sw_ulb_rev/01-GEN.usfm

2909 lines
193 KiB
Plaintext

\id GEN
\ide UTF-8
\h Mwanzo
\toc1 Mwanzo
\toc2 Mwanzo
\toc3 gen
\mt Mwanzo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
\v 2 Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.
\s5
\v 3 Mungu akasema, "na kuwe nuru," na kulikuwa na nuru.
\v 4 Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.
\v 5 Mungu akaiita nuru " mchana" na giza akaliita "usiku." Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
\s5
\v 6 Mungu akasema, " na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji."
\v 7 Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo.
\v 8 Mungu akaita anga "mbingu." Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili.
\s5
\v 9 Mungu akasema, "maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane." Ikawa hivyo.
\v 10 Mungu aliita ardhi kavu "nchi," na maji yaliyo kusanyika akayaita "bahari." Akaona kuwa ni vyema.
\s5
\v 11 Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake." Ikawa hivyo.
\v 12 Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\v 13 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.
\s5
\v 14 Mungu akasema, "kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
\v 15 Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi." Ikawa hivyo.
\s5
\v 16 Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
\v 17 Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi,
\v 18 kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\v 19 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne.
\s5
\v 20 Mungu akasema, "maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu."
\v 21 Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\s5
\v 22 Mungu akavibariki, akisema, "zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi."
\v 23 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.
\s5
\v 24 Mungu akasema, " nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake." Ikawa hivyo.
\v 25 Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaaho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwani vyema.
\s5
\v 26 Mung akasema, "na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi."
\v 27 Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba.
\s5
\v 28 Mungu akawabariki na akawaambia, "zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,"
\v 29 Mungu akasema, "tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.
\s5
\v 30 Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai ni metoa kila mmea kwa ajili ya chakula." ikawa hivyo.
\v 31 Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi.
\v 2 Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
\v 3 Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
\s5
\v 4 Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu.
\v 5 Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.
\v 6 Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi.
\s5
\v 7 Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.
\v 8 Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba.
\s5
\v 9 Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
\v 10 Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne.
\s5
\v 11 Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu.
\v 12 Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. pia kuna bedola na jiwe shohamu.
\s5
\v 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni. Huu unatiririka kupitia nchi yote ya kushi.
\v 14 Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
\s5
\v 15 Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
\v 16 Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, "kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.
\v 17 Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika."
\s5
\v 18 Kisha Yahwe Mungu akasema, "siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa."
\v 19 Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.
\v 20 Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.
\s5
\v 21 Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.
\v 22 Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu.
\v 23 Mwanaume akasema, "kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume.
\s5
\v 24 Kwa hiyo mwanaume atawaacha baba yake na mama yake, ataungamanika na mke wake, na watakuwa mwili mmoja.
\v 25 Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, "Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?"
\v 2 Mwanamke akamwambia nyoka, "Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani,
\v 3 lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'"
\s5
\v 4 Nyoka akamwambia mwanamke, "hakika hamtakufa.
\v 5 Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya."
\v 6 Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala.
\s5
\v 7 Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe.
\v 8 Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu.
\s5
\v 9 Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, " uko wapi?"
\v 10 Mwanaume akasema, "nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha."
\v 11 Mungu akasema, "Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?"
\s5
\v 12 Mwanaume akasema, " Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala."
\v 13 Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, " Nini hiki ulichofanya?" mwanamke akasema, "nyoka alinidanganya, na nikala."
\s5
\v 14 Yahwe Mungu akamwambia nyoka, " kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.
\v 15 Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake."
\s5
\v 16 Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala."
\s5
\v 17 Kwa Adam akasema, "kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, " usile matunda yake', ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako.
\v 18 Ardhi itazaa miiba na mbigili kwa ajili yako, na utakula mimea ya shambani.
\v 19 Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi."
\s5
\v 20 Mwanaume akaita mke wake jina Hawa kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.
\v 21 Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha.
\s5
\v 22 Yahwe Mungu akasema, " sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele."
\v 23 Kwa hiyo Yahwe Mungu akamuondoa kutoka kwenye bustani ya Edeni, kwenda kulima ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa.
\v 24 Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, " nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe."
\v 2 Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.
\s5
\v 3 Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe.
\v 4 Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,
\v 5 lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana.
\s5
\v 6 Yahwe akamwambia Kaini, " kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana?
\v 7 Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde.
\s5
\v 8 Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, " twende mashambani." Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
\v 9 Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, "Ndugu yako Habili yuko wapi?" Akasema, "sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"
\s5
\v 10 Yahwe akasema, "umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini.
\v 11 Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako kutoka mikononi mwako.
\v 12 Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani."
\s5
\v 13 Kaini akamwambia Yahwe, "Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili.
\v 14 Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua."
\v 15 Yahwe akamwambia, "ikiwa mtuyeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba." Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu awayeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.
\s5
\v 16 Kwa hiyo Kaini akatoka mbele ya uwepo wa Yahwe na akaishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.
\v 17 Kaini akamjua mke wake na akapata mimba. Akamzaa Henoko. Akajenga mji na akauita kwa jina la mwanae Henoko.
\s5
\v 18 Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki.
\v 19 Lameki akajitwalia wake wawili: jinala mmoja alikuwa Ada, na jina la yule mwingine alikuwa Sila.
\s5
\v 20 Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama.
\v 21 Ndugu yake aliitwa Yubali. Huyu alikuwa baba yao na wale wapigao kinubi na filimbi.
\v 22 Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama.
\s5
\v 23 Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua.
\v 24 Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba."
\s5
\v 25 Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, " Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa."
\v 26 Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
\v 2 Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
\s5
\v 3 Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
\v 4 Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
\v 5 Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
\s5
\v 6 Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
\v 7 Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.
\v 8 Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
\s5
\v 9 Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
\v 10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 11 Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
\s5
\v 12 Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
\v 13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 14 Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
\s5
\v 15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
\v 16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 17 Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
\s5
\v 18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.
\v 19 Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.
\v 20 Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
\s5
\v 21 Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
\v 22 Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 23 Henoko aliishi miaka 365.
\v 24 Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
\s5
\v 25 Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
\v 26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 27 Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
\s5
\v 28 Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
\v 29 Akamuita jina lake Nuhu, akisema, "Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani."
\s5
\v 30 Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.
\v 31 Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
\s5
\v 32 Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao,
\v 2 wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.
\v 3 Yahwe akaema, " roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120."
\s5
\v 4 Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
\s5
\v 5 Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu.
\v 6 Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamuhuzunisha moyo wake.
\s5
\v 7 Kwa hiyo Yahwe akasema, "Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba."
\v 8 Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.
\s5
\v 9 Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.
\v 10 Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti.
\s5
\v 11 Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.
\v 12 Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.
\s5
\v 13 Mungu akamwambia Nuhu, "Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.
\v 14 Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje.
\v 15 Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.
\s5
\v 16 Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu.
\v 17 Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa.
\s5
\v 18 Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao.
\v 19 Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume.
\s5
\v 20 Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama.
\v 21 Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao."
\v 22 Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Yahwe akamwambia Nuhu, "Njoo, wewe na nyumba yako wote, katika safina, kwa kuwa nimeona kuwa wewe ni mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki.
\v 2 Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, lete wawili wawili, wakiume na wakike.
\v 3 Pia na kwa ndege wa angani, lete saba wa kiume na saba wa kike, ili kuhifadhi kizazi chao juu ya uso wa nchi yote.
\s5
\v 4 Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi."
\v 5 Nuhu alifanya yote ambayo Yahwe alimuagiza.
\s5
\v 6 Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia sita wakati gharika ilipokuja juu ya nchi.
\v 7 Nuhu, watoto wake wa kiume, mke wake, na wake za watoto wake waliingia katika safina pamoja kwa sababu ya maji ya gharika.
\s5
\v 8 Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi,
\v 9 wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu.
\v 10 Ikawa kwamba baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya nchi.
\s5
\v 11 Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka.
\v 12 Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.
\s5
\v 13 Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina.
\v 14 Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa.
\s5
\v 15 Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina.
\v 16 Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango.
\s5
\v 17 Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi.
\v 18 Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.
\s5
\v 19 Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa.
\v 20 Maji yakaongezeka dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima.
\s5
\v 21 Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu.
\v 22 Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa.
\s5
\v 23 Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa mchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia.
\v 24 Maji haya kuzama chini ya nchi kwa muda wa siku miamoja na hamsini.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.
\v 2 Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.
\v 3 Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi. na mwisho wa siku miamoja na hamsini maji yakawa yamezama chini.
\s5
\v 4 safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.
\v 5 Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
\s5
\v 6 Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.
\v 7 Akatuma kunguru na akaruka hadi maji yalipo kauka katika nchi.
\s5
\v 8 Kisha akatuma njiwa kuona kama maji yamezama chini kutoka kwenye uso wa nchi,
\v 9 lakini njiwa hakuona sehemu ya kutua unyayo wake, na akarudi kwake ndani ya safina, kwa kuwa maji yalikuwa bado yamefunika nchi yote. Akanyoosha mkono wake, akamchukua na kumuweka ndani ya safina pamoja naye.
\s5
\v 10 Akasubiri siku saba zingine akatuma tena njiwa kutoka kwenye safina.
\v 11 Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi.
\v 12 Akasubiri siku saba zingine na akamtuma njiwa tena. Njiwa hakurudi kwake tena.
\s5
\v 13 Ikawa kwamba katika mwaka wa mia sita na moja, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, Tazama, uso wa nchi ulikuwa umekauka.
\v 14 Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa imekauka.
\s5
\v 15 Mungu akamwambia Nuhu,
\v 16 "Toka nje ya safina, wewe, mke wako, wanao wa kiume, na wake wa wanao pamoja nawe.
\v 17 Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi."
\s5
\v 18 Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na watoto wake wa kiume, mke wake, na wake wa wa wanawe pamoja naye.
\v 19 Kila kiumbe hai, kila kitambaacho, na kila ndege, na kila kiendacho juu ya nchi, kwa kabila zao, wakaiacha safina.
\s5
\v 20 Nuhu akajenga madhabahu kwa Yahwe. Akachukua baadhi ya wanyama walio safi na baadhi ya ndege walio safi, na kutoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.
\v 21 Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, " Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya.
\v 22 Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha Mungu akambariki Nuhu na wanawe, na kuwaambia, "Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi.
\v 2 Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai juu ya nchi, juu ya kila ndege wa angani, juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi, na juu ya samaki wote wa baharini. Vimetolewa katika mikono yenu.
\s5
\v 3 Kila kitu kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula kwa ajili yenu. Kama nilivyo wapa mimea, sasa nawapa kila kitu.
\v 4 Lakini msile nyama pamoja na uhai wake - yaani damu yake - ndani yake.
\s5
\v 5 Lakini kwa ajili ya damu yenu, uhai uliomo katika damu yenu nitataka malipo. Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka. Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.
\v 6 Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa, kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu.
\v 7 Na hivyo nanyi zaeni na kuongezeka, sambaeni katika inchi yote na muongezeke juu yake."
\s5
\v 8 Kisha Mungu akazungumza na Nuhu na wanae pamoja naye, akisema,
\v 9 "Kwa ajili yangu, sikiliza! Ninakwenda kulithibitisha agano langu pamoja nawe na uzao wenu baada yenu,
\v 10 na kwa kila kiumbe hai kilicho pamoja nawe, pamoja na ndege, mnyama wa kufugwa, na kila kiumbe cha nchi pamoja nawe, kuanzia kwa wote waliotoka kwenye safina, mpaka kwa kila kiumbe hai juu ya nchi.
\s5
\v 11 Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi."
\v 12 Mungu akasema, " na hii ndiyo ishara ya agano ambalo ninafanya kati yangu na ninyi pamoja na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote vya baadaye:
\v 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua katika wingu, na itakuwa ndiyo ishara ya agano kati yangu na nchi.
\s5
\v 14 Hata itakuwa nitakapoleta wingu juu ya nchi na upinde wa mvua ukaonekana katika wingu,
\v 15 ndipo nitakumbuka agano langu, ambalo ni kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili. Maji hayatafanyika tena gharika kuharibu wote wenye mwili.
\s5
\v 16 Upinde wa mvua utakuwa katika mawingu na nitauona, ili kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na kila kiumbe hai cha wote wenye mwili ambacho kiko juu ya nchi."
\v 17 Kisha Mungu akamwambia Nuhu, " Hii ni ishara ya agano ambalo nimelithibitisha kati yangu na wenye mwili wote ambao wako juu ya nchi."
\s5
\v 18 Wana wa Nuhu ambao walitoka katika safina walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Na Hamu akamzaa kanaani.
\v 19 Watatu hawa walikuwa ndio wana wa Nuhu, na kutokea kwa hawa nchi yote ikajaa watu.
\s5
\v 20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, na akapanda mizabibu.
\v 21 Akanywa sehemu ya divai na akalewa. Akawa amelala hemeani uchi.
\s5
\v 22 Kisha Hamu, baba yake na Kanaani, akaona uchi wa baba yake na akawaambia ndugu zake wawili waliokuwa nje.
\v 23 Kwa hiyo Shemu na Yafethi wakachukua kanzu wakaitanda juu ya mabega yao, na wakatembea kinyumenyume na wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zikiwa zimegeuka nyuma upande mwingine, kwa hiyo hawakuona uchi wa baba yao.
\s5
\v 24 Nuhu alipozinduka kutoka katika ulevi wake, alijua ni jambo gani mtoto wake mdogo amemfanyia.
\v 25 Hivyo akasema, "Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake."
\s5
\v 26 Akasema pia, Yahwe, Mungu wa Shemu, abarikiwe, Kanaani na awe mtumwa wake.
\v 27 Mungu na apanuwe mipaka ya Yafethi, na afanye makazi yake katika hema za Shemu. Kanaani na awe mtumwa wake."
\s5
\v 28 Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka miatatu na hamsini.
\v 29 Siku zote za Nuhu zilikuwa ni miaka mia tisa na hamsini, na kisha alikufa.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.
\s5
\v 2 Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.
\v 3 Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.
\v 4 Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.
\v 5 Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.
\s5
\v 6 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.
\v 7 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
\s5
\v 8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.
\v 9 Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, "Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe."
\v 10 Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari.
\s5
\v 11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,
\v 12 na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.
\v 13 Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,
\v 14 Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.
\s5
\v 15 Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
\v 16 pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,
\v 17 Mhivi, Mwarki, Msini,
\v 18 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.
\s5
\v 19 Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.
\v 20 Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.
\s5
\v 21 Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.
\v 22 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.
\v 23 Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
\s5
\v 24 Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.
\v 25 Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.
\s5
\v 26 Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
\v 27 Hadoram, Uzali, Dikla,
\v 28 Obali, Abimaeli, Sheba,
\v 29 Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
\s5
\v 30 Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.
\v 31 Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.
\s5
\v 32 Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja.
\v 2 Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale.
\s5
\v 3 Wakasemezana, "Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu." Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.
\v 4 Wakasema, "njoni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote."
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga.
\v 6 Yahwe akasema, "Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Hivikaribuni halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya.
\v 7 Njoni, tushuke na tuvuruge lugha yao pale, ili kwamba wasielewane."
\s5
\v 8 Kwa hiyo Yahwe akawatawanya kutoka pale kwenda pande zote za uso wa nchi na wakaacha kujenga mji.
\v 9 Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote.
\s5
\v 10 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa miaka mia moja, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika.
\v 11 Shemu akaishi miaka miatano baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 12 Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na mitano akamzaa Shela.
\v 13 Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 14 Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
\v 15 Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 16 Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.
\v 17 Eberi aliishi miaka 430 baada ya kumzaa Pelegi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 18 Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu.
\v 19 Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumza a Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 20 Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na miwili, alimzaa Serugi.
\v 21 Reu aliishi miaka207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 22 Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.
\v 23 Seregu aliishi miaka mia mbili baada ya kumzaa Nahori. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 24 Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera.
\v 25 Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\v 26 Baada ya Tera kuishi miaka sabini, akamzaa Abram, Nahori, na Haran.
\s5
\v 27 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera alimzaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu.
\v 28 Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo.
\s5
\v 29 Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska.
\v 30 Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto.
\s5
\v 31 Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale.
\v 32 Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Yahwe akamwambia Abram, "Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako, na kwa jamaa za baba yako, uende katika nchi nitakayo kuonesha.
\v 2 Nitakufanya uwe taifa kubwa, na nitakubariki na kulifanya jinalako kuwa kubwa, na utafanyika baraka.
\v 3 Nitawabariki wakubarikio, lakini asiye kuheshimu nita mlaani. Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa.
\s5
\v 4 Kwa hiyo Abram akaondoka kama vile Yahwe alivyo mwambia kufanya, na Lutu akaenda pamoja naye. Abram alikuwa na miaka sabini na mitano wakati alipotoka Harani.
\v 5 Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 6 Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo.
\v 7 Yahwe akamtokea Abram, na kusema, "Nitawapa uzao wako nchi hii." Kwa hiyo Abram akamjengea madhabahu, Yahwe ambaye alimtokea.
\s5
\v 8 Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe.
\v 9 Kisha Abram akaendelea kusafiri, akielekea upande wa Negebu.
\s5
\v 10 Kulikuwa na njaa katika nchi, kwa hiyo Abram akaenda kukaa Misri, kwa kuwa njaa ilikua kali katika nchi.
\v 11 Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, "tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri.
\v 12 Wamisri watakapokuona watasema, huyu ni mke wake, na wataniua mimi, lakini watakuacha wewe hai.
\v 13 Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumba maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako."
\s5
\v 14 Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana.
\v 15 Wakuu wa Farao wakamuona, na kumsifia kwa Farao, na huyu mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao.
\v 16 Farao akamtendea kwa wema Abram kwa ajili yake, na akampatia kondoo, maksai, punda waume watumishi wa kiume, watumishi wa kike, punda wake, na ngamia.
\s5
\v 17 Kisha Yahwe akampiga Farao na nyumba yake kwa mapigo makuu kwa sababau ya Sarai, mke wa Abram.
\v 18 Farao akamwita Abram na kusema, "Nini hiki ambacho umenifanyia? Kwa nini hukuniambia kuwa alikuwa mke wako?
\v 19 Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako."
\v 20 Kisha Farao akatoa amri kwa watu wake kuhusiana naye, na wakamuondoa, yeye pamoja na mke wake na vyote alivyokuwa navyo.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kwa hiyo Abram akaondoka akatoka Misri na akaenda Negebu, Yeye, mke wake, na vyote alivyokuwa navyo. Lutu pia akaenda pamoja naye.
\v 2 Na sasa Abram alikuwa tajiri wa mifugo, fedha na dhahabu.
\s5
\v 3 Aliendelea na safari yake kutoka Negebu hadi Betheli, mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo, kati ya Betheli na mji wa Ai.
\v 4 Akaenda mahali ambapo madhabahu ilikuwa imejengwa mwanzoni. Hapa akaliitia jina la Yahwe.
\s5
\v 5 aliyekuwa anasafiri na Abram, alikuwa pia na ngo'mbe, makundi ya mifugo, na mahema.
\v 6 Nchi haikuwatosha wote kukaa pamoja karibu kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana, kiasi kwamba hawakuweza kukaa pamoja.
\v 7 Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo.
\s5
\v 8 Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, "Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia.
\v 9 Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto."
\s5
\v 10 Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora.
\v 11 Kwa hiyo Lutu akajichagulia yeye mwenyewe nchi tambarare ya Yorodani na akasafiri mashariki, na ndugu hawa wakatengana wao kwa wao.
\s5
\v 12 Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma.
\v 13 Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe.
\s5
\v 14 Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, "Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi.
\v 15 Nchi yote hii uionayo, nitakupatia wewe pamoja na uzao wako milele.
\s5
\v 16 Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama mavumbi ya nchi, kiasi kwamba kama kuna mtu anaweza kuhesabu mavumbi ya nchi, ndipo na uzao wako pia utahesabika.
\v 17 Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia."
\v 18 Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Ikiwa katika siku za Amrafeli, mfalme wa shinari, Arioko, mfalme wa Elasari, Kedorlaoma, mfalme wa Elam na Tidali, mfalme wa Goimu,
\v 2 walifanya vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha, mfalme wa Gomora, Shinabu, mfalme wa Adma, Shemeberi, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela(pia ikiitwa Soari).
\s5
\v 3 Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi).
\v 4 Kwa miaka kumi na mbili walimtumikia Kedorlaoma, lakini katika mwaka wa kumi na tatu waliasi.
\v 5 Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu,
\v 6 na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa.
\s5
\v 7 Kisha wakarudi wakaja En Misifati (Pia ikiitwa Kadeshi), na kuishinda nchi yote ya Waamaleki, na pia Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari.
\v 8 Kisha mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari) walikwenda na kuandaa vita
\v 9 dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafme wanne dhidi ya wale watano.
\s5
\v 10 Na sasa bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, na wafalme wa Sodoma na Gomora walipokimbia, wakaanguka pale. Wale waliosalia wakakimbilia milimani.
\v 11 Kwa hiyo adui akachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, na wakaenda zao,
\v 12 walipoondoka, wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake na Abram ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote.
\s5
\v 13 Mmoja ambaye alitoroka alikuja na kumwambia Abram mwebrania. Alikuwa anaishi katika mialoni ya Mamre, mwamori ambaye alikuwa ni ndugu wa Eshkoli na Aneri ambao walikuwa washirika wa Abram.
\v 14 Abram aliposikia kuwa maadui wamemteka ndugu yake, akawaongoza wanaume waliofunzwa na kuzaliwa nyumbani mwake 318 na akawaongoza hadi Dani.
\s5
\v 15 Akawagawanya watu wake dhidi yao usiku na kuwavamia, na kuwafukuza mpaka Hoba, ambayo iko kaskazini mwa Dameski.
\v 16 Kisha akarudisha mali zote, pia akamrudisha ndugu yake Lutu na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.
\s5
\v 17 Baada ya Abram kurudi kutoka kumpiga Kadorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae, mfalme wa Sodoma akatoka kuonana nae katika bonde la Shawe (pia iliitwa bonde la mfalme).
\v 18 Melkizedeki, mfalme wa Salem, akaleta mkate na divai. Alikuwa ni kuhani wa Mungu aliye juu sana.
\s5
\v 19 Alimbariki akisema, "Abarikiwea Abram na Mungu aliye juu sana, muumba wa mbingu na nchi.
\v 20 Abarikiwe Mungu aliye juu sana, ambaye amekupatia adui zako katika mikono yako." Kisha Abram akampatia sehemu ya kumi ya kila kitu.
\s5
\v 21 Mfalme wa Sodama akamwambia Abram, "Nipatie watu, na ujichukulie wewe mwenyewe mali."
\v 22 Abram akamwambia mfalme wa Sodoma, "Nimeinua juu mkono wangu kwa Yahwe, Mungu aliye juu sana, muumbaji wa mbingu na nchi,
\v 23 kwamba sitachukua uzi wala gidamu ya kiatu, au kitu chochote ambacho ni chako, 'ili kwamba usiseme, nimemfanya Abram kuwa tajiri.'
\v 24 Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula na sehemu za watu waliokwenda nami. Aneri, Eskoli, na Mamre na wachukue sehemu zao."
\s5
\c 15
\p
\v 1 Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, "Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana."
\v 2 Abram akasema, "Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?"
\v 3 Abram akasema, "Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu."
\s5
\v 4 Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, "Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako."
\v 5 Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu." Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.
\s5
\v 6 Akamwamini Yahwe, na akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki.
\v 7 Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi."
\v 8 Akasema, "Bwana Yahwe, nitajua je kuwa nitairithi?"
\s5
\v 9 Kisha akamwambia, "Nipatie ndama wa umri wa miaka mitatu, mbuzi mke wa umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa umri wa miaka mitatu, na njiwa na mwana njiwa."
\v 10 Akamletea hivi vyote, akavipasua katika sehemu mbili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuawapasua.
\v 11 Wakati ndege walipokuja juu ya mizoga, Abram akawafukuza.
\s5
\v 12 Kisha wakati jua lilipokuwa likizama, Abram akalala usingizi mzito na tazama, hofu ya giza kuu ikamfunika.
\v 13 Kisha Yahwe akamwambia Abram, "Ujuwe kwa hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si ya kwao, na watatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne.
\s5
\v 14 Nitahukumu taifa ambalo watalitumikia, na baadye watatoka wakiwa na mali nyingi.
\v 15 Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema.
\v 16 Katika kizazi cha nne watakuja tena hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujafikia mwisho wake."
\s5
\v 17 Jua lilipokuwa limezama na kuwa giza, tazama, chungu cha moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande.
\v 18 Siku hiyo Yahwe akafanya agano na Abram, akisema, "Ninatoa nchi hii kwa uzao wako, kutoka mto wa Misri hadi kwenye mto mkuu, Frati -
\v 19 Mkeni, Mkenizi, na Mkadmoni,
\v 20 Mhiti, Mperizi, Mrefai,
\v 21 Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri.
\v 2 Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, "Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye." Abram akasikiliza sauti ya Sarai.
\v 3 Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake.
\v 4 Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake.
\s5
\v 5 Kisha Sarai akamwambia Abram, "Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe."
\v 6 Lakini Abram akamwambia Sarai, "Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake." Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.
\s5
\v 7 Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri.
\v 8 Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?" Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai."
\s5
\v 9 Malaika wa Yahwe akamwambia, " Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake."
\v 10 Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, "Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika."
\s5
\v 11 Malaika wa Yahwe pia akamwambia, " Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako.
\v 12 Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote."
\s5
\v 13 Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, "Wewe ni Mungu unionaye mimi," kwa kuwa alisema, "je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?"
\v 14 Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
\s5
\v 15 Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli.
\v 16 Abram alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, "Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu.
\v 2 Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana.
\s5
\v 3 Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema,
\v 4 "Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi.
\v 5 Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi.
\v 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako.
\s5
\v 7 Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako.
\v 8 Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao."
\s5
\v 9 Kisha Mungu akamwambia Abraham, "nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.
\v 10 Hili ndilo agano langu, ambalo utalishika, kati yangu na wewe na wazao wako baada yako: Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe.
\v 11 Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi.
\s5
\v 12 Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako.
\v 13 Mtu ambaye amezaliwa katika nyumba yako na yule aliye nunuliwa kwa fedha yako lazima atahiriwe. Hivyo agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele.
\v 14 Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu."
\s5
\v 15 Mungu akamwambia Abraham, "kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara.
\v 16 Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye.
\s5
\v 17 Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?"
\v 18 Abraham akamwambia Mungu, "Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!"
\s5
\v 19 Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake.
\v 20 Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu.
\v 21 Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani."
\s5
\v 22 Alipo kuwa amemaliza kuzungumza naye, Mungu akaondoka kwa Abraham.
\v 23 Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema.
\s5
\v 24 Abraham alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
\v 25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
\v 26 Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo
\v 27 wanaume wote wa nyumba yake walitahiriwa pia, hawa ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yahwe alimtokea Abraham katika Mialoni ya Mamre, alipokua ameketi mlangoni pa hema wakati wa jua.
\v 2 Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama mbele yake. Alipo waona, alikimbia kupitia mlango wa hema kuwalaki na kuinama chini hadi ardhini.
\s5
\v 3 Akasema, "Bwana, kama nimepata upendelea machoni pako, nakuomba usinipite na kuniacha mtumishi wako.
\v 4 Naomba maji kidogo yaletwe, mnawe miguu yenu, na mjipumzishe chini ya mti.
\v 5 Nami acha nilete chakula kidogo, ili kwamba mjiburudishe wenyewe. Ndipo baadae mwaweza kwenda zenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu." Nao wakasema, "Fanya kama ulivyo sema."
\s5
\v 6 Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, "Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate."
\v 7 Kisha Abraham akakimbia kundini, akachukua ndama wa ng'ombe aliye laini na mzuri, na akampatia mtumishi na kwa haraka akamwandaa.
\v 8 Akatwaa siagi na maziwa na ndama aliye kwisha andaliwa, na akaweka chakula mbele yao, naye akasimama karibu nao chini ya mti wakati wanakula.
\s5
\v 9 Wakamwambia, "Mke wako Sara yuko wapi?" akajibu. "pale hemani."
\v 10 akasema, "Hakika nitarejea kwako majira ya machipuko, na tazama Sara mkeo atakuwa na mtoto wa kiume." Sara alikuwa akisikiliza mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake.
\s5
\v 11 Abraham na Sara walikuwa wazee, umri wao ulikuwa umeendelea sana, na Sara alikuwa amepita umri ambao mwanamke anaweza kuzaa watoto.
\v 12 Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, "baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?"
\s5
\v 13 Yahwe akamwambia Abraham, "Kwa nini Sara amecheka na kusema, Je ni kweli nitazaa mtoto, nikiwa mzee'?
\v 14 Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume."
\v 15 Kisha Sara akakataa na kusema, "sikucheka," kwa kuwa aliogopa. Yahwe akasema, "hapana ulicheka."
\s5
\v 16 Kisha wale wanaume walisimama kuondoka na wakatazama chini kuelekea Sodoma. Abraham akafuatana nao kuona njia yao.
\v 17 Lakini Yahwe akasema, Je ni mfiche Abraham kile ninacho kusudia kufanya,
\v 18 Ikiwa kwa hakika Abraham atakuwa mkuu na taifa lenye nguvu, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
\v 19 Kwa kuwa nimemchagua ili awaelekeze wanawe na nyumba yake baada yake waishike njia ya Yahwe, watende utakatifu na haki, ili kwamba Yahwe ampatie Abraham yale aliyo yasema kwake."
\s5
\v 20 Kisha Yahwe akasema, "Kwa sababu kilio cha Sodoma na Gomora ni kikuu, na kwa kuwa dhambi yao ni kubwa,
\v 21 sasa nitashuka pale na kuona kilio kilicho nifikia dhidi yake, ikiwa kweli wamefanya au hawakufanya, nitajua."
\s5
\v 22 Kwa hiyo wale wanaume wakageuka toka pale, na kuelekea Sodoma, lakini Abraham akabaki amesimama mbele ya Yahwe.
\v 23 Kisha Abraham alikaribia na kusema, "Je utawafutilia mbali watakatifu pamoja na waovu?
\s5
\v 24 Huenda wakawepo wenye haki hamsini katika mji. Je utawakatilia mbali na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo?
\v 25 Hasha usifanye hivyo, kuwauwa watakatifu pamoja na waovu, ili kwamba watakatifu watendewe sawa na waovu. Hasha! Je muhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?"
\v 26 Yahwe akasema, "Katika Sodoma nikipata watakatifu hamsini kwenye mji, nita uacha mji wote kwa ajili ya hao."
\s5
\v 27 Abraham akajibu na kusema, "Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu!
\v 28 Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?" Akasema, "Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale."
\s5
\v 29 Akaongea naye tena, na kusema, "Itakuwaje ikiwa arobaini watapatikana pale?" Akajibu, "Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini."
\v 30 Akasema, Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale." Akajibu, 'Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale."
\v 31 Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale." Akajibu, "Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini."
\s5
\v 32 Akasema, "Tafadhali usikasirike, Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule." Na akasema, sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi."
\v 33 Yahwe akaendelea na njia yake mara tu baada ya kumaliza kuongea na Abraham, na Abraham akarudi nyumbani.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Malaika wawili wakaja Sodoma jioni, wakati ambao Lutu alikuwa amekaa langoni mwa Sodoma. Lutu akawaona, akainuka kuwalaki, na akainama uso wake chini ardhini.
\v 2 Akasema, Tafadhari Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke." Nao wakasema, "Hapana, usiku tutalala mjini."
\v 3 Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja nae, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala.
\s5
\v 4 Lakini kabla hawaja lala, wanaume wa mji, wa Sodoma, vijana kwa wazee wakaizunguka nyumba, wanaume wote kutoka kila kona ya mji.
\v 5 Wakamwita Lutu, na kumwambia, "Wale wanaume walioingia kwako usiku wakowapi? watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao."
\s5
\v 6 Lutu akatoka nje na akafunga mlango.
\v 7 Akasema, "Nawasihi, ndugu zangu, msitende uovu.
\v 8 Tazama, nina mabinti wawili ambao hawajawahi kulala na mwanaume yeyote. Nawaomba tafadhari niwalete kwenu, na muwafanyie lolote muonalo kuwa jema machoni penu. Msitende lolote kwa wanaume hawa, kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha dari yangu."
\s5
\v 9 Wakasema, "Ondoka hapa!" Wakasema pia, huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao." Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango.
\s5
\v 10 Lakini wale wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga mlango.
\v 11 Kisha wale wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume waliokuwa nje ya nyumba, vijana na wazee kwa pamoja, kiasi kwamba wakachoka wakati wakiutafuta mlango.
\s5
\v 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je una mtu mwingine yeyote hapa? wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa.
\v 13 Kwa kuwa tunakaribia kuiangamiza sehemu hii, kwa sababu mashitaka dhidi yake mbele ya Yahwe yamezidi kiasi kwamba ametutuma kuuangamiza."
\s5
\v 14 Lutu akatoka na akazungumza na wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake, akawambia, "Ondokeni upesi mahali hapa, kwa kuwa Yahwe anakaribia kuuangamiza mji." Lakini kwa wakwe zake alionekana kuwa anawatania.
\v 15 Alfajiri, malaika wakamsihi Lutu, wakisema, ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili ambao wako hapa, ili kwamba usipotelee katika adhabu ya mji huu."
\s5
\v 16 Lakini akakawia-kawia. Kwa hiyo watu wale wakamshika mkono wake, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa sababu Yahwe alimhurumia. Wakawatoa nje, na kuwaweka nje ya mji.
\v 17 Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, "jiponye nafsi yako! usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali."
\s5
\v 18 Lutu akawambia, "Hapana, tafadhali bwana zangu!
\v 19 Mtumishi wenu amepata kibali machoni pako, na umenionesha wema ulio mkuu kwa kuokoa maisha yangu, lakini sitaweza kutorokea milimani, kwa sababu mabaya yataniwahi na nitakufa.
\v 20 Tazama, ule mji pale uko karibu nijisalimishe pale, na ni mdogo. Tafadhari niacheni nikimbilie pale ( Je Siyo mdogo ule?), na maisha yangu yataokolewa."
\s5
\v 21 Akamwambia, "Sawa, nimekubali ombi hili pia, kwamba sitaangamiza mji ambaoumeutaja.
\v 22 Harakisha! toroka uende pale, kwa kuwa sitafanya chochote mpaka ufike pale." kwa hiyo mji ule ukaitwa Soari.
\s5
\v 23 Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi wakati Lutu alipofika Soari.
\v 24 Kisha Yahwe akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto toka kwa Yahwe mbinguni.
\v 25 Akaharibu miji ile, na bonde lote, na vyote vilivyomo katika miji, na mimea iliyo chipua juu ya ardhi.
\s5
\v 26 Lakini mke wa Lutu aliye kuwa nyuma yake, akatazama nyuma, na akawa nguzo ya chumvi.
\v 27 Abraham akaamuka asubuhi na mapema akaenda mahali alipokuwa amesimama mbele ya Yahwe.
\v 28 Akatazama chini kuelekea Sodoma na Gomora na kuelekea katika nchi yote bondeni. Akaona na tazama, moshi ulikuwauki ukienda juu kutoka chini kama moshi wa tanuru.
\s5
\v 29 Wakati Mungu alipoharibu miji ya bondeni, Mungu akamkumbuka Abraham. Akamtoa Lutu kutoka katika maangamizi alipoangamiza miji ambayo katika hiyo Lutu aliishi.
\s5
\v 30 Lakini Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima akiwa pamoja na binti zake wawili, kwa sababu aliogopa kuishi Soari. Kwa hiyo akaishi pangoni, yeye na binti zake wawili.
\s5
\v 31 Yule wa kwanza akamwambia yule mdogo, "Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali popote wa kulala na sisi kulingana na desturi ya dunia yote.
\v 32 Njoo na tumnyweshe baba yetu mvinyo na tulale naye ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu."
\v 33 Kwa hiyo wakamnywesha baba yako mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka.
\s5
\v 34 Siku iliyo fuata yule wa kwanza akamwambia mdogowake, "Sikiliza, usiku wa jana nililala na baba yangu. Na tumnyweshe mvinyo usiku wa leo pia, na uingie ukalale naye. Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu."
\v 35 Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule pia, na yule mdogo akaenda na akalala naye. Baba yake hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka.
\s5
\v 36 Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.
\v 37 Wa kwanza akazaa mwana wa kiume, na akamwita jina lake Moabu. Akawa ndiye baba wa wamoabu hata leo.
\v 38 Nayule mdogo naye akazaa mwana wa kiume, na akamwita Benami. Huyu ndiye baba wa watu wa Waamoni hata leo.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Abraham akasafiri kutoka pale hadi nchi ya Negebu, na akakaa kati ya Kadeshi na Shuri. Akawa mgeni akiishi Gerari.
\v 2 Abraham akasema kususu mkewe Sara, "ni dada yangu." Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara.
\v 3 Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, "Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu."
\s5
\v 4 Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, "Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki?
\v 5 Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia."
\s5
\v 6 Kisha Mungu akasema naye katika ndoto, "Kweli, ninajua pia kwamba umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako, na pia nilikuzuia usitende dhambi dhidi yangu mimi. Ndiyo maana sikuruhusu umshike.
\v 7 Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujuwe kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika.
\s5
\v 8 Abimeleki akaamka asubuhi na mapema akawaita watumishi wake wote waje kwake. Akawasimulia mambo haya yote, na watu wale wakaogopa sana.
\v 9 Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, "Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa."
\s5
\v 10 Abimeleki akamwambia Abraham, "Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?"
\v 11 Abraham akasema, "Ni kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.'
\v 12 Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu.
\s5
\v 13 Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, "Ni kaka yangu."'''
\v 14 Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham.
\s5
\v 15 Abimeleki akasema, Tazama, Nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapopendezewa."
\v 16 Na kwa Sara akasema, Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki."
\s5
\v 17 Kisha Abraham akaomba kwa Mungu, Na Mungu akamponya Abimeleki, mkewe, na watumwa wake wa kike kiasi kwamba wakaweza kupata watoto.
\v 18 Kwa kuwa Yahwe alikuwa amewafanya wanawake wote wa nyumaba ya Abimeleki kuwa tasa kabisa, kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yahwe akamsikiliza Sara kwa umakini kama alivyo kuwa amemwambia, Yahwe akamfanyia Sara kama alivyo kuwa amemwahidi.
\v 2 Sara akachukua mimba na akamzalia Abraham mtoto wa kiume katika uzee wake, katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia.
\v 3 Abraham akamwita jina mwanawe, ambaye alizaliwa kwake, na Sara, Isaka.
\v 4 Abraham akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza.
\s5
\v 5 Abraham alikuwa na umri wa miaka mia moja wakati mwanawe Isaka anazaliwa kwake.
\v 6 Sara akasema, "Mungu amenifanya nicheke; kila mtu atakaye sikia atacheka pamoja na nami."
\v 7 Pia akasema, "Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto, na sasa kweli nimemzalia mtoto wakiume katika uzee wake!"
\s5
\v 8 Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya, na Abraham akafanya sherehe kubwa katika siku ambayo Isaka aliachishwa.
\v 9 Sara akamwona mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alikuwa amezaliwa kwa Abraham, akidhihaki.
\s5
\v 10 Kwa hiyo akamwambia Abraham, "Mfukuze huyu mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake: kwa kuwa mtoto huyu wa mwanamke mtumwa hawezi kuwa mrithi pamoja na mwanangu Isaka."
\v 11 Jambo hili likamuhuzunisha sana Abraham kwa sababu ya mwanawe.
\s5
\v 12 Lakini Mungu akamwambia Abraham, "Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa.
\v 13 Nitamfanya pia mtoto wa mjakazi kuwa taifa, kwa sababu ni uzao wako."
\s5
\v 14 Abraham akaamka asubuhi na mapema, akachukua mkate na kiriba cha maji, akampatia Hajiri, akiweka juu ya bega lake. Akamtoa kijana akampatia Hajiri na akawaondoa. Hajiri akaondoka akapotea katika jangwa la Beerisheba.
\v 15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba akamtelekeza kijana katika moja ya vichaka.
\v 16 Kisha akaondoka, na akakaa umbali kidogo na yule kijana, umbali kama wa kutupa mshale, kwa vile alisema, "Na nisitazame kifo cha mtoto." Alipokuwa amekaa kumkabili, akapaza sauti yake akalia.
\s5
\v 17 Mungu akasikia kilio cha kijana, na malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, "Nini kinakusumbua? Usiogope, kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha kijana mahali alipo.
\v 18 Inuka msimamishe mtoto, na umtie moyo; kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa."
\s5
\v 19 Kisha Mungu akayafunua macho ya Hajiri, natazama akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji, na akampatia kijana akanywa.
\v 20 Mungu akawa pamoja na kijana, na akakua. Akaishi jangwani akawa mwindaji.
\v 21 Akaishi katka jangwa la Parani, na mama yake akampatia mke kutoka Misri.
\s5
\v 22 Ikawa kwamba katika wakati ule Abimeleki na Fikoli kamanda wa jeshi lake akamwambia Abraham, akisema, "Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo.
\v 23 Sasa niapie kwa Mungu kwamba hutanifanyia baya, wala mwanangu, wala uzao wangu. Onesha kwangu na kwa nchi ambayo umekuwa ukikaa agano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonesha wewe."
\v 24 Abraham akasema, "Nina apa."
\s5
\v 25 Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya.
\v 26 Abimeleki akasema, "Sijui ni nani amefanya jambo hili. Hukuniambia mapema; na sijalisikia ila leo hii."
\v 27 Kwa hiyo Abraham akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki, na wawili hawa wakafanya agano.
\s5
\v 28 Kisha Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba pekeyao.
\v 29 Abimeleki akamwambia Abraham, "Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga pekeyao?"
\v 30 Akajibu, "Hawa wanakondoo wa kike saba utawapokea kutoka mkonono mwangu, ili kwamba uwe ushahidi kwangu, kuwa nichimba kisima hiki."
\s5
\v 31 Kwa hiyo akaita mahali pale Beerisheba, kwa sababu mahali pale wote wawili wali apa kiapo.
\v 32 Walifanya agano hapo Bersheba, kisha Abimeleki na Fikoli, amiri wa jeshi, wakarudi katika nchi ya Wafilisti.
\s5
\v 33 Abraham akapanda mti wa mkwaju katika Beerisheba. Na pale akamwabudu Yahwe, Mungu wa milele.
\v 34 Abraham akasalia kuwa mgeni katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, "Abraham!" Abraham akasema, "Mimi hapa."
\v 2 Kisha Mungu akasema, "Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia."
\v 3 Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.
\s5
\v 4 Siku ya tatu Abraham akatazama juu na akaona mahali pakiwa mbali.
\v 5 Abraham akawambia vijana wake, "kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu."
\v 6 Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja.
\s5
\v 7 Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, "Baba yangu," naye akasema, " Ndiyo mwanangu." Akasema, "Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"
\v 8 Abraham akasema, "Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu." Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.
\s5
\v 9 Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
\v 10 Abraham akanyoosha mkono wake akachukua kisu ili kumuua mwanawe.
\s5
\v 11 Ndipo malaika wa Yahwe akamwita kutoka mbinguni na kusema, "Abraham, Abraham!" naye akasema, "Mimi hapa."
\v 12 Akasema, "usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru, kwa kuwa sasa najua unamcha Mungu, kwa kuona kuwa hukumzuilia mwanao, mwanao wa pekee, kwa ajili yangu."
\s5
\v 13 Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
\v 14 Kwa hiyo Abraham akapaita mahali pale, Yahwe atatoa," na panaitwa hivyo hata leo. "Juu ya mlima wa Yahwe itatolewa."
\s5
\v 15 Malaika wa Yahwe akamwita Abraham kwa mara ya pili kutoka mbinguni
\v 16 na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe, "Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa kwamba kwa kuwa umefanya jambo hili, na hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
\v 17 hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
\s5
\v 18 Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa, kwa sababu umetii sauti yangu."
\v 19 Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba.
\s5
\v 20 Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, "Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori."
\v 21 Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu,
\v 22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli.
\s5
\v 23 Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham.
\v 24 Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.
\v 2 Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.
\s5
\v 3 Kisha Abraham akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa, akanena na watoto wa kiume wa Hethi, akisema,
\v 4 "Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhari nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu."
\s5
\v 5 Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema,
\v 6 "Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako."
\s5
\v 7 Abraham akainuka na kusujudu chini kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi.
\v 8 Akawaambia, akisema, "ikiwa mmekubali mimi kuzika wafu wangu, ndipo nisikilizeni, msihini Efroni mwana wa Sohari kwa ajili yangu.
\v 9 Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia."
\s5
\v 10 Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi, hivyo Efroni Mhiti akamjibu Abraham alipowasikia wana wa Hethi, wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake, akasema,
\v 11 "Hapana, bwana wangu, nisikilize. Ninakupatia shamba na pango ambalo limo ndani yake. Ninakupatia mbele ya wana wa watu wangu. Ninakupatia uzike wafu wako."
\s5
\v 12 Kisha Abraham akasujudu chini mbele ya watu wa nchi ile.
\v 13 Akamwambia Efroni watu wa nchi ile wakisikiliza, akasema, ikiwa uko radhi, tafadhari nisikilize. Nitalipia shamba. Chukua fedha kwangu, na nitazika wafu wangu pale."
\s5
\v 14 Efroni akamjibu Abraham, akisema,
\v 15 "Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako."
\v 16 Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
\s5
\v 17 Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa
\v 18 kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake.
\s5
\v 19 Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
\v 20 Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Basi Abraham alikuwa mzee sana na Yahwe akawa amembariki katika mambo yote.
\v 2 Abraham akamwambia mtumwa wake, ambaye alikuwa mkubwa kuliko wote wa nyumbani mwake na mkuu wa vyote alivyo kuwa navyo."Weka mkono wako chini ya paja langu
\v 3 na nitakufanya uape kwa Yahwe, Mungu wa Mbingu na nchi, kwamba hutampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, miongoni mwao wale nikaao kati yao.
\v 4 Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke."
\s5
\v 5 Yule mtumwa wake akamwambia, "Itakuwaje ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kufuatana nami hadi katika nchi hii? Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka?"
\v 6 Abraham akamwambia, "Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule!
\v 7 Yahwe, Mungu wa mbingu, ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu na kutoka katika nchi ya ndugu zangu, na ambaye aliniahidia kwa kiapo maalumu akisema, 'Nitawapa uzao wako nchi hii,' atatuma malaika wake mbele yako, na utapata mke kwa ajili ya mwanangu kutoka huko.
\s5
\v 8 Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari, ndipo utakuwa huru katika hiki kiapo changu. Cha muhimu tu ni kwamba usije ukamrudisha mwanangu huko."
\v 9 Kwa hiyo mtumwa akaweka mkono wake jini ya paja la Abraham bwana wake, na akaapa kuhusiana na jambo hili.
\s5
\v 10 Mtumwa akachukua ngamia kumi wa bwana wake na akaondoka. Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake. Akaondoka na kwenda katika mkoa wa Aramu Naharaimu, mji wa Nahori.
\v 11 Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji. Ilikuwa jioni wakati ambao wanawake huenda kuchota maji.
\s5
\v 12 Kisha akasema, "Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, anijalie kufanikiwa leo na aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abraham.
\v 13 Tazama, nimesimama hapa karibu na chemchemi ya maji na binti za watu wa mji wanakuja kuteka maji.
\v 14 Na itokee hivi kwamba. Nikimwambia msichana, tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,' na akiniambia, 'Kunywa, na kwamba nitawanywesha ngamia wako pia,' huyo ndiye awe ambaye umemchagulia mtumwa wako Isaka. Kwa njia hii nitajua kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu."
\s5
\v 15 Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham.
\v 16 Msichana huyu alikuwa mzuri na alikuwa bikira. Hapana mwanaume aliye kuwa amekwisha lala naye. Akashuka kisimani na kuujaza mtungi wake, na kupanda juu.
\s5
\v 17 Kisha mtumwa yule akakimbia kumlaki yule msichana, na kusema, "Tafadhari nipatie maji kidogo ya kunywa kutoka katika mtungi wako."
\v 18 Akasema, "kunywa tafadhari bwana wangu," na kwa haraka akatua mtungi wake juu ya mkono wake, na akampatia maji ya kunywa.
\s5
\v 19 Alipokuwa amemaliza kumpatia maji, akasema, "Nitachota maji kwa ajili ya ngamia wako pia, mpaka watakapomaliza kunywa."
\v 20 Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini kwenye chombo cha kunywshea mifugo, kisha akakimbia tena kisimani kuchota maji, na kuwanywesha ngamia wake wote.
\s5
\v 21 Yule mtu akamtazama msichana akiwa kimya kuona kama Yahwe amefanikisha njia yake au la.
\v 22 Ngamia walipomaliza kunywa maji, yule mtu akaleta pete ya pua ya dhahabu yenye uzito wa nusu shekeli, na bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa shekeli kumi,
\v 23 akamuuliza, "wewe ni binti wa nani? Niambie tafadhali, Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako kwa ajili yetu kupumzika usiku?"
\s5
\v 24 Akamwambia, "Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori."
\v 25 Akasema pia, "Tunayo malisho tele na chakula, na iko nafasi kwa ajili yako kulala usiku."
\s5
\v 26 Kisha yume mtu akainama chini na kumwabudu Yahwe.
\v 27 Akasema, "Abarikiwe Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye hakuacha agano lake la uaminifu na kweli yake mbele ya bwana wangu. Kwa vile Yahwe ameniongoza moja kwa moja kwenye nyumba ya ndugu zake bwana wangu."
\s5
\v 28 Kisha yule msichana akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake juu ya mambo yote haya.
\v 29 Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima.
\v 30 Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, "Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia," alikwenda kwa yule mtu, na, Tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani.
\s5
\v 31 Labani akasema, "Njoo, wewe uliye barikiwa na Yahwe. Kwa nini umesimama nje? nimekwisha andaa nyumba, pamoja na mahali kwa ajili ya ngamia."
\v 32 Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba na akashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia. Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa kuosha miguu yake pamoja na miguu ya wale watu aliokuwa pamoja nao.
\s5
\v 33 Wakaandaa chakula mbele yake ale, lakini akasema, "Sitakula mpaka niseme kile ninacho paswa kusema." Kwa hiyo Labani akmwambia, "Sema."
\v 34 Akasema, "Mimi ni mtumwa wa Abraham.
\v 35 Yahwe amembariki sana bwana wangu na amekuwa mtu mkuu. Amempatia mifugo na makundi ya wanyama, fedha, dhahabu, watumwa wa kiume na watumwa wa kike, pamoja na ngamia na punda.
\s5
\v 36 Sara, mke wa bwana wangu, alimzalia mwana bwana wangu alipokuwa mzee, na amempatia mwanawe kila kitu anachomiliki.
\v 37 Bwana wangu aliniapisha, akisema, "Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi.
\v 38 Badala yake, lazima uende kwa familia ya baba yangu, na kwa ndugu zangu, na kupata mke kwa ajili ya mwanangu.'
\s5
\v 39 Nikamwambia bwana wangu, pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami.'
\v 40 Lakini akaniambia, Yahwe, ambaye ninakwenda mbele yake, atatuma malaika wake pamoja nawe na atakufanikisha njia yako, kwamba utapata mke kwa ajili ya mwangu kutoka miongoni mwa ndugu zangu na kutoka katika ukoo wa baba yangu.
\v 41 Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu.
\s5
\v 42 Hivyo nimefika leo kisimani, na nikasema, 'O Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, tafadhari, ikiwa kweli umekusudia kuifanya safari yangu kuwa yenye kufanikiwa -
\v 43 tazama niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji - na iwe kwamba binti ajaye kuchota maji, nitakaye mwambia, "Tafadhari unipatie maji kidoka kutoka kwenye mtungi wako ninywe," mwanamke atakaye niabia,
\v 44 "Kunywa, na nitakuchotea pia maji kwa ajili ya ngamia wako" - na awe ndiye ambaye wewe Yahwe, umemchagulia mtoto wa bwana wangu."
\s5
\v 45 Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.'
\v 46 Ndipo kwa haraka alipoushusha mtungi wake begani mwake na akasema, 'Kunywa, na pia nitawapatia maji ngamia wak.' Kwa hiyo nikanywa, na akawanywesha ngamia pia.
\s5
\v 47 Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake.
\v 48 Kisha nikainama chini nikamwabudu Yahwe, na kumbariki Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye ameniongoza katika njia sahihi kumpata binti wa ndugu za bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.
\s5
\v 49 Kwa hiyo, ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni. Lakini kama sivyo, niambieni, ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto."
\s5
\v 50 Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, "Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri.
\v 51 Tazama, Rebeka yu mbele yako. Mchukue na uende, ili awe mke wa mtoto wa bwana wako, kama Yahwe alivyosema."
\s5
\v 52 Mtumwa wa Abraham aliposikia maneno yao, akainama mwenyewe chini ardhini kwa Yahwe.
\v 53 Mtumwa akaleta vipande vya fedha na vipande vya dhahabu, na nguo, akampatia Rebeka. Akampatia pia kaka yake na mama yake zawadi zenye thamani.
\s5
\v 54 Kisha yeye na watu aliokuwa nao wakala na kunywa. wakakaa pale mpaka usiku, na walipoamka asubuhi, akasema, Niruhusuni niende kwa bwana wangu."
\v 55 Kaka yake na mama yake wakasema, mwache binti abaki nasi kwa siku chache zingine, angalau siku kumi. baada ya hapo anaweza kwenda."
\s5
\v 56 Lakini akawambia, msinizuie, kwa kuwa Yahwe amefanikisha njia yangu. Niruhusuni niende kwa bwana wangu."
\v 57 Wakasema, "Tutamwita binti na kumuuliza."
\v 58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, "Je utakwenda na mtu huyu?" Akajibu, "Nitakwenda."
\s5
\v 59 Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka, pamoja na watumishi wake wa kike, kwenda njiani pamoja na mtumishi wa Abraham na watu wake.
\v 60 Wakambarikia Rebeka, na wakamwambia, "Ndugu yetu, na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu, uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia."
\s5
\v 61 Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake kwa hesabu ya ngamia, na wakamfuata yule mtu. Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao.
\v 62 Nyakati hizo Isaka alikuwa anakaa katika Negebu, na alikuwa tu amerejea kutoka Beerlahairoi.
\s5
\v 63 Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija!
\v 64 Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia.
\v 65 Akamwambia mtumwa, "mtu huyo ni nani anaye tembea shambani akija kutupokea?" Mtumwa akasema, "Ni bwana wangu." Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.
\s5
\v 66 Mtumwa akamwambia Isaka mambo yote ambayo amefanya.
\v 67 Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Abraham akaoa mke mwingine; jina lake aliitwa Ketura.
\v 2 Akamzalia Zimrani, Jokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua.
\v 3 Jokshani akamzaa Sheba na Dedani. Wana wa Dedani walikuwa ni Waashuru, Waletushi, na Waleumi.
\v 4 Wana wa Midiani walikuwa ni Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Hawa wote walikuwa ni wana wa Ketura.
\s5
\v 5 Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo.
\v 6 Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanae.
\s5
\v 7 Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abraham alizoishi, miaka 175.
\v 8 Abraham akapumua pumzi ya mwisho na akafa katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku, na akakusanywa kwa watu wake.
\s5
\v 9 Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre.
\v 10 Shamba hili Abraham alilinunua kwa watoto wa Hethi. Abraham akazikwa pale pamoja na Sara mkewe.
\v 11 Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanae, na Isaka akaishi karibu na Beerlalahairoi.
\s5
\v 12 Na sasa hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, mwana wa Abraham, ambaye Hajiri Mmisri mtumishi wake Sara, alizaa kwa Abraham.
\s5
\v 13 Haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Ishimaeli, kuanzia mzaliwa wa kwanza: Nebayothi - mzaliwa wa kwanza wa Ishimaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
\v 14 Mishma, Duma, Masa,
\v 15 Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi, na Kedema.
\v 16 Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao.
\s5
\v 17 Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake.
\v 18 Walioshi toka Havila mpaka Shuri, ambayo iko karibu na Misri, kuelekea Ashuru. Waliishi kwa uadui kati yao.
\s5
\v 19 Haya ndiyo yalikuwa matukio kumuhusu Isaka, mwana wa Abraham: Abraham alimzaa Isaka.
\v 20 Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami.
\s5
\v 21 Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.
\v 22 Watoto hawa walipokuwa tumboni mwake wakasumbuka, naye akasema, "Kwa nini jambo hili linatokea kwangu mimi?" Akaenda kumuuliza Yahwe kuhusu jambo hili.
\s5
\v 23 Yahwe akamwambia, "Mataifa mawili yako katika tumbo lako, na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako. Taifa moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, na yule mkubwa atamtumikia mdogo.
\s5
\v 24 Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake.
\v 25 Wakwanza akatoka akiwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.
\v 26 Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto.
\s5
\v 27 Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema.
\v 28 Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
\s5
\v 29 Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa.
\v 30 Esau akamwambia Yakobo, "Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!" Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu.
\s5
\v 31 Yakobo akasema, "Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza."
\v 32 Esau akasema, "Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?"
\v 33 Yakobo akasema, "Kwanza uape kwangu mimi," kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo.
\v 34 Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari.
\s5
\v 2 Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, "Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia.
\v 3 Kaa katika nchi hii hii niliyokuambia, nami nitakuwa pamoja nawe na kukubariki; kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote, nami nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
\s5
\v 4 Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote. Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.
\v 5 Nitalifanya hili kwa sababu Ibrahimu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu."
\s5
\v 6 Hivyo Isaka akakaa Gerari.
\v 7 Watu wa eneo hilo walipomwuliza juu ya mke wake, alisema, "Yeye ni dada yangu." Aliogopa kusema, "Yeye ni mke wangu," kwa kuwa alidhani, "Watu wa nchi hii wataniua ili wamchukue Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa uso."
\v 8 Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake.
\s5
\v 9 Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, "Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?" Isaka akamwambia, "Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue."
\v 10 Abimeleki akamwambia, "Ni jambo gani hili ulilotufanyia? Mmojawapo wa watu angeweza bila shaka kulala na mke wako, nawe ungeweza kuleta hatia juu yetu."
\v 11 Hivyo Abimeleki akawaonya watu wote na kusema, "Mtu yeyote atakayemgusa mtu huyu au mke wake atauwawa."
\s5
\v 12 Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo na kuvuna mwaka huo vipimo mia, kwa kuwa Yahwe alimbariki.
\v 13 Mtu huyo akawa tajiri, naye akaongezeka zaidi hata akawa mkuu sana.
\v 14 Alikuwa na kondoo na ngombe na familia kubwa. Wafilisiti wakamwonea wivu.
\s5
\v 15 Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwawamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kwa kuvijaza kifusi.
\v 16 Abimeleki akamwambia Isaka, "Ondoka kati yetu, kwa kuwa wewe una nguvu kuliko sisi."
\v 17 Hivyo Isaka akaondoka pale na kukaa katika bonde la Gerari, na kuishi pale.
\s5
\v 18 Kwa mara nyingine tena Isaka akachimba visima vya maji, vilivyokuwa vimechimbwa siku za Ibrahimu baba yake. Wafilisiti walikuwa wamevizuia baada ya kufa kwake Ibrahimu. Isaka akaviita visima kwa majina aliyokuwa ameviita baba yake.
\s5
\v 19 Watumishi wa Isaka walipochimba katika bonde, wakaona kisima cha maji yaliyokuwakuwa yakibubujika.
\v 20 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka, na kusema, "Haya ni maji yetu."Hivyo Isaka akakiita kisima hicho "Eseki," kwa sababu waligombana naye.
\s5
\v 21 Wakachimba kisima kingine, wakakigombania hicho nacho, hivyo akakiita "Sitina."
\v 22 Akatoka hapo na akachimba kisima kingine, lakini hicho hawakukigombania. Hivyo akakiita Rehobothi, na akasema, "Sasa Yahwe ametufanyia nafasi, na tutafanikiwa katika nchi."
\s5
\v 23 Kisha Isaka akaenda Beersheba.
\v 24 Yahwe akamtokea usiku huohuo na akasema, "Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi nipo pamoja nawe na nitakubariki na kuvidisha vizazi vyako, kwa ajili ya mtumishi wangu Ibrahimu."
\v 25 Isaka akajenga madhabahu pale na akaliita jina la Yahwe. Akapiga hema yake pale, na watumishi wake wakachimba kisima.
\s5
\v 26 Kisha Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi, rafiki yake, na Fikoli, jemedari wa jeshi.
\v 27 Isaka akawambia, "Kwa nini mmekuja kwangu, kwani mlinichukia na kunifukuza kwenu.
\s5
\v 28 Nao wakasema, "Tumeona yakini kwamba Yahwe amekuwa nawe. Hivyo tukaamua kwamba kuwe na kiapo kati yetu, ndiyo, kati yetu nawe. Hivyo na tufanye agano nawe,
\v 29 kwamba hautatudhuru, kama ambavyo sisi hatukukudhuru, na kama sisi tulivyokutendea vema wewe na tumekuacha uondoke kwa amani. Kwa kweli, Yahwe amekubariki."
\s5
\v 30 Hivyo Isaka akawaandalia sherehe, na wakala na kunywa.
\v 31 Wakaamuka mapema asubuhi na wakaapiana kiapo. Kisha Isaka akawaruhusu kuondoka, nao wakamwacha katika amani.
\s5
\v 32 Siku hiyohiyo watumishi wake wakaja na kumwambia juu ya kisima walichokuwa wamekichimba. Wakasema, "Tumeona maji."
\v 33 Akakiita kile kisima Shiba, hivyo jina la mji ule ni Beersheba hata leo.
\s5
\v 34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akajitwalia mke, Yudithi binti Beeri Mhiti, na Basemathi binti Eloni Mhiti.
\v 35 Wakamhuzunisha Isaka na Rebeka.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Isaka alipozeeka na macho yake kuwa mazito kiasi cha kutokuona, alimwita Esau, mwanawe mkubwa, na akamwambia, "Mwanangu. Yeye akasema, "Mimi hapa."
\v 2 Akamwambia, "Tazama, mimi nimezeeka. Sijui siku ya kufa kwangu.
\s5
\v 3 Kwahiyo chukua silaha zako, podo lako na upinde wako, na uende uwandani ukaniwindie mnyama.
\v 4 Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo, uniletee ili nikile na kukubariki kabla sijafa.
\s5
\v 5 Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo.
\v 6 Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, "Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema,
\v 7 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.'
\s5
\v 8 Kwa hiyo sasa, mwanangu, usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza,
\v 9 Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo.
\v 10 Utakipeleka kwa baba yako, ili kwamba akile, na kukubariki kabla hajafa."
\s5
\v 11 Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, "Tazama, Ndugu yangu Esau ni mtu mwenye manyoya, na mimi ni mtu laini.
\v 12 Pengine baba yangu atanigusa, nami nitaonekana kama mdanganyifu kwake. Nami nitajiletea laana badala ya baraka."
\s5
\v 13 Mama yake akamwambia, "Mwanangu, acha laana yoyote iwe juu yangu. Wewe sikiliza sauti yangu, nenda, uniletee."
\v 14 Hivyo Yakobo alikwenda na kuchukua wanambuzi na kuwaleta kwa mama yake, na mama yake akaandaa chakula kitamu, kama alichokipenda baba yake.
\s5
\v 15 Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau, mwanawe mkubwa, alizokuwa nazo nyumbani mwake, na akamvika Yakobo, mwanawe mdogo.
\v 16 Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake na katika sehemu laini za shingo yake.
\v 17 Akaweka katika mikono ya Yakobo kile chakula kitamu na mkate aliokuwa ameuandaa.
\s5
\v 18 Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, "Babangu." Yeye akasema, "Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?"
\v 19 Yakobo akamwambia baba yake, "Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki."
\s5
\v 20 Isaka akamwambia mwanawe, "Imekuwaje umepata kwa haraka hivyo, mwanangu?" Akasema, "Ni kwa sababu Yahwe Mungu wako ameniletea."
\v 21 Isaka akamwambia Yakobo, "Njoo karibu nami, ili nikuguse, mwanangu, ili nijue kama kweli wewe ni mwanangu Esau au hapana."
\s5
\v 22 Yakobo akamkaribia Isaka baba yake; na Isaka akamgusa na kusema, "Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mkikono ya Esau."
\v 23 Isaka hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na manyoya, kama mikono ya Esau ndugu yake, hivyo Isaka akambariki."
\s5
\v 24 Akasema, "Wewe kweli ni mwanangu Esau?" Naye akasema, "Ni mimi."
\v 25 Isaka akasema, "Kilete chakula kwangu, na nile mawindo yako, ili nikubariki." Yakobo akakileta chakula kwake. Isaka akala, na Yakobo akamletea mvinyo, akanywa.
\s5
\v 26 Kisha Isaka baba yake akamwambia, "Sogea karibu nami na unibusu, mwanangu."
\v 27 Yakobo akasogea na kumbusu, naye akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki. Akasema, "Tazama, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilolibariki Yahwe.
\s5
\v 28 Mungu akupe sehemu ya umande wa mbinguni, sehemu ya unono wa nchi, na wingi wa nafaka na mvinyo mpya.
\s5
\v 29 Watu na wakutumikie na mataifa yainame chini yako. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wainame chini yako. Kila anayekulaani na alaaniwe; na kila anayekubariki abarikiwe."
\s5
\v 30 Mara Isaka alipomaliza kumbariki Yakobo, na Yakobo ndo ametoka mbele ya Isaka baba yake, Esau ndugu yake akaja kutoka kuwinda.
\v 31 Yeye pia akaandaa chakula kitamu na kukileta kwa baba yake. Akamwambia baba yake, "Baba, inuka na ule baadhi ya mawindo ya mwanao, ili uweze kunibariki."
\s5
\v 32 Isaka baba yake akamwambia, "U nani wewe? Akasema, "Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza."
\v 33 Isaka akatetemeka sana na kusema, "Alikuwa nani aliyewinda mawindo nakuniletea? Nilikula chote kabla haujaja, nami nimembariki. Atabarikiwa, kwa kweli."
\s5
\v 34 Esau aliposikia maneno ya baba yake, akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana, na akamwambia baba yake, "Unibariki nami, mimi pia, babangu."
\v 35 Isaka akasema, "Ndugu yako alikuja hapa kwa hila na amechukua baraka yako."
\s5
\v 36 Esau akasema, "Je hakuitwa Yakobo kwa haki? Kwa maana amenidanganya mara mbili hizi. Alichukua haki ya uzaliwa wangu wa kwanza, na tazama, sasa amechukua baraka yangu." Na akasema, "Je haukuniachia baraka?
\v 37 Isaka akajibu na kumwambia Esau, "Tazama, nimemfanya kuwa bwana wako, na nimempa ndugu zake kuwa watumishi wake. Na nimempa nafaka na divai. Je nikufanyie nini mwanangu?
\s5
\v 38 Esau akamwambia babaye, "Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu? Nibariki nami, hata mimi pia, babangu." Esau akalia kwa sauti.
\s5
\v 39 Isaka baba yake akajibu na kumwambia, "Tazama, mahali unapoishi patakuwa mbali na utajiri wa nchi, mbali na umande juu angani.
\v 40 Kwa upanga wako utaishi, nawe utamtumikia ndugu yako. lakini utakapoasi, utaiondoa nira yake shingoni mwako."
\s5
\v 41 Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka ambayo baba yake alimpa. Esau akajisemea moyoni, "Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia; baada ya hapo nitamwua Yakobo ndugu yangu."
\v 42 Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa. Hivyo akatuma na kumwita Yakobo mwanawe mdogo na kumwambia, "Tazama, Esau ndugu yako anajifariji juu yako kwa kupanga kukuuwa.
\s5
\v 43 Kwa hiyo sasa, mwanangu, unisikie na kukimbilia kwa Labani, ndugu yangu, huko Harani.
\v 44 Ukae naye kitambo, mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua,
\v 45 hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea, na kusahau ulivyomtenda. Kisha nitatuma na kukurudisha kutoka pale. Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja?
\s5
\v 46 Rebeka akamwambia Isaka, "Nimechoka na maisha kwa sababu ya hawa binti za Hethi. Ikiwa Yakobo atachukua mmojawapo wa binti wa Hethi kuwa mkewe, kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi, maisha yatakuwa na maana gani kwangu?"
\s5
\c 28
\p
\v 1 Isaka akamwita Yakobo, akambariki, na kumwagiza, "Usichukuwe mwanamke katika wanawake wa Kikanaani.
\v 2 Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako.
\s5
\v 3 Mungu Mwenyezi na akubariki, akupe uzao na akuzidishe, hata uwe wingi wa watu.
\v 4 Na akupe baraka ya Ibrahimu, wewe, na uzao wako baada yako, kwamba uweze kumilki nchi ambapo umekuwa ukiishi, ambayo Mungu alimpa Ibrahimu."
\s5
\v 5 Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
\s5
\v 6 Basi Esau alipoona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, "Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani."
\v 7 Esau pia akaona kwamba Yakobo alikuwa amemtii baba yake na mama yake, na alikuwa amekwenda Padani Aramu.
\s5
\v 8 Esau akaona kwamba wanawake wa Kanaani hawakumpendeza Isaka baba yake.
\v 9 Hivyo akaenda kwa Ishmaeli, na kuchukua, mbali na wake aliokuwa nao, Mahalathi binti Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, dada wa Nebayothi, kuwa mke wake.
\s5
\v 10 Yakobo akatoka Beersheba na akaelekea Harani.
\v 11 Akaja mahali fulani na akakaa pale usiku kucha, kwa kuwa jua lilikuwa limekuchwa. Akachukua mojawapo ya mawe katika eneo hilo, akaliweka chini ya kichwa chake, na akalala usingizi katika eneo hilo.
\s5
\v 12 Akaota na kuona ngazi imewekwa juu ya nchi. Ncha yake ilifika hata mbinguni na malaika wa Mungu walikuwa wakishuka na kupanda juu yake.
\v 13 Tazama, Yahwe amesimama juu yake na kusema, "Mimi ni Yahwe, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi uliyolala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.
\s5
\v 14 Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi, na utaenea mbali kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini. Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa.
\v 15 Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi."
\s5
\v 16 Yakobo akaamka katika usingizi, na akasema, "Hakika Yahwe yupo mahali hapa, sikujua hili."
\v 17 Akaogopa na kusema, "Eneo hili linatisha kama nini! Hili sio kingine zaidi ya nyumba ya Mungu. Hili ni lango la mbinguni."
\s5
\v 18 Yakobo akaamka mapema asubuhi na akachukua jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake. Akaliweka kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.
\v 19 Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu.
\s5
\v 20 Yakobo akatoa nadhiri, kusema, "Ikiwa Mungu atakuwa nami na atanilinda katika njia nipitayo, na atanipa mkate wa kula, na mavazi ya kuvaa,
\v 21 hata nikarudi salama katika nyumba ya baba yangu, ndipo Yahwe atakapokuwa Mungu wangu.
\v 22 Kisha jiwe hili nililoliweka kama nguzo litakuwa jiwe takatifu. Kutoka katika kila utakachonipa, kwa hakika nitakupa tena sehemu ya kumi."
\s5
\c 29
\p
\v 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika katika nchi ya watu wa mashariki.
\v 2 Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa.
\v 3 Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.
\s5
\v 4 Yakobo akawambia, "Ndugu zangu, ninyi mnatokea wapi?" nao wakasema, "Tunatoka Harani."
\v 5 Akawambia, "Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?" Wakasema, "Tunamfahamu."
\v 6 Akawambia, "Je hajambo?" Wakasema, "Hajambo, na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo."
\s5
\v 7 Yakobo akasema, "Tazama, ni mchana. Siyo wakati wa kukusanya kondoo pamoja. Mnapaswa kuwanywesha kondoo na kisha mkaenda na kuwaacha wachunge."
\v 8 Wakamwambia, "Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja. Ndipo wanaume watakapovingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na ndipo tutakapowanywesha kondoo."
\s5
\v 9 Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga.
\v 10 Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.
\s5
\v 11 Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti.
\v 12 Yakobo akamwambia Raheli kwamba alikuwa ni ndugu wa baba yake, na kwamba alikuwa mwana wa Rebeka. Kisha yeye akakimbia kumwambia baba yake.
\s5
\v 13 Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo mwana wa dada yake, akaenda kukutana naye, akamkumbatia, akambusu, na kumleta nyumbani kwake. Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote.
\v 14 Labani akamwambia, "Kwa hakika wewe ni mfupa wangu na nyama yangu." Kisha Yakobo akakaa naye kama mwezi mmoja.
\s5
\v 15 Kisha Labani akamwambia Yakobo, "Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje?
\v 16 Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli.
\v 17 Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano.
\v 18 Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, "Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo."
\s5
\v 19 Labani akasema, Itakuwa vema kukupa wewe, kuliko kumpa mtu mwingine. Kaa nami."
\v 20 Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake.
\s5
\v 21 Kisha Yakobo akamwambia Labani, "Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe!
\v 22 Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe.
\s5
\v 23 Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye.
\v 24 Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea.
\v 25 Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, "Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa?
\s5
\v 26 Labani akamwambia, "Siyo utamaduni wetu kumtoa bindi mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza.
\v 27 Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba."
\s5
\v 28 Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.
\v 29 Lakini pia Labani akampa Raheli binti yake Bilha, kuwa mjakazi wake.
\v 30 Hivyo Yakobo akalala na Raheli, pia, lakini akampenda Raheli zaidi ya Lea. Hivyo Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka saba mingine.
\s5
\v 31 Yahwe akaona kwamba Lea hakupendwa, hivyo akalifungua tumbo lake, lakini Raheli hakuwa na mtoto.
\v 32 Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, "Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda."
\s5
\v 33 Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Kwa sababu Yahwe amesikia kwamba sipendwi, kwa hiyo amenipa mwana mwingine," na akamwita Simoni.
\v 34 Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Wakati huu mme wangu ataungana nami, kwa kuwa nimemzalia wana watatu." Kwa hiyo akaitwa Lawi.
\s5
\v 35 Akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Wakati huu nitamsifu Yahwe." Kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; kisha akaacha kuzaa watoto.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, "Nipe watoto, sivyo nitakufa."
\v 2 Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, "Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?
\s5
\v 3 Akasema, "Tazama, kuna mjakazi wangu Bilha. Lala naye, hivyo aweze kuzaa watoto magotini pangu, nami nitapata watoto kwake.
\v 4 Hivyo akampa Bilha mjakazi kama mke wake, na Yakobo akalala naye.
\s5
\v 5 Bilha akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana.
\v 6 Kisha Raheli akasema, "Mungu ameamua kwa faida yangu. Ameyasikiliza maombi yangu na kunipa mwana." Kwa sababu hiyo akamwita jina lake Dani
\s5
\v 7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili.
\v 8 Raheli akasema, "Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu na kushinda." Akamwita jina lake Naftali.
\s5
\v 9 Lea alipoona kwamba ameacha kuzaa, akamchukua Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo kama mke wake.
\v 10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.
\v 11 Lea akasema, "Hii ni bahati njema!" Hivyo akamwita jina lake Gadi.
\s5
\v 12 Kisha Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
\v 13 Lea akasema, "Nina furaha! Kwa maana mabinti wataniita furaha." Hivyo akamwita jina lake Asheri.
\s5
\v 14 Siku za mavuno ya ngano Rubeni akaenda shambani na kuona tunguja. Akazileta kwa mama yake. Kisha Raheli akamwambia Lea, "Nipe baadhi ya tunguja za mwanao."
\v 15 Lea akamwambia, "Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, "Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao.
\s5
\v 16 Jioni Yakobo akaja kutoka uwandani. Lea akaenda kumlaki na kusema, "Leo usiku utalala nami, kwani nimekuajiri kwa tunguja za mwanangu." Hivyo Yakobo akalala na Lea usiku huo.
\v 17 Mungu akamsikia Lea, na akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana wa tano.
\v 18 Lea akasema, "Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nilimpa mme wangu mjakazi wangu." Akamwita jina lake Isakari.
\s5
\v 19 Lea akashika mimba tena na kuzaa mwana wa tano kwa Yakobo.
\v 20 Lea akasema, "Mungu amenipa zawadi njema. Sasa mme wangu ataniheshimu, kwa sababu nimemzalia wana sita." Akamwita jina lake Zabuloni.
\v 21 Baadaye akazaa binti na kumwita jina lake Dina.
\s5
\v 22 Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba.
\v 23 Akashika mimba na kuzaa mwana. Akasema, "Mungu ameiondoa aibu yangu."
\v 24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Yahwe ameniongeza mwana mwingine."
\s5
\v 25 Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, "Niache niande, ili kwamba niende nyumbani kwetu na katika nchi yangu.
\v 26 Nipe wake zangu na watoto wangu niliokutumikia kwa ajili yao, na uniache niondoke, kwani unafahamu nilivyokutumikia.
\s5
\v 27 Labani akamwambia, "Ikiwa nimepata kibali machoni pako, subiri, kwa sababu nimejifunza kwa kutumia uaguzi kwamba Yahwe amenibariki kwa ajili yako."
\v 28 Kisha akasema, "Taja ujira wako, nami nitalipa."
\s5
\v 29 Yakobo akamwambia, "Unajua nilivyokutumikia, na jinsi ambavyo mifugo wako wamekuwa nami.
\v 30 Kwani walikuwa wachache kabla sijaja, na wameongezeka kwa wingi. Popote nilipokutumikia Mungu amekubariki. Je ni lini mimi nitaandaa kwa ajili ya nyumba yangu pia?"
\s5
\v 31 Hivyo Labani akasema, "Je nikulipe nini? Yakobo akasema, 'Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza.
\v 32 Niache nipite kati ya kundi lako lote leo, kwa kuondoa kila kondoo mwenye milia na mabaka, na kila kondoo mweusi kati yao, na kati ya wenye mabaka na milia katika mbuzi. Hawa watakuwa ujira wangu.
\s5
\v 33 Uadilifu wangu utashuhudia kwa ajili yangu hapo baadaye, utakapokuja kuangalia ujira wangu. Kila ambaye hana milia na hana madoa miongoni mwa mbuzi, na mweusi kati ya kondoo, ikiwa wataonekana kwangu, watahesabiwa kuwa wameibwa."
\v 34 Labani akasema, "Nakubali. Na iwe kama yalivyo maneno yako."
\s5
\v 35 Siku hiyo Labani akaondoa mabeberu yaliyokuwa na milia na madoa, na majike ya mbuzi yaliyokuwa na milia na madoa, kila aliyekuwa mweupe, na weusi wote katika mbuzi, akawakabidhi katika mikono ya wanaye.
\v 36 Pia Labani akaweka safari ya siku tatu kati yake na Yakobo. Hivyo Yakobo akabaki kuchunga wale kondoo wa Labani waliosalia.
\s5
\v 37 Yakobo akachukua matawi mabichi yaliyokatwa ya mipopla, mlozi na mwaramoni mbichi akatoa maganda ili michilizi myeupe ionekane, na akaifanya sehemu nyeupe ya ndani ya mti iliyokuwa ndani ya fito ionekane.
\v 38 Kisha akaziweka fito alizokuwa amezibambua mbele ya makundi ya kondoo, mbele ya mabirika yakunyweshea walipokuja kunywa maji. Wakashika mimba walipokuja kunywa maji.
\s5
\v 39 Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa.
\v 40 Yakobo akawatenga hawa wanakondoo, lakini akawafanya waliosalia kuelekea wanyama wenye milia na kondoo weusi wote katika kundi la Labani. Kisha akayatenga makundi yake mwenyewe pekee na hakuwaweka pamoja na wale wa Labani.
\s5
\v 41 Pindi kondoo wenye nguvu katika kundi walipopandana, Yakobo alilaza fito katika mabirika ya maji mbele ya macho ya kundi, ili kwamba washike mimba kati ya fito.
\v 42 Lakini wakati waliodhaifu walipokuja, hakuweka fito mbele yao. Hivyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wenye nguvu wakawa wa Yakobo.
\s5
\v 43 Mtu huyo akastawi sana. Akawa na kundi kubwa la kondoo, wajakazi na wajoli, ngamia na punda.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, "Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu, na ni kutoka katika mali ya baba yetu amepata utajiri wake."
\v 2 Yakobo akaona mwonekano katika uso wa Labani. Akaona kwamba nia yake imebadilika.
\v 3 Kisha Yahwe akamwambia Yakobo, "Rudi katika nchi ya baba zako na ya ndugu zako, nami nitakuwa nawe."
\s5
\v 4 Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwandani katika kundi lake la kondoo
\v 5 naye akawambia, "Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa nami.
\v 6 Nanyi mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu.
\s5
\v 7 Baba yenu amenidanganya na amebadilisha ujira wangu mara kumi, lakini Mungu hakumruhusu kunidhuru.
\v 8 Ikiwa alisema, 'Wanyama wenye mabaka watakuwa ujira wako,' ndipo kondoo wote walipozaa watoto wenye mabaka. Na aliposema, wenye milia watakuwa ujira wako,' ndipo kundi lote lilipozaa watoto wenye milia.
\v 9 Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi.
\s5
\v 10 Wakati fulani wa majira ya kupandana, niliona katika ndoto mabeberu yaliyowapanda kundi. Mabeberu yalikuwa ya milia, mabaka na madoa.
\v 11 Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.'
\s5
\v 12 Akasema, 'Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea.
\v 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa.
\s5
\v 14 Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, "Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu?
\v 15 Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu.
\v 16 Mali zote ambazo sasa Mungu amemnyang'anya baba yetu ni zetu na watoto wetu. Sasa basi, lolote Mungu alilokuambia, fanya.
\s5
\v 17 Kisha Yakobo akainuka na kuwapandisha wanawe na wakeze kwenye ngamia.
\v 18 Akawaongoza mifugo wake wote mbele yake, pamoja na mali zake zote, wakiwemo wanyama aliowapata huko Padani Aramu. Kisha akaenda kuelekea kwa Isaka baba yake katika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 19 Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake, Raheli akaiba miungu ya nyumba ya baba yake.
\v 20 Yakobo pia akamdanganya Labani Mwarami, kwa kutomtaarifu kwamba anaondoka.
\v 21 Hivyo akaondoka na vyote alivyokuwa navyo na kwa haraka akavuka mto, na akaenda kuelekea nchi ya vilima ya Gileadi.
\s5
\v 22 Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia.
\v 23 Hivyo akawachukua ndugu zake pamoja naye na kumfuatia kwa safari ya siku saba. Akampata katika nchi ya vilima ya Gileadi.
\s5
\v 24 Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, "Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya."
\v 25 Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi.
\s5
\v 26 Labani akamwambia Yakobo, "Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita?
\v 27 Kwa nini umekimbia kwa siri na kunihadaa kwa kutokuniambia? Ningekuruhusu uondoke kwa sherehe na kwa nyimbo, kwa matari na vinubi.
\v 28 Haukuniacha niwabusu wajukuu wangu na binti zangu kwa kuwaaga. Basi umefanya upumbavu.
\s5
\v 29 Iko katika uwezo wangu kukudhuru, lakini Mungu wa baba yako alisema nami usiku wa leo na kuniambia, 'Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari.'
\v 30 Na sasa, umeondoka kwa sababu umeitamani sana nyumba ya baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?
\s5
\v 31 Yakobo akajibu na kumwambia Labani, "Ni kwa sababu niliogopa na kudhani kuwa ungeninyang'anya binti zako kwa nguvu ndiyo maana nikaondoka kwa siri.
\v 32 Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi. Mbele ya ndugu zetu, onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue." Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba.
\s5
\v 33 Labani akaingia katika hema ya Yakobo, katika hema ya Lea, na katika hema za wale wajakazi wawili, lakini hakuviona. Akatoka katika hema ya Lea na kuingia katika hema ya Raheli.
\s5
\v 34 Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona.
\v 35 Akamwambia baba yake, "Usikasirike, bwana wangu, kwamba siwezi kusimama mbele yako, kwani nipo katika kipindi changu." Hivyo akatafuta lakini hakuiona miungu ya nyumbani mwake.
\s5
\v 36 Yakobo akakasirika na kuojiana na Labani. Akamwambia, "Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?
\v 37 Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili.
\s5
\v 38 Kwa miaka ishirini nimekuwa nawe. Kondoo wako na mbuzi wako hawakutoa mimba, wala sikula dume lolote la kondoo katika wanyama wako.
\v 39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea. Badala yake, nilichukua upotevu huo, kwamba wameibwa mchana au usiku.
\v 40 Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi.
\s5
\v 41 Miaka hii ishirini nimekuwa katika nyumba yako. Nilikufanyia kazi miaka kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya wanyama wako. Umebadili ujira wangu mara kumi.
\v 42 Isipokuwa Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu, yule Isaka anayemwofu, amekuwa nami, bila shaka sasa ungenipeleka mikono mitupu. Mungu ameliona teso langu na jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii, na hivyo akakukemea usiku wa leo.
\s5
\v 43 Labani akajibu na kumwambia Yakobo, "Mabinti hawa ni mabinti zangu, wajukuu ni wajukuu wangu, na wanyama ni wanyama wangu. Yote uyaonayo ni yangu. Lakini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa?
\v 44 Hivyo sasa, na tufanye agano, wewe nami, na liwe shahidi kati yangu nawe."
\s5
\v 45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe na kuliweka kama nguzo.
\v 46 Yakobo akawambia ndugu zake, "Kusanyeni mawe." Hivyo wakachukua mawe na kufanya rundo. Kisha wakala pale kati ya lile rundo.
\v 47 Labani aliliita Yega Saha Dutha, lakini Yakobo akaiita Galeedi
\s5
\v 48 Labani akasema, "Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo." Kwa hiyo jina lake likaitwa Galedi.
\v 49 Inaitwa pia Mispa, kwa sababu Labani alisema, "Yahwe na atuangalie mimi nawe, tunapokuwa hatuonani.
\v 50 Ikiwa utawatesa binti zangu, au ikiwa utachukua wanawake wengine mbali na binti zangu, japokuwa hakuna mwingine yupo nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati yangu nawe."
\s5
\v 51 Labani akamwambia Yakobo, Tazama rundo hili, na tazama nguzo, nililoliweka kati yako nami.
\v 52 Rundo hili ni shahidi, na nguzo ni shahidi, kwamba sitapita rundo hili kuja kwako, na kwamba wewe hautapita rundo hili kuja kwangu, kwa madhara.
\v 53 Mungu wa Ibrahimu, na mungu wa Nahori, miungu ya baba zao, waamue kati yetu."Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.
\s5
\v 54 Yakobo akatoa sadaka juu ya mlima na akawaita ndugu zake kula chakula. Walikula na kukaa usiku kucha juu ya mlima.
\v 55 Labani akaamka asubuhi na mapema, akawabusu wajuu zake na binti zake na kuwabariki. Kisha Labani akaondoka na kurudi kwake.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Yakobo pia akaendelea na safari yake, na malaika wa Mungu wakakutana naye.
\v 2 Yakobo alipowaona, akasema, "Hii ni kambi ya Mungu," hivyo akapaita mahali pale Mahanaimu.
\s5
\v 3 Yakobo akatuma wajumbe mbele yake waende kwa Esau ndugu yake katika nchi ya Seiri, katika eneo la Edomu.
\v 4 Aliwaagiza, kusema, "Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: 'Nimekuwa nikikaa na Labani, naye amekawilisha kurudi kwangu hata sasa.
\v 5 Nina ng'ombe, punda, na kondoo, wajori na wajakazi. Nimetuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili kwamba nipate kibali mbele zako."
\s5
\v 6 Wajumbe wakarudi kwa Yakobo na kusema, "Tulikwenda kwa Esau ndugu yako. Anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye."
\v 7 Ndipo Yakobo alipoogopa sana na kutaabika. Hivyo akagawanya watu aliokuwa nao katika kambi mbili, na kondoo pia, mbuzi na ngamia.
\v 8 Akasema, "Ikiwa Esau ataishambulia kambi moja, ndipo kambi nyingine itakaposalimika."
\s5
\v 9 Yakobo akasema, "Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe, uliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha,'
\v 10 Mimi sistahili matendo yako yote ya agano la uaminifu na ustahilifu wote uliomfanyia mtumishi wako. Kwa maana nilikuwa na fimbo tu nilipovuka mto huu wa Yordani, na sasa nimekuwa matuo mawili.
\s5
\v 11 Tafadhari niokoe kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau, kwa maana namwogopa, kwamba atakuja na kunishambulia mimi na wamama na watoto.
\v 12 Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari, ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake."
\s5
\v 13 Yakobo akakaa pale usiku huo. Akachukua baadhi ya alivyokuwa navyo kama zawadi kwa Esau, ndugu yake:
\v 14 mbuzi majike mia mbili na mabeberu ishirini, kondoo majike mia mbili na madume ya kondoo ishirini,
\v 15 ngamia wakamwao thelathini na wana wao, ng'ombe madume arobaini na madume kumi ya ng'ombe, punda wa kike ishirini na madume yake ishirini.
\v 16 Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake. Akawambia watumishi, "Tangulieni mbele yangu na mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama."
\s5
\v 17 Akamwagiza mtumishi wa kwanza, akisema, "Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, akasema, 'Ninyi ni wa nani? Mnakwenda wapi? Na wanyama hawa mbele yenu ni wa nani?
\v 18 Ndipo umwambie, 'Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu."
\s5
\v 19 Yakobo akatoa maelekezo kwa kundi la pili pia, la tatu, na watu wote walioyafuata makundi ya wanyama. Akasema, mseme vilevile kwa Esau mtakapokutana naye.
\v 20 Mnapaswa pia kusema, 'mtumwa wako Yakobo pia anakuja nyuma yetu." Kwani alifikiri, "nitamtuliza Esau kwa zawadi nilizozituma mbele yangu. Kisha baadaye, nitakapomwona, bila shaka atanipokea."
\v 21 Hivyo zawadi zikatangulia mbele yake. Yeye mwenyewe akakaa kambini usiku huo
\s5
\v 22 Yakobo akaamka wakati wa usiku, na akawachukua wakeze, wajakazi wake na wanaye kumi na wawili. Akawawavusha kijito cha Yaboki.
\v 23 Kwa njia hii akawapeleka kupitia chemichemi pamoja na mali yake yote.
\s5
\v 24 Yakobo akaachwa peke yake, na mtu akashindana naya mpaka alfajiri.
\v 25 Mtu yule alipoona kwamba hawezi kumshinda, akalipiga paja lake. Paja la Yakobo likatenguka alipokuwa akishindana naye.
\v 26 Yule mtu akasema, "Niache niende, kwani kunakucha." Yakobo akasema, sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki."
\s5
\v 27 Yule mtu akamwuliza, "Jina lako ni nani?" Yakobo akasema, "Yakobo." Yule mtu akasema,
\v 28 "Jina lako halitakuwa Yakobo tena, ila Israeli. Kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu na umeshinda."
\s5
\v 29 Yakobo akamwambia, "Tafadhari niambie jina lako." Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?" Kisha akambariki pale.
\v 30 Yakobo akapaita mahali pale Penieli kwani alisema, "Nimemwona Mungu uso kwa uso, na maisha yangu yamesalimika."
\s5
\v 31 Jua likatoka wakati Yakobo anaipita Penieli. Alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake.
\v 32 Ndiyo maana wana wa Israeli hawali kano ya paja iliyopo katika nyonga ya paja, kwa sababu yule mtu aliziumiza hizo kano alipotegua paja la Yakobo.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Yakobo akainua macho yake na, tazama, Esau alikuwa anakuja, na alikuwa na watu mia nne pamoja naye. Yakobo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli, na wale wajakazi wawili.
\v 2 Kisha akawaweka wajakazi na wanao mbele, wakifuatiwa na Lea na watoto wake, Raheli na Yusufu wakafuata mwisho wa wote.
\v 3 Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao. Akasujudu mara saba kuelekea ardhi, hata alipomkaribia ndugu yake.
\s5
\v 4 Esau akakimbia kumlaki, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu. Kisha wakalia.
\v 5 Esau alipoinua macho, aliona wanawake na watoto. Akauliza, "Hawa watu pamoja nawe ni kinanani?" Yakobo akasema, Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema."
\s5
\v 6 Kisha wajakazi wakakaribia pamoja na watoto wao, nao wakasujudia.
\v 7 Akafuata Lea pia na watoto wake wakaja na kusujudia. Mwisho Yusufu na Raheli wakaja na kusujudia.
\v 8 Esau akasema, Unamaanisha nini kwa makundi haya yote niliyokutana nayo?" Yakobo akasema, "Kutafuta kibali mbele za bwana wangu.
\s5
\v 9 Esau akasema, "Ninayo ya kutosha, ndugu yangu. Tunza uliyonayo kwa ajili yako mwenyewe."
\v 10 Yakobo akasema, "Hapana, tafadhari, ikiwa nimeona kibali mbele zako, basi upokee zawadi yangu kutoka mkononi mwangu, na ni kama kuona uso wa Mungu, na umenipokea.
\v 11 Tafadhari pokea zawadi yangu uliyoletewa, kwa sababu Mungu amenitendea kwa neema, na kwa sababu ninavyo vya kutosha." Hivyo Yakobo akamsihi, na Esau akamkubali.
\s5
\v 12 Kisha Esau akasema, "Haya na tuondoke. Nitakutangulia."
\v 13 Yakobo akamwambia, "Bwana wangu anajua kwamba watoto ni wadogo, na kwamba kondoo na ng'ombe wananyonyesha ndama wao. Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moja, wanyama wote watakufa.
\v 14 Tafadhari bwana wangu na amtangulie mtumishi wake. Nitasafiri polopole, kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu, na kadili ya watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri."
\s5
\v 15 Esau akasema, haya nikuachie baadhi ya watu wangu waliopamoja nami." Yakobo akasema, "Kwa nini kufanya hivyo? Bwana wangu amekuwa mkalimu kwangu kiasi cha kutosha."
\v 16 Hivyo Esau akaanza kurudi Seiri.
\v 17 Yakobo akasafiri kuelekea Sukothi, akajijengea nyumba, na akafanya mazizi kwa ajili ya mifugo wake. Hivyo jina la eneo linaitwa Sukothi.
\s5
\v 18 Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, akafika salama katika mji wa Shekemu, uliyo katika nchi ya Kanaani. Akapiga kambi karibu na mji.
\v 19 Kisha akanunu sehemu ya ardhi alipokuwa ameweka hema yake kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha.
\v 20 Akajenga madhabahu pale na kuiita El Elohe Israeli.
\s5
\c 34
\p
\v 1 Basi Dina, Binti wa Lea aliyemzalia Yakobo, akaenda kuwaona wasichana wa nchi.
\v 2 Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mwana mfalme wa nchi, akamwona na akamkamata kwa nguvu na kulala naye.
\v 3 Akavutiwa na Dina, binti Yakobo. Akampenda msichana na kuongea naye kwa upole.
\s5
\v 4 Shekemu akamwambia Hamori baba yeke, kusema, "Nipe msichana huyu kuwa mke wangu."
\v 5 Basi Yakobo akasikia kwamba alikuwa amemchafua Dina binti yake. Wanawe walikuwa pamoja na wanyama uwandani, hivyo Yakaobo akawangoja hata walipokuja.
\s5
\v 6 Hamori baba wa Shekemu akaenda kuongea na Yakobo.
\v 7 Wana wa Yakobo waliposikia neno hili wakaja kutoka uwandani. Watu hawa walichukizwa sana. Walikasirika sana kwa sababu alikuwa amemwaibisha Israeli kwa kumlazimisha binti wa Yakobo, kwa maana jambo kama hilo halikupasa kutendeka.
\s5
\v 8 Hamori akaongea nao, akisema, "Shekemu mwanangu anampenda binti yenu. Tafadhari mpeni kuwa mke wake.
\v 9 Mwoane nasi, tupeni binti zenu, na mjichukulie binti zetu kwa ajili yenu wenyewe.
\v 10 Mtaishi nasi, na nchi itakuwa wazi kwa ajili yenu kufanya biashara humo, na kupata mali."
\s5
\v 11 Shekemu akamwambia baba yake na ndugu zake, "Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa.
\v 12 Niambieni kiasi kikubwa chochote cha mahari na zawadi kama mtakavyo, nami nitatoa chochote msemacho, lakini mnipe msichana kuwa mke wangu."
\v 13 Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila, kwa sababu Shekemu alikuwa amemnajisi Dina dada yao.
\s5
\v 14 Wakawambia, "Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu mtu yeyote ambaye hajatailiwa; kwani hiyo ni aibu kwetu.
\v 15 Kwa sharti hili peke yake tutakubaliana nanyi: iwapo mtatailiwa kama sisi, ikiwa kila mtu mme miongoni mwenu atatailiwa.
\v 16 Ndipo tutakapowapa binti zetu, nasi tutachukua binti zenu kwetu sisi wenyewe, na tutaishi nanyi na kuwa wamoja.
\v 17 Lakini kama hamtusikilizi na kutailiwa, ndipo tutakapomchukua dada yetu na kuondoka.
\s5
\v 18 Maneno yao yakawafurahisha Hamori na Shekemu mwanaye.
\v 19 Kijana hakukawia kufanya walichokisema, kwa maana alipendezwa na binti Yakobo, na kwa sababu alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika nyumba ya babaye.
\s5
\v 20 Hamori na Shekemu mwanaye wakaenda katika lango la mji wao na kuongea na watu wa mji, kusema,
\v 21 "Watu hawa wanaamani nasi, hivyo na waishi katika nchi na kufanya biashara humo kwa maana, kweli, nchi ni kubwa ya kuwatosha. Haya na tuwachukue binti zao kuwa wake, nasi tuwape binti zetu.
\s5
\v 22 Kwa shariti hili pekee watu hawa wanakubali kuishi nasi na kuwa wamoja: ikiwa kila mwanamme miongoni mwetu atatailiwa, kama wao.
\v 23 Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu? Haya na tukubaliane nao, nao wataishi kati yetu."
\s5
\v 24 Watu wote wa mji wakamsikiliza Hamori na Shekemu, mwanaye. Kila mwanamme akatailiwa.
\v 25 Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakauwa wanamme wote.
\v 26 Wakamwua Hamori na Shekemu kwa makali ya upanga. Wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka.
\s5
\v 27 Wale wana wengine wa Yakobo wakaja kwa maiti na kuuteka nyara mji, kwa sababu watu wale walikuwa wamemnajisi dada yao.
\v 28 Wakachukua makundi yao ya kondoo, mbuzi, punda, na kila kitu ndani ya mji na viunga vyake
\v 29 utajiri wote. Watoto na wake zao wote, wakawachukua. Hata wakachukua kila kitu kilichokua katika nyumba.
\s5
\v 30 Yakobo akawambia Simoni na Lawi, "Mmeleta shida juu yangu, kunifanya ninuke kwa wenyeji wa nchi, Wakanaani na Waperizi. Mimi nina watu wachache. Ikiwa watajikusanya pamoja kinyume changu na kunishambulia."
\v 31 Lakini Simoni na Lawi wakasema, "Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?"
\s5
\c 35
\p
\v 1 Mungu akamwambia Yakobo, "Inuka, panda kwenda Betheli, na ukae pale. Unijengee madhabahu pale, niliyekutokea pale ulipomkimbia Esau kaka yako."
\v 2 Kisha Yakobo akawambia nyumba yake na wote aliokuwa nao, "Wekeni mbali miungu yote ya kigeni iliyo kati yenu, jitakaseni wenyewe, na kubadili mavazi yenu.
\v 3 Kisha tuondoke na kwenda Betheli. Nitajenga pale madhabahu kwa Mungu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, naye amekuwa pamoja nami kila nilikokwenda.
\s5
\v 4 Hivyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni iliyokuwa mikononi mwao, na heleni zilizokuwa katika masikio yao. Yakobo akazifukia chini ya mwaloni uliokuwa karibu na Shekemu.
\v 5 Kwa kadili walivyo safiri, Mungu akaifanya miji yote iliyokuwa karibu nao kuhofu, hivyo watu hao hawakuwafuatia wana wa Yakobo.
\s5
\v 6 Hivyo Yakobo akafika Luzu(ndiyo Betheli), ulioko katika nchi ya Kanaani, yeye na watu wote aliokuwa nao.
\v 7 Alijenge madhabahu na kuliita eneo hilo El Betheli, kwa sababu Mungu alikuwa amejifunua kwake, alipokuwa akimkimbia ndugu yake.
\v 8 Debora, mlezi wa Rebeka, akafa. Akazikwa chini kutoka Betheli chini ya mwaloni, hivyo ikaitwa Aloni Bakuthi.
\s5
\v 9 Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, Mungu akamtokea tena na kumbariki.
\v 10 Mungu akamwambia, "Jina lako ni Yakobo, lakini jina lako halitakuwa Yakobo tena. Jina lako litakuwa Israeli." Hivyo Mungu akamwita jina lake Israeli.
\s5
\v 11 Mungu akamwambia, "Mimi ni Mungu Mwenyezi, Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka. Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako.
\v 12 Nchi ambayo nilimpa Ibrahimu na Isaka, nitakupa wewe. Nami nitaupa pia uzao wako baada yako nchi hii."
\v 13 Mungu akapanda kutoka mahali alipoongea naye.
\s5
\v 14 Yakobo akaweka nguzo katika eneo ambalo Mungu alikuwa ameongea naye, nguzo ya jiwe. Akamimina juu yake sadaka ya kinywaji na akamimina mafuta juu yake.
\v 15 Yakobo akaiita sehemu Mungu aliyoongea naye, Betheli
\s5
\v 16 Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu.
\v 17 Akawa na utungu mzito. Alipokuwa katika utungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, "Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume."
\v 18 Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini.
\v 19 Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).
\v 20 Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo.
\s5
\v 21 Israeli akaendelea na safari na akaweka hema yake kuvuka mnara wa walinzi wa kondoo.
\v 22 Yakobo alipokuwa akiishi katika nchi hiyo, Rubeni akalala na Bilha suria wa baba yake, na Israeli akasikia kuhusu hilo. Basi Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili.
\s5
\v 23 Wanawe kwa Lea walikuwa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni.
\v 24 Wanawe kwa Raheli walikuwa Yusufu na Benjamini.
\v 25 Wanawe kwa Bilha, mjakazi wa Raheli walikuwa Dani na Naftali.
\s5
\v 26 Wana wa Zilpa, mjakazi wa Lea, walikuwa Gadi na Asheri. Hawa wote walikuwa wana wa Yakobo waliozaliwa kwake huko Padani Aramu.
\v 27 Yakobo akaja kwa Isaka, baba yake, huko Mamre katika Kiriathi Arba (jina sawa na Hebroni), alipoishi Ibrahimu na Isaka.
\s5
\v 28 Isaka akaishi miaka mia moja na themanini.
\v 29 Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa kwa wahenga wake, na mtu mzee amejaa siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.
\s5
\c 36
\p
\v 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom).
\v 2 Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na
\v 3 Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi.
\s5
\v 4 Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli.
\v 5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu, na Kora. Hawa walikuwa wana wa Esau waliozaliwa kwake katika nchi ya Kananaani.
\s5
\v 6 Esau akawachukua wakeze, wanawe, binti zake, na watu wote wa nyumba yake, mifugo wake - wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani, na akaenda katika nchi iliyoko mbali kutoka kwa Yakobo nduguye.
\v 7 Alifanya hivi kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana kwa wao kuishi pamoja. Nchi waliyokuwa wamekaa isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao.
\v 8 Hivyo Esau, aliyejulikana pia kama Edomu, akakaa katika nchi ya kilima Seiri.
\s5
\v 9 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, babu wa Waedomu katika nchi ya mlima Seiri.
\v 10 Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 11 Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi.
\v 12 Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau.
\s5
\v 13 Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 14 Hawa walikuwa wana wa Oholibama, mkewe Esau, aliyekuwa binti Ana na mjukuu wa Zibeoni. Alimzalia Esau Yeushi, Yalamu, na Kora.
\s5
\v 15 Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora,
\v 16 Gatamu, na Amaleki. Hivi vilikuwa vizazi vya koo kutoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Ada.
\s5
\v 17 Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 18 Hizi zilikuwa koo za Oholibama, mkewe Esau: Yeushi, Yalamu, Kora. Hizi ni koo zilizotoka kwa Oholibama mkewe Esau, binti Ana.
\v 19 Hawa walikuwa wana wa Esau na koo zao.
\s5
\v 20 Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana,
\v 21 Dishoni, Ezeri, na Dishani. Hizi zilikuwa koo the Wahori, wenyeji wa Seiri katika nchi ya Edomu.
\v 22 Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani.
\s5
\v 23 Hawa walikuwa wana wa Shobali: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu.
\v 24 Hawa walikuwa wana wa Zibeoni: Aia na Ana. Huyu ndiye Ana aliyeona chemichemi za moto nyikani, alipokuwa akichunga punda wa Zibeoni babaye.
\s5
\v 25 Hawa walikuwa watoto wa Ana: Dishoni na Oholibama, binti Ana.
\v 26 Hawa walikuwa wana wa Dishoni: Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
\v 27 Hawa walikuwa wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani, na Akani.
\v 28 Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani.
\s5
\v 29 Hizi zilikuwa koo za Wahori: Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana,
\v 30 Dishoni, Ezeri, Dishani: hizi zilikuwa koo za Wahori, kulingana na ukoo ulivyoorodheshwa katika nchi ya Seiri.
\s5
\v 31 Hawa walikuwa wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kumilika juu ya Waisraeli:
\v 32 Bela mwana wa Beori, alitawala huko Edomu, na jina la mji wake lilikuwa Dinhaba.
\v 33 Bela alipofariki, kisha Yobabu mwana wa Zera kutoka Bozra, akatawala mahali pake.
\s5
\v 34 Yobabu alipofariki, Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani, akatawala mahali pake.
\v 35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu, akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Avithi.
\v 36 Hadadi alipofariki, kisha Samla wa Masreka akatawala mahali pake.
\s5
\v 37 Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake.
\v 38 Shauli alipofariki, kisha Baali Hanani mwana wa Akbori akatawala mahali pake.
\v 39 Baali Hanani mwana wa Akbori, alipokufa, kisha Hadari akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Pau. Jina la mkewe lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.
\s5
\v 40 Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi,
\v 41 Oholibama, Ela, Pinoni,
\v 42 Kenazi, Temani, Mbza,
\v 43 Magdieli, na Iramu. Hawa walikuwa wakuu wa ukoo wa Edomu, kwa kufuata makao yao katika nchi waliyomiliki. Nao ni Esau, baba wa Waedomu.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Yakobo akaishi katika nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani.
\v 2 Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo. Yusufu, aliyekuwa kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akilichunga kundi pamoja na ndugu zake. Alikuwa pamoja na wana wa Bilha na pamoja na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akaleta taarifa yao mbaya kwa baba yao.
\s5
\v 3 Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote kwa sababu alikuwa mwana wa uzee wake. Akamshonea vazi zuri.
\v 4 Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema.
\s5
\v 5 Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi.
\v 6 Aliwambia, "Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota.
\s5
\v 7 Tazama, tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani na tazama, mganda wangu ukainuka na kusimama wima, na tazama, miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu"
\v 8 Ndugu zake wakamwambia, "Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu? Hata wakamchukia zaidi kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake.
\s5
\v 9 Akaota ndoto nyingine na kuwasimulia ndugu zake. Alisema, "Tazama, nimeota ndoto nyingine: Jua na mwezi na nyota kumi na moja ziliniinamia."
\v 10 Akamwambia baba yake vile vile alivyowambia ndugu zake, na baba yake akamkemea. Akamwambia, Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako na mimi na ndugu zako kweli tutakuja kukuinamia mpaka chini?"
\v 11 Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliwema jambo hilo moyoni.
\s5
\v 12 Ndugu zake wakaenda kulichunga kundi la baba yao huko Shekemu.
\v 13 Israeli akamwambia Yusufu, 'Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao." Yusufu akamwambia, "nipo tayari."
\v 14 Akamwambia, "Basi nenda, uwaone ndugu zako na kundi wanaendeleaje, na uniletee neno." Hivyo Yakobo akamtuma kutoka katika bonde la Hebroni, na Yusufu akaenda Shekemu.
\s5
\v 15 Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni. Yule mtu akamwuliza, "Unatafuta nini?"
\v 16 Yusufu akamwambia, "Nawatafuta ndugu zangu. Tafadhari, niambie, wananalichunga wapi kundi."
\v 17 Yule mtu akasema, "Waliondoka mahali hapa, kwa maana niliwasikia wakisema, 'Haya twende Dothani." Yusufu akawafuata ndugu zake na kuwaona huko Dothani.
\s5
\v 18 Wakamwona kutokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakapanga njama ya kumwua.
\v 19 Ndugu zake wakaambiana wao kwa wao, "Tazama, mwotaji anakaribia.
\v 20 Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje."
\s5
\v 21 Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, "Tusiuondoe uhai wake."
\v 22 Rubeni aliwambia, "Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake" - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake.
\s5
\v 23 Ikawa Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua vazi lake zuri.
\v 24 Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji.
\s5
\v 25 Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri.
\v 26 Yuda akawambia ndugu zake, "Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake?
\s5
\v 27 Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu." Ndugu zake wakamsikiliza.
\v 28 Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
\s5
\v 29 Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake.
\v 30 Akarudi kwa ndugu zake na kusema, "Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?"
\s5
\v 31 Wakachinja mbuzi na kisha wakalichukua vazi la Yusufu na kulichovya katika damu.
\v 32 Kisha wakalipeleka kwa baba yao na kusema, "Tumeiona hii. Tafadhari angalia kwamba ni vazi la mwanao au hapana."
\v 33 "Yakobo akaitambua na kusema, "Ni nguo ya mwanangu. Mnyama wa mwitu amemrarua. Bila shaka Yusufu ameraruliwa katika vipande.
\s5
\v 34 Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi.
\v 35 Wanawe na binti zake wote wakainuka na kumfariji, lakini alikataa kufarijiwa. Akasema, "Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea mwanangu." Babaye akamlilia.
\v 36 Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifa, afisa wa Farao, kepteni wa walinzi.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Ikawa wakati ule Yuda akawaacha ndugu zake na kukaa na Mwadulami fulani, jina lake Hira.
\v 2 Pale akakutana na binti Mkanaani jina lake Shua. Akamwoa na kulala naye.
\s5
\v 3 Akawa mjamzito na kuzaa mwana. Akaitwa Eri.
\v 4 Akawa mjamzito tena na kuzaa mwana tena. Akamwita jina lake Onani.
\v 5 Akazaa mwana mwingine akamwita jina lake Shela. Alikuwa huko Kezibu alipomzaa.
\s5
\v 6 Yuda akaona mke kwa ajili ya Eri, mzaliwa wake wa kwanza. Jina lake Tamari.
\v 7 Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua.
\s5
\v 8 Yuda akamwambia Onani, "Lala na mke wa nduguyo. Fanya wajibu wa shemeji kwake, na umwinulie nduguyo mwana."
\v 9 Onani alijua kwamba mtoto asingekuwa wake. Pindi alipolala na mke wa kaka yake, alimwaga mbegu juu ya ardhi ili kwamba asimpatie nduguye mtoto.
\v 10 Alilolifanya lilikuwa ovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua pia.
\s5
\v 11 Kisha Yuda akamwambia Tamari, mkwewe, "Ukakae mjane katika nyumb aya baba yako hadi Shela, mwanangu, atakapokuwa." Kwani aliogopa, "Asije akafa pia, kama nduguze." Tamari akaondoka na kuishi katika nyumba ya babaye.
\s5
\v 12 Baada ya muda mrefu, binti Shua, mkewe Yuda, alikufa. Yuda akafarijika na kwenda kwa wakatao kondoo wake manyoya huko Timna, yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami.
\v 13 Tamari akaambiwa, "Tazama, mkweo anakwenda Timna kukata kondoo wake manyoya."
\v 14 Akavua mavazi yake ya ujane na akajifunika kwa ushungi. Akakaa katika lango la Enaimu, lililoko kando ya njia iendayo Timna. Kwa maana aliona kwamba Shela amekua lakini akupewe kuwa mke wake.
\s5
\v 15 Yuda alipomwona alidhani ni kahaba kwa maana alikuwa amefunika uso wake.
\v 16 Akamwendea kando ya njia na kusema, "Njoo, tafadhari uniruhusu kulala nawe" - kwani hakujua kwamba alikuwa ni mkwewe - naye akasema, "Utanipa nini ili ulale nami?
\s5
\v 17 Akasema, "Nitakuletea mwana mbuzu wa kundi." Akasema, "Je utanipa rehani hata utakapo leta?"
\v 18 Akasema, "Nikupe rehani gani?" Naye akasema, "Mhuri wako na mshipi, na fimbo iliyo mkononi mwako." Akampa na kulala naye. Akawa mjamzito.
\s5
\v 19 Akaamka na kuondoka. Akavua ushungi wake na kuvaa vazi la ujane wake.
\v 20 Yuda akatuma mwana mbuzi kutoka kundini kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami ili aichukue rehani kutoka katika mkono wa mwanamke, lakini hakumwona.
\s5
\v 21 Kisha Mwadulami akauliza watu wa sehemu hiyo,"Yupo wapi kahaba aliyekuwa Enaimu kando ya njia?" Wakasema, hapajawai tokea kahaba hapa."
\v 22 Akarudi kwa Yuda na kusema, "Sikumwona. Pia watu wa eneo hilo wamesema, 'Hajawai kuwapo kahaba hapa."
\v 23 Yuda akasema, "Mwache akae na vitu, tusije tukaaibika. Hakika, nimemletea mwanambuzi, lakini hukumwona."
\s5
\v 24 Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, "Tamari mkweo amefanya ukahaba, na kwa hakika, yeye ni mjamzito." Yuda akasema, "Mleteni hapa ili achomwe."
\v 25 Alipoletwa nje, alipeleka ujumbe kwa mkwewe, "Mimi ni mjamzito kwa mtu mwenye vitu hivi." Akasema, "Tambua tafadhari, mhuri huu na mshipi na fimbo ni vya nani."
\v 26 Yuda akavitambua na kusema, "Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwani sikumpa Shela, mwanangu awe mme wake." Hakulala naye tena.
\s5
\v 27 Muda wake wa kujifungua ukafika, tazama, mapacha walikuwa tumboni mwake.
\v 28 Ikawa alipokuwa akijifungua mmoja akatoa mkono nje, na mkunga akachukua kitambaa cha rangi ya zambarau na kukifunga katika mkono wake na kusema, "Huyu ametoka wa kwanza."
\s5
\v 29 Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka kwanza. Mkunga akasema, "Umetokaje" Na akaitwa Peresi.
\v 30 Kisha ndugu yake akatoka, akiwa na utepe wa zambarau juu ya mkono wake, naye akaitwa Zera.
\s5
\c 39
\p
\v 1 Yusufu akaletwa Misri. Potifa, aliyekuwa afisa wa Farao mkuu wa walinzi na Mmisri, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli, waliokuwa wamempeleka pale.
\v 2 Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na akawa mtu aliyefanikiwa. Aliishi katika nyumba ya Mmisri bwana wake.
\s5
\v 3 Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye na kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya.
\v 4 Yusufu akapata kibali mbele zake. Akamtumikia Potifa. Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki, akakiweka chini ya uangalizi wake.
\s5
\v 5 Ikawa alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki, Yahwe akaibariki nyumba ya Mmisri kwa sababu ya Yusufu. Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani.
\v 6 Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu. Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu. Basi Yusufu alikuwa kijana mzuri na wa kuvutia.
\s5
\v 7 Ikawa baada ya hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu. Akamwambia, "Lala nami."
\v 8 Lakini yeye alikataa na kumwambia mke wa bwana wake, "Tazama, bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani, na ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu.
\v 9 Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanidhuiria chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?
\s5
\v 10 Akamwambia Yusufu siku baada ya siku, lakini yeye akakataa kulala naye wala kuwa naye.
\v 11 Ikawa siku moja aliingia ndani kufanya kazi yake. Hakuna mtu yeyote wa nyumbani aliyekuwepo pale ndani.
\v 12 Akashika nguo zake na kusema, "Lala nami." Akaacha nguo zake mikononi mwake, akakimbia, na kutoka nje.
\s5
\v 13 Ikawa, alipoona kwamba ameziacha nguo zake mikononi mwake na kwamba amekimbia nje,
\v 14 akawaita watu wa nyumbani mwake na kuwambia, "Tazama, Potifa ameleta Mwebrania huyu kutudhihaki. Aliingia kulala nami, na nikapiga kelele.
\v 15 Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha na nguo yake, akakimbia, na kutoka nje."
\s5
\v 16 Akaweka nguo zake karibu naye hata bwana yake alipokuja nyumbani.
\v 17 Akamwambia maelelezo haya, "Yule mtumishi Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kunidhihaki.
\v 18 Ikawa nilipopiga kelele, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje."
\s5
\v 19 Ikawa, bwana wake aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe, "Hivi ndivyo mtumishi wako alivyonitenda," alikasirika sana.
\v 20 Bwana wa Yusufu akamchukua na kumweka gerezani, mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme. Akawa pale kifungoni.
\s5
\v 21 Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na kumwonyesha uaminifu wa agano. Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza.
\v 22 Mlinzi wa gereza akawaweka mikononi mwa Yusufu wafungwa wote waliokuwa gerezani. Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.
\v 23 Mlinzi wa gereza hakuwa na wasiwasi juu ya chochote kilichokuwa mkononi mwake, kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye. Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.
\s5
\c 40
\p
\v 1 Ikawa baada ya mambo haya, mnyweshaji wa mfalme wa Misri na mwokaji wa mfalime walimkosa bwana wao, mfalme wa Misri.
\v 2 Farao akawakasirikia hawa maafsa wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji.
\v 3 Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi, katika gereza lile Yusufu alimofungwa.
\s5
\v 4 Kapteni wa walinzi akamweka Yusufu kuwa mtumishi wao. Walikaa kifungoni kwa muda fulani.
\v 5 Wote wakaota ndoto - mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliokuwa wamefungwa gerezani - kila mmoja akaota ndoto usiku huo huo, na kila ndoto ilikuwa na tafsiri yake.
\s5
\v 6 Yusufu akaja kwao asubuhi na kuwaona. Tazama, walikuwa na uzuni.
\v 7 Akawauliza maafsa wa Farao waliokuwa pamoja naye kifungoni katika nyumba ya bwana wake, kusema, "Kwa nini leo mnaoneka wenye uzuni?"
\v 8 Wakamwambia, Sisi wote tumeota ndoto na hakuna wakuitafsiri." Yusufu akawambia, "Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Niambieni, tafadhari."
\s5
\v 9 Mkuu wa wanyweshaji akamwambia Yusufu ndoto yake. Akamwambia, "Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu.
\v 10 Na kulikuwa na matawi matatu katika mzabibu huo. Ulipochipua, ukachanua maua na kuzaa vichala vya zabibu.
\v 11 Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikachukua zabibu na kuzikamua katika kikombe cha Farao, na kukiweka kikombe katika mkono wa Farao."
\s5
\v 12 Yusufu akamwambia, "Tafsiri yake ni hii. Yale matawi matatu ni siku tatu.
\v 13 Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake.
\s5
\v 14 Lakini unikumbuke ukifanikiwa, na unionesha wema. Unitaje kwa Farao na kuniondoa hapa gerezani.
\v 15 Maana hakika nilitekwa kutoka katika nchi ya Waebrania. Na hapa sijafanya chochote kinachonipasa niwekwe gerezani."
\s5
\v 16 Mkuu wa waokaji alipoona kwamba tafsiri ilikuwa ya kuvutia, akamwambia Yusufu, "Mimi pia niliota ndoto, na tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu.
\v 17 Katika kikapu cha juu kulikuwa na kila aina za bidhaa ya kuokwa kwa Farao, lakini ndege wakavila ndani ya kikapu juu ya kichwa changu."
\s5
\v 18 Yusufu akajibu na kusema, "Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu.
\v 19 Ndani ya siku tatu Fareao atakiinua kichwa chako kutoka kwako na atakutundika juu ya mtu. Ndege watakula mwili wako."
\s5
\v 20 Ikawa siku ya tatu ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Farao. Akafanya sherehe kwa watumishi wake wote. "Akakiinua juu" kichwa cha mkuu wa wanyweshaji na kichwa cha mkuu wa waokaji, kati ya watumishi wake.
\v 21 Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika majukumu yake, na akakiweka tena kikombe katika mkono wa Farao.
\v 22 Lakini akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyokuwa amewatafsiria.
\v 23 Hata hivyo mkuu wa wanyweshaji hakukumbuka kumsaidia Yusufu. Badala yake, alimsahau.
\s5
\c 41
\p
\v 1 Ikawa mwishoni mwa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto.
\v 2 Tazama, alikuwa amesimama kando ya Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi.
\v 3 Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine.
\s5
\v 4 Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa.
\v 5 Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri.
\v 6 Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
\s5
\v 7 Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.
\v 8 Ikawa wakati wa asubuhi roho yake ikafadhaika. Akatuma na kuwaita waganga na wenye hekima wote wa Misri. Farao akawasimlia ndoto zake, lakini hakuna aliyeweza kumtafsiria Farao.
\s5
\v 9 Kisha mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao, "Leo ninayafikiri makosa yangu.
\v 10 Farao aliwakasirikia watumishi wake, na kutuweka kifungoni katika nyumba ya kapteni wa walinzi, mkuu wa waokaji na mimi.
\v 11 Tuliota ndoto usiku huo mmoja, yeye na mimi. Kila mmoja aliota kwa kadili ya tafsiri yake.
\s5
\v 12 Pamoja nasi kulikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi wa kapteni wa walinzi. Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu. Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
\v 13 Ikawa kama alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa. Farao alinirudisha katika nafasi yangu, lakini akamtundika yule mwingine."
\s5
\v 14 Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.
\v 15 Farao akamwambia Yusufu, "Nimeoda ndoto, lakini hakuna wa kuitafsiri. Lakini nimesikia kuhusu wewe, kwamba unaposikia ndoto unaweza kuitafsiri."
\v 16 Yusufu akamjibu Farao, kusema, "Siyo katika mimi. Mungu atamjibu Farao kwa uhakika."
\s5
\v 17 Farao akamwambia Yusufu, "Katika ndoto yangu, tazama, nilisimama katika ukingo wa Nile.
\v 18 Tazama, ng'ombe saba wakatoka ndani ya Nile, wanene na wakuvutia, nao wakajilisha katika nyasi.
\s5
\v 19 Tazama, ng'ombe wengine saba wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya, na wembaba. Sijawao kuona wabaya kama hao katika nchi yote ya Misri.
\v 20 Wale ng'ombe wembamba na wabaya wakawala wale ng'ombe saba na wanene.
\v 21 Walipokuwa wamemaliza kuwala wote, haikujulikana kama walikuwa wamewala, kwani walibaki wabaya kama mwanzo. Kisha nikaamka.
\s5
\v 22 Niliona katika ndoto yangu, na tazama, masuke saba yakatoka katika bua moja, jema na limejaa.
\v 23 Tazama, masuke saba zaidi, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
\v 24 Yale masuke membamba yakayameza masuke saba mema. Niliwaambia waganga ndoto hizi, lakini hakuna aliyeweza kunielezea."
\s5
\v 25 Yusufu akamwambia Farao, "Ndoto za Farao ni moja. Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya.
\v 26 Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba, na masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.
\s5
\v 27 Na wale ng'ombe saba wembamba na wabaya waliokuja baadaye ni miaka saba, na pia masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki itakuwa miaka saba ya njaa.
\v 28 Hilo ni jambo nililomwambia Farao. Mungu amemfunulia Farao jambo analokwenda kulifanya.
\v 29 Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri.
\s5
\v 30 Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiaribu nchi.
\v 31 Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana.
\v 32 Kwamb ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu, na Mungu atalitimiza hivi karibuni.
\s5
\v 33 Basi Farao atafute mtu mwenye maharifa na busara, na kumweka juu ya nchi ya Misri.
\v 34 Farao na afanye hivi: achague wasimamizi juu ya nchi. Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri katika miaka saba ya shibe.
\s5
\v 35 Na wakusanye chakula chote cha hii miaka myema ijayo na kuitunza nafaka chini ya mamlaka ya Farao, kwa chakula kutumika katika miji. Wakiifadhi.
\v 36 Chakula kitakuwa matumizi ya nchi kwa miaka saba ya njaa itakayokuwa katika nchi ya Misri. Kwa njia hii nchi haitaaribiwa na njaa."
\s5
\v 37 Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote.
\v 38 Farao akawambia watumishi wake, "Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu?"
\s5
\v 39 Hivyo Farao akamwambia Yusufu, "Kwa vile Mungu amekuonesha yote haya, hakuna mtu mwenye ufahamu na busara kama wewe.
\v 40 Utakuwa juu ya nyumba yangu, watu wangu watatawaliwa kwa kadili ya neno lako. Katika kiti cha enzi peke yake mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe."
\v 41 Farao akamwambia Yusufu, "Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri."
\s5
\v 42 Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
\v 43 Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho. Watu wakapiga kelele mbele yake, "Pigeni magoti." Farao akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
\s5
\v 44 Farao akamwambia Yusufu, "Mimi ni Farao, mbali na wewe, hakuna mtu atakayeinua mkono wake au mguu wake katika nchi ya Misri."
\v 45 Farao akamwita Yusufu jina la Zafenathi Panea." Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, kuwa mke wake. Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri.
\s5
\v 46 Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya Farao, na kwenda katika nchi yote ya Misri.
\v 47 Katika miaka saba ya shibe nchi ilipozaa kwa wingi.
\s5
\v 48 Akakusanya chakula chote cha miaka saba iliyokuwako katika nchi ya Misri na kukiweka chakula katika miji. Akaweka katika kila mji chakula cha mashamba yaliyokizunguka.
\v 49 Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari, kingi kiasi kwamba akaacha kuhesabu, kwa sababu kilikuwa hakihesabiki.
\s5
\v 50 Kabla miaka ya njaa kuingia Yusufu akapata wana wawili, ambao Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, alimzalia.
\v 51 Yusufu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, kwani alisema, "Mungu amenisahaurisha shida zangu zote na nyumba yote ya baba yangu."
\v 52 Akamwita mwanawe wa pili Efraimu, kwani alisema, Mungu amenipa uzao katika nchi ya mateso yangu."
\s5
\v 53 Miaka saba ya shibe iliyokuwa katika nchi ya Misri ikafika mwisho.
\v 54 Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.
\s5
\v 55 Nchi yote ya Misri ilipokuwa na njaa, watu wakapiga kelele kwa Farao kwa ajili ya chakula. Farao akawambia Wamisri wote, "Nendeni kwa Yusufu na mfanye atakavyosema."
\v 56 Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi. Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri. Njaa ilikuwa kali sana katika nchi ya Misri.
\v 57 Dunia yote ikaja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwani njaa ilikuwa kali katika dunia yote.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Basi Yakobo akafahamu kwamba kuna nafaka huko Misri. Akawambia wanawe, "Kwa nini mnatazamana?
\v 2 Akasema, "Tazama, nimesikia kwamba kuna nafaka huko Misri. Shukeni huko mkatununulie chakula ili tuishi wala tusife."
\v 3 Ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri kununua chakula.
\v 4 Lakini Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma na ndugu zake, kwani alihofu kwamba madhara yaweza kumpata.
\s5
\v 5 Wana wa Israeli wakaja kununua miongoni mwao waliokuja, kwani njaa ilikuwapo katika nchi ya Kanaani.
\v 6 Basi Yusufu alikuwa mtawala juu ya nchi. Ndiye aliyekuwa akiwauzia watu wote wa nchi. Ndugu zake Yusufu wakaja na kumwinamia na nyuso zao hata chini.
\s5
\v 7 Yusufu akawaona ndugu zake na kuwatambua, lakini alijibadili kwao na kuongea nao kwa ukali. Akawambia, "Mmetoka wapi?" Wakasema, "Kutoka nchi ya Kanaani ili kununua chakula."
\v 8 Yusufu akawatambua ndugu zake, lakini wao hawakumtambua.
\s5
\v 9 Yusufu akazikumbuka ndoto aliyoziota kuhusu wao. Akawambia, "Ninyi ni wapelelezi. Mmekuja kuona sehemu za nchi zisizolindwa."
\v 10 Wakamwambia, "Hapana, bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula.
\v 11 Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Ni watu wa kweli. Watumishi wako siyo wapelelezi."
\s5
\v 12 Akawambia, "Hapana, mmekuja kuangalia sehemu za nchi zisizolindwa."
\v 13 Wakasema, "Sisi watumishi wako tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja katika nchi ya Kanaani. Tazama, mdogo yupo na baba yetu, na mwingine hayupo hai tena."
\s5
\v 14 Yusufu akawambia, "Ndivyo nilivyowambia; ninyi ni wapelelezi.
\v 15 Mtajaribiwa kwa njia hii. Kama aishivyo Farao, hamtaondoka hapa, mdogo wenu asipokuja hapa.
\v 16 Mtumeni mmoja wenu amlete mdogo wenu. Mtabaki gerezani, hata maneno yenu yatakapothibitishwa, kwamba kuna ukweli ndani yenu."
\v 17 Akawaweka kifungoni kwa siku tatu.
\s5
\v 18 Katika siku ya tatu Yusufu akaongea nao, "Fanyeni hivi nanyi mtaishi, kwani ninamcha Mungu.
\v 19 Kama ninyi ni watu wa kweli, mmoja wenu atazuiliwa hapa gerezani, lakini ninyi nendeni, chukueni nafaka kwa ajili ya nyumba zenu.
\v 20 Mleteni mdogo wenu kwangu ili kwamba maneno yenu yathibitishwe nanyi hamtakufa." Wakafanya hivyo.
\s5
\v 21 Wakasemezana wao kwa wao, "Kwa kweli tuna hatia juu ya ndugu yetu kwani tuliona tabu ya nafsi yake alipotusihi nasi hatukusikia. Kwa hiyo taabu hii imeturudia."
\v 22 Rubeni akawajibu, "Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu."
\s5
\v 23 Lakini hawakuja kwamba Yusufu anawaelewa, kwani kulikuwa na mkalimani kati yao.
\v 24 Akatoka kwao na kulia. Akarudi kwao na kuongea nao. Akamchukua Simoni miongoni mwao na kumfunga mbele ya macho yao.
\v 25 Kisha Yusufu akaagiza watumishi kujaza mifuko yao kwa nafaka, na kurudisha pesa ya kila mmoja katika gunia lake, nakuwapa mahitaji kwa safari. Wakatendewa hivyo.
\s5
\v 26 Hawa ndugu wakapandisha chakula chao juu ya punda zao na kuondoka pale.
\v 27 Mmoja wao alipofungua gunia lake ili kumlisha punda wao katika sehemu waliyokuwa, akaona pesa yake. Tazama, ilikuwa mdomoni mwa gunia lake.
\v 28 Akawambia ndugu zake, "Pesa yangu imerudishwa. Tazama, imo katika gunia langu."Mioyo yao ikazimia na wakageukiana kila mmoja huku wakitetemeka. Wakasema, "Ni nini hiki alichotutendea Mungu?"
\s5
\v 29 Wakaenda kwa Yakobo, baba yao katika nchi ya Kanaani na kumwambia yote yaliyowapata.
\v 30 Wakasema, "Yule mtu, bwana wa nchi, aliongea nasi kwa ukali na kutudhania kuwa wapelelezi katika nchi.
\v 31 Tukamwambia, 'Tu watu wa kweli sisi. Sisi siyo wapelelezi.
\v 32 Tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayupo hai tena, na mdogo yupo na baba yetu katika nchi ya Kanaani."
\s5
\v 33 Yule mtu, bwana wa nchi, akatwambia, 'Kwa hili nitajua kwamba ni watu wa kweli ninyi. Mwacheni mmojawapo wa ndugu zenu, chukueni chakula kwa ajili ya njaa katika nyumba zenu, na mwondoke.
\v 34 Mleteni mdogo wenu kwangu. Ndipo nitakapojua kwamba ninyi si wapelelezi, lakini ni watu wa kweli. Kisha nitamwachilia ndugu yenu, na mtafanya biashara katika nchi."
\s5
\v 35 Ikawa walipoyafungua magunia yao, na tazama, kila mfuko wa fedha wa mmojawao ulikuwa katika gunia lake. Wakati wao na baba yao walipoona mifuko yao ya fedha, wakaogopa.
\v 36 Yakobo baba yao akawambia, "Mmeniharibia watoto wao. Yusufu hayupo hai tena, Simoni ameondoka, nanyi mmpeleke Benjamini naye. Mambo haya yote ni kunyume changu."
\s5
\v 37 Rubeni akamwambia baba yake, kusema, "Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha Benjamini kwako. Mweke mikononi mwangu, nami nitamrudisha tena kwako."
\v 38 Yakobo akasema, "Mwanangu atashuka pamoja nanyi. Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki. Ikiwa madhara yatampata katika njia mnayoiendea, ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni."
\s5
\c 43
\p
\v 1 Njaa ilikuwa kali katika nchi.
\v 2 Ikawa walipokuwa wametumia chakula chote walichokitoa Misri, baba yao akawambia, "Nendeni tena; mtununulie chakula."
\s5
\v 3 Yuda akamwambia, "Yule mtu alituonya kwa ukali, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi.'
\v 4 Ikiwa utamtuma ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kuwanunulia chakula.
\v 5 Lakini usipompeleka, hatutashuka. Kwa maana yule mtu alitwambia, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi."
\s5
\v 6 Israeli akawambia, "Kwa nini mlinitendea mimi vibaya hivyo kwa kumwambia mtu huyo kwamba mnaye ndugu mwingine?"
\v 7 Wakasema, "Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?'Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?"
\s5
\v 8 Yuda akamwambia Israeli baba yake, "Mtume kijana pamoja nami. Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu.
\v 9 Mimi nitakuwa mdhamini wake. Utaniwajibisha mimi. Kama nisipomleta na kumweka mbele yako, basi nibebe lawama daima.
\v 10 Kwani kama tusingekawia, bila shaka hata sasa tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili."
\s5
\v 11 Israeli baba yao akawambia, "Kama ni hivyo, basi fanyeni hivi. Chukueni baadhi ya mazao mazuri ya nchi katika mifuko yenu. Mchukulieni yule mtu zawadi: baadhi ya malhamu, asali, viungo na manemane, jozi na lozi.
\v 12 Chukueni pesa mara mbili mikononi mwenu. Pesa iliyorudishwa katika magunia yenu, muichukue tena katika mikono yenu. Pengine walikosea.
\s5
\v 13 Mchukueni ndugu yenu pia. Inukeni na mwende tena kwa mtu yule.
\v 14 Mungu Mwenyezi na awape kuona rehema mbele ya huyo mtu, hivyo kwamba awafungulie ndugu yenu mwingine na Benjamini. Kama nikipotelewa na watoto, nimepotelewa."
\v 15 Watu wale wakachukua zawadi hii, na katika mikono yao wakachukua mara mbili ya kiasi cha pesa, pamoja na Benjamini. Wakaamka na kushuka Misri na kusimama mbele ya Yusufu.
\s5
\v 16 Yusufu alipomwona Benjamini akiwa nao, akamwambia mtunzaji wa nyumba yake, "Walete watu hao ndani ya nyumba, chinja mnyama na umwandae, kwani watu hawa watakula chakula cha mchana pamoja nami."
\v 17 Mtunzaji wa nyumba akafanya kama Yusufu alivyosema. Akawaleta wale watu nyumbani kwa Yusufu.
\s5
\v 18 Wale ndugu wakaogopa kwa vile walivyoletwa katika nyumba ya Yusufu. Wakasema, "Ni kwa sababu ya pesa iliyorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tulipoletwa ndani, kwamba atafute nafasi kinyume chetu. Kwamba aweze kutukamata na kutuchukua kama watumwa, na kuchukua punda wetu." Wakamsogelea mtunzaji wa nyumba ya Yusufu,
\v 19 nao wakaongea naye mlangoni mwa nyumba,
\v 20 wakisema, "Bwana wangu, tulikuja mara ya kwanza kununua chakula.
\s5
\v 21 Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu.
\v 22 Tumekuja na pesa nyingine pia mikonon mwetu ili kununua chakula. Hatujui aliyeziweka pesa katika magunia yetu."
\v 23 Mtunzaji wa nyumba akasema, "Amani iwe kwenu, msiogope. Mungu wenu na Mungu wa baba yenu ndiye aliyeweka pesa katika magunia yenu. Nilipokea pesa yenu." Kisha mtunzaji wa nyumba akamleta Simoni kwao.
\s5
\v 24 Msimamizi wa nyumba akawapeleka watu hao katika nyumba ya Yusufu. Akawapa maji, nao wakaosha miguu yao. Akawalisha punda wao.
\v 25 Wakaandaa zawadi kwa ajili ya Yusufu aliyekuwa akija mchana, kwani walikuwa wamesikia kwamba watakula pale.
\s5
\v 26 Yusufu alipokuja nyumbani, wakaleta nyumbani zawadi iliyokuwa mikononi mwao, nao wakainama mbele yake hata chini.
\v 27 Akawauliza juu ya hali zao na kusema,"Je baba yenu hajambo, yule mzee mliyemnena? Je bado yu hai?"
\s5
\v 28 Wakasema, "Mtumishi wako baba yetu hajambo. Na bado yu hai" Wakajinyenyekeza na kuinama chini.
\v 29 Alipoinua macho yake akamwona Benjamini ndugu yake, mwana wa mamaye, naye akasema, "Je huyu ndiye mdogo wenu mliyemsema?" Na kisha akasema, "Mungu na awe mwenye neema kwako, mwanangu."
\s5
\v 30 Yusufu akaharakisha kutoka chumbani, kwani aliguswa sana kuhusu nduguye. Akatafuta mahali pa kulia. Akaingia chumbani mwake na kulia umo.
\v 31 Akaosha uso wake na kutoka nje. Akajizuia mwenyewe, akasema, "karibuni chakula."
\s5
\v 32 Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri.
\v 33 Wale ndugu wakakaa mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa kulingana na haki yake ya uzaliwa, na mdogo kulingana na ujana wake. Wale watu wakashangaa wote.
\v 34 Yusufu akapeleka sehemu kwao kutoka katika chakula kilichokuwa mbele yake. Lakini sehemu ya Benjamini ilikuwa mara tano zaidi ya kila ndugu zake. Wakanywa na wakamfurahia.
\s5
\c 44
\p
\v 1 Yusufu akamwamru msimamizi wa nyumba yake, akisema, "Jaza magunia ya watu hawa kwa chakula, kiasi wawezacho kubeba, na uweke pesa ya kila mtu katika mdomo wa gunia lake.
\v 2 Uweke kikombe changu, cha fedha, katika mdomo wa gunia la mdogo, na pesa yake ya chakula pia." Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyosema.
\s5
\v 3 Kukapambazuka asubuhi, na wale watu wakaruhusiwa kuondoka, wao na punda zao.
\v 4 Walipokuwa wametoka mjini lakini hawajafika mbali, Yusufu akamwambia msimamizi wa nyumba yake, "Inuka, uwafuatie wale watu, na utakapowapata, wambie, 'Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema?
\v 5 Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi? Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya."
\s5
\v 6 Msimamizi wa nyumba akawapata na kuwambia maneno haya.
\v 7 Wakasema, "Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya? Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili.
\s5
\v 8 Tazama, pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu, tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani. Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu?
\v 9 Yeyote kitakayeonekana kwake miongoni mwa watumishi wako, atakufa, nasi sote tutakuwa watumwa wa bwana wangu."
\v 10 Msimamizi akasema, "Basi na iwe kwa kadili ya maneno yenu. Yeye ambaye kikombe kitaonekana kwake atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine mtakuwa bila hatia."
\s5
\v 11 Kisha kila mtu akaharakisha na kulishusha gunia lake chini. na kila mtu akalifungua gunia lake.
\v 12 Msimamizi akatafuta. akaanza na mkubwa wa wote na kumaliza kwa mdogo wa wote, na kikombe kikaonekana katika gunia la Benjamini.
\v 13 Wakararua mavazi yao. Kila mtu akapakia juu ya punda wake nao wakarudi mjini.
\s5
\v 14 Yuda na ndugu zake wakaja katika nyumba ya Yusufu. Bado alikuwepo pale, nao wakainama mbele zake hata chini.
\v 15 Yusufu akawambia, "Je ni nini hili mlilolifanya? Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi.
\s5
\v 16 Yuda akasema, "Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe? Mungu ameona uovu wa watumishi wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, wote sisi na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake."
\v 17 Yusufu akasema, "Na iwe mbali nami kwamba naweza kufanya hivyo. Mtu ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake, huyu ndiye atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine, nendeni kwa amani kwa baba yenu."
\s5
\v 18 Ndipo Yuda alipomkaribia na kusema, "Bwana wangu, tafadhari mwache mtumishi wako aseme neno katika masikio ya bwana wangu, na usiziache hasira zako kuwaka dhidi ya mtumishi wako, kwani wewe ni kama Farao.
\v 19 Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, kusema, Je mnaye baba au ndugu?'
\s5
\v 20 Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba, ni mzee, na mwana wa uzee wake, ni mdogo. Na ndugu yake alishakufa, na yeye peke yake ndiye amebaki kwa mama yake, na baba yake anampenda.'
\v 21 Nawe ukawambia matumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.'
\v 22 Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi kumwacha babaye. Kwani akimwacha babaye baba yake angekufa.'
\s5
\v 23 Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.'
\v 24 Na ikawa tulipokwenda kwa mtumishi wako baba yangu, tulimwambia maneno ya bwana wangu.
\v 25 Na baba yetu akasema, Nendeni tena, mkatununulie chakula.'
\v 26 Nasi tukasema, "Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu atakuwa nasi, ndipo tutakaposhuka, kwani hatuwezi kuuona uso wa mtu yule mdogo wetu asipokuwa pamoja nasi.'
\s5
\v 27 Mtumishi wako baba yetu akatwambia, 'Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili.
\v 28 Na mmoja akatoka kwangu nami nikasema, "Bila shaka ameraruliwa vipande, na tangu hapo sijamwona."
\v 29 Nanyi mkimchukua huyu naye kutoka kwangu mabaya yanaweza kumpata, mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni.
\s5
\v 30 Kwa hiyo, basi, nitapokuja kwa mtumishi wako baba yangu, na kijana hayupo nasi, kwa kuwa uhai wake umefungamanishwa katika uhai wa kijana,
\v 31 itakuwa, atakapoona kwamba kijana hayupo nasi atakufa. Na watumishi wako watazishusha mvi za mtumishi wako baba yetu kaburini kwa masikitiko.
\v 32 Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu na alisema, 'Ikiwa sitamleta kwako, ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu daima."
\s5
\v 33 Kwa hiyo sasa, tafadhari mwache mtumishi wake akae kama mtumwa kwa bwana wangu badala ya kijana, na umwache kijana aende na ndugu zake.
\v 34 Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami? Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu."
\s5
\c 45
\p
\v 1 Ndipo Yusufu hakuweza kujizuia mwenyewe mbele ya watumishi waliosimama kando yake. Akasema kwa sauti, "Kila mtu aondoke." Hivyo hakuna mtumishi aliyesimama kando yake wakati Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake.
\v 2 Akalia kwa sauti, Wamisri wakasikia, na nyumba ya Farao wakasikia kuhusu hilo.
\v 3 Yusufu akawambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu. Je baba yangu ni mzima bado? Ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walitishwa na uwepo wake.
\s5
\v 4 Kisha Yusufu akawambia ndugu zake, "Nikaribieni, tafadhari." Nao wakasogea. Akawambia, "Mimi ni Yusufu ndugu yenu, mliyemwuza Misri.
\v 5 Lakini sasa msihuzunike au kukasirika miongoni mwenu kwamba mliniuza huku, kwani Mungu alinituma mbele yenu ili kutunza uhai.
\v 6 Maana ni miaka miwili njaa imekuwa katika nchi, na bado kuna miaka mitano ambayo hakutakuwa na kulima wala kuvuna.
\s5
\v 7 Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhi kama masalia duniani, na kuwaweka hai kwa ukombozi mkuu.
\v 8 Hivyo si ninyi mlionipeleka huku bali ni Mungu, na amenifanya baba kwa Farao, bwana wa nyumba yake yote, na mtawala wa nchi yote ya Misri.
\s5
\v 9 Fanyeni haraka mwende kwa baba yangu na mmwambie, 'Hivi ndivyo asemavyo Yusufu mwanao, "Mungu amenifanya bwana kwa Wamisri wote. Shuka kwangu, usikawie.
\v 10 Utaishi katika nchi ya Gosheni, nawe utakuwa karibu nami, wewe na watoto wako na watoto wa watoto wako, na kondoo wako na mbuzi wako, na yote uliyonayo.
\v 11 Nami nitakuhudumia pale, kwa maana bado kuna miaka mitano ya njaa, hivyo usije ukaingia katika uhitaji, wewe, nyumba yako, na yote uliyonayo."
\s5
\v 12 Tazama, macho yenu yanaona, na macho ya Benjamini ndugu yangu, kwamba ni kinywa changu kinachoongea nanyi.
\v 13 Mtamwambia baba yangu juu ya heshima yangu yote huku Misri na yote mliyoyaona. Mtaharakisha na kumleta baba yangu huku."
\s5
\v 14 Akaikumbatia shingo ya Benjamini ndugu yake na kulia, na Benjamini akalia shongoni mwake.
\v 15 Akawabusu ndugu zake wote na kulia kwa ajili yao. Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye.
\s5
\v 16 Habari ya jambo hili ikasemwa katika nyumba ya Farao: "Ndugu zake Yusufu wamekuja." Ikampendeza sana Farao na watumishi wake.
\v 17 Farao akamwambia Yusufu, "Wambie ndugu zako, 'Fanyeni hivi: Wapakieni wanyama wenu na mwende katika nchi ya Kanaani.
\v 18 Mchukueni baba yenu na nyumba zenu mnijie. Nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.'
\s5
\v 19 Basi mmeamriwa, 'Fanyeni hivi, chukueni mikokoteni kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na kwa ajili ya wake zenu. Mchukueni baba yenu na kuja.
\v 20 Msijari kuhusu mali zenu, kwani mema yote ya nchi ya Misri ni yenu."
\s5
\v 21 Wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yusufu akawapa mikokoteni, kwa kadili ya agizo la Farao, na akawapa mahitaji ya safari.
\v 22 Akawapa wote mavazi ya kubadilisha, lakini akampa Benjamini vipande mia tatu vya fedha na mavazi matano ya kubadilisha.
\v 23 Akampelekea baba yake: punda kumi waliobeba mema ya Misri, punda majike kumi wamebeba nafaka, mikate, na mahitaji mengine kwa baba yake kwa ajili ya safari.
\s5
\v 24 Hivyo akawaruhusu ndugu zake nao wakaondoka. Akawambia, "Angalieni msijemkagombana njiani."
\v 25 Wakapanda kutoka Misri na kuja katika nchi ya Kanaani, kwa Yakobo baba yao.
\v 26 Wakamwambia "Yusufu bado yu hai, na ndiye mtawala juu ya nchi yote ya Misri." Na moyo wake ulishikwa na ushangao, kwani hakuwaamini.
\s5
\v 27 Wakamwambia maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewambia. Yakobo alipoona mikokoteni Yusufu aliyokuwa amepeleka kuwabeba, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
\v 28 Israeli akasema, "Inatosha. Yusufu mwanangu yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa."
\s5
\c 46
\p
\v 1 Israeli akasafiri na yote aliyokuwa nayo na akaja Beersheba. Pale akatoa sadaka kwa Mungu wa Isaka baba yake.
\v 2 Mungu akamwambia Israeli katika ndoto usiku, akisema, "Yakobo, Yakobo."
\v 3 Akasema, "Mimi hapa." Akasema, "Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko.
\v 4 Nitakwenda pamoja nawe huko Misri, Nami nitakupandisha huku tena bila shaka. Na Yusufu akayafunika macho yako kwa mikono wake."
\s5
\v 5 Yakobo akainuka kutoka Beersheba. Wana wa Israeli wakamsafirisha Yakobo baba yao, watoto wao, na wake wao, katika mikokotene ambayo Farao alikuwa ameipeleka kuwachukua.
\v 6 Wakachukua mifugo yao na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani. Wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.
\v 7 Akaja Misri pamoja na wanawe na wana wa wanawe, binti zake na wana wa binti zake, na uzao wake wote.
\s5
\v 8 Haya ni majina ya watoto wa Israeli waliokuja Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo;
\v 9 wana wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi;
\v 10 wana wa Simoni, Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli, wana wa mwanamke Mkanaani;
\v 11 wana wa Lawi Gershoni, Kohathi, na Merari.
\s5
\v 12 Wana wa Yuda: Eri, Shela, Peresi, na Zera, (Lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani). Na wana wa Peresi walikuwa Hezroni na Hamuli.
\v 13 Wana wa Isakari walikuwa Tola, Puva, Lobu, na Shimroni;
\v 14 Wana wa Zabuloni walikuwa Seredi, Eloni, na Yahleeli
\v 15 Hawa walikuwa wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padani Aramu, pamoja na na Dina binti yake. Wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.
\s5
\v 16 Wana wa Gadi walikuwa Zifioni, Hagi, Shuni, Ezboni, Eri, Arodi, na Areli.
\v 17 Wana wa Asheri walikuwa Imna, Ishva, Ishvi, na Beria; na Sera alikuwa dada yao. Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malkieli.
\v 18 Hawa walikuwa wana wa Zilpa, ambaye Labani alikuwa amempa Lea binti yake. Wana aliomzalia Yakobo wote walikuwa kumi na sita.
\s5
\v 19 Wana wa Raheli mkewe Yakobo walikuwa Yusufu na Benjamini.
\v 20 Huko Misri Manase na Efraimu walizaliwa kwa Yusufu na Asenathi, binti Potifera kuhani wa Oni.
\v 21 Wana wa Benjamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi.
\v 22 Hawa walikuwa wana wa Raheli waliozaliwa kwa Yakobo - jumla yao kumi na wanne.
\s5
\v 23 Mwana wa Dani alikuwa Hushimu.
\v 24 Wana wa Naftali walikuwa Yahzeeli, Guni, Yezeri, na Shilemi.
\v 25 Hawa walikuwa wana Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alimpa Raheli binti yake - wote walikuwa saba.
\s5
\v 26 Wate waliokwenda na Yakobo, waliokuwa uzao wake, bila kuhesabu wake wa wana wa Yakobo walikuwa sitini na sita.
\v 27 Pamoja na wana wawili wa Yusufu waliozaliwa kwake huko Misri, watu wa familia yake waliokwenda Misri walikuwa sabini jumla yao.
\s5
\v 28 Yakobo akamtuma Yuda kuwatangulia mbele kwa Yusufu kuonesha njia mbele yake kwenda Gosheni, nao wakaja katika eneo la Gosheni.
\v 29 Yusufu akaandaa kibandawazi chake na akaenda kumlaki baba yake huko Gosheni. Akamwona, akaikumbatia shingo yake, na akalia shingoni mwake kwa kitambo.
\v 30 Israeli akamwambia Yusufu, "Basi na nife sasa, kwa kuwa nimeuona uso wako, kwamba bado uko hai."
\s5
\v 31 Yusufu akawambia ndungu zake na nyumba ya baba yake, "Nitakwenda na kumwambia Farao, kusema, 'Ndugu zangu na nyumba ya baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.
\v 32 Watu hawa ni wafugaji, kwani wamekuwa watunza wanyama. Wamekuja na makundi yao ya kondoo, na mbuzi, na vyote walivyonavyo.'
\s5
\v 33 Itakuwa, Farao atakapowaita na kuwauliza, 'Kazi yenu ni ipi?'
\v 34 mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa watunza wanyama tangu ujana wetu mpaka sasa, sisi, na baba zetu.' Fanyeni hivyo ili mweze kuishi katika nchi ya Gosheni, kwani kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri."
\s5
\c 47
\p
\v 1 Kisha Yusufu akaingia kwa Farao na kumwambia, "Baba yangu na ndugu zangu, kondoo wao, mbuzi wao, na yote waliyonayo, wamefika kutoka katika nchi ya Kanaani. Tazama, wapo katika nchi ya Gosheni."
\v 2 Akawachukua watano katika ndugu zake na kuwatambulisha kwa Farao.
\s5
\v 3 Farao akawambia ndugu zake, "Kazi yenu ni nini?" Wakamwambia Farao, "Watumishi wako ni wafugaji, kama mababu zetu."
\v 4 Kisha wakamwambia Farao, "Tumekuja kukaa kwa muda katika nchi. Hakuna malisho kwa ajili ya makundi ya watumishi wako, kwa maana njaa ni kali sana katika nchi ya Kanaani. Hivyo, tafadhari waache watumishi wako wakae katika nchi ya Gosheni."
\s5
\v 5 Kisha Farao akamwambia Yusufu, kusema, "Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako.
\v 6 Nchi ya Misri iko mbele yako. Mkalishe baba yako na ndugu zako katika eneo zuri, nchi ya Gosheni. Ikiwa unafahamu watu wenye uwezo miongoni mwao, uwaweke kuwatunza wanyama wangu."
\s5
\v 7 Kisha Yusufu akamwingiza Yakobo baba yake na kumweka mbele ya Farao. Yakobo akambariki Farao.
\v 8 Farao akamwambia Yakobo, "Umeishi kwa muda gani?"
\v 9 Yakobo akamwambia Farao, "Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu."
\v 10 Kisha Yakobo akambariki Farao na kuondoka mbele zake.
\s5
\v 11 Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake. Akawapa eneo katika nchi ya Misri, sehemu nzuri sana ya nchi, katika eneo la Ramesesi, kama Farao alivyokuwa ameagiza.
\v 12 Yusufu akamhudumia baba yake kwa chakula, ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake, kulingana na hesabu ya wahitaji wao.
\s5
\v 13 Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa.
\v 14 Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao.
\s5
\v 15 Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, "Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?"
\v 16 Yusufu akasema, "Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu."
\v 17 Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.
\s5
\v 18 Mwaka ule ulipokwisha, wakaja kwake mwaka uliofuata na kumwambia, "Hatutaficha kwa bwana wangu kwamba pesa yetu yote imekwisha, na wanyama ni wa bwana wangu. Hakuna kilichobaki mbele za bwana wangu, isipokuwa miili yetu na nchi yetu.
\v 19 Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu.
\s5
\v 20 Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao.
\v 21 Na watu, akawafanya kuwa watumwa kutoka mpaka mmoja wa Misri hata mkapa mwingine.
\v 22 Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua, kwa maana makuhani walikuwa wakipewa posho. Walikula katika sehemu aliyowapa Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
\s5
\v 23 Kisha Yusufu akawambia watu, "Tazama, nimewanunua ninyi na nchi yenu leo kwa ajili ya Farao. Basi mbegu hii hapa kwa ajili yenu, nanyi mtapanda katika nchi.
\v 24 Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu, kwa mbegu za shamba na kwa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu."
\s5
\v 25 Wakasema, "Umeokoa maisha yetu. Na tupate kibali machoni pako. Tutakuwa watumishi wa Farao."
\v 26 Hivyo Yusufu akaifanya kuwa sheria inayofanya kazi hata leo katika nchi ya Misri, kwamba moja ya tano ni ya Farao. Eneo la makuhani peke yake ndo halikufanywa kuwa la Farao.
\s5
\v 27 Hivyo Israeli akaishi katika nchi ya Misri, katika eneo la Gosheni. Watu wake wakapata umiliki pale. Walikuwa wenye kuzaa na kuongezeka sana.
\v 28 Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka mia moja arobaini na saba.
\s5
\v 29 Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia, alimwita Yusufu mwanaye na kumwambia, "Ikiwa nimepata kibali mbele zako, weka mkono wako chini ya paja langu, na unitendee kwa uaminifu na kweli. Tafadhari usinizike Misri.
\v 30 Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu." Yusufu akasema, "Nitafanya kama ulivyosema."
\v 31 Israeli akasema, "Niapie," na Yusufu akamwapia. Kisha Israeli akainama chini mbele ya kitanda chake.
\s5
\c 48
\p
\v 1 Ikawa baada ya mambo haya, mmojawapo akamwambia Yusufu, "Tazama, baba yako ni mgonjwa." Hivyo akaondoka pamoja na wanawe wawili, Manase na Efrahimu.
\v 2 Yakobo alipoambiwa, "Tazama, mwanao Yusufu amekuja kukuona," Israeli akakusanya nguvu na kukaa juu ya kitanda.
\s5
\v 3 Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na
\v 4 kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele.'
\s5
\v 5 Na sasa wanao wawili, waliozaliwa kwako katika nchi ya Misri kabla sijaja Misri, ni wangu. Efrahimu na Manase watakuwa wangu, kama walivyo Rubeni na Simioni.
\v 6 Watoto utakaowapata baada ya hapo ni wako; watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao.
\v 7 Lakini kwangu mimi, nilipokuja kutoka Padani, kwa uzuni yangu Raheli alikufa njiani katika nchi ya Kanaani, wakati kungalipo kitambo kwenda Efrathi. Nilimzika pale katika njia iendayo Efrathi" (ndio, Bethlehemu).
\s5
\v 8 Israeli alipowaona wana wa Yusufu, akasema, "Ni nani hawa?"
\v 9 Yusufu akamwambia baba yake, "Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa:" Israeli akasema, "Walete kwangu, kwamba niwabariki."
\v 10 Basi macho ya Israeli yalikuwa yanashindwa kwa ajili ya umri wake, hivyo hakuweza kuona. Hivyo Yusufu akawasogeza karibu yake, na akawabusu na kuwakumbatia.
\s5
\v 11 Israeli akamwambia Yusufu, "Sikutazamia kuuona uso wako tena, Lakini Mungu ameniruhusu kuwaona hata wanao."
\v 12 Yusufu akawaondoa kati ya magoti ya Israeli, na kisha akainama na uso wake juu ya nchi.
\v 13 Yusufu akawachukua wote wawili, Efrahimu katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, na akawasogeza kwake.
\s5
\v 14 Israeli akainua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto juu ya kichwa cha Manase. Akaipishanisha mikono yake, kwani Manase ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza.
\v 15 Israeli akambariki Yusufu, akisema, Mungu ambaye mbele zake baba zangu Ibrahimu na Isaka walitembea, Mungu aliyenilinda hata leo,
\v 16 malaika walionilinda na madhara yote, awabariki vijana hawa. Jina langu na litajwe kwao, na majina ya baba zangu Ibrahimu na Isaka. Na wawe makutano ya watu juu ya nchi."
\s5
\v 17 Yusufu alipoona baba yake ameweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efrahimu, haikumpendeza. Akauchukuwa mkono wa baba yake auweke katika kichwa cha Manase.
\v 18 Yusufu akamwambia baba yake, "Sivyo babangu; kwani huyu ndiye mzaliwa wa kwanza. Uweke mkono wako juu ya kichwa chake."
\s5
\v 19 Baba yake akakataa na kusema, "Ninafahamu, mwanangu, nafahamu. Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu. Lakini mdogo wake atakuwa mkuu kuliko yeye, na uzao wake utakuwa wingi wa mataifa."
\v 20 Israeli akawabariki siku hiyo kwa maneno haya, "Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema, Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase'. "Kwa njia hii, Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase.
\s5
\v 21 Israeli akamwambia Yusufu, "Tazama, ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu.
\v 22 Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu."
\s5
\c 49
\p
\v 1 Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: "Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.
\v 2 Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.
\s5
\v 3 Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu, aliyesalia katika heshima na nguvu.
\v 4 Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia.
\s5
\v 5 Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu.
\v 6 Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe.
\s5
\v 7 Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.
\s5
\v 8 Yuda, ndugu zako watakusifu. Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watainama mbele zako
\s5
\v 9 Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je nana atakayejaribu kumwamsha?
\s5
\v 10 Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake, hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii.
\s5
\v 11 Kumfunga punda wake kwenye mzabibu, na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri, amefua mavazi yake katika divai, na kanzu yake katika damu ya vichala vya mzabibu.
\v 12 Macho yake yatakuwa mausi kama mvinyo, na meno yake meupe kama maziwa.
\s5
\v 13 Zabuloni atakaa katika fukwe ya bahari. Atakuwa bandari kwa ajili ya meli, na mpaka wake utakuwa hata Sidoni.
\s5
\v 14 Isakari ni punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya kondoo.
\v 15 Anaona mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza. Atainamisha bega lake kwa mzigo na kuwa mtumishi wake.
\s5
\v 16 Dani atawaamua watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
\v 17 Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.
\v 18 Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.
\s5
\v 19 Gadi - wapanda farasi watamshambulia, lakini yeye atawapiga katika visigino vyao.
\v 20 Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme.
\v 21 Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.
\s5
\v 22 Yusufu ni tawi lizaalo, tawi lizaalo karibu na kijito, ambaye matawi yake yako juu wa ukuta.
\v 23 Mpiga mishale atamshambulia na kumrushia na kumsumbua.
\s5
\v 24 Lakini upinde wake utakuwa imara, na mikono yake itakuwa hodari kwa sababu ya mikono ya Mwenyenguvu wa Yakobo, kwa ajili ya jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli.
\s5
\v 25 Mungu wa baba yako atakusaidia na Mungu Mwenye enzi atakubariki kwa baraka mbinguni juu, baraka za vilindi vilivyo chini, na baraka za maziwa na tumbo.
\s5
\v 26 Baraka za baba yako ni kuu kuliko baraka za milima ya zamani au vitu vilivyotamaniwa vya milima ya kale. Na viwe katika kichwa cha Yusufu, hata juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake.
\s5
\v 27 Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa. Wakati wa asubuhi atalarua mawindo, na jioni atagawa mateka."
\s5
\v 28 Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.
\v 29 Kisha akawaelekeza na kuwaambia, "Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti,
\v 30 katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia.
\s5
\v 31 Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea.
\v 32 Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi."
\v 33 Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake
\s5
\c 50
\p
\v 1 Yusufu akahuzunika sana hata akauangukia uso wa baba yake, akamlilia, na kumbusu.
\v 2 Yusufu akawaagiza watumishi wake matabibu kumtia dawa babaye. Hivyo matabibu wakampaka dawa Israeli.
\v 3 Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini
\s5
\v 4 Siku za maombolezo zilipotimia, Yusufu akaongea na watumishi wa baraza la kifalme wa Farao kusema, "Ikiwa nimepata kibali machoni penu, tafadharini ongeeni na Farao, kusema,
\v 5 'Baba yangu aliniapisha, kusema, "Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika." Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi."
\v 6 Farao akajibu, "Nenda na umzika baba yako, kama alivyokuwapisha."
\s5
\v 7 Yusufu akaenda kumzika baba yake. Maofisa wa Farao wote wakaenda pamoja naye - washauri wa nyumba yake, maofisa waandamizi wote wa nchi ya Misri,
\v 8 pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake. Lakini watoto wao, kondoo wao na makundi ya mbuzi wao yaliachwa katika nchi ya Gosheni.
\v 9 Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu.
\s5
\v 10 Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale.
\v 11 Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, "Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri." Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani.
\s5
\v 12 Hivyo wanawe wakamfanyia Yakobo kama alivyokuwa amewaagiza.
\v 13 Wana wake wakampeleka katika nchi ya Kanaani na wakamzika katika pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre. Ibrahimi alikuwa amelinunua pango pamoja na shamba kwa ajili ya eneo la kuzikia. Alikuwa amelinunua kutoka kwa Efroni Mhiti.
\v 14 Baada ya kuwa amemzika babaye, Yusufu akarudi Misri, yeye, pamoja na ndugu zake, na wote waliokuwa wamemsindikiza ili kumzika babaye.
\s5
\v 15 Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, "Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?"
\v 16 Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, "Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema,
\v 17 'Mwambieni hivi Yusufu, "Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda." Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako." Yusufu akalia walipomwambia.
\s5
\v 18 Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, "Tazama, sisi ni watumishi wako."
\v 19 Lakini Yusufu akawajibu, "Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu?
\v 20 Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo.
\v 21 Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo." Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.
\s5
\v 22 Yusufu akakaa Misri, pamoja na familia ya baba yake. Akaishi miaka mia moja na kumi.
\v 23 Yusufu akawaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu. Pia aliwaona wana wa Makiri mwana wa Manase, waliowekwa katika magoti ya Yusufu.
\s5
\v 24 Yusufu akawambia ndugu zake, "Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nch aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo."
\v 25 Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, "Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukuwa mifupa yangu kutoka hapa."
\v 26 Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.