sw_ulb_rev/03-LEV.usfm

1665 lines
130 KiB
Plaintext

\id LEV
\ide UTF-8
\h Mambo ya Walawi
\toc1 Mambo ya Walawi
\toc2 Mambo ya Walawi
\toc3 lev
\mt Mambo ya Walawi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mungu alimwita Musa na alisema naye kutoka kweye hema la kukutania, akasema,
\v 2 "Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi."
\s5
\v 3 Kama matoleo yake ni ya sadaka ya kutekezwa kutoka katika kundi, atatoa dume asiyekuwa na kasoro. Atamtoa katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania, ili iwe imekubaliwa mbele za Bwana.
\v 4 Ataweka mikono yake kichwani pa sadaka ya kuteketezwa, na ndipo itakuwa imekubaliwa badala yake kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 5 Ndipo atapaswa kuchinja ng'ombe mbele ya Bwana. Watoto wa Aroni, makuhani wataleta damu na kuinyunyizia katika madhabahu iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema la kukutania.
\v 6 Ndipo ataichuna sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande.
\s5
\v 7 Kisha wana wa Haruni kuhani wataweka moto katika madhabahu na kuweka kuni ili kuchochea moto.
\v 8 Wana wa Haruni, makuhani wataweka vipande, kichwa na mafuta, watazipanga juu ya kuni zilizoko juu ya moto ulio madhabahuni.
\v 9 Lakini matumbo yake na miguu lazima ataiosha kwa maji. Kisha kuhani atateketeza kila kitu kilicho juu ya madhabahu kama sadaka ya kuteketeza. Italeta harufu nzuri sana kwangu; itakuwa sadaka iliyotolewa kwa moto kwa ajili yangu.
\s5
\v 10 Kama sadaka kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza kutoka kundi, kondoo au mbuzi, lazima atoe dume asiye na kasoro.
\v 11 Lazima atamchinja juu ya madhabahu iliyo katika upande wa kaskazini mbele ya Bwana. Wana wa Haruni makuhani, watanyunyiza damu kila upande wa madhabahu.
\s5
\v 12 Kisha ataikata katika vipande, pamoja na kichwa na mafuta yake, kuhani atavipanga juu ya kuni zilizo katika moto ulio madhabahuni,
\v 13 lakini matumbo yake na miguu yake lazima ioshwe kwa maji. Kisha kuhani atatoa yote na kuiteketeza juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa, italeta harufu nzuri kwa ajili ya Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\s5
\v 14 Kama sadaka yake kwa Bwana itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa ni ndege, ndipo ataleta kama sadaka yake aidha ni huwa au kinda la njiwa.
\v 15 Kuhani ataileta madhabahuni, atamnyonga kichwa chake, na kuiteketeza juu ya madhabahu. Kisha damu yake itachuruzishwa juu ya pande za madhabahu.
\s5
\v 16 Kisha atakiondoa kibofu chake pamoja na uchafu wake, na kukiweka upande wa mashariki mwa madhabahu, katika sehemu ya majivu.
\v 17 Kisha atapasua mabawa yake, lakini hatagawanya katika vipande viwili. Kisha Kuhani atamtekeza katika madhabahu, juu ya kuni amabazo ziko juu ya moto. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa, na italeta harufu nzuri sana kwa Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake.
\v 2 Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\v 3 Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto.
\s5
\v 4 Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.
\v 5 Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta.
\s5
\v 6 Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka.
\v 7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta.
\s5
\v 8 Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, italeta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu.
\v 9 Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataitekeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana.
\v 10 Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto.
\s5
\v 11 Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautatekeza chachu wala asali kama matoleo yatakayotekezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana.
\v 12 Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu.
\v 13 Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi.
\s5
\v 14 Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa.
\v 15 Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka.
\v 16 Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kama mtu atoa dhabihu ambayo ni matoleo ya amani ya mnyama kutoka katika kundi, dume au jike, lazima atatoa mnyama asiyena kasoro mbele ya Bwana.
\v 2 Ataweka mikono yake juu ya sadaka yake na atamchinja mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Kisha wana wa Haruni makuhani watanyunyizia damu yake katika pande za madhabahu.
\s5
\v 3 Mtu akitoa dhabihu ya amani itolewayo kwa moto kwa ajili ya Bwana. Mafuta yanayofunika au yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
\v 4 figo mbili na mafuta yaliyofunika kiunoni na yanayozunguka ini, pamoja na figo atayatoa pamoja.
\v 5 Wana wa Haruni watayachoma hayo katika madhabahu pamoja na sadaka ya kutekezwa, juu ya kuni zilizo kwenye moto. Zitaleta harufu nzuri mbele ya Bwana; itakuwa sadaka ya itolewayo kwake kwa moto.
\s5
\v 6 Kama dhabihu ya amani ya mtu itolewayo kwa Bwana ni kutoka katika mifugo ni mbuzi au kondoo ni dume au jike, atatoa dhabihu isiyo na kasoro.
\v 7 Kama atatoa mwanakondoo kwa ajili ya dhabihu yake, atamtoa mbele za Bwana.
\v 8 Ataweka mkono wake juu ya ya kichwa cha dhabihu yake na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande za madhabahu.
\s5
\v 9 Mtu akitoa sadaka ya dhabihu ya amani kama sadaka ya kusogezwa kwa moto kwa Bwana. Mafuta, mafuta ya mkia yatakatwa hapo karibu na mfupa wa kiuno, na mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yaliyo katika matumbo,
\v 10 na figo zote mbili na mafuta yanayofunika yaliyo karibu na kiuno kitambi kilicho karibu na ini na figo ataziondoa zote.
\v 11 Na kuhani atayatekeza yote kwa moto katika madhabahu kama sadaka ya chakula isogezwayo kwa moto kwa Bwana.
\s5
\v 12 Kama matoleo ya mtu ni mbuzi, ndipo ataitoa mbele ya Bwana.
\v 13 Ataweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande zote za madhabahu.
\v 14 Mtu akitoa dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto. Ataondoa mafuta yanayozunguka matumbo, na mafuta yote yanayozunguka matumbo.
\s5
\v 15 Ataondoa pia figo mbili na mafuta yanayozunguka, ambayo yanazunguka kiuno na kitambi cha maini pamoja na figo.
\v 16 Kuhani atateketeza yote juu ya madhabahu kama matoleo ya chakula yatolewayo kwa moto, ni sadaka ya kuleta harufu nzuri sana. Mafuta yote ni ya Bwana.
\v 17 Itakuwa ni amri ya kudumu kwa kizazi cha watu katika maeneo yote mtakapotengeneza makazi, kwamba hamtakula mafuta au damu."'
\s5
\c 4
\p
\v 1 Bwana alisema na Musa na kumwambi,
\v 2 "Waambie wana wa Israeli 'mtu yeyote akifanya dhambi bila kukusudia, kufanya chochote ambacho Bwana ameagiza kutofanya, na kama akifanya chochote kilichozuiliwa, yafuatayo lazima yatatendeka.
\v 3 Kama ni kuhani mkuu aliyetenda dhambi na kuleta hatia kwa watu, atatoa dume asiyekuwa na kasoro kwa Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda kama sadaka ya dhambi.
\s5
\v 4 Ataleta dume mbele ya mlango wa hema ya kukutania mbele ya Bwana, ataweka mikono juu ya dume, na atamchinja huyo dume mbele za Bwana.
\v 5 Kuhani aliyewekewa mafuta atachukua damu ya dume na kuileta mbele ya hema ya kukutania.
\s5
\v 6 Kuhani atazamisha kidole chake katika damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Bwana, mbele ya pazia la mahali pa takatifu.
\v 7 Na kuhani ataweka kiasi cha damu ya huyo dume juu ya pembe za madhabahu ya kuvukizia uvumba mbele za Bwana, katika hema ya kukutania na ataimwaga yote iliyobaki chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mahali pa kuinglia katika hema ya kukutania.
\s5
\v 8 Atakata mafuta yote ya dume wa sadaka ya dhambi, mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
\v 9 figo mbili na mafuta yaliyopo pamoja nazo, yaliyo karibu na kiuno na kitambi cha maini pamoja na hizo figo.
\v 10 Ataondoa zote vile vile kama yanavyoondolewa katika dume wa sadaka ya dhabihu ya amani. Kuhani atatekeza sehemu hizo katika madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.
\s5
\v 11 Ngozi ya dume na mabaki yoyote ya nyama, pamoja na kichwa chake, miguu yake, matumbo yake na mavi yake,
\v 12 mabaki yote ya dume atayachukua nje ya mji mahali palipo safi, mahali wanapomwaga majivu; watateketeza sehemu zote juu ya kuni. Watateketeza sehemu zote mahali wanapomwaga majivu.
\s5
\v 13 Kama mkutano wote wa wana wa Israeli wakitenda dhambi bila kukusudia, na mkutano hawatakumbuka kwamba wametenda dhambi, na kufanya vile Bwana aliagiza wasifanye na wakajisikia hatia.
\v 14 Na dhambi waliyofanya ikajulikana, mkutano watatoa ng'ombe dume mchanga kuwa sadaka ya dhambi watamleta mbele ya hema ya kukutania.
\v 15 Wazee wa mkutano wataweka mikono yao juu ya kichwa cha ng'ombe mbele za Bwana, na ng'ombe atachinjwa mbele za Bwana.
\s5
\v 16 Kuhani aliyetiwa mafuta ataleta damu ya ng'ombe katika hema ya kukutania,
\v 17 kuhani atachovya kidole chake katika damu na kuinyunyizia mara saba mbele za Bwana mbele ya pazia.
\s5
\v 18 Ataweka kiasi cha damu katika pembe za madhabahu mbele za Bwana iliyo katika hema ya kukutania na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania.
\v 19 Atakata mafuta yote na kuyatekeza katika madhabahu.
\s5
\v 20 Hivyo ndivyo atakavyomfanya huyo ng'ombe, kama alivyomfanya ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia vivyo hivyo huyu ng'ombe, kuhani atawafanyia upatanisho watu nao watasamehewa.
\v 21 Atamchukua huyo ng'ombe nje ya mji na kumteketeza kama alivyomteketeza ng, ombe wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.
\s5
\v 22 Mtawala akitenda dhambi bila kukusudia kufanya moja ya yale Bwana Mungu wake ameagiza kutotenda, na anajisikia hatia
\v 23 na kama dhambi yake aliyotenda anaifahamu, ataleta dhabihu yake mbuzi mme asiye na kasoro.
\s5
\v 24 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi na kumchinja mahali ambapo huchinja sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
\v 25 Kuhani atachukua damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuiweka juu ya pembe za madhabahu kwa dhabihu ya kuteketezwa, na atamwaga damu chini ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa.
\s5
\v 26 Atateketeza mafuta yote katika madhabahu, kama vile mafuta ya dhabihu ya sadaka ya amani, Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtawala kulingana na dhambi yake, na mtawala atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 27 Kama yeyote wa watu wa kawaida akitenda dhambi bila kukusudia, kufanya vitu ambavyo Bwana ameagiza kutokufanywa na kama ana hatia,
\v 28 ndipo dhambi yake aliyoitenda ikajulikana kwake, ndipo ataleta mbuzi mke asiyekuwa na kasoro awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zake alizotenda.
\s5
\v 29 Ataweka mikono yake juu ya sadaka ya dhambi na kuchinja sadaka ya dhambi mahali pa sadaka ya kuteketezwa.
\v 30 Kuhani atachukua kiasi cha damu kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa. Damu yote iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu.
\s5
\v 31 Atayaondoa mafuta yote, kama alivyoondoa mafuta katika dhabihu ya amani. Kuhani ataiteketeza katika madhabahu ili kuwa harufu nzuri kwa Bwana. Kuhani atafanya upatanisho kwa mtu, na atasamehewa.
\s5
\v 32 Kama mtu ataleta mwanakondoo kama dhabihu yake kwa sadaka ya dhambi, ataleta jike asiye na kasoro.
\v 33 Ataweka mikono kichwani mwa sadaka ya dhambi na atamchinja kuwa sadaka ya dhambi mahali wanapochinjwa sadaka ya kuteketezwa.
\s5
\v 34 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu.
\v 35 Ataondoa mafuta yote, kama akatavyo mafuta ya mwanakondoo dhabihu ya sadaka ya amani na kuhani ataiteketeza juu ya madhabahu juu ya sadaka ya Bwana itolewayo kwa moto. Kuhani ataleta upatanisho kwa dhambi aliyoifanya, naye atasamehewa.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kama mtu atatenda dhambi kwa sababu hakusema ukweli wakati alipotakiwa kutoa ushahidi fulani kuhusu kile alichotakiwa, ameona au kufahamu habari zake, yeye anastahili adhabu.
\v 2 Au mtu akigusa kitu chochote ambacho Mungu amekitaja kuwa ni najisi hata kama ni mzoga wa wanyama wa porini au ni mzoga wa wanyama wa kufugwa au wataambaao hata kama mtu huyo hakukusudia kumgusa, yeye ni najisi na mwenye hatia.
\s5
\v 3 Au amegusa kitu chochote kilicho kichafu, kwa vyovyote kama hakujua, ndipo atakuwa na hatia akijua vile.
\v 4 Au kama yeyote akiapa bila kufikiri kwa midomo yake kufanya ubaya, au kufanya vyema kwa vyovyote vile mtu ameapa kwa haraka atakapotambua atakuwa na hatia kwa vitu hivyo.
\s5
\v 5 Mtu yeyote akiwa na hatia kwa vitu hivi, lazima akiri kwa yoyote dhambi aliyotenda.
\v 6 Ndipo atakapoleta sadaka yake ya hatia mbele za Bwana kwa dhambi aliyokwisha tenda. Ataleta kondoo jike au mbuzi kutoka katika kundi lake kuwa matoleo ya dhambi, kuhani atafanya upatanisho kuhusu dhambi yake.
\s5
\v 7 Kama hataweza kununua mwana kondoo ataleta kama sadaka ya hatia, hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana, mmoja kwa sadaka ya dhambi na mwingine ni sadaka ya kutekeketezwa.
\v 8 Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
\v 9 Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.
\s5
\v 10 Ndipo ataoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 11 Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
\s5
\v 12 Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
\v 13 Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'"
\s5
\v 14 Bwana akamwambia Musa, akasema,
\v 15 "Kama mtu akikiuka amri na kufanya dhambi kinyume na mambo matakatifu ya Bwana, lakini akifanya bila kukusudia ataleta sadaka ya hatia kwa Bwana. Sadaka hii itakuwa ni kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi; thamani yake halisi kifedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kama sadaka ya hatia.
\v 16 Lazima atalipa kwa Bwana kwa kile alichokosa kulingana na kitakatifu, na ataongezea moja ya tano na kumpa kuhani. Ndipo kuhani ataweka upatanisho kwa ajili yake pamoja na kondoo wa sadaka ya hatia, na mtu atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 17 Kama mtu akitenda dhambi kwa kufanya kile ambacho Bwana aliagiza kisifanyike, hata kama hakujuwa, atakuwa na hatia na ataibeba hatia yake.
\v 18 Lazima ataleta kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi, anayestahili thamani ya fedha, kama sadaka ya hatia kwa kuhani. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kulingana na dhambi aliyotenda, ambayo hakujua atakuwa amesamehewa.
\v 19 Ni sadaka ya hatia, na amekuwa na hatia mbele za Bwana."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Bwana alisema na Musa kumwabia,
\v 2 "Kama mtu akifanya dhambi na kuvunja amri kinyume na Bwana, kama kujihusisha na uongo dhidi ya jirani yake kuhusu kitu fulani cha kutokuwa mwaminifu, au kama akidanganya au kuiba au amemdhurumu jirani.
\v 3 Au akiokota kitu fulani ambacho jirani yake amepoteza na kusema uongo kuhusu hicho, na kuapa kwa uongo au kwa mambo kama haya ambayo watu wanaweza kutenda dhambi.
\v 4 Ndipo itakuwa hivi, kama ametenda dhambi na hatia, kwamba lazima akirudishe kwa vyovyote alichoiba au kudanganya au amedhurumu au kitu kilichopotea naye kukiokota.
\s5
\v 5 Au kama amedanganya kwa jambo lolote, lazima atakirudisha kamilina kuongezea sehemu ya tano kwa kumlipa anayedai, kwa siku ile anayopatikana na hatia.
\v 6 Ataleta sadka ya hatia kwa Bwana: kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi lake kulingana na thamani yake, kama sadaka ya hatia kwa kuhani.
\v 7 Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele ya Bwana, atakuwa amesamehewa kulingana na chochote kilicho mfanya kuwa na hatia."
\s5
\v 8 Ndipo Bwana alisema na Musa kumwambia,
\v 9 "Mwagize Haruni na wanawe, kusema, 'hii ni sheria ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa lazima iwe juu ya makaa ya madhabahu usiku wote hata asubuhi, na moto wa madhabahu utaendelea kuwaka.
\s5
\v 10 Kuhani atavaa nguo zake za kitani na atavaa nguo za kitani ndani yake. Atatoa majivu yaliyobaki baada ya moto kutekeza sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu, na ataweka majivu pembeni mwa madhabahu.
\v 11 Atavua mavazi haya na kuvaa mavazi mengine ili kuchukua majivu nje ya kambi na kupeleka mahali palipo safi.
\s5
\v 12 Moto katika madhabahu utaendelea kuwaka. Usizimike, na kuhani ataongeza kuni kila asubuhi. Atapanga juu yake sadaka ya kuteketezwa kama inavyotakiwa, na atateketeza juu yake mafuta ya sadaka ya amani.
\v 13 Moto lazima utaendelea kuwaka katika madhabahu, kamwe usizimike.
\s5
\v 14 Hii ni sheria ya sadaka ya nafaka. Wana wa Haruni watatoa mbele ya Bwana katika madhabahu.
\v 15 Kuhani atachukua konzi ya unga laini wa sadaka ya nafaka na mafuta na ubani ambao uko juu ya sadaka ya nafaka, atateketeza juu ya madhabahu kuleta harufu nzuri ya shukrani ya kumpendeza Bwana.
\s5
\v 16 Haruni na wanae watakula sadaka inayobaki, italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu. Watakula katika ua ya hema ya kukutania.
\v 17 Haitaokwa pamoja na chachu. Nimewapa kama sehemu ya sadaka yangu itolewayo kwa moto, ni takatifu sana, kama sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
\v 18 Kwa nyakati zote zijazo kupitia watu wa kizazi chako, mwanaume yeyote mzaliwa kutoka kwa Haruni aweza kula ni sehemu yake, ichukuliwayo katika sadaka ya Bwana kwa moto. Yeyote anayeigusa atakuwa mtakatifu."
\s5
\v 19 Bwana aliongea tena na Musa kumwambia,
\v 20 "Hii ni sadaka ya Haruni na wanawe ambayo watatoa kwa Bwana katika siku ambayo kila mwana atawekwa wakfu: sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kama kawaida sadaka ya nafaka nusu yake asubuhi na nusu yake jioni.
\s5
\v 21 Itatengenezwa na mafuta katika kikaango, utaileta ikiwa imeandaliwa imeokwa katika vipande utatoa sadaka ya nafaka ili kuleta harufu nzuri kwa Bwana.
\v 22 Mwana wa Kuhani Mkuu atakayekuwa Kuhani Mkuu mpya kutoka miongoni mwa wanawe ataitoa. Kama amri ya milele, yote itateketezwa kwa Bwana.
\v 23 Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itatekezwa yote. Haitaliwa kamwe."
\s5
\v 24 Bwana alisema tena Musa, kumwambia,
\v 25 "Sema na Haruni na watoto wake kwamba, 'Hii ni sheria ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi lazima kuchinjwa mahali pa sadaka ya kuteketezwa itachinjwa mbeleya Bwana. Ni takatifu sana.
\v 26 Kuhani atakayeitoa kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila. Italiwa mahali patakatifu katika ua wa hema ya kukutania.
\s5
\v 27 Yeyote atakayeigusa nyama yake atakuwa ni mtakatifu na kama damu itadondokea mavazi yatafuliwa mahali palipodondokewa, mahali patakatifu.
\v 28 Lakini chungu kikipikiwa kitavunjwa, kama imepikiwa katika chombo cha shaba, lazima kitasuguliwa na kusafishwa kwa maji.
\s5
\v 29 Mwanaume yeyote miongoni mwa makuhani anaweza kula nyama hiyo kwa sababu ni takatifu sana.
\v 30 Na hakuna sadaka ya dhambi italiwa ambayo damu yake imeletwa katika hema ya kukutania kufanya upatanisho katika mahali patakatifu. Ni lazima iteketezwe.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya hatia. Kwa sababu hiyo ni sadaka takatifu sana.
\v 2 Ni lazima waichinje sadaka ya hatia mahali panapostali kuchinjwa, na ni lazima watainyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
\v 3 Mafuta yote yaliyomo ndani yake yataondolewa: mafuta ya mkiani, mafuta yaliyo sehamu za ndani,
\v 4 zile figo mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake, yaliyo karibu na kiuno, na yanayofunika ini—nyama hii yote lazima iondolewe pamoja na hizo figo.
\s5
\v 5 Kuhani ataviteketeza vipande hivi juu ya madhabahu viwe dhabihu iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia
\v 6 Kila mwanaume miongoni mwa familia ya kuhani anaweza kula sehemu ya sadaka hii. Lakini ni lazima iliwe ndani ya mahali patakatifu kwa sababu ni takatifu sana.
\s5
\v 7 Nayo sadaka ya dhambi ni kama ilivyo sadaka ya hatia. Ni sheria ileile hutumika kwa zote mbili. Zote ni mali ya kuhani azitumiaye kufanya upatanisho.
\v 8 Kuhani atoaye sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuchuku ngozi ya sadaka hiyo kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 9 Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
\v 10 Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Aroni kwa usawa.
\s5
\v 11 Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahweh.
\v 12 Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahweh, basi ataitoa pamoja na dhabih uya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.
\s5
\v 13 Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.
\v 14 Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahweh. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.
\s5
\v 15 Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.
\v 16 Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.
\s5
\v 17 Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.
\v 18 Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi mwenyewe yake.
\s5
\v 19 Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.
\v 20 Hata hivyo, mtu najisi anayekula nyama kutoka kwenye dhabihu ya matoleo ya amani ambayo ni ya Yahweh yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
\s5
\v 21 Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilichonajisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliyenajisi, au wa kitu fulani kilichonajisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahweh, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
\s5
\v 22 Kisha Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 23 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
\v 24 Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
\s5
\v 25 Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
\v 26 Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
\v 27 Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'"
\s5
\v 28 Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
\v 29 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
\v 30 Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
\s5
\v 31 Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
\v 32 Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.
\s5
\v 33 Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Aroni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.
\v 34 Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Aroni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.
\s5
\v 35 Huu ndiyo mgao wa Aroni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahweh katika kazi ya kuhani.
\v 36 Huu ndio mgao ambao Yahweh aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.
\s5
\v 37 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,
\v 38 ni sheria ambazo Yahweh alizitoa kwa Musa kwenye Mlima Sinai siku aliyowaamru watu wa Israeli kutoa dhabihu zao kwa Yahweh katika jangwa la Sinai.'"
\s5
\c 8
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Walete Aroni na wanawe pamoja naye, mavazi na mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili, na kikapu cha mkate usio na hamira.
\v 3 Ita kusanyiko lote kwenye ingilio la hema la kukutania."
\s5
\v 4 Kwa hiyo Musa akafanya kama Yahweh alivyomwamru, nalo kusanyiko lilikuja pamoja mbele ya ingilio la hema la kukutania. Kisha Musa akaliambia kusanyiko,
\v 5 "Hivi ndivyo alivyotuamru Yahweh tutende."
\s5
\v 6 Musa akamleta Aroni na wanawe na kuwaosha kwa maji.
\v 7 Akamvika Aroni kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini na kumfunga ukumbuu kiunoni mwake, akamvika joho la nje lenye mikono mirefu na kumvika kile kizibao chenye vipande viwili tumboni na mgongoni na kukifunga kuzunguka kiunoni mwake kwa mshipi uliosokotwa kwa ustadi na kukikaza mwilini mwake.
\s5
\v 8 Kisha Musa akaweka kifuko kifuani mwa Aroni, na ndani ya kifuko hicho akaweka Urimu na Thumimu.
\v 9 Na kisha akamfunga kiremba kichwani, na juu ya kiremba kwa mbele, akaweka bamba la dhahabu; liwe taji takatifu, kama Yahweh alivyomwamru yeye.
\s5
\v 10 Musa akayatwaa hayo mafuta ya upako, akalipaka lile hema la kukutania na kila kitu kilichokuwamo ndani yake na kuvitenga kwa ajili ya Yahweh.
\v 11 Akayanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kisha akaipaka mafuta hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na sinia la kunawia na kitako chake ili kuvitenga wa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 12 Akamimina sehemu ya mafuta ya upako juu ya kichwa cha Aroni na kisha akampaka mafuta ili kumtenga.
\v 13 Musa akawaleta wana wa Aroni na kuwavika kila mmoja kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini. Kila mmoja wao akamfunga kwa ukumbuu kiunoni mwake na kuwafunga vitambaa vya kitani kichwani pao, kama vile Yahweh alivyokuwa amemru Musa.
\s5
\v 14 Musa akamleta huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha fahali ambaye wamemelete kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
\v 15 Musa akamchinja, na kisha akachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuiweka juu ya mpembe za madhabahu, akaitakasa hiyo madhabahu, na kuitenga kwa Mungu, ambapo kwa kufanya hivyo, aliisababisha madhabahu kuwa sehemu ya kufaa kwa kufanyia upatanisho.
\s5
\v 16 Akachukua mafuta yote yaliyokuwa sehemu za ndani, kile kiwambo cha ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake, Musa akaichoma hiyo nyama yote juu ya madhabahu.
\v 17 Lakini yule fahali, ngozi yake, nyama yake na kinyesi chake, akavichoma nje ya kambi, kama vile Yehweh alivyokuwa amemwamru yeye.
\s5
\v 18 Musa akamleta yule konndoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo kondoo.
\v 19 Musa akamchinja kondoo na kuinyunyizia damu yake kila upande wa madhabahu.
\s5
\v 20 Naye akamkatakata kondoo vipande vipande na akakiteketeza kichwa chake pamoja na vile vipande na mafuta.
\v 21 Akaziosha kwa maji zile sehemu za ndani pamoja na miguu na akamteketeza kandoo mzima juu ya madhabahu. Ilikuwa ni dhabihu ya kuteketezwa na ilitoa harufu ya kupendeza, sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
\s5
\v 22 Kisha Musa akamleta yule kondoo dume mwingine, kondoo wa kuwekwa wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo.
\v 23 Aroni akamchinja, naye Musa akachukua sehemu ya damu na kuiweka kwenye ncha ya sikio la Aroni la kulia, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye kidole kikumbwa cha mguu wake wa kulia.
\v 24 Akawaleta wana wa Aroni, naye akaweka sehemu ya damu ya kondoo yule kwenye ncha ya sikio lao la kulia, kwenye dole gumba lao cha mkono wa kulia na kwenye kidole chao kikubwa cha mguu wa kulia. Kisha Musa akainyunyiza damu ya huyo kila upande wa madhabahu
\s5
\v 25 Naye akayatwaa yale mafuta, mafuta ya mkiani, mafuta liyolikuwa sehemu za ndani, na mafuta yafunikayo ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.
\v 26 Akachukua mkate mmoja kutoka kwenye kikapu cha mikate isiyo na hamira ambayoo ilikuwa mbele za Yahweh, akatwaa mkate moja usio na hamira, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na mkate mwemba wa kaki na akaiweka juu ya mafuta na juu ya paja la kulia la kondoo.
\v 27 Akaiweka yote mikoni mwa Aroni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahweh kuwa sadaka ya kutikiswa
\s5
\v 28 Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto.
\v 29 Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.
\s5
\v 30 Musa akatwaa sehemu ya mafuta ya upako na damu iliyokuwa juu ya madhabahu; naye akayanyunyiza haya juu ya nguo za Aroni, juu ya nguo zake mwenyewe na juu ya nguo za wana wa Aruni waliokua pamoja naye. Kwa njia hii alimtenga Aroni na nguo zake, na wanawe na nguo zao kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 31 Kwa hiyo Musa akawambia Aruni na wanawe, "Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyoamriwa, kusema, 'Aroni na wanawe wataila.'
\v 32 Masalio yoyote ya nyama na mikate utayateketeza kwa moto.
\v 33 Na hamtatoka kwenye ingilio la hema la kukutania kwa muda wa siku saba, hata zitakapotimia siku za kuwekwa mikono kwenu. Kwa kuwa kwa muda wa siku saba, Yahweh atawaweka wakfu.
\s5
\v 34 Kilichotendeka siku hii— Yahweh ndiye amekiamru kitendekeke ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
\v 35 Mtakaa kwenye ingilio la hema la kukutania mchana na usiku siku saba, nanyi ishikeni amri ya Yahweh ili msije mkafa, kwa sababu hivi ndivyo ilivyoamriwa.
\v 36 Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya mambo yote ambayo Yahweh alikuwa amewaamru kwa kinywa cha Musa.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Katika siku ya nane, Musa akawaita Aroni na wanawe pamoja na wazee wa Israeli.
\v 2 Akamwambia Aroni, "Twaa ndama dume kutoka kundini kwa ajili ya sadaka ya dhambi zako, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, na uwatoe mbele za Yahweh.
\s5
\v 3 Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Twaeni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi na ndama na mwana-kondoo, hawa wawili wawe na umri wa mwaka mmoja na bila dosari, ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
\v 4 pia twaeni fahali na kondoo dume kwa sadaka za amani ili kuwatoa mbele za Yahweh, na sadaka za nafaka iliyochanganywa na mafuta, kwa sababu leo Yahweh atajidhihirisha kwenu.
\v 5 Kwa hiyo wakaleta kwenye hema la kukutania vyote ambavyo Musa aliagiza, nalo kusanyiko lote la Israeli likakaribia na kusimama mbele za Yahweh.
\s5
\v 6 Kisha Musa akasema, "Hivi ndivyo Yahweh amewaamru nyinyi mfanye, ili kwamba utukufu wake uweze kuonekana kwenu.
\v 7 "Musa akamwambia Aroni, "Njoo karibu na Madhabahu na uteo sadaka yako ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu ili kufanya upatanisho kwa ajili yao kama vile ambavyo Yahweh amekwishaamru."
\s5
\v 8 Kwa hiyo Aroni akaikaribia madhabahu na akamchinja yule ndama kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe.
\v 9 Nao wana wa Aroni wakamletea hiyo damu, naye akakichofya kidole chake kwenye damu na kuiweka kwenye pembe za madhabahu, kisha akaimwaga damu chini ya kitako cha madhabahu.
\s5
\v 10 Hata hivyo, aliyateketeza hayo mafuta, figo, na mafuta yanafunika ini juu ya madhabahu kuwa sadaka ya dhambi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
\v 11 Na akaiteketeza hiyo nyama pamoja na ngozi nje ya kambi
\s5
\v 12 Aroni akaichinja sadaka ya kuteketezwa, nao wanawe wakampa hiyo damu, ambayo aliinyunza pande zote za madhabahu.
\v 13 Kisha wakampa ile sadaka ya kuteketezwa, kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
\v 14 Akaziosha sehemu za ndani pamoja na miguu na kuziteketeza juu ya dhabihu ya kuteketezwa juu ya Madhabahu.
\s5
\v 15 Aroni akaleta dhabihu ya watu— mbuzi, kisha akamtoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi yao naye akamchinja, akaitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi, kama alivyofanya kwa yule mbuzi wa kwanza.
\v 16 Akaileta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama Yahweh alivyokuwa ameamru.
\v 17 Akaileta sadaka ya nafaka; akakijaza kiganja chake nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa.
\s5
\v 18 Pia akamchinja fahali na yule kondoo dume, dhabihu kwa ajili ya sadaka ya amani, ambayo ilikuwa kwa ajili ya watu. Nao wana wa Aronni wakampa damu, ambayo aliinyunyiza kila upande wa mdhabahu.
\v 19 Hata hivyo, waliyakata mafuta ya fahali na ya yule kondoo dume, mafuta ya kwenye mkia, mafuta yafunikayo sehemu za ndani, figo, na yale mafuta yaliyofunika mapafu.
\s5
\v 20 Wakazichukua hizi sehemu zilizokatwa wakaziweka juu ya vidari, na kisha Aroni akateketeza mafuta juu ya madhabahu.
\v 21 Naye Aroni akavitikisa vidari na paja la kulia kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh, kama vile Musa alivyokuwa ameamru,
\s5
\v 22 Kisha Aroni akainua juu mikono yake mbele ya watu na kuwabariki, kisha akashuka chini kutoka mahali alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani.
\v 23 Musa na Aroni wakaingia ndani ya hema la kukutania, kisha wakatoka nje tena na kuwabariki watu, na utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote.
\v 24 Moto ukashuka kutoka kwa Yahweh na ukairamba sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wlipoona jambo hili, wakapiga kelele na kulala chini.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua kila mtu kifukizo chake, akaweka moto ndani yake, na kisha uvumba. Kisha wakatoa moto usiokuabalika mbele za Yahweh, moto ambao hakuwaamru wao kuutoa.
\v 2 Kwa hiyo moto ukashuka chini mbele za Yahweh na kuwala, nao wakafa mbele za Yahweh.
\s5
\v 3 Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'" Naye Aroni hakusema neno lolote.
\v 4 Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Aroni, naye akamwambia, "njoo huku na uwatowe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema."
\s5
\v 5 Hivyo wakakaribia na kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani, nao wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyokuwa ameelekeza. Kisha Musa akamwambia Aroni na wanawe wengine wawili, Eliezari na Ithamari, "
\v 6 Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahweh asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto.
\v 7 Msiende nje kutoka kwenye ingilio la hema la kukutania, ama sivyo mtakufa, kwa kuwa mafuta ya Yahweh ya upako yako juu yenu." Kwa hiyo wakatenda sawasawa na maelekezo ya Musa.
\s5
\v 8 Mungu akazungumza na Aroni, akisema,
\v 9 "Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,
\v 10 ili kupaambanua kati ya mambo matakatifu na mambo ya kawaida, na kati ya najisi na safi,
\v 11 ili kwamba mweze kuwafundisha watu wa Israeli amri zote ambazo Yahweh ameziamru kwa kinywa cha Musa.
\s5
\v 12 Musa akazungumza na Aroni na wanawe wawili waliosalia; Eliazari naIthamari, Twaeni sadaka ya nafaka inayobaki kutokana na sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto, nanyi ileni kando ya madhabahu bila hamiara, kwa kuwa ni takatifu sana.
\v 13 lazima mtaila mahali patatifu kwa sababu huo ni mgao wako wewe na mgao wa wanao wa matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, kwa kuwa hivi ndivyo limeamriwa niwaambie.
\s5
\v 14 Kile kidari kitikiswacho na lile paja ambalo hutolewa kwa Yahweh, yapasa mzile mahali palipo safi panapokubalika kwa Mungu. Wewe mwenyewe, wanao na binti zako waliopamoja nawe mtakula sehemu hizo, kwa kuwa zimetolewa kuwa mgao wako na mgao wa wanao kutokana na dhabihu ya sadaka ya ushirika wa watu wa Israeli.
\v 15 Lile paja lililotolewa na kidari kilichotikiswa, ni lazima ziletwe pamoja na sadaka ya mafuta iliyofanywa kwa moto, ili kutikiswa mbele za Yahweh. Nazo zitakuwa zako wewe na wanao kuwa mgao wenu daima, kama Yahweh alivyoamru.
\s5
\v 16 Kisha Musa akauliza kuhusu yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye akagundua kwamba alikuwa ametekezwa kwa moto. Kwa hiyo akawakasirikia Eliazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia; akawaambia,
\v 17 "Kwa nini hamjaila sadaka ya dhambi katika eneo la hema, kwa kuwa ni takatifu sana, na kwa kuwa Yahweh amishaitoa kwenu ili kuchukua uovu wa kusanyiko, ili kufanya upatanisho kwa aijli yao mbele zake?
\v 18 Tazama, damu yake haikuletwa ndani ya hema, kwa hiyo iliwapasa kwa hakika kuwa mekwisha ila kwenye eneo la hema, kama nilivyoagiza?
\s5
\v 19 Kisha Aroni akamjibu Musa, " Tazama, leo walitoa sadaka yao ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa mbele za Yahweh, na jambo hili vilevile limetendeka kwangu leo. Ikiwa nimeshakula sadaka ya dhambi leo, Je! Isingekuwa imeshapendeza mbele za Yahweh?"
\v 20 Naye Musa aliposikia hivyo, akaridhika.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na Aroni, akasema,
\v 2 "Sungumzeni na watu wa Israeli muwaambie, 'Hivi ndivyo viumbe vyenye uhai ambavyo mwaweza kula miongoni mwa wanyama walioko juu ya nchi.
\s5
\v 3 Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua.
\v 4 Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
\s5
\v 5 Pimbi pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyo pia ni najisi kwenu.
\v 6 Na sungura pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyu naye ni najisi kwenu.
\v 7 Na nguruwe pia: ingawaje yeye anazo kwato zilizogawanyika lakini hacheui, kwa hiyo yeye ni najisi kwenu.
\v 8 Msile aina yoyote ya nyama yao, wala msiiguse mizoga yao. Hao ni najisi kwenu.
\s5
\v 9 Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.
\v 10 Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa watakuwa chukizo, msile nyama yao, pia mizoga yao sharti itakuwa chukizo.
\v 12 Chochote kisichokuwa na mapezi au magamba kilichomo majini ni lazima kiwe chukizo kwenu.
\s5
\v 13 Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,
\v 14 mwewe mwekundu, aina yoyote ya kipanga,
\v 15 kila aina ya kunguru,
\v 16 kiruka-njia, kipasuasanda, Shakwe, na aina yoyote ya mwewe.
\s5
\v 17 Ni lazima pia bundi mdogo na bundi mkubwa muwaone kuwa chukizo, mnandi,
\v 18 bundi mweupe na mwari,
\v 19 korongo na ina zote za koikoi, huduhudi na popo pia.
\s5
\v 20 Wadudu wote wenye mabawa wanatembea kwa miguu minne kwenu ni machukizo.
\v 21 Lakini manaweza kula wadudu wenye mabawa wanaotembea kwa miguu minne ya kurukia ardhini yenye vifundo.
\v 22 Na manaweza kula kula aina zote za nzige, senene, parare, au panzi.
\v 23 Lakini wadudu wote warukao wenye miguu minne ni chulkizo kwenu.
\s5
\v 24 Nanyi mtakuwa najisi hata jioni kutokana na wanyama hawa endapo mtagusa mizogo yao.
\v 25 Na yeyote atakayeokota mojawapo wa mizoga yao ni lazima atazifua ngua zake naye atakuwa najisi hata jioni.
\s5
\v 26 Mnyama yeyote ambaye anazo kwato ziliachana ambazo hazikugawanyika kabisa au hacheui huyo ni najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa najisi.
\v 27 Mnyama yeyote anayetembea kwa vitanga vyake miongoni mwa wanyama waendao kwa miguu yote minne ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mzoga kama huo atakuwa najisi hata jioni.
\v 28 Na yeyote aokotaye mzoga kama huo ni zazima atazifua nguo zake na kuwa najisi hata jioni. Wanyama hawa watakuwa najisi kwenu.
\s5
\v 29 Kuhusiana na wanyama wataambaao juu ya ardhi, hawa ndiyo walio najisi kwenu: kicheche, panya, aina zote za mijusi mikubwa, guruguru,
\v 30 kenge, mijusi ya ukutani, goromoe, na kinyonga.
\s5
\v 31 Wanyama hawa wote ambao hutambaa, hawa ndiyo watakuwa najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa njisi hata jioni.
\v 32 Na iwapo mmoja wao anakufa na kuanguka juu ya chombo, chombo hicho kitakuwa najisi, ama kiwe kimetengenezwa kwa mbao, nguo, ngozi, au gunia. Kiwe chombo cha namna gani na kiwe kwa matumizi gani, ni lazima kitalowekwa katika maji nacho kitakuwa najisi hata jio. Kisha kitakuwa safi.
\v 33 Kwa hiyo kila chungu ambacho mnyama najisi atakiangukia juu yake au ndani yake, chochote kilichomo kwenye chungu hicho kitakuwa najisi, na ni lazima mtakivunja chungu hicho.
\s5
\v 34 Vyakula vyote ambavyo ni safi na kilichuhusiwa kuliwa, lakini kikaingiwa na maji kutoka kwenye chungu najisi kilichoanguka, nacho kitakuwa najisi.
\v 35 Na kitu chochote kinachoweza kunywewa kutoka kwenye chungu kama hicho kitakuwa najisi. Kila kitu kitakachoangukiwa juu yake na kipande cha mzoga wa mnyama najisi nacho kitakuwa najisi, ama liwe ni jiko au vyungu vya kupikia. Ni najisi na ni lazima kiwe najisi kwenu.
\s5
\v 36 Chemchemi au kisima cha maji ya kunywa yanapokusanyika patabaki kuwa safi iwapo kiumbe najisi kama hicho kitaangukia humo. Lakini ikiwa yeyote anaugusa mzoga wa mnyama aliye najisi uliomo ndani ya maji, yeye atakuwa najisi.
\v 37 Iwapo sehehemu yoyote ya mzoga wa mnyama aliyenajisi inaangukia juu ya mbegu zozote zilizo kwa ajili ya kupanda. Mbegu hizo zitakuwa bado zingali safi.
\v 38 Lakini kama maji yanawekwa juu ya mbegu, na kama sehemu ya mzoga unaangukia juu yake, nazo zitakuwa najisi kwenu.
\s5
\v 39 Iwapo mnyama yeyote awezaye kuliwa anakufa, naye yeyote amgusaye atakuwa najisi hata jioni.
\v 40 Na yeyote alaye chochote cha mzoga huo atalazimika kufua nguo zake naye atakuwa anjisi hata jioni. Na yeyote aokotaye mzoga kama huo atafua nguo zake na kuwa najisi hata jioni.
\s5
\v 41 Kila mnyama atambaaye juu ya ardhi atakuwa chukizo; hatakuwa wa kuliwa.
\v 42 Chochote kitambaacho kwa kujivuta juu ya tumbo lake, na chochote kitembeacho kwa miguu yake yote minne, au chochote kilicho na miguu mingi—wanyama wote ambao hutambaa juu ya nchi, hawa msiwale, kwa sababu watakuwa machukizo.
\s5
\v 43 Msijinajisi wenyewe kwa kiumbe chochote nnajisi kitaambacho; msijinasi wenyewe kwavyo, ili kwamba msije mkachafuliwa navyo.
\v 44 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu. Nanyi lazima muwe watakatifu, kwa hiyo na iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu. Haiwapasi kujichafua kwa aina yoyote ya kiendacho juu ya nchi.
\v 45 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh, aliyewaleta ninyi kutoka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo lazima muwe watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.
\s5
\v 46 Hii ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho majini, na ya kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi,
\v 47 kwa jili ya kilie kinachopaswa kutofautishwa kati ya kilicho najisi na kilicho safi, na kati ya vitu vilivyokufa na vilivyo hai ambavyo vyaweza kuliwa na vitu vyenye uihai visivyoweza kuliwa."
\s5
\c 12
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa,
\v 2 "zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi.
\v 3 Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.
\s5
\v 4 Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.
\v 5 Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa mud wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini sita.
\s5
\v 6 Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,
\s5
\v 7 Kisha atawatoa mbele za Yahweh na kufanya sadaka ya upatanisho kwa ajili yake, naye atatakaswa kutokana kutiririka kwa damu yake. Hii ndiyo sheria kuhusu mwanamke aifunguaye ama mtoto wa kiume au wa kike.
\v 8 Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili ya njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na Aroni, akasema,
\v 2 Mtu yeyote anayeonekana na uvimbe au pele au doa ling'aalo juu ya ngozi ya mwili wake, na likawa limeambukizwa ugonjwa wa ngozi mwilini mwake, ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani mkuu au kwa mmoja wa wanawe makuhani.
\s5
\v 3 Naye kuhanai atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada cha kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.
\v 4 Iwapo lile doa ling'aalo katika ngozi yake ni jeupe, na kuonekana kwake halikwenda chini zaidi ya ngozi, na iwapo malaika za eneo lenye ugonjwa hazijabadilika kuwa nyeupe, naye kuhani atamtenga mgonjwa kwa siku saba.
\s5
\v 5 Katika siku ya saba, huyo kuhani itambidi kumchunguza tena ili kuona kama katika maamzi yake huo ugonjwa siyo mbaya, na kama haujaenea kwenye ngozi. Iwapo haujaenea, basi, kuhani atamtenga kwa siku saba zaidi.
\v 6 Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
\s5
\v 7 Lakini endapo ule upele utakuwa umishasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.
\v 8 Naye kuhani atamchunguza ilikuona kama huo upele umsambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\s5
\v 9 Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhan.
\v 10 Kuhani atamchunguza ili kuona kama kunauvimbe mweupe katika ngozi yake, endapo malaika zitakuwa zimebadilika kuwa nyeupe, au kumekuwa na nyama mbichi kwenye uvimbe.
\v 11 Kama ipo, basi, huo ni ugonjwa sugu wa ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga kwa kuwa yeye tayari ni najisi.
\s5
\v 12 Iwapo huo ugonjwa unajitokeza na kupanuka zaidi kwenye ngozi, na kuifunika ngozi ya mtu kwa ugonjwa tangu kichwani pake hata miguuni, maadamu anajitokeza kwa kuhani,
\v 13 naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo ugonjwa umeshaenea mwili wake wote. Ikiwa imetokeo hivyo, kuhani atamtangaza mtu huyo aliye na ugonjwa kuwa ni safi. Ikiwa amebadilika kuwa mweupe, huyo ni safi.
\v 14 Lakini ikiwa nyama mbichi imeonekana juu yake, atakuwa najisi.
\s5
\v 15 Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi na kumtanga kuwa najisi kwa sababu hiyo nyama mbichi ni najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\v 16 Lakini endapo hiyo nyama mbichi inageuka kuwa nyeupe tena, naye huyo mtu hana budi kwenda kwa kuhani.
\v 17 Kuhani atamchunguza ili kuona kama hiyo nyama imebadilika kuwa nyeupe. Kama imekuwa hivyo naye kuhani atatangaza kwamba mtu huyo kuwa ni safi.
\s5
\v 18 Mtu anapokuwa na jipu juu yangozi yake na limishapona,
\v 19 na mahali pa jipu pamekuwa na uvimbe au doa lenye kung'aa, wekundu unaochanganyikana na weupe, yapasa kuonyeshwa kwa kuhani.
\v 20 Naye kuhani atalichunguza ili kuona kama linaonekana limekwenda chini ya ngozi, na kama hizo malaika zimebadilika kuwa nyeupe, kama ni hivyo, kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza, endapo utakuwa umezalishwa mahali lilipokuwa jipu hilo.
\s5
\v 21 Lakini endapo kuhani atakuwa amelichunguza na haoni malaika nyeupe ndani yake, na kwamba iliko chini ya ngozi bali limefifia, kisha kuhani atamtenga kwa siku saba.
\v 22 Kama linaenea kwa kupanuka kwenye ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\v 23 Lakini kama hilo doa lenye kung'ara linabaki mahali pake na halijasambaa, basi hilo ni kovu la jipu, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
\s5
\v 24 Ngozi inapoungua na nyama mbichi ya inamekuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,
\v 25 kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\s5
\v 26 Lakini endapo kuahani analichunguza na naona kwamba hakuna malaika nyeupe kwenye doa, na kwamba halikuenda chini ya ngozi bali linafifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
\v 27 Kisha yapasa kuahani kumchunguza tena katika siku ya saba. Iwapo litakuwa limesambaa kwa upana kwenye ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugojwa wa kuambukiza.
\v 28 Iwapo hilo doa lisalia mahali pake na halitakuwa limesambaa kwenye ngozi bali limefifia, ni uvimbe tu kutokana na kuungua moto, naye kuhani atamtangaza kuwa safi, kwa kuwa siyo zaidi ya jeraha la kuungua.
\s5
\v 29 Iwapo mwanaume au mwanamke ana ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni pake,
\v 30 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo kwa ajili ya ugonjwa wa kuambukiza ili kuona kama unakwenda ndani zaidi ya ngozi, na kama kuna nywele za manjano, nyembamba ndani yake. endapo zinaonekana, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni mwasho, ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni.
\s5
\v 31 Iwapo kuhani anachunguza ugonjwa wa mwasho na anagundu kuwa hauko chini ya ngozi, na kama hakuna nywele nyeusi ndani yake, kisha kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
\s5
\v 32 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena huo ugonjwa ili kuona kama umesambaa, Endapo hakuna malaika za manjano, na iwapo ugonjwa uko usawa ngozi tu,
\v 33 basi, yapasa mtu huyo kunyolewa., lakini sehemu yenye ugonjwa haitanyolewa, naye kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
\s5
\v 34 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena ugonjwa ili kuona kama umacha kusambaa ndani ya ngozi. Iwapo unaonekana kuwa hukwenda chini zaidi ya ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa safi. Mtu huyo yapasa kufua nguo zake, na kisha atakuwa safi.
\s5
\v 35 Lakini ikiwa ugonjwa wa mwasho umeenea kwa sehemu kubwa kwenye ngozi baada ya kuhani kutangaza kuwa alikuwa safi,
\v 36 naye kuhani itabidi amchunguze tena. Iwapo ugonjwa utakuwa umesambaa katika ngozi, kuhani hahitajiki kutafuta nywele za manjano. Mtu huyo ni najisi.
\v 37 Lakini iwapo katika mtazamo wa kuhani inaonekana kuwa huo ugonjwa wa mwasho umekoma kusambaa, basi huo ugonjwa umekwisha pona. Yeye ni safi, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
\s5
\v 38 Iwapo mwanume au mwanamke ana madoa juu ya ngozi,
\v 39 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo ili kuona kama hayo madoa ni meupe kwa kufiifia, ambalo ni kovu tu lililojitokeza kwenye ngozi. Yeye yu safi.
\s5
\v 40 Iwapo nywele za mtu zimenyonyoka kichwani, yeye ni kipara lakini yu safi.
\v 41 Na iwapo nywele zake zimenyonyoka upande wa mbele wa kichwa chake, na iwapo paji lake la uso lina kipara, yeye yu safi.
\s5
\v 42 Lakini endapo kuna kidonda chenye wekundu uliochanganyika na weupe, juu ya kipara chake au paji lake la uso, huo ni ugonjwa wa kuambukiza uliojitokeza.
\v 43 Naye kuhani atamchunguza ili kuona iwapo uvimbe wa eneo linaugua juu ya upara wake au paji lake la uso lina wekundu uliochanganyika na weupe, kama kuonekana kwa ugonjwa wa kuambukiza kwenye ngozi.
\v 44 Ikionekana hivyo, basi huyo ana ugonjwa wa kuambukiza naye ni najisi. Hakika kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya ugonjwa wake kichwani pake.
\s5
\v 45 Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, 'Najisi, najisi.'
\v 46 Naye atakuwa najisi siku zote za ugonjwa wake wa kuambukiza. Kwa sababu anao ugonjwa unaosambaa, yapasa kuishi peke yake nje ya kambi.
\s5
\v 47 Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,
\v 48 au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi.
\v 49 Iwapo sehemu iliyochafuliwa ina rangi ya kijani au nyekundu katika vazi, ngozi, kifaa kilichosukwa au kufumwa, basi huo ni ukungu uanasambaa, ni lazima uonyeshwe kwa kuhani.
\s5
\v 50 Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.
\v 51 Naye atauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.
\v 52 Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilichoonekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.
\s5
\v 53 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa na kuona kwamba ukungu haujaenea kwenye vazi au chombo kilichosukwa au kusokotwa kutokana na sufu, kitani au ngozi,
\v 54 basi atawaagiza wakisafishe hicho kifaa kilichopatikana na ukungu, naye yampasa kukitenga kwa siku saba zaidi.
\v 55 Kisha kuhani atakichunguza tena hicho kifaa chenye ukungu baada ya kuwa kimesafinshwa. Kama ukungu haukubadilika rangi yake, hata kama haukusambaa, kifaa hicho ni najisi. Yapasa kichomwe, haijalishi ni wapi ukungu huo utakuwa umekichafua.
\s5
\v 56 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa, na kama ukungu umefifia baada ya kuwa umeoshwa, basi atakirarua kile kipande kilichochaufuliwa kutoka kwenye vazi au kutoka kwenye ngozi, au kutoka kwenye chombo kilichosukwa au kusokotwa.
\v 57 Ikiwa ukungu unazidi kuonekana katika vazi, ama katika chombo kilichosukwa au kufumwa, au katika kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, basi, ukungu utakuwa unasambaa. Kifaa chochote kilicho na ukungu ni lazima kichomwe.
\v 58 Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi.
\s5
\v 59 Hii ndiyo sheria ihusuyo ukungu katika vazi la sufu au kitani, au kwenye kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au kitu chochote kilichotengenewa kwa ngozi, ili kwamba mweze kuvitangaza kuwa safi au najisi.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Hii itakuwa sheria kwaajili ya mtu aliyekufa kwenye siku ya utakaso. Lazima aletwe kwa kuhani.
\s5
\v 3 Kuhani atakwenda nje ya kambi kumchunguza mtu kuona kama madhara ya ugonjwa wa ngozi yameponywa.
\v 4 Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
\v 5 Kuhani atamwamuru kuua moja ya hao ndege juu ya maji safi yaliyo kwenye chungu cha udongo.
\s5
\v 6 Ndipo kuhani atamchukua ndege aliyehai na mti wa mwerezi, na kitani nyekundu na hisopo, na vyote hivi, pamoja na ndege aliyehai atavichovya kwenye damu ya ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi.
\v 7 Ndipo kuhani atanyunyiza maji haya mara saba juu ya mtu anayetakaswa katika ugonjwa, na ndipo kuhani atamtangaza kuwa msafi. Ndipo kuhani atamwachia ndege aliyehai katika eneo wazi.
\s5
\v 8 Mtu aliyetakaswa atafua nguo zake, atanyoa nywele zake zote, ataoga kwa maji, na ndipo atakuwa safi. Baada ya hayo lazima aje kwenye kambi, lakini ataishi nje ya hema lake kwa siku saba.
\v 9 Katika siku ya saba lazima anyoe nywele za kichwa chake, na lazima pia anyoe ndevu zake na nyusi. Lazima anyoe nywele zake zote, na lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji; ndipo atakuwa safi.
\s5
\v 10 Katika siku ya nane lazima achukue dume wa wana kondoo wawili wasio na lawama, mwana kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na lawama, na tatu ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa mafuta kama sadaka ya nafaka, na kipimo kimoja cha mafuta.
\v 11 Kuhani ambaye amemtakasa mtu atamsimamisha mtu ambaye aliyemtakasa, pamoja na vile vitu, mbele ya Yahwe mahali pa kuingilia kwenye hema ya mkutano.
\s5
\v 12 Kuhani atachukua mmoja wa wanakondoo dume na kumtoa kama sadaka ya hatia, pamoja na kipimo cha mafuta; atavitikisa kwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Yahwe.
\v 13 Lazima aue mwana kondoo dume mahali ambapo wanapochinjia sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, katika eneo la hema, sababu sadaka ya dhambi ni ya kuhani, kama afanyavyo sadaka ya hatia, kwasababu ni takatifu zaidi.
\s5
\v 14 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu yule wa kutakaswa, katika dole gumba la kulia, katika dole la mguu wa kulia.
\v 15 Ndipo kuhani atachukua mafuta kutoka chombo na kuyamimina katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, na kuzamisha kidole chake katika mafuta hayo yaliyo kwenye mkono wa kushoto,
\v 16 na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.
\s5
\v 17 kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.
\v 18 Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwaajili yake mbele za Yahwe.
\s5
\v 19 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwaajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na badaye ataua sadaka ya kuchomwa.
\v 20 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.
\s5
\v 21 Kwa namna hiyo, kama mtu ni masikini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,
\v 22 pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.
\v 23 Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwaajili ya utakaso, pakuigilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.
\s5
\v 24 Kuhani atachukua mwana kondoo kwaajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.
\v 25 Atamuua mwana kondoo kwaajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.
\s5
\v 26 Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,
\v 27 na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.
\s5
\v 28 Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.
\v 29 Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe.
\s5
\v 30 Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -
\v 31 moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.
\v 32 Hii ni sheria kwaajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwaajili ya utakaso wake."
\s5
\v 33 Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
\v 34 "Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
\v 35 ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.' "
\s5
\v 36 Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Badaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.
\v 37 Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.
\v 38 Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyuma na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.
\s5
\v 39 Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.
\v 40 Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji.
\s5
\v 41 Yeye atataka kuta zote za ndani ya nyumba zikwanguliwe, na lazima achukue vitu vilivyochafuliwa na hivyo vilivyokwanguliwa nje ya mji na kuvitupa kwenye eneo lisilosafi.
\v 42 Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba.
\s5
\v 43 Kama ukungu unakuja tena na unaingia katika nyumba ambayo mawe yameondolewa na kuta zimekwanguliwa na kupigwa lipu upya,
\v 44 ndipo kuhani lazima aje aingie ndani na kuchunguza nyumba kuona kama ukungu umeenea ndani ya nyumba. Kama hivyo, huo ni ukungu mbaya, na nyumba ni najisi.
\s5
\v 45 Nyumba hiyo lazima iangushwe chini. Hayo mawe, mbao, na lipu yote ndani ya nyumba lazima vibebwe kupelekwa nje ya mji kwenye sehemu najisi.
\v 46 Kwa nyongeza, yeyote anaenda ndani ya nyumba wakati imefungwa atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 47 Na yeyote aliyelala ndani ya nyumba lazima afue nguo zake, na yeyote aliyekula ndani ya nyumba lazima afue nguo zake.
\s5
\v 48 Kama kuhani akaingia hiyo kuichunguza kuona ikiwa ukungu umeenea katika nyumba baada ya nyumba kupigwa lipu, ndipo, kama ukungu umetoweka, ataitangaza nyumba hiyo kuwa ni safi.
\s5
\v 49 Ndipo kuhani lazima achukue ndege wawili kuitakasa nyumba, na mti wa mwelezi, na sufu nyekundu, na hisopo.
\v 50 Atamuua ndege mmojawapo katika maji masafi kwenye dumu la udongo.
\v 51 Atachukua mti wa mwerezi, hisopo, sufu nyekundu na ndege aliyehai, na kuvichovya kwenye damu ya ndege aliyekufa, kwenye maji safi, na kunyunyizia nyumba mara saba.
\s5
\v 52 Ataitakasa nyumba kwa damu ya ndege na maji safi, pamoja na ndege aliyehai, mti wa mwerezi, hisopo, na sufu nyekundu. Lakini atamwachia ndege aliyehai aende nje ya mji mashambani.
\v 53 Kwa njia hii lazima afanye upatanisho kwaajili ya nyumba, na itakuwa safi.
\s5
\v 54 Hii ni sheria kwa aina zote za athari ya ugonjwa wa ngozi na vitu vyote vinavyosababisha ugonjwa kama huo, na kwaajili ya kuwashwa,
\v 55 na kwa ukungu kwenye mavazi na nyumba,
\v 56 kwaajili ya uvimbe, kwaajili ya vipele, madoa,
\v 57 kutambua wakati wowote tatizo hili ni najisi au lini limetakaswa. Hii ni sheria kwaajili ya athari za ugonjwa wa ukungu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
\v 2 "Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, 'Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi.
\v 3 Unajisi wake unatokana na athari ya kisonono. Iwe mwili wake unatoa ugiligili au umekoma, huo ni unajisi."
\s5
\v 4 Kitanda chochote anachokilalia kitakuwa najisi, na kila kitu ambacho anakaa juu yake kitakuwa najisi.
\v 5 Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na awe amenajisika mpaka jioni.
\s5
\v 6 Yeyote anayekaa katika kitu chochote ambacho mtu ambaye ameathiriwa na kisonono alikaa, mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 7 Na yeyote anayegusa mwili wa ambaye ameathirika na kisonono lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na awe najisi hadi jioni.
\s5
\v 8 Kama mtu ambaye anaona majimaji kama hayo kwa mtu fulani ambaye ametakasika, ndipo mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na atakuwa najisi hata jioni.
\v 9 Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.
\s5
\v 10 Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.
\v 11 Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 12 Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.
\s5
\v 13 Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwaajili yake siku saba kwaajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.
\v 14 Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
\v 15 Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.
\s5
\v 16 Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.
\v 17 Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazama paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.
\v 18 Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.
\s5
\v 19 Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 20 Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
\s5
\v 21 Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 22 Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
\v 23 Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
\s5
\v 24 Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
\s5
\v 25 Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.
\v 26 Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.
\v 27 Na yeyote anayegusa kitu kati ya vitu hivyo atakuwa najisi; lazima yeye afue nguo zake na aoge mwenyewe kwenye maji, na atakuwa amenajisika mpaka jioni.
\s5
\v 28 Lakini kama mwanamke ametakasika katika kutokwa na damu, ndipo atahesabu kwaajili yake siku saba, baada ya hizo atakuwa safi.
\v 29 Katika siku ya nane atachukua kwake njiwa wawili au kinda wawili wa njiwa na atawaleta kwa kuhani pakuingilia hema ya mkutano.
\v 30 Huyo kuhani atatoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa, na atafanya upatanisho kwaajili ya huyo mbele ya Yahwe kwaajili unajisi wa mwanamke atokwaye damu.
\s5
\v 31 Hivi ndivyo lazima uwatenge watu wa Israeli katika unajisi wao, hivyo hawatakufa tokana na unajisi wao, kwa kuchafua hema langu, ambapo naishi kati yao.
\s5
\v 32 Huu ndio utaratibu kwa kila ambaye anakisonono, kwaajili kila mwanaume ambaye shahawa yake inatoka na inamfanya kuwa najisi,
\v 33 kwaajili ya mwanamke ambaye yuko katika kipindi cha hedhi, kwaajili ya yeyote aliye na kisonono, awe mwanaume au mwanamke, na kwaajili ya yeyote anayelala na mwanamke najisi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa - hii ni baada vifo vya wana wawili wa Haruni, walipomkaribia Yahwe na ndipo wakafa.
\v 2 Yahwe alimwambia Musa, "Ongea na Haruni kaka yako na umwambie hapana kuja tu wakati wowote katika patakatifu pa patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kifuniko cha upatanisho kilicho juu ya sanduku. Akifanya hivyo, anakufa, kwasababu naonekana katika wingu juu ya kifuniko cha upatanisho.
\s5
\v 3 Hivi ndivyo jinsi Haruni lazima aje katika patakatifu pa patakatifu. Yeye lazima aingie pamoja na ndama kama sadaka ya dhambi, na kondoo dume kama sadaka ya dhambi.
\v 4 Ni lazima avae kanzu ya kitatani, na lazima avae ndani yake nguo ya kitani, na lazima avae mshipi wa kitani na kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu. Lazima aoge mwili wake katika maji na avae mavazi haya.
\v 5 Lazima achukue kwenye umati wa watu wa Israeli mbuzi wawili waume kama sadaka ya dhambi na kondoo dume moja ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa.
\s5
\v 6 Ndipo Haruni lazima alete ng'ombe kama sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwaajili yake mwenyewe, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na familia yake.
\v 7 Ndipo lazima achukue mbuzi wawili na kuwaweka mbele ya Yahwe katika mlango wa kuingilia kwenye hema ya mkutano.
\s5
\v 8 Ndipo Haruni lazima apige kura kwaajili ya mbuzi hao wawili, kura moja kwaajili ya Yahwe, na kura nyingine kwaajili ya msingiziwa.
\v 9 Ndipo Haruni lazima awasilishe mbuzi ambaye kura imeangukia kwa Yahwe, na kumtoa mbuzi huyo kama sadaka ya dhambi.
\v 10 Lakini mbuzi ambaye kura ya usingiziwa imemwangukia lazima aletwe kwa Yahwe akiwa hai, kufanya upatanisho kwa kumwachia aende porini kama, mbuzimsingiziwa.
\s5
\v 11 Pia Haruni lazima alete ng'ombe kwaajili ya sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwaajili yake mwenyewe, lazima afanye upatanisho kwaajili yake mwenyewe na familia yake, hivyo lazima yeye amuue huyo ng'ombe kama sadaka ya dhambi kwaajili yake mwenyewe.
\s5
\v 12 Haruni lazima achukue chetezo iliyojaa mkaa wa moto kutoka kwenye madhabahu mbele ya Yahwe, na mikono imejaa ubani mzuri, na kuleta vitu hivi ndani ya pazia.
\v 13 Hapo lazima aweke ubani juu ya moto mbele za Yahwe ili kwamba wingu kutoka kwenye ubani liweze kufunika kifuniko cha agano la imani ya upatanisho. Yeye afanye hivyo ili kwamba asife.
\s5
\v 14 Ndipo lazima achukue kiasi cha damu ya ng'ombe na kuinyunyiza kwa kidole chake mbele ya kifuniko cha upatanisho. Lazima anyunyize kiasi cha damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kifuniko cha upatanisho.
\s5
\v 15 Ndipo lazima aue mbuzi kwaajili ya sadaka ya dhambi ambayo ni kwaajili ya watu na kuileta damu yake ndani kwenye pazi. Hapo lazima aifanyie damu kama alivyofanya kwenye damu ya fahali: lazima ainyunyize juu ya kifuniko cha upatanisho na mbele ya kifunuko cha upatanisho.
\v 16 Yeye lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu kwa sababu ya matendo ya unajisi ya watu wa Israeli, na kwa sababu ya uasi na dhambi zao zote. Yeye pia lazima afanye haya kwaajili ya hema ya mkutano, ambapo Yahwe anaishi kati yao, katika uwepo wa matendo yao ya unajisi.
\s5
\v 17 Hakuna mtu anayetakiwa kuwepo katika hema ya mkutano wakati Haruni anaingia kufanya upatanisho katika mahali patakatifu pa patakatifu, na mpaka atoke nje na amemaliza kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya familia yake, na kwaajili umati wa Israeli.
\v 18 Yeye lazima aende nje kwenye madhabahu hapo mbele za Yahwe na kufanya upatanisho kwaajili ya hiyo, na lazima achukue kiasi cha damu ya mbuzi na kuiweka juu ya pembe za madhabahu yote kuzunguka.
\v 19 Anatakiwa anyunyize kiasi cha damu juu yake kwa kidole chake mara saba kuitakasa na kuitenga maalumu kwa Yahwe, mbali kutoka matendo ya unajisi wa watu wa Israeli.
\s5
\v 20 Atakapo maliza kupatanisha kwaajili ya mahali patakatifu sana, hema la mkutano, na madhabahu, lazima amlete mbuzi aliyehai.
\v 21 Haruni lazima aweke mikono yake yote juu ya kichwa cha mbuzi huyu aliyehai na akiri juu yake maovu yote ya watu wa Israeli, uasi wao wote, dhambi zao zote. Ndipo lazima aweke dhambi hizo juu ya kichwa cha mbuzi na amwachie katika uangalizi wa mtu aliyetari kumwongoza mbuzi huyo porini.
\v 22 Mbuzi lazima abebe juu yake mwenyewe uovu wote kwenda mahali pakiwa. Kule msituni, huyo mtu amwache mbuzi aende huru.
\s5
\v 23 Ndipo Haruni anapaswa kwenda tena humo kwenye hema ya mkutano na kuvua mavazi ya kitani ambayo amayavaa kabla hajaenda mahali patakatifu sana, na anatakiwa kuyaacha mavazi hayo pale.
\v 24 Anapaswa aoshe mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na avae nguo zake za kawaida; pia lazima atoke nje kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa kwaajili ya wale watu, na kwa njia hii anafanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya watu.
\s5
\v 25 Lazima yeye achome mafuta ya sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.
\v 26 Huyu mtu anayemwacha mbuzi msingiziwa aende huru anafua nguo zake na kuosha mwili wake katika maji; baada ya hayo, anaweza kurudi tena kambini.
\s5
\v 27 Yule fahali kwaajili ya sadaka ya dhambi na mbuzi kwaajili ya sadaka za dhambi, ambaye damu yake ililetwa kufanya upatanisho katika mahali patakatifu, lazima ipelekwe nje ya kambi. kule lazima wachome, ngozi zao, nyama yao na kinyesi chao.
\v 28 Huyu anayechoma sehemu hizo lazima afue nguo zake na aoge mwili wake katika maji; baada ya hapo, anaweza kurudi tena kwenye kambi.
\s5
\v 29 Hii itakuwa sharti kwaajili yenu kwamba katika mwezi wa saba, kwenye siku ya kumi ya mwezi, mtanyenyekea wenyewe na msifanye kazi, iwe mwenyeji wa kuzaliwa au mgeni anayeishi kati yenu.
\v 30 Hii ni kwasababu katika siku hii ya upatanisho utafanywa kwaajili yenu, kuwatakasa ninyi kutoka dhambi zenu zote ili mwe safi mbele za Yahwe.
\v 31 Hii ni maalumu kwa Sabato ya kupumzika kwaajili yenu, na lazima mnyenyekee wenyewe na msifanye kazi. Hili litakuwa sharti kati yenu.
\s5
\v 32 Kuhani mkuu, ambaye atapakwa mafuta na kuwekwa wakfu kuwa kuhani mkuu katika nafasi ya baba yake, lazima afanye upatanisho huu na kuvaa mavazi ya kitani, hayo ni mavazi matakatifu.
\v 33 Lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu sana; lazima afanye upatanisho kwaajili ya hema ya mkutano na madhabahu, na lazima afanye upatanisho kwaajili ya makuhani na kwaajili ya kusanyiko la watu.
\s5
\v 34 Hii daima itakuwa sharti kwaajili yako, kufanya upatanisho kwaajili ya watu wa Israeli kwasababu ya dhambi zao zote, mara moja kwa kila mwaka." Na ilikuwa ikifanika kama Yahwe alivyomwamuru Musa.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa,
\v 2 "Zungumza na Aroni na wanawe, na watu wote wa Israeli. Waambie mambo ambayo ameamru Yahweh:
\v 3 Mtu yeyote wa Isreli anayeua fahali au mwana—kondoo au mbuzi kambini, au amuuaye nje ya kambi, ili kumtoa dhabihu—
\v 4 kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahweh mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mabali kutoka miongoni mwa watu wake.
\s5
\v 5 Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.
\v 6 Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahweh.
\s5
\v 7 Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
\s5
\v 8 Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
\v 9 na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
\s5
\v 10 Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
\v 11 Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai
\s5
\v 12 Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.
\v 13 Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi.
\s5
\v 14 Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyeote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
\s5
\v 15 Mtu yeyote alaye mnyama aliyekufa au ambaye amelaruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.
\v 16 Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake".
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 3 Msitende mambo ambayo watu wa Misri huyatenda, mahali mlikokuwa mkiishi awali. Na ni lazima msitende mambo yale wanayoyatenda watu wa Kanaani, nchi ambayo ninawapeleka nyinyi. Msifuate desturi zao.
\s5
\v 4 Sheria zangu ndizo mtakazozitenda, na amri zangu ndizo mtakazozishika, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 5 Kwa hiyo ni lazima mzitunze hukumu zangu na sheria zangu. Ikiwa mtu amezitii, ataishi kwa sababu ya hizo. Mimi Ndimi Yahweh.
\s5
\v 6 Pasiwepo kwenu atakayelala na yeyote aliye na uhusiano wa karibu naye. Mimi ndimi Yahweh.
\v 7 Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye.
\v 8 Usilale na yeyote wa wake za baba yako; Usimfedheheshe namna hiyo baba yako.
\s5
\v 9 Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.
\v 10 Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.
\v 11 Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.
\s5
\v 12 Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.
\v 13 Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.
\v 14 Usimfedheheshe ndug wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.
\s5
\v 15 Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
\v 16 Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
\s5
\v 17 Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
\v 18 Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
\s5
\v 19 Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
\v 20 Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
\s5
\v 21 Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 22 Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
\v 23 Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
\s5
\v 24 Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
\v 25 Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
\s5
\v 26 Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
\v 27 Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
\v 28 Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
\s5
\v 29 Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.
\v 30 Kw a hiyo inawapasa kuzishika amri zangu na sitende mojawapo ya desturi hizi zenyekuchukiza ambazo zilitendwa hapo kabla yenu, ili msijinajisi wenyewe kwa hizo. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema.
\v 2 Zungumza na kusanyiko lote la watu wa Israeli na uwaambie, 'Ni lazima muwe watakatifu, kwa kuwa mimi Yahweh Mungu wenu ni mtakatifu.
\v 3 Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 4 Msizigeukie sanamu zisizo na thamani, wala kujitengenezea wenyewe miungu kutokana na chuma. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 5 Unapotoa dhabihu za sadaka ya ushirika kwa Yahweh, utatoa ili kupata kibali.
\v 6 Ni sharti iliwe siku hiyo hiyo uliyoitoa, au siku inayofuata.
\v 7 Kama kinabaki kitu cho chote hata siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. Kama kitaliwa katika siku ya tatu kitakuwa najisi. Hakitakubalika,
\v 8 lakini kila akilaye ni lazima atachukua hatia yake kwa sababu amekivunjia heshima kilicho kitakatifu kwa Yahweh. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
\s5
\v 9 Unapovuna mavuno ya ardhi yako, usivune hata pembezo mwa shamba lako kabisa, wala hutakusanya mabaki ya mavuno yako yote.
\v 10 Usikusanye kila zabibu kutoka katika mizabibu yako, wala usiziokote dhabibu zilizoanguka chini katika shamba la mizabibu. Ni lazima uziache kwa ajili ya masikini na kwa ajili ya wageni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 11 Usiibe. Usiseme uongo. Msidanganyane.
\v 12 Usiape kwa jina langu kwa uongo na kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh
\s5
\v 13 Usimgandamize jirani yako wala kumwibia. Usishikilie malipo ya kibarua usiku kucha hata asubuhi.
\v 14 Usimlaani kiziwi au kuweka kikwazo mbele ya kipofu. Badala yake, yakupasa umwogope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 15 Usisababishe hukumu ikawa ya uongo. Usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni masikini na usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni mtu muhimu. Badala yake, amua juu ya jirani yako kwa haki.
\v 16 Usiende huku na huko ukisema habari za uchochezi miongoni mwa watu wako, bali tafuta kuyalinda maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Mkemee jirani yako kwa heshima ili kwamba usishiriki katika dhambi kwa sababu yake.
\v 18 Usijilipize kisasi au kuwa na chuki yoyote dhidi ya mtu yeyote wa watu wako, lakini badala yake mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 19 Shika amri zangu. Usiwazalishe wanyama wako kwa kutumia wanyama wa aina nyingine tofauti. Usichanganye aina mbili tofauti za mbegu unapopanda shamba lako. Usivae vazi lililofumwa kwa kutumia nyuzi za rangi mbili tofauti zilizochanganywa pamoja.
\s5
\v 20 Yeyote anayelala na msichana mtumwa aliyeposwa na mume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa au hajaachwa huru, lazima waadhibiwe. Hawatauawa kwa sababu yule msichana hakuwa huru.
\v 21 Ni lazima mtu huyo alete sadaka yake ya hatia kwenye ingilio la hema la kukutania—kondoo dume iwe sadaka ya hatia.
\v 22 Kisha kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kandoo dume mbele za Yahweh kutokana na dhambi aliyoitenda. Nayo dhambi iliyotendwa itasamehewa.
\s5
\v 23 Mtakapoingia katika nchi na kupanda aina zote za miti kwa chakula, kisha mtayahesabu matunda yatakayozaliwa kuwa yamekatazwa kuliwa. Tunda litakatazwa kwako kwa miaka mitatu. Halitaliwa.
\v 24 Lakini katika mwaka wa nne matunda yote yatakuwa matakatiifu, matoleo ya sifa kwa Yahweh.
\v 25 Katika mwaka wa tano unaweza kula tunda, ambalo umelisubiri ili kwamba mti uweze kuzaa zaidi. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 26 Usile nyama yoyote amabayo damu ingalimo ndani yake. Usiulize kwa roho juu ya wakati ujao,
\v 27 Usitafute kuwadhibiti wengine kwa njia ya nguvu za kichawi. Msifuate tabia za kipagani kama vile kunyoa denge au kunyoa pembe za ndevu zeu.
\v 28 Usiukate mwili wako kwa ajili ya wafu au kuchanja chale juu ya mwili wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 29 Usimwaibishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo taifa litaangukia kwenye ukahaba na nchi itajawa na uovu.
\v 30 Utazitunza Sabato zangu na kupaheshimu mahali patakatifu pa hema langu la kukutania. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 31 Msiwageukie wale wanaoongea na wafu au roho wachafu. msiwatafute, la sivyo watawanajisi ninyi, Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 32 Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwegope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 33 Mgeni anapoishi miongoni mwenu katika nchi yanu, usimtendee lolote lililobaya.
\v 34 Mgeni anayeishi pamoja nanyi ni lazima awe kama mwenyeji Mwisraeli mzaliwa anayeishi kwenu, na sharti umpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe, ni kwa sababu wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 35 Unapopima urefu, uzito, au wingi usitumie vipimo vya udanganyifu.
\v 36 Tumia mizani iliyo halali, mawe ya kupimia uzito yaliyo halali, efa halali, hini iliyo halali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya utumwa ya Misri.
\v 37 Utayatii maagizo yangu na sheria zangu zote na kuzitenda. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
\v 2 "Waambie watu wa Waisraeli, 'mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe.
\s5
\v 3 Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu.
\v 4 Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake,
\v 5 Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki.
\s5
\v 6 Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au na wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
\v 7 Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 8 Mtazitunza amari zangu na kuzifuta. Mimi ndimi Yahweh anayewatenga ninyi muwe watakatifu.
\v 9 Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa.
\s5
\v 10 Mwanaume yeyote afanyaye uzinzi na mke wa mwanaume mwingine, yaani, yeyote anayezini na mke wa jirani yake—yule mwanaume mzinzi na mwanamke mzinzi ni lazima wote wawili wauawe.
\v 11 Mwanaume yeyote anayelala na mke wa baba yake ili kukutana naye kimwili amemfedhehesha baba yake mwenye. Wote wawili; mwana huyo na mke huyo wa baba yake kwa hakika watauawa. wanahatia na wanastahili kufa.
\v 12 Kama mwanaume atalala na mke wa mwanawe, wote wawili; mwanaume huyo na mke huyo wa mwanawe hakika watauawa. Wametenda upotovu. Wana hatia na wanastahili kufa.
\s5
\v 13 Kama mwanaume analala na mwanaume mwingine kama alalavyo na mwanamke, wote wawili watakuwa wamefanya jambo lililo ovu. Hakika watauawa. Wana hatia na wanastahili kufa.
\v 14 Ikiwa mwanaume atamwoa mwanamke na pia akamwoa mama wa mwanamke huyo, huu ni uovu. Ni lazima wachomwe kwa moto, wote wawili, mwanaume huyo na manamke huyo, ili kwamba hapatakuwepo na uovu miongoni mwenu.
\s5
\v 15 Ikiwa mwanaume analala na mnyama, hakika atauawa, ni lazima mumuue na mnyama huyo pia.
\v 16 Ikiwa mwanamke anamkaribia mnyama ili kulala naye, ni lazima mmuuwe mwanamke huyo pamoja na mnyama. Kwa hakika ni lazima wauawe. wana hatia na wanastahili kufa.
\s5
\v 17 Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake.
\v 18 Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lizima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao.
\s5
\v 19 Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe.
\v 20 Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.
\v 21 Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.
\s5
\v 22 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.
\v 23 Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao.
\s5
\v 24 Nami nikawaambia ninyi, "Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo amaziwa na asali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine.
\v 25 Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanya najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi.
\s5
\v 26 Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahweh, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu.
\s5
\v 27 Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa, "Zungumza na makuhani, wana wa Aroni, nawe waambie, 'hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakayejitia unajisi kwa wale wanaokufa miongoni mwa watu wake,
\v 2 isipokuwa yule aliye ndugu wa karibu—mama yake, baba yake, mwanawe, bintiye, nduguye,
\v 3 au dada yake bikira anayemtegemea, kwa kuwa hana mume—kwake huyo anaweza kujitia unajisi.
\s5
\v 4 Lakini hatajitia unajisi na kujichafu kwa ajili ya jamaa wengine.
\v 5 Makuhanai hawatanyoa vichwa vyo wala kunyoa pembeni mwa ndevu zao, wala hawatachanja chale miili yao.
\v 6 Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala hawataliaibisha jina la Mungu wao, kwa sababu makuhani hutoa sadaka ya Yahweh ya chakula, mkate wa Mungu wao. Kwa hiyo makuhani lazima wawe watakatifu.
\s5
\v 7 Hawataoa mwanamke aliye kahaba na aliyetiwa unajisi, na hawataoa mwanamke aliyetalikiwa kutoka kwa mume wake kwa sababu wametengwa kwa ajili ya Mungu wao.
\v 8 Utamtenga kwa sababu yeye ndiye anayetoa mkate kwa Mungu wako. Ni lazima awe mtakatifu, kwa sababu—Mimi, Yahweh, ndimi niwatakasaye nyinyi—pia Mimi mwenyewe ni mtakatifu.
\v 9 Binti yeyote wa kuhani anayejitia unajisi kwa kujifanya kahaba anajifedhehesha mwenyewe. Ni lazima ateketezwe kwa moto.
\s5
\v 10 Mtu ambaye ni kuhani mkuu miongoni mwa nduguze, ambaye mafuta ya upako yamekwisha kumiminwa kichwani pake, na ambaye amekwisha kuwekwa wakfu ili kuvaa mavazi maalum ya kuhani mkuu, kamwe hataziacha wazi nywele zake wala hatazirarua nguo zake.
\v 11 Hataingia kamwe mahali popote ambapo kuna maiti na kujitia unajisi, hata kama ni maiti ya baba yake au ya mama yake.
\v 12 Kuhani mkuu hataondoka eneo takatifu la hema la kukutania au kupatia unajisi patakatifu pa Mungu wake, kwa sababu amewekwa wakfu kuwa kuhani mkuu kwa kutiwa mafuta ya upako ya Mungu wake. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 13 Kuhani mkuu nilazima aoe bikira kuwa mke wake.
\v 14 Hataoa mjene, mwanamke mtalaka au mwanamke aliye kahaba. Anaweza kuoa mwanamke bikira kutoka kwa watu wake,
\v 15 kwa hiyo asiwatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. kwa kuwa Mimi Yahweh, ndimi ninayemfanya yeye mtakatifu."
\s5
\v 16 Yahweh akamwambia Musa, akasema,
\v 17 Zungumza na Aroni na umwambie, 'mtu yeyote wa ukoo wako katika vizazi vyako vyote mwenye kasoro mwilini mwake, asisogee kutoa chakula kwa Mungu wake.
\s5
\v 18 Mtu yeyote mwenye kasoro mwilini mwake asimkaribie Yahweh,
\v 19 mtu kama vile: kipofu au mtu asiyeweza kutembea, mtu aliyeharibiwa uso au kupungukiwa na viungo mwilini, mtu aliye na mguu au mkono wenye ulemavu,
\v 20 mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.
\v 21 Hakutakuwa na mtu miongoni mwa ukoo wa Aroni kuhani mkuu mwenye kasoro mwilini atakayekaribia kutoa matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh. Mtu kama huyo mwenye kasoro mwilini hatakaribia ili kutoa mkate wa Mungu wake.
\s5
\v 22 Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu.
\v 23 Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh anayewafanya watakatifu."
\v 24 Kwa hiyo Musa akamwambia maneno haya Aroni, wanawe, na watu wote wa Israeli.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, kusema,
\v 2 "Ongea na Aroni na wanawe, waambie wajiepushe na vitu vitakatifu vya watu wa Israeli wanavyovitenga kwangu. Wasilinajisi jina langu. Mimi ndimi Yahweh.
\v 3 Waambie, 'Ikiwa mmoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote anakaribia vitu vitakatiifu vile ambavyo watu wa Israeli wamevitenga kwa Yahweh, wakati akiwa najisi, sharti mtu huyo akatiliwe mbali atoke mbele zangu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 4 Hatakuwapo yeyote wa uzao wa Aroni aliye na ungonjwa wa ngozi wa kuambukiza, au maambukizi yatirirkayo kutoka mwilini mwake, atakayekula sehemu yoyote ya dhabihu inatolewayo kwa Yahweh mpaka atakapotakasika. Yeyote agusaye kitu chochote kilichonajisi kwa njia ya kugusa maiti, au kwa kumgusa mtu yeyote aliyetokwa na shahawa,
\v 5 au yeyote agusaye mnyama atakayemtia unajisi, au mtu yeyote atakayemfanya najisi, kwa hiyo unajisi wowote unaweza kuwa—
\v 6 kuhani yeyote agusaye kitu chochote kisichosafi atakuwa najisi hata jioni. Hatakula chochote cha vitu vitakatifu, isipokuwa ameuosha mwili wake katika maji.
\s5
\v 7 Jua linapotua, ndipo atakuwa safi. Baada ya machweo anaweza kula kutoka katika vitu vitakatifu, kwasababu hivyo ni vyakuala vyake.
\v 8 Asile mzoga wowote uliookotwa au mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori, ambaye kwake atajitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh.
\v 9 Ni lazima makuhani wafuate maagizo yangu, ama sivyo watakuwa na hatia ya dhambi na wangeweza kufa kwa kunitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh ninayewafanya wao watakatifu.
\s5
\v 10 Hakuna mtu kutoka nje ya familia ya kuahani, wakiwemo wageni wa kuhani au watumwa wake wa kuajiliwa, atakayeweza kula kitu chochote kilicho kitakatifu.
\v 11 Lakini kama huyo kuhani amenunua mtumwa kwa fedha yake mwenyewe, mtumwa huyo anaweza kula kutoka katika vitu vilivyotengwa kwa Yahweh. Na watu wa familia ya kuhani na watumwa waliozaliwa nyumbani mwake, pia wanaweza kula pamoja naye kutoka katika vitu hivyo.
\s5
\v 12 Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, hataweza kula chochote cha mchango wa matoleo matakatifu.
\v 13 Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi knyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani anatakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.
\s5
\v 14 Kama mtu anakula chakula kitakatifu bila ya kukijua, naye atamlipa kuahani kwa ajili ya hicho; itampasa kuongeza moja ya tano juu yake na kukirejesha kwa kuhani.
\v 15 Haiwapasi watu wa Israeli kutoheshimu vitu vitakatifu ambavyo vimeinuliwa juu na kuletwa kwa Yahweh,
\v 16 kisha wakajisababishia wenyewe kuchukua dhambi amabyo ingewafanya kuwa na hatia ya kula chakula kitakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Yahweh awafanyaye wao watakatifu."
\s5
\v 17 Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
\v 18 "Sema na Aroni na wanawe, na kwa watu wa Israeli wote. Waambie, Mwisraeli yeyote, au Mgeni anayeishi katika Israeli, waletapo dhabihu—iwe ni kutimiza kiapo, au iwe ni sadaka ya hiari, au wanaleta kwa Yahweh sadaka ya kuteketezwa kwa moto,
\v 19 ikiwa wanataka ikubalike, ni lazima watowe mnyama dume asiye na dosari, kutoka kwenye kundi la ng'ombe, kondoo au mbuzi
\s5
\v 20 Lakini hamtatoa chochote kilicho na dosari. Sitakipokea kwa niaba yenu.
\v 21 Yeyote atoae dhabihu ya sadaka ya ushirika kutoka katika kundi la ng'ombe au la kondoo kwa Yahweh ili kutimiza kiapo, au kama sadaka ya hiari, ili ikubalike, ni lazima isiwe na kilema. Ni lazima pasiweko na kasoro katika mnyama.
\s5
\v 22 Msitoe kabisa wanyama waliovipofu, waliojeruhiwa, wala walio na kilema, wenye upele, vidonda vitokavyo usaha, wala wenye vigaga. Msiwatoe hawa kuwa dhabihu ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Yahweh juu ya madhabahu.
\v 23 Unaweza kumleta makisai au mwana-kondoo mlemavu au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini sadaka kama hiyo kwa ajili kutimiza kiapo, haitapokelewa.
\s5
\v 24 Usitoe kwa Yahweh mnyama yeyote aliyetiwa jeraha, kupondwa, au kukatwa korodani zake.
\v 25 Usifanye haya katika nchi yako. Usilete mkate wa Mungu wako kutoka mkononi mwa mgeni. Hao wanyama wenye vilema na dosari ndani yao, hawatapokelewa kabisa kwa ajili yako.
\s5
\v 26 Yahweh akamwambia Musa na akasema,
\v 27 "Wakati ndama, mwana—kondo au mwana—mbuzi azaliwapo, sharti abaki na mama yake kwa muda wa siku saba. Ndipo kuanzia siku ya nane na kuendelea, anaweza kupokelewa kuwa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh.
\s5
\v 28 Usimchinje ng'ombe jike pamoja na ndama wake au mbuzi jike pamoja na kitoto chake kwa siku moja.
\v 29 Utoapo sadaka ya shukrani kwa Yahweh utaitoa kwa njia iliyokubalika.
\v 30 Ni lazima iliwe siku iyo hiyo inayotolewa. Hutakiwi kubakiza chochote hata asubuhi. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 31 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Yahweh.
\v 32 Msiliabishe jina langu takatifu. Ni lazima nitambuliwe kuwa ni mtakatifu na watu wa Israeli. Mimi ndimi Yahweh niwafanyaye ninyi watakatifu,
\v 33 ambaye amewaleta kutoka katika nchi ya Misri ili niwe Mungu wenu: Mimi ndimi Yahweh."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa:
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli, na uwaambie, 'Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo ni lazima mzitangaze kuwa makusanyiko matakatifu, ni sikukuu zangu za mara kwa mara.
\s5
\v 3 Mnaweza kufanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika kabisa. Usifanye kazi kwa sababu ni Sabato kwa ajili ya Yahweh mahali pote mnaposhi.
\s5
\v 4 Hizi ndizo sikukuu za Yahweh zilizoamriwa, Makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilioamriwa:
\v 5 Katika mwenzi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi kwenye mwanga hafifu wa machweo ya jua, ni Pasaka ya Yahweh.
\v 6 Siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu ya mikate isiotiwa hamira kwa ajili ya Yahweh. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiotiwa hamira.
\s5
\v 7 Siku ya kwanza ni lazima mjitenge kwa pamoja, hamtafanya kazi ya kawaida.
\v 8 Kwa siku saba mtamletea Yahweh matoleo ya chakula. Siku ya saba ni ya kusanyiko takatifu lililotengwa kwa ajili ya Yahweh, nanyi katika siku hiyo hamtafanya kazi yoyote ya kawaida."
\s5
\v 9 Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 10 "Sema na watu wa Israeli uwaambie, 'mtakapika kwenye nchi nitakayowapa nyinyi, na mtakapovuna mazao yake, nanyi yawapasa kumletea kuhani fungu la masuke ya nafaka ya matunda yake ya kwanza.
\v 11 Naye ataliinua hilo fungu la masuke ya nafaka mbele za Yahweh na kulileta kwake, kwa kuwa litakubalika kwa niaba yenu. Nalo litaletwa siku baada ya Sabato ili kwamba kuhani ataliinua na kulileta kwangu.
\s5
\v 12 Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh.
\v 13 Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahweh, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.
\v 14 Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.
\s5
\v 15 Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lie fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.
\v 16 Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahweh.
\s5
\v 17 Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh.
\v 18 Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.
\s5
\v 19 Ni lazima mtowe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.
\v 20 Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahweh na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahweh kwa ajili ya kuhani.
\v 21 Mtatoa tangazo siku iyo hiyo. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
\s5
\v 22 Mtakapovuna mazao ya nchi yenu, Msivune kabisa kabisa pembeni mwa mashamba yenu, wala msivune mazazo ya mavuno yenu. Inawapasa kuyaacha kwa ajili ya masikini na mgeni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu."
\s5
\v 23 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 24 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza itakuwa siku ya pumzika makini kwa ajili yenu, kumbukumbu pamoja na kupigwa kwa tarumbeta na kusanyiko takatifu,
\v 25 Hamtafanya kazi ya kawaida, na ni lazima mtoe dhabihu inayofanywa kwa moto kwa Yahweh."
\s5
\v 26 Kisha Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 27 "Sasa, siku ya kumi ya mwezi huu wa saba, ni Siku ya Upatanisho. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na ni lazima mjinyenyekeze na kuleta kwa Yahweh matoleo kwa moto.
\s5
\v 28 Hamtafanya kazi katika siku hiyo kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Yahweh Mungu wenu.
\v 29 Yeyote asiyejinyenyekeza siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
\s5
\v 30 Yeye afanyaye kazi yoyote katika siku hiyo, Mimi, Yahweh, nitamwangamiza atoke miongoni mwa watu wake.
\v 31 Msifanye kazi ya aina yoyote katika siku hiyo. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
\v 32 Siku hii itakuwa Sabato ya pumziko lenye utlivu, na ni lzima siku ya tisa ya mwezi mjinyenyekeze katika majira ya jioni. Tangu jioni hata jioni mtaishika Sabato yenu."
\s5
\v 33 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 34 "Zungumza na watu ISraeli, uwaambie 'Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahweh. nayo itadumu siku saba.
\s5
\v 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi ya kawaida.
\v 36 Kwa muda wa siku saba mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu, nanyi mtato dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Hili ni kusanyiko lenye utulivu, nanyi msifanye kazi yoyote ya kawaida.
\s5
\v 37 Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo mnapaswa kuzitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu ya kutoa dhabihu kwa moto kwa Yahweh, matoleo ya kuteketezwa na matoleo ya nafaka, dhabihu na matoleo ya vinywaji, kila moja kwa siku yake.
\v 38 Sikukuu hizi zitakuwa nyongeza kwa Sabato za Yahweh na zawadi zenu, viapo vyenu vyote, na sadaka zenu zote za hiari mzitoazo kwa Yahweh.
\s5
\v 39 Kuhusu Sikukuu ya vibanda, siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmeyakusanya ndani matunda ya nchi, ni lazima muitunze sikukuu hii ya Yehweh kwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza itakuwa ya pumziko lenye utulivu, na siku ya nane pia itakuwa ya pumziko lenye utulivu.
\s5
\v 40 Siku ya kwanza mtachuma tunda lililobora kutoka kwenye miti, mtakata makuti ya mtende, na matawi ya miti minene yenye majani mengi, na majani ya mierebi kutoka chemchemi za maji, nanyi mtashangilia mbele za Yahweh Mungu wenu kwa siku saba.
\v 41 Kwa muda wa siku saba kila mwaka, mtaisherehekea sikukuu hii kwa Yahweh. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali potepote mtakapoishi. Mtaisherehekea sikukuu hii katika mwezi wa saba.
\s5
\v 42 Mtaishi kwenye vibanda vidogovidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogovidogo kwa siku saba,
\v 43 ili kwamba wazao wenu, kizazi baada ya kizazi, waweze kujifunza nilivyowafanya wana wa Israeli kuishi kwenye vibanda kama hivi nilipowaongoza kutoka katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.'"
\v 44 Katika njia hii Musa akazitangaza kwa watu wa ISraeli sikukuu zilizoamria kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 2 "Waamru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.
\s5
\v 3 Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Aroni ataiwasha daima taa mbele za Yahweh, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu.
\v 4 Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahweh, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.
\s5
\v 5 Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate.
\v 6 Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,
\s5
\v 7 Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh.
\v 8 Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahweh kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.
\v 9 Sadaka hii itakuwa kwa ajili ya Aroni na wanawe, na ni lazima waile mahali palipo patakatifu, kwa kuwa ni sehemu ya matoleo kwa Yahweh yaliyofanywa kwa moto."
\s5
\v 10 Sasa ilitokea kwamba mwana wa mwanamke Mwisraeli, ambaye baba yake alikuwa Mmisri, alikwenda miongoni mwa watu wa Israeli. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akagombana na mwanume Mwisraeli kambini.
\v 11 Mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru jina la Yahweh na kumlaani Mungu, kwa hiyo watu wakamleta kwa Musa. Jina la mama yake aliitwa Shelomithi, binti wa Dibri, kutoka kabila la Dani.
\v 12 Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.
\s5
\v 13 Kisha Yahweh akamwambia Musa,
\v 14 "Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.
\s5
\v 15 Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, 'Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.
\v 16 Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
\s5
\v 17 Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
\v 18 Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
\s5
\v 19 Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
\v 20 Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
\v 21 Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.
\s5
\v 22 Ni lazima mwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wanu."
\v 23 Kwa hiyo Musa akazungumza na watu wa Israeli, nao watu wakamleta mwanaume huyo nje ya kambi, yule ambaye alikuwa amemlaani Yahweh. Wakampiga kwa mawe. Watu waisraeli wakaitekeleza amri ya Yahweh aliyoitoa kupitia Musa.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapa, kisha hiyo nchi lazima ifanywe iwe ya kuishika Sabato kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 3 Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.
\v 4 Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.
\s5
\v 5 Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
\v 6 Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
\v 7 Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
\s5
\v 8 Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
\v 9 Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.
\s5
\v 10 Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
\s5
\v 11 Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
\v 12 Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
\s5
\v 13 Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
\v 14 Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
\s5
\v 15 Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
\v 16 Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
\v 17 Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 18 Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
\v 19 Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.
\s5
\v 20 Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu."
\v 21 Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
\v 22 Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
\s5
\v 23 Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
\v 24 Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.
\v 25 Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
\s5
\v 26 Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
\v 27 kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
\v 28 Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
\s5
\v 29 Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
\v 30 Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
\s5
\v 31 Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
\v 32 Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
\s5
\v 33 Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.
\v 34 Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao hayataweza kuuzwa kwa sababu hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.
\s5
\v 35 Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
\v 36 Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
\v 37 Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
\v 38 Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
\s5
\v 39 Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
\v 40 Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
\v 41 Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
\s5
\v 42 Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.
\v 43 Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.
\v 44 Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaowezao kuwapata kutok kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.
\s5
\v 45 Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale wtoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.
\v 46 Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtawezi kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miogoni mwa watu wa Israeli.
\s5
\v 47 Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,
\v 48 baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa maliopo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.
\s5
\v 49 Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.
\v 50 Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.
\s5
\v 51 Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni uwino wa idadi ya miaka hiyo.
\v 52 Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.
\s5
\v 53 Naye atatendewa kama mtu aliyeajiriwa mwaka kwa mwaka. Utahakikisha kwamba hatendewi kwa ukali.
\v 54 Iwapo hakukombolewa katika njia hizi, basi atatumika mpaka mwaka wa Yubile, yeye pamoja na watoto wake.
\v 55 Kwangu mimi watu wa Israeli ni watumishi. Wao ni watumishi wangu ambao Niliwatoa katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Msijitengenezee sanamu, wala msisimamishe kinyago cha kuchonga au nguzo ya jiwe ya kuabudia, na msisimamisha sura ya jiwe la kuchonga katika nchi yenu mtayoiinamia, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 2 Ni lazima muitunze Sabato Yangu na kupaheshimu patakatifu pangu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 3 Iwapo mtatembea katika sheria zangu na kuzishika amri zangu na kuzitii,
\v 4 Nami nitawapa ninyi mvua katika majira yake; nayo nchi itatoa mazao yake, na miti ya shambani itatoa matunda yake.
\s5
\v 5 Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupada mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.
\v 6 Nitawapa amani; mtalala bila ya kitu chochote kuwatia hofu. Nitawaondolea mbali wanyama waliohatari katika nchi, na upanga hautapita katika nchi yenu.
\s5
\v 7 Mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga.
\v 8 Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi; adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
\s5
\v 9 Nitawatazama kwa upendeleo na kuwafanya nyinyi mzae na kuwazidisha nyinyi.
\v 10 Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.
\s5
\v 11 Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami stachukizwa nanyi.
\v 12 Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
\v 13 Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.
\s5
\v 14 Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,
\v 15 na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—
\s5
\v 16 —kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.
\v 17 Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.
\s5
\v 18 Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.
\v 19 Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
\v 20 Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
\s5
\v 21 Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
\v 22 Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
\s5
\v 23 Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
\v 24 ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.
\s5
\v 25 Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.
\v 26 Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
\s5
\v 27 Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,
\v 28 kisha nami nitakwenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.
\s5
\v 29 Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.
\v 30 Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.
\s5
\v 31 Nitaigeuza miji yennu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.
\v 32 Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.
\v 33 Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.
\s5
\v 34 Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za daui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.
\v 35 Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.
\v 36 Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo yatawaogofyeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na awafukuzaye.
\s5
\v 37 Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya daui zenu.
\v 38 Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.
\v 39 Wale watakosalia miongoni mwenu watapotelea katika dhambi zao, huko kwenye nchi za adui zenu, na kwa sababu ya dhambi zao, na kwa sababu ya dhambi za baba zao watapotelea mbali pia.
\s5
\v 40 Lakini kama watakiri dhambi zao na dhambi ya baba zao, na usaliti wao ambao kwao hawakuwa waaminifu kwangu, pia na mwenendo wao dhidi yangu—
\v 41 ambao ulinisababisha kuwa kinyume nao, na kuwaleta katika nchi ya adui zao—iwapo mioyo yao isiyotahiriwa itanynyekezwa,
\v 42 na iwapo wataikubali adhabu kwa ajili ya dhambi zao, nami nitalikumbuka agano langu na Yakobo, agano langu na Isaka, agano langu na Abrahamu; Pia, nitaikumbuka nchi.
\s5
\v 43 Nchi itakayotelekezwa na wao, hivyo itapendezwa na Sabato zake inapobaki imetelekezwa na wao. Itawapasa kulipa hatia kwa dhambi zao kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walioyakataa maagizo yangu na kuzichukia sheria zangu.
\s5
\v 44 Lakini pamoja na haya yote, watapokuwa katika nchi ya adui zao, Mimi stawakataa wao, wala sitawachukia ili kuwaangamiza kabisa na kulifutilia mbali agano langu nilililoagana nao, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wao.
\v 45 Bali kwa ajili yao, nitalikumbuka agano langu na baba zao, niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri machoni pa mataifa, ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Yahweh."
\s5
\v 46 Hizi ndizo amri, hukumu, na sheria ambazo Yahweh alifanya baina yake na watu wa Israeli kwenye Mlima Sinai kwa kupitia Musa.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Iwapo mtu yeyote anatoa kiapo maalum cha kuwa mnathiri kwa Yahweh, tumieni tathmini zifuatazo:
\s5
\v 3 Viwango vyenu vya thamani kwa mwanaume aliye na umri kati ya miaka ishirini na miaka sitini yaweza kuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na vipimo vya shekeli ya mahali pa patakatifu.
\v 4 Kwa mwanamke wa umri uleule viwango vyenu vya thamani yapasa viwe shekeli thelathini vya fedha.
\s5
\v 5 Tangu wenye umri wa miaka mitano mpaka wa miaka ishirini viwango vyenu vya thamani kwa mwananume vitakuwa shekeli ishirini za fedha, na kwa mwanamke ni shekeli kumi za fedha,
\v 6 Kwa wenye umri wa tangu mwezi mmoja mpaka miaka mitano viwango vyenu vya thamani kwa mawanaume vitakuwa shekeli tano za fedha na kwa mwanamke shekeli tatu za fedha.
\s5
\v 7 Tangu wenye umri wa miaka sitini na zaidi kwa mwanaume viwango vyenu vya thamani vitakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke ni shekeli kumi.
\v 8 Lakini kama mtu atoaye kiapo cha mnadhiri hawezi kulipa kiwango hicho cha thamani, kisha huyo mtu anayetolewa lazima atapelekwa kwa kuhani, naye kuhani atamthamanisha huyo atolewaye kwa kiasi anachoweza kutoa yule anayetoa kiapo cha mnadhiri.
\s5
\v 9 Iwapo mtu anataka kutoa sadaka ya mnyama kwa Yahweh, na iwapo Yahweh ataikubali, kisha huyo mnyama atatengwa kwake.
\v 10 Mtu huyo hataruhusiwa kumtoa madhabahuni au kumbadilisha huyo mnyama, mzuri kwa mbaya au mbaya kwa mzuri. endapo atatoa mnyama badala ya mwingine, kisha wanyama hao wawili; yule anayetolewa na yule anayebadilishwa wanakuwa watakatifu.
\s5
\v 11 Hata hivyo, iwapo kile mtu amishaapa kumtolea Yahweh kwa uhalisia siyo kisafi, kwa hiyo, Yahweh hatakikubali, naye huyo mtu atalazimika kumleta huyo mnyama kwa kuhani.
\v 12 Kuhani atamthamanisha, kwa thamani ya soko la mnyama. Thamani yoyote kuhani atakayoiweka juu ya mnyama, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake.
\v 13 Na kama mmiliki anapenda kumkomboa, kisha tano ya thamani yake itaongezwa kwenye gharama yake ya ukombozi.
\s5
\v 14 Mtu aitengapo nyumba yake iwe zawadi takatifu kwa Yahweh, kisha kuhani ataweka thamani yake ama iwe ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote itakayowekwa na kuhani juu yake, ndiyo itakuwa thamani yake.
\v 15 Lakini kama mmiliki wake anayeitenga nyumba yake anapenda kuikomboa, atalazimika kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake kwenye gharama ya ukombozi wake, nayo nyumba itakuwa yake.
\s5
\v 16 Iwapo mtu anatenga sehemu ya ardhi yake mwenye, kisha tathmini yake itakuwa katika uwiano kwa kiwango cha kiasi cha mbegu inayotakiwa kuipanda katika ardhi hiyo—homeri moja ya mbegu za shairi ambayo itathamanishwa kwa shekeli hamsini za fedha.
\s5
\v 17 Na kama analitenga shamba lake katika mwaka wa Yubile, tathmini yake ya awali itabaki kuwa ileile.
\v 18 Lakini endapo atalitenga shamba hilo baada ya mwaka wa Yubile, kisha kuhani atalazimika kukokotoa thamani yake kwa idadi ya miaka inayobaki mpaka mwaka wa Yubile, na thamani yake lazima ishushwe.
\s5
\v 19 Iwapo mtu anayelitenga shamba lake anapenda kuliko, mboa, naye atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani, nalo shamba litakuwa lake tena.
\v 20 Iwapo halikomboi shamba, au iwapo amishaliuza shamba kwa mtu mwingine, haliwezi kukombolewa tena.
\v 21 Badala yake, shamba hilo litakapoachwa huru katika mwaka wa Yubile, litakuwa zawadi takatifu kwa Yahweh, kama lilivyo shamba lililotolewa kabisa kwa Yahweh. Nalo litakuwa mali ya kuhani.
\s5
\v 22 Iwapo mtu anatenga shamba alilolinunua, lakini hilo shamba siyo sehemu ya ardhi ya familia yake,
\v 23 kuhani atafanya tathmini yake mpaka mwaka wa Yubile, na mtu huyo lazima atalipa thamani yake katika siku hiyo hiyo kuwa zawadi takatifu kwa Yahweh.
\s5
\v 24 Katika mwaka wa Yubile, shamba litarejeshwa kwa mtu yule ambaye lilikuwa limenunuliwa, kwa mmiliki wa ardhi.
\v 25 Tathmani yote lazima ifanywe kwa uzani wa shekeli ya mahali pa patakatifu. Gera ishirini kwa shekeli moja.
\s5
\v 26 Asiwepo mtu atakayetenga mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wanyama, kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama tayari ni mali ya Yahweh; iwe ni maksai au kondoo, ni wa Yahweh.
\v 27 Na kama ni mnyama aliye najisi, kisha mmiliki wake anaweza kumnunua tena sawasawa na thamani yake, na sehemu ya tano lazima itaongezwa kwenye thamani hiyo. Na kama mnyama hakombolewi, naye atauzwa kwa thamani iliyowekwa.
\s5
\v 28 Hakutakuwa na kitu amabacho mtu anakitoa kwa Yahweh, kutoka katika vyote alivyonavyo, iwe ni mwanadamu au mnyama, au ardhi ya familia yake, ambacho chaweza kuuzwa au kukombolewa. Kila kitu kitolewacho ni kitakatifu sana kwa Yahweh.
\v 29 Hakuna fidia inayoweza kulipwa kwa ajili ya mtu aliyetolewa ili kuangamizwa. Mtu huyo sharti auawe
\s5
\v 30 Zaka yote iliyo ya ardhini, iwe nafaka ichipukayo juu ya ardhi au tunda kutoka kwenye miti, ni mali ya Yahweh. Ni takatifu kwa Yahweh.
\v 31 Iwapo mtu anakomboa chochote cha zaka yake, atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani yake.
\s5
\v 32 Na kwa kila mnyama wa kumi wa kundi la ng'ombe au la kondoo, yeyote anayepita chini ya fimbo ya mchungaji, atatengwa kwa ajili ya Yahweh.
\v 33 Mchungaji hatatafuta wanyma waliobora au wabaya kabisa, na haruhusiwi kubadili mnyama mmoja kwa mnyama mwingine. Iwapo anambadilisha kwa namna yoyote ile, kisha wote wawili yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa watakuwa watakatifu. Mnyama huyo atolewaye hawezi kukombolewa.'"
\s5
\v 34 Hizi ndizo amri ambazo Yahweh alimpa Musa kwenye mlima Sinai kwa ajili ya watu wa Israeli.