sw_ulb_rev/09-1SA.usfm

1673 lines
127 KiB
Plaintext

\id 1SA
\ide UTF-8
\h 1Samweli
\toc1 1Samweli
\toc2 1Samweli
\toc3 1sa
\mt 1Samweli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu; jina lake aliitwa Elikana mwana Yerohamu mwana Elihu mwana wa Tohu mwana wa Sufu, Mwefraimu.
\v 2 Mtu huyo alioa wanawake wawili, jina la mke wa kwanza aliitwa Hana, na yule wa pili aliitwa Penina, Penina alizaa watoto, lakini Hana hakuzaa.
\s5
\v 3 Kila mwaka, mtu huyu aliondoka mjini kwake kwenda kuabudu na kutoa dhabihu kwa BWANA wa majeshi huko Shilo. Wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwepo huko Shilo.
\v 4 Kila mwaka zamu ya Elikana ya kutoa dhabihu ilipofika, alikuwa daima akimpa sehemu ya nyama Penina mkewe, watoto wake wote wa kiume na wakike
\s5
\v 5 Lakini kwa mgawo wa Hana daima alimpa mara mbili zaidi, kwa sababu alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.
\v 6 Hasimu wake alimchokoza sana ili kumkasilisha, kwa sababu BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.
\s5
\v 7 Hivyo kila mwaka, alipokuwa akienda katika nyumba ya BWANA pamoja na familia yake, hasimu wake alizidi kumchokoza, Hatimaye alikuwa mtu wa kulia kila wakati na hakula kitu chochote.
\v 8 Elikana mmewe kila wakati alimuuliza, "Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli chakula? Kwa nini una huzuni moyoni mwako? Mimi sibora kwako kuliko wana kumi?
\s5
\v 9 Wakati fulani, walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alinyanyuka. Wakati huo Eli, kuhani alikuwa amekaa juu ya kiti chake mlangoni kuelekea nyumba ya BWANA.
\v 10 Hana alijawa na uchungu sana; akamwomba BWANA na akalia mno.
\s5
\v 11 Aliweka nadhili na kusema, "BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo nitamtoa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe".
\s5
\v 12 1 Samweli 1: 12-14 Hana kiendelea kuomba mbele za BWANA, Eli alikitazama kinywa chake.
\v 13 Hana aliongea moyoni mwake. Midomo yake ilitikisika, lakini sauti yake haikusikika. Hivyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
\v 14 Eli akamwambia, "Utakuwa mlevi mpaka lini? Weka mbali divai yako."
\s5
\v 15 Hana akajibu, "Sivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni. Sijanywa divai wala kinywaji chochote cha kulevya, bali nimekuwa nikiimimina nafsi yangu mbele za BWANA."
\v 16 Usimchukulie mjakazi wako kama mwanamke duni; nimekuwa nikiongea kutokana na maumivu na masikitiko yangu."
\s5
\v 17 Kisha Eli alimjibu na kusema, "Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akupatie kile ulichomuomba."
\v 18 Hana akasema, " Na mjakazi wako apate kibali machoni pako." Ndipo huyo mwanamke alienda zake na kula chakula na hakuhuzunika tena.
\s5
\v 19 Waliamka asubuhi na mapema wakaenda wakamtukuza BWANA, na baadaye walirudi nyumbani kwao Rama. Elikana alilala na mke wake Hana, na BWANA akamkumbuka.
\v 20 Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, "Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA."
\s5
\v 21 Mara nyingine, Elikana na nyumba yake, walipanda kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya Mwaka na kuondoa nadhiri yake.
\v 22 Lakini Hana hakwenda huko; alikuwa amekwisha mwambia mmewe, "Sitaenda huko hadi mtoto aache kunyonya; ndipo nitamleta, ili ahudhurie mbele za BWANA na akae huko daima."
\v 23 Mme wake Hana, Elikana, akamwambia, "Fanya yale yakupendezayo. Ngojea hadi utakapokuwa umemwachisha kunyonya; BWANA aweze peke yake kuthibitisha neno lake." Hivyo yule mwanamke alibaki akimnyonyesha mtoto wake mpaka pale alipomwachisha ziwa.
\s5
\v 24 Alipokuwa amemwachisha kunyonya, alimbeba, akimchukua pamoja ng'ombe dume wa miaka mitatu, unga kama kilo thelathini na chupa ya mvinyo, akampeleka katika nyumba ya BWANA huko Shilo. Na mtoto huyo alikuwa bado mdogo.
\v 25 Walimchinja yule ng'ombe, na wakamkabidhi mtoto kwa Eli.
\s5
\v 26 Akasema, "Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, Mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA.
\v 27 Niliomba kwa ajili ya mtoto huyu na BWANA akawa amenijibu ombi la dua yangu nililomwomba.
\v 28 Nami nimemtoa kwa BWANA; kwa maisha yake yote, nimempa BWANA." Ndipo Elikana na familia yake wakamtukuza BWANA huko Shilo.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hana aliomba akasema, "moyo wangu wamtukuza BWANA. Pembe yangu imejulikana katika BWANA. Kinywa changu kinatamba dhidi ya maadui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
\s5
\v 2 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA, kwa kuwa hakuna mwingine zaidi yako; hakuna mwamba kama Mungu wetu.
\s5
\v 3 Msijivune sana hivyo kwa kiburi; vinywa vyenu visitoke majivuno. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa; yeye huyapima matendo kwa mizani.
\v 4 Pinde za mashujaa zimevunjika, bali wale wanaojikwaa hujivika nguvu kama mshipi.
\s5
\v 5 Wale walio na shibe ya kutosha wamejikodisha ili wapate chakula; wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Hata yule aliye kuwa tasa amezaa watoto saba, bali mwanamke mwenye watoto wengi amenyong'onyea.
\s5
\v 6 BWANA huua na huuisha. Hushusha kuzimu na huleta tena juu.
\v 7 BWANA humfanya maskini, na yeye ndiye humtajirisha mtu. Yeye hudhili, lakini pia hukweza
\s5
\v 8 Yeye humwinua juu maskini toka mavumbini: Huwainua wahitaji toka jalalani na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwarithisha kiti cha enzi cha utukufu. Kwa kuwa nguzo za dunia ni za BWANA na ameukalisha ulimwengu juu yake.
\s5
\v 9 Yeye atazilinda nyayo za watu wake waaminifu, bali waovu watanyamazishwa gizani, kwa maana hakuna atayeshinda kwa nguvu zake.
\s5
\v 10 Wale wampingao BWANA watavunjwa vipande vipande; atawapiga radi kutokea mbinguni. BWANA atahukumu miisho ya dunia; atampa nguvu mfalme wake na kuinua pembe ya mtiwa mafuta wake."
\s5
\v 11 Nndipo Elikana akenda Rama, nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA machoni pa Eli, kuhani.
\s5
\v 12 Basi, watoto wa Eli walikuwa wakorofi. Wao hawakumheshimu BWANA.
\v 13 Desturi ya makuhani na watu ilikuwa kwamba endapo mtu yeyote ametoa dhabihu, mtumishi wa kuhani angekuja akiwa na uma wa meno matatu mkononi mwake, nyama ilipokuwa inatokoswa.
\v 14 Naye angeutia uma huo sufuriani, au birikani au chomboni au chunguni; nyama yote ambayo ingeinuliwa na uma huo ingetwaliwa na kuhani mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokwenda huko.
\s5
\v 15 Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, mtumishi wa kuhani alikuja, na kumwambia aliyekuwa akitoa dhabihu, " Tenga nyama ya kuchoma kwa ajili ya kuhani; kwa sababu hataikubali ile ya kutokosa kutoka kwako, bali tu ile mbichi."
\v 16 Ikiwa mtu atamwambia, "Wachome mafuta kwanza, na kisha uchukue kiasi utakacho." Ndipo angesema, "Hapana, utanipatia sasa hivi; la sivyo; Nitaichukua kwa lazima."
\v 17 Dhambi ya vijana hawa ilikuwa mbaya sana mbele za BWANA, kwa sababu waliidharau dhabihu ya BWANA.
\s5
\v 18 Lakini Samweli alimtumikia BWANA akiwa mdogo akivaa nguo ya naivera ya kitani.
\v 19 Kila mwaka mama yake alimtengenezea kanzu dogo na kumletea, wakati wakija na mmewe kutoa dhabihu ya kila mwaka.
\s5
\v 20 Eli aliwabariki Elikana na mke wake na kusema, "BWANA akupatie watoto zaidi kwa mwanamke huyu kwa sababu ya ahadi yake aliyoitoa kwa BWANA." Baadaye walirudi nyumbani kwao.
\v 21 BWANA alimsaidia tena Hana, akawa amebeba mimba nyingine. Akazaa watoto watatu wa kiume na wa kike wawili. Wakati huo huo mtoto Samweli akakua akiwa mbele za BWANA.
\s5
\v 22 Basi Eli alikuwa mzee sana, akayasikia yote ambayo watoto wake walikuwa wakiwafanyia Waisraeli wote, na jinsi walivyotembea na mwanamke aliyekuwa akitumika katika lango la hema ya kukutania.
\v 23 Akawaambia, "Kwa nini mnafanya mambo hayo? Kwa maana nasikia matendo yenu maovu kutoka kwa watu hawa wote."
\v 24 Sivyo hivyo, watoto wangu, maana hii ninayoisikia siyo taarifa njema. Mnawakosesha watu wa BWANA.
\s5
\v 25 "Kama mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; Lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea mtu huyo?" Lakini hawakuitii sauti ya baba yao, sababu BWANA alinuia kuwaua.
\v 26 Yule mtoto Samweli aliongezeka umri, na kupata kibali kwa BWANA na kwa watu pia.
\s5
\v 27 Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli na kumwambia, "BWANA asema, 'Je, sikujifunua mwenyewe kwa nyumba ya baba zako, walipokuwa Misri utumwani nyumbani mwa Farao?
\v 28 Mimi nilimchagua yeye kutoka makabila yote ya Israeli awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu, na kufukiza uvumba, na kuvaa kanzu ya naivera mbele yangu. Niliwapa nyumba ya baba zako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto.
\s5
\v 29 Kwanini basi, unaidharau dhabihu yangu na sadaka ambazo ninazitaka mahali ninapoishi? Kwanini unawaheshimu watoto wako kuliko mimi, kwa kujinenepesha ninyi wenyewe kwa uzuri wa kila sadaka ya watu wangu Israeli?'
\v 30 Maana, BWANA, Mungu wa Isareli, asema, niliahidi kwamba nyumba yako, na nyumba ya baba yako, yawapasa kwenda mbele zangu milele,' Lakini sasa BWANA asema. 'Mambo haya yapishe mbali. nami nisifanye hivi, maana nitawaheshimu wanaoniheshimu, bali wanaonidharau mimi hawatakuwa na thamani.
\s5
\v 31 Tazama, siku zinakuja nitakapoondoa nguvu zako na nguvu za nyumba za baba yako, ili kwamba pasije kuwepo mtu mzee katika nyumba yako.
\v 32 Nawe utalitazama hangaiko katika makao yangu. Ingawa Israeli watapewa jambo jema, hapatakuwapo tena mtu yeyote mzee katika nyumba yako.
\v 33 Yeyote miongoni mwenu nisiye mwondoa kutoka madhabahuni pangu, Nitasababisha macho yenu yaanguke, na ita nitasababisha huzuni maishani mwenu. Wanaume wote waliozaliwa katika familia yako watakufa.
\s5
\v 34 Hii ndiyo itakuwa ishara kwako ambayo itawaijia watoto wako wakiume wawili, juu ya Hofni na Finehasi: Wote wawili watakufa siku moja.
\v 35 Nami nitamwinua juu kuhani wangu mwaminifu atakaye fanya kile kilichomo moyoni mwangu na nafisini mwangu. Nami nitamjengea nyumba madhubuti; naye atakwenda mbele ya mfalme wangu mbarikiwa milele.
\s5
\v 36 Kila mmoja aliyebakia nyumbani mwako atakuja na kusujudu mbele ya mtu huyo, akiomba kipande cha fedha na mkate mmoja, naye atasema, "Tafadhali uniajiri katika moja ya nafasi za kuhani ili niweze kula kipande cha mkate'"'
\s5
\c 3
\p
\v 1 Yule mtoto Samweli alimtumikia BWANA chini ya uangalizi wa Eli. Neno la BWANA halikupatikana kwa wingi siku hizo; hapakuwa na maono ya mara kwa mara ya kinabii.
\v 2 Wakati huo, nguvu ya macho ya Eli ilikuwa imefifia kiasi cha kutoweza kuona vizuri, na alikuwa amelala kitandani mwake.
\v 3 Ile taa ya BWANA bado ilikuwa bado inawaka, na Samweli alikuwa amelala katika nyumba ya BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu.
\v 4 BWANA akamwita Samweli, naye akaitika, "Niko hapa"
\s5
\v 5 Samweli alimwedea Eli na kusema, "Niko hapa, sababu uliniita." Eli akasema, "Sikukuita; kalale tena." Hivyo Samweli akarudi na kulala.
\v 6 BWANA akamwita tena, "Samweli." Saamweli aliamka tena na kwenda kwa Eli na kusema, Niko hapa, sababu umeniita." Eli akajibu, "Sijakuita, mwanangu; kalale tu tena."
\s5
\v 7 Basi Samweli bado hakuwa na uzoefu kuhusu Bwana, wala hakuwahi kupata ujumbe wowote kutoka kwa BWANA ukifunuliwa kwake.
\v 8 BWANA akamwita tena Samweli kwa mara ya tatu. Samweli alinyanyuka tena na kwenda kwa Eli na kusema, "Niko hapa, sababu uliniita," Ndipo Eli alitambua kwamba BWANA alimwita kijana.
\s5
\v 9 Kisha Eli aka, mwambia Samweli, "Nenda ukalale tena; ikiwa atakuita tena, sharti useme, 'Sema, BWANA, maana mtumwa wako anasikiliza."' Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake tena.
\s5
\v 10 BWANA alikuja na kusimama; akaita vilevile kama vile mwanzoni, "Samweli, Samweli." Ndipo Samweli akasema, "Nena, kwa sababu mtumwa wako anasikiliza."
\v 11 BWANA akasema na Samweli, "Tazama, Niko tayari kufanya jambo katika Israeli ambalo masikio ya kila mmoja akisikia atashtuka.
\s5
\v 12 Siku hiyo nitatimiza kila kitu nilichokisema dhidi ya Eli kuhusu nyumba yake, kutoka mwanzo hadi mwisho.
\v 13 Nimemwambia kwamba niko tayari kuhukumu nyumba yake mara moja kwa ile dhambi aliyoifahamu, kwa sababu watoto wake walijiletea laana juu yao wenyewe na hakuwazuia.
\v 14 Hii ndiyo sababu nimeapa kwa nyumba ya Eli, kwamba dhambi za nyumba yake hazitasahehewa kwa dhabihu au kwa sadaka kamwe."
\s5
\v 15 Samweli akalala hadi asubuhi; baadaye alifungua milango ya nyumba ya BWANA. Lakini Samweli aliogopa kumwambia Eli kuhusu maono hayo.
\v 16 Kisha Eli akamwita Samweli na kusema, "Samweli, mwanangu." Samweli akasema, "Niko hapa."
\s5
\v 17 Akamuuliza, "Ni neno gani alilokusemesha? Tafadhali usinifiche jambo hilo. Mungu akutendee hivyo na kukuzidishia, endapo utanificha kitu chochote kati ya yote ambayo amesema nawe."
\v 18 Samweli akamweleza kila kitu; hakumficha jambo lolote. Eli akasema, "Ni BWANA. Na afanye linaloonekana jema kwake."
\s5
\v 19 Samweli akakua, na BWANA alikuwa pamoja naye na hakuacha kutimiza maneno yake ya unabii.
\v 20 Israeli yote tokea Dani hadi Beersheba walijua kwamba Samweli aliteuliwa kuwa nabii wa BWANA.
\v 21 Naye BWANA alionekana tena huko Shilo, maana alijifunua mwenyewe kwa Samweli huko Shilo kwa neno lake.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Neno la Samweli likawafikia Israeli wote. Basi Israeli wakatoka kupigana dhidi ya Wafilisti. Nao wakaweka kambi hapo Ebenezeri, na Wafilisti waliweka kambi yao huko Afeki.
\v 2 Nao Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita dhidi ya Waisraeli. Vita ilipopamba moto, Israeli ilishindwa na Wafilisti, wakauawa watu wapatao elfu nne kwenye uwanja wa vita.
\s5
\v 3 Watu walipokuja kambini, wazee wa Israeli walisema, "Kwa nini BWANA ametushinda leo mbele ya Wafilisti? Hebu tulilete hapa sanduku la ushuhuda wa BWANA kutoka Shilo, ili kwamba liwe hapa pamoja nasi, ili litufanye tuwe salama kutokana na nguvu za maadui zetu."
\v 4 Hivyo waliwatuma watu huko Shilo; kutokea huko walilibeba sanduku la ushuhuda wa BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi. Hofni na Finehasi, watoto wawili wa Eli, walikuwapo pamoja na lile sanduku la ushuhuda wa Mungu.
\s5
\v 5 Sanduku la ushuhuda wa BWANA lilipofika kambini, watu wote wa Israeli walipiga yowe, na nchi ikavuma.
\v 6 Wafilisti waliposikia kelele za mayowe, wakasema, "sauti hii ya mayowe katika kambi ya Waebrania inamaanisha nini?" Baadaye walitambua kwamba sanduku la BWANA limefika kambini.
\s5
\v 7 Wafilisti waliogopa sana, "Mungu ameingia kambini." Wakasema, "Ole wetu! Jambo kama hili halijawahi kutokea huko nyuma!
\v 8 Ole wetu! Ni nani atatulinda dhidi ya nguvu za Mungu mwenye uwezo? Huyu ndiye Mungu aliyewashambulia Wamisri kwa aina tofauti za mapigo mengi jangwani.
\v 9 Enyi Wafilisti, iweni hodari, na fanyeni kiume, vinginevyo mtakuwa watumwa wa Waebrabia, kama walivyokuwa watumwa wenu. Fanyeni kiume, na piganeni nao."
\s5
\v 10 Wafilisti walipigana, na Waisraeli wakashindwa. Kila mtu alikimbilia nyumbani kwake, na mauaji yalikuwa makubwa sana; maana askari wa Israeli elfu thelathini waendao kwa miguu vitani, walianguka.
\v 11 Lile sanduku la Mungu lilichukuliwa, na watoto wa Eli, Hofni na Finehasi waliuawa.
\s5
\v 12 Mtu mmoja wa Benjamini alikimbia kutoka uwanja wa vita akaja Shilo siku iyo hiyo, aliwasili na mavazi yake yamechanika na matope kichwani pake.
\v 13 Alipofika, Eli alikuwa amekaa kitini pake karibu na barabara akitazama kwa sababu moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kutoa taarifa, mji wote ulilia.
\s5
\v 14 Eli aliposikia kelele ya kilio kile, alisema, "Kilio hicho kina maana gani?" Kwa haraka mtu yule alikuja na kumweleza Eli.
\v 15 Basi Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane; macho yake yamepofuka, na hakuweza kuona.
\s5
\v 16 Yule mtu akamwambia Eli, "Mimi ndiye nimechomoka kutoka vitani. Nimetoroka kutoka kwenye mapigano leo." Eli akasema, "Mambo yalienda namna gani, mwanangu?"
\v 17 Yule mtu aliyeleta hizo habari alijibu na kusema, "Israeli wamewakimbia Wafilisti. Pia watu wengi wameuwawa. Watoto wako, Hofni na Finehasi, wamekufa, na sanduku la Mungu limechukuliwa."
\s5
\v 18 Alipotamka sanduku la Mungu, Eli alianguka chali kutoka kwenye kiti chake karibu na mlango. akavunjika shingo lake, na kufariki, kwa sababu alikuwa mzee tena mzito. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka arobaini.
\s5
\v 19 Basi mkwewe, mke wa Finihasi, alikuwa mjamzito akikaribia kujifungua. aliposikia habari kwamba sanduku la Mungu limetekwa nyara na kwamba baba mkwe na mme wake wamefariki, alichuchumaa chini akajifungua, lakini utungu wake ulimzidi na ulimtaabisha sana.
\v 20 Alipokaribia kufariki, wanawake waliokuwa wakimhudumia walisema, "Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume." Lakini hakuwajibu lolote au kuzingatia alichoambiwa.
\s5
\v 21 Akamwita mtoto Ikabodi, akisema, "Utukufu umetoweka Israeli!" Kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyara, na kwa sababu ya kifo cha baba mkwe na mme wake.
\v 22 Na alisema, "Utukufu umetoweka kutoka Israeli, kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyala."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Basi Wafilisti wakawa wamelitwaa sanduku la Mungu, wakalileta kutoka Ebenezeri hadi Ashdodi.
\v 2 Wafilisti walilichukua sanduku la Mungu, wakalileta ndani ya nyumba ya Dagoni, na wakalikalisha pembeni mwa Dagoni.
\v 3 Watu wa Ashdodi walipoamka mapema siku ya pili, tazama, Dagoni ilianguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Hivyo waliichukua Dagoni na kuisimamisha tena katika sehemu yake.
\s5
\v 4 Lakini walipoamka mapema kesho yake, tazama, Dagoni alikuwa ameanguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Kichwa cha Dagoni na vitanga vyake miwili vilikatika na kulala mlangoni. Kiwiliwili cha Dagoni ndicho kilibaki tu.
\v 5 Na hii ndiyo sababu, makuhani wa Dagoni na yeyote aingiae ndani ya nyumba ya Dagoni, hata leo, hawezi kukanyaga mlango wa Dagoni katika Ashdodi.
\s5
\v 6 Mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi. Aliwaangamiza akawatesa kwa majipu, Ashdodi na wilaya zake kwa pamoja.
\v 7 Watu wa Ashdodi walipotambua kilichokuwa kinatokea, walisema, "Sanduku la Mungu wa Israeli lisikae kwetu, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya mungu wetu Dagoni."
\s5
\v 8 Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, "Tufanye nini na sanduku la Mungu wa Israeli?" Wakawajibu, "Sanduku la Mungu wa Israeli lihamishwe na kupelekwa Gathi." Basi wakalihamisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli hadi huko Gathi.
\v 9 Lakini baada ya kulipeleka huko, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, ukasababisha machafuko makubwa. Akawatesa watu wa mji huo, wakubwa kwa wadogo; na majipu yakaota juu ya miili yao.
\s5
\v 10 Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu hadi Ekroni. Lakini mara tu sanduku la Mungu lilipoingia Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele wakisema, "Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli kutuua sisi na watu wetu."
\s5
\v 11 Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, "Lipelekeni mbali sanduku la Mungu wa Israeli, na lirudishwe katika makao yake, ili lisije kutuua sisi na watu wetu." Kwa maana kulikuwa na hofu ya kutisha mjini mwote; Mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
\v 12 Watu ambao hawakufa waliteswa na majipu, na kilio cha mji kilipanda hadi mbinguni.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Basi sanduku la BWANA lilikaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba.
\v 2 Ndipo Wafilisti wakawaita makuhani na waganga; wakawaambia, "Tulifanyie nini sanduku la BWANA? Twambieni jinsi ambavyo tunapaswa kulirudisha sanduku katika nchi yake."
\s5
\v 3 Makuhani na waganga wakasema, "Kama mtalirudisha sanduku la Mungu wa Israeli, msilipeleke bila zawadi; kwa namna yoyote ile mpelekeeni sadakaa ya hatia. Hapo ndipo mtapona, na mtajua ni kwanini mkono wake hadi sasa haujaondoka juu yenu."
\v 4 Ndipo wakawauliza, "Sadaka ya hatia itakuwa nini kwamba tunampelekea?" Wakawajibu, "Majipu matano ya dhahabu na panya watano wa dhahabu, Idadi hiyo ya watano ni sawa na idadi ya viongozi wa Wafilisti. Kwa sababu tauni ya aina moja iliwashambulia ninyi na viongozi wenu.
\s5
\v 5 Kwa hiyo, nilazima mtengeneze mifano ya majipu yenu, na mifano ya panya wenu ambayo huiharibu nchi, na mpeni utukufu Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka juu yenu, kutoka juu ya miungu yenu, na kutoka juu ya nchi yenu.
\v 6 Kwanini mfanye mioyo yenu kwa migumu, kama vile Wamisri na Farao walifanya mioyo yao kuwa migumu? Hicho ni kipindi ambacho Mungu wa Israeli aliwashughilikia sana; Je, Wamisri hawakuwaachilia watu, na wakaondoka?
\s5
\v 7 Basi sasa, andaeni mkokoteni mpya pamoja na ng'ombe wawili wake wanaonyonyesha, ambao hawajawahi kufungwa nira. Wafungeni ng'ombe hao kwenye mkokoteni, lakini warudisheni wale ndama wao nyumbani.
\v 8 Kisha lichukueni sanduku la BWANA na kuliweka ndani ya mkokoteni. Wekeni ndani ya kasha yale maumbo ya dhahabu mnayompelekea ambyo ni sadaka ya hatia kando yake. Ndipo mlipeleke lipate kuondoka.
\v 9 Kisha muwe makini; kama litapanda kwenda kwa njia hadi nchini mwake hadi Beth Shemeshi, basi mjue kuwa BWANA ndiye aliyetenda pigo hili kubwa. Lakini kama halitakwenda, ndipo tutajua kwamba siyo mkono wake uliotupatia mateso; badala yake tutajua kuwa yaliyotupata ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu.
\s5
\v 10 Watu hao wakafanya kama walivyoambiwa, walichukuwa ng'ombe wawili wanaonyonyesha, wakawafunga kwenye mkokoteni, na kuwabakiza ndama wao nyumbani.
\v 11 Wakaliweka sanduku la BWANA juu ya mkokoteni, pamoja na lile kasha lililobeba panya wa dhahabu na yale maumbo ya majipu yao.
\v 12 Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata nija moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hwakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi.
\s5
\v 13 Nao watu wa Beth Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao katika bonde. Waliponyanyua macho yao juu na kuliona sanduku, wakafurahi.
\s5
\v 14 Huo mkokoteni ulifikia ndani ya shamba la Yoshua wa Beth Shemeshi na ukasimama hapo. Kulikuapo jiwe kubwa mahali hapo, wakatayarisha kuni kutokana na mkokoteni huo, na wakawatoa ng'ombe hao kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA.
\v 15 Walawi walilitelemsha sanduku la BWANA chini pamoja na kasha lake lililoyatunza yale maumbo ya dhahabu, wakaweka vitu hivyo juu ya hilo jiwe kubwa. Watu wa Beth Shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa na kutoa dhabihu kwa BWANA siku iyo hiyo.
\s5
\v 16 Hao viongozi watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.
\s5
\v 17 Haya ndiyo majipu ya dhahabu ambayo Wafilisti walirudisha kama sadaka ya hatia kwa BWANA: moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni.
\v 18 Idadi ya wale panya wa dhahabu ilikuwa sawa na ile ya idadi ya miji yote ya Wafilisti inayomilikiwa na viongozi watano, kwa miji iliyojengewa maboma na vijiji vya mashambani. Lile jiwe kubwa, ambalo kando yake waliweka sanduku la BWANA, lipo kama ushuhuda hadi leo katika shamba la Yoshua Mbeth- Shemeshi.
\s5
\v 19 BWANA akawashambulia baadhi ya watu wa Bethi Shemeshi kwa sababu walichungulia ndani ya sanduku lake. Aliwaua watu sabini. Watu wakaomboleza, kwa sababu BWANA aliwapa watu pigo kubwa mno.
\v 20 Watu wa Bethi Shemeshi wakasema, "Ni nani mwenye uwezo wa kushindana na BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na atampandia nani akitoka kwetu."" Je, ni nani awezaye kusimama mbele ya BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na ni kwa nani ambako sanduku litaenda likitoka hapa."
\s5
\v 21 Wakawatuma wajumbe kwenda kwa wenyeji wa Kiriath Yearimu, wakisema, "Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; teremkeni na mkalipeleke kwenu."
\s5
\c 7
\p
\v 1 Watu wa Kiriath Yearimu walikuja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu mlimani iliyokuwa kilimani. Wakamteua Eleazari, mwanawe, kulitunza sanduku la BWANA.
\v 2 Tangu siku ambayo sanduku lilikaa huko Kiiriath Yearimu, ulipita muda mrefu, miaka ishirini. Nyumba yote ya Israeli iliomboleza na ikaazimu kumrudia BWANA.
\s5
\v 3 Samweli akawaambia watu wote wa Israeli, "Kama mtamrudia BWANA kwa moyo wenu wote, mkaiondoa miungu migeni na Ashtorethi kutoka katikati yenu, igeuzeni mioyo yenu kwa BWANA, na mwabuduni yeye peke yake, ndipo atawaokoa kutoka mkono wa Wafilisti."
\v 4 Ndipo watu wa Israeli wakamuondoa Baali na Ashtorethi, na wakamwabudu BWANA peke yake.
\s5
\v 5 Ndipo Samweli akasema, "Waleteni Israeli wote hadi Mizpa, nami nitamwomba BWANA kwa ajili yenu."
\v 6 Wakakusanyika Mispa, wakateka maji na kuyamwaga chini mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na kusema, "Tumemfanyia BWANA dhambi." Hapo Mispa ndipo Samweli aliwaamu na kuwaongoza watu wa Iraeli.
\s5
\v 7 Basi Wafilisti waliposikiakwamba Waisraeli wamekusanyika hapo Mispa, viongozi wa Wafilisti waliwashambulia Israeli. Waisraeli waliposikia hivyo, waliwaogopa Wafilisti.
\v 8 Ndipo Waisraeli wakamwambia Samweli, "Usiache kumwomba BWANA Mungu wetu kwa ajili yetu, ili atuokoe kutoka mkono wa Wafilisti."
\s5
\v 9 Samweli alimchukua kondoo mchanga nakumtoa sadaka ya kuteketezwa kikamilifu kwa BWANA. Ndipo Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli, na BWANA akamjibu.
\s5
\v 10 Hata Samweli alipokuwa akitoa sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu kuwashambulia Israeli; lakini BWANA alipiga kwa nguromo ya sauti kubwa siku hiyo dhidi ya Wafilisti na kuwatia kiwewe, na wakashindwa mbele ya Israeli.
\v 11 Waisraeli wakaondoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti na kuwaua hadi kufika chini ya Beth kari.
\s5
\v 12 KIsha Samweli akachukua jiwe akalisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita hilo jiwe Ebeneza, akisema, "Hata sasa BWANA ametusaidia."
\s5
\v 13 Kwa hiyo, Wafilisti walishindwa na hawakuingia katika mipaka ya Israeli. Mkono wa BWANA uliwalemea Wafilisti siku zote za Samweli.
\v 14 Miji ambayo Wafilisti waliitwaa kutoka kwa Israeli ilirudishwa, kutokea Ekroni hadi Gathi; Israeli ikarudisha tena sehemu za nchi zake kutoka kwa Wafilisti. Ndipo ikawa amani kati ya Israeli na Waamori.
\s5
\v 15 Samweli akawa mwamuzi wa Israeli siku zote za maisha yake.
\v 16 Kila mwaka alienda Betheli kwa kuzunguka, akienda Gilgali, na huko Mispa.
\v 17 Kisha angerudi Rama, kwa sababu mji wake ulikuwa huko; na huko pia aliwaamua Waisiraeli. Hata huko Rama, pia alimjengea BWANA madhabahu.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Samweli alipozeeka, aliwaweka watoto wake wawe waamuzi juu ya Israeli.
\v 2 Mtoto wake wa kwanza aliitwa Yoeli, na mtoto wake wa pili aliitwa Abiya. Hawa walikuwa waamuzi katika Bersheba.
\v 3 Watoto wake hawakuenenda katika njia za baba yao, bali walipiga mbio kutafuta mapato ya udhalimu. Walipokea rushwa na na kupotosha hukumu.
\s5
\v 4 Ndipo wazee wote wa Israeli walikutana pamoja na kumwendea Samweli huko Rama.
\v 5 Wakamwambia, "Angalia, wewe umekuwa mzee, na watoto wako hawaenendi katika njia zako. Tuchagulie mfalme wakutuamua kama yalivyo mataifa yote."
\s5
\v 6 Lakini haikumpendeza Sameli waliposema, "Utupatie mfalme wa kutuamua." Hivyo akamwomba BWANA.
\v 7 Na BWANA akamwambia Samweli, "Sikiliza sauti ya watu kwa kila jambo wanalokwambia; kwa sababu hwajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.
\s5
\v 8 Sasa wanafanya kama vile walivyotenda tangu siku ile nilipowatoa huko Misri, kwa kuniacha, na kuwatumikia miungu mingine, na ndivyo hivyo pia wanakufanyia na wewe.
\v 9 Basi sasa uwasikilize; lakini uwaonye sawasawa na uwafahamishe tabia ya mfalme atakaye waongoza.
\s5
\v 10 Kwa hiyo Samweli akawaambia watu waliokuwa wakiomba mfalme maneno yote ya BWANA.
\v 11 Akasema, "Hivi ndivyo jinsi mfalme atakavyowatawala.
\v 12 Atawachukua watoto wenu wa kiume na kuwaweka juu ya magari ya vita na kuwa wapanda farasi wake, na kukimbia mbele ya magari yake. Atawaweka ma- kapteni wake juu ya maelfu ya askari, na ma-kapteni juu ya askari hamsini. Wengine atawafanya wakulima wamashamba yake, wengine wavunaji wa mazao yake, wengine watatengeneza silaha zake na zana za magari yake.
\s5
\v 13 Naye atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi, na waoka mikate.
\v 14 Atachukua mashamba yenu mazuri, mashamba ya mizabibu, na yale ya mizeituni na kuwapa watumishi wake.
\v 15 Atachukua moja ya kumi ya nafaka zenu na mizabibu na na kuwapa maofisa na watumishi wake.
\s5
\v 16 Atawachukua watumwa wenu na wajakazi wenu na vijana wenu waliowazuri na punda wenu; atawatumikisha wote kwa ajili yake.
\v 17 Atawatoza moja ya kumi ya mifugo yenu, na mtakuwa watumwa wake.
\v 18 Ndipo mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyemchagua kwa ajili yenu; lakini siku ile BWANA hatawajibu
\s5
\v 19 Lakini watu walikataa kumsikiliza Samweli; wakasema, "Hapana!" Lazima awepo mfalme juu yetu.
\v 20 Ili tuweze kuwa kama mataifa mengine yote, na hivyo mfalme wetu aweze kutuamua na atoke mbele yetu na atupiganie vita yetu.
\s5
\v 21 Naye Samweli aliposikia maneno yote ya watu, akayarudia katika masiko ya BWANA.
\v 22 BWANA akamwambia Samweli, "Sikiliza sauti yao na uwafanyie mfalme." Hivyo Samweli akawaambia watu wa Israeli, "Kila mtu na arudi mjini kwake."
\s5
\c 9
\cl Samweli 9
\p
\v 1 Basi kulikuwa na mtu mmoja kutoka Benyamini, mtu mashuhuri. Jina lake aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Zerori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini.
\v 2 Huyu alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Sauli, kijana mzuri wa uso. Hapakuwapo mwanaume mzuri wa uso kuliko huyu miongoni mwa watu wote wa Israeli. Kutoka mabegani kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wengine.
\s5
\v 3 Na punda wa Kishi, baba yake na Sauli walipotea. hivyo Kishi akamwambia Sauli mwanawe, "Mchukue mmoja wa watumishi; uamke uende kuwatafuta punda,"
\v 4 Sauli akapita katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu na akaenda akapita katika nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona. Kisha walipita katika nchi ya Shaalimu, lakini hawakuwa huko. Baadaye alipita katika nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwaona wale punda.
\s5
\v 5 Na walipofika nchi ya Sufu, Sauli alimwambia mtumishi wake aliyekuwa naye, "Njoo na turudi, pengine baba aweza kuacha kuchunga punda na kuanza kutuhofia sisi."
\v 6 Lakini mtumishi akamwmbia, "Sikiliza, Yupo mtu wa Mungu katika mji huu. Naye ni mtu wa kuheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Hebu twende huko; labda anaweza kutuambia tupitie wapi katika safari yetu."
\s5
\v 7 Ndipo Sauli akamwambia mtumish iwake, "Lakini kama tukienda kwake, twaweza kumpelekea nini? Maana hata mkate katika mfuko wetu umekwisha, na hakuna zawadi ya kumpelekea mtumishi wa Mungu. Tuna kitu gani?
\v 8 Huyo mtumishi akamjibu Sauli na kusema, "Hapa, ninayo robo ya shekeli ya fedha ambayo nitampa mtumishi wa Mungu, atuambie ni njia ipi yatupasa tuiendee."
\s5
\v 9 (Zamani katika Israeli, mtu alipotaka kujua neno kuhusu mapenzi ya Mungu, alisema, "Njoo, haya twende kwa mwonaji." Kwa maana nabii wa leo, zamani aliitwa Mwonaji).
\v 10 Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, "Umesema vyema. Haya, njoo twende." Basi wakaenda katika mji ambao mtu wa Mungu alikuwamo.
\v 11 Walipopanda mlima kuelekea mjini, walikutana na wasichana wakienda kuteka maji; Sauli na mtumishi wake wakawauliza, "Mwonaji hupo hapa?"
\s5
\v 12 Nao wakawajibu, na kusema, "Yupo; tazameni, yuko mbele yenu. Harakisheni, kwa maana anakuja mjini leo, sababu leo watu wanatoa dhabihu zao mahali pa juu.
\v 13 Mara tu mtakapoingia mjini mtamuona, kabla hajapanda mahali pa juu kla chakula. Watu hawatakula hata atakapokuja, kwa sababu ndiye ataibariki dhabihu; na baadaye wale ambao wamealikwa hula. Basi pandeni, mtamuona sasa hivi."
\s5
\v 14 Kwa hiyo walikwea kwenda mjini. Walipokuwa wakiingia mjini, walimuona Samweli akija mbele yao, akipanda kwenda mahali pa juu.
\s5
\v 15 Siku moja kabla Sauli hajafika, BWANA alikuwa amemfunulia Samweli:
\v 16 "Kesho wakati kama huu nitakutumia mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe utamtia mafuta awe mfalme juu ya watu wangu Israeli. Atawaokoa watu wangu kutoka mkono wa Wafilisti. Kwa kuwa nimewaonea huruma watu wangu na kilio cha kutaka msaada kimenifikia."
\s5
\v 17 Samweli alipomuona Sauli, BWANA akamwambia, "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu."
\v 18 Ndipo Sauli akaja karibu na Samweli katika lango na kusema, "Niambie nyumba ya Mwonaji iko wapi?
\v 19 Samweli akamjibu Sauli akisema, "Mimi ndiye mwonaji. Tangulia mbele hadi mahali pa juu, nami nitakueleza kila kitu kilichomoyoni mwako.
\s5
\v 20 Kama punda wenu waliopotea siku tatu zilizopita, msihofu kuhusu hao punda, kwa kuwa wamekwishapatikana. Na yote yaliyotamanika kwa ajili ya Israeli yanamwangukia nani? Siyo kwako na nyumba ya baba yako yote?"
\v 21 Sauli akamjibu na kusema, Siyo mimi Mbenyamini, kutoka kabila lililo dogo sana kwa makabila ya Israeli? Siyo ukoo wangu ulio mdogo sana kwa kabila la Benyamini? Kwa nini basi unaniambia kwa namna hii?"
\s5
\v 22 Hivyo Samweli akamchukua Sauli na mtumishi wake, akawaingiza ukumbini, akawakalisha mahali pa heshima pa wale walioalikwa, idadi yao takribani watu thelathini.
\s5
\v 23 Samweli akamwambia mpishi, "Lete sehemu niliyokupatia, sehemu ambayo nilikwambia hivi, "Itenge."'
\v 24 Basi mpishi alichukua paja lililokuwa limeinuliwa katika dhabihu na kile kilichokuwa pamoja nalo, akaitenga mbele ya Sauli. Kisha Samweli akasema, "Angalia kile kilichokuwa kimetunzwa kwa ajili yako! Kula, kwa sababu kilitunzwa hadi wakati maalum ufike kwa ajili yako. Na kwa sasa waweza kusema, 'Nimewaalika watu."' Kwa hiyo Sauli alikula pamoja na Samweli siku hiyo.
\s5
\v 25 Walipokuwa wamekwisha shuka chini kutoka sehemu ya juu na kuingia mjini, Samweli akazungumza na Sauli darini.
\v 26 Na kulipopambazuka, Samweli alimwita Sauli darini na kusema, "Amka, kusudi nikusindikize uende zako," Hivyo Sauli aliamka, na wote wawili, yeye na Samweli walitoka kwenda mtaani.
\s5
\v 27 Walipokuwa wakienda nje ya viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, "Mwambie mtumishi wako atanguliye mbele yetu(na alitangulia mbele), Lakini wewe sharti usubiri kidogo, nipate kukuambia ujumbe wa Mungu."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ndipo Samweli akachukua chupa ya mafuta, akayamimina juu ya kichwa cha Sauli, na akambusu. Akasema, "Je, Mungu hajakutia mafuta uwe mtawala juu ya urithi wake?
\v 2 Utakapoondoka kwangu leo, utawaona wanaume wawili na kaburi la Raheli, katika nchi ya Benyamini hapo Selsa. Watu hao watakuambia, 'Wale punda mliokuwa mkiwatafuta wamepatikana. Sasa, Baba yako ameacha kuwatunza punda, na ana hofu juu yenu, anasema, "Nitafanya nini kuhusu mwanangu?"
\s5
\v 3 Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na utafika katika mwaloni wa Tabori. Utakutana na watu watatu hapo wakienda kwa Mungu huko Betheli, mmoja akibeba wana-mbuzi watatu, mwingine akibeba mikate mitatu, na mwingine akibeba kiriba cha divai.
\v 4 Watawasalimu na watawapatia mikate miwili, kutoka mikononi mwao.
\s5
\v 5 Baada ya hayo, utafika katika mlima wa Mungu, mahali ilipo ngome ya Wafilisti. Utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakiteremka chini kutoka mahali pa juu wakiwa na kinanda, tari, kinubi na filimbi mbele yao; na watakuwa wakitabiri.
\v 6 Roho ya BWANA itakujaza, nawe utatabiri pamoja nao, na utabadilishwa na kuwa mtu tofauti.
\s5
\v 7 Basi, ishara hizi zikikufikia, fanya lolote ambalo mikono yako itaona ifanye, kwa sababu Mungu yu pamoja nawe.
\v 8 Nenda ushuke mbele yangu hadi Gilgali. Kisha nitakufuata huko nitoe dhabihu za kuteketezwa na kutoa dhabihu za amani. Nisubiri kwa muda wa siku saba hadi nije kwako na nikuoneshe unachopaswa kufanya."
\s5
\v 9 Sauli alipotega mgongo amuache Samweli, Mungu akampa moyo mwingine. Ndipo ishara zote hizi zikatimia siku hiyo.
\v 10 Walipofika mlimani, kundi la manabii lilikutana naye, na Roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu ili atabiri pamoja nao.
\s5
\v 11 Kila mtu aliyemfahamu kabla hajamwona akitabiri pamoja na manabii, watu waliambizana wao kwa wao, "Kitu gani kimempata mtoto wa Kishi? Hivi Sauli ni mmoja wa manabii siku hizi?"
\v 12 Mtu mmoja kutoka eneo hilo akajibu, "Na ni nani baba yao?" Kwa sababu ya jambo hili, ukawapo msemo, "Hivi Sauli naye ni mmoja wa manabii?"
\v 13 Alipomaliza kutabiri, akafika mahali pa juu.
\s5
\v 14 1 Samweli 10: 14-16 Ndipo baba yake mdogo na akamuuliza Sauli na mtumishi wake, "Mlienda wapi?" Naye akamjibu, "Kuwatafuta punnda; tulipoona kwamba hatuwezi kuwapata, tukaenda kwa Samweli."
\v 15 Baba yake mdogo akasema, "Tafadhali niambie kile alichosema kwako Samweli,"
\v 16 Sauli akamjibu baba yake mdogo, "Alituambia waziwazi kwamba punda wamepatikana." Lakini kuhusu swala la ufalme alilosema Samweli hakumwambia.
\s5
\v 17 Basi Samweli aliwaita watu pamoja huko Mispa.
\v 18 Akwaambia watu wa Israeli, "Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli asemavyo: 'Niliwatoa Israeli kutoka Misri, na niliwaokoa kutoka nchi ya Wamisri, na kutoka mkono wa falme zote zilizowaonea.'
\v 19 Lakini leo mmemkataa Mungu wenu, awaokoaye kutoka kwenye majanga na mahangaiko; na mmemwambia, ' Tuwekee mfalme juu yetu; Sasa jihudhurisheni wenyewe mbele za BWANA kwa kabila na jamaa zenu."
\s5
\v 20 Kisha Samweli akawaleta kabila zote za Isareli karibu, na kulichagua kabila la Benyamini.
\v 21 Akawasogeza karibu kabila la Benyamini kwa kufuata jamaa zao; na jamaa ya Wamatri ikachaguliwa; na Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipokwenda kumtafuta, hakuweza kuonekana.
\s5
\v 22 Kisha watu walitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, "Bado yupo mtu mwingine ajaye?" BWANA akajibu, " Yeye mwenyewe kajificha kwenye mizigo."
\v 23 Wakaenda mbio na kumleta Sauli kutoka humo. Aliposimama kati yao, alikuwa mrefu kuliko watu wote kuanzia mabega yake kwenda juu.
\s5
\v 24 Kisha Samweli akawaambia watu, "Je, mnamuona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hakuna mtu kama yeye kati ya watu wote." Watu wote wakapiga Kelele, "Mfalme na aishi"
\s5
\v 25 Ndipo Samweli akawaambia watu desturi na sheria za ufalme, akaziandika katika kitabu, na kuziweke mbele za BWANA. Baadaye Samweli akawaruhusu watu waondoke kila mtu aende nyumbani kwake.
\s5
\v 26 Sauli pia alienda nyumbani kwake huko Gibea, akiwa na baadhi ya watu wenye nguvu, wenye mioyo iliyoguswa na Mungu.
\v 27 Lakini baadhi ya watu wasiofaa walisema, "Huyu mtu atatuokoaje?" Watu hawa walimdharau Sauli na hawakumletea zawadi zozote. Lakini Sauli alinyamaza kimya.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ndipo Nahashi Mwamoni akaenda na kupiga kambi kuzunguka Yabeshi Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, "Fanya mkataba nasi, na tutakutumikia,"
\v 2 Nahashi Mwamoni akawajibu, "Kwa sharti hili nitafanya mkataba na ninyi, kwamba wote niwang'oe macho ya kulia, na kwa kitendo hiki kilete fedheha katika Israeli yote."
\s5
\v 3 Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, "Tuache kwa siku saba, ili tuwatume wajumbe katika nchi yote ya Israeli. Ndiposa, kama hakuna mtu wa kutuokoa, tutasalimu amri kwako."
\s5
\v 4 Nao wajumbe wakafika Gibea, alipoishi Sauli, na wakawaeleza watu kile kilichotokea. Watu wote wakalia kwa sauti kuu.
\v 5 Na Sauli alikuwa akiwafuata nyuma maksai kutoka shambani. Sauli akauliza, "Watu wamepatwa na nini hadi wanalia?" Ndipo wakamweleza Sauli kile ambacho watu wa Yabeshi walikisema.
\s5
\v 6 Sauli aliposikia kile walichosema, Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, na akakasirika.
\v 7 Akashika nira ya maksai, akawakata hao ng'ombe vipande vipande, na akavituma hivyo vipande katika nchi yote ya Israeli kwa kuwatumia wajumbe, Akasema, "Yeyote asiyejitokeza akimfuata Sauli na Samweli, hivi ndivyo ng'ombe wake watakavyofanywa." Na hofu ya BWANA ikawaingia watu, na wakajitokeza wote kwa pamoja.
\v 8 Alipowahesabu hapo Beseki, watu wa Israeli walikuwa elfu mia tatu, na watu wa Yuda elfu thelathini.
\s5
\v 9 Wakawaambia wale wajumbe waliotumwa, "Mtawaambia watu wa Yabeshi Gileadi, 'Kesho, wakati wa jua kali, Mtaokolewa."' Basi wale wajumbe wakaenda na kuwaambia watu wa Yabeshi, na watu wakafurahi.
\v 10 Ndipo watu wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, "Kesho tutasalimu amri kwako, na utaweza kutufanyia chochote unachoona kinakupendeza."
\s5
\v 11 Siku iliyofuata Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu. Wakafika katikati ya Kambi wakati wa asubuhi, wakawashambulia na kuwashinda Waamoni ilipofika mchana. Waliosalimika nao walitawanyika, kiasi kwamba hata watu wawili hawakuachwa pamoja.
\s5
\v 12 Ndipo watu wakamwambia Samweli, "Wako wapi waliosema, 'Hivi kweli Sauli atatutawala?' Walete watu hao, ili tuwauwe."
\v 13 Lakini Sauli akasema, "Hakuna atakayeuwawa siku ya leo, kwa sababu leo BWANA amemuokoa Isreli."
\s5
\v 14 Kisha Samweli akawaambia watu, "Njoni, twendeni Gilgali na tuimarishe ufalme tena huko."
\v 15 Hivyo watu wote wakaenda Gilgali na wakamsimika Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA huko Gilgali. Na huko walitoa sadaka za amani mbele za BWANA, na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Samweli aksema na Israeli wote, "Nimesikia kila kitu mlichoniambia, na nimemweka mfalme juu yenu.
\v 2 Basi, yupo hapa mfalme aliyeko mbele yenu, mimi nimezeeka nakujaa mvi; na watoto wangu wako pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu hadi leo.
\s5
\v 3 Mimi niko hap, Nishuhudieni mbele za BWANA na mbele za mtiwa mafuta wake. Nimechukua ng'ombe wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimemdhulumu? Nimemwonea nani? Nimepokea rushwa kutoka mikono ya nani inipofushe macho yangu? Nishuhudieni, nami nitawarudishia
\s5
\v 4 Nao wakasema, Haujatudanganya, kutuonea, au kuiba chochote kutoka mkono wa mtu yeyote."
\v 5 Akawaambia, "BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake leo ni shahidi, kwamba hamkuona kitu mkononi mwangu." Na wao wakajibu, "BWANAni shahidi."
\s5
\v 6 Samweli akawaambia watu, "BWANA ndiye aliyemteua Musa na Haruni, na ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.
\v 7 Basi sasa, jihudhurisheni, ili niweze kutoa utetezi juu yenu kwa BWANA kuhusu matendo yote ya haki ya BWANA, ambayo aliwafanyia ninyi na baba zenu.
\s5
\v 8 Yakobo alipokuwa amefika Misri, na babu zenu walimlilia BWANA. BWANA alimtuma Musa na Haruni, waliowaongoza babu zenu kutoka Misri na wakaja kukaa sehemu hii.
\v 9 Lakini walimsahau BWANA Mungu wao; akawauza katika mkono wa Sisera, jemedari wa majeshi ya Hazori, katika mkono wa Wafilisti, na katika mkono wa mfalme wa Moabu; hawa wote walipigana na babu zenu.
\s5
\v 10 Wakamlilia BWANA mkasema, 'Tumefanya dhambi, kwa sababu tumemwacha BWANA na tumewatumikia Mabaali na Mashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya maadui zetu, na tutakutumikia.'
\v 11 Hivyo BWANA akawatuma Yerubu Baali, Bedani, Yefta na Samweli, na akawapa ushindi dhidi ya maadui zenu wote waliowazunguka, na kwamba mliishi kwa amani.
\s5
\v 12 Mlipoona kwamba Nahashi mfalme wa watu wa Amoni amekuja dhidi yenu, mkaniambia, 'Hapana! Badala yake, mfalme awepo atawale juu yetu'- ingawa BWANA, Mungu wenu, alikuwa mfalme wenu.
\v 13 Sasa yupo hapa mfalme ambaye mmemchagua, mliyemuomba na ambaye BWANA amemteua awe mfalme juu yenu.
\s5
\v 14 Ikiwa mnamhofu BWANA, mtumikieni, muitii sauti yake, msikaidi amri ya BWANA, basi wote wawili ninyi na mfalme anayewatawala mtakuwa wafuasi wa BWANA Mungu wenu.
\v 15 Kama hamtaitii sauti ya BWANA, mkaasi amri za BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya babu zenu.
\s5
\v 16 Hata sasa muwepo kabisa na muone jambo kubwa ambalo BWANA atalifanya mbele ya macho yenu.
\v 17 Je, leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, naye ataleta ngurumo na mvua. Ndipo mtajua na kuona kwamba uovu wenu ni mwingi, mlioufanya machoni pa BWANA, kujiombea mfalme wenu ninyi wenyewe."
\v 18 Hivyo Samweli akamwomba BWANA; na siku iyo hiyo BWANA akatuma ngurumo na mvua. Ndipo watu wote wakamwogopa sana BWANA pamoja na Samweli.
\s5
\v 19 Kisha watu wote wakamwambia Samweli, "Waombee watumishi wako kwa BWANA Mungu wako, ili tusife. Kwa maana tumeongeza uovu huu juu ya dhambi zetu tulipojiombea mfalme sisi wenyewe."
\v 20 Samweli akawajibu, "Msiogope. Mmefanya uovu wote huu, lakini msigeukie mbali na BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wenu wote.
\v 21 Wala msigeuke na kufuata mambo matupu yasiyo na faida au kuwaokoa, kwa sababu ni ubatili.
\s5
\v 22 Kwa ajili ya jina lake kuu, BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu kwa ajili yake.
\v 23 Kwangu mimi, iwe mbali nami kumtenda BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi. Badala yake, nitawafundisha njia iliyo njema na sahihi.
\s5
\v 24 Mcheni BWANA tu na mtumikieni yeye katika kweli kwa moyo wenu wote. Tafakarini mambo makuu aliyowatendeeni.
\v 25 Lakini kama mtadumu kufanya uovu, ninyi wote na mfalme wenu mtaangamizwa."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sauli alikwa na umri wa miaka [thelathini] alipoanza kutawala; alipokuwa ametawala Israeli kwa miaka [arobaini],
\v 2 aliwachagua wanaume elfu tatu wa Israeli. Elfu mbili walikuwa pamoja naye huko Mikmashi na katika nchi ya milima ya Betheli, wakati huo wale elfu moja walikuwa pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini. Askari waliobaki aliwarudisha nyumbani, kila mtu hemani kwake.
\s5
\v 3 Yonathani akaishinda ngome ya jeshi la Wafilisti iliyokuwa Geba na Wafilisti wakasikia habari hiyo. Baadaye Sauli alipiga tarumbeta katika nchi yote, akisema, "Sikieni enyi Waebrania."
\v 4 Israeli yote imesikia kwamba Sauli ameipiga ngome ya Wafilisti, na pia kwamba Israeli imekuwa uvundo kwa Wafilisti. Ndipo askari wakaitwa kwa pamoja kuungana na Sauli huko Gilgali.
\s5
\v 5 Wafilisti walijikusanya pamoja kupigana dhidi ya Waisraeli: magari elfu tatu, watu elfu sita wakuendesha magari, na majeshi mengi kama mchanga ufukoni mwa bahari. Wakapanda na kupiga kambi huko Mikimashi, mashariki mwa Beth aveni.
\s5
\v 6 Watu wa Israeli walipoona kuwa wapo katika matatizo -kwa maana watu walikata tamaa, wakajificha kwenye mapango, kwenye vichaka, kwenye miamba, kwenye visima na katika mashimo.
\v 7 Baadhi ya Waebrania walipanda kwenda Yordani katika nchi ya Gadi na Gileadi. Lakini Sauli alibaki Gilgali, na watu waliomfuata wakitetemeka.
\s5
\v 8 Alisubiri kwa siku saba, muda uliopangwa na Samweli. Lakini Samweli hakufika huko Gilgali, na watu wakatawanyika mbali na Sauli.
\v 9 Sauli akasema, "Nileteeni sadaka ya kuteketezwa na sdaka ya amani." Kisha akatoa sadaka ya kuteketezwa.
\v 10 Mara tu alipomaliza kutoa sadaka ya kuteketezwa Samweli akawasili. Sauli akatoka nje wakutane na kumsalimia.
\s5
\v 11 Basi Samweli akasema, "Umefanya nini?" Sauli akajibu, "Nilipoona kwamba watu wanaiacha, na kwamba umechelewa hukufika kwa muda uliopangwa, na kwamba Wafilisti wamekwisha jikusanya huko Mikmashi,
\v 12 nikasema, 'Sasa Wafilisti watashuka dhidi yangu huko Gilgali, na sijaomba kibali cha BWANA.' Kwa hiyo nikajilazimisha mwenyewe kutoa sadaka ya kuteketezwa."
\s5
\v 13 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, "Umetenda mambo ya kipumbavu. Hukuheshimu amri ya BWANA Mungu wako aliyokupatia. Kwa maana BWANA angeutengeneza utawala wako juu ya Israeli milele.
\v 14 Lakini sasa utawala wako hautaendelea. BWANA ametafuta mtu anayekubaliwa na moyo wake, kwa sababu wewe hukutii alichokuamuru."
\s5
\v 15 Ndipo Samweli akasimama akapanda kutoka Gilgali hadi Gibea ya Benyamini. Basi Sauli akawahesabu watu waliokuwapo pamoja naye, idadi yao ilikuwa kama watu mia sita.
\v 16 Sauli, mtoto wake Yonathani, na watu waliokuwa pamoja nao, wakabaki Geba ya Benyamimni. Lakini Wafilisti wakapiga kambi huko Mikmashi.
\s5
\v 17 Wateka nyara makundi matatu wakaja kutoka kambi ya Wafilisti. Kundi moja likapinda kuelekea Ofra, hadi nchi ya Shuali.
\v 18 Kundi jingine likageuka kuelekea Bethholoni, na kundi jingine likaelekea katika mpaka kulikabili bonde la Seboimu kuelekea jangwani.
\s5
\v 19 Hakuna hata mhunzi aliyeonekana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walisema, " Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki."
\v 20 Lakini Waisraeli wote huwa wakiteremka kwa Wafilisti, kila mtu kunoa jembe lake, sululu yake, shoka lake na mundu wake.
\v 21 Gharama za kunoa ncha za majembe, sululu, mashoka na kunyoosha michokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
\s5
\v 22 Hivyo siku ya vita, hakukuwa na mapanga au mikuki iliyoonekana katika mikono yoyote ya askali waliokuwa na Sauli na Yonathani; Ni Sauli na mtoto wake tu ndio walikuwa nazo.
\v 23 Vikosi vya Wafilisti wakatokeza katika nija ya Mikmashi.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Siku moja, Yonathani mwana wa Sauli alimwambia mbeba silaha wake aliye mdogo, "Njoo, hebu twende hadi upande mwingine kwenye ngome ya Wafilisti." Lakini hakumjulisha baba yake.
\s5
\v 2 Sauli alikuwa akikaa nje ya mji wa Gibea chini ya mti wa mkomamanga ulio katika Migroni. Takribani watu mia sita walikwa pamoja naye,
\v 3 akiwemo Ahiya mwana wa Ahitubu (nduguye Ikabodi) mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Watu hao hawakujua kwamba Yonathani ameondoka.
\s5
\v 4 Katikati ya vichochoro, ambavyo Yonathani alinuia kuvipita hadi ngome ya Wafilisti, kulikuwa na mwamba wenye mteremko mkali upande mmoja, na mteremko mkali upande mwingine. Jabali moja liliitwa Bosesi, na jingine liliitwa Sene.
\v 5 Lile jabali lenye mteremko mkali zaidi liliinuka upande wa kaskazini mbele ya Mikmashi, na jingine upande wa kusini mbele ya Geba.
\s5
\v 6 Yonathani akamwambia kijana mbeba silaha, "Njoo, na tuvuke hadi ngome ya hawa wasiotahiriwa. Pengine BWANA atatenda kwa niaba yetu, kwa maana hakuna kitu kiwezacho kumzuia BWANA asiokoe kwa wengi au kwa watu wachache."
\v 7 Mbeba silaha wake akajibu, "Fanya kila kitu kilicho ndani ya moyo wako. Songa mbele, tazama, niko pamoja nawe, nitatii maagizo yako yote."
\s5
\v 8 Ndipo Yonathani akasema, "Tutavuka twende kwa watu hao, na tutajionesha wenyewe kwao.
\v 9 Kama watatuambia, 'Subirini hapo hadi tutakapokuja kwenu' - basi tutabaki katika sehemu yetu na hatutavuka kwenda kwao.
\v 10 Lakini kama watajibu, 'Njoni kwetu,' ndipo tutavuka; kwa sababu BWANA amewaweka mkononi mwetu. Hii ndiyo itakuwa ishara yetu."
\s5
\v 11 Kwa hiyo wote wawili wakajifunua mbele ya ngome ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, "Angalia, Webrania wanakuja kutokea kwenye mashimo walimojificha."
\v 12 Ndipo watu wa ile ngome wakamwita Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, "Njoni huku kwetu, tutawaonesha jambo fulani." Na Yonathani akamwambia mbeba silaha wake; "Nifuate nyuma yangu, kwa sababu BWANA amewaweka katika mkono wa Israeli."
\s5
\v 13 Yonathani alipanda juu kwa mikono na miguu yake, na mbeba silaha akimfuata nyuma yake. Wafilisti waliuwawa mbele ya Yonathani, na mbeba silaha wake akiwaua baadhi nyuma yake.
\v 14 Hilo shambulio la kwanza walilofanya Yonathani na mbeba silaha wake, waliua watu wapatao ishirini katika urefu wa nusu handaki kwenye eka moja ya ardhi.
\s5
\v 15 Kukawa na hofu kubwa katika kambi, uwandani, na katika watu. Hata ngome ya jeshi na watekaji nyara nao wakawa na hofu kubwa
\s5
\v 16 Ndipo walinzi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona kundi la askari wa Wafilisti likitawanyika, wakienda kule na huku.
\v 17 Kisha Sauli akawaambia watu aliokuwa nao, "Mjihesabu ili muone nani hayupo hapa."Walipokuwa wamehesabu, wakagundua kuwa Yonathani na mbebaji wa silaha zake hawapo.
\s5
\v 18 Sauli akamwambia Ahiya, "Lete hapa naivera ya Mungu"- kwa maana siku hiyo Ahiya alivaa naivera akiwa pamoja na askari wa Israeli.
\v 19 Wakati Sauli akiongea na kuhani, kelele na ghasia kubwa iliendelea na kuongezeka katika kambi ya Wafilisti. dipo sauli akamwambia kuhani, "Acha kazi unayofanya."
\s5
\v 20 Sauli na watu wote aliokuwa nao wakajipanga na kwenda kwenye mapigano. Upanga wa kila Mfilisti ulikwa juu ya Mfilisti mwenzake, na kulikuwa na ghasia kubwa.
\v 21 Basi Waebrania ambao mwanzoni walijiunga na Wafilisti, na kwenda kwenye kambi yao, wao pia waliungana na Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani.
\s5
\v 22 Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika milima karibu na Efraimu waliposikia kwamba Wafilisti wamekimbia, nao pia wakawafuata Wafilisti nakuwafukuza kwenye hiyo vita.
\v 23 Hivyo siku hiyo BWANA aliwaokoa Israeli, na mapigano yalivuka kupitiliza Beth aveni.
\s5
\v 24 Siku hiyo watu wa Israeli walifadhaika kwa sababu Sauli aliwaweka watu chini ya kiapo akasema, "Na alaaniwe mtu atakaye kula chakula kabla ya jioni na kabla sijalipiza kisasi kwa maadui zangu." Hivyo hakuna hata mmoja kati ya watu wote aliyeonja chakula.
\v 25 Ndipo watu wote wakaingia msituni na kuona asali ikiwa juu ya ardhi.
\v 26 Watu walipoingia humo msituni, asali ilitiririka, lakini hakuna aliyeweka mkono wake kinywani kwa maana watu waliogopa kiapo.
\s5
\v 27 Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kwamba baba yake amewaagiza watu kwa kiapo. Akanyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya kwenye sega la asali. Kisha akanyoosha mkono wake hadi kinywani mwake, na macho yake yakaangaziwa.
\v 28 Ndipo mmoja wa watu hao, akamwambia, "Baba yako aliwaagiza watu kwa mkazo na kwa kiapo, kwa kusema, 'Alaaniwe mtu atakaye kula chakula kwa siku ya leo,' ingawa watu wamedhoofika kwa ajili ya njaa."
\s5
\v 29 Baadaye Yonathani alisema, "Baba yangu amefanya matatizo katika nchi. Angalia jinsi macho yangu alivyotiwa nuru kwa sababu nilionja asali hii kidogo.
\v 30 Je, siyo vivuri sana kama leo watu wangekula bila kizuizi nyara walizopata kutoka kwa maadui zao? Kwa sababu sasa mauaji hayakuwa makubwa katikati ya Wafilisti."
\s5
\v 31 Siku hiyo waliwashambulia Wafilisti kutoka Mikmashi hadi Aiyaloni. Na watu walikuwa wamechoka sana.
\v 32 Hivyo watu wakazivamia nyara na kuchukua kondoo, ng'ombe na ndama na kuwachinja hapo chini. Watu walikula nyama zao pamoja na damu.
\s5
\v 33 KIsha wakamwambia Sauli, "Tazama, watu wanamtenda BWANA dhambi kwa kula pamoja na damu." Sauli akasema, "Mmetenda isivyo haki. Sasa, viringisheni jiwe kubwa kwangu." Sauli akasema,
\v 34 "Nendeni kati watu, na muwaambie, 'Kila mtu alete ng'ombe na kondoo wake, wawachinje hapa, na kuwala. Msimtende BWANA dhambi kwa kula na damu."' Kwa hiyo watu wote wakaleta kila mtu na ng'ombe wake usiku huo na kuwachinja mahali hapo.
\s5
\v 35 Sauli akamjengea BWANA madhabahu, ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kumjengea BWANA.
\s5
\v 36 Ndipo Sauli akasema, "Haya tuwafukuze Wafilisti usiku na kuwateka nyara hadi asubuhi; tusimwache hata mtu mmoja akiwa hai." Nao wakamjibu, "Fanya unaloona linakupendeza." Lakini kuhani akasema, "Hebu na tumkaribie Mungu mahali hapa."
\v 37 Sauli alitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, "Je, inanipasa kuwafukuza Wafilisti? Je, utawaweka katika mkono wa Israeli?" Lakini siku hiyo BWANA hakumjibu kitu.
\s5
\v 38 Ndipo Sauli akasema, "Njoni hapa, viongozi wote wa watu; mjue na kuona jinsi dhambi hii ilivyotokea leo.
\v 39 Kwa maana, kama BWANA aishivyo, aliyewaokoa Israeli, hata kama angekuwa mwanangu Yonathani, atapaswa kufa." Lakini hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa watu aliye mjibu neno.
\s5
\v 40 Basi akawaambia Waisraeli wote, "Simameni upande mmoja, na mimi na Yonathani tutasimama upande mwingine." Kisha watu wakamwambia Sauli, "Fanya lile unaloona jema kwako."
\v 41 Kwa hiyo, Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, "Tuoneshe Thumimu." Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu walinusurika kuchaguliwa.
\v 42 Basi Sauli akasema, "Tupa mawe ya bahati nasibu tuone kati yangu na mwanangu Yonathani." Ndipo Yonathani akatwaliwa.
\s5
\v 43 Kisha Sauli akamwambia Yonathani, "Niambie umefanya nini." Yonathani akamwambia baba yake, "Nilionja asali kidogo kwa kutumia ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwangu. Niko hapa; Nitakufa."
\v 44 Sauli akasema, "Mungu afanye hivyo na kuzidi hata kwangu, kama Yonathani hautakufa."
\s5
\v 45 Basi watu wakamuuliza Sauli, "Je, inampasa Sauli afe, ni nani aliyetekeleza ushindi huu mkubwa kwa ajili ya Israeli? Mbali na hayo! Kama BWANA aishivyo, hata unywele mmoja wa kichwa chake hautaanguka chini, kwa maana leo amefanya kazi pamoja na Mungu." Hivyo hao watu walimuokoa Yonathani ili asife.
\v 46 Basi Sauli akasita kuwafuatia Wafilisti, nao wakarudi katika makao yao.
\s5
\v 47 Sauli alipoanza kutawala juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote kila upande. Alipigana dhidi ya Moabu, dhidi ya watu wa Amoni, Edomu, wafalme wa Zoba, na Wafilisti. Popote alipogeukia aliwapiga kwa adhabu adui zake.
\v 48 Alitenda kwa ushujaa mkubwa na kuwashinda Waamaleki. Aliwaokoa Israeli kutoka mikono ya watu ambao waliwateka nyara.
\s5
\v 49 Basi wana wa Sauli walikuwa ni hawa Yonathani, Ishvi, na Malkishua. Na majina ya binti zake wawili yalikuwa ni haya, Merabu mzaliwa wa kwanza, na mdogo aliitwa Mikali.
\v 50 Jina la mke wa Sauli aliitwa Ahinoamu; naye alikuwa binti Ahimaasi. Na jina la Jemedari wa jeshi lake aliitwa Abneri mwana wa Neri, baba mdogo wa Sauli.
\v 51 Kishi alikuwa baba yake Sauli; na Neri alikuwa baba yake na Abneri, wote walikuwa wana wa Abieli.
\s5
\v 52 Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti katika siku zote za Sauli. Naye alipomwona mtu yeyote mwenye nguvu, au mtu yeyote jasiri, alimuunganisha kwake.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Samweli akamwambia Sauli, "BWANA alinituma nikutie mafuta uwe mfalme wa watu wake Israeli. Basi sikiliza maneno ya BWANA.
\v 2 Hivi ndivyo BWANA wa majeshi asemavyo, 'Nilichunguza jinsi Amaleki alivyomfanyia Israeli kwa kuwapinga njiani, walipopanda kutoka Misri.
\v 3 Sasa nenda umshambulie Amaleki na ukaangamize kabisa vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache, ua wote mwanamme na mwanamke, mtoto na mtoto mchanga, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."'
\s5
\v 4 Sauli akwaita watu na kuwahesabu katika mji wa Talemu: watu mia mbili elfu waendao kwa miguu, na watu elfu kumi kutoka Yuda.
\v 5 Kisha Sauli akaja hadi mji wa Amaleki akangoja huko bondeni.
\s5
\v 6 Ndipo Sauli akawaambia Wakeni, "Nendeni, muondoke, mkajitenge na Waamaleki, nisije kuwaangamiza pamoja nao. Kwa maana ulionesha wema kwa watu wote wa Israeli, walipotoka Misri." Kwa hiyo Wakeni wakajitenga na Waamaleki.
\v 7 Kisha sauli akawashambulia Waamaleki, kutoka Havila hadi kufika Shuri, ulio mashariki mwa Misri.
\s5
\v 8 Basi akamchukua Agagi mfalme wa Waamaleki akiwa hai; aliwaangamiza kabisa watu wote kwa ncha ya upanga.
\v 9 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi akiwa hai, pamoja na kondoo wazuri, ng'ombe, ndama wanono, na wanakondoo. Kila kitu kilichokuwa kizuri, hawakukiangamiza. Bali waliangamiza kabisa chochote kilichodharaulika na kisicho na thamani.
\s5
\v 10 Baadaye neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,
\v 11 "Inanihuzunisha kwamba nimemchagua Samweli awe mfalme, kwa maana aligeuka nyuma asinifuate na hakutekeleza maagizo yangu." Samweli alikasirika; akamlilia BWANA usiku kucha.
\s5
\v 12 Samweli aliamka mapema akutane na Sauli wakati wa asubuhi. Samweli aliambiwa, "Sauli alifika Karmeli na amejijengea ukumbusho kwa ajili yake, kisha aligeuka na kuendelea chini hadi Gilgali." Ndipo
\v 13 Samweli akamwendea Sauli, na Sauli akamwambia, "Umebarikiwa na BWANA! Nami nimetekeleza amri ya BWANA."
\s5
\v 14 Samweli akasema, "Hicho kilio cha kondoo ni cha nini basi masikioni mwangu, na hiyo milio ya ng'ombe ninayosikia?
\v 15 Sauli akamjibu, "Wao wamewaleta kutoka kwa Waamaleki. Kwa sababu watu waliwaacha hai kondoo wazuri na ng'ombe, kwa ajili ya sadaka kwa BWANA Mungu wako. Zilizobaki tuliziangamiza kabisa."
\v 16 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, "Subiri nitakumbia kile ambacho BWANA amekisema kwangu usiku." Sauli akamwambia, "Sema!"
\s5
\v 17 Samweli akasema, "Ingawa wewe ni mdogo machoni pako mwenyewe, je, hukufanywa mkuu wa kabila za Israeli? Na BWANA akakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli;
\v 18 BWANA alikutuma katika safari yako akisema, 'nenda na uangamize kabisa wenye dhambi, Waamaleki, na upigane dhidi yao hadi wameangamizwa.'
\v 19 Kwa nini basi haukuitii sauti ya BWANA, bali badala yake ulishikilia nyara na ukafanya uovu machoni pa BWANA?"
\s5
\v 20 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, "Kweli kabisa niliitii sauti ya BWANA, Na nimeifuata njia ambayo BWANA alinituma. Nimemteka Agagi, mfalme wa Waamaleki, na kuwaangamiza kabisa Waamaleki.
\v 21 Lakini watu walichukua baadhi ya nyara-kondoo na ng'ombe, na vitu vizuri vilivyokusudiwa kuangamizwa, ili wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali."
\s5
\v 22 Samweli akajibu, "Je, BWANA hufurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama ilivyo kuitii sauti yake? Utii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia ni bora kuliko mafuta ya beberu.
\v 23 Kwa maana uasi ni sawa na dhambi ya uchawi, na ukaidi ni sawa na uovu na udhalimu. Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, naye pia amekukataa usiwe mfalme."
\s5
\v 24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, "Nimetenda dhambi; kwa maana nimevunja amri ya BWANA na maneno yako, kwa sababu niliwaogopa watu na kuitii sauti yao.
\v 25 Sasa, tafadhali nisamehe dhambi yangu, na urudi nami ili nipate kumcha BWANA."
\s5
\v 26 Samweli akamwambia Sauli, "Sitarudi pamoja na wewe; kwa sababu umekataa neno la BWANA, naye BWANA amekukataa usiwe mfalme juu ya Israeli."
\v 27 Samweli alipogeuka kuondoka, Sauli akashika pindo la kanzu yake, na likachanika.
\s5
\v 28 Samweli akamwambia, "BWANA ameuchana ufalme wa Israeli kutoka kwako leo na amempa ufalme huo jirani yako, aliye bora kuliko wewe.
\v 29 Pia, yeye ni Uwezo wa Israeli hatasema uongo wala kubadili nia yake; kwa sababu si mwanadamu, kwamba abadili nia yake."
\s5
\v 30 Kisha Sauli akasema, "Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali nipe heshima wakati huu mbele ya wakuu wa watu wangu na mbele ya Israeli. Urudi tena pamoja nami, kusudi niweze kumcha BWANA, Mungu wako."
\v 31 Hivyo Samweli akamrudia tena Sauli, na Sauli akamcha BWANA.
\s5
\v 32 Kisha Samweli akasema, "Mmlete hapa kwangu Agagi mfalme wa Waamaleki." Agagi akafika kwake akiwa amefungwa minyororo na kusema, "Hakika uchungu wa kifo umepita."
\v 33 Naye Samweli akamjibu, "Jinsi upanga wako ulivyofanya wanawake wapoteze watoto, vivyo hivyo mama yako naye hatakuwa na mtoto miongoni mwa wanawake." Kisha Samweli akamkata Agagi vipande vipande mbele za BWANA huko Gilgali.
\s5
\v 34 Samweli akaenda Rama, na Sauli akapanda kwenda nyumbani kwake Gibea ya Sauli.
\v 35 Samweli hakumuona tena Sauli hadi siku ya kifo chake, lakini alimwombolezea Sauli. Na BWANA alijuta kwa kumfanya Sauli awe mfalme juu ya Israeli.
\s5
\c 16
\p
\v 1 BWANA akamwambia Samweli, "Utamlilia Sauli kwa muda gani, ikiwa nimemkataa asiwe mfalme juu ya Israeli? Ijaze pembe yako mafuta na uende. Nitakutuma kwa Yese akaaye Bethlehemu, maana nimejichagulia mfalme katika wanawe.
\s5
\v 2 Samweli akasema, "Jinsi gani nitaenda? Kama Sauli akisikia jambo hili, ataniua." BWANA akasema, "chukua mtamba na useme, 'Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA.'
\v 3 Umwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonesha kile utakachofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakaye kuambia."
\s5
\v 4 Samweli akafanya kama BWANA alivyosema na akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji walikuwa wakitetemeka walipokuja kuonana naye na wakasema, "Je, umekuja kwa amani?"
\v 5 Naye akasema, "kwa amani; Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA. Jitoeni wenyewe kwa BWANA kwa ajili ya dhabihu na muandamane nami," Na akamweka wakfu Yese na watoto wake kwa BWANA, na baadaye aliwaita wote kwenye dhabihu.
\s5
\v 6 Walipofika, akamwangalia Eliabu na akajisemea mwenyewe kwamba mtiwa mafuta wa BWANA hakika amesimama mbele yake.
\v 7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, "Usimwangalie sura yake ya nje, au kimo cha umbo lake; kwa sababu nimemkataa. Maana BWANA haangalii kama mtu aangaliavyo; mtu hutazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo."
\s5
\v 8 Kisha Yese akamwita Abinadabu akamwambia apite mbele ya Samweli. Na Samweli akasema, "Hata huyu BWANA hakumchagua."
\v 9 Kisha Yese akmwambia Shama apite karibu. Na Samweli akasema, "Hata huyu BWANA hakumchagua."
\v 10 Yese akawaleta watoto wake saba wakapita mbele ya Samweli. Na Samweli akamwambia Yese, "Hakuna hata mmoja aliyechaguliwa na BWANA kati ya hawa."
\s5
\v 11 Kisha Samweli akamuulia Yese, "Je, watoto wako wote wako hapa?" Naye akajibu, "Yupo mdogo kabisa lakini anachunga kondoo." Samweli akamwambia Yese, "Tuma watu wakamwite; maana hatutakaa chini hadi atakapofika hapa."
\v 12 Yese akawatuma watu wakamleta. Naye kijana huyu alikuwa mwekundu na mwenye macho mazuri na mwenye muonekano mzuri. BWANA akasema, "Amka, umtie mafuta; maana huyu ndiye."
\s5
\v 13 Ndipo Samweli akachukua pembe yenye mafuta na kumtia mafuta katikati ya kaka zake. Roho wa BWANA akamwijia Daudi kwa nguvu tangu siku hiyo na kuendelea. Kisha Samweli akanyanyuka na kwenda Rama.
\s5
\v 14 Basi Roho wa BWANA akamwacha Sauli, badala yake roho ya ubaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua.
\v 15 Watumishi wa Sauli wakamwambia, "Tazama, roho ya ubaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.
\v 16 Haya bwana wetu hebu sasa amuru watumishi wako walio mbele yako wamtafute mtu mwenye ujuzi wa kupiga kinubi. Basi ikwa roho wa ubaya kutoka kwa Mungu yuko juu yako, atakipiga kinubi nawe utajisikia vizuri."
\s5
\v 17 Sauli akawaambia watumishi wake, "Mnitafutie mtu anayeweza kupiga vizuri na mmlete kwangu."
\v 18 Ndipo kijana mmoja kati yao akajibu, na kusema, "Nimemuona mtoto wa Yese Mbethtelehemu, aliye mjuzi katika kupiga, ni mwenye nguvu, mtu jasiri, mtu wa vita, mwenye busara aongeapo, mtu mzuri kwa uso; na BWANA yuko pamoja naye."
\v 19 Hivyo Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, na kusema, "Nitumie mtoto wako Daudi, anayewatunza kondoo."
\s5
\v 20 Yese akamchukua punda aliyebeba mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, na akamtuma kwa Sauli pamoja na vitu hivyo.
\v 21 Ndipo Daudi akafika kwa Sauli na kuanza kazi yake. Sauli alimpenda sana Daudi, na akawa mbeba silaha wake.
\s5
\v 22 Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, akisema, "Mruhusu Daudi awe mbele yangu, maana amepata kibali machoni pangu."
\v 23 Wakati wowote roho ya usumbufu kutoka kwa Mungu ikiwapo juu ya Sauli, Daudi alichukuwa kinubi na kukipiga. Hivyo Sauli angeburudishwa na kupona, na huyo roho wa usumbufu angemtoka.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Basi Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa ajili ya vita. Walikusanyika huko Soko, iliyoko Yuda. Nao wakapiga kambi kati ya Soko na Aseka katika Efesdamimu.
\s5
\v 2 Sauli na watu wa Israeli alijikusanya na kuweka kambi katika bonde la Ela, na wakapanga vita kukutana na Wafilisti.
\v 3 Wafilisti walisimama juu ya mlima upande mmoja, na Iraeli nao walisimama juu ya mlima upande mwingine wakitenganishwa na bonde kati yao.
\s5
\v 4 Mtu mmoja mwenye nguvu akatoka katika kambi ya Wafilisti, mtu huyo aliitwa Goliathi wa Gathi, kimo chake mikono sita na shubiri moja.
\v 5 Alikuwa na chepeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya chuma. Hiyo dirii ilikuwa na uzito wa shekeli elfu hamsini za shaba.
\s5
\v 6 Alikuwa na mabampa ya shaba kwenye miguu yake na mkuki wa shaba katikati ya mabega yake.
\v 7 Ule mpini wa mkuki wake ulikuwa mkubwa, wenye kamba iliyo na kitanzi kwa ajili ya kuutupia kama kamba ya sindano ya mfumaji. Kichwa cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa shekeli mia sita za chuma. Aliyembebea ngao alitembea mbele yake.
\s5
\v 8 Alisimama akayapigia kelele majeshi ya Israeli, "Kwa nini mmekuja na mmejipanga kwa ajili ya vita? Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Chagueni mtu kutoka kwenu ateremke na kuja kwangu.
\v 9 Kama anaweza kupigana nami na kuniua, hapo ndipo tutakuwa watumwa wenu. Lakini kama nitamshinda na kumuua, basi mtakuwa watumwa wetu na kututumikia."
\s5
\v 10 Mfilisti huyo akasema tena, "Leo ninayapa changamoto majeshi ya Israeli. Mnipe mtu ili tuweze kupigana naye."
\v 11 Sauli na Israeli wote waliposikia alichosema Mfilisti huyo, walikata tamaa na kuogopa sana.
\s5
\v 12 Basi Daudi alikuwa mwana wa Mwefraimu wa Bethtelehemu ya Yuda, aliyeitwa Yese. Naye alikuwa na watoto wanane wa kiume. Yese alikuwa mtu mzee katika siku za Sauli, mwenye umri mkubwa kati ya watu.
\v 13 Watoto watatu wakubwa wa Yese walimfuata Sauli vitani. Majina ya watoto wake watatu waliokwenda vitani yalikwa ni Eliabu mzaliwa wa kwanza, aliyemfuata Abinadabu, na watatu aliitwa Shama.
\s5
\v 14 Daudi ndiye aliyekuwa mdogo kabisa. Hao wakubwa watatu walimfuata Sauli.
\v 15 Basi Daudi alikwenda na kurudi akipita kati ya majeshi ya Sauli akiwa na kondoo za baba yake huko Bethtelehemu, ili kuwachunga.
\v 16 Kwa muda wa siku arobaini yule Mfilisti mwenye nguvu alikuwa akijitokeza asubuhi na jioni kwa ajili ya vita.
\s5
\v 17 Kisha Yese akamwambia mwanawe Daudi, "Wapelekee kaka zako efa ya bisi na hii mikate kumi, na uzipeleke upesi kule kambini kwa ajili ya kaka zako.
\v 18 Pia peleka hizi jibini kumi kwa jemedari wa kikosi chao cha elfu. Ukawaangalie wako na hali gani kisha uniletee habari kuhusu wanavyoendelea vizuri.
\s5
\v 19 Kaka zako wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli katika bonde la Ela, wanapigana na Wafilisti."
\v 20 Daudi aliamka asubuhi na mapema na kuliacha kundi chini ya uangalizi wa mchungaji. Akachukua vile vitu na kuondoka, kama Yese alivyomwamuru. Akafika kambini wakati jeshi linaondoka kwenda uwanja wa vita wakipiga kelele za vita.
\v 21 Nao Israeli na Wafilisti walijipanga kivita, jeshi dhidi ya jeshi.
\s5
\v 22 Daudi aliviacha vitu vyake kwa mtunza mahitaji, akalikimbilia jeshi, na kuwasalimia kaka zake.
\v 23 Alipoongea nao, yule mtu mwenye nguvu, Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akajitokeza kutoka majeshi ya Wafilisti, naye akasema maneno yaleyale kama hapo mwanzo. Naye Daudi akayasikia.
\v 24 Watu wote wa Israeli walipomwona Goliathi, walimkimbia na waliogopa sana.
\s5
\v 25 Watu wa Israeli walisema, "Umemuona mtu huyu aliyejitokeza? Amekuja kuipa changamoto Israeli. Basi mfalme atampa mali nyingi mtu atakayemua, atamuozesha binti yake, na familia ya baba yake haitalipa kodi katika Israeli."
\s5
\v 26 Daudi akawauliza watu waliosimama karibu naye, "Atafanyiwa nini mtu ambaye atamuua Mfilisti huyu na kuiondolea Israeli fedheha? Ni nani Mfilisti huyu asiyetahiriwa ayatukanaye majeshi ya Mungu aliye hai?"
\v 27 Ndipo watu wakarudia kile walichokuwa wamesema na kumwambia, "Ndivyo iitakavyofanyika kwa mtu atakayemuua."
\s5
\v 28 Kaka yake mkubwa Eliabu, alisikia wakati akisema na watu. Hasira ya Eliabu ikawaka moto dhidi ya Daudi, naye akamuuliza, "Kwa nini umekuja hapa? Wale kondoo wachache umewaacha na nani huko nyikani? Nakijua kiburi chako, na utundu wa moyo wako; maana umekuja hapa ili uweze kuona mapigano."
\v 29 Naye Daudi akamjibu, "Nimefanya nini sasa? Mimi si nuliuliza swali tu?
\v 30 Akamgeukia mtu mwingine na kumwacha huyo, na kusema vivyo hivyo. Nao watu wakajibu vilevile kama mwanzo.
\s5
\v 31 Maneno aliyosema Daudi yaliposikika, askari waliyasema tena kwa Sauli, naye akawatuma kwa Daudi.
\v 32 Kisha Daudi akamwambia Sauli, "Pasiwepo moyo wa mtu atakayezimia kwa sababu ya Mfilisti huyo; Mtumishi wako atakwenda kupigana na Mfilisti huyu."
\v 33 Sauli akamwambia Daudi, "Huwezi kumpinga Mfilisti ama kupigana naye; wewe ni kijana tu, na yeye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake."
\s5
\v 34 Lakini Daudi akamwambia Sauli, "Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake. Mara simba au dubu alikuja akamchukua mwana kondoo kutoka kundini,
\v 35 Nilimfukuza na kumshambulia na kumpokonya kutoka kinywani mwake. Na aliponirukia, nilimshika ndevu zake, nilimpiga, na kumuua.
\s5
\v 36 Mtumishi wako amekwisha kmuua simba na dubu. N huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa wanyama hao, kwa kuwa ameyadharau majeshi ya Mungu aliye hai."
\s5
\v 37 Daudi akasema, "BWANA aliyeniokoa kutoka makucha ya simba na makucha ya dubu. Ataniokoa kutoka mkono wa Mfilisti huyu." Kisha Sauli akamwambia Daudi, "Nenda, BWANA awe pamoja nawe."
\v 38 Sauli akamvika Daudi vazi lake la vita. Akamvika chepeo ya shaba kichwani pake, na akamvika koti la chuma.
\s5
\v 39 Daudi akaufunga upanga wake juu ya vazi la Sauli. Lakini hakuweza kutembea, kwa sababu hakupata mafunzo kwa mavazi hayo. Ndipo Daudi akamwambia Sauli, "Siwezi kwenda kupigana nikiwa na haya, maana sikupata mafunzo kwa haya." Kwa hiyo Daudi akayavua.
\v 40 Akachukua fimbo mkononi mwake na akachagua mawe matano laini kutoka katika kijito; akayaweka kwenye mfuko wake wa kichungaji. Kombeo lake lilikuwa mkononi akawa anamsogelea yule Mfilisti.
\s5
\v 41 Yule Mfilisti akaja na kumsogelea Daudi, mbeba ngao yake akiwa mbele yake.
\v 42 Mfilisti alipotazama kila upande na kumuona Daudi, akamdharau, maana alikuwa kijana tu, mwekundu, na umbo la kupendeza.
\v 43 Ndipo Mfilisti akamuuliza Daudi, "Je, mimi ni mbwa, hata ukanijia na fimbo? Naye Mfilisti kwa miungu yake akamlaani Daudi.
\s5
\v 44 Huyo Mfilisti akamwambia Daudi, "Njoo kwangu, na nyama yako nitawatupia ndege wa angani na wanyama wa mwituni."
\v 45 Daudi akamjibu Mfilisti, "Unaniijia kwa upanga, kwa mkuki na mkuki mdogo. Bali mimi nakuijia kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa Majeshi ya Israeli, uliyemdharau.
\s5
\v 46 Leo BWANA atanipa ushindi dhidi yako, na nitakuua na kukiondoa kichwa chako kwenye kiwiliwili. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni walioko duniani mizoga ya jeshi la Wafilisti, ili dunia yote ijue kwamba yupo Mungu katika Israeli,
\v 47 na kusanyiko hili lote lijue kwamba BWANA hatoi ushindi kwa upanga wala kwa mkuki. Kwa kuwa vita ni ya BWANA, na atawaweka katika mkono wetu."
\s5
\v 48 Mfilisti aliponyanyuka na kukaribia akutane na Daudi, ndipo Daudi akakimbia kwa haraka kuelekea jeshi la adui ili akutane naye.
\v 49 Daudi aliweka mkono wake mfukoni, akachukua jiwe kutoka humo, akalitupa kwa kombeo, na likampiga Mfilisti kwenye paji la uso, akaanguka chini kifudifudi.
\s5
\v 50 Daudi alimshinda Mfilisti kwa kombeo na kwa jiwe moja. Alimpiga huyo Mfilisti na kumuua. Mkononi mwa Daudi hakukuwa na upanga.
\v 51 Ndipo Daudi akakimbia akasimama juu ya Mfilisti na kutwaa upanga wake, akauchomoa kutoka alani, akamuua, na kukata kichwa chake kwa upanga huo.
\s5
\v 52 Ndipo watu wa Israeli na wale wa Yuda wakaamka kwa kelele, na kuwafukuza Wafilisti kuvuka bonde na malango ya Ekroni. Na maiti za Wafilisti walilala katika njia iendayo Shaaraimu, na njia yote kuelekea Gathi na Ekroni.
\v 53 Watu wa Israeli wakarejea kutoka kuwafukuza Wafilisti, na wakateka nyara kambi yao.
\v 54 Daudi akachukua kichwa cha Mfilisti na kukipeleka Yerusalemu, lakini akaliweka vazi la vita katika hema lake.
\s5
\v 55 Sauli alipomuona Daudi akienda kukabiliana na yule Mfilisti, akamwambia Abneri, jemedari wa jeshi, "Abneri, kijana huyu ni mtoto wa nani? Abneri akasema, "Kama uishivyo, mfalme, mimi sijui."
\v 56 Naye mfalme akasema, "Waulize wanaoweza kufahamu, mvulana huyu ni kijana wa nani."
\s5
\v 57 Daudi aliporudi kutoka kumuua yule Mfilisti, Abneri alimchukuwa, na kumleta mbele ya Sauli akiwa na kichwa cha Mfilisti mkononi mwake.
\v 58 Sauli akamuuliza, "Kijana, wewe ni mtoto wa nani? Na Daudi akamjibu, "Mimi ni mtoto wa mtumishi wako Yese Mbethlehemu."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Daudi alipokuwa amemaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ilishikana na roho ya Daudi, na Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
\v 2 Sauli akamweka kazini Daudi siku hiyo, hakumwacha arudi nyumbani kwa baba yake.
\s5
\v 3 Kisha Yonathani na Daudi wakafanya makubaliano ya urafiki kwa sababu Yonathani alimenda kama roho yake mwenyewe.
\v 4 Yonathani akavua kanzu aliyokuwa amevaa na kumpa Daudi, akampa na vazi lake la kivita, pamoja na upanga, upinde, na mshipi.
\s5
\v 5 Daudi alikwenda popote ambapo Sauli alimtuma, naye alifanikiwa. Sauli akamteua Daudi awe mkuu wa wapiganaji. Jambo hili lilipendeza machoni pa watu na katika macho ya watumishi wa Sauli.
\s5
\v 6 Wakati wanarudi nyumbani kutoka kuwapiga Wafilisti, wanawake walitoka miji yote ya Israeli, wakiimba na kucheza, ili kukutana na mfalme Sauli, wakiwa na matowazi, wenye furaha, na wakiwa na ala za muziki.
\v 7 Hao wanawake waliimba kwa kupokezana huku wakicheza; Wakiimba: "Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi ameua makumi elfu yake."
\s5
\v 8 Sauli alikasirika sana, na wimbo huu haukumpendeza. Naye akasema, "Wamemsifia Daudi juu ya makumi elfu, lakini wamenisifia melfu tu mimi! Atapata kitu gani zaidi isipokuwa ufalme?
\v 9 Kuanzia siku hiyo na kuendelea, Sauli alimuangalia Daudi kwa mashaka.
\s5
\v 10 Kesho yake yule roho ya ubaya kutoka kwa Mungu ikamwingia Sauli kwa nguvu. Naye akawa anafanya kama mwendawazimu nyumbani mwake. Hivyo Daudi akapiga kifaa chake, kama alivyofanya kila siku. Sauli alikuwa na mkuki wake mkononi.
\v 11 Sauli akatupa mkuki wake, kwani alifikiri, "Nitampigilia ukutani." Lakini Daudi mara mbili aliepa uwepo wa Sauli.
\v 12 Sauli alimwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, lakini hakuwa na Sauli tena.
\s5
\v 13 Hivyo Sauli alimuondoa Daudi mbele yake na akamteua kuwa kamanda wa kikosi cha askari elfu moja. Kwa namna hii David alitoka na kuingia mbele ya watu.
\v 14 Daudi alikuwa akistawi kwa mambo yake yote, maana BWANA alikuwa pamoja naye.
\s5
\v 15 Sauli alipoona kwamba Daudi anastawi, alimwogopa.
\v 16 Lakini Israeli yote na Yuda walimpenda Daudi, maana alitoka na kuingia mbele yao.
\s5
\v 17 Kisha Sauli akamwambia Daudi, "Huyu hapa ni binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupatia awe mke wako. Ila tu uwe jasiri kwa ajili yangu na upigane vita vya BWANA." Maana Sauli alifikiri, "Usije mkono wangu ukawa juu yake, ila acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake."
\v 18 Daudi akamwambia Sauli, "Mimi ni nani, na maisha yangu yana nini, au hata maisha ya familia ya baba yangu katika Israeli, kiasi cha kuwa mkwe wa mfalme?"
\s5
\v 19 Lakini wakati ambao Merabu, binti Sauli, ilipasa kuwa ameolewa na Daudi, aliozwa kwa Adrieli Mmeholathi.
\s5
\v 20 Lakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi. Na watu walimwambia Sauli, na jambo hilo likampendeza.
\v 21 Ndipo Sauli akafikiri, "Nitampatia huyu awe mke wake, ili uwe mtego kwake, na hivyo mkono wa Wafilisti pengine uwe juu yake." Kwa hiyo Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, "Wewe utakuwa mkwe wangu."
\s5
\v 22 Sauli akawaamuru watumishi wake, "Ongeeni na Daudi kwa njia ya siri, na mseme, 'Tazama, mfalme anakufurahia, na watumishi wake wote wanakupenda. Sasa basi, uwe mkwe wa mfalme.'"
\s5
\v 23 Hivyo watumishi wa Sauli wakayasema maneno haya kwa Daudi. Na Daudi akasema, "Kwenu ninyi mnaona ni jambo dogo kuwa mkwe wa mfalme, mimi ni maskini, na heshima yangu ni ndogo."
\v 24 Watumishi wa Sauli wakarudisha kwake taarifa ya maneno ambayo Daudi aliyasema.
\s5
\v 25 Na Sauli akasema, "Hivi ndivyo mtakavyo mwambia Daudi, 'Mfalme haitaji mahari yoyote, isipokuwa govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi kwa adui wa mfalme."' Basi Sauli alifikiri atamwangusha Daudi kwa mkono wa Wafilisti.
\v 26 Watumishi wake walipomwambia maneno haya, yakamvutia Daudi awe mkwe wa mfalme.
\s5
\v 27 Kabla siku hizo hazijapita, Daudi aliondoka na watu wake na kuwaua Wafilisti mia mbili. Daudi akazileta govi zao, na kumkadhi mfalme kulingana na idadi yake, ili aweze kufanyika mkwe wa mfalme. Kwa hiyo Sauli akamwoza Mikali, binti yake, awe mkewe.
\v 28 Basi Sauli aliona na kufahamu kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi. Mikali, binti Sauli, akampenda Daudi.
\v 29 Sauli akazidi kumwogopa Daudi. Sauli akawa adui wa Daudi daima.
\s5
\v 30 Ndipo wakuu wa Wafilisti wakajitokeza kwa ajili ya vita, na mara zote walipojitokeza Daudi alifanikiwa zaidi kuliko watumishi wote wa Sauli, hivyo jina lake likapata heshima kubwa.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Sauli akamwambia Yonathani mwanawe na watumishi wake wote kwamba wanapaswa kumuua Daudi. Lakini Yonathani, mwana wa Sauli, alitamani sana akae na Daudi.
\v 2 Hivyo Yonathani akamwambia Daudi, "Baba yangu Sauli anatafuta kukuua. Kwa hiyo uwe macho wakati wa asubuhi na jifiche mahali pa siri.
\v 3 Nami nitatoka nje na kusimama kando ya baba yangu huko shambani uliko wewe, na nitazungumza na baba yangu kuhusu wewe. Kama nikijua jambo lolote nitakuambia."
\s5
\v 4 Yonathani alimsifia Daudi mbele ya Sauli baba yake akisema, "Mfalme asije akafanya dhambi dhidi ya mtumishi wake Daudi. Maana yeye hajakutenda dhambi, mambo aliyofanya yamekusaidia sana.
\v 5 Maana alijitoa maisha yake na kumuua yule Mfilisti, naye BWANA akawaletea Waisraeli wote wokovu mkuu. Tena uliuona na kufurahi. Kwa nini utende dhambi juu damu isiyo na hatia kwa kumuua Daudi bila sababu?"
\s5
\v 6 Sauli alimsikiliza Yonathani. Sauli akaapa, "Kama BWANA aishivyo, Yonathani hatauawa."
\v 7 Ndipo Yonathani akamwita Daudi na kumwambia mambo hayo yote. Na Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye Daudi akawa mbele zake kama zamani.
\s5
\v 8 Baadaye kukawa na vita tena. Daudi akatoka na kupigana na Wafilisti na kuwashinda kwa mauaji makubwa mno. Nao wakakimbia mbele yake.
\v 9 Yule roho wa ubaya kutoka kwa BWANA ikamjia Sauli alipokuwa ameketi nyumbani mwake na mkuki mkononi mwake, na Daudi akiwa anapiga chombo chake.
\s5
\v 10 Sauli alijaribu kumpigilia Daudi ukutani kwa mkuki wake, lakini akaponyoka kutoka machoni pake, na kwamba Sauli akashindilia mkuki ndani ya ukuta. Daudi alikimbia na kutoroka usiku huo.
\v 11 Bado Sauli aliwatuma wajumbe nyumbani kwa Daudi wamvizie kusudi aweze kumuua asubuhi. Mkewe Daudi, Mikali, akamwambia, "Usipoyaokoa maisha yako usiku huu, kesho utauwawa."
\s5
\v 12 Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupita dirishani. Naye akaenda, akakimbia na kutoroka.
\v 13 Mikali alichukua kinyago na kukilaza juu ya kitanda. Kisha akaweka mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na akakifunika na nguo.
\s5
\v 14 Sauli alipowatuma wajumbe kumchukua Daudi, mkewe akasema, " Daudi ni mgonjwa."
\v 15 Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumtazama; akisema, "Mleteni kwangu akiwa kitandani, ili nimuue."
\s5
\v 16 Wale wajumbe walipoingia ndani, tazama, kile kinyago kilikuwa kitandani pamoja na mto wa singa za mbuzi kichwani.
\v 17 Sauli akamuuliza Mikali, "Kwa nini umenidanganya na kumwachilia adui yangu aende, na tena ametoroka?" Mikali akamjibu Sauli, "Aliniambia, 'Acha niende. Kwa nini nikuuwe?"'
\s5
\v 18 Basi Daudi akakimbia na kutoroka, na akaenda kwa Samweli huko Rama na kumweleza yote ambayo Sauli amemtendea. Ndipo yeye na Samweli wakaenda na kukaa Nayothi.
\v 19 Naye Sauli akaambiwa kwamba, "Tazama, Daudi yuko huko Nayothi iliyoko Rama."
\v 20 Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumkamata Daudi. Nao walipowaona kundi la manabii wakitabiri, na Samweli akisimama kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akawaingia wale wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
\s5
\v 21 Sauli alipoambiwa hivyo, akawatuma wajumbe wengine, nao pia wakatabiri. Basi Sauli aliwatuma tena wajumbe kwa mara ya tatu, na hao pia wakatabiri.
\v 22 Kisha naye akaenda Rama na kufika katika kisima kirefu kilichoko huko Seku. Akauliza, "Samweli na Daudi wako wapi?" Mtu mmoja akasema, "Angalia, Wako Nayothi huko Rama."
\s5
\v 23 Hivyo Sauli akaenda Nayothi huko Rama. Ndipo Roho wa Mungu pia akaja juu yake, naye alipokuwa akienda alitabiri, hadi alipofika Nayothi huko Rama.
\v 24 Na yeye pia, alirarua mavazi yake, naye pia akatabiri mbele ya Samweli siku hiyo akilala uchi mchana kutwa na usiku kucha. Kwa sababu ya jambo hili, watu husema, "Je, Sauli pia ni miongoni mwa manabii?"
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akaenda na kumwambia Yonathani, "Nimefanya nini? Uovu wangu ni upi? Dhambi yangu ni ipi kwa baba yako, inayofanya atafute kuutoa uhai wangu."
\v 2 Yonathani akamwambia Daudi, "La hasha; hautakufa. Baba yangu hafanyi jambo kubwa wala dogo bila kunijulisha. Kwa nini inamlazimu baba yangu anifiche jambo hili? La, siyo hivyo?"
\s5
\v 3 Bado Daudi aliapa tena na akasema, "Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, 'Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.' Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti."
\s5
\v 4 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, "Lolote utakalosema, nitakufanyia."
\v 5 Daudi akamwambia Yonathani, "Kesho ni siku ya mwezi mpya, na inanibidi kukaa na kula pamoja na mfalme. Lakini acha niende, ili niweze kujificha katika shamba hadi siku ya tatu jioni.
\s5
\v 6 Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, 'Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.'
\v 7 Kama atasema kuwa ni vyema, 'basi mtumishi wako atakuwa na amani. Lakini kama atakasirika sana, ndipo utajua kwamba ameamua kunitendea uovu.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, umtendee wema mtumishi wako. Kwa maana umemweka mtumishi katika agano la BWANA pamoja na wewe. Lakini kama kuna dhambi ndani yangu, wewe mwenyewe uniuwe; maana kwa nini basi unipeleke kwa baba yako?"
\v 9 Yonathani akasema, "La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?"
\s5
\v 10 Ndipo Daudi akamwambia Yonathani, "Ni nani ataniambia ikiwa imetokea, baba yako akakujibu kwa ukali?"
\v 11 Yonathani akamwambia Daudi, "Njoo, hebu twende huko shambani." Ndipo wote wakaondoka kwenda shambani.
\s5
\v 12 Yonathani akamwambia Daudi, "Na BWANA, Mungu wa Israeli, awe shahidi. Kesho muda kama huu, nitakuwa nimemuuliza baba yangu, au siku ya tatu, tazama, ikiwa kutakuwa na jambo zuri upande wa Daudi; je, nisikutumie taarifa na kulidhihirisha kwako?
\v 13 Na kama ikimpendeza baba yangu akufanyie madhara, Basi BWANA ayafanye hayo kwa Yonathani na kuzidi ikiwa sitakujulisha jambo na kukupeleka mbali, ili kwamba uende kwa amani. Na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa na baba yangu.
\s5
\v 14 Kama bado nikiwa hai, hautanionesha uaminifu wa agano la BWANA, kwamba siwezi kufa?
\v 15 Na usivunje kabisa uaminifu wako wa agano kati yako na nyumba yangu, hata wakati BWANA atakapowaodoa kila mmoja wa adui za Daudi kutoka uso wa dunia."
\v 16 Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi na kusema, "Naye BWANA atawaondoa maadui wa Daudi." (KISWAHILI IDIOM? ==== ULB ENGLISH IDIOM)
\s5
\v 17 Yonathani akamtaka Daudi aape tena kwa sababu ya upendo aliokuwa nao juu yake, kwa sababu alimpenda kama alivyopenda roho yake mwenyewe.
\v 18 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, "Kesho ni siku ya mwezi mpya. Hautakuwapo, kwa sababu kiti chako kitakuwa wazi.
\v 19 Utakapokuwa umekaa huko siku tatu, uende upesi hadi mahala ulipojificha mara ya kwanza, wakati shughuli ikifanyika, na ukaye karibu jiwe Ezeli.
\s5
\v 20 Nitatupa mishale mitatu pembeni mwa jiwe, kama vile ninalenga kitu fulani.
\v 21 Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, 'Nenda utafute hiyo mishale.' Kama nitamwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue," ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo.
\s5
\v 22 "Lakini kama nikimwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko mbele yako,' ndipo utakapokwenda zako, maana BWANA ametaka uende zako.
\v 23 Kulingana na makubaliano ambayo mimi na wewe tumeongea, angalia, BWANA yupo kati yangu na wewe milele.'"
\s5
\v 24 Kwa hiyo Daudi akajificha mle shambani. Pindi mwezi ulipoandama, mfalme aliketi chini ale chakula.
\v 25 Mfalme alikaa juu ya kiti chake, kama kawaida kwenye kiti karibu na ukuta. Yonathani alisimama wima, na Abneri alikaa ubavuni mwa Sauli. Lakini nafasi ya Daudi ilikuwa wazi.
\s5
\v 26 Hata hivyo Sauli hakusema kitu siku hiyo, kwa sababu alifikiri, "Kuna jambo limempata Daudi. Hayuko safi; hakika hayuko safi."
\v 27 Lakini siku ya pili, siku moja baada ya mwandamo wa mwezi, bado nafasi ya Daudi ilikuwa tupu. Ndipo Sauli akamuuliza Yonathani mwanaye, "Kwa nini mwana wa Yese hakuja kwenye chakula, jana na hata leo?"
\s5
\v 28 Yonathani akamjibu Sauli, "Daudi aliomba kwangu ruhusa kwa dhati ili aende Bethlehemu.
\v 29 Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii."
\s5
\v 30 Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, "Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako?
\v 31 Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa."
\s5
\v 32 Yonathani akamjibu Sauli baba yake, "Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?"
\v 33 Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi.
\v 34 Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
\s5
\v 35 Ikawa asubuhi, Yonathani akaenda huko shambani kama walivyoahidiana na Daudi, akiwa pamoja na kijana wake.
\v 36 Akamwambia yule kijana wake, "Kimbia utafute ile mishale niliyoitupa." Na kijana alikimbia, akatupa mshale mwingine mbele yake.
\v 37 Kijana alipofika katika eneo ambapo mshale ulitua, ule alioutuma Yonathani, akamwita tena kijana, na kusema, "Huo mshale hauko mbele yako?"
\s5
\v 38 Kisha Yonathani akamwita yule kijana, "Upesi, harakisha, usikawie!" Hivyo kijana wa Yonathani akaikusanya mishale na kurudi kwa bwana wake.
\v 39 Lakini huyo kijana hakujua lolote. Ni Yonathani na Daudi tu ndio walijua habari yenyewe.
\v 40 Yonathani akampa kijana wake silaha na kumwambia, "Nenda, uzipeleke mjini."
\s5
\v 41 Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.
\v 42 Yonathani akamwambia Daudi, "Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, 'BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.'" Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha Daudi akafika Nobu kumuona Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akaja akutane na Daudi huku akitetemeka na kumwambia, "Kwa nini uko peke yako huna mtu wa kuambatana na wewe?"
\v 2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, "Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, 'Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.' Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani.
\s5
\v 3 Sasa basi chakula gani kinapatikana hapa? Nipatie mikate mitano, au chochote kilichopo hapa."
\v 4 Huyo Kuhani alimjibu Daudi na kusema, "Hakuna mkate wa kawaida mkononi, lakini ipo mikate takatifu- kama vijana hawajatembea na wanawake."
\s5
\v 5 Daudi akamjibu kuhani, "Hakika hatujatembea na wanawake kwa siku hizi tatu. Nilipoanza safari, miili ya vijana iliwekwa wakfu kwa BWANA, ingawa ilikuwa safari ya kawaida. Je, si zaidi sana leo miili yao ikawekwa wakfu kwa BWANA."
\v 6 Hivyo kuhani akampa mikate iliyokuwa imewekwa wakfu kwa BWANA. Maana haikuwepo mikate mingine hapo, isipokuwa tu ile ya wonyesho, ambayo iliondolewa kutoka kwa BWANA, ili sehemu yake iwekwe mikate ya moto, inapokuwa imeondolewa.
\s5
\v 7 Basi siku hiyo mmoja wa watumishi wa Sauli alikuwapo mahali hapo, ameshilkiliwa mbele za BWANA. Jina la mtu huyo aliitwa Doegi Mwedomu, mkuu wa wachungaji wa Sauli.
\s5
\v 8 Daudi akamwambia Ahimeleki, "Je, hakuna hata mkuki wowote au upanga? Maana mimi sikubeba upanga wangu wala silaha zangu, maana ile shughuli ya mfalme ilikuwa ya muhimu."
\v 9 Kuhani akasema, "Ule upanga wa Mfilisti Goliathi, uliyemuua katika bonde la Ela, uko hapa umefunikwa katika nguo nyuma ya naivera. kama unataka kuuchukua huo, uchukue, maana hakuna silaha nyingine hapa." Daudi akasema, "Hakuna silaha nyingine kama hiyo, nipatie hiyo."
\s5
\v 10 Daudi aliamka na kukimbia mbali na Sauli na akaenda kwa Akishi, mfalme wa Gathi.
\v 11 Mtumishi wa Akishi akamwambia, "huyu siye Daudi mfalme wa nchi hii? Je, wanawake hawakupokezana wakiimba na kucheza, 'Sauli ameua maelfu yake, na Daudi makumi elfu yake?"'
\s5
\v 12 Daudi akayaweka maneno hayo moyoni mwake na akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.
\v 13 Daudi akabadili mwenendo wake mbele yao na akajifanya kuwa mwendawazimu machoni pao; akachora-chora alama kwenye vizingiti vya milango huku akitiririsha mate yake chini ya ndevu zake.
\s5
\v 14 Ndipo Akishi akawaambia watumishi wake, "Tazameni, mnaona mtu huyu ni mwehu.
\v 15 Kwa nini mmemleta kwangu? Je, mimi nina haja na wehu, kumbe mmemleta mtu huyu ili anifanyie hayo mbele yangu? Hivi kweli huyu ataingia nyumbani mwangu?
\s5
\c 22
\p
\v 1 Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko.
\v 2 Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye.
\s5
\v 3 Kisha Daudi alitoka huko akaenda Mispa huko Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, "Tafadhali waruhusu baba na mama yangu wakae kwako hadi hapo nitakapojua kitu gani ambacho Mungu atafanya kwa ajili yangu."
\v 4 Basi akawaacha kwa Mfalme wa Moabu. Baba na mama yake wakakaa na mfalme kwa muda wote ambao Daudi alikuwa kwenye ngome yake.
\v 5 Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, "Usikae tena katika ngome yako. Ondoka na uende katika nchi ya Yuda." Kwa hiyo Daudi akatoka hapo na akaenda katika msitu wa Harethi.
\s5
\v 6 Sauli akasikia kwamba Daudi amepatikana, akiwa pamoja na watu aliokuwa nao. Wakati huo Sauli alikuwa akikaa Gibea chini ya mti wa mkwaju huko Rama, akiwa na mkuki wake mkononi mwake, na watumishi wake wote walikuwa wamesimama wamemzunguka.
\s5
\v 7 Sauli akawaambia watumishi wake, Sasa sikilizeni, watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya nyote kuwa majemedari wa maelfu na majemedari wa mamia,
\v 8 hata ninyi nyote mnapanga njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anafanya agano na mwana wa Yese. Hakuna hata mmoja wenu anayenionea huruma. Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anamchochea mtumishi wangu Daudi awe kinyume changu. Leo mejificha na ananisubiri ili anishambulie."
\s5
\v 9 Kisha Doegi Mwedomu, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akajibu, Nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu.
\v 10 Alimwomba BWANA ili apate kumsaidia, na alimpatia mahitaji na upanga wa Goliathi, Mfilisti"
\s5
\v 11 Kisha Mfalme akamtuma mtu amwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu na watu wote wa nyumba ya baba yake, makuhani waliokuwa huko Nobu. Wote walifika mbele ya mfalme.
\v 12 Sauli akasema, "Sasa sikiliza, mwana wa Ahitubu," Naye akajibu, "Niko hapa, bwana wangu."
\v 13 Sauli akamwambia, "Kwa nini unapanga njama dhidi yangu, wewe pamoja na mwana wa Yese, kwa kumpatia mikate, na upanga, na umemwomba Mungu kusudi amsaidie Daudi, kusudi aniasi mimi, na kujificha sehemu ya siri, kama alivyofanya leo?"
\s5
\v 14 Ndipo Ahimeleki akamjibu mfalme na kusema, "Je, ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliyemwaminifu kama Daudi, ni nani mkwe wa mfalme na yuko juu ya walinzi wako, na mwenye heshima nyumbani mwako?
\v 15 Je, leo ni mara ya kwanza kwangu kumuomba Mungu apate kumsaidia? Hapana! Mfalme usinilaumu mimi mtumishi wako kwa jambo lolote wala jamaa zangu wote. Maana mimi mtumishi wako sijui lolote kuhusu kadhia hii."
\s5
\v 16 Mfalme akamjibu, "Hakika utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya nyumba ya baba yako."
\v 17 Mfalme akamwambia mlinzi aliyesimama karibu naye, "Geuka na uwauwe makuhani wa BWANA. Kwa sababu wanamuunga mkono Daudi, na sababu walijua kwamba alikimbia, lakini hawakunijulisha." Lakini watumishi wa mfalme hawakunyoosha mkono wao kuwaua makuhani wa BWANA.
\s5
\v 18 Ndipo mfalme akamwambia Doegi, "Geuka na uwauwe makuhani." Hivyo Doegi Mwedomu akageuka na kuwapiga makuhani; akawaua watu themanini na watano waliovaa naivera ya kitani siku hiyo.
\v 19 Kwa ncha ya upanga, aliupiga Nobu, mji wa makuhani, akiwaua wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na punda na kondoo. Wote aliwaua kwa ncha ya upanga.
\s5
\v 20 Lakini mmoja wa wana wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari, aliponyoka na kukimbilia kwa Daudi.
\v 21 Abiathari akamwambia Daudi kwamba Sauli amewaua manabii wa BWANA.
\s5
\v 22 Daudi akamwambia Abiathari, "Nilifahamu kuwa siku hiyo, Doegi Mwedomu alikuwa mahali pale, kwamba hakika angemwambia Sauli. Nina wajibika kwa kifo cha kila mtu katika familia ya baba yako!
\v 23 Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Wakamwambia Daudi, "Tazama, Wafilisti wanaupiga Keila na wanapora nafaka inayopurwa."
\v 2 Hivyo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, na akamuuliza," Je, niondoke niwapige hawa Wafilisti? BWANA akamwambia Daudi, "Nenda ukawapige Wafilisti na kuokoa Keila."
\s5
\v 3 Daudi akaambiwa na watu wake, "Angalia, hapa Yuda tunaogopa. Je, si zaidi sana kama tutaenda Keila kupambana na majeshi ya Wafilisti?"
\v 4 Ndipo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, bado tena, BWANA akamjibu, "Amka, uteremke hadi Keila. Maana nitakupatia ushindi dhidi ya Wafilisti."
\s5
\v 5 Daudi na watu wake wakaenda Keila na kupigana na Wafilisti. Wakahamisha ng'ombe wao na kuwapiga kwa mauaji makubwa mno. Hivyo Daudi akawaokoa wenyeji wa Keila.
\v 6 Abiathari mwana wa Ahimeleki alipokuwa amekimbilia kwa Daudi huko Keila, alibeba naivera mkononi mwake.
\s5
\v 7 Sauli aliambiwa kwamba Daudi amekwenda Keila. Sauli akasema, "Mungu amemweka mkononi mwangu. Bila shaka amefungiwa ndani kwa sababu ameingia katika mji ulio na malango na makomeo."
\v 8 Sauli akayaita majeshi yake yote kwa ajili ya vita, waende hadi Keila, wamteke Daudi na watu wake.
\v 9 Daudi alijua kwamba Sauli alikuwa anapanga njama za kumdhuru yeye. Ndipo akamwambia kuhani Abiathari kuhani, "Ulete hapa naivera."
\s5
\v 10 Kisha Daudi akasema, "BWANA, Mungu wa Israeli, mtumishi wako hakika amesikia kwamba Sauli anatafuta namna ya kuja Keila, ili auteketeze mji kwa ajili yangu.
\v 11 Je, watu wa Keila watanisalimisha mkononi mwake? Je, Sauli atashuka hadi huko, kama mtumishi wako alivyosikia? BWANA, Mungu wa Israeli, nakusihi, tafadhali mwambie mtumishi wako. "BWANA akasema, "Atakuja huko."
\s5
\v 12 Kisha Daudi akauliza, "Je, watu wa Keila watanisalimisha mimi na watu wangu katika mkono wa Sauli?" BWANA akasema, "Watu hao watawasalimisha kwao."
\s5
\v 13 Kisha Daudi na watu wake, waliokuwa kama mia sita, walitoka na kwenda mbali na Keila, na wakazunguka kila sehemu. Kisha Sauli akaambiwa kwamba Daudi ametoroka kutoka Keila, hivyo akasitisha kumfuatia.
\v 14 Daudi alikaa ngomeni katika jangwa, kwenye nchi ya milima katika jangwa la Zifu. Kila siku Sauli alimtafuta, lakini Mungu hakumweka mkononi mwake.
\s5
\v 15 Daudi aliona kwamba Sauli amejitokeza kuangamiza maisha yake; basi Daudi alikuwa katika jjangwa la Zifu huko Horeshi.
\v 16 Kisha Yonathani, mwana wa Sauli, akaamuka akaenda kwa Daudi huko Horshi, naye akamtia moyo amtumainie Mungu.
\s5
\v 17 Akamwambia, "Usiogope. Kwa maana mkono wa baba yangu Sauli hautakupata. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa msaidizi wako. Baba yangu Sauli pia anajua hivyo."
\v 18 Basi wote wawili wakafanya agano mbele za BWANA. Kisha Daudi alibaki Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani.
\s5
\v 19 Nndipo Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea wakisema, "Je, Daudi hakujificha kati yetu kwenye ngome huko Horeshi, juu ya mlima wa Hakila, ulioko kusini mwa Yeshimoni?
\v 20 Basi uje, mfalme! Kulingana na matakwa yako, uje! Kazi yetu itakuwa kumtia katika mkono wa mfalme."
\s5
\v 21 Sauli akasema, "Mbarikiwe na BWANA. Kwa sababu mmenihurumia.
\v 22 Nendeni, mhakikishe sawasawa. Tafuteni na kujua maficho yake yako wapi na ni nani amemwona huko. Nimeambiwa kwamba yeye ni mjanja sana.
\v 23 Kwa hiyo chunguzeni, mjue sehemu zote anakojificha. Baadaye rudini kwangu mkiwa na taarifa kamili, na kisha nitaongozana nanyi. Ikiwa yupo katika nchi, nitamtafuta kutoka miongoni mwa elfu zote za Yuda."
\s5
\v 24 Ndipo wakaamka na kwenda hadi Zifu mbele ya Sauli. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa katika jangwa la Maoni, huko Araba upande wa kusini mwa Yeshimoni.
\v 25 Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta Daudi. Na Daudi akaambiwa habari hiyo, hivyo akateremka hadi kwenye mlima wa miamba na akakaa katika jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hivyo, akamfukuza Daudi katika Jangwa la Maoni.
\s5
\v 26 Sauli akaenda akawa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa wakienda upande mwingine wa mlima. Daudi kwa haraka akatoweka akae mbali na Sauli. Kwa sababu Sauli na watu wake walikuwa wakimzunguka Daudi na watu wake wawakamate,
\v 27 mjumbe mmoja akaja kwa Sauli na kusema, "Njoo, harakisha maana Wafilisti wamepanga uvamizi juu ya nchi."
\s5
\v 28 Kwa hiyo Sauli akarudi asimfuatie Daudi na akaenda kupambana na Wafilisti. Kwa hiyo sehemu ile iliitwa Mwamba wa Maficho.
\v 29 Daudi akapanda kutoka huko na kukaa katika ngome ya Engedi.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Sauli aliporudi kuwafukuza Wafilisti, akaambiwa kwamba, "Daudi yuko katika jangwa la Engedi."
\v 2 Ndipo Sauli akachukua watu elfu tatu waliochaguliwa kutoka Iraeli yote, wakaenda kumtafuta Daudi na watu wake katika miamba ya Mbuzi Mwitu.
\s5
\v 3 Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, mahali palipokuwa na pango. Sauli akaingia ndani yake kujisaidia. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa wamekaa mbali zaidi ndani ya pango lilelile.
\v 4 Watu wake Daudi wakamwambia, "Hii ndiyo siku ambayo BWANA aliisema akikuambia, 'Nitamweka adui wako mkononi mwako, ili umtendee kama unavyotaka."' Kisha Daudi akainuka na kumnyemelea kwa mbele kimya kimya na kulikata pindo la kanzu ya Sauli.
\s5
\v 5 Baadaye moyo wa Daudi ukamchoma kwa sababu alilikata pindo la kanzu ya Sauli.
\v 6 Akawaambia watu wake, "BWANA anisamehe, sikupaswa kumtendea jambo hili bwana wangu, Mtiwa mafuta wa BWANA, kwa kunyoosha mkono wangu juu yake, maana yeye ni masihi wa BWANA."
\v 7 Hivyo Daudi akawakemea watu wake kwa maneno haya, na kuwazuia wasimpige Sauli. Sauli akasimama, akatoka pangoni, na kwenda zake.
\s5
\v 8 Baadaye tena, Daudi akasimama juu, akatoka pangoni, na kumwita Sauli: "Bwana wangu mfalme." Sauli alipotazama nyuma, Daudi akasujudu hadi chini na kuonyesha heshima.
\v 9 Daudi akamwambia Sauli, "Kwa nini unawasikiliza watu ambao wanasema, "Angalia, Daudi anatafuta kukudhuru?'
\s5
\v 10 Leo macho yako yameona jinsi BWANA alivyokuweka mkononi mwangu tulipokuwa ndani ya pango. Wengine waliniambia nikuuwe, lakini nilikuacha hai. Nikasema, 'Sitanyoosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa kuwa ni masihi wa BWANA.'
\v 11 Tazama, baba yangu, angalia pindo la kanzu yako mkononi mwangu. Kwa maana kama nilikata pindo la kanzu yako na sikukuua, basi ujuwe na uone kwamba sina uovu au kosa katika mkono wangu, na sijafanya dhambi juu yako, ingawa unawinda kuutoa uhai wangu.
\s5
\v 12 BWANA aamue kati yangu na wewe, na BWANA anilipizie kisasi juu yako, lakini mkono wangu kamwe hautakuwa juu yako.
\v 13 Kama mithali ya wazee isemavyo, 'Katika waovu hutoka uovu.' Lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.
\s5
\v 14 Mfalme wa Israeli ametoka kumuandama nani? Unamsaka nani? Unasaka mzoga wa mbwa! Unasaka kiroboto!
\v 15 BWANA na awe mwamuzi na atoe hukumu kati yangu na wewe, na akaione, na akatetee sababu yangu na aniruhusu kuepuka mkono wako."
\s5
\v 16 Daudi alipomaliza kuongea maneno haya kwa Sauli, Sauli akasema, "Hii ni sauti yako, mwanangu Daudi?" Sauli alinyanyua sauti yake akalia.
\s5
\v 17 Akamwambia Daudi, "Wewe ni mwenye haki kuliko mimi. Kwa sababu umenilipa mazuri, wakati mimi nimekulipa maovu.
\v 18 Leo umetangaza jinsi ulivyonitendea mazuri, kwa sababu hukuniua wakati BWANA aliponiweka katika rehema yako.
\s5
\v 19 Kwa kuwa mtu akimpata adui yake, atamwacha aende zake salama? Na BWANA akuzawadie mema kwa kile ulichonifanyia leo.
\v 20 Basi, najua kwa hakika kwamba utakuwa mfalme na kwamba ufalme wa Israeli utaimarika katika mkono wako.
\s5
\v 21 Niapie kwa BWANA kwamba baada yangu hautawakatilia mbali uzao wangu, na kwamba hautaliharibu jina langu katika nyumba ya baba yangu."
\v 22 Hivyo Daudi akamwapia Sauli kiapo. Kisha Sauli akaenda nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Basi Samweli akafariki. Waisraeli wote wakakusanyika pamoja na kumwomboleza, na wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akainuka na akashuka hadi jangwa la Parani.
\s5
\v 2 Kulikuwa na mtu mmoja huko Maoni, na mali zake zilikuwa huko Karmali. Mtu huyo alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja. Naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.
\v 3 Na mtu huyo aliitwa Nabali, na jina la mke wake aliitwa Abigaili. Mwanamke huyo alikuwa mwenye busara na mzuri kwa sura. Lakini mwanaume alikwa mkaidi na mwovu katika mambo yake. Alikuwa wa uzao wa nyumba ya Kalebu.
\s5
\v 4 Daudi akasikia akiwa jangwani kwamba Nabali alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake.
\v 5 Hivyo Daudi aliwatuma kwake vijana kumi. Akawaambia wale vijana, "Pandeni kwanda Karmeli, mwendeeni Nabali, na mkamsalimie kwa jina langu.
\v 6 Mtamwambia, 'Uishi katika baraka, Uwe na amani na nyumba yako iwe na amani, na wote ulionao wawe na amani.
\s5
\v 7 Nasikia kwamba unao wakata manyoya. Wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, na hatukuwafanyia ubaya, na muda wote wakiwa Karmeli hawakupotelewa kitu chochote.
\v 8 Waulize vijana wako, nao watakuambia. Basi vijana wangu wapate kibali machoni pako, maana tumefika siku ya sherehe. Tafadhali utoe cho chote ulicho nacho mkononi kwa watumishi wako na kwa Daudi mwanao.'"
\s5
\v 9 Vijana wa Daudi walipofika, walimwambia Nabali yote haya kwa niaba ya Daudi na kisha wakasubiri.
\v 10 Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, "Daudi ni nani? Na ni nani mwana wa Yese? Siku hizi wapo watumishi wengi wanaotoroka bwana zao.
\v 11 Je, nichukue mkate wangu na maji yangu na nyama yangu ambayo nimewachinjia wakata manyoya wangu, na niwape watu wanaotoka nisikokujua?"
\s5
\v 12 Hivyo vijana wa Daudi waligeuka na kurudi, nakumwambia kila kitu kilichosemwa.
\v 13 Daudi akawaambia watu wake, "Kila mtu ajifunge upanga wake." Kila mtu akajifunga upanga wake. Daudi naye pia akajifunga upanga wake. Yapata kama watu mia nne wakafuatana na Daudi, na wengine mia mbili walibaki kulinda mizigo yao.
\s5
\v 14 Lakini kijana mmojawapo alimwambia Abigaili, mke wa Nabali akasema, "Daudi aliwatuma wajumbe kutoka jangwani waje wamsalimu bwana wetu, na yeye akawatukana.
\v 15 Bado watu hawa walitutendea mema. Hatukudhurika na hatukupoteza chochote wakati wote tulipotembea nao tulipokuwa mbugani.
\s5
\v 16 Walikuwa ukuta wetu usiku na mchana, wakati wote tulikuwa pamoja nao tukichunga kondoo.
\v 17 Kwa hiyo tambua hili na zingatia utafanya nini, maana ubaya unamvizia bwana wetu, na utakuwa juu ya nyumba yake yote. Yeye ni mtu asiyefaa na hakuna awezaye kushauriana naye."
\s5
\v 18 Ndipo Abigaili akaharakisha na akachukuwa mikate mia mbili, chupa mbili za divai, kondoo watano waliokwisha andaliwa, vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu, na mikate mia mbili ya tini na akavipakia juu ya punda.
\v 19 Akamwambia kijana wake, "Tangulia mbele yangu, nami nitakuja nyuma yako." Lakini hakumwambia mmewe Nabali.
\s5
\v 20 Alipokuwa akienda juu ya punda wake na kutelemka penye kificho cha mlima, Daudi na watu wake walishuka chini wakimwelekea Abigaili, naye akakutana nao.
\s5
\v 21 Basi Daudi alikuwa amesema, "Hakika nimelinda bure vyote alivyonavyo mtu huyu huko nyikani, na vyote alivyonavyo hakuna kilichopotea, pamoja na hayo amenilipa mabaya badala ya mema.
\v 22 Mungu na anitendee hivyo mimi, Daudi, pia iwe zaidi, iwapo nitamwacha hata mtu mmoja wa kwake akiwa hai ifikapo kesho asubuhi.
\s5
\v 23 Abigaili alipomwona Daudi, aliharakisha na kushuka chini ya punda wake, akalala kifudifudi na kujiinamisha hadi chini.
\v 24 Akamwangukia miguuni pake na kusema, "Juu yangu tu, bwana wangu, na uwe uovu. Tafadhali acha mjakazi wako aseme nawe, tena uyasikilize maneno ya mjakazi wako.
\s5
\v 25 Nakusihi bwana wangu usimjali mtu huyu asiyefaa, Nabali, kwa maana kama jina lake lilivyo, ndivyo alivyo. Jina lake ni Nabali, na upumbavu uko pamoja naye. Lakini mimi mjakazi wako sikuwaona vijana wa bwana wangu, uliowatuma.
\v 26 Sasa basi, bwana wangu, kama BWANA aishivyo, na kama unavyoishi, kwa kuwa BWANA amekuondoa kutoka kumwaga damu, na kuacha kulipiza kisasi kwa mkono mwenyewe, basi adui zako, na wale ambao wanatafuta kumfanyia uovu bwana wangu, wawe kama Nabali
\s5
\v 27 Na sasa zawadi hii ambayo mjakazi wako ameileta kwa bwana wangu, na wapewe vijana ambao wanamfuata bwana wangu.
\v 28 Tafadhali ulisamehe kosa la mjakazi wako, maana BWANA hakika atamfanyia bwana wangu nyumba imara, kwa sababu bwana wangu anapigana vita vya BWANA; na uovu hautaonekana ndani yako maadamu unaishi.
\s5
\v 29 Na ingawa watu wangeinuka na kukuandama ili wakuue, bado uhai wa bwana wangu utafungwa katika furushi la walio hai na BWANA Mungu wako; na atayatupa maisha ya adui zako mbali, kama vile kutoka katika mfuko wa kombeo.
\s5
\v 30 Na itakuwa, BWANA atakapokuwa amemtimizia bwana wangu mambo yote mazuri ambayo amekuahidi, na alivyokufanya kiongozi juu ya Israeli,
\v 31 jambo hili halitakuwa huzuni kwako, wala chukizo moyoni kwa bwana wangu, kwa sababu hukumwaga damu bila sababu, na hujajilipizia kisasi. Na BWANA akikuletea mafanikio, umkumbuke mjakazi wako."
\s5
\v 32 Ndipo Daudi akamwambia Abigaili, "BWANA, Mungu wa Israeli, abarikiwe, aliyekutuma uonane na mimi leo.
\v 33 Na hekima yako ibarikiwe, nawe umebarikiwa, kwa sababu leo umenizuia nisiwe na hatia ya kumwaga damu, na kutojilipizia kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.
\s5
\v 34 Kwa kweli, kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisikuumize, kama usinge harakisha kuja ukutane nami, kwa hakika kesho asubuhi asinge salia hata mtoto mmoja wa kiume kwa Nabali."
\v 35 Kwa hiyo Daudi akavipokea kutoka mkononi mwake vile alivyokuwa amemletea; akamwambia, "Nenda kwa amani hadi nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako na nimekubali."
\s5
\v 36 Abigaili akarudi kwa Nabali; tazama, alikuwa akifanya sherehe katika mji wake, kama sherehe ya mfalme; na moyo wa Nabali ulifurahi ndani yake, kwa sababu alikwa amelewa sana. Kwa hiyo hakumwambia chochote kabisa hadi kulipopambazuka
\s5
\v 37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, basi mkewe akamwambia mambo hayo; moyo wake ukafa ndani yake, na akawa kama jiwe.
\v 38 Ikawa baada ya siku kumi BWANA alimpiga Nabali naye akafa.
\s5
\v 39 Naye Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, "BWANA abarikiwe, aliyenichukulia hatua ya shutuma yangu kutoka mkono wa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asifanye maovu. Na amemrudishia Nabali tendo la uovu juu ya kichwa chake mwenyewe." Ndipo Daudi akawatuma watu wakaongee na Abigaili, ili amchukue awe mke wake.
\v 40 Watumishi wake Daudi walipofika kwa Abigaili huko Karmeli, wakaongea naye na kusema, "Daudi ametutuma kwako tukuchukue hadi kwake uwe mke wake."
\s5
\v 41 Abigaili aliinuka, akainamisha uso chini, na akasema, "Tazama, mjakazi wako ni mtumwa aoshaye miguu ya watumishi wa bwana wangu."
\v 42 Akaharakisha na kuamka, akapanda punda akiwa na vijakazi wake watano waliofuatana naye; akawafuata wajumbe wa Daudi, na akawa mke wake.
\s5
\v 43 Daudi pia alimchukua Ahinoamu wa Yezreeli akamwoa; wote wawili wakawa wake zake.
\v 44 Wakati huo Sauli alikuwa amempa Palti, mwana wa Laishi mtu wa Galimu, Mikali, binti yake, aliyekuwa mke wa Daudi.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, "Je, Daudi akujificha katika vilima vya Hakila, ambavyo viko mbele ya jangwa?"
\v 2 Kisha Sauli akaamka na kwenda chini ya jangwa la Zifu, akiwa na watu elfu tatu waliochaguliwa katika Israeli, wamtafute Daudi katika jangwa la Zifu.
\s5
\v 3 Sauli akaweka kambi kwenye kilima cha Hakila, kilicho mbele ya jangwa, kando ya barabara. Lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, na akaona kwamba Sauli alikuwa anamfuatia huko jangwani.
\v 4 Hivyo Daudi akawatuma wapelelezi na akafahamu kwamba hakika Sauli alikuwa amekuja.
\s5
\v 5 Daudi akaamka na kwenda hadi mahali ambapo Sauli alipiga kambi; akaona mahali alipolala Sauli, na Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi lake; Sauli alilala katikati ya kambi, na watu walipiga kambi kumzunguka, na wote wamesinzia.
\s5
\v 6 Ndipo Daudi akamwambia Ahimeleki Mhiti, na Abishai mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, "Ni nani atakwenda nami kambini kwa Sauli? Abishai akasema, "Mimi nitashuka pamoja nawe."
\v 7 Hivyo Daudi na Abishai wakaliendea jeshi usiku. Na Sauli alikuwapo akisinzia ndani ya kambi, mkuki wake umechomekwa chini pembeni mwa kichwa chake. Abneri na Askari wake wamelala kwa kumzunguka.
\v 8 Kisha Abishai akamwambia Daudi, "Leo Mungu amemweka adui yako mkononi mwako. Basi tafadhali acha nimchome mkuki nimtoboe hadi chini kwa pigo moja. Sitampiga mara mbili."
\s5
\v 9 Daudi akamwambia Abishai, "Usimwangamize; kwa maana nani awezaye kunyoosha mkono wake dhidi ya mtiwa mafuta wa BWANA na asiwe na hatia?"
\v 10 Daudi akasema, "Kama BWANA aishivyo, BWANA atamuua, au siku ya kufa kwake itakuja, au atakwenda katika vita na ataangamia.
\s5
\v 11 BWANA apishe mbali nisinyooshe mkono wangu dhidi ya mtiwa mafuta wake; lakini sasa, nakusihi chukua mkuki uliokichwani pake na jagi la maji, tuondoke."
\v 12 Hivyo Daudi akachukua mkuki na jagi la maji kutoka kichwani pa Daudi, wakatoweka. Hakuna mtu aliyewaona au kufahamu habari hii, wala hakuna aliyetoka usingizini, maana wote walisinzia, kwa sababu usingizi mzito kutoka kwa BWANA uliwaangukia.
\s5
\v 13 Kisha Daudi akaenda upande mwingine na akasimama juu ya mlima mbali sana; ukiwepo umbali mkubwa katikati yao.
\v 14 Daudi akawapigia kelele watu hao na Abneri mwana Neri; akisema, "Hujibu neno, Abneri?" Ndipo Abneri akajibu na kusema, "Wewe ni nani unayempigia mfalme kelele?"
\s5
\v 15 Daudi akamwambia Abneri, "Wewe siye mtu jasiri? Ni nani yuko kama wewe katika Israeli? Kwa nini basi hukukaa macho kumlinda bwana wako mfalme? Kwa maana mtu fulani aliingia kumuua mfalme, bwana wako.
\v 16 Jambo hili ulilolifanya siyo zuri. Kama BWANA aishivyo, unapaswa kufa kwa sababu hukumlinda bwana wako, mtiwa mafuta wa BWANA. Na sasa tazama ulipo mkuki wa mfalme, na jagi la maji lililokuwa kichwani pake."
\s5
\v 17 Sauli aliitambua sauti ya Daudi akasema, "Hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?" Daudi akasema, "Ni sauti yangu, mfalme, bwana wangu."
\v 18 Daudi akasema, "Kwa nini bwana wangu anamwandama mtumishi wake? Nimefanya nini? Mkononi mwangu kuna uovu gani?
\s5
\v 19 Kwa hiyo sasa, nakusihi, bwana wangu mfalme asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama ni BWANA ndiye amekuchochea dhidi yangu, na aikubali sadaka; lakini kama ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA, maana leo wamenifukuza, nisishikamane na urithi wa BWANA; wameniambia, 'Nenda ukaabudu miungu mingine.'
\v 20 Kwa hiyo, sasa, usiiachilie damu yangu ianguke ardhini mbali na uwepo wa BWANA; kwa kuwa mfalme wa Israeli ametoka nje kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware milimani."
\s5
\v 21 Kisha Sauli akasema, "Nimefanya dhambi. Rudi, Mwanangu, Daudi; maana sitakudhuru tena, kwa sababu leo maisha yangu yalikuwa yenye thamani machoni pako. Tazama, nimetenda upumbavu na nimekosa sana."
\s5
\v 22 Daudi akajibu na akasema, "Tazama, mkuki wako uko hapa, mfalme! Mruhusu kijana mmojawapo aje auchukue na aulete kwako.
\v 23 Na BWANA amlipe kila mtu kwa ajili ya uadilifu wake na kwa uaminifu wake; kwa sababu leo BWANA alikuweka mkononi mwangu, lakini nisinge mpiga mtiwa mafuta wake.
\s5
\v 24 Na tazama, kama maisha yako leo yalivyokuwa ya thamani machoni pangu, vivyo hivyo maisha yangu yathaminiwe sana machoni pa BWANA, na aweze kuniokoa katika shida zote."
\v 25 Ndipo Sauli akamwambia Daudi, "Na ubarikiwe, mwanangu Daudi, ili uweze kutenda mambo makuu, na hakika uweze kufanikiwa." Ndipo Daudi akaenda zake, na Sauli akarudi kwake.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Daudi alisema moyoni mwake, "Basi, siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jambo zuri kwangu kuliko kutoroka hadi nchi ya Wafilisti; Sauli atakata tamaa asinitafute tena ndani ya mipaka yote ya Israeli; kwa njia hii nitaponyoka kutoka mkono wake."
\s5
\v 2 Daudi akaondoka na kuvuka, akiwa pamoja na watu mia sita hadi kwa Akishi mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.
\v 3 Daudi akaishi na Akishi huko Gathi pamoja na watu wake, na kila mtu na familia yake, na Daudi akiwa na wake zake wawili, Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili Mkarmeli aliyekuwa mke wa Nabali.
\v 4 Sauli akaambiwa kuwa Daudi amekimbilia Gathi, hivyo hakumtafuta tena.
\s5
\v 5 Daudi akamwambia Akishi, "Kama nimepata kibali machoni pako, wanipatie mahali katika mojawapo ya miji ya nchi, ili nikae huko: kwa nini mtumishi wako akae pamoja na wewe katika mji wa kifalme?"
\v 6 Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi Ziklagi; ndiyo sababu mji wa Ziklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hadi leo.
\v 7 Idadi ya siku ambazo Daudi aliishi katika nchi ya Wafilisti ulikuwa mwaka mmoja na miezi minne.
\s5
\v 8 Daudi na watu wake walizipiga sehemu mbalimbali, wakiteka nyara Wageshuri, Wagirizi, na Waamaleki; kwa maana mataifa hayo ndio walikuwa wakaaji wa nchi, kwa uelekeo wa kwenda Shuri hadi kufika nchi ya Misri. Walikuwa wamekaa katika nchi hiyo toka nyakati za zamani.
\v 9 Daudi aliipiga nchi na hakumwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai; akatwaa kondoo, ng'ombe, punda, ngamia, na nguo; kisha alirudi na kufika tena kwa Akishi.
\s5
\v 10 Ndipo Akishi humuuliza, "Je, leo umefanya mashambulizi dhidi ya nani?" Daudi humjibu, "Nimefanya dhidi ya kusini mwa Yuda," au dhidi ya kusini mwa Wayerameeli," au "dhidi ya kusini mwa Wakeni."
\s5
\v 11 Daudi asingemwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai awalete hadi Gathi, akisema, "ili wasije kututeta, 'Daudi amefanya hivi na vile."' Hivi ndivyo alivyofanya kwa kipindi chote alichokaa katika nchi ya Wafilisti.
\v 12 Akishi alimwamini Daudi, akisema, "Amesababisha watu wake Israeli wamchukie kabisa; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu milele."
\s5
\c 28
\p
\v 1 Ikawa katika siku hizo Wafilisti walikusanya majeshi yao pamoja kwa ajili ya vita, wapigane na Israeli. Akishi akamwambia Daudi, "Ujue kwa hakika kwamba utakwenda nami ndani ya jeshi, wewe na watu wako."
\v 2 Naye Daudi akamwambia Akishi, "Sasa utajua kile ambacho mtumishi wako anaweza kufanya." Akishi akamwambia Daudi, "Basi sasa, nitakufanya uwe mlinzi wangu binafsi daima."
\s5
\v 3 Samweli alikuwa amefariki; Waisraeli wote walimwomboleza na kumzika huko Rama, katika mji wake mwenyewe. Wakati huo Sauli alikuwa amewafukuza kutoka nchini wote walioongea na wafu au pepo.
\v 4 Wafilisti walijikusanya wao wenyewe wakaja na kuweka kambi huko Shunemu; na Sauli akawakusanya Israeli wote pamoja, na wakaweka kambi yao huko Gilboa.
\s5
\v 5 Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, aliogopa na moyo wake ukatetemeka sana.
\v 6 Sauli alipomuomba BWANA kwa ajili ya msaada, BWANA hakumjibu - si kwa ndoto wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
\v 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, "Mnitafutie mwanamke ambaye anaweza kuongea na wafu, ili ni mwendee na kutafuta msaada wake." Watumishi wake wakamwambia, "Tazama, yupo mwanamke huko Endori awezaye kuongea na wafu."
\s5
\v 8 Basi Sauli akajigeuza, akavaa nguo nyingine tofauti, akaondoka yeye pamoja na watu wawili; wakamwendea yule mwanamke wakati wa usiku. Akasema, "Nitabirie, nakuomba, kwa kuongea na wafu, na uniinulie yule nitakayekutajia."
\v 9 Yule mwanamke akamwambia, "Tazama, unajua alichofanya Sauli, jinsi alivyowafukuza kutoka katika nchi wanaoongea na wafu au mizimu. Basi kwa nini mnatega mtego kwa ajili ya uhai wangu, ili kuniua?"
\v 10 Sauli akamwapia kwa BWANA na kusema, "Kama BWANA aishivyo, hakuna adhabu utakayopata kutokana na jambo hili."
\s5
\v 11 Kisha yule mwanamke akasema, "Je, nikuinulie nani?" Sauli akasema, "Niinulie Samweli."
\v 12 Yule mwanamke alipomwona Samweli, akalia kwa sauti kuu na kusema na Sauli, akisema, "Kwa nini umenidanganya? Maana wewe ni Sauli."
\s5
\v 13 Mfalme akamwambia, "Usiogope. Unaona kitu gani?" Yule mwanamke akamwambia Sauli, "Naona mungu akitoka katika nchi." Akamuuliza mwanamke,
\v 14 "Je, anafanana na nani?" Mwanamke akajibu, "Mtu mzee anazuka; naye amevaa kanzu." Sauli akafahamu kuwa huyo ni Samweli, naye Sauli akainamisha uso wake hadi chini akionesha heshima.
\s5
\v 15 Samweli akamwambia Sauli, "Kwa nini umenisumbua na kuniinua juu?" Sauli akajibu, "Nimetaabika sana, maana Wafilisti wamepanga vita dhidi yangu, na Mungu ameniacha na hanipi majibu tena, si kwa manabii, wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita, ili unijulishe kile nitakachofanya."
\s5
\v 16 Samweli akasema, "Kwa kuwa BWANA amekuacha, basi unaniuliza nini, naye amekuwa adui yako?
\v 17 BWANA amekutendea kile alichosema kuwa angekifanya. BWANA amerarua ufalme kutoka mkononi mwako na amempa ufalme mtu mwingine - amempa Daudi.
\s5
\v 18 Kwa sababu hukuitii sauti ya BWANA na hukutekeleza hasira yake kali juu ya Amaleki, kwa hiyo leo naye amefanya hili kwako.
\v 19 Zaidi ya hayo, BWANA atamweka Israeli pamoja na wewe katika mkono wa Wafilisti. Kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia ataliweka jeshi la Israeli katika mkono wa Wafilisti."
\s5
\v 20 Ndipo ghafla Sauli alianguka chini kifudifudi na aliogopa kwa sababu ya yale maneno ya Samweli. Aliishiwa nguvu mwilini mwake, kwa kuwa siku hiyo alikuwa hajala chakula, hata kwa usiku huo wote.
\v 21 Ndipo yule mwanamke akaja kwa Sauli na akaona kwamba Sauli amepata shida, naye akamwambia, "Tazama, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako; Nimeyaweka maisha yangu mkononi mwangu na nimeyasikiliza maneno uliyoniambia.
\s5
\v 22 Hivyo basi, nakusihi, sikiliza pia sauti ya mjakazi wako, na uniruhusu nilete chakula kidogo mbele yako. Ule ili upate nguvu za kwenda kule uendako."
\v 23 Lakini Sauli alikataa na kusema, "Sitakula." Lakini watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha hatimaye alisikiliza sauti zao. Hivyo aliinuka kutoka chini na kukaa kitandani.
\s5
\v 24 Yule mwanamke alikuwa na ndama mnono hapo nyumbani; akafanya haraka na kumchinja; akachua unga, akaukanda, na akatengeneza mikate isiyotiwa chachu kwa unga huo.
\v 25 Akaileta mbele ya Sauli na watumishi wake, nao wakala. Baaadaye waliinuka na kuondoka usiku huo.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Basi Wafilisti walikusanya pamoja majeshi yao yote huko Afeki; Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.
\v 2 Nao wakuu wa Wafilisti wakapitwa na mamia kwa maelfu; Daudi na watu wake wakapita wakiwa wa mwisho pamoja na Akishi.
\s5
\v 3 Kisha wakuu wa Wafilisti wakasema, "Hawa Waebrania wanafanya nini hapa?" Akishi akawaambia wakuu wengine wa Wafilisti, "Huyu si Daudi, mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amekaa nami kwa siku hizi, au kwa miaka hii, nami nimeona hana kosa tangu aje kwangu hadi leo?"
\s5
\v 4 Lakini wale wakuu wa Wafilisti walimkasirikia Akishi; wakamwabia, Mfukuze mtu huyo, aende kwake kule ulikompatia; usimruhusu aende nasi vitani, ili asiwe adui yetu katika vita. Kwa jinsi gani mtu huyu angeweza kufanya amani na bwana wake? Siyo kwa gharama ya vichwa vya watu wetu?
\s5
\v 5 Je, huyu siye Daudi ambaye walimuimba kwa kupokezana na kucheza, wakisema: 'Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi makumi elfu yake?"'
\s5
\v 6 Ndipo Akishi alimwita Daudi na kumwambia, "Kama BWANA aishivyo, umekuwa mwema, na kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema kama nionavyo mimi; maana sijaona kosa kwako tangu siku unakuja kwangu hadi siku hii ya leo. Hata hivyo, wakuu hawakupendi.
\v 7 Basi sasa rudi na uende kwa amani, ili usiwakwaze wakuu wa Wafilisti."
\s5
\v 8 Daudi akamwambia Akishi, "Lakini nimefanya nini? Kitu gani umekiona kwa mtumishi wako kwa muda ambao nimekuwa mbele yako hadi leo, kiasi kwamba nisiende kupigana na adui za bwana wangu mfalme?"
\v 9 Akishi akajibu na kumwambia Daudi, "Najua kwamba hauna lawama mbele zangu kama alivyo malaika wa Mungu; hata hivyo, wale wakuu wa Wafilisti wamesema, Kamwe hatapanda pamoja nasi hadi vitani.'
\s5
\v 10 Basi sasa amka asubuhi na mapema na watumishi wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; mara tu muamkapo asubuhi na mapema na kupata mwanga, ondokeni."
\v 11 Hivyo Daudi aliamka mapema, yeye pamoja na watu wake, waondoke asubuhi, warudi kule katika nchi ya Wafilisti. Lakini Wafilisti walipanda kwenda Yezreeli.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Ziklagi siku ya tatu, Waamaleki walifanya mashambulizi katika Negevu na Ziklagi. Waliupiga Ziklagi, wakauchoma moto mji,
\v 2 na kuwachukua mateka wanawake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake, mkubwa kwa mdogo. Wao hawakuua hata mmoja, lakini waliwachukua watu na kuondoka nao.
\s5
\v 3 Daudi na watu wake walipofika kwenye mji, ulikuwa umechomwa moto - na wake zao, watoto wao wakiume na wakike walichukuliwa mateka.
\v 4 Ndipo Daudi na watu aliokuwa nao wakapaza sauti zao na kulia hadi walipokuwa hawana nguvu zaidi za kulia.
\s5
\v 5 Wake wawili wa Daudi walichukuliwa mateka, yaani Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili aliyekuwa mke wa Nabali Mkarmeli.
\v 6 Daudi aliguswa sana, maana watu walikuwa wanaongea kuhusu kumpiga mawe, kwa sababu roho za watu wote walihuzunika, kila mtu kwa ajili ya mtoto wake wakiume na wakike, lakini Daudi alijiimarisha katika BWANA, Mungu wake.
\s5
\v 7 Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, "Tafadhali, niletee hapa ile naivera."Abiathari akaileta hiyo naivera kwa Daudi.
\v 8 Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya mwongozo, akisema, "Je, kama nikiliandama jeshi hili, nitalipata?" BWANA akamjibu, "Wafuate, maana kweli utawapata, na kwa hakika utarudisha kila kitu."
\s5
\v 9 Kwa hiyo Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye; nao wakafika katika kijito cha Bethori, mahali walipokaa wale walioachwa nyuma.
\v 10 Lakini Daudi aliendelea kuwafuata, yeye na watu mia nne; maana wale mia mbili walibaki nyuma, wakiwa wamechoka kiasi cha kutoweza kuvuka kijito cha Besori.
\s5
\v 11 Nao walimkuta Mmisri shambani na wakamleta kwa Daudi; wakampatia mkate, na akala; wakampa maji ya kunywa;
\v 12 kisha walimpa kipande cha keki ya tini na vishada viwili vya zabibu. Alipomaliza kula, akapata nguvu tena, kwa kuwa alikuwa hajala mkate wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.
\s5
\v 13 Ndipo Daudi akamuuliza, "Wewe ni mtu wa nani? Je, unatoka wapi?" Naye akajibu, "Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu siku tatu zilizopita nilikuwa mgonjwa.
\v 14 Tulifanya mashambulizi dhidi ya Negevu ya Wakerethi, na iliyochini ya Yuda, na ile Negevu ya Kalebu, na kuichoma moto Ziklagi."
\s5
\v 15 Daudi akamwambia, "Je, utanipeleka hadi kwa jeshi lililofanya mashabulizi?" Huyo Mmisri akasema, "Uniapie kwa Mungu kwamba hautaniua au kunisaliti na kuniweka katika mikono ya bwana wangu, nami nitakupeleka liliko hilo jeshi."
\s5
\v 16 Yule Mmisri alipompeleka huko Daudi, hao wateka nyara walikuwa wametawanyika kila sehemu, wakila na kunywa, na wakicheza, kwa sababu ya nyara zote walizokuwa wamezitwaa kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka nchi ya Yuda.
\v 17 Daudi akawashambulia tangu jua lilipozama hadi jioni ya siku ya pili. Hakuna mtu aliyeponyoka isipokuwa vijana mia nne, waliopanda ngamia na kukimbia.
\s5
\v 18 Daudi akarudisha vyote ambavyo Waamaleki walikuwa wamevichukua; na Daudi akawaokoa wake zake wawili.
\v 19 Hakuna kilichopotea, si kidogo wala kikubwa, si watoto wa kiume wala wa kike, si mali iliyotekwa, wala chochote ambacho wavamizi alikichukuwa kwa ajili yao. Daudi akawa amerejesha kila kitu.
\v 20 Akachukua makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambayo watu waliyatanguliza mbele ya ng'ombe wengine. Wakisema, "Hizi ni nyara za Daudi."
\s5
\v 21 Daudi akafika kwa wale watu mia mbili waliokuwa wamechoka kufuatana naye, wale walioachwa wakae katika kijito cha Besori. Watu hawa wakajitokeza kumlaki na watu waliokuwa naye.
\v 22 Ndipo watu wote waovu na wasiofaa miongoni mwa waliokwenda na Daudi wakasema, "Kwa sababu watu hawa hawakwenda nasi, hatutawapa chochote kutoka katika nyara tulizorudisha. Isipokuwa kila mtu aweza kuchukuwa mke na watoto wake, wawatoe na kwenda zao."
\s5
\v 23 Ndipo Daudi akasema, "Ndugu zangu, msifanye hivyo, kwa vitu ambavyo BWANA ametupatia. Ametuhifadhi na kuwaweka mkononi mwetu wavamizi waliotuinukia.
\v 24 Ni nani atawasikiliza kuhusu jambo hili? Kwa maana mgawo ni kwa yeyote aendae vitani, basi pia mgawo ni kwa yeyote aliyelinda mizigo; Nao watapata tena kilicho sawa."
\v 25 Ilikuwa hivyo tangu siku hiyo hadi leo, maana Daudi aliamua iwe sheria na amri kwa Israeli.
\s5
\v 26 Daudi alipofika Ziklagi, alituma sehemu ya nyara kwa wazee wa Yuda, kwa rafiki zake, akisema, "Tazama, hii ni zawadi yenu kutokana na nyara za adui wa BWANA."
\v 27 Zawadi zilienda kwa wazee waliokuwa Bethueli, na kwa hao waliokuwa Ramothi iliyoko kusini, na kwa hao waliokuwa Yatiri,
\v 28 na kwa hao waliokuwa Aroeri, na kwa hao waliokuwa Sifmothi, na kwa hao waliokuwa Eshtemoa
\s5
\v 29 Pia kwa wazee waliokuwa Rakali, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wayerameeli, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wakeni,
\v 30 na kwa hao waliokuwa Horma, na kwa hao waliokuwa Borashani, na kwa hao waliokuwa Athaki,
\v 31 na kwa hao waliokuwa Hebroni, na kwa sehemu zote ambazo Daudi mwenyewe na watu wake walizoea kwenda.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Waisraeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti na wakaanguka chini wakafa katika mlima wa Gilboa.
\v 2 Wafilisti wakamwandama Sauli na wanawe kwa karibu. Wakawaua wanawe Yonathani, Abinadabu, and Malkishua.
\v 3 Vita vikamwelemea Sauli, na wapiga upinde wakampata. Akapata maumivu makali kwa sababu yao.
\s5
\v 4 Kisha Sauli akamwambia mbeba silaha wake, "Chomoa upanga wako unichome nao. Vinginevyo, hawa wasiotahiriwa watakuja na kuninyanyasa." Lakini mbeba silaha wake hakukubali, kwa kuwa aliogopa sana. Hivyo Sauli alichukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
\v 5 Yule mbeba silaha akaona kwamba Sauli amekufa, yeye naye vivyo hivyo akauangukia upanga wake akafa pamoja naye.
\v 6 Kwa hiyo Sauli alikufa, wanawe watatu, na mbeba silaha wake - watu hawa wote walikufa pamoja siku iyo hiyo.
\s5
\v 7 Watu wa Israeli waliokuwa upande mwingine wa bonde, na hao waliokuwa ng'ambo ya Yordani, walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliiacha miji yao na kukimbia, nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.
\v 8 IKawa katika siku iliyofuata, Wafilisti wakafika kuchukua nyara za waliokufa, ndipo wakamuona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.
\s5
\v 9 Nao wakakata kichwa chake na kuondoa silaha zake, na wakawatuma wajumbe kwenda pande zote katika nchi ya Wafilisti kutangaza habari hizo katika mahekalu yao ya sanamu na kwa watu.
\v 10 Wakaziweka silaha zake katika hekalu la Ashtorethi, nao wakakitundika kiwiliwili chake kwenye ukuta wa mji wa Bethi Shani.
\s5
\v 11 Na wenyeji wa Yabeshi Gileadi waliposikia kile Wafilisti walichomfanyia Sauli,
\v 12 wapiganaji wote wakainuka na kwenda usiku wote na wakauondoa mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka ukuta wa Bethi Shani. Nao wakaenda Yabeshi na wakaichoma moto hiyo miili huko.
\v 13 Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.