetu waliyojifunza.
\v 9 (Sisi ni wa jana tu na hatujui chochote kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli).
\v 10 Je hawatakufunza wao na kukuambia? Je hawatatamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
\s5
\v 11 Je hayo mafunjo yaota pasipo matope? Je mafunjo yaota pasipo maji?
\v 12 Wakati yakiwa bado ya kijani na hayajakatwa, hunyauka kabla ya mmea mwingine.
\s5
\v 13 Hivyo pia njia ya wote wamsahauo Mungu, na matumaini ya asiyeamini Mungu yatatoweka.
\v 14 Ujasiri wake utavunjika, na matumaini yake ni dhaifu kama utando wa buibui.
\v 15 Ataitegemea nyumba yake, lakini haitamsaidia; atashikamana nayo, lakini isidumu.
\s5
\v 16 Yeye huwa mti mbichi chini ya jua, na machipukizi yake huenea katika bustani yake yote.
\v 17 Mizizi yake hujifunga funga kwenye rundo la mawe; huangalia mahali pazuri katikati ya mawe;
\v 18 Lakini mtu huyu aking'olewa mahali pake, kisha mahali pale patamkana, na kusema, 'mimi sikukuona.'
\s5
\v 19 Tazama, hii ni "furaha" ya mtu mwenye tabia hiyo; mimea mingine itachipuka toka katika udongo ule ule mahali pake.
\v 20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu asiye na kosa; wala hatawathibitisha watendao uovu.
\s5
\v 21 Yeye atakijaza kinywa chako na kicheko, midomo yako na shangwe.
\v 22 Wale ambao wanakuchukia wewe watavishwa aibu; nayo hema yake mwovu haitakuwepo tena.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
\v 3 Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
\s5
\v 4 Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
\v 5 ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
\v 6 ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
\s5
\v 7 Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
\v 8 ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
\v 9 ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
\s5
\v 10 Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
\v 11 Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
\v 12 Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
\s5
\v 13 Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
\v 14 Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
\v 15 Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
\s5
\v 16 Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
\v 17 kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
\v 18 Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.
\s5
\v 19 Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
\v 20 Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
\s5
\v 21 Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
\v 22 Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
\v 23 Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
\v 24 Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
\s5
\v 25 Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
\v 26 Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
\s5
\v 27 Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
\v 28 Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
\v 29 Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
\s5
\v 30 Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
\v 31 Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
\s5
\v 32 Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
\v 33 Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
\s5
\v 34 Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
\v 35 Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nimechoka na maisha yangu; Nitanena wazi manung'uniko yangu; nitasema kwa uchungu wa roho yangu.
\v 2 Nitamwambia Mungu, 'Usinihukumie makosa; nionyeshe sababu za wewe kunilaumu mimi. Je
\v 3 ni vizuri kwako wewe kunionea mimi, kudharau kazi ya mikono yako wakati unafurahia juu ya mipango ya waovu?
\s5
\v 4 Je wewe una macho ya kimwili? Je wewe unaona kama mtu aonavyo?
\v 5 Je siku zako ni kama siku za wanadamu au miaka yako ni kama miaka ya watu,
\v 6 hata ukauliza habari za uovu wangu na kuitafuta dhambi yangu,
\v 7 ingawa wewe wafahamu mimi sina kosa na hapana mwingine awezaye kuniokoa mimi na mkono wako?
\s5
\v 8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga kwa wakati mmoja nawe kunizunguka, hata hivyo unaniangamiza.
\v 9 Kumbuka, nakuomba, ulivyonifinyanga kama vile udongo; je utanirudisha mavumbini tena?
\s5
\v 10 Je wewe hukunimimina kama maziwa na kunigandisha mfano wa jibini?
\v 11 Umenivika ngozi na nyama na kuniunganisha pamoja kwa mifupa na misuli..
\s5
\v 12 Wewe umenizawadia mimi uhai na ahadi ya upendeleo na usaidizi wako umeilinda roho yangu.
\v 13 Hata hivyo mambo haya uliyaficha moyoni mwako - nafahamu kwamba hivi ndivyo ufikirivyo:
\v 14 kuwa kama nimefanya dhambi, wewe utaizingatia; hutaniachilia na uovu wangu.
\s5
\v 15 Kama mimi ni muovu, ole wangu; hata kama ni mwenye haki, sitaweza kuinua kichwa changu, kwa kuwa nimejaa aibu na kuyaangalia mateso yangu.
\v 16 Kama kichwa changu kikijiinua chenyewe, waniwinda kama simba; tena wajionyesha mwenyewe kuwa ni mwenye nguvu kwangu.
\s5
\v 17 Wewe unaleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira zako dhidi yangu; wanishambulia na majeshi mapya.
\s5
\v 18 Kwa nini, basi, ulinitoa tumboni? Natamani ningekata roho na ili jicho lolote lisinione.
\v 19 Ningelikuwa kama asiyekuwepo; ningelichukuliwa kutoka tumboni mpaka kaburini.
\s5
\v 20 Je si siku zangu pekee ni chache? Acha basi, usinisumbue, ili kwamba nipate kupumzika kidogo
\v 21 kabla sijaenda huko ambako sitarudi, kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti,
\v 22 ni nchi ya giza kama usiku wa manane, nchi ya kivuli cha mauti, isiyokuwa na mpangilio, ambayo nuru yake ni kama usiku wa manane.'"
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ndipo Sofari Mnaamathi alijibu na kusema,
\v 2 " Huo wingi wa maneno haupaswi kujibiwa? Mtu huyu, aliyejaa maneno mengi awe wa kuaminiwa?
\v 3 Kujivuna kwako kunapaswa kuwafanya wengine wabaki wamenyamaza? Wakati unapoyadhihaki mafundisho yetu, hakuna awaye yote atakayekufanya wewe ujisikie mwenye aibu?
\s5
\v 4 Kwa kuwa wewe unasema kwa Mungu, 'Imani yangu ni safi, Mimi sina waa lolote machoni pako.'
\v 5 Lakini, laiti, Mungu huyo angesema na kufungua midomo yake dhidi yako;
\v 6 hivyo angekuonyesha wewe siri za hekima! Kwa kuwa yeye ni mkuu katika ufahamu. Tena tambua huyo Mungu anataka kutoka kwako kidogo kuliko uovu wako unavyostahili.
\s5
\v 7 Je, wewe unaweza kumfahamu Mungu kwa kumtafuta yeye? Unaweza kumtambua aliye mkuu kwa ukamilifu?
\v 8 Upeo uko juu kama mbingu; unaweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kirefu kuliko kuzimu; waweza kufahamu nini wewe?
\v 9 Vipimo vyake ni virefu kuliko nchi, na vipana kuliko bahari.
\s5
\v 10 kama yeye akipita kati na kumyamazisha mtu yeyote, kama yeye akimwita mtu yeyote hukumuni, tena ni nani anayeweza kumzuia yeye?
\v 11 Kwa maana anawajua watu waongo; wakati anapoona uovu, hawezi yeye kuukumbuka?
\v 12 Lakini watu wapumbavu hawana ufahamu; wataupata wakati punda mwitu atakapozaa mtu.
\s5
\v 13 Lakini ikiwa umeuelekeza moyo wako kwa haki na umeunyosha mkono wako karibu na Mungu;
\v 14 ikiwa huo uovu ulikuwa katika mikono yako, lakini hivyo tena unauweka mbali nawe, na haukuruhusu kutokuwa mwenye haki kukaa hemani mwako.
\s5
\v 15 Ndipo kwa hakika ungeinua juu uso wako bila ishara ya aibu; Ni dhahiri, ungethibitika na usingeogopa.
\v 16 Wewe ungesahau mateso yako; ungeyakumbuka hayo tu kama maji ambayo yametiririka mbali.
\v 17 Maisha yako yangekuwa angavu kuliko adhuhuri; japokuwa kulikuwa na giza, litakuwa kama asubuhi.
\s5
\v 18 Ungekuwa salama kwa sababu kuna tumaini; ni dhahiri, wewe utapata usalama juu yako na utachukua pumziko lako katika usalama.
\v 19 Pia ungelala chini katika pumziko, na hakuna ambaye angekufanya wewe uogope; hakika wengi wangetafuta upendeleo wako.
\s5
\v 20 Lakini macho ya watu waovu yatashindwa; hawatakuwa na njia ya kukimbia; tumaini lao la pekee litakuwa pumzi yao ya mwisho ya uhai.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo.
\v 3 Lakini nina ufahamu kama vile ninyi; Mimi siyo duni kwenu. Ni dhhiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi?
\s5
\v 4 Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani-Mimi, ni mmoja aliyemwita Mungu na ambaye alijibiwa na yeye! Mimi, ni mwenye haki na mtu asiyekuwa na hatia-Mimi sasa nimekuwa kitu cha kuchekwa.
\v 5 Katika mawazo yake mtu fulani aliye katika kufurahi, kuna kudharau kwa mashaka; hufikiri katika njia ambayo huleta mambo mabaya zaidi kwa wale ambao miguu yao inateleza.
\v 6 Hema za wezi hufanikiwa, na wale ambao humkasirisha Mungu huhisi salama; mikono yao wenyewe ni miungu wao.
\s5
\v 7 Lakini sasa waulize hao wanyama wa mwituni, na watakufundisha wewe; waulize ndege wa angani, na watakuambia wewe.
\v 8 Au iambie ardhi, na itakufundisha wewe; samaki wa baharini watakutangazia wewe.
\s5
\v 9 Ni myama yupi miongoni mwa hawa asiyefahamu kuwa mkono wa Yahwe umetenda haya?
\v 10 Katika mkono wake mna uzima wa kila kiumbe hai na pumzi ya wanadamu wote.
\s5
\v 11 Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile kaakaa lionjavyo chakula chake?
\v 12 Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.
\s5
\v 13 Pamoja na Mungu mna hekima na ukuu; yeye anayo mashauri na ufahamu.
\v 14 Tazama, yeye huangusha chini, na haiwezekani kujengwa tena; kama yeye akimtia gerezani mtu yeyote, hakutakuwa tena kufunguliwa.
\v 15 Tazama, kama yeye akiyazuia maji, yanakauka; na kama akiyaachilia nje yanaitaabisha ardhi.
\s5
\v 16 Pamoja na yeye mna nguvu na hekima; watu ambao wamedanganywa na mdanganyi wote pamoja wako katika nguvu zake.
\v 17 Yeye huwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu katika huzuni; huwarudisha hakimu katika upumbavu.
\v 18 Yeye Huondoa minyororo ya mamlaka kutoka kwa wafalme; yeye hufunika viuno vyao kwa nguo.
\s5
\v 19 Yeye huwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu na kuwapindua watu wakuu.
\v 20 Yeye huondoa hotuba ya wale waliokuwa wameaminiwa na huondoa mbali ufahamu wa wazee.
\v 21 Yeye humwaga aibu juu ya binti za wafalme na hufungua mishipi ya watu wenye nguvu.
\s5
\v 22 Yeye huweka wazi vitu vya kina kutoka katika giza na kuvileta nje kumuika vivuli mahali ambapa watu waliokufa wapo.
\v 23 Yeye huyafanya mataifa kuwa na nguvu, na pia huyaharibu; Yeye pia huyakuza mataifa, na pia yeye huyaongoza mbali kama wafungwa.
\s5
\v 24 Yeye huondoa mbali ufahamu kutoka kwa viongozi wa watu wa nchi; huwafanya wao kutangatanga msituni mahali pasipo na njia.
\v 25 Wao wanapapasa katika giza bila kuwa na mwanga; yeye huwafanya wao kuweweseka kama mtu mlevi.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Tazama, jicho langu limeyaona haya yote; sikio langu limeyasikia na kuyaelewa hayo.
\v 2 Kile mnachokifahamu, ndicho hicho mimi pia ninachokifahamu; Mimi siyo duni kwenu ninyi.
\s5
\v 3 Hata hivyo, Mimi ningeweza kuzungumza na mwenye nguvu; Mimi natamani kusemezana na Mungu.
\v 4 Lakini ninyi mnauficha ukweli kwa uongo; ninyi nyote ni tabibu msiokuwa na thamani.
\v 5 Laiti, kwamba kwa pamoja mngeshikilia amani yenu! Hilo lingekuwa hekima yenu ninyi.
\s5
\v 6 Sikia sasa kuhoji kwangu; Sikiliza kusihi kwa midomo yangu mwenyewe.
\v 7 Ninyi mtazungumza visivyo haki kwa ajili ya Mungu, na ninyi mtazungumza udanganyifu kwa yeye? Ni kweli ninyi mngeonyesha ukarimu kwa yeye?
\v 8 Ni kweli ninyi mngetetea katika mahakama kama mawakili wa Mungu?
\s5
\v 9 Je, kweli ingekuwa vizuri kwenu wakati yeye akiwatafuta ninyi? Mngeweza ninyi kumdanganya yeye kama mlivyoweza kuwadanganya watu?
\v 10 Yeye kwa hakika angewathibitisha upya ninyi ikiwa katika siri ninyi mmeonyesha kutokukamilika.
\s5
\v 11 Je, ukuu wake usingewafanya ninyi muogope? Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?
\v 12 Hadithi zenu za misemo ya kukariri, ni mithali zimetengenezwa kwa majivu; utetezi wenu ni utetezi uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.
\s5
\v 13 Shikilieni amani yenu, mniache peke yangu, ili ya kwamba nipate kusema, acheni yaje yale yanayoweza kuja kwangu.
\v 14 Nitaichukua nyama yangu mwenywewe katika meno yangu; Nitayachukua maisha yangu katika mikono yangu.
\v 15 Tazama, ikiwa ataniua mimi, sitakuwa na tumaini lililobakia; hata hivyo, nitazitetea njia zangu mbele zake yeye.
\s5
\v 16 Hiki kitakuwa sababu ya kutohesabiwa hatia, kwamba mimi sikuja mbele zake kama mtu asiyemcha Mungu.
\v 17 Mungu, sikiliza kwa makini kuzungumza kwangu; ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.
\s5
\v 18 Tazama sasa, Nimeuweka utetezi wangu katika mpangilio, Mimi ninafahamu kwamba mimi sina hatia.
\v 19 Ni nani anayeweza kushindana na mimi katika mahakama? Ikiwa mlikuja kufanya hivyo, na kama mimi nilithibitishwa kukosea, ndipo ningekuwa kimya na kuyatoa maisha yangu.
\s5
\v 20 Mungu, fanya mambo mawili kwa ajili yangu, na tena Mimi sitajificha kutoka katika uso wako.
\v 21 Ondoa kutoka kwangu mkono wako unaotesa, na usiache utisho wako unifanye mimi kuogopa.
\v 22 Ndipo niite mimi, na mimi nitakujibu; au uniache mimi niseme na wewe na wewe unijibu mimi.
\s5
\v 23 Je, maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
\v 24 Kwa nini unaficha uso wako kutoka kwangu mimi na kunitendea mimi kama adui yako?
\v 25 Je, wewe utalitesa jani linalopeperushwa? Je, utaendelea kulifuatilia bua kavu?
\s5
\v 26 Kwa maana wew unaandika chini vitu vichungu dhidi yangu mimi; wewe unanifanya mimi kurithi uovu wa ujana wangu.
\v 27 Wewe pia unaiweka miguu yangu katika nguo nyembamba; wewe waangalia njia zangu zote; wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.
\v 28 japokuwa mimi ni kama kitu kilichooza ambacho hutupwa mbali, kama vazi lile ambalo nondo wamelila.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, huishi siku chache tu na amejaa mahangaiko.
\v 2 Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu.
\v 3 Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi?
\s5
\v 4 Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote.
\v 5 Siku za mwanadamu zimeamriwa. Idadi ya miezi yake unayo wewe; umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka.
\v 6 Tazama mbali kutoka kwake kwamba yeye aweze kupumzika, ili kwamba aweze kufurahia siku yake kama mtu aliyekodishwa kama yeye anaweza kufanya hivyo.
\s5
\v 7 Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti; kama ukikatwa chini, unaweza kuchipua tena, hivyo chipukizi lake halitapotea.
\v 8 Japokuwa mizizi yake inakua na kuzeeka katika ardhi, na shina lake kufa katika udongo,
\v 9 hata kama bado lina harufu ya maji pekee, litachipua tena na kutoa nje matawi kama mche.
\s5
\v 10 Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye?
\v 11 Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka,
\v 12 vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.
\s5
\v 13 Laiti, kwamba ungenificha mimi mbali katika kuzimu mbali kutoka katika mahangaiko, na kwamba ungenitunza mimi katika siri hadi hasira yake imalizike, kwamba ungeniwekea mimi muda maalumu wa kukaa huko na kisha kuniita mimi katika fahamu!
\v 14 Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena? Ikiwa hivyo, ningependa kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja.
\s5
\v 15 Wewe ungeita, na mimi ningekujibu wewe. Wewe ungekuwa na shauku ya kazi ya mikono yako.
\v 16 Wewe ungehesabu na kutunza nyayo zangu; Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu.
\v 17 Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba; wewe ungeufunga uovu wangu.
\s5
\v 18 Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake;
\v 19 maji yaliyokuwa chini ya mawe; kufurika kwake huondoa mbali mavumbi ya nchi. Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu.
\s5
\v 20 Ninyi daima humshinda yeye, na yeye hupita mbali; Ninyi mnabadilisha uso wake na kumtuma yeye mbali kufa.
\v 21 Kama watoto wake wa kiume ni wa kuheshimiwa, yeye, hatambui hicho; na kama wakishushwa chini, yeye haoni hicho.
\v 22 Yeye hujisikia tu maumivu ya mwili wake mwenyewe, na hujiombolezea yeye mwenyewe.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ndipo Elifazi Mtemani alijibu na kusema,
\v 2 Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?
\v 3 Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema?
\s5
\v 4 Dhahiri, wewe wafifisha heshima ya Mungu; Wewe wazuia heshima kwa yeye,
\v 5 kwa maana uovu wako hufundisha midomo yako; Wewe wachagua kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila.
\v 6 Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu; hakika, midomo yako mwenyewe hushuhudia dhidi yako wewe.
\s5
\v 7 Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa? Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo?
\v 8 Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu? Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe?
\v 9 Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui? Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi?
\s5
\v 10 Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee zaidi kuliko baba yako.
\v 11 Je, faraja ya Mungu ni ndogo sana kwako, maneno ambayo ni ya upole dhidi yako wewe?
\s5
\v 12 Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali? Kwa nini macho yako yananga'ra,
\v 13 ili ya kwamba kuirejesha roho yako kwa Mungu na kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako?
\v 14 Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi? Yeye mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki?
\s5
\v 15 Tazama, Mungu haweki tumaini lake hata kwa mmoja wake aliye mtakatifu; Hakika, mbingu haziko safi machoni pake yeye;
\v 16 jinsi gani asivyo safi ni mmoja aliye mbaya na mla rushwa, mtu ambaye hunywa uovu kama maji!
\s5
\v 17 Mimi nitakuonyesha wewe; Nisikilize mimi; Mimi nitakutangazia wewe vitu ambavyo nimeviona,
\v 18 vitu ambavyo watu wenye hekima wamepita chini yake kutoka kwa baba zao, vile vitu ambavyo mababu zao hawakuvificha.
\s5
\v 19 Hawa walikuwa mababu zao, ambao kwao pekee nchi walipewa, na miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita.
\v 20 Mtu mwovu hupitia katika maumivu siku zake zote, idadi ya miaka iliyowekwa juu kwa mtesaji kuteseka.
\v 21 Sauti ya vitisho katika masikio yake; pindi yeye yuko katika kufanikiwa, mharibu atakuja juu yake yeye.
\s5
\v 22 Yeye hafikiri kwamba yeye atarudi kutoka katika giza; Upanga humngojea yeye.
\v 23 Yeye huenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya mkate, akisema, 'Kiko wapi? ' Yeye anatambua kuwa siku ya giza iko mkononi.
\v 24 Dhiki na mateso makali humfanya aogope; wao hushinda dhidi yake yeye, kama mfalme tayari kwa vita.
\s5
\v 25 Kwa sababu yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu na ameishi kwa kiburi dhidi ya aliye mkuu,
\v 26 huyu mtu mwovu hukimbia kwa Mungu na shingo ngumu, kwa vifundo vikubwa vya ngao.
\s5
\v 27 Hii ni kweli, hata ingawa yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake,
\v 28 na ameishi katika miji yenye ukiwa; katika nyumba ambazo hakuna mwanadamu anayeishi humo sasa na ambazo zilikuwa tayari kuwa magofu.
\s5
\v 29 Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu; hata kivuli chake hakitadumu katika nchi.
\v 30 Yeye hatatoka nje ya giza; mwali wa moto utakausha matawi yake; katika pumzi ya kinywa cha Mungu yeye ataenda zake.
\s5
\v 31 Mwacheni yeye asitumaini katika vitu visivyofanya kazi, akijidanganya yeye mwenyewe; maana upuuzi utakuwa mshahara wake yeye.
\v 32 Itatokea kabla ya wakati wake yeye atapaswa kufa; tawi lake halitakuwa kijani.
\v 33 Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama mzabibu; yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni.
\s5
\v 34 Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu utakuwa tasa; moto utateketeza hema za rushwa.
\v 35 Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Mimi nimevisikia vitu hivyo vingi; ninyi nyote ni wafariji wenye kuhuzunisha.
\v 3 Maneno yenye upuuzi daima yanaweza kuwa na mwisho? Nini kimeharibika kwenu kwamba mnajibu kama hivi?
\s5
\v 4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi mnavyofanya, kama ninyi mngekuwa katika nafasi yangu; Mimi ningekusanya na kuunganisha maneno pamoja dhidi yenu na kutikisa kichwa changu kwenu ninyi katika dhihaka.
\v 5 Laiti, jinsi gani Mimi ningewatia moyo na midomo yangu! Jinsi gani faraja kutoka midomo yangu ingenga'risha huzuni yenu!
\s5
\v 6 Ikiwa Mimi ninazungumza, kuomboleza kwangu hakujasikilizwa; Ikiwa nikiendelea katika kuzungumza, jinsi gani mimi ninaidiwa?
\v 7 Lakini sasa, Mungu,
\v 8 wewe umenifanya mimi kuchoka; wewe umeifanya familia yangu yote kuwa ukiwa. Wewe umenifanya mimi kukauka, ambayo yenyewe ni ushuhuda dhidi yangu mimi; kukonda kwa mwili wangu huinuka dhidi yangu, na kunashuhudia dhidi ya macho yangu.
\s5
\v 9 Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande.
\v 10 Watu wameachama na midomo iliyowazi juu yangu; wamenipiga mimi katika shavu kwa kunitukana; wamekusanyika pamoja kinyume changu mimi.
\s5
\v 11 Mungu amenikabidhi mimi juu ya watu wasio mcha Mungu, na kunitupa mimi ndani ya mikono ya watu waovu.
\v 12 Mimi nilikuwa katika wepesi, na yeye amenivunjavunja mimi vipande. Hakika, amenichukua mimi kwa shingo na ameniponda mimi vipande vipande; yeye pia ameniweka mimi juu kama shabaha yake.
\s5
\v 13 Wapiga upinde wake wote wamenizunguka mimi; Mungu huzikata vipande vipande figo zangu, na haniokoi mimi; yeye humwaga nje nyongo yangu juu ya ardhi.
\v 14 yeye hukanyaga kanyaga kupitia ukuta wangu tena na tena; yeye hukimbia juu yangu mimi kama shujaa.
\s5
\v 15 nguo ya magunia juu ya ngozi yangu; Mimi nimeisukuma kwa nguvu pembe yangu ndani ya ardhi.
\v 16 Uso wangu ni mwekundu na kuomboleza; juu ya ngozi inayofunika macho kuna kivuli cha mauti
\v 17 ingawa hakuna dhuluma katika mikono yangu, na kuomba kwangu ni safi.
\s5
\v 18 Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi; acha kulia kwangu kuwe hakuna mahali pa kupumzika.
\v 19 Hata sasa, tazama, ushuhuda wangu uko mbinguni; yeye ambaye ashuhudiaye kwa ajili yangu mimi yuko juu.
\s5
\v 20 Rafiki zangu wananicheka kwa dharau, lakini jicho langu linamwaga machozi kwa Mungu.
\v 21 Mimi ninaomba ule ushuhuda ulioko mbinguni kumtetea mtu huyu na Mungu kama mwanadamu afanyavyo na jirani yake.
\v 22 Kwa maana wakati miaka michache itakapokuwa imepita, Mimi nitakwenda mahali ambapo mimi sitaweza kurudi.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Roho yangu imemezwa, na siku zangu zimekwisha; kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi.
\v 2 Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami; ni lazima daima jicho langu litazame kukasirisha kwao.
\v 3 Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe; nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi?
\s5
\v 4 Kwa kuwa wewe Mungu umemeitunza mioyo yao kutoka katika ufahamu; kwa hiyo, wewe hautawaheshimisha wao juu yangu mimi.
\v 5 Yeye ambaye huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
\s5
\v 6 Lakini amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu; wao wananitemea mate katika uso wangu mimi.
\v 7 Jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni; sehemu zangu zote za mwili ni nyembamba kama vivuli.
\v 8 Watu wanyoofu watapendezwa na hiki; mtu asiye na hatia atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi ya watu wasiomcha Mungu.
\s5
\v 9 Mtu mwenye haki ataendelea katika njia yake; yeye ambaye ana mikono iliyo safi ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi.
\v 10 Lakini kama ilivyo kwenu ninyi nyote, njooni sasa; Mimi sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu ninyi.
\s5
\v 11 Siku zangu zimepita; mipango yangu imenyamazishwa na hivyo ni matumaini ya moyo wangu.
\v 12 Watu hawa, wenye kukejeli, badili usiku kuwa mchana; mchana uko karibu kuwa giza.
\s5
\v 13 Tangu mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu; tangu Mimi nimetandaza kiti changu katika giza;
\v 14 tangu Mimi nimesema na shimo 'Wewe ni baba yangu,' na kwa funza, 'Wewe ni mama yangu au dada yangu;
\v 15 liko wapi tena tumaini langu? Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote?
\v 16 Tumaini litakwenda pamoja na mimi katika milango ya Kuzimu wakati sisi tutakapokwenda katika mavumbi?
\s5
\c 18
\p
\v 1 Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema, "
\v 2 Je, lini utaacha kusema kwako? Fikiri, na baadaye tutazungumza.
\s5
\v 3 Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama mwitu; kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako?
\v 4 Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako, nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?
\s5
\v 5 Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra.
\v 6 Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa nje.
\s5
\v 7 Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi; mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini.
\v 8 Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko.
\s5
\v 9 Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake.
\v 10 Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia.
\v 11 Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote; wao watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake.
\s5
\v 12 Utajiri wake utageuka kuwa njaa, na majanga yatakuwa tayari upande wake.
\v 13 Sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa; Hakika, mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye.
\s5
\v 14 Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake na hakuweza kutembea kwenda kwa mfalme mwenye utisho.
\v 15 Watu ambao siyo wa kwake wataishi kwenye hema yake baada ya kuona ule moto mesambaa ndani ya nyumba yake yeye.
\s5
\v 16 Mizizi yake itanyauka chini yake; juu tawi lake yeye litakatwa.
\v 17 Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa.
\s5
\v 18 Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu.
\v 19 Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa.
\v 20 Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho.
\s5
\v 21 Hakika hizo ni nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 lini mtanifanya mimi kuteseka na kunivunja vunja mimi vipande vipnde kwa maneno?
\s5
\v 3 Mara kumi hivi mmenishutumu mimi; ninyi hamuoni aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili.
\v 4 Kama ni dhahiri kweli mimi nimekosa, makosa yangu hubaki kuwa wajibu wangu.
\s5
\v 5 Kama ni dhahiri ninyi mtajiinua juu yangu mimi na kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi,
\v 6 kisha ninyi mnapaswa kutambua kwamba Mungu amefanya mabaya kwangu mimi na amenikamata mimi katika mtego wake yeye.
\s5
\v 7 Tazama, Mimi ninalia kwa sauti, "dhuluma!" lakini sipati jibu. Mimi ninaita kwa ajili ya msaada, lakini hakuna haki.
\v 8 Yeye ameiwekea ukuta njia yangu, ili kwamba mimi nisiweze kupita, na yeye ameweka giza katika njia yangu.
\v 9 Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu, na ameichukua taji kutoka kwenye kichwa changu mimi.
\s5
\v 10 Yeye amenivunjavunja mimi chini kwa kila upande, na Mimi nimetoweka; yeye amelikokota juu tumaini langu kama mti.
\v 11 Yeye pia ameiongeza ghadhabu yake dhidi yangu mimi; yeye ananihesabu mimi kama mmoja wa adui zake.
\v 12 Majeshi yake huja juu pamoja; wao wananikosesha tumaini kwa kuniteka nyara kwa kundi kubwa kupigana na mimi wakizunguka hema yangu.
\s5
\v 13 Yeye amewaweka ndugu zangu mbali kutoka kwangu mimi; watu wangu wa karibu wote wamejitenga kutoka kwangu mimi.
\v 14 Vizazi vyangu vimeniangusha mimi; rafiki zangu wa karibu wamenisahamu mimi.
\s5
\v 15 Wale ambao mwanzoni walikaa kama wageni ndani ya nyumba yangu na watumishi wangu wa kike, hunihesabu mimi kama mgeni. Mimi nimekuwa mgeni katika macho yao.
\v 16 Mimi ninamwita mtumishi wangu, lakini yeye hanipi jibu japokuwa Mimi nimemsihi yeye kwa midomo yangu.
\s5
\v 17 Pumzi yangu mimi ni chukizo kwa mke wangu; Hata mimi ninachukiwa na wale ambao walizaliwa kutoka katika tumbo la mama yangu mimi.
\v 18 Hata watoto wachanga wananichukia mimi; ikiwa Mimi nitainuka kuzungumza, wao huzungumza dhidi yangu mimi.
\v 19 Rafiki zangu wote ninaowazoea wananichukia sana mimi; wale ambao Mimi ninawapenda wamegeuka kinyume na mimi.
\s5
\v 20 Mifupa yangu inashikamana kwenye ngozi yangu na kwenye mwili wangu; Mimi ninaishi tu kwa ngozi ya meno yangu.
\v 21 Iweni na huruma juu yangu mimi, muwe na huruma juu yangu mimi, rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mimi.
\v 22 Kwa nini mnanitesa mimi kama ninyi mlikuwa Mungu? kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu?
\s5
\v 23 Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini! Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu!
\v 24 Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote!
\s5
\v 25 Lakini kama ilivyo kwangu mimi, Mimi ninafahamu kwamba mkombozi wangu anaishi, na kwamba hata mwisho atasimama katika nchi;
\v 26 baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa, ndipo katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu.
\v 27 Mimi nitamwona yeye kwa macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine. Moyo wangu hushindwa ndani yangu mimi.
\s5
\v 28 Kama mnatasema, 'Kwa jinsi gani tutamtesa yeye? Mzizi wa mahangaiko yake unakaa katika yeye;
\v 29 ndipo uwe umeogopeshwa kwa ule upanga, kwa sababu ghadhabu huleta hukumu ya upanga, hivyo kwamba wewe uweze kutambua kuna hukumu."
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ndipo Sofari, Mnaamathi alijibu na kusema,
\v 2 "Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.
\v 3 Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi, lakini roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.
\s5
\v 4 Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale, wakati Mungu alipomweka mwanadamu juu ya nchi:
\v 5 ushindi wa mtu mwovu ni mfupi, na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?
\s5
\v 6 Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu, na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu,
\v 7 bado mtu huyo atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe; wale waliokuwa wamemuona yeye watasema, 'Yuko wapi yeye'?
\s5
\v 8 Yeye atapaa mbali kama ndoto na hataonekana; ndivyo ilivyo, yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la
\v 9 usiku. Jicho ambalo lilimuona yeye halitamuona yeye tena; mahali pake hapatamuona yeye tena.
\s5
\v 10 Watoto wake wataomba msamaha kwa watu maskini, mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.
\v 11 Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani, lakini zitalala naye chini katika mavumbi.
\s5
\v 12 Japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake yeye, japokuwa yeye anauficha chini ya ulimi wake yeye,
\v 13 japokuwa anaushikilia pale na hauruhusu kwenda lakini bado huushikilia katika mdomo wake yeye -
\v 14 chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu; hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.
\s5
\v 15 Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.
\v 16 Yeye atamumunya sumu ya majoka; ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.
\s5
\v 17 Yeye hatafurahia vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.
\v 18 Yeye atayarudisha matunda ya kazi yake na hataweza kuyala; yeye hatafurahia utajiri alioupata kwa biashara zake yeye.
\v 19 Kwa kuwa yeye amewakandamiza na kuwasahau watu maskini; yeye kwa uonevu, amezichukua mbali nyumba ambazo hakuzijenga yeye.
\s5
\v 20 Kwa sababu yeye mwenyewe hakujua utoshelevu wowote, yeye hataweza kuokoa kitu chochote katika kile ambacho alijifurahisha.
\v 21 Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza; kwa hiyo mafanikio yake yeye hayatakuwa ya kudumu.
\v 22 katika wingi wa utajiri wake yeye ataanguka katika mahangaiko; mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.
\s5
\v 23 Wakati akiwa katika kulijaza tumbo lake, Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye; Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye wakati yeye anakula.
\v 24 Ingawa mtu huyo atakimbia kutoka katika silaha ya chuma, upinde wa shaba utampiga yeye.
\v 25 Mshale utatoboa kupitia mgongoni mwake na utatokezea; ni dhahiri, ncha inayong'ra itatokezea nje kupitia ini lake yeye; watesi huja tena juu yake.
\s5
\v 26 Giza lliilo kamilika limetunzwa kwa akiba zake; moto usiopulizwa utamla yeye kwa haraka; utameza kile kilichoachwa katika hema yake.
\v 27 Mbingu zitauweka wazi uovu wake, na nchi itainuka juu dhidi yake yeye kama shahidi.
\s5
\v 28 Utajiri wa nyumba yake utatoweka; bidhaa zake zitamwagika mbali siku ya ghadhabu ya Mungu.
\v 29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu, urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye."
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Sikilizeni hotuba yangu kwa makini, hii na iwe faraja yenu.
\v 3 Nimeteswa, lakini pia nitasema; nikisha kusema, endeleeni kudhihaki.
\s5
\v 4 Lakini kwangu mimi, malalamikio yangu ni kwa mtu? Kwa nini nisiwe mwenye subira?
\v 5 Nitazameni na mshangae, nanyi wekeni mkono wenu midomoni mwenu.
\v 6 Ninapoyafikiria mateso yangu, ninaumizwa, mwili wangu unaogopa.
\s5
\v 7 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wanazeeka, na kuwa na uwezo katika madaraka?
\v 8 Wazao wao wanathibitishwa mbele zao, na uzao wao unaimarika machoni pao.
\v 9 Nyumba zao ziko salama mbali na hofu; wala fimbo ya Mungu haiko juu yao.
\s5
\v 10 Dume lao la ng'ombe linazalisha; halishindwi kufanya hivyo; ng'ombe wao anazaa na hafishi ndama wake akiwa mchanga.
\v 11 Wanawapeleka wadogo wao kama kundi la kondoo, na watoto wao hucheza.
\v 12 Wanaimba kwa tari na vinubi na hufurahi kwa muziki na zomari.
\s5
\v 13 Wanatumia siku zao katika mafanikio, na wanashuka kuzimu kwa utulivu.
\v 14 Wanamwambia Mungu, 'Ondoka kwetu kwani hatutaki ufahamu wowote juu ya njia zako.
\v 15 Mwenye enzi ni nani, hata tumwabudu? Tutafaidika na nini tukimwabudu? Tutapata faida gani ikiwa tutamwomba?
\s5
\v 16 Tazama, je mafanikio yao hayamo katika mikono yao wenyewe? Sina cha kufanya na ushauri wa waovu.
\v 17 Mara ngapi taa za waovu huzimwa, au kwamba majanga huja juu yao? Mara ngapi inatokea kwamba Mungu husambaza huzuni kwao kwa hasira?
\v 18 Ni mara ngapi inatokea kwamba wanakuwa kama mabua mbele ya upepo au kama makapi yanayopeperushwa na dhoruba?
\s5
\v 19 Mnasema, 'Mungu huweka hatia ya mtu kwa watoto wake kuilipa.' Na alipe yeye mwenyewe, ili kwamba aweze kujua hatia yake mwenyewe.
\v 20 Acha macho yake yaone uangamivu wake mwenyewe, na acha anywe gadhabu ya Mwenyezi.
\v 21 Kwani anaangaliaje familia yake mbele yake idadi ya miezi yake inapokwisha.
\s5
\v 22 Je kuna mtu anaweza kumfundisha Mungu maarifa kwa kuwa yeye huwaukumu hata walio juu?
\v 23 Mtu mmoja ufa katika nguvu zake kamili, akiwa na utulivu kabisa na kwa amani.
\v 24 Mwili wake hauna uhitaji, na kiini cha mifupa yake ina unyevu na afya njema.
\s5
\v 25 Mtu mwingine ufa kwa uchungu wa nafsi, bila kujifurahisha kwa jambo lolote jema.
\v 26 Wanazikwa kaburini wote kwa pamoja, funza wanawafunika wote.
\s5
\v 27 Tazama, nayajua mawazo yenu, na jinsi mnavyotaka kunikosesha.
\v 28 Kwa kuwa mwasema, 'Iko wapi sasa nyumba ya mwana wa mfalme? Liko wapi kao alipokaa mwovu?'
\s5
\v 29 Je hamjawauliza wasafiri? Hamfahamu wanavyoweza kusema,
\v 30 kwamba mwovu anaepushwa na siku ya shida, na kwamba anawekwa mbali na siku ya gadhabu?
\s5
\v 31 Ni nani atakaye ituhumu siku ya mwovu mbele yake? Ni nani atakayemwadhibu kwa alichokifanya?
\v 32 Hata hivyo atapelekwa kaburini; watu wataliona kaburi lake.
\v 33 Udongo wa bondeni utakuwa mtamu kwake; watu wote watamfuata, hata kuwe na watu wengi mbele yake.
\s5
\v 34 Ni jinsi gani basi mtanifariji bila kufikiri, kwa kuwa majibu yenu hayana lolote ila uongo?"
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
\v 2 Je mtu anaweza kumfaa Mungu "Je mwenye hekima anaweza kufaa kwake.
\v 3 Je inafurahisha kwa Mwenyezi ikiwa u mwenye haki? Je ni faida yake ukiyafanya safi maisha yako?
\s5
\v 4 Je ni kwa sababu ya uchaji wako kwake hata akukemee na kukuadhibu?
\v 5 Je si kwa sababu ya wingi wa uovu wako? Je hakuna mwisho wa makosa yako?
\s5
\v 6 Kwa maana umechukua dhamana kutoka kwa ndugu yako bila sababu; umechukua mavazi ya mtu na kumwacha uchi.
\v 7 Haukuwapa wenye kiu maji ya kunywea; umewanyima chakula wenye njaa
\v 8 japokuwa wewe, mwenye uwezo, uliimiliki nchi, japokuwa wewe, mwenye kuheshimiwa, uliishi ndani yake.
\s5
\v 9 Umewaacha wajane waondoke bila kitu; umewatesa yatima.
\v 10 Kwa hiyo, mabaya yanakuzunguka, na hofu za ghafla zinakusumbua.
\v 11 Kuna giza, hata usione; gharika inakufunika.
\s5
\v 12 Je Mungu hayupo juu mbinguni? Anaangalia juu ya nyota, jinsi zilivyo juu!
\v 13 Unasema, 'Mungu anajua nini? Je anaweza kuamua kupitia giza totoro?
\v 14 Mawingu ni kifuniko chake, hata asituone; anatembea anga la mbinguni.'
\s5
\v 15 Je utayaishi maisha ya zamani walioishi waovu -
\v 16 walioondolewa kabla ya siku zao, ambao misingi yao imeondolewa kama mto,
\v 17 waliomwambia Mungu, 'Ondoka kwetu'; waliosema, 'Mwenyezi anaweza kututenda nini?
\s5
\v 18 Hata hivyo bado alizijaza nyumba zao kwa mema; mipango ya waovu iko mbali nami.
\v 19 Wenye haki wanayaona yawapatayo waovu na kufurahi; wasio na hatia wanawacheka kwa dhihaka.
\v 20 Wanasema, 'Bila shaka walioinuka kinyume chetu wameondolewa; moto umeteketeza mali zao.'
\s5
\v 21 Basi patana na Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hiyo, mema yatakujia.
\v 22 Nakusihi, pokea, maelekezo yake; uyatii maneno yake.
\s5
\v 23 Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa, ukiacha kutenda uovu makaoni mwako.
\v 24 Weka hazina zako mavumbini, dhahabu ya Ofiri kati ya mawe ya vijito,
\v 25 na Mwenyezi atakuwa hazina zako, fedha ya thamani kwako.
\s5
\v 26 Nawe utajifurahisha katika Mwenyezi; utamwangalia Mungu.
\v 27 Utamwomba, naye atakusikiliza; utamtolea nadhiri.
\v 28 Lakini pia utatamka lolote, nawe utapewa; nuru itaangaza maishani mwako.
\s5
\v 29 Mungu humshusha mwenye kiburi, naye humwinua mnyenyekevu.
\v 30 Atamwokoa asiye na hatia; utaokolewa kupitia usafi wa mikono yako."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
\s5
\v 3 Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
\v 4 Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
\v 5 Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
\s5
\v 6 Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
\v 7 Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
\s5
\v 8 Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
\v 9 Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
\s5
\v 10 Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
\v 11 Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
\v 12 Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
\s5
\v 13 Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
\v 14 Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
\s5
\v 15 Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
\v 16 Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
\v 17 Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija?
\s5
\v 2 Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao.
\v 3 Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana.
\v 4 Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao.
\s5
\v 5 Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao.
\v 6 Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu.
\v 7 Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi.
\s5
\v 8 Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao.
\v 9 Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini.
\v 10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula.
\s5
\v 11 Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu.
\v 12 Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao.
\s5
\v 13 Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake.
\v 14 Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku.
\s5
\v 15 Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha.
\v 16 Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru.
\v 17 Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro.
\s5
\v 18 Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu.
\v 19 Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi.
\s5
\v 20 Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti.
\v 21 Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane.
\s5
\v 22 Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha.
\v 23 Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao.
\s5
\v 24 Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka.
\v 25 Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?"
\s5
\c 25
\p
\v 1 Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema,
\v 2 "Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni.
\v 3 Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake?
\s5
\v 4 Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye?
\v 5 Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake.
\v 6 Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!"
\s5
\c 26
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Mmemsaidiaje aliyedhaifu!
\v 3 Jinsi gani mmemshauri asiye na hekima na kutamka maneno yenye maarifa kwake!
\v 4 Kwa msaada wa nani mmesema maneno haya? Ni roho ya nani iliyotoka ndani yenu?
\s5
\v 5 Maiti inatetemeka chini ya maji, na vyote wilivyomo ndani yake.
\v 6 Kuzimu kuko wazi mbele ya Mungu; uharibifu hauna kizuizi dhidi yake.
\s5
\v 7 Huitandaza kaskazi juu ya nafasi wazi na kuining'iniza dunia hewani.
\v 8 Huyafunga maji katika mawingu yake mazito, lakini hayagawanyiki chini yake.
\s5
\v 9 Huufunika uso wa mwezi na kueneza mawingu yake juu yake.
\v 10 Amechora ukingo wa duara juu ya maji kama mpaka kati ya nuru na giza.
\s5
\v 11 Nguzo za mbinguni zinatikisika na zimestushwa na kukemea kwake.
\v 12 Aliituliza bahari kwa uwezo wake; kwa ufahamu wake alimwaribu Rahab
\s5
\v 13 Kwa pumzi yake, aliziondoa mbingu kwa dhorubu; mbingu ziliondolewa kwa dhorubu; mkono wake ulimchoma nyoka anayekimbia.
\v 14 Tazama, hizi si zaidi ya madogo ya njia zake; Jinsi gani tunasikia akitunong'oneza! Ni nani awezaye kufahamu uwezo wake.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Ayubu akaendelea kuoengea na kusema,
\v 2 "Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu,
\v 3 kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu.
\s5
\v 4 Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo.
\v 5 Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu.
\s5
\v 6 Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi.
\v 7 Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki.
\s5
\v 8 Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake?
\v 9 Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat?
\v 10 Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote
\s5
\v 11 Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi.
\v 12 Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana.
\s5
\v 13 Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi.
\v 14 Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa.
\s5
\v 15 Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea.
\v 16 Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi,
\v 17 na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali.
\s5
\v 18 Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi.
\v 19 Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu.
\s5
\v 20 Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku.
\v 21 Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake.
\s5
\v 22 Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake.
\v 23 Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Hakika kuna machimbo ya fedha, wanaposafisha dhahabu.
\v 2 Chuma uchimbwa; shaba uyeyushwa kutoka katika jiwe.
\s5
\v 3 Mtu anaondoa giza na kutafuta, katika mpaka wa mbali, mawe hayaonekani na giza totoro.
\v 4 Huchimba shimo mbali na makazi ya watu, mahali pasipopitwa na mtu. Huning'inia mbali na watu; uharakisha kwenda na kurudi.
\s5
\v 5 Kwa nchi, kizalishwapo chakula, inapinduliwa kama kwa moto.
\v 6 Mawe yake yana johari, na vumbi lake lina dhahabu.
\s5
\v 7 Hata ndege mwindaji hapajui, wala jicho la kipanga halijapaona.
\v 8 Ndege mwenye majivuna hajawai kuiona njia hiyo, wala simba mkali kupita pale.
\s5
\v 9 Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake.
\v 10 Huweka njia katika miamba; macho yake pale kila kilicho cha thamani.
\v 11 Hufunga vyanzo hata wasiondoke; kilichofichika pale hukifunua.
\s5
\v 12 Hekima itakuwa wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
\v 13 Mtu hafahamu thamani yake; wala haipatikani katika nchi ya walio hai.
\v 14 Vilindi vya maji chini ya nchi husema, 'Haiko kwangu'; bahari husema, 'Haipo pamoja nami.'
\s5
\v 15 Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha.
\v 16 Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari.
\v 17 Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi.
\s5
\v 18 Hailinganishwi na marijani wala yaspi; hakika, thamani ya hekima inapita madini ya rubi.
\v 19 Topazi ya Ethiopia hailinganishwi nayo; wala kuthamanishwa kwa dhahabu safi.
\s5
\v 20 Je hekima inatoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
\v 21 Hekima imejificha mbali na macho ya viumbe wote na ndege wa angani.
\v 22 Mauti na uharibifu husema, 'Tumesikia tu tetesi kwa masikio yetu.'
\s5
\v 23 Mungu hufahamu njia ya kuipata; anapafahamu ilipo.
\v 24 Kwani uona miisho yote ya dunia na huona chini ya mbingu zote.
\v 25 Hapo kale, alifanya nguvu za upepo na kuyagawanya maji kwa kipimo.
\s5
\v 26 Aliiwekea mvua tamko na njia ya radi na munguromo.
\v 27 Kisha akaiona hekima na kuitangaza; aliianzisha, bila shaka, na kuipima.
\v 28 Aliwambia watu, 'Tazameni, kumcha Bwana - ni hekima; kuacha uovu ni ufahamu."
\s5
\c 29
\p
\v 1 Ayubu akaendelea na kusema,
\v 2 Ee, ningekuwa kama nilivyokuwa miezi iliyopita wakati Mungu aliponiagalia,
\v 3 taa yake ilipowaka kichwani pangu, na pale nilipotembea gizani kwa nuru yake.
\s5
\v 4 Ee, kwamba ningekuwa kama nilivyokuwa katika siku za ujana wangu uhusiano wangu na Mungu ulivyokuwa mzuri,
\v 5 wakati Mwenyezi alipokuwa pamoja nami, na wanangu walipokuwa karibu nami,
\v 6 wakati maisha yangu yalipokuwa yamejawa na utele, na mwamba uliponichuruzishia chemichemi za mafuta.
\s5
\v 7 Nilipokwenda langoni mwa mji, nilipokaa katika eneo la mji,
\v 8 vijana waliniona na walikaa mbali kwa kuniheshimu, na wazee waliinuka na kusimama kwa ajili yangu.
\s5
\v 9 Wana wa mfalme waliacha kuongea nilipofika; wangeweka mkono wao katika vinywa vyao.
\v 10 Sauti za waheshimiwa zililazimishwa, na ndimi zao hazikuweza kuongea vinywani mwao.
\s5
\v 11 Kwani baada ya kunisikia, wangenibariki; waliponiona, wangeniona na kuniheshimu
\v 12 kwa maana nilikuwa nikiwasaidia masikini waliokuwa wakiteseka, na yatima, asiye na msaada.
\v 13 Baraka zao waliokuwa karibu kuangamia zilinipata; niliufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
\s5
\v 14 Nilijivika utakatifu, nao ulinifunika; haki yangu ilikuwa kama kanzu na kilemba.
\v 15 Niliwasaidia vipofu; niliwasaidia walemavu.
\v 16 Niliwasaidia wahitaji; niliwasaidia hata wasionijua.
\s5
\v 17 Nilimnyamazisha mwovu; nilimpokonya manusura kutoka katika meno yake.
\v 18 Kisha nilisema nitakufa mahali salama; nitazizidisha siku zangu kama mchanga.
\v 19 Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu.
\s5
\v 20 Heshima yangu ni mpya daima, na nguvu za upinde wangu zipo katika mkono wangu kila wakati.
\v 21 Watu walinisikiliza; walinisubiri; walisikiliza ushauri wangu.
\v 22 Nilipo maliza kuongea hawakunena tena, maneno yangu yaliwatia nguvu kama mvua.
\s5
\v 23 Waliningoja kama kungoja mvua; waliyathamini maneno yangu, kama walivyotamani mvua iliyokawia.
\v 24 Niliwafurahia bila wao kutarajia; hawakukataa uzuri wa uso wangu.
\s5
\v 25 Nilikuwa kama mfalme wao na kuwachagulia cha kufanya; nilikuwa kama mfalme katika jeshi lake, kama awafarijiye waombolezaji mazishini.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Sasa vijana wananidhihaki - vijana ambao baba zao wasingeweza hata kuwahudumia mbwa wa kundi langu.
\v 2 Kwa kweli, nguvu za mikono ya baba zao, zingenisaidia nini - watu ambao hawakuwa na nguvu wakati wa kukua kwao?
\v 3 Walidhoofishwa na umasikini na njaa; walisaga nchi kavu mafichoni.
\s5
\v 4 Walichuma mche chumvi na majani ya vichaka; mizizi ya mti wa ufagio ilikuwa ndiyo chakula chao.
\v 5 Waliondolewa miongoni mwa watu waliopiga kelele nyuma yao kama ambavyo mtu angempigia kelele mwizi.
\v 6 Hivyo walipaswa kuishi katika mabonde ya mto, katika mashimo ya ardhi na miamba.
\s5
\v 7 Walilia kwa uchungu porini kama punda; chini ya vichaka walikutana.
\v 8 Walikuwa uzao wa wapumbavu, hakika, wa watu wasiofaa; waliondolewa duniani kama waarifu.
\s5
\v 9 Lakini sasa, nimekua sababu ya wimbo wa dhihaka kwa wana wao; hakika, nimekuwa mzaa kwao.
\v 10 Wananichukia na kusimama mbali nami; hawaachi kunitemea usoni.
\v 11 Kwa maana Mungu ameondoa kamba katika upinde wangu na amenipiga, na hivyo watu hawa wanashindwa kujizuia mbele yangu.
\s5
\v 12 Kundi la vijana wabaya wanashambulia nguvu zangu; wananiondolea mbali na kukusanya kinyume changu rundo la kuhusuru.
\v 13 Wanaharibu maisha yangu; wanapeleka mbele maangamizi yangu, watu wasio na wakuwazuia.
\s5
\v 14 Wanakuja kinyume changu kama jeshi katika tundu pana katika ukuta wa mji; katikati ya maangamizi wanajizungusha juu yangu.
\v 15 Hofu zimeniandama; heshima yangu imeondolewa mbali nami kama kwa upepo; mafanikio yangu yameondolewa kama wingu.
\s5
\v 16 Sasa uhai wangu umeondolewa ndani yangu; siku nyingi za maumivu zimenipita.
\v 17 Mifupa inauma ndani yangu wakati wa usiku; maumivu yanayonisaga hayaishi.
\s5
\v 18 Nguvu kuu ya Mungu imeshika mavazi yangu; yananizunguka kama kala ya vazi langu.
\v 19 Amenitupa matopeni; nimekuwa kama vumbi na majivu.
\s5
\v 20 Nakulilia wewe, Mungu, lakini haunijibu; ninasimama, nawe unaniangalia tu.
\v 21 Umegeuka na kuwa mkali kwangu; kwa nguvu za mkono wako umenitesa.
\s5
\v 22 Unaniinua katika upepo na kuufanya unikokote; unanirusha huku na kule katika dhoruba.
\v 23 Kwa maana najua ya kwamba utanipeleka mautini, nyumba ya hatima kwa viumbe vyote.
\s5
\v 24 Lakini, je hakuna ainuaye mkono wake kuomba msaada aangukapo? Je hakuna aombaye msaada akiwa tabuni?
\v 25 Je sikulia kwa ajili yake aliyekuwa tabuni? Je sijahuzunika kwa ajili ya mwitaji?
\v 26 Nilipotazamia mema, ndipo yalipokuja mabaya; niliposubiri nuru, giza lilikuja badala yake.
\s5
\v 27 Moyo wangu umetaabika na hautulii; siku za mateso zimenipata.
\v 28 Nimekuwa na ngozi nyeusi lakini si kwa sababu ya jua; nasimama katika kusanyiko na kulilia msaada.
\v 29 Nimekuwa ndugu kwa mbwea, mshirika wa mbuni.
\s5
\v 30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi na inapukutika; mifupa yangu imeunguzwa na joto.
\v 31 Kwa hiyo kinubi changu kimefunguliwa kwa nyimbo za maombolezo, zomari yangu kwa kuimba kwao waombolezao.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Nimefanya patano na macho yangu; ni kwa namna gani tena napaswa kumtazama mwanamwali kwa tamaa?
\v 2 Ni sehemu gani kutoka kwa Mungu juu, na urithi gani kutoka kwake mwenye nguvu aliye juu?
\s5
\v 3 Nilikuwa nafikiri kwamba majanga ni kwa watu wasio na haki, na misiba ni kwa ajili ya watu watendao mabaya.
\v 4 Je Mungu hazioni njia zangu na kuzihesabu hatua zangu zote?
\s5
\v 5 Kama nimetembea katika udanganyifu, kama mguu wangu umeharakisha katika uongo,
\v 6 na nipimwe katika vipimo vilivyo sawa ili kwamba Mungu aujue uadilifu wangu.
\s5
\v 7 Kama hatua zangu zimegeuka kutoka katika njia sahihi, kama moyo wangu umetembea kwa kufuata macho yangu, na kama doa lolote la uchafu limeng'ang'ania katika mikono yangu,
\v 8 na kisha mimi nipande na mtu mwingine na ale; mavuno na yang'olewe katika shamba langu.
\s5
\v 9 Na kama moyo wangu umevutiwa na mwanamke mwingine, ikiwa nimelala na mke wa jirani yangu katika hali ya kusubiria katika mlango wake,
\v 10 na ndipo mke wangu na asage nafaka kwa mwanaume mwingine, na wanaume wengine na walale naye.
\s5
\v 11 Na kwa hilo litakuwa ni kosa kubwa; kwa kweli, utakuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi.
\v 12 Kwa kuwa ni moto ambao unateketeza kila kitu kwa uharibifu, na kwamba utaunguza mavuno yangu yote.
\s5
\v 13 Ikiwa nilikataa ombi la haki kutoka kwa watumishi wangu wa kiume na wa kike wakati walipohojiana nami,
\v 14 kisha nini basi ningefanya wakati Mungu anapoinuka ili kunishitaki mimi? Atakapokuja kunihukumu, nitamjibuje?
\v 15 Je yeye aliyenifanya mimi tumboni hakuwafanya wao pia? Je yeye si yeye yule aliyetuumba sisi wote katika tumbo?
\s5
\v 16 kama nimewanyima watu masikini matakwa yao, au kama nimesababisha macho ya wajane yafifie kwa kulia,
\v 17 au ikiwa kama nimekula kipande changu na sijawaruhusu wale wasio na baba kukila pia -
\v 18 kwasababu tangu ujana wangu yatima walikua pamoja nami kama kuwa na baba, nami nimemwongoza mama yake, mjane, tangu katika tumbo la mama yangu mwenyewe.
\s5
\v 19 ikiwa nimemwona yeyote akiangamia kwa kwa kukosa mavazi, au kama nimemwona mtu mhitaji akiwa hana nguo;
\v 20 ikiwa moyo wake haujanibariki kwasababu amekuwa hajatiwa joto na sufu ya kondoo zangu,
\v 21 ikiwa nimeinua juu mkono wangu kinyume na watu wasio na baba kwa kuwa niliona msaada wangu katika lango la mji, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu.
\s5
\v 22 Ndipo bega langu na lianguake kutoka katika sehemu yake, na mkono wangu uvunjike katika kiungo chake.
\v 23 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu; kwasababu ya mawazo ya ukuu wake, nisingeweza kufanya mambo hayo.
\s5
\v 24 Kama ningeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, na kama ningesema kwa dhahabu safi, 'wewe unanifanya kuwa na tumaini';
\v 25 na kama nimefurahi kwasababu ya utajiri wangu ulikuwa mkubwa, kwa kuwa mkono wangu umepata mali nyingi, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu!
\s5
\v 26 Ikiwa nimeliona jua lilipowaka, au mwezi ukitembea katika mng'ao wake,
\v 27 na kama moyo wangu umevutwa kwa siri, ili kwamba mdomo wangu umeubusu mkono wangu katika ibada yao -
\v 28 hili nalo pia lingekuwa ni ubaya wa kuadhibiwa na waamuzi, kwa kuwa ningekuwa nimemkana Mungu aliyejuu.
\s5
\v 29 Ikiwa nimefurahia uharibifu wa yeyote ambaye ananichukia mimi, au kuwapa hongera wakati majanga yanapowapata, ndipo ulete mashitaka dhidi yangu!
\v 30 Kwa kweli sijauruhusu hata mdomo wangu kutenda dhambi kwa kuuomba uhai wake kwa laana.
\s5
\v 31 Ikiwa watu wa hema yangu hawajasema,' Nani aweza kumpata mtu ambaye hayashibishwa na chakula cha Ayubu?
\v 32 (hata mgeni hajawahi kukaa katika pembe ya mji, kwa kuwa siku zote nimefungua milango yangu kwa ajili ya wasafiri), na kama haiko hivyo, ndipo mlete mashitaka kinyume nami!
\s5
\v 33 Ikiwa, kama binadamu nimezificha dhambi zangu kwa kuficha hatia ndani ya kanzu yangu -
\v 34 kwa kuwa niliogopa kusanyiko kubwa, kwasababu ya matwezo ya familia yaliniogopesha, hivyo basi nilinyamaza kimya na sikuweza kwenda nje, basi nileteni mashitaka dhidi yangu!
\s5
\v 35 Ee, kama nilikuwa na mtu wa kunisikiliza! Ona, hii ni saini yangu; na Mwenye nguvu na anijibu! Ikiwa nilikuwa na shitaka rasmi ambalo adui yangu ameliandika!
\v 36 Hakika ningelibeba hadharani juu ya bega langu; ningeliweka juu kama taji.
\v 37 Ningemweleza hesabu ya hatua zangu; na kama mwana wa mfalme mwenye kujiamini ningepanda kwenda kwake.
\s5
\v 38 Kama nchi yangu ingelia dhidi yangu, na matuta yake yaomboleza pamoja,
\v 39 ikiwa nimekula mavuno yake bila kulipia au kama nimesababisha wamiliki wake kupoteza maisha yao,
\v 40 ndipo miiba na iote badala ya ngano na magugu badala ya shayiri." Maneno ya Ayubu yamemalizika.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Hivyo hawa watu watatu walikoma kumjibu Ayubu kwasababu alikuwa ni mwenye haki katika macho yake mwenyewe.
\v 2 Ndipo iliwaka hasira ya Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi, wa familia ya Ramu, iliwaka dhidi ya Ayubu kwa kuwa alijihesabia haki mwenyewe kuliko Mungu.
\s5
\v 3 Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu kwasababu hawakupata jibu kwa ajili ya Ayubu, na bado walimhukumu Ayubu.
\v 4 Sasa Elihu alikuwa amemsubiri Ayubu ili aweze kuzungumza naye kwa kuwa watu wengine walikuwa wakubwa kuliko yeye.
\v 5 Hata hivyo, wakati Elihu alipoona ya kuwa hapakuwa na jibu katika midomo ya watu hawa watatu, hasira yake iliwaka.
\s5
\v 6 Ndipo Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi alinena na kusema, "Mimi ni mdogo, na ninyi ni wazee. Hii ndio sababu nilijizuia na sikuthubutu kuzungumza mawazo yangu mwenyewe.
\v 7 Nilisema, "Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima.
\s5
\v 8 Lakini kuna roho ndani ya mtu; pumzi ya Mwenye nguvu humpa yeye ufahamu.
\v 9 Si tu watu wakubwa ndio wenye hekima, wala watu wazee pekee ambao hufahamu haki.
\v 10 Hivyo basi nakwambia wewe, "Nisikilizeni mimi; Nitakwambia pia uelewa wangu.'
\s5
\v 11 Tazama, niliyasubiria maneno yenu; nilisikiliza hoja zenu wakati mlipokuwa mnafikiri juu ya kile cha kusema.
\v 12 Hakika, niliwajali sana ninyi, lakini, tazama, hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kumshawishi Ayubu wala ambaye aliweza kumjibu maneno yake.
\s5
\v 13 Iweni waangalifu msije mkasema, 'Tumepata hekima!' Mungu atakuwa amemshinda Ayubu; mtu wa kawaida hawezi akafanya hivyo.
\v 14 Kwa kuwa Ayubu hajasema mojamoja maneno yake juu yangu, basi sitamjibu kwa maneno yenu.
\s5
\v 15 Hawa watu watatu wamep igwa bumbuwazi; hawawezi kuendelea kumjibu Ayubu; hawana neno zaidi la kusema.
\v 16 Je ninapaswa kusubiria kwasababu hawazungumzi, kwa kuwa wamesimama pale kimya na wala hawajibu zaidi?
\s5
\v 17 La, nitajibu pia upande wangu; Nitawaambia pia ufahamu wangu.
\v 18 Kwa kuwa nimejawa na maneno mengi, roho ndani yangu inanisukuma.
\v 19 Tazama, kifua changu ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka.
\s5
\v 20 Nitazungumza ili kwamba niweze kuburudishwa; nitafungua kimya changu na kusema.
\v 21 Sitaonesha upendeleo; wala sitatoa sifa za majina kwa mtu yeyote.
\v 22 Kwa kuwa sijui namna ya kutoa sifa; kama nitafanya hivyo, Muumba wangu atanikatilia mimi mbali.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Kwahiyo sasa, nakuomba wewe, Ayubu, usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote.
\v 2 Tazama sasa, nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu.
\v 3 Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu; yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.
\s5
\v 4 Roho ya Mungu imeniumba; pumzi ya Mwenye nguvu imenipatia uhai.
\v 5 Kama unaweza, nijibu; weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame.
\s5
\v 6 Tazama, niko kama wewe ulivyo mbele za Mungu; nimeumbwa pia kutoka katika udongo.
\v 7 Ona, tishio langu halitakufanya wewe uogope; wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.
\s5
\v 8 Umesema kwa hakika katika masikio yangu; nimeisikia sauti ya maneno yakeo yakisema,
\v 9 'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.
\s5
\v 10 Tazama, Mungu huona nafasi za kunishambulia mimi; huniangalia mimi kama adui yake.
\v 11 Huweka miguu yangu akiba; naye huangalia njia zangu zote.'
\v 12 Tazama, katika hili hauko sawa, nitakujibu, kwa kuwa Mungu ni mkuu kuliko mtu.
\s5
\v 13 Kwanini unashindana naye? Huwa hahesabu matendo yake yoyote.
\v 14 Kwa kuwa Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili, ingawa mwanadamu hawezi kutambua.
\v 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani -
\s5
\v 16 basi Mungu hufungua masikio ya watu, na kuwatisha kwa vitisho,
\v 17 kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.
\v 18 Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.
\s5
\v 19 Mtu huadhidibiwa pia na maumivu kitandani mwake, na maumivu makali yanayodumu katika mifupa yake,
\v 20 ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri.
\s5
\v 21 Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania.
\v 22 Hakika, roho yake inasogea shimoni, na uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.
\s5
\v 23 Lakini kama kuna malaika anayeweza kuwa mpatanishi kwa ajili yake, mpatanishi mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika, kumwonesha kile kilicho cha haki ili atende haki,
\v 24 na kama malaika ni mpole kwake na kumwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake,'
\s5
\v 25 kisha mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto, atazirudia siku za nguvu za ujana wake.
\v 26 Atamwomba Mungu, na Mungu atakuwa mwema kwake, ili kwamba auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha. Mungu atampa mtu ushindi wake.
\s5
\v 27 Ndipo mtu huyo ataimba mbele ya watu wengine na kusema, 'Nilitenda dhambi na kuasi kile kilichokuwa cha haki, lakini dhambi yangu haikuadhibiwa.
\v 28 Mungu ameiokoa roho yangu isiende chini shimoni; maisha yangu yataendelea kuuona mwanga.'
\s5
\v 29 Tazama, Mungu hufanya mambo haya yote pamoja na mwanadamu, mara mbili, naam, hata mara tatu,
\v 30 kuirudisha roho yake kutoka shimoni, ili kwamba aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.
\s5
\v 31 Ayubu, zingatia na unisikilize mimi; nyamaza nami nitasema.
\v 32 Ikiwa una kitu cha kusema, na unijibu; sema, maana nataka kuhakikisha kwamba wewe uko katika haki.
\v 33 Kama sivyo, basi nisikilize, ubaki kimya, nami nitakufundisha wewe hekima."
\s5
\c 34
\p
\v 1 Zaidi ya hayo, Elihu aliendelea kusema:
\v 2 "Sikilizeni maneno yangu, ninyi watu wenye hekima; nisikieni, ninyi mlio na maarifa.
\v 3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama ambavyo kaakaa huonja chakula.
\s5
\v 4 Na tujichagulie sisi wenyewe yale yenye adili: na tujigundulie miongoni mwetu yale yaliyo mazuri.
\v 5 Kwa kuwa Ayubu amesema, 'mimi ni mwenye haki, lakini Mungu ameondoa haki zangu.
\v 6 Pamoja na haki zangu, ninaangaliwa kama mwongo. Kidonda changu hakiponyeki, ingawa mimi sina dhambi.'
\s5
\v 7 Ni mtu gani aliye kama Ayubu ambaye hunywa dharau kama maji,
\v 8 ambaye huzunguka katika ushirika wa watu ambao ni waovu, na ambaye hutembea pamoja na watu waovu?
\v 9 Kwa kuwa anasema, ' Hakuna faida kwa mtu kujifurahisha kwa kufanya mambo ambayo Mungu anayataka.'
\s5
\v 10 Basi nisikilizeni mimi, enyi watu wenye ufahamu: na iwe mbali na Mungu kwamba atatenda uovu;
\v 11 na iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi. Kwa kuwa humlipa mtu kutokana na kazi yake; na humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe.
\v 12 Kwa hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.
\s5
\v 13 Ni nani aliyemweka kuwa mtawala wa dunia? Ni nani aliyeiweka dunia yote chini yake?
\v 14 Ikiwa aliweka makusudio yake juu yake mwenyewe, na kama amejikusanyia mwenyewe nafsi yake na pumzi yake,
\v 15 basi miili yote itateketea pamoja; mwanadamu angerudi mavumbini tena.
\s5
\v 16 Kama sasa mna ufahamu, sikilizeni haya; sikilizeni sauti ya maneno yangu.
\v 17 Je yeye anayeichukia haki aweza kutawala? Je mtamhukumu Mungu kuwa ni mwenye makosa, ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu?
\s5
\v 18 Mungu ambaye humwambia mfalme, ' Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?
\v 19 Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
\v 20 Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
\s5
\v 21 Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
\v 22 Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
\v 23 Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
\s5
\v 24 Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
\v 25 Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
\s5
\v 26 Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
\v 27 kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
\v 28 Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
\s5
\v 29 Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
\v 30 ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
\s5
\v 31 Fikiria mtu akimwambia Mungu, ' Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
\v 32 nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
\v 33 Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
\s5
\v 34 Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,
\v 35 Ayubu anazungumza bila maarifa; maneno yake hayana hekima.'
\s5
\v 36 Kama Ayubu alijaribiwa kwa kitu kidogo kabisa katika kesi yake kwasababu ya kuongea kwake kama watu waovu.
\v 37 Kwa kuwa anaongeza uasi juu ya dhambi yake; anapiga makofi ya dharau kati yetu; anaweka maneno kinyume na Mungu."
\s5
\c 35
\p
\v 1 Aidha, Elihu aliendelea kusema,
\v 2 "Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
\v 3 Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
\s5
\v 4 Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
\v 5 Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
\s5
\v 6 Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
\v 7 Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
\v 8 Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
\s5
\v 9 Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
\v 10 Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
\v 11 ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
\s5
\v 12 Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
\v 13 Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
\v 14 Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
\s5
\v 15 Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
\v 16 Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa."
\s5
\c 36
\p
\v 1 Elihu aliendelea na kusema,
\v 2 "Niruhusu niseme kidogo zaidi, nami nitakuonesha baadhi ya mambo kwasababu nina maneno machache ya kusema kwa ajili ya Mungu.
\v 3 Nitapata maarifa yangu kutoka mbali; nitatambua kwamba haki ni ya Muumba wangu.
\s5
\v 4 Kwa kweli, maneno yangu hayatakuwa ya uongo; mtu fulani aliyekomaa katika maarifa yu pamoja nawe.
\v 5 Angalia, Mungu ni mwenye nguvu, na hamdharau mtu yeyote; yeye ni mwenye nguvu katika uweza wa ufahamu.
\s5
\v 6 Yeye huwa hayahifadhi maisha ya watu waovu bali badala yake hufanya yaliyo ya haki kwa wale wanaoteseka.
\v 7 Haondoi macho yake kwa wenye haki bali badala yake huwaweka juu ya viti vya enzi kama wafalme milele, nao wameinuliwa juu.
\s5
\v 8 Ikiwa wamefungwa minyororo na kunaswa katika kamba za mateso,
\v 9 kisha huwafunulia kile walichokifanya, na maovu yao na kiburi chao.
\s5
\v 10 Hufungua pia masikio yao kwa ajili ya agizo lake, na huwaamuru wageuke kutoka katika uovu.
\v 11 Ikiwa watamsikiliza na kumwabudu yeye, wataishi katika mafanikio katika siku zao, na miaka yao katika hali ya kuridhika.
\v 12 Hata hivyo, kama hawatasikiliza, wataangamia kwa upanga; watakufa kwasababu hawana maarifa.
\s5
\v 13 Na wale wasiomjua Mungu hutunza hasiria zao katika mioyo; hawaombi msaada hata wakati ambapo Mungu huwafunga.
\v 14 Hawa hufa katika ujana wao; na maisha yao hukoma kati ya makahaba.
\s5
\v 15 Mungu huwainua watu walioonewa kwa njia ya mateso yao; hufungua masikio yao kwa njia ya uonevu wao.
\v 16 Kwa hakika, yeye angependa kuwatoa ninyi katika mateso na kuwaweka katika sehemu pana ambapo hakuna masumbufu na mahali ambapo meza yenu ingewekwa ikiwa na chakula kilichojaa mafuta.
\s5
\v 17 Lakini wewe umejaa hukumu juu ya watu waovu; hukumu na haki umeziachilia.
\v 18 Usiuache utajiri ukuvute katika udanganyifu; na sehemu kubwa ya rushwa isikugeuze upande kutoka katika haki.
\s5
\v 19 Je utajiri wako waweza kukunufaisha, ili kwamba usiwe katika taabu, au nguvu zako zote za uwezo zaweza kukusaidia?
\v 20 Usiutamani usiku ili utende dhambi dhidi ya wengine wakati ambapo mataifa hukatiliwa mbali katika nafasi zao.
\v 21 Uwe mwangalifu ili kwamba usigeukie dhambi kwasababu unajaribiwa kwa mateso ili kwamba ukae mbali na dhambi.
\s5
\v 22 Angalia, Mungu ameinuliwa katika nguvu zake; ni nani aliye mwalimu kama yeye?
\v 23 Ni nani alishamwalekeza njia yake? Nani anayeweza kumwambia, 'Wewe umetenda mambo yasiyo ya haki?'
\v 24 Kumbuka kuyasifu matendo yake, ambayo watu wameyaimba.
\s5
\v 25 Watu wote wameshayatazama hayo matendo, lakini wanayaona tu matendo hayo kwa mbali sana.
\v 26 Tazama, Mungu ni mkuu, lakini sisi hatumfahamu yeye vizuri; hesabu ya miaka yake haihesabiki.
\s5
\v 27 Kwa kuwa yeye huvuta matone ya maji ili kuyachuja kama mvua katka mvuke wake,
\v 28 ambayo mawingu yake huyamwaga chini na kuyandondosha kwa wingi kwa mwanadamu.
\v 29 Hakika, kuna hata mmoja awezaye kuelewa kwa undani kusambaa kwa mawingu na radi kutoka katika nyumba yake?
\s5
\v 30 Angalia, hueneza mwanga wake kumzunguka na kufunika mizizi ya bahari.
\v 31 Kwa namna hii huyahukumu mataifa na kuwapa chakula kwa wingi.
\s5
\v 32 Yeye huuijaza mikono yake kwa mwanga mpaka pale anapouamuru kupiga shabaha yake.
\v 33 Na muungurumo wake huonya kwa dhoruba, wanyama wanaweza kusikia kuja kwake.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Hakika, moyo wangu hutetemeka kwa hili; umeondolewa kutoka katika sehemu yake.
\v 2 Sikia, Ee, Sikia kelele za sauti yake, sauti inayotoka katika mdomo wake.
\v 3 Huiagiza sauti chini ya mbingu yote, na huutuma mwanga wake katika mipaka ya dunia.
\s5
\v 4 Sauti huunguruma baada yake; yeye huunguruma kwa sauti ya ukuu wake; hauzuii mshindo wa mwanga wakati sauti yake inaposikika.
\v 5 Mungu huunguruma kwa sauti yake kwa namna ya ajabu; yeye hufanya mambo makubwa ambayo sisi hatuwezi kuyafahamu.
\v 6 Kwa kuwa huiambia theluji, 'Angukeni juu ya dunia'; hali kadhalika kwa manyunyu ya mvua, 'Iweni manyunyu makubwa ya mvua.'
\s5
\v 7 Huuzuia mkono wa kila mtu usifanye kazi, ili kwamba watu wote aliowaumba wataona matendo yake.
\v 8 Kisha hayawani huenda na kujificha na kukaa katika mapango yake.
\v 9 Dhoruba hutoka katika chumba chake upande wa kusini na baridi kutoka katika pepo zilizotawanyika katika upande wa Kaskazini.
\s5
\v 10 Barafu imetolewa kwa pumzi ya Mungu; upana wa maji umeganda kama chuma.
\v 11 Hakika, huyapima mawingu manene yenye unyevu; yeye huusambaza mwanga wake katika mawingu.
\s5
\v 12 Yeye huyazungusha mawingu kwa uongozi wake, ili yafanye chochote anayoyaagiza juu ya uso wote wa ulimwengu.
\v 13 Huyafanya haya yote yatokee; wakati mwingine hutokea kwa ajili ya kusahihisha, wakati mwingine kwa ajili ya nchi yake, na wakati mwingine ni kwa matendo ya agano la uaminifu.
\s5
\v 14 Yasikilize haya, Ayubu; acha na ufikiri juu matendo ya ajabu ya Mungu.
\v 15 Je unajua ni kwa namna gani Mungu hushurutisha mawingu na kuufanya mwanga wa radi ung'ae ndani yake?
\s5
\v 16 Je unafahamu kuelea kwa mawingu, matendo ya ajabu ya Mungu, Je ni nani aliyemkamilifu katika maarifa?
\v 17 Je unafahamu ni kwa jinsi gani mavazi yako huwa ya moto wakati nchi ikiwa imetulia kwasababu ya upepo unaotoka upande wa kusini?
\s5
\v 18 Je unaweza kulitandaza anga kama anavyofanya - anga ambalo lina nguvu kama kioo cha chuma kigumu?
\v 19 Tufundishe sisi kile tunachopaswa kumwambia yeye, kwa kuwa hatuwezi kutoa hoja zetu katika mpangilio kwasababu ya kiza katika akili zetu.
\v 20 Je anapaswa kuambiwa kwamba ninapenda kuongea naye? Je mtu angependa kumezwa?
\s5
\v 21 Sasa, watu hawawezi kulitazama jua wakati linang'aa katika anga baada ya upepo kupita katikati yake na umelisafisha kwa mawingu yake.
\v 22 Kutoka upande wa kaskazini hutokea fahari ya dhahabu - juu ya Mungu kuna ukuu wa kutisha.
\s5
\v 23 Na kuhusu Mwenye nguvu, hatuwezi kumpata; yeye ni mkuu katika nguvu na haki. Yeye hatesi watu.
\v 24 Hivyo basi, watu humwogopa. Yeye huwa hawajali wale ambao ni wenye hekima katika akili zao wenyewe."
\s5
\c 38
\p
\v 1 Ndipo Yahweh alimwita Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kumwambia,
\v 2 "Huyu ni nani aletaye giza katika mipango kwa njia ya maneno bila maarifa?
\v 3 Basi sasa jifunge kiunoni mwako kama mwanaume kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
\s5
\v 4 Wewe ulikuwa wapi wakati nilipoitandaza misingi ya dunia? Niambie, kama unao ufahamu zaidi.
\v 5 Je ni nani aliyeamuru vipimo vyake? Niambie, kama unajua, ni nani alivinyosha vipimo juu yake?
\s5
\v 6 Misingi yake ilitandazwa juu ya nini? Ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni
\v 7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
\s5
\v 8 Ni nani huifunga bahari kwa milango wakati inapofurika, kana kwamba inatoka katika tumbo,
\v 9 wakati nilipoyafanya mawingu kuwa ni mavazi yake, na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia?
\s5
\v 10 Hapo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu, na nilipoweka makomeo yake na milango,
\v 11 na wakati nilipoiambia, 'Unaweza kuja hapa kutoka mbali, lakini si zaidi; na hapa ndipo nitauweka mpaka kwa fahari ya mawimbi yako.'
\s5
\v 12 Je tangu mwanzo wa siku zako, ulishawahi kuigiza asubuhi ianze, na kuyafanya mapambazuko yajue sehemu yake katika mpangilio wa vitu,
\v 13 ili kwamba ishikilie sehemu za dunia ili watu waovu watikiswe mbali nayo.
\s5
\v 14 Dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhuri; vitu vyote husimama juu yake dhahiri kama cha kibindo cha nguo.
\v 15 'Mwanga' wao umeondolewa kutoka kwa watu waovu; na mkono wao ulioinuliwa umevunjwa.
\s5
\v 16 Je umeshaenda kwenye vyanzo vya maji ya bahari? Je umeshatembea sehemu za chini kabisa za kilindi?
\v 17 Je malango ya mauti yamefunuliwa kwako? Je umeshaona malango ya uvuli wa mauti?
\v 18 Je umeifahamu dunia katika upana wake? Niambie kama unayajua yote hayo.
\s5
\v 19 Je iko wapi njia ya sehemu ya kupumzikia kwa mwanga, na kama ilivyo kwa giza, iko wapi sehemu yake?
\v 20 Je unaweza kuuongoza mwanga na giza katika sehemu zake za kazi? Waweza kuitambua njia ya kurudi katika nyumba zao?
\v 21 Bila shaka unajua, kwa kuwa ulizaliwa wakati huo; hesabu ya siku zako ni kubwa sana!
\s5
\v 22 Je ulishaingia katika ghala ya barafu, au umeshaiona ghala ya mawe ya mvua,
\v 23 vitu hivi nimeviweka kwa ajili ya siku za mateso, kwa siku za mapigano na vita?
\v 24 Je iko wapi njia ya mshindo wa mwanga hutokea au je upepo husambazwa kutoka mashariki juu ya dunia?
\s5
\v 25 Ni nani aliyezitengeneza mifereji ya gharika ya mvua, au ni nani aliyezifanya njia za milipuko ya radi,
\v 26 na kuifanya mvua inyeshe juu ya nchi ambazo hakuna mtu aishiye ndani yake, na juu ya jangwa, ambayo ndani yake hakuna mtu yeyote,
\v 27 kwa kusudi la kutimiza mahitaji ya mikoa iliyo kame na yenye ukiwa, na kuyastawisha majani mororo?
\s5
\v 28 Je kuna baba wa mvua? Ni nani aliyeyafanya matone ya umande?
\v 29 Je barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na ni nani aliyeizaa theluji nyeupe katika anga?
\v 30 Maji hujificha menyewe na kuwa kama jiwe; sehemu za juu za vilindi huwa kama barafu.
\s5
\v 31 Je unaweza kuzifunga minyororo ya Kilimia, au kuvifungua vifundo vya Orioni?
\v 32 Je unaweza kuziongoza nyota kutokea katika nyakati zake? Je waweza kuongoza dubu pamoja na watoto wake?
\v 33 Je unazijua sheria za anga? Wewe uliweza kuanzisha sheria za anga juu ya dunia?
\s5
\v 34 Je waweza kupaza sauti yako hadi mawinguni, ili kwamba maji mengi ya mvua yakufunike?
\v 35 Je waweza kuagiza miali ya mwanga ili itokee, na kukwambia, 'Sisi tupo hapa'?
\s5
\v 36 Ni nani ameweka hekima katika mawingu au ni nani ameweka ufahamu kwa ukungu?
\v 37 Nani anaweza kuyahesabu mawingu kwa maarifa yake? Na ni nani awezaye kuvimwaga viriba vya anga
\v 38 wakati mavumbi yanapoungana kuwa kitu kigumu na mabonge ya dunia yanaposhikama kwa pamoja?
\s5
\v 39 Je waweza kuwinda mawindo kwa ajili ya simba jike au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba
\v 40 wakati wanapokwaruza kwaruza katika pango lao na kukaa katika kificho ili kulala katika hali ya kuvizia?
\s5
\v 41 Ni nani aletaye mawindo kwa ajili ya kunguru wakati ambapo watoto wao wanapomlilia Mungu na kutangatanga kwa kukosa chakula?
\s5
\c 39
\p
\v 1 Je unajua ni wakati gani mbuzi mwitu huzaa watoto wao katika miamba? Je waweza kuwangalia paa wakati wanapozaa watoto wao?
\v 2 Waweza kuhesabu miezi ya kuchukua mimba? Je unaujua muda ambao huzaa watoto wao?
\s5
\v 3 Wanainama chini na kuzaa watoto wao, na kisha maumivu yao ya uzazi yanaishi.
\v 4 Watoto wao huwa na nguvu na kukua katika uwanda wa wazi; hutoka nje na hawarudi tena.
\s5
\v 5 Ni nani huwaacha punda mwitu waende huru? Je nani amevilegeza vifungo vya punda wepesi,
\v 6 ni nyumba ya nani nimeifanya katika Araba, au nyumba yake katika nchi ya chumvi?
\s5
\v 7 Hucheka kwa dharau katika kelele katika mji; hasikilizi kelele za mwongozaji.
\v 8 Hutembeatembea juu ya milima kama malisho yake; huko hutafuta kila mmea ulio wa kijani kwa ajili ya kula.
\s5
\v 9 Je nyati atakuwa na furaha kukutumikia? Je atakubali kukaa katika zizi lako?
\v 10 Waweza kumwongoza nyati kulima mtaro kwa kamba? Je atachimba bonde kwa ajili yako?
\s5
\v 11 Je waweza kumtumaini kwasababu ya nguvu zake nyingi? Je waweza kumwachia kazi yako ili aifanye?
\v 12 Je waweza kumtegemea akuletee nyumbani nafaka, au kukusanya nafaka katika uwanda wako wa kupuria?
\s5
\v 13 Mabawa ya mbuni hupunga kwa majivuno, bali je mabawa na manyoya yana upendo?
\v 14 Kwa maana huuacha mayai yake katika nchi, na huyaacha yapate joto katika mavumbi;
\v 15 husahau kuwa mguu waweza kuyaharibu au kwamba mnyama mwitu aweza kuyakanyaga.
\s5
\v 16 Huyatendea vibaya makinda yake kana kwamba si yake; haogopi kwamba kazi yake yaweza kupotea bure,
\v 17 kwasababu Mungu amemnyima hekima na hajampa ufahamu wowote.
\v 18 Na wakati anapokimbia kwa haraka, huwacheka kwa dharau farasi na mpanda farasi wake.
\s5
\v 19 Je umempa farasi nguvu zake? Je umeivika shingo yake kwa manyoya?
\v 20 Je umemfanya aruke kama panzi? Enzi ya mlio wake ni wa kutisha.
\s5
\v 21 Hurarua kwa nguvu na kufurahia katika nguvu zake; hukimbia upesi kukutana na silaha.
\v 22 Huidharau hofu na hashangazwi; huwa harudi nyuma kutoka katika upanga.
\v 23 Podo hugongagonga ubavuni mwake, pamoja na mkuki unaong'aa na fumo.
\s5
\v 24 Huimeza nchi kwa hasira na ghadhabu; katika sauti ya tarumbeta, hawezi kusimama sehemu moja.
\v 25 Wakati wowote tarumbeta inapolia, husema, 'Ooh! Huisikia harufu ya vita kutoka mbali - vishindo vya radi za makamanda na makelele.
\s5
\v 26 Je ni kwa hekima yako kwamba mwewe hupaa juu, na ya kuwa huyanyosha mabawa yake kwa upande wa kusini?
\s5
\v 27 Je ni kwa agizo lako kwamba tai huruka juu na kufanya kiota chake katika sehemu za juu?
\v 28 Huishi katika majabali na hufanya makao yake katika vilele vya majabali, na ngomeni.
\s5
\v 29 Kutoka huko hutafuta mawindo; macho yake huyaona mawindo kutoka mbali.
\v 30 Makinda yake hunywa damu pia; na pale walipo watu wafu, ndipo na yeye alipo.
\s5
\c 40
\p
\v 1 Yahweh aliendelea kuongea na Ayubu na kusema,
\v 2 "Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi? Na yeye anayehojiana na Mungu, na ajibu yeye."
\s5
\v 3 Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, "
\v 4 Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu.
\v 5 Ninazungumza mara moja, na sitakujibu; hakika, mara mbili, lakini sitaendelea zaidi."
\s5
\v 6 Kisha Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kusema,
\v 7 "Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume, kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
\s5
\v 8 Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki? Je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki?
\v 9 Je una mkono kama wa Mungu? Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye?
\s5
\v 10 Jivike sasa katika utukufu na katika utu; jivalie mwenyewe heshima na enzi.
\v 11 Sambaza ziada ya hasira yako; mtazame kila mmoja mwenye kiburi na umshushe chini.
\s5
\v 12 Mwangalie kila mmoja mwenye kiburi na umweke chini; wakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama.
\v 13 Wazike ardhini pamoja; zifunge nyuso zao katika sehemu zilizositirika.
\v 14 Ndipo pia nitakapokubali ya kwamba mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
\s5
\v 15 Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe.
\v 16 Ona sasa, nguvu zake ziko katika viuno vyake; nguvu zake zi katika mishipa ya tumbo lake.
\s5
\v 17 Yeye huuondoa mkia wake kama mti wa mwerezi; mishipa ya paja lake imeunganishwa pamoja.
\v 18 Mifupa yake ni kama ya mirija ya shaba; na miguu yake ni kama kipande cha chuma.
\s5
\v 19 Yeye ni mkuu wa viumbe vya Mungu. Ni Mungu pekee, ambaye alimwumba, anaweza kumshinda.
\v 20 Kwa kuwa milima humpatia chakula; hayawani wa mashambani hucheza karibu.
\v 21 Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope.
\s5
\v 22 Miti yenye vivuli humfunika katika vivuli vyake; mierebi ya kijito inamzunguka pande zote.
\v 23 Tazama, kama mto utazigharikisha kingo zake, hatikisiki; yeye anajiamini, hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake.
\v 24 Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano, au kuichoma pua yake kwa mtego?
\s5
\c 41
\p
\v 1 Je waweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki? Au kumfunga taya zake kwa kamba?
\v 2 Je waweza kuweka kamba katika pua zake, au kumtoboa taya yake kwa ndoano?
\v 3 Je atafanya maombi mengi kwako? Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?
\s5
\v 4 Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?
\v 5 Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege? Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?
\v 6 Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara? Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?
\s5
\v 7 Je waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?
\v 8 Weka mkono wako juu yake mara moja, nawe utaikumbuka vita na hautaendelea kufanya hivyo tena.
\v 9 Tazama, matumaini ya kila mtu ambaye hufanya hivyo ni uongo; je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?
\s5
\v 10 Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba; Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?
\v 11 Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa? Chochote kilicho chini ya anga ni changu.
\v 12 Sitanyamaza kimya kuhusu miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.
\s5
\v 13 Nani awezaye kuiondoa ngozi yake? Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?
\v 14 Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?
\v 15 Mgongo wake umefanywa kwa magamba yenye mistari, yamefungwa kwa pamoja kama chapa.
\s5
\v 16 Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.
\v 17 Yameunganishwa moja kwa jingine; yamegandamana kwa pamoja, ili kwamba hayawezi kutenganishwa.
\v 18 Mwanga hung'ara kutoka katika kupumua kwake; macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi.
\s5
\v 19 Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje.
\v 20 Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.
\v 21 Pumzi yake huwasha mkaa na kuwa mwali; moto hutoka katika mdomo wake.
\s5
\v 22 Katika shingo yake kuna nguvu, na kitisho hucheza mbele yake.
\v 23 Nofu za mwili wake zimeunganishwa pamoja; ziko imara katika yeye; wala haziwezi kuondolewa.
\v 24 Moyo wake ni mgumu kama jiwe - hakika, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.
\s5
\v 25 Na anaposimama mwenyewe, hata miungu huogopa; hurudi nyuma kwasababu ya hofu.
\v 26 Na ikiwa atapigwa kwa upanga, hauwezi kumfanya kitu chochote, wala mkuki, wala mshale, wala aina yoyote ya silaha iliyochongoka.
\v 27 Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza.
\s5
\v 28 Mshale hauwezi akamfanya akimbie; kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.
\v 29 Marungu huyaangalia kama majani makavu; yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma.
\v 30 Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu; huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.
\s5
\v 31 Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto; huifanya bahari kama chungu cha lihamu.
\v 32 Yeye huifanya njia ing'are nyuma yake; mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.
\s5
\v 33 Hakuna cha kumlinganisha juu ya dunia, ambaye yeye alikuwa ameumbwa kuishi pasipo hofu.
\v 34 Hukiona kila kitu chenye kiburi; yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi."
\s5
\c 42
\p
\v 1 Kisha Ayubu akamjibu Yahweh na kusema,
\v 2 "Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa.
\v 3 Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango? Kwa kweli nilisema mambo ambayo sikuyaelewa, mambo magumu kwangu kuyafahamu, ambayo juu yake sikujua chochote.
\s5
\v 4 Uliniambia, 'Sikiliza sasa, nami nitasema; nitakuuliza mambo, nawe utaniambia.'
\v 5 Nimekuwa nikikusikia kwa usikivu wa sikio langu, lakini sasa jicho langu linakuona wewe.
\v 6 Basi ninajidharau mwenyewe; ninatubu kwa mavumbi na majivu."
\s5
\v 7 Ilitokea baada ya kuwa amekwisha kusema maneno hata kwa Ayubu, Yahweh alimwambia Elifazi Mtemani, " Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na dhidi ya marafiki zako wawili kwa kuwa hamkusema maneno ya haki juu yangu kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.
\v 8 Sasa basi, jitwalieni mafahari saba na mabeberu saba, kisha mmwendee mtumishi wangu Ayubu na mtoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Ndipo Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, nami nitayapokea maombi yake, ili kwamba nisiwashughulikie sawasawa na upumbavu wenu. Maana hamkusema mambo ya haki juu yangu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu."
\v 9 Basi Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Zofari Mnaamathi walienda na kufanya kama vile Yahweh alivyowaamuru, na Mungu alimtakabali Ayubu.
\s5
\v 10 Na wakati Ayubu alimpowaombea rafiki zake, Yahweh alirejeza bahati yake. Yahweh alimjalia mara mbili ya kile alichokimiliki hapo awali.
\v 11 Ndipo ndugu zake na Ayubu, na wale jamaa zake wote walikuwa wanajuana naye hapo mwanzo, walikuja hapo kwake na kula chakula pamoja naye katika nyumba yake. Waliomboleza pamoja naye na walimfariji kwa ajili majanga yote ambayo Yahweh alikuwa ameyaleta juu yake. Kila mtu alimpa Ayubu kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
\s5
\v 12 Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
\v 13 Pia alikuwa na wana saba na mabinti watatu.
\v 14 Binti wa kwanza alimwita Yemima, na wa pili Kezia, na wa tatu Kerenihapuki.
\s5
\v 15 Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao.
\v 16 Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne.
\v 17 Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.