sw_ulb_rev/15-EZR.usfm

532 lines
34 KiB
Plaintext

\id EZR
\ide UTF-8
\h Ezra
\toc1 Ezra
\toc2 Ezra
\toc3 ezr
\mt Ezra
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Yahwe akatimiza neno lake ambalo Yeremia alisema, na kuinua roho ya Koreshi. Sauti ya Koreshi ikasambaa na kusikika katika ufalme wake. Hiki ndicho kilichoandikwa na kusemwa:
\v 2 "Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa mimi ufalme wote wa dunia, na ameniteua mimi kumjengea yeye nyumba katika Yerusalem ya Yuda.
\s5
\v 3 Yeyote katika watu wake (Mungu awe pamoja naye) anaweza kwenda Yerusalem na kujenga nyumba kwa ajili ya Yahwe, Mungu wa Israel, Mungu ambaye yuko Yerusalem.
\v 4 Watu wa kila sehemu katika ufalme waliosalia katika nchi na kuishi wanapaswa kuwapa wao fedha na dhahabu, mali na wanyama, pamoja na kutoa kwa hiari kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem."
\s5
\v 5 Ndipo wakuu wa jamii ya Yuda na Benjamini, makuhani na walawi, na kila mmoja ambaye Roho wa Mungu alimwinua kuondoka na kujenga nyumba yake alisimama.
\v 6 Wale waliowazunguka karibu waliwasaidia kwa kuwapa fedha na vitu vya dhahabu, mali, wanyama, vitu vya thamani, na kutoa kwa hiari.
\s5
\v 7 Mfalme Koreshi akarusu vitu ambavyo vilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambavyo Nebukadreza alitoa kutoka Yerusalem na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.
\v 8 Koreshi akavikabidhi kwenye mikono ya Mithredathi mtunza fedha, ambaye akavitoa na kuhesabu kwa Sheshbaza, kiongozi wa Yuda
\s5
\v 9 Hii ilikuwa idadi yake: beseni thelathini za dhahabu, beseni elfu moja za fedha, beseni zingine ishirini na tisa,
\v 10 mabakuli thelathini ya dhahabu, mabakuli madogo ya fedha 410, na vitu elfu moja vya kuongezea.
\v 11 Kulikuwa na vitu 5, 400 vya fedha na dhahabu. Sheshbaza akavileta vyote wakati wa uhamisho kutoka Babeli kwenda Yerusalem.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hawa ndio watu katika jimbo waliochukuliwa mateka na kwenda na mfalme Nebukadneza, yeye aliwachukua utumwani Babeli, watu wakarudi katika miji yao ya Yerusalem na Yuda.
\v 2 Walikuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari., Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndio idadi ya wanaume ya watu wa Israeli.
\s5
\v 3 Waporoshi: 2, 172
\v 4 Wana wa Shefatia: 372
\v 5 Wana wa Ara: 775.
\v 6 Wana wa Path-Moabu, kupitia Yeshua na Yoabu: 2, 812.
\s5
\v 7 Wana wa Eliamu: 1, 254.
\v 8 Wana wa Zatu: 945.
\v 9 Wana wa Zakai: 760.
\v 10 Wana wa Binui: 642.
\s5
\v 11 Wana wa Bebai: 623.
\v 12 Wana wa Azgadi: 1, 222.
\v 13 Wana wa Adonikamu: 666.
\v 14 Wana wa Bigwai: 2, 056.
\s5
\v 15 Wana wa Adini: 454.
\v 16 Wana wa Ateri kupitia Hezekiah: tisini na nane.
\v 17 Wana wa Besai: 323.
\v 18 Wana wa Harifu: 112.
\s5
\v 19 Wanaume wa Hashimu: 223.
\v 20 Wanaume wa Gibeoni: Tisini na tano.
\v 21 Wanaume wa Bethlehemu: 123.
\v 22 Wanaume wa Netofa: Hamsini na sita.
\s5
\v 23 Wanaume wa Anathothi: 128.
\v 24 Wanaume wa Beth-Azmawethi: Arobaini na mbili.
\v 25 Wanaume wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi: Mia saba arobaini na tatu.
\v 26 Wanaume wa Rama na Geba: 621.
\s5
\v 27 Wanaume wa Mikmashi: 122.
\v 28 Wanaume wa Betheli, na Ai: 223.
\v 29 Wanaume wa Nebo: Hamsini na mbili.
\v 30 Wanaume wa Magbishi: 156.
\s5
\v 31 Wanaume wengine wa Elamu: 1, 254.
\v 32 nne. Wanaume wa Harimu: 320.
\v 33 Wanaume wa Lodi, na Hadidi, na Ono: 725.
\s5
\v 34 Wanaume wa Yeriko: 345.
\v 35 Wanaume wa Senaa: 3, 630.
\s5
\v 36 Wana wa Yedaya kuhani wa nyumba ya Yoshua: 973.
\v 37 Wana wa Imeri: 1, 052.
\v 38 Wana wa Pashuri: 1, 247.
\v 39 Wana wa Harimu: 1, 017.
\s5
\v 40 Walawi: Wana wa Yeshua, na Kadmieli, wana wa Hodavia: Sabini na
\v 41 nne. Waimbaji hekaluni wana wa Asafu: 128.
\v 42 Walinzi: wana wa Shalumu, Ateri na, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai: 139 jumla.
\s5
\v 43 Wale walichaguliwa kuhudumu ndani ya Hekalu: wana wa Siha, Hasufa, Tabaothi:
\v 44 Keros, Siaha, Padoni.
\v 45 Lebana, Hagaba, Akubu,
\v 46 Hagabu, Salmai, Hanani
\s5
\v 47 Wana wa Gideli, Gahari, Reaya,
\v 48 Resini, Nekoda, Gazamu,
\v 49 Uza, Pasea, Besai,
\v 50 Asna, Meunimu, Nefusimu:
\s5
\v 51 Wana wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri:
\v 52 Basluthi, Mehida, Barsha:
\v 53 Barkosi, Sisera, Tema:
\v 54 Nesia, Tefa
\s5
\v 55 Wana wa watumishi wa Selemani: Wana wa Sotai, Soferethi, Peruda,
\v 56 Yaala, Darkoni, Gideli,
\v 57 Shefatia, Hatili, Pokereth-Sebaimu, Amoni,
\v 58 Walikuwa jumla ya watumishi mia tatu tisini na mbili waliochaguliwa kutumika katika Hekalu pamoja na wana wa watumishi wa Selemani.
\s5
\v 59 Wale ambao walitoka Tel-mela, Tel-harsha, Kerubu, Adani, na Imeri, Lakini hawakuweza kuthibitisha kizazi chao kilitoka Israeli-
\v 60 pamoja na mia sita hamsini na mbili wana wa Delaya, Tobia na Nekoda.
\s5
\v 61 Vilevile, kutoka kwa wana wa kuhani: Wana wa Habaya, Hakosi, Barzilai {ambaye alipata mke kutoka kwa binti ya Barzilai, Mgileadi na akaitwa kwa jina lao}
\v 62 Walitafuta kumbukumbu ya kizazi chao, lakini haikupatikana, hivyo wakaondolewa kwenye ukuhani kama wasiosafi.
\v 63 Hivyo kiongozi akawakataza wasile kitu chochote kitakatifu kilichotakaswa mpaka kuhani mwenye Urimu na Thumimu athibitishe.
\s5
\v 64 Jumla ya kundi 42, 360,
\v 65 ukiondoa watumishi na wasaidizi (wao walikuwa 7, 337) waimbaji Hekaluni wanaume na wanawake (mia mbili)
\s5
\v 66 Farasi wao: 736, Nyumbu wao: 245.
\v 67 Ngamia wao: 435. Punda wao: 6, 720.
\s5
\v 68 Walipokwenda kwenye nyumba ya Yahwe Yerusalem, wakuu wa mababa walijitoa kwa hiari kujenga nyumba.
\v 69 Walitoa kadiri ya uwezo wao katika kufadhili kazi: Dhahabu za darkoni sitini na moja elfu, mane za fedha elfi tano na mavazi mia moja ya makuhani.
\s5
\v 70 Basi makuhani na walawi, watu, waimbaji hekaluni, na walinzi wa getini, na wale waliochaguliwa kutumika katika Hekalu walikaa katika miji yao. Watu wote katika Israel walikuwa katika miji yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ilikuwa miezi saba baaada ya watu wa Israeli kurudi kwenye miji yao, ndipo walipojikusanya pamoja kama mtu mmoja katika Yerusalem.
\v 2 Yeshua mwana wa Yosadaki na kaka yake kuhani, na Zerubabeli mwana wa Sheatieli na kaka yake wakainuka na kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli na kutoa sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa katika sheria ya Musa, Mtu wa Mungu.
\s5
\v 3 Ndipo wakaanzisha madhabahu juu ya msingi, kwa hofu waliokuwa nayo kwa sababu ya watu wa nchi/ Wakatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe asubuhi na jioni.
\v 4 Pia vilevile wakaichunguza sikukuu ya vibanda kama ilivyoandikwa na wakatoa sadaka ya kuteketezwa siku kwa siku kama ilivyoagizwa, kila siku kwa siku yake.
\v 5 Kulikuwa na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa na mwezi mara moja na sadaka za siku ya Yahwe za kudumu, pamoja na sadaka zote za hiari.
\s5
\v 6 Walianza kutoa sadaka za kuteketezwa za Yahwe siku ya kwanza ya mwezi wa saba, ingawa hekalu lilikuwa halijaanza kujengwa.
\v 7 Hivyo wakatoa fedha kwa wahunzi na fundi wa mkono, na wakawapa chakula, vinywaji na mafuta kwa watu wa Sidoni na Tiro, ili kwamba walete miti ya mierezi kupitia baharini kutoka Lebanoni mpaka Yafa, na kama walivyo ruhusiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi.
\s5
\v 8 Ndipo mwezi wa pili katika mwaka wa pili baadae wakaja kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem, Zerubabeli, Yoshua mwana wa Yosadaki, na baadhi ya makuhani na walawi na wale walikuja kutoka uhamishoni kurudi Yerusalem wakaanza kazi. Wakawachagua walawi walikuwa na miaka ishirini na zaidi kusimamia kazi ya nyumba ya Yahwe,
\v 9 Yoshua akamsimamisha kijana wake na kaka yake, Kadmiel na watoto wake, na kizazi cha yuda kusimamia kufanya kazi katika nyumba ya Mungu. Pamoja na wao kulikuwa na wana wa Henadadi, na uzao wao, na pia jamaa zao walawi.
\s5
\v 10 Wajenzi wakasimamisha msingi wa Hekalu la Yahwe, Na hii ikawawezesha makuhani kusimama na mavazi yao wakiwa na tarumbeta, na walawi wana wa Asafu, kumtukuza Yahwe kwa matoazi, kama mkono wa mfalme Daudi wa Israel alivyoagiza.
\v 11 Waliimba kwa kumsifu na kumshukuru Yahwe. "Yeye ni mwema! Agano lake ni kweli kwa Israel ladumu milele."Watu wote wakapiga kelele kwa sauti kuu za shangwe wakimsifu Yahwe kwa sababu misingi ya Hekalu ilikuwa imekamilika.
\s5
\v 12 Lakini wengi wa Makuhani, walawi, wakuu wa kale, na wazeee wa zamani walioiona nyumba ya kwanza, wakati misingi ilipowekwa wakaishuhudia kwa macho yao, walilia kwa sauti. Lakiniwengi walipiga kelele kwa sauti za shangwe na furaha na sauti za kushangaza.
\v 13 Na matokeo yake, watu hawakuweza kutofautisha sauti za furaha na sauti za shangwe na sauti za watu waliokuwa wanalia, kwa kuwa watu walikuwa wanalia kwa sauti kuu ya shangwe na sauti ilisikika kutoka mbali.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ndipo maadui wa Yuda na Benjamini waliposikia kwamba watu waliokuwa uhamishoni walikuwa wanajenga Hekalu la Yahwe, Mungu wa Israel.
\v 2 Hivyo wakamkaribia Zerubabeli na wakuu wa jamii yao. Wakawaambia,: Mturuhusu tujenge pamoja nanyi, kama ninyi, tunamtafuta mungu wenu, na tumejitoa kwake tangu siku ambapo, Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru alipotuleta mahali hapa."
\s5
\v 3 Lakini Zerubabeli, Yoshua na wakuu wa kale wa jamii wakasema, "sio wewe, lakini sisi ndio tunaowajibika kujenga nyumba ya Mungu wetu, Sisi ndio tutakaomjengea Yawe, Mungu wa Israel, kama vile mfalme koreshi mfalme wa Ashuru alivyoagiza."
\s5
\v 4 Hivyo watu wa nchi wakadhoofisha mikono ya wayahudi, wakawafanya wayahudi waogope kujenga nyumba.
\v 5 Pia wakawahonga washauri ili kuwachanganya katika mipango yao. Walitenda haya kipindi chote cha Koreshi na kipindi cha utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.
\v 6 Tena katika kuanza kutawala kwake Ahasuero wakaandika mashitaka dhidi ya wenyeji wa Yuda na Yerusalem
\s5
\v 7 Ilikuwa siku za Ahasuero ambazo Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzake wakamwandikia Ahasuero. Barua iliandikwa Kiaramu na kutafsiliwa.
\v 8 Rehumu jemedari na Shimshai mwandishi wakaandika hivi kwa Artashasta kuhusu Yerusalem.
\s5
\v 9 Tena Rehumu, Shimshai na wenzao ambao ni waamuzi na maofisa wengine wa Serikali, kutoka Waarkewi, Wababeli na washushami katika Waelami,
\v 10 nao wakaandika barua na waliungana na watu wakuu na mheshimiwa Asur - bani - pali aliwalazimisha kukaa Samalia pamoja na waliobaki katika mji ngambo ya mto.
\s5
\v 11 Hii ni nakala waliotuma kwa Artashasta: "Watumishi wako, watu wa mji ngambo ya mto, waandika hivi:
\v 12 Mfalme atambue kwamba Wayahudi waliotoka kwako wamefanya kinyume chetu hapa Yerusalem wamejenga mji wa uasi. Wamekamilisha ukuta na marekebisho ya misingi.
\s5
\v 13 Sasa mfalme atambue kwamba endapo mji utajengwa na kuta zake kukamilika, hawatatoa ushuru na kodi, lakini watawadhuru wafalme.
\s5
\v 14 Hakika kwa kuwa tumekula chumvi ya Ikulu, haitopendeza sisi kuona heshima ya mfalme inavunjwa, kwa sababu hiyo tunamtaarifu mfalme
\v 15 kufanya uchunguzi wa kumbukumbu ya baba yake, na kujiridhisha kuwa mji huu ulikuwa wa uharibifu ambao utawadhuru wafalme na miji. Ulisababisha matatizo mengi kwa wafalme na miji. Ilikuwa ni kitovu cha uhalibifu tokea siku nyingi. Ni kwa sababu hiyo mji uliteketezwa.
\v 16 Tunamtaarifu mfalme kuwa endapo mji na ukuta ukijengwa, Hakuna kitakachobakia kwa ajili yako katika mji ngambo ya mto."
\s5
\v 17 Ndipo mfalme akarudisha majibu kwa Rehumu na Shimshai na wenzao katika Samalia na waliobaki katika mji ngambo ya mto. "Amani iwe pamoja nanyi.
\v 18 Barua mliyonitumia imetafsiliwa na kusomwa kwangu.
\v 19 Hivyo niliagiza uchunguzi ufanywe na ikabainika kwamba zamani uliasi na kuwafitinisha wafalme.
\s5
\v 20 Wafalme wakuu walitawala Yerusalem yote na kuongoza kila sehemu ya mji ngambo ya mto. Ada na kodi walilipwa.
\v 21 Sasa, wekeni agizo kwa watu hawa wasiendelee na kujenga mji mpaka nitakapotoa amri.
\v 22 Muwe waangalifu msipuuze hili. Kwa nini kuruhusu tishio hili kuongezeka na kusababisha hasara kwa matakwa ya ufalme?
\s5
\v 23 Baada ya amri ya mfalme Artashasta kusomwa mbele ya Rehumu, Shimshai na wenzao, wakaondoka haraka kwenda Yerusalem, na wakawalazimisha Wayahudi kuacha kujenga.
\v 24 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu Yerusalem ikasitishwa mpaka kutawala mara ya pili kwa mfalme Dario wa Uajemi.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ndipo Hagai nabii na Zakaria mtoto wa Ido nabii wakatabiri kwa jina la Mungu wa Israel kwa wayahudi wa Yuda na Yerusalem.
\v 2 Zerubabeli mtoto wa Shealtieli na Yoshua mtoto wa Yosadaki wakainuka na kuanza kujenga nyumba ya Mungu Yerusalem pamoja na manabii ambao waliwahamasisha wao.
\s5
\v 3 Ndipo Tatenai Mkuu wa mji ngambo ya mto, Shethar - Bozenai, na mshirika wao, wakaja na kusema kwao, "Nani aliyewapa agizo la kujenga nyumba hii na kukamilisha ukuta?"
\v 4 Vilevile walisema, "Ni majina ya watu gani wanaoshughulika na ujenzi huu?"
\v 5 Lakini jicho la Mungu lilikuwa pamoja na viongozi wa Wayahudi na maadui wao hawakuweza kuwazuia. Walikuwa wakisubiri barua kutumwa kwa mfalme na amri kurudi kwao kwa ajili ya suala hili.
\s5
\v 6 Hii ni nakala ya barua kwa Tatenai, mkuu wa mji ngambo ya mto, na Shethar - Bozenai na wenzao katika mji ngambo ya Mto, ambao waliwatuma kwa mfalme Dario.
\v 7 Wakatuma ujumbe, wakiandika kwa mfalme Dario, "Amani tele iwe kwako"
\s5
\v 8 Mfalme atambue kwamba tulikwenda Yuda kwenye nyumba ya Mungu Mkuu. Imeshajengwa kwa mawe makubwa na mbao zimewekwa katika kuta. Hii kazi inafanyika kwa utaratibu na inaendelea vizuri kwa mikono yao.
\v 9 Tukawauliza wazee, ni nani aliyewapa agizo la kujenga nyumba na ukuta?'
\v 10 Pia tuliwauliza majina yao ili kwamba ujue majina ya kila mtu ambaye aliwaongoza.
\s5
\v 11 Nao wakatujibu na kusema, "Sisi tu watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi na sisi tunaijenga nyumba hii ambayo ilijengwa miaka mingi iliyopita wakati mfalme mkuu wa Israel alijenga na kuikamisha.
\s5
\v 12 Ingawa, watangulizi wetu walipomchukiza Mungu wa mbinguni, Mungu akawatia katika mikono ya mfalme wa Babeli Nebukadineza, ambaye alivunja nyumba na kuwachukua watu mateka Babeli.
\v 13 Pia, katika mwaka wa kwanza wa kutawala Koreshi mfalme wa Babeli, Koreshi aliamuru nyumba ya Mungu kujengwa.
\s5
\v 14 Mfalme Koreshi pia alirudisha vitu vya dhahabu na fedha vya nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kwenye hekalu Yerusalem na kuvipeleka kwenye hekalu Babeli. Naye akavitunza kwa Sheshbaza, ambaye alimchagua kuwa kiongozi.
\v 15 Naye akamwambia, "Chukua hivi vitu. Uondoke na kuviweka kwenye Hekalu Yerusalem. Na nyumba ya Mungu ijengwe kule."
\s5
\v 16 Ndipo huyu Sheshbaza akaja na kuweka msingi kwa nyumba ya Mungu katika Yerusalem: na ikaendelea kujengwa, lakini bado haijakamilika
\s5
\v 17 Sasa ikiwa itampendeza mfalme, na uchunguzi ufanyike kwenye nyumba ya ukumbusho Babeli Ikiwapo hukumu ya mfalme wa Koreshi ya kujenga nyumba ya Mungu Yerusalem. Na mfalme anaweza kutuma uamuzi wake kwetu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Na mfalme dario akaamuru uchunguzi ufanyike katika nyumba ya kumbukumbu Babeli.
\v 2 Na katika mji wa Akmetha huko media chuo kilionekana: Kumbukumbu yake ilisema:
\s5
\v 3 "Katika mwaka wa kwanza mfalme Koresh, Koreshi alitoa amri kuhusu nyumba ya Mungu Yerusalem:'Na nyumba ijengwe iwe sehemu ya kutoa dhabihu, misingi yake iwekwe, urefu wake uwe sitini,
\v 4 na upana wake uwe sitini, sehemu tatu za mawe makubwa na sehemu moja ya mbao mpya, na gharama hizo zitalipwa kutoka nyumba ya mfalme.
\v 5 Sasa vilirudishwe tena vitu vya dhahabu na fedha vilivyokuwa kwenye nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kuvipeleka Babeli kutoka kwenye Hekalu Yerusalem. Na avirudishe tena Yerusalem Hekaluni. Na utaviweka tena kwenye nyumba ya Mungu.
\s5
\v 6 Sasa Tetanai, mkuu wa jimbo ngambo ya mto, Shethar - Bozenai na wenzao walio katika mji ngambo ya mto, wakajitenga,
\v 7 wakaacha kazi ya nyumba ya Mungu pekee. Viongozi na wazee wa kiyahudi watajenga nyumba ya Mungu mahali pake.
\s5
\v 8 Ninatoa agizo kwamba lazima lifanyike kwa wazee wa kiyahudi wanaojenga nyumba ya Mungu: Mchango kutoka kwa mfalme ushuru ngambo ya mto, utatumika katika kuwalipa watu hawa ili kwamba kazi yao isiweze kusimama.
\v 9 Chochote kitakachohitajika, ngombe wachanga, kondoo au kondoo wa sadaka ya kutekezwa kwa ajili ya Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kadri ya maagizo ya makuhani wa Yerusalem - wapatie vitu hivi kila siku bila kikomo.
\v 10 fanya hivyo ili kwamba wataleta sadaka kwa Mungu wa mbinguni na wataomba kwa ajili yangu mfalme na watoto wangu.
\s5
\v 11 Mimi nina agiza kwamba yeyote atakayevunja amri hii, Chuma kitolewe katika nyumba yake. Na awekwe juu yake. Na nyumba yake itabadilishwa kuwa takataka kwa sababu hii.
\v 12 Mungu huyu aliyesababisha jina lake kuwepo atamwondoa mfalme au mtu atakayebadili agizo hili au kuondosha nyumba ya Mungu katika Yerusalem. Mimi Dario nimeagiza hili, lifanyike kwa makini.
\s5
\v 13 Na kwa sababu ya amri iliyotumwa na mfalme Dario, Tatenai kiongozi mji ngambo ya mto na Sheshthar -Bozenai na wenzao. wakafanya kila kitu kama Mfalme Dario alivyoagiza.
\v 14 Hivyo wazee wa kiyahudi wakajenga kama Hagai na Zakaria walivyoelekeza kwa kutabiri. Wakajenga kama amri ilivyotolewa na Mungu wa Israel na Koreshi, Dario na Artashasta mfalme wa Uajemi.
\v 15 Nyumba ikakamilika siku ya tatu ya mwezi wa adari, katika mwaka wa sita wa kutawala mfalme Dario.
\s5
\v 16 watu wa Israel, makuhani, walawi na watu waliobaki wa uhamisho wakasheherekea kuweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.
\v 17 Wakatoa ngombe mia moja, kondoo mia moja na kondoo wengine mia nne kwa ajili ya kuweka wakfu nyumba ya Mungu. Mbuzi wa kiume kumi na wawili walitolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya waisrael wote kila kabila katika Israel.
\v 18 Pia wakawapa wajibu makuhani na walawi kufanya mgawanyo wa kazi ya Mungu katika Yerusalem. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa.
\s5
\v 19 Hivyo wale waliokuwa utumwani wakasherehekea pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
\v 20 Makuhani na walawi wakajitakasa wenyewe na wakachinja pasaka ya sadaka kwa ajili ya waliokuwa mateka wakiwemo na wao wenyewe.
\s5
\v 21 watu wa Israel ambao walikula nyama ya Pasaka ni wale waliorudi kutoka uhamishoni na walikuwa wamejitenga wenyewe kutoka kwa watu wasio safi wa nchi ile na kumchagua Yahwe, Mungu wa Israel.
\v 22 Walifurahi na kushangilia siku kuu ya mikate isiyochacha kwa siku saba, kwa sababu Yahwe amewarejeshea furaha na ameugeuza moyo wa mfalme wa Ashuru, na kuwatia nguvu kwa kazi ya nyumba, nyumba ya Mungu wa Israel.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Sasa baada ya hili, kipindi cha kutawala Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra akaja kutoka Babeli. Watangulizi wa Ezra walikuwa: Seraya, Azaria, Hilkia,
\v 2 Shalumu, Sadoki, Ahitubu,
\v 3 Amaria, Azaria, Merayothi,
\v 4 Zerahia, Uzi, Buki,
\v 5 Abishaua, Fineasi, Eliazari ambaye ni mtoto wa Haruni kuhani mkuu.
\s5
\v 6 Ezra akaja kutoka Babeli na alikuwa mtalaam mwandishi wa sheria ya Musa, ambayo Yahwe, Mungu wa Israel aliwapa. Mfalme akampatia kila kitu alichooomba kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa pamoja naye.
\v 7 Baadhi ya wazao wa Israel, na makuhani, walawi, waimbaji, walinzi, na wale waliochaguliwa kuhudumu katika Hekalu pia wakaenda Yerusalem katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.
\s5
\v 8 Naye akafika Yerusalem mwezi wa tano kama mwaka huo.
\v 9 Naye akaondoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. Ilikuwa siku ya kwanza ya mwezi wa tano ambapo alifika Yerusalem, kwa kuwa mkono mzuri wa Mungu ulikuwa pamoja naye.
\v 10 Ezra alikuwa ametoa moyo wake kusoma, kutenda, na kufundisha maagizo na sheria za Yahwe.
\s5
\v 11 Hii ndio amri ambayo mfalme Artashasta alimpa Ezra kuhani na mwandishi wa sheria za Yahwe na maagizo kwa Israeli.
\v 12 Mfalme wa wafalme Artashasta, kwa kuhani Ezra, mwandishi wa sheria za Mungu wa mbinguni.
\v 13 Ninatoa amri kwamba mtu yeyote Israel katika ufalme wangu pamoja na makuhani na walawi ambao wanatamani kwenda Yerusalem, wanaweza kwenda pamoja na wewe.
\s5
\v 14 Mimi mfalme na washauri wangu saba, tunawatuma wote kwenda kufahamu kuhusu Yuda na Yerusalem kuhusiana na sheria ya Mungu, ambayo iko mkononi mwako.
\v 15 Itakupasa kuleta Dhahabu na fedha ambazo walitoa kwa ajili ya Mungu wa Israel, ambaye makazi yake ni Yerusalem.
\v 16 Fedha iliyotolewa kwa hiari na Dhahabu yote iliyotolewa Babeli pamoja na matoleo ya hiari waliotoa watu na makuhani kwa ajili ya nyumba ya Mungu katika Yerusalem.
\s5
\v 17 Basi ununue vyote sadaka ya kondoo, beberu, kondoo, unga na kinywaji, uvitoe kwenye madhabahu ambayo ni nyumba ya Mungu wako katika Yerusalem.
\v 18 Fanya hivyo pamoja na sehemu ya fedha na dhahabu, vyovyote utakavyoona inakupendeza wewe na ndugu zako, kumpendeza Mungu.
\s5
\v 19 Viweke vitu vilivyotolewa kwa hiari mbele yako kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu Yerusalem.
\v 20 Kitu chochote kingine ambacho kinahitajika kwenye nyumba ya Mungu wako ambacho unahitaji, Gharama yake itatoka kwenye hazina yangu.
\s5
\v 21 Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa wotunza hazina wote mjini ngambo ya mto, chochote Ezra atakachoomba kwenu anapaswa kupewa chote,
\v 22 hata zaidi ya talanta mia moja za fedha, vipimo mia vya ngano, bathi mia za divai na bathi mia za mafuta, pia na chumvi isiyo na kikomo.
\v 23 Chochote ambacho kimeamriwa kutoka kwa Mungu wa mbinguni, kifanye hicho kwa utukufu wa nyumba yake. Kwa nini hasira yake ije kwenye ufalme wangu na watoto wangu?
\s5
\v 24 Tutawapa taarifa wao kuhusu ninyi kwamba wasiwatoze ushuru wowote au kodi kwa kuhani, mlawi, mwimbaji, mlinzi au kwa mtu aliyechaguliwa kwenye huduma ya Hekalu na mtumishi katika nyumba ya Mungu.
\s5
\v 25 Ezra, kwa hekima aliyokupa Mungu, inakulazimu kuteua waamuzi na mtu muelewa kuwahudumia watu katika mji ngambo ya mto na kusaidia yeyote anayejua sheria za Mungu wako. Pia inakubidi ufundishe wale ambao hawajui sheria.
\v 26 Toa adhabu kwa yeyote asiyetii sheria ya Mungu au sheria ya mfalme, ikiwezekana kwa kifo, kuhamishwa, kuchukuliwa mali zake au kufungwa.
\s5
\v 27 Atukuzwe, Yahwe, Mungu wa watangulizi wetu, ambaye aliweka ndani ya moyo wa mfalme ili kutuza Nyumba ya Yahwe Yerusalem,
\v 28 ambaye akaendeleza agano kwangu kwa uaminifu mbele ya mfalme, na washauri wake na wakuu wake wenye mamlaka, nilitiwa nguvu na mikono ya Yahwe, Mungu wangu, nami nikawakusanya viongozi kutoka Israel kwenda pamoja nami.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Hawa ni viongozi wa watangulizi familia ambazo zilitoka babeli pamoja nami kipindi cha utawala wa mfalme Artashasta.
\v 2 Mwana wa Finehasi, Gershoni. Mwana wa Ithamari, Daniel. Mwana wa Daudi, Hatushi ambaye ni mwana Shekania,
\v 3 ambaye pia ni mwana wa Paroshi na Zekaria na pamoja na yeye kulikuwa na wanaume mia moja na hamsini walitajwa kwenye idadi ya ukoo wake.
\s5
\v 4 Wana wa Pahath- Moabu, Eliehoenai mwana wa Zerahia na pamoja naye wanaume mia mbili. Wana wa
\v 5 Shekaniah, Yahazieli na pamoja naye wanaume mia tatu. Wana wa
\v 6 adini, Ebedi mwana wa Yonathani na pamoja naye waliorodheshwa wanaume hamsini.
\v 7 Wana wa Elamu, Yeshaya mwana wa Athalia na pamoja naye waliorodheshwa wanaume sabini.
\s5
\v 8 Wana wa Shefatia, Zebadia, mwana wa Mikaeli na pamoja naye waliorodheshwa wanaume themanini.
\v 9 Wana wa Yoabu, Obadia mwana wa Yehieli pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia mbili kumi na wanane. Wana wa Binui,
\v 10 Sheromithi, mwana wa Yosifia na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na sitini.
\v 11 Wana wa Bebai, zekaria mwana wa Bebai na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume ishirini na wanane.
\s5
\v 12 Wana wa Azgadi, Yohana mwana wa Hakatani na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na kumi.
\v 13 Wale wana wa Adonikamu wakaja baadaye. Na haya ndio majina yao: Elifereti, Yeueli na Shemaya na pamoja na wao wakaja wanaume sitini.
\v 14 Wana wa Bigwai, Uthai, mwana wa zabudi na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume sabini
\s5
\v 15 Nikawakusanya wasafiri bandari iliyokuwa inaelekea Ahava. Tukaweka kambi muda wa siku tatu, nikawachunguza watu na makuhani, lakini sikuwaona wana wa Levi miongoni.
\v 16 Hivyo nikatuma kwa Eliezeri, arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu na Elnathani na Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na kwa Yoyaribu na Elnathani ambao walikuwa ni walimu.
\s5
\v 17 Tena nikawatuma kwa Ido, kiongozi wa Kasifia. Nikawaaambia kile watachomweleza Ido. na jamaa zake, watumishi wa Hekalu waliishi Kasifia, kwa hiyo, kutuma kwetu watumishi kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
\s5
\v 18 Hivyo wakatutuma sisi kwa Mungu na mkono mzuri wa mtu aliyeitwa Ishekeli. Alikuwa mwana wa mali Mwana wa Levi mwana wa Israel. Akaja na wana kumi na wanane na ndugu,
\v 19 pamoja naye Hashabia, pamoja na Yeshaya wa wana wa Merari na ndugu zake na wana wake jumla watu ishirini wote. Miongoni
\v 20 mwao walichaguliwa kutumika katika Hekalu, ambapo Daudi na wakuu waliwapa kuwahudumia walawi: mia mbili ishirini kila mmoja wao aliagizwa kwa majina.
\s5
\v 21 Tena nikatangaza kufunga mto Ahava ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, kutafuta njia iliyoonyoka kutoka kwake kwa ajili yetu, watoto wetu na mali zetu,
\v 22 Niliona aibu kumwomba mfalme kwa ajili ya jeshi au mpandafarasi kwa ajili ya kutulinda tunapokuwa njiani, tangu tumemwambia mfalme "mkono wa Mungu uko pamoja na wote wanaomtafuta kwa mazuri. lakini uweza wake na ghazabu yake ni juu ya wale wote wanaomwasi yeye.
\v 23 Hivyo tulifunga na kumsihi Mungu kwa jambo hilo.
\s5
\v 24 Tena nikachagua watu kumi na wawili kutoka kwa kuhani: Sherebia na Hashabia na ndugu zao wengine kumi.
\v 25 Nikapima kwa ajili yao fedha, dhahabu na vyombo na sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu kwa wafalme, washauri, na wakuu na Israel wote walitoa kwa hiari.
\s5
\v 26 Hivyo nikawapimia kwenye mikono yao talanta za fedha mia sita na hamsini, talanta mia moja ya vyombo vya fedha, talanta mia moja za dhahabu.
\v 27 vifaa ishirini vya dhahabu kwa pamoja vilikuwa na thamani ya elfu moja darkoni na vitu viwili vya sanamu vivyonakshiwa kama dhahabu ya kupendeza.
\s5
\v 28 Kisha nikawaambia, mmewekwa wakfu kwa Bwana, na hivi vyombo pia na fedha na dhahabu, vimetolewa kwa hiari kwa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu.
\v 29 mviangalie na kuvitunza hadi mtakapovipima mbele ya makuhani, walawi, na viongozi wa wataangulizi wa jamii ya Israel katika Yerusalem katika nyumba ya Mungu.
\v 30 Makuhani na walawi walikubali vipimo vya fedha na dhahabu na vyombo kwa ajili ya kuvichukua na kuvipeleka Yerusalem, kwenye nyumba ya Mungu wetu.
\s5
\v 31 Tukatoka kwenda mto Ahava siku ya kumi na mbili katika mwezi wa kwanza kwenda Yerusalem, Mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, ulitulinda na mikono ya adui na wale waliotaka kutufanyia fujo njiani.
\v 32 Hivyo tukaingia Yerusalem na kukaa humo kwa siku tatu.
\s5
\v 33 Tena siku ya nne fedha na dhahabu na vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa mikono ya Meremothi mwana wa Uria kuhani, na pamoja nao alikuwepo Eleazari mwana wa Finehasi, Yozabadi mwana wa Yeshua, na Noadia mwana wa Binui, Walawi.
\v 34 Idadi na uzito wa kila kitu uliweza kujulikana. Uzito wote uliweza kuandikwa katika kipindi hicho
\s5
\v 35 Na wale waliokuja kutoka matekani, watu wa uhamisho, wakatoa sadaka ya kutekezwa kwa Mungu wa Israel, kondoo tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi wa kiume kumi na wawili kama sadaka ya dhambi. Zote zilikuwa sadaka za kutekezwa kwa ajili ya Yahwe.
\v 36 Tena wakawapa amri za mfalme kwa wakuu wa wafalme na wakuu katika mji ngambo ya mto, na wakawasaidia watu na nyumba ya Mungu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kipindi mambo hayo yanatendeka, wakuu wakaja kwangu na kuniambia,"Watu wa Israel, Makuhani na walawi hawakuweza kujitenga wenyewe kutoka kwa watu wa nchi zingine na maovu yao: Wakanaani, Wahiti, Waperuzi, wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.
\v 2 Kwa kuwa wamewachukua baadhi ya binti na watoto wa kiume, wamejichanganya watu watakatifu na watu wa nchi nyingine na wakuu na viongozi wamekuwa wa kwanza katika imani hii potofu.
\s5
\v 3 Niliposikia haya, nikachana nguo zangu na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na nikakaa chini kutafakari.
\v 4 Na wale wote waliotetemeka kwa neno la Mungu wa Israel kuhusu imani potofu walikusanyika kwangu wakati nimakaa chini nikiwa na aibu hadi kufikia kipindi cha sadaka za jioni.
\s5
\v 5 Lakini katika sadaka ya jioni nikasimama kwenye nafasi yangu nikiwa mnyenyekevu na nguo ilichanika na kanzu, na nikapiga magoti na kunyoosha mikono yangu kwa Yahwe Mungu wangu. Nikasema
\v 6 "Mungu wangu, nina aibu na sistahili kuinua uso wangu kwako, makosa yetu yamekuwa hadi kuvuka kichwani na maovu yetu yameongezeka kufika mbinguni.
\s5
\v 7 Kuanzia siku ya watangulizi wetu mpaka sasa tumekuwa katika maovu makuu. Makosa yetu, viongozi, makuhani, walikuwa katika mikono ya mfalme wa dunia hii, katika upanga, matekani na kunyanyaswa na tuna aibu ya uso hata leo.
\s5
\v 8 sasa kwa kipindi kifupi, neema kutoka kwa Yahwe Mungu wetu imekuja kutuacha mabaki wachache na kutupa kuhimmili sehemu takatifu. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya Mungu wetu kututia nuru macho yetu na kutupa unafuuu sisi tulio watumwa.
\v 9 Kwa kuwa sisi tu watumwa, lakini Mungu bado hajatusahau lakini ameongeza agano la uaminifu kwetu, ameyatenda haya mbele ya macho ya mfalme wa Uajemi ili kwamba haweze kutupatia nguvu mpya. Ili kwamba tuweze kujenga nyumba ya Mungu na tuweze kuondoa majuto. Alitenda hayo ili kwamba aweze kutupatia msingi wa usalama katika Yuda na Yerusalem.
\s5
\v 10 Lakini sasa Mungu wetu, tuseme nini baaada ya haya? Tumesahau amri zako.
\v 11 amri ambazo uliwapa manabii watumishi wako, pale uliposema, "Nchi hii mnayoingia kuimiliki ni nchi chafu. Imechanganyikana na watu wasio na utaratibu. ameenea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa uchafu wao.
\v 12 Hivyo sasa, msiwape binti zenu kwa watoto wao, msichukue binti zao kwa ajili ya watoto wenu, msitafute amani kwao na fadhili, ili kwamba muweze kuwa imara na kula vizuri vya nchi, hivyo utasababisha watoto wenu kumiliki kwa wakati wote."
\s5
\v 13 Baada ya yote kutokea kwetu kwa sababu ya uovu wetu na makosa yetu makuu, tokea hapo, Mungu wetu, hukutazama makosa yetu na kutuadhibu tulivyostahili na ukatuacha kama mabaki.
\v 14 Tunaweza kuvunja tena amri zako na kuingiliana katika ndoa, na hawa watu wasiofuata utaratibu? Je hautachukia na kututowesha sote hakuna wa kubaki, hakuna wa kutoroka?
\s5
\v 15 Yahwe, Mungu wa Israel, wewe ni mwenye haki, kwa kuwa tumebaki wachache mabaki hadi siku ya leo. Tazama, tuko mbele yako na makosa yetu, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayeweza kusimama mbele kwa sababu ya hili.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa la wanaume Israel, wanawake na watoto wakakusanyika kwake, kwa kuwa watu walikuwa wakilia sana.
\v 2 Shekania mtoto wa Yehieli, mwana wa Elamu akamwambia Ezra, "Tumekuwa sio waaminifu kwa Mungu na tumeoa wanawake wa kigeni kutoka nchi nyingine. Lakini pamoja na hilo, bado kuna tumaini kwa Israel.
\s5
\v 3 sasa natuweke agano pamoja na Mungu wetu kuwaondoa wanawake wote na watoto wao kulingana na maelekezo ya Bwana, na maelekezo ya wale wanaotetemeka kutokana na amri za Mungu wetu. na hii ifanyike kutokana na sheria.
\v 4 Simama, jambo hili linakuhusu wewe, na sisis tuko pamoja na wewe, Uwe imara na kufanya hili.
\s5
\v 5 Hivyo Ezra akasimama na kufanya makuhani na walawi na waisrael wote wakaahidi kufanya kwa njia hiyo. Hivyo wote wakatoa kiapo.
\v 6 Ndipo Ezra akainuka kutoka mbele ya nyumba ya Mungu na kwenda kwenye chumba ya Yehohanani mtoto wa Eliashibu, Yeye hakula mkate au kunywa maji. Tangu alipokuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
\s5
\v 7 Hivyo wakatuma neno katika Yuda na Yerusalem kwa watu wote waliorudi kutoka utumwani kukusanyika Yerusalem.
\v 8 Yeyote ambaye hakuja katika siku tatu kutokana na maelekezo kutoka kwa wakuu na viongozi atachukuliwa mali zote na atatengwa na kusanyiko kuu la watu ambao walikuja kutoka uhamisho.
\s5
\v 9 Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
\v 10 Ezra kuhani akasimama na kusema, "Ninyi wenyewe mmefanya uasi, ninyi mmeishi na wanawake wa kigeni na kuongeza makosa ya Israel.
\s5
\v 11 Lakini sasa mpeni sifa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu, na mfanye mapenzi yake, mjitenge na watu wa nchi na wanawake wa kigeni.
\s5
\v 12 Kusanyiko lote likajibu kwa sauti. "Tutatenda kama ulivyosema,
\v 13 haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
\s5
\v 14 Hivyo wakuu wetu wawakilishe kusanyiko lote, iwe kwamba wote walioruhusu wanawake wa kigeni kuishi katika miji yetu waje katika muda uliopangwa na viongozi wa mji na waamuzi wa mji hadi hapo hasira ya Mungu itakapoondoka kutoka kwetu.
\v 15 Yonathan mtoto Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa wakapinga hili, Meshulamu na Shabethai mlawi wakawaunga mkono wao.
\s5
\v 16 Hivyo watu waliotoka uhamishoni wakafanya hivi, Ezra kuhani akachagua wanaume, viongozi watamgulizi wa ukoo na nyumba, wao wote kwa majina na wakaliangalia suala hili siku ya kwanza ya mwezi wa kumi.
\v 17 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kuchunguza wale wanaume walioishi na wanawake wa kigeni.
\s5
\v 18 Miongoni mwa wana wa kikuhani kuna wale walioishi na wanawake wa kigeni. Miongoni mwa wana wa Yoshua mtoto wa Yosadaki na kaka zake ambao walikuwa Maasela, Eliazeri, na Yaribu na Gedalia.
\v 19 Hivyo wakaamua kuwaondoa wake zao. kwa kuwa walikuwa na makosa, wakatoa sadaka ya kondoo kwenye mifugo kwa ajili ya makosa yao.
\s5
\v 20 Miongoni mwa wana wa Imeri, Hanani, na Zebadia.
\v 21 Miongoni mwa wana wa Harimu, Maaseya, na Eliya na Shemaya, na Yehieli na Uzia.
\v 22 Miongoni mwa wana wa Pashuri, Elasa
\s5
\v 23 Miongoni mwa walawi: Yozabadi na Shimei na Kelaya (ndiye Kelita) na Pethaia, na Yuda na Eliezeri. Miongoni mwa waimbaji Eliashibu na. Miongoni mwa walinzi Shalumu, Telemu na Uri.
\v 24 Miongoni mwa Israel waliobaki -
\v 25 Miongoni mwa wana wa Paroshi, Ramia na Izia na Malkiya na Miyamini na Eliazari na Malkiya na Benaya
\s5
\v 26 Miongoni mwa wana wa Elamu Mataniana Zekaria, na yeehieli, na Abdi na Yeremothi na Eliya.
\v 27 Miongoni mwa wana wa Zatu: Elionai, na Eliashibu, na Matania na Yeremothi na Zabadi na Aziza.
\v 28 Miongoni mwa wana wa Bebai Yehohanani, na Hanania na Zakai na Athlai.
\v 29 Miongoni mwa wana wa bani: Meshulami na Maluki, na Adaya na Yashubu na Sheali na Yeremothi.
\s5
\v 30 Miongoni mwa wana wa Pahath-Moabu, Adna, na kelali, na Benaya na Maaseya, na Matania, na Besaleli na Binti na Manase.
\v 31 Na miongoni mwa wana wa Harimu: Eliezeri na Ishiya, na Malkiya na Shemaya na Shimeoni, na
\v 32 Benyamini na Maluki na Shemaria
\s5
\v 33 Miongoni mwa wana Hashumu: Matenai, na Matatana Zabadi, na Elifereti na Yeremai, na Manase, na Shimei.
\v 34 Miongoni mwa wana wa Bani: Maadai, na Amramu na Aueli, na
\v 35 Benaya, na Bedeya na Keluhi, na
\v 36 wania, na Meremothi, Eliashibu,
\s5
\v 37 Matania, na Matenai. na
\v 38 Yaasi. Miongoni mwa wana wa Binui: Shimei,
\v 39 Sheremia, na Nathani, na Adaya, na
\v 40 Maknadebai, na Shashai, na Sharai
\s5
\v 41 Azareri, na Sheremia, na Shemaria, na
\v 42 Shalumu, na Amaria, na Yusufu.
\v 43 Miongoni wa wana wa Nebo: Yeieli, na Mathiana zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli na Benaya.
\v 44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni na walikuwa wamezaa watoto baadhi yao.