initial upload

This commit is contained in:
Larry Versaw 2017-11-08 14:23:27 -07:00
parent fab9e05565
commit ef6eb4efe6
28 changed files with 15496 additions and 0 deletions

1997
41-MAT.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1997 @@
\id MAT
\ide UTF-8
\h Mathayo
\toc1 Mathayo
\toc2 Mathayo
\toc3 mat
\mt Mathayo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
\v 2 Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.
\v 3 Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.
\s5
\v 4 Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.
\v 5 Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,
\v 6 Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.
\s5
\v 7 Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.
\v 8 Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.
\s5
\v 9 Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.
\v 10 Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.
\v 11 Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.
\s5
\v 12 Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.
\v 13 Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.
\v 14 Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.
\s5
\v 15 Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.
\v 16 Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.
\v 17 Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.
\s5
\v 18 Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
\v 19 Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.
\s5
\v 20 Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
\v 21 Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''
\s5
\v 22 Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,
\v 23 "Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli"-- maana yake, "Mungu pamoja nasi."
\s5
\v 24 Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.
\v 25 Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema,
\v 2 "Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu."
\v 3 Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.
\s5
\v 4 Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, "Kristo atazaliwa wapi?"
\v 5 Wakamwabia, "Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
\v 6 Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli."
\s5
\v 7 Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana.
\v 8 Akawatuma Bethelehem, akisema, "Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu."
\s5
\v 9 Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa.
\v 10 Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.
\s5
\v 11 Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane.
\v 12 Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.
\s5
\v 13 Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, "Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.
\v 14 Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri.
\v 15 Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, "Kutoka Misri nimemwita mwanangu."
\s5
\v 16 Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.
\s5
\v 17 Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia,
\v 18 "Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena."
\s5
\v 19 Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema,
\v 20 "Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa."
\v 21 Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.
\s5
\v 22 Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya
\v 23 na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema,
\v 2 "Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu."
\v 3 Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, "sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; 'wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake."'
\s5
\v 4 Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
\v 5 Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake.
\v 6 Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.
\s5
\v 7 Lakini alipowaona wengi wa mafarisayo na masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, ''Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
\v 8 Zaeni matunda yaipasayo toba.
\v 9 Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, 'Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.' Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.
\s5
\v 10 Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto.
\v 11 Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
\v 12 Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
\s5
\v 13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana.
\v 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, "Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?''
\v 15 Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu.
\s5
\v 16 Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake.
\v 17 Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, "Huyu ni mwanangu mpendwa. Ninaye pendezwa sana naye.''
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi.
\v 2 Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.
\v 3 Mjarabu akaja na akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate."
\v 4 Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, "Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.'''
\s5
\v 5 Kisha ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu,
\v 6 na kumwambia,'' kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, 'Ataamuru malaika wake waje wakudake,' na, 'watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe."
\s5
\v 7 Yesu akamwambia, ''Tena imeandikwa, 'Usimjaribu Bwana Mungu wako.'''
\v 8 Kisha, ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote.
\v 9 Akamwambia, "Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu."
\s5
\v 10 Kisha Yesu akamwambia, "Nenda zako utoke hapa, Shetani! Kwa maana imeandikwa, 'Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.'"
\v 11 Kisha ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.
\s5
\v 12 Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya.
\v 13 Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.
\s5
\v 14 Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya,
\v 15 "Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea Baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa!
\v 16 Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.''
\s5
\v 17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
\s5
\v 18 Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.
\v 19 Yesu akawaambia, "Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu."
\v 20 Mara moja waliziacha nyavu na walimfuata.
\s5
\v 21 Na Yesu alipokuwa akiendelea kutoka hapo aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita,
\v 22 na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.
\s5
\v 23 Yesu alienda karibia Galilaya yote, akifundisha katika Masinagogi yao, akihubiri injili ya ufalme, na akiponya kila aina ya maradhi na magonjwa miongoni mwa watu.
\v 24 Habari zake zilienea Siria yote, na watu wakawaleta kwake wale wote waliokuwa wakiugua, wakiwa na maradhi mbalimbali na maumivu, waliokuwa na mapepo, na wenye kifafa na waliopooza. Yesu aliwaponya.
\v 25 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.
\v 2 Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,
\v 3 "Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
\v 4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
\s5
\v 5 Heri wenye upole, maana watairithi nchi.
\v 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.
\v 7 Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema.
\v 8 Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.
\s5
\v 9 Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
\v 10 Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
\s5
\v 11 Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.
\v 12 Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.
\s5
\v 13 Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.
\v 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.
\s5
\v 15 Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.
\v 16 Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.
\s5
\v 17 Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza.
\v 18 Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.
\s5
\v 19 Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
\v 20 Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.
\s5
\v 21 Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, "usiue" na 'yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.'
\v 22 Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, 'Wewe ni mtu usiyefaa!' atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, 'Wewe mjinga!' atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.
\s5
\v 23 Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako,
\v 24 iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.
\s5
\v 25 Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.
\v 26 Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.
\s5
\v 27 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Usizini.'
\v 28 Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
\s5
\v 29 Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.
\v 30 Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.
\s5
\v 31 Imenenwa pia, yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.'
\v 32 Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.
\s5
\v 33 Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, 'Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.'
\v 34 Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu;
\v 35 wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Jerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.
\s5
\v 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
\v 37 Bali maneno yenu yawe, 'Ndiyo, ndiyo, Hapana, hapana.' Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
\s5
\v 38 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.'
\v 39 Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.
\s5
\v 40 Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia.
\v 41 Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.
\v 42 Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.
\s5
\v 43 Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.'
\v 44 Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,
\v 45 Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.
\s5
\v 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?
\v 47 Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?
\v 48 Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni.
\v 2 Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
\s5
\v 3 Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia,
\v 4 ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
\s5
\v 5 Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao.
\v 6 Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
\v 7 Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.
\v 9 Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako.
\v 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
\s5
\v 11 Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku.
\v 12 utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu.
\v 13 Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.'
\s5
\v 14 Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi.
\v 15 Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
\s5
\v 16 Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
\v 17 Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako.
\v 18 Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.
\s5
\v 19 Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.
\v 20 Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.
\v 21 Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.
\s5
\v 22 Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru.
\v 23 Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani!
\v 24 Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.
\s5
\v 25 Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
\v 26 Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?
\s5
\v 27 Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake?
\v 28 Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.
\v 29 Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.
\s5
\v 30 Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?
\v 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au "Je tutakunywa nini?" au "Je tutavaa nguo gani?"
\s5
\v 32 Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo.
\v 33 Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
\v 34 Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.
\v 2 Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.
\s5
\v 3 Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?
\v 4 Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?
\v 5 Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.
\s5
\v 6 Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.
\s5
\v 7 Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
\v 8 Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.
\v 9 Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe?
\v 10 Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
\s5
\v 11 Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?
\v 12 Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.
\s5
\v 13 Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo.
\v 14 Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.
\s5
\v 15 Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali.
\v 16 Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti?
\v 17 Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.
\s5
\v 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.
\v 19 Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.
\v 20 Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.
\s5
\v 21 Si kila mtu aniambiaye mimi, 'Bwana, Bwana,' ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
\v 22 Watu wengi wataniambia siku hiyo, 'Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?'
\v 23 Ndipo nitawaambia wazi, 'sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!'
\s5
\v 24 Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
\v 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
\s5
\v 26 Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
\v 27 Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika."
\s5
\v 28 Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake,
\v 29 kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.
\v 2 Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, "Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi".
\v 3 Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, "Niko tayari. Uwe msafi." Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.
\s5
\v 4 Yesu akamwambia, "Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao"
\s5
\v 5 Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza
\v 6 akisema, "Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha."
\v 7 Yesu akamwambia, "Nitakuja na kumponya".
\s5
\v 8 Jemedari akajibu na kumwambia, "Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa.
\v 9 Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu "Nenda' na huenda, na kwa mwingine 'Njoo' na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, 'Fanya hivi,' na yeye anafanya hivyo"
\v 10 Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, "Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.
\s5
\v 11 Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni.
\v 12 Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno."
\v 13 Yesu akamwambia Jemadari, "Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako". Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.
\s5
\v 14 Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa.
\v 15 Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. kisha akaamka akaanza kumhudumia.
\s5
\v 16 Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya.
\v 17 Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, "Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu"
\s5
\v 18 Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa Bahari ya Galilaya.
\v 19 Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, "Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda."
\v 20 Yesu akamwambia, "Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake."
\s5
\v 21 Mwanafunzi mwingine akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu."
\v 22 Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao."
\s5
\v 23 Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini.
\v 24 Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala.
\v 25 Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!"
\s5
\v 26 Yesu akawaambia, "kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?" Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu,
\v 27 wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, "Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?"
\s5
\v 28 Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.
\v 29 Tazama, walipaza sauti na kusema, "Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?"
\s5
\v 30 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa,
\v 31 pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. "Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe."
\v 32 Yesu akawaambia, "Nendeni!" Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.
\s5
\v 33 Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, hususani kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo.
\v 34 Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.
\v 2 Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. alipooiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, uwe na furaha, Dhambi zako zimesamehewa"
\s5
\v 3 Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, "Huyu mtu anakufuru"
\v 4 Yesu akatambua mawazo yao na kusema, "Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?
\v 5 Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?'
\v 6 Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi..." aliyasema haya kwa yule aliyepooza, "Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako"
\s5
\v 7 Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.
\v 8 Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.
\v 9 Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, "Nifuate mimi" Naye akasimama na kumfuata.
\s5
\v 10 Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake.
\v 11 Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi "Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?"
\s5
\v 12 Yesu aliposikia hayo, naye alisema " Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa.
\v 13 Inawapasa muende mkajifunze maana yake, "Ninapenda rehema na siyo dhabihu" Kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.
\s5
\v 14 Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, "Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?"
\v 15 Yesu akawaambia, Je wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.
\s5
\v 16 Hakuna mtu anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani, kiraka kitatatuliwa kutoka kwenye nguo na mpasuko mkubwa utatokea.
\s5
\v 17 Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika chombo cha mvinyo wa zamani, ikiwa watafanya, ngozi itachanika, mvinyo utatoweka na ngozi itaharibika. Badala yake, huweka mvinyo mpya katika ngozi mpya na vyote vitakuwa salama.
\s5
\v 18 Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, Naye akasema, " Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena.
\v 19 Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia.
\s5
\v 20 Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake.
\v 21 Kwa kuwa alisema, "Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji."
\v 22 Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. "Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone," Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji muda huo.
\s5
\v 23 Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.
\v 24 Naye akasema, "Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala. Lakini wao walicheka na kumkebehi.
\s5
\v 25 Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka.
\v 26 Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.
\s5
\v 27 Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, "Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi."
\v 28 Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, "Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?" Nao wakamwambia "Ndiyo, Bwana"
\s5
\v 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema "Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo"
\v 30 Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema "Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili."
\v 31 Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.
\s5
\v 32 Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, Tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu.
\v 33 Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema "Hii haijawahi kutokea katika Israel.
\v 34 Lakini mafarisayo walikuwa wakisema " Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo"
\s5
\v 35 Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.
\v 36 Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.
\s5
\v 37 Naye akawaambia wanafunzi wake. "Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache.
\v 38 Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maladhi na aina zote za magonjwa.
\s5
\v 2 Majina ya mitume kumi na wawili ni haya. La kwanza simeoni (ambaye pia anaitwa Petro), na Andrea kaka yake, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake:
\v 3 Philipo, na Bartelemayo, Thomaso, na Mathayo mtoza ushuru, Yakobo mwana wa Alfayo, na Tadeo,
\v 4 Simoni mkananayo, na Yuda iskariote, ambaye alimsaliti.
\s5
\v 5 Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema "Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya wasamalia.
\v 6 Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel.
\v 7 Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ufalme wa mbinguni umekaribia.'
\s5
\v 8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.
\v 9 Msichue dhahabu, almasi au shaba kwenye pochi zenu.
\v 10 Usichukue mkoba katika safari yenu, au nguo za ziada, viatu au fimbo, kwa kuwa mfanyakazi anastahili chakula chake.
\s5
\v 11 Mji wowote au kijiji mtakachoingia, tafuteni ambaye anastahili na mkae pale mpaka mtakapoondoka.
\v 12 Mtakapoingia katika nyumba salimieni,
\v 13 endapo nyumba inastahili, amani yenu ibaki pale, lakini kama nyumba haistahili, amani yenu iondoke pamoja nanyi.
\s5
\v 14 Na kwa wale wasiowapokea ninyi au kusikiliza maneno yenu, wakati mnaondoka kwenye nyumba au mji huo, jipanguseni mavumbi ya nyayo zenu mahali hapo.
\v 15 Kweli ninawaambia, itakuwa ya kustahimili zaidi miji ya Sodoma na Gomorah siku ya hukumu kuliko mji huo.
\s5
\v 16 Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.
\v 17 Muwe waangalifu na watu, watawapeleka kwenye mabaraza, na watawapiga kwenye masinagogi.
\v 18 Na mtaletwa mbele ya wakuu na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao na kwa mataifa.
\s5
\v 19 Pindi watakapowashutumu, msiwe na wasiwasi jinsi gani au nini cha kuongea, kwa kuwa kitu cha kusema mtapewa kwa wakati huo.
\v 20 Kwa kuwa sio ninyi mtakaoongea, lakini Roho wa Baba yenu ataongea ndani yenu.
\s5
\v 21 Ndugu atamwinukia ndugu yake kumwua, na baba kwa mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi, na kuwasababishia kifo.
\v 22 Nanyi mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini yeyote atakayevumilia mpaka mwisho mtu huyo ataokolewa.
\v 23 Pindi wanapowatesa katika mji huu, kimbilieni mji unaofuata, kwa kweli ninawaambia, hamtakuwa mmekwenda kwenye miji yote ya Israeli kabla ya mwana wa Adam hajarudi.
\s5
\v 24 Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya Bwana wake.
\v 25 Inatosha kwa mwanafunzi kwamba awe kama mwalimu wake, na mtumishi kama Bwana wake. Ikiwa wamemwita Bwana wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi watawakashifu wa nyumba yake!
\s5
\v 26 Hivyo basi msiwahofu wao, kwa kuwa hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililofichika ambalo halitajulikana.
\v 27 Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba.
\s5
\v 28 Msiwaogope wale ambao wanaua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho. Badala yake, mwogopeni yule ambaye awezaye kuangamiza mwili na roho kule kuzimu.
\v 29 Je kasuku wawili hawauzwi kwa senti ndogo? Hata hivyo hakuna anayeweza kuanguka chini bila Baba yenu kufahamu.
\v 30 Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa.
\v 31 Msiwe na hofu, kwa kuwa mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi.
\s5
\v 32 Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
\v 33 Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
\s5
\v 34 Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga.
\v 35 Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.
\v 36 Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake.
\s5
\v 37 Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili.
\v 38 Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili.
\v 39 Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata.
\s5
\v 40 Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi.
\v 41 Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki.
\s5
\v 42 Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
\v 2 na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
\v 3 na wakamuuliza, "Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?"
\s5
\v 4 Yesu akajibu na kusema kwao "Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.
\v 5 Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema.
\v 6 Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.
\s5
\v 7 Pindi watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, "Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa __tete likitikiswa na upepo?
\v 8 Lakini nini mlikwenda kuona__mtu aliyevaa mavazi mololo? Hakika, wale wavaao mavazi mololo hukaa katika nyumba za wafalme.
\s5
\v 9 Lakini mliondoka kuona nini-Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.
\v 10 Huyu ndiye aliyeandikiwa, 'Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.
\s5
\v 11 Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.
\v 12 Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.
\s5
\v 13 Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.
\v 14 Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.
\v 15 Aliye na masikio ya kusikia na asikie.
\s5
\v 16 Nikilinganishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana
\v 17 na kusema, 'Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.'
\s5
\v 18 Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, 'Ana pepo.'
\v 19 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''
\s5
\v 20 Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu,
\v 21 Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yangetendeka Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka hapa, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.
\v 22 Lakini itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko kwako.
\s5
\v 23 Wewe, Kapernaum, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo.
\v 24 Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.
\s5
\v 25 Katika muda huo Yesu alisema, "Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.
\v 26 Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.
\v 27 Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.
\s5
\v 28 Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.
\v 29 Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu.
\v 30 Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.
\v 2 Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu "Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda siku yasiyo yuhusiwa siku ya Sabato''
\s5
\v 3 Lakini Yesu akawaambia, "Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao?
\v 4 Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate ya wonyesho, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa Makuhani?
\s5
\v 5 Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato Makuhani ndani ya hekalu huinajisi Sabato, lakini hawana hatia?
\v 6 Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa.
\s5
\v 7 Kama mngalijua hii ina maanisha nini; nataka rehema na siyo dhabihu; msingaliwahukumu wasio na hatia,
\v 8 Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato."
\s5
\v 9 Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao.
\v 10 Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. "Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?" ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi.
\s5
\v 11 Yesu akawaambia, "Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?
\v 12 Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo! Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.''
\s5
\v 13 Kisha Yesu akamwambia yule mtu," Nyoosha mkono wako" Akaunyoosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.
\v 14 Lakini Mafarisayo wakatoka njena wakapanga jinsi ya kumwangamiza walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua.
\s5
\v 15 Yesu alipoelewa hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaaponya wote.
\v 16 Aliwaagiza wasije wakamfanya afahamike kwa wengine,
\v 17 kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema,
\s5
\v 18 Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa Mataifa.
\s5
\v 19 Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani.
\v 20 Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda.
\v 21 Na Mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake.
\s5
\v 22 Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona.
\v 23 Makutano wote walishangaa na kusema,"Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?"
\s5
\v 24 Lakini pindi Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, "Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo.
\v 25 "Lakini Yesu alifahamu fikra zao na kuwaambia, "Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama.
\s5
\v 26 Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe.
\v 27 Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu huwatatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu.
\s5
\v 28 Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu.
\v 29 Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndiyo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba.
\v 30 Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya.
\s5
\v 31 Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.
\v 32 Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao
\s5
\v 33 Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake.
\v 34 Nyinyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni.
\v 35 Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu.
\s5
\v 36 Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.
\v 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa."
\s5
\v 38 Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema" Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako."
\v 39 Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, "Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.
\v 40 Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.
\s5
\v 41 Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Yona yuko hapa.
\s5
\v 42 Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Selemani yupo hapa.
\s5
\v 43 Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni
\v 44 Kisha husema, 'nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.' Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari.
\v 45 Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu.
\s5
\v 46 Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.
\v 47 Mtu mmoja akamwambia, "Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe".
\s5
\v 48 Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, "Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?"
\v 49 Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, "Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!
\v 50 Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu".
\s5
\c 13
\p
\v 1 Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.
\v 2 Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama kando ya bahari.
\s5
\v 3 Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, "Tazama, mpanzi alienda kupanda.
\v 4 Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.
\v 5 Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.
\v 6 Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.
\s5
\v 7 Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.
\v 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini
\v 9 Aliye na masikio na asikie.
\s5
\v 10 Wanafunzi walikuja na kumwambia Yesu, "Kwa nini unazungumza na makutano kwa mifano?"
\v 11 Yesu alijibu kuwaambia, "Mmepewa upendeleo wa kufahamu siri za ufalme wa mbinguni, bali kwao hawajapewa.
\v 12 Lakini yeyote aliyenacho, kwake yeye ataongezewa zaidi, na atapata faida kubwa. Ilasiye nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa.
.
\s5
\v 13 Hivyo naongea nao kwa mifano kwa sababu ingawa wanaona, wasione kweli. Na ingawa wanasikia wasisikie wala kufahamu.
\v 14 Unabii wa Isaya umetimia kwao, ule usemao, "Msikiapo msikie, lakini kwa namna yoyote hamtaelewa; wakati mwonapo muweze kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue.
\s5
\v 15 Na mioyo ya watu hawa imekuwa giza, ni vigumu kusikia, na wamefumba macho yao, ili wasiweze kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao, au kufahamu kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena, na ningewaponya.'
\s5
\v 16 Bali macho yenu yamebarikiwa, kwa kuwa yanaona, na masikio yenu kwa kuwa yanasikia.
\v 17 Hakika nawaambia manabii wengi na watu wenye haki walikuwa na hamu ya kuyaona mambo yale myaonayo, na hawakuweza kuyaona. Walitamani kusikia mambo yale mnayosikia, hawakuyasikia.
\s5
\v 18 . Sasa sikilizeni mfano wa mpanzi.
\v 19 Wakati yeyote asikiapo neno la ufalme na asilifahamu, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kupandwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.
\s5
\v 20 Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.
\v 21 Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.
\s5
\v 22 Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.
\v 23 Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.''
\s5
\v 24 Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, "Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake
\v 25 Lakini watu waliposinzia, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake.
\v 26 Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia.
\s5
\v 27 Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, 'Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu?
\v 28 Akawaambia, Adui ametenda hili.' Watumishi walimwambia, "Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?"
\s5
\v 29 Mwenye shamba akisema, 'Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano.
\v 30 Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, 'Kwanza yang'oeri magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.''''
\s5
\v 31 Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, "Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake.
\v 32 Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake."
\s5
\v 33 Akawaambia mfano mwingine tena."Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke.
\s5
\v 34 Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao.
\v 35 Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, "Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu".
\s5
\v 36 Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, "Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.''
\v 37 Yesu alijibu na kusema, "Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
\v 38 Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni ibilisi.
\v 39 Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.
\s5
\v 40 Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu.
\v 41 Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi.
\v 42 Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\v 43 Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na sikie.
\s5
\v 44 Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba.
\v 45 Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani.
\v 46 Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.
\s5
\v 47 Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina.
\v 48 Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali.
\s5
\v 49 Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki.
\v 50 Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno.
\s5
\v 51 Mmefahamu mambo yote haya? Wanafunzi walimjibu, ''Ndiyo.''
\v 52 Kisha Yesu akawambia, ''Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.''
\v 53 IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo.
\s5
\v 54 Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, "Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?
\v 55 Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda?
\v 56 Na dada zake tunao hapa petu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?".
\s5
\v 57 Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, "Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao.
\v 58 Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu..
\v 2 Akawaambia watumishi wake, "Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake."
\s5
\v 3 Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.
\v 4 Kwa kuwa Yohana alimwambia, "Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake."
\v 5 Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.
\s5
\v 6 Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.
\v 7 Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.
\s5
\v 8 Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, "Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\v 9 Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.
\s5
\v 10 Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani
\v 11 ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.
\v 12 Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.
\s5
\v 13 Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.
\v 14 Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao.
\s5
\v 15 Jioni ilipotimia, wanafunzi wakaja kwake na kusema, "Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao.
\s5
\v 16 Lakini Yesu akawaambia, ''Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula"
\v 17 Wakamwambia, ''Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu."''
\v 18 Yesu akasema, "Ileteni kwangu."
\s5
\v 19 Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini ya nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati.
\v 20 Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili.
\v 21 Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.
\s5
\v 22 Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.
\v 23 Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.
\v 24 Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mpisho.
\s5
\v 25 Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.
\v 26 Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, "Ni mzuka,'' na kupaaza sauti katika hali ya uoga.
\v 27 Yesu akawaambia mara moja, akisema, "Jipeni moyo! ni mimi! msiogope."
\s5
\v 28 Petro alimjibu kwa kusema, "Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.''
\v 29 Yesu akasema, "Njoo.'' Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.
\v 30 Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, "Bwana, niokoe!''
\s5
\v 31 Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, "Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?"
\v 32 Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulikoma kuvuma.
\v 33 Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, "Kweli wewe ni Mwana wa Mungu."
\s5
\v 34 Na walipokwisha kuvuka, walifika katika nchi ya Genesareti.
\v 35 Na watu katika eneo lile walipomtambua Yesu, walituma ujumbe kila sehemu za kando, na kuleta kila aliyekuwa mgonjwa.
\v 36 Walimsihi kwamba waweze kugusha pindo la vazi lake, na wengi walioligusa waliponywa.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,
\v 2 "Kwa nini wanafunzi wanayahalifu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.''
\v 3 Yesu akawajibu na kuwaambia, "Nanyi__kwa nini mnaihalifu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?
\s5
\v 4 Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.'
\v 5 Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '"Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,'''
\v 6 "Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
\s5
\v 7 Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,
\v 8 'Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
\v 9 Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu."'
\s5
\v 10 Ndipo akawaita makutano na kuwaambia," Sikilizeni na mfahamu__
\v 11 Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.''
\s5
\v 12 Ndipo wanafunzi wakamwendea na kusema na Yesu, "Je!, Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?"
\v 13 Yesu aliwajibu na kusema, "Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.
\v 14 Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni."
\s5
\v 15 Petro akajibu na kumwambia Yesu," Tuelezee mfano huu kwetu,
\v 16 Yesu akajibu, ''Nanyi pia bado hamuelewi?
\v 17 Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?.
\s5
\v 18 Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.
\v 19 Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.
\v 20 Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi."
\s5
\v 21 Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.
\v 22 Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, ''Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.''
\v 23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsihi, wakisema, ''Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.''
\s5
\v 24 Yesu aliwajibu na kusema, Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.''
\v 25 Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, ''Bwana nisaidie.''
\v 26 Alimjibu na kusema, "Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa,"
\s5
\v 27 Akasema, "Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao."
\v 28 Ndipo Yesu akajibu na akisema "Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo." Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.
\s5
\v 29 Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko.
\v 30 Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya.
\v 31 Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.
\s5
\v 32 Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, " Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani."
\v 33 Wanafunzi wake wakamwambia, "Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkuwbwa hivi?"
\v 34 Yesu akawaambia, "Mna mikate mingapi?" Wakasema, "Saba, na samaki wadogo wachache."
\v 35 Yesu akawaamuru umati uketi chini.
\s5
\v 36 Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.
\v 37 Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.
\v 38 Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.
\v 39 Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Mafarisayo na Masadukayo walimjia na kumjaribu Yesu awaonyeshe ishara inayotoka angani.
\v 2 Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kuwa "Ikiwa ni jioni mnasema kuwa hali ya hewa ni nzuri, kwa kuwa anga ni jekundu.
\s5
\v 3 Na asubuhi mnasema 'Hali ya hewa leo si nzuri kwa kuwa anga ni jekundu na mawingu yameifunika anga lote.' Mnajua kufasiri mwonekano wa anga, lakini hamwezi kufasiri ishara za nyakati.
\v 4 Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakuna ishara yoyote kitakachopewa, isipokuwa ile ya Yona. Kisha Yesu akawaacha na akaenda zake.
\s5
\v 5 Wanafunzi wakaja upande wa pili, lakini walikuwa wamesahau kuchukua mikate.
\v 6 Yesu akawaambia " Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo."
\v 7 Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. "Ni kwa sababu hatukuchukua mikate."
\v 8 Yesu alitambua hilo na kusema, "Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate?
\s5
\v 9 Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya?
\v 10 Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlikuchukua?
\s5
\v 11 Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo."
\v 12 Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
\s5
\v 13 Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, "Watu wanasema kuwa Mwana wa Mtu ni nani?"
\v 14 Wakasema," Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii.
\v 15 Akawaambia, ninyi mwasema mimi ni nani?
\v 16 Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, "Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai"
\s5
\v 17 Yesu akamjibu na kumwambia, "Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
\v 18 Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda.
\s5
\v 19 Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni."
\v 20 Kisha Yesu akawaamuru wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye alikuwa ni Kristo.
\s5
\v 21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.
\v 22 Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, kwa kusema, "Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako.
\v 23 Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, "Rudi nyuma yangu shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu."
\s5
\v 24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kama mtu yeyote akitaka kunifuata mimi, ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.
\v 25 Kwa kuwa anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na kwa yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
\v 26 Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?
\s5
\v 27 Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika wake. Naye atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.
\v 28 Kweli nawaambieni kuna baadhi yenu mliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.
\v 2 Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.
\s5
\v 3 Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.
\v 4 Petro akajibu na kumwambia Yesu, "Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya."
\s5
\v 5 Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye."
\v 6 Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.
\v 7 Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, "Inukeni wala msiogope."
\v 8 Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.
\s5
\v 9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, "Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu."
\v 10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, " Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?
\s5
\v 11 Yesu akawajibu na kusema, "Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.
\v 12 Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao."
\v 13 Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.
\s5
\v 14 Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,
\v 15 "Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.
\v 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
\s5
\v 17 Yesu akajibu akisema, "Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu."
\v 18 Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.
\s5
\v 19 Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, "Kwanini hatukuweza kumfukuza?"
\v 20 Yesu akawaambia, "Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.
\v 21 (Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 "Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga" hayaonekani katika nakala bora za kale).
\s5
\v 22 Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, "Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.
\v 23 Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka." Wanafunzi walihuzunika sana.
\s5
\v 24 Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, "Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?"
\v 25 Akasema, "Ndiyo" Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, " Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni?
\s5
\v 26 Na wakati Petro aliposema, "Kutoka kwa wageni" Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.
\v 27 Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, "Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?"
\v 2 Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao,
\v 3 na kusema, "Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
\s5
\v 4 Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.
\v 5 Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi.
\v 6 Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari.
\s5
\v 7 Ole kwa dunia kwa sababu ya wakati wa kukwazwa! kwa kuwa haina budi kwa nyakati hizo kuja, lakini ole kwake kwa mtu yule nyakati hizo zitakuja kwa ajili yake!
\v 8 kama mkono wako au mguu wako ukikusababishia kukwazika, ukate na uutupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe kuingia kwenye uzima ukiwa bila mkono au kilema, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote au miguu yote.
\s5
\v 9 Kama jicho lako likikukwaza, uling`oe na ulitupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe uingie kwenye uzima na jicho moja, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na macho yote.
\s5
\v 10 Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
\v 11 (Zingatia: Maneno yanayoonekana kama ya msitari wa 11, "Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichokuwa kimepotea" hayakuonekana katika nakala bora za kale).
\s5
\v 12 Mnafikiri nini? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je hatawaacha tisini na tisa ya mlimani na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea?
\v 13 Na akiisha kumpata, kweli nawaambieni, anamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
\v 14 Vivyo hivyo, siyo mapenzi ya Baba yenu wa mbinguni kuwa mmoja wa wadogo hawa aangamie.
\s5
\v 15 Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako.
\v 16 Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa.
\s5
\v 17 Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
\s5
\v 18 Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa.
\v 19 Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya.
\v 20 Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.
\s5
\v 21 Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, "Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?"
\v 22 Yesu akamwambia, "Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba.
\s5
\v 23 Kwa sababu hiyo ufalme wa mbinguni ni sawa na mfalme fulani aliyetaka kusahihisha hesabu kutoka kwa watumwa wake.
\v 24 Alipoanza kusahihisha hesabu, mtumwa moja akaletwa kwake ambaye alikuwa anamdai talanta elfu kumi.
\v 25 Kwa kuwa hakuwa na njia ya kulipa, bwana wake aliagiza auzwe, mke wake pamoja na watoto wake na kila kitu alichokuwa nacho, na malipo yafanyike.
\s5
\v 26 Hivyo mtumwa alianguka, akapiga magoti mbele yake, akisema, 'Bwana, uwe na uvumilivu pamoja nami, na nitakulipa kila kitu.'
\v 27 Hivyo bwana wa yule mtumwa, kwa kuwa alisukumwa sana na huruma, alimwachilia na kumsamehe deni hilo
\s5
\v 28 Lakini mtumwa yule alitoka na kumpata mmoja kati ya watumwa wenzake, aliyekuwa anamdai denari mia. Alimvuta, akamkaba kooni, na kumwambia, 'Nilipe kile ninachokudai.'
\v 29 Lakini yule mtumwa mwenzake alianguka na kumsihi sana, akisema, 'Uwe na uvumilivu nami, na nitakulipa.'
\s5
\v 30 Lakini mtumwa yule wa kwanza alikataa. Badala yake, alienda na kumtupa gerezani, mpaka atakapo mlipa kile anachomdai.
\v 31 Na walipoona watumwa wenzake kile kilichotokea. Walisikitishwa sana. Walikuja na kumwambia bwana wao kila kitu kilichotokea.
\s5
\v 32 Ndipo yule bwana wa mtumwa yule alimwita, na kumwambia, 'Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni langu lote kwa sababu ulinisihi sana.
\v 33 Je! Haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio, kama mimi nilivyokuhurumia wewe?
\s5
\v 34 Bwana wake alikasirika na kumkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa kiasi chote alichokuwa anadaiwa.
\v 35 Hivyo ndivyo Baba yangu wa Mbinguni atakavyowafanyia, kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwenu."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ilitokea wakati Yesu alipomaliza maneno hayo, akaondoka Galilaya, na akaenda mpakani mwa Yudea mbele ya mto Jordani.
\v 2 Umati mkubwa ukamfuata, na akawaponya huko.
\s5
\v 3 Mafarisayo wakamjia, wakamjaribu, wakamwambia, "Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?"
\v 4 Yesu akajibu na kusema, "Hamkusoma, kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke?
\s5
\v 5 Na tena akasema, 'Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?'
\v 6 Hivyo siyo wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, kile alichokiunganisha Mungu, mtu yeyote asikitenganishe."
\s5
\v 7 Wakamwambia, "Sasa kwa nini Musa alituamuru kutoa hati ya talaka na kumwacha?"
\v 8 Akawaambia, "Kwa ugumu wenu wa mioyo Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.
\v 9 Nawaambieni, kwamba yeyote atayemwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, na akamwoa mwingine, amezini. Na mwanaume atakayemwoa mke aliyeachwa amezini."
\s5
\v 10 Wanafunzi wakamwambia Yesu, "Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa."
\v 11 Lakini Yesu akawaambia, "Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea.
\v 12 Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vilevile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee."
\s5
\v 13 Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea.
\v 14 Bali Yesu akasema, "Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.
\v 15 Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.
\s5
\v 16 Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, "Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?"
\v 17 Yesu akamwambia, "Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu."
\s5
\v 18 Yule mtu akamwuliza, "Ni sheria zipi?" Yesu akasema, "Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,
\v 19 waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako."
\s5
\v 20 Mtu yule akamwambia, "Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini?
\v 21 "Yesu akamwambia, "Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate."
\v 22 Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na amemiliki mali nyingi.
\s5
\v 23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kweli nawaambieni, ni vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.
\v 24 Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 25 Wanafunzi waliposikia hivyo, wakashangaa sana na kusema, "Ni yupi basi atakayeokoka?"
\v 26 Yesu akawatazama na kusema, "Kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana."
\v 27 Kisha Petro akamjibu na kumwambia, "Tazama, tumeacha vyote na kukufuata wewe. Ni kitu gani tutakachopata?"
\s5
\v 28 Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, yeye aliyenifuata mimi, katika uzao mpya wakati Mwana wa Adam atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake, ninyi pia mtaketi juu ya viti kumi na viwili vya enzi, kuwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
\s5
\v 29 Kila mmoja wenu aliyeacha nyumba, kaka, dada, baba, mama, watoto, au shamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele.
\v 30 Lakini wengi walio wa kwanza sasa, watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu.
\v 2 Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.
\s5
\v 3 Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.
\v 4 Akawaambia, 'Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.' Hivyo wakaenda kufanya kazi.
\s5
\v 5 Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo.
\v 6 Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, 'kwanini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?
\v 7 Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, 'Nanyi ninyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.'
\s5
\v 8 Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, 'Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.'
\v 9 Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.
\v 10 Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu.
\s5
\v 11 Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba.
\v 12 Wakasema, 'Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.'
\s5
\v 13 Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, 'Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja?
\v 14 Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe.
\s5
\v 15 Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?
\v 16 Hivyo wa mwisho atakuwa kwanza na wa kwanza wa mwisho''
\s5
\v 17 Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,
\v 18 ''Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo
\v 19 na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulibisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.''
\s5
\v 20 Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake.
\v 21 Yesu akamwambia, "Unataka nini?" Akamwambia, ''Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.''
\s5
\v 22 Lakini Yesu akajibu na kusema, "Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?" wakamwambia, "Tunaweza."
\v 23 Akawaambia, "Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu."
\v 24 Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.
\s5
\v 25 Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, "Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao.
\v 26 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
\v 27 Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
\v 28 Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi."
\s5
\v 29 Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.
\v 30 Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, "Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie."
\v 31 Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, "Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie."
\s5
\v 32 Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
\v 33 Wakamwambia, "Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe."
\v 34 Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethfage, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,
\v 2 akiwaambia, "Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. wafungueni na kuwaleta kwangu.
\v 3 Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, `Bwana anawahitaji, ` na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao"
\s5
\v 4 Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,
\v 5 Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme, mwana punda mchanga.
\s5
\v 6 Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.
\v 7 Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.
\v 8 Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.
\s5
\v 9 Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema,"Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!"
\v 10 Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, "Huyu ni nani?
\v 11 "Umati ulijibu, "Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya."
\s5
\v 12 Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.
\v 13 Akawaambia, "Imeandikwa, `'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi, `lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang`anyi."
\v 14 kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.
\s5
\v 15 Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, "Hosana kwa Mwana wa Daudi," walishikwa na hasira.
\v 16 Wakamwambia, "Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?" Yesu akawaambia, "Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, 'Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?''
\v 17 Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.
\s5
\v 18 Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.
\v 19 Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, "Kusiwe na matunda kwako daima tena." Na mara hiyo mtini ule ukanyauka.
\s5
\v 20 Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, "Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?"
\v 21 Yesu akajibu na kuwaambia, "Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ` uchukuliwe na ukatupwe baharini, `na itafanyika.
\v 22 Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea."
\s5
\v 23 Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, "Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?"
\v 24 Yesu akajibu na kuwaambia, "Nami tena nitawauliza swali moja. kama mkiniambia, nami vilevile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
\s5
\v 25 Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?" Wakahojiana wenyewe, wakisema, tukisema, ulitoka mbinguni, `atatuambia, kwa nini hamkumwamini? `
\v 26 Lakini tukisema, `ulitoka kwa wanadamu, `tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii."
\v 27 Kisha wakamjibu Yesu na kusema, "Hatujui" Akawaambia pia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.
\s5
\v 28 Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, `Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu
\v 29 leo. `Mwana akajibu na kusema, `sitakwenda, ' Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda.
\v 30 Na Mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kilekile. Mwana huyu akajibu na kusema, `nitakwenda, bwana', lakini hakwenda.
\s5
\v 31 Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, "Mwana wa kwanza." Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia.
\v 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.
\s5
\v 33 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.
\v 34 Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.
\s5
\v 35 Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.
\v 36 Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile.
\v 37 Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, `'Watamheshimu mwanangu.'`
\s5
\v 38 Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, `'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.'
\v 39 `Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.
\s5
\v 40 Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?"
\v 41 Wakamwambia, "Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva."
\s5
\v 42 Yesu akawaambia, "Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?'
\s5
\v 43 Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.
\v 44 Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga."
\s5
\v 45 Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.
\v 46 Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,
\v 2 "Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.
\v 3 Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.
\s5
\v 4 Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. "Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi."
\s5
\v 5 Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.
\v 6 Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua.
\v 7 Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
\s5
\v 8 Kisha aliwaambia watumishi wake, "Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.
\v 9 Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi."
\v 10 Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.
\s5
\v 11 Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!
\v 12 Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote.
\s5
\v 13 Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, "Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\v 14 Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache."
\s5
\v 15 Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.
\v 16 Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, "Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.
\v 17 Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?"
\s5
\v 18 Yesu alifahamu uovu wao na akasema, "Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?
\v 19 Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi." Ndipo wakamletea dinari.
\s5
\v 20 Yesu akawauliza, "Sura na jina hili ni vya nani?"
\v 21 Wakamjibu, "Vya Kaisari." Ndipo Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu."
\v 22 Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.
\s5
\v 23 Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,
\v 24 wakisema, "Mwalimu, Musa alisema, Ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.
\s5
\v 25 Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.
\v 26 Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.
\v 27 Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.
\v 28 Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa."
\s5
\v 29 Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, "Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.
\v 30 Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.
\s5
\v 31 Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,
\v 32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
\v 33 Wakati kusanyiko waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.
\s5
\v 34 Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.
\v 35 Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.
\v 36 "Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?"
\s5
\v 37 Yesu akamjibu, "Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
\v 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.
\s5
\v 39 Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
\v 40 Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili."
\s5
\v 41 Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.
\v 42 Akisema, "J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?" Nao wakamjibu, "Ni mwana wa Daudi."
\s5
\v 43 Yesu akawajibu, "Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,
\v 44 'Bwana alimwambia Bwana wangu, "Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako."'?"
\s5
\v 45 Kama Daudi anamwita Kristo "Bwana," jinsi gani atakuwa mtoto wake?"
\v 46 Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema,
\v 2 "Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.
\v 3 Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.
\s5
\v 4 Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.
\v 5 Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.
\s5
\v 6 Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,
\v 7 na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa "Walimu" na watu.
\s5
\v 8 Lakini ninyi hampaswi kuitwa "Walimu," Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.
\v 9 Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.
\v 10 Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.
\s5
\v 11 Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.
\v 12 Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
\s5
\v 13 Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.
\v 14 (Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 "Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane").
\v 15 Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ngambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo.
\s5
\v 16 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao,, Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.
\v 17 Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?
\s5
\v 18 Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.
\v 19 Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?
\s5
\v 20 Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
\v 21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.
\v 22 Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.
\s5
\v 23 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.
\v 24 Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!
\s5
\v 25 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.
\v 26 Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.
\s5
\v 27 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila kitu kilicho kichafu.
\v 28 Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.
\s5
\v 29 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.
\v 30 Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.
\v 31 Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.
\s5
\v 32 Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.
\v 33 Enyi nyoka, wana wa vipiribao, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu?
\s5
\v 34 Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.
\v 35 Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.
\v 36 Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.
\s5
\v 37 Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, lakini haukukubali!
\v 38 Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.
\v 39 Nami nakuambia, Kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, 'Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana."'
\s5
\c 24
\p
\v 1 Yesu alitoka hekaluni na kwenda zake. Wanafunzi wake walimwendea na kumuonesha majengo ya hekalu.
\v 2 Laikni aliwajibu na kuwaambia, "Je, hamuyaoni mambo haya yote? Kweli nawaambia, hakuna jiwe litalobaki juu ya lingine bila kubomolewa."
\s5
\v 3 Na alipokaa katika Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, "Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?"
\v 4 Yesu aliwajibu na kuwaambia, "Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha.
\v 5 Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, 'Mimi ndiye Kristo', na watawapotosha wengi.
\s5
\v 6 Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado.
\v 7 Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali.
\v 8 Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 9 Ndipo watawatoa kwa ajili ya mateso na kuwaua. Mtachukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.
\v 10 Ndipo wengi watajikwaa na kusalitiana na watachukiana wenyewe kwa wenyewe.
\v 11 Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.
\s5
\v 12 Kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapoa.
\v 13 Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
\v 14 Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote. Na ndipo ule mwisho utafika.
\s5
\v 15 Kwa hiyo, mtakapoona chukizo la uharibifu, lililosemwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu [asomaye na afahamu],
\v 16 ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani.
\v 17 Na yule aliyeko juu ya paa la nyumba asiweze kuteremka chini kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya nyumba yake,
\v 18 naye aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.
\s5
\v 19 Lakini ole wao ambao wana mtoto na wale ambao wananyonyesha katika siku hizo!
\v 20 Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
\v 21 Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi sasa, na wala haitakuwapo tena.
\v 22 Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka. Lakini kwa sababu ya wateule, siku hizo zitafupishwa.
\s5
\v 23 Kisha ikiwa mtu yeyote atawaambia 'Tazama, Kristo yuko hapa! au, 'Kristo yuko kule' msiamini maneno hayo.
\v 24 Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo watakuja na kuonesha ishara kubwa na maajabu, kwa kusudi la kupotosha, kama ingewezekana hata na wateule.
\v 25 Tazameni, nimewatahadharisha kabla ya mambo hayo kutokea.
\s5
\v 26 Kwa hiyo, ikiwa watawaambia, ''Kristo yuko jangwani,' msiende huko jangwani. Au, 'Tazameni, yuko ndani ya nyumba,' msiamini maneno hayo.
\v 27 Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\v 28 Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.
\s5
\v 29 Lakini mara baada ya dhiki kuu ya siku zile, Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbinguni zitatikisika.
\s5
\v 30 Ndipo ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na makabila yote ya dunia wataomboleza. Watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu ya angani kwa nguvu na utukufu mkuu.
\v 31 Atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine.
\s5
\v 32 Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.
\v 33 Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango.
\s5
\v 34 Kweli nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.
\v 35 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\s5
\v 36 Lakini kuhusu siku ile na saa hakuna mtu ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, bali Baba peke yake.
\s5
\v 37 Kama vile ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\v 38 Kwa kuwa katika siku hizo kabla ya gharika watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa hadi siku ile ambayo Nuhu aliingia katika safina,
\v 39 na hawakujua kitu chochote hadi gharika ilipokuja na kuwasomba wote - ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.
\s5
\v 40 Ndipo watu wawili watakuwa shambani- mmoja atachukuliwa, na mmoja ataachwa nyuma.
\v 41 Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja - mmoja atachukuliwa, na mmoja atabaki.
\v 42 Kwa hiyo, kuweni macho kwa sababu hamjui ni siku gani ambayo atakuja Bwana wenu.
\s5
\v 43 Lakini mjue kwamba, ikiwa bwana mwenye nyumba angejua ni saa ipi ambayo mwizi angekuja, angekesha na asingeruhusu nyumba yake kuvamiwa.
\v 44 Kwa hiyo, pia mnapaswa kuwa tayari, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika saa msiyoitarajia.
\s5
\v 45 Hivyo ni nani aliye mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake amempa madaraka juu ya walio katika nyumba yake, ili awape chakula kwa wakati unaofaa?
\v 46 Amebarikiwa mtumishi huyo, ambaye bwana wake atamkuta akifanya hivyo wakati ajapo.
\v 47 Kweli nawaambia kwamba bwana atamweka juu ya kila kitu kilicho chake.
\s5
\v 48 Lakini kama mtumwa mwovu akisema moyoni mwake, 'Bwana wangu amekawia,'
\v 49 na akaanza kuwapiga watumishi wake, na akala na kulewa vileo,
\v 50 Bwana wa mtumwa huyo atakuja katika siku ambayo haitarajii, na katika saa ambayo haijui.
\v 51 Bwana wake atamkata vipande viwili na kumweka katika nafasi moja sawa na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi.
\v 2 Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu.
\v 3 Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote.
\v 4 Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.
\s5
\v 5 Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala.
\v 6 Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.'
\s5
\v 7 Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao.
\v 8 Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.'
\v 9 Lakini wale welevu waliwajibu na kuwaambia, 'Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.'
\s5
\v 10 Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa.
\v 11 Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.'
\v 12 Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.'
\v 13 Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.
\s5
\v 14 Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake.
\v 15 Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake.
\v 16 Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.
\s5
\v 17 Vilevile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili.
\v 18 Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.
\s5
\v 19 Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao.
\v 20 Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, 'Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.'
\v 21 Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
\s5
\v 22 Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, 'Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,'
\v 23 Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
\s5
\v 24 Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, 'Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia.
\v 25 Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.'
\s5
\v 26 Lakini bwana wake alijibu na kusema, 'Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.
\v 27 Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.
\s5
\v 28 Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi.
\v 29 Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa.
\v 30 Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.'
\s5
\v 31 Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu.
\v 32 Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi.
\v 33 Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto.
\s5
\v 34 Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, 'Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.
\v 35 Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;
\v 36 Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.'
\s5
\v 37 Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji?
\v 38 Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo?
\v 39 Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia?
\v 40 Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.'
\s5
\v 41 Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, 'Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake,
\v 42 kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji;
\v 43 Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.'
\s5
\v 44 Ndipo wao pia watamjibu na kusema, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia?
\v 45 Kisha atawajibu na kusema, 'Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.'
\v 46 Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele."
\s5
\c 26
\p
\v 1 Wakati Yesu alipomaliza kusema maneno yote hayo, aliwaambia wanafunzi wake,
\v 2 "Mnajua kwamba baada ya siku mbili kutakuwa na sikukuu ya pasaka, na mwana wa Adamu atatolewa ili asulibiwe."
\s5
\v 3 Baadaye wakuu wa makuhani na wazee wa watu walikutana pamoja katika makao ya Kuhani Mkuu, aliye kuwa anaitwa Kayafa.
\v 4 Kwa pamoja walipanga njama ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.
\v 5 Kwa kuwa walisema, "Isifanyike wakati wa sikukuu, kusudi isije ikazuka ghasia miongoni mwa watu."
\s5
\v 6 Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,
\v 7 alipokuwa amejinyoosha mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa amebeba mkebe wa alabasta iliyokuwa na mafuta yenye thamani kubwa, na aliyamimina juu ya kichwa chake.
\v 8 Lakini wanafunzi wake walipoona jambo hilo, walichukia na kusema, "Nini sababu ya hasara hii?
\v 9 Haya yangeweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa na kupewa maskini."
\s5
\v 10 Lakini Yesu, akiwa anajua hili, aliwaambia, "Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Kwa kuwa amefanya kitu kizuri kwangu.
\v 11 Masikini mnao siku zote, lakini hamtakuwa pamoja nami daima.
\s5
\v 12 Kwa sababu alipomimina mafuta haya juu ya mwili wangu, alifanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.
\v 13 Kweli nawaambieni, popote Injili hii itakapohubiriwa katika ulimwengu mzima, kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka."
\s5
\v 14 Ndipo mmoja wa wale Kumi na wawili, aliyeitwa Yuda Iskariote, alienda kwa wakuu wa makuhani
\v 15 na kusema, "Mtanipatia nini nikimsaliti?" Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.
\v 16 Tangu muda huo alitafuta nafasi ya kumsaliti.
\s5
\v 17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, "Wapi unataka tukuandalie ule chakula cha Pasaka?"
\v 18 Akawaambia, "Nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni, Mwalimu anasema, "Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.""
\v 19 Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza, na waliandaa chakula cha Pasaka.
\s5
\v 20 Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi Kumi na Wawili.
\v 21 Walipokuwa wanakula chakula, alisema, "Kweli nawaambia kwamba mmoja wenu atanisaliti."
\v 22 Walihuzunika sana, na kila mmoja alianza kumuuliza, "Je, hakika siyo mimi, Bwana?"
\s5
\v 23 Akawajibu, "Yule ambaye anachovya mkono wake pamoja nami katika bakuli ndiye atakaye nisaliti.
\v 24 Mwana wa Adamu ataondoka, kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu ambaye atamsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama asingezaliwa."
\v 25 Yuda, ambaye angemsaliti alisema, "Je!, Ni mimi Rabi?" Yesu akamwambia, "Umesema jambo hilo wewe mwenyewe."
\s5
\v 26 Walipokuwa wakila chakula, Yesu aliutwaa mkate, akaubariki, na kuumega. Akawapa wanafunzi wake akisema, "Chukueni, mle. Huu ni mwili wangu."
\s5
\v 27 Akatwaa kikombe na kushukuru, akawapa na kusema, "Kunyweni wote katika hiki.
\v 28 Kwa kuwa hii ni damu ya agano langu, inayomwagwa kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.
\v 29 Lakini nawaambieni, sitakunywa tena matunda ya mzabibu huu, hadi siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu."
\s5
\v 30 Walipokuwa wamemaliza kuimba wimbo, walitoka kwenda Mlima wa Mizeituni.
\v 31 Kisha Yesu aliwaambia, "Usiku huu ninyi nyote mtajikwaa kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika.
\v 32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya."
\s5
\v 33 Lakini Petro alimwambia, "Hata kama wote watakukataa kwa sababu ya mambo yatakayokupata, mimi sitakukataa."
\v 34 Yesu akamjibu, "kweli nakuambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
\v 35 Petro akamwambia, "hata kama ingenipasa kufa na wewe, sitakukana." Na wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
\s5
\v 36 Baadaye Yesu alienda nao mahali panapoitwa Gethsemane na aliwaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa wakati nikienda huko na kuomba."
\v 37 Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo na akaanza kuhuzunika na kusononeka.
\v 38 Kisha aliwaambia, "Roho yangu ina huzuni kubwa sana, hata kiasi cha kufa. Bakini hapa na mkeshe pamoja nami."
\s5
\v 39 Akenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, na kuomba. Akasema, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniepuke. Isiwe kama ninavyotaka mimi, bali kama utakavyo wewe."
\v 40 Akawaendea wanafunzi na akawakuta wamelala usingizi, na akamwambia Petro, "Kwa nini hamkuweza kukesha nami kwa saa moja?
\v 41 Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
\s5
\v 42 Akaenda zake mara ya pili na kuomba, akasema, "Baba yangu, kama jambo hili haliwezi kuepukika na ni lazima nikinywee kikombe hiki, mapenzi yako yatimizwe."
\v 43 Akarudi tena na kuwakuta wamelala usingizi, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito.
\v 44 Kisha akawaacha tena akaenda zake. Akaomba mara ya tatu akisema maneno yaleyale.
\s5
\v 45 Baadaye Yesu aliwaendea wanafunzi wake na kuwaambia, "Bado mmelala tu na kujipumzisha? Tazameni, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
\v 46 Amkeni, tuondoke. Tazama, yule anaye nisaliti amekaribia."
\s5
\v 47 Wakati alipokuwa bado anaongea, Yuda mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Kundi kubwa lilifika pamoja naye likitokea kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu. Walikuja na mapanga na marungu.
\v 48 Tena mtu aliyekusudia kumsaliti Yesu alikuwa amewapa ishara, akisema, "Yule nitakayembusu, ndiye yeye. Mkamateni."
\s5
\v 49 Mara hiyo alikuja kwa Yesu na kusema, "Salamu, Mwalimu!" Na akambusu.
\v 50 Yesu akamwambia, "Rafiki, lifanye lile ambalo limekuleta." Ndipo wakaja, na kumnyooshea mikono Yesu, na kumkamata.
\s5
\v 51 Tazama, mtu mmoja aliyekuwa pamoja na Yesu, alinyosha mkono wake, akachomoa upanga wake, na akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, na kumkata sikio lake.
\v 52 Ndipo Yesu akamwambia, rudisha upanga wako pale ulipoutoa, kwa kuwa wote watumiao upanga wataangamizwa kwa upanga.
\v 53 Mnadhani kuwa siwezi kumwita Baba yangu, naye akanitumia majeshi zaidi ya kumi na mawili ya malaika?
\v 54 Lakini basi jinsi gani maandiko yangeweza kutimizwa, hivi ndivyo inapasa kutokea?"
\s5
\v 55 Wakati huo Yesu akauambia umati, "Je! Mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi? Kila siku nilikaa hekaluni nikifundisha, na hamkunishika!
\v 56 Lakini yote haya yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie." Ndipo wanafunzi wake wakamwacha na kukimbia.
\s5
\v 57 Wale waliomkamata Yesu alimpeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, mahali ambapo waandishi na wazee walikuwa wamekusanyika pamoja.
\v 58 Lakini Petro alimfuata nyuma kwa mbali hadi katika ukumbi wa Kuhani Mkuu. Aliingia ndani na kukaa pamoja na walinzi aone kitakachotokea.
\s5
\v 59 Basi wakuu wa makuhani na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu, kusudi wapate kumuua.
\v 60 Ingawa walijitokeza mashahidi wengi, Lakini hawakupata sababu yoyote. Lakini baadaye mashahidi wawili walijitokeza mbele
\v 61 na kusema, " Mtu huyu alisema, ''Naweza kulivunja hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu."'
\s5
\v 62 Kuhani Mkuu alisimama na kumwuliza, "Hauwezi kujibu? Hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?"
\v 63 Lakini Yesu alikaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, "Kama Mungu aishivyo, nakuamuru utwambie, kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu."
\v 64 Yesu akamjibu, "Wewe mwenyewe umesema jambo hilo. Lakini nakuambia, toka sasa na kuendelea utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wenye Nguvu, na akija katika mawingu ya mbinguni."
\s5
\v 65 Ndipo Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake na kusema, "Amekufuru! Je, twahitaji tena ushahidi wa nini? Angalia, tayari mmesikia akikufuru.
\v 66 Je! Mnawaza nini? Wakajibu na kusema, "Anastahili kifo."
\s5
\v 67 Kisha walimtemea mate usoni na kumpiga ngumi, na kumchapa makofi kwa mikono yao,
\v 68 na kusema, "Tutabirie, wewe Kristo. Ni nani amekuchapa?"
\s5
\v 69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa nje katika ukumbi, na mtumishi wa kike alimwendea na kusema, "Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."
\v 70 Lakini alikana mbele yao wote, akisema, Sijui kitu unachosema."
\s5
\v 71 Alipoenda nje ya lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona na kuwaambia waliokuwepo hapo, "Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti."
\v 72 Akakana tena kwa kiapo, "Mimi simjui mtu huyu."
\s5
\v 73 Muda mfupi baadaye, wale waliokuwa wamesimama karibu, walimwendea na kusema na Petro, "Kwa hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa kuwa hata lafudhi yako inaonesha."
\v 74 Ndipo alianza kulaani na kuapa, "Mimi simfahamu mtu huyu," na mara hiyo jogoo akawika.
\v 75 Petro alikumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, "Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu."
\s5
\c 27
\p
\v 1 Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.
\v 2 Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.
\s5
\v 3 Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,
\v 4 na akasema, "Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia." Lakini wakajibu, "Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe."
\v 5 Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.
\s5
\v 6 Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, "Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu."
\v 7 Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
\v 8 Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, "Shamba la damu" hadi leo hii.
\s5
\v 9 Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, "Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,
\v 10 na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza."
\s5
\v 11 Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, "Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu alimjibu, "Wewe wasema hivyo."
\v 12 Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.
\v 13 Kisha Pilato alimwambia, "Hujayasikia mashitaka yote dhidi yako?"
\v 14 Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao.
\s5
\v 15 Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.
\v 16 Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.
\s5
\v 17 Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, "Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?" Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?"
\v 18 Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
\v 19 Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, "Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake."
\s5
\v 20 Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.
\v 21 Liwali aliwauliza, "Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?" Walisema, "Baraba."
\v 22 Pilato akawaambia, "Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?" Wote wakajibu, "Msulibishe"
\s5
\v 23 Naye akasema, "Kwa nini, ni kosa gani ametenda?" Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, "Msulibishe."
\v 24 Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, "Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe."
\s5
\v 25 Watu wote wakasema, "Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu."
\v 26 Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.
\s5
\v 27 Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika.
\v 28 Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.
\v 29 Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, "Salamu, Mfalme wa Wayahudi?"
\s5
\v 30 Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.
\v 31 Wakati walipokuwa wakimkejeri, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.
\s5
\v 32 Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.
\v 33 Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, "Eneo la fuvu la Kichwa."
\v 34 Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.
\s5
\v 35 Wakati walipokuwa wamemsulibisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.
\v 36 Na waliketi na kumwangalia.
\v 37 Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, "Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi."
\s5
\v 38 Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.
\v 39 Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao
\v 40 na kusema, "Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!"
\s5
\v 41 Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,
\v 42 "Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.
\s5
\v 43 Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'"
\v 44 Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.
\s5
\v 45 Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
\v 46 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, "Eloi, Eloi, lama thabakithan?" akimaanisha, "Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?"
\v 47 Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, "Anamwita Eliya."
\s5
\v 48 Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.
\v 49 Nao waliosalia wakasema, "Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa."
\v 50 Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.
\s5
\v 51 Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
\v 52 Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.
\v 53 Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.
\s5
\v 54 Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, "Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu."
\v 55 Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.
\v 56 Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo
\s5
\v 57 Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
\v 58 Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.
\s5
\v 59 Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na nguo ya sufi safi,
\v 60 na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
\v 61 Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.
\s5
\v 62 Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.
\v 63 Wakamwambia, "Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, 'Baada ya siku tatu atafufuka tena.'
\v 64 Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.' Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza."
\s5
\v 65 Pilato akawaambia, "Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo."
\v 66 Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi.
\v 2 Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.
\s5
\v 3 Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
\v 4 Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.
\s5
\v 5 Yule malaika akawafafanulia wale wananawake akisema, "msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulibiwa.
\v 6 Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala.
\v 7 Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, 'Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.' Tazama mimi nimewaambia."
\s5
\v 8 Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.
\v 9 Tazama Yesu akakutana nao na kusema, "Salamu."wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu.
\v 10 Kisha Yesu akawaambia, "msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.
\s5
\v 11 Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea.
\v 12 Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari
\v 13 na kuwaambia, "Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.'
\s5
\v 14 Kama taarifa hii itamfikia liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote."
\v 15 Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.
\s5
\v 16 Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza.
\v 17 Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka.
\s5
\v 18 Yesu akaja kwao akawambia akisema, "Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni.
\v 19 Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.
\s5
\v 20 Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.

1255
42-MRK.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1255 @@
\id MRK
\ide UTF-8
\h Marko
\toc1 Marko
\toc2 Marko
\toc3 mrk
\mt Marko
\s5
\c 1
\p
\v 1 Huu ni mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
\v 2 Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, "Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako.
\v 3 Sauti ya mtu aitaye nyikani, "Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake".
\s5
\v 4 Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi.
\v 5 Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao.
\v 6 Yohana alikuwa anavaa vazi la manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini.
\s5
\v 7 Alihubiri na kusema, "Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake.
\v 8 Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu."
\s5
\v 9 Ilitokea katika siku hizo kwamba Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, na alibatizwa na Yohana katika mto Yordani.
\v 10 Wakati Yesu alipoinuka kutoka majini, aliona mbingu zimegawanyika wazi na Roho akishuka chini juu yake kama njiwa.
\v 11 Na sauti ilitoka mbinguni, "Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe."
\s5
\v 12 Kisha mara moja Roho akamlazimisha kwenda nyikani.
\v 13 Alikuwako nyikani siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walimhudumia.
\s5
\v 14 Sasa baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alikuja Galilaya akitangaza injili ya Mungu,
\v 15 akisema, "Muda umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini katika injili".
\s5
\v 16 Na akipita kando ya bahari ya Galilaya, alimwona Simoni na Andrea ndugu wa Simoni wakitupa nyavu zao katika bahari, kwa kuwa walikuwa wavuvi.
\v 17 Yesu aliwaambia, "Njoni, nifuateni, na nitawafanya wavuvi wa watu."
\v 18 Na mara moja waliacha nyavu na wakamfuata.
\s5
\v 19 Wakati Yesu alipotembea umbali kidogo, alimwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; walikuwa kwenye mtumbwi wakitengeneza nyavu.
\v 20 Mara aliwaita na wao walimwacha baba yao Zebedayo ndani ya mtumbwi na watumishi waliokodiwa, wakamfuata.
\s5
\v 21 Na walipofika Kaperinaumu, siku ya Sabato, Yesu aliingia kwenye sinagogi na kufundisha.
\v 22 Walilishangaa fundisho lake, kwa vile alikuwa akiwafundisha kama mtu ambaye ana mamlaka na siyo kama waandishi.
\s5
\v 23 Wakati huo huo kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mchafu, na alipiga kelele,
\v 24 akisema, "Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani. Wewe ni Mtakatifu pekee wa Mungu!"
\v 25 Yesu alimkemea pepo na kusema, "Nyamaza na utoke ndani yake!"
\v 26 Na roho mchafu alimwangusha chini na akatoka kwake wakati akilia kwa sauti ya juu.
\s5
\v 27 Na watu wote walishangaa, hivyo wakaulizana kila mmoja, "Hii ni nini? Fundisho jipya lenye mamlaka? Hata huamuru pepo wachafu nao wanamtii!"
\v 28 Na habari kuhusu yeye mara moja zikasambaa kila mahali ndani ya mkoa wote wa Galilaya.
\s5
\v 29 Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.
\v 30 Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake.
\v 31 Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia.
\s5
\v 32 Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, au waliopagawa na pepo.
\v 33 Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango.
\v 34 Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa pepo wengi, bali hakuruhusu pepo kuongea kwa sababu walimjua.
\s5
\v 35 Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.
\v 36 Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta.
\v 37 Walimpata na wakamwambia, "Kila mmoja anakutafuta"
\s5
\v 38 Aliwaambia, "Twendeni mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa."
\v 39 Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea pepo.
\s5
\v 40 Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimsihi; alipiga magoti na alimwambia, "Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi."
\v 41 Akisukumwa na huruma, Yesu alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, "Ninataka. Uwe msafi."
\v 42 Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa safi.
\s5
\v 43 Yesu akamwonya vikali na akamwambia aende mara moja,
\v 44 Alimwambia, "Hakikisha hausemi neno kwa yeyote, lakini nenda, ujionyeshe kwa kuhani, na utoe dhabihu kwa ajili ya utakaso ambayo Musa aliagiza, kama ushuhuda kwao."
\s5
\v 45 Lakini alikwenda na kuanza kumwambia kila mmoja na kueneza neno zaidi hata Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru. Hivyo alikaa mahali pa faragha na watu walikuja kwake kutoka kila mahali.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Aliporudi Kaperinaumu baada ya siku chache, ilisikika kwamba alikuwa nyumbani.
\v 2 Watu wengi sana walikuwa wamekusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya pale mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.
\s5
\v 3 Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.
\v 4 Wakati waliposhindwa kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu ya mahali pale alipokuwa. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
\s5
\v 5 Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, "mwanangu, dhambi zako zimesamehewa."
\v 6 Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,
\v 7 "Anawezaje mtu huyu kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
\s5
\v 8 Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, "Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
\v 9 Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama, chukua kitanda chako, na utembee?'
\s5
\v 10 Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,
\v 11 "Nakuambia wewe, inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako."
\v 12 Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alikwenda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote walishangaa na walimpa Mungu utukufu, na wakasema "Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili."
\s5
\v 13 Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.
\v 14 Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, "Nifuate." Alisimama na kumfuata.
\s5
\v 15 Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.
\v 16 Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, "Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?"
\s5
\v 17 Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, "Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi."
\s5
\v 18 Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, "Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
\v 19 Yesu aliwaambia, "Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga."
\s5
\v 20 Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.
\v 21 Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitabanduka kutoka katika hilo, kipya kubanduka kutoka katika kikuukuu, na kutakuwepo mpasuko mbaya.
\s5
\v 22 Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya."
\s5
\v 23 Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.
\v 24 Na Mafarisayo walimwambia, "Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?"
\s5
\v 25 Aliwaambia, "Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?
\v 26 Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani—na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?"
\s5
\v 27 Yesu alisema, "Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.
\v 28 Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, hata kwa Sabato."
\s5
\c 3
\p
\v 1 Na tena aliingia ndani ya sinagogi na mle palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza.
\v 2 Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili kwamba wamshitaki.
\s5
\v 3 Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, " Inuka na usimame katikati ya umati huu."
\v 4 Kisha akawaambia watu, "Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?" Lakini walibaki kimya.
\s5
\v 5 Akawaangalia kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, "Nyoosha mkono wako". Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.
\v 6 Mafarisayo wakaenda nje na mara wakafanya njama pamoja na Maherode dhidi yake ili kumuua.
\s5
\v 7 Kisha Yesu, pamoja na wanafunzi wake, walienda baharini, na umati mkubwa wa watu uliwafuata ukitokea Galilaya na Uyahudi
\v 8 na kutoka Yerusalemu na kutoka Idumaya na mbele ya Yorodani na jirani ya Tiro na Sidoni, umati mkubwa, uliposikia kila kitu alichokuwa anakifanya, walikuja kwake.
\s5
\v 9 Na aliwaambia wanafunzi wake kuandaa mtubwi mdongo kwa ajili yake kwa sababu ya umati, ili kwamba wasije wakamsonga.
\v 10 Kwa kuwa aliponya wengi, ili kila mtu aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumfikia ili amguse.
\s5
\v 11 Popote roho wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia, na walisema, "Wewe ni Mwana wa Mungu".
\v 12 Aliwaamuru kwa msisitizo wasifanye ajulikane.
\s5
\v 13 Alienda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakaenda kwake.
\v 14 Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri,
\v 15 na kuwa na mamlaka ya kutoa mapepo.
\v 16 Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro,
\s5
\v 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,
\v 18 na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
\v 19 na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.
\s5
\v 20 Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakaja pamoja tena, hata wasiweze kula hata mkate.
\v 21 Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, " Amerukwa na akili".
\v 22 Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, " Amepagawa na Beelzebuli," na, " Kwa mtawala wa mapepo anatoa mapepo".
\s5
\v 23 Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, " Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani?
\v 24 Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
\v 25 Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
\s5
\v 26 Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake.
\v 27 Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga mwenye nguvu kwanza, na kisha kukusanya kilichomo nyumbani.
\s5
\v 28 Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,
\v 29 lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele".
\v 30 Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, "Ana roho chafu".
\s5
\v 31 Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita.
\v 32 Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, "mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe".
\s5
\v 33 Aliwajibu, "Ni nani mama yangu na ndugu zangu?"
\v 34 Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, "Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!
\v 35 Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu".
\s5
\c 4
\p
\v 1 Tena alianza kufundisha kandokando ya bahari. Na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka, akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kukaa. Umati wote walikuwa pembeni mwa bahari ufukweni.
\v 2 Na akawafundisha mambo mengi kwa mifano, na akasema kwao kwa mafundisho yake.
\s5
\v 3 Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda.
\v 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila.
\v 5 Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Mara zikanyauka, kwa sababu hazikuwa na udongo wakutosha.
\s5
\v 6 Lakini jua lilipochomoza, zilinyauka, na kwa sababu hazikuwa na mzizi, zilikauka.
\v 7 Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yeyote.
\s5
\v 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka, zingine zilizaa mara thelathini zaidi, na zingine sitini, na zingine mia".
\v 9 Na akasema, "Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!"
\s5
\v 10 Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mifano.
\v 11 Akasema kwao, "Kwenu mmepewa siri za ufalme wa Mungu. Lakini kwa walio nje kila kitu ni mifano,
\v 12 ili wakitazama, ndiyo hutazama, lakini hawaoni, na kwa hiyo wanaposikia ndiyo husikia, lakini hawaelewi, amasivyo wangegeuka na Mungu angeliwasamehe."
\s5
\v 13 Na akasema kwao, "Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?.
\v 14 Mpanzi alipanda neno.
\v 15 Baadhi ni wale walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao.
\s5
\v 16 Na baadhi ni wale waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa haraka wanalipokea kwa furaha.
\v 17 Na hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda mfupi. Halafu tabu na masumbufu vinapokuja kwa sababu ya neno, mara hujikwaa.
\s5
\v 18 Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno,
\v 19 lakini masumbufu ya dunia, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda.
\v 20 Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia moja."
\s5
\v 21 Yesu akawaambia, " Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango.
\v 22 Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitawekwa wazi.
\v 23 Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!"
\s5
\v 24 Akawaambia, " Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu.
\v 25 Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kutoka kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo."
\s5
\v 26 Na akasema, "Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo.
\v 27 Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea.
\v 28 Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa.
\v 29 Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia."
\s5
\v 30 Na akasema, "tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?.
\v 31 Ni kama mbegu ya haradali, ambapo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani.
\v 32 Hata, wakati imepandwa, inakuana kuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa mbinguni huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake."
\s5
\v 33 Kwa mifano mingi alifundisha na alisema neno kwao, kwa kadiri walivyoweza kuelewa,
\v 34 na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, akawaelezea kila kitu wanafunzi wake.
\s5
\v 35 Katika siku hiyo, wakati wa jioni ulipowadia, akasema kwao, "Twendeni upande wa pili".
\v 36 Hivyo wakauacha umati, wakamchukua Yesu, wakati huo tayari alikuwa ndani ya mtumbwi. Mitumbwi mingine ilikuwa pamoja naye.
\v 37 Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa.
\s5
\v 38 Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, "Mwalimu, haujali sisi tunakufa?"
\v 39 Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, "'Iwe shwari, amani". Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa.
\s5
\v 40 Na akasema kwao, "Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?"
\v 41 Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakasemezana wao kwa wao, " Huyu ni nani tena, kwa sababu hata upepo na bahari vya mtii?".
\s5
\c 5
\p
\v 1 Walikuja mpaka upande mwingine wa bahari, katika mkoa wa Gerasi
\v 2 Na ghafla wakati Yesu alipokuwa akitoka nje ya mtumbwi, mtu mwenye roho chafu alikuja kwake kutoka makaburini.
\s5
\v 3 Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia zaidi, hakuna hata kwa minyororo.
\v 4 Alikuwa amefungwa nyakati nyingi kwa pingu na minyororo. Aliikata minyororo na pingu zake zilivunjwa. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
\s5
\v 5 Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata yeye mwenyewe kwa mawe makali.
\v 6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alikimbilia kwake na kuinama mbele yake.
\s5
\v 7 Alilia kwa sauti kuu, "Wataka nikufanyie nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Ninakusihi kwa Mungu mwenyewe, usinitese."
\v 8 Kwa kuwa alikuwa amemwambia, "Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu."
\s5
\v 9 Naye alimwuliza, "Jina lako ni nani?" Naye alimjibu, "Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi."
\v 10 Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.
\s5
\v 11 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likilishwa juu ya kilima,
\v 12 nao walimsihi, wakisema, "Tutume kwa nguruwe; tuingie ndani yao."
\v 13 Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.
\s5
\v 14 Na wale waliokuwa wakiwalisha nguruwe walikimbia na kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na katika nchi. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.
\v 15 Ndipo walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyepagawa na pepo—aliyekuwa na Jeshi—amekaa chini, amevikwa, na akiwa katika akili yake timamu, nao waliogopa.
\s5
\v 16 Wale waliokuwa wameona kilichotokea kwa mtu aliyekuwa amepagawa na pepo waliwaambia kilichotokea kwake na pia kuhusu nguruwe.
\v 17 Nao walianza kumsihi aondoke katika mkoa wao.
\s5
\v 18 Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.
\v 19 Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, "Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alikufanyia Bwana, na rehema aliyokupa."
\v 20 Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.
\s5
\v 21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari.
\v 22 Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.
\v 23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, " Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili kwamba aweze kupata afya na kuishi."
\v 24 Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati mkubwa ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka.
\s5
\v 25 Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa imetoka kwa miaka kumi na miwili.
\v 26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakusaidika kwa chochote, lakini badala yake alizidi kuwa na hali mbaya.
\v 27 Alisikia habari kuhusu Yesu. Hivyo alikuja nyuma yake wakati alipokuwa akitembea ndani ya umati, naye aliligusa vazi lake.
\s5
\v 28 Kwa kuwa alisema, "Kama nikiyagusa mavazi yake tu, nitakuwa mzima."
\v 29 Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba aliponywa kutoka kwenye mateso yake.
\s5
\v 30 Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Na aligeuka huku na huku katika umati wa watu na kuuliza, "Ni nani aliyeligusa vazi langu?"
\v 31 Wanafunzi wake walimwambia, "Unaona umati huu umekusonga ukikuzunguka, nawe wasema, 'Ni nani aliyenigusa?'"
\v 32 Lakini Yesu alitazama huku na huku kuona ambaye aliyekuwa amefanya hili.
\s5
\v 33 Mwanamke, akijua kilichotokea kwake, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote.
\v 34 Alisema kwake, "Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe kutoka kwenye ugonjwa wako."
\s5
\v 35 Alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakisema, "Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?"
\s5
\v 36 Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, "Usiogope. Amini tu."
\v 37 Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo.
\v 38 Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu, kulia kwingi na kuomboleza.
\s5
\v 39 Alipoingia nyumbani, aliwaambia, "Kwa nini mmesikitika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala."
\v 40 Walimcheka, lakini yeye, aliwatoa wote nje, alimchukua baba wa mtoto na mama na wale waliokuwa pamoja naye, na aliingia ndani alimokuwa mtoto.
\s5
\v 41 Aliuchukua mkono wa mtoto na alimwambia, "Talitha koum," ambayo ni kusema, "Binti mdogo, nakuambia, amka."
\v 42 Ghafla mtoto aliamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa.
\v 43 Aliwaamuru kwa nguvu kwamba hakuna yeyote anapaswa kujua kuhusu hili. Na aliwaambia wampatie yule binti chakula.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao, na wanafunzi wake wakamfuata.
\v 2 Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikia na wakashangazwa. Wakasema, "Amepata wapi mafundisho haya?" "Ni hekima gani hii aliyopewa?" "Anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?"
\v 3 "Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?" Na hawakufurahishwa na Yesu.
\s5
\v 4 Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na miongoni mwa ndugu zake na nyumbani mwake."
\v 5 Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya.
\v 6 Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.
\s5
\v 7 Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,
\v 8 na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni;
\v 9 lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili.
\s5
\v 10 Na akawaambia, "Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.
\v 11 Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao."
\s5
\v 12 Nao wakaenda wakitangaza watu watubu na kuacha dhambi zao.
\v 13 Waliwafukuza pepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.
\s5
\v 14 Mfalme Herode aliposikia hayo, kwa kuwa jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Baadhi walisema, "Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake."
\v 15 Baadhi yao wakasema, "Huyu ni Eliya," Bado wengine wakasema, "Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani."
\s5
\v 16 Lakini Herode aliposikia haya akasema, "Yohana, niliyemkata kichwa amefufuliwa."
\v 17 Maana Herode mwenyewe aliagiza Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake Filipo) kwa sababu yeye alikuwa amemuoa.
\s5
\v 18 Kwa maana Yohana alimwambia Herode, "Si halali kumuoa mke wa kaka yako."
\v 19 Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuua, lakini hakuweza,
\v 20 maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza alihuzunika sana, lakini alifurahi kumsikiliza.
\s5
\v 21 Hata ilipofika wakati mwafaka ikiwa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake karamu, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.
\v 22 Ndipo binti wa Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, "Niombe chochote unachotaka nami nitakupa."
\s5
\v 23 Akamwapia na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu."
\v 24 Akatoka nje akamuuliza mama yake, "Niombe nini?" Akasema, "Kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\v 25 Na mara moja akaingia kwa mfalme akaanza kusema, "Nataka unipatie ndani ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji."
\s5
\v 26 Mfalme alisikitishwa sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake.
\v 27 Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa akiwa kifungoni.
\v 28 Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake.
\v 29 Na wanafunzi wake waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini.
\s5
\v 30 Na mitume, walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.
\v 31 Naye akawaambia, "Njooni wenyewe mahali pa faragha na tupumzike kwa muda." Watu wengi walikuwa wanakuja na kuondoka, hata hawakupata nafasi ya kula.
\v 32 Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha peke yao.
\s5
\v 33 Lakini waliwaona wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa miguu kutoka miji yote, nao wakafika kabla yao.
\v 34 Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.
\s5
\v 35 Muda ulipoendelea sana, wanafunzi wakamjia wakamwambia,"Hapa ni mahali pa faragha na muda umeendelea.
\v 36 Uwaage waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula."
\s5
\v 37 Lakini akawajibu akisema, "Wapeni ninyi chakula." Wakamwambia, "Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?"
\v 38 Akawambia," Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie." walipopata wakamwambia, "Mikate mitano na samaki wawili."
\s5
\v 39 Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi.
\v 40 Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.
\v 41 Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akaibariki kisha akawapa wanafunzi waweke mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili kwa watu wote.
\s5
\v 42 Walikula wote hadi wakatosheka.
\v 43 Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki.
\v 44 Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate.
\s5
\v 45 Mara akawaambia wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.
\v 46 Walipokuwa wamekwisha kuondoka, akaenda mlimani kuomba.
\v 47 Kulipokuwa jioni, na mashua yao wakati huo ikiwa katikati ya bahari, naye alikuwa peke yake nchi kavu.
\s5
\v 48 Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
\v 49 Lakini walipomwona anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu hata wakapiga kelele.
\v 50 kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara akasema nao akawaambia, "Muwe wajasiri! ni mimi! Msiwe na hofu."
\s5
\v 51 Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa kabisa.
\v 52 Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa na uelewa mdogo.
\s5
\v 53 Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.
\v 54 Walipotoka nje ya mashua, mara wakamtambua.
\v 55 Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta wagonjwa kwa machela, kila waliposikia anakuja.
\s5
\v 56 Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na wakamsihi awaruhusu kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Mafarisayo na baadhi ya waandishi ambao walikuwa wametokea Yerusalemu walikusanyika kumzunguka yeye.
\s5
\v 2 Na waliona kuwa baadhi ya wanafunzi wake walikula mkate kwa mikono najisi; ambayo haikuoshwa.
\v 3 (kwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali mpaka wameosha mikono yao vizuri; wanashikilia utamaduni wa wazee. Wakati
\v 4 Mafarisayo wanaporudi kutoka mahali pa soko, hawali mpaka wameoga kwanza. Na kuna sheria zingine ambazo wanazifuata kabisa, ikiwa ni pamoja na kuosha vikombe, masufuria, vyombo vya shaba, na hata viti vinavyotumika wakati wa chakula.)
\s5
\v 5 Mafarisayo na waandishi walimuuliza Yesu, " Kwa nini wanafunzi wako hawaishi kulingana na tamaduni za wazee, kwani wanakula mkate pasipo kunawa mikono?"
\s5
\v 6 Lakini yeye aliwaambia, "Isaya alitabiri vizuri kuhusu ninyi wanafiki, aliandika, 'Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na mimi.
\v 7 Wananifanyia ibaada zisizo na maana, wakifundisha sheria za wanadamu kama mapokeo yao.'
\s5
\v 8 Mmeiacha sheria ya Mungu na kushikilia kwa wepesi tamaduni za wanadamu."
\v 9 Na akasema kwao, "Mmeikataa amri ya Mungu kwa urahisi ili kwamba mtunze tamaduni zenu!
\v 10 Kwa kuwa Musa alisema, 'mheshimu baba yako na mama yako,' na 'Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa.'
\s5
\v 11 Lakini mnasema, 'kama mtu akisema kwa baba yake au mama, "Msaada wowote ambao mngepokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu,"' (hiyo ni kusema kwamba, 'imetolewa kwa Mungu')
\v 12 hivyo haumruhusu kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake.
\v 13 Mnaifanya amri ya Mungu kuwa bure kwa kuleta tamaduni zenu. Na mambo mengi ya jinsi hiyo mnayoyafanya."
\s5
\v 14 Aliwaita makutano tena na kuwaambia, "Mnisikilize mimi, ninyi nyote, na mnielewe.
\v 15 Hakuna chochote kutoka nje ya mtu ambacho chaweza kumchafua mtu kiingiapo kwake. Bali ni kile kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho.
\v 16 (Zingatia: mstari huu, "kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia, na asikie" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 17 Yesu alipowaacha makutano na kuingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu mfano huo.
\v 18 Yesu akasema, "Na ninyi pia bado hamjaelewa? Hamuoni kwamba chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua,
\v 19 kwa sababu hakiwezi kwenda kwenye moyo wake, lakini kinaingia katika tumbo lake na kisha kinapita kwenda chooni." Kwa maelezo haya Yesu alivifanya vyakula vyote kuwa safi.
\s5
\v 20 Alisema, "Ni kile ambacho kinamtoka mtu ndicho kimchafuacho.
\v 21 Kwa kuwa hutoka ndani ya mtu, nje ya moyo, hutoka mawazo maovu, zinaa, wizi, mauaji,
\v 22 uasherati, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, kujamiiana, wivu, kashfa, majivuno, ujinga.
\v 23 Maovu haya yote yanatoka ndani, ndiyo yale yamchafuayo mtu."
\s5
\v 24 Aliamka kutoka pale na kuondoka kwenda katika mkoa wa Tiro na Sidoni. Aliingia ndani na hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa hapo, lakini haikuwezekana kumficha.
\v 25 Lakini ghafla mwanamke, ambaye mtoto wake mdogo alikuwa na roho mchafu, alisikia habari zake, akaja, na akaanguka miguuni pake.
\v 26 Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoeniki. Alimsihi yeye amfukuze pepo kutoka kwa binti yake.
\s5
\v 27 Yesu akamwambia mwanamke, "Waache watoto walishwe kwanza, kwa kuwa sio sawa kuuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa."
\v 28 Lakini mwanamke akamjibu na kusema, "Ndiyo Bwana, hata mbwa chini ya meza hula mabaki ya chakula cha watoto."
\s5
\v 29 Akamwambia, "Kwa kuwa umesema hivi, uko huru kwenda. Pepo ameshamtoka binti yako."
\v 30 Mwanamke alirudi nyumbani kwake na akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo alikuwa amemtoka.
\s5
\v 31 Yesu alitoka tena nje ya mkoa wa Tiro na kupitia Sidoni kuelekea Bahari ya Galilaya mpaka kanda ya Dikapolisi.
\v 32 Na wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, walimsihi Yesu aweke mikono juu yake.
\s5
\v 33 Alimtoa nje ya kusanyiko kwa siri, na akaweka vidole vyake kwenye masikio yake, na baada ya kutema mate, aligusa ulimi wake.
\v 34 Alitazama juu mbinguni, akahema na kumwambia, "Efata," hiyo ni kusema "funguka!"
\v 35 Na muda ule ule masikio yakafunguka, na kilichokuwa kimezuia ulimi kiliharibiwa na akaweza kuongea vizuri.
\s5
\v 36 Na aliwaamuru wasimwambie mtu yeyote. Lakini kadri alivyowaamuru, ndivyo walivyotangaza habari hizo kwa wingi.
\v 37 Hakika walishangazwa, na kusema, "Amefanya kila kitu vizuri. Hata amewafanya viziwi kusikia na mabubu kuongea."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,
\v 2 "Ninauhurumia umati huu, wameendelea kuwa nami kwa siku tatu na hawana chakula.
\v 3 Nikiwatawanya warudi majumbani kwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana."
\v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, "Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwashibisha watu hawa katika eneo hili lililoachwa?"
\s5
\v 5 Akawauliza, "mna vipande vingapi vya mikate?" Wakasema, "Saba".
\v 6 Aliuamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.
\s5
\v 7 Pia walikuwa na samaki wadogo wachache, na baada ya kushukuru, aliwaamuru wanafunzi wake wawagawie hivi pia.
\v 8 Walikula na wakatosheka. Na walikusanya vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba.
\v 9 Walikaribia watu elfu nne. Na aliwaacha waende.
\v 10 Mara aliingia kwenye mashua na wanafunzi wake, na wakaenda katika ukanda ya Dalmanuta.
\s5
\v 11 Kisha Mafarisayo walitoka nje na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, kwa kumjaribu.
\v 12 Akatafakari kwa kina moyoni mwake akasema, "Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki."
\v 13 Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.
\s5
\v 14 Wakati huo wanafunzi walisahau kuchukua mikate. Hawakuwa na mikate zaidi ya kipande kimoja kilichokuwa kwenye mashua.
\v 15 Aliwaonya na kusema, "Muwe macho na mjilinde dhidi ya chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.
\s5
\v 16 Wanafunzi wakasemezana wao kwa wao, "Ni kwa sababu hatuna mikate."
\v 17 Yesu alilitambua hili, na akawaambia, "Kwa nini mnasemezana kuhusu kutokuwa na mikate? Hamjajua bado? Hamuelewi? Mioyo yenu imekuwa miepesi?
\s5
\v 18 Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?
\v 19 Nilipoigawanya mikate mitano kwa watu elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?" Wakamjibu, "kumi na mbili."
\s5
\v 20 "Na nilipoigawanya mikate saba kwa watu elfu nne, mlichukua vikapu vingapi?"
\v 21 Wakasema, "Saba." Akawaambia, "Bado hamuelewi?"
\s5
\v 22 Wakaja Bethsaida. Watu hao walimleta kwa Yesu mtu kipofu na wakamsihi Yesu amguse.
\v 23 Yesu akamshika kwa mkono yule kipofu, na kumwongoza nje ya kijiji. Alipotema mate juu ya macho yake na kunyosha mikono yake juu yake, alimuuliza, "Unaona chochote?"
\s5
\v 24 Alitazama juu na kusema, "Naona watu wanaonekana kama miti inatembea."
\v 25 Ndipo akanyosha tena mikono yake juu ya macho yake, mtu yule akafungua macho yake, aliona tena, na akaona kila kitu vizuri.
\v 26 Yesu alimwacha aende nyumbani na akamwambia, "Usiingie mjini."
\s5
\v 27 Yesu aliondoka na wanafunzi wake kwenda vijiji vya Kaiseria ya Filipi. Wakiwa njiani aliwauliza wanafunzi, "Watu wanasema mimi ni nani?"
\v 28 Wakamjibu wakasema, "Yohana mbatizaji. Wengine wanasema, 'Eliya' na wengine, 'Mmoja wa Manabii."
\s5
\v 29 Akawauliza, "Lakini ninyi mnasema mimi ni nani?" Petro kamwambia, "Wewe ni Kristo."
\v 30 Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye.
\s5
\v 31 Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na viongozi na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.
\v 32 Alisema haya kwa uwazi. Ndipo Petro akamchukua pembeni na akaanza kumkemea.
\s5
\v 33 Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na akamkemea Petro na kusema, "Pita nyuma yangu Shetani! Hujali mambo ya Mungu, isipokuwa mambo ya watu."
\v 34 Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, "Kama kuna mtu anataka kunifuata, ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake, na anifuate.
\s5
\v 35 Kwa kuwa yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, atayaokoa.
\v 36 Inamfaidia nini mtu, kupata ulimwengu wote, na kisha kupata hasara ya maisha yake?
\v 37 Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake?
\s5
\v 38 Yeyote anioneaye aibu na maneno yangu katika kizazi hiki cha wazinzi na kizazi cha wenye dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea aibu atakapokuja katika ufalme wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Na alisema kwao, "Hakika nasema kwenu, baadhi yenu kuna watu waliosimama hapa hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu."
\v 2 Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye mlimani, pekee yao. Ndipo alianza kubadilika mbele yao.
\v 3 Mavazi yake yakaanza kung'aa sana, meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani.
\s5
\v 4 Ndipo Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu.
\v 5 Petro alijibu akamwambia Yesu, "Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya."
\v 6 (Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana.)
\s5
\v 7 Wingu lilitokea na kuwafunika. Ndipo sauti ikatoka mawinguni ikisema, " Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye."
\v 8 Ghafla, walipokuwa wakitazama, hawakumuona yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu.
\s5
\v 9 Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.
\v 10 Ndipo waliyatunza mambo wao wenyewe. Lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake "kufufuliwa kutoka kwa wafu"
\s5
\v 11 Walimwuliza Yesu,"Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?"
\v 12 Akawaambia, "hakika Eliya atakuja kwanza kuokoa vitu vyote. Kwa nini imeandikwa Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi na achukiwe?
\v 13 Lakini nasema kwenu Eliya alikwisha kuja, na walimfanya kama walivyopenda, kama vile maandiko yasemavyo kuhusu yeye."
\s5
\v 14 Na waliporudi kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na Masadukayo walikuwa wanabishana nao.
\v 15 Na mara walipomwona, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia.
\v 16 Aliwauliza wanafunzi wake, "Mnabishana nao juu ya nini?"
\s5
\v 17 Mmoja wao katika kundi alimjibu, "Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu ambayo humfanya asiweze kuongea,
\v 18 na humsababishia kutetemeka na kumwangusha chini, na kutoka povu mdomoni na kusaga meno na kukakamaa. Niliwaomba wanafunzi wako kumtoa pepo, lakini hawakuweza.
\v 19 Aliwajibu, "Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi kwa muda gani? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni kwangu."
\s5
\v 20 Walimleta mtoto wake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.
\v 21 Yesu alimwuliza baba yake, "Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?" Baba alisema, " Tangu utoto.
\v 22 Mara nyingine huanguka katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie."
\s5
\v 23 Yesu alimwambia, "Kama uko tayari? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye."
\v 24 Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, " Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu."
\v 25 Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, "wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru mwache, usiingie kwake tena."
\s5
\v 26 Alilia kwa nguvu na kumhangaisha mtoto na roho alimtoka. Mtoto alionekana kama amekufa, Ndipo wengi walisema, "Amekufa,"
\v 27 Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mtoto alisimama.
\s5
\v 28 Wakati Yesu alipoingia ndani, wanafunzi wake walimwuliza faragha, "Kwa nini hatukuweza kumtoa?"
\v 29 Aliwaambia, " kwa namna hii hatoki isipokuwa kwa maombi."
\s5
\v 30 Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,
\v 31 kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, "Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena."
\v 32 Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza.
\s5
\v 33 Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani"?
\v 34 Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
\v 35 Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, "Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote."
\s5
\v 36 Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema,
\v 37 "Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma."
\s5
\v 38 Yohana alimwambia, "Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati."
\v 39 Lakini Yesu alisema, "Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
\s5
\v 40 Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
\v 41 Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
\s5
\v 42 Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.
\v 43 Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto "usiozimika".
\v 44 (Zingatia: Mstari hii, "Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika." haumo katika nakala za kale).
\s5
\v 45 Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili.
\v 46 (Zingatia: Mstari huu, "Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 47 Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu.
\v 48 Mahali palipo na funza wasiokufa, na moto usiozimika.
\s5
\v 49 Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto.
\v 50 Chumvi ni nzuri, kama chumvi ikipoteza ladha yake, utaifanyaje iwe na ladha yake tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe, na muwe na amani kwa kila mmoja."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.
\v 2 Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, "Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?"
\v 3 Yesu akawajibu, "Musa aliwaamuru nini?"
\v 4 Wakasema, "Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke."
\s5
\v 5 "Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii," Yesu aliwaambia.
\v 6 "Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.'
\s5
\v 7 Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,
\v 8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
\v 9 Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."
\s5
\v 10 Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.
\v 11 Akawaambia, "Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.
\v 12 Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi."
\s5
\v 13 Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
\v 14 Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, "Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
\s5
\v 15 Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 16 Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.
\s5
\v 17 Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima ya milele?"
\v 18 Na Yesu akasema, "Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.
\v 19 Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'."
\s5
\v 20 Mtu yule akasema, "Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana."
\v 21 Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, "Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. Ndipo uje unifuate."
\v 22 Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondoka akiwa mwenye huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
\s5
\v 23 Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, "Ni jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 24 Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, "Watoto, ni jinsi gani ilivyo vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 25 Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 26 Walishangazwa sana na wakasemezana, "Hivyo nani ataokoka"
\v 27 Yesu akawaangalia na kusema, " Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana."
\v 28 "Petro akaanza kuzungumza naye, "Angalia tumeacha vyote na tumekufuata."
\s5
\v 29 Yesu akasema, "Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
\v 30 ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.
\v 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."
\s5
\v 32 Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaambia ambacho kitamtokea hivi karibuni:
\v 33 "Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
\v 34 Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka."
\s5
\v 35 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, "Mwalimu, tunakuhitaji utufanyie chochote tukuombacho."
\v 36 Aliwaambia, "Mnataka niwatendee nini?"
\v 37 Wakasema, "Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto."
\s5
\v 38 Lakini Yesu aliwajibu, "Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?"
\v 39 Wakamwambia, "Tunaweza" Yesu akawaambia, "Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.
\v 40 Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa."
\s5
\v 41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.
\v 42 Yesu akawaita kwake na kusema, "Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala, na watu wao mashuhuri huwaonyesha mamlaka juu yao."
\s5
\v 43 Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,
\v 44 na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.
\v 45 Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi."
\s5
\v 46 Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
\v 47 Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
\v 48 Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
\s5
\v 49 Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, "Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita."
\v 50 Akalitupa pembeni koti lake, akakimbia zaidi, na kuja kwa Yesu.
\s5
\v 51 Yesu akamjibu na kusema, "Unataka nikufanyie nini?" Yule mwanaume kipofu akamjibu, "Mwalimu, ninataka kuona."
\v 52 Yesu akamwambia, "Nenda. Imani yako imekuponya." Hapo hapo macho yake yakaona; na akamfuata Yesu barabarani.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Wakati huo walipokuja Yerusalemu, walipokaribia Besthfage na Bethania, katika Mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake
\v 2 na aliwaambia, "Nendeni katika kijiji kinachokabiliana nasi. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu.
\v 3 Na kama yeyote akiwaambia, 'Kwa nini mnafanya hivi'?, mnapaswa kusema, 'Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa'."
\s5
\v 4 Walikwenda na kumkuta mwanapunda amefungwa nje mlangoni kwenye mtaa ulio wazi, nao walimfungua.
\v 5 Na baadhi ya watu walikuwa wamesimama pale na waliwaambia, "Mnafanya nini, kumfungua mwanapunda huyo?"
\v 6 Waliwaambia kama Yesu alivyowaambia, na watu wakawaacha waende.
\s5
\v 7 Wanafunzi wawili walimleta mwanapunda kwa Yesu na walitandika mavazi yao juu yake ili Yesu aweze kumpanda.
\v 8 Watu wengi wakatandika mavazi yao barabarani, na wengine wakatandika matawi waliyoyakata kutoka mashambani.
\v 9 Wale waliokwenda mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, "Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.
\v 10 Ubarikiwe ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Hosana kwa aliye juu"
\s5
\v 11 Ndipo Yesu aliingia Yerusalemu na alikwenda hekaluni na alitazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alikwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili.
\v 12 Siku iliyofuata, wakati walipokuwa wakirudi kutoka Bethania, alikuwa na njaa.
\s5
\v 13 Na akaona mti wa mtini uliokuwa na majani kwa mbali, alikwenda kutazama kama angeweza kupata chochote juu yake. Na wakati alipokwenda kwa huo, hakupata chochote isipokuwa majani, kwa kuwa haikuwa majira ya mtini.
\v 14 Aliuambia, "Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena". Na wanafunzi wake wakasikia.
\s5
\v 15 Walikuja Yerusalemu, naye aliingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Alizipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
\v 16 Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa.
\s5
\v 17 Aliwafundisha na akasema, "Je haikuandikwa, 'nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote'? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi".
\v 18 Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwua. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake.
\v 19 Na kila wakati jioni ilipofika, waliondoka mjini.
\s5
\v 20 Walipokuwa wakitembea asubuhi, waliuona mti wa mtini umekauka mpaka kwenye mizizi yake.
\v 21 Petro alikumbuka na kusema, "Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka".
\s5
\v 22 Yesu aliwajibu, "Muwe na imani katika Mungu.
\v 23 Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya.
\s5
\v 24 Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu.
\v 25 Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.
\v 26 (Zingatia: Mstari huu, "Lakini msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatasamehe dhambi zenu" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 27 Walikuja Yerusalemu tena. Na Yesu alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu, waandishi na wazee walikuja kwake.
\v 28 Walimwambia, "Kwa mamlaka gani unafanya mambo haya?" Na ni nani aliyekupa mamlaka kuyafanya haya?"
\s5
\v 29 Yesu aliwaambia, "Nitawauliza swali moja. Niambieni na mimi nitawaambia kwa mamlaka gani ninayafanya mambo haya.
\v 30 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au ulitoka kwa wanadamu? Nijibuni."
\s5
\v 31 Walijadiliana miongoni mwao na kushindana na kusema, "Kama tukisema, 'Kutoka mbinguni,' atasema, 'Kwa nini basi hamkumwamini?'
\v 32 Lakini kama tukisema, 'Kutoka kwa wanadamu,'..." Waliwaogopa watu, kwa kuwa wote walishikilia kwamba Yohana alikuwa Nabii.
\v 33 Ndipo walimjibu Yesu na kusema, "Hatujui. Ndipo Yesu akawaambia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nayafanya mambo haya.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, "Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.
\v 2 Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.
\v 3 Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.
\s5
\v 4 Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu.
\v 5 Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua.
\s5
\v 6 Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, "Watamheshimu mwanangu".
\v 7 Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, "Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu."
\s5
\v 8 Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.
\v 9 Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.
\s5
\v 10 Hamjapata kusoma andiko hili? "Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.
\v 11 Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu."
\v 12 Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.
\s5
\v 13 Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.
\v 14 Walipofika, wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?
\v 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, "Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama."
\s5
\v 16 Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, "Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, "Ya Kaisari."
\v 17 Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu." Wakamstaajabia.
\s5
\v 18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
\v 19 "Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
\s5
\v 20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
\v 21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
\v 22 Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa.
\v 23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake."
\s5
\v 24 Yesu aliwaambia, "Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?"
\v 25 Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
\s5
\v 26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?'
\v 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka."
\s5
\v 28 Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, "Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?"
\v 29 Yesu alimjibu, "Iliyo ya muhimu ni hii, "Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
\v 30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.'
\v 31 Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi."
\s5
\v 32 Mwandishi akasema, "Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.
\v 33 Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza."
\v 34 Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, "Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu." Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.
\s5
\v 35 Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, "Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
\v 36 Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.'
\v 37 Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?" Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
\s5
\v 38 Katika mafundisho yake Yesu alisema, "Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko
\v 39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu.
\v 40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu."
\s5
\v 41 Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.
\v 42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.
\s5
\v 43 Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, "Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.
\v 44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, "Mwalimu, tazama mawe haya yakushangaza na majengo!"
\v 2 Akamwambia, Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini".
\s5
\v 3 Naye alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni nyuma ya hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri,
\v 4 "Tuambie, mambo haya yatakuwa lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?"
\s5
\v 5 Yesu alianza kuwaambia, "Kuweni makini kwamba mtu yoyote asiwapotoshe.
\v 6 Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, 'Mimi ndiye', na watawapotosha wengi.
\s5
\v 7 Mtakaposikia vita na tetesi za vita, msiogope; mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho bado.
\v 8 Taifa litainuka kinyume na taifa jingine, na ufalme kinyume na ufalme. Patakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali, na njaa. Huu ni mwanzo wa utungu.
\s5
\v 9 Iweni macho. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapingwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao.
\v 10 Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.
\s5
\v 11 Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Ndani ya muda huo, mtapewa nini cha kusema; hamtakuwa ninyi mtakaoongea, bali Roho Mtakatifu.
\v 12 Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa, baba na mtoto wake. Watoto watasimama kinyume cha baba zao na kuwasababisha kuuawa.
\v 13 Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.
\s5
\v 14 Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama pale lisipotakiwa kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yuda wakimbilie milimani,
\v 15 naye aliyeko juu ya nyumba asishuke chini ya nyumba, au kuchukua chochote kilichoko nje,
\v 16 na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.
\s5
\v 17 Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo!
\v 18 Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi.
\v 19 Kwani patakuwa na mateso makubwa, ambayo hayajawahi kutokea, tangu Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka sasa, hapana, wala haitatokea tena.
\v 20 Mpaka Bwana atakapopunguza siku, hakuna mwili utakaookoka, lakini kwa ajili ya wateule, atakaowachagua, atapunguza namba za siku.
\s5
\v 21 Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yuko hapa!' au 'Tazama, yuko pale!' msiamini.
\v 22 Kwani Wakristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule.
\v 23 Iweni macho! Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.
\s5
\v 24 Lakini baada ya mateso ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake,
\v 25 nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika.
\v 26 Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu.
\v 27 Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
\s5
\v 28 Kwa mtini jifunzeni. Kama tawi liwezavyo kutoa na kuweka haraka majani yake, ndipo mtajua kwamba kiangazi kiko karibu.
\v 29 Ndivyo ilivyo, mtakapoona mambo haya yakitokea, jueni kwamba yuko karibu, na malango.
\s5
\v 30 Kweli, nawambieni, hiki kizazi hakitapita mbali kabla mambo haya hayajatokea.
\v 31 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\v 32 Lakini kuhusu siku hiyo au saa, hakuna ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
\s5
\v 33 Iweni macho, Tazama, kwa sababu hamjui ni muda gani yatatokea. (Zingatia: Mstari huu, "Muwe waangalifu, Tazameni na ombeni kwa sababu..." haumo kwenye nakala za kale).
\v 34 Ni kama mtu anayeenda safarini: akaacha nyumba yake, na kumweka mtumwa wake kuwa mtawala wa nyumba, kila mmoja na kazi yake. Na kumwamuru mlinzi kukaa macho.
\s5
\v 35 Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi.
\v 36 Kama akija ghafla, asikukute umelala.
\v 37 Kile nikisemacho kwako nakisema kwa kila mtu: Kesheni"!
\s5
\c 14
\p
\v 1 Ilikuwa siku mbili tu baada ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta namna ya kumkamata Yesu kwa hila na kumuua.
\v 2 Kwa kuwa walisema, "Sio wakati huu wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia."
\s5
\v 3 Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake.
\v 4 Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Waliambiana wao kwa wao wakisema, "Ni nini sababu ya upotevu huu?
\v 5 Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini." Nao walimkemea.
\s5
\v 6 Lakini Yesu alisema, "Mwacheni peke yake. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu.
\v 7 Siku zote maskini mnao, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote.
\v 8 Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.
\v 9 Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.
\s5
\v 10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa wakuu wa makuhani ili kwamba apate kumkabidhi kwao.
\v 11 Wakati wakuu wa Makuhani waliposikia hivyo, walifurahi na wakaahidi kumpa fedha. Alianza kutafuta nafasi ya kumkabidhi kwao.
\s5
\v 12 Katika siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu, wakati walipotoa mwanakondoo wa pasaka, wanafunzi wake walimwambia, "Unataka twende wapi tukaandae ili upate kula mlo wa Pasaka?"
\v 13 Aliwatuma wanafuzi wake wawili na kuwaambia, "Nendeni mjini, na mwanamume ambaye amebeba mtungi ataonana nanyi. Mfuateni.
\v 14 Nyumba atakayoingia, mfuateni na mmwambie mwenye nyumba hiyo, 'Mwalimu asema, "Kiko wapi chumba cha wageni mahali nitakapokula Pasaka na wanafunzi wangu?"
\s5
\v 15 Atawaonesha chumba cha juu kikubwa chenye samani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale."
\v 16 Wanafunzi waliondoka wakaenda mjini; walikuta kila kitu kama alivyokuwa amewaambia, na wakaandaa mlo wa Pasaka.
\s5
\v 17 Wakati ilipokuwa jioni, alikuja na wale Kumi na wawili.
\v 18 Na walipokuwa wakiikaribia meza na kula, Yesu alisema, "Kweli nawaambia, mmoja kati yenu anayekula pamoja nami atanisaliti."
\v 19 Wote walisikitika, na mmoja baada ya mwingine walimwambia, "Hakika siyo mimi?"
\s5
\v 20 Yesu alijibu na kuwaambia, "Ni mmoja wa Kumi na wawili kati yenu, mmoja ambaye sasa anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.
\v 21 Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake. Lakini ole wake mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa! Ingekuwa vizuri zaidi kwake kama mtu yule asingezaliwa."
\s5
\v 22 Na walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, akaubariki, na kuumega. Aliwapa akisema, "Chukueni. Huu ni mwili wangu."
\v 23 Alichukua kikombe, akashukuru, na akawapatia, na wote wakakinywea.
\v 24 Aliwaambia, "Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi.
\v 25 Kweli nawaambia, sitakunywa tena katika zao hili la mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 26 Walipokwisha kuimba wimbo, walikwenda nje katika Mlima wa Mizeituni.
\v 27 Yesu aliwaaambia, "Ninyi nyote mtajitenga mbali kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, 'Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.'
\s5
\v 28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia mbele yenu Galilaya."
\v 29 Petro alimwambia, "Hata kama wote watakuacha, mimi sitakuacha."
\s5
\v 30 Yesu alimwambia, "Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu."
\v 31 Lakini Petro alisema, "Hata itanilazimu kufa pamoja nawe, sitakukana." Wote walitoa ahadi ile ile.
\s5
\v 32 Walikuja kwenye eneo lililoitwa Gethsemane, na Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa wakati nasali."
\v 33 Aliwachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye, akaanza kuhuzunika na kutaabika sana.
\v 34 Aliwaambia, "Nafsi yangu ina huzuni sana, hata kufa. Bakini hapa na mkeshe."
\s5
\v 35 Yesu alienda mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba, kama ingewezekana, kwamba saa hii ingemwepuka.
\v 36 Alisema, "Aba, Baba, Mambo yote kwako yanawezekana. Niondolee kikombe hiki. Lakini siyo kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako."
\s5
\v 37 Alirudi na kuwakuta wamelala, na akamwambia Petro, "Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?
\v 38 Kesheni na muombe kwamba msije mkaingia katika majaribu. Hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
\v 39 Alienda tena na kuomba, na alitumia maneno yaleyale.
\s5
\v 40 Alikuja tena akawakuta wamelala, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito na hawakujua nini cha kumwambia.
\v 41 Alikuja mara ya tatu na kuwaambia, "Bado mmelala na kupumzika? Yatosha! Saa imefika. Tazama! Mwana wa Adamu atasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
\v 42 Amkeni, twendeni. Tazama, yule anayenisaliti yuko karibu."
\s5
\v 43 Mara tu alipokuwa bado anaongea, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, alifika, na kundi kubwa kutoka kwa wakuu wa makuhani, waandishi na wazee wenye mapanga na marungu.
\v 44 Wakati huo msaliti wake alikuwa amewapa ishara, akisema, Yule nitakayembusu, ndiye. Mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi."
\v 45 Wakati Yuda alipofika, moja kwa moja alienda kwa Yesu na kusema, "Mwalimu!" Na akambusu.
\v 46 Kisha wakumtia chini ya ulinzi na kumkamata.
\s5
\v 47 Lakini mmoja kati yao aliyesimama karibu naye alichomoa upanga wake akampiga mtumishi wa kuhani mkuu na kumkata sikio.
\v 48 Yesu aliwaambia, "Mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama mnyang'anyi?
\v 49 Wakati kila siku nilikuwa nanyi na nikifundisha hekaluni, hamkunikamata. Lakini hili limefanyika ili maandiko yatimie.
\v 50 Na wale wote waliokuwa na Yesu walimwacha na kukimbia.
\s5
\v 51 Kijana mmoja alimfuata, aliyekuwa amevaa shuka tu aliyokuwa amejifunika kumzunguka; walimkamata lakini
\v 52 aliwaponyoka akaiacha shuka pale akakimbia uchi.
\s5
\v 53 Walimwongoza Yesu kwa kuhani mkuu. Pale walikusanyika pamoja naye makuhani wakuu wote, wazee, na waandishi.
\v 54 Petro naye alimfuata Yesu kwa mbali, kuelekea kwenye ua wa kuhani mkuu. Aliketi pamoja na walinzi, waliokuwa karibu na moto wakiota ili kupata joto.
\s5
\v 55 Wakati huo makuhani wakuu wote na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua. Lakini hawakuupata.
\v 56 Kwa kuwa watu wengi walileta ushuhuda wa uongo dhidi yake, lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\s5
\v 57 Baadhi walisimama na kuleta ushahidi wa uongo dhidi yake; wakisema,
\v 58 "Tulimsikia akisema, 'Nitaliharibu hekalu hili lililotengenezwa kwa mikono, na ndani siku tatu nitajenga lingine lisilotengenezwa kwa mikono.'"
\v 59 Lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\s5
\v 60 Kuhani mkuu alisimama katikati yao na akamwuliza Yesu, "Je, huna jibu? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?"
\v 61 Lakini alikaa kimya na hakujibu chochote. Mara Kuhani mkuu alimwuliza tena, "Je wewe ni Kristo, mwana wa Mbarikiwa?"
\v 62 Yesu alisema, "Mimi ndiye. Na utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa nguvu akija na mawingu ya mbinguni."
\s5
\v 63 Kuhani mkuu alirarua mavazi yake na kusema, "Je, bado tunahitaji mashahidi?
\v 64 Mmesikia kufuru. Uamuzi wenu ni upi?" Na wote walimhukumu kama mmoja aliyestahili kifo.
\v 65 Baadhi wakaanza kumtemea mate na kumfunika uso na kumpiga na kumwambia, "Tabiri!" Maafisa walimchukua na kumpiga.
\s5
\v 66 Na Petro alipokuwa bado yuko chini uani, mtumishi mmoja wa wasichana wa kuhani mkuu alikuja kwake.
\v 67 Alimwona Petro alipokuwa amesimama akiota moto, na alimtazama kwa kumkaribia. Kisha alisema, "Nawe pia ulikuwa na Mnazareti, Yesu".
\v 68 Lakini alikataa, akisema, "Sijui wala sielewi kuhusu kile unachosema!" Kisha alitoka akaenda nje uani. (Zingatia; Mstari huu, "Na jogoo akawika" haumo kwenye nakala za kale).
\s5
\v 69 Lakini mtumishi wa kike pale, alimwona na alianza kuwaambia tena wale ambao walikuwa wamesimama pale, "Mtu huyu ni mmoja wao!"
\v 70 Lakini alikana tena. Baadaye kidogo wale waliokuwa wamesimama pale walikuwa wakimwambia Petro, "Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya."
\s5
\v 71 Lakini alianza kujiweka mwenyewe chini ya laana na kuapa, "Simjui mtu huyu mnayemsema."
\v 72 Kisha jogoo aliwika mara ya pili. Kisha Petro alikumbuka maneno ambayo Yesu aliyokuwa amemwambia: "Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu." Na alianguka chini na kulia.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Asubuhi na mapema wakuu wa makuhani walikutana pamoja na wazee na waandishi na baraza zima la wazee. Kisha wakamfunga Yesu wakampeleka kwa Pilato. Pilato akamwuliza, "wewe ni Mfalme wa Wayahudi?"
\v 2 "Akamjibu, "Wewe umesema hivyo."
\v 3 Wakuu wa makuhani wakaeleza mashitaka mengi juu ya Yesu.
\s5
\v 4 Pilato akamwuliza tena, "Hujibu chochote? Huoni jinsi wanavyokushtaki kwa mambo mengi?
\v 5 Lakini Yesu hakumjibu Pilato, na hiyo ilimshangaza.
\s5
\v 6 Kwa kawaida wakati wa sikukuu humfungulia mfungwa mmoja, mfungwa waliyemwomba.
\v 7 Kulikuwapo wahalifu gerezani, miongoni mwa wauaji kati ya walioasi wanaotumikia makosa yao. Alikuwepo mtu mmoja aitwaye Baraba.
\v 8 Umati ulikuja kwa Pilato, na kumwomba afanye kama alivyofanya huko nyuma.
\s5
\v 9 Pilato akawajibu na kusema, "Mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?"
\v 10 Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake.
\v 11 Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba afunguliwe Baraba badala yake.
\s5
\v 12 Pilato akawajibu tena na kusema, "Nimfanye nini Mfalme wa Wayahudi?
\v 13 Wakapiga kelele tena, "Msulibishe!"
\s5
\v 14 Pilato akasema, "Amefanya jambo gani baya?" Lakini wakazidi kupiga kelele zaidi na zaidi "Msulibishe."
\v 15 Pilato akitaka kuwaridhisha umati, akawafungulia Baraba. Akampiga Yesu mijeledi kisha akamtoa ili asulibiwe.
\s5
\v 16 Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ule ulio ndani ya kambi) na walikusanyika pamoja kikosi cha askari.
\v 17 Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.
\v 18 Wakaanza kumdhihaki na kusema, "Salam, Mfalme wa Wayahudi!"
\s5
\v 19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.
\v 20 Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulibisha.
\v 21 Wakamlazimisha mpita njia kumsaidia, aliyekuwa anaingia mjini kutoka shamba. Aitwaye Simoni Mkirene (baba yake Iskanda na Rufo); wakamlazimisha kubeba msalaba wa Yesu.
\s5
\v 22 Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa).
\v 23 Wakampa mvinyo iliyochanganywa na manemane, lakini hakunywa.
\v 24 Wakamsulibisha na wakagawana mavazi yake, wakayapigia kura kuamua kipande atakachopata kila askari.
\s5
\v 25 Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.
\v 26 Wakaweka juu yake ubao ulioandikwa shitaka, "Mfalme wa Wayahudi."
\v 27 Walimsubisha pamoja na majambazi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine kushoto kwake.
\v 28 (Zingatia: Mstari huu, "Na maandiko yakatimia yaliyonena" haumo katika nakala za kale).
\s5
\v 29 Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, "Aha! wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,
\v 30 jiokoe mwenyewe na ushuke chini toka msalabani!"
\s5
\v 31 Kwa namna ile ile wakuu wa makuhani walimdhihaki wakisemezana, pamoja na waandishi na kusema, "Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe.
\v 32 Kristo Mfalme wa Israel, shuka chini sasa toka msalabani, ili tuweze kuona na kuamini." Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimdhihaki.
\s5
\v 33 Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.
\v 34 Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lama sabaktani?" ikiwa na maana "Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?"
\v 35 Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, "Tazama, anamwita Eliya."
\s5
\v 36 Mtu mmoja akakimbia, akajaza siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, "Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini."
\v 37 Kisha Yesu akalia kwa sauti kubwa na akafa.
\v 38 Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini.
\s5
\v 39 Ofisa mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, "Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu."
\v 40 Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome.
\v 41 Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.
\s5
\v 42 Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,
\v 43 Yusufu wa Arimathaya alikuja pale. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza anayeheshimiwa mtu anayeutarajia Ufalme wa Mungu. Kwa ujasiri akaenda kwa Pilato, na kuuomba mwili wa Yesu.
\v 44 Pilato akashangazwa kwamba Yesu tayari amekufa; akamwita yule afisa akamwuliza kama Yesu amekufa.
\s5
\v 45 Alipopata uhakika kwa afisa kwamba amekufa, alimruhusu Yusufu kuuchukua mwili.
\v 46 Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.
\v 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yose waliona sehemu alipozikwa Yesu.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake na Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu kwa ajili ya maziko.
\v 2 Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza.
\s5
\v 3 Wakisemezana wao kwa wao, "Nani ataliviringisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?"
\v 4 Wakati walipotazama, walimuona mtu amekwisha kulivingirisha jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana.
\s5
\v 5 Wakaingia kwenye kaburi na wakamwona kijana amevaa joho jeupe, ameketi upande wa kulia, na wakashangazwa.
\v 6 Akawaambia, "Msiogope. Mnamtafuta Yesu, wa Nazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayupo hapa. Tazama mahali pale walipokuwa wamemweka.
\v 7 Nendeni, mkawaambie wanafunzi wake na Petro ya kuwa amewatangulia kuelekea Galilaya. Huko mtamwona, kama alivyokua amewaambia."
\s5
\v 8 Wakaondoka na kukimbia kutoka kwenye kaburi; walitetemeka na walishangazwa. Hawakusema chochote kwa mtu yeyote sababu waliogopa sana.
\s5
\v 9 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba.
\v 10 Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakihuzunika na kutoa machozi.
\v 11 Walisikia kwamba ni mzima na ameonekana naye, lakini hawakumwamini.
\s5
\v 12 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Baada ya hayo, akajitokeza katika namna tofauti kwa watu wengine wawili, wakati walipokuwa wakitembea kutoka katika nchi.
\v 13 Walienda na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini.
\s5
\v 14 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wameegama katika meza, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
\v 15 Akawaambia, " Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote.
\v 16 Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa.
\s5
\v 17 (Zingatia: Nakala za kale hazina Marko 16: 9-20) Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya.
\v 18 Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kufisha hakitawadhuru. Wataweka mikono kwa wagonjwa, nao watakuwa wazima".
\s5
\v 19 Baada ya Bwana kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
\v 20 Wanafunzi wakaondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana akifanya kazi nao na kulithibitisha neno kwa miujiza na ishara zikifuatana nao.

2188
43-LUK.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2188 @@
\id LUK
\ide UTF-8
\h Luka
\toc1 Luka
\toc2 Luka
\toc3 luk
\mt Luka
\s5
\c 1
\p
\v 1 Wengi wamejitahidi kuweka katika mpangilio simulizi kuhusu masuala ambayo yametimizwa kati yetu,
\v 2 kama walivyotupatia sisi, ambao tangu mwanzo ni mashahidi wa macho na watumishi wa ujumbe.
\v 3 Hivyo nami pia, baada ya kuchuguza kwa uangalifu chanzo cha mambo haya yote tokea mwanzo - nimeona ni vema kwangu pia kukuandikia katika mpangilio wake - mheshimiwa sana Theofilo.
\v 4 Ili kwamba uweze kujua ukweli wa mambo uliyofundishwa.
\s5
\v 5 Katika siku za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani fulani aliyeitwa Zekaria, wa ukoo wa Abiya. Mke wake alitoka kwa binti za Haruni, na jina lake aliitwa Elizabeti.
\v 6 Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu; walitembea bila lawama katika amri zote na maagizo ya Bwana.
\v 7 Lakini hawakuwa na mtoto, kwasababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
\s5
\v 8 Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.
\v 9 Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.
\v 10 Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.
\s5
\v 11 Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.
\v 12 Zakaria alitishika alipomuona; hofu ikamwangukia.
\v 13 Lakini malaika akamwambia, "Usiogope Zakaria, kwasababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.
\s5
\v 14 Utakuwa na furaha na uchangamfu, na wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
\v 15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
\s5
\v 16 Na watu wengi wa Israel watageuzwa kwa Bwana Mungu wao.
\v 17 Atakwenda mbele za uso wa Bwana katika roho na nguvu ya Eliya. Atafanya hivi ili kurejesha mioyo ya baba kwa watoto, ili kwamba wasiotii wataenenda katika hekima ya wenye haki. Atafanya hivi kuweka tayari kwa Bwana watu ambao wameandaliwa kwa ajili yake."
\s5
\v 18 Zakaria akamwambia malaika, "Nitawezaje kujua hili? Kwasababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana."
\v 19 Malaika akajibu na kumwambia, "Mimi ni Gabrieli, ambaye husimama mbele za Mungu. Nilitumwa kukwambia, kukuletea habari hii njema.
\v 20 Na tazama, hutaongea, utakuwa kimya, hutaweza kuongea mpaka siku ile mambo haya yatakapotokea. Hii ni kwasababu ulishindwa kuamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati mwafaka."
\s5
\v 21 Sasa watu walikuwa wakimsubiri Zakaria. Walishangazwa kwamba alikuwa anatumia muda mwingi hekaluni.
\v 22 Lakini alipotoka nje, hakuweza kuongea nao. Wakatambua kwamba alikuwa amepata maono alipokuwa hekaluni. Aliendelea kuonesha ishara na alibaki kimya.
\v 23 Ikatokea kwamba siku za huduma yake zilipokwisha aliondoka kurudi nyumbani kwake.
\s5
\v 24 Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema,
\v 25 "Hili ndilo amabalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu."
\s5
\v 26 Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti,
\v 27 kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake lilikuwa Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.
\v 28 Akaja kwake na akasema, "Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe."
\v 29 Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake.
\s5
\v 30 Malaika akamwambia, "Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu.
\v 31 Na tazama, utabeba mimba katika tumbo lako na utazaa mwana. Nawe utamwita jina lake 'Yesu.'
\v 32 Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.
\v 33 Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
\s5
\v 34 Mariamu akamwambia malaika, hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote?
\v 35 Malaika akajibu na akamwambia, "Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu.
\s5
\v 36 Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.
\v 37 Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu."
\v 38 Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako." Kisha malaika akamwacha.
\s5
\v 39 Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea.
\v 40 Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti.
\v 41 Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
\s5
\v 42 Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, "umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
\v 43 Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu?
\v 44 Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha.
\v 45 Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana."
\s5
\v 46 Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana,
\v 47 na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
\s5
\v 48 Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
\v 49 Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu.
\s5
\v 50 Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye.
\v 51 Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
\s5
\v 52 Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
\v 53 Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
\s5
\v 54 Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
\v 55 (kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele."
\s5
\v 56 Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
\v 57 Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
\v 58 Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
\s5
\v 59 Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, "Zekaria," kwa kuzingatia jina la baba yake,
\v 60 Lakini mama yake akajibu na kusema, "Hapana; ataitwa Yohana."
\v 61 Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili."
\s5
\v 62 Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
\v 63 Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, "Jina lake ni Yohana." Wote wakashangazwa na hili.
\s5
\v 64 Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
\v 65 Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.
\v 66 Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, " Mtoto huyu kuwa wa namna gani?" Kwasababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
\s5
\v 67 Baba yake Zekaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
\v 68 "Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
\s5
\v 69 Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
\v 70 kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
\v 71 Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
\s5
\v 72 Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
\v 73 kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
\v 74 Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu.
\v 75 katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
\s5
\v 76 Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
\v 77 kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.
\s5
\v 78 Hili litatokea kwa sababu ya huruma ya Mungu wetu, sababu ambayo jua tokea juu litatujia,
\v 79 kuangaza kwao wakaao gizani na katika uvuli wa mauti. Atafanya hivi kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani."
\s5
\v 80 Sasa, yule mtoto akakua na kuwa mwenye nguvu rohoni na alikaa nyikani mpaka siku ya kujitokeza kwake kwa Israeli.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani.
\v 2 Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria.
\v 3 Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.
\s5
\v 4 Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo ya Daudi.
\v 5 Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto.
\s5
\v 6 Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia.
\v 7 Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.
\s5
\v 8 Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.
\v 9 Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana.
\s5
\v 10 Ndipo malaika akwaambia, "Msiogope, kwasababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote.
\v 11 Leo Mwokozi kazaliwa kwaajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana!
\v 12 Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama."
\s5
\v 13 Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema,
\v 14 "Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao."
\s5
\v 15 Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, " Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha."
\v 16 Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama.
\s5
\v 17 Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto.
\v 18 Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji.
\v 19 Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake.
\v 20 Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.
\s5
\v 21 Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
\s5
\v 22 zao zilizotakiwa za utakaso zilipopita, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.
\v 23 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, "Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana."
\v 24 Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, "Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa."
\s5
\v 25 Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
\v 26 Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.
\s5
\v 27 Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,
\v 28 ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
\v 29 "Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
\s5
\v 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
\v 31 ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
\v 32 Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo kwa Wamataifa na utukufu wa watu Israeli."
\s5
\v 33 Baba na Mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.
\v 34 Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, "Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.
\v 35 Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike".
\s5
\v 36 Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,
\v 37 na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
\v 38 Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
\s5
\v 39 Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.
\v 40 Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
\s5
\v 41 Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka.
\v 42 Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
\v 43 Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
\v 44 Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
\s5
\v 45 Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
\v 46 Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
\v 47 Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
\s5
\v 48 Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, "Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa."
\v 49 Akawaambia, "Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?
\v 50 Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.
\s5
\v 51 Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.
\v 52 Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberia, wakati Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo ndugu yake alikuwa mkuu wa mkoa wa Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
\v 2 na wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria, jangwani.
\s5
\v 3 Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi
\s5
\v 4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, "sauti ya mtu aliaye nyikani, "Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
\s5
\v 5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
\v 6 Watu wote watauona wokovu wa Mungu."
\s5
\v 7 Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, "Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
\s5
\v 8 Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, "Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu; kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
\s5
\v 9 Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
\s5
\v 10 Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, "Sasa tunatakiwa tufanyeje?"
\v 11 Alijibu na kuwaambia, "kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo."
\s5
\v 12 Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, "Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?
\v 13 Akawaambia, "Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya."
\s5
\v 14 Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, "Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?" Akawambia, "Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu."
\s5
\v 15 Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.
\v 16 Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, "Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
\s5
\v 17 Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
\s5
\v 18 Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.
\v 19 Yohana alimkemea pia Herode mkuu wa mkoa kwa kumuoa Herodia, mke wa ndugu yake na kwa maovu mengine mengi ambayo Herode alikuwa ameyatenda.
\v 20 Lakini baadaye Herode alifanya uovu mwingine mbaya sana. Alimfunga Yohana gerezani.
\s5
\v 21 Kisha ilitokea kwamba, wakati watu wote walipokuwa wakibatizwa na Yohana, naye Yesu alibatizwa pia. Wakati alipokuwa akiomba, mbingu zikafunguka.
\v 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama njiwa, wakati huo huo sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema, "Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe."
\s5
\v 23 Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyotadhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli,
\v 24 mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu,
\s5
\v 25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai,
\v 26 mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda,
\s5
\v 27 mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
\v 28 mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
\v 29 mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri,, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi,
\s5
\v 30 mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu,
\v 31 mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
\v 32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
\s5
\v 33 mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni,, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda,
\v 34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
\v 35 mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
\s5
\v 36 mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki,
\v 37 mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani,
\v 38 mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha, Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Mto Jordani, na aliongozwa na Roho jangwani
\v 2 kwa siku arobaini, na huko alijaribiwa na Ibilisi. Wakati huo hakula chochote, na mwisho wa wakati huo alihisi njaa.
\s5
\v 3 Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, liamru jiwe hili kuwa mkate."
\v 4 Yesu akamjibu, "Imeandikwa; 'mtu hataishi kwa mkate pekee."
\s5
\v 5 Kisha Ibilisi alimwongoza juu kwenye kilele cha mlima, na akamwonyesha falme zote za dunia kwa muda mfupi.
\v 6 Ibilisi akamwambia, "Nitakupa mamlaka ya kutawala falme hizi zote pamoja na fahari zake. Naweza kufanya hivyo kwa sababu vyote vimekabidhiwa kwangu nivitawale, na ninaweza kumpa yeyote nitakaye kumpa.
\v 7 Kwahiyo, kama utaniinamia na kuniabudu, vitu hivi vyote vitakuwa vyako."
\s5
\v 8 Lakini Yesu alijibu na kumwambia, "Imeandikwa, "lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na lazima umtumikie Yeye peke yake."
\s5
\v 9 Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.
\v 10 Kwa sababu imeandikwa, "Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,
\v 11 na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe."
\s5
\v 12 Yesu akijibu alimwambia, "Imenenwa, "usimjaribu Bwana Mungu wako."
\v 13 Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.
\s5
\v 14 Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.
\v 15 Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.
\s5
\v 16 Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.
\v 17 Alikabidhiwa gombo la nabii Isaya, hivyo, alilifungua gombo na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
\s5
\v 18 "Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,
\v 19 kuutangaza mwaka ambao Bwana ataonesha wema wake."
\s5
\v 20 Kisha akalifunga gombo, akamrudishia kiongozi wa sinagogi, na akaketi chini. Macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yalimwangalia yeye.
\v 21 Alianza kuzungumza nao akisema, "Leo andiko hili limetimizwa masikioni mwenu."
\v 22 Kila mmoja pale alishuhudia kile alichokisema Yesu, na wengi miongoni mwao walishangazwa na maneno ya hekima yaliyokuwa yakitoka katika kinywa chake. Walikuwa wakisema, "huyu ni kijana tu wa Yusufu, siyo hivyo?"
\s5
\v 23 Yesu akawaambia, "hakika mtasema methali hii kwangu, "Tabibu, jiponye mwenyewe. Chochote tulichosikia ukifanya Kapernaumu, kifanye hapa pia kijijini kwako."
\v 24 Pia alisema, "hakika nawaambia ninyi, hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake."
\s5
\v 25 Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na nvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
\v 26 Lakini Eliya hakutumwa kwa yeyote mmoja wao, lakini kwa mjane mmoja tu aliyeishi Sarepta karibu na mji wa Sidoni.
\v 27 Pia, kulikuwa na wakoma wengi Israel katika kipindi cha Elisha nabii, lakini hakuna hatammoja wao aliyeponywa isipokuwa Naamani mtu wa Siria.
\s5
\v 28 Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na gadhabu walipoyasikia haya yote.
\v 29 Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima wa mji ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
\v 30 Lakini alipita salama katikati yao na akaenda zake.
\s5
\v 31 Kisha alitelemkia Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato moja alikuwa akifundisha watu ndani ya sinagogi.
\v 32 Walishangazwa na mafundisho yake, kwasababu alifundisha kwa mamlaka.
\s5
\v 33 Sasa siku hiyo ndani ya sinagogi, kulikuwa na mtu aliyekuwa na roho ya pepo mchafu, na alilia kwa sauti ya juu,
\v 34 "Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani! Wewe ni mtakatifu wa Mungu!"
\s5
\v 35 Yesu alimkemea pepo akisema, "Nyamaza kimya, na umtoke mtu huyu!" Pepo yule alipomtupa mtu yule chini katikati yao, alimtoka yule mtu bila ya kumsababishia maumivu yoyote.
\v 36 Watu wote walishangaa, na waliendelea kuzungumzia jambo hilo kila mmoja na mwenzake. Wakasema, "Ni maneno ya aina gani haya?" Anawaamuru roho wachafu kwa mamlaka na nguvu na watondoka."
\v 37 Hivyo, habari juu ya Yesu zilienea kila sehemu katika maeneo yanayozunguka mkoa huo.
\s5
\v 38 Kisha Yesu aliondoka katika mji huo na akaingia katika nyumba ya Simoni. Sasa, mama mkwe wake na Simoni alikuwa anaumwa homa kali, na wakamsihi kwa niaba yake.
\v 39 Hivyo, Yesu alimsogelea, akaikemea ile homa na ikamwachia. Ghafla alisimama na akaanza kuwatumikia.
\s5
\v 40 Jua lilipokuwa likizama, watu walimletea Yesu kila mmoja aliyekuwa mgonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na akawaponya wote.
\v 41 Mapepo pia yaliwatoka wengi wao yakilia kwa sauti na kusema, "Wewe ni mwana wa Mungu!" Yesu aliwakemea mapepo na hakuwaruhusu waongee, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa ni Kristo.
\s5
\v 42 Wakati kulipopambazuka, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao.
\v 43 Lakini akawaambia, "Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa."
\v 44 Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Basi ilitokea wakati watu walipomkusanyikia na kumzunguka Yesu na kusikiliza neno la Mungu, ambapo alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti.
\v 2 Aliona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao.
\v 3 Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.
\s5
\v 4 kuongea, akamwambia Simoni, "Ipeleke mashua yako mpaka kwenye kilindi cha maji nakushusha nyavu zako ili kuvua samaki."
\v 5 Simon akajibu na kusema, Bwana, tumefanya kazi usiku wote, na hatukukamata chochote, lakini kwa neno lako, nitazishusha nyavu.
\v 6 Walipofanya hivyo walikusanya kiasi kikubwa cha samaki na nyavu zao zikaanza kukatika.
\v 7 Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waja na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.
\s5
\v 8 Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema,"Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana."
\v 9 Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.
\v 10 Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, "Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu."
\v 11 Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.
\s5
\v 12 Ilitokea kwamba alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, "Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa."
\v 13 Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, "Nataka. Takasika." Na saa ileile ukoma ukamwacha.
\s5
\v 14 "Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, "Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao."
\s5
\v 15 Lakini habari kumuhusu yeye zikaenea mbali zaidi, na umati mkubwa wa watu ukaja pamoja kumsikiliza akifundisha na kuponywa magonjwa yao.
\v 16 Lakini mara kwa mara alijitenga faraghani na kuomba.
\s5
\v 17 Ilitokea siku moja kati ya hizo siku alikuwa akifundisha, na walikuwapo Mafarisayo na waalimu wa sheria wamekaa hapo ambao walikuja wakitokea vijiji vingi tofauti katika mkoa wa Galilaya na Yudea, na pia kutokea katika mji wa Yerusalemu. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kuponya.
\s5
\v 18 watu kadhaa walikuja, wamembeba kwenye mkeka mtu aliyepooza, na wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ili kumlaza chini mbele ya Yesu.
\v 19 Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.
\s5
\v 20 Akiangalia imani yao, Yesu alisema, "Rafiki, dhambi zako umesamehewa."
\v 21 Waandishi na Mafarisayo waliaanza kuhoji hilo, wakisema, "Huyu ni nani anayeongea makufuru? Ni nani anaweza kusamehe dhambi ila Mungu pekee yake?"
\s5
\v 22 Lakini Yesu, akitambua nini walichokuwa wakifikiri, aliwajibu na kuwaambia, "Kwa nini mnaulizana hili mioyoni mwenu?
\v 23 Kipi ni rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama utembee?'
\v 24 Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi, Nakwambia wewe, 'Amka, chukua mkeka wako na uende nyumbani kwako.'"
\s5
\v 25 Wakati huo huo akaamka mbele yao na akachukua mkeka wake aliokuwa ameulalia. Kisha akariudi nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
\v 26 Kila mmoja alishangazwa na wakamtukuza Mungu. Walijawa na hofu, wakisema, "Tumeona mambo yasiyo ya kawaida leo."
\s5
\v 27 Baada ya mambo haya kutokea, Yesu alitoka huko na akamwona mtoza ushuru aliyeitwa Lawi amekaa eneo la kukusanyia kodi. Akamwambia, "Nifuate."
\v 28 Hivyo Lawi akanyanyuka na kumfuata, akiacha kila kitu nyuma.
\s5
\v 29 Kisha Lawi akaandaa nyumbani kwake karamu kubwa kwa ajili ya Yesu. Walikuwapo watozaushuru wengi kule na watu wengi walioketi mezani wakila pamoja nao.
\v 30 Lakini Mafarisayo na waandishi wao walikuwa wakiwanung'unikia wanafunzi, wakisema, "Kwa nini mnakula na kunywa na watoza ushuru pamoja na watu wengine wenye dhambi?"
\v 31 Yesu akawajibu, "Watu walio katika afya njema hawahitaji tabibu, ni wale tu wanaoumwa ndiyo watakao mhitaji mmoja.
\v 32 Sikuja kuwaita watu wenye haki haki wapate kutubu, bali kuwaita wenye dhambi wapate kutubu."
\s5
\v 33 Wakamwambia, "Wanafunzi wa Yohana mara nyingi hufunga na kuomba, na wanafunzi wa Mafarisayo nao hufanya vivyo hivyo. Lakini wanafunzi wako hula na kunywa."
\v 34 Yesu akawaambia, "Inawezekana mtu yeyote akawafanya waliohudhuria harusi ya Bwana Arusi kufunga wakati Bwana Arusi bado yu pamoja nao?
\v 35 Lakini siku zitakuja wakati Bwana Arusi atakapoondolewa kwao, ndipo katika siku hizo watafunga."
\s5
\v 36 Kisha Yesu aliongea pia kwao kwa mfano. "Hakuna anayechana kipande cha nguo kutoka kwenye vazi jipya na kukitumia kurekebisha vazi la zamani. Kama akifanya hivyo, ataichana nguo mpya, na kipande cha nguo kutoka vazi jipya kisengefaa kutumika na nguo ya vazi la zamani.
\s5
\v 37 pia, hakuna mtu ambaye huweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai mpya ingepasua kile chombo, na divai ingemwagika, na viriba vingeharibika.
\v 38 Lakini divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.
\v 39 Na hakuna mtu baada ya kunywa divai ya zamani, hutataka mpya, kwa sababu husema, 'Ya zamani ni bora."'
\s5
\c 6
\p
\v 1 Sasa ilitokea kwenye Sabato kwamba Yesu alikuwa akipita katika ya shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma masuke, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka.
\v 2 Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, "Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato"?
\s5
\v 3 Yesu, akawajibu, akisema, "Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye?
\v 4 Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hatakama ilikuwa halali kwa makuhani kuila."
\v 5 Kisha akawaambia, "Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato."
\s5
\v 6 Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza.
\v 7 Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa.
\v 8 Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, "Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja." Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale.
\s5
\v 9 Yesu akasema kwao, "Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?" Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu,
\v 10 "Nyoosha mkono wako." Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.
\v 11 Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.
\s5
\v 12 Ilitokea siku hizo kwamba alikwenda mlimani kuomba. Aliendelea usiku mzima kumuomba Mungu.
\v 13 Ilipokuwa asubuhi, aliwaita wanafunzi wake kwake, na akawachagua kumi na wawili kati yao, ambao pia aliwaita "mitume."
\s5
\v 14 Majina ya wale mitume yalikuwa Simoni (ambaye pia alimwita Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,
\v 15 Mathayo, Tomaso na Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni, ambaye aliitwa Zelote,
\v 16 Yuda mwana Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye alikuwa msaliti msaliti.
\s5
\v 17 Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
\v 18 Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia.
\v 19 Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote.
\s5
\v 20 Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, "Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.
\v 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.
\s5
\v 22 Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.
\v 23 Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
\s5
\v 24 Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu.
\v 25 Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye.
\s5
\v 26 Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo.
\s5
\v 27 Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.
\v 28 Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.
\s5
\v 29 Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu.
\v 30 Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.
\s5
\v 31 Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo.
\v 32 Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwamaana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
\v 33 Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
\v 34 Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena.
\s5
\v 35 Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
\v 36 Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
\s5
\v 37 Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
\s5
\v 38 Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi."
\s5
\v 39 Kisha akawaambia mfano pia. "Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?
\v 40 Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.
\s5
\v 41 Na kwa nini basi wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti lililo ndani ya jicho lako huliangalii?
\v 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, 'Ndugu, naomba nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,' nawe huangalii boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza itoe boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.
\s5
\v 43 Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
\v 44 Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma.
\s5
\v 45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake.
\s5
\v 46 Kwanini mnaniita, 'Bwana, Bwana', na bado hamyatendi yale nisemayo?
\v 47 Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo.
\v 48 Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
\s5
\v 49 Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile ilitopata maangamizi makubwa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu.
\s5
\v 2 Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa.
\v 3 Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule Akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife.
\v 4 Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, "anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake,
\v 5 kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu".
\s5
\v 6 Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. "Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu.
\v 7 Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona.
\v 8 Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu "Nenda" na huenda, na kwa mwingine, "Njoo" naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya".
\s5
\v 9 Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema."Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.
\v 10 Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
\s5
\v 11 fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu.
\v 12 Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye.
\v 13 Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, "Usilie".
\v 14 Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema "Kijana nasema amka"
\v 15 Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
\s5
\v 16 Kisha hofu ikawajaa wote. wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema "Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu" na "Mungu amewaangalia watu wake"
\v 17 Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.
\s5
\v 18 Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.
\v 19 Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema "Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?
\v 20 Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, "Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?"
\s5
\v 21 kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.
\v 22 Yesu akajibu na kusema kwao. "Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.
\v 23 Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa".
\s5
\v 24 Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, "Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?
\v 25 lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.
\v 26 lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.
\s5
\v 27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, "Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu,
\v 28 Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana."
\s5
\v 29 Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
\v 30 Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.
\s5
\v 31 Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasai?
\v 32 Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, 'Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. tumeomboleza na hamkulia.'
\s5
\v 33 Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema "Ana pepo.
\v 34 Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, "Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!
\v 35 Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote."
\s5
\v 36 Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.
\v 37 Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato.
\v 38 Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
\s5
\v 39 Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, "Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.
\v 40 Yesu akajibu na kumwambia, "Simoni nina kitu cha kukuambia. "Akasema" "Kiseme tu mwalimu!"
\s5
\v 41 Yesu akasema "Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini.
\v 42 Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?
\v 43 Simoni akamjibu na kusema, "Nadhani aliyesamehewa zaidi."Yesu akamwambia, "Umehukumu kwa usahihi."
\s5
\v 44 Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, "Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake.
\v 45 Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.
\s5
\v 46 Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato.
\v 47 Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu."
\s5
\v 48 Baadaye akamwambia mwanamke, "Dhambi zako zimesamehewa"
\v 49 Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, "Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?"
\v 50 Na Yesu akamwambia mwanamke, "Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani"
\s5
\c 8
\p
\v 1 Ilitokea muda mfupi baadaye kwamba Yesu alianza kusafiri katika miji na jiji mbalimbali, akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu na wale kumi wawili walikwenda pamoja naye,
\v 2 vilevile wanawake fulani waliokuwa wameponywa kutoka kwa roho wachafu na magonjwa mbalimbali. Walikuwa ni Mariamu aliyeitwa Magdalena ambaye alikuwa ametolewa pepo saba.
\v 3 Yoana mke wa Kuza na meneja wa Herode, Susana, na wanawake wengine wengi, waliotoa mali vyao kwa ajili yao wenyewe.
\s5
\v 4 Nabaada ya umati wa watu kukusanyika pamoja, wakiwemo na watu waliokuja kwake kutoka miji mbalimbali, akazungumza nao kwa kutumia mifano.
\v 5 "mpandaji alienda kupanda mbegu, alipokuwa apanda, baadhi ya mbegu hizo ziliangukia kando ya njia zikakanyagwa chini ya miguu, na ndege wa angani wakazila.
\v 6 Mbegu zingine zilianguka juu ya udongo wa miamba na zilipoota na kuwa miche zilipooza kwa sababu hakukuwa na unyevunyevu.
\s5
\v 7 Mbegu zingine ziliangukia kwenye miti ya miiba, nayo hiyo miti ya miiba ikakua pamoja na zile mbegu na zikasongwa.
\v 8 Lakini mbegu zingine ziliangukia kwenye udongo unaofaa na zikazaa mazao mara mia zaidi. "Baada ya Yesu kusema mambo haya, alipaza sauti,"Yeyote aliye na masikio ya kusikia na asikie."
\s5
\v 9 Tena wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo,
\v 10 Yesu akawaambia, "Mmepewa upendeleo wa kujua siri ya ufalme wa Mungu, lakini watu wengine watafundishwa tu kwa mifano, ili kwamba 'wakiona wasione na wakisikia wasielewe.'
\s5
\v 11 Na hii ndiyo maana ya mfano huu. Mbegu ni neno la Mungu.
\v 12 Mbegu zile zilizoanguka kando kando ya njia ndiyo wale watu wanaolisikia neno, na baadaye mwovu shetani hulichukua mbali kutoka moyoni, ili kwamba wasiamini na kuokolewa.
\v 13 Kisha na zile zilizoangukia kwenye mwamba ni watu wale wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha lakini hawana mizizi yeyote, wanaamini tu kwa muda mfupi, na wakati wa majaribu huanguka.
\s5
\v 14 Na mbegu zile zilizoangukia kwenye miiba ni watu wanaosikia neno, lakini wanapoendelea kukua husongwa na huduma na utajiri na ubora wa maisha haya na hawazai matunda.
\v 15 Lakini zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri ni wale watu, ambao ni wanyeyekevu na mioyo mizuri, baada ya kulisikia neno hulishikilia na likawa salama na kuazaa matunda ya uvumilivu.
\s5
\v 16 Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka kwenye kinara cha taa ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona.
\v 17 Kwa kuwa hakuna kitakachojificha ambacho hakitajulikana, au chochote kilicho sirini ambacho hakitajulikana kikiwa kwenye mwanga.
\v 18 kwa hiyo kuwa makini unapokuwa unasikiliza. Kwa sababu aliye nacho, kwake ataongezewa zaidi, lakini asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitachukuliwa."
\s5
\v 19 baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakaribia kwa sababu ya umati wa watu.
\v 20 Na akataarifiwa, "Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe.
\v 21 Lakini, Yesu akajibu akasema "Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii."
\s5
\v 22 Ilitokea siku moja kati ya siku zile Yesu na wanafunzi wake alipanda kwenye mtumbwi, na akawaambia, "Na tuvuke ng'ambo ya pili ya ziwa." Wakaandaa mashua yao.
\v 23 Lakini walipoanza kuondoka, Yesu akalala usingizi, na dhoruba kali yenye upepo, na mashua yao ikaanza kujaa maji na walikuwa kwenye katika kubwa sana.
\s5
\v 24 baadaye wanafunzi wake wakaja kwake na kumwamsha, wakisema, "Bwana mkubwa! Bwana mkubwa! tuko karibu kufa!" Akaamka na akaukemea upepo na mawimbi ya maji vikatulia na kukawa na utulivu.
\v 25 Tena akawaambia, "Imani yenu iko wapi?" Wakaogopa, Walishangaa, wakasemezana kia mmoja na mwenzake,"Huyu ni nani, kiasi kwamba anaamuru hata upepo, na maji na humtii?"
\s5
\v 26 Wakafika kwenye mji wa Gerasini iliyo upande wa nyuma ya Galilaya.
\v 27 Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.
\s5
\v 28 Alipomwona Yesu akalia kwa sauti, na akaanguka chini mbele yake. kwa sauti kubwa akisema, Nimefanya nini kwako, Yesu mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, Usiniadhibu mimi"
\v 29 Yesu akaamuru roho chafu imtoke mtu yule, kwa kuwa mara nyingi amepamgaa. hata kama alikuwa amefungwa minyororo na kubanwa na kuwekwa chini ya ulinzi, alivunja vifungo na kuendeshwa na mapepo mpaka jangwani.
\s5
\v 30 Yesu akamwuliza, "Jina lako nani?" akajibu akisema, "Legioni" Kwa maana mapepo mengi yameingia kwake.
\v 31 Wakaendelea kumsihi usituamuru twende kwenye shimo.
\s5
\v 32 Kundi la Nguruwe lilikuwa likichunga juu ya kilima, wakamsihi awaruhusu wakaingie kwa hao nguruwe. Na akawaruhusu kufanya hivyo.
\v 33 kwa hiyo wale mapepo wakamtoka mtu yule na kuingia kwa wale nguruwe, na lile kundi likakimbia kwenye mwinuko wa mlima mpaka ziwani na wakazama humo.
\s5
\v 34 wale watu waliokuwa wanachunga wale nguruwe walipoona kilichotokea, wakakimbia na wakatoa taarifa pale mjini na nje katika miji iliyowazunguka.
\v 35 Watu waliposikia hayo walienda kuona kilichotokea, na wakaja kwa Yesu na wakamwona mtu ambaye mapepo yalikuwa yamemtoka. alikuwa amevaa vizuri na mwenye akili timamu, amekaa kwenye miguu ya Yesu, na waliogopa.
\s5
\v 36 ndipo mmoja wao aliyeona kilichotokea alianza kuwasimlia wengine jinsi huyu mtu aliyekuwa anaongozwa na mapepo alivyoponywa.
\v 37 Watu wote wa mkoa wa Wagerasi na maeneo yaliyozunguka walimwomba Yesu aondoke kwao kwa sababu walikuwa na hofu kuu. Na aliingia kwenye mtumbwi ili arudi.
\s5
\v 38 Mtu yule aliyetokwa na pepo alimsihi Yesu kwenda naye, lakini Yesu alimwambia aende na kusema,
\v 39 "Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea" Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.
\s5
\v 40 Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.
\v 41 Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,
\v 42 kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na wibili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakisongama dhidi yake.
\s5
\v 43 Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,
\v 44 alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.
\s5
\v 45 Yesu akasema, "Nani ambaye kanigusa?" Walipokataa wote, Petro akasema, Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga."
\v 46 Lakini Yesu akasema, "Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu."
\s5
\v 47 Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.
\v 48 Kisha akasema kwake, "Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani."
\s5
\v 49 Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, "Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu."
\v 50 Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, "Usiogope. Amini tu, na ataokolewa."
\s5
\v 51 Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.
\v 52 Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, "Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu."
\v 53 Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.
\s5
\v 54 Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, "Mtoto, inuka"
\v 55 roho yake ikamrudia, na akainuka wakati huohuo. Akaamrisha kwamba, apewe kitu furani kwa ili ale.
\v 56 Wazazi wake wakashangaa, lakini aliwaamuru wasimwambie mtu kilichokuwa kimetokea.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa.
\v 2 Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
\s5
\v 3 Akawaambia, "Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala pesa wala msichukue kanzu mbili.
\v 4 Nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo.
\s5
\v 5 Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao".
\v 6 Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.
\s5
\v 7 Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababuu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu,
\v 8 na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena.
\v 9 Herode alisema, "nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake? Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu.
\s5
\v 10 Wakati waliporudi wale waliotumwa, wakamwamwambia kila kitu walicho fanya. Akawachukua pamoja naye, akaenda peke yake katika mji uitwao Bethsadia.
\v 11 Lakini makutano wakasikia kuhusu hili wakamfuata, na aliwakaribisha, na akaongea nao kuhusu ufalme wa Mungu, na aliwaponya wale waliohitaji uponyaji.
\s5
\v 12 Siku ikaanza kuisha, na wale kumi na wawili wakaenda kwake na kusema, "Watawanye makutano kwamba waende katika vijiji vya karibu na mijini wakatafute mapumziko na chakula, kwa sababu tupo eneo la nyikani."
\v 13 Lakini akawaambia, "Nyie wapeni kitu cha kula." Wakasema "Hatuna zaidi ya vipande vitano vya mikate na samaki wawili, isipokuwa tungeenda na kununua chakula kwa ajili ya kusanyiko hili la watu."
\v 14 Kulikua na wanaume wapatao elfu tano pale. Akawambia wanafunzi wake. "Wakalisheni chini katika makundi ya watu wapatao hamsini kwa kila kundi.
\s5
\v 15 Kwa hiyo wakafanya hivyo na watu wa wakaketi chini.
\v 16 Akachukua mikate mitano na samaki wawili na akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvimega katika vipande, akawapa wanafunzi wake ili waviweke mbele ya makutano.
\v 17 Wote wakala na wakashiba, na vipande vya chakula vilivyo baki viliokotwa na kujaza vikapu kumi na viwili.
\s5
\v 18 Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, "watu husema mimi ni nani?"
\v 19 Wakijibu, wakasema, "Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena."
\s5
\v 20 Akawambia, "Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?" Akijibu Petro akasema, "Kristo kutoka kwa Mungu."
\v 21 Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili,
\v 22 akasema kwamba mwana wa Adamu lazma ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.
\s5
\v 23 Akawambia wote, "kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate.
\v 24 Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa.
\v 25 Je kitamfaidia nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake?
\s5
\v 26 Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu.
\v 27 Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu."
\s5
\v 28 Ikatokea yapata siku nane baada ya Yesu kusema maneno haya kwamba akawachukua pamoja nae Petro, Yohana na, Yakobo, wakapanda mlimani kuomba.
\v 29 Na alipokuwa katika kuomba, muonekano wa uso wake ulibadilika, na mavazi yake yakawa meupe na ya kung'aa.
\s5
\v 30 Na tazama, walikuwepo wanaume wawili wakiongea naye! Walikuwa Musa na Elia,
\v 31 walionekana katika utukufu. Waliongea kuhusu kuondoka kwake, jambo ambalo alikaribia kulitimiza Yerusalem.
\s5
\v 32 Sasa Petro na wale waliokua pamoja naye walikuwa katika usingizi mzito. Lakini walipokuamka, waliuona utukufu wake na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja nae.
\v 33 Ikatokea kwamba, walipokuwa wakiondoka kwa Yesu, Petro akamwambia, "Bwana, ni vizuri kwetu kukaa hapa na inatupasa tutengeneze makazi ya watu watatu. Tutengeneze moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa, na moja kwa ajili ya Eliya." Hakuelewa alichokuwa akiongelea.
\s5
\v 34 Alipokuwa akisema hayo, likaja wingu na likawafunika; na waliogopa walipoona wamezunguwa na wamezungukwa na wingu.
\v 35 Sauti ikatoka kwenye wingu ikasema, "Huyu ni Mwanangu mteule. Msikilizeni yeye."
\v 36 Sauti iliponyamaza, Yesu alikuwa peke yake. walikaa kimya, na katika siku hizo hawakumwambia yeyote lolote miongoni mwa waliyoyaona.
\s5
\v 37 Siku iliyofuata, baada ya kutoka mlimani, kusanyiko kubwa la watu lilikutana naye.
\v 38 Tazama, mwanaume kutoka kwenye kusanyiko alilia kwa sauti, akisema, "Mwalimu ninakuomba umtazame mwanangu, kwa kuwa ni mwanangu wa pekee.
\v 39 Unaona roho chafu humshika, na mara hupiga kelele, na pia humfanya achanganyikiwe na kutokwa povu kinywani. Nayo humtoka kwa shida, ikimsababshia maumivu makali.
\v 40 Naliwasihi wanafunzi wako kuikea itoke. lakini hawakuweza."
\s5
\v 41 Yesu akajibu akasema, "Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka, mpaka lini nitkaa nanyi na kuchukuliana nanyi? Mlete mwanao hapa."
\v 42 Kijana aliokuwa anakuja, roho cha ikamuangusha chini na kumtikisa kwa fujo. Lakini Yesu aliikemea ile roho chafu, alimponya mvulana, na kamkabidhi kwa baba yake.
\s5
\v 43 Wote walishangazwa na ukuu wa Mungu. Lakini walipokuwa wakistaajabu wote kwa mambo yote aliyo yaliyotedeka, akasema kwa wanafunzi wake,
\v 44 "Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu."
\v 45 Lakni hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo.
\s5
\v 46 Kisha mgogoro ulianza ulizuka miongoni mwao i juu ya nani angekuwa mkuu.
\v 47 Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake,
\v 48 na akasema, " kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu"
\s5
\v 49 Yohana akajibu akasema, "Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi."
\v 50 Lakini Yesu akamwambia, "Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu"
\s5
\v 51 Ikatokea kwamba, kulinga na siku zilivyokua zikikaribia zsiku zake za kwenda mbinguni, kwa uimara alielekeza uso wake Yerusalemu.
\v 52 Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
\v 53 Lakini watu huko hawakumpokea, kwasababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu.
\s5
\v 54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, "Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?"
\v 55 Lakini aliwageukia akawakemea.
\v 56 Kisha walikwenda kijiji kingine.
\s5
\v 57 Walipokuwa wakienda katika njia yao, mtu mmoja akamwambia, "Nitakufuata popote uendapo."
\v 58 Yesu akamwambia, "Mbweha wanamashimo, ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pakulaza kichwa chake."
\s5
\v 59 Ndipo akamwambia mtu mwingine, "Nifuate." Lakini yeye akasema, "Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzika baba yangu,"
\v 60 Lakini yeye akamwambia, "Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu kila mahali."
\s5
\v 61 Pia mtu mwingine akasema. "Nitakufuata, Bwana, lakini niruhusu kwanza nikawaage walio katika nyumba yangu."
\v 62 Laki Yesu akamwambia hakuna mtu, atiaye mkono wake kulima na kuangalia nyuma atakayefaa kwa ufalme wa Mungu."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda.
\v 2 Akawaambia, "Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake.
\s5
\v 3 Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu.
\v 4 Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani.
\s5
\v 5 Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.'
\v 6 kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu.
\v 7 Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine.
\s5
\v 8 Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu,
\v 9 na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu'
\s5
\v 10 Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni,
\v 11 'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.'
\v 12 Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.
\s5
\v 13 Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, Wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu.
\v 14 Lakini itakuwa usitahamilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu.
\v 15 Wewe Kapernaumu, Unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu
\s5
\v 16 Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi anmtakaa aliyenituma"
\s5
\v 17 Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, "Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako."
\v 18 Yesu akawaambia, "Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
\v 19 Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
\v 20 Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni."
\s5
\v 21 Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, "Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako."
\s5
\v 22 "Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake."
\s5
\v 23 Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, "Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.
\v 24 Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia."
\s5
\v 25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, "Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?"
\v 26 Yesu akamwambia, "Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?"
\v 27 Akajibu akasema, "Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe."
\v 28 Yesu akasema, "Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi."
\s5
\v 29 Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, Akamwambia Yesu, "Na jirani yangu ni nani?"
\v 30 Yesu akijibu akasema, "Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu..
\s5
\v 31 Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
\v 32 Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.
\s5
\v 33 Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. alipomuona, alisukumwa kwa huruma.
\v 34 Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.
\v 35 Siku ilyofuata alichukua dinari mbili, na akampatia mmiliki wa nyumba ya wageni na kumwambia, 'Muhudumie na chochote cha ziada utakacho tumia, nitakulipa nitakaporudi.'
\s5
\v 36 Ni yupi kati ya hawa watatu, unafikiri, alikuwa ni jirani kwake yeye aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?"
\v 37 Mwalimu alisema, "Ni yule aliyeonesha huruma kwake." Yesu akamwambia, "Nenda na ukafanye vivyo hivyo"
\s5
\v 38 Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake.
\v 39 Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake.
\s5
\v 40 Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, "Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie."
\v 41 Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, "Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi,
\v 42 lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ilitokea wakati Yesu alipokuwa anaomba mahali fulani, mmoja wa mwanafunzi wake alimwambia, "Bwana, tufundishe sisi kuomba kama Yohana alivyo wafundisha wanafunzi wake'.
\s5
\v 2 Yesu akawaambia, Msalipo, semeni, 'Baba, Jina lako litakazwe. Ufalme wako uje.
\s5
\v 3 Utupe mkate wetu wa kila siku.
\v 4 Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe wote waliotukosea. Usituongoze katika majaribu."
\s5
\v 5 Yesu akawaambia, "Ni nani kwenu atakuwa na rafiki, ambaye atamuendea usiku, na kumwambia, Rafiki niazime mikate mitatu.
\v 6 Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.'
\v 7 Na yule aliyeko ndani akamjibu, usinitaabishe, Mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate.
\v 8 Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako.
\s5
\v 9 Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa.
\v 10 Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake.
\s5
\v 11 Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.?
\v 12 Au akimuomba yai atampa nge badala yake?.
\v 13 Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?"
\s5
\v 14 Baadaye, Yesu akawa anakemea pepo, na mtu mwenye pepo alikuwa bubu. Ikawa pepo lilipomtoka, mtu huyo aliweza kuongea. Umati wakastaajabu sana.
\v 15 Lakii watu wengine wakasema, huyu anaondo mapepo kwa Beelzebul, mkuu wa mapepo
\s5
\v 16 Wengine walimjaribu na kumtaka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
\v 17 Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao na kuwaambia, "Kila ufalme utakaogawanyika itakuwa ukiwa, na nyumba iliyo gawanyika itaanguka.
\s5
\v 18 Kama Shetani atakuwa amegawanyika, ufalme wake utasimamaje? Kwa sababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli
\v 19 Kama mimi natoa mapepo kwa Belzebuli, je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani? Kwa sababu hii, wao watawahukumu ninyi.
\v 20 Lakini, kama natoa mapepo kwa kidole cha Mungu, basi uflame wa Mungu umewajia.
\s5
\v 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha akilinda nyumba yake, vitu vyake vitakaa salama.
\v 22 Lakini akivamiwa na mtu mwenye nguvu zaidi, Yule mtu mwenye nguvu atamnyang'anya silaha zake, na kuzichukua mali zake zote.
\v 23 Yeye asiye pamoja nami yuko kinyume nami, na yeye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.
\s5
\v 24 Pepo mchafu amtokapo mtu, huenda na kutafuta mahali pasipo na maji ili ajipumzishe. Atakapokuwa amekosa, husema, 'nitarudi nilipotoka.
\v 25 Akirudi na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri.
\v 26 Hivyo huenda na kutafuta mapepo saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe na kuwaleta waje wakae mahali pale. Na hali ya mtu huyo huwa mbaya kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza."
\s5
\v 27 Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipasa sauti yake zaidi ya wote kwanye mkutano wa watu na kusema " Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya"
\v 28 Lakini yeye akasema, wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.
\s5
\v 29 Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema " Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona.
\v 30 Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki
\s5
\v 31 Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni.
\s5
\v 32 Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona.
\s5
\v 33 Hakuna Mtu yeyote, awashaye taa na kuiweka sehemu ya chini yenye giza isiyoonekana au chini ya kikapu, ila huwasha na kuweka juu ya kitu ili kila mtu aingiaye aweze kuona mwanga.
\v 34 Jicho lako ni taa ya mwili. Jicho lako likiwa zuri basi mwili wako wote utakuwa kwenye mwanga. Lakini jicho lako likiwa baya basi mwili wako wote utakuwa kwenye giza.
\v 35 Kwa hiyo, mjihadhari ili mwanga ulio ndani yenu usitiwe giza.
\v 36 Hivyo basi, kama mwili wako wote uko kwenye mwanga, na hakuna sehemu iliyo katika giza, basi mwili wako utakuwa sawa na taa iwakayo na kutoa mwanga kwenu."
\s5
\v 37 Alipomaliza kuongea, Farisayo alimwalika akale chakula nyumbani kwake, naye Yesu akaingia ndani na kuwa pamoja nao.
\v 38 Na Mafarisayo wakashangaa kwa jinsi ambavyo hakunawa kwanza kabla ya chakula cha jioni.
\s5
\v 39 Lakini Bwana akawaambia, "Ninyi Mafarisayo mnaosha nje ya vikombe na bakuli, lakini ndani yenu mmejaa tamaa na uovu.
\v 40 Ninyi watu msio na ufahamu, Je yeye aliyeumba nje hakuumba na ndani pia?
\v 41 Wapeni masikini yaliyo ndani, na mambo yote yatakuwa safi kwenu.
\s5
\v 42 Lakini ole wenu Mafarisayo, kwani mnatoa zaka ya mnanaa na mchicha na kila aina ya mboga ya bustani. Lakini mmeacha mambo ya haki na kumpenda Mungu. Ni muhimu zaidi kufanya yaliyo ya haki na kumpenda Mungu, bila kuacha kufanya na hayo mengine pia.
\s5
\v 43 Ole wenu Mafarisayo, kwa kuwa mnapenda kukaa katika viti vya mbele kwenye masinagogi na kuamkiwa kwa salamu za heshima sokoni.
\v 44 Ole wenu, kwani mnafanana na makaburi yasiyo na alama ambayo watu hutembea juu yake pasipokujua."
\s5
\v 45 Mwalimu mmoja wa sheria za Kiyahudi akamjibu na kumwambia, "Mwalimu, unachokisema kinatuudhi pia sisi."
\v 46 Yesu akasema, "Ole wenu, waalimu wa sheria! kwani mnawapa watu mizigo mikubwa wasiyoweza kuibeba, walakini ninyi hamgusi mizigo hiyo hata kwa moja ya vidole vyenu.
\s5
\v 47 Ole wenu, kwa sababu mnajenga na kuweka kumbukumbu kwenye makaburi ya manabii' ambao waliuwawa na mababu zenu.
\v 48 Hivyo ninyi mwashuhudia na kukubaliana na kazi walizozifanya mababu zenu, kwa sababu hakika waliwauwa manabii ambao mnajenga kumbukumbu katika makaburi yao.
\s5
\v 49 Kwa sababu hiyo pia, hekima ya Mungu inasema, 'Nitawatumia manabii na mitume nao watawatesa na kuwaua baadhi yao.
\v 50 Kizazi hiki kitawajibika kwa damu ya manabii waliouawa tangu kuanza kwa dunia,
\v 51 Kutoka damu ya Abeli hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa katikati ya madhabahu na patakatifu. Ndiyo, nawaambia ninyi, kizazi hiki kitawajibika.
\s5
\v 52 Ole wenu waalimu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu mmechukua funguo za ufahamu; nyie wenyewe hamuingii, na wale wanaotaka kuingia mnawazuia."
\s5
\v 53 Baada ya Yesu kuondoka pale, Waandishi na Mafarisayo walimpinga na kubishana naye juu ya mambo mengi.
\v 54 wakijaribu kumnsana kwa maneno yake.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, "Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki"
\s5
\v 2 Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana.
\v 3 Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
\s5
\v 4 Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,
\v 5 Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo.
\s5
\v 6 Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.
\v 7 Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
\s5
\v 8 Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
\v 9 Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
\v 10 Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
\s5
\v 11 Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
\v 12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo."
\s5
\v 13 Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, "Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu."
\v 14 Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu.?
\v 15 Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo."
\s5
\v 16 Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
\v 17 na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
\v 18 Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
\v 19 Nitaiambia nafsi yangu, "Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe."
\s5
\v 20 Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
\v 21 Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
\s5
\v 22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu__ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu __ya kuwa mtavaa nini
\v 23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
\s5
\v 24 Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
\v 25 Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
\v 26 Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?.
\s5
\v 27 Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
\v 28 Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
\s5
\v 29 Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
\v 30 Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
\s5
\v 31 Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
\v 32 msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
\s5
\v 33 Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa__hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
\v 34 Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
\s5
\v 35 Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
\v 36 na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
\s5
\v 37 Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
\v 38 Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
\s5
\v 39 Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
\v 40 Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
\s5
\v 41 Petro akasema, "Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu.?
\v 42 Bwana akawaambia, "Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
\v 43 Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
\v 44 Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
\s5
\v 45 Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, "bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
\v 46 bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu'
\s5
\v 47 Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
\v 48 Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
\s5
\v 49 Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka,
\v 50 Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika!
\s5
\v 51 Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
\v 52 Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.
\v 53 Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.
\s5
\v 54 Yesu akawa anawaambia makutano pia, "Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa,
\v 55 Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa.
\v 56 Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?
\s5
\v 57 Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?
\v 58 Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani.
\v 59 Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kwa wakataihuo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao.
\v 2 Yesu akajibu na kuwaambia, "Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo?
\v 3 Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo.
\s5
\v 4 Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu?
\v 5 Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia.
\s5
\v 6 Yesu aliwaambia mfano huu, "Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata.
\v 7 Akamwambia mtunza bustani, 'Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani ulete uharibifu wa ardhi?
\s5
\v 8 Mtunza bustani akajibu na kusema, 'uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake.
\v 9 Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate.!"'
\s5
\v 10 Sasa Yesu alikuwa akifundisha katika mojawapo ya Masinagogi wakati wa Sabato.
\v 11 Tazama, alikuwepo mama mmoja ambaye kwa miaka kumi na minane alikuwa na rohomchafu wa udhaifu, na yeye alikuwa amepinda na hana uwezo kabisa wa kusimama.
\s5
\v 12 Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, "Mama, umewekwa huru kutoka kwenye udhaifu wako."
\v 13 Akaweka mikono yake juu yake, na mara mwili wake akajinyoosha na akamtukuza Mungu.
\v 14 Lakini mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo mtawala akajibu akawambia makutano, "Kuna siku sita ambazo ni lazima kufanya kazi. Njoni kuponywa basi, si katika siku ya Sabato. '
\s5
\v 15 Bwana akamjibu na akasema, "wanafiki! Hakuna kila mmoja wenu kufungua punda wako au ng'ombe kutoka zizini na kuwaongoza kumpeleka kunywa siku ya Sabato?
\v 16 Hivyo pia binti wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga kwa miaka kumi na minane, je haikumpasa kifungo chake kisifunguliwe siku ya sabato?"
\s5
\v 17 Alipokuwa akisema maneno hayo, wale wote waliompinga waliona aibu, bali makutano wote wa wengine walishangilia kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyotenda.
\s5
\v 18 Yesu akasema, "Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini?
\v 19 Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake.
\s5
\v 20 Tena akasema, "Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?
\v 21 Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganyakwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka."
\s5
\v 22 Yesu alitembelea kila mji na kijiji njiani akielekea Yerusalemu na kuwafundisha.
\v 23 Mtu mmoja akauliza, "Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?" Hivyo akawaambia,
\v 24 "Jitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa sababu wengi watajaribu na hawataweza kuingia.
\s5
\v 25 Mara baada ya mmiliki wa nyumba kusimama na kufunga mlango, basi mtasimama nje na kupiga hodi mlangoni na kusema, Bwana, Bwana, tufungulie yeye atajibu na kuwaambia, siwajui ninyi wala mtokako.'
\v 26 Ndipo mtasema, Tulikula na kunywa mbele yako na wewe ulifundisha katika mitaa yetu."
\v 27 Lakini yeye atawajibu, `nawaambia, siwajui mtokako, ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!'
\s5
\v 28 Kutakuwa na kilio na kusaga meno wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka, Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mumetupwa nje.
\v 29 Watafika kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, na kupumzika katika meza ya chakula cha jioni katika ufalme wa Mungu.
\v 30 Na tambua hili, wa mwisho ni wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho."
\s5
\v 31 Muda mfupi baadaye, baadhi ya Mafarisayo walikuja na kumwambia, "Nenda na ondoka hapa kwa sababu Herode anataka kukuua."
\v 32 Yesu akasema, "Nendeni mkamwambie yule mbweha, `Tazama, ninawafukuza pepo na kufanya uponyaji leo na kesho, na siku ya tatu nitatimiza lengo langu.
\v 33 Katika hali yoyote, ni muhimu kwa ajili yangu kuendelea leo, kesho, na siku iliyofuata, kwa vile haikubaliki kumuua nabii mbali na Yerusalemu.
\s5
\v 34 Yerusalemu, Yerusalemu, nani anawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wenu kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini humkulitaka hili.
\v 35 Tazama, nyumba yako imetelekezwa. Nami nawaambia, hamuwezi kuniona hata mtakaposema 'Amebarikiwa huyo ajaye kwa jina la Bwana.'"
\s5
\c 14
\p
\v 1 Iltokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu.
\v 2 Tazama, pale mbele yake alikuwa mtu ambaye anasumbuliwa na uvimbe.
\v 3 Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, "Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?"
\s5
\v 4 Lakini wao walikuwa kimya, kwahiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake.
\v 5 Naye akawaambia, "Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe anatumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?"
\v 6 Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.
\s5
\v 7 Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia,
\v 8 "Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketi katika nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe.
\v 9 Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, "mpishe mtu huyu nafasi yako," na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho.
\s5
\v 10 Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, `Rafiki, nenda mbele zaidi." ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani.
\v 11 Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa. '
\s5
\v 12 Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
\s5
\v 13 Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu,
\v 14 na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki."
\s5
\v 15 Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwambia, "Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!"
\v 16 Lakini Yesu akamwambia, "Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi.
\v 17 Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, `'Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.'
\s5
\v 18 Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, 'Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.'
\v 19 Na mwingine akasema, `'Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.'
\v 20 Na mtu mwingine akasema, 'Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.'
\s5
\v 21 Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, `'Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu."
\v 22 Mtumimishi akasema, `Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.'
\s5
\v 23 Bwana akamwambia mtumishi, 'Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.
\v 24 Kwamaana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu. '
\s5
\v 25 Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,
\v 26 'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
\v 27 Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
\s5
\v 28 Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?
\v 29 Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki,
\v 30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.'
\s5
\v 31 Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
\v 32 Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani.
\v 33 Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
\s5
\v 34 Chumvi ni nzuri, lakini ikiwa Chumvi imepoteza ladha yake, jinsi gani inaweza kuwa chumvi tena?
\v 35 Haina matumizi kwa udongo au hata kwa mbolea. hutupwa mbali. Yeye aliye na masikio ya kusikia, na asikie."
\s5
\c 15
\p
\v 1 Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza.
\v 2 Mafarisayowaote na waandishi wakanung'unika wakisema, "Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao."
\s5
\v 3 Yesu akasema mfano huu kwao, akisema
\v 4 "Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
\v 5 Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.
\s5
\v 6 Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.'
\v 7 nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu
\s5
\v 8 Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?
\v 9 Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.
\v 10 Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye."
\s5
\v 11 Na Yesu akasema, "Mtu mmoja alikua na wana wawili
\v 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao.
\s5
\v 13 Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.
\v 14 Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.
\s5
\v 15 Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
\v 16 Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.
\s5
\v 17 Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema 'ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!
\v 18 Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, "Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.
\v 19 Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako."
\s5
\v 20 Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
\v 21 Yule mwana akamwambia, 'baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.'
\s5
\v 22 Yule baba aliwaambia watumishi wake, 'lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.
\v 23 Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.
\v 24 Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana wakaanza kushangilia.
\s5
\v 25 Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.
\v 26 Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini?
\v 27 Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.'
\s5
\v 28 Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi.
\v 29 Ila akamjibu babayake akisema, 'Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu.
\v 30 Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.
\s5
\v 31 Baba akamwambia, 'Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.
\v 32 Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana."
\s5
\c 16
\p
\v 1 Yesu aliwaambia tena wanafunzi wake, "Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyekuwa na meneja, na alitaarifiwa ya kwamba meneja huyu anatapanya mali zake.
\v 2 Hivyo tajiri akamwita, akamwambia, "Ni nini hii ninayo isikia juu yako? Toa hesabu ya umeneja wako, kwa kuwa huwezi kuwa meneja tena.'
\s5
\v 3 Yule meneja akasema moyoni mwake, Nifanye nini, maana bwana wangu ananiondolea kazi yangu ya umeneja? Sina nguvu za kulima, na kuomba naona haya.
\v 4 Najua nitakalotenda ili nitakapotolewa katika kazi yangu ya uwakili watu wanikaribishe nyumbani mwao.
\s5
\v 5 Hivyo wakili akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja akamwambia wa kwanza, 'unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?'
\v 6 Akasema vipimo mia moja vya mafuta akamwambia 'chukua hati yako keti upesi andika hamsini.'
\v 7 kisha akamwambia mwingine na wewe unadaiwa kiasi gani?' akasema 'vipimo mia moja vya unga vya ngano.' Akamwambia 'twaa hati yako andika themanini.'
\s5
\v 8 Yule bwana akamsifu meneja dhalimu kwa vile alivyotenda kwa wereu. Kwakua watoto wa ulimwengu huu ni werevu nyingi na hushughulika kwa ujanja na watu wa upande wao kuliko walivyo watoto wa nuru.
\v 9 Nami nawaambia jifanyieni marafiki kwa mali ya udhalimu ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
\s5
\v 10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia. na aliye dhalimu katika lililo dogo huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
\v 11 Kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu ni nani atakayewaamini katika mali ya kweli?
\v 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika kutumia mali ya mtu mwingine ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
\s5
\v 13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwamaana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali."
\s5
\v 14 Basi Mafarisayo, ambao walikuwa wanapenda fedha waliyasikia haya yote na wakamdhihaki.
\v 15 Na akawaambia, "Ninyi ndiyo mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.
\s5
\v 16 Sheria na manabii vilikuwapo mpaka Yohana alivyokuja. Tangu wakati huo, habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujaribu kujiingiza kwa nguvu.
\v 17 Lakini ni rahisi kwa mbingu na nchi vitoweke kuliko hata herufi moja ya sheria ikosekane.
\s5
\v 18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini, naye amwooaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.
\s5
\v 19 Palikua na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi na alikua akifurahia kila siku utajiri wake mkubwa.
\v 20 Na maskini mmoja jina lake Lazaro aliwekwa getini pake, na ana vidonda.
\v 21 Naye alikua akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.
\s5
\v 22 Ikawa yule maskini alikufa na akachukuliwa na Malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa akazikwa.
\v 23 Na kule kuzimu alipokua katika mateso aliyainua macho yake akamuona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake.
\s5
\v 24 Akalia akasema, 'Baba Ibrahimu, nihurumue umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
\s5
\v 25 Lakini Ibrahimu akasema, 'Mwanangu kumbuka ya kwamba katika maisha yako uliyapokea mambo yako mema, na Lazaro vivyo alipata mabaya. Ila sasa yupo hapa anafarijiwa na wewe unaumizwa.
\v 26 Na zaidi ya hayo, kumewekwa shimo kubwa na refu kati yetu, ili wale wanaotaka kutoka huku kwenda kwenu wasiweze wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'
\s5
\v 27 Yule tajiri akasema, 'Nakuomba Baba Ibrahimu, kwamba umtume nyumbani kwa baba yangu
\v 28 kwa kuwa ninao ndugu watano ili awaonye, kwa hofu kwamba wao pia watkuja mahali hapa pa mateso. '
\s5
\v 29 Lakini Ibrahimu akasema, 'Wanao Musa na manabii. Waache wawasikilize wao.
\v 30 Yule tajiri akasema, 'hapana, Baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu watatubu.'
\v 31 Lakini Ibrahimu akamwambia, 'wasipowasikia Musa na manabii hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, "mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, Lakini ole wake mtu anayeyasababisha!
\v 2 Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.
\s5
\v 3 Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe.
\v 4 Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, 'ninatubu,' msamehe!"
\s5
\v 5 Mitume wake wakamwambia Bwana, "tuongezee imani yetu."
\v 6 Bwana akasema, "kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, 'n'goka na ukaote baharini,' nao ungewatii.
\s5
\v 7 Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, 'Njoo haraka na keti ule chakula?
\v 8 Je hatamwambia, 'Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa?
\s5
\v 9 Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa?
\v 10 Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni 'Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.'
\s5
\v 11 Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya.
\v 12 Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali
\v 13 wakapaza sauti wakasema "Yesu, Bwana tuhurumie."
\s5
\v 14 Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." nao walipokua wakienda wakatakasika.
\v 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu.
\v 16 Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.
\s5
\v 17 Yesu akajibu, akasema, "Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?
\v 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?"
\v 19 Akamwambia, "Inuka na uende zako imani yako imekuponya."
\s5
\v 20 Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, "Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana.
\v 21 Wala watu hawatasema, 'Angalia hapa!' au, 'Angalia kule!' kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu."
\s5
\v 22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona.
\v 23 Watawaambia, 'Angalia, kule! Angalia, hapa!' Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata,
\v 24 kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake.
\s5
\v 25 Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.
\v 26 Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokua katika siku ya Mwana wa Adam.
\v 27 Walikula, walikunywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile ambayo Nuhu alipoingia katika safina na gharika ikaja na kuwaangamiza wote.
\s5
\v 28 Ndivyo ilivyokua katika siku za Lutu, walikula, kunywa, wakinunua na kuuza, kulima na walijenga.
\v 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ikawaangamiza wote.
\s5
\v 30 Hivyo ndivyo itakavyo kuwa siku ile ya Mwana wa Adamu atakapofunuliwa.
\v 31 Siku hiyo, usimruhusu aliye kwenye dari ya nyumba ashuke kuchukue bidhaa zake ndani ya nyumba. Na usimruhusu aliyeko shambani kurudi nyumbani.
\s5
\v 32 Mkumbuke mke wa Lutu.
\v 33 Ye yote anaejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.
\s5
\v 34 Nakwambia, usiku huo kutakua na watu wawili katika kitanda kimoja. Mmoja atachukuliwa, na mwingine ataachwa.
\v 35 Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."
\v 36
\s5
\v 37 Wakamwuliza, "Wapi, Mungu?" Akawaambia, "Pale ulipo mzoga, ndipo tai hukusanyika kwa pamoja."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Kisha akawaambia mfano wa namna wanavyopaswa kuomba daima, na wasikate tamaa.
\v 2 akaisema, 'Kulikuwa na hakimu katika mji fulani, ambaye hakuwa anamwogopa Mungu na hakuwaheshimu watu.
\s5
\v 3 Kulikuwa na mjane katika jiji hilo, naye alimwendea mara nyingi, akisema, 'Nisaidie kupata haki dhidi ya mpinzani wangu.'
\v 4 Kwa muda mrefu hakuwa tayari kumsaidia, lakini baada ya muda akasema moyoni mwake, `Ingawa mimi simwogopi Mungu au kuheshimu mtu,
\v 5 lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua nitamsaidia kupata haki yake, ili asije akanichosha kwa kunijia mara kwa mara. ''
\s5
\v 6 Kisha Bwana akasema, 'Sikiliza alivyosema huyo hakimu dhalimu.
\v 7 Je Mungu pia hataleta haki kwa wateule wake ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, yeye hatakuwa mvumilivu kwao?
\v 8 Nawaambia kwamba ataleta haki kwao upesi. Lakini wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atakuta imani duniani? '
\s5
\v 9 Ndipo akawaambia mfano huu kwa baadhi ya watu ambao wanajiona wenyewe kuwa wenye haki na kuwadharau watu wengine,
\v 10 'Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo mwingine mtoza ushuru.
\s5
\v 11 Farisayo akasimama akaomba mambo haya juu yake mwenyewe, 'Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang'anyi, watu wasio waadilifu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru.
\v 12 Nafunga mara mbili kila wiki. Natoa zaka katika mapato yote ninayopata. '
\s5
\v 13 Lakini yule mtoza ushuru, alisimama mbali, bila hakuweza hata kuinua macho yake mbinguni, akagonga kifua chake akisema, 'Mungu, nirehemu mimi mwenye dhambi.'
\v 14 Nawaambia, mtu huyu alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki kuliko yule mwingine, kwa sababu kila ajikwezaye atashushwa, lakini kila mtu anayejinyenyekeza atainuliwa. '
\s5
\v 15 Watu walimletea watoto wao wachanga, ili aweze kuwagusa, lakini wanafunzi wake walipoona hayo, wakawazuia.
\v 16 Lakini Yesu akawaita kwake akisema, 'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie. Maana ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao.
\v 17 Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto ni dhahiri hatauingia. '
\s5
\v 18 Mtawala mmoja akamwuliza, akisema, 'Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?'
\v 19 Yesu akamwambia, 'Kwa nini unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema, ila Mungu peke yake.
\v 20 Unazijua amri- usizini, usiue, Usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.
\v 21 Yule mtawala akasema, 'Mambo haya yote nimeyashika tangu nilipokuwa kijana.'
\s5
\v 22 Yesu alipoyasikia hayo akamwambia, '"Umepungukiwa jambo moja. Lazima uuze vyote ulivyonavyo na uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni -kisha njoo, unifuate. '
\v 23 Lakini tajiri aliposikia hayo, alihuzunika sana, kwa sababu alikuwa tajiri sana.
\s5
\v 24 Kisha Yesu, akamwona alivyohuzunika sana akasema, 'Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
\v 25 Maana ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu. '
\s5
\v 26 Wale waliosikia hayo, wakasema, 'Nani basi, atakayeweza kuokolewa?'
\v 27 Yesu akajibu, 'Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana."
\s5
\v 28 Petro akasema, 'Naam, sisi tumeacha kila kitu na tumekufuata wewe. '
\v 29 Kisha Yesu akawaambia, Amin, nawaambia kwamba hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto, kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
\v 30 ambaye hatapokea mengi zaidi katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao, uzima wa milele. '
\s5
\v 31 Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawibili, akawaambia, 'Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa.
\v 32 Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate.
\v 33 Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka. '
\s5
\v 34 Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.
\s5
\v 35 Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada,
\v 36 aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza nini kinatokea.
\v 37 Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita.
\s5
\v 38 Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, 'Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.'
\v 39 wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, 'Mwana wa Daudi, unirehemu.
\s5
\v 40 Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza,
\v 41 'Unataka nikufanyie nini?' Akasema, 'Bwana, nataka kuona.'
\s5
\v 42 Yesu akamwambia, 'Upate kuona. Imani yako imekuponya. '
\v 43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko.
\v 2 Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
\s5
\v 3 Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo.
\v 4 Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.
\s5
\v 5 Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, 'Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.'
\v 6 Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha.
\v 7 Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, 'Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.'
\s5
\v 8 Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne. '
\v 9 Yesu akamwambia, 'Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.
\v 10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea. '
\s5
\v 11 Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.
\v 12 Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.
\s5
\v 13 Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.'
\v 14 Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.'
\v 15 Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.
\s5
\v 16 Wa kwanza akaja, akasema, `Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. '
\v 17 Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. '
\s5
\v 18 Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.'
\v 19 Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.'
\s5
\v 20 Na mwingine akaja, akasema, `Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,
\v 21 kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. '
\s5
\v 22 Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
\v 23 Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
\s5
\v 24 Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.'
\v 25 Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi. '
\s5
\v 26 'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
\v 27 Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. ''
\s5
\v 28 Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
\s5
\v 29 Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
\v 30 akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
\v 31 Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua? ' Semeni, "Bwana anamhitaji. ''
\s5
\v 32 Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
\v 33 Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'
\v 34 Wakasema, `Bwana anamhitaji. '
\v 35 Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
\v 36 Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
\s5
\v 37 Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,
\v 38 wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!'
\s5
\v 39 Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. '
\v 40 Yesu akajibu, akasema, `Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. '
\s5
\v 41 Yesu alipoukaribia mji aliulilia,
\v 42 akisema, laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
\s5
\v 43 Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande.
\v 44 Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa'.
\s5
\v 45 Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,
\v 46 akiwaambia, "Imeandikwa, 'Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,' lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi".
\s5
\v 47 Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,
\v 48 lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walimwendea pamoja na wazee.
\v 2 Walizungumza, wakimwambia, 'Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya? "
\s5
\v 3 Naye akajibu, akawaambia, 'Nami pia nitawauliza swali. Niambieni
\v 4 ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu? '
\s5
\v 5 Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, 'Tukisema, `litoka mbinguni, atatuuliza, ` Basi, mbona hamkumwamini?'
\v 6 Na tukisema; ilitoka kwa wanadamu; watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii. '
\s5
\v 7 Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka.
\v 8 Yesu akawaambia, '"Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya."
\s5
\v 9 Aliwaambia watu mfano huu, "Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.
\v 10 Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.
\s5
\v 11 Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.
\v 12 Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.
\s5
\v 13 Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu. '
\v 14 Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, `Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu. '
\s5
\v 15 Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?
\v 16 Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine". 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa'
\s5
\v 17 Lakini Yesu akawatazama, akasema, "Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'?
\v 18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda. '
\s5
\v 19 Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
\v 20 Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
\s5
\v 21 Nao wakamwuliza, wakisema, "Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
\v 22 Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?"
\s5
\v 23 Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
\v 24 "Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?" Walisema, ' "Ya Kaisari."
\s5
\v 25 Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
\v 26 Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
\s5
\v 27 Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
\v 28 wakamwuliza, wakisema, "Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
\s5
\v 29 Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
\v 30 na wa pili pia.
\v 31 Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
\v 32 Baadaye yule mwanamke pia akafa.
\v 33 Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa. '
\s5
\v 34 Yesu akawaambia, "Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.
\v 35 Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.
\v 36 Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.
\s5
\v 37 Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
\v 38 Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake. "
\s5
\v 39 Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema. '
\v 40 Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
\s5
\v 41 Yesu akawaambia, "Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
\v 42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
\v 43 mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako. '
\v 44 Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?"
\s5
\v 45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,
\v 46 'Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na wapenda salamu maalum sokoni na viti vya heshima katika masinagogi, na maeneo ya heshima karamuni.
\v 47 Wao pia hula nyumba za wajane, na wanajifanya wanasali sala ndefu. Hawa watapokea hukumu kubwa zaidi. '
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina.
\v 2 Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili.
\v 3 Hivyo akasema, "Kweli nawaambieni, huyu Mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote.
\v 4 Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake."
\s5
\v 5 Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema,
\v 6 "Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa."
\s5
\v 7 Hivyo wakamuuliza, wakasema, "Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?"
\v 8 Yesu akajibu, "Muwe waangalifu kwamba msidanganywe. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, 'Mimi ndiye, 'na 'Muda umekaribia'. Msiwafuate.
\v 9 Mkisikia vita na vuruguvurugu msiogope, kwa sababu haya mambo lazima yatokee kwanza, lakini mwisho hautatokea upesi."
\s5
\v 10 Kisha akawaambia, "Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine.
\v 11 Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni.
\s5
\v 12 Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu.
\v 13 Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu.
\s5
\v 14 Kwahiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema,
\v 15 kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana.
\s5
\v 16 Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.
\v 17 Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu.
\v 18 Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
\v 19 Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.
\s5
\v 20 Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.
\v 21 Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia.
\v 22 Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika.
\s5
\v 23 Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa.
\v 24 Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.
\s5
\v 25 Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.
\v 26 Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
\s5
\v 27 Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.
\v 28 Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu."
\s5
\v 29 Yesu akawaambia kwa mfano, "Uangalieni mtini, na miti yote.
\v 30 Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.
\v 31 Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
\s5
\v 32 Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.
\v 33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\s5
\v 34 Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla
\v 35 kama mtego. Kwasababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima.
\s5
\v 36 Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu."
\s5
\v 37 Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.
\v 38 Watu wote walimjia asubuhi na mapemaili kumsikiliza ndani ya hekalu.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Basi Sikukuu ya Mkate Usiyotiwa Chachu ilikuwa imekaribia, ambayo inaitwa Pasaka.
\v 2 Makuhani wakuu na waandishi wakajadiliana namna ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu.
\s5
\v 3 Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na mbili.
\v 4 Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao.
\s5
\v 5 Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha.
\v 6 Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu.
\s5
\v 7 Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe.
\v 8 Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, "Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile."
\v 9 Wakamuuliza, "Wapi unataka tuyafanyie hayo maandalizi?"
\s5
\v 10 Akawajibu, "Sikilizeni, mtakapokuwa mmeingia mjini, mwanamume ambaye amebeba mtungi wa maji atakutana na ninyi. Mfuateni kwenye nyumba ambayo ataingia.
\v 11 Kisha mwambieni bwana wa nyumba, "Mwalimu anakwambia, "Kiko wapi chumba cha wageni, mahali ambapo nitakula Pasaka na wanafunzi wangu?"
\s5
\v 12 Atawaonyesha chumba cha ghorofani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi humo."
\v 13 Hivyo wakaenda, na wakakuta kila kitu kama alivyowaambia. Kisha wakaandaa chakula cha Pasaka.
\s5
\v 14 Muda ulipofika alikaa na wale mitume.
\v 15 Kisha akawaambia, "Nina shauku kubwa ya kula sikukuu hii ya Pasaka na ninyi kabla ya kuteswa kwangu.
\v 16 Kwa maana nawaambieni, sitakula tena mpaka itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu."
\s5
\v 17 Kisha Yesu akachukua kikombe, na alipokwisha kushukuru, akasema, "Chukueni hiki, na mgawane ninyi kwa ninyi.
\v 18 Kwa maana nawaambia, sitakunywa tena mzao wa mzabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja."
\s5
\v 19 Kisha akachukua mkate, na alipokwisha kushukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, "Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi."
\v 20 Akachukua kikombe vivyo hivyo baada ya chakula cha usiku akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, ambayo imemwagika kwa ajili yenu.
\s5
\v 21 Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.
\v 22 Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!"
\v 23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili.
\s5
\v 24 Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote.
\v 25 Akawaambia, "Wafalme wa watu wa mataifa wana ubwana juu yao, na wale mwenye mamlaka juu yao wanaitwa waheshimiwa watawala.
\s5
\v 26 Lakini haitakiwi kabisa kuwa hivi kwenu ninyi. Badala yake, acha yule ambaye ni mkubwa kati yenu awe kama mdogo. Na yule ambaye ni wa muhimu sana awe kama atumikaye.
\v 27 Kwa sababu yupi mkubwa, yule akaaye mezani au yule anayetumika? Je si yule aketie mezani? Na mimi bado ni kati yenu kama atumikaye.
\s5
\v 28 Lakini ninyi ndio ambao mmeendelea kuwa nami katika majaribu yangu.
\v 29 Nawapa ninyi ufalme, kama vile Baba alivyonipa mimi ufalme,
\v 30 kwamba mpate kula na kunywa mezani kwangu kwenye ufalme wangu. Na mtakaa kwenye viti vya enzi mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israel.
\s5
\v 31 Simoni, Simoni, fahamu kwamba, Shetani ameomba awapate ili awapepete kama ngano.
\v 32 Lakini nimekuombea, kwamba imani yako isishindwe. Baada ya kuwa umerudi tena, waimarishe ndugu zako."
\s5
\v 33 Petro akamwambia, "Bwana, niko tayari kwenda na wewe gerezani na hata katika mauti."
\v 34 Yesu akajibu, "Nakwambia, Petro, Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua."
\s5
\v 35 Kisha Yesu akawaambia, "Nilipowapeleka ninyi bila mfuko, kikapu cha vyakula, ua viatu, je mlipungukiwa na kitu?" Wakajibu "Hakuna."
\v 36 Kisha akawaambia, "Lakini sasa, kila mwenye mfuko, na auchukue pamoja na kikapu cha vyakula. Yule ambaye hana upanga imempasa auze joho lake anunue mmoja.
\s5
\v 37 Kwa sababu nawaambia, yote ambayo yameandikwa kwa ajili yangu lazima yatimilike, 'Na alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati.' Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu kinatimizwa."
\v 38 Kisha wakasema, "Bwana, tazama! Hizi hapa panga mbili." Na akawaambia"yatosha."
\s5
\v 39 Baada ya chakula cha usiku, Yesu aliondoka, kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara, akaenda mlima wa Mzeituni, na wanafunzi wakamfuata.
\v 40 Walipofika, aliwaambia, "Ombeni kwamba msiingie majaribuni."
\s5
\v 41 Akaenda mbali na wao kama mrusho wa jiwe, akapiga magoti akaomba,
\v 42 akisema, "Baba, kama unataka, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nitakavyo mimi, lakini mapenzi yako yafanyike."
\s5
\v 43 Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.
\v 44 Akiwa katika kuugua, akaomba kwa dhati zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yakidondoka chini.
\s5
\v 45 Wakati alipoamka kutoka katika maombi yake, alikuja kwa wanafunzi, na akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni yao,
\v 46 na akawauliza, "Kwanini mnalala? Amkeni muombe, kwamba msiingie majaribuni."
\s5
\v 47 Wakati alipokuwa bado akiongea, tazama, kundi kubwa la watu likatokea, na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili akiwaongoza. Akaja karibu na Yesu ili ambusu,
\v 48 lakini Yesu akamwambia, "Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?"
\s5
\v 49 Wakati wale waliokuwa karibu na Yesu walipoona hayo yanayotokea, wakasema, "Bwana, je tuwapige kwa upanga?"
\v 50 Kisha mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
\v 51 Yesu akasema, "hii inatosha. Na akagusa sikio lake, akamponya.
\s5
\v 52 Yesu akasema kwa kuhani mkuu, na kwa wakuu wa hekalu, na kwa wazee waliokuja kinyume chake, "Je mnakuja kana kwamba mnakuja kupambana na mnyang'anyi, na marungu na mapanga?
\v 53 Nilipokuwa pamoja nanyi siku zote kwenye hekalu, hamkuweka mikono yenu juu yangu. Lakini hii ni saa yako, na mamlaka ya giza."
\s5
\v 54 Wakamkamata, wakamuongoza, wakamleta nyumbani mwa kuhani mkuu. Lakini Petro akamfuatilia kwa mbali.
\v 55 Baada ya kuwa wamewasha moto katika ule uwanda wa ndani na walipokwisha kukaa chini pamoja, Petro akakaa katikati yao.
\s5
\v 56 Mtumishi mmoja wa kike akamuona Petro alipokuwa amekaa katika mwanga utokanao na moto, akamtazama akamwambia, "Huyu mtu pia alikuwa pamoja naye."
\v 57 Lakini Petro akakana, akasema, "mwanamke, mimi simjui."
\v 58 Baada ya muda kidogo, mtu mwingine akamuona akasema "Wewe pia ni mmoja wao". Lakini Petro akajibu, "Mwanaume, mimi siyo."
\s5
\v 59 Baada ya kama saa moja hivi, mwanaume mmoja akasisitiza akasema, "Kweli kabisa huyu mtu pia alikuwa pamoja naye, maana ni Mgalilaya."
\v 60 Lakini Petro akasema, "Mwanaume, sijui usemalo." Na mara, wakati akiongea, jogoo akawika.
\s5
\v 61 Akageuka, Bwana akamtazama Petro. Na Petro akalikumbuka neno la Bwana, pale alipomwambia, "Kabla ya jogoo kuwika leo, utanikana mimi mara tatu."
\v 62 Akienda nje, Petro akalia kwa uchungu mwingi.
\s5
\v 63 Kisha wale wanaume waliokuwa wakimlinda Yesu, wakamdhihaki na kumpiga.
\v 64 Baada ya kumfunika macho, wakamuuliza, wakisema, "Tabiri! Ni nani aliyekupiga?"
\v 65 Wakaongea mambo mengine mengi kinyume cha Yesu na kumkufuru yeye.
\s5
\v 66 Mara ilipokuwa asubuhi, wazee wa watu walikusanyika pamoja, wakuu wa makuhani na waandishi. Wakampeleka kwenye Baraza,
\v 67 wakisema, "Kama wewe ni Kristo, tuambie." Lakini yeye akawaambia, "Kama nikiwaambia, hamtaniamini,
\v 68 na kama nikiwauliza hamtanijibu."
\s5
\v 69 Lakini kuanzia sasa na kuendelea, Mwana wa Adamu atakuwa amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu."
\v 70 Wote wakasema, "Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?" Na Yesu akawaambia, "Ninyi mmesema mimi ndiye."
\v 71 Wakasema, "Kwa nini bado tunahitaji tena ushahidi? Kwa sababu sisi wenyewe tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Mkutano wote wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.
\v 2 Wakaanza kumshutumu, wakisema, "Tumemkuta mtu huyu akipotosha taifa letu, kwa kukataza tusitoe kodi kwa Kaisari, na akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, Mfalme."
\s5
\v 3 Pilato akamuuliza, akisema, "Je wewe ni Mfalme wa Wayahudi?" Na Yesu akamjibu akisema, "Wewe wasema hivyo".
\v 4 Pilato akamuambia kuhani mkuu na makutano, "Sioni kosa kwa mtu huyu".
\v 5 Lakini wao wakasisitiza, wakisema, " Amekuwa akiwachochea watu, akifundisha katika Uyahudi yote, kuanzia Galilaya na sasa yuko hapa."
\s5
\v 6 Pilato aliposikia haya, akaulizia kama mtu huyo ni wa Galilaya?
\v 7 Alipotambua kuwa alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka Yesu kwa Herode, ambaye naye alikuwa Yerusalemu kwa siku hizo.
\s5
\v 8 Herode alipomuona Yesu, alifurahi sana kwasababu alitaka kumuona kwa siku nyingi. Alisikia habari zake na alitamani kuona moja ya miujiza ikifanywa na yeye.
\v 9 Herode alimhoji Yesu kwa maneno mengi, lakini Yesu hakumjibu chochote.
\v 10 Makuhani wakuu pamoja na waandishi walisimama kwa ukali wakimshitaki.
\s5
\v 11 Herode pamoja na maaskari wake, walimtukana na kumdhihaki, na kumvika mavazi mazuri, kisha akamrudisha Yesu kwa Pilato.
\v 12 Herode na Pilato wakawa marafiki kuanzia siku hiyo, (kabla ya hapo walikuwa maadui).
\s5
\v 13 Pilato akawaita pomoja makuhani wakuu na watawala na umati wa watu,
\v 14 Akawaambia, "Mmeniletea mtu huyu kama mtu anaye waongoza watu wafanye mabaya, na tazama, baada ya kuwa nimemhoji mbele yenu, sikuona kosa kwa mtu huyu kuhusu mambo yote ambayo ninyi mnamshitaki yeye.
\s5
\v 15 Hapana, wala Herode, kwa maana amemrudisha kwetu, na tazama hakuna chochote alichokifanya kinachostahili adhabu ya kifo.
\v 16 Kwahiyo basi nitamuadhibu na kumuachilia.
\v 17 (Sasa, Pilato anawajibika kumuachilia mfungwa mmoja kwa wayahudi wakati wa sikukuu).
\s5
\v 18 Lakini wote wakapiga kelele pamoja, wakisema, "Mwondoe huyo, na tufungulie Baraba!"
\v 19 Baraba alikuwa ni mtu ambaye amewekwa gerezani kwa sababu ya uasi fulani katika jiji na kwa kuua.
\s5
\v 20 Pilato akawaambia tena, akitamani kumwachilia Yesu.
\v 21 Lakini wao wakapiga kelele, wakisema, "Msulibishe, msulibishe."
\v 22 Akawauliza kwa mara ya tatu, "kwa nini, huyu mtu amefanya maovu gani? Sikupata kosa linalostahili adhabu ya kifo kwake. Kwahiyo nitakapo maliza kumuadhibu nitamuachilia."
\s5
\v 23 Lakini wakasisitiza kwa sauti ya juu, wakitaka asulubiwe. Na sauti zao zikamshawishi Pilato.
\v 24 Hivyo Pilato akaamua kuwapatia matakwa yao.
\v 25 Akamuachilia yule waliyemtaka ambaye alifungwa kwa kusababisha ghasia na kuua. Lakini akamtoa Yesu kwa matakwa yao.
\s5
\v 26 Walipokuwa wakimpeleka, walimkamata mtu mmoja aitwaye Simoni wa Ukirene, akitokea katika nchi, wakamtwika msalaba ili abebe, akimfuata Yesu.
\s5
\v 27 umati mkubwa wa watu, na wanawake ambao walihuzunika na kuomboleza kwa ajili yake, walikuwa wakimfuata.
\v 28 Lakini akawageukia, Yesu akawaambia, 'Mabinti wa Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe na kwa ya ajili watoto wenu.
\s5
\v 29 Tazama, siku zinakuja ambazo watasema, "Wamebarikiwa walio tasa na matumbo yasiyozaa, na matiti ambayo hayakunyonyesha.
\v 30 Ndipo watakapo anza kuiambia milima, 'Tuangukieni,' na vilima, 'Mtufunike.'
\v 31 Maana kama wakifanya mambo haya ikiwa mti mbichi, itakuwaje ukiwa mkavu?"
\s5
\v 32 wanaume wengine, wahalifu wawili, walipelekwa pamoja naye ili wauwawe.
\s5
\v 33 Walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo wakamsulubisha pamoja na wale wahalifu, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
\v 34 Yesu alisema, "Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. "Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.
\s5
\v 35 Watu walikuwa wamesimama wakiangalia huku watawala wakimdhihaki, wakisema, "Aliwaokoa wengine. Sasa ajiokoe mwenyewe, kama yeye ni Kristo wa Mungu, mteule".
\s5
\v 36 Askari pia walimdharau, walimkaribia yeye na wakumpa siki,
\v 37 wakisema, "Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi jiokoe mwenyewe"
\v 38 Kulikuwa pia na alama juu yake iliyoandikwa "HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI."
\s5
\v 39 Mmoja wa wahalifu aliyesulubishwa alimtukana akisema, "Wewe si Kristo? jiokoe mwenyewe na sisi"
\v 40 Lakini yule mwingine akajibu, akimkemea na akisema, "Je wewe humuogopi Mungu, nawe uko katika hukumu hiyo hiyo?
\v 41 Sisi tupo hapa kwa haki, kwa maana sisi tunapokea kile tunachostahili kwa matendo yetu. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya."
\s5
\v 42 Na aliongeza, "Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako."
\v 43 Yesu akamwambia, "Amini nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso."
\s5
\v 44 Hapo ilikuwa karibu saa ya sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa ya tisa,
\v 45 Mwanga wa jua ulizimika. Kisha pazia la hekalu likagawanyika katikati kuanzia juu.
\s5
\v 46 Akilia kwa sauti kuu, Yesu alisema, "Baba mikononi mwako naiweka roho yangu," baada ya kusema haya, akafa.
\v 47 Wakati Akida alipoona yaliyotendeka alimtukuza Mungu akisema, "Hakika huyu alikuwa mtu mwenye haki."
\s5
\v 48 Wakati umati wa watu waliokuja pamoja kushuhudia walipoona mambo yaliyofanyika, walirudi huku wakipiga vifua vyao.
\v 49 Lakini marafiki zake, na wanawake waliomfuata toka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiangalia hayo mambo.
\s5
\v 50 Tazama, palikuwepo na mtu aitwaye Yusufu, ambaye ni mmoja wa baraza, mtu mzuri na mwenye haki,
\v 51 (alikuwa hajakubaliana na maamuzi au matendo yao), kutoka Armathaya, mji wa Kiyahudi, ambao ulikua ukisubiria ufalme wa Mungu.
\s5
\v 52 Mtu huyu, alimkaribia Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
\v 53 Alimshusha, na akauzungushia sanda, na akaumweka katika kaburi lililokuwa limechongwa katika jiwe, ambalo hakuna aliyewahi kuzikwa.
\s5
\v 54 Ilikuwa ni siku ya maandalizi, na Sabato inakaribia.
\v 55 Wanawake, waliokuja nao kutoka Galilaya, walimfuata, na wakaona kaburi na jinsi mwili wake ulivyolazwa.
\v 56 Walirudi na kuanza kuandaa manukato na marashi. Kisha siku ya sabato walipumzika kwa mujibu wa sheria.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa.
\v 2 Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi.
\v 3 Wakaingia ndani, lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu.
\s5
\v 4 Ilitokea kwamba, wakati wamechanganyikiwa kuhusu hili, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi ya kung'aa.
\v 5 Wanawake wakiwa wamejaa hofu na wakiinamisha nyuso zao chini, wakawaambia wanawake, "Kwanini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu?
\s5
\v 6 Hayupo hapa, ila amefufuka! Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa angali Galilaya,
\v 7 akisema kwamba Mwana wa Adamu lazima atolewe kwenye mikono ya watu wenye dhambi na asulubishwe, na siku ya tatu, afufuke tena."
\s5
\v 8 Wale wanawake wakakumbuka maneno yake,
\v 9 na wakarudi kutoka kaburini na wakawaambia mambo haya yote wale kumi na moja na wengine wote.
\v 10 Basi Maria Magdalena, Joana, Maria mama wa Yakobo, na wanawake wengine pamoja nao wakatoa taarifa hizi kwa mitume.
\s5
\v 11 Lakini ujumbe huu ukaonekana kama mzaha tu kwa mitume, na hawakuwaamini wale wanawake.
\v 12 Hata hivyo Petro aliamka, na akakimbia kuelekea kaburini, na akichungulia na kuangalia ndani, aliona sanda peke yake. Petro kisha akaondoka akaenda nyumbani kwake, akistaajabu nini ambacho kimetokea.
\s5
\v 13 Na tazama, wawili miongoni mwao walikuwa wakienda siku hiyo hiyo katika kijiji kimoja kiitwacho Emmau, ambacho kilikuwa maili sitini kutoka Yerusalemu.
\v 14 Wakajadiliana wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotokea.
\s5
\v 15 Ikatokea kwamba, wakati walipokuwa wakijadiliana na kuulizana maswali, Yesu akasogea karibu akaambatana nao.
\v 16 Lakini macho yao yalizuiliwa katika kumtambua yeye.
\s5
\v 17 Yesu akawaambia, "Nini ambacho ninyi wawili mnakiongelea wakati mnatembea?" Wakasimama pale wakionekana na huzuni.
\v 18 Mmoja wao, jina lake Cleopa, akamjibu, "Je wewe ni mtu pekee hapa Yerusalemu ambaye hajui mambo yaliyotokea huko siku hizi?"
\s5
\v 19 Yesu akawaambia, "Mambo gani?" Wakamjibu, "Mambo kuhusu Yesu Mnazareti, ambaye alikuwa nabii, muweza katika matendo na maneno mbele za Mungu na watu wote.
\v 20 Na kwa jinsi ambayo wakuu wa makuhani na viongozi wetu walivyomtoa kuhukumiwa kifo na kumsulubisha.
\s5
\v 21 Lakini tulitumaini kwamba yeye ndiye atakaye waweka huru Israeli. Ndiyo, mbali na haya yote, sasa ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.
\s5
\v 22 Lakini pia, baadhi ya wanawake kutoka katika kundi letu walitushangaza, baada ya kuwapo kaburini asubuhi na mapema.
\v 23 Walipoukosa mwili wake, wakaja, wakisema kwamba waliona pia maono ya malaika waliosema kwamba yu hai.
\v 24 Baadhi ya wanaume ambao walikuwa pamoja nasi walienda kaburini, na kukuta ni kama vile wanawake walivyosema. Lakini hawakumuona yeye."
\s5
\v 25 Yesu akawaambia, "Ninyi watu wajinga na wenye mioyo mizito ya kuamini yote ambayo manabii wamesema!
\v 26 Je haikuwa lazima Yesu kuteseka kwa mambo haya, na kuingia katika utukufu wake?"
\v 27 Kisha kuanzia kutoka kwa Musa na manabii wote, Yesu akawatafsiria mambo yanayomuhusu yeye katika maandiko yote.
\s5
\v 28 Walipokaribia kile kijiji, huko walikokuwa wakienda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea mbele.
\v 29 Lakini walimlazimisha, wakisema, "Kaa pamoja nasi, maana inaelekea jioni na siku ni kama imeisha." Hivyo Yesu akaingia kwenda kukaa nao.
\s5
\v 30 Ilitokea kwamba, wakati amekaa nao kula, alichukua mkate, akaubariki, na kuuvunja, akawapa.
\v 31 Kisha macho yao yakafunguliwa, wakamjua, na akatoweka ghafla mbele ya macho yao.
\v 32 Wakasemezana wao kwa wao, "Hivi mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, wakati alipoongea nasi njiani, wakati alipotufungulia maandiko?"
\s5
\v 33 Wakanyanyuka saa hiyo hiyo, na kurudi Yerusalemu. Wakawakuta wale kumi na mmoja wamekusanyika pamoja, na wale waliokuwa pamoja nao,
\v 34 wakisema, "Bwana amefufuka kwelikweli, na amemtokea Simoni."
\v 35 Hivyo wakawaambia mambo yaliyotokea njiani, na namna Yesu alivyodhihirishwa kwao katika kuumega mkate.
\s5
\v 36 Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, "Amani iwe kwenu."
\v 37 Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho.
\s5
\v 38 Yesu akawaambia, Kwanini mnafadhaika? Kwanini maswali yanainuka mioyoni mwenu?
\v 39 Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo."
\v 40 Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake.
\s5
\v 41 Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, "Je mna kitu chochote cha kula?"
\v 42 Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa.
\v 43 Yesu akakichukua, na kukila mbele yao.
\s5
\v 44 Akawaambia, "Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike."
\s5
\v 45 Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko.
\v 46 Akawaambia, "Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu.
\v 47 Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu.
\s5
\v 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
\v 49 Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu.
\s5
\v 50 Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki.
\v 51 Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni.
\s5
\v 52 Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu.
\v 53 Waliendelea kuwepo hekaluni, wakimbariki Mungu.

1648
44-JHN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1648 @@
\id JHN
\ide UTF-8
\h Yohana
\toc1 Yohana
\toc2 Yohana
\toc3 jhn
\mt Yohana
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.
\v 2 Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu.
\v 3 Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika.
\s5
\v 4 Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote.
\v 5 Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha.
\s5
\v 6 Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana.
\v 7 Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.
\v 8 Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru
\s5
\v 9 Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja
\s5
\v 10 Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua.
\v 11 Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea.
\s5
\v 12 Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu,
\v 13 Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe.
\s5
\v 14 Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.
\v 15 Yohana alishuhudia kuhusu yeye, na alipaza sauti akisema, "Huyu ndiye ambaye nilisema habari zake nikisema, "Yule ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu amekuwako kabla yangu."
\s5
\v 16 Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa.
\v 17 Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo.
\v 18 Hakuna mwanadamu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mtu pekee ambaye ni Mungu, aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane.
\s5
\v 19 Na huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati makuhani na walawi waliotumwa kwake na Wayahudi kumwuliza, "Wewe ni nani?"
\v 20 Bila kusitasita na hakukana, bali alijibu, "Mimi sio Kristo."
\v 21 Hivyo wakamuuliza, "kwa hiyo wewe ni nani sasa?" Wewe ni Eliya? Akasema, "Mimi siye." Wakasema, Wewe ni nabii? Akajibu," Hapana."
\s5
\v 22 Kisha wakamwambia, "Wewe ni nani, ili kwamba tuwape jibu waliotutuma"? Wajishuhudiaje wewe mwenyewe?"
\v 23 Akasema, "Mimi ni sauti yake aliaye nyikani: 'Inyosheni njia ya Bwana,' kama nabii Isaya alivyosema."
\s5
\v 24 Basi kulikuwa na watu wametumwa pale kutoka kwa Mafarisayo. Wakamuuliza na kusema,
\v 25 "Kwa nini unabatiza basi kama wewe sio Kristo wala Eliya wala nabii?"
\s5
\v 26 Yohana aliwajibu akisema, "Ninabatiza kwa maji. Hata hivyo, miongoni mwenu anasimama mtu msiyemtambua.
\v 27 Huyu ndiye ajaye baada yangu. Mimi sisitahili kulegeza kamba za viatu vyake."
\v 28 Mambo haya yalitendeka huko Bethania, ng'ambo ya Yordani, mahali ambapo Yohana alikuwa akibatiza.
\s5
\v 29 Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, " Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!
\v 30 huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, "Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.'
\v 31 Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, kwamba nilikuja nikibatiza kwa maji."
\s5
\v 32 Yohana alishuhudia, "Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa hua, na ilibaki juu yake.
\v 33 Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, 'yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.'
\v 34 Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu."
\s5
\v 35 Tena siku iliyofuata Yohana alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili,
\v 36 walimwona Yesu akitembea na Yohana akasema, "Tazama, Mwana kondoo wa Mungu!"
\s5
\v 37 Wanafunzi wawili walimsikia Yohana akisema haya wakamfuata Yesu.
\v 38 Tena Yesu aligeuka na kuwaona wanafunzi wale wakimfuata, na akawambia, "Mnataka nini?" Wakajibu, "Rabbi, (maana yake 'mwalimu,' unaishi wapi?"
\v 39 Akawambia, "Njooni na mwone."Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi; walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.
\s5
\v 40 Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro.
\v 41 Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, "Tumempata Masihi" (ambayo inatafsiriwa Kristo).
\v 42 Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, "Wewe ni Simoni mwana wa Yohana" utaitwa Kefa," (maana yake 'Petro').
\s5
\v 43 Siku iliyofuata wakati Yesu alipotaka kuondoka kwenda Galilaya, alimpata Filipo na akamwambia, "Nifuate mimi."
\v 44 Filipo alikuwa ni mwenyeji wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro.
\v 45 Filipo alimpata Nathanaeli na kumwambia, Tumempata yule ambaye Musa aliandika habari zake katika sheria na Manabii. Yesu mwana wa Yusufu, kutoka Nazareti.
\s5
\v 46 Nathanaeli akamwambia, "Je kitu chema chaweza kutokea Nazareti?" Filipo akamwambia, Njoo na uone."
\v 47 Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake na akasema, "Tazama, Mwisraeli kweli kweli asiye na udanganyifu ndani yake!"
\v 48 Nathanaeli akamwambia, "Umenifahamuje mimi?" Yesu akajibu na akamwambia, "Kabla Filipo hajakuita ulipokuwa chini ya mtini, nalikuona."
\s5
\v 49 Nathanaeli akajibu, "Rabi wewe u Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli"!
\v 50 Yesu akajibu akamwambia, Kwa sababu nilikuambia 'nilikuona chini ya mtini' je waamini? utaona matendo makubwa kuliko haya."
\v 51 Yesu akasema, "Amini amini nawambieni mtaziona mbingu zikifunguka, na kuwaona malaika wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya siku tatu, kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya na mama yake Yesu alikuwa huko.
\v 2 Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa katika arusi.
\s5
\v 3 Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, "Hawana divai."
\v 4 Yesu akajibu, "Mwanamke hiyo inanihusu nini mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia."
\v 5 Mama yake akawambia watumishi, "Chochote atakachowambia fanyeni."
\s5
\v 6 Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu.
\v 7 Yesu akawambia, "Ijazeni maji mitungi ya mawe." Wakajaza hadi juu.
\v 8 Kisha akawambia wale watumishi, "Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza." Wakafanya kama walivyoagizwa.
\s5
\v 9 Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na
\v 10 kumwambia, "Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa"
\s5
\v 11 Muujiza huu wa Kana ya Galilaya, ulikuwa ndio mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini.
\s5
\v 12 Baada ya hii, Yesu, mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake walienda katika mji wa Kapernaum na wakaa huko kwa siku chache.
\s5
\v 13 Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.
\v 14 Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu.
\s5
\v 15 Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.
\v 16 Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, "Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko."
\s5
\v 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, "Wivu wa nyumba yako utanila."
\v 18 Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?"
\v 19 Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu."
\s5
\v 20 Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, "Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?"
\v 21 Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.
\v 22 Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.
\s5
\v 23 Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka, wakati wa sikukuu watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya.
\v 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote.
\v 25 Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Basi kulikuwa na Farisayo ambaye jina lake Nikodemo, mmoja wa wajumbe wa baraza la Wayahudi.
\v 2 Mtu huyu alimwendea Bwana Yesu usiku na akamwambia, "Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu kutoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kutenda ishara hizi zote Mungu asipokuwa pamoja naye."
\s5
\v 3 Yesu akamjibu, "Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili."
\v 4 Nikodemo akasema," Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?"
\s5
\v 5 Yesu akajibu, "Amini, amini mtu sipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
\s5
\v 7 Usishangae kwa sababu nilikuwambia, 'ni lazima kuzaliwa mara ya pili.'
\v 8 Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho.
\s5
\v 9 Nikodemo akajibu, kwa kusema, "Mambo haya yawezekanaje?"
\v 10 Yesu akamjibu, "Wewe u mwalimu wa Israeli, hata hauyajui mambo haya?
\v 11 Amini, amini, nakuambia, kile tunachokifahamu twakishuhudia kwa kile tulichokiona. Lakini hampokei ushuhuda wetu.
\s5
\v 12 Kama nimewambia mambo ya hapa duniani na hamuamini, mtawezaje kuamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni?
\v 13 Maana hakuna aliyepanda juu kutoka mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka, Mwana wa Adamu.
\s5
\v 14 Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe,
\v 15 ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele.
\s5
\v 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele.
\v 17 Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
\v 18 Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ameshahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
\s5
\v 19 Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu.
\v 20 kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi.
\v 21 Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.
\s5
\v 22 Baada ya haya, Yesu pamoja na wanafunzi walienda katika nchi ya Yudea. Huko alitumia muda pamoja nao na alikuwa akibatiza.
\v 23 Sasa Yohana pia alikuwa akibatiza huko Ainea karibu na Salim maana kulikuwa na maji mengi pale. Watu walikuwa wakija kwake na kubatizwa,
\v 24 kwa kuwa Yohana alikuwa hajatupwa gerezani.
\s5
\v 25 Kisha palitokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi kuhusu sikukuuu za utakaso.
\v 26 Wakaenda kwa Yohana wakamwambia, "Rabi, yeye uliyekuwa naye ng'ambo ya Mto Yorodani, yeye uliyeshuhudia habari zake, tazama, anabatiza na wote wanaenda wanamfuata."
\s5
\v 27 Yohana akajibu mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa kama amepewa kutoka mbinguni.
\v 28 Ninyi wenyewe mwashuhudia kuwa nalisema kuwa, 'mimi sio Kristo', badala yake nilisema, 'nimetumwa mbele yake.'
\s5
\v 29 Yeye aliye na bibi arusi ni bwana harusi. Sasa rafiki wa bwana arusi, asimamaye na kusikiliza hufurahia sana kwa sababu ya sauti ya bwana arusi. Hii sasa ni furaha yangu iliyotimilika.
\v 30 Anapaswa kuzidi, nami napaswa kupungua.
\s5
\v 31 Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote.
\v 32 Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake.
\v 33 Yeye aliye pokea ushuhuda wake amehakikisha kuwa Mungu ni mkweli.
\s5
\v 34 Kwa sababu yeye aliyetumwa na Mungu huongea maneno ya Mungu. Kwa kuwa hampi Roho kwa kipimo.
\v 35 Baba humpenda Mwana na amempa vitu vyote mikononi mwake.
\v 36 Yeye amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini kwa yeye asiye mtii Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hushikamana juu yake.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Basi Yesu alipofahamu kuwa Mafarisayo wamesikia kuwa Yesu alikuwa anafuasa na kuwabatiza zaidi ya Yohana,
\v 2 (ingawa Yesu mwenyewe alikuwa habatizi ila wanafunzi wake),
\v 3 alitoka Judea na akaenda Galilaya.
\s5
\v 4 Hivyo ilikuwa muhimu kupitia Samaria.
\v 5 Na akafika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari, karibu na eneo ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.
\s5
\v 6 Na kisima cha Yakobo kilikuwa hapo. Yesu alikuwa amechoka kwa ajili ya safari na akakaa karibu na kisima. Ilikuwa muda wa mchana.
\v 7 Mwanamke Msamaria alikuja kuteka maji, na Yesu akamwambia, "Nipe maji ninywe."
\v 8 Kwa sababu wanafunzi wake walikuwa wameenda zao mjini kununua chakula.
\s5
\v 9 Yule mwanamke akamwambia, "Inakuaje wewe Myahudi, kuniomba mimi mwanamke Msamaria, kitu cha kunywa?" Kwa sababu Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.
\v 10 Yesu akamjibu, "Kama ungelijua karama ya Mungu, na yule anayekuambia 'Nipe maji, ' ungelimwomba, na angelikupa maji ya uzima."
\s5
\v 11 Mwanamke akajibu, "Bwana hauna ndoo ya kuchotea, na kisima ni kirefu. Utayapata wapi Maji ya Uzima.?
\v 12 Je wewe ni mkuu, kuliko baba yetu Yakobo, ambaye alitupa kisima hiki, na yeye mwenyewe na watoto wake pamoja na mifugo yake wakanywa maji ya kisima hiki?"
\s5
\v 13 Yesu akajibu, "Yeyote anywae maji haya atapata kiu tena,
\v 14 lakini yeye atakaye kunywa maji nitakayompa hatapata kiu tena. Badala yake maji nitakayompa yatakuwa chemchemi inayobubujika hata milele."
\s5
\v 15 Yule mwanamke akamwambia, "Bwana, nayaomba maji hayo ili nisipate kiu, na nisihangaike kuja hapa kuchota maji."
\v 16 Yesu akamwambia, "Nenda kamwite mumeo, kisha urudi."
\s5
\v 17 Mwanamke akamwambia, "Sina mume." Yesu akajibu, "Umesema vyema, 'Sina mume;'
\v 18 kwa maana umekuwa na wanaume watano, na mmoja ambaye unaye sasa sio mume wako. Katika hili umesema kweli!"
\s5
\v 19 Mwanamke akamwambia, "Bwana naona yakuwa wewe ni nabii.
\v 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi mwasema ya kuwa Yerusalemu ndiyo sehemu ambayo watu wanapaswa kuabudu."
\s5
\v 21 Yesu akamjibu, "Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu au Yerusalemu.
\v 22 Ninyi watu mwaabudu kile msichokijua, lakini sisi twaabudu tunachokijua, kwa sababu wokovu watoka kwa Wayahudi."
\s5
\v 23 Hatahivyo, wakati unakuja, na sasa upo hapa, wakati waabuduo kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli, kwa sababu Baba anawatafuta watu wa namna hiyo kuwa watu wake wanao mwabudu.
\v 24 Mungu ni Roho, na wale wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu kwa roho na kweli."
\s5
\v 25 Mwanamke akamwambia, "Ninajua kuwa Masihi anakuja, (aitwaye Kristo). Huyo atakapokuja atatwambia yote."
\v 26 Yesu akamwambia, "Mimi unayesema nami ndiye."
\s5
\v 27 Wakati huo huo wanafunzi wake wakarudi. Nao walishangaa kwa nini alikuwa akizungumza na mwanamke, lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza, "Unataka nini?" au "Kwa nini unazungumza naye.?"
\s5
\v 28 Hivyo mwanamke akauacha mtungi wake na akaenda mjini na akawambia watu,
\v 29 "Njooni mwone mtu aliyeniambia mambo yangu yote niliyoyatenda, je yawezekana akawa ndiye Kristo?"
\v 30 Wakatoka mjini wakaja kwake.
\s5
\v 31 Wakati wa mchana wanafunzi wake walimsihi wakisema, "Rabi kula chakula."
\v 32 lakini yeye aliwambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi."
\v 33 Wanafunzi wakaambizana, hakuna aliyemletea kitu chochotekula,"Je walileta?"
\s5
\v 34 Yesu akawambia, "Chakula changu ni kufanya mapenzi yake yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake.
\v 35 Je, hamsemi, 'Bado miezi mitano na mavuno yatakuwa tayari?' Ninawambieni tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno!
\v 36 Yeye avunaye hupokea mishahara na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.
\s5
\v 37 Kwa kuwa msemo huu ni wa kweli, 'Mmoja apanda na mwingine avuna.'
\v 38 Niliwatuma kuvuna ambacho hamkukihangaikia, Wengine wamefanya kazi na ninyi mmeingia katika furaha ya kazi yao."
\s5
\v 39 Wasamaria wengi katika mji ule walimwani kwa sababu ya taarifa ya yule mwanamke aliyekuwa akishuhudia, "Aliyeniambia mambo yote niliyoyafanya."
\v 40 Hivyo Wasamaria walipokuja walimsihi akae pamoja nao na akakaa kwao kwa siku mbili.
\s5
\v 41 Na wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.
\v 42 Wakamwambia yule mwanamke, "Tunaamini sio tu kwa maneno yako, kwa sababu sisi wenyewe tumesikia, na sasa twafahamu kuwa hakika yeye ni mwokozi wa ulimwengu."
\s5
\v 43 Baada ya siku hizo mbili, akaondoka na kuelekea Galilaya.
\v 44 Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe.
\v 45 Alipokuja kutoka Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.
\s5
\v 46 Alikuja tena Kana ya Galilaya huko alikoyabadilisha maji kuwa divai. Palikuwa na ofisa ambaye mwana wake alikuwa ni mgonjwa huko Kapernaumu.
\v 47 Aliposikia kuwa Yesu alitoka Judea na kwenda Galilaya, alienda kwa Yesu na kumsihi atelemke amponye mwanawe, ambaye alikuwa karibu kufa.
\s5
\v 48 Ndipo Yesu akamwambia, "Ninyi msipoona ishara na maajabu hamwezi kuamini.
\v 49 Kiongozi akasema, " Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa."
\v 50 Yesu akamwambia, "Nenda mwanao ni mzima." Yule mtu akaamini neno alilolisema Yesu na akaenda zake.
\s5
\v 51 Alipokuwa akishuka, watumishi wake walimpokea na kumwambia mwana wake alikuwa mzima.
\v 52 Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, "Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha."
\s5
\v 53 Ndipo baba yake akatambua kuwa ni muda ule ule Yesu aliosema, "Mwana wako ni mzima." Hivyo yeye na familia yake wakaamini.
\v 54 Hii ilikuwa ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipotoka Yudea kwenda Galilaya.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Baada ya hapo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.
\v 2 Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiebrania Bethzatha, nalo lina matao matano.
\v 3 Idadi kubwa ya wagonjwa ilikuwemo, vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika matao hayo. {Zingatia: Maneno ya mstari wa 3 hayaonekani katika nakala nzuri za kale. "Wakisubiri maji kutibuliwa.") Kwa hakikia wakati fulani malaika alishuka ndani ya Bwana na kuyatibua maji.
\v 4 Kwahiyo, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani ya baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.
\s5
\v 5 Na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane alikuwa ndani ya matao.
\v 6 Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu Yesu alimwambia, "Je unataka kuwa mzima?"
\s5
\v 7 Yule mgonjwa akamjibu, "Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapojaribu kuingia mtu mwingine hunitangulia."
\v 8 Yesu akamwambia, "Inuka na uchukue godoro lako na uende."
\s5
\v 9 Mara yule mtu akaponywa, akachukua kintanda chake na akaenda. Na siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
\s5
\v 10 Hivyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, "Leo ni siku ya Sabato, na hauruhusiwi kubeba godoro lako."
\v 11 Akajibu, yeye aliyeniponya ndiye aliyeniambia, "Chukua godoro lako na uende."
\s5
\v 12 Wakauliza, "Ni nani aliyekuambia 'Chukua godoro lako na uende?'''
\v 13 Ingawa, yule aliyeponywa hakumjua, kwa sababu Yesu alikuwa ameondoka kwa siri. Kwa kuwa kulikuwa na watu wengi katika sehemu hiyo.
\s5
\v 14 Baada ya hapo Yesu alimkuta yule mtu hekaluni na akamwambia, "Tazama, umepona! "Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi."
\v 15 Yule mtu akaenda na kuwataarifu Wayahudi kuwa Yesu ndiye aliyemponya.
\s5
\v 16 Hivyo, kwa sababu ya mambo hayo Wayahudi walimtesa Yesu, kwa sababu alifanya mambo haya siku ya Sabato.
\v 17 Yesu akawambia, "Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami nafanya kazi."
\v 18 Kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kumtafuta ili wamuue sio tu kwa sababu ya kuivunja Sabato, bali kwa kumwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.
\s5
\v 19 Yesu akawajibu, "Amini, amini, Mwana hawezi kufanya kitu chochote isipokuwa kile ambacho amemwona Baba yake anakifanya, kwa kuwa chochote Baba akifanyacho ndicho na Mwana atakachofanya.
\v 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, na amwonyesha kila kitu anachokifanya na atamwonyesha mambo makubwa kuliko haya ili kwamba mzidi kushangaa."
\s5
\v 21 Kwa kuwa kama vile ambavyo Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, halikadhalika Mwana pia humpa yeyote ampendaye.
\v 22 Kwa kuwa Baba hamhukumu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote
\v 23 ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.
\s5
\v 24 Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.
\s5
\v 25 Amini, amini, nawambia wakati unakuja na sasa upo ambao wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wote watakao sikia wataishi.
\s5
\v 26 Kwa kuwa kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake mwenyewe,
\v 27 kadhalika amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake, na Baba amempa Mwana mamlaka ili kwamba ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.
\s5
\v 28 Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
\v 29 nao watatoka nje: kwa waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
\s5
\v 30 Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\v 31 Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
\v 32 Kuna mwingine anayeshuhudia kuhusu mimi na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
\s5
\v 33 Mmetuma kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
\v 34 Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
\v 35 Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
\s5
\v 36 Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
\v 37 Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
\v 38 Hamna neno lake likikaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
\s5
\v 39 Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
\v 40 hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
\s5
\v 41 Sipokei sifa kutoka kwa watu,
\v 42 lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.
\s5
\v 43 Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.
\v 44 Je mnawezaje kuamini ninyi ambao mnapokea sifa kutoka kwa kila mmoja wenu lakini hamtafuti sifa itokayo kwa Mungu wa pekee?
\s5
\v 45 Msidhani mimi nitawashitaki mbele za Baba. Anayewashitaki ninyi ni Musa, ambaye ninyi mmeweka matumaini yenu kwake.
\v 46 Kama mngekuwa mnamwamini Musa, mngeniamini mimi kwa sababu aliandika kuhusu habari zangu.
\v 47 Kama hamuamini maandiko yake, mtawezaje kuamini maneno yangu.?
\s5
\c 6
\p
\v 1 Baada ya mambo haya, Yesu alienda pande za Bahari ya Galilaya, pia huitwa Bahari ya Tiberia.
\v 2 Mkutano mkubwa ulikuwa ukimfuata kwa sababu waliona ishara alizozifanya kwa waliokuwa wagonjwa.
\v 3 Yesu alipanda juu hadi upande wa juu wa mlima na akakaa huko na wanafunzi wake
\s5
\v 4 (Na Pasaka, Sikukuu ya Wayahudi ilikuwa imekaribia).
\v 5 Yesu alipoinua macho yake juu na kuona umati mkubwa unakuja kwake, akamwambia Filipo, "Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula"?
\v 6 (Lakini Yesu aliyasema haya kwa Filipo kwa kumjaribu kwa kuwa yeye mwenyewe alijua atakachofanya).
\s5
\v 7 Filipo akamjibu, "Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo."
\v 8 Andrea, mmoja wa wanafunzi wake ndugu yake Simoni Petro akamwambia
\v 9 Yesu, "Kuna mvulana hapa ana mikate mitano na samaki wawili, lakini hii yafaa nini kwa watu wengi namna hii?"
\s5
\v 10 Yesu akawambia, "Waketisheni watu chini" (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini.
\v 11 Kisha Yesu akachukua ile mikate mitano akashukuru akawawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile wavyohitaji.
\v 12 Watu waliposhiba, aliwambia wanafunzi wake, "Vikusanyeni vipande vya mabaki, vilivyobaki ili kwamba kisipotee chochote."
\s5
\v 13 Basi wakakusanya na kujaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri- vipande vilivyosazwa na wale waliokula.
\v 14 Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, "Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni."
\v 15 Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao, alijitenga, tena na akaenda mlimani yeye peke yake.
\s5
\v 16 Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake walishuka kwenda ziwani.
\v 17 Wakapanda kwenye mtumbwi na walikuwa wakivuka kuelekea Kapernaumu. (Giza lilikuwa limeingia na Yesu alikuwa bado hajaja kwao).
\v 18 Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukivuma, na bahari ilikuwa ikendelea kuchafuka.
\s5
\v 19 Tena wanafunzi wake walipokuwa wamepiga makasia kama ishirini na matano au thelathini, wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari kuukaribia mtumbwi, na wakaogopa.
\v 20 Lakini akawambia, "Ni mimi! Msiogope."
\v 21 Tena walikuwa tayari kumbeba kwenye mtumbwi, na mara mtumbwi ulifika kwenye nchi mahali walipokuwa wakienda.
\s5
\v 22 Siku iliyofuata, mkutano uliokuwa umesimama upande wa bahari waliona kuwa hakuna mtumbwi mwingine isipokuwa ule ambayo Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaupanda lakini wanafunzi wake walikuwa wameenda zao wenyewe.
\v 23 (Ingawa, kulikuwa na baadhi ya mitumbwi iliyotoka Tiberia karibu na mahali walipokula mikate baada ya Bwana kutoa shukrani).
\s5
\v 24 Wakati makutano walipotambua kuwa sio Yesu wala wanafunzi wake walikuwa kule, wao wenyewe walipanda ndani ya mitumbwi wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.
\v 25 Baada ya kumpata upande mwingine wa ziwa wakamuuliza, "Rabbi ulikuja lini huku?"
\s5
\v 26 Yesu akawajibu, akawambia, Amini, amini, mnanitafuta mimi, sio kwa sababu mliziona ishara, bali kwa sababu mlikula mikate na kushiba.
\v 27 Acheni kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali mkifanyie kazi chakula kidumucho hata milele kile ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa kuwa Mungu Baba ameweka muhuri juu yake."
\s5
\v 28 Kisha wakamwambia, "Ni nini tunapaswa kufanya ili kuzifanya kazi za Mungu?"
\v 29 Yesu akajibu, "Hii ndiyo kazi ya Mungu: kwamba mmwamini yeye aliyemtuma."
\s5
\v 30 Basi wakamwambia, "Ni ishara zipi utakazofanya, kwamba tunaweza kuziona na kukuamini? Utafanya nini?
\v 31 Baba zetu walikula manna jangwani, kama ilivyo andikwa, "Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale."
\s5
\v 32 Kisha Yesu akawajibu, "Amini, amini, sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni.
\v 33 Kwa kuwa mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupatia uzima ulimwengu.
\v 34 Basi wakamwambia, "Bwana tupatie huu mkate wakati wote."
\s5
\v 35 Yesu akawambia, "Mimi ndiye mkate wa uzima, yeye ajaye kwangu hatapata njaa na yeye aniaminiye hatahisi kiu kamwe."
\v 36 Ingawa niliwaambia kwamba, mmeniona, na bado hamuamini.
\v 37 Wote ambao Baba anaonipa watakuja kwangu, na yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kabisa.
\s5
\v 38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni, sio kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\v 39 Na haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali nitawafufua siku ya mwisho.
\v 40 Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
\s5
\v 41 Kisha wayahudi wakamnung`unikia kumhusu yeye kwa sababu alisema, "Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni."
\v 42 Wakasema, "Huyu siyo Yesu mwana wa Yusuph, ambaye baba yake na mama yake tunamfahamu? Imekuwaje sasa anasema, 'Nimeshuka kutoka mbinguni`?"
\s5
\v 43 Yesu akajibu, akawambia, "Msinung'unikiane miongoni mwenu wenyewe.
\v 44 Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.
\v 45 Kwa kuwa imeandikwa katika manabii, 'Watafundishwa na Mungu.' Kila aliyesikia na amejifunza kutoka kwa Baba, huja kwangu.
\s5
\v 46 Sio kwamba kuna mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu- amemwona Baba.
\v 47 Amini, amini yeye aaminiye anao uzima wa milele.
\s5
\v 48 Mimi ni mkate wa uzima.
\v 49 mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa.
\s5
\v 50 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife.
\v 51 Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu."
\s5
\v 52 Wayahudi wakakasirika wenyewe kwa wenyewe na wakaanza kubishana wakisema, "Mtu huyu anawezaje kutupa mwili wake tuule?"
\v 53 Kisha Yesu akawambia, "Amini, amini, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamta kuwa na uzima ndani yenu.
\s5
\v 54 Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.
\v 55 Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
\v 56 Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake.
\s5
\v 57 Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, na yeye pia ataishi kwa sababu yangu.
\v 58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele.
\v 59 Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.
\s5
\v 60 Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, "Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?"
\v 61 Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza?
\s5
\v 62 Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla?
\v 63 Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima.
\s5
\v 64 Bado kuna watu kati yenu wasioamini." kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti.
\v 65 Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba."
\s5
\v 66 Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena.
\v 67 Yesu akawambia wale kumi na wawili, "Je na ninyi mnataka kuondoka?"
\v 68 Simoni Petro akamjibu, "Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,
\v 69 na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu."
\s5
\v 70 Yesu akawambia, "Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni ibilisi?
\v 71 Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
\v 2 Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
\s5
\v 3 Ndipo ndugu zake walipomwambia, "Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
\v 4 Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu."
\s5
\v 5 Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
\v 6 Ndipo Yesu alipowaambia, "Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
\v 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
\s5
\v 8 Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado."
\v 9 Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
\s5
\v 10 Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
\v 11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, "Yuko wapi?"
\s5
\v 12 Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, "Ni mtu mwema." Wengine walisema, "Hapana, huwapotosha makutano."
\v 13 Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
\s5
\v 14 Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
\v 15 Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, "Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe."
\v 16 Yesu akawajibu na kuwaambia, "Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
\s5
\v 17 Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
\v 18 Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
\s5
\v 19 Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
\v 20 Makutano wakajibu, "Una pepo. Nani anataka kukuua?"
\s5
\v 21 Yesu akajibu na akawaambia, "Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
\v 22 Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahili mtu.
\s5
\v 23 Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
\v 24 Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa haki.
\s5
\v 25 Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, "Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
\v 26 Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
\v 27 Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka."
\s5
\v 28 Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, "Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
\v 29 Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma."
\s5
\v 30 Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\v 31 Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, "Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?"
\v 32 Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.
\s5
\v 33 Ndipo Yesu aliposema, "Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.
\v 34 Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja."
\s5
\v 35 Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, "Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa Waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
\v 36 Ni neno gani hili alilolisema, 'Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja'?"
\s5
\v 37 Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, "Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
\v 38 Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima."
\s5
\v 39 Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
\s5
\v 40 Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, "Kweli huyu ni nabii."
\v 41 Wengine walisema, "Huyu ni Kristo." Lakini wengine walisema, "nini, Kristo aweza kutoka Galilaya?
\v 42 Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?
\s5
\v 43 Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.
\v 44 Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake.
\s5
\v 45 Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, "Kwa nini hamjamleta?"
\v 46 Maofisa wakajibu, "Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla."
\s5
\v 47 Ndipo Mafarisayo walipowajibu, "Na nyinyi pia mmepotoshwa?
\v 48 Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?
\v 49 Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa."
\s5
\v 50 Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),
\v 51 "Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?"
\v 52 Walijibu na kumwambia, "Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya."
\s5
\v 53 (Zingatia: Baadhi ya maneno ya Yohana 7: 53 - 8: 11 hayamo katika nakala bora za kale). Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.
\s5
\c 8
\p
\v 1 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Yesu alienda mlima wa Mizeituni.
\v 2 Mapema asubuhi akaja tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; akakaa na kuwafundisha.
\v 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha kuzini. Wakamweka katikati.
\s5
\v 4 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Ndipo wakamwambia Yesu, "Mwalimu, mwanamke huyu amekamatwa katika uzinzi, katika kitendo kabisa.
\v 5 Sasa, katika sheria, Musa ametuamuru kuwaponda mawe watu kama hawa, unasemaje juu yake?
\v 6 Walisema haya ili kumtega ili kwamba wapate jambo la kumshitaki, lakini Yesu akainama chini akaandika katika ardhi kwa kidole chake.
\s5
\v 7 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Walipoendelea kumwuliza, alisimama na kuwaambia, "Yeye asiyekuwa na dhambi miongoni mwenu, awe wa kwanza kumponda mawe."
\v 8 Akainama tena chini, akaandika katika ardhi kwa kidole chake.
\s5
\v 9 (Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7: 53 - 8: 11 hapo juu). Waliposikia hayo, waliondoka mmoja baada ya mwingine, kuanzia aliye mzee. Mwishowe Yesu aliachwa peke yake, pamoja na mwanamke aliyekuwa katikati yao.
\v 10 Yesu alisimama na kumwambia, "Mwanamke, waliokushitaki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?"
\v 11 Akasema, "Hakuna hata mmoja Bwana." Yesu akasema, "Hata mimi sikuhukumu. Nenda njia yako; kuanzia sasa na kuendelea usitende dhambi tena."
\s5
\v 12 Tena Yesu akazungumza na watu akisema, "Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeye anifuataye hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya uzima."
\v 13 Mafarisayo wakamwambia, "Unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako siyo wa kweli."
\s5
\v 14 Yesu alijibu akawaambia, "Hata kama nitajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli. Ninajua mahali nilikotoka na kule ninakoenda, lakini ninyi hamjui mahali ninapotoka au kule ninakoenda.
\v 15 Nyinyi mnahukumu kimwili; mimi simhukumu yeyote.
\v 16 Mimi hata nikihukumu, hukumu yangu ni kweli kwa sababu siko peke yangu, bali niko pamoja na baba aliyenituma.
\s5
\v 17 Ndiyo, na katika sheria yenu imeandikwa kwamba ushuhuda wa watu wawili ni kweli.
\v 18 Mimi ndiye ninayejishuhudia, na Baba aliyenituma ananishuhudia."
\s5
\v 19 Wakamwambia, "Baba yako yuko wapi?" Yesu akajibu, "mimi hamnijui wala Baba yangu hammjui; mngelikuwa mnanijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia."
\v 20 Alisema maneno haya akiwa karibu na hazina alipokuwa akifundisha hekaluni, na hakuna hata mmoja aliyemkamata kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\s5
\v 21 Basi akawaambia tena, "Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja."
\v 22 Wayahudi wakasema, "Atajiua mwenyewe, yeye ambaye alisema, 'kule niendako hamuwezi kuja'?"
\s5
\v 23 Yesu akawaambia, "Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa Ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu.
\v 24 Kwa hiyo, naliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu".
\s5
\v 25 Kwa hiyo wakamwambia, "Wewe ni nani?" Yesu akawaambia, Yale niliyowaambia tangu mwanzo.
\v 26 Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa Ulimwengu."
\v 27 Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba.
\s5
\v 28 Yesu akasema, "Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya.
\v 29 Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza."
\v 30 Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi walimwamini.
\s5
\v 31 Yesu akasema kwa wale Wayahudi waliomwamini, "Ikiwa mtakaa katika neno langu, ndipo mtakuwa wanafunzi wangu kweli,
\v 32 nanyi mtaijua kweli, na kweli itawaweka huru."
\v 33 Walimjibu, "Sisi ni uzao wa Ibrahimu na kamwe hatujawahi kwa chini ya utumwa wa yeyote; utasemaje, "Tutawekwa huru?"
\s5
\v 34 Yesu aliwajibu, "Amini, amini, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
\v 35 Mtumwa hakai nyumbani wakati wote; mwana hudumu siku zote.
\v 36 Kwa hiyo, ikiwa Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kabisa."
\s5
\v 37 Ninajua kwamba ninyi ni uzao wa Ibrahimu; mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.
\v 38 Ninasema mambo ambayo nimeyaona pamoja na Baba yangu, na ninyi vile vile mnafanya mambo ambayo mliyasikia kutoka kwa baba yenu."
\s5
\v 39 Walijibu na kumwambia, "Baba yetu ni Abrahamu." Yesu akawaambia, Kama mngelikuwa watoto wa Ibrahimu, mngefanya kazi za Ibrahimu.
\v 40 Hata sasa mnatafuta kuniua, mtu aliyewaambia ukweli kwamba nilisikia kutoka kwa Mungu. Abrahamu hakufanya hivi.
\v 41 Mnafanya kazi za baba yenu." Wakamwambia, "Hatukuzaliwa katika uzinzi, tunaye Baba mmoja, Mungu."
\s5
\v 42 Yesu akawaambia, "Ikiwa Mungu ni Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nimetoka kwa Mungu; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye alinituma.
\v 43 Kwa nini hamyaelewi maneno yangu? Kwa sababu hamuwezi kuvumilia kuyasikia maneno yangu.
\v 44 Ninyi ni wa baba yenu, shetani, na mnataka kuzitenda tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.
\s5
\v 45 Hata sasa, kwa sababu ninasema iliyo kweli, hamniamini.
\v 46 Ni nani kati yenu anayenishuhudia kuwa nina dhambi? ikiwa ninasema iliyo kweli, kwa nini hamniamini?
\v 47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; ninyi hamyasikii kwa sababu ninyi si wa Mungu."
\s5
\v 48 Wayahudi wakamjibu na kumwambia, hatujasema kweli kuwa wewe ni Msamaria na una pepo?"
\v 49 Yesu akajibu, sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.
\s5
\v 50 Sitafuti utukufu wangu; kuna mmoja atafutaye na kuhukumu.
\v 51 Amini, amini, nawaambia, iwapo yeyote atalishika neno langu, hataona mauti kamwe."
\s5
\v 52 Wayahudi wakamwambia, "Sasa tumejua kuwa una pepo. Abrahamu na mabii walikufa; lakini unasema, 'Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti'.
\v 53 Wewe si mkuu kuliko baba yetu Abrahamu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?"
\s5
\v 54 Yesu akajibu, "Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu.
\v 55 Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, 'simjui,' nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika.
\v 56 Baba yenu Abrahamu alishangilia atakavyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi."
\s5
\v 57 Wayahudi wakamwambia,"Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?"
\v 58 Yesu akawaambia, "Amini, amini, nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, MIMI NIKO."
\v 59 Ndipo waliokota mawe wapate kumpiga, lakini Yesu alijificha na akatoka nje ya hekalu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Wakati, kama Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu kipofu tangu kuzaliwa kwake.
\v 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, "Rabi, nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?"
\s5
\v 3 Yesu akawajibu, "Siyo huyu mtu wala wazazi wake waliotenda dhambi, bali kazi za Mungu zipate kufunuliwa kupitia kwake.
\v 4 Tunapaswa kufanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana. Usiku waja wakati ambapo hakuna atakayeweza kufanya kazi.
\v 5 Wakati niwapo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu."
\s5
\v 6 Baada ya Yesu kusema maneno haya, alitema kwenye ardhi, alifanya tope kwa mate, na akampaka yule mtu machoni na lile tope.
\v 7 Akamwambia, nenda kaoge katika kisima cha Siloam (Inayotafsiriwa kama 'aliyetumwa')." Kwa hiyo huyo mtu alienda, akanawa, na akarudi, anaona.
\s5
\v 8 Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji walisema, Je! huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?" wengine walisema, "Ni yeye."
\v 9 Na wengine walisema, "Hapana, bali anafanana naye." Lakini alikuwa akisema, "Ni mimi."
\s5
\v 10 Wakamwambia, "Sasa macho yako yalifunguliwaje?"
\v 11 Alijibu, mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, 'Nenda Siloam ukanawe.' Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena."
\v 12 Wakamwambia, "Yuko wapi?" Alijibu, "Sijui."
\s5
\v 13 Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.
\v 14 Nayo ilikuwa siku ya Sabato wakati Yesu alipotengeneza tope na kuyafumbua macho yake.
\v 15 Ndipo tena Mafarisayo wakamwuliza alipataje kuona. Aliwaambia, "Aliweka tope katika macho yangu, nikanawa, na sasa naweza kuona."
\s5
\v 16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, "Mtu huyu hajatoka kwa Mungu kwa sababu haishiki Sabato." Wengine walisema, "Inawezekanaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?" Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati yao.
\v 17 Ndipo walipomwuliza yule kipofu tena, "Unasemaje juu yake kwa sababu aliyafungua macho yako?" Kipofu akasema, "Ni nabii."
\v 18 Hata wakati huu Wayahudi hawakumwamini kwamba alikuwa kipofu naye amepata kuona mpaka walipowaita wazazi wake yeye aliyepata kuona.
\s5
\v 19 Waliwauliza wazazi, Je, huyu ni mtoto wenu mnayesema alizaliwa kipofu? amewezaje sasa kuona?"
\v 20 Hivyo wazazi wake wakamjibu, "Tunajua kuwa huyu ni mtoto wetu na kwamba alizaliwa kipofu.
\v 21 Jinsi gani sasa anaona, hatujui, na yeye aliyemfumbua macho yake, hatumjui. Mwulizeni yeye. Ni mtu mzima. Anaweza kujieleza mwenyewe."
\s5
\v 22 Wazazi wake walisema mambo haya, kwa sababu waliwaogopa Wayahudi. Kwa vile Wayahudi walikuwa wamekubaliana tayari kuwa, ikiwa yeyote atakiri kuwa Yesu ni Kristo, atatengwa na Sinagogi.
\v 23 Kwa sababu hii, wazazi wake walisema, "Ni mtu mzima, mwulizeni yeye."
\s5
\v 24 Kwa hiyo kwa mara ya pili, walimwita yule mtu aliyewahi kuwa kipofu na kumwambia, "Mpe Mungu utukufu. Tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi."
\v 25 Ndipo yule mtu alijibu, "Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui. Kitu kimoja ninachokijua: nilikuwa kipofu, na sasa ninaona."
\s5
\v 26 Ndipo walipomwambia, "Amekufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?"
\v 27 Alijibu, "Nimekwishawaambia tayari, na nyinyi hamkusikiliza! Kwa nini mnataka kusikia tena? Nanyi hamtaki kuwa wanafunzi wake pia, sivyo?
\v 28 Walimtukana na kusema, "Wewe ni mwanafunzi wake, lakini sisi ni wanafunzi wa Musa.
\v 29 Tunajua kwamba Mungu alizungumza na Musa, lakini kwa huyu mtu, hatujui kule atokako."
\s5
\v 30 Yule mtu akajibu na kuwaambia, "Kwa nini, hili ni jambo la kushangaza, kwamba hamjui anakotoka, na bado ameyafumbua macho yangu.
\v 31 Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.
\s5
\v 32 Tangu kuanza kwa Ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
\v 33 Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote."
\v 34 Walijibu na kumwambia, "Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?" Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
\s5
\v 35 Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, "Unamwamini Mwana wa Mtu?"
\v 36 Alijibu na kusema, "Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?"
\v 37 Yesu akamwambia, "Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye."
\v 38 Yule mtu akasema, "Bwana, Naamini." Ndipo akamsujudia.
\s5
\v 39 Yesu akasema, "Kwa hukumu nimekuja katika Ulimwengu huu ili kwamba wale wasioona wapate kuona na wale wanaoona wawe vipofu."
\v 40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye wakasikia maneno hayo na kumwuliza, "Na sisi pia ni vipofu?"
\v 41 Yesu akawaambia, "Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, 'Tunaona,' dhambi yenu inakaa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
\v 2 Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
\s5
\v 3 Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje.
\v 4 Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.
\s5
\v 5 Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni."
\v 6 Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
\s5
\v 7 Yesu akasema nao tena, "Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
\v 8 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
\s5
\v 9 Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
\v 10 Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
\s5
\v 11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
\v 12 Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
\v 13 Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
\s5
\v 14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
\v 15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
\v 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
\s5
\v 17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
\v 18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba."
\s5
\v 19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
\v 20 Wengi wao wakasema, "Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?"
\v 21 Wengine wakasema, "Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?"
\s5
\v 22 Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
\v 23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
\v 24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, "Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
\s5
\v 25 Yesu akawajibu, "Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
\v 26 Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
\s5
\v 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
\v 28 Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
\s5
\v 29 Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
\v 30 Mimi na Baba tu mmoja."
\v 31 Wakabeba mawe ili wamponde tena.
\s5
\v 32 Yesu akawajibu, "Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?"
\v 33 Wayahudi wakamjibu, "Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu."
\s5
\v 34 Yesu akawajibu, "Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, "Ninyi ni miungu"'?"
\v 35 Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
\v 36 mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'?
\s5
\v 37 "Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
\v 38 Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba."
\v 39 Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.
\s5
\v 40 Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.
\v 41 Watu wengi wakaja kwa Yesu. Waliendelea kusema, "Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli."
\v 42 Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Alitokea Bethania, kijiji cha Mariamu na dada yake Martha.
\v 2 Alikuwa ni Mariamu yule yule aliyempaka Bwana Marhamu na kumfuta miguu yake kwa nywele zake, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa ni mgonjwa.
\s5
\v 3 Ndipo dada hawa walituma ujumbe kwa Yesu na kusema, "Bwana, angalia yule umpendaye anaumwa."
\v 4 Yesu aliposikia alisema, "Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo Ugonjwa."
\s5
\v 5 Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.
\v 6 Aliposikia kuwa Lazaro ni mgonjwa, Yesu alikaa siku mbili zaidi mahali alipokuwa.
\v 7 Ndipo baada ya hili aliwaambia wanafunzi wake, "Twendeni Uyahudi tena."
\s5
\v 8 Wanafunzi wakamwambia, "Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukuponda mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?"
\v 9 Yesu akawajibu, "Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana.
\s5
\v 10 Hata hivyo, ikiwa atatembea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haiko ndani yake."
\v 11 Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini."
\s5
\v 12 Ndipo wanafunzi wakamwambia, "Bwana, kama amelala, ataamka.
\v 13 Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
\v 14 Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, "Lazaro amekufa.
\s5
\v 15 Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake."
\v 16 Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, "Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu."
\s5
\v 17 Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.
\v 18 Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita arobaini na tano hivi.
\v 19 Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.
\v 20 Ndipo Martha aliposikia kuwa Yesu anakuja, alienda kukutana naye, lakini Mariamu aliendelea kukaa nyumbani.
\s5
\v 21 Ndipo Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa.
\v 22 Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia."
\v 23 Yesu akamwambia, kaka yako atafufuka tena."
\s5
\v 24 Martha akamwambia, najua kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho."
\v 25 Yesu akamwambia, "Mimi ni ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;
\v 26 na yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa. Unaamini hili?"
\s5
\v 27 Akamwambia, "Ndiyo, Bwana naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye katika ulimwengu."
\v 28 Alipokwisha kusema hili, alienda zake na kumwita dada yake Mariamu faraghani. Akasema, "Mwalimu yuko hapa na anakuita."
\v 29 Mariamu aliposikia haya, aliinuka kwa haraka na kwenda kwa Yesu.
\s5
\v 30 Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.
\v 31 Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.
\v 32 Ndipo Mariamu, alipofika pale Yesu alipokuwa alimuona na, alianguka chini ya miguu yake na kumwambia, "Bwana, kama ungelikuwa hapa, ndugu yangu asingelikufa."
\s5
\v 33 Yesu alipomuona analia, na Wayahudi waliokuja pamoja naye walikuwa wakilia pia, aliomboleza katika roho na kufadhaika;
\v 34 akasema, "Mmemlaza wapi? wakamwambia, Bwana, njoo utazame."
\v 35 Yesu akalia.
\s5
\v 36 Ndipo Wayahudi wakasema, "Angalia alivyompenda Lazaro!"
\v 37 Lakini wengine kati yao wakasema, "Siyo huyu, mtu aliyeyafumbua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya huyu mtu asife?"
\s5
\v 38 Ndipo Yesu, hali akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.
\v 39 Yesu akasema, "Liondoweni jiwe." Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, "Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne."
\v 40 Yesu akamwambia, "Mimi sikukuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?"
\s5
\v 41 Kwa hiyo wakaliondoa jiwe. Yesu akainua macho yake juu na kusema, "Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikiliza.
\v 42 Nilijua kwamba unanisikia mara zote, lakini ni kwa sababu ya kusanyiko ambalo limesimama kunizunguka kwamba nimesema haya, ili kwamba wapate kuamini kuwa wewe umenituma."
\s5
\v 43 Baada ya kusema haya, alilia kwa sauti kubwa, "Lazaro, toka nje!"
\v 44 Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa." Yesu akawaambia, "Mfungueni mkamwache aende."
\s5
\v 45 Ndipo Wayahudi wengi waliokuja kwa Mariamu na kuona Yesu alichofanya, walimwamini;
\v 46 lakini baadhi yao walienda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo aliyoyafanya Yesu.
\s5
\v 47 Ndipo wakuu wa Makuhani na Mafarisayo wakakusanyika pamoja katika baraza na kusema, "Tutafanya nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi.
\v 48 Ikiwa tutamwacha hivi peke yake, wote watamwamini; Warumi watakuja na kuchukua vyote mahali petu na taifa letu."
\s5
\v 49 Hata hivyo, mtu mmoja kati yao, Kayafa, aliyekuwa kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, " Hamjui chochote kabisa.
\v 50 Hamfikirii kwamba yafaa kwa ajili yenu kwamba mtu mmoja yapasa kufa kwa ajili ya watu kuliko taifa lote kuangamia."
\s5
\v 51 Haya hakuyasema kwa sababu yake mwenyewe, badala yake, kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa;
\v 52 na si kwa taifa peke yake, bali Yesu apate vile vile kuwakusanya watoto wa Mungu ambao wametawanyika sehemu mbali mbali.
\v 53 Kwa hiyo kuanzia siku hiyo na kuendelea wakapanga namna ya kumwua Yesu.
\s5
\v 54 Yesu hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bali aliondoka hapo na kwenda nchi iliyo karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Hapo alikaa na wanafunzi.
\v 55 Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, na wengi wakapanda kwenda Yerusalemu nje ya mji kabla ya Pasaka ili wapate kujitakasa wenyewe.
\s5
\v 56 Walikuwa wakimtafuta Yesu, na kuzungumza kila mmoja walipokuwa wamesimama hekaluni, "Mnafikiri nini? Kwamba hatakuja katika sikukuu?"
\v 57 Wakati huu wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba ikiwa mmoja atajua Yesu alipo, anapaswa kutoa taarifa ili kwamba wapate kumkamata.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu.
\v 2 Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu.
\v 3 Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.
\s5
\v 4 Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi wake, ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
\v 5 "Kwanini manukato haya yasingeuzwa kwa dinari mia tatu na wakapewa maskini?"
\v 6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 7 Yesu alisema, "Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
\v 8 Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote."
\s5
\v 9 Basi umati mkubwa wa Wayahudi walipata kujua ya kuwa Yesu yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila wamwone na Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka katika wafu.
\v 10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri ili wamue Lazaro;
\v 11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walienda zao na wakamwamini Yesu.
\s5
\v 12 Na siku ya pili yake umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
\v 13 walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, "Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli."
\s5
\v 14 Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,
\v 15 "Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda."
\s5
\v 16 Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.
\s5
\v 17 Basi lile kundi la watu waliokuwepo pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, wakashuhudia kwa wengine.
\v 18 Na ilikuwa kwa sababu hii pia kwamba kundi la watu walikwenda kumlaki kwasababu walisikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.
\v 19 Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, "Tazama, sasa hamwezi kufanya lolote; tazama, ulimwengu umekwenda kwake."
\s5
\v 20 Sasa baadhi ya Wayunani walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakienda kuabudu kwenye sikukuu.
\v 21 Hawa walimwendea Filipo, ambaye alitoka Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, "Bwana, sisi tunatamani kumwona Yesu."
\v 22 Filipo akaenda akamwambia Andrea; Andrea na Filipo wakaenda na kumwambia Yesu.
\s5
\v 23 Yesu akawajibu akasema, "Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
\v 24 Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi.
\s5
\v 25 Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele.
\v 26 Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.
\s5
\v 27 Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? 'Baba, uniokoe katika saa hii'? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii.
\v 28 Baba, ulitukuze jina lako." Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, "Nimelitukuza nami nitalitukuza tena."
\v 29 Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, "Malaika amesema naye."
\s5
\v 30 Yesu akajibu na kusema, "Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.
\v 31 Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje.
\s5
\v 32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu."
\v 33 Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.
\s5
\v 34 Mkutano wakamjibu, "Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, 'Mwana Adamu lazima ainuliwe juu'? Huyu Mwana wa Mtu ni nani?"
\v 35 Basi Yesu akawaambia, "Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako.
\v 36 Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru." Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.
\s5
\v 37 Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini
\v 38 ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: "Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?"
\s5
\v 39 Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,
\v 40 "Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya."
\s5
\v 41 Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.
\v 42 Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakatengwa na sinagogi.
\v 43 Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
\s5
\v 44 Yesu akapaza sauti na kusema, "Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi,
\v 45 naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma.
\s5
\v 46 Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
\v 47 Ikiwa mtu yeyote atayasikia maneno yangu lakini asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.
\s5
\v 48 Yeye anikataye mimi na asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
\v 49 Maana mimi sikunena kwa nafsi yangu tu. Bali ni Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
\v 50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi - kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sasa kabla ya sikukuu ya pasaka, kwa sababu Yesu alifahamu kuwa saa yake imefika ambayo atatoka katika dunia hii kwenda kwa baba, akiwa amewapenda watu wake ambao walikuwa duniani, aliwapenda upeo.
\v 2 Na ibilisi alikuwa amewekwa tayari katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.
\s5
\v 3 Yesu alifahamu kuwa baba ameweka vitu vyote katika mikono yake na kwamba ametoka kwa Mungu na alikuwa anakwenda tena kwa Mungu.
\v 4 Aliamka chakulani na akatandika chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.
\v 5 Kisha akatia maji katika bakuli na akaanza kuwaosha miguu wanafunzi wake na kuwafuta na taulo ambayo alijifunga yeye mwenyewe.
\s5
\v 6 Akaja kwa Simoni Petro, na Petro akamwambia, "Bwana, Unataka kuniosha miguu yangu?"
\v 7 Yesu akajibu na kumwambia, "Nifanyalo hulijui sasa, lakini utaelewa baadaye."
\v 8 Petro akamwambia, "Hutaniosha miguu yangu kamwe." Yesu akamjibu, "Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami."
\v 9 Simoni Petro akamwambia, "Bwana, usinioshe miguu yangu tuu, bali pia na mikono na kichwa changu."
\s5
\v 10 Yesu akamwambia, "Yeyote ambaye amekwisha kuoga haitaji kuoga isipokuwa miguu yake, na amekuwa safi mwili wake wote; ninyi mmekuwa safi, lakini si nyote."
\v 11 Kwa kuwa Yesu alijua yule atakaye msaliti; hii ndiyo sababu alisema, si nyote mmekuwa safi."
\s5
\v 12 Wakati Yesu alipokuwa amewaosha miguu yao na akiisha chukua vazi lake na kukaa tena, aliwaambia, "Je Mnaelewa kile ambacho nimewafanyia?
\v 13 Mnaniita mimi "Mwalimu" na Bwana hii mnasema kweli, maana ndivyo nilivyo.
\v 14 Ikiwa mimi Bwana na mwalimu, nimewaosha miguu yenu, ninyi pia imewapasa kuwaosha wenzenu miguu.
\v 15 Kwa kuwa nimewapa mfano ili kwamba ninyi pia mfanye kama mimi nilivyo fanya kwenu.
\s5
\v 16 Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa ni mkuu kuliko yule aliye mtuma.
\v 17 Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda.
\v 18 Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: 'Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.'
\s5
\v 19 Ninawambia hili sasa kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, muweze kuamini kuwa mimi NDIYE.
\v 20 "Amini, amini, nawambia, anipokeaye mimi humpokea ambaye nina mtuma, na yule anipokeaye mimi humpokea yule aliye nituma mimi."
\s5
\v 21 Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, "Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti."
\v 22 Wanafunzi wake wakatazamana, wakishangaa ni kwa ajili ya nani alizungumza.
\s5
\v 23 Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.
\v 24 Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, "Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza."
\v 25 Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, "Bwana, ni nani?"
\s5
\v 26 Kisha Yesu alijibu, "Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia." Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.
\v 27 Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, "Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka."
\s5
\v 28 Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.
\v 29 Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, "Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu," au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.
\v 30 Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje harak; na ilikuwa usiku.
\s5
\v 31 Wakati Yuda alipokuwa ameondoka, Yesu alisema, "Sasa mwana wa Adam ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa katika yeye.
\v 32 Mungu atamtukuza katika yeye mwenyewe, na atamtukuza haraka.
\v 33 Watoto wadogo, niko pamoja nanyi kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama nilivyowambia Wayahudi, 'Niendako, hamuwezi kuja.' sasa nawambia ninyi, pia.
\s5
\v 34 Ninawapa amri mpya, kwamba mpendane; kama mimi nilivyo wapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pia imewapasa kupendana ninyi kwa ninyi.
\v 35 Kwa ajili ya hili watu watatambua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu, ikiwa mna upendo kwa kila mmoja na mwingine."
\s5
\v 36 Simoni Petro alimwambia, "Bwana, unakwenda wapi?" Yesu akajibu, "Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye."
\v 37 Petro akamwambia, "Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako."
\v 38 Yesu akajibu, "Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu."
\s5
\c 14
\p
\v 1 "Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
\v 2 Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi ya kukaa; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.
\v 3 Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo.
\s5
\v 4 Mnajua njia mahali ninakoenda."
\v 5 Tomaso alimwambia Yesu, "Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia?
\v 6 Yesu alimwambia, " Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
\v 7 Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye."
\s5
\v 8 Philipo alimwambia Yesu, "Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha."
\v 9 Yesu akamwambia, "Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba'?
\s5
\v 10 Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.
\v 11 Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa.
\s5
\v 12 Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.
\v 13 Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
\v 14 Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.
\s5
\v 15 Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.
\v 16 Na nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele,
\v 17 Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
\s5
\v 18 Sitawaacha peke yenu; Nitarudi kwenu.
\v 19 Kwa muda kitambo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.
\v 20 Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu.
\s5
\v 21 Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye mmoja ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na Nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake."
\v 22 Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, "Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?
\s5
\v 23 Yesu alijibu akamwambia, "Kama yeyote danipendaye, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.
\v 24 Yeyote ambaye hanipendi mimi, hashiki maneno yangu. Neno ambalo mnasikia siyo langu bali la Baba ambaye alinituma.
\s5
\v 25 Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.
\v 26 Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.
\v 27 Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.
\s5
\v 28 Mlisikia vile nilivyowaambia, 'Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.' Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.
\v 29 Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.
\v 30 Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,
\v 31 lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Mimi ni mzabibu wa huu kweli, na baba yangu ni mkulima wa mzabibu.
\v 2 Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi.
\s5
\v 3 Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.
\v 4 Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu.
\s5
\v 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
\v 6 Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.
\v 7 Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.
\s5
\v 8 Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.
\v 9 Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.
\s5
\v 10 Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.
\v 11 Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.
\s5
\v 12 Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi.
\v 13 Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.
\s5
\v 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.
\v 15 Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba.
\s5
\v 16 Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
\v 17 Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.
\s5
\v 18 Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
\v 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao; Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.
\s5
\v 20 Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, 'Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.' Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, wangelishika la kwenu pia.
\v 21 Watawatendeeni mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.
\v 22 Kama nisingekuja na kuwaambia waambia, wasingalikuwa wamefanya dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
\s5
\v 23 Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.
\v 24 Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.
\v 25 Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: 'Wananichukia mimi bila sababu.'
\s5
\v 26 Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.
\v 27 Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nimewaambia mambo haya ili msiweze kukwazwa.
\v 2 Watawatoa nje ya masinagogi; hakika saa inakuja ambayo kila atakayewaua atafikiri kuwa anafanya kazi njema kwa ajili ya Mungu.
\s5
\v 3 Watawatendea mambo haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi.
\v 4 Nimewaambia mambo haya ili kwamba wakati ukifika wa haya kutokea, mnaweza kuyakumbuka na jinsi nilivyowaambia muweze wao. Sikuwaambia kuhusu mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
\s5
\v 5 Japokuwa, sasa naenda kwa yule aliyenituma; lakini hakuna kati yenu anayeniuliza, "Unaenda wapi?"
\v 6 Kwa sababu nimesema maneno haya kwenu, huzuni imejaa mioyoni mwenu.
\v 7 Hata hivyo, nawaambia ukweli: ni vyema kwenu nikiondoka; kwa maana nisipoondoka, mfariji hatakuja kwen; lakini nikienda ntamtuma kwenu.
\s5
\v 8 Akija, huyo mfariji ataubitisha ulimwengu kuhusiana na dhambi, kuhusiana na haki na kuhusiana na hukumu.
\v 9 Kuhusiana na dhambi, kwa sababu hawakuniamini mimi,
\v 10 kuhusiana na haki, kwa sababu naenda kwa baba, na hamtaniona tena;
\v 11 na kuhusiana na hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa.
\s5
\v 12 Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa.
\v 13 Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atayadhihirisha kwenu mambo yatakayokuja.
\v 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa sababu atayachukua mambo yangu na atayatangaza kwenu.
\s5
\v 15 Vitu vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; kwa hiyo, nimesema kwamba Roho atachukua mambo yangu na atayadhihirisha kwenu.
\v 16 Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi tena, mtaniona."
\s5
\v 17 Baadhi ya wanafunzi wake wakaambizana, "Ni nini anachotuambia, "muda mfupi, na hamtaniona tena,' na, kisha, mda mfupi mtaniona,' na, 'kwa sababu naenda kwa Baba?"
\v 18 Kwa hiyo wakasema, "Ni kitu gani anachosema, 'Bado mda mfupi'? Hatujui asemavyo."
\s5
\v 19 Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, "Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, 'Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona'?
\v 20 Amin, amin, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
\v 21 Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
\s5
\v 22 Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu.
\v 23 Siku hiyo hamtaniuliza maswali. Amin, Amin, nawaambia, Mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu.
\v 24 Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu ikamilike.
\s5
\v 25 Nimezungumza na ninyi kwa lugha isiyoeleweka, lakini saa inakuja ambapo sitazungumza kwa lugha isiyoeleweka lakini badala yake nitawaambia waziwazi kuhusu Baba.
\s5
\v 26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitaomba kwa Baba kwa ajili yenu;
\v 27 Kwa kuwa Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na kwa sababu mmeniamini kuwa nimetoka kwa Baba.
\v 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni; tena, naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba".
\s5
\v 29 Wanafunzi wake wakamwambia, "Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo.
\v 30 Sasa, tunajua kwamba unajua mambo yote, na hauhitaji mtu yoyote akuulize maswali. Kwa sababu hii tunaamini kuwa unatoka kwa Mungu.
\v 31 Yesu akawajibu, "Sasa mmeamini?"
\s5
\v 32 Tazama, saa inakuja, ndiyo na hakika imefika, ambapo mtatawanyika kila mmoja na kwa wa kwao mtaniacha mwenyewe. Lakini siko peke yangu kwa sababu Baba yupo nami.
\v 33 Nawaambia mambo haya ili kwamba ndani yangu muwe na amani. Duniani mna matatizo, lakini jipeni moyo, nimeushinda ulimwengu.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yesu aliyasema mambo haya; kisha akainua macho yake kuelelea mbinguni na akasema, "Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe -
\v 2 kama vile ulivyompatia mamlaka juu ya vyote vyenye mwili ili awape uzima wa milele wale wote uliompatia.
\s5
\v 3 Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo.
\v 4 Nilikutukuza hapa duniani, na kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye.
\v 5 Sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja na wewe mwenyewe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ya ulimwengu kuumbwa.
\s5
\v 6 Nililifunua jina lako kwa watu ulionipa hapa duniani. Walikuwa watu wako; lakini ulinikabidhi mimi. nao wamelishika neno lako.
\v 7 Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,
\v 8 kwa maneno yale uliyonipatia mimi-- Nimekwisha wapatia wao maneno hayo. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\s5
\v 9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.
\v 10 Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.
\v 11 Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa sisi ili wao nao wawe na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo na umoja.
\s5
\v 12 Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.
\v 13 Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
\v 14 Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
\s5
\v 15 Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
\v 16 Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
\v 17 Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
\s5
\v 18 Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
\v 19 Kwa ajili yao mimi mwenyewe ninajitoa kwako ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli.
\s5
\v 20 Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao
\v 21 ili kwamba wao nao wawe na umoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\s5
\v 22 Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa na umoja, kama vile sisi tulivyo umoja -
\v 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.
\s5
\v 24 Baba, kile ulichonipa mimi - Natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.
\s5
\v 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua wewe, lakini mimi nakujua wewe; na wanajua kwamba ulinituma.
\v 26 Nililifanya jina lako lijulikane kwao, na nitalifanya lijulikane ili kwamba lile pendo ambalo kwalo ulinipenda mimi liweze kuwa ndani yao, na mimi niweze kuwa ndani yao."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.
\v 2 Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake.
\v 3 Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.
\s5
\v 4 Naye Yesu, hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, "Ni nani mnayemtafuta?"
\v 5 Nao wakamjibu, "Yesu Mnazareth." Yesu akawaambia, "Mimi ndiye" Naye Yuda aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.
\s5
\v 6 Kwa hiyo alipowaambia, "Mimi ndiye" walirudi kinyume na kuanguka chini.
\v 7 Halafu akawauliza tena, "Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena "Yesu mnazareth."
\s5
\v 8 Yesu akawajibu, "Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende."
\v 9 Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; "Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja."
\s5
\v 10 Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
\v 11 Yesu akamwambia Petro, "Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?"
\s5
\v 12 Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
\v 13 Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.
\v 14 Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
\s5
\v 15 Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;
\v 16 lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
\s5
\v 17 Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, "Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?" Naye akasema, "Mimi siye."
\v 18 Na wale watumishi na wakuu walikuwa wakisimama mahali pale; wamekoka moto wa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.
\s5
\v 19 Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
\v 20 Yesu akamjbu, "Nimeuambia waziwazi ulimwengu; Mimi nilifundisha mara kwa mara kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.
\v 21 Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.
\s5
\v 22 Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa wakuu aliyekuwa amesimama akampiga Yesu kwa mkono wake na kisha akasema, "Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?"
\v 23 Naye Yesu akamjibu, "Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?
\v 24 Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.
\s5
\v 25 Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. "Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?" Akakana akisema "Mimi siye."
\v 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, "Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?"
\v 27 Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.
\s5
\v 28 Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
\v 29 Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. "Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?"
\v 30 Wakamjibu na kumwambia, "Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako."
\s5
\v 31 Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu." Nao Wayahudi wakamwambia, "Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote."
\v 32 Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
\s5
\v 33 Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?"
\v 34 Yesu akamjibu, "Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?"
\v 35 Naye Pilato akamjibu, "Mimi si Myahudi, au sivyo?" Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
\s5
\v 36 Yesu akajibu; "Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa" Basi
\v 37 Pilato akamwambia, "Je, wewe basi u mfalme?" Yesu akajibu, "wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
\s5
\v 38 Pilato akamwambia, "Kweli ni nini?" Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia "Siona katika lolote mtu huyu.
\v 39 Ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi."
\v 40 Kisha walipiga kelele wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba." Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Basi Pilato alimchukua Yesu na kumchapa.
\v 2 Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.
\v 3 Wakamjia na kusema, "Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao.
\s5
\v 4 Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, "Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake."
\v 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, "Tazameni mtu huyu hapa!"
\v 6 Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, "Msulubishe, msulubishe." Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake."
\s5
\v 7 Wayahudi wakamjibu Pilato, "Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu."
\v 8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
\v 9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, "Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
\s5
\v 10 Kisha Pilato akamwambia, "Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?"
\v 11 Yesu akamjibu, "Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa."
\s5
\v 12 Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, "Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cah kaisari."
\v 13 Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.
\s5
\v 14 Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni mfalme wenu huyu hapa!"
\v 15 Wakapiga kelele, "Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!" Pilato akawaambia, "Je, nimsulubishe mfalme wenu?" Naye Kuhani mkuu akajibu, "Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari."
\v 16 Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulibiwe.
\s5
\v 17 Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.
\v 18 Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao.
\s5
\v 19 Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI.
\v 20 Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.
\s5
\v 21 Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, "Usiandike, 'Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi."
\v 22 Naye Pilato akawajibu, "Niliyoandika nimeandika."
\s5
\v 23 Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
\v 24 Kisha wakasemezana wao kwa wao, "Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani." Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura."
\s5
\v 25 Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
\v 26 Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, "Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!"
\v 27 Kisha akamwambia yule mwanfunzi, "Tazama, huyu hapa mama yako. "Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
\s5
\v 28 Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, "Naona kiu."
\v 29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
\v 30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, "Imekwisha." Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
\s5
\v 31 Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
\v 32 Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
\v 33 Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.
\s5
\v 34 Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu.
\v 35 Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini.
\s5
\v 36 Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, "Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa."
\v 37 Tena andiko lingine husema, "Watamtazama yeye waliyemchoma"
\s5
\v 38 Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.
\v 39 Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja.
\s5
\v 40 Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika.
\v 41 Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo.
\v 42 Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
\v 2 Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, "wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza."
\s5
\v 3 Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini.
\v 4 Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza.
\v 5 Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani.
\s5
\v 6 Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale
\v 7 na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake.
\s5
\v 8 Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini.
\v 9 Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu.
\v 10 Kisha wanafunzi wakaenda tena nyumbani kwao.
\s5
\v 11 Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama kaburini akilia, alivyokuwa akiendelea kulia alisimama kisha akatazama kaburini.
\v 12 Akaona malaika wawili wenye sura nyeupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala.
\v 13 Nao wakamwambia, "Mwanamke, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka."
\s5
\v 14 Alipokwisha sema hayo, aligeuka na kumwona Yesu akiwa amesimama. Lakini hakutambua kama huyo alikuwa Yesu.
\v 15 Naye Yesu akamwambia, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Naye huku akidhani kuwa ni mtunza bustani akamwambia, "Bwana, kama ni wewe uliyemchukua, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."
\s5
\v 16 Yesu akamwambia, "Mariamu." Naye akageuka mwenyewe na kumwambia kwa Kiaramu, "Raboni," yaani hii ni kusema, "Mwalimu."
\v 17 Yesu akamwambia, "Usiniguse, kwani bado sijapaa kwenda kwa baba; bali uende kwa ndugu zangu ukawaambie kuwa nitapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."
\v 18 Mariamu Magdalena akaja kuwaambia wanafunzi, "Nimemwona Bwana," na kwamba amemwambia mambo haya.
\s5
\v 19 Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, "Amani iwe kwenu."
\v 20 Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi.
\s5
\v 21 Kisha Yesu akawaambia tena, "Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi."
\v 22 Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
\v 23 Yeyote mmsameheye dhambi, wamesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa."
\s5
\v 24 Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja.
\v 25 Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, "Tumemwona Bwana." Naye akawambia, "Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini."
\s5
\v 26 Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. na akasema, "Amani na iwe nanyi."
\v 27 Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye."
\s5
\v 28 Naye Thomaso akajibu na kumwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu."
\v 29 Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona."
\s5
\v 30 Kisha Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi, ambazo hazijawahi kuandikwa katika kitabu hiki;
\v 31 bali hizi zimeandikwa ili kwamba muweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu, na kwamba muaminipo muwe na uzima katika jina lake.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika Bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe:
\v 2 Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu.
\v 3 Simon Petro akawaambia, "Mimi naenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Sisi, pia tutaenda nawe." Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.
\s5
\v 4 Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu.
\v 5 Kisha Yesu akawambia, "Vijana, mna chochote cha kula?" Nao wakamjibu, "Hapana."
\v 6 Akawambia, "Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi." Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa cha samaki.
\s5
\v 7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, "Ni Bwana." Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini.
\v 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki.
\v 9 Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.
\s5
\v 10 Yesu akawambia, "Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi."
\v 11 Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.
\s5
\v 12 Yesu akawaambia, "Njoni mpate kifungua kinywa." Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, "Wewe ni nani?" Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.
\v 13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki.
\v 14 Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.
\s5
\v 15 Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, "Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?" Petro akajibu, "Ndiyo, Bwana; "Wewe wajua kuwa mimi nakupenda." Yesu akamwambia, "Lisha wanakondoo wangu."
\v 16 Akamwambia mara ya pili, "Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?" Petro akamwambia, "Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. "Yesu akamwambia, "Chunga kondoo wangu."
\s5
\v 17 Akamwambia tena mara ya tatu, "Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?" Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, "Je Wewe wanipenda?" Naye akamwambia, "Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda." Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
\v 18 Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda."
\s5
\v 19 Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, "Nifuate."
\s5
\v 20 Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, "Bwana, ni nani atakayekusaliti?"
\v 21 Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, "Bwana, Huyu mtu atafanya nini?"
\s5
\v 22 Yesu akamjibu, "Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?" Nifuate."
\v 23 Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, "Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?"
\s5
\v 24 Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
\v 25 Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.

1871
45-ACT.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1871 @@
\id ACT
\ide UTF-8
\h Matendo ya Mitume
\toc1 Matendo ya Mitume
\toc2 Matendo ya Mitume
\toc3 act
\mt Matendo ya Mitume
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kitabu cha zamani nilikiandika, Theofilo, nikisema yote Yesu aliyoanza kufanya na kufundisha,
\v 2 mpaka siku ambayo Yeye alipokelewa juu. Hii ilikuwa baada ya kutoa amri kupitia Roho Mtakatifu kwa mitume aliokuwa amewachagua.
\v 3 Baada ya mateso yake, Yeye alionekana kwao akiwa hai pia na vithibitisho vingi vikishuhudia. Kwa siku arobaini alijidhihirisha kwao, na alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu.
\s5
\v 4 Alipokuwa akikutana pamoja nao, aliwaamuru wasiondoke Yerusalemu, lakini wasubiri kwa ajili ya ahadi ya Baba, ambayo, alisema, "Mlisikia kutoka kwangu
\v 5 kwamba Yohana alibatiza kabisa kwa maji, lakini mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku hizi chache."
\s5
\v 6 Na walipokuwa wamekutanika pamoja walimuuliza, "Bwana, hivi huu ndio muda utakaowarudishia Israeli ufalme?"
\v 7 Yeye akawaambia, "Siyo sawa kwenu kujua wakati au majira ambayo Baba amekusudia kwa mamlaka yake mwenyewe."
\v 8 Lakini mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu kote katika Yerusalemu na Uyahudi yote na Samaria mpaka mwisho wa nchi."
\s5
\v 9 Bwana Yesu alipokwisha yasema haya, wakiwa wanatazama juu, Yeye aliinuliwa juu, na wingu likamfunika wasimwone kwa macho yao.
\v 10 Wakati wanatazama mbinguni kwa makini akienda, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi meupe.
\v 11 Walisema, "Enyi watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama hapa mkitazama mbinguni?" Huyu Yesu aliyepaa juu mbinguni atarudi kwa namna ile ile kama mlivyomuona akienda mbinguni.
\s5
\v 12 Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, mwendo wa siku ya Sabato.
\v 13 Walipofika walikwenda ghorofani walikokuwa wakikaa. Nao ni Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Thomaso, Batholomayo, Mathayo, Yakobo Mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda Mwana wa Yakobo.
\v 14 Wote waliungana kama mtu mmoja, kwa juhudi walikuwa wakiendelea katika maombi. Pamoja na hao walikuwepo wanawake, Mariamu Mama yake Yesu, na kaka zake.
\s5
\v 15 Katika siku zile Petro alisimama katikati ya ndugu, kama watu 120, akasema,
\v 16 Ndugu, ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe, ambapo zamani Roho Mtakatifu alisema kwa kinywa cha Daudi kuhusiana na Yuda, ambaye aliwaelekeza wale waliomkamata Yesu.
\s5
\v 17 Kwa kuwa yeye alikuwa mmoja wetu na alipokea fungu lake la faida katika hii huduma."
\v 18 (Sasa mtu huyu alinunua eneo kwa kile alichokipokea kwa uovu wake na hapo alianguka akitanguliza kichwa, mwili ukapasuka na matumbo yake yote yakawa wazi yakamwagika.
\v 19 Wote walioishi Yerusalemu walisikia kuhusu hili, hivyo eneo hilo wakaliita kwa lugha yao "Akeldama" hilo ni "shamba la damu.")
\s5
\v 20 "Kwenye kitabu cha Zaburi imeandikwa, 'Ngoja eneo lake liwe hame na isiruhusiwe hata mmoja kuishi pale;' na, 'Ruhusu mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi.'
\s5
\v 21 Hiyo ni muhimu, kwa hiyo, mmoja wa wanaume ambao waliambatana nasi wakati Bwana Yesu alipotoka na kuingia kati yetu,
\v 22 kuanzia kwenye ubatizo wa Yohana mpaka siku ile alipotwaliwa juu, lazima awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi.
\v 23 "Wakaweka mbele wanaume wawili, Yusufu aitwaye Barnaba, ambaye pia aliitwa Yusto na Mathia.
\s5
\v 24 Wao waliomba wakisema, "Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, hivyo weka wazi yupi kati ya wawili hawa ambaye umemchagua
\v 25 kuchukua nafasi katika huduma na utume, ambapo Yuda alitenda uovu na kwenda mahali pake."
\v 26 Wakapiga kura kwa ajili yao, na kura ikamwangukia Mathia ambaye alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na moja.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja.
\v 2 Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
\v 3 Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao.
\v 4 Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema.
\s5
\v 5 Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu.
\v 6 Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe.
\v 7 waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, "Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?
\s5
\v 8 Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo?
\v 9 Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,
\v 10 katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi,
\v 11 Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu."
\s5
\v 12 Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, "Hii ina maana gani?"
\v 13 Lakini wengine walidhihaki wakisema, "Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya."
\s5
\v 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, "Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
\v 15 Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
\s5
\v 16 Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli:
\v 17 Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
\s5
\v 18 Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.
\v 19 Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi.
\s5
\v 20 Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana.
\v 21 itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.'
\s5
\v 22 Watu wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mwanadamu aliyethibitishwa na Mungu kwenu kwa matendo ya uweza na maajabu, na ishara ambazo Mungu kupitia Yeye katikati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua-
\v 23 Kwa sababu ya mpango uliokusudiwa tangu mwanzo, na maarifa ya Mungu, alitolewa, na ninyi, kwa mikono ya watu wahalifu, mlimsulibisha na kumuua,
\v 24 ambaye Mungu alimwinua, akauondoa uchungu wa mauti kwake, kwasababu haikuwezekana kwake kumilikiwa na huo.
\s5
\v 25 Hivyo Daudi anasema kuhusu yeye, 'Nilimwona Bwana daima mbele ya uso wangu, yeye yuko mkono wangu wa kulia hivyo basi sitasogezwa.
\v 26 Kwa hiyo moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulifurahishwa. Pia mwili wangu utaishi katika ujasiri.
\s5
\v 27 Hutaiacha nafsi yangu iende kuzimu, wala hutaruhusu Mtakatifu wako kuona uozo.
\v 28 Wewe umedhihirisha kwangu njia za uzima; utanifanya nijae furaha mbele ya uso wako.'
\s5
\v 29 Ndugu, ninaweza kuzungumza kwenu kwa ujasiri kuhusu baba yetu Daudi: yeye alikufa na akazikwa, na kaburi lake liko pamoja nasi hata hivi leo.
\v 30 Hivyo, alikuwa nabii na alijua kuwa Mungu alishaapa kwa kiapo kwake, kwamba ataweka mmoja katika uzao wake kwenye kiti cha enzi.
\v 31 Aliliona hili mapema, na akasema kuhusu ufufuo wa Kristo, 'wala alikuwa hakuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuoza.'
\s5
\v 32 Huyu Yesu - Mungu alimfufua, ambaye sisi wote ni mashahidi.
\v 33 Kwa hiyo, akiwa ameinuliwa katika mkono wa kuume wa Mungu, na akiwa amepokea ahadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba, yeye amemimina hii ahadi, ambaye ninyi mnaona na kusikia.
\s5
\v 34 Kwani Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, 'BWANA alisema kwa Bwana wangu,
\v 35 "keti mkono wangu wa kulia, mpaka nitakapowafanya adui zako kigoda kwa ajili ya miguu yako.
\v 36 Kwa hiyo nyumba yote ya Israeli na ijue kwa hakika kwamba Mungu amemfanya Yeye kuwa Bwana na Kristo, huyu Yesu ambaye mlimsulibisha."
\s5
\v 37 Sasa waliposikia hivyo, wakachomwa katika mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, "Ndugu, tufanyeje?"
\v 38 Na Petro akawaambia, "Tubuni na Mbatizwe, kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zenu, na mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.
\v 39 Kwani kwenu ni ahadi na kwa watoto wenu na kwa wale wote walioko mbali, watu wengi kwa kadri Bwana Mungu wetu atakavyowaita."
\s5
\v 40 Kwa maneno mengi alishuhudia na kuwasihi; alisema, "Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu."
\v 41 Ndipo wakayapokea maneno yake na wakabatizwa, hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama nafsi elfu tatu.
\v 42 Wakaendelea katika mafundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.
\s5
\v 43 Hofu ikaja juu ya kila nafsi, na maajabu mengi na ishara zikafanyika kupitia mitume.
\v 44 Wote walioamini walikuwa pamoja na kuwa na vitu vyao kwa pamoja,
\v 45 na waliuza vitu na milki zao na kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.
\s5
\v 46 Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu, na walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na unyenyekevu wa moyo;
\v 47 walimsifu Mungu na wakiwa na kibali na watu wote. Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa Peter na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa.
\v 2 Mtu fulani, kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu uitwao mzuri, ili aweze kuomba sadaka kutoka kwa watu waliokuwa wakielekea hekaluni.
\v 3 Alipowaona Petro na Yohana wanakaribia kuingia hekaluni, aliomba sadaka.
\s5
\v 4 Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, alisema,"tutazame sisi."
\v 5 Kiwete akawatazama, akitazamia kupokea kitu fulani kutoka kwao.
\v 6 Lakini Petro akasema, "fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitatoa kwako. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea."
\s5
\v 7 Petro akamchukua kwa mkono wake wa kulia, na akamwinua juu: mara moja miguu yake na vifundo vya mifupa yake vikapata nguvu.
\v 8 Akiruka juu, mtu kiwete alisimama na akaanza kutembea; akaingia hekaluni pamoja na Petro na Yohana, akitembea, akiruka, na kumsifu Mungu.
\s5
\v 9 Watu wote walimwona akitembea na akimsifu Mungu.
\v 10 Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu ambaye alikuwa akikaa akiomba sadaka kwenye mlango mzuri wa hekalu; walijawa na mshangao na kustaajabu kwa sababu ya kile kilichotokea kwake.
\s5
\v 11 Namna alivyokuwa amewashikilia Petro na Yohana, watu wote kwa pamoja wakakimbilia kwenye ukumbi uitwao wa Sulemani, wakishangaa sana.
\v 12 Petro alipoliona hili, yeye akawajibu watu, "Enyi watu wa Israel, kwa nini mnashangaa? Kwa nini mnayaelekeza macho yenu kwetu, kama kwamba tumemfanya huyu atembee kwa nguvu zetu wenyewe au uchaji wetu?."
\s5
\v 13 Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu. Huyu ndiye ambaye ninyi mlimkabidhi na kumkataa mbele ya uso wa Pilato, japo yeye alikuwa ameamua kumwachia huru.
\v 14 Mlimkataa Mtakatifu na Mwenye Haki, na badala yake mkataka muuaji aachwe huru.
\s5
\v 15 Ninyi mlimuua Mfalme wa uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu - Sisi ni mashahidi wa hili.
\v 16 Sasa, kwa imani katika jina lake, mtu huyu ambaye mnamwona na kujua, alifanywa kuwa na nguvu. Imani ambayo inapitia kwa Yesu imempa yeye afya hii kamilifu, mbele yenu ninyi nyote.
\s5
\v 17 Sasa, Ndugu, najua kwamba mlitenda katika ujinga, ndivyo pia walivyofanya viongozi wenu.
\v 18 Lakini mambo ambayo Mungu aliwaambia mapema kwa vinywa vya manabii wote, kwamba huyu Kristo atateseka, sasa ameyatimiza.
\s5
\v 19 Kwa hiyo, tubuni na mgeuke, ili kwamba dhambi zenu ziweze kuondolewa kabisa, kusudi zije nyakati za kuburudika kutokana na uwepo wa Bwana;
\v 20 na kwamba aweze kumtuma Kristo ambaye ameshateuliwa kwa ajili yenu, Yesu.
\s5
\v 21 Yeye ndiye ambaye lazima mbingu zimpokee mpaka wakati wa kurejeshwa kwa vitu vyote, ambavyo Mungu alizungumzia zamani za kale kwa vinywa vya manabii watakatifu.
\v 22 Hakika Musa alisema, 'Bwana Mungu atainua nabii kama mimi kutoka katika ndugu zenu. Mtamsikiliza kila kitu ambacho atawaambia ninyi.
\v 23 Itatokea kwamba kila mtu ambaye hasikilizi kwa nabii huyo ataangamizwa kabisa atoke kati ya watu.'
\s5
\v 24 Ndiyo, na manabii wote tokea Samweli na wale waliofuata baada yake, walizungumza na walitangaza siku hizi.
\v 25 Ninyi ni wana wa manabii na wa agano ambalo Mungu alilifanya pamoja na mababu, kama alivyosema kwa Abrahamu, 'Katika mbegu yako familia zote za dunia zitabarikiwa.'
\v 26 Baada ya Mungu kumwinua mtumishi wake, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki ninyi kwa kugeuka kutoka katika uovu wenu."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakizungumza na watu, makuhani na mlinzi wa hekalu na masadukayo waliwaendea.
\v 2 Walikuwa wameudhika sana kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wanawafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
\v 3 Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni.
\v 4 Lakini watu wengi waliokuwa wamesikia ujumbe waliamini; na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini walikadiliwa kuwa elfu tano.
\s5
\v 5 Hata ilipofika asubuhi siku iliyofuata, kwamba wakuu wao, wazee na waandishi, kwa pamoja walikusanyika Yerusalemu.
\v 6 Anasi kuhani mkuu alikuwepo, na Kayafa, na Yohana, na Iskanda, na wote waliokuwa ni ndugu wa kuhani mkuu.
\v 7 Walipokuwa wamewaweka Petro na Yohana katikati yao, waliwauliza, "Kwa uwezo gani, au kwa jina gani mmefanya hili?"
\s5
\v 8 Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akawaambia, "Ninyi wakuu wa watu, na wazee,
\v 9 kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa - kwa namna gani mtu huyu alifanywa mzima?
\v 10 Hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel, kwamba kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye mlimsulibisha, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, ni kwa njia yake kwamba mtu huyu anasimama hapa mbele yenu akiwa mwenye afya.
\s5
\v 11 Yesu Kristo ni jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilidharau, lakini ambalo limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni.
\v 12 Hakuna wokovu katika mtu mwingine awaye yote. Kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa watu, ambalo kwa hilo tunaweza kuokolewa."
\s5
\v 13 Sasa walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na wakagundua kwamba walikuwa ni watu wakawaida wasio na elimu, walishangaa, wakafahamu kwamba Petro na Yohana wamekuwa pamoja na Yesu.
\v 14 Kwa sababu walimwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao, hawakuwa na kitu cha kusema dhidi ya hili.
\s5
\v 15 Lakini walipokuwa wamekwisha kuwaamuru mitume waondoke mbele ya mkutano wa baraza, walizungumza wao kwa wao.
\v 16 Walisema, tutawafanyaje watu hawa? Ni kweli kwamba muujiza wa ajabu umefanyika kupitia wao unajulikana na kila mmoja anayeishi Yerusalemu; hatuwezi kulikataa hilo.
\v 17 Lakini, ili kwamba jambo hili lisienee miongoni mwa watu, hebu tuwaonye wasinene tena kwa mtu yeyote kwa jina hili.
\v 18 Waliwaita Petro na Yohana ndani na kuwaamuru kamwe wasinene wala kufundisha kwa jina la Yesu.
\s5
\v 19 Lakini Petro na Yohana walijibu na kuwaambia, "Kama ni sahihi machoni pa Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu, hukumuni wenyewe.
\v 20 Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo ambayo tumeyaona na kuyasikia."
\s5
\v 21 Baada ya kuwaonya sana Petro na Yohana, waliwaacha waende. Hawakuweza kupata sababu yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetendeka.
\v 22 Mtu aliyekuwa amepokea muujiza wa uponyaji alipata kuwa na umri zaidi ya miaka arobaini.
\s5
\v 23 Baada ya kuwaacha huru, Petro na Yohana walikuja kwa watu wao na kuwataarifu yote ambayo makuhani wakuu na wazee walikuwa wamewaambia.
\v 24 Walipoyasikia, walipaza sauti zao kwa pamoja kwa Mungu na kusema, "Bwana, wewe uliyeumba mbingu na dunia na bahari na kila kitu ndani yake,
\v 25 wewe ambaye, kwa Roho Mtakatifu, kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ulisema, "Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa?
\s5
\v 26 Wafalme wa dunia wamejipanga pamoja, na watawala wamekusanyika kwa pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya masihi wake."
\s5
\v 27 Ni hakika, wote Herode na Pontio Pilato, pamoja na watu wa mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika kwa pamoja katika mji huu dhidi ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, ambaye ulimpaka mafuta.
\v 28 Walikusanyika kwa pamoja kufanya yote ambayo mkono wako na mapenzi yako yaliyaamuru tangu awali kabla hayajatokea.
\s5
\v 29 Sasa, Bwana, yaangalie matisho yao, na ukawajaalie watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri wote. Ili
\v 30 kwamba unaponyosha mkono wako kuponya, ishara na maajabu viweze kutokea kupitia jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu."
\v 31 Walipomaliza kuomba, eneo ambalo walikusanyika kwa pamoja likatikiswa, na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, na walinena neno la Mungu kwa ujasili.
\s5
\v 32 Idadi kubwa ya wale walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: na hakuna hata mmoja wao aliyesema kwamba chochote alichomiliki kilikuwa cha kwake mwenyewe; badala yake walikuwa na vitu vyote shirika.
\v 33 Kwa nguvu kubwa mitume walikuwa wakiutangaza ushuhuda wao kuhusu ufufuo wa Bwana Yesu, na neema kubwa ilikuwa juu yao wote.
\s5
\v 34 Hapakuwa na mtu yeyote miongoni mwao aliyepungukiwa na mahitaji, kwa sababu watu wote waliokuwa na hati za viwanja au nyumba, waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza
\v 35 na kuviweka chini ya miguu ya mitume. Na mgawanyo ulifanywa kwa kila muumini, kulingana na kila mmoja alivyokuwa na hitaji.
\s5
\v 36 Yusufu, mlawi, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnabasi na mitume (hiyo ikitafasiriwa, ni mwana wa faraja).
\v 37 Akiwa na shamba, aliliuza na akaleta fedha, akaziweka chini ya miguu ya mitume.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Hivyo, mtu mmoja aliyeitwa Anania, na Safira mkewe, waliuza sehemu ya mali,
\v 2 na akaficha sehemu ya fedha waliyouza (mke wake pia alilijua hili), na akaleta sehemu iliyobakia na kuiweka kwenye miguu ya mitume.
\s5
\v 3 Lakini Petro akasema, "Anania, kwa nini shetani ameujaza moyo wako kusema uongo kwa Roho Mtakatifu na kuficha sehemu ya mali ya shamba?
\v 4 Wakati lilipokuwa halijauzwa, halikuwa ni mali yako? Na baada ya kuuzwa, halikuwa chini ya uamuzi wako? Ilikuwaje uwaze jambo hili moyoni mwako? Hujawadanganya wanadamu, bali umemdanganya Mungu."
\v 5 Katika kusikia maneno haya, Anania alidondoka chini na akakata roho. Na hofu kubwa iliwajia wote waliolisikia hili.
\v 6 Vijana wakaja mbele na kumtia katika sanda, na kumpeleka nje na kumzika.
\s5
\v 7 Baada ya masaa matatu hivi, mke wake aliingia ndani, asijue ni nini kilichokuwa kimetokea.
\v 8 Petro akamwambia, "Niambie, kama mliuza shamba kwa thamani hiyo." Akasema, "Ndiyo, kwa thamani hiyo."
\s5
\v 9 Kisha Petro akamwambia, "Inakuwaje kwamba mmepatana kwa pamoja kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu ya wale waliomzika mme wako iko mlangoni, na watakubeba na kukupeleka nje."
\v 10 Ghafla akadondoka miguuni pa Petro, akakata roho, na wale vijana wakaja ndani wakamkuta ameshakufa. Wakambeba kumpeleka nje, na kumzika karibu na mmewe.
\v 11 Hofu kubwa ikaja juu ya kanisa zima, na juu ya wote walioyasikia mambo haya.
\s5
\v 12 Ishara nyingi na maajabu vilikuwa vinatokea miongoni mwa watu kupitia mikono ya mitume. Walikuwa pamoja katika ukumbi wa Sulemani.
\v 13 Lakini, hakuna mtu mwingine tofauti aliyekuwa na ujasiri wa kuambatana nao; hata hivyo, walipewa heshima ya juu na watu.
\s5
\v 14 Na pia, waamini wengi walikuwa wakiongezeka kwa Bwana, idadi kubwa ya wanaume na wanawake,
\v 15 kiasi kwamba hata waliwabeba wagonjwa mitaani, na kuwalaza vitandani na kwenye makochi, ili kwamba Petro akiwa anapita, kivuli chake kiweze kushuka juu yao.
\v 16 Hapo pia, idadi kubwa ya watu walikuja kutoka miji iliyozunguka Yerusalem, wakiwaleta wagonjwa na wote waliopagawa na roho wachafu, na wote waliponywa.
\s5
\v 17 Lakini kuhani mkuu aliinuka, na wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa dhehebu la masadukayo); na walijawa na wivu
\v 18 wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume na kuwaweka ndani ya gereza la jumla.
\s5
\v 19 Na wakati wa usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya gereza na kuwaongoza nje na kusema,
\v 20 "Nendeni, mkasimame hekaluni na kuwaambia watu maneno yote ya Uzima huu."
\v 21 Waliposikia hili, waliingia hekaluni wakati wa kupambazuka na kufundisha. Lakini, kuhani mkuu alikuja na wote waliokuwa naye, na kuitisha baraza lote kwa pamoja, na wazee wote wa watu wa Israeli, na kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume.
\s5
\v 22 Lakini watumishi waliokwenda, hawakuwakuta gerezani, walirudi na kutoa taarifa,
\v 23 "Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani."
\s5
\v 24 Sasa wakati jemedari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia maneno haya, waliingiwa na shaka kubwa kwa ajili yao wakiwaza litakuwaje jambo hili.
\v 25 Kisha mmoja akaja na kuwaambia, "Watu mliowaweka gerezani wamesimama hekaluni na wanafundisha watu."
\s5
\v 26 Hivyo jemedari alienda pamoja na watumishi, na wakawaleta, lakini bila ya kufanya vurugu, kwa sababu waliwaogopa watu wangeweza kuwapiga kwa mawe.
\v 27 Walipokwisha kuwaleta, waliwaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu aliwahoji
\v 28 akisema, "Tuliwaamuru msifundishe kwa jina hili, na bado mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu, na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu."
\s5
\v 29 Lakini Petro na mitume wakajibu, "Lazima tumtii Mungu kuliko watu.
\v 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, mliyemuua, kwa kumtundika juu ya mti.
\v 31 Mungu alimtukuza katika mkono wake wa kuume, na kumfanya kuwa Mkuu na mwokozi, kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi.
\v 32 Sisi ni mashahidi wa mambo haya, na Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amemtoa kwa wale wanaomtii."
\s5
\v 33 Wajumbe wa baraza waliposikia hivi, walishikwa na hasira wakataka kuwaua mitume.
\v 34 Lakini pharisayo aliyeitwa Gamalieli, mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, alisimama na kuwaamuru mitume wachukuliwe nje kwa muda mfupi.
\s5
\v 35 Kisha akawaambia, "Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa.
\v 36 Kwa sababu, zamani zilizopita, Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu, na idadi ya watu, wapata mia nne walimfuata. Aliuawa, na wote waliokuwa wanamtii walitawanyika na kupotea.
\v 37 Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake. Naye pia alipotea na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika.
\s5
\v 38 Sasa nawaambia, jiepusheni na watu hawa na muwaache wenyewe, kwa sababu, kama mpango huu au kazi hii ni ya watu itatupwa.
\v 39 Lakini kama ni ya Mungu, hamtaweza kuwazuia; mnaweza mkajikuta hata mnashindana na Mungu." Hivyo, walishawishika na maneno yake.
\s5
\v 40 Kisha, waliwaita mitume ndani na kuwachapa na kuwaamuru wasinene kwa jina la Yesu, na wakawaacha waende zao.
\v 41 Waliondoka mbele ya baraza wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuteseka na kutoheshimiwa kwa ajili ya Jina hilo.
\v 42 Kwa hiyo, kila siku, ndani ya hekalu na kutoka nyumba hadi nyumba waliendelea kufundisha na kuhubiri Yesu kuwa ni Masihi.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Sasa katika siku hizi, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa inaongezeka, lalamiko la Wayahudi wa Kiyunani lilianza dhidi ya Waebrania, kwa sababu wajane wao walikuwa wanasahaulika katika mgao wa kila siku wa chakula.
\s5
\v 2 Mitume kumi na wawili waliwaita kusanyiko lote la wanafunzi na kusema, "Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu na kuhudumia mezani.
\v 3 Kwa hiyo, ndugu, chagueni, wanaume saba, kutoka miongoni mwenu, watu wema, waliojaa Roho na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi huduma hii.
\v 4 Na sisi, tutaendelea daima katika kuomba na katika huduma ya neno."
\s5
\v 5 Hotuba yao ikaupendeza mkutano wote. Hivyo, wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena, na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia.
\v 6 Waumini waliwaleta watu hawa mbele ya mitume, walioomba na badaye wakawawekea mikono yao.
\s5
\v 7 Hivyo, neno la Mungu lilienea; na idadi ya wanafunzi ilizidi kuongezeka huko Yesrusalem; na idadi kubwa ya makuhani wakaitii imani.
\s5
\v 8 Na Stefano, aliyejaa neema na nguvu, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa miongoni mwa watu.
\v 9 Lakini hapo wakainuka baadhi ya watu wafuasi wa Sinagogi liitwalo Sinagogi la Mahuru, na la Wakirene na la Waeskanderia, na baadhi kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa walikuwa wakihojiana na Stefano.
\s5
\v 10 Lakini, hawakuweza kushindana na hekima na Roho ambayo Stefano alikuwa akitumia katika kuzungumza.
\v 11 Kisha waliwashawishi baadhi ya watu kwa siri kusema, "Tumesikia Stefano akizungumza maneno ya kufuru dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu."
\s5
\v 12 Waliwashurutisha watu, wazee, na waandishi, na kumwendea Stefano, wakamkamata, na kumleta mbele ya baraza.
\v 13 waliwaleta mashahidi wa uongo, waliosema, "mtu huyu haachi kunena maneno mabaya dhidi ya eneo hili takatifu na sheria.
\v 14 Kwani tumemsikia akisema kwamba huyu Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali hapa na kuzibadili desturi tulizokabidhiwa na Musa."
\v 15 Kila mmoja aliyekuwa katika baraza, akaelekeza macho yake kumwangalia Stefano, nao wakauona uso wake ulikuwa kama uso wa malaika.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Kuhani mkuu akasema,"mambo haya ni ya kweli"?
\v 2 Stephano akasema, "Ndugu na mababa zangu, nisikilizeni mimi: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu wakati alipokuwa Mesopotamia, kabla hajaishi Harani,'
\v 3 akamwambia,' Ondoka katika nchi yako na jamaa zako na uende katika nchi nitakayokuonyesha'.
\s5
\v 4 Kisha akaondoka katika nchi ya Ukaldayo akaishi Harani, kutoka hapo, baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta kwenye nchi hii, wanayoishi sasa.
\v 5 Hakumpa chochote kama urithi wake, hapakuwa na sehemu hata ya kuweka mguu. Lakini Abrahamu aliahidiwa hata kabla hajapata mtoto kuwa atapewa nchi kama miliki yake na uzao wake.
\s5
\v 6 Mungu alinena naye hivi, ya kwamba wazao wake wangeishi katika nchi ya ugeni, na kwamba wenyeji wa huko watawafanya kuwa watumwa wao na kuwatenda vibaya kwa muda wa miaka mia nne.
\v 7 Na Mungu akasema, nitalihukumu taifa ambalo litawafanya mateka, na baada ya hapo watatoka na kuniabudu katika sehemu hii.'
\v 8 Na akampa Abrahamu agano la tohara, hivyo Abrahamu akawa baba wa Isaka akamtahiri siku ya nane; Isaka akawa baba wa Yakobo, na Yakobo akawa baba wa mababu zetu kumi na wawili.
\s5
\v 9 Mababu zetu wakamwonea wivu Yusufu wakamuuza katika nchi ya Misri, na Mungu alikuwa pamoja naye,
\v 10 na akamwokoa katika mateso yake, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao mfalme wa Misri. Farao akamfanya awe mtawala juu ya Misri na juu ya nyumba yake yote.
\s5
\v 11 Basi kukawa na njaa kuu na mateso mengi katika nchi ya Misri na Kanani, na baba zetu hawakupata chakula.
\v 12 Lakini Yakobo aliposikia kuna nafaka Misri, aliwatuma baba zetu kwa mara ya kwanza.
\v 13 Katika safari ya pili Yusufu akajionyesha kwa ndugu zake, familia ya Yusufu ikajulikana kwa Farao.
\s5
\v 14 Yusufu akawatuma ndugu zake kwenda kumwambia Yakobo baba yao aje Misri, pamoja na jamaa yake, jumla ya watu wote ni sabini na tano.
\v 15 Hivyo Yakobo akashuka Misri; kisha akafa yeye pamoja na baba zetu.
\v 16 Wakachukuliwa hata Shekemu wakazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alilinunua kwa vipande vya fedha kutoka kwa wana wa Hamori huko Shekemu.
\s5
\v 17 Wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimwahidi Abrahamu ulipokaribia, watu wakiwa wameongezeka huko Misri,
\v 18 wakati huo aliinuka mfalme mwingine juu ya Misri, mfalme asiyejua kuhusu Yusufu.
\v 19 Huyo mfalme mwingine akawadanganya watu wetu na kuwatenda mabaya baba zetu, na kuwatupa watoto wao wachanga ili wasiishi.
\s5
\v 20 Katika kipindi kile Musa alizaliwa; alikuwa mzuri mbele za Mungu, akalelewa miezi mitatu katika nyumba ya baba yake.
\v 21 Wakati alipotupwa, binti wa Farao alimchukua akamlea kama mwanaye.
\s5
\v 22 Musa alifundishwa mafundisho yote ya Kimisri; alikuwa na nguvu katika maneno na matendo.
\v 23 Lakini baada ya kutimiza miaka arobaini, ikamjia katika moyo wake kuwatembelea ndugu zake, wana wa Israeli.
\v 24 Alipomwona Mwisraeli akitendewa mabaya, Musa alimtetea na kulipiza kisasi aliyekuwa akimwonea kwa kumpiga Mmisiri:
\v 25 akifikiri kuwa ndugu zake watafahamu kwamba Mungu anawaokoa kwa mkono wake, lakini hawakufahamu.
\s5
\v 26 Siku iliyofuata akaenda kwa baadhi ya Waisraeli waliokuwa wanagombana; akajaribu kuwapatanisha; akisema,' Mabwana, Ninyi ni ndugu; mbona mnakoseana ninyi kwa ninyi,?
\v 27 Lakini aliyemkosea jirani yake akamsukumia mbali, na kusema, 'Nani kakufanya mtawala na muhukumu wetu?
\v 28 Wewe unataka kuniua, kama ulivyomuua Mmisri jana?"
\s5
\v 29 Musa akakimbia baada ya kusikia hivyo; akawa mgeni katika nchi ya Midiani, ambapo akawa baba wa wana wawili.
\v 30 Baada ya miaka arobaini kupita, malaika akamtokea katika jangwa la mlima Sinai, katika mwali wa moto ndani ya kichaka.
\s5
\v 31 Wakati Musa alipoona moto, alishangaa na kustaajabia kile alichokiona, na alipojaribu kukisogelea ili kukitazama, sauti ya Bwana ikamjia Ikisema,
\v 32 'Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Yakobo'. Musa alitetemeka na hakuthubutu kuangalia.
\s5
\v 33 Bwana akamwambia, 'Vua viatu vyako, sehemu uliposimama ni mahali patakatifu.
\v 34 Nimeona mateso ya watu wangu waliopo Misri; Nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka ili niwaokoe; sasa njoo, nitakutuma wewe Misri.'
\s5
\v 35 Huyu Musa ambaye waliyemkataa, wakati waliposema, 'nani kakufanya kuwa mtawala na mwamuzi wetu?'_ alikuwa ndiye ambaye Mungu alimtuma awe mtawala na mkombozi. Mungu alimtuma kwa mkono wa malaika ambaye alimtokea Musa kichakani.
\v 36 Musa aliwaongoza kutoka Misri baada ya kufanya miujiza na ishara katika Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa kipindi cha miaka arobaini.
\v 37 Ni Musa huyu ndiye aliyewambia watu wa Isiraeli kuwa, 'Mungu atawainulieni nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu, nabii kama mimi'.
\s5
\v 38 Huyu ni mtu ambaye alikuwa katika mkutano jangwani na malaika ambaye aliongea naye katika mlima Sinai. Huyu ndiye mtu ambaye alikuwa na baba zetu, huyu ni mtu ambaye alipokea neno lililo hai na kutupatia sisi.
\v 39 Huyu ni mtu ambaye baba zetu walikataa kumtii; walimsukumia mbali, na katika mioyo yao waligeukia Misri.
\v 40 Katika kipindi hicho walimwambia Haruni.'tutengenezee miungu itakayotuongoza. Huyo Musa, aliyekuwa akituongoza kutoka katika nchi ya Misri, hatujui kilichompata.'
\s5
\v 41 Hivyo wakatengeneza ndama kwa siku hizo na wakatoa sadaka kwa hiyo sananmu na wakafurahi kwa sababu ya kazi ya mikono yao.
\v 42 Lakini Mungu aliwageuza na kuwapa waabudu nyota wa angani, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha manabii, 'Je Mmenitolea mimi sadaka za wanyama mliowachinja jangwani kwa muda wa miaka arobaini, nyumba ya Israeli?
\s5
\v 43 Mmekubali hema ya kukutania ya Moleki na nyota ya mungu refani, na picha mliyoitengeneza na kuwaabudu wao: na nitawapeleka mbali zaidi ya Babeli.'
\s5
\v 44 Baba zetu walikuwa na hema ya kukutania ya ushuhuda jangwani, kama Mungu alivyoamuru alipoongea na Musa, kwamba angeitengeneza kwa mfano wa ule aliouona.
\v 45 Hili ni hema ambalo baba zetu, kwa wakati wao, waliletwa katika nchi na Joshua. Hii ilitokea wakati walipoingia kumiliki taifa ambalo Mungu aliwafukuza kabla ya uwepo wa baba zetu. Hii ilikuwa hivi hadi siku za Daudi,
\v 46 ambaye alipata kibali machoni pa Mungu,' na akaomba kutafuta makao kwa Mungu wa Yakobo.
\s5
\v 47 Lakini Selemani alimjengea nyumba ya Mungu.
\v 48 Hata hivyo Aliye Juu haishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono; hii ni kama nabii alivyosema,
\v 49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni sehemu ya kuwekea miguu yangu. Nyumba ya aina gani mtanijengea?, asema Bwana: au ni wapi sehemu yangu ya kupumzikia?
\v 50 Siyo mkono wangu uliofanya hivi vitu vyote?'
\s5
\v 51 Enyi watu wenye shingo ngumu msiotahiriwa mioyo na masikio, kila mara mnampinga Roho Mtakatifu,' mnatenda kama baba zenu walivyotenda.
\v 52 Ni nabii gani katika manabii ambaye baba zenu hawakumtesa?. Waliwaua manabii wote waliotokea kabla ya ujio wa Mmoja mwenye Haki,'na sasa mmekuwa wasaliti na wauaji wake pia,
\v 53 enyi watu mliopokea sheria ile iliyoagizwa na malaika lakini hamkuishika."
\s5
\v 54 Kisha wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya, walichomwa mioyo yao, wakamsagia meno Stefano.
\v 55 Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni kwa makini na akauona utukufu wa Mungu,' na kumwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
\v 56 Stefano akasema, "Angalia nimeona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adam amesimama mkono wa kuume wa Mungu."
\s5
\v 57 Lakini wajumbe wa baraza wakapiga kelele kwa sauti za juu, wakaziba masikio yao, wakamkimbilia kwa pamoja,
\v 58 wakamtupa nje ya mji na wakampiga mawe: na mashahidi wakavua nguo zao za nje na kuweka chini karibu na miguu ya kijana aliyeitwa Sauli.
\s5
\v 59 Walipokuwa wakimpiga mawe Stefano, aliendelea kumwita Bwana na kusema, "Bwana Yesu, pokea roho yangu,".
\v 60 Akapiga magoti na kuita kwa sauti kubwa, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii. "Aliposema haya, akakata roho.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. siku hiyo ndipo alipoanza kuwatesa kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote waliotawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume.
\v 2 Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake.
\v 3 Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwaburuza nje wanawake na waume, na kuwatupia gerezani.
\s5
\v 4 waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walilihubiri neno.
\v 5 Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko.
\s5
\v 6 Baada ya makutano kusikia na kuona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichosema.
\v 7 Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa, na wengi waliopooza na viwete waliponywa.
\v 8 Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.
\s5
\v 9 Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu.
\v 10 Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;"mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu."
\v 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.
\s5
\v 12 Lakini wakati walipoamini kuwa Filipo alihubiri juu ya ufalme wa Mungu na juu ya jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanaume kwa wanawake.
\v 13 Na Simoni mwenyewe aliamini: baada ya kubatizwa, aliendelea kuwa na Filipo; alipoona ishara na miujiza iliyokuwa ikitendeka, alishangaa.
\s5
\v 14 Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana.
\v 15 Wakati walipokuwa wakishuka wakawaombea; kwamba wampokee Roho Mtakatifu.
\v 16 Mpaka muda huo, Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
\v 17 Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
\s5
\v 18 Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa,
\v 19 Akasema, "Nipeni hii nguvu, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu."
\s5
\v 20 Lakini Petro akamwambia; pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali, kwa sababu umedhani kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa.
\v 21 Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu.
\v 22 Hivyo basi tubu maovu yako na kumwomba Mungu labda utasamehewe fikra za moyo wako.
\v 23 Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi."
\s5
\v 24 Simoni akajibu na kusema, "Mwombeni Bwana kwa ajili yangu, kwa kuwa mambo yote mliyozungumza yaweza kunitokea.
\s5
\v 25 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wameshuhudia na kuhubiri neno la Bwana, walirudi Yerusalemu kwa njia hiyo; walihubiri injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.
\s5
\v 26 Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, "Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza." ( Njia hii iko katika jangwa).
\v 27 Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu.
\v 28 Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.
\s5
\v 29 Roho akasema na Filipo, "Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo.
\v 30 "Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?"
\v 31 Muethiopia akasema, "nitawezaje mtu asiponiongoza?" Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye.
\s5
\v 32 Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake:
\v 33 Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi."
\s5
\v 34 Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, "nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine"?.
\v 35 Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu.
\s5
\v 36 Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, "Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?,
\v 37 maneno haya, "Hivyo Muethiopia akajibu "naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu," hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame.
\v 38 Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza.
\s5
\v 39 Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia.
\v 40 Lakini Philipo akatokea Azoto. Alipita katika mkoa ule na kuhubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Lakini Sauli, aliendelea kusema vitisho hata vya kifo kwa wanafunzi wa Bwana, alikwenda kwa kuhani mkuu
\v 2 na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
\s5
\v 3 Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,'
\v 4 naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia,"Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?"
\s5
\v 5 Sauli akajibu, U nani wewe Bwana? Bwana akasema, " Mimi ndiye Yesu unayeniudhi;
\v 6 Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda
\v 7 Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakatulia kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu.
\s5
\v 8 Sauli akainuka katika nchi na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
\v 9 Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi.
\s5
\v 10 Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania, Bwana alisema naye katika maono, "Anania." Na akasema, "Tazama, nipo hapa, Bwana.
\v 11 "Bwana akamwambia, "Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba;
\v 12 na alimwona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili kwamba apate kuona.
\s5
\v 13 Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, kwa kiasi gani alivyowatendea mabaya watakatifu wa huko Yerusalemu;
\v 14 Hapa ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja anayeliitia jina lako.
\v 15 Lakini Bwana akamwambia, "Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, alichukue jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Israeli.
\v 16 Maana nitawaonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu".
\s5
\v 17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.
\v 18 Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu.
\v 19 Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi.
\s5
\v 20 Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
\v 21 Na wote waliosikia walishangaa na kusema, "Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani."
\v 22 Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri na kuwafanya Wayahudi waliokaa Dameski wachanganyikiwe na kuthibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
\s5
\v 23 Baada ya siku nyingi, Wayahudi wakafanya shauri pamoja ili wamuue.
\v 24 Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.
\v 25 Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu.
\s5
\v 26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi.
\v 27 Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, Na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyosema nae, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski.
\s5
\v 28 Alikutana nao walipoingia na kutoka Yerusalemu. Akanena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu,
\v 29 akihojiana na Wayahudi wa Kiyunani lakini wakijaribu mara kwa mara kumuua.
\v 30 Wakati ndugu walipojua jambo hilo, wakamchukua mpaka Kaisaria, na wampeleke aende Tarso.
\s5
\v 31 Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na kutembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi.
\v 32 Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, akawateremkia waumini waishio katika mji wa Lida.
\s5
\v 33 Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, mtu huyo amekuwa kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.
\v 34 Petro akamwambia, "Ainea, Yesu Kristo akuponye; Amka na ujitandikia kitanda chako," Mara akaamka.
\v 35 Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni walipomuona mtu huyo, walimgeukia Bwana.
\s5
\v 36 Palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha, ambalo lilitafsiriwa kama "Dorcas" Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya rehema aliyoyafanya kwa maskini.
\v 37 Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza..
\s5
\v 38 Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, "Njoo kwetu bila kuchelewa".
\v 39 Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha koti na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati akiwa pamoja nao.
\s5
\v 40 Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, "Tabitha, amka". Akafungua macho yake na alipomwona Petro akakaa chini.
\v 41 Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita waamini na wajane, akawakabidhi kwao akiwa hai
\v 42 Jambo hili likajulikana Yafa yote, na watu wengi wakamwamini Bwana.
\v 43 Ilitokea Petro akakaa siku nyingi Yafa pamoja na mtu aitwaye Simoni, mtengeneza ngozi.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kulikuwa na mtu fulani katika mji wa kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia.
\v 2 Alikuwa mchamungu na alimwabudu Mungu na nyumba yake yote; alitoa pesa nyingi kwa wayahudi na aliomba kwa Mungu siku zote.
\s5
\v 3 Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia "Kornelio!
\v 4 Kornelio akamwangalia malaika na alikuwa na hofu kubwa sana akasema "Hii ni nini mkuu?" Malaika akamwambia "Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu".
\v 5 Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu mmoja anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro.
\v 6 Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari."
\s5
\v 7 Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka, Kornelio akawaita watumishi wa nyumbani kwake wawili, na askari aliyekuwa akimwabudu Mungu kati ya maaskari waliokuwa wanamtumikia.
\v 8 Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.
\s5
\v 9 Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
\v 10 Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono,
\v 11 akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne.
\v 12 Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.
\s5
\v 13 Tena sauti ikasema kwake "Amka, Petro chinja na ule".
\v 14 Lakini Petro akasema "Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu.
\v 15 Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili "Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu".
\v 16 Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.
\s5
\v 17 Na wakati Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa juu ya hayo maono yanamaanisha nini, Tazama, watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakasimama mbele ya lango, wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba.
\v 18 Na wakaita na kuuliza kama Simoni ambaye pia aliitwa Petro kama alikuwa anakaa pale.
\s5
\v 19 Wakati huo Petro alipokuwa akiwaza juu ya hayo maono, Roho akasema naye, "Tazama watu watatu wanakutafuta.
\v 20 Amka na ushuke chini na uende nao. Usiogope kwenda nao, kwa sababu nimewatuma."
\v 21 Petro akashuka chini kwao na kusema "Mimi ni yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?"
\s5
\v 22 Wakasema, "Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu wa haki na hupenda kumwabudu Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, ameambiwa na malaika wa Mungu kukutuma ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako."
\v 23 Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja naye, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye.
\s5
\v 24 Siku iliyofuata walikuja Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu.
\s5
\v 25 Wakati Petro akiingia ndani, Kornelio akamlaki na kuinama hadi chini kwenye miguu yake kwa kumheshimu.
\v 26 Lakini Petro akamwinua na kusema "Simama; mimi mwenyewe pia ni mwanadamu."
\s5
\v 27 Wakati Petro akiwa anaongea naye, alienda ndani akakuta watu wamekusanyika pamoja.
\v 28 Akawaambia, "Ninyi wenyewe mnajua kuwa siyo sheria ya kiyahudi kushirikiana au kutembelewa na mtu ambaye si wa taifa hili. Lakini Mungu amenionesha mimi kuwa sipaswi kumwita mtu yeyote ni najisi au mchafu.
\v 29 Na ndiyo maana nimekuja bila kubisha, nilipotumwa kwa ajili ya hiyo. Kwa hiyo niwaulize kwa nini mlitumwa kwa ajili yangu."
\s5
\v 30 Kornelio akasema, "Siku nne zilizopita, wakati kama huu nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Nikaona mbele yangu mtu amesimama akiwa na mavazi meupe,
\v 31 Akaniambia "Kornelio maombi yako yamesikiwa na Mungu, na zawadi zako kwa masikini zimekuwa ukumbusho mbele za Mungu.
\v 32 Kwa hiyo tuma mtu Yafa na akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako, ambaye pia huitwa Petro. ambaye anaishi kwa mtengenezaji wa Ngozi mmoja aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko pembeni mwa bahari.
\v 33 Zingatia: Msatri huu, "Naya atakapokuja atasema nanyi," haumo kwenye maandiko ya kale.
\s5
\v 34 Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema "Kweli, nimeamini kuwa Mungu hawezi kuwa na upendeleo.
\v 35 Badala yake, kila taifa mtu yeyote anayemwabudu na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake.
\s5
\v 36 Unajua ujumbe alioutoa kwa watu wa Israel, alipokuwa akitangaza habari njema ya amani kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote-
\v 37 ninyi wenyewe mnajua tukio lililotokea, ambalo limetokea Yudea yote na lilianzia Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza.
\v 38 tukio lililokuwa linamhusu Yesu Kristo jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Alienda akifanya mema na kuponya wote walioteswa na ibilsi, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.
\s5
\v 39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika nchi za Uyahudi na katika Yerusalemu- huyu ni Yesu waliyemuua na kumtundika mtini.
\v 40 Huyu mtu Mungu alimfufua siku ya tatu na kumpa kujulikana,
\v 41 si kwa watu wote, lakini kwa mashahidi waliochaguliwa kabla na Mungu. - sisi wenyewe, tulio kula naye na kunywa naye baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
\s5
\v 42 Ametuagiza kuhubiri kwa watu na kushuhudia kuwa huyu ndiye ambaye Mungu alimchagua kuwa mwamuzi wa walio hai na waliokufa.
\v 43 Katika yeye manabii wote washuhudie, ili kwamba kila anayeamini katika yeye atapokea msamaha wa dhambi kupitia jina lake."
\s5
\v 44 Wakati Petro akiendelea kusema haya, Roho Mtakatifu akawajaza wote waliokuwa wakisikiliza ujumbe wake.
\v 45 Watu wale wanaohusika na kikundi cha waamini waliotahiriwa- wale wote waliokuja na Petro- walishangazwa, kwa sababu ya karama ya Roho Mtakatifu aliyemwagwa pia kwa wamataifa.
\s5
\v 46 Kwa kuwa walisikia hawa wamataifa wanaongea kwa lugha zingine na kumwabudu Mungu. Petro akajibu,
\v 47 "Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi?"
\v 48 Ndipo akawaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Baadaye wakamwomba akae nao kwa siku kadhaa.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Mitume na ndugu wale waliokuwa huko Yudea walisikia kuwa wamataifa wamelipokea neno la Mungu.
\v 2 Petro alipokuja huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa, Wakisema,
\v 3 "Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!"
\s5
\v 4 Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema,
\v 5 "Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu.
\v 6 Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani.
\s5
\v 7 Kisha nikasikia sauti ikisema nami, "Amka, Petro, chinja naj ule!"
\v 8 Nikasema, "Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu"
\v 9 Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi,
\v 10 Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.
\s5
\v 11 Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu.
\v 12 Roho akaniambia kwenda nao, na nisitofautiane nao. Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu mmoja.
\v 13 Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, "Nitume Yafa nikamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro.
\v 14 Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote."
\s5
\v 15 Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni.
\v 16 Nakumbuka maneno ya Bwana, alivyosema, "Yohana alibatiza kwa maji; lakini mtabatizwa katika Roho mtakatifu."
\s5
\v 17 Pia kama Mungu ametoa zawadi kama alizotupa sisi tulipoamini katika Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani, kwamba naweza kumpinga Mungu?
\v 18 Waliposikia mambo haya, hawakurudisha, bali walimsifu Mungu na kusema, "Mungu ametoa toba kwa ajili ya wa mataifa pia"
\s5
\v 19 Basi waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali, hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia. Waliwaambia ujumbe kuhusu Yesu peke yake kwa wayahudi na si kwa mwingine awaye yote.
\v 20 Lakini baadhi yao ni watu kutoka Kipro na Krene, walikuja Antiokia na kusema na wayunani na kumhubiri Bwana Yesu.
\v 21 Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na watu wengi waliamini na kumgeukia Bwana.
\s5
\v 22 Habari zao zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalem: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia.
\v 23 Alipokuja na kuona karama ya Mungu alifurahi; na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika mioyo yao.
\v 24 Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana.
\s5
\v 25 Baadaye Barnaba alienda Tarso kumwona Sauli.
\v 26 Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia.
\s5
\v 27 Na katika siku hizi manabii wakashuka kutoka Yerusalemu mpaka Antiokia.
\v 28 Mmoja wao ni Agabo ndilo jina lake, akasimama akiashiriwa na Roho kuwa njaa kali itatokea ulimwenguni mwote. Hii ilitokea wakati wa siku za Klaudio.
\s5
\v 29 Kwa hiyo, wanafunzi, kila mmoja alivyo fanikiwa, waliamua kupeleka misaada kwa ndugu walioko Uyahudi.
\v 30 Walifanya hivi; Walituma pesa kwa mkono wa Barnaba na Sauli.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Wakati huo mfalme Herode akanyosha mkono wake kwa baadhi ya wale wanaotoka kwenye kusanyiko ili kuwatesa.
\v 2 Akamwuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga.
\s5
\v 3 Baada ya kuona kuwa inawapendeza Wayahudi, akamkamata na Petro tena. Hii ilikuwa wakati wa mikate isiyochachwa.
\v 4 Alipomkamata, akamweka gerezani na akaweka vikosi vinne vya askari ili kumlinda, alikuwa akitarajia kumpeleka kwa watu baada ya Pasaka.
\s5
\v 5 Petro akawekwa gerezani, lakini maombi yakafanywa kwa bidii na kusanyiko kwa ajili yake kwa Mungu.
\v 6 Siku kabla Herode hajaenda kumtoa, Usiku huo Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, na walinzi mbele ya mlango walikuwa wakilinda gereza.
\s5
\v 7 Tazama, malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, "Amka haraka."ndipo minyororo aliyokuwa amefungwa ikafunguka kutoka mikononi mwake.
\v 8 Malaika akamwambia, "Vaa nguo zako na vaa viatu vyako." Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, "Vaa vazi lako na unifuate."
\s5
\v 9 Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakuamini kilichofanywa na malaika kama ni cha kweli. Alidhani anaona maono.
\v 10 Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye geti la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha.
\s5
\v 11 Petro alipojitambua, akasema, "Sasa nimeamini kuwa Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mikono ya Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi."
\v 12 Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye ni Marko; Wakristo wengi walikusanyika wakiomba.
\s5
\v 13 Alipobisha kwenye mlango wa kizuizi, mtumishi mmoja msichana anayeitwa Roda akaja kufungua.
\v 14 Alipotambua ni sauti ya Petro, kwa furaha akashindwa kuufungua mlango; badala yake, akakimbia ndani ya chumba; na kuwajulisha kuwa Petro amesimama mbele ya Mlango.
\v 15 Hivyo, Wakasema kwake, "Wewe ni mwendawazimu" lakini alikazia kuwa ni kweli ni yeye. Wakasema "Huyo ni malaika wake."
\s5
\v 16 Lakini Petro aliendelea kubisha, na walipofungua mlango, wakamwona na wakashangaa sana. Petro akawanyamazisha kwa mkono kimya kimya na akawaambia jinsi Bwana alivyomtoa kutoka Gerezani. akasema,
\v 17 "Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu zake." Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
\s5
\v 18 Kulipokuwa mchana, kukawa na huzuni kubwa kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro.
\v 19 Baada ya Herode kumtafuta na hakumwona akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. Akaenda kutoka uyahudi mpaka Kaisaria na kukaa huko.
\s5
\v 20 Herode alikuwa na hasira juu ya watu wa Tiro na Sidoni. Wakaenda kwa pamoja kwake. Wakawa na urafiki na Blasto msaidizi wa mfalme, ili awasaidie. Kisha wakaomba amani, kwa sababu nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme.
\v 21 Siku iliyokusudiwa Herode alivaa mavazi ya kifalme na kukaa kwenye kiti chake cha kifalme, na akawahutubia.
\s5
\v 22 Watu wakapiga kelele, "Hii ni sauti ya mungu wala si sauti ya mwanadamu!"
\v 23 Mara ghafla malaika akampiga, kwa sababu alikuwa hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango na akafa
\s5
\v 24 Lakini neno la Mungu likakua na kusambaa.
\v 25 Baada ya Barnaba na Sauli kukamilisha huduma yao wakatoka pale wakarejea Yerusalemu, wakamchukua na Yohana ambaye jina la kuzaliwa ni Marko.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni( ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli.
\v 2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, "Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia."
\v 3 Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.
\s5
\v 4 Kwa hiyo Barnabas na Sauli walimtii Roho Mtakatifu na walitelemka kuelekea Seleukia; Kutoka huko walisafiri baharini kuelekea kisiwa cha Kipro.
\v 5 Walipokuwa katika mji wa Salami, walilitangaza neno la Mungu katika Masinagogi ya Wayahudi. Pia walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.
\s5
\v 6 Walipokwenda katika kisiwa chote mpaka Pafo, walikuta mtu fulani mchawi, Myahudi nabii wa uongo, ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu.
\v 7 Mchawi huyu alishirikiana na Liwali Sergio Paulus, aliyekuwa mtu mwenye akili. Mtu huyu aliwaalika Barnaba na Sauli, kwa sababu alihitaji kusikia neno la Mungu.
\v 8 Lakini Elima "yule mchawi" (hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa) aliwapinga; alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani.
\s5
\v 9 Lakini Sauli aliyeitwa Paulo, alikuwa amejazwa na Roho Mtakatikfu, akamkazia macho
\v 10 na akasema "Ewe mwana wa Ibilisi, umejazwa na aina zote za udanganyifu na udhaifu. Wewe ni adui wa kila aina ya haki. Hautakoma kuzigeuza njia za Bwana, zilizonyooka, je utaweza?
\s5
\v 11 Sasa tazama, mkono wa Bwana upo juu yako, na utakuwa kipofu. Hautaliona Jua kwa muda" mara moja ukungu na giza vilianguka juu ya Elimas; alianza kuzunguka pale akiomba watu wamwongoze kwa kumshika mkono.
\v 12 Baada ya liwali kuona kilichotokea, aliamini, kwa sababu alishangazwa kwa mafundisho kuhusu Bwana.
\s5
\v 13 Sasa Paulo na rafiki zake walisafiri majini kutoka Pafo na wakafika Perge katika Pamfilia. Lakini Yohana aliwaacha na kurudi Yerusalemu.
\v 14 Paulo na rafiki yake walisafiri kutoka Perge na wakafika Antiokia ya Pisidia. Huko walikwenda katika sinagogi siku ya Sabato na kukaa chini.
\v 15 Baada ya kusoma sheria na manabii, viongozi wa sinagogi aliwatumia ujumbe wakisema, "Ndugu, kama mnao ujumbe wa kutia moyo watu hapa, semeni"
\s5
\v 16 Kwa hiyo Paulo alisimama na kuwapungia mkono; alisema, "Wanaume wa Israeli na enyi mnao mtii Mungu, sikilizeni.
\v 17 Mungu wa hawa watu wa Israeli aliwachagua baba zetu na kuwafanya watu wengi walipokaa katika nchi Misri, na kwa mkono wake kuinuliwa aliwaongoza nje yake.
\v 18 Kwa miaka arobaini aliwavumilia katika jangwa.
\s5
\v 19 Baada ya kuyaharibu mataifa saba katika nchi ya Kaanani, aliwapa watu wetu nchi yao kwa urithi.
\v 20 Matukio haya yote yalitokea zaidi ya miaka mia nne na hamsini. Baada ya vitu hivi vyote, Mungu aliwapa waamuzi mpaka Samweli Nabii.
\s5
\v 21 Baada ya haya, watu waliomba mfalme, hivyo Mungu aliwapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila la Benjamini, kuwa mfalme kwa miaka arobaini.
\v 22 Kisha baada ya Mungu kumuondoa katika ufalme, alimwinua Daudi kuwa mfalme wao. Ilikuwa ni kuhusu Daudi kwamba Mungu alisema, 'Nimempata Daudi mwana wa Yese kuwa mtu apendezwaye na moyo wangu; ambaye atafanya kila kitu nipendacho.'
\s5
\v 23 Kutoka kwenye ukoo wa mtu huyu Mungu ameiletea Israeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi kufanya.
\v 24 Hili lilianza kutokea, kabla ya Yesu kuja, Yohana kwanza alitangaza ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli.
\v 25 Naye Yohana alipokuwa akimalizia kazi yake, alisema, 'Mwanifikiri mimi ni nani? mimi si yule. Lakini sikilizeni, ajaye nyuma yangu, sisitahili kulegeza viatu vya miguu yake.'
\s5
\v 26 Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa.
\v 27 Kwa wale waishio Yerusalemu, na watawala wao, hawakumtambua kwa uhalisia, na wala hawakuutambua ujumbe wa manabii ambao husomwa kila Sabato; kwa hiyo walitimiliza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kifo Yesu.
\s5
\v 28 Japokuwa hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake, walimwomba Pilato amuue.
\v 29 Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye, walimshusha kutoka mtini na kumlaza kaburini.
\s5
\v 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu.
\v 31 Alionekana kwa siku nyingi kwa wale waliokwenda pamoja naye kutoka Galilaya kuelekea Yerusalemu. Watu hawa sasa ni mashahidi wa watu.
\s5
\v 32 Hivyo tunawaletea habari njema kuhusu ahadi walizopewa mababu zetu.
\v 33 Mungu aliweka ahadi hizi kwetu, watoto wao, katika hilo alimfufua Yesu na kumrudisha tena katika uhai. Hili pia liliandikwa katika Zaburi ya pili: 'Wewe ni Mwanangu, leo nimekuwa Baba yako'
\v 34 Pia kuhusu ukweli ni kwamba alimfufua kutoka wafu ili kwamba mwili wake usiharibike, ameongea hivi: 'Nitakupatia utakatifu na baraka halisi za Daudi'
\s5
\v 35 Hii ndiyo sababu kasema pia katika zaburi nyingine, 'Hautaruhusu mtakatifu wako kuuona uozo.'
\v 36 Kwa kuwa baada ya Daudi kutumikia mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alilala, alilazwa pamoja na baba zake, na aliuona uaharibifu,
\v 37 Lakini aliyefufuliwa na Mungu hakuuona uharibifu.
\s5
\v 38 Hivyo na ifahamike kwenu, ndugu, kupitia mtu huyu, msamaha wa dhambi umehubiriwa.
\v 39 Kwa yeye kila aaminiye anahesabiwa haki na mambo yote ambayo sheria ya Musa isingewapatia haki.
\s5
\v 40 Hivyo basi kuweni waangalifu kwamba kitu walichokiongelea manabii kisitokee kwenu:
\v 41 'Tazama, enyi mnaodharau, na mkashangae na mkaangamie; kwa vile nafanya kazi katika siku zenu, Kazi ambayo hamwezi kuiamini, hata kama mtu atawaeleza."
\s5
\v 42 Wakati Paulo na Barnaba walipoondoka, watu wakawaomba waongee maneno haya siku ya Sabato ijayo.
\v 43 Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha, Wayahudi wengi na waongofu thabiti waliwafuata Paulo na Barnaba, ambao waliongea nao na waliwahimiza waendelee katika neema ya Mungu.
\s5
\v 44 Sabato iliyofuata, karibu mji mzima ulikusanyika kusikia neno la Mungu.
\v 45 Wayahudi walipoona makutano, walijawa na wivu na kuongea maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo na walimtukana.
\s5
\v 46 Lakini Paulo na Barnaba waliongea kwa ujasiri na kusema, "Ilikuwa ni muhimu kwamba neno la Mungu liongelewe kwanza kwenu. Kwa kuwa mnalisukumia mbali kutoka kwenu nakujiona kuwa hamkusitahili uzima wa milele, angalieni tutawageukia Mataifa.
\v 47 Kama ambavyo Bwana ametuamuru, akisema, 'Nimewaweka ninyi kama nuru kwa watu wa mataifa, kwamba mlete wokovu kwa pande zote za dunia."
\s5
\v 48 Mataifa waliposikia hili, walifurahi na kulisifu neno la Bwana. Wengi waliochaguliwa kwa uzima wa milele waliamini.
\v 49 Neno la Bwana lilienea nchi yote.
\s5
\v 50 Lakini wayahudi waliwasihi waliojitoa na wanawake muhimu, pia na viongozi wa mji. Haya yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na waliwatupa nje ya mipaka ya mji.
\v 51 Lakini Paulo na Barnaba walikung'uta vumbi ya miguu yao. Kisha walienda kwenye mji wa Ikonia.
\v 52 Na wanafunzi walijawa na furaha pamoja na Roho mtakatifu.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Ikatokea ndani ya Ikonio kwamba Paulo na Barnaba waliingia pamoja ndani ya sinagogi la Wayahudi nakuongea namna ambayo kundi kubwa la watu Wayahudi na Wayunani waliamini.
\v 2 Lakini wayahudi wasiotii waliwachochea akili wamataifa na kuwafanya kuwa wabaya dhidi ya ndugu.
\s5
\v 3 Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku akitoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya hivi kwa kutoa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba.
\v 4 Lakini eneo kubwa la mji liligawanyika: baadhi ya watu walikuwa pamoja na Wayahudi, na baadhi pamoja na mitume.
\s5
\v 5 Wakati wamataifa na Wayahudi walipojaribu kuwashawishi viongozi wao kuwatendea vibaya na kuwaponda mawe Paulo na Barnaba,
\v 6 wakalitambua hilo na kukimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale,
\v 7 na huko waliihubiri injili.
\s5
\v 8 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hajawahi kutembea.
\v 9 Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa.
\v 10 Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, "Simama kwa miguu yako." Na yule mtu aliruka juu na kuanza kutembea.
\s5
\v 11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, "miungu imetushukia kwa namna ya binadamu."
\v 12 Walimwita Barnaba "Zeu," na Paulo "Herme" kwa sababu alikuwa msemaji mkuu.
\v 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka.
\s5
\v 14 Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka walikwenda nje kwenye umati, wakilia
\v 15 na kusema, "Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama za kwenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo.
\v 16 Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe.
\s5
\v 17 Lakini bado, hakuondoka pasipo shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha"
\v 18 Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka.
\s5
\v 19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa.
\v 20 Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, wakaingia mjini. Siku ya pili, aliende Derbe na Barnaba.
\s5
\v 21 Baada ya kufundisha injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikoniamu, na hadi Antiokia.
\v 22 Waliendelea kuimarisha nafsi za wanafunzi na kutiwa moyo kuendelea katika imani, akasema, "Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia mateso mengi."
\s5
\v 23 Walipo wateua kwa ajili yao wazee wa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini.
\v 24 Kisha walipita katika Pisidia, walifika Pamfilia.
\v 25 Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia.
\v 26 Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha.
\s5
\v 27 Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kusanyiko la pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa.
\v 28 Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, "msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa."
\v 2 Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa na mapambano na mjadala pamoja nao, ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili.
\s5
\v 3 Kwa hiyo, kwa kutumwa kwao na kanisa, walipitia Foinike na Samaria wakitangaza kugeuzwa nia kwa wamataifa. Walileta furaha kuu kwa ndugu wote,
\v 4 Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao.
\s5
\v 5 Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, "ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa."
\v 6 Hivyo mitume na wazee walisimama pamoja kulifikiria hili swala.
\s5
\v 7 Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama na kusema kwao, "Ndugu mwatambua kwamba kitambo kizuri kilichopita Mungu alifanya chaguo kati yenu, kwamba kwa mdomo wangu Mataifa wasikie neno la injili, na kuamini.
\v 8 Mungu, anayefahamu mioyo, anashuhudia kwao, anawapa Roho mtakatifu, kama alivyofanya kwetu;
\v 9 na hakutengeneza utofauti kati yetu na wao, akiifanya mioyo yao safi kwa imani.
\s5
\v 10 Kwa hiyo, kwa nini mnamjaribu Mungu kwamba muweke nira juu ya shingo za wanafunzi ambayo hata baba zetu wala sisi hatukuweza kustahimili?
\v 11 Lakini twaamini kwamba tutaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu, kama walivyokuwa."
\s5
\v 12 Kusanyiko lote lilinyamaza walipokua wakimsikiliza Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoa taarifa ya ishara na maajabu ambayo Mungu alifanya pamoja nao kati ya watu wa mataifa.
\s5
\v 13 Walipoacha kuongea, Yakobo alijibu akisema, "Ndugu nisikilizeni.
\v 14 Simoni ameelezea jinsi kwanza Mungu kwa neema aliwasaidia Mataifa ili kwamba ajipatie kutoka kwao watu kwa ajili ya jina lake.
\s5
\v 15 Maneno ya manabii yanakubaliana na hili kama lilivyoandikwa.
\v 16 'Baada ya mambo haya nitarudi na kuijenga tena hema ya Daudi, iliyoanguka chini; nitainua na kuhuisha uhararibifu wake,
\v 17 ili kwamba watu waliobaki wamtafute Bwana, pamoja na watu wa Mataifa walioitwa kwa jina langu.'
\v 18 Hivi ndivyo asemavyo Bwana aliyefanya mambo haya yajulikanayo tangu enzi za zamani.
\s5
\v 19 Hivyo basi, ushauri wangu ni, kwamba tusiwapatie shida watu wa Mataifa wamgeukiao Mungu;
\v 20 lakini tuandike kwao kwamba wajiepushe mbali na uharibifu wa sanamu, tamaa za uasherati, na vilivyonyongwa, na damu.
\v 21 Kutoka vizazi vya wazee kuna watu katika kila mji wahubirio na kumsoma Musa katika masinagogi kila Sabato."
\s5
\v 22 Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Silas, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba.
\v 23 Waliandika hivi, "Mitume, wazee na ndugu, kwa ndugu wa Mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu.
\s5
\v 24 Tulisika kwamba watu fulani ambao hatukuwapatia amri hiyo, walitoka kwetu na wamewataabisha kwa mafundisho yaletayo shida nafsini mwenu.
\v 25 Kwa hiyo imeonekana vyema kwetu sote kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,
\v 26 watu walio hatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 27 Kwa hiyo tumemtuma Yuda na Sila, watawaambia mambo yayo hayo.
\v 28 Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima:
\v 29 kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu vitolewavyo kwa sanamu, damu, vitu vya kunyongwa, na uasherati. Kama mtajiweka mbali na hivi, itakuwa vyema kwenu. Kwa herini."
\s5
\v 30 Hivyo basi, walivyotawanyishwa, waliteremkia Antiokia; baada ya kukusanya kusanyiko pamoja, waliwasilisha barua.
\v 31 Walipokua wameisoma, walifurahi kwa sababu ya kutiwa moyo.
\v 32 Yuda na Sila, na manabii, waliwatia moyo ndugu kwa maneno mengi na kuwatia nguvu.
\s5
\v 33 Baada ya kukaa muda fulani huko, walitawanyishwa kwa amani kutoka kwa ndugu kwa wale waliowatuma.
\v 34 [ Lakini ilionekana vyema Sila kubaki huko ]
\v 35 Lakini Paulo na wengine walikaa Antiokia pamoja na wengine wengi, ambapo walifundisha na kuhubiri neno la Bwana.
\s5
\v 36 Baada ya siku kadhaa Paulo alisema kwa Barnaba, "Na turudi sasa na kuwatembelea ndugu katika kila mji tulipohubiri neno la Bwana, na kuwaona walivyo.
\v 37 Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja nao Yohana aliyeitwa Marko.
\v 38 Lakini Paulo alifikiria haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi.
\s5
\v 39 Kisha hapo kukatokea mabishano makubwa kwa hiyo walitengana, na Barnaba alimchukua Marko na kusafiri kwa meli mpaka Kipro,
\v 40 Lakini Paulo alimchagua Sila na kuondoka, baada ya kukabidhiwa na ndugu katika neema ya Bwana.
\v 41 Na alienda kupitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Paulo pia alipokuja Derbe na Lystra; na tazama, pale palikuwepo na mwanafunzi aitwaye Timotheo, ni Kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye ni muumini na baba yake ni Mgiriki.
\v 2 Watu wa Listra na Ikonia walimshudia vizuri.
\v 3 Paulo alimtaka ili asafiri naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwako huko kwani wote walimjua kuwa baba yake ni Mgiriki.
\s5
\v 4 Walipokuwa wakienda walipita kwenye miji na kutoa maagizo kwa makanisa ili kuyatii maagizo hayo yaliandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu.
\v 5 Hivyo makanisa yakaimarishwa katika imani na walioamini wakaongezeka kwa idadi kila siku.
\s5
\v 6 Paulo na mwenzake wakaenda Firigia na Galatia, kwani Roho wa Mungu aliwakataza kuhubiri neno huko kwenye jimbo la Asia.
\v 7 Walipokaribia Misia, walijaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu akawakataza.
\v 8 Kwa hiyo wakapita Misia wakaja mpaka Mji wa Troa.
\s5
\v 9 Maono yalimtokea Paulo usiku, kulikuwa na mtu wa Makedonia amesimama, akimwita na kusema "Njoni mtusaidie huku Makedonia".
\v 10 Paulo alipoona maono, mara tukajiandaa kwenda Makedonia, akijua kwamba Mungu alituita kwenda kuwahubiria injili.
\s5
\v 11 Hivyo tukaondoka kutoka Troa, tukaenda moja kwa moja Samothrake, na siku iliyofuata tukafika mji wa Neapoli.
\v 12 Kutoka hapo tukaenda Filipi ambao ni moja ya mji wa Makedonia, mji muhimu katika wilaya na utawala wa Kirumi na tukakaa siku kadhaa.
\v 13 Siku ya Sabato, tulikwenda nje ya lango kwa njia ya mto, sehemu ambayo tulidhania kutakuwa na mahali pa kufanyia maombi. Tulikaa chini na kuongea na akinamama waliokuja pamoja.
\s5
\v 14 Mwanamke mmoja aitwaye Lidia, muuzaji wa zambarau, kutoka katika mji wa Tiatira, mwenye kumwabudu Mungu, alitusikiliza. Bwana alimfungua moyo wake na kuweka maanani maneno yaliyosemwa na Paulo.
\v 15 Baada ya kubatizwa, yeye na nyumba yake yote, alitusihi akisema " kama mmeniona kuwa mimi ni mwaminifu katika Bwana, basi nawasihi muingie na kukaa kwangu". Akatusihi sana.
\s5
\v 16 Ikawa kwamba, tulipokuwa tunaenda mahali pa kuomba, msichana mmoja aliyekuwa na pepo la utambuzi akakutana nasi. Alimletea bwana wake faida nyingi kwa kubashiri.
\v 17 Mwanamke huyu alimfuata Paulo pamoja na sisi, akipiga kelele na kusema "Hawa wanaume ni watumishi wa Mungu aliye Mkuu, wanaowatangazia ninyi habari ya wokovu".
\v 18 Alifanya hivyo kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa amekasirishwa na tendo hilo, aligeuka nyuma na kumwambia pepo, " Nakuamuru kwa Jina la Yesu umtoke ndani yake." Naye akatoka na kumwacha mara moja.
\s5
\v 19 Mabwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limeondoka, waliwakamata Paulo na Sila na kuwaburuza sokoni mbele ya wenye mamlaka.
\v 20 Walipowafikisha kwa mahakimu, walisema, "Hawa wanaume ni Wayahudi na wanasababisha ghasia kubwa katika mji wetu.
\v 21 Wanafundisha mambo ambayo siyo sheria sisi kuyapokea wala kuyafuata kama Warumi."
\s5
\v 22 Umati ukawainukia kinyume Paulo na Sila, mahakimu wakararua nguo zao na kuwavua na kuamuru wachapwe viboko
\v 23 Baada ya kuwachapa viboko vingi, waliwatupa gerezani na kumuamuru askari wa gereza kuwalinda vyema.
\v 24 Baada ya kupokea amri hiyo, askari wa gereza aliwatupa katika chumba cha ndani ya gereza na kuwafunga miguu yao kwenye sehemu alipowahifadhi.
\s5
\v 25 Wakati wa usiku wa manane, Paulo na Sila wakawa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwasikiliza,
\v 26 Ghafla kukatokea tetemeko kuu na misingi ya gereza ikatikiswa, milango ya gereza ikafunguka, na minyororo ya wafungwa wote ikalegezwa.
\s5
\v 27 Mlinzi wa Gereza aliamka kutoka usingizini na akaona milango yote ya gereza imefunguliwa; hivyo akachukua upanga wake maana alitaka kujiua kwa sababu alifikiri wafungwa wote walikwishatoroka,
\v 28 Lakini, Paulo akapiga kelele kwa sauti kuu, akisema "usijidhuru kwa sababu wote tuko mahali hapa".
\s5
\v 29 Mlinzi wa gereza aliomba taa ziletwe na akaingia ndani ya gereza kwa haraka, akitetemeka na kuogopa, akawaangukia Paulo na Sila,
\v 30 na kuwatoa nje ya gereza na kusema, "Waheshimiwa, nifanye nini ili nipate kuokoka?"
\v 31 Nao wakamwambia, "Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."
\s5
\v 32 Walinena neno la Bwana kwake, pamoja na watu wote wa nyumbani kwake,
\v 33 Mlinzi wa gereza aliwachukua usiku ule na kuwaosha sehemu walizoumia, yeye pamoja na watu wa nyumbani mwake wakabatizwa mara.
\v 34 Akawaleta Paulo na Sila nyumbani kwake na kuwatengea chakula. Naye akawa na furaha kuu pamoja na watu wa nyumbani mwake kwa sababu walimwamini Mungu.
\s5
\v 35 Ilipokuwa mchana, mahakimu walituma ujumbe kwa yule mlinzi wa gereza wakisema, "Waruhusu wale watu waende",
\v 36 Mlinzi wa gereza akamjulisha Paulo juu ya maneno hayo ya kuwa, "Mahakimu walituma ujumbe niruhusu mwondoke: hivyo tokeni nje na mwende kwa amani."
\s5
\v 37 Lakini Paulo akawaambia, "Walitupiga hadharani, watu ambao ni Warumi bila kutuhukumu na waliamua kututupa gerezani; halafu sasa wanataka kututoa kwa siri? Hapana, haitawezekana, wao wenyewe waje kututoa mahali hapa".
\v 38 Walinzi wakawajulisha mahakimu juu ya maneno hayo, mahakimu wakaogopa sana pale walipojua kuwa Paulo na Sila ni Warumi.
\v 39 Mahakimu wakaja na kuwasihi watoke, na walipowatoa nje ya gereza, waliwaomba Paulo na Sila watoke nje ya mji wao.
\s5
\v 40 Kwa hiyo Paulo na Sila wakatoka nje ya gereza wakaja nyumbani kwa Lidia. Paulo na Sila walipowaona ndugu, waliwatia moyo na kisha kuondoka katika mji huo.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Na walipopita katika miji ya Amfipoli na Apolonia, walikuja mpaka mji wa Thesalonike ambao kulikuwa na sinagogi la Wayahudi.
\v 2 Kama ilivyo kawaida ya Paulo, alienda kwao, na kwa muda wa siku tatu za Sabato alijadiliana nao juu ya maandiko.
\s5
\v 3 Alikuwa akiwafungulia maandiko na kuwaeleza kuwa, ilimpasa Kristo ateseke na kisha kufufuka tena kutoka kwa wafu. Aliwaambia, "Huyu Yesu ninayewaambia habari zake ndiye Kristo"
\v 4 Baadhi ya Wayahudi walishawishika na kuungana na Paulo na Sila, pamoja na Wagiriki wachamungu, akinamama wengi waongofu na kundi kubwa la watu.
\s5
\v 5 Lakini baadhi ya Wayahudi wasioamini, waliojawa na wivu, walienda sokoni na kuwachukuwa baadhi ya watu waovu, wakakusanya umati wa watu pamoja, na kusababisha ghasia mjini, kisha wakaivamia nyumba ya Jason, wakitaka kuwakamata Paulo na Sila ilikuwaleta mbele za watu.
\v 6 Lakini walipowakosa, walimkamata Yasoni na baadhi ya ndugu wengine na kuwapeleka mbele ya maofisa wa mji, wakipiga kelele, " Hawa wanaume walioupindua ulimwengu wamefika mpaka huku pia,
\v 7 Wanaume hawa waliokaribishwa na Yasoni wanaihalifu sheria ya Kaisari, wanasema kuna mfalme mwingine anayeitwa Yesu"
\s5
\v 8 Umati na maofisa wa mji waliposikia mambo hayo, waliingiwa na wasiwasi.
\v 9 Baada ya kuwa wamekwisha kuchukua fedha ya thamani ya ulinzi kutoka kwa Yason na wengine, waliwaachia waende.
\s5
\v 10 Usiku ule ndugu walimtuma Paulo na Sila Beroya. Na walipofika kule walikwenda katika sinagogi la Wayahudi.
\v 11 Watu wale walikuwa wenye werevu mkubwa kuliko wale watu wa Thesalonike, kwa sababu walikuwa na utayari wa kulipokea neno kwa akili zao, na kuchunguza maandiko kila siku ili kuona kama maneno yaliyonenwa ndivyo yalivyo.
\v 12 Kwa hiyo wengi wao waliamini, wakiwemo wanawake wenye ushawishi mkubwa wa Kigiriki na wanaume wengi.
\s5
\v 13 Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo anatangaza neno la Mungu huko Beroya, walienda huko na kuchochea na kisha kuanzisha ghasia kwa watu.
\v 14 Kwa haraka, ndugu wakampeleka Paulo kwa njia ya ziwa, lakini Sila na Timotheo wakabaki pale.
\v 15 Wale ndugu waliompeleka Paulo walienda naye hadi Athene, walipomwacha Paulo huko, walipokea maagizo kutoka kwake kuwa, Sila na Timotheo waje kwake kwa haraka iwezeanavyo.
\s5
\v 16 Na wakati akiwasubiri huko Athene, roho yake ilikasirishwa ndani yake kwa jinsi alivyouona mji ulivyojaa sanamu nyingi.
\v 17 Hivyo akajadiliana katika sinagogi na wayahudi wale waliomcha Mungu na kwa wale wote aliokutana nao kila siku sokoni.
\s5
\v 18 Lakini baathi ya Wanafalsafa wa Waepikureo na Wastoiko wakamkabili. Na wengine wakasema, " Ni nini anachokisema huyu mwongeaji mchanga? Wengine wakasema, "inaonekana anahubiri habari ya mungu mgeni," kwasababu anahubiri habari ya Yesu na ufufuo.
\s5
\v 19 Wakamchukua Paulo na kumleta Areopago, wakisema, "Twaweza kujua haya mafundisho mapya unayoyaongea?
\v 20 Kwasababu unaleta mambo mapya katika masikio yetu. Kwahivyo tunataka kujua haya mambo yana maana gani?"
\v 21 (Na watu wote wa Athene pamoja na wageni waliopo kwao, hutumia muda wao aidha katika kuongea na kusikiliza juu ya jambo jipya.)
\s5
\v 22 Kwa hiyo Paulo akasimama katikati ya watu wa Areopago na kusema, "Enyi watu wa Athene, naona kuwa ninyi ni watu wa dini kwa kila namna,
\v 23 Kwani katika kupita kwangu na kuangalia vitu vyenu vya kuabudu, nimeona maneno yalioandikwa kwenye moja ya madhabahu yenu, ikisema "KWA MUNGU ASIYEJULIKANA". Hivyo basi, huyo mnayemwabudu pasipokujua, ndiye ninayewajulisha ninyi.
\s5
\v 24 Mungu aliyeumba dunia na kila kitu kilichoko ndani, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hawezi kukaa katika mahekalu yaliyotengenezwa na mikono.
\v 25 Na pia hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu kwao, kwani yeye mwenyewe huwapa watu uzima na pumzi na vitu vingine vyote.
\s5
\v 26 Kupitia mtu mmoja, alifanya mataifa yote ya watu waishio juu ya uso wa dunia, na akawawekea nyakati na mipaka katika maeneo wanaoishi.
\v 27 Kwa hiyo, wanatakiwa kumtafuta Mungu, na yamkini wamfikie na kumpata, na kwa uhakika hayupo mbali na kila mmoja wetu.
\s5
\v 28 Kwake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu, kama vile mtunzi wenu mmoja wa shairi aliposema 'tu wazaliwa wake.'
\v 29 Kwa hiyo, ikiwa sisi ni wazaliwa wa Mungu, hatupaswi kufikiri kuwa uungu ni kama dhahabu, au shaba, au mawe, sanamu iliyochongwa kwa ustadi na mawazo ya watu.
\s5
\v 30 Kwa hiyo, Mungu alinyamazia nyakati zile za ujinga, lakini sasa anaamuru watu wote kila mahali wapate kutubu.
\v 31 Hii ni kwa sababu ameweka siku atakayo ihukumu dunia kwa haki kwa mtu ambaye alimchagua. Mungu alitoa uhakika wa mtu huyu kwa kila mtu pale alipomfufua katoka kwa wafu.
\s5
\v 32 Na watu wa Athene waliposikia habari ya kufufuliwa kwa wafu, baadhi yao wakamdhihaki Paulo, ila wengine wakasema "Tutakusikiliza tena kwa habari ya jambo hili"
\v 33 Baada ya hapo, Paulo akawaacha.
\v 34 Lakini baadhi ya watu waliungana naye wakaamini, akiwemo Dionisio Mwareopago, na Mwanamke anaitwa Damari na wengine pamoja nao.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya mambo hayo, Paulo aliondoka Athene kwenda Korintho.
\v 2 Huko akampata Myahudi aitwaye Akwila mtu wa kabila la Ponto, yeye na mke wake aitwaye Prisila walikuja kutoka huko Italia, kwa sababu Klaudia aliamuru Wayahudi wote waondoke Roma; Paulo akaja kwao;
\v 3 Paulo akaishi na kufanya kazi nao kwani yeye anafanya kazi inayofanana na yao. Wao walikuwa ni watengeneza mahema.
\s5
\v 4 Paulo akajadiliana nao katika sinagogi kila siku ya Sabato. Aliwashawishi Wayahudi pamoja na Wagiriki.
\v 5 Lakini Sila na Timotheo walipokuja kutoka Makedonia, Paulo alisukumwa na Roho kuwashuhudia Wayahudi kuwa Yesu ndiye Kristo.
\v 6 Wakati Wayahudi walipompinga na kumdhihaki, hivyo Paulo akakung'uta vazi lake mbele yao, na kuwaambia, "Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu wenyewe; Mimi sina hatia. Kutoka sasa na kuendelea, nawaendea Mataifa".
\s5
\v 7 Hivyo akaondoka kutoka pale akaenda kwenye nyumba ya Tito Yusto, Mtu anayemwabudu Mungu. Nyumba yake iko karibu na sinagogi.
\v 8 Krispo, kiongozi wa sinagogi pamoja na watu wa nyumbani mwake wakamwamini Bwana. Watu wengi wa Korintho waliomsikia Paulo akiongea waliamini na kubatizwa.
\s5
\v 9 Bwana akamwambia Paulo usiku kwa njia ya maono, "Usiogope, lakini ongea na usinyamaze.
\v 10 Kwani Mimi niko pamoja nawe, na hakuna atakayejaribu kukudhuru, maana nina watu wengi katika mji huu".
\v 11 Paulo akakaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha neno la Mungu miongoni mwao.
\s5
\v 12 Lakini Galio alipofanywa mtawala wa Akaya, Wayahudi walisimama pamoja kinyume na Paulo na kumpeleka mbele ya kiti cha hukumu,
\v 13 wakisema, "Mtu huyu huwashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria".
\s5
\v 14 Wakati Paulo alipokuwa akitaka kusema, Galio akawaambia Wayahudi, "Ninyi Wayahudi, kama ingelikuwa ni kosa au uhalifu, ingekuwa halali kuwashughulikia.
\v 15 Lakini kwa sababu ni maswali, yanayohusu maneno na majina, na sheria zenu, basi hukumuni ninyi wenyewe. Mimi sitamani kuwa hakimu kwa habari ya mambo hayo."
\s5
\v 16 Galio akawaamuru waondoke mbele ya kiti cha hukumu,
\v 17 Hivyo, wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Lakini Galio hakujali walichokifanya.
\s5
\v 18 Paulo, baada ya kukaa pale kwa muda mrefu, aliwaacha ndugu na kwenda kwa meli Siria pamoja na Prisila na Akwila. Kabla ya kuondoka bandarini, alinyoa nywele zake kwani alikuwa ameapa kuwa Mnadhiri.
\v 19 Walipofika Efeso, Paulo alimwacha Prisila na Akwila pale, lakini yeye mwenyewe akaingia kwenye sinagogi na kujadiliana na Wayahudi.
\s5
\v 20 Walipomwambia Paulo akae nao kwa muda mrefu, yeye alikataa.
\v 21 Lakini akaondoka kwao, akawaambia, "Nitarudi tena kwenu, ikiwa ni mapenzi ya Mungu". Baada ya hapo, akaondoka kwa meli kutoka Efeso.
\s5
\v 22 Paulo alipotua Kaisaria, alipanda kwenda kusalimia Kanisa la Yerusalemu, kisha akashuka chini kwa kanisa la Antiokia.
\v 23 Baada ya kukaa kwa muda pale, Paulo aliondoka kupitia maeneo ya Galatia na Frigia na kuwatia moyo wanafunzi wote.
\s5
\v 24 Myahudi mmoja aitwaye Apolo, aliyezaliwa huko Alexandria, alikuja Efeso. Alikuwa na ufasaha katika kuongea na hodari katika Maandiko.
\v 25 Apollo alikuwa ameelekezwa katika mafundisho ya Bwana. Kwa jinsi alivyokuwa na bidii katika roho, aliongea na kufundisha kwa usahihi mambo yanayomuhusu Yesu, ila alijua tu ubatizo wa Yohana.
\v 26 Apolo akaanza kuzungumza kwa ujasiri katika hekalu. Lakini Prisila na Akwila walipomsikia, walifanya urafiki naye na wakamwelezea juu ya njia za Mungu kwa usahihi.
\s5
\v 27 Alipotamani kuondoka kwenda Akaya, ndugu walimtia moyo na kuwaandikia barua wanafunzi walioko Akaya ili wapate kumpokea. Alipowasili, kwa neema aliwasaidia sana wale waliomini.
\v 28 Kwa nguvu zake na maarifa, Apolo aliwazidi Wayahudi hadharani akionesha kupitia maandiko ya kuwa Yesu ndiye Kristo.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko.
\v 2 Paulo akawaambia, "Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?" Wakamwambia, "Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu."
\s5
\v 3 Paul alisema, "Sasa ninyi mlibatizwaje?" Wakasema, "Katika ubatizo wa Yohana.
\v 4 Basi Paulo akajibu, "Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu."
\s5
\v 5 Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
\v 6 Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri.
\v 7 Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili.
\s5
\v 8 Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwavuta watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu.
\v 9 Lakini Wayahudi wengine walikuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea kila siku katika ukumbi wa Tirano.
\v 10 Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani.
\s5
\v 11 Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo,
\v 12 kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua leso na nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo.
\s5
\v 13 Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, "Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri."
\v 14 Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa.
\s5
\v 15 Roho wachafu wakawajibu, "Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? "
\v 16 Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.
\v 17 Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.
\s5
\v 18 Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya.
\v 19 Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.
\v 20 Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika nguvu.
\s5
\v 21 ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso, Roho akamwongoza kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, "Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia."
\v 22 Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda.
\s5
\v 23 Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia.
\v 24 Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi.
\v 25 Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, "Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi.
\s5
\v 26 Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba hakuna miungu ambayo imefanywa kwa mikono.
\v 27 Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu."
\s5
\v 28 Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, "Diana wa Waefeso ni mkuu."
\v 29 Mji wote ukajaa ghasia, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia.
\s5
\v 30 Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia.
\v 31 Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo.
\v 32 Baadhi ya watu walikuwa wakisema kitu hiki na wengine jambo lile, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja.
\s5
\v 33 Wayahudi wakamleta Iskanda nje ya umati wa watu na kumuweka juu mbele ya watu. Iskanda akatoa ishara kwa mkono wake kutoa maelezo kwa watu.
\v 34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, "Diana ni mkuu wa Wafeso."
\s5
\v 35 Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, 'Enyi wanaume wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Diana mkuu na ile picha ilivyoanguka kutoka mbinguni?
\v 36 Kuona Basi kwamba mambo haya hayatawezekana, tunapaswa kuwa na utulivu na msifanye chochote kwa haraka.
\v 37 Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu mke.
\s5
\v 38 Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri.
\v 39 Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali.
\v 40 Kwa kweli tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza.
\v 41 Baada ya kusema haya, aliwatawanya makutano.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Baada ya ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi na kuwatia moyo. Kisha kuwaaga na akaondoka kwenda Makedonia.
\v 2 Naye akiishakupita mikoa hiyo na alikuwa akiwatia moyo waamuni, akaingia Uyunani.
\v 3 Baada ya yeye kuwa pale kwa muda wa miezi mitatu, njama ziliundwa dhidi yake na Wayahudi alipokuwa akikaribia kusafiri kwa njia ya bahari kuelekea Shamu, hivyo aliazimu kurudi kupitia Makedonia.
\s5
\v 4 Walioandamana naye hadi Asia walikuwa Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea; Aristariko na Sekundo, wote kutoka waamini wa Wathesalonike; Gayo wa Derbe; Timotheo; Tikiko na Trofimo kutoka Asia.
\v 5 Lakini watu hawa wamekwisha tangulia na walikuwa wanatungojea kule Troa.
\v 6 kwa njia ya Bahari kutoka Filipi baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, na katika siku tano tukawafikia huko Troa. Tulikaa huko kwa siku saba.
\s5
\v 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.
\v 8 Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.
\s5
\v 9 Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
\v 10 Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, "Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai."
\s5
\v 11 Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka.
\v 12 Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.
\s5
\v 13 Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paul kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paul huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu.
\v 14 Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.
\s5
\v 15 Kisha sisi tukatweka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto.
\v 16 Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.
\s5
\v 17 Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa.
\v 18 Walipofika kwake, akawaambia, ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote.
\v 19 Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi.
\v 20 Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu kitu chochote ambacho kilikuwa muhimu, na jinsi mimi nilivyowafundisha wazi wazi na pia kwenda nyumba kwa nyumba.
\v 21 Mnajua jinsi mimi nilivyoendelea kuwaonya Wayahudi na Wayunani juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu.
\s5
\v 22 Na sasa, angalieni, mimi, nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko,
\v 23 ila kwa kuwa Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi katika kila mji na anasema kwamba minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea.
\v 24 Lakini mimi si kufikiria kwamba maisha yangu ni kwa njia yoyote ya thamani kwangu, ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu, kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.
\s5
\v 25 Na sasa, tazama, najua kwamba wote, miongoni mwa wale nilioenda kuwahubiri Ufalme, hamtaniona uso tena.
\v 26 Kwa hiyo nawashuhudia leo hii, kwamba sina hatia kwa damu ya mtu yeyote.
\v 27 Kwa maana sikujizuia kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.
\s5
\v 28 Kwa hiyo iweni waangalifu juu yenu ninyi wenyewe, na juu ya kundi lolote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi. Iweni waangalifu kulichunga kusanyiko la Bwana, ambalo alilinunua kwa damu yake mwenyewe.
\v 29 Najua kwamba baada ya kuondoka kwangu, mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, na wasilihurumie kundi.
\v 30 Najua kwamba hata miongoni mwenu wenyewe baadhi ya watu watakuja na kusema mambo mapotovu, ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao.
\s5
\v 31 Kwa hiyo muwe macho. Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuweza kuacha kuwafundisha kila mmoja wenu kwa machozi usiku na mchana.
\v 32 Na sasa mimi nawakabidhi kwa Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliowekwa wakfu kwa Mungu.
\s5
\v 33 Sikutamani fedha, dhahabu, au mavazi.
\v 34 Mnajua ninyi wenyewe kwamba mikono hii imenipatia mahitaji yangu mwenyewe na mahitaji ya wale waliokuwa pamoja nami.
\v 35 Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: "Ni heri kutoa kuliko kupokea."
\s5
\v 36 Baada ya kusema namna hii, alipiga magoti akaomba pamoja nao.
\v 37 Wote wakalia sana na kumwangukia Paulo shingoni na kumbusu.
\v 38 Walihuzunika zaidi ya yote kwa sababu ya kile ambacho alikuwa amesema, kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Kisha wakamsindikiza merikebuni.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Wakati tulipokua tumeachana nao, na tunasafiri baharini, tukafika moja kwa moja kwenye mji wa Kosi, na kesho yake tukafika mji wa Rodo, na kutoka huko tukafika mji wa Patara.
\v 2 Tulipopata meli inayovuka kwenda Foinike, tulipanda tukasafiri.
\s5
\v 3 Tulipofika mbele ya kisiwa cha Kipro, tukaiacha upande wa kushoto, tukasafiri hadi Siria, tukaweka nanga katika mji wa Tiro, kwa sababu huko ndiko meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
\v 4 Baada ya kuwaona wanafunzi, tukakaa huko siku saba. Wanafunzi hawa wakamwambia Paulo kupitia kwa Roho kwamba yeye asikanyage Yerusalemu.
\s5
\v 5 Hata tulipotimiza siku zile, sisi tukaondoka tukaenda zetu. Wote pamoja, na wanawake zao na watoto wao, walitusindikiza katika njia zetu hadi tulipotoka nje ya mji. Kisha tukapiga magoti pwani, tukaomba, tukaagana kila mmoja.
\v 6 Tukapanda meli, huku nao wakarudi nyumbani kwao tena.
\s5
\v 7 Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro, tukafika Tolemai. Pale tulisalimia ndugu, na kukakaa nao kwa siku moja.
\v 8 Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisaria. Sisi tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, nasi tukakaa pamoja naye.
\v 9 Mtu huyu alikuwa na mabinti wanne mabikira ambao walitabiri.
\s5
\v 10 Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa, akashuka kutoka Uyahudi nabii mmoja aitwaye Agabo.
\v 11 Yeye alikuja kwetu na akautwaa mkanda wa Paulo. kwa huo alijifunga miguu na mikono yake mwenyewe na kusema, "Roho Mtakatifu asema hivi," "Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu, nao watamkabidhi mikononi mwa watu wa mataifa."
\s5
\v 12 Tuliposikia mambo hayo, sisi na watu waliokuwa wakiishi mahali pale tulimsihi Paulo asipande kwende Yerusalemu.
\v 13 Ndipo Paulo alijibu, "Mnafanya nini, mnalia na kunivunja moyo wangu? Kwa maana niko tayari, siyo tu kufungwa, lakini pia kufia huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu."
\v 14 Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, " Basi mapenzi ya Bwana yafanyike."
\s5
\v 15 Baada ya siku hizi, tulichukua mifuko yetu na tukapanda Yerusalemu.
\v 16 Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria pia walifuatana nasi. Wakamleta mtu mmoja aitwaye Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tulikaa naye.
\s5
\v 17 Tulipofika Yerusalemu, ndugu walitukaribisha kwa furaha.
\v 18 Kesho yake Paulo alienda pamoja nasi kwa Yakobo, na wazee wote walikuwepo.
\v 19 Baada ya kuwasalimu, aliwapa taarifa moja baada ya nyingine ya mambo ambayo Mungu aliyotenda miongoni mwa mataifa kwa kupitia huduma yake.
\s5
\v 20 Wakati waliposikia hayo, wakamsifu Mungu, na wakamwambia, "Unaona, ndugu, kuna maelfu wangapi wameamini miongoni mwa Wayahudi. Wao wote wana nia ya kushika sheria.
\v 21 Wameambiwa kuhusu wewe, kwamba unafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya mataifa kuachana na Musa, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao, na wasifuate desturi za zamani.
\s5
\v 22 Tunapaswa tufanye nini? Bila shaka watasikia kwamba wewe umekuja.
\v 23 Hivyo fanya kile sisi tunachokuambia sasa: tunao watu wanne ambao wameweka nadhiri.
\v 24 Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao, na uwalipie gharama zao, ili waweze kunyoa vichwa vyao. Hivyo kila mmoja apate kujua kwamba mambo waliyoambiwa kuhusu wewe ni ya uongo. Watajifunza kwamba wewe pia unafuata sheria.
\s5
\v 25 Lakini kwa habari za mataifa ambao wamekuwa waumini, tuliandika na kutoa maagizo kwamba wanapaswa kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu, na damu, kutokana na kile kilichonyongwa, na wajiepushe na uasherati."
\v 26 Ndipo, Paulo aliwatwaa wanaume, na siku ya pili, akajitakasa mwenyewe pamoja nao, akaingia Hekaluni, kutangaza kipindi cha siku za kujitakasa, hadi sadaka itolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.
\s5
\v 27 Siku hizo saba zilipokaribia kumalizika, baadhi ya Wayahudi kutoka Asia wakamuona Paulo Hekaluni, na makutano wakakasirika, na wakamnyoshea mikono.
\v 28 Walikuwa wanapiga kelele, "Watu wa Israeli, tusaidieni. Huyu ni yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo ambayo ni kinyume na watu, sheria, na mahali hapa. Pia amewaleta Wayunani katika Hekalu na kupanajisi mahali hapa patakatifu."
\v 29 Kwa kuwa mwanzoni walikuwa wamemwona Trofimo Muefeso akiwa pamoja naye mjini, nao walidhani kwamba Paulo alimleta hekaluni.
\s5
\v 30 Mji wote ulikuwa na taharuki, na watu wakakimbia pamoja na kumkamata Paulo. Wakamtoa nje ya Hekalu, na milango mara ikafungwa.
\v 31 Walipokuwa wakijaribu kumuua, habari zilimfikia mkuu wa jeshi la walinzi kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.
\s5
\v 32 Mara hiyo akawachukua askari na jemadari akaukimbilia umati. Wakati Watu walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
\v 33 Kisha mkuu wa jeshi alimkaribia na akamshika Paulo, na akaamuru afungwe minyororo miwili. Akamuuliza yeye ni nani na amefanya nini.
\s5
\v 34 Baadhi ya watu kwenye umati walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kingine. Kwa kuwa jemadari hakuweza kuwaambia chochote kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo aletwe ndani ya ngome.
\v 35 Basi alipofika kwenye ngazi, akachukuliwa na askari kwa sababu ya ghasia za umati.
\v 36 Maana umati wa watu walimfuata na waliendelea kupiga kelele, "Mwondoeni huyu!"
\s5
\v 37 Paulo alipokuwa analetwa ndani ya ngome, alimwambia mkuu wa jeshi, "Naweza kukwambia kitu?" Yule mkuu wa jeshi akasema, "Je unaongea Kiyunani?
\v 38 Je, wewe si yule Mmisri ambaye awali aliongoza uasi na alichukua magaidi elfu nne nyikani?"
\s5
\v 39 Paulo akasema, "Mimi ni Myahudi, kutoka mji wa Tarso ya Kilikia. Mimi ni raia wa mji maarufu. Nawaomba, mniruhusu nizungumze na watu."
\v 40 Wakati jemadari alipompa ruhusa, Paulo akasimama penye ngazi na akatoa ishara kwa watu kwa mkono wake. Wakati kulipokuwa na ukimya sana, akaongea nao kwa Kihebrania. Akasema,
\s5
\c 22
\p
\v 1 "Ndugu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu nitakaofanya kwenu sasa."
\v 2 Makutano walipo sikia Paulo akiongea nao kwa kiebrania, wakanyamaza. Akasema,
\s5
\v 3 "Mimi ni myahudi, nimezaliwa mji wa Tarso eneo la Kilikia, ila nilipata elimu katika mji huu, miguuni pa Gamalieli. Nilifundishwa kulingana na njia sahihi za sheria za baba zetu. Mimi ninabidii ya Mungu, kama ninyi nyote mlivyo leo.
\v 4 Niliwatesa kwa njia hii hadi kufa; nikawafunga wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.
\v 5 Hata kuhani mkuu na wazee wote wanaweza kutoa ushahidi kwamba nilipokea barua kutoka kwao kwa ajili ya ndugu walio Dameski, kwangu mimi kusafiri kwenda huko. Ilikuwa niwalete watu Yerusalemu wa njia ile ili wafungwe na kuadhibiwa.
\s5
\v 6 Ilitokea kwamba pale nilipokua nikisafiri nakaribia Dameski, majira ya mchana ghafla nuru kuu ikatokea mbinguni ikaanza kuniangaza.
\v 7 Nikaanguka chini na kusikia sauti ikiniambia, 'Sauli, Sauli kwanini unaniudhi?'
\v 8 Nikajibu, 'wewe ni nani, Bwana?' Akaniambia, 'Mini ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.'
\s5
\v 9 Wale waliokuwa na mimi waliiona nuru, ila hawakusikia sauti ya yule alie ongea na mimi.
\v 10 Nikasema, 'Nifanye nini, Bwana?' Bwana akaniambia, 'Simama na uingie Dameski; huko utaambiwa kila kitu unachopaswa kufanya.'
\v 11 Sikuweza kuona kwa sababu ya muangaza wa nuru ile, ndipo nikaenda Dameski kwa kuongozwa na mikono ya wale waliokuwa na mimi.
\s5
\v 12 Huko nikakutana na mtu aitwaye Anania, alikuwa mtu aliyeshika sheria na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote walioishi huko.
\v 13 Akaja kwangu, akasimama mbele yangu, na kusema, 'Ndugu yangu Sauli, upate kuona.'Kwa muda ule ule nikamuona.
\s5
\v 14 Akasema, 'Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, kumuona yule mwenyehaki, na kusikia sauti itokayo kwenye kinywa chake.
\v 15 Kwa sababu utakuwa shahidi kwake kwa watu wote juu ya uliyoyaona na kusikia.
\v 16 Basi sasa kwa nini unasubiri? Amka, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliita jina lake.'
\s5
\v 17 Baada ya kurejea Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, ikatokea kwamba nikapewa maono.
\v 18 Nikamuona akiniambia, 'Hima na utoke Yerusalemu haraka, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako kuhusu mimi.'
\s5
\v 19 Nikasema, 'Bwana, wao wenyewe wanajua niliwafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini katika kila sinagogi.
\v 20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, Mimi pia nilikuwa nimesimama karibu na kukubali na nilikuwa nalinda nguo za wale waliomwua.'
\v 21 Lakini aliniambia, 'Enenda, kwa sababu mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa mataifa."'
\s5
\v 22 Watu wakamruhusu aongee juu ya neno hili. Lakini baadaye walipaza sauti na kusema, "mwondoe mtu huyu katika nchi: kwa sababu sio sahihi aishi."
\v 23 Walipokuwa wakipaza sauti, na kutupa mavazi yao na kutupa mavumbi juu,
\v 24 jemedari mkuu akaamuru Paulo aletwe ngomeni. Akaamuru aulizwe huku anapigwa mijeledi, ili yeye mwenyewe ajue kwa nini walikuwa wanampigia kelele namna ile.
\s5
\v 25 Hata walipokuwa wamemfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliye simama karibu naye, "Je! ni haki kwenu kumpiga mtu aliye Mrumi na bado hajahukumiwa?"
\v 26 Yule akida aliposikia maneno haya, akaenda kwa jemedari mkuu na kumwambia, akisema, "Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni mrumi."
\s5
\v 27 Jemedari mkuu akaja na kumwambia, "Niambie, je wewe ni raia wa Rumi?" Paulo akasema, "Ndiyo."
\v 28 Jemedari akamjibu, "Ni kupitia kiasi kikubwa cha pesa ndipo nilipata uraia." Lakini Paulo akamwambia, "Mimi ni mrumi wa kuzaliwa."
\v 29 Basi wale waliokuwa tayari kwenda kumuuliza wakaondoka na kumwacha wakati huo huo. Na jemedari naye akaogopa, alipojua kuwa Paulo ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
\s5
\v 30 Siku iliyofuatayo, jemedari mkuu alitaka kujua ukweli kuhusu mashtaka ya Wayahudi dhidi ya Paulo. Hivyo akamfungua vifungo vyake akaamuru wakuu wa makuhani na baraza lote wakutane. Akamleta Paulo chini, na kumweka katikati yao.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Paulo akawaangalia moja kwa moja watu wa baraza na kusema, "Ndugu zangu, nimeishi mbele za Mungu kwa dhamira nzuri hadi hivi leo."
\v 2 Kuhani mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake.
\v 3 Ndipo Paulo akamwambia, "Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Umekaa ukinihukumu kwa sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?"
\s5
\v 4 Wale waliokuwa wamesimama karibu naye wakasema, "Hivi ndivyo unavyomtukana kuhani mkuu wa Mungu?"
\v 5 Paulo akasema, "ndugu zangu, mimi sikujua kwamba huyu ni kuhani mkuu. Kwa kuwa imeandikwa, hutazungumza vibaya juu ya mtawala wa watu wako."
\s5
\v 6 Paulo alipoona ya kwamba upande mmoja wa baraza ni Masadukayo na wengine Mafarisayo, akapaza sauti na kusema, "ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Ni kwa sababu hii nategemea kwa ujasiri ufufuo wa wafu ninao hukumiwa nao."
\v 7 Alipoyasema haya, malumbano makubwa yakatokea baina ya Mafarisayo na Masadukayo, na mkutano ukagawanyika.
\v 8 Kwani Masadukayo husema hakuna ufufuo, malaika wala hakuna roho, ila Mafarisayo husema haya yote yapo.
\s5
\v 9 Ghasia kubwa ikatokea na baadhi ya waandishi waliokuwa upande wa Mafarisayo wakasimama na kujadili, wakisema, "hatujaona chochote kibaya dhidi ya mtu huyu. Vipi kama roho au malaika ameongea na yeye?"
\v 10 Wakati kulitokea hoja kubwa, mkuu wa majeshi aliogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipande vipande na wao, hivyo akaamuru wanajeshi washuke chini na kumchukua kwa nguvu kutoka kwa wajumbe wa baraza, na kumleta katika ngome.
\s5
\v 11 Usiku uliofuata Bwana alisimama karibu naye na kusema, "Usiogope, kwa kuwa umenishuhudia katika Yerusalemu, hivyo utatoa ushahidi pia katika Roma."
\s5
\v 12 Kulipokucha, baadhi ya Wayahudi walifanya agano na kuita laana juu yao wenyewe: walisema ya kwamba hawatakula wala kunywa chochote mpaka watakapomuua Paulo.
\v 13 Kulikuwa na watu zaidi ya arobaini ambao walifanya njama hii.
\s5
\v 14 wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee na kusema, "Tumejiweka wenyewe kwenye laana kuu, tusile chochote hadi tutakapomwua Paulo.
\v 15 Hivyo sasa, baraza limwambie jemadari mkuu amlete kwenu, kana kwamba mnaamua kesi yake kwa usahihi. Kwetu sisi tuko tayari kumwua kabla hajaja hapa."
\s5
\v 16 Lakini mtoto wa dada yake na Paulo akasikia kwamba kulikuwa na njama, akaenda akaingia ndani ya ngome na kumwambia Paulo.
\v 17 Paulo akamwita akida mmoja akasema, "Mchukue kijana huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwambia."
\s5
\v 18 Basi akida akamchukua yule kijana akampeleka kwa jemedari mkuu akamwambia, "Paulo yule mfungwa aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwako. Ana neno la kukuambia."
\v 19 Yule jemadari mkuu akamshika kwa mkono akajitenga naye kando, na akamwuliza, "Ni kitu gani unachotaka kuniambia?"
\s5
\v 20 Kijana yule akasema, "Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo kesho kwenye baraza kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahili zaidi.
\v 21 Basi wewe usikubali kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamvizia. Wamejifunga kwa laana, wasile wala wasinywe hata watakapomwua. Hata sasa wako tayari, wakisubiria kibali toka kwako."
\s5
\v 22 Basi yule jemadari mkuu akamwacha kijana aende zake, baada ya kumwagiza "usimwambie mtu yeyote ya kwamba umeniarifu haya."
\v 23 Akawaita maakida wawili akasema watayarisheni askari mia mbili kwenda Kaisaria na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, mtaondoka zamu ya tatu ya usiku.
\v 24 Akawaambia kuweka wanyama tayari ambaye Paulo atamtumia na kumchukua salama kwa Feliki Gavana.
\s5
\v 25 Akaandika barua kwa namna hii,
\v 26 Klaudio Lisia kwa Liwali mtukufu Feliki, salamu.
\v 27 Mtu huyu alikamatwa na wayahudi wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni raia wa kirumi.
\s5
\v 28 Nilitaka kujua kwa nini wamemshtaki, hivyo nikampeleka kwenye baraza.
\v 29 Nikaona kwamba alikuwa ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
\v 30 Kisha ikajulikana kwangu kwamba kuna njama dhidi yake, hivyo kwa haraka nikamtuma kwako, na kuwaagiza wanaomshitaki pia walete mashitaka dhidi yake mbele yako. Wakaagana."
\s5
\v 31 Basi wale askari wakatii amri: wakamchukua Paulo wakampeleka hata Antipatri usiku.
\v 32 Siku iliyofuata, maaskari wengi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja naye, nao wakarudi zao ngomeni.
\v 33 Na wapanda farasi walipofika Kaisaria, na kumpa liwali ile barua, wakamweka Paulo mbele yake.
\s5
\v 34 Naye liwali alipoisoma barua, alimuuliza Paulo alitokea jimbo gani; alipojua ya kwamba ni mtu wa Kilikia,
\v 35 akasema, "Nitakusikia wewe watakapo kuja wale waliokushitaki," akaamuru awekwe katika ikulu ya Herode.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Baada ya siku tano, Anania kuhani mkuu, baadhi ya wazee na msemaji mmoja aitwaye Tertulo, wakaenda pale. Watu hawa wameleta mashtaka dhidi ya Paulo kwa gavana.
\v 2 Paulo alipo simama mbele ya gavana, Tertulo akaanza kumshitaki na kusema kwa gavana, "kwa sababu yako tuna amani kuu; na kwa maono yako yanaleta mageuzi mazuri katika taifa letu;
\v 3 basi kwa shukurani yote tunapokea kila kitu ukifanyacho, Wasalam mheshimiwa Feliki.
\s5
\v 4 Lakini nisikuchoshe zaidi, nakusihi unisikilize maneno machache kwa fadhili zako.
\v 5 Kwa maana tumempata mtu huyu mkorofi, na anasababisha Wayahudi wote kuasi duniani. Tena ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazorayo. (Zingatia: Sehemu ya maneno ya mstari huu 24: 6
\v 6 Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi hivyo tukamkamata., haumo kwenye nakala bora za kale).
(Zingatia: Mstari huu
\s5
\v 7 Lisiasi, afisa, alikuja na akamchukua kwa nguvu mikononi mwetu., haumo kwenye nakala bora za maandiko ya kale).
\v 8 Ukimwuliza Paulo kuhusu mambo haya, hata utaweza kujifunza ni kitu gani tumemshtakia."
\v 9 Wayahudi nao wakamshtaki Paulo, wakisema kwamba haya mambo yalikuwa kweli.
\s5
\v 10 Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, "Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako.
\v 11 Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu.
\v 12 Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji;
\v 13 na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.
\s5
\v 14 Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia iyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu. Mimi ni mwaminifu kwa yote yaliyoko kwenye sheria na maandiko ya manabii.
\v 15 Nina ujasiri ule ule kwa Mungu ambao hata hao nao wanaungojea, kuja kwa ufufuo wa wafu, kwa wote wenye haki na wasio na haki pia;
\v 16 na kwa hili, ninafanya kazi ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu kupitia mambo yote.
\s5
\v 17 Sasa Baada ya miaka mingi nimekuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha.
\v 18 Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia.
\v 19 Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote.
\s5
\v 20 Au watu hawa wenyewe na waseme ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele za baraza la kiyahudi;
\v 21 isipokuwa kwa ajili ya kitu kimoja nilichokisema kwa sauti niliposimama katikati yao, ' ni kwa sababu ya ufufuo wa wafu ninyi mnanihukumu."'
\s5
\v 22 Feliki alikuwa ametaarifiwa vizuri kuhusu njia, na akauahirisha mkutano. Akasema, "Lisia jemedari atakapokuja chini kutoka Yerusalemu nitatoa maamuzi dhidi ya mashitaka yenu."
\v 23 Ndipo akamwamuru akida amlinde Paulo, ila awe na nafasi na hata asiwepo mtu wakuwakataza marafiki zake wasimsaidie wala wasimtembelee.
\s5
\v 24 Baada ya siku kadhaa, Feliki akarudi na Drusila mkewe aliyekuwa Myahudi, akatuma kumwita Paulo na akasikiliza toka kwake habari za imani ndani ya Kristo Yesu.
\v 25 Ila Paulo alipokuwa akijadiliana naye kuhusu haki, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akapata hofu akajibu, "nenda mbali kwa sasa, ila nikipata muda tena, nitakuita."
\s5
\v 26 Muda uo huo, alitegemea kwamba Paulo atampa fedha kwa hiyo alimwita mara nyingi akaongea naye.
\v 27 Ila miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akawa Liwali baada ya Feliki, ila Feliki alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, hivyo akamwacha Paulo chini ya uangalizi.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Ndipo Festo alipoingia katika jimbo hilo na baada ya siku tatu alienda toka Kaisaria hadi Yerusalemu.
\v 2 Kuhani mkuu na Wayahudi mashuhuri walileta shutuma dhidi ya Paulo kwa Festo, na walizungumza kwa nguvu kwa Festo.
\v 3 Na walimwomba Festo fadhili juu ya habari za Paulo apate kumwita Yerusalemu ili waweze kumwua njiani.
\s5
\v 4 Lakini Festo alijibu kwamba Paulo alikuwa mfungwa katika Kaisaria, na kwamba yeye mwenyewe atarudi huko haraka.
\v 5 Alisema "Kwa hiyo, wale ambao wanaweza, wanaweza kwenda huko na sisi. Kama kuna kitu kibaya kwa mtu huyu, mnapaswa kumshtaki."
\s5
\v 6 Baada ya kukaa siku nane au kumi zaidi, akarudi Kaisaria. Na siku iliyofuata akakaa katika kiti cha hukumu na kuamuru Paulo aletwe kwake.
\v 7 Alipofika, Wayahudi kutoka Yerusalemu wakasimama karibu, Wakatoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
\v 8 Paulo alijitetea na kusema, 'Si dhidi ya jina la Wayahudi, si juu ya hekalu, na si juu ya Kaisari, nimefanya mabaya.'
\s5
\v 9 Lakini Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, na hivyo akamjibu Paulo kwa kusema, 'Je, unataka kwenda Yerusalemu na kuhukumiwa na mimi kuhusu mambo haya huko?'
\v 10 Paulo alisema, 'ninasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari ambapo napaswa kuhukumiwa. Sijawakosea Wayahudi, kama wewe ujuavyo vema.
\s5
\v 11 Ikiwa nimekosa na kama nimefanya kinachostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama shutuma zao si kitu, hakuna mtu anaweza kunikabidhi kwao. Ninamwomba Kaisari. '
\v 12 Baada ya Festo kuongea na baraza akajibu, " unamwomba Kaisari; utaenda kwa Kaisari."
\s5
\v 13 Baada ya siku kadhaa, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisaria kufanya ziara rasmi kwa Festo.
\v 14 Baada ya kukaa hapo kwa siku nyingi, Festo aliwasilisha kesi ya Paulo kwa mfalme; Akasema, 'Mtu mmoja aliachwa hapa na Feliki kama mfungwa.
\v 15 Nilipokuwa Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka juu ya mtu huyu kwangu, nao waliuliza juu ya hukumu dhidi yake.
\v 16 Kwa hili mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu kwa upendeleo badala yake, mtuhumiwa anapaswa kuwa na nafasi ya kuwakabili washitaki wake na kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.
\s5
\v 17 Kwa hiyo, walipokuja pamoja hapa, sikuweza kusubiri, lakini siku iliyofuata niliketi katika kiti cha hukumu na kuamuru mtu huyo aletwe ndani.
\v 18 Wakati washitaki waliposimama na kumshtaki, nilifikiri kwamba hakuna mashtaka makubwa yaliyoletwa dhidi yake.
\v 19 Badala yake, walikuwa na mabishano fulani pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu Yesu ambaye alikuwa amekufa, lakini Paulo anadai kuwa yu hai.
\v 20 Nilikuwa nimefumbwa jinsi ya kuchunguza suala hili, na nikamwuliza kama angeenda Yerusalemu kuhukumiwa kuhusu mambo haya.
\s5
\v 21 Lakini Paulo alipoitwa awekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uamuzi wa Mfalme, niliamuru awekwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari. '
\v 22 Agripa alizungumza na Festo, "ningependa pia kumsikiliza mtu huyu." "Festo, akasema, "kesho utamsikiliza."
\s5
\v 23 Hivyo kesho yake, Agripa na Bernike walifika na sherehe nyingi; walifika katika ukumbi na maafisa wa kijeshi, na watu mashuhuri wa mji. Na Festo alipotoa amri, Paulo aliletwa kwao.
\v 24 Festo akasema, "Mfalme Agripa, na watu wote ambao wapo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu; jumuiya yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wametaka niwashauri, na wao wakapiga kelele kwangu kwamba asiishi.
\s5
\v 25 Naliona kwamba hakufanya lolote linalostahili kifo; lakini kwa sababu amemwita Mfalme, niliamua kumpeleka kwake.
\v 26 Lakini sina kitu dhahiri cha kuandika kwa Mfalme. Kwa sababu hii, nimemleta kwako, hasa kwako wewe, Mfalme Agripa, ili nipate kuwa na kitu cha kuandika kuhusu kesi.
\v 27 kwa kuwa naona haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Hivyo, Agripa akamwambia Paulo, `Unaruhusiwa kujitetea. ' Ndipo Paulo akanyoosha mkono wake akajitetea hivi.
\v 2 "Najiona mwenye furaha, Mfalme Agripa, ili kufanya kesi yangu mbele yako leo dhidi ya mashtaka yote ya Wayahudi.
\v 3 Hasa, kwa sababu wewe ni mtaalamu wa desturi za Wayahudi na maswali. Hivyo naomba unisikilize kwa uvumilivu.
\s5
\v 4 Kweli, Wayahudi wote wanajua jinsi nilivyoishi tangu ujana wangu katika taifa langu huko Yerusalemu.
\v 5 Wananijua tangu mwanzo na wanapaswa kukubali kwamba niliishi kama Mfarisayo, dhehebu lenye msimamo mkali kwenye dini yetu.
\s5
\v 6 Sasa nimesimama hapa nihukumiwe kwa sababu mimi naliangalia ahadi ambayo Mungu aliifanya na baba zetu.
\v 7 Hii ni ahadi ambayo makabila yetu kumi na mbili yanatumaini kupokea kama wakimwabudu Mungu kwa bidii usiku na mchana. Ni kwa ajili ya tumaini hili, mfalme Agripa, kwamba Wayahudi wananishitaki.
\v 8 Kwa nini yeyote kati yenu anafikiri ni ajabu kwamba Mungu hufufua wafu?
\s5
\v 9 Wakati mmoja nilifikiria mwenyewe kwamba ningefanya mambo mengi dhidi ya jina la Yesu wa Nazareti.
\v 10 Nilifanya haya katika Yerusalemu; Niliwafunga waamini wengi gerezani, na nilikuwa na mamlaka kutoka kwa wakuu wa makuhani kufanya hivyo; na wakati wanauawa, nilipiga kura dhidi yao.
\v 11 Mara nyingi niliwaadhibu katika masinagogi yote na nilijaribu kuwafanya waikane imani yao. Nilikuwa na hasira sana juu yao na niliwafukuza hata katika miji ya ugenini.
\s5
\v 12 Wakati nilipokuwa nikifanya haya, nilienda Dameski, nikiwa na mamlaka na maagizo kutoka kwa makuhani wakuu;
\v 13 nilipokuwa njiani wakati wa mchana, Mfalme, niliona mwanga kutoka mbinguni uliokuwa mkali kuliko jua na uling'aa kutuzunguka mimi na watu waliokuwa wakisafiri pamoja nami.
\v 14 Sisi sote tulipoanguka chini, nalisikia sauti ikizungumza na mimi ikisema katika lugha ya Kiebrania: `Sauli, Sauli! Kwa nini unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.
\s5
\v 15 Ndipo nikasema, 'Wewe ni nani, Bwana?' Bwana akajibu, 'Mimi ni Yesu ambaye unanitesa.
\v 16 Sasa inuka usimame kwa miguu yako; sababu kwa kusudi hili mimi nimeonekana kwako, nimekuteua kuwa mtumishi na shahidi juu ya mambo ambayo unajua kuhusu mimi sasa na mambo nitakayokuonyesha baadaye;
\v 17 na Nitakuokoa kutoka kwa watu na watu wa Mataifa ambapo ninakutuma,
\v 18 kufungua macho yao na kuwatoa gizani kwenda kwenye mwanga na kutoka kwenye nguvu za shetani wamgeukie Mungu; ili wapate kupokea kutoka kwa Mungu msamaha wa dhambi na urithi ambao nimewapa wale niliowatenga kwa imani iliyo kwangu.
\s5
\v 19 Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuasi maono ya mbinguni,
\v 20 lakini, kwa wale walio katika Dameski kwanza, na kisha Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine, nilihubiri kwamba watubu na kumgeukia Mungu, wafanye matendo yanayostahili toba.
\v 21 Kwa sababu hiyo Wayahudi walinikamata hekaluni, wakajaribu kuniua.
\s5
\v 22 Mungu amenisaidia mpaka sasa, hivyo nasimama na kushuhudia kwa watu wa kawaida na kwa wale wakubwa juu ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatokea na si vingine;
\v 23 kwamba Kristo lazima atateseka na atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu na kutangaza mwanga kwa Wayahudi na watu wa mataifa.
\s5
\v 24 Paulo alipomaliza kujitetea, Festo alisema kwa sauti kubwa, 'Paulo, wewe ni mwendawazimu! masomo yako yamekufanya uwe mwendawazimu.
\v 25 Lakini Paulo akasema, Mimi si mwendawazimu, mheshimiwa Festo; lakini kwa ujasiri nasema maneno ya ukweli mtupu.
\v 26 Kwa kuwa mfalme anajua kuhusu mambo haya; na hivyo, ninaongea kwa uhuru kwake, kwa maana nina hakika kwamba hakuna lolote lililofichwa kwake; kwa kuwa hili halijafanywa pembeni.
\s5
\v 27 Je, unaamini manabii, Mfalme Agripa? Najua kwamba unaamini. '
\v 28 Agripa akamwambia Paulo, 'Kwa muda mfupi unaweza kunishawishi mimi na kunifanya Mkristo?
\v 29 Paulo akasema, '"Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu, bali pia wote wanaonisikia leo, wawe kama mimi, lakini bila hii minyororo ya gerezani."
\s5
\v 30 Ndipo mfalme alisimama, na liwali, na Bernike pia, na wale waliokuwa wamekaa pamoja nao,
\v 31 walipoondoka ukumbini, walizungumzia wao kwa wao na kusema, 'Mtu huyu hastahili kifo wala kifungo.'
\v 32 Agripa akamwambia Festo, "Mtu huyu angeweza kuwekwa huru kama asingekata rufani kwa Kaisari."
\s5
\c 27
\p
\v 1 Ilipoamuliwa kwamba tunatakiwa tusafiri kwa maji kwenda Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa afisa mmoja wa jeshi la Kiroma aliyeitwa Julio, wa Kikosi cha Agustani.
\v 2 Tukapanda meli kutoka Adramitamu, ambayo ilikuwa isafiri kandokando ya pwani ya Asia. Hivyo tukaingia baharini. Aristaka kutoka Thesolanike ya Makedonia akaenda pamoja nasi.
\s5
\v 3 Siku iliyofuata tukatua nanga katika mji wa Sidoni, ambapo Julio alimtendea Paulo kwa ukarimu na akamruhusu kwenda kwa rafiki zake kupokea ukarimu wao.
\v 4 Kutoka hapo tukaenda baharini tukasafiri kuzunguka kisiwa cha Kipro ambacho kilikuwa kimeukinga upepo, kwa sababu upepo ulikuwa ukitukabili.
\v 5 Baada ya kuwa tumesafiri katika maji yaliyo karibu na Kilikia na Pamfilia, tukaja Mira, mji wa Lisia.
\v 6 Pale yule afisa wa jeshi la Kiroma, akaikuta meli kutoka Alexandria ambayo ilikuwa isafiri kuelekea Italia. Akatupandisha ndani yake.
\s5
\v 7 Baada ya kuwa tumesafiri polepole kwa siku nyingi na hatimaye tukawa tumefika kwa taabu karibu na Kinidas, upepo haukuturuhusu tena kuelekea njia hiyo, hivyo tukasafiri kandokando ya kivuli cha Krete tukiukinga upepo, mkabala na Salmone.
\v 8 Tukasafiri kandokando ya pwani kwa ugumu, mpaka tukafika mahali palipoitwa Fari Haveni ambayo iko karibu na mji wa Lasi.
\s5
\v 9 Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
\v 10 na kusema, "Wanaume, naona safari ambayo tunataka tuichukue itakuwa na madhara na hasara nyingi, siyo tu ya mizigo na meli, lakini pia ya maisha yetu."
\v 11 Lakini afisa wa jeshi la Kiroma akamsikiliza zaidi bwana wake na mmiliki wa meli, kuliko mambo yale ambayo yalizungumzwa na Paulo.
\s5
\v 12 Kwa sababu bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi, mabaharia wengi wakashauri tusafiri kutoka pale, ili kwa namna yoyote tukiweza kuufikia mji wa Foinike, tukae pale wakati wa baridi. Foinike ni bandari huko Krete, na inatazama kaskazini mashariki na kusini mashariki.
\v 13 Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma polepole, mabaharia wakafikiri wamepata kile ambacho walikuwa wanakihitaji. Wakang'oa nanga na kusafiri kandokando ya Krete karibu na pwani.
\s5
\v 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa Wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa.
\v 15 Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo, tukakubaliana na hali hiyo, tukasafirishwa nao.
\v 16 Tukakimbia kupitia ule upande uliokuwa unaukinga upepo wa kisiwa kiitwacho Kauda; na kwa taabu sana tulifanikiwa kuuokoa mtumbwi.
\s5
\v 17 Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.
\v 18 Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini.
\s5
\v 19 Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.
\v 20 Wakati ambapo jua na nyota hazikutuangazia kwa siku nyingi, bado dhoruba kubwa ilitupiga, na matumaini kwamba tungeokolewa yalitoweka.
\s5
\v 21 Baada ya kuwa wameenda muda mrefu bila chakula, hapo Paulo akasimama katikati ya mabaharia akasema, "Wanaume, mlipaswa mnisikilize, na tusingengo'a nanga kutoka Krete, ili kupata haya madhara na hasara.
\v 22 Na sasa nawafariji mjitie moyo, kwa sababu hakutakuwa upotevu maisha kati yenu, isipokuwa hasara ya meli tu.
\s5
\v 23 Kwa sababu usiku uliopita malaika wa Mungu, ambaye huyo Mungu mimi ni wake, na ambaye ninamwabudu pia - malaika wake alisimama pembeni mwangu
\v 24 na kusema, "Usiogope Paulo. Lazima usimame mbele ya Kaisari, na tazama, Mungu katika wema wake amekupa hawa wote ambao wanasafiri pamoja nawe.
\v 25 Hivyo, wanaume, jipeni moyo, kwa sababu namwamini Mungu, kwamba itakuwa kama nilivyoambiwa.
\v 26 Lakini lazima tuumie kwa kupigwa katika baadhi ya visiwa."
\s5
\v 27 Ulipofika usiku wa kumi na nne, tulipokuwa tukiendeshwa huko na huko kwenye bahari ya Adratik, kama usiku wa manane hivi, mabaharia walifikiri kwamba wamekaribia nchi kavu.
\v 28 Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba.
\v 29 Waliogopa kwanza tunaweza kugonga miamba, hivyo wakashusha nanga nne kutoka katika sehemu ya kuwekea nanga na wakaomba kwamba asubuhi ingekuja mapema.
\s5
\v 30 Wale mabaharia walikuwa wanatafuta namna ya kuitelekeza ile meli na walizishusha majini boti ndogo ndogo za kuokolea maisha, na wakajifanya kwamba wanatupa nanga kutoka sehemu ya mbele ya boti.
\v 31 Lakini Paulo akamwambia yule askari wa jeshi la Kiroma na wale askari, "Hamuwezi kuokoka isipokuwa hawa watu wanabaki kwenye meli".
\v 32 Kisha wale askari wakakata kamba za ile boti na ikaachwa ichukuliwe na maji.
\s5
\v 33 Wakati mwanga wa asubuhi ulipokuwa unajitokeza, Paulo akawasihi wote angalau wale kidogo. Akasema, "Hii ni siku ya kumi na nne mnasuburi bila kula, hamjala kitu.
\v 34 Hivyo nawasihi mchukue chakula kidogo, kwa sababu hii ni kwa ajili ya kuishi kwenu; na hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
\v 35 Alipokwisha kusema hayo, akachukua mkate akamshukuru Mungu mbele ya macho ya kila mtu. Kisha akaumega mkate akaanza kula.
\s5
\v 36 Kisha wote wakatiwa moyo na wao wakachukua chakula.
\v 37 Tulikuwa watu 276 ndani ya meli.
\v 38 Walipokwisha kula vya kutosha, waliifanya meli nyepesi kwa kutupa ngano ndani ya bahari.
\s5
\v 39 Ilipokuwa mchana, hawakuitambua nchi kavu, lakini wakaona sehemu ya nchi kavu iliyoingia majini iliyokuwa na mchanga mwingi. wakajadiliana kama wanaweza kuiendesha meli kuelekea hapo.
\v 40 Hivyo wakazilegeza nanga wakaziacha baharini. Katika muda huo huo wakazilegeza kamba za tanga na wakaiinua sehemu ya mbele kuelekea kwenye upepo, hivyo wakaelekea kwenye hiyo sehemu ya mchanga mwingi.
\v 41 Lakini wakaja mahali ambapo mikondo miwili ya maji inakutana, na meli ikaelekea mchangani. Na ile sehemu ya mbele ya meli ikakwama pale na haikuweza kutoka, lakini sehemu ya mbele ya meli ikaanza kuvunjika kwa sababu ya ukali wa mawimbi.
\s5
\v 42 Mpango wa wale askari ulikuwa ni kuwaua wafungwa, ili kwamba hakuna ambaye angeogelea na kutoroka.
\v 43 Lakini yule askari wa jeshi la Kiroma alitaka kumwokoa Paulo, hivyo akausimamisha mpango wao; na akawaamuru wale ambao wanaweza kuogelea, waruke kutoka melini kwanza na waende nchi kavu.
\v 44 Kisha wanaume wengine watafuata, wengine juu ya vipande vya mbao na wengine juu ya vitu vingine kutoka kwenye meli. Kwa njia hii ikatokea kwamba wote tutafika salama nchi kavu.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Tulipofikishwa salama, tulitambua kwamba kisiwa kinaitwa Malta.
\v 2 Watu wenyeji wa pale si tu kwamba walitupa ukarimu wa kawaida, bali waliwasha moto na kutukaribisha sote, kwa sababu ya mvua na baridi iliyokuwa ikiendelea.
\s5
\v 3 Lakini Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni, nyoka mdogo mwenye sumu akatoka kwenye zile kuni kwa sababu ya lile joto, na akajizungusha kwenye mkono wake.
\v 4 Watu wenyeji wa pale walipoona mnyama ananing'inia kutoka kwenye mkono wake, wakasemezana wao kwa wao, "Mtu huyu hakika ni muuaji ambaye ametoroka baharini, lakini haki haimuruhusu kuishi."
\s5
\v 5 Lakini yeye akamtupia huyo mnyama katika moto na hakupata madhara yoyote.
\v 6 Wao walimngojea avimbe kwa homa au aanguke ghafla na kufa. Lakini baada ya kumwangalia kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna jambo ambalo si la kawaida kwake, walibadilisha mawazo yao na kusema alikuwa mungu.
\s5
\v 7 Basi mahali pale karibu palikuwa na ardhi ambayo ilikuwa mali ya mkuu wa kisiwa, mtu aliyeitwa Pablio. Alitukaribisha na kutukarimu kwa siku tatu.
\v 8 Ilitokea kwamba baba wa Pablio alishikwa na homa na ugonjwa wa kuhara. Na Paulo alipomwendea, aliomba, akaweka mikono juu yake, na kumponya.
\v 9 Baada ya hili kutokea, watu wengine pale kisiwani waliokuwa wanaumwa pia walikwenda na waliponywa.
\v 10 Watu wakatuheshimu kwa heshima nyingi. Tulipokuwa tunajiandaa kusafiri, walitupa vile tulivyovihitaji.
\s5
\v 11 Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha.
\v 12 Baada ya kuwa tumetua katika mji wa Sirakusa, tulikaa pale siku tatu.
\s5
\v 13 Kutokea pale tulisafiri tukafika katika mji wa Regio. Baada ya siku moja upepo wa kusini ulitokea ghafla, na baada ya siku mbili tukafika katika mji wa Putoli.
\v 14 Huko tuliwakuta baadhi ya ndugu na tulikaribishwa kukaa nao kwa siku saba. Kwa njia hii tukaja Rumi.
\v 15 Kutoka huko wale ndugu, baada ya kuwa wamesikia habari zetu, walikuja kutupokea huko soko la Apias na Hotel tatu. Paulo alipowaona wale ndugu alimshukuru Mungu akajitia ujasiri.
\s5
\v 16 Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda.
\v 17 Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale wanume waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, "Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi.
\v 18 Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo.
\s5
\v 19 Lakini wale Wayahudi walipoongea kinyume cha shauku yao, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, japokuwa haikuwa kana kwamba naleta mashtaka juu ya taifa langu.
\v 20 Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki.
\s5
\v 21 Kisha wakamwambia, "Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote baya kuhusu wewe.
\v 22 Lakini tunataka kusikia kutoka kwako unafikiri nini kuhusu hili kundi la watu hawa, kwa sababu inajulikana kwetu kwamba linaongea kinyume kila mahali."
\s5
\v 23 Walipokuwa wametenga siku kwa ajili yake, watu wengi zaidi walimwijia mahali alipokuwa anaishi. Alisema lile jambo kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Mungu. Alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote mbili kutoka katika sheria za Musa na kutoka kwa manabii, kuanzia asubuhi hadi jioni.
\v 24 Baadhi yao walishawishika kuhusu mambo yale yaliyosemwa, wakati wengine hawakuamini.
\s5
\v 25 Waliposhindwa kukubaliana wao kwa wao, waliondoka baada ya Paulo kulisema jambo hili moja, "Roho Mtakatifu alisema vyema kupitia Isaya nabii kwa baba zenu.
\v 26 Alisema, 'Nenda kwa watu hawa useme, "Kwa masikio yenu mtasikia, lakini hamtaelewa; Na kwa macho yenu mtaona lakini hamtatambua.
\s5
\v 27 Kwa ajili ya mioyo ya watu hawa imekuwa dhaifu, masikio yao yamesikia kwa taabu, wamefumba macho yao; ili kwamba wasijekutambua kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, na kugeuka tena, na ningeliwaponya."'
\s5
\v 28 Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, na watasikiliza." (Zingatia: Mstari huu
\v 29 "Wakati alipokuwa amesema mambo haya, wayahudi waliondoka, wakiwa na mashindano makubwa kati yao.," haumo kwenye nakala bora za kale).
\s5
\v 30 Paulo alikaa katika nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote miwili, na aliwakaribisha wote waliokuja kwake.
\v 31 Alikuwa akihubiri ufalme wa Mungu na alikuwa akifundisha mambo juu ya Bwana Yesu Kristo kwa ujasiri wote. Hakuna aliyemzuia.

866
46-ROM.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,866 @@
\id ROM
\ide UTF-8
\h Warumi
\toc1 Warumi
\toc2 Warumi
\toc3 rom
\mt Warumi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtumishi wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.
\v 2 Hii ndio ile Injili aliyoiahidi zamani kupitia manabii wake katika maandiko matakatifu.
\v 3 Ni kuhusu Mwana wake, aliyezaliwa kutoka ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili.
\s5
\v 4 Yeye alitangazwa kwa Mwana wa Mungu kwa nguvu ya Roho ya utakatifu kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.
\v 5 Kupitia yeye tumepokea neema na utume kwa utii wa imani kati ya mataifa yote, kwa ajili ya jina lake.
\v 6 Kati ya mataifa haya, ninyi pia mmeitwa kuwa wa Yesu Kristo.
\s5
\v 7 Barua hii ni kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watu watakatifu. Neema na iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 8 Kwanza, namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.
\v 9 Kwa maana Mungu ni shahidi wangu, ambaye ninamtumikia kwa roho yangu katika injili ya Mwana wake, jinsi ninavyodumu katika kuwataja.
\v 10 Daima naomba katika sala zangu kwamba kwa njia yoyote nipate mwishowe kuwa na mafanikio sasa kwa mapenzi ya Mungu katika kuja kwenu.
\s5
\v 11 Maana natamani kuwaona, ili nipate kuwapa ninyi baadhi ya karama za rohoni, nipate kuwaimarisha.
\v 12 Yaani, natazamia kutiwa moyo pamoja nanyi, kwa njia ya imani ya kila mmoja wetu, yenu na yangu.
\s5
\v 13 Sasa ndugu, sitaki mkose kufahamu kwamba, mara nyingi nimekusudia kuja kwenu, lakini nimezuiliwa mpaka sasa. Nilitaka hivi ili kuwa na matunda kwenu kama ilivyo pia miongoni mwa watu wa mataifa.
\v 14 Nadaiwa na Wayunani na wageni pia, werevu na wajinga.
\v 15 Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi niko tayari kutangaza injili kwenu pia ninyi mlio huko Roma.
\s5
\v 16 Kwa maana siionei haya injili, kwa kuwa ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia.
\v 17 Kwa maana haki ya Mungu imedhihirishwa kutoka imani hata imani, kama ilivyo andikwa, "Mwenye haki ataishi kwa imani."
\s5
\v 18 Maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa watu, ambao kwa njia ya udhalimu huificha kweli.
\v 19 Hii ni kwa sababu, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao. Maana Mungu amewafahamisha.
\s5
\v 20 Maana mambo yake yasioonekana vizuri yamekuwa wazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Yanaeleweka kupitia vitu vilivyoumbwa. Mambo haya ni uwezo wake wa milele na asili ya uungu. Matokeo yake, watu hawa hawana udhuru.
\v 21 Hii ni kwa sababu, ingawa walijua kuhusu Mungu, hawakumtukuza yeye kama Mungu, wala hawakumpa shukrani. Badala yake, wamekuwa wapumbavu katika mawazo yao, na mioyo yao yenye ujinga ilitiwa giza.
\s5
\v 22 Walijiita kuwa ni werevu, lakini wakawa wajinga.
\v 23 Waliubadili utukufu wa Mungu asie na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, ya wanyama wenye miguu minne, na ya viumbe vitambaavyo.
\s5
\v 24 Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa za mioyo yao kwa uchafu, kwa miili yao kufedheheshwa baina yao.
\v 25 Ni wao walioibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, na ambao waliabudu na kutumikia viumbe badala ya Muumbaji, ambaye anasifiwa milele. Amina.
\s5
\v 26 Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, kwa kuwa wanawake wao walibadilisha matumizi yao ya asili kwa kile kilicho kinyume na asili.
\v 27 Hali kadhalika, wanaume pia wakaacha matumizi yao ya asili kwa wanawake na kuwakwa na tamaa dhidi yao wenyewe. Hawa walikuwa wanaume ambao walifanya na wanaume wenzao yasiyo wapasa, na ambao walipokea adhabu iliyostahili upotovu wao.
\s5
\v 28 Kwa sababu walikataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye mambo yale yasiyofaa.
\s5
\v 29 Wamejawa na udhalimu wote, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu, na nia mbaya.
\v 30 Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji, na wenye kumchukia Mungu. Wenye vurugu, kiburi, na majivuno. Wao ni watunga mabaya, na wasiotii wazazi wao.
\v 31 Wao hawana ufahamu; wasioaminika, hawana mapenzi ya asili, na wasio na huruma.
\s5
\v 32 Wanaelewa kanuni za Mungu, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo wanastahili kifo. Lakini si tu wanafanya mambo hayo, wao pia wanakubaliana na wale wanaofanya mambo hayo.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo hauna udhuru, wewe uhukumuye, kwa maana katika yale uhukumuyo mwingine wajitia hatiani mwenyewe. Kwa maana wewe uhukumuye unafanya mambo yale yale.
\v 2 Lakini twajua kwamba hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao mambo kama hayo.
\s5
\v 3 Lakini wewe tafakari hili, wewe ambaye unahukumu wale wanaotenda mambo hayo ingawa nawe unafanya mambo yayo hayo. Je utaepuka hukumu ya Mungu?
\v 4 Au unafikiri kidogo sana juu ya wingi wa wema wake, kuchelewa kwa adhabu yake, na uvumilivu wake? Je, hujui kwamba wema wake unapaswa kukuelekeza katika toba?
\s5
\v 5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu kwa siku ile ya ghadhabu, yaani, siku ile ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.
\v 6 Yeye atamlipa kila mtu kipimo sawa na matendo yake:
\v 7 kwa wale ambao kwa uthabiti wa matendo mema wametafuta sifa, heshima na kutokuharibika, atawapa uzima wa milele.
\s5
\v 8 Lakini kwa wale ambao ni wabinafsi, wasioitii kweli bali hutii dhuluma, ghadhabu na hasira kali itakuja.
\v 9 Mungu ataleta dhiki na shida juu ya kila nafsi ya binadamu aliyefanya uovu, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
\s5
\v 10 Lakini sifa, heshima na amani itakuja kwa kila mtu atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
\v 11 Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.
\v 12 Kwa maana kama vile wengi waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na kama vile wengi waliokosa kulingana na sheria watahukumiwa kwa sheria.
\s5
\v 13 Maana si wasikiaji wa sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.
\v 14 Kwa maana watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanafanya kwa asili mambo ya sheria, wao, wamekuwa sheria kwa nafsi zao, ingawa wao hawana sheria.
\s5
\v 15 Kwa hili wanaonesha kwamba matendo yanayohitajika kwa mujibu wa sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia zinawashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama huwashitaki au huwalinda wao wenyewe
\v 16 na pia kwa Mungu. Haya yatatokea katika siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu wote, sawasawa na injili yangu, kwa njia ya Yesu Kristo.
\s5
\v 17 Tuseme kwamba unajiita mwenyewe Myahudi, aliyekaa katika sheria, shangilia kwa kujisifu katika Mungu,
\v 18 yajue mapenzi yake, na kupima mambo ambayo yanatofautiana nayo, baada ya kuagizwa na sheria.
\v 19 Na tuseme kwamba una ujasiri kwamba wewe mwenyewe ni kiongozi wa kipofu, mwanga kwa wale walio gizani,
\v 20 msahihishaji wa wajinga, mwalimu wa watoto, na kwamba unayo katika sheria jinsi ya elimu na kweli.
\s5
\v 21 Wewe basi, uhubiriye mwingine, je, hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kutokuiba, je wewe huiba?
\v 22 Wewe usemae usizini, je unazini? Wewe uchukiaye sanamu, je unaiba hekaluni?
\s5
\v 23 Wewe ujisifuye katika sheria, je haumfedheheshi Mungu katika kuvunja sheria?
\v 24 Kwa maana "jina la Mungu linafedheheshwa kati ya watu wa mataifa kwa sababu yenu," kama ilivyoandikwa.
\s5
\v 25 Kwa maana Kutahiriwa kweli kwafaa kama ukitii sheria, lakini kama wewe ni mkiukaji wa sheria, kutahiriwa kwako kunakuwa kutokutahiriwa.
\v 26 Basi, ikiwa, mtu asiyetahiriwa anaendelea kushika matakwa ya sheria, je kutokutahiriwa kwake hakutachukuliwa kana kwamba ametahiriwa?
\v 27 Na yeye asiyetahiriwa kwa asili hatakuhukumu kama akitimiza sheria? Hii ni kwa sababu una maandiko yaliyoandikwa na tohara pia lakini bado u mkiukaji wa sheria!
\s5
\v 28 Kwa maana yeye si Myahudi aliye kwa hali ya nje; wala kutahiriwa si kule ambako ni kwa nje tu katika mwili.
\v 29 Lakini yeye ni Myahudi aliye kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko. Sifa ya mtu wa namna hiyo haitokani na watu bali yatoka kwa Mungu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kisha ni faida gani aliyo nayo Myahudi? Na faida ya tohara ni nini?
\v 2 Ni vyema sana kwa kila njia. Awali ya yote, Wayahudi walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu.
\s5
\v 3 Lakini, itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa batili?
\v 4 La hasha. Badala yake, acha Mungu aonekane kuwa kweli, hata kama kila mtu ni mwongo. Kama ilivyokuwa imeandikwa, "Ya kwamba uweze kuonekana kuwa mwenye haki katika maneno yako, na uweze kushinda uingiapo katika hukumu."
\s5
\v 5 Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu.
\v 6 La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu?
\s5
\v 7 Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi?
\v 8 Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, "Tufanye uovu, ili mema yaje"? Hukumu juu yao ni ya haki.
\s5
\v 9 Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi.
\v 10 Hii ni kama ilivyoandikwa: "Hakuna mwenye haki, hata mmoja.
\s5
\v 11 Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu.
\v 12 Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.
\s5
\v 13 Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao.
\v 14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
\s5
\v 15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
\v 16 Uharibifu na mateso yapo katika njia zao.
\v 17 Watu hawa hawajajua njia ya amani.
\v 18 Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao."
\s5
\v 19 Sasa tunajua kwamba chochote sheria isemacho, husema na wale walio chini ya sheria. Hii ni ili kwamba kila kinywa kifungwe, na hivyo kwamba ulimwengu wote uweze kuwajibika kwa Mungu.
\v 20 Hii ni kwa sababu hakuna mwili utakaohesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele za macho yake. Kwa kuwa kupitia Sheria huja ufahamu wa dhambi.
\s5
\v 21 Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii,
\v 22 hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti.
\s5
\v 23 Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
\v 24 Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
\s5
\v 25 Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita
\v 26 katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu.
\s5
\v 27 Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani.
\v 28 Hivyo tunahitimisha kwamba mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
\s5
\v 29 Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia.
\v 30 Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani.
\s5
\v 31 Je sisi twaibatilisha sheria kwa imani? La hasha! Kinyume cha hayo, sisi twaithibitisha sheria.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Tutasema nini tena kwamba Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili, amepatikana?
\v 2 Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, angekuwa na sababu ya kujisifu, lakini si mbele za Mungu.
\v 3 Kwani maandiko yanasemaje? "Abrahamu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki."
\s5
\v 4 Sasa kwa mtu afanyaye kazi, malipo yake hayahesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
\v 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtaua, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.
\s5
\v 6 Daudi pia hunena baraka juu ya mtu ambaye Mungu amhesabia haki pasipo matendo.
\v 7 Alisema, "Wamebarikiwa wale ambao maovu yao yamesamehewa na ambao dhambi zao zimefunikwa.
\v 8 Amebarikiwa mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi."
\s5
\v 9 Basi je baraka hizi ni kwa wale waliotahiriwa tu, au pia kwa wale wasiotahiriwa? Kwa maana twasema, "kwa Abrahamu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki."
\v 10 Hivyo ilihesabiwaje basi? Wakati Abrahamu alikuwa katika tohara, au kabla hajatahiriwa? Haikuwa katika kutahiriwa, bali katika kutotahiriwa.
\s5
\v 11 Abrahamu alipokea alama ya kutahiriwa. Huu ulikuwa muhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo tayari kabla hajatahiriwa. Matokeo ya ishara hii ni kwamba alifanyika kuwa baba wa wote waaminio, hata kama wapo katika kutotahiriwa. Hii ina maana kwamba haki itahesabiwa kwao.
\v 12 Hii pia ilimaanisha kuwa Abrahamu alifanyika baba wa tohara si tu kwa wale wanaotokana na tohara, bali pia wale wanaozifuata nyayo za baba yetu Abrahamu. Na hii ndiyo imani aliyokuwa nayo kwa wasiotahiriwa.
\s5
\v 13 Kwa maana haikuwa kwa sheria kwamba ahadi ilitolewa kwa Abrahamu na uzao wake, ahadi hii ya kwamba watakuwa warithi wa dunia. isipokuwa, ilikuwa kupitia haki ya imani.
\v 14 Kwa maana kama wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.
\v 15 Kwa sababu sheria huleta ghadhabu, lakini pale ambapo hakuna sheria, pia hakuna kutotii.
\s5
\v 16 Kwa sababu hii hili hutokea kwa imani, ili iwe kwa neema. Matokeo yake, ahadi ni dhahiri kwa uzao wote. Na wazawa hawa si tu wale wanaojua sheria, bali pia wale ambao ni wa imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sisi sote,
\v 17 kama ilivyoandikwa, "Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi." Abrahamu alikuwa katika uwepo wa yule aliyemwamini, yaani, Mungu ambaye huwapa wafu uzima na kuyaita mambo ambayo hayapo ili yaweze kuwepo.
\s5
\v 18 Licha ya hali zote za nje, Abrahamu kwa ujasiri alimuamini Mungu kwa siku zijazo. Hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kulingana na kile kilichonenwa,"... Ndivyo utakavyokuwa uzao wako."
\v 19 Yeye hakuwa dhaifu katika imani. Abrahamu alikiri kwamba mwili wake mwenyewe ulikwisha kufa - alikuwa na umri wa karibu miaka mia moja. Pia alikubaliana na hali ya kufa ya tumbo la Sara.
\s5
\v 20 Lakini kwa sababu ya ahadi ya Mungu, Abrahamu hakusita katika kutokuamini. Bali, alitiwa nguvu katika imani na alimsifu Mungu.
\v 21 Alikuwa akijua hakika ya kuwa kile ambacho Mungu ameahidi, alikuwa pia na uwezo wa kukikamilisha.
\v 22 Kwa hiyo hii pia ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.
\s5
\v 23 Sasa haikuandikwa tu kwa faida yake, kwamba ilihesabiwa kwake.
\v 24 Iliandikwa kwa ajili yetu pia, kwa waliowekewa kuhesabiwa, sisi ambao tunaamini katika yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka wafu.
\v 25 Huyu ni yule ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 2 Kupitia yeye sisi pia tuna fursa kwa njia ya imani katika neema hii ambayo ndani yake tunasimama. Tunafurahi katika ujasiri atupao Mungu kwa ajili ya baadaye, ujasiri ambao tutashiriki katika utukufu wa Mungu.
\s5
\v 3 Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu.
\v 4 Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye.
\v 5 Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.
\s5
\v 6 Kwa tulipokuwa tungali tu dhaifu, kwa wakati muafaka Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
\v 7 Kwa kuwa itakuwa vigumu mmoja kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki. Hii ni kwamba, pengine mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
\s5
\v 8 Lakini Mungu amehakikisha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
\v 9 Kisha zaidi ya yote, sasa kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa kwa hiyo kutoka katika gadhabu ya Mungu.
\s5
\v 10 Kwa kuwa, ikiwa wakati tulipokuwa maadui, tulipatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumekwisha patanishwa, tutaokolewa kwa maisha yake.
\v 11 Siyo hivi tu, bali pia tunafurahi katika Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo, kupitia yeye ambaye sasa tumepokea upatanisho huu.
\s5
\v 12 Kwa hiyo basi, kama kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani, kwa njia hii kifo kiliingia kwa njia ya dhambi. Na kifo kikasambaa kwa watu wote, kwa sababu wote walifanya dhambi.
\v 13 Kwa kuwa hadi sheria, dhambi ilikuwa duniani, lakini dhambi haihesabiki wakati hakuna sheria.
\s5
\v 14 Hata hivyo, kifo kilitawala kutoka Adamu hadi Musa, hata juu ya wale ambao hawakufanya dhambi kama kutotii kwa Adamu, ambaye ni mfano wa yeye ambaye angekuja.
\v 15 Lakini hata hivyo, zawadi ya bure si kama kosa. Kwa kuwa ikiwa kwa kosa la mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na zawadi kwa neema ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imezidi kuongezeka kwa wengi.
\s5
\v 16 Kwa kuwa zawadi si kama matokeo ya yule ambaye alifanya dhambi. Kwa kuwa kwa upande mwingine, hukumu ya adhabu ilikuja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Lakini kwa upande mwingine, kipawa cha bure kinachotoka katika kuhesabiwa haki kilikuja baada ya makosa mengi.
\v 17 Kwa maana, ikiwa kwa kosa la mmoja, kifo kilitawala kupitia mmoja, zaidi sana wale ambao watapokea neema nyingi pamoja na kipawa cha haki watatawala kupitia maisha ya mmoja, Yesu Kristo.
\s5
\v 18 Hivyo basi, kama kupitia kosa moja watu wote walikuja kwenye hukumu, ingawa kupitia tendo moja la haki kulikuja kuhesabiwa haki ya maisha kwa watu wote.
\v 19 Kwa kuwa kama kupitia kutotii kwa mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, hivyo kupitia utii wa mmoja wengi watafanywa wenye haki.
\s5
\v 20 Lakini sheria iliingia pamoja, ili kwamba kosa liweze kuenea. Lakini mahali ambapo dhambi ilizidi kuwa nyingi, neema iliongezeka hata zaidi.
\v 21 Hii ilitokea ili kwamba, kama dhambi ilivyotawala katika kifo, ndivyo hata neema inaweza kutawala kupitia haki kwa ajili ya maisha ya milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Tuseme nini basi? Tuendelee katika dhambi ili neema iongezeke?
\v 2 La hasha. Sisi tuliokufa katika dhambi, tunawezaje tena kuishi katika hiyo?
\v 3 Je hamjui ya kuwa wale waliobatizwa katika Kristo walibatizwa katika mauti yake?
\s5
\v 4 Tulikuwa tumezikwa pamoja naye kupitia ubatizo katika kifo. Hii ilifanyika ili kwamba kama vile Kristo alivyoinuliwa kutoka mauti kupitia utukufu wa Baba, ili kwamba nasi tuweze kutembea katika upya wa maisha.
\v 5 Maana ikiwa tumeunganishwa pamoja naye katika mfano wa kifo chake, pia tutaunganishwa katika ufufuo wake.
\s5
\v 6 Sisi tunajua hivi, utu wetu wa zamani ulisulubiwa pamoja naye, ili kwamba mwili wa dhambi uharibiwe. Hii ilitokea ili kwamba tusiendelee kuwa watumwa wa dhambi.
\v 7 Yeye aliyekufa amefanywa mwenye haki kulingana na dhambi.
\s5
\v 8 Lakini kama tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pamoja naye pia.
\v 9 Tunajua kwamba Kristo amefufuliwa kutoka katika wafu, na kwamba si mfu tena. Kifo hakimtawali tena.
\s5
\v 10 Maana kwa habari ya kifo alichokufa kwa dhambi, alikufa mara moja kwa ajili ya wote. Hata hivyo, maisha anayoishi, anaishi kwa ajili ya Mungu.
\v 11 Kwa njia iyo hiyo, nanyi pia mnapaswa kujihesabu kuwa wafu katika dhambi, bali hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
\s5
\v 12 Kwa sababu hiyo usiruhusu dhambi itawale mwili wako ili kusudi uweze kuzitii tamaa zake.
\v 13 Usitoe sehemu za mwili wako katika dhambi kama vyombo visivyo na haki, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu, kama walio hai kutoka mautini. Na zitoeni sehemu za miili yenu kama vyombo vya haki kwa Mungu.
\v 14 Msiiruhusu dhambi iwatawale. Kwa kuwa hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.
\s5
\v 15 Nini basi? Tutende dhambi kwa kuwa hatupo chini ya sheria, bali chini ya neema? La hasha.
\v 16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa wenyewe kama watumishi ndiye ambaye ninyi mnakuwa watumishi wake, yeye mnayepaswa kumtii? Hii ni kweli hata kama ninyi ni watumwa katika dhambi ambayo inapelekea mauti, au watumwa wa utii unaopelekea haki.
\s5
\v 17 Lakini ashukuriwe Mungu! Kwa kuwa mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mmetii kutoka moyoni ile namna ya fundisho mliopewa.
\v 18 Mmefanywa huru kutoka kwenye dhambi, na mmefanywa watumwa wa haki.
\s5
\v 19 Ninazungumza kama mtu kwa sababu ya madhaifu ya miili yenu. Kwa maana kama vile mlivyotoa viungo vya miili yenu kuwa watumwa kwa uchafu na uovu, kwa jinsi iyo hiyo, sasa toeni viungo vya miili yenu kuwa watumwa wa haki kwa utakaso.
\v 20 Kwa kuwa mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.
\v 21 Kwa wakati huo, mlikuwa na tunda lipi kwa mambo ambayo kwa sasa mnaona aibu kwayo? Kwa kuwa matokeo ya mambo hayo ni kifo.
\s5
\v 22 Lakini kwa kuwa sasa mmefanywa huru mbali na dhambi na mmefanyika watumwa kwa Mungu, mna tunda kwa ajili ya utakaso. Tokeo ni uzima wa milele.
\v 23 Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, bali zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Au hamjui, ndugu zangu (kwa kuwa naongea na watu wanaoijua sheria), kwamba sheria humtawala mtu anapokuwa hai?
\s5
\v 2 Kwa maana mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria kwa yule mme wake anapokuwa hai, lakini ikiwa mme wake atakufa, atakuwa amewekwa huru kutoka sheria ya ndoa.
\v 3 Hivyo basi, wakati mme wake angali akiishi, ikiwa anaishi na mwanamme mwingine, ataitwa mzinzi. Lakini ikiwa mme wake akifa, yuko huru dhidi ya sheria, hivyo hatakuwa mzinzi ikiwa anaishi na mwanamme mwingine.
\s5
\v 4 Kwa hiyo, ndugu zangu, ninyi pia mlifanywa wafu kwa sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Imekuwa hivi ili mpate kuunganishwa na mwingine, kwake yeye ambaye alifufuliwa kutoka wafu ili tuweze kumzalia Mungu matunda.
\v 5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi ziliamshwa katika viungo vyetu kwa njia ya sheria na kuizalia mauti matunda.
\s5
\v 6 Lakini sasa tumefunguliwa kutoka katika sheria. Tumeifia ile hali iliyotupinga. Ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya Roho, na si katika hali ya zamani ya andiko.
\s5
\v 7 Tusemeje basi? Sheria ni dhambi? La hasha. Hata hivyo, nisingelitambua dhambi, isingelikuwa kwa njia ya sheria. Kwa kuwa nisingelijua kutamani kama sheria isingelisema, "Usitamani."
\v 8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikaleta ndani yangu kila aina ya kutamani. Kwa maana dhambi pasipo sheria imekufa.
\s5
\v 9 Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria, lakini ilipokuja ile amri, dhambi ilipata uhai, nami nikafa.
\v 10 Ile amri na ambayo ingelileta uzima iligeuka kuwa mauti kwangu.
\s5
\v 11 Kwa maana dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikanidanganya. Kupitia ile amri, iliniua.
\v 12 Hivyo sheria ni takatifu, na ile amri ni takatifu, ya yaki, na njema.
\s5
\v 13 Hivyo basi ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Isiwe hivyo kamwe. Lakini dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa kupitia ile njema, ilileta mauti ndani yangu. Hii ilikuwa ili kwamba kupitia ile amri, dhambi izidi kuwa mbaya mno.
\v 14 Kwa maana twajua ya kuwa sheria asili yake ni ya rohoni, lakini mimi ni mtu wa mwilini. Nimeuzwa chini ya utumwa wa dhambi.
\s5
\v 15 Maana nifanyalo, silielewi dhahiri. Kwa kuwa lile nilipendalo kutenda, silitendi, na lile nilichukialo, ndilo ninalolitenda.
\v 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, nakubaliana na sheria ya kuwa sheria ni njema.
\s5
\v 17 Lakini sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
\v 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema. Kwa kuwa tamaa ya lililo jema imo ndani yangu, lakini silitendi.
\s5
\v 19 Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile ovu nisilolipenda ndilo nilitendalo.
\v 20 Sasa kama natenda lile nisilolipenda, si mimi binafsi nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
\v 21 Nimefahama, tena, imo kanuni ndani yangu ya kutaka kutenda lililo jema, lakini uovu hakika umo ndani yangu.
\s5
\v 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani.
\v 23 Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu.
\s5
\v 24 Mimi ni mtu wa huzuni! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
\v 25 Lakini shukrani kwa Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi. Mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu. Bali, kwa mwili naitumikia kanuni ya dhambi.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
\v 2 Kwa kuwa kanuni ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imenifanya mimi kuwa huru mbali na kanuni ya dhambi na mauti.
\s5
\v 3 Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya. Alimtuma Mwana wake wa pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi awe sadaka ya dhambi, na akaihukumu dhambi katika mwili.
\v 4 Alifanya hivi ili maagizo ya sheria yatimilizwe ndani yetu, sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali kwa kufuata mambo ya Roho.
\v 5 Wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, lakini wale waifuatao Roho huyafikiri mambo ya Roho.
\s5
\v 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya Roho ni uzima na amani.
\v 7 Hii ni kwa sababu ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
\v 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
\s5
\v 9 Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake.
\v 10 Kama Kristo yumo ndani yenu, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, bali roho ni hai kwa mambo ya haki.
\s5
\v 11 Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.
\s5
\v 12 Hivyo basi, ndugu zangu, sisi tu wadeni, lakini si kwa mwili kwamba tuishi kwa jinsi ya mwili.
\v 13 Maana ikiwa mnaishi kwa jinsi ya mwili, mpo karibu kufa, lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili, nanyi mtaishi.
\s5
\v 14 Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu.
\v 15 Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, "Abba, Baba!"
\s5
\v 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu.
\v 17 Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.
\s5
\v 18 Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.
\v 19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
\s5
\v 20 Kwa maana uumbaji pia ulitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha. Ni katika tumaini
\v 21 kwamba uumbaji wenyewe nao utawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, na kuingizwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
\v 22 Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa.
\s5
\v 23 Si hivyo tu, ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho - sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukisubiri kufanywa wana, yaani ukombozi wa miili yetu.
\v 24 Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa. Lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena, kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
\v 25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.
\s5
\v 26 Kwa jinsi iyo hiyo, Roho naye hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
\v 27 Na yeye aichunguzaye mioyo huijua akili ya Roho, kwa sababu huomba kwa niaba yao walioamini kulingana na mapenzi ya Mungu.
\s5
\v 28 Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake.
\v 29 Kwa sababu wale wote aliowajua tangu asili, pia aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miogoni mwa ndugu wengi.
\v 30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao aliwaita pia. Na wale aliowaita, hao aliwahesabia haki. Na wale aliowahesabia haki, hao pia akawatukuza.
\s5
\v 31 Tuseme nini basi juu ya mambo haya? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
\v 32 Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
\s5
\v 33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
\v 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili yetu, na zaidi ya hayo, yeye pia alifufuliwa. Naye anatawala pamoja na Mungu mahali pa heshima, na tena ndiye anayetuombea sisi.
\s5
\v 35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Dhiki, au shida, au mateso, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
\v 36 Kama ilivyoandikwa, "Kwa faida yako tunauawa mchana kutwa. Tulihesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa."
\s5
\v 37 Katika mambo haya yote sisi tu zaidi ya washindi katika yeye aliyetupenda.
\v 38 Kwa maana nimekwisha kushawishika kwamba wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala mamlaka, wala vitu vilivyopo, wala vitu vijavyo, wala nguvu,
\v 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote, hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu, ambaye ni Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu,
\v 2 kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu.
\s5
\v 3 Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili.
\v 4 Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi.
\v 5 Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.
\s5
\v 6 Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia. Maana si kila mtu aliye Israeli ni Mwiisraeli halisi.
\v 7 Sivyo hata kwa uzao wa Abrahamu kuwa ni watoto wake halisi. Lakini, "ni kupitia Isaka uzao wako utaitwa."
\s5
\v 8 Hii ni kwamba, watoto wa mwili si watoto wa Mungu. Lakini watoto wa ahadi wanatazamwa kuwa kama uzao.
\v 9 Maana hili ndilo neno la ahadi: "Katika majira haya nitakuja, na Sara atapewa mtoto."
\s5
\v 10 Si hili tu, lakini baada ya Rebeka kupata mimba kwa mtu mmoja, Isaka baba yetu-
\v 11 kwamba watoto walikuwa bado hawajazaliwa na alikuwa hajafanya jambo lolote zuri au baya, ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisimame, wala si kwa matendo, lakini ni kwa sababu ya yule aitae.
\v 12 Ilinenwa kwake, "Mkubwa atamtumikia mdogo."
\v 13 Kama ilivyo kwisha andikwa: "Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia."
\s5
\v 14 Basi tena tutasema nini? Je kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha.
\v 15 Kwa kuwa anasema kwa Musa, "nitakuwa na rehema kwa yule nitakayemrehemu, na nitakuwa na huruma kwa yule nitakayemhurumia."
\v 16 Kwa hiyo basi, si kwa sababu ya yeye atakaye, wala si kwa sababu ya yeye ambaye hukimbia, lakini kwa sababu ya Mungu, ambaye huonesha rehema.
\s5
\v 17 Kwa kuwa maandiko husema kwa Farao, "Kwa kusudi hili maalumu nilikuinua, ili kwamba nioneshe nguvu zangu katika wewe, na ili kwamba jina langu litangazwe katika nchi yote."
\v 18 Hivyo basi, Mungu huwa na rehema kwa yeyote ampendaye, na kwa ambaye humpenda, humfanya kuwa mkaidi.
\s5
\v 19 Kisha utasema kwangu, "Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?"
\v 20 Kinyume chake, mwanadamu, wewe ni nani ujibue kinyume na Mungu? Kuna uwezekano wowote wa kilichofinyangwa kusema kwa mfinyanzi, "Kwanini ulinifanya hivi mimi?"
\v 21 Je mfinyazi huwa hana haki juu ya udongo kutengeneza chombo kwa matumizi maalumu kutokana na bonge lile lile, na chombo kingine kwa matumizi ya kila siku?
\s5
\v 22 Vipi kama Mungu, ambaye ana utayari wa kuonesha gadhabu yake na kufanya nguvu yake kujulikana, alistahimili kwa uvumilivu wa kutosha vyombo vya gadhabu vilivyoandaliwa kwa kuangamiza?
\v 23 Vipi kama alifanya hivi ili kwamba aoneshe wingi wa utukufu wake juu ya vyombo vya rehema, ambavyo alikwisha kuviandaa kwa ajili ya utukufu?
\v 24 Vipi kama alifanya hii pia kwetu, ambaye pia alituita, si tu kutoka kwa Wayahudi, lakini pia kutoka kwa watu wa Mataifa?
\s5
\v 25 Kama asemavyo pia katika Hosea: "Nitawaita watu wangu ambao hawakuwa watu wangu, na mpendwa wake ambaye hakupendwa.
\v 26 Na itakuwa kwamba pale iliposemwa kwao, 'Ninyi si watu wangu,' pale wataitwa 'wana wa Mungu aliye hai."'
\s5
\v 27 Isaya analia kuhusiana na Israeli, "Kama hesabu ya wana wa Israeli ingekuwa kama mchanga wa bahari, itakuwa ni masalia ambao wataokolewa.
\v 28 Kwa kuwa Bwana atalichukua neno lake juu ya nchi, mapema na kwa utimilifu.
\v 29 Na kama jinsi Isaya alivyosema awali, "Kama Bwana wa majeshi hakutuachia nyuma uzao kwa ajili yetu, tungekuwa kama Sodoma, na tungefanywa kama Gomora.
\s5
\v 30 Tutasema nini basi? kwamba watu wa Mataifa ambao walikuwa hawatafuti haki, walipata haki, haki kwa imani.
\v 31 Lakini Israeli, ambaye alitafuta sheria ya haki, hakuifikia.
\s5
\v 32 Kwanini si hivyo? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani, bali kwa matendo. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa,
\v 33 kama ilivyo kwisha andikwa, "Tazama, nimelaza jiwe la kujikwaa katika Sayuni na mwamba wa kukosa. Yeye ambaye huamini katika hili hataaibika."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ndugu, nia ya moyo wangu na ombi langu kwa Mungu ni kwa ajili yao, kwa ajili ya wokovu wao.
\v 2 Kwa kuwa nawashuhudia kwamba wanajuhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si kwa ajili ya ufahamu.
\v 3 Kwa kuwa hawajui haki ya Mungu, na wanatafuta kujenga haki yao wenyewe. Hawakuwa watiifu kwa haki ya Mungu.
\s5
\v 4 Kwa kuwa Kristo ndiye utimilifu wa sheria kwa ajili ya haki ya kila mtu aaminiye.
\v 5 Kwa kuwa Musa anaandika kuhusu haki ambayo huja kutokana na sheria: "Mtu ambaye hutenda haki ya sheria ataishi kwa haki hii."
\s5
\v 6 Lakini haki ambayo inatokana na imani husema hivi, "Usiseme moyoni mwako, 'Nani atapaa kwenda mbinguni?' (Hii ni kumleta Kristo chini).
\v 7 Na usiseme, 'Nani atashuka katika shimo?"' (Hii ni, kumleta Kristo juu kutoka kwa wafu).
\s5
\v 8 Lakini inasema nini? "Neno liko karibu na wewe, katika kinywa chako na katika moyo wako." Hilo ni neno la imani, ambalo tunatangaza.
\v 9 Kwa kuwa kama kwa kinywa chako unamkiri Yesu ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.
\v 10 Kwa kuwa kwa moyo mtu huamini na kupata haki, na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa andiko lasema, "Kila amwaminiye hata aibika."
\v 12 kwa kuwa hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani. Kwa kuwa Bwana yule yule ni Bwana wa wote, na ni tajiri kwa wote wamwitao.
\v 13 Kwa kuwa kila mtu ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.
\s5
\v 14 Kwa jinsi gani wanaweza kumwita yeye ambaye hawajamwamini? Na jinsi gani wanaweza kuamini katika yeye ambaye hawajamsikia? Na watasikiaje pasipo muhubiri?
\v 15 Na jinsi gani wanaweza kuhubiri, isipokuwa wametumwa? - Kama ilivyoandikwa, "Jinsi gani ni mizuri miguu ya wale ambao wanatangaza habari za furaha za mambo mema!"
\s5
\v 16 Lakini wote hawakusikiliza injili. Kwa kuwa Isaya hunena, "Bwana, ni nani aliyesikia ujumbe wetu?"
\v 17 Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo.
\s5
\v 18 Lakini nasema, "Je hawakusikia?" Ndiyo, kwa hakika sana. "Sauti yao imekwisha toka nje katika nchi yote, na maneno yao kwenda miisho ya dunia."
\s5
\v 19 Zaidi ya yote, Ninasema, "Je Israel hakujua?" Kwanza Musa hunena, "Nitawachokoza kuwatia wivu kwa watu ambao si taifa. Kwa njia ya taifa lisilo na uelewa, nitawachochea hadi mkasirike."
\s5
\v 20 Na Isaya ni jasiri sana na husema, "Nilipatikana na wale ambao hawakunitafuta. Nilionekana kwa wale ambao hawakunihitaji."
\v 21 Lakini kwa Israel husema, "Siku zote nilinyoosha mikono yangu kwa wasiotii na kwa watu wagumu."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi nasema, je, Mungu aliwakataa watu wake? Hata kidogo. Kwa kuwa mimi pia ni Mwiisraeli, wa ukoo wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.
\v 2 Mungu hakuwakataa watu wake, aliowajua tangu mwanzo. Je hamjui andiko linasema nini kuhusu Eliya, jinsi alivyomsihi Mungu juu ya Israeli?
\v 3 "Bwana, wamewaua manabii wako, nao wamebomoa madhabahu zako. Mimi peke yangu nimesalia, nao wanatafuta uhai wangu."
\s5
\v 4 Lakini jibu la Mungu lasema nini kwako? "Nimetunza kwa ajili yangu watu elfu saba ambao hawampigii magoti Baali."
\v 5 Hata hivyo, wakati huu wa sasa pia kuna walio salia kwa sababu ya uchaguzi wa neema.
\s5
\v 6 Lakini ikiwa ni kwa neema, si tena kwa matendo. Vinginevyo neema haitakuwa tena neema.
\v 7 Ni nini basi? Jambo ambalo Israeli alikuwa akitafuta, hakukipata, bali wateule walikipata, na wengine walitiwa uzito.
\v 8 Ni kama ilivyoandikwa: "Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie, mpaka leo hii."
\s5
\v 9 Naye Daudi anasema, "Acha meza zao na ziwe wavu, mtego, sehemu ya kujikwaa, na kulipiza kisasi dhidi yao.
\v 10 Acha macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona. Ukawainamishe migongo yao daima."
\s5
\v 11 Basi nasema, "Je, wamejikwaa hata kuanguka?" Isiwe hivyo kamwe. Badala yake, kwa kushindwa kwao, wokovu umefika kwa Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.
\v 12 Sasa ikiwa kushindwa kwao ni utajiri wa ulimwengu, na kama hasara yao ni utajiri wa mataifa, ni kiasi gani zaidi itakuwa kukamilika kwao?
\s5
\v 13 Na sasa naongea nanyi watu wa Mataifa. Kwa kuwa nimekuwa mtume kwa watu wa Mataifa mengine, najivunia huduma yangu.
\v 14 Labda nitawatia wivu walio mwili mmoja na mimi. Labda tutawaokoa baadhi yao.
\s5
\v 15 Maana ikiwa kukataliwa kwao ni maridhiano ya dunia, kupokelewa kwao kutakuwaje ila uhai toka kwa wafu?
\v 16 Kama matunda ya kwanza ni akiba, ndivyo ilivyo kwa donge la unga. Kama mzizi ni akiba, matawi nayo kadhalika.
\s5
\v 17 Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, kama wewe, tawi pori la mzeituni, ulipandikizwa kati yao, na kama ulishiriki pamoja nao katika mizizi ya utajiri wa mzeituni,
\v 18 usijisifu juu ya matawi. Lakini kama unajisifu, si wewe ambaye unaisaidia mizizi, bali mizizi inakusaidia wewe.
\s5
\v 19 Basi utasema, "Matawi yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika shina."
\v 20 Hiyo ni kweli. Kwa sababu ya kutoamini kwao walikatwa, lakini wewe ulisimama imara kwa sababu ya imani yako. Usijifikirie mwenyewe kwa hali ya juu sana, bali ogopa.
\v 21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, hatakuhurumia wewe pia.
\s5
\v 22 Angalia, basi, matendo mema na ukali wa Mungu. Kwa upande mmoja, ukali ulikuja juu ya Wayahudi ambao walianguka. Lakini kwa upande mwingine, wema wa Mungu huja juu yako, kama utadumu katika wema wake. Vinginevyo wewe pia utakatiliwa mbali.
\s5
\v 23 Na pia, kama hawataendelea katika kutoamini kwao, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
\v 24 Kwa maana ikiwa ninyi mlikatwa nje kwa ulio kwa asili mzeituni mwitu, na kinyume cha asili mlipandikizwa katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana hawa Wayahudi, ambao ni kama matawi ya asili kuweza kupandikizwa tena ndani ya mzeituni wao wenyewe?
\s5
\v 25 Kwa maana ndugu sitaki msijue, kuhusiana na siri hii, ili kwamba msiwe na hekima katika kufikiri kwenu wenyewe. Siri hii ni kwamba ugumu umetokea katika Israeli, hadi kukamilika kwa mataifa kutakapokuja.
\s5
\v 26 Hivyo Israeli wote wataokoka, kama ilivyoandikwa: "Kutoka Sayuni atakuja Mkombozi. Atauondoa uovu kutoka kwa Yakobo.
\v 27 Na hili litakuwa agano langu pamoja nao, wakati nitakapoziondoa dhambi zao."
\s5
\v 28 Kwa upande mmoja kuhusu injili, wanachukiwa kwa sababu yenu. Kwa upande mwingine kutokana na uchaguzi wa Mungu, wamependwa kwa sababu ya mababu.
\v 29 Kwa kuwa zawadi na wito wa Mungu haubadiliki.
\s5
\v 30 Kwa kuwa awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmeipokea rehema kwa sababu ya kuasi kwao.
\v 31 Kwa njia iyo hiyo, sasa hawa Wayahudi wameasi. Matokeo yake ni kwamba kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi wanaweza pia kupokea rehema.
\v 32 Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi, ili aweze kuwahurumia wote.
\s5
\v 33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hazichunguziki hukumu zake, na njia zake hazigunduliki!
\v 34 "Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani amekuwa mshauri wake?
\s5
\v 35 Au ni nani kwanza aliyempa kitu Mungu, ili alipwe tena?"
\v 36 Kwa maana kutoka kwake, na kwa njia yake na kwake, vitu vyote vipo. Kwake uwe utukufu milele. Amina.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kwa hiyo nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika kwa Mungu. Hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
\v 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu.
\s5
\v 3 Kwa maana nasema, kwa sababu ya neema niliyopewa, kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yake mwenyewe kuliko inavyompasa kufikiri. Bali, imempasa kufikiri kwa hekima, kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.
\s5
\v 4 Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja.
\v 5 Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.
\s5
\v 6 Tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa. Ikiwa karama ya mtu ni unabii, na itendeke kwa kadiri ya imani yake.
\v 7 Ikiwa karama ya mtu ni huduma, na atumike. Ikiwa mwingine ana karama ya kufundisha, basi, afundishe.
\v 8 Ikiwa karama ya mtu ni faraja, basi, afariji. Ikiwa karama ya mtu ni kutoa, afanye hivyo kwa ukarimu. Ikiwa karama ya mtu ni kuongoza, na litendeke kwa uangalifu. Ikiwa karama ya mtu ni katika kuonesha huruma, na litendeke kwa furaha.
\s5
\v 9 Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.
\v 10 Kuhusu upendo wa ndugu, pendaneni ninyi kwa ninyi. Kuhusu heshima, heshimianeni ninyi kwa ninyi.
\s5
\v 11 Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.
\v 12 Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.
\v 13 Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.
\s5
\v 14 Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.
\v 15 Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
\v 16 Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe.
\s5
\v 17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote.
\v 18 Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.
\s5
\v 19 Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana."
\v 20 "Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake."
\v 21 Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kila nafsi na iwe na utii kwa mamlaka ya juu, kwa kuwa hakuna mamlaka isipokuwa imetoka kwa Mungu. Na mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu.
\v 2 Kwa hiyo ambaye anapinga mamlaka hiyo hupinga amri ya Mungu; na wale waipingao watapokea hukumu juu yao wenyewe.
\s5
\v 3 Kwa kuwa watawala si tishio kwa watendao mema, bali kwa watendao maovu. Je unatamani kutoogopa mamlaka? Fanya yaliyo mema, na utasifiwa nayo.
\v 4 Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Bali kama utatenda yaliyo maovu, ogopa; kwa kuwa habebi upanga bila sababu. Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, mlipa kisasi kwa ghadhabu juu ya yule afanyaye uovu.
\v 5 Kwa hiyo inakupasa utii, si tu kwa sababu ya gadhabu, bali pia kwa sababu ya dhamiri.
\s5
\v 6 Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili.
\v 7 Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima.
\s5
\v 8 Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria.
\v 9 Kwa kuwa, "Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani," na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: "Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe."
\v 10 Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.
\s5
\v 11 Kwa sababu ya hili, mnajua wakati, kwamba tayari ni wakati wa kutoka katika usingizi. Kwa kuwa wokovu wetu umekaribia zaidi ya wakati ule tulio amini kwanza.
\v 12 Usiku umeendelea, na mchana umekaribia. Na tuweke pembeni matendo ya giza, na tuvae silaha za nuru.
\s5
\v 13 Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.
\v 14 Bali tumvae Bwana Yesu Kristo, na tusiweke nafasi kwa ajili ya mwili, kwa tamaa zake.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Mpokeeni yeyote ambaye ni dhaifu katika imani, bila kutoa hukumu kuhusu mawazo yake.
\v 2 Mtu mmoja ana imani ya kula chochote, mwingine ambaye ni dhaifu anakula mboga tu.
\s5
\v 3 Mtu ambaye anakula kila kitu asimdharau yeye asiyekula kila kitu. Na yeye ambaye hali kila kitu asimuhukumu mwingine ambaye hula kila kitu. Kwa kuwa Mungu amekwisha mpokea.
\v 4 Wewe ni nani, wewe ambaye unamuhukumu mtumishi ambaye ni miliki ya mtu mwingine? Ni mbele ya Bwana wake kwamba husimama au huanguka. Lakini atainuliwa, kwa kuwa Bwana anaweza kumfanya asimame.
\s5
\v 5 Mtu mmoja huthamini siku moja kuliko nyingine. Mwingine huthamini kila siku sawa sawa. Hebu kila mtu na ashawishike katika akili yake mwenyewe.
\v 6 Yeye ambaye anashika siku, anashika kwa ajili ya Bwana. Na kwa yeye alaye, hula kwa ajili ya Bwana, kwa kuwa anampa Mungu shukrani. Yeye ambaye hali, hujizuia kutokula kwa ajili ya Bwana. Yeye pia hutoa shukrani kwa Mungu.
\s5
\v 7 Kwa kuwa hakuna aishie kwa nafsi yake, na hakuna afae kwa ajili yake mwenyewe.
\v 8 Kwa kuwa ikiwa tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na ikiwa tunakufa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi ikiwa tunaishi au tunakufa tu mali ya Bwana.
\v 9 Kwa kuwa ni kwa kusudi hili Kristo alikufa na kuishi tena, kwamba awe Bwana wa wote wafu na waishio.
\s5
\v 10 Lakini wewe, kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe, kwa nini unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
\v 11 Kwa kuwa imeandikwa, "Kama niishivyo," asema Bwana, "Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu."
\s5
\v 12 Hivyo basi, kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu.
\v 13 Kwa hiyo, tusiendelee tena kuhukumiana, lakini badala yake amua hivi, kwamba hakuna atakaye weka kikwazo au mtego kwa ndugu yake.
\s5
\v 14 Ninajua na nimeshawishika katika Bwana Yesu, kwamba hakuna kitu kilicho najisi chenyewe. Ni kwa yeye tu anayedhani kuwa chochote ni najisi, kwa kuwa kwake ni najisi.
\v 15 Ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anahuzunika, hautembei tena katika upendo. Usimharibu kwa chakula chako mtu ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa.
\s5
\v 16 Hivyo msiruhusu matendo yenu mema yakasababisha watu kuwadhihaki.
\v 17 Kwa kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya chakula na kinywaji, bali ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.
\s5
\v 18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo kwa jinsi hii amekubalika kwa Mungu na amekubalika kwa watu.
\v 19 Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine.
\s5
\v 20 Usiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya chakula. Vitu vyote kwa kweli ni safi, lakini ni vibaya kwa mtu yule ambaye hula na kumsababisha yeye kujikwaa.
\v 21 Ni vyema kutokula nyama, wala kunywa divai, wala chochote ambacho kwa hicho ndugu yako hukwazwa.
\s5
\v 22 Hizi imani maalumu ulizo nazo, ziweke kati yako mwenyewe na Mungu. Amebalikiwa yule ambaye hajihukumu mwenyewe katika kile anachokikubali.
\v 23 Aliye na mashaka amehukumiwa ikiwa anakula, kwa sababu haitokani na imani. Na chochote kisichotokana na imani ni dhambi.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Sasa sisi tulio na nguvu tunapaswa kuuchukua udhaifu wa walio dhaifu, na hatupaswi kujipendeza wenyewe.
\v 2 Kila mmoja wetu ampendeze jirani yake kwani ni jambo jema, kwa lengo la kumjenga.
\s5
\v 3 Kwani hata Kristo hakujipendeza mwenyewe. Badala yake, ilikuwa kama ilivyoandikwa, "Matusi ya wale waliokutukana yamenipata mimi."
\v 4 Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza, kwa kusudi kwamba kupitia uvumilivu na kupitia kutiwa moyo na maandiko tungekuwa na ujasiri.
\s5
\v 5 Sasa Mungu wa uvumilivu na wa kutia moyo awape kuwa na nia sawa kwa kila mmoja kulingana na Yesu Kristo.
\v 6 Aweze kufanya hivi kwa nia moja muweze kumsifu kwa kinywa kimoja Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 7 Kwa hiyo mpokeeni kila mmoja, kama vile Kristo alivyowapokea, kwa utukufu wa Mungu.
\s5
\v 8 Kwani nasema kwamba Kristo amefanywa mtumishi wa tohara kwa niaba ya ukweli wa Mungu. Alifanya hivi ili kwamba aweze kuthibitisha ahadi zilizotolewa kwa mababa,
\v 9 na kwa mataifa kumtukuza Mungu kwa neema yake. Kama ambavyo imeandikwa, "Kwa hiyo nitatoa sifa kwako miongoni mwa mataifa na kuimba sifa katika jina lako."
\s5
\v 10 Tena inasema, "Furahini, ninyi watu wa mataifa, pamoja na watu wake."
\v 11 Na tena, "Msifuni Bwana, ninyi mataifa yote; acha watu wa mataifa yote wamsifu yeye."
\s5
\v 12 Tena Isaya asema, "Kutakuwa na shina la Yese, na mmoja atakayeinuka kutawala juu ya mataifa. Mataifa watakuwa na tumaini katika yeye."
\s5
\v 13 Sasa Mungu wa tumaini awajaze na furaha yote na amani kwa kuamini, ili kwamba muweze kuzidi katika tumaini, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
\s5
\v 14 Mimi mwenyewe pia nimeshawishiwa nanyi, ndugu zangu. Nimeshawishiwa kwamba pia ninyi wenyewe mmejazwa na wema, mmejazwa na maarifa yote. Ninashawishiwa kwamba, ninyi mwaweza pia kuhimizana kila mmoja na mwenzake.
\s5
\v 15 Lakini ninaandika kwa ujasiri zaidi kwenu juu ya mambo fulani ili kuwakumbusha tena, sababu ya kipawa nilichopewa na Mungu.
\v 16 Kipawa hiki kilikuwa kwamba niweze kuwa mtumishi wa Yesu Kristo aliyetumwa kwa mataifa, kujitoa kama kuhani wa injili ya Mungu. Ningeweza kufanya hivi ili kujitoa kwangu kwa mataifa kuwe kumekubaliwa, kumetengwa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.
\s5
\v 17 Hivyo furaha yangu iko katika Kristo Yesu na katika mambo ya Mungu.
\v 18 Kwani sitaweza kuthubutu kunena lolote isipokuwa kwamba Kristo amekamilisha kupitia kwangu utii wa mataifa. Haya mambo yametimizwa kwa neno na tendo,
\v 19 kwa nguvu za ishara na maajabu, na kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ili kwamba kutoka Yerusalem, na kuzungukia mbali kama Iliriko, niweze kuichukua nje kwa ukamilifu injili ya Kristo.
\s5
\v 20 Kwa njia hii, nia yangu imekuwa kuitangaza injili, lakini si mahali Kristo anajulikana kwa jina, ili kwamba nisiweze kujenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
\v 21 Kama ilivyoandikwa: "Ambao kwa yeye hawana habari zake alikuja watamwona, na wale ambao hawakumsikia watamfahamu."
\s5
\v 22 Kwahiyo nilikuwa pia nimezuiliwa mara nyingi kuja kwenu.
\v 23 Lakini sasa, sina tena sehemu yoyote katika mikoa hii, na nimekuwa nikitamani kwa miaka mingi kuja kwenu.
\s5
\v 24 Hivyo mara zote nikienda Hispania, ninatumaini kuwaona nikipita, na kuweza kupelekwa njia yangu na ninyi, baada ya kuwa nimefurahia ushirika na ninyi kwa muda.
\v 25 Lakini sasa ninakwenda Yerusalemu kuwahudumia waumini.
\s5
\v 26 Maana iliwapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo maalumu kwa masikini miongoni mwa waumini huko Yerusalemu.
\v 27 Ndiyo, ilikuwa kwa upendo wao, na hakika, wamekuwa wadeni wao. Maana ikiwa mataifa wameshiriki katika mambo yao ya kiroho, wanadaiwa na wao pia kuwahudumia katika mahitaji ya vitu.
\s5
\v 28 Kwahiyo, wakati nimekamilisha hivi na kuwa na utoshelevu wa tunda hili kwao, mimi nitakwenda njiani pamoja nanyi huko Hispania.
\v 29 Najua kwamba, wakati nikija kwenu, nitakuja katika utimilifu wa baraka za Kristo.
\s5
\v 30 Sasa ninawasihi, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, kwamba mshiriki pamoja nami katika maombi yenu kwa Mungu kwa ajili yangu.
\v 31 Ombeni kwamba niweze kuokolewa kutoka kwao wasio na utii katika Yudea, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu iweze kupokelewa na waumini.
\v 32 Ombeni kwamba ninaweza kuja kwenu kwa furaha kupitia mapenzi ya Mungu, na kwamba niweze kuwa pamoja nanyi, kupata kupumzika.
\s5
\v 33 Na Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amina
\s5
\c 16
\p
\v 1 Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,
\v 2 ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.
\s5
\v 3 Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
\v 4 ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
\v 5 Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
\s5
\v 6 Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
\v 7 Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.
\v 8 Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
\s5
\v 9 Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.
\v 10 Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.
\v 11 Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.
\s5
\v 12 Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,
\v 13 Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu.
\v 14 Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.
\s5
\v 15 Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.
\v 16 Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
\s5
\v 17 Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.
\v 18 Kwa maana watu kama hawa hawamtumikii Kristo Bwana, bali matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo wanadanganya mioyo ya wasio na hatia.
\s5
\v 19 Kwa mfano wa utii wenu mwamfikia kila mmoja. Kwa hiyo, nafurahi juu yenu, lakini nawataka ninyi mwe na busara katika hali ya wema, na kutokuwa na hatia mbele ya uovu.
\v 20 Mungu wa amani hatakawia kumwangamiza shetani chini ya nyayo zenu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
\s5
\v 21 Timotheo, mtendakazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, Yasoni na Sospeter, jamaa zangu.
\v 22 Mimi, Tertio, niliyeuandika waraka huu, nawasalimu katika jina la Bwana.
\s5
\v 23 Gayo, aliyenitunza na kwa kanisa lote, lawasalimu. Erasto, mtunza hazina wa mji, awasalimu, pamoja na Kwarto aliye ndugu.
\v 24 (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. Tazama Warumi 16: 20. "Neema ya Bwana Yesu Kristo ikae nanyi nyote. Amina.")
\s5
\v 25 Sasa kwake yeye aliye na uwezo kufanya msimame kulingana na injili na mafundisho ya Yesu Kristo, kulingana na ufunuo wa siri iliyofichwa kwa muda mrefu,
\v 26 lakini sasa imekwisha funuliwa na kufanywa kujulikana na maandiko ya unabii kulingana na amri ya Mungu wa milele, kwa utii wa imani miongoni mwa mataifa yote?
\s5
\v 27 Kwa Mungu pekee mwenye hekima, kupitia Yesu Kristo, kuwe na utukufu milele yote. Amina

832
47-1CO.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,832 @@
\id 1CO
\ide UTF-8
\h 1 Wakorintho
\toc1 1 Wakorintho
\toc2 1 Wakorintho
\toc3 1co
\mt 1 Wakorintho
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, aliyeitwa na Kristo Yesu kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
\v 2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.
\v 3 Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 4 Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.
\v 5 Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote.
\v 6 Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.
\s5
\v 7 Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 8 Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.
\s5
\v 10 Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.
\v 11 Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu.
\s5
\v 12 Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, "Mimi ni wa Paulo," au "Mimi ni wa Apolo", au "Mimi ni wa Kefa" au "Mimi ni wa Kristo".
\v 13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
\s5
\v 14 Namshukuru Mungu kuwa sikumbatiza yeyote, isipokuwa Krispo na Gayo.
\v 15 Hii ilikuwa kwamba hakuna yeyote angesema mlibatizwa kwa jina langu.
\v 16 (Pia niliwabatiza wa nyumba ya Stephania. Zaidi ya hapo, sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
\s5
\v 17 Kwa kuwa, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwamba nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.
\s5
\v 18 Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaokufa. Lakini kwa wale ambao Mungu anawaokoa, ni nguvu ya Mungu.
\v 19 Kwa kuwa imeandikwa, "Nitaiharibu hekima ya wenye busara. Nitauharibu ufahamu wa wenye akili."
\s5
\v 20 Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga?
\v 21 Tangu dunia imekuwa katika hekima yake haikumjua Mungu, ilimpendeza Mungu katika ujinga wao wa kuhubiri ili kuokoa wale wanaoamini.
\s5
\v 22 Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima.
\v 23 Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani.
\s5
\v 24 Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu.
\v 25 Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
\s5
\v 26 Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.
\v 27 Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.
\s5
\v 28 Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.
\v 29 Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.
\s5
\v 30 Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.
\v 31 Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, "Anayejisifu, ajisifu katika Bwana."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Nilipokuja kwenu kaka na dada zangu, sikuja kwa maneno ya ushawishi na hekima kama nilivyohubiri kweli iliyofichika kuhusu Mungu.
\v 2 Niliamua kutojua chochote nilipokuwa miongoni mwenu isipokuwa Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa.
\s5
\v 3 Na nilikuwa nanyi katika udhaifu, na katika hofu, na katika kutetemeka sana.
\v 4 Na ujumbe wangu na kuhubiri kwangu hakukuwa katika maneno ya ushawishi na hekima. Badala yake, yalikuwa katika kumdhihirisha Roho na ya nguvu,
\v 5 ili kwamba imani yenu isiwe katika hekima ya wanadadamu, bali katika nguvu ya Mungu.
\s5
\v 6 Sasa tunaizungumza hekima miongoni mwa watu wazima, lakini si hekima ya dunia hii, au ya watawala wa nyakati hizi, ambao wanaopita.
\v 7 Badala yake, tunaizungumza hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, hekima iliyofichika ambayo Mungu aliichagua kabla ya nyakati za utukufu wetu.
\s5
\v 8 Hakuna yeyote wa watawala wa nyakati hizi aliyeijua hekima hii, Kama wangeifahamu katika nyakati zile, wasingelimsulubisha Bwana wa utukufu.
\v 9 Lakini kama ilivyoandikwa, "Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye."
\s5
\v 10 Haya ni mambo ambayo Mungu ameyafunua kwetu kupitia Roho, Kwa kuwa Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu.
\v 11 Kwa kuwa nani afahamuye mawazo ya mtu, isipokuwa roho ya mtu ndani yake? Hivyo pia, hakuna ajuaye mambo ya ndani ya Mungu, isipokuwa Roho wa Mungu.
\s5
\v 12 Lakini hatukupokea roho ya dunia, lakini Roho ambaye anatoka kwa Mungu, ili kwamba tuweze kujua kwa uhuru mambo tuliyopewa na Mungu.
\v 13 Tunasema mambo haya kwa maneno, ambayo hekima ya mtu haiwezi kufundisha, lakini ambayo Roho hutufundisha. Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho.
\s5
\v 14 Mtu asiye wa kiroho hapokei mambo ambayo ni ya Roho wa Mungu, kwa kuwa hayo ni upuuzi kwake. Hawezi kuyajua kwa sababu yanatambuliwa kiroho.
\v 15 Kwa yule wa kiroho huhukumu mambo yote. Lakini huhukumiwa na wengine.
\v 16 "Ni nani anaweza kuyajua mawazo ya Bwana, ambaye anaweza kumfundisha yeye?" Lakini tuna mawazo ya Kristo.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Na mimi, kaka na dada zangu, sikusema nanyi kama watu kiroho, lakini kama na watu wa kimwili. Kama na watoto wadogo katika Kristo.
\v 2 Niliwanywesha maziwa na si nyama, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa kula nyama. Na hata sasa hamjawa tayari.
\s5
\v 3 Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?
\v 4 Kwa kuwa mmoja husema, "Namfuata Paulo" Mwingine husema "Namfuata Apolo," hamuishi kama wanadamu?
\v 5 Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.
\s5
\v 6 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu akakuza.
\v 7 Kwa hiyo, si aliye panda wala aliyetia maji ana chochote. Lakini ni Mungu anayekuza.
\s5
\v 8 Sasa apandaye na atiaye maji wote ni sawa, na kila mmoja atapokea ujira wake kulingana na kazi yake.
\v 9 Kwa kuwa sisi tu watendakazi wa Mungu, ninyi ni bustani ya Mungu, jengo la Mungu.
\s5
\v 10 Kutokana na neema ya Mungu niliyopewa kama mjenzi mkuu, niliuweka msingi, na mwingine anajenga juu yake. Lakini mtu awe makini jinsi ajengavyo juu yake.
\v 11 Kwa kuwa hakuna mwingine awezaye kujenga msingi mwingine zaidi ya uliojengwa, ambao ni Yesu Kristo.
\s5
\v 12 Sasa, kama mmoja wenu ajenga juu yake kwa dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, nyasi, au majani,
\v 13 kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.
\s5
\v 14 Kama chochote mtu alichojenga kitabaki, yeye atapokea zawadi.
\v 15 Lakini kama kazi ya mtu ikiteketea kwa moto, atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama vile kuepuka katika moto.
\s5
\v 16 Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
\v 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.
\s5
\v 18 Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama "mjinga" ndipo atakuwa na hekima.
\v 19 Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, "Huwanasa wenye hekima kwa hila zao"
\v 20 Na tena "Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili."
\s5
\v 21 Hivyo mtu asijivunie wanadamu! Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu.
\v 22 Kama ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au dunia, au maisha, au kifo, au vitu vilivyopo, au vitakavyokuwepo. Vyote ni vyenu,
\v 23 na ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Hivi ndivyo mtu atuhesabu sisi, kama watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za kweli za Mungu.
\v 2 Katika hili, kinachotakiwa kwa uwakili ni kwamba wawe wa kutumainiwa.
\s5
\v 3 Lakini kwangu mimi ni kitu kidogo sana kuwa ninahukumiwa na ninyi au hukumu ya kibinadamu. Kwa kuwa sijihukumu hata mimi mwenyewe.
\v 4 Sijihukumu mimi mwenyewe, hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye.
\s5
\v 5 Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu.
\s5
\v 6 Sasa, kaka na dada zangu, mimi mwenyewe na Apolo nimetumia kanuni hizi kwa ajili yenu. Ili kwamba kutoka kwetu mnaweza kujifunza maana ya usemi, "Usiende zaidi ya kilivyoandikwa." Hii ni kwamba hakuna mmoja wenu ajivunaye juu ya mwingine.
\v 7 Maana ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine? Ni nini ulicho nacho hukukipokea bure? Kama umekwisha kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo?
\s5
\v 8 Tayari mnavyo vyote ambavyo mngetaka! Tayari mmekuwa na utajiri! Mmeanza kutawala-na kwamba mnamiliki zaidi yetu sisi! Kweli, nawatakia umililki mwema ili kwamba tumiliki pamoja nanyi.
\v 9 Kwa hiyo ninadhani Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha wa mwisho katika mustari wa maandamano na kama watu waliohukumiwa kuuawa. Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu.
\s5
\v 10 Sisi ni wajinga kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye hekima katika Kristo. Tu wanyonge, lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakina sisi tunadharauliwa.
\v 11 Hata saa hii tuna njaa na kiu, hatuna nguo, tuna mapigo, na tena hatuna makazi.
\s5
\v 12 Tunafanya kazi kwa bidii, kwa mikono yetu wenyewe. Tunapodharauliwa, twabariki. Wakati tunapoteswa, twavumilia.
\v 13 Tunapotukanwa, twarudisha kwa upole. Tumekuwa, na tu bado tunahesabiwa kuwa kama kukataliwa na dunia na takataka kwa mambo yote.
\s5
\v 14 Siandiki mambo haya kuwaaibisha ninyi, lakini kuwarudi ninyi kama watoto wangu niwapendao.
\v 15 Hata kama mna waalimu makumi elfu katika Kristo, hamna baba wengi. Kwa kuwa nimekuwa baba yenu katika Yesu Kristo kupitia injili.
\v 16 Hivyo ninawasihi mniige mimi.
\s5
\v 17 Hiyo ndiyo sababu nilimtuma kwenu Timotheo, mpendwa wangu na mtoto mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia zangu katika Kristo, kama ninavyofundisha kila mahali na kila kanisa.
\v 18 Sasa baadhi yenu wanajisifu, wakitenda kana kwamba sitakuja kwenu.
\s5
\v 19 Lakini nitakuja kwenu kitambo, kama Bwana akipenda. Ndipo nitajua si maneno yao tu wanaojisifu, lakini nitaona nguvu zao.
\v 20 Kwa kuwa ufalme wa Mungu hauwi katika maneno bali katika nguvu.
\v 21 Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo au kwa upendo na katika roho ya upole?
\s5
\c 5
\p
\v 1 Tumesikia taarifa kuwa kuna zinaa miongoni mwenu, aina ya zinaa ambayo haipo hata katikati ya watu wa Mataifa. Tuna taarifa kwamba mmoja wenu analala na mke wa baba yake.
\v 2 Nanyi mwajisifu! Badala ya kuhuzunika? Yule aliyefanya hivyo anapaswa kuondolewa miongoni mwenu.
\s5
\v 3 Ingawa sipo pamoja nanyi kimwili lakini nipo nanyi kiroho, nimekwisha mhukumu yeye aliyefanya hivi, kama vile nilikuwepo.
\v 4 Mnapokutanika pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu, na roho yangu ipo pale kama kwa nguvu za Bwana wetu Yesu, nimekwisha mhukumu mtu huyu.
\v 5 Nimekwisha kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani ili kwamba mwili wake uharibiwe, ili roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.
\s5
\v 6 Majivuno yenu si kitu kizuri. Hamjui chachu kidogo huharibu donge zima?
\v 7 Jisafisheni ninyi wenyewe chachu ya kale, ili kwamba muwe donge jipya, ili kwamba mwe mkate usiochachuliwa. Kwa kuwa, Kristo, Mwana Kondoo wetu wa pasaka amekwisha kuchinjwa.
\v 8 Kwa hiyo tusherekee karamu si kwa chachu ya kale, chachu ya tabia mbaya na uovu. Badala yake, tusherekee na mkate usiotiwa chachu wa unyenyekevu na kweli.
\s5
\v 9 Niliandika katika barua yangu kuwa msichangamane na wazinzi.
\v 10 Sina maana wazinzi wa dunia hii, au na wenye tamaa au wanyang'anyi au waabudu sanamu kwa kukaa mbali nao, basi ingewapasa mtoke duniani.
\s5
\v 11 Lakini sasa nawaandikia kutojichanganya na yeyote anayeitwa kaka au dada katika Kristo, lakini anaishi katika uzinzi au ambaye ni mwenye kutamani, au mnyang'anyi, au mwabudu sanamu, au mtukanaji au mlevi. Wala msile naye mtu wa namna ile.
\v 12 Kwa hiyo nitajihusishaje kuwahukumu walio nje ya Kanisa? Badala yake, ninyi hamkuwahukumu walio ndani ya kanisa?
\v 13 Lakini Mungu anawahukumu walio nje. "Mwondoeni mtu mwovu miongoni mwenu"
\s5
\c 6
\p
\v 1 Mmoja wenu anapokuwa na tatizo na mwenzake, anathubutu kwenda kwa mahakama ya wasio haki kuliko mbele ya waumini?
\v 2 Hamjui kuwa waumini watauhukumu ulimwengu? Na kama mtauhukumu ulimwengu, hamuwezi kuamua mambo yasiyo muhimu?
\v 3 Hamjui kuwa tutawahukumu malaika? Kwa kiasi gani zaidi, tunaweza kuamua mambo ya maisha haya?
\s5
\v 4 Kama tunaweza kuhukumu mambo ya maisha haya, kwa nini mnathubutu kupeleka mashitaka mbele ya wasiosimama kanisani?
\v 5 Nasema haya kwa aibu yenu. Hakuna mwenye busara miongoni mwenu wa kutosha kuweka mambo sawa kati ya ndugu na ndugu?
\v 6 Lakini kama ilivyo sasa, mwamini mmoja huenda mahakamani dhidi ya muumini mwingine, na mashitaka hayo huwekwa mbele ya hakimu asiyeamini!
\s5
\v 7 Ukweli ni kwamba kuna matatizo katikati ya Wakristo yaliyoleta tayari usumbufu kwenu. Kwanini msiteseke kwa mabaya? Kwanini mnakubali kudanganywa?
\v 8 Lakini mmetenda uovu na kudanganya wengine, na hao ni kaka na dada zenu!
\s5
\v 9 Hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msiamini uongo. Waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, wafiraji, walawiti,
\v 10 wevi, wachoyo, walevi, wanyang'anyi, watukanaji-hakuna miongoni mwao atakayeurithi ufalme wa Mungu.
\v 11 Na hao walikuwa baadhi yao ni ninyi. Lakini mmekwisha kutakaswa, lakini mmekwisha kuoshwa, lakini mmekwisha kutengwa kwa Mungu, lakini mmefanywa haki mbele za Mungu katika jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.
\s5
\v 12 "Vitu vyote ni halali kwangu", lakini si kila kitu kina faida. "Vitu vyote ni halali kwangu," lakini sitatawaliwa na kimoja cha hivyo.
\v 13 "Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula," lakini Mungu atavitowesha vyote. Mwili haujaumbwa kwa ajili ya ukahaba, badala yake, mwili ni kwa ajili ya Bwana, na Bwana atauhudumia mwili.
\s5
\v 14 Mungu alimfufua Bwana na sisi pia atatufufua kwa nguvu zake.
\v 15 Hamjui kwamba miili yenu ina muunganiko na Kristo? Mwawezaje kuvitoa viungo vya Kristo na kwenda kuviunganisha na kahaba? Haiwezekani!
\s5
\v 16 Hamjui kwamba anayeungana na kahaba amekuwa mwili mmoja naye? Kama andiko lisemavyo, "Wawili watakuwa mwili mmoja."
\v 17 Lakini anayeungana na Bwana anakuwa roho moja pamoja naye.
\s5
\v 18 Ikimbieni zinaa! "Kila dhambi aifanyayo mtu ni nje na mwili wake. Lakini zinaa, mtu hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
\s5
\v 19 Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe?
\v 20 Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Kuhusu mambo mliyoniandikia: Kuna wakati ambapo ni vizuri mwanaume asilale na mke wake.
\v 2 Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe.
\s5
\v 3 Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe.
\v 4 Si mke aliye na mamlaka juu ya mwili wake, ni mme. Na vile vile, mme naye hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke anayo.
\s5
\v 5 Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi.
\v 6 Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri.
\v 7 Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile.
\s5
\v 8 Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi.
\v 9 Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa heri kwao kuolewa kuliko kuwaka tamaa.
\s5
\v 10 Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. "Mke asitengane na mme wake."
\v 11 Lakini kama akijitenga kutoka kwa mmewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mmewe. Na "Mme asimpe talaka mke wake."
\s5
\v 12 Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
\v 13 Kama mwanamke ana mme asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.
\v 14 Kwa mme asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mmewe aaminiye. Vinginevyo watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.
\s5
\v 15 Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka na aende. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani.
\v 16 Unajuaje kama mwanamke, huenda utamwokoa mmeo? Au unajuaje kama mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?
\s5
\v 17 Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote.
\v 18 Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa.
\v 19 Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.
\s5
\v 20 Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini.
\v 21 Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hiyo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo.
\v 22 Kwa mmoja aliyeitwa na Bwana kama mtumwa ni mtu huru katika Bwana. Kama vile, mmoja aliye huru alipoitwa kuamini ni mtumwa wa Kristo.
\v 23 Mmekwisha nunuliwa kwa thamani, hivyo msiwe watumwa wa wanadamu.
\v 24 Kaka na dada zangu, katika maisha yoyote kila mmoja wetu tulipoitwa kuamini, tubaki kama vile.
\s5
\v 25 Sasa, wale wote ambao hawajaoa kamwe, sina amri kutoka kwa Bwana. Lakini nawapa maoni yangu kama nilivyo. Kwa huruma za Bwana, zinazo aminika
\v 26 Kwa hiyo, ninafikiri hivyo kwa sababu ya usumbufu, ni vyema mwanaume abaki kama alivyo.
\s5
\v 27 Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke.
\v 28 Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.
\s5
\v 29 Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana.
\v 30 Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote.
\v 31 Na wote wanaoshughulika na ulimwengu, wawe kama hawakushughulika nao. Kwa kuwa mitindo ya dunia inafikia mwisho wake.
\s5
\v 32 Ninataka muwe huru kwa masumbufu yote. Mwanaume asiyeoa anajihusisha na vitu vinavyo mhusu Bwana, namna ya kumpendeza yeye.
\v 33 Lakini mwanaume aliyeoa hujihusisha na mambo ya dunia, namna ya kumpendeza mkewe,
\v 34 amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.
\s5
\v 35 Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.
\s5
\v 36 Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi.
\v 37 Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa.
\v 38 Hivyo, anayemwoa mwanamwali wake afanya vyema, na yeyote ambaye anachagua kutooa atafanya vyema zaidi.
\s5
\v 39 Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu.
\v 40 Bado katika maamuzi yangu, atakuwa na furaha zaidi kama akiishi kama alivyo. Na ninafikiri kuwa nami pia nina Roho wa Mungu.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Sasa kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua ya kwamba "sisi sote tuna maarifa." Maarifa huleta majivuno, bali upendo hujenga.
\v 2 Ikiwa mtu yeyote anadhani kwamba anajua jambo fulani, mtu huyo bado hajui kama impasavyo kujua.
\v 3 Lakini ikiwa mmoja wapo akimpenda Mungu, mtu huyo anajulikana naye.
\s5
\v 4 Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa "sanamu si kitu katika dunia hii," na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu."
\v 5 Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo "miungu na mabwana wengi."
\v 6 "Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo."
\s5
\v 7 Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.
\s5
\v 8 Lakini chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu. Sisi sio wabaya sana kama tusipo kula, wala wema sana ikiwa tutakula.
\v 9 Lakini iweni makini ya kwamba uhuru wenu usiwe sababu ya kumkwaza aliye dhaifu katika imani.
\v 10 Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?
\s5
\v 11 Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa.
\v 12 Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo.
\v 13 Kwa hiyo, ikiwa chakula kinasababisha kumkwaza kaka au dada, sitakula nyama kamwe, ili nisimsababishe kaka au dada yangu kuanguka.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana?
\v 2 Ikiwa mimi si mtume kwa wengine, angalau ni mtume kwenu ninyi. Kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana.
\s5
\v 3 Huu ndio utetezi wangu kwa wale wanaonichunguza mimi.
\v 4 Je hatuna haki ya kula na kunywa?
\v 5 Hatuna haki kuchukua mke aliye amini kama wafanyavyo mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
\v 6 Au ni mimi peke yangu na Barnaba ambao tunapaswa kufanya kazi?
\s5
\v 7 Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mzabibu na asile matunda yake? Au ni nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake?
\v 8 Je ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu? Sheria nayo haisemi haya?
\s5
\v 9 Kwa kuwa imeandikwa katika sheria ya Musa, "usimfunge ng'ombe kinywa apulapo nafaka." Ni kweli kwamba hapa Mungu anajali ng'ombe?
\v 10 Au je hasemi hayo kwa ajili yetu? imeandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu yeye alimaye nafaka inampasa kulima kwa matumaini, naye avunaye inampasa avune kwa matarajio ya kushiriki katika mavuno.
\v 11 Ikiwa tulipanda vitu vya rohoni miongoni mwenu, Je! Ni neno kubwa kwetu tukivuna vitu vya mwilini kutoka kwenu?
\s5
\v 12 Ikiwa wengine walipata haki hii kutoka kwenu, Je! Sisi si zaidi? Hata hivyo, hatukuidai haki hii. Badala yake, tulivumilia mambo yote badala ya kuwa kikwazo cha injili ya Kristo.
\v 13 Hamjui ya kuwa wote wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni? Hamjui ya kuwa wote watendao kazi madhabahuni hupata sehemu ya kile kilichotolewa madhabahuni?
\v 14 Kwa jinsi iyo hiyo, Bwana aliagiza ya kuwa wote wanaoitangaza injili sharti wapate kuishi kutokana na hiyo injili.
\s5
\v 15 Lakini sijawadai haki zote hizi. Na siandiki haya ili jambo lolote lifanyike kwa ajili yangu. Ni heri mimi nife kuliko mtu yeyote kubatilisha huku kujisifu kwangu.
\v 16 Maana ikiwa naihubiri injili, sina sababu ya kujisifu, kwa sababu ni lazima nifanye hivi. Na ole wangu nisipoihubiri injili!
\s5
\v 17 Kwa maana nikifanya hivi kwa hiari yangu, nina thawabu. Lakini ikiwa si kwa hiari, bado nina jukumu nililopewa kuwa wakili.
\v 18 Basi thawabu yangu ni nini? Ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili pasipo gharama na bila kutumia kwa utimilifu wa haki yangu niliyonayo katika Injili.
\s5
\v 19 Maana japo nimekuwa huru kwa wote, nilifanyika mtumwa wa wote, ili kwamba niweze kuwapata wengi zaidi.
\v 20 Kwa Wayahudi nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao aliye chini ya sheria ili niwapate wale walio chini ya sheria. Nilifanya hivyo ingawa mimi binafsi sikuwa chini ya sheria.
\s5
\v 21 Kwa wale walio nje ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao nje ya sheria, ingawa mimi binafsi sikuwa nje ya sheria ya Mungu, bali chini ya sheria ya Kristo. Nilifanya hivyo ili niwapate wale walio nje ya sheria.
\v 22 Kwa walio wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate walio wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi.
\v 23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya injili, ili nipate kushiriki katika baraka.
\s5
\v 24 Hamjui ya kuwa katika mbio wote washindanao hupiga mbio, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Hivyo pigeni mbio ili mpate tuzo.
\v 25 Mwana michezo hujizuia katika yote awapo katika mafunzo. Hao hufanya hivyo ili wapokee taji iharibikayo, lakini sisi tunakimbia ili tupate taji isiyoharibika.
\v 26 Kwa hiyo mimi sikimbii bila sababu au napigana ngumi kama kupiga hewa.
\v 27 Lakini nautesa mwili wangu na kuufanya kama mtumwa, ili kwamba nijapokwisha kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisiwe wa kukataliwa.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nataka ninyi mjue kaka na dada zangu, ya kuwa baba zetu walikuwa chini ya wingu na wote walipita katika bahari.
\v 2 Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari,
\v 3 na wote walikula chakula kile kile cha roho.
\v 4 Wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho. Maana walikunywa kutoka katika mwamba wa roho uliowafuata, na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
\s5
\v 5 Lakini Mungu hakupendezwa sana na wengi wao, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
\v 6 Basi mambo haya yote yalikuwa mifano kwetu, ili sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya kama na wao walivyofanya.
\s5
\v 7 Msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, "Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi."
\v 8 Tusifanye uasherati kama wengi wao walivyofanya. Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu kwa sababu hiyo.
\s5
\v 9 Wala tusimjaribu Kristo, kama wengi wao walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka.
\v 10 Na pia msinung'unike, kama wengi wao walivyonung'unika na kuharibiwa na malaika wa mauti.
\s5
\v 11 Basi mambo hayo yalitendeka kama mifano kwetu. Yakaandikwa ili kutuonya sisi - tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
\v 12 Kwa hiyo kila ajionaye amesimama awe makini asije akaanguka.
\v 13 Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
\s5
\v 14 Kwa hiyo, wapendwa wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
\v 15 Nasema nanyi kama watu wenye akili, ili muamue juu ya ninalosema.
\v 16 Kikombe cha baraka tubarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
\v 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja. Sisi sote twapokea mkate mmoja kwa pamoja.
\s5
\v 18 Watazameni watu wa Israeli: Je! Wale wote walao dhabihu si washiriki katika madhabahu?
\v 19 Nasema nini basi? Ya kuwa sanamu ni kitu? Au ya kuwa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?
\s5
\v 20 Lakini nasema juu ya vitu vile wavitoavyo sadaka watu wapagani wa Mataifa, ya kuwa wanatoa vitu hivi kwa mapepo na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi kushirikiana na mapepo!
\v 21 Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo. Hamwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.
\v 22 Au twamtia Bwana wivu? Tuna nguvu zaidi yake?
\s5
\v 23 "Vitu vyote ni halali," lakini si vyote vifaavyo. "Vitu vyote ni halali," lakini si vyote viwajengavyo watu.
\v 24 Hakuna hata mmoja angetafuta mazuri yake tu. Badala yake, kila mmoja angetafuta mazuri ya mwenzake.
\s5
\v 25 Mnaweza kula kila kitu kiuzwacho sokoni bila kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri.
\v 26 Maana "dunia ni mali ya Bwana, na vyote viijazavyo."
\v 27 Na mtu asiyeamini akiwaalika kula, na mnataka kwenda, kuleni chochote awapacho pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.
\s5
\v 28 Lakini mtu akiwaambia, "Chakula hiki kimetokana na sadaka ya wapagani," msile. Hii ni kwa ajili yake aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.
\v 29 Nami simaanishi dhamiri zenu, bali dhamiri ya yule mwingine. Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
\v 30 Ikiwa mimi natumia chakula kwa shukrani, kwanini nitukanwe kwa kitu ambacho nimeshukuru kwacho?
\s5
\v 31 Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
\v 32 Msiwakoseshe Wayahudi au Wayunani, au kanisa la Mungu.
\v 33 Jaribuni kama mimi ninavyojaribu kuwapendeza watu wote kwa mambo yote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, bali ya wengi. Nami nafanya hivi ili wapate kuokolewa.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Nifuateni mimi, kama na mimi ninavyomfuata Kristo.
\v 2 Sasa nawasifu kwasababu ya vile mnavyonikumbuka katika mambo yote. Nawasifu kwasababu mmeyashika mapokeo kama nilivyoyaleta kwenu.
\v 3 Basi nataka mfahamu ya kuwa Kristo ni kichwa cha kila mwanaume, naye mwanaume ni kichwa cha mwanamke, na ya kuwa Mungu ni kichwa cha Kristo.
\v 4 Kila mwanaume aombaye au atoae unabii akiwa amefunika kichwa anakiabisha kichwa chake.
\s5
\v 5 Lakini kila mwanamke aombae au kutoa unabii hali kichwa chake kikiwa wazi anakiaibisha kichwa chake. Kwa maana ni sawa sawa na kama amenyolewa.
\v 6 Ikiwa kama mwanamke hatafunika kichwa chake, na akatwe nywele zake ziwe fupi. Maana ikiwa ni aibu mwanamke kukata nywele zake au kunyolewa, basi afunike kichwa chake.
\s5
\v 7 Kwani haimpasi mwanamume kufunika kichwa chake, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
\v 8 Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Bali mwanamke alitokana na mwanamume.
\s5
\v 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke. Bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
\v 10 Hii ndio sababu mwanamke anapaswa kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake, kwa sababu ya malaika.
\s5
\v 11 Hata hivyo, katika Bwana, mwanamke hayupo peke yake pasipo mwanamume, au mwanamume pasipo mwanamke.
\v 12 Maana kama vile mwanamke alitoka kwa mwanamume, vile vile mwanamume alitoka kwa mwanamke. Na vitu vyote hutoka kwa Mungu.
\s5
\v 13 Hukumuni wenyewe: Je! ni sahihi mwanamke amuombe Mungu hali kichwa chake kikiwa wazi?
\v 14 Je hata asili peke yake haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?
\v 15 Je asili haiwafundishi ya kwamba mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Maana amepewa zile nywele ndefu kama vazi lake.
\v 16 Lakini ikiwa mtu yeyote anataka kubishana juu ya hili, sisi hatuna namna nyingine, wala makanisa ya Mungu.
\s5
\v 17 Katika maagizo yafuatayo, mimi siwasifu. Maana mnapokusanyika, sio kwa faida bali kwa hasara.
\v 18 Maana kwanza, nasikia ya kuwa mkutanikapo kanisani, kuna migawanyiko kati yenu, na kwa sehemu ninaamini.
\v 19 Kwa maana ni lazima iwepo misuguano kati yenu, ili kwamba wale waliokubaliwa wajulikane kwenu.
\s5
\v 20 Kwa maana mkutanikapo, mnachokula sio chakula cha Bwana.
\v 21 Mnapokula, kila mmoja hula chakula chake mwenyewe kabla wengine hawajala. hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.
\v 22 Je hamna nyumba za kulia na kunywea? Je mnalidharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na Kitu? Niseme nini kwenu? Niwasifu? Sitawasifu katika hili!
\s5
\v 23 Maana nilipokea kutoka kwa Bwana kile ambacho nimewapa ninyi ya kuwa Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alichukua mkate.
\v 24 Baada ya kushukuru, aliuvunja na kusema, "Huu ndio mwili wangu, ulio kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi."
\s5
\v 25 Na vivi hivi akachukua kikombe baada ya kula, na kusema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi."
\v 26 Kwa kila muda mlapo mkate huu na kukinywea kikombe, mwaitangaza mauti ya Bwana mpaka atakapokuja.
\s5
\v 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
\v 28 Mtu ajihoji mwenyewe kwanza, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.
\v 29 Maana alaye na kunywa bila kuupambanua mwili, hula na kunywa hukumu yake mwenyewe.
\v 30 Hii ndiyo sababu watu wengi kati yenu ni wagonjwa na dhaifu, na baadhi yenu wamekufa.
\s5
\v 31 Lakini tukijichunguza wenyewe hatutahukumiwa.
\v 32 Ila tunapohukumiwa na Bwana, twarudiwa, ili tusije tukahukumiwa pamoja na dunia.
\s5
\v 33 Kwa hiyo, kaka na dada zangu, mkutanikapo mpate kula, ngojeaneni.
\v 34 Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kwamba mkutanikapo pamoja isiwe kwa hukumu. Na kuhusu mambo mengine mliyoandika, nitawaelekeza nitakapokuja.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kuhusu karama za rohoni, kaka na dada zangu sitaki mkose kufahamu.
\v 2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa wapagani mliongozwa kufuata sanamu zisizoongea, kwa njia zozote mliongozwa nazo.
\v 3 Kwa hiyo, nataka mfahamu kwamba hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu akisema, "Yesu amelaaniwa." Hakuna yeyote atakayesema, "Yesu ni Bwana," isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
\s5
\v 4 Basi kuna karama tofauti tofauti, bali Roho ni yeye yule.
\v 5 Na kuna huduma tofauti tofauti, bali Bwana ni yeye yule.
\v 6 Na kuna aina mbalimbali za kazi, lakini Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
\s5
\v 7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.
\v 8 Maana mtu mmoja amepewa na Roho neno la hekima, na mwingine neno la maarifa kwa Roho yule yule.
\s5
\v 9 Kwa mwingine humpa imani kwa Roho yeye yule, na kwa mwingine karama ya uponyaji kwa Roho mmoja.
\v 10 Kwa mwingine matendo ya nguvu, na mwingine unabii. Na kwa mwingine uwezo wa kupambanua roho, mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingnine tafsiri za lugha.
\v 11 Lakini Roho ni yule yule atendaye kazi hizi zote, kumpa kila mtu karama kwa kadiri ya uchaguzi wake mwenyewe.
\s5
\v 12 Kwa maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote ni vya mwili ule ule, vivyo hivyo na Kristo.
\v 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wayunani, kwamba tu watumwa au huru, na wote tulinyweshwa Roho mmoja.
\s5
\v 14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
\v 15 Ikiwa mguu utasema, "kwa kuwa mimi si mkono, mimi si sehemu ya mwili," hiyo haiufanyi kutokuwa sehemu ya mwili.
\v 16 Na ikiwa sikio litasema, "kwa kuwa mimi si jicho, mimi si sehemu ya mwili," hiyo hailifanyi kutokuwa sehemu ya mwili.
\v 17 Kama mwili wote utakuwa jicho, kungekuwa wapi kusikia? Kama mwili wote ukiwa sikio, kungekuwa wapi kunusa?
\s5
\v 18 Lakini Mungu aliweka kila kiungo cha mwili mahali pake kama alivyopanga mwenyewe.
\v 19 Na kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
\v 20 Hivyo sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja.
\s5
\v 21 Jicho haliwezi kuuambia mkono, "sina haja na wewe." Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi."
\v 22 Lakini viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa na heshima kidogo vyahitajika zaidi.
\v 23 Na viungo vya mwili tunavyodhani vina heshima kidogo, twavipa heshima zaidi, na viungo vyetu visivyo na mvuto vina uzuri zaidi.
\v 24 Na sasa viungo vyetu vilivyo na mvuto havina haja ya kupewa heshima, kwa kuwa tayari vina heshima. Lakini Mungu ameviunganisha viungo vyote pamoja, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa.
\s5
\v 25 Alifanya hivyo ili pasiwepo mgawanyiko katika mwili, bali viungo vyote vitunzane kwa upendo wa mmoja.
\v 26 Na wakati kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote vyaumia kwa pamoja. Au wakati kiungo kimoja kikiheshimiwa, viungo vyote vifurahi kwa pamoja.
\v 27 Sasa ninyi ni mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
\s5
\v 28 Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha.
\v 29 Je sisi sote ni mitume? Sisi sote ni manabii? Sisi sote ni waalimu? Je sisi sote tunafanya matendo ya miujiza?
\s5
\v 30 Je sisi sote tuna karama ya uponyaji? Sisi sote tunaongea kwa lugha? Sisi sote tunatafsiri lugha?
\v 31 Tafuteni sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonesha njia iliyo bora zaidi.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Tuseme kwamba ninanena kwa lugha za wanadamu na za malaika. Lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao.
\v 2 Na kwamba nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima. Lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.
\v 3 Na tuseme kwamba ninatoa milki yangu yote na kuwalisha masikini, na kwamba ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto. Lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu.
\s5
\v 4 Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi
\v 5 au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.
\v 6 Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.
\v 7 Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.
\s5
\v 8 Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.
\v 9 Kwa kuwa tunajua kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu.
\v 10 Lakini ijapo ile iliyo kamili, ile isiyo kamili itapita.
\s5
\v 11 Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, nilifikiri kama mtoto, niliamua kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima, niliweka mbali nami mambo ya kitoto.
\v 12 Kwa kuwa sasa tunaona kama kwa kioo, kama sura gizani, lakini wakati ule tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kwa sehemu, lakini wakati ule nitajua sana kama na mimi ninavyojulikana sana.
\v 13 Lakini sasa mambo haya matatu yanadumu: imani, tumaini lijalo, na upendo. Lakini lililo kuu zaidi ya haya ni upendo.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Utafuteni upendo na kutamani sana karama za rohoni, zaidi sana mpate kutoa unabii.
\v 2 Maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu bali husema na Mungu. Maana hakuna aelewaye kwa sababu anena mambo yaliyofichika katika Roho.
\v 3 Lakini yeye atoaye unabii, asema na watu na kuwajenga, kuwatia moyo, na kuwafariji.
\v 4 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, lakini yeye atoaye unabii hulijenga kanisa.
\s5
\v 5 Sasa natamani kwamba ninyi nyote mnene kwa lugha. Lakini zaidi ya hayo, natamani ya kwamba mtoe unabii. Yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha (labda awepo wa kutafasiri), ili kwamba kanisa lipate kujengwa.
\v 6 Lakini sasa, kaka na dada zangu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini ninyi? Siwezi, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya maarifa, au unabii, au kwa njia ya fundisho.
\s5
\v 7 Ikiwa vitu visivyo na uhai kama filimbi au kinubi visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni chombo gani kinachezwa?
\v 8 Kwa maana ikiwa baragumu itatoa sauti isiyojulikana, ni jinsi gani mtu atatambua ya kuwa ni muda wa kujiandaa kwa vita?
\v 9 Vivyo hivyo na ninyi. Mkitoa kwa ulimi neno lisilo dhahiri, ni jinsi gani mtu ataelewa mnachosema? Mtakuwa mkiongea, na hakuna atakayewaelewa.
\s5
\v 10 Hakuna shaka kwamba kuna lugha nyingi mbalimbali duniani, na hakuna hata moja isiyo na maana.
\v 11 Lakini ikiwa sijui maana ya lugha, nitakuwa mgeni kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mgeni kwangu.
\s5
\v 12 Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani sana kuona uthihirisho wa Roho, takeni kwamba mzidi sana kulijenga kanisa.
\v 13 Hivyo, yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kutafasiri.
\v 14 Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
\s5
\v 15 Nifanye nini? Nitaomba kwa roho yangu, lakini pia nitaomba kwa akili zangu. Nitaimba kwa roho yangu, na nitaimba kwa akili zangu pia.
\v 16 Vinginevyo, ukimsifu Mungu kwa roho, yeye aliye mgeni ataitikaje "Amina" utoapo shukurani, akiwa hayajui usemayo?
\s5
\v 17 Maana ni kweli wewe washukuru vema, lakini yule mwingine hajengwi.
\v 18 Namshukuru Mungu kwa kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote.
\v 19 Lakini katika kanisa ni heri ninene maneno matano kwa ufahamu wangu ili nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.
\s5
\v 20 Kaka na dada zangu, msiwe watoto katika kufikiri kwenu. Badala yake, kuhusiana na uovu, iweni kama watoto wachanga. Lakini katika kufikiri kwenu mkawe watu wazima.
\v 21 Imeandikwa katika sheria, "Kwa watu wa lugha nyingine na kwa midomo ya wageni nitasema na watu hawa. Wala hata hivyo hawatanisikia," asema Bwana.
\s5
\v 22 Hivyo, ndimi ni ishara, sio kwa walioamini, bali kwa wasioamini. Lakini kutoa unabii ni ishara, sio kwa wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.
\v 23 Haya, ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja na wote wanene kwa lugha, na wageni na wasioamini wameingia, je hawawezi kusema kwamba mna wazimu?
\s5
\v 24 Lakini ikiwa wote mnatoa unabii na asiyeamini au mgeni akaingia, atashawishiwa na yote asikiayo. Atahukumiwa na yote yasemwayo.
\v 25 Siri za moyo wake zingefunuliwa. Matokeo yake, angeanguka kifudifudi na kumwabudu Mungu. Angekiri ya kwamba Mungu yu kati yenu.
\s5
\v 26 Nini kifuatacho basi, kaka na dada zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana Zaburi, mafundisho, mafunuo, lugha au tafsiri. Fanyeni kila kitu ili kwamba mlijenge kanisa.
\v 27 Kama yeyote ananena kwa lugha, wawepo wawili au watatu, na kila mmoja katika zamu. Na mtu lazima atafasiri kilichosemwa.
\v 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafasiri, basi kila mmoja wao akae kimya ndani ya kanisa. Basi kila mmoja aongee peke yake na kwa Mungu.
\s5
\v 29 Na manabii wawili au watatu wanene, na wengine wasikilize kwa kupambanua kilichosemwa.
\v 30 Lakini aliyeketi akifunuliwa jambo katika huduma, yule ambaye alikuwa ananena na anyamaze.
\s5
\v 31 Kwa kuwa kila mmoja wenu anaweza kutoa unabii mmoja baada ya mwingine ili kwamba kila mmoja aweze kujifunza na wote waweze kutiwa moyo.
\v 32 Kwa kuwa roho za manabii ziko chini ya uangalizi wa manabii.
\v 33 Kwa kuwa Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani. Kama ilivyo katika makanisa yote ya waumini,
\s5
\v 34 imewapasa wanawake wakae kimya katika kanisa. Kwa kuwa hawaruhusiwi kuzungumza. Badala yake, wanapaswa kuwa katika unyenyekevu, kama pia sheria inavyosema.
\v 35 Kama kuna chochote wanatamani kujifunza, basi wawaulize waume zao nyumbani. Kwa kuwa ni aibu kwa mwanamke kuongea katika kanisa.
\v 36 Je neno la Mungu lilitoka kwenu? Je limewafikia ninyi tu?
\s5
\v 37 Kama mtu akijiona kuwa ni nabii au wa rohoni, inampasa ayatambue mambo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
\v 38 Lakini asipotambua haya, mwacheni asitambuliwe.
\s5
\v 39 Hivyo basi, kaka na dada zangu, takeni sana kutoa unabii, na msimzuie mtu yeyote kunena kwa lugha.
\v 40 Lakini mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Sasa ninawakumbusha, akina kaka na akina dada, juu ya injili niliyowahubiria, ambayo mliipokea na kusimama kwayo.
\v 2 Ni katika injili hii mmeokolewa, kama mkilishika imara neno nililowahubiri ninyi, isipokuwa mliamini bure.
\s5
\v 3 Kama kwanza nilivyo ipokea kwa umuhimu niliileta kwenu kama ilivyo: kwamba kutokana na maandiko, Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,
\v 4 kutokana na maandiko alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu.
\s5
\v 5 Na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili.
\v 6 Kisha aliwatokea kwa wakati mmoja akina kaka na akina dada zaidi ya mia tano. Wengi wao bado wako hai, lakini baadhi yao wamelala usingizi.
\v 7 Kisha alimtokea Yakobo, kisha mitume wote.
\s5
\v 8 Mwisho wa yote, alinitokea mimi, kama vile kwa mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi.
\v 9 Kwa kuwa mimi ni mdogo kati ya mitume. Sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu.
\s5
\v 10 Lakini kwa neema ya Mungu nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya bidii kuliko wote. Lakini haikuwa mimi, bali neema ya Mungu iliyo ndani yangu.
\v 11 Kwa hiyo kama ni mimi au wao, tuna hubiri hivyo na tunaamini hivyo.
\s5
\v 12 Sasa kama Kristo alihubiriwa kama aliyefufuka kwa wafu, iweje baadhi yenu mseme hakuna ufufuo wa wafu?
\v 13 Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo pia hakufufuka.
\v 14 Na kama Kristo hakufufuka, hivyo mahubiri yetu ni bure, na imani yenu ni bure.
\s5
\v 15 Na tumepatikana kuwa mashahidi wa uongo kumuhusu Mungu, kwa sababu tulimshushuhudia Mungu kinyume, kusema alimfufua Kristo, wakati hakumfufua.
\v 16 Kama ikiwa wafu hawafufuliwi, Yesu pia hakufufuliwa.
\v 17 Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni bure na bado mko kwenye dhambi zenu.
\s5
\v 18 Hivyo hata wale waliokufa katika Kristo pia wameangamia.
\v 19 Ikiwa kwa maisha haya peke yake tunaujasiri kwa wakati ujao ndani ya Kristo, watu wote, sisi niwakuhurumiwa zaidi ya watu wote.
\s5
\v 20 Lakini sasa Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wale waliokufa.
\v 21 Kwa kuwa kifo kilikuja kupitia mwanadamu, pia kupitia mwanadamu ufufuo wa wafu.
\s5
\v 22 Kwa kuwa kama katika Adam wote wanakufa, hivyo pia katika Kristo wote watafanywa hai.
\v 23 Lakini kila moja katika mpango wake: Kristo, matunda ya kwanza, na kisha wale walio wa Kristo watafanywa hai wakati wa kuja kwake.
\s5
\v 24 Ndipo utakuwa mwisho, pale Kristo atakapo kabidhi ufalme kwa Mungu Baba. Hii ni pale atakapo komesha utawala wote na mamlaka yote na nguvu.
\v 25 Kwa kuwa lazima atawale mpaka atakapoweka maadui zake wote chini ya nyayo zake.
\v 26 Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo.
\s5
\v 27 Kwa kuwa "ameweka kila kitu chini ya nyayo zake." Lakini inaposema "ameweka kila kitu," ni wazi kwamba hii haihusishi wale walioweka kila kitu chini yake mwenyewe.
\v 28 Wakati vitu vyote vimewekwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe atawekwa chini kwake Yeye ambaye aliviweka vitu vyote chini yake. Hii itatokea ili kwamba Mungu Baba awe yote katika vyote.
\s5
\v 29 Au pia watafanya nini wale waliobatizwa kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kabisa, kwa nini tena wanabatizwa kwa ajili yao?
\v 30 Na kwa nini tuko katika hatari kila saa?
\s5
\v 31 Kaka na dada zangu, kupitia kujisifu kwangu katika ninyi, ambayo ninayo katika Kristo Yesu Bwana wetu, natangaza hivi: nakufa kila siku.
\v 32 Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? "Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa."
\s5
\v 33 Msidanganywe: "Makundi mabaya huharibu tabia njema.
\v 34 "Muwe na kiasi! muishi katika haki! msiendelee kutenda dhambi. Kwa kuwa baadhi yenu hamna maarifa ya Mungu. Nasema hivi kwa aibu yenu.
\s5
\v 35 Lakini mtu mwingine atasema, "Jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?"
\v 36 Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa.
\s5
\v 37 Na kile unachopanda sio mwili ambao utakuwa, bali ni mbegu iliyochipua. Inaweza kuwa ngano au kitu kingine.
\v 38 Lakini Mungu ataipa mwili kama apendavyo, na katika kila mbengu mwili wake mwenyewe.
\v 39 Miili yote haifanani. Isipokuwa, kuna mwili mmoja wa wanadamu, na mwili mwingine wa wanyama, na wili mwingine wa ndege, na mwingine kwa ajili ya samaki.
\s5
\v 40 Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani. Lakini utukufu wa miili ya mbinguni ni aina moja na utukufu wa duniani ni mwingine.
\v 41 Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.
\s5
\v 42 Hivyo ndivyo ulivyo pia ufufuo wa wafu. Kinacho pandwa kinaharibika, na kinacho ota hakiharibiki.
\v 43 Kimepandwa katika matumizi ya kawaida, kinaoteshwa katika utukufu. Kimepandwa katika udhaifu, kinaoteshwa katika nguvu.
\v 44 Kimepandwa katika mwili wa asili, kinaoteshwa katika mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, kuna mwili wa kiroho pia.
\s5
\v 45 Hivyo pia imeandikwa, "Mtu wa kwanza Adamu alifanyika roho inayo ishi." Adamu wa mwisho alifanyika roho itoayo uhai.
\v 46 Lakini wa kiroho hakuja kwanza bali wa asili, na kisha wa kiroho.
\s5
\v 47 Mtu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi. Mtu wa pili anatoka mbinguni.
\v 48 Kama vile yule aliyetengenezwa kwa mavumbi, hivyo pia wale waliotengenezwa kwa mavumbi. Kama vile mtu wa mbinguni alivyo, hivyo pia wale wa mbinguni.
\v 49 Kama ambavyo tumebeba mfano wa mtu wa mavumbi, tutabeba pia mfano wa mtu wa mbinguni.
\s5
\v 50 Sasa nawaambia, kaka na dada zangu, kwamba mwili na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu. Wala wakuharibika kurithi wakutoharibika.
\v 51 Tazama! Nawaambia ninyi siri ya kweli: Hatutakufa wote, bali wote tutabadilishwa.
\s5
\v 52 Tutabadilishwa katika wakati, katika kufumba na kufumbua kwa jicho, katika tarumbeta ya mwisho. Kwa kuwa tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa na hali ya kutoharibika, na tutabadilishwa.
\v 53 Kwani huu wa kuharibika lazima uvae wa kutoharibika, na huu wa kufa lazima uvae wa kutokufa.
\s5
\v 54 Lakini wakati huu wa kuharibika ukivikwa wa kutokuharibika, na huu wa kufa ukivaa wa kutokufa, ndipo utakuja msemo ambao umeandikwa, "Kifo kimemezwa katika ushindi."
\v 55 "Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?"
\s5
\v 56 Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria.
\v 57 Lakini shukurani kwa Mungu, atupaye sisi ushindi kupitia Bwana wetu Yesu Kristo!
\s5
\v 58 Kwa hiyo, wapendwa kaka na dada zangu, iweni imara na msitikisike. Daima itendeni kazi ya Bwana, kwa sababu mnajua kuwa kazi yenu katika Bwana siyo bure.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Sasa kuhusu michango kwa ajili ya waumini, kama nilivyo elekeza makanisa ya Galatia, vivyo hivyo mwapaswa kufanya.
\v 2 Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija.
\s5
\v 3 Na nitakapofika, yeyote mtakayemchagua, nitamtuma pamoja na barua kutoa sadaka yenu huko Yerusalem.
\v 4 Na kama ni sahihi kwa mimi kwenda pia, watakwenda pamoja nami.
\s5
\v 5 Lakini nitakuja kwenu, wakati ninapitia Makedonia. Kwa kuwa nitapitia Makedonia.
\v 6 Labda naweza kukaa nanyi au hata kumaliza majira ya baridi, ili kwamba muweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendako.
\s5
\v 7 Kwa kuwa sitarajii kuwaona sasa kwa muda mfupi. Kwani ninatumaini kukaa nanyi kwa muda fulani, kama Bwana ataniruhusu.
\v 8 Lakini nitakaa Efeso mpaka Pentekoste,
\v 9 kwa kuwa mlango mpana umefunguliwa kwa ajili yangu, na kuna maadui wengi wanipingao.
\s5
\v 10 Sasa wakati Timotheo akija, muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa, anafanya kazi ya Bwana, kama ninavyofanya.
\v 11 Mtu yeyote asimdharau. Mumsaidie katika njia yake kwa amani, ili kwamba aweze kuja kwangu. Kwa kuwa ninamtarajia aje pamoja na ndugu.
\v 12 Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi.
\s5
\v 13 Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu.
\v 14 Basi yote myafanyayo yafanyike katika upendo.
\s5
\v 15 Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu,
\v 16 kuweni wanyenyekevu kwa watu kama hao, na kwa kila mtu anayesaidia katika kazi na watenda kazi pamoja nasi.
\s5
\v 17 Na ninafurahi kwa ujio wa Stefana, Fotunato, na Akiko. Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa.
\v 18 Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo sasa, watambueni watu kama hawa.
\s5
\v 19 Makanisa ya Asia wametuma salamu kwenu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao.
\v 20 Kaka na dada zangu wote wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
\s5
\v 21 Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu.
\v 22 Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake. Bwana wetu, njoo!
\v 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
\v 24 Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo Yesu.

510
48-2CO.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,510 @@
\id 2CO
\ide UTF-8
\h 2 Wakorintho
\toc1 2 Wakorintho
\toc2 2 Wakorintho
\toc3 2co
\mt 2 Wakorintho
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, na kwa waumini wote walioko katika mkoa wote wa Akaya.
\v 2 Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote.
\v 4 Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi.
\s5
\v 5 Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo huongezeka kwa ajili yetu, vile vile faraja yetu huongezeka kupitia Kristo.
\v 6 Lakini kama tunataabishwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na kama tunafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu. Faraja yenu inafanya kazi kikamilifu mnaposhiriki mateso kwa uvumilivu kama sisi pia tunavyoteseka.
\v 7 Na ujasiri wetu juu yenu ni thabiti. Tunajua kwamba kama vile ambavyo mnashiriki mateso, vile vile mnashiriki faraja.
\s5
\v 8 Kwa kuwa hatutaki ninyi muwe wajinga, ndugu, kuhusu matatizo tuliyokuwa nayo huko Asia. Tulionewa zaidi ya vile tuwezavyo kubeba, kana kwamba hatukuwa hata na tumaini la kuishi tena.
\v 9 Kweli, tulikuwa na hukumu ya kifo juu yetu. Lakini hiyo ilikuwa ni kutufanya sisi tusiweke tumaini juu yetu wenyewe, badala yake tuweke tumaini katika Mungu, afufuaye wafu.
\v 10 Alituokoa sisi kutoka hayo maafa ya mauti, na atatuokoa tena. Tumeweka ujasiri wetu katika yeye ya kwamba atatuokoa tena.
\s5
\v 11 Atafanya hivi kama vile ninyi pia mtusaidiavyo kwa maombi yenu. Hivyo wengi watatoa shukurani kwa niaba yetu kwa ajili ya upendeleo wa neema tuliyopewa sisi kupitia maombi ya wengi.
\s5
\v 12 Tunajivunia hili: ushuhuda wa dhamiri yetu. Kwa kuwa ni katika nia safi na usafi wa Mungu kwamba tulienenda wenyewe katika dunia. Tumefanya hivi hasa na ninyi, na sio katika hekima ya ulimwengu, lakini badala yake ni katika neema ya Mungu.
\v 13 Hatuwaandikii chochote ambacho hamwezi kukisoma au kuelewa. Ninaujasiri
\v 14 kwamba kwa sehemu mumekwisha kutuelewa. Na ninaujasiri kwamba katika siku ya Bwana Yesu tutakuwa sababu yenu kwa ajili ya kiburi chenu, kama vile mtakavyokuwa kwetu.
\s5
\v 15 Kwa sababu nilikuwa na ujasiri kuhusu hili, nilitaka kuja kwenu kwanza, ili kwamba muweze kupokea faida ya kutembelewa mara mbili.
\v 16 Nilikuwa napanga kuwatembelea wakati nikielekea Makedonia. Tena nilitaka kuwatembelea tena wakati nikirudi kutoka Makedonia, na kisha ninyi kunituma mimi wakati nikielekea Uyahudi.
\s5
\v 17 Nilipokuwa nafikiria namna hii, je, nilikuwa nasitasita? Je ninapanga mambo kulingana na viwango vya kibinadamu, ili kwamba niseme "Ndiyo, ndiyo" na "Hapana, hapana" kwa wakati mmoja?
\v 18 Lakini kama vile Mungu alivyo mwaminifu, hatusemi vyote "Ndiyo" na "Hapana."
\s5
\v 19 Kwa kuwa mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye Silvano, Timotheo na mimi tulimtangaza miongoni mwenu, siyo "Ndiyo" na "Hapana." Badala yake, yeye wakati wote ni "Ndiyo."
\v 20 Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni "Ndiyo" katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema "Amina" kwa utukufu wa Mungu.
\s5
\v 21 Sasa ni Mungu ambaye hututhibitisha sisi pamoja nanyi katika Kristo, na alitutuma sisi.
\v 22 Aliweka muhuri juu yetu na alitupa Roho katika mioyo yetu kama dhamana ya kile ambacho angetupatia baadaye.
\s5
\v 23 Badala yake, namsihi Mungu kunishuhudia mimi kwamba sababu iliyonifanya nisije Korintho ni kwamba nisiwalemee ninyi.
\v 24 Hii sio kwa sababu tunajaribu kudhibiti jinsi imani yenu inavyotakiwa kuwa. Badala yake, tunafanya pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu, kama mnavyosimama katika imani yenu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo niliamua kwa sehemu yangu mwenyewe kwamba nisingekuja tena kwenu katika hali ya uchungu.
\v 2 Kama niliwasababishia ninyi maumivu, ni nani angenifurahisha mimi, lakini ni yule ambaye aliumizwa na mimi?
\s5
\v 3 Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote.
\v 4 Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu.
\s5
\v 5 Kama kuna yeyote amesababisha maumivu, hajasababisha tu kwangu, lakini kwa kiwango fulani - bila kuweka ukali zaidi - kwenu ninyi nyote.
\v 6 Hii adhabu ya mtu huyo kwa wengi inatosha.
\v 7 Kwa hiyo sasa badala ya adhabu, mnapaswa kumsamehe na kumfariji. Fanyeni hivi ili kwamba asiweze kushindwa na huzuni iliyozidi.
\s5
\v 8 Kwa hiyo ninawatia moyo kuthibitisha upendo wenu hadharani kwa ajili yake.
\v 9 Hii ndiyo sababu niliandika, ili kwamba niweze kuwajaribu na kujua kuwa kama ni watii katika kila kitu.
\s5
\v 10 Kama mkimsamehe yeyote, na mimi pia namsamehe mtu huyo. Kile nilicho kisamehe - kama nimesamehe chochote-kimesamehewa kwa faida yenu katika uwepo wa Kristo.
\v 11 Hii ni kwamba Shetani asije akatufanyia madanganyo. Kwa kuwa sisi sio wajinga kwa mipango yake.
\s5
\v 12 Mlango ulifunguliwa kwangu na Bwana nilipokuja kwenye mji wa Troa kuhubiri injili ya Kristo pale.
\v 13 Hata hivyo, sikuwa na amani ya moyo, kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito pale. Hivyo niliwaacha na nikarudi Makedonia.
\s5
\v 14 Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye katika Kristo mara zote hutuongoza sisi katika ushindi. Kupitia sisi husambaza harufu nzuri ya maarifa yake mahala pote.
\v 15 Kwa kuwa sisi kwa Mungu, ni harufu nzuri ya Kristo, wote kati ya wale waliookolewa na kati ya wale wanaoangamia.
\s5
\v 16 Kwa watu ambao wanaangamia, ni harufu kutoka kifo hadi kifo. Kwa wale wanaookolewa, ni harufu nzuri kutoka uzima hadi uzima. Ni nani anayestahili vitu hivi?
\v 17 Kwa kuwa sisi sio kama watu wengi wanaouza neno la Mungu kwa faida. Badala yake, kwa usafi wa nia, tunanena katika Kristo, kama vile tunavyotumwa kutoka kwa Mungu, mbele ya Mungu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji?
\v 2 Ninyi wenyewe ni barua yetu ya mapendekezo, iliyoandikwa kwenye mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na watu wote.
\v 3 Na mnaonesha kwamba ninyi ni barua kutoka kwa Kristo, iliyotolewa na sisi. Iliandikwa siyo kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu.
\s5
\v 4 Na huu ndiyo ujasiri tulio nao katika Mungu kupitia Kristo.
\v 5 Hatujiamini wenyewe kwa kudai chochote kama kutoka kwetu. Badala yake, kujiamini kwetu kunatoka kwa Mungu.
\v 6 Ni Mungu ambaye alitufanya tuweze kuwa watumishi wa agano jipya. Hili ni agano sio la barua bali ni la Roho. Kwa kuwa barua huua, lakini roho inatoa uhai.
\s5
\v 7 Sasa kazi ya kifo iliyokuwa imechongwa katika herufi juu ya mawe ilikuja kwa namna ya utukufu kwamba watu wa Israeli hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wa Musa. Hii ni kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unafifia.
\v 8 Je, kazi ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?
\s5
\v 9 Kwa kuwa kama huduma ya hukumu ilikuwa na utukufu, ni mara ngapi zaidi huduma ya haki huzidi sana katika utukufu!
\v 10 Ni kweli kwamba, kile kilichofanywa utukufu kwanza hakina utukufu tena katika heshima hii, kwa sababu ya utukufu unaouzidi.
\v 11 Kwa kuwa kama kile ambacho kilikuwa kinapita kilikuwa na utukufu, ni kwa kiasi gani zaidi kile ambacho ni cha kudumu kitakuwa na utukufu!
\s5
\v 12 Kwa kuwa tunajiamini hiyo, tunaujasiri sana.
\v 13 Hatuko kama Musa, aliyeweka utaji juu ya uso wake, ili kwamba watu wa Israel wasiweze kuangalia moja kwa moja kwenye mwisho wa utukufu ambao ulikuwa unatoweka.
\s5
\v 14 Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa. Hata mpaka siku hii utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale. Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali.
\v 15 Lakini hata leo, wakati wowote Musa asomwapo, utaji hukaa juu ya mioyo yao.
\v 16 Lakini mtu anapogeuka kwa Bwana, utaji unaondolewa.
\s5
\v 17 Sasa Bwana ni Roho. Palipo na Roho wa Bwana, kuna uhuru.
\v 18 Sasa sisi sote, pamoja na nyuso zisizo wekewa utaji, huona utukufu wa Bwana. Tunabadilishwa ndani ya muonekano uleule wa utukufu kutoka shahada moja ya utukufu kwenda nyingine, kama ilivyo kutoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, kwa sababu tuna huduma hii, na kama ambavyo tumeipokea rehema, hatukati tamaa.
\v 2 Badala yake, tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika. Hatuishi kwa hila, na hatulitumii vibaya neno la Mungu. Kwa kuwasilisha iliyo kweli, tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu.
\s5
\v 3 Lakini kama injili yetu imefichika, imefichika kwa wale tu wanaoangamia.
\v 4 Katika uchaguzi wao, mungu wa ulimwengu huu amewapofusha fahamu zao zisizoamini. Matokeo yake, hawawezi kuona nuru ya injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu.
\s5
\v 5 Kwa kuwa hatujitangazi wenyewe, bali Kristo Yesu kama Bwana, na sisi wenyewe kama watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
\v 6 Kwa kuwa Mungu ndiye ambaye aliyesema, "Mwanga utaangaza toka gizani." Ameangaza katika mioyo yetu, kutoa mwanga wa maarifa ya utukufu wa Mungu katika uwepo wa Yesu Kristo.
\s5
\v 7 Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kwamba ieleweke kuwa nguvu kuu sana ni ya Mungu na sio yetu.
\v 8 Tunataabika katika kila hali, lakini hatusongwi. Twaona shaka lakini hatujawi na kukata tamaa.
\v 9 Tunateswa lakini hatujatelekezwa. Twatupwa chini lakini hatuangamizwi.
\v 10 Siku zote tunabeba katika mwili wetu kifo cha Yesu, ili kwamba uzima wa Yesu uonekane pia katika miili yetu.
\s5
\v 11 Sisi tulio hai siku zote tumetolewa kufa kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uhai wa Yesu uonekane katika miili yetu ya kibinadamu.
\v 12 Kwa sababu hii, kifo kinafanya kazi ndani yetu, bali uzima unafanya kazi ndani yenu.
\s5
\v 13 Lakini tuna roho ileile ya imani kulingana na kile kilicho andikwa: "Niliamini, na hivyo nilinena." Sisi pia tunaamini, na hivyo pia tunanena.
\v 14 Tunajua kuwa yule aliye mfufua Bwana Yesu pia atatufufua sisi pamoja naye. Tunajua kuwa atatuleta sisi pamoja nanyi katika uwepo wake.
\v 15 Kila kitu ni kwa ajili yenu ili kwamba, kwa kadri neema inavyo enea kwa watu wengi, shukurani zizidi kuongezeka kwa utukufu wa Mungu.
\s5
\v 16 Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku.
\v 17 Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote.
\v 18 Kwa kuwa hatutazami kwa ajili ya vitu ambavyo vinaonekana, bali kwa ajili ya vitu visivyoonekana. Vitu tunavyoweza kuviona ni vya muda tu, bali vitu ambayo havionekani ni vya milele.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Tunajua kwamba kama maskani ya ulimwenguni ambayo tunaishi humo yanaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu. Ni nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali ni nyumba ya milele, katika mbingu.
\v 2 Kwa kuwa katika hema hii tunaugua, tukitamani kuvikwa kwa maskani yetu mbinguni.
\v 3 Tunatamani kwa ajili ya hii kwa sababu kwa kuivaa hatutaonekana kuwa tu uchi.
\s5
\v 4 Kwa hakika wakati tuko ndani ya hema hii, twaugua tukilemewa. Hatutaki kuvuliwa. Badala yake, tunataka kuvalishwa, ili kwamba kile kilicho kufa kiweze kumezwa na uzima.
\v 5 Yule aliyetuandaa sisi kwa kitu hiki ni Mungu, ambaye alitupa sisi Roho kama ahadi ya kile kitakacho kuja.
\s5
\v 6 Kwa hiyo muwe na ujasiri siku zote. Muwe macho kwamba wakati tuko nyumbani katika mwili, tuko mbali na Bwana.
\v 7 Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri.
\v 8 Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili na nyumbani pamoja na Bwana.
\s5
\v 9 Kwa hiyo tunaifanya kuwa lengo letu, kama tukiwa nyumbani au mbali, tumpendeze yeye.
\v 10 Kwa kuwa lazima wote tuonekane mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kwamba kila mmoja aweze kupokea kile kinachostahili kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, ikiwa ni kwa uzuri au kwa ubaya.
\s5
\v 11 Kwa hiyo, kwa kuijua hofu ya Bwana, tunawashawishi watu. Jinsi tulivyo, inaonekana wazi na Mungu. Ninatumaini kuwa inaeleweka pia kwenye dhamiri zenu.
\v 12 Hatujaribu kuwashawishi ninyi tena kutuona sisi kama wakweli. Badala yake, tunawapa ninyi sababu ya kujivuna kwa ajili yetu, ili kwamba muweze kuwa na jibu kwa wale wanaojivunia kuhusu mwonekano lakini sio kile kilicho ndani ya moyo.
\s5
\v 13 Kwa kuwa ikiwa kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu. Na kama tuko kwenye akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.
\v 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa.
\v 15 Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa.
\s5
\v 16 Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena.
\v 17 Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.
\s5
\v 18 Vitu vyote hivi vyatoka kwa Mungu. Alitupatanisha sisi kwake mwenyewe kupitia Kristo, na ametupatia huduma ya upatanisho.
\v 19 Hiyo ni kusema, katika Kristo, Mungu anaupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe, sio kuhesabu makosa yao dhidi yao. Anawekeza kwetu ujumbe wa upatanisho.
\s5
\v 20 Kwa hiyo tunateuliwa kama wawakilishi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa anafanya rufaa yake kupitia sisi. Tunawasihi ninyi kwa ajili ya Kristo: "Mpatanishwe kwa Mungu!"
\v 21 Alimfanya Kristo kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ndiye ambaye hakutenda dhambi. Alifanya hivi ili tuweze kufanyika haki ya Mungu katika yeye.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo.
\v 2 Kwa kuwa anasema, "Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia." Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu.
\v 3 Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya.
\s5
\v 4 Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
\v 5 kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,
\v 6 katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi.
\v 7 Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
\s5
\v 8 Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli.
\v 9 Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa.
\v 10 Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
\s5
\v 11 Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.
\v 12 mioyo yenu haizuiliwi na sisi, bali mnazuiliwa na hisia zenu wenyewe.
\v 13 Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - fungueni mioyo yenu kwa upana.
\s5
\v 14 Msifungamanishwe pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna uhusiano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
\v 15 Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?
\v 16 Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: "Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu."
\s5
\v 17 Kwa hiyo, "Tokeni kati yao, na mkatengwe nao," asema Bwana. "Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.
\v 18 Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike," asema Bwana Mwenyezi.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu.
\s5
\v 2 Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote.
\v 3 Nasema hili siyo kwa kuwalaumu. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja.
\v 4 Nina ujasiri mwingi ndani yenu, na ninajivuna kwa ajili yenu. Nimejawa na faraja. Ninajawa na furaha hata katikati ya mateso yetu yote.
\s5
\v 5 Tulikuja Makedonia, miili yetu haikuwa na pumziko. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani.
\v 6 Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito.
\v 7 Haikuwa kwa ujio wake tu kwamba Mungu alitufariji. ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na mlivyokuwa na wasiwasi kwa ajili yangu. Hivyo nimezidi kuwa na furaha zaidi.
\s5
\v 8 Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. lakini ninaujutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni. lakini mlikuwa na huzuni kwa muda mfupi.
\v 9 Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na shida, lakini kwa sababu huzuni zenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hivyo mliteswa si kwa hasara kwa sababu yetu.
\v 10 Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.
\s5
\v 11 Angalieni huzuni hii ya kiungu ilizalisha azma gani kubwa ndani yenu. Jinsi gani azma ilikuwa kubwa ndani yenu kuthibitisha kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia.
\v 12 Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu.
\s5
\v 13 Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote.
\v 14 Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, Majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli.
\s5
\v 15 Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka.
\v 16 Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.
\v 2 Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu.
\s5
\v 3 Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza.
\v 4 Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini.
\v 5 Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.
\s5
\v 6 Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu.
\v 7 Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu.
\s5
\v 8 Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.
\v 9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.
\s5
\v 10 Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo. Lakini mlitamani kulifanya.
\v 11 Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.
\v 12 Kwa kuwa mnashauku ya kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.
\s5
\v 13 Kwa kuwa kazi hii siyo kwa ajili kwamba wengine waweze kupata nafuu na ninyi mweze kulemewa. Badala yake, kuwe na usawa.
\v 14 Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na usawa.
\v 15 Hii ni kama ilivyoandikwa; "Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote."
\s5
\v 16 Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.
\v 17 Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
\s5
\v 18 Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.
\v 19 Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.
\s5
\v 20 Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.
\v 21 Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.
\s5
\v 22 Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.
\v 23 Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.
\v 24 Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kuhusiana na huduma kwa ajili ya waumini, ni bora zaidi kwangu kuwaandikia.
\v 2 Ninajua kuhusu shauku yenu, ambayo nilijivunia kwa watu wa Makedonia. Niliwaambia kwamba Akaya imekuwa tayari tangu mwaka uliopita. Hamu yenu imewatia moyo wengi wao kutenda.
\s5
\v 3 Sasa, nimewatuma ndugu ili kwamba majivuno yetu kuhusu ninyi yasiwe ya bure, na ili kwamba mngekuwa tayari, kama nilivyosema mngekuwa.
\v 4 Vinginevyo, kama mtu yeyote wa Makedonia akija pamoja nami na kuwakuta hamjawa tayari, tungeona haya --- sisemi chochote kuhusu ninyi--kwa kuwa jasiri sana katika ninyi.
\v 5 Hivyo niliona ilikuwa muhimu kuwasihi ndugu kuja kwenu na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi mlizoahidi. Hii ni hivyo ili kwamba ziwe tayari kama baraka, na si kama kitu kilichoamriwa.
\s5
\v 6 Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.
\v 7 Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha.
\s5
\v 8 Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema.
\v 9 Ni kama ilivyoandikwa: "Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele."
\s5
\v 10 Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu.
\v 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili kwamba muweze kuwa wakarimu. Hii italeta shukrani kwa Mungu kupitia sisi.
\s5
\v 12 Kwa kufanya huduma hii sio tu inagusa mahitaji ya waumini. Pia huzidisha katika matendo mengi ya shukrani kwa Mungu.
\v 13 Kwa sababu ya kupimwa kwenu na kuthibitishwa kwa huduma hii, pia mtamtukuza Mungu kwa utii kwa ukiri wenu wa injili ya Kristo. Pia mtamtukuza Mungu kwa ukarimu wa karama yenu kwao na kwa kila mmoja.
\v 14 Wanawatamani, na wanaomba kwa ajili yenu. Wanafanya hivi kwa sababu ya neema kubwa ya Mungu iliyo juu yenu.
\v 15 Shukrani ziwe kwa Mungu kwa karama yake isiyoelezeka!
\s5
\c 10
\p
\v 1 Mimi Paulo, mwenyewe nawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo. Mimi ni mpole wakati nikiwa mbele yenu, Lakini ninaujasiri kwenu wakati nikiwa mbali nanyi.
\v 2 Nawaomba ninyi kwamba, wakati nikiwepo pamoja nanyi, sitahitaji kuwa jasiri na kujiamini kwangu mwenyewe. Lakini nafikiri nitahitaji kuwa jasiri wakati nikiwapinga wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa jinsi ya mwili.
\s5
\v 3 Kwa kuwa hata kama tunatembea katika mwili, hatupigani vita kwa jinsi ya mwili.
\v 4 Kwa kuwa silaha tunazotumia kupigana si za kimwili. Badala yake, zina nguvu ya kiungu ya kuharibu ngome. Zinaondosha kabisa mijadara inayopotosha.
\s5
\v 5 Pia, tunaharibu kila chenye mamlaka kijiinuacho dhidi ya maarifa ya Mungu. Tunalifanya mateka kila wazo katika utii kwa Kristo.
\v 6 Na tunapata utayari wa kuadhibu kila matendo lisilo na utii, mara tu utii wenu unapokuwa kamili.
\s5
\v 7 Tazama kile kilichowazi mbele yenu. Kama yeyote anashawishika kwamba yeye ni wa Kristo, na hebu ajikumbushe yeye mwenyewe kwamba kama tu alivyo ni wa Kristo, hivyo ndiyo na sisi pia tuko hivyo.
\v 8 Kwa kuwa hata nikijivuna kidogo zaidi kuhusu mamlaka yetu, ambayo Bwana aliyatoa kwa ajili yetu kuwajenga ninyi na siyo kuwaharibu, sitaona haya.
\s5
\v 9 Sihitaji hili lionekane kwamba nawatisha ninyi kwa nyaraka zangu.
\v 10 Kwa vile baadhi ya watu husema, " Nyaraka zake ni kali na zina nguvu, lakini kimwili yeye ni dhaifu. Maneno yake hayastahili kusikilizwa."
\s5
\v 11 Hebu watu wa jinsi hiyo waelewe kwamba kile tusemacho kwa waraka wakati tukiwa mbali, ni sawasawa na vile tutakavyotenda wakati tukiwa pale.
\v 12 Hatuendi mbali mno kama kujikusanya wenyewe au kujilinganisha wenyewe na wale ambao hujisifia wenyewe. Lakini wanapojipima wenyewe na kila mmoja wao, hawana akili.
\s5
\v 13 Sisi, hata hivyo, hatutajivuna kupita mipaka. Badala yake, tutafanya hivyo tu ndani ya mipaka ambayo Mungu ametupimia sisi, mipaka inayofika umbali kama wenu ulivyo.
\v 14 Kwa kuwa hatukujizidishia wenyewe tulipowafikia ninyi. Tulikuwa wa kwanza kufika kwa umbali kama wenu kwa injili ya Kristo.
\s5
\v 15 Hatujajivuna kupita mipaka kuhusu kazi za wengine. Badala yake, tunatumaini kama imani yenu ikuwavyo kwamba eneo letu la kazi litapanuliwa sana, na bado ni ndani ya mipaka sahihi.
\v 16 Tunatumaini kwa hili, ili kwamba tuweze kuhubiri injili hata kwenye mikoa zaidi yenu. Hatutajivuna kuhusu kazi inayofanywa katika maeneo mengine.
\s5
\v 17 "Lakini yeyote ajivunaye, ajivune katika Bwana."
\v 18 Kwa maana siyo yule ajithibitishaye mwenyewe anathibitishwa. Isipokuwa, ni yule ambaye Bwana humthibitisha.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Nahisi kwamba mngevumiliana na mimi katika baadhi ya upumbavu. Lakini kwa kweli mnavumiliana na mimi.
\v 2 Kwa kuwa ni mwenye wivu kuhusu ninyi. Nina wivu wa Mungu kwa ajili yenu, tangu nilipowaahidi ninyi kwenye ndoa ya mume mmoja. Niliahidi kuwaleta ninyi kwa Kristo kama bikra safi.
\s5
\v 3 Lakini ninaogopa kwamba kwa namna fulani, kama nyoka alivyomdanganya Eva kwa hila yake, mawazo yenu yanaweza kupotoshwa mbali kutoka kwenye ibada halisi na safi kwa Kristo.
\v 4 Kwa kuwa kwa mfano kwamba mtu fulani akaja na kutangaza Yesu mwingine tofauti na yule tuliyewahubiri. Au kwa mfano kwamba mkapokea roho mwingine tofauti na yule mliyempokea. Au kwa mfano kwamba mkapokea injili nyingine tofauti na ile mliyoipokea. Mkavumilia mambo haya vema inatosha!
\s5
\v 5 Kwa kuwa nadhani kwamba mimi si miongoni mwa walio duni kwa hao wanaoitwa mitume-bora.
\v 6 Lakini hata kama mimi sijafundishwa katika kutoa hotuba, siko hivyo katika maarifa. Kwa kila namna na katika mambo yote tumelifanya hili kujulikana kwenu.
\s5
\v 7 Je, nilifanya dhambi kwa kujinyenyekeza mwenyewe ili ninyi muweze kuinuliwa? Kwa kuwa nilihubiri kwa uhuru injili ya Mungu kwenu.
\v 8 Nilinyang'anya makanisa mengine kwa kupokea msaada kutoka kwao ili kwamba ningeweza kuwahudumia ninyi.
\v 9 Wakati nilipokuwa nanyi na nilikuwa katika uhitaji, sikumlemea yeyote. Kwa kuwa mahitaji yangu yalitoshelezwa na ndugu waliokuja kutoka Makedonia. Katika kila kitu nimejizuia mwenyewe kutokuwa mzigo kwenu, na nitaendelea kufanya hivyo.
\s5
\v 10 Kama kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, huku kujisifu kwangu, hakutanyamazishwa katika sehemu za Akaya.
\v 11 Kwa nini? Kwa sababu siwapendi? Mungu anajua nawapenda.
\s5
\v 12 Lakini kile ninachokifanya, nitakifanya pia. Nitakifanya ili kwamba niweze kuzuia nafasi ya wale wanaotamani nafasi ya kuwa kama tulivyo katika kile kile wanachojivunia.
\v 13 Kwa kuwa watu wale ni mitume wa uongo na watendakazi wadanganyifu. Wanajigeuza wenyewe kama mitume wa Kristo.
\s5
\v 14 Na hii haishangazi, kwa kuwa hata Shetani hujigeuza mwenyewe kama malaika wa nuru.
\v 15 Hii haina mshangao mkubwa kama watumishi wake pia kujigeuza wenyewe kama watumishi wa haki. Hatma yao itakuwa kama matendo yao yastahilivyo.
\s5
\v 16 Nasema tena: Basi na asiwepo mtu yeyote anayefikiri mimi ni mpumbavu. Lakini kama mkifanya, nipokeeni mimi kama mpumbavu ili niweze kujisifu kidogo.
\v 17 Kile ninachosema kuhusu huku kujiamini kwa kujivuna hakuhukumiwi na Bwana, lakini nazungumza kama mpumbavu.
\v 18 Kwa vile watu wengi hujivuna kwa jinsi ya mwili, nitajivuna pia.
\s5
\v 19 Kwa kuwa mlichukuliana kwa furaha na wapumbavu, ninyi wenyewe mna busara!
\v 20 Kwa kuwa mnachukuliana na mtu kama akikutia utumwani, kama husababisha mgawanyiko kati yenu, kama akiwatumia ninyi kwa faida yake, kama akijiweka juu hewani, au kama akiwapiga usoni.
\v 21 Nitasema kwa aibu yetu kwamba sisi tukuwa dhaifu sana kufanya hivyo. Na bado kama yeyote akijivuna-- nazungumza kama mpumbavu-- mimi pia nitajivuna.
\s5
\v 22 Je, wao ni Wayahudi? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni Waisraeli? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni uzao wa Abrahamu? Na mimi ni hivyo.
\v 23 Je, wao ni watumishi wa Kristo? {Nanena kama nilirukwa na akili zangu. } Mimi ni zaidi. Nimekuwa hata katika kazi ngumu zaidi, mbali zaidi ya kuwa vifungoni, katika kupigwa kupita vipimo, katika kukabili hatari nyingi za kifo.
\s5
\v 24 Kutoka kwa Wayahudi nimepokea mara tano "mapigo arobaini kutoa moja."
\v 25 Mara tatu nilipigwa kwa fimbo. Mara moja nilipigwa mawe. Mara tatu nilinusurika melini. Nimetumia usiku na mchana katika bahari wazi.
\v 26 Nimekuwa katika safari za mara kwa mara, katika hatari za mito, katika hatari za majambazi, katika hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, katika hatari kutoka kwa watu wa mataifa, katika hatari ya mji, katika hatari ya jangwa, katika hatari ya bahari, katika hatari kutoka kwa ndugu waongo.
\s5
\v 27 Nimekuwa katika kazi ngumu na katika maisha magumu, katika usiku mwingi wa kutolala, katika njaa na kiu, mara nyingi katika kufunga, katika baridi na uchi.
\v 28 Mbali na kila kitu kingine, kuna msukumo wa kila siku juu yangu wa wasiwasi wangu kwa ajili ya makanisa.
\v 29 Nani ni dhaifu, na mimi siyo dhaifu? Nani amesababisha mwingine kuanguka dhambini, na mimi siungui ndani?
\s5
\v 30 Kama ni lazima nijivune, nitajivunia kuhusu kile kinachoonyesha udhaifu wangu.
\v 31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anatukuzwa milele, anajua kwamba mimi sidanganyi.
\s5
\v 32 Kule Dameski, mkuu wa mkoa chini ya mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Dameski ili kunikamata.
\v 33 Lakini niliwekwa kikapuni, kupitia dirishani katika ukuta, na nikanusurika kutoka mikononi mwake.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ni lazima nijivune, lakini hakuna kinachoongezwa na hilo. Bali nitaendelea kwenye maono na mafunuo kutoka kwa Bwana.
\v 2 Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita ambaye---ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua---alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu.
\s5
\v 3 Na ninajua kwamba mtu huyu---ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua--
\v 4 alichukuliwa juu hadi paradiso na kusikia mambo matakatifu sana kwa mtu yeyote kuyasema.
\v 5 Kwa niaba ya mtu kama huyo nitajivuna. lakini kwa niaba yangu mwenyewe sitajivuna. Isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.
\s5
\v 6 Kama nikitaka kujivuna, nisingekuwa mpumbavu, kwa kuwa ningekuwa ninazungumza ukweli. Lakini nitaacha kujivuna, ili kwamba asiwepo yeyote atakayenifikiria zaidi ya hayo kuliko kinachoonekana ndani yangu au kusikika kutoka kwangu.
\v 7 Sitajivuna pia kwa sababu ya hayo mafunuo ya aina ya ajabu. Kwa hiyo, hivyo sitajawa na kiburi, mwiba uliwekwa ndani ya mwili wangu, mjumbe wa shetani kunishambulia mimi, ili nisigeuke kuwa mwenye majivuno.
\s5
\v 8 Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili yeye kuundoa kutoka kwangu.
\v 9 Naye akaniambia, "Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu. Hivyo, ningetamani zaidi kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu.
\v 10 Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.
\s5
\v 11 Mimi nimekuwa mpumbavu! ninyi mlinilazimisha kwa hili, kwa kuwa ningekuwa nimesifiwa na ninyi. Kwa kuwa sikuwa duni kabisa kwa hao waitwao mitume--bora, hata kama mimi si kitu.
\v 12 Ishara za kweli za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu, ishara na maajabu na matendo makuu.
\v 13 Kwa namna gani mlikuwa wa muhimu wa chini kuliko makanisa yaliyobaki, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kwa kosa hili!
\s5
\v 14 Tazama! mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto.
\v 15 Nitafurahi zaidi kutumia na kutumiwa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama ninawapenda zaidi, natakiwa kupendwa kidogo?
\s5
\v 16 Lakini kama ilivyo, sikuwalemea mzigo ninyi. Lakini kwa kuwa mimi ni mwerevu sana, mimi ni yule aliyewashika ninyi kwa nimekuwa ambaye aliyewapata kwa udanganyifu.
\v 17 Je, nilichukua kwa kujifanyia faida kwa yeyote niliyemtuma kwenu?
\v 18 Nilimsihi Tito kuja kwenu, na nilituma ndugu mwingine pamoja naye. Je, Tito aliwafanyia faida ninyi? Je, hatukutembea katika njia ile ile? Je, hatukutembea katika nyayo zile zile?
\s5
\v 19 Mnadhani kwa muda huu wote tumekuwa tukijitetea sisi wenyewe kwenu? Mbele za Mungu, na katika Kristo, tumekuwa tukisema kila kitu kwa ajili ya kuwaimarisha ninyi.
\s5
\v 20 Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza nisiwapate ninyi kama ninavyotamani. Nina hofu kwamba mnaweza msinipate mimi kama mnavyotamani. Nahofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi.
\v 21 Nina hofu kwamba nitakaporudi tena, Mungu wangu anaweza kuninyenyekeza mbele yenu. Nina hofu kwamba ninaweza kuhuzunishwa na wengi ambao wamefanya dhambi kabla ya sasa, na ambao hawakutubu uchafu, na uasherati na mambo ya tamaa wanayoyatenda.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Hii ni mara ya tatu kwamba nakuja kwenu. "Kila shitaka lazima lijengwe na uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu."
\v 2 Nimekwishashasema kwa hao waliotenda dhambi kabla na kwa wengine wote wakati nilipokuwa huko mara ya pili, na ninasema tena: Nitakapokuja tena, sitawavumilia.
\s5
\v 3 Nawaambia ninyi hili kwa sababu mnatafuta ushahidi kwamba Kristo ananena kupitia mimi. Yeye sio dhaifu kwenu, badala yake, yeye ni mwenye nguvu ndani yenu.
\v 4 Kwa kuwa alisulibiwa katika udhaifu, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Kwa kuwa sisi pia tu dhaifu ndani yake, lakini tutaishi naye kwa nguvu za Mungu miongoni mwenu.
\s5
\v 5 Jichunguzeni wenyewe muone kama mko katika imani. Jipimeni wenyewe. Hamgundui kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Yeye yumo, vinginevyo kama hamjathibitishwa.
\v 6 Na nina ujasiri kwamba ninyi mtagundua kwamba sisi hatukukataliwa.
\s5
\v 7 Sasa tunaomba kwa Mungu kwamba msiweze kufanya chochote kibaya. Siombi kwamba sisi tuweze kuonekana tumepita jaribu, badala yake ninaomba kwamba muweze kufanya kilicho sahihi, Ingawa tunaweza kuonekana tumeshindwa jaribu.
\v 8 Kwa kuwa sisi hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, lakini ni kwa ajili ya kweli tu.
\s5
\v 9 Kwa kuwa tunafurahi wakati tunapokuwa dhaifu nanyi mkiwa na nguvu. Tunaomba pia kwamba muweze kufanywa wakamilifu.
\v 10 Nayaandika mambo haya wakati nikiwa mbali nanyi, ili kwamba wakati nikiwa pamoja nanyi sihitaji kuwaonesha ukali ninyi. Sihitaji kutumia mamlaka Bwana aliyonipaa mimi niwajenge na siyo kuwaharibu chini.
\s5
\v 11 Hatimaye, ndugu wa kiume na wa kike, furahini! fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, kubalianeni ninyi kwa ninyi, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
\v 12 Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu.
\s5
\v 13 Waumini wote wanawasalimu.
\v 14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja nanyi nyote.

288
49-GAL.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,288 @@
\id GAL
\ide UTF-8
\h Wagalatia
\toc1 Wagalatia
\toc2 Wagalatia
\toc3 gal
\mt Wagalatia
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mimi ni Paulo mtume. Mimi sio mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.
\v 2 Pamoja na ndugu wote na mimi, ninayaandikia makanisa ya Galatia.
\s5
\v 3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo,
\v 4 aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba.
\v 5 Kwake uwe utukufu milele na milele.
\s5
\v 6 Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo.
\v 7 Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishieni nyinyi matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo.
\s5
\v 8 Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe.
\v 9 Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, "Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe."
\v 10 Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
\s5
\v 11 Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu.
\v 12 Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu.
\s5
\v 13 Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.
\v 14 Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu.
\s5
\v 15 Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake
\v 16 kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu
\v 17 na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki.
\s5
\v 18 Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano.
\v 19 Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana.
\v 20 Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu.
\s5
\v 21 Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia.
\v 22 Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,
\v 23 lakini walikuwa wakisikia tu, "Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu."
\v 24 Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa ajili yangu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya miaka kumi na nne nilienda tena Yerusalemu pamoja na Barnaba. Pia nilimchukua Tito pamoja nami.
\v 2 Nilienda kwa sababu Mungu alijidhihirisha kwangu kwamba nilipaswa kwenda. Niliweka mbele yao Injili ambayo niliitangaza kwa watu wa mataifa. (Lakini niliongea kwa siri kwa waliosemekana kuwa viongozi muhimu). Nilifanya hivi ili kuhakikisha kwamba nilikuwa sikimbii, au nilikimbia bure.
\s5
\v 3 Lakini hata Tito, aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, alilazimishwa kutahiriwa.
\v 4 Jambo hili lilitokea kwa sababu ya ndugu wa uongo waliokuja kwa siri kupeleleza uhuru tuliokuwa nao katika Kristo Yesu. Walitamani kutufanya sisi kuwa watumwa wa sheria.
\v 5 Hatukujitoa kuwatii hata kwa saa moja, ili kwamba injili ya kweli ibaki bila kubadilika kwenu.
\s5
\v 6 Lakini wale waliosemwa kuwa walikuwa viongozi hawakuchangia chochote kwangu. Chochote walichokuwa wakikifanya hakikuwa na maana kwangu. Mungu hakubali upendeleo wa wanadamu.
\v 7 Badala yake, waliniona kwamba nimeaminiwa kuitangaza injili kwa wale ambao hawakutahiriwa. Ilikuwa kama Petro atangaze injili kwa waliotahiriwa.
\v 8 Kwa maana Mungu, aliyefanya kazi ndani ya Petro kwa ajili ya utume kwa wale waliotahiriwa, pia alifanya kazi ndani yangu kwa watu wa mataifa.
\s5
\v 9 Wakati Yakobo, Kefa, na Yohana, waliotambulika kuwa waliojenga Kanisa, walifahamu neema niliyopewa mimi, walitupokea katika ushirika mimi na Barnaba. Walifanya hivi ili kwamba twende kwa watu wa mataifa, na ili kwamba waweze kwenda kwa wale waliotahiriwa.
\v 10 Pia walitutaka sisi kuwakumbuka masikini. Mimi pia nilikuwa natamani kufanya jambo hili.
\s5
\v 11 Wakati Kefa alipokuja Antiokia, nilimpinga waziwazi kwa sababu alikuwa amekosea.
\v 12 Kabla ya watu kadhaa kuja kutoka kwa Yakobo, Kefa alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa. Lakini hawa watu walipokuja, aliacha na kuondoka kutoka kwa watu wa mataifa. Alikuwa anaogopa watu ambao walihitaji tohara.
\s5
\v 13 Vilevile Wayahudi wengine waliungana na unafiki huu pamoja na Kefa. Matokeo yake yalikuwa kwamba hata Barnaba alichukuliwa na unafiki wao.
\v 14 Lakini nilipoona kwamba walikuwa hawafuati injili ya kweli, nilimwambia Kefa mbele yao wote, "Kama ninyi ni Wayahudi lakini mnaishi tabia za watu wa mataifa badala ya tabia za Kiyahudi, kwa nini mnawalazimisha watu wa mataifa kuishi kama Wayahudi?"
\s5
\v 15 Sisi ambao ni Wayahudi kwa kuzaliwa na siyo "Watu wa mataifa wenye dhambi "
\v 16 fahamu kwamba hakuna anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Badala yake, wanahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Tulikuja kwa imani ndani ya Kristo Yesu ili kwamba tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Kristo na siyo kwa matendo ya sheria. Kwa matendo ya sheria hakuna mwili utakao hesabiwa haki.
\s5
\v 17 Lakini kama tunapomtafuta Mungu kwa kutuhesabia haki ndani ya Kristo, tunajikuta wenyewe pia kuwa wenye dhambi, je Kristo alifanywa mtumwa wa dhambi? Siyo hivyo!
\v 18 Maana kama nikijenga tegemeo langu juu ya kutunza sheria, tegemeo ambalo nilikwisha liondoa, najionesha mwenyewe kuwa mvunja sheria.
\v 19 Kupitia sheria nilikufa kwa sheria, kwa hiyo napaswa kuishi kwa ajili ya Mungu.
\s5
\v 20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha ninayoishi katika mwili ninaishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda na akajitoa kwa ajili yangu.
\v 21 Siikani neema ya Mungu, maana kama haki ilikuwepo kupitia sheria, basi Kristo angekuwa amekufa bure.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Wagalatia wajinga, ni jicho gani ovu lililowaharibu? Je Yesu Kristo hakuoneshwa kama msulubiwa mbele ya macho yenu?
\v 2 Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu. Je mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa kuamini kile mlichosikia?
\v 3 Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Je mlianza katika Roho ili mmalize katika mwili?
\s5
\v 4 Je mliteseka kwa mambo mengi bure, kama kweli yalikuwa ya bure?
\v 5 Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?
\s5
\v 6 Abraham "Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki".
\v 7 Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu.
\v 8 Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: "katika wewe mataifa yote yatabarikiwa".
\v 9 Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani.
\s5
\v 10 Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, "Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote."
\v 11 Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa "Mwenye haki ataishi kwa imani".
\v 12 Sheria haitokani na imani, lakini badala yake "Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria."
\s5
\v 13 Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, "Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti."
\v 14 Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Ibrahimu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani.
\s5
\v 15 Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.
\v 16 Sasa ahadi zilisemwa kwa Ibrahim na kwa kizazi chake. Haisemi, "kwa vizazi," kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, "kwa kizazi chako," ambaye ni Kristo.
\s5
\v 17 Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.
\v 18 Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
\s5
\v 19 Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Ibrahimu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi.
\v 20 Sasa mpatanishi humaanisha zaidi ya mtu mmoja, bali Mungu ni mmoja peke yake.
\s5
\v 21 Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria.
\v 22 Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.
\s5
\v 23 Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani.
\v 24 Kwa hiyo sheria ilifanyika kiongozi wetu hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani.
\v 25 Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi.
\v 26 Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu.
\s5
\v 27 Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo.
\v 28 Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.
\v 29 Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Ibrahimu, warithi kwa mujibu wa ahadi.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ninasema kwamba maadamu mrithi ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, hata ingawa ni mmiliki wa mali yote.
\v 2 Badala yake, yuko chini ya waangalizi na wadhamini mpaka wakati uliowekwa na baba yake.
\s5
\v 3 Kadhalika pia na sisi, tulipokuwa watoto, tulishikiliwa katika utumwa wa kanuni za kwanza za ulimwengu.
\v 4 Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe, mzaliwa wa mwanamke, mzaliwa chini ya sheria.
\v 5 Alifanya hivi ili kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria, ili kwamba tupokee hali ya kuwa kama wana.
\s5
\v 6 Kwa sababu ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, "Abba, Baba."
\v 7 Kwa sababu hii wewe si mtumwa tena bali mwana. Kama ni mwana, basi wewe pia ni mrithi kupitia Mungu.
\s5
\v 8 Hata kabla, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa watumwa kwa wale ambao kwa asili si miungu kabisa.
\v 9 Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena?
\s5
\v 10 Mnashika kwa uangalifu siku maalumu, miandamo ya miezi, majira, na miaka. Ninaogopa kwa ajili yenu.
\v 11 Ninaogopa kwamba kwa namna fulani nimejitaabisha bure.
\s5
\v 12 Ninawasihi, ndugu, muwe kama nilivyo, kwa kuwa pia nimekuwa kama mlivyo. Hamkunikosea.
\v 13 Bali mnajua kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya ugonjwa wa mwili kwamba nilihubiri injili kwenu kwa mara ya kwanza.
\v 14 Ingawa hali yangu ya mwili iliwaweka katika jaribu, hamkunidharau au kunikataa. Badala yake mlinipokea kama malaika wa Mungu, kana kwamba nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe.
\s5
\v 15 Kwa hiyo, iko wapi sasa furaha yenu? kwa kuwa ninashuhudia kwenu kwamba, ikiwezekana, mungelin'goa macho yenu na kunipa mimi.
\v 16 Hivyo sasa, je nimekuwa adui yenu kwa sababu ninawaambia ukweli?
\s5
\v 17 Wanawatafuta kwa shauku, bali si kwa mema. Wanataka kuwatenganisha ninyi na mimi ili muwafuate.
\v 18 Ni vyema daima kuwa na shauku kwa sababu zilizo njema, na si tu wakati ninapokuwa pamoja nanyi.
\s5
\v 19 Wanangu wadogo, ninaumwa uchungu kwa ajili yenu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.
\v 20 Ningependa kuwepo pale pamoja nanyi sasa na kugeuza sauti yangu, kwa sababu ninamashaka juu yenu.
\s5
\v 21 Niambieni, ninyi ambao mnatamani kuwa chini ya sheria, hamsikii sheria isemavyo?
\v 22 Kwa kuwa imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wa kiume wawili, mmoja kwa yule mwanamke mtumwa na mwingine kwa mwanamke huru.
\v 23 Hata hivyo, yule wa mtumwa alizaliwa kwa mwili tu, bali yule wa mwanamke huru alizaliwa kwa ahadi.
\s5
\v 24 Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, kwa kuwa wanawake hawa wanafanana na maagano mawili. Mojawapo kutoka katika mlima Sinai. Huzaa watoto ambao ni watumwa. huyu ni Hajiri.
\v 25 Sasa Hajiri ni mlima Sinai ulioko Arabuni. Hufananishwa na Yerusalem ya sasa, kwa kuwa ni mtumwa pamoja na watoto wake.
\s5
\v 26 Bali Yerusalemu ambayo iko juu ni huru, na hii ndiyo mama yetu.
\v 27 Kwa kuwa imeandikwa, "Furahi, wewe mwanamke uliye tasa, wewe usiye zaa. Paza sauti na upige kelele kwa furaha, wewe ambaye huna uzoefu wa kuzaa. kwa maana wengi ni watoto wa aliye tasa, zaidi ya wale wa yule ambaye ana mume."
\s5
\v 28 Sasa ndugu, kama Isaka, ninyi ni watoto wa ahadi.
\v 29 Kwa wakati ule ambao mtu ambaye alizaliwa kwa mujibu wa mwili alimtesa yule aliyezaliwa kwa mujibu wa Roho. Kwa sasa ni vilevile.
\s5
\v 30 Maandiko husemaje? "Muondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe wa kiume. Kwa kuwa mtoto wa mwanamke mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru."
\v 31 Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali ni wa mwanamke huru.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ni kwa sababu Kristo alitupa uhuru ili tuwe huru. Hivyo, simameni imara wala msinaswe tena katika kongwa la utumwa.
\v 2 Tazama, Mimi Paulo, ninawaambia kwamba ikiwa mtatahiriwa, Kristo hatawafaidia kwa njia yoyote ile.
\s5
\v 3 Tena, namshuhudia kila mwanaume aliyetahiriwa kwamba anapaswa kuwajibika kwa sheria yote.
\v 4 Mmetengwa mbali na Kristo, wale wote "mnaohesabiwa haki" kwa sheria. Mmeanguka mbali na neema.
\s5
\v 5 Maana kwa njia ya Roho, kwa imani tunasubiri ujasiri wa haki.
\v 6 Katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuna maana yoyote. Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo ndiyo humaanisha kitu.
\v 7 Mlikuwa mnapiga mbio vizuri. Nani aliwazuia kutokuitii kweli?
\v 8 Ushawishi wa kufanya hivyo hautoki kwake yeye anayewaita ninyi.
\s5
\v 9 Chachu kidogo huathiri donge zima.
\v 10 Nina matumaini na ninyi katika Bwana kwamba hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote. Yeyote yule atakayewapotosha atabeba hukumu yake yeye mwenyewe, yeyote yule.
\s5
\v 11 Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwanini bado ninateswa? Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa.
\v 12 Ni matakwa yangu kuwa wale wanaowaongoza vibaya watajihasi wenyewe.
\s5
\v 13 Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi.
\v 14 Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni "Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe."
\v 15 Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi.
\s5
\v 16 Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.
\v 17 Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya.
\v 18 Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria.
\s5
\v 19 Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,
\v 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu,
\v 21 wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
\s5
\v 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,
\v 23 upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.
\v 24 Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya.
\s5
\v 25 Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.
\v 26 Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe.
\v 2 Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
\s5
\v 3 Ikiwa mtu yeyote anajiona ni bora wakati si kitu, anajidanganya mwenyewe.
\v 4 Kila mmoja na aipime kazi yake. Kisha atakuwa na kitu mwenyewe peke yake cha kujisifu, bila kujilinganisha mwenyewe na mtu yeyote.
\v 5 Maana kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.
\s5
\v 6 Mtu aliyefundishwa neno lazima amshirikishe mazuri yote mwalimu wake.
\v 7 Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna pia.
\v 8 Kila apandaye mbegu katika asili yake ya dhambi atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye mbegu katika Roho, atavuna uzima wa milele kutoka kwa Roho.
\s5
\v 9 Tusichoke katika kutenda mema, maana kwa wakati wake tutavuna ikiwa hatutakata tamaa.
\v 10 Hivyo basi, wakati tutakapokuwa na nafasi, tutende mema kwa kila mmoja. Tutende mema zaidi hasa kwa walio ndani ya imani.
\s5
\v 11 Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe.
\v 12 Wale wanaotaka kufanya mema kwa mtazamo wa mwili ndiyo wenye kuwalazimisha mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo.
\v 13 Maana hata hao waliotahiriwa wenyewe hawaishiki sheria. Badala yake wanataka ninyi mtahiriwe ili waweze kujivunia miili yenu.
\s5
\v 14 Isitokee nikajivuna isipokuwa kwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni katika yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu na mimi katika ulimwengu.
\v 15 Kwa kuwa haijalishi kutahiriwa au kutokutahiriwa kuwa ni kitu. Badala yake uzao mpya ni muhimu.
\v 16 Kwa wote wenye kuishi kwa kanuni hii, wawe na amani na rehema iwe juu yao wote, na juu ya Israel ya Mungu.
\s5
\v 17 Tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu.
\v 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu, ndugu. Amina.

296
50-EPH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,296 @@
\id EPH
\ide UTF-8
\h Waefeso
\toc1 Waefeso
\toc2 Waefeso
\toc3 eph
\mt Waefeso
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kwa waliotengwa kwa ajili ya Mungu walioko Efeso na ambao ni waaminifu katika Kristo Yesu.
\v 2 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa. Ni yeye aliyetubariki kwa kila baraka za kiroho, katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo.
\v 4 Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake.
\s5
\v 5 Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani.
\v 6 Matokeo yake ni kwamba Mungu anatukuzwa kwa neema ya utukufu wake. Hiki ndicho alichotupatia bure kwa njia ya mpendwa wake.
\s5
\v 7 Kwa kuwa katika mpendwa wake, tunaukombozi kupitia damu yake, msamaha wa dhambi. Tunalo hili kwa sababu ya utajiri wa neema yake.
\v 8 Alifanya neema hii kuwa nyingi kwa ajili yetu katika hekima na ufahamu.
\s5
\v 9 Mungu alifanya ijulikane kwetu ile kweli iliyofichika ya mpango, kutokana na hamu iliyodhihirishwa ndani ya Kristo.
\v 10 Wakati nyakati zimetimia kwa utimilifu wa mpango wake, Mungu ataviweka pamoja kila kitu cha mbinguni na cha juu ya nchi ndani ya Kristo.
\s5
\v 11 Katika Kristo tulikuwa tumechaguliwa na kukusudiwa kabla ya wakati. Hii ilikuwa ni kutokana na mpango wa anayefanya vitu vyote kwa kusudi la mapenzi yake.
\v 12 Mungu alifanya hivyo ili kwamba tuweze kuwapo kwa sifa ya utukufu wake. Tulikuwa wa kwanza kuwa na ujasiri ndani ya Kristo.
\s5
\v 13 Ilikuwa kwa njia ya Kristo kwamba mlisikia neno la kweli, injili ya wokovu wenu kwa njia ya Kristo. Ilikuwa katika yeye pia kwamba mmeamini na kutiwa mhuri na Roho Mtakatifu aliye ahidiwa.
\v 14 Roho ndiyo dhamana ya urithi wetu mpaka umiliki utakapopatikana. Hii ilikuwa ni kwa sifa ya utukufu wake.
\s5
\v 15 Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake.
\v 16 Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu.
\s5
\v 17 Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake.
\v 18 Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.
\s5
\v 19 Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake.
\v 20 Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu.
\v 21 Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia.
\s5
\v 22 Mungu amevitiisha vitu vyote chini ya miguu ya Kristo. Amemfanya yeye kichwa juu ya vitu vyote katika kanisa.
\v 23 Ni kanisa kwamba ndilo mwili wake, ukamilifu wake ambaye hujaza vitu vyote katika njia zote.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
\v 2 Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi.
\v 3 Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
\s5
\v 4 Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
\v 5 Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa.
\v 6 Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
\v 7 Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu.
\s5
\v 8 Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.
\v 9 Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.
\v 10 Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
\s5
\v 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa "msio na tohara" kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
\v 12 Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
\s5
\v 13 Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
\v 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
\v 15 Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
\v 16 Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.
\s5
\v 17 Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani kwao wale waliokuwa karibu.
\v 18 Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.
\s5
\v 19 Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
\v 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
\v 21 Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
\v 22 Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa sababu ya hii mimi, Paulo, ni mfungwa wa Yesu Kristo kwa ajili yenu Mataifa.
\v 2 Na amini ya kwamba mmesikia juu ya kazi ya neema ya Mungu aliyo nipa kwa ajili yenu.
\s5
\v 3 Nawaandikieni kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu. Huu ni ukweli uliyofichika ambao niliandika kwa kifupi kwenye barua nyingine.
\v 4 Usomapo kuhusu haya, utaweza kutambua busara yangu katika ukweli huu uliofichika kuhusu Kristo.
\v 5 Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa wana wa watu. Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho kwa Mitume waliotengwa na Manabii.
\s5
\v 6 Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili.
\v 7 Na kwa hili nimefanyika mtumishi kwa zawadi ya neema ya Mungu iliyotolewa kwangu kupitia utendaji wa nguvu yake.
\s5
\v 8 Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote katika wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo.
\v 9 inanipasa kuwaangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote.
\s5
\v 10 Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu.
\v 11 Haya yangetokea kupitia mpango wa milele ambao aliukamilisha ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\v 12 Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake.
\v 13 Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwasababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu.
\s5
\v 14 Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba.
\v 15 ambaye kwa yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina.
\v 16 Ninaomba kwamba apate kuwanemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu.
\s5
\v 17 Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani.
\v 18 Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo.
\v 19 Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu.
\s5
\v 20 Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu,
\v 21 kwake yeye kuwe utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita.
\v 2 Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo.
\v 3 Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
\s5
\v 4 Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu.
\v 5 Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
\v 6 na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.
\s5
\v 7 Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo.
\v 8 Ni kama maandiko yasemavyo: "Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu."
\s5
\v 9 Ni nini maana ya, "Alipaa," isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia?
\v 10 Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote.
\s5
\v 11 Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu.
\v 12 Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo.
\v 13 Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.
\s5
\v 14 Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka.
\v 15 Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo.
\v 16 Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
\s5
\v 17 Kwa hiyo, nasema hili, na nawasihi katika Bwana: Msitembee tena kama watu wa mataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao.
\v 18 Wametiwa giza katika mawazo yao. Wamefukuzwa kutoka katika uzima wa Mungu kwa ujinga ulio ndani yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
\v 19 Hawajisikii aibu. Wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu, katika kila aina ya uchoyo.
\s5
\v 20 Lakini, hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo.
\v 21 Nadhani kwamba mmesikia kuhusu yeye. Nadhani kwamba mmekuwa mkifundishwa katika yeye, kama tu ukweli ulivyo ndani ya Yesu.
\v 22 Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu.
\s5
\v 23 Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu.
\v 24 Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.
\s5
\v 25 Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. "Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake," kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake.
\v 26 Mwe na hasira, lakini msitende dhambi." Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.
\v 27 Msimpe Ibilisi nafasi.
\s5
\v 28 Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.
\v 29 Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.
\v 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
\s5
\v 31 Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi.
\v 32 Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.
\v 2 Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
\s5
\v 3 Zinaa au uchafu wowote na tamaa mbaya lazima visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
\v 4 wala machukizo yasitajwe, mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
\s5
\v 5 Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo nimwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
\v 6 Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
\v 7 Hivyo usishiriki pamoja nao.
\s5
\v 8 Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.
\v 9 Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
\v 10 Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.
\v 11 Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.
\v 12 Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.
\s5
\v 13 Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,
\v 14 kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, "Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako."
\s5
\v 15 Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
\v 16 Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
\v 17 Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.
\s5
\v 18 Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.
\v 19 Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.
\v 20 Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.
\v 21 Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.
\s5
\v 22 Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana.
\v 23 Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.
\v 24 Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.
\s5
\v 25 Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
\v 26 Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
\v 27 Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
\s5
\v 28 Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
\v 29 Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
\v 30 Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.
\s5
\v 31 "Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja".
\v 32 huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.
\v 33 Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
\v 2 "Mheshimu baba yako na mama yako" (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
\v 3 "ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi."
\s5
\v 4 Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
\s5
\v 5 Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
\v 6 Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
\v 7 watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
\v 8 mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.
\s5
\v 9 Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
\s5
\v 10 Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
\v 11 Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.
\s5
\v 12 kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu.
\v 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
\s5
\v 14 Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani.
\v 15 Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
\v 16 Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu.
\s5
\v 17 Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
\v 18 pamoja na maombi na dua. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.
\s5
\v 19 Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
\v 20 Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema.
\s5
\v 21 Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.
\v 22 Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.
\s5
\v 23 Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
\v 24 Neema na iwe pamoja na wote wanampenda Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo kufa.

193
51-PHP.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,193 @@
\id PHP
\ide UTF-8
\h Wafilipi
\toc1 Wafilipi
\toc2 Wafilipi
\toc3 php
\mt Wafilipi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu, Kwa wale walitengwa katika Kristo wanaoishi Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi.
\v 2 Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka ninyi nyote.
\v 4 Mara zote katika kila ombi langu kwa ajili yenu ninyi nyote, huwa na furahi ninapowaombea.
\v 5 Nina shukrani nyingi kwa sababu ya ushirika wenu katika injili tangu siku ya kwanza mpaka leo.
\v 6 Nina hakika kuwa yeye aliyeanzisha kazi njema ndani yenu ataendelea kuikamilisha mpaka siku ya Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 7 Ni sawa kwangu kujisikia hivi juu yenu ninyi nyote kwa sababu nimewaweka moyoni wangu. Maana ninyi mmekuwa washirika wenza katika neema katika kifungo changu na katika utetezi na uthibitishaji wangu wa injili.
\v 8 Mungu ni shahidi wangu, jinsi nilivyo na shauku juu ya yenu nyote katika undani wa pendo la Kristo Yesu.
\s5
\v 9 Na ninaomba kwamba: upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote.
\v 10 Ninaomba kwa ajili ya hili ili muwe na uwezo wa kupima na kuchagua mambo yaliyo bora sana. Pia ninawaombea ili muwe safi pasipokuwa na hatia yoyote katika siku ya Kristo.
\v 11 Na pia ili mjazwe na tunda la haki lipatikanalo katika Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
\s5
\v 12 Sasa ndugu zangu, nataka mjue kuwa, mambo yaliyotokea kwangu yameifanya injili iendelee sana.
\v 13 Ndiyo maana vifungo vyangu katika Kristo, vimejulikana kwa walinzi wa ikulu yote na kwa kila mtu pia.
\v 14 Na ndugu wengi katika Bwana, kwa sababu ya vifungo vyangu, wameshawishika na kuthubutu kulihubiri Neno pasipo hofu.
\s5
\v 15 Baadhi kweli hata humtangaza Kristo kwa fitina na ugomvi, na pia wengine kwa nia njema.
\v 16 Wale wanaomtangaza Kristo kwa upendo wanajua kuwa nimewekwa hapa kwa ajili ya utetezi wa injili.
\v 17 Bali wengine wanamtangaza Kristo kwa ubinafsi na nia mbaya. Hudhani kuwa wanasababisha matatizo kwangu katika minyororo yangu.
\s5
\v 18 Kwa hiyo? Sijali, aidha njia ikiwa ni kwa hila au kwa kweli, Kristo anatangazwa, na katika hili ninafurahia! Ndiyo, nitafurahia.
\v 19 kwa kuwa ninajua ya kuwa hili litaleta kufunguliwa kwangu. Jambo hili litatokea kwa sababu ya maombi yenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo.
\s5
\v 20 Kulingana na matarajio yangu ya uhakika na kweli ni kwamba, sitaona aibu. Badala yake, kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, natarajia kuwa Kristo atainuliwa katika mwili wangu, ikiwa katika uzima au katika kifo.
\v 21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.
\s5
\v 22 Lakini, kama kuishi katika mwili huzaa tunda katika kazi yangu, kwa hiyo sijui ni lipi la kuchagua.
\v 23 Maana ninasukumwa sana na mawazo haya mawili. Nina hamu ya kuuacha mwili na kuwa pamoja na Kristo, kitu ambacho ni cha thamani sana sana.
\v 24 Ingawa, kubaki katika mwili huu ni jambo la muhimu sana kwa ajili yenu.
\s5
\v 25 Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili, ninajua nitabaki na kuendelea kuwa pamoja nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo na furaha ya imani yenu.
\v 26 Na hii italeta furaha yenu kubwa katika Kristo Yesu, kwasababu yangu itaongezeka, kwa sababu ya uwepo wangu tena pamoja nanyi.
\v 27 Mnatakiwa kuishi maisha yenu katika mwenendo mzuri uipasayo injili ya Kristo. fanyeni hivyo ili nikija kuwaona au nisipokuja, nisikie kuwa mmesimama imara katika roho moja. natamani kusikia kuwa mna roho moja, mkiishindania imani ya injili kwa pamoja.
\s5
\v 28 na msitishwe na kitu chochote kinachofanywa na maadui zenu. Hii kwao ni ishara ya uharibifu. Bali kwenu ni ishara ya wokovu kutoka kwa Mungu.
\v 29 kwa maana ninyi mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa pia katika Yeye.
\v 30 kwa maana mna mgogoro uleule kama mliouona kwangu na mnasikia kwamba ninao hata sasa.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ikiwa kuna kutiwa moyo katika Kristo. Ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake. Ikiwa kuna ushirika wa Roho. Ikiwa kuna rehema na huruma.
\v 2 Ikamilisheni furaha yangu kwa kunia mamoja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja.
\s5
\v 3 Msifanye kwa ubinafsi na majivuno. Isipokuwa kwa unyenyekevu mkiwaona wengine kuwa bora zaidi yenu.
\v 4 Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.
\s5
\v 5 Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu.
\v 6 Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho.
\v 7 Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu.
\v 8 Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba.
\s5
\v 9 Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina.
\v 10 Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi.
\v 11 Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
\s5
\v 12 Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka.
\v 13 Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye.
\s5
\v 14 Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano.
\v 15 Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu.
\v 16 Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
\s5
\v 17 Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote.
\v 18 Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami.
\s5
\v 19 Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu.
\v 20 Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu.
\v 21 Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo.
\s5
\v 22 Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili.
\v 23 Kwa hiyo ninatumaini kumtuma haraka pindi tu nitakapofahamu nini kitatokea kwangu.
\v 24 Lakini nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja hivi karibuni.
\s5
\v 25 Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 26 Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.
\v 27 Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
\s5
\v 28 Kwa hiyo ninamrejesha kweny haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi.
\v 29 Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye.
\v 30 Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwa mko mbali nami.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.
\v 2 Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.
\v 3 Kwa kuwa sisi nndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.
\s5
\v 4 Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
\v 5 Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.
\s5
\v 6 Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa. Kwa tuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria.
\v 7 Lakini katika mambo yote niliyoyaona kuwa ya faida kwangu mimi, niliyahesabu kama takataka kwa sababu ya kumfahamu Kristo.
\s5
\v 8 Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo
\v 9 na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.
\v 10 Sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,
\v 11 angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu.
\s5
\v 12 Siyo kweli kwamba tayari nimeishayapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.
\v 13 Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.
\v 14 Najitahidi kufikia lengo kusudi ili nipate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.
\s5
\v 15 Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunuao hiilo kwenu.
\v 16 Hata hivyo, hatua ifikia na tuenende katika mtindo huo.
\s5
\v 17 Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.
\v 18 Wengi wanaoishi niwale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi -wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
\v 19 Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
\s5
\v 20 Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 21 Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.
\v 2 Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.
\v 3 Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
\s5
\v 4 katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.
\v 5 Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.
\v 6 Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.
\v 7 Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
\s5
\v 8 Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.
\v 9 Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.
\s5
\v 10 Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
\v 11 Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
\v 12 Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji.
\v 13 Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
\s5
\v 14 Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.
\v 15 Ninyi wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.
\v 16 Hata nilipokuwa Thesaslonika, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 17 Simaanishi kwamba natafuta msaada. Bali nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu.
\s5
\v 18 Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.
\v 19 Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
\v 20 Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina.
\s5
\v 21 Salamu zangu zimfikie kila muumini katika Kristo Yesu. Wapendwa nilio nao hapa wanawasalimieni.
\v 22 Pia waumini wote hapa wanawasalimieni, hususani wale wa familia ya Kaisari.
\v 23 Na sasa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu.

180
52-COL.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,180 @@
\id COL
\ide UTF-8
\h Wakolosai
\toc1 Wakolosai
\toc2 Wakolosai
\toc3 col
\mt Wakolosai
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,
\v 2 kwa waumini na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
\v 3 Tunatoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na tunawaombea mara kwa mara.
\s5
\v 4 Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa wale wote waliotengwa kwa ajili ya Mungu.
\v 5 Mna upendo huu kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu. Mlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika kabla katika neno la kweli, injili,
\v 6 ambayo imekuja kwenu. Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni kote. Imekuwa ikifanya hivi ndani yenu pia tangu siku mlipoisikia na kujifunza kuhusu neema ya Mungu katika kweli.
\s5
\v 7 Hii ndiyo injili mliyojifunza kutoka kwa Epafra, mpendwa wetu mtumishi mwenzetu, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
\v 8 Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho.
\s5
\v 9 Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujaacha kuwaombea. Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho.
\v 10 Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa Bwana katika njia zipendezazo. Tumekuwa tukiomba kwamba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu.
\s5
\v 11 Tunaomba mweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wake katika uvumilivu na ustahimilivu wote.
\v 12 Tunaomba kwamba, kwa furaha, mtatoa shukrani kwa Baba, aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru.
\s5
\v 13 Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza na kutuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa.
\v 14 Katika Mwanae tuna ukombozi, msamaha wa dhambi.
\s5
\v 15 Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana. Ni mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote.
\v 16 Kwakuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
\v 17 Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
\s5
\v 18 Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote.
\v 19 Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake,
\v 20 na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Mungu alipatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni.
\s5
\v 21 Nanyi pia, kwa wakati mmoja mlikuwa wageni kwa Mungu na mlikuwa maadui wake katika akili na matendo maovu.
\v 22 Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo. Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake,
\v 23 kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa mbali kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hi ndiyo injili iliyotangazwa kwa kila mtu aliyeumbwa chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi.
\s5
\v 24 Sasa nafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa.
\v 25 Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulijaza neno la Mungu.
\v 26 Huu ni ukweli wa siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika Yeye.
\v 27 Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua kulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli huu miongoni mwa Mataifa. Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao.
\s5
\v 28 Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo.
\v 29 Kwa jili hii, mimi najibidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa kuwa nataka mfahamu jinsi ambavyo nimekuwa na taabu nyingi kwa ajili yenu, kwa wote walioko Laodikia na kwa wote ambao hawajaona uso wangu katika mwili.
\v 2 Nafanya kazi ili kwamba mioyo yao iweze kufarijiwa kwa kuletwa pamoja katika upendo na katika utajiri wote wa wingi wa uhakika kamili wa maarifa, katika kuijua siri ya kweli ya Mungu, ambaye ni Kristo.
\v 3 Katika Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.
\s5
\v 4 Nasema hivi ili kwamba mtu yeyote asije akawafanyia hila kwa hotuba yenye ushawishi.
\v 5 Na ingawa sipo pamoja nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Ninafurahi kuona utaratibu wenu mzuri na nguvu ya imani yenu katika Kristo.
\s5
\v 6 Kama mlivyompokea Kristo Bwana, tembeeni katika yeye.
\v 7 Mwimarishwe katika yeye, mjengwe katika yeye, mwimarishwe katika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa katika shukrani nyingi.
\s5
\v 8 Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.
\v 9 Kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi katika mwili.
\s5
\v 10 Nanyi mmejazwa katika yeye. Yeye ni kichwa cha kila uweza na mamlaka.
\v 11 Katika yeye pia mlitahiriwa kwa tohara isiyofanywa na wanadamu katika kuondolewa mwili wa nyama, lakini ni katika tohara ya Kristo.
\v 12 Mlizikwa pamoja naye katika ubatizo. Na kwa njia ya imani katika yeye mlifufuliwa kwa uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.
\s5
\v 13 Na mlipokuwa mmekufa katika makosa yenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu, aliwafanya hai pamoja naye na kutusamehe makosa yetu yote.
\v 14 Alifuta kumbukumbu ya madeni iliyoandikwa, na taratibu zilizokuwa kinyume nasi. Aliiondoa yote na kuigongomea msalabani.
\v 15 Aliziondoa nguvu na mamlaka. Aliyaweka wazi na kuyafanya kuwa sherehe ya ushidi kwa njia ya msalaba wake.
\s5
\v 16 Kwa hiyo, mtu yeyote asiwahukumu ninyi katika kula au katika kunywa, au kuhusu siku ya sikukuu au mwezi mpya, au siku za Sabato.
\v 17 Hivi ni vivuli vya mambo yajayo, lakini kiini ni Kristo.
\s5
\v 18 Mtu awaye yote asinyang'anywe tuzo yake kwa kutamani unyenyekevu na kwa kuabudu malaika. Mtu wa jinsi hiyo huingia katika mambo aliyoyaona na kushawishiwa na mawazo yake ya kimwili.
\v 19 Yeye hakishikilii kichwa. Ni kutoka katika kichwa kwamba mwili wote kupitia viungo vyake na mifupa huungwa na kushikamanishwa kwa pamoja; na hukua kwa ukuaji utolewao na Mungu.
\s5
\v 20 Ikiwa mlikufa pamoja na Kristo kwa tabia za dunia, mbona mnaishi kama mnawajibika kwa dunia:
\v 21 "Msishike, wala kuonja, wala kugusa"?
\v 22 Haya yote yameamuriwa kwa ajili ya uharibifu ujao na matumizi, kutokana na maelekezo na mafundisho ya wanadamu.
\v 23 Sheria hizi zina hekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili. Lakini hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ikiwa tena Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu.
\v 2 Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani.
\v 3 Kwa kuwa mmekufa, na maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
\v 4 Wakati Kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtaonekana naye katika utukufu.
\s5
\v 5 Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, zinaa, uchafu, shauku mbaya, nia mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu.
\v 6 Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii.
\v 7 Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao.
\v 8 Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.
\s5
\v 9 Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake.
\v 10 Mmevaa utu mpya, ambao unafanywa upya katika maarifa kutokana mfano wa yule aliye muumba.
\v 11 Katika maarifa haya, hakuna Myunani na Myahudi, kutahiriwa na kutokutahiriwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, asiye mtumwa, lakini badala yake Kristo ni mambo yote katika yote.
\s5
\v 12 Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
\v 13 Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ilele ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi.
\v 14 Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.
\s5
\v 15 Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani.
\v 16 Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu.
\v 17 Na chochote mfanyacho, katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.
\s5
\v 18 Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
\v 19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao.
\v 20 Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.
\v 21 Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
\s5
\v 22 Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama watu wa kufurahisha tu, bali kwa moyo wa kweli. Mwogopeni Mungu.
\v 23 Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.
\v 24 Mnajua ya kwamba mtapokea tuzo ya umilkaji kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia.
\v 25 Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mabwana, toeni kwa watumwa mambo yaliyo haki na ya adili. Mnajua pia kwamba mnaye Bwana mbinguni.
\s5
\v 2 Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.
\v 3 Ombeni pamoja kwa ajili yetu pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo.
\v 4 Na ombeni kwamba niweze kuliweka wazi, kama inavyonipasa kusema.
\s5
\v 5 Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.
\v 6 Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu.
\s5
\v 7 Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana.
\v 8 Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi na pia kwamba aweze kuwatia moyo.
\v 9 Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.
\s5
\v 10 Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, "kama akija kwenu, mpokeeni,"
\v 11 Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa jili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu.
\s5
\v 12 Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hufanya bidii katika maombi kwa ajili, ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu.
\v 13 Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli.
\v 14 Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu.
\s5
\v 15 Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.
\v 16 Barua hii itakapokuwa imesomwa miongoni mwenu, isomwe pia kwa kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.
\v 17 Sema kwa Arkipo, ''Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza."
\s5
\v 18 Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.

170
53-1TH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,170 @@
\id 1TH
\ide UTF-8
\h 1 Wathesalonike
\toc1 1 Wathesalonike
\toc2 1 Wathesalonike
\toc3 1th
\mt 1 Wathesalonike
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani iwe nanyi.
\s5
\v 2 Tunatoa shukrani kwa Mungu kila mara kwa ajili yenu nyote, wakati tunapowataja katika maombi yetu.
\v 3 Tunaikumbuka bila kukoma mbele ya Mungu na baba yetu kazi yenu ya imani, juhudi ya upendo, na uvumilivu wenye ujasiri kwa ajili ya baadaye katika Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 4 Ndugu Mnaopendwa na Mungu, tunajua wito wenu.
\v 5 Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu.
\s5
\v 6 Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.
\v 7 Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini.
\s5
\v 8 Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote.
\v 9 Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli.
\v 10 Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure.
\v 2 Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi.
\s5
\v 3 Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila.
\v 4 Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu.
\s5
\v 5 Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote wote, kama mjuavyo, wala ukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu.
\v 6 Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo.
\s5
\v 7 Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe.
\v 8 Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mmekuwa wapendwa wetu.
\v 9 Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu.
\s5
\v 10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini.
\v 11 Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia
\v 12 kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake.
\s5
\v 13 Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini.
\s5
\v 14 Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe watu wa kuiga makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.
\v 15 walikuwa ni Wayahudi ndiyo waliomuua Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni Wayahudi ambao walitufukuza tutoke nje. Hawampendezi Mungu na ni maadui kwa watu wote.
\v 16 Walituzuia tusiseme na Mataifa ili wapate kuokolewa. Matokeo yake ni kwamba wanaendelea na dhambi zao. Mwisho ghadhabu imekuja juu yao.
\s5
\v 17 Sisi, ndugu, tulikuwa tumetengana nanyi kwa muda mfupi, kimwili, si katika roho. Tulifanya kwa uwezo wetu na kwa shauku kuu kuona nyuso zenu.
\v 18 Kwa kuwa tulitaka kuja kwenu, mimi Paulo, kwa mara moja na mara nyingine, lakini shetani alituzuia.
\v 19 Kwa kuwa kujiamini kwetu ni nini kwa baadaye, au furaha, au taji ya kujivunia mbele za Bwana wetu Yesu wakati wa kuja kwake? Je si ninyi zaidi kama walivyo wengine?
\v 20 Kwa kuwa ninyi ni utukufu na furaha yetu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa hiyo, tulipo kuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuwa vema kubaki kule Athene peke yetu.
\v 2 Tulimtuma Timotheo, ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika injili ya Kristo, kuwaimalisha na kuwafariji kuhusiana na imani yenu.
\v 3 Tulifanya haya ili kusudi asiwepo yeyote wa kuteteleka kutokana na mateso haya, kwa kuwa wenyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili.
\s5
\v 4 Kwa kweli, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitangulia kuwaeleza ya kuwa tulikuwa karibu kupata mateso, na hayo yalitokea kama mjuavyo.
\v 5 Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma ilikusudi nipate kujua juu ya imani yenu. Huenda mjaribu alikuwa angalau amewajaribu, na kazi yetu ikawa ni bure.
\s5
\v 6 Lakini Timotheo alikuja kwetu kutokea kwenu na akatuletea habari njema juu ya imani na upendo wenu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu yetu, na kuwa mnatamani kutuona kama ambavyo nasi twatamani kuwaona ninyi.
\v 7 Kwa sababu hii, ndugu tulifarijika sana na ninyi kwa sababu ya imani yenu, katika taabu na mateso yetu yote.
\s5
\v 8 Kwa sasa tunaishi, kama mkisimama imara kwa Bwana,
\v 9 Kwani ni shukurani zipi tumpe Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tuliyonayo mbele za Mungu juu yenu?
\v 10 Tunaomba sana usiku na mchana ili tuweze kuziona nyuso zenu na kuwaongezea kinachopungua katika imani yenu.
\s5
\v 11 Mungu wetu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia yetu tufike kwenu.
\v 12 Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi katika pendo, mkipendana na kuwapenda watu wote, kama tunavyowafanyia ninyi.
\v 13 Na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu na Baba yetu katika ujio wa Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Hatimaye, ndugu, twawatia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maelekezo toka kwetu namna iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kwa njia hiyo pia muenende na kutenda zaidi.
\v 2 Kwa kuwa mwajua ni maelekezo gani tuliyowapa kupitia Bwana Yesu.
\s5
\v 3 Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wenu - kwamba muepuke zinaa,
\v 4 Kwamba kila mmoja wenu anajua namna ya kumiliki mke wake mwenyewe katika utakatifu na heshima.
\v 5 Usiwe na mke kwa ajili ya tamaa za mwili (kama Mataifa wasiomjua Mungu).
\v 6 Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia.
\s5
\v 7 Kwa kuwa Bwana hakutuita kwa uchafu, bali kwa utakatifu.
\v 8 Kwa hiyo anayelikataa hili hawakatai watu, bali anamkataa Mungu, anayewapa Roho Mtakatifu wake.
\s5
\v 9 Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja ya mtu yeyote kukuandikia, kwa kuwa mmefundishwa na Mungu kupendana ninyi kwa ninyi.
\v 10 Hakika, mlifanya haya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote, lakini twawasihi, ndugu, mfanye hata na zaidi.
\v 11 Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru.
\v 12 Fanya haya ili uweze kuenenda vizuri na kwa heshima kwa hao walio nje ya imani, ili usipungukiwe na hitaji lolote.
\s5
\v 13 Hatutaki ninyi muelewe isivyo sahihi, enyi ndugu, juu ya hao waliolala, ili msije mkahuzunika kama wengine wasio na uhakika kuhusu wakati ujao.
\v 14 Iwapo tunaamini kuwa Yesu alikufa na akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti katika yeye.
\v 15 Kwa ajili ya hayo twawaambia ninyi kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaokuwepo wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti.
\s5
\v 16 Kwa kuwa Bwana mwenyewe atashuka toka mawinguni. Atakuja na sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza.
\v 17 Kisha sisi tulio hai, tuliobaki, tutaungana katika mawingu pamoja nao kumlaki Bwana hewani. Kwa njia hii tutakuwa na Bwana siku zote.
\v 18 Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Sasa, kwa habari ya muda na nyakati, ndugu, hamna haja kwamba kitu chochote kiandikwe kwenu.
\v 2 Kwa kuwa ninyi wenyewe mwajua kwa usahihi ya kuwa siku ya Bwana inakuja kama mwizi ajapo usiku.
\v 3 Pale wasemapo kuna "Amani na usalama", ndipo uharibifu huwajia ghafla. Ni kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba. Hawataepuka kwa njia yeyote.
\s5
\v 4 Lakini ninyi, ndugu hampo kwenye giza hata ile siku iwajie kama mwizi.
\v 5 Kwa maana ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi siyo wana wa usiku au wa gizani.
\v 6 Hivyo basi, tusilale kama wengine walalavyo. Bali tukeshe na kuwa makini.
\v 7 Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku.
\s5
\v 8 Kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, tuwe makini. Tuvae ngao ya imani na upendo, na, kofia ya chuma, ambayo ni uhakika wa wokovu wa wakati ujao.
\v 9 Kwa kuwa Mungu hakutuchagua mwanzo kwa ajili ya gadhabu, bali kwa kupata wokovu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo.
\v 10 Yeye ndiye aliyetufia ili kwamba, tukiwa macho au tumelala, tutaishi pamoja naye.
\v 11 Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.
\s5
\v 12 Ndugu, twawaomba muwatambue wale wanaotumika miongoni mwenu na wale walio juu yenu katika Bwana na wale wanao washauri.
\v 13 Tunawaomba pia muwatambue na kuwapa heshima katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Muwe na amani miongoni mwenu ninyi wenyewe.
\v 14 Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote.
\s5
\v 15 Angalieni asiwepo mtu yeyote anayelipa baya kwa baya kwa mtu yeyote. Badala yake, fanyeni yaliyo mema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
\v 16 Furahini siku zote.
\v 17 Ombeni bila kukoma.
\v 18 Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.
\s5
\v 19 Msimzimishe Roho.
\v 20 Msiudharau unabii.
\v 21 Yajaribuni mambo yote. Mlishike lililo jema.
\v 22 Epukeni kila mwonekano wa uovu.
\s5
\v 23 Mungu wa amani awakamilishe katika utakatifu. Roho, nafsi na mwili vitunzwe pasipo mawaa katika kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 24 Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda.
\s5
\v 25 Ndugu, tuombeeni pia.
\v 26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.
\v 27 Nawasihi katika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu wote.
\v 28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

96
54-2TH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,96 @@
\id 2TH
\ide UTF-8
\h 2 Wathesalonike
\toc1 2 Wathesalonike
\toc2 2 Wathesalonike
\toc3 2th
\mt 2 Wathesalonike
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
\v 2 Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 3 Imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu. Maana hivi ndivyo itupasavyo, kwa kuwa imani yenu inakua sana, na upendo wenu kwa kila mtu uongezeke mwingi.
\v 4 Hivyo sisi wenyewe tunaongea kwa fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu. Tunazungumza habari ya saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote. Tunaongea kwa habari ya mateso mnayostahimili.
\v 5 Hii ndiyo ishara ya hukumu ya haki ya Mungu. Matokeo ya haya ni kuwa ninyi mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu ambao kwa ajili yake mnateswa.
\s5
\v 6 Kwa kuwa ni haki kwa Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi,
\v 7 na kuwapa raha ninyi mteswao pamoja nasi. Atafanya hivi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake.
\v 8 Katika mwali wa moto atawalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu.
\s5
\v 9 Watateseka kwa maangamizi ya milele wakiwa wametengwa na uwepo wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.
\v 10 Atafanya wakati atakapokuja ili kutukuzwa na watu wake na kustaajabishwa na wote walioamini. Kwa sababu ushuhuda wetu kwenu ulisadikiwa kwenu.
\s5
\v 11 Kwa sababu hii twawaombea ninyi siku zote. Twaomba kwamba Mungu wetu awahesabu kuwa mlistahili kuitwa. Twaomba kwamba apate kutimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu.
\v 12 Tunaomba mambo haya ili mpate kulitukuza jina la Bwana Yesu. Tunaomba kwamba mpate kutukuzwa naye, kwa sababu ya neema ya Mungu na ya Bwana Yesu Kristo.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Sasa kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa pamoja ili tuwe naye: tunawaomba ninyi ndugu zetu,
\v 2 kwamba msisumbuliwe wala kutabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonkana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja.
\s5
\v 3 Mtu na asiwadanganye kwa namna yoyote. Kwa kuwa haitakuja mpaka lile anguko litokee kwanza na mtu wa uasi afunuliwe, yule mwana wa uharibifu.
\v 4 Huyu ndiye apingaye naye hujiinua mwenyewe akimpinga Mungu na chochote kinachoabudiwa. Na matokeo yake, hukaa kwenye hekalu la Mungu na kujionyesha yeye kuwa kama Mungu.
\s5
\v 5 Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa nanyi niliwaambia juu ya mambo haya?
\v 6 Sasa mnajua kile kinachomzuia, ili kwamba aweze kufunuliwa kwa wakati sahihi utakapowadia.
\v 7 Kwa kuwa siri ya yule mtu mwenye kuasi inafanya kazi mpaka sasa, ila tu kuna anaye mzuia sasa mpaka atakapotolewa njiani.
\s5
\v 8 Ndipo yule mwenye kuasi atakapofunuliwa, amabaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake. Bwana atamfanya kuwa si chochote kwa ufunuo wa ujio wake.
\v 9 Ujio wa yule mwenye kuasi utakuwa kwa sababu ya kazi ya shetani kwa nguvu zote, ishara na maajabu ya uongo,
\v 10 na uongo wote wenye udhalimu. Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea, kwa sababu hawakuupokea upendo wa kweli kwa ajili ya kuokolewa kwao.
\s5
\v 11 Kwa sababu hiyo Mungu anawatumia kazi yenye uovu ili waamini uongo.
\v 12 Matokeo yake ni kwamba wote watahukumiwa, wale ambao hawakuamini ukweli bali wao hujifurahisha katika udhalimu.
\s5
\v 13 Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli.
\v 14 Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 15 Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu.
\s5
\v 16 Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema,
\v 17 awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu.
\v 2 Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani.
\v 3 Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.
\s5
\v 4 Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza.
\v 5 Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.
\s5
\v 6 Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu.
\v 7 Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu.
\v 8 Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi.
\v 9 Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.
\s5
\v 10 Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, "Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile."
\v 11 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu.
\v 12 Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
\s5
\v 13 Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi.
\v 14 Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika.
\v 15 Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu.
\s5
\v 16 Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote.
\v 17 Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo.
\v 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.

222
55-1TI.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,222 @@
\id 1TI
\ide UTF-8
\h 1Timotheo
\toc1 1Timotheo
\toc2 1Timotheo
\toc3 1ti
\mt 1Timotheo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, Mtume wa Kristo Yesu, kulingana na amri ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliye ujasiri wetu,
\v 2 kwa Timotheo mwanangu wa kweli katika imani: Neema, rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\v 3 Kama nilivyokusihi nilipoondoka kwenda Makedonia, ubaki Efeso ili kwamba uweze kuwaamru watu fulani wasifundishe mafundisho tofauti.
\v 4 Pia wasisikilize hadithi na orodha za nasaba zisizo na mwisho. Haya husababisha mabishano zaidi kuliko kuwasaidia kuendeleza mpango wa Mungu wa imani.
\s5
\v 5 Basi lengo la agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi, katika dhamiri nzuri na katika imani ya kweli.
\v 6 Baadhi ya watu wamelikosa lengo wakayaacha mafundisho haya na kugeukia mazungumzo ya kipumbavu.
\v 7 Wanataka kuwa waalimu wa sheria, lakini hawafahamu wanachosema au wanachosisitiza.
\v 8 lakini tunajua kwamba sheria ni njema kama mtu ataitumia kwa usahihi.
\s5
\v 9 Tunajua kuwa, sheria haikutungwa kwa ajili ya mtu mwenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, watu wasio wataua na wenye dhambi, na ambao hawana Mungu na waovu. Imetungwa kwa ajili ya wauao baba na mama zao, kwa ajili ya wauaji,
\v 10 kwa ajili ya waasherati, kwa ajili ya watu wazinzi, kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kuwafanya watumwa, kwa ajili ya waongo, kwa ajili ya mashahidi wa uongo, na yeyote aliye kinyume na maelekezo ya uaminifu.
\v 11 Malekezo haya yanatokana na injili yenye utukufu ya Mungu mwenye kubarakiwa ambayo kwayo nimeaminiwa.
\s5
\v 12 Ninamshukuru Yesu Kristo Bwana wetu. Alinitia nguvu, kwa kuwa alinihesabu mimi kuwa mwaminifu, na akaniweka katika huduma.
\v 13 Nilikuwa mtu wa kukufuru, mtesaji na mtu wa vurugu. Lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda kwa ujinga kwa kutoamini.
\v 14 Lakini neema ya Mungu wetu imejaa imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.
\s5
\v 15 Ujumbe huu ni wa kuaminika na unastahili kupokelewa na wote, ya kuwa Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi. Mimi ni mbaya zaidi ya wote.
\v 16 Lakini kwa sababu hii mimi nilipewa rehema ili kwamba ndani yangu mimi, awali ya yote, Kristo Yesu adhihirishe uvumilivu wote. Alifanya hivyo kama kielelezo kwa wote watakaomtumaini Yeye kwa ajili ya uzima wa milele.
\v 17 Na sasa kwa Mfalme asiye na ukomo, asiyekufa, asiyeonekana, Mungu pekee, iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
\s5
\v 18 Ninaliweka agizo hili mbele yako Timotheo, mtoto wangu. Nafanya hivi kulingana na unabii uliotolewa hapo kwanza kukuhusu wewe, ili kwamba uhusike katika vita njema.
\v 19 Fanya hivyo ili kwamba uwe na imani na dhamiri njema. Baadhi ya watu wameyakataa haya wakaangamiza imani.
\v 20 Kama vile Himeneyo na Alekizanda ambao nimempa shetani ili wafundishwe wasikufuru.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo awali ya yote, nahitaji maombi, na dua, na maombezi, na shukrani vifanyike kwa ajili ya watu wote,
\v 2 kwa ajili ya wafalme na wote ambao wako kwenye mamlaka, ili kwamba tuweze kuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na heshima.
\v 3 Hili ni jema na lenye kukubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu.
\v 4 Yeye hutamani kuwa watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli.
\s5
\v 5 Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu.
\v 6 Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka.
\v 7 Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. Nasema kweli. Sisemi uongo. Mimi ni mwalimu watu Mataifa katika imani na kweli.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.
\v 9 Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.
\v 10 Pia nataka wavae mavazi yanayowastahili wanawake wanaokiri uchaji kwa kupitia matendo mema.
\s5
\v 11 Mwanamke na ajifunze katika hali ya utulivu na kwa utii wote.
\v 12 Simruhusu mwanamke kufundisha, au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume bali aishi katika hali ya ukimya.
\s5
\v 13 Kwa kuwa Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva.
\v 14 Adamu hakudanganywa, lakini mwanamke alidanganywa kabisa katika uasi.
\v 15 Hata hivyo, ataokolewa kwa kupitia kuzaa watoto, kama wataendelea katika imani na upendo na katika utakaso na akili njema.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema.
\v 2 Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi,, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe uwezo wa kufundisha.
\v 3 Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha.
\s5
\v 4 Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote.
\v 5 Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu?
\s5
\v 6 Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu.
\v 7 Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu.
\s5
\v 8 Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa.
\v 9 Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa.
\v 10 Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama.
\s5
\v 11 Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote.
\v 12 Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao.
\v 13 Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
\s5
\v 14 Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni.
\v 15 Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli.
\s5
\v 16 Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: "Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa
\v 2 katika uongo na unafiki. Dhamiri zao zitabadilishwa.
\s5
\v 3 Watawazuia kuoa na kupokea vyakula ambavyo Mungu aliviumba vitumiwe kwa shukrani miongoni mwao waaminio na wenye kuijua kweli.
\v 4 Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu amekiumba ni chema. Hakuna ambacho tunapokea kwa shukrani kinastahili kukataliwa.
\v 5 Kwa sababu kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi.
\s5
\v 6 Kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu, utakuwa mtumishi mzuri wa Yesu Kristo. Kwa sababu umestawishwa kwa maneno ya imani na kwa mafundisho mazuri ambayo umeyafuata.
\v 7 Lakini zikatae hadithi za kidunia ambazo zinapendwa na wanawake wazee. Badala yake, jifunze mwenyewe katika utaua.
\v 8 Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.
\s5
\v 9 Ujumbe huu ni wakuaminiwa na unastahili kukubaliwa kabisa.
\v 10 Kwa kuwa ni kwa sababu hii tunataabika na kufanya kazi kwa bidii sana. Kwa kuwa tunao ujasiri katika Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, lakini hasa kwa waaminio.
\s5
\v 11 Uyaseme na kuyafundisha mambo haya.
\v 12 Mtu yeyote asiudharau ujana wako. Badala yake, uwe mfano kwa wote waaminio, katika usemi, mwenendo, upendo, uaminifu, na usafi.
\v 13 Mpaka nitakapokuja, dumu katika kusoma, katika kuonya, na katika kufundisha.
\s5
\v 14 Usiipuuze karama iliyomo ndani yako, ambayo ulipewa kupitia unabii, kwa kuwekewa mikono na wazee.
\v 15 Uyajali mambo haya. Ishi katika hayo ili kukua kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Zingatia sana mwenendo wako na mafundisho.
\v 16 Dumu katika mambo haya. Maana kwa kufanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.
\v 2 Uwatiye moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote.
\s5
\v 3 Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli.
\v 4 Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.
\s5
\v 5 Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
\v 6 Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai.
\s5
\v 7 Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.
\v 8 Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini.
\s5
\v 9 Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.
\v 10 Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
\s5
\v 11 Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili dhidi ya Kristo, wanataka kuolewa.
\v 12 Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.
\v 13 Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
\s5
\v 14 Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.
\v 15 Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.
\v 16 Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.
\s5
\v 17 Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu.
\v 18 Kwa kuwa maandiko yanasema, "Usimfumbe ng'ombe kinywa apulapo nafaka," na "Mfanya kazi anastahili mshahara wake."
\s5
\v 19 Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu.
\v 20 Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.
\s5
\v 21 Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uzitunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
\v 22 Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe usafi.
\s5
\v 23 Hakupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.
\v 24 Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.
\v 25 Vivyo hivyo, baadhi ya kazi njema hujulikana kwa uwazi, lakini hata zingine hazitafichika.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote, wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe.
\v 2 Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.
\s5
\v 3 Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa.
\v 4 Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya,
\v 5 na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiri"
\s5
\v 6 Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
\v 7 Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani.
\v 8 Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.
\s5
\v 9 Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.
\v 10 Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.
\s5
\v 11 Lakini wewe mtu wa Mungu, yakimbie mambo hayo. Fuata haki, utauwa, uaminifu, upendo, usitahimilivu, na upole.
\v 12 Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema.
\s5
\v 13 Nakupa amri hii mbele za Mungu, anayesababisha vitu vyote kuishi, na mbele ya Yesu Kristo, aliyenena iliyo kweli kwa Pontio Pilato:
\v 14 itunze amri kwa ukamilifu, pasipo mashaka, hadi ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 15 Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza.
\v 16 Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiriwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina.
\s5
\v 17 Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie.
\v 18 Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa.
\v 19 Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.
\s5
\v 20 Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yenye kujipinga ambayo kwa kwa uongo huitwamaarifa.
\v 21 Baadhi ya watu huyatangaza mambo haya, na hivyo wameikosa imani. Neema na iwe pamoja nawe.

158
56-2TI.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,158 @@
\id 2TI
\ide UTF-8
\h 2 Timotheo
\toc1 2 Timotheo
\toc2 2 Timotheo
\toc3 2ti
\mt 2 Timotheo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, sawasawa na ahadi ya uzima ulio ndani ya Kristo Yesu,
\v 2 kwa Timotheo mwana mpendwa: Neema, rehema na amani toka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.
\s5
\v 3 Ninamshukuru Mungu, ambaye ninamtumikia kwa nia njema kama walivyofanya baba zangu, ninapokumbuka daima katika maombi yangu. Usiku na
\v 4 mchana ninatamani kukuona, ili kwamba nijawe na furaha. Ninayakumbuka machozi yako.
\v 5 Nimekuwa nikikumbushwa kuhusu imani yako halisi, ambayo hapo kwanza ilikaa kwa bibi yako Loisi na mama yako Yunisi. Na nina hakika ya kwamba imani hiyo inakaa ndani yako pia.
\s5
\v 6 Hii ndiyo sababu nakukumbusha kuchochea karama ya Mungu iliyomo ndani yako kwa njia ya kuwekewa mikono yangu.
\v 7 Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu.
\s5
\v 8 Kwa hiyo usiuonee haya ushuhuda kuhusu Bwana wetu, wala wangu mimi Paulo mfungwa wake. Bali ushiriki mateso kwa ajili ya injili sawasawa na uweza wa Mungu.
\v 9 Ni Mungu aliyetuokoa na kutuita kwa wito mtakatifu. Hakufanya hivi kulingana na kazi zetu bali kulingana na neema na mpango wake mwenyewe. Alitupatia mambo haya katika Kristo Yesu kabla ya nyakati kuanza.
\v 10 Lakini sasa wokovu wa Mungu umekwishafunuliwa kwa kuja kwa mwokozi wetu Kristo Yesu. Ni Kristo aliyeikomesha mauti na kuleta uzima usiokoma kwa nuru ya injili.
\v 11 Kwa sababu hiyo nilichaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu.
\s5
\v 12 Kwa sababu hii nateseka pia, lakini sioni haya kwa kuwa namjua yeye niliyekwisha kumuamini. Nina hakika kuwa yeye anaweza kukitunza kile nilichokikabidhi kwake hata siku ile.
\v 13 Ukumbuke mfano wa ujumbe wa uaminifu uliousikia toka kwangu, pamoja na imani na upendo ulio ndani ya Kristo Yesu.
\v 14 Yatunze Mambo mazuri aliyokukabidhi Mungu kupitia Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu.
\s5
\v 15 Unajua ya kuwa, wote waishio katika Asia waliniacha. Kwenye kundi hili wamo Figelo na Hemogene.
\v 16 Bwana airehemu nyumba ya Onesiforo kwa kuwa mara nyingi aliniburudisha na hakuionea aibu minyororo yangu.
\v 17 Badala yake, alipokuwa Roma alinitafuta kwa bidii na akanipata.
\v 18 Mungu amjalie kupata rehema kutoka kwake siku ile. Kama alivyonisaidia nilipokuwa Efeso, wewe wajua vyema.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo, wewe mwanangu, utiwe nguvu katika neema iliyondani ya Kristo Yesu.
\v 2 Na mambo uliyoyasikia kwangu miongoni mwa mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu waaminifu ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.
\s5
\v 3 Shiriki mateso pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
\v 4 Hakuna askari atumikae wakati huo huo akijihusisha na shughuli za kawaida za maisha haya, ili kwamba ampendeze ofisa wake mkuu.
\v 5 Pia kama mtu akishindana kama mwanariadha, hatapewa taji asiposhindana kwa kufuata kanuni.
\s5
\v 6 Ni Muhimu kwamba mkulima mwenye bidii awe wa kwanza kupokea mgao wa mazao yake.
\v 7 Tafakari kuhusu nisemacho, kwa maana Bwana atakupa uelewa katika mambo yote.
\s5
\v 8 Mkumbuke Yesu Kristo, kutoka uzao wa Daudi, ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu. Hii ni kulingana na ujumbe wangu wa Injili,
\v 9 ambao kwa sababu ya huo ninateswa hata kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi kwa minyororo.
\v 10 Kwa hiyo, navumilia mambo yote kwa ajili ya wale ambao Mungu amekwishawachagua, ili kwamba nao pia waupate wokovu ulio katika Kristo Yesu pamoja na utukufu wa milele.
\s5
\v 11 Usemi huu ni wakuaminika: "Ikiwa tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia,
\v 12 kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia, kama tukimkana yeye, naye pia atatukana sisi.
\v 13 kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe."
\s5
\v 14 Endelea kuwakumbusha juu ya mambo haya. Waonye mbele za Mungu waache kubishana kuhusu maneno. Kwa sababu hakuna manufaa katika jambo hili. Kutokana na hili kuna uharibifu kwa wale wanaosikiliza.
\v 15 Fanya bidii kujionesha kuwa umekubalika kwa Mungu kama mtenda kazi asiye na sababu ya kulaumiwa. Litumie neno la kweli kwa usahihi.
\s5
\v 16 Jiepushe na majadiliano ya kidunia, ambayo huongoza kwa zaidi na zaidi ya uasi.
\v 17 Majadiliano yao yatasambaa kama donda ndugu. Miongoni mwao ni Himenayo na Fileto.
\v 18 Hawa ni watu walioukosa ukweli. Wanasema ya kuwa ufufuo tayari umishatokea. Wanapindua imani ya baadhi ya watu.
\s5
\v 19 Hata hivyo, msingi imara wa Mungu unasimama, wenye uandishi huu, "Bwana anawajua walio wake, na kila alitajaye jina la Bwana ni lazima ajitenge na udhalimu."
\v 20 Kwenye nyumba ya kitajiri, siyo kwamba vimo vyombo vya dhahabu na shaba tu. Pia kuna vyombo vya miti na udongo. Baadhi ya hivi ni kwa ajili ya matumizi ya heshima na baadhi yake ni kwa matumizi yasiyo ya heshima.
\v 21 Ikiwa mtu atajitakasa mwenyewe kutoka kwenye matumizi yasiyo ya heshima, yeye ni chombo chenye kuheshimika. Ametengwa maalumu, mwenye manufaa kwa Bwana, na ameandaliwa kwa kila kazi njema.
\s5
\v 22 Zikimbie tamaa za ujanani. Ukifuata haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
\v 23 Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi.
\s5
\v 24 Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu.
\v 25 Ni lazima awaelimishe kwa upole wale wampingao. Yamkini Mungu aweze kuwapatia toba kwa kuifahamu kweli.
\v 26 Waweze kupata ufahamu tena na kuepuka mtego wa Shetani, baada ya kuwa wametekwa na yeye kwa ajili ya mapenzi yake.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Lakini fahamu hili: katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu.
\v 2 kwa sababu watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye majivuno, wenye dhihaka, wasiotii wazazi wao, wasiokuwa na shukurani na waovu.
\v 3 Wasio na upendo wa asili, wasiotaka kuishi kwa amani na yeyote, wachonganishi, wasingiziaji, wasioweza kujizuia, wenye vurugu, wasiopenda mema.
\v 4 Watakuwa wasaliti, wakaidi, wenye kujipenda wenyewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
\s5
\v 5 Kwa nje watakuwa na sura ya ucha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe na watu hao.
\v 6 Kwa kuwa baadhi yao ni wanaume wanaoingia kwenye familia za watu na kushawishi wanawake wajinga. Hawa ni wanawake waliojawa dhambi na wenye kuongozwa na tamaa za kila aina.
\v 7 Wanawake hawa hujifunza siku zote, lakini kamwe hawawezi kuufikia ufahamu wa ile kweli.
\s5
\v 8 Kama vile ambavyo Yane na Yambre walisimama kinyume na Musa. Kwa njia hii walimu hawa wa uongo husimama kinyume na kweli. Ni watu walioharibiwa katika fikira zao, wasiokubalika kuhusiana na imani.
\v 9 Lakini hawataendelea mbali. Kwa kuwa upumbavu wao utawekwa wazi kwa watu wote, kama ulivyokuwa wa wale watu.
\s5
\v 10 Lakini wewe umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu na ustahimilivu wangu,
\v 11 mateso, maumivu na yaliyonipata kule Antiokia, Ikonio na Listra. Niliyavumilia mateso. Bwana aliniokoa katika yote hayo.
\v 12 Wote wanaotaka kuishi katika maisha ya kumcha Mungu katika Kristo Yesu watateswa.
\v 13 Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi. Watawapotosha wengine. Wao wenyewe wamepotoshwa.
\s5
\v 14 Lakini wewe, dumu katika mambo uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti. Kwa kuwa unajua umejifunza kwa nani.
\v 15 Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani katika kristo Yesu.
\s5
\v 16 Kila andiko limetiwa pumzi na Mungu. Linafaa kwa mafundisho yenye faida, kwa kushawishi, kwa kurekebisha makosa, na kwa kufundishia katika haki.
\v 17 Hii ni kwamba mtu wa Mungu awe kamili, akiwa amepewa nyenzo zote kwa ajili ya kutenda kila kazi njema.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ninakupa agizo hili lenye uzito mbele za Mungu na Kristo Yesu, atakaye wahukumu walio hai na wafu, na kwa sababu ya kufunuliwa kwake na Ufalme wake:
\v 2 Hubiri Neno. Uwe tayari kwa wakati ufaao na usiofaa. Waambie watu dhambi zao, kemea, himiza, kwa uvumilivu wote na mafundisho.
\s5
\v 3 Kwa maana wakati utakuja ambao watu hawatachukuliana na mafundisho ya kweli. Badala yake, watajitafutia walimu wa kufundisha kulingana na tamaa zao. kwa njia hii masikio yao yatakuwa yametekenywa.
\v 4 Wataacha kusikiliza mafundisho ya kweli, na kugeukia hadithi.
\v 5 Lakini wewe uwe mwaminifu katika mambo yote, vumilia magumu, fanya kazi ya mwinjilisti; timiza huduma yako.
\s5
\v 6 Kwa maana mimi tayari nimekwisha kumiminwa. Muda wa kuondoka kwangu umewadia.
\v 7 Nimeshindana katika haki, Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.
\v 8 Taji ya haki imewekwa kwa ajili yangu, ambayo Bwana, anayehukumu kwa haki, atanipa siku ile. Na siyo kwangu tu bali pia kwa wote wanaongojea kwa shauku kuonekana kwake.
\s5
\v 9 Jitahidi kuja kwagu haraka.
\v 10 Kwa kuwa Dema ameniacha. Anaupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia, na Tito alikwenda Dalmatia.
\s5
\v 11 Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko uje naye kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma.
\v 12 Nimemtuma Tikiko Efeso.
\v 13 Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi.
\s5
\v 14 Alekizanda mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake.
\v 15 Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu.
\v 16 Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia.
\s5
\v 17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba.
\v 18 Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amen
\s5
\v 19 Msalimie Priska, Akila na nyumba ya Onesiforo.
\v 20 Erasto alibaki huko Korintho, lakini Trifimo nilimuacha Mileto akiwa mgonjwa.
\v 21 Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote.
\v 22 Mungu awe pamoja na roho yako, Neema iwe nawe.

107
57-TIT.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,107 @@
\id TIT
\ide UTF-8
\h Tito
\toc1 Tito
\toc2 Tito
\toc3 tit
\mt Tito
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli iletayo utauwa.
\v 2 Wapo katika tumaini la uzima wa milele ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele.
\v 3 Kwa wakati muafaka, alilifunua neno lake katika ujumbe alionipa mimi kuhubiri. Ilinipasa kufanya hivi kwa amri ya Mungu mwokozi wetu.
\s5
\v 4 Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani yetu. Neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu.
\v 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, kwamba uyatengeneze mambo yote yaliyokuwa hayajakamilika na kuweka wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza.
\s5
\v 6 Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasioshuhudiwa mabaya au wasio na nidhamu.
\v 7 Ni muhimu kwa mwangalizi, kama msimamizi wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu wa kelele au asiye jizuia. Lazima asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi, asiwe mtu wa kusababisha ugomvi, na asiwe mwenye tamaa.
\s5
\v 8 Badala yake: awe mtu mkaribishaji, apendaye wema. Lazima awe mtu mwenye akili timamu, mwenye haki, mcha Mungu, anayejitawala mwenyewe.
\v 9 Awezaye kusimamia mafundisho ya kweli yaliyofundishwa, ili aweze kuwatia moyo kwa mafundisho mazuri na awezaye kuwarekebisha wote wanaompinga.
\s5
\v 10 Kwa kuwa kuna waasi wengi, hasa wale wa tohara. Maneno yao ni ya upuuzi. Wanadanganya na kuwaongoza watu katika upotovu.
\v 11 Ni lazima kuwazuia watu kama hao. Wanafundisha yale wasiyopaswa kwa faida za aibu na kuharibu familia zote.
\s5
\v 12 Mmoja wao, mtu mwenye busara, alisema, "Wakrete wana uongo usio na mwisho, wabaya na wanyama wa hatari, wavivu na walafi."
\v 13 Haya maelezo ni ya kweli, kwa hiyo uwazuie kwa nguvu ili kwamba waweze kusema kweli katika imani.
\s5
\v 14 Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli.
\s5
\v 15 Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Lakini kwa wote walio wachafu na wasioamini, hakuna kilicho kisafi. Kwa kuwa mawazo yao na dhamira zao zimechafuliwa.
\v 16 Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni waovu na wasiotii. Hawakuthibitishwa kwa tendo lolote jema.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Lakini wewe yaseme yale yanayoendana na maelekezo ya kuaminika.
\v 2 Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu.
\s5
\v 3 Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe.
\v 4 Wanapaswa kufundisha yaliyo mazuri ili kuwaandaa wasichana kwa busara kuwapenda waume zao na watoto wao.
\v 5 Wanapaswa kuwafundisha kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na watii kwa waume zao wenyewe. Inawalazimu kufanya mambo haya ili kwamba neno la Mungu lisitukanwe.
\s5
\v 6 katika namna iyo hiyo, watieni moyo vijana wa kiume wawe na busara.
\v 7 Katika njia zote jiwekeni wenyewe kuwa mfano katika kazi nzuri; na mfundishapo, onesheni uadilifu na heshima.
\v 8 Ongeeni ujumbe wenye afya na usio na dosari, ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe kwa sababu hana baya la kusema juu yetu.
\s5
\v 9 Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu. Wanapaswa kuwafurahisha na sio kubishana nao.
\v 10 Hawapaswi kuiba. Badala yake, wanapaswa kuonesha imani yote nzuri ili kwamba katika njia zote wayapambe mafundisho yetu kumhusu Mungu mwokozi wetu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa watu wote.
\v 12 Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia. Inatufundisha kuishi kwa busara, kwa haki, na katika njia za kimungu kwa wakati huu.
\v 13 Wakati tunatarajia kupokea tumaini letu lenye baraka, mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
\s5
\v 14 Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili kutukomboa kutoka katika uasi na kutufanya wasafi, kwa ajili yake, watu maalumu walio na hamu ya kufanya kazi nzuri.
\s5
\v 15 Yaseme na kuyasisitiza mambo haya. Kemea kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Uwakumbushe kuwanyenyekea viongozi na mamlaka, kuwatii na kuwa tayari katika kila kazi njema.
\v 2 Wakumbushe kutokumtendea mtu yeyote ubaya, waepuke majibizano, wawape nafasi watu wengine katika kufanya maamuzi, na kuonesha unyenyekevu kwa watu wote.
\s5
\v 3 Kwa kuwa sisi pia tulikuwa na mawazo potofu na wakaidi. Tulikuwa upotevuni na tulifanywa watumwa kwa tamaa nyingi na starehe. Tuliishi katika wivu na uovu. Tulichukiza na kuchukiana.
\s5
\v 4 Lakini wakati huruma ya Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana,
\v 5 haikuwa kwa matendo yetu ya haki tuliyofanya, bali alituokoa kwa neema yake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na katika kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu.
\s5
\v 6 Mungu alimwaga Roho Mtakatifu kwa wingi juu yetu kupitia Yesu Kristo mwokozi wetu.
\v 7 Alifanya hivi ili kwamba, tukiwa tumehesabiwa haki kwa neema yake, tuwe washirika katika uhakika wa maisha ya milele.
\s5
\v 8 Huu ni ujumbe wa kuaminika. Ninawataka myanene kwa ujasiri mambo haya, ili kwamba wale wanaomwamini Mungu wawe na dhamira juu ya kazi nzuri ambayo aliiweka mbele yao. Mambo haya ni mazuri na yanafaida kwa ajili ya watu wote.
\s5
\v 9 Lakini jiepusheni na mijadala ya kipumbavu, nasaba, mashindano, na migongano kuhusu sheria. Mambo hayo hayana maana wala faida.
\v 10 Mkataeni yeyote anayesababisha migawanyiko kati yenu. Baada ya onyo moja ama mawili,
\v 11 jueni kwamba mtu wa jinsi hiyo ameiacha njia iliyo sahihi na anatenda dhambi na kujihukumu mwenyewe.
\s5
\v 12 Nitakapomtuma kwako Artemi au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi.
\v 13 Harakisha na umtume Zena mtaalamu katika sheria, na Apolo, pasipo kupungukiwa na kitu.
\s5
\v 14 Watu wetu lazima wajifunze kujishughulisha katika kazi nzuri ambazo zinagusa mahitaji muhimu ili kwamba wasije wakawa wasiozaa matunda.
\s5
\v 15 Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu wale watupendao katika imani. Neema iwe nanyi nyote.

50
58-PHM.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,50 @@
\id PHM
\ide UTF-8
\h Filemoni
\toc1 Filemoni
\toc2 Filemoni
\toc3 phm
\mt Filemoni
\s5
\c 1
\p
\v 1 Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na ndugu Timotheo kwa Filemoni, mpendwa rafiki yetu na mtenda kazi pamoja nasi,
\v 2 na kwa Afia dada yetu, na kwa Arkipas askari mwenzetu, na kwa kanisa lile linalokutana nyumbani kwako.
\v 3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 4 Wakati wote namshukuru Mungu. Ninakutaja katika maombi yangu.
\v 5 Nimesikia upendo na imani uliyonayo katika Bwana Yesu na kwa ajili ya waumini wote.
\v 6 Ninaomba kwamba ushirika wa imani yenu iwe na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema lililoko kati yetu katika Kristo.
\v 7 Kwa kuwa nimekuwa na furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa sababu mioyo ya waumini imekuwa ikitulizwa nawe, ndugu.
\s5
\v 8 Kwa hiyo, ingawa nina ujasiri wote katika Kristo kukuamuru wewe kufanya kile unachoweza kufanya,
\v 9 lakini kwa sababu ya upendo, badala yake nakusihi - mimi, Paulo niliye mzee, na sasa ni mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu.
\s5
\v 10 Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesmo, niliyemzaa katika vifungo vyangu.
\v 11 Kwa kuwa mwanzoni hakukufaa, lakini sasa anakufaa wewe na mimi.
\v 12 Nimemtuma- yeye ambaye ni wa moyo wangu hasa - kurudi kwako.
\v 13 Nataraji angeendelea kubaki pamoja nami, ili anitumikie badala yako, wakati niwako kifungoni kwa ajili ya injili.
\s5
\v 14 Lakini sikutaka kufanya jambo lolote bila ruhusa yako. Nilifanya hivi ili kwamba jambo lolote zuri lisifanyike kwa sababu nilikulazimisha, bali kwa sababu ulipenda mwenyewe kulitenda.
\v 15 Labda ni sababu alitengwa nawe kwa muda, ilikuwa hivyo ili uwe pamoja naye milele.
\v 16 Ili kwamba asiwe tena mtumwa, bali bora zaidi ya mtumwa, kama ndugu mpendwa, hasa kwangu, na zaidi sana kwako, katika mwili na katika Bwana.
\s5
\v 17 Na hivyo kama wanichukulia mimi mshirika, mpokee kama ambavyo ungenipokea mimi.
\v 18 Lakini kama amekukosea jambo lolote, au unamdai kitu chochote, kidai hicho kutoka kwangu.
\v 19 Mimi Paulo, ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe: mimi nitakulipa. Sisemi kwako kwamba nakudai maisha yako hasa.
\v 20 Naam ndugu, acha nipate furaha ya Bwana toka kwako: uburudishe moyo wangu katika Kristo.
\s5
\v 21 Nikiwa na imani kuhusu utii wako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya vile ninavyokuomba.
\v 22 Wakati huo huo andaa chumba cha wageni kwa ajili yangu, kwa kuwa ninatumaini kupitia maombi yako nitakutembelea hivi karibuni.
\s5
\v 23 Epafra, mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu anakusalimu,
\v 24 na kama afanyavyo Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi pamoja nami.
\v 25 Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho yako. Amina.

580
59-HEB.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,580 @@
\id HEB
\ide UTF-8
\h Wahebrania
\toc1 Wahebrania
\toc2 Wahebrania
\toc3 heb
\mt Wahebrania
\s5
\c 1
\p
\v 1 Nyakati zilizopita Mungu alizungumza na mababu zetu kupitia manabii mara nyingi na kwa njia nyingi.
\v 2 Lakini katika siku hizi tulizonazo, Mungu ameongea nasi kupitia Mwana, ambaye alimweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia yeye pia aliumba ulimwengu.
\v 3 Mwanawe ni nuru ya utukufu wake, tabia pekee ya asili yake, na anayeendeleza vitu vyote kwa neno la nguvu zake. Baada ya kukamilisha utakaso wa dhambi, aliketi chini mkono wa kulia wa enzi huko juu.
\s5
\v 4 Amekuwa bora kuliko malaika, kama vile jina alilolirithi lilivyo bora zaidi kuliko jina lao.
\v 5 Kwa maana ni kwa malaika gani aliwahi kusema, "Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako?" Na tena, "Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana kwangu?"
\s5
\v 6 Tena, wakati Mungu alipomleta mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, husema, "Malaika wote wa Mungu lazima wamwabudu."
\v 7 Kuhusu malaika asema, "Yeye ambaye hufanya malaika zake kuwa roho, na watumishi wake kuwa ndimi za moto."
\s5
\v 8 Lakini kuhusu Mwana husema, "Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele. Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
\v 9 Umependa haki na kuchukia uvunjaji wa sheria, kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekupaka mafuta ya furaha kuliko wenzako."
\s5
\v 10 Hapo mwanzo, Bwana, uliweka msingi wa dunia. Mbingu ni kazi za mikono yako.
\v 11 Zitatoweka, lakini wewe utaendelea. Zote zitachakaa kama vazi.
\v 12 Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilika kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule, na miaka yako haitakoma."
\s5
\v 13 Lakini ni kwa malaika yupi Mungu alisema wakati wowote, "Keti mkono wangu wa kulia mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa kiti cha miguu yako"?
\v 14 Je, malaika wote siyo roho zilizotumwa kuwahudumia na kuwatunza wale watakaourithi wokovu?
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo ni lazima tuweke kipaumbele zaidi kwa yale tuliyosikia, ili kwamba tusije tukatengwa mbali nayo.
\s5
\v 2 Kwa maana ikiwa ujumbe uliozungumzwa na malaika ni halali, na kila kosa na uasi hupokea adhabu tu,
\v 3 tutapataje kuepuka kama tusipojali wokovu huu mkuu? —wokuvu ambao kwanza ulitangazwa na Bwana na kuthibitishwa kwetu na wale waliousikia.
\v 4 Mungu pia aliuthibitisha kwa ishara, maajabu, na kwa matendo makuu mbalimbali, na kwa zawadi za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake mwenyewe.
\s5
\v 5 Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika.
\v 6 Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, "Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze?
\s5
\v 7 mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. "Na umemuweka juu ya kazi ya mikono yako.)
\v 8 Umeweka kila kitu chini ya miguu yake." Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake.
\s5
\v 9 Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu.
\v 10 Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake.
\s5
\v 11 Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu.
\v 12 Anasema, "Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko."
\s5
\v 13 Tena asema, "Nitaamini katika yeye." Na tena, "Tazama, hapa nipo na watoto ambao Mungu amenipa."
\v 14 Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vilevile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni ibilisi.
\v 15 Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa.
\s5
\v 16 Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abraham.
\v 17 Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu.
\v 18 Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
\v 2 Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu.
\v 3 Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.
\v 4 Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.
\s5
\v 5 Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao.
\v 6 Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini.
\s5
\v 7 Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, "Leo, kama utasikia sauti yake,
\v 8 Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani.
\s5
\v 9 Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu.
\v 10 Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu.
\v 11 Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu."
\s5
\v 12 Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai.
\v 13 Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
\s5
\v 14 Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.
\v 15 Kuhusu hili imekwisha kusemwa, "Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi."
\s5
\v 16 Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri?
\v 17 Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani?
\v 18 Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye?
\v 19 Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, tunapaswa kuwa makini ili kwamba kati yenu asiwepo hata mmoja atakayeonekana kushindwa kufikia ahadi endelevu ya kuingia katika pumzika la Mungu.
\v 2 Kwani tumekuwa na habari njema kuhusu pumziko la Mungu lililotangazwa kwetu kama Waisrael walivyokuwa nayo, lakini ujumbe huo haukuwasaidia wale ambao waliusikia bila kuunganisha imani kwa hilo.
\s5
\v 3 Kwa sisi, ambao tumekwisha amini-sisi ndio miongoni tutakaoingia katika lile pumuziko, Kama inavyosema, "Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika pumziko mwangu." Alisema hili, ingawa kazi zote alizotengeneza zilikuwa zimekamilika tangu mwanzo wa ulimwengu.
\v 4 Kwani ameshasema sehemu fulani kuhusu siku ya saba, "Mungu alipumzika siku ya saba katika yote aliyoyafanya."
\v 5 Tena ameshasema, "Hawataingia kwenye pumziko langu."
\s5
\v 6 Kwa sababu hiyo, tangu pumziko la Mungu bado ni akiba kwa ajili ya baadhi kuingia, na tangu Waisraeli wengi ambao walisikia habari njema kuhusu pumziko lake hawakuingia kwa sababu ya kutotii,
\v 7 Mungu aliweka tena siku fulani, iitwayo "Leo." Yeye aliiongeza siku hii alipozungumza kupitia Daudi, ambaye alisema kwa muda mrefu baada ya yaliyosemwa kwanza, "Leo kama mtasikia sauti yake, msifanye mioyo yenu kuwa migumu."
\s5
\v 8 Kwani kama Yoshua aliwapatia pumziko, Mungu asingelisema juu ya siku nyingine.
\v 9 Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu.
\v 10 Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye.
\v 11 Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya.
\s5
\v 12 Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na linaukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho. Na lenye kuweza kufahamu fikira za moyo nia yake.
\v 13 . Hakuna kilichoumbwa kilichojificha katika uso wa Mungu. Badala yake, kila kitu ni dhahiri na wazi kwa macho ya mmoja ambaye ni lazima tutoe hesabu.
\s5
\v 14 Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu.
\v 15 Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi.
\v 16 Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kwani kila kuhani mkuu, aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa watu, amechaguliwa kusimama badala yao katika vitu vinavyohusiana na Mungu, ili aweze kutoa kwa pamoja zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
\v 2 Anaweza kujishughulisha kwa upole na wajinga na wabishi kwa kuwa yeye mwenyewe pia amezungukwa na udhaifu.
\v 3 Kwa sababu ya hili, ana wajibu wa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake kama afanyavyo kwa dhambi za watu.
\s5
\v 4 Na hakuna mtu achukuaye heshima hii kwa ajili yake mwenyewe, lakini badala yake, lazima aitwe na Mungu, kama alivyokuwa Haruni.
\v 5 Hata Kristo hakujipa heshimu mwenyewe kwa kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Badala yake, Mungu alisema kwake, " Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako."
\s5
\v 6 Ni kama asemavyo pia sehemu nyingine, " Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki."
\s5
\v 7 Wakati wa kipindi chake katika mwili, aliomba na kuombea, alimwomba Mungu kwa machozi, kwa yeye awezaye kumwokoa kutoka kwenye kifo. Kwa sababu ya unyenyekevu wake kwa Mungu, alisikiwa.
\v 8 Ijapokuwa alikua mwana, alijifunza kutii kwa mambo yaliyomtesa.
\s5
\v 9 Alikamilishwa na kwa njia hii alifanyika kwa kila mtu amwaminiye kuwa sababu ya wokovu wa milele,
\v 10 kwa kutengwa na Mungu kama kuhani Mkuu baada ya zamu ya Melkizedeki.
\v 11 Tuna mengi ya kusema kuhusu Yesu, lakini ni vigumu kuwaelezea kwa kuwa ninyi ni wavivu wa kusikia.
\s5
\v 12 Ijapokuwa kwa kipindi hiki mlipaswa kuwa walimu, bado kuna umuhimu wa mtu kuwafundisha mafundisho ya awali ya kanuni za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa na si chakula kigumu.
\v 13 Kwa kuwa yeyote anywaye maziwa tu hana uzoefu katika ujumbe wa haki, kwa kuwa bado ni mtoto.
\v 14 Kwa upande mwingine, chakula kigumu ni cha watu wazima, wale ambao kwa sababu ya uzoefu wao katika kutofautisha haki na ubaya wamefundishwa kutambua jema na ovu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kwa hiyo, tukiacha tulichojifunza kwanza kuhusu ujumbe wa Kristo, twapaswa kuwa na juhudi kuelekea kwenye ukomavu, tusiweke tena misingi ya toba kutoka katika kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu,
\v 2 wala misingi ya mafundisho ya ubatizo, na kuwawekea mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele.
\v 3 Na tutafanya hivi ikiwa Mungu ataruhusu.
\s5
\v 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa wale ambao waliipata nuru awali, ambao walionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu,
\v 5 na ambao walionja uzuri wa neno la Mungu na kwa nguvu za wakati ujao,
\v 6 na kisha wakaanguka - haiwezekani kuwarejesha tena katika toba. Hii ni kwa sababu wamemsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, wakimfanya kuwa chombo cha dhihaka hadharani.
\s5
\v 7 Kwa kuwa ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake, na ikatoa mazao muhimu kwa hao waliofanya kazi katika ardhi, hupokea baraka kutoka kwa Mungu.
\v 8 Lakini ikiwa huzaa miiba na magugu, haina tena thamani na ipo katika hatari ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuteketezwa.
\s5
\v 9 Ijapokuwa tunazungumza hivi, rafiki wapenzi, tunashawishiwa na mambo mazuri yawahusuyo ninyi na mambo yahusuyo wokovu.
\v 10 Kwa kuwa Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na kwa upendo mliouonesha kwa ajili ya jina lake, katika hili mliwatumikia waamini na bado mngali mnawatumikia.
\s5
\v 11 Na tunatamani sana kwamba kila mmoja wenu aweze kuonesha bidii ile ile mpaka mwisho kwa uhakika wa ujasiri.
\v 12 Hatutaki muwe wavivu, lakini muwe wafuasi wa wale warithio ahadi kwa sababu ya imani na uvumilivu.
\s5
\v 13 Kwa maana Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa nafsi yake, kwa kuwa asingeliapa kwa mwingine yeyote aliye mkubwa kuliko yeye.
\v 14 Alisema, "Hakika nitakubariki, na nitauongeza uzao wako zaidi."
\v 15 Kwa njia hii, Abrahamu alipokea kile alichoahidiwa baada ya kusubiria kwa uvumilivu.
\s5
\v 16 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, na kwao ukomo wa mashindano yote ni kiapo kwa kuyathibitisha.
\v 17 Wakati Mungu alipoamua kuonesha kwa uwazi zaidi kwa warithi wa ahadi kusudi lake zuri lisilobadilika, alilithibitisha kwa kiapo.
\v 18 Alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tulioikimbilia hifadhi tupate kutiwa moyo kushikilia kwa nguvu tumaini lililowekwa mbele yetu.
\s5
\v 19 Tunao ujasiri huu kama nanga imara na ya kutegemea ya roho zetu, ujasiri ambao unaingia sehemu ya ndani nyuma ya pazia.
\v 20 Yesu aliingia sehemu ile kama mtangulizi wetu, akisha kufanyika kuhani mkuu hata milele baada ya utaratibu wa Melkizedeki.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki.
\v 2 Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake "Melkizedeki " maana yake" mfalme wa haki" na pia "mflame wa Salemu" ambayo ni "mfalme wa amani."
\v 3 Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu.
\s5
\v 4 Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani.
\v 5 Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Wairaeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu.
\v 6 Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi.
\s5
\v 7 Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa.
\v 8 Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi.
\v 9 Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alilipa moja ya kumi kwa Abrahamu,
\v 10 kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu.
\s5
\v 11 Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni?
\v 12 Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika.
\s5
\v 13 Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni.
\v 14 Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani.
\s5
\v 15 Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki.
\v 16 Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika.
\v 17 Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: "Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki."
\s5
\v 18 Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai.
\v 19 Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu.
\s5
\v 20 Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote.
\v 21 Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, "Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele."
\s5
\v 22 Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora.
\v 23 Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine.
\v 24 Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki.
\s5
\v 25 Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.
\v 26 Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.
\s5
\v 27 Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe.
\v 28 Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Sasa jambo ambalo tunasema ni hili: tunaye kuhani mkuu aliyekaa chini katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi Mbinguni.
\v 2 Yeye ni mtumishi katika mahali patakatifu, hema la kweli ambalo Bwana ameliweka, siyo mtu yeyote wa kufa.
\s5
\v 3 Kwa maana kila kuhani mkuu huwekwa kutoa zawadi na dhabihu; kwa hiyo ni muhimu kuwa na kitu cha kutoa.
\v 4 Sasa kama Kristo alikuwa juu ya nchi, yeye asingekuwa kuhani zaidi ya hapo. Kwa kuwa walikuwa tayari wale waliotoa vipawa kulingana na sheria.
\v 5 Walihudumu kitu ambacho kilikuwa nakala na kivuli cha vitu vya mbinguni, sawa kama Musa alipoonywa na Mungu wakati alipotaka kujenga hema. "Ona," Mungu akasema, "kwamba tengeneza kila kitu kulingana na muundo ulioonyeshwa juu ya mlima".
\s5
\v 6 Lakini sasa Kristo amepokea huduma bora zaidi kwa sababu yeye pia ni mpatanishi wa agano zuri, ambalo limekwisha kuimarishwa kwa ahadi nzuri.
\v 7 Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili.
\s5
\v 8 Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, "Tazama, siku zinakuja, 'asema Bwana, 'wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
\v 9 Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,' asema Bwana.
\s5
\v 10 Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,' asema Bwana. 'nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
\s5
\v 11 Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, "Mjue Bwana," hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao.
\v 12 Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena."
\s5
\v 13 Kwa kusema "Mpya," amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Sasa hata agano la kwanza lilikuwa na sehemu ya ibada hapa duniani na taratibu za ibada.
\v 2 Kwani katika hema kulikuwa na chumba kimeandaliwa, chumba cha nje, paliitwa mahali patakatifu. Katika eneo hili palikuwa na kinara cha taa, meza na mikate ya wonyesho.
\s5
\v 3 Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi.
\v 4 Mlikuwemo madhabahu ya dhahabu kwa kuvukizia uvumba. Pia mlikuwemo sanduku la agano, ambalo lilikuwa limejengwa kwa dhahabu tupu. Ndani yake kulikuwa na bakuli la dhahabu lenye manna, fimbo ya Haruni iliyoota majani, na zile mbao za mawe za agano.
\v 5 Juu ya sanduku la agano maumbo ya maserafi wa utukufu wafunika mabawa yao mbele ya kiti cha upatanisho, ambacho kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa kina.
\s5
\v 6 Baada ya vitu hivi kuwa vimekwisha andaliwa, Makuhani kawaida huingia chumba cha nje cha hema kutoa huduma zao.
\v 7 Lakini kuhani mkuu huingia kile chumba cha pili pekee mara moja kila mwaka, na pasipo kuacha kutoa dhabihu kwa ajili yake binafsi, na kwa dhambi za watu walizozitenda pasipo kukusudia.
\s5
\v 8 Roho Mtakatifu anashuhudia kwamba, njia ya mahali patakatifu zaidi bado haijafunuliwa kwa vile ile hema la kwanza bado linasimama.
\v 9 Hili ni kielelezo cha muda huu wa sasa. Vyote zawadi na dhabihu ambavyo vinatolewa sasa haviwezi kukamilisha dhamiri ya anayeabudu.
\v 10 Ni vyakula na vinywaji pekee vimeunganishwa katika namna ya taratibu za ibada ya kujiosha. Vyote hivi vilikuwa taratibu za kimwili vilivyokuwa vimeandaliwa hadi ije amri mpya itakayowekwa mahali pake.
\s5
\v 11 Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa.
\v 12 Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele.
\s5
\v 13 Kama kwa damu ya mbuzi na mafahari na kunyunyiziwa kwa majivu ya ndama katika hao wasiosafi walitengwa kwa Mungu na kufanya miili yao safi,
\v 14 Je si zaidi sana damu ya Kristo ambaye kupitia Roho wa milele alijitoa mwenyewe bila mawaa kwa Mungu, kuosha dhamiri zetu kutoka matendo mafu kumtumikia Mungu aliye hai?
\v 15 Kwa sababu hiyo, Kristo ni mjumbe wa agano jipya. Hii ndiyo sababu mauti imewaacha huru wote walio wa agano la kwanza kutoka katika hatia ya dhambi zao, ili kwamba wote walioitwa na Mungu waweze kupokea ahadi ya urithi wao wa milele.
\s5
\v 16 Kama kuna agano linadumu, ni lazima kuthibitishwa kwa kifo cha mtu yule aliyelifanya.
\v 17 Kwani agano linakuwa na nguvu mahali kunatokea mauti, kwa sababu hakuna nguvu wakati mwenye kulifanya akiwa anaishi.
\s5
\v 18 Hivyo hata si lile agano la kwanza lilikuwa limewekwa pasipo damu.
\v 19 Wakati Musa alipokuwa ametoa kila agizo la sheria kwa watu wote, alichukua damu ya ng'ombe na mbuzi, pamoja na maji, kitambaa chekundu, na hisopo, na kuwanyunyizia gombo lenyewe na watu wote.
\v 20 Kisha alisema, "Hii ni damu ya agano ambayo Mungu amewapa amri kwenu".
\s5
\v 21 Katika hali ileile, aliinyunyiza damu juu ya hema na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa huduma ya ukuhani.
\v 22 Na kulingana na sheria, karibu kila kitu kinatakaswa kwa damu. Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha.
\s5
\v 23 Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba nakala za vitu vya mbinguni sharti visafishwe kwa hii dhabihu ya wanyama. Hata hivyo, vitu vya mbinguni vyenyewe vilipaswa kusafishwa kwa dhabihu iliyo bora zaidi.
\v 24 Kwani Kristo hakuingia mahali patakatifu sana palipofanywa na mikono, ambayo ni nakala ya kitu halisi. Badala yake aliingia mbingu yenyewe, mahali ambapo sasa yuko mbele za uso wa Mungu kwa ajili yetu.
\s5
\v 25 Hakuingia kule kwa ajili ya kujitoa sadaka kwa ajili yake mara kwa mara, kama afanyavyo kuhani mkuu, ambaye huingia mahali patakatifu zaidi mwaka baada ya mwaka pamoja na damu ya mwingine,
\v 26 kama hiyo ilikuwa kweli, basi ingekuwa lazima kwake kuteswa mara nyingi zaidi tangu mwanzo wa ulimwengu. Lakini sasa ni mara moja hadi mwisho wa miaka aliyojifunua kuiondoa dhambi kwa dhabihu yake mwenyewe.
\s5
\v 27 Kama ilivyo kwa kila mtu kufa mara moja, na baada ya hiyo huja hukumu,
\v 28 ndivyo hivyo Kristo naye ambaye alitolewa mara moja kuziondoa dhambi za wengi, atatokea mara ya pili, si kwa kusudi la kushughulikia dhambi, bali kwa ukombozi kwa wale wamgojeao kwa saburi.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka.
\v 2 Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi.
\v 3 Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka.
\v 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi.
\s5
\v 5 Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, "Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu.
\v 6 Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi.
\v 7 Kisha nilisema, "Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo".
\s5
\v 8 Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: "Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake" dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria.
\v 9 Kisha alisema, "Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako". Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili.
\v 10 Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.
\s5
\v 11 Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi.
\v 12 Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu,
\v 13 akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake.
\v 14 Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu.
\s5
\v 15 Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema,
\v 16 "Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao".
\s5
\v 17 Kisha alisema, "Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu".
\v 18 Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
\s5
\v 19 Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.
\v 20 Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia.
\v 21 Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu,
\v 22 na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.
\s5
\v 23 Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
\v 24 Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.
\v 25 Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.
\s5
\v 26 Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.
\v 27 Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.
\s5
\v 28 Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
\v 29 kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema?
\s5
\v 30 Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, "Kisasi ni changu, nitalipa". Na tena, "Bwana atawahukumu watu wake".
\v 31 Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai!
\s5
\v 32 Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali.
\v 33 Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo.
\v 34 Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.
\s5
\v 35 Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu.
\v 36 Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake.
\v 37 Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia.
\s5
\v 38 Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye."
\v 39 Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana.
\v 2 Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao.
\v 3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana.
\s5
\v 4 Ilikuwa kwa sababu ya imani kwamba Habili alimtolea Mungu sadaka ya kufaa kuliko alivyofanya Kaini. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisifiwa kuwa mwenye haki. Mungu alimsifu kwa sababu ya zawadi alizoleta. Kwa sababu hiyo, Habili bado ananena, ingawa amekufa.
\s5
\v 5 Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. "Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua" kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu.
\v 6 Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao.
\s5
\v 7 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Nuhu, akiwa ameonywa na Mungu kuhusiana na mambo ambayo hayakuwa yameonekana, kwa heshima ya ki Mungu alitengeneza safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Kwa kufanya hivi, aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ambayo huja kupitia imani.
\s5
\v 8 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, alipoitwa alitii na kwenda mahali ambapo alipaswa kupokea kama urithi. Alitoka bila kujua mahali gani alikuwa anakwenda.
\v 9 Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishi katika nchi ya ahadi kama mgeni. Aliishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi wenzake wa ahadi ile ile.
\v 10 Hii ni kwa sababu alitarajia kuupata mji ambao mwenye kuubuni na mjenzi wake angelikuwa ni Mungu.
\s5
\v 11 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, na Sara mwenyewe, walipokea nguvu ya kutunga mimba ingawa walikuwa wazee sana, kwa kuwa walimuona Mungu kuwa mwaminifu, ambaye aliwaahidia mtoto wa kiume.
\v 12 Kwa hiyo pia kutoka kwa mtu huyu mmoja ambaye alikuwa amekaribia kufa wakazaliwa watoto wasiohesabika. Walikuwa wengi kama nyota za angani na wengi kama mbegu za mchanga katika ufukwe wa bahari.
\s5
\v 13 Hawa wote walikufa katika imani pasipo kupokea ahadi. Isipokuwa, wakiwa wameziona na kuzikaribisha kwa mbali, walikiri kwamba walikuwa wageni na wapitaji juu ya nchi.
\v 14 Kwa wale wasemao mambo kama haya wanaweka bayana kuwa wanatafuta nchi yao wenyewe.
\s5
\v 15 Kwa kweli, kama wangekuwa wakiifikiria nchi ambayo kwayo walitoka, wangelikuwa na nafasi ya kurejea.
\v 16 Lakini kama ilivyo, wanatamani nchi iliyo bora, ambayo, ni ya kimbingu. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa ametayarisha mji kwa ajili yao.
\s5
\v 17 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu baada ya kujaribiwa, alimtoa Isaka. Ndiyo, yeye ambaye alipokea kwa furaha ahadi, alimtoa mwanawe wa pekee,
\v 18 ambaye juu yake ilinenwa, "Kutoka kwa Isaka uzao wako utaitwa."
\v 19 IbrahImU alijua kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua Isaka kutoka katika wafu, na kwa kuzungumza kwa lugha ya maumbo, alimpokea.
\s5
\v 20 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Isaka alimbariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yajayo.
\v 21 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yakobo alipokuwa katika hali ya kufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yusufu. Yakobo akaabudu, akiegemea juu ya fimbo yake.
\v 22 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yusufu wakati wake wa mwisho ulipokaribia, alinena juu ya kutoka kwa wana wa Israel Misri na akawaagiza kuchukua pamoja nao mifupa yake.
\s5
\v 23 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipozaliwa, alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake kwa sababu walimuona kuwa ni mtoto mchanga aliyekuwa mzuri, na hawakutishwa na amri ya mfalme.
\v 24 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mtoto wa binti Farao.
\v 25 Badala yake, alichagua kushiriki mateso pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia anasa za dhambi kwa kitambo.
\v 26 Alifikiri aibu ya kumfuata Kristo kuwa ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri kwa kuwa alikaza macho yake katika zawadi ya wakati wake ujao.
\s5
\v 27 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa alitoka Misri. Hakuhofia hasira ya Mfalme, kwa kuwa alivumilia kwa kutazama kwa asiyeonekana.
\v 28 Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishika pasaka na kunyunyiza damu, ili kwamba mharibu wa mzaliwa wa kwanza asiweze kuwagusa wazaliwa wa kwanza wa kiume wa waisrael.
\s5
\v 29 Ilikuwa ni kwa imani kwamba walipita katika bahari ya shamu kama katika nchi kavu. Wakati wamisri walipojaribu kupita, walimezwa.
\v 30 Ilikuwa ni kwa imani kwamba ukuta wa Yeriko ulianguka chini, baada ya kuuzunguka kwa siku saba.
\v 31 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Rahabu yule kahaba hakuangamia pamoja na wale ambao hawakuwa watiifu, kwa sababu alikuwa amewapokea wapelelezi na kuwahifadhi salama.
\s5
\v 32 Na niseme nini zaidi? Maana muda hautoshi kusimulia ya Gideoni, Barak, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samwel na za manabii,
\v 33 ambao kupitia imani walizishinda falme, walitenda haki, na wakapokea ahadi. Walizuia vinywa vya simba,
\v 34 walizima nguvu za moto, walikwepa ncha ya upanga, waliponywa kutoka katika magonjwa, walikuwa mashujaa vitani, na walisababisha majeshi wageni kukimbia.
\s5
\v 35 Wanawake walipokea wafu wao kwa njia ya ufufuo. Wengine waliteswa, bila kukubali kuachwa huru ili kwamba waweze kupata uzoefu wa ufufuo ulio bora zaidi.
\v 36 Wengine waliteswa kwa dhihaka na kwa vichapo, naam, hata kwa vifungo na kwa kutiwa gerezani.
\v 37 Walipondwa mawe. Walikatwa vipande kwa misumeno. Waliuawa kwa upanga. Walikwenda kwa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi walikuwa wahitaji, wakiendelea katika maumivu na wakitendewa mabaya
\v 38 (ambayo ulimwengu haukustahili kuwa nao), wakitangatanga nyikani, milimani, katika mapango na katika mashimo ya ardhini.
\s5
\v 39 Ingawa watu wote hawa walikubaliwa na Mungu kwa sababu ya imani yao, hawakupokea alichoahidi.
\v 40 Mungu alitangulia kutupatia kitu kilichobora, ili kwamba bila sisi wasingeweza kukamilishwa.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kwahiyo, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa la mashaidi, na tutupe kila kitu kinacho tulemea pamoja na dhambi ambayo inatuzingira kwa urahisi. Tupige mbio kwa saburi katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu.
\v 2 Tuyaelekeze macho yetu kwa Yesu, aliye mwanzilishi na mwenye kutimiliza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahmili msalaba, akiidharau aibu yake, na akakaa chini mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
\v 3 Maana mtafakarini yeye aliye stahimili maneno ya chuki kutoka kwa wenye dhambi, dhidi yake mwenyewe ili kwamba msije mkachoka au kuzimia mioyo yenu.
\s5
\v 4 Hamjataabika au kuteseka mkishindana na dhambi kiasi cha kuishiwa damu.
\v 5 Tena mmesahau kule kutiwa moyo ambako kunawaelekeza kama watoto wa kiume: "Mwanangu, usiyachukuwe kwa wepesi marudia ya Bwana, wala usikate tamaa unapo rekebishwa na yeye."
\v 6 Kwa kuwa Bwana humrudi yeyote ambaye anampenda, na humwadhibu kila mwana ambaye humpokea.
\s5
\v 7 Stahimili majaribu kama kurudiwa. Mungu hushughulika nanyi kama anavyoshughulika na watoto, maana ni mtoto yupi ambaye baba yake hawezi kumrudi?
\v 8 Lakini kama hakuna kurudiwa, ambako sisi sote tunashiriki, basi ninyi ni haramu na si watoto wake.
\s5
\v 9 Zaidi ya yote, tulikuwa na baba zetu kidunia wa kuturudi, na tuliwaheshimu. Je haitupasi hata zaidi kumtii Baba wa kiroho na kuishi?
\v 10 Kwa hakika baba zetu walituadhibu kwa miaka michache kama ilivyoonekana sawa kwao, lakini Mungu hutuadhibu kwa faida yetu ili tushiriki utakatifu wake.
\v 11 Hakuna adhabu inayofurahisha kwa wakati huo. Huwa na maumivu. Hata hivyo, baadaye huzaa tunda la amani ya utauwa kwa wale waliofundishwa nayo.
\s5
\v 12 Kwa hiyo inueni mikono yenu iliyolegea na kufanya magoti yenu yaliyo dhaifu kuwa yenye nguvu tena;
\v 13 nyosheni mapito ya nyayo zenu, ili kwamba yeyote aliye mlemavu hataongozwa upotevuni lakini apate kuponywa.
\s5
\v 14 Tafuteni amani na watu wote, na pia utakatifu ambao bila huo hakuna atakayemwona Bwana.
\v 15 Muwe waangalifu ili kwamba asiwepo atakayetengwa mbali na neema ya Mungu, na kwamba lisije shina la uchungu litakalochipuka na kusababisha shida na kukengeusha wengi.
\v 16 Angalieni kuwa hakuna zinaa au mtu asiye mtauwa kama vile Esau, ambaye kwa sababu ya mlo mmoja aliuza haki yake ya kuzaliwa.
\v 17 Kwa kuwa mnajua kwamba baadaye, alipotamani kurithi baraka, alikataliwa, kwa sababu hakupata fursa ya kutubu pamoja na baba yake, hata ingawa alitafuta sana kwa machozi.
\s5
\v 18 Kwa kuwa hamkuja katika mlima ambao unaweza kuguswa, Mlima unaowaka moto, giza, kukatisha tamaa na dhoruba.
\v 19 Hamkuja kwa sauti za tarumbeta, au kwa maneno yatokanayo na sauti ambayo ilisababisha kila wasikiao wasiombe neno lolote kusemwa kwao.
\v 20 Kwa kuwa hawakuweza kuvumilia kile kilichoamuliwa: "Ikiwa hata mnyama agusaye mlima, lazima apigwe kwa mawe."
\v 21 Ya kutisha zaidi aliyoyaona Musa alisema, "Nimeogopa sana kiasi cha kutetemeka".
\s5
\v 22 Badala yake, mmekuja mlima Sayuni na katika mji wa Mungu aliye hai, Yerualem ya mbinguni, na kwa malaika elfu kumi wanaosherehekea.
\v 23 Mmekuja katika kusanyiko la wazaliwa wa kwanza wote waliosajiliwa mbinguni, kwa Mungu hakimu wa wote, na kwa roho za watakatifu ambao wamekamilishwa.
\v 24 Mmekuja kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa ambayo hunena mema zaidi kuliko damu ya Habili.
\s5
\v 25 Angalia kuwa usije ukamkataa mmoja ambaye anenaye. Kwa kuwa kama hawakuepuka walipomkataa mmoja aliye waonya duniani, kwa hakika hatutaepuka ikiwa tutageuka mbali kutoka kwa yule atuonyaye kutoka mbinguni.
\v 26 Kwa wakati huo sauti yake ilitikisa dunia. Lakini sasa ameahidi na kunena, "Bado mara nyingine tena sitatikisa dunia pekee, bali mbingu pia."
\s5
\v 27 Maneno haya, "Mara moja tena," inaonesha kutoweshwa kwa vitu vile vitetemeshwavyo, hivi ni, vitu vile ambavyo vimeumbwa, ili kwamba vile vitu visivyotetemeshwa vibakie.
\v 28 Kwa hiyo, tupokee ufalme ambao hautetemeshwi, tufurahi katika hali ya kumwabudu Mungu kwa kukubali pamoja na kunyenyekea katika kicho,
\v 29 kwa maana Mungu wetu ni moto ulao.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Basi upendo wa ndugu na uendelee.
\v 2 Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
\s5
\v 3 Kumbuka wote waliomo gerezani, kana kwamba mulikuwa nao kule pamoja nao, na kama miili yenu ilitendewa kama wao.
\v 4 Basi ndoa na iheshimiwe na wote na basi kitanda cha ndoa kifanywe kuwa safi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
\s5
\v 5 Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, "Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi."
\v 6 Basi tulidhikeni ili tusema kwa ujasiri, "Bawa ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?"
\s5
\v 7 Wafikirieni wale walio waongoza, wale waliongea neno la Mungu kwenu, na kumbukeni matokeo ya mienendo yao; igeni imani zao.
\v 8 Yesu Kristo ni yeye jana, leo, na ata milele.
\s5
\v 9 Usije ukaongozwa na mafundisho mbalimbali ya kigeni kwani ni vizuri kwamba moyo ujengwe kwa neema, na siyo kwa sheria kuhusu chakula hayo hayatawasaidia wale wanaoishi kwa hayo.
\v 10 Tunayo madhabau ambayo wale wanaotumika ndani ya hekalu hawana haki ya kula.
\v 11 Kwa kuwa damu za wanyama, zilizotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi, ililetwa na kuhani mkuu ndani ya sehemu takatifu, lakini miili yao ilichomwa nje ya kambi.
\s5
\v 12 Kwa hiyo Yesu naye aliteseka nje ya lango la mji, hili kwamba kuweka wakfu watu kwa Mungu kupitia damu yake.
\v 13 Na kwa hiyo twendeni kwake nje ya kambi, tukizibeba fadheha zake.
\v 14 Kwani hatuna makao ya kudumu katika mji huu. Badala yake tutafute mji ambao unakuja.
\s5
\v 15 Kupitia Yesu mnapaswa mara kwa mara kujitoa sadaka ya kumtukuza Mungu, kumsifu kwamba tunda la midomo yetu likili jina lake.
\v 16 Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni kwa sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana.
\v 17 Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia.
\s5
\v 18 Tuombeni, kwani tuna uhakikwa kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote.
\v 19 Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni.
\s5
\v 20 Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele,
\v 21 Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina.
\s5
\v 22 Sasa ninakutia moyo, ndugu, kuchukualiana na neno la kutia moyo ambalo kwa ufupi nililiandika kwenu.
\v 23 Fahamu kwamba ndugu yetu Timotheo ameshaachiwa huru, ambaye pamoja naye nitawaona kama atakuja hivi karibuni.
\s5
\v 24 Salimia viongozi wako wote na waumini wote. Wale wanaotoka Italia wanakusalimia.
\v 25 Na neema iwe nanyi nyote.

209
60-JAS.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,209 @@
\id JAS
\ide UTF-8
\h Waraka wa Yakobo
\toc1 Waraka wa Yakobo
\toc2 Waraka wa Yakobo
\toc3 jas
\mt Waraka wa Yakobo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mbili yaliyotawanyika, salaam.
\v 2 Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali,
\v 3 mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu.
\s5
\v 4 Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
\v 5 Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
\s5
\v 6 Lakini omba kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katika bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko.
\v 7 Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana;
\v 8 mtu huyu ana nia mbili, si imara katika njia zake zote.
\s5
\v 9 Ndugu maskini anapaswa kujivuna katika kusimama kwake juu,
\v 10 wakati huo huo ndugu tajiri katika unyenyekevu wake, kwa sababu atatoweka kama ua la kondeni katika shamba analopita.
\v 11 Jua huchomoza na joto la kuunguza kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hufa. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao.
\s5
\v 12 Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.
\v 13 Mtu yeyote hapaswi kusema anapojaribiwa, "Jaribu hili linatoka kwa Mungu," kwa sababu Mungu hajaribiwi na uovu, na Mungu mwenyewe hamjaribu yeyote.
\s5
\v 14 Kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mbaya zinazomshawishi na kumvuta mbali.
\v 15 Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.
\v 16 Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.
\s5
\v 17 Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo.
\v 18 Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
\s5
\v 19 Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,
\v 20 kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.
\v 21 Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu.
\s5
\v 22 Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe.
\v 23 Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo.
\v 24 Hujitathimini uso wake, na huenda zake na baada ya muda mfupi husahau anavyofanana.
\v 25 Bali mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili, sheria ya uhuru, na kuendelea kuitii, si kwa sababu yeye ni msikilizaji anayesahau, huyu mtu atabarikiwa anapoitenda.
\s5
\v 26 Ikiwa mtu yeyote atafikiri mwenyewe kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, huudanganya moyo wake na dini yake ni bure.
\v 27 Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ndugu zangu msiifuate imani ya Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, kwa kupendelea watu fulani.
\v 2 Kama mtu fulani akiingia kwenye mikutano yenu amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia masikini mwenye mavazi machafu,
\v 3 na mkaonyesha kumjali zaidi yule mwenye mavazi mazuri na kusema, "Tafadhari wewe keti hapa mahali pazuri" lakini mkamwambia yule masikini, "Wewe simama pale," au "Kaa chini ya miguu yangu."
\v 4 Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya?
\s5
\v 5 Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa, je, Mungu hakuwachagua masikini wa dunia kuwa matajiri katika imani na kurithi ufalme aliowaahidia wampendao?
\v 6 Lakini mmewadharau masikini! Je, sio matajiri wanaowatesa ninyi, na sio wao wanaowaburuta mahakamani?
\v 7 Je, si matajiri wanaolitukana jina lile zuri ambalo kwalo mnaitiwa?
\s5
\v 8 Hata hivyo, kama mwaitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa katika maandiko, "Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe," mwafanya vyema.
\v 9 Lakini kama mkipendelea baadhi ya watu, mnatenda dhambi, mwahukumiwa na sheria kuwa ni wavunja sheria.
\s5
\v 10 Kwa kuwa yeyote atiiye sheria yote, na bado akajikwaa katika nukta moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote!
\v 11 Kwa kuwa Mungu aliyesema, "Usizini," ndiye pia aliyesema, "Usiue." Kama hauzini, lakini una uwa, umekwishavunja sheria ya Mungu.
\s5
\v 12 Kwa hiyo zungumzeni na kutii kama wale ambao mko karibu kuhukumiwa na sheria ya uhuru.
\v 13 Kwa kuwa hukumu huja pasipo huruma kwa wale wasio na huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
\s5
\v 14 Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo? Je, imani hiyo yaweza kumwokoa?
\v 15 Kama ndugu wa kiume au wa kike ni muhitaji wa mavazi au chakula cha kila siku,
\v 16 na mmoja wenu akawaambia, "Nendeni kwa amani, mkaote moto na mle vizuri," lakini hamuwapi mahitaji muhimu ya mwili, hiyo yafaaa nini?
\v 17 Hali kadhalika, imani pekee, kama haina matendo, imekufa.
\s5
\v 18 Bado mtu fulani anaweza kusema, " Una imani, na mimi ninayo matendo." Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
\v 19 Waamini kuwa kuna Mungu mmoja; uko sahihi. Lakini mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.
\v 20 Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo isivyofaa?
\s5
\v 21 Je, si baba yetu Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo alipomtoa mwanawe Isaka juu ya madhabahu?
\v 22 Mnaona kuwa imani yake ilifanya kazi na matendo yake, na kwa matendo yake, imani yake ilifikia kusudio lake.
\v 23 Maandiko yalitimizwa yasemayo, "Abrahamu alimwamini Mungu, na akahesabiwa kuwa ni mwenye haki." Hivyo Abrahamu aliitwa rafiki wa Mungu.
\v 24 Mwaona kuwa kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu.
\s5
\v 25 Hali kadhalika, je, hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe na kuwapeleka kwa barabara nyingine?
\v 26 Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ndugu zangu, siyo wengi wenu mnapaswa kuwa walimu, mkijua kwamba tutapokea hukumu kubwa zaidi.
\v 2 Kwa kuwa wote tunakosea katika njia nyingi. Kama yeyote huwa hajikwai katika maneno yake, huyo ni mtu mkamilifu, aweza kudhibiti mwili wake wote pia.
\s5
\v 3 Sasa kama tunaweka lijamu za farasi katika vinywa vyao wanatutii, na tunaweza kuigeuza miili yao yote.
\v 4 Tambua pia kwamba meli, ingawa ni kubwa na husukumwa na upepo mkali, zinaongozwa kwa usukani mdogo sana kwenda popote anakotaka nahodha.
\s5
\v 5 Vivyo hivyo, ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini hujisifia makuu sana. Angalia msitu mkubwa unavyoweza kuwashwa kwa cheche ndogo ya moto!
\v 6 Ulimi pia ni moto, ni ulimwengu wa uovu, umewekwa miongoni mwa viungo vya mwili wetu, ambao hunajisi mwili wote na huiweka juu ya moto njia ya maisha, na wenyewe kuchomwa moto wa kuzimu.
\s5
\v 7 Kila aina ya mnyama wa polini, ndege, kitambaacho na kiumbe cha baharini kinadhibitiwa na wanadamu.
\v 8 lakini hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye anaweza kudhibiti ulimi; ni uovu usiotulia, umejaa sumu ya kufisha.
\s5
\v 9 Kwa ulimi twamtukuza Bwana na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
\v 10 Katika kinywa hichohicho husema maneno ya baraka na laana. Ndugu zangu mambo haya hayapaswi kuwa.
\s5
\v 11 Je, kisima kimoja huweza kutoa maji matamu na machungu?
\v 12 Ndugu zangu, Je, mti wa mtini unaweza kuzaa matunda ya mzeituni, au mzabibu unazaa matunda ya mtini? Wala chemchemi ya maji chumvi haitoi maji yasio na chumvi.
\s5
\v 13 Ni nani miongoni mwenu aliye na hekima na ufahamu? Hebu mtu huyo na aoneshe maisha mema katika kazi zake kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
\v 14 Lakini kama mnao wivu mkali na nia ya ubinafsi mioyoni mwenu, msijivune na kusema uongo mkiupinga ukweli.
\s5
\v 15 Hii siyo hekima ile ishukayo kutoka juu, lakini badala yake ni ya kidunia, si ya kiroho, na ni ya kipepo.
\v 16 Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu
\v 17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli.
\v 18 Na tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale ambao wanatenda mambo ya amani.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?
\v 2 Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu.
\v 3 Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.
\s5
\v 4 Enyi wazinzi! Hamjui kwamba urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu? Kwa hiyo, yeyote aamuaye kuwa rafiki wa ulimwengu hujifanya mwenyewe adui wa Mungu.
\v 5 Au mnadhani maandiko hayana maana yasemapo kwamba Roho aliyoweka ndani yetu ana wivu sana kwa ajili yetu?
\s5
\v 6 Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, "Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu."
\v 7 Hivyo, jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.
\s5
\v 8 Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi. Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
\v 9 Huzunikeni, ombolezeni, na kuria! Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo.
\v 10 Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.
\s5
\v 11 Msineneane kinyume ninyi kwa ninyi, ndugu. Mtu anenaye kinyume na ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, hunena kinyume na sheria na huihukumu sheria ya Mungu. Mkiihukumu sheria, hamuitii sheria, bali mnaihukumu.
\v 12 Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu, Mungu, yeye ambaye ana uwezo wa kuokoa na kuangamiza. Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?
\s5
\v 13 Sikilizeni, ninyi msemao, "Leo au kesho tutakwenda katika mji huu, na kukaa mwaka huko, na kufanya biashara, na kutengeneza faida."
\v 14 Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho, na maisha yenu ni nini hasa? Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.
\s5
\v 15 Badala yake mngesema, "kama ni mapenzi ya Bwana, tutaishi na tutafanya hiki au kile."
\v 16 Lakini sasa mnajivuna juu ya mipango yenu. Majivuno yote hayo ni uovu.
\v 17 Kwahiyo, kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Njoni sasa, enyi mlio matajiri, lieni kwa sauti ya juu kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu.
\v 2 Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu.
\v 3 Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani, na uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu na kuangamiza miili yenu kama moto. Mmejiwekea hazina yenu katika siku za mwisho.
\s5
\v 4 Tazameni, malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa kwa kuvuna katika mashamba yenu- wanalia! Na kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimeyafikia masikio ya Bwana wa Majeshi.
\v 5 Mmeishi kwa anasa duniani na kujifurahisha ninyi wenyewe. Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo.
\v 6 Mmemhukumu na kumuua mwenye haki asiyeweza kuwapinga.
\s5
\v 7 Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima husubiri mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha.
\v 8 Pia ninyi muwe wavumilivu; kazeni mioyo yenu, kwa sababu kuja kwake Bwana ni karibu.
\s5
\v 9 Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, kusudi msije mkahukumiwa. Tazama, hakimu anasimama mlangoni.
\v 10 Kwa mfano, ndugu, angalieni mateso na uvumilivu wa manabii walionena katika jina la Bwana.
\v 11 Tazama, twawaita wale wanaovumilia, "heri." Mmesikia uvumilivu wa Ayubu, na mnalijua kusudi la Bwana kwa ajili ya Ayubu, ni kwa jinsi gani Bwana amejaa huruma na rehema.
\s5
\v 12 Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, aidha kwa mbingu ama kwa nchi, au kwa kiapo cha aina nyingine. Bali hebu "ndiyo" yenu na imaanishe "ndiyo" na "hapana" yenu na imaanishe "hapana," ili kwamba msije kuangukia chini ya hukumu.
\s5
\v 13 Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe. Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa.
\v 14 Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao wazee wa kanisa waombe juu yake, wakimpaka mafuta katika jina la Bwana,
\v 15 na maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama atakuwa ametenda dhambi, Mungu atamsamehe.
\s5
\v 16 Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana kila mmoja na mwenzake, ili muweze kuponywa. Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa.
\v 17 Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
\v 18 Na Eliya aliomba tena, na mbingu zilimwaga mvua juu ya nchi na nchi ikatoa mavuno.
\s5
\v 19 Ndugu zangu, kama yeyote miongoni mwenu anapotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha,
\v 20 hebu na ajue kuwa yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.

208
61-1PE.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,208 @@
\id 1PE
\ide UTF-8
\h 1 Petro
\toc1 1 Petro
\toc2 1 Petro
\toc3 1pe
\mt 1 Petro
\s5
\c 1
\p
\v 1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wageni wa utawanyiko, kwa wateule, katika Ponto yote, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia,
\v 2 kutokana na ufahamu wa Mungu, Baba, kwa kutakaswa na Roho Mtakatifu, kwa utiifu wa Yesu Kristo, na kwa kunyunyuziwa damu yake. Neema iwe kwenu, na amani yenu iongezeke.
\s5
\v 3 Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na abarikiwe. Katika ukuu wa rehema yake, alitupa kuzaliwa upya kwa ujasiri wa urithi kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka katika wafu,
\v 4 kwa urithi usioangamia, hautakua na uchafu wala kupungua. Umehihifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu.
\v 5 Kwa uwezo wa Mungu mnalindwa kupitia imani kwa wokovu ambao upo tayari kufunuliwa katika nyakati za mwisho.
\s5
\v 6 Furahini katika hili, ingawaje sasa ni lazima kwenu kujisikia huzuni katika majaribu ya aina mbalimbali.
\v 7 Hii, ni kwa sababu imani yenu iweze kujaribiwa, imani ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ambayo inapotea katika moto ambao hujaribu imani yenu. Hii hutokea ili imani yenu ipate kuzaa sifa, utukufu, na heshima katika ufunuo wa Yesu Kristo.
\s5
\v 8 Hamjamuona yeye, lakini mnampenda. Hamumuoni sasa, lakini mnaamini katika yeye na mna furaha isiyoweza kuelezeka kwa furaha ambayo imejawa na utukufu.
\v 9 Sasa mnapokea wenyewe matokeo ya imani yenu, wokovu wa nafsi zenu.
\v 10 Manabii walitafuta na kuuliza kwa umakini kuhusu wokovu huu, kuhusu neema ambayo ingekuwa yenu.
\s5
\v 11 Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata.
\v 12 Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.
\s5
\v 13 Kwa hiyo fungeni viuno vya akili zenu. Muwe watulivu katika fikra zenu. Muwe na ujasiri mkamilifu katika neema ambayo italetwa kwenu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo.
\v 14 Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu.
\s5
\v 15 Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.
\v 16 Kwa kuwa imeandkwa, "Iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu."
\v 17 Na kama mkiita "Baba" yule ahukumuye kwa haki kulingana na kazi ya kila mtu, tumia muda wa safari yako katika unyenyekevu.
\s5
\v 18 Mnafahamu kwamba haikuwa kwa fedha au dhahabu - vitu vinavyoharibika- ambavyo mmekombolewa kutoka kwenye tabia zenu za ujinga ambazo mlijifunza kutoka kwa baba zenu.
\v 19 Lakini mmekombolewa kwa damu ya heshima ya Kristo, kama ya kondoo asiye na hila wala doa.
\s5
\v 20 Kristo alichaguliwa kabla ya misingi ya dunia, lakini sasa siku hizi za mwisho, amefunuliwa kwenu.
\v 21 Mnamwamini Mungu kupitia yeye, ambaye Mungu alimfufua toka kwa wafu na ambaye alimpa utukufu ili kwamba imani yenu na ujasiri uwe katika Mungu.
\s5
\v 22 Mmefanya nafsi zenu kuwa safi kwa utii wa ile kweli, kwa dhumuni la pendo la kidugu lililo na unyofu, hivyo pendaneni kwa bidii toka moyoni.
\v 23 Mmekwisha zaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, lakini kutoka katika mbegu isiyoharibika, kupitia uzima na neno la Mungu lililosalia.
\s5
\v 24 Kwa maana " miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
\v 25 lakini neno la Bwana hubakia milele." Huu ni ujumbe ambao ulitangazwa kama injili kwenu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kwa hiyo wekeni pembeni uovu wote, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa.
\v 2 Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwamba mweze kukua ndani ya wokovu,
\v 3 kama mmeonja kwamba Bwana ni mwema.
\s5
\v 4 Njoni kwake aliye jiwe hai linaloishi ambalo limekataliwa na watu, lakini hilo limechaguliwa na Mungu na ni la thamani kwake.
\v 5 Ninyi pia ni kama mawe yaliyo hai yanayojengwa juu kuwa nyumba ya kiroho, ili kuwa ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.
\s5
\v 6 Andiko husema hivi, "Tazama, nimeweka katika Sayuni jiwe la pembeni, kuu na lililochaguliwa na la thamani. Yeyote aaminiye katika yeye hataona aibu".
\s5
\v 7 Hivyo heshima ni yenu kwenu ninyi mnaoamini. Lakini, "jiwe lililokataliwa na wajenzi, hili limekuwa jiwe kuu la pembeni"-
\v 8 na, "jiwe la kujikwaa na mwamba wa kujikwaa."Wao hujikwaa, wanaolikataa neno, kwa lile ambalo pia walikuwa wameteuliwa kwalo.
\s5
\v 9 Lakini ninyi ni ukoo uliochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kutangaza matendo ya ajabu ya yule aliyewaita kutoka gizani kuja kwenye nuru yake ya ajabu.
\v 10 Ninyi kwanza hamkuwa watu, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Ninyi hamkupokea rehema, lakini sasa mmepokea rehema.
\s5
\v 11 Wapendwa, nimewaita kama wageni na wazurujaji kujinyima kutoka kwenye tamaa mbaya za dhambi, ambazo zinapigana vita na roho zenu.
\v 12 Mnapaswa kuwa na tabia njema kati ya mataifa, ili kwamba, kama watawasema kama kwamba mmefanya mambo maovu, wataziangalia kazi zenu njema na kumsifu Mungu katika siku ya kuja kwake.
\s5
\v 13 Tii kila mamlaka ya mwanadamu kwa ajili ya Bwana, ikiwa mfalme kama mkuu,
\v 14 ikiwa watawala waliotumwa kuwaadhibu watenda mabaya na kuwasifu wale wanaotenda mema.
\v 15 Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kufanya mema mwanyamazisha mazungumzo ya kipuuzi ya watu wapumbavu.
\v 16 Kama watu huru, msiutumie uhuru wenu kama kifuniko kwa maovu, bali muwe kama watumishi wa Mungu.
\v 17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mwogopeni Mungu. Mweshimuni mfalme.
\s5
\v 18 Watumwa, watiini bwana zenu kwa heshima yote, siyo tu bwana walio wazuri na wapole, lakini pia walio waovu.
\v 19 Kwa kuwa ni sifa kama yeyote atavumilia maumivu wakati anapoteseka pasipo haki kwa sababu ya dhamiri yake kwa Mungu.
\v 20 Ni faida gani iliyopo kama mwadumu kutenda dhambi kisha mwendelee kuadhibiwa? Lakini kama mmefanya mema na ndipo mteseke kwa kuhukumiwa, hii ni sifa njema kwa Mungu.
\s5
\v 21 Kwa hili mliitwa, kwa sababu Kristo pia aliteswa kwa ajili yenu, amewaachia mfano kwa ajili yenu kufuata nyayo zake.
\v 22 Yeye hakufanya dhambi, wala haukuonekana udanganyifu wowote kinywani mwake.
\v 23 Wakati yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteseka, hakutisha bali alijitoa mwenyewe kwake Yeye ahukumuye kwa haki.
\s5
\v 24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake kwenye mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena katika dhambi, na kwamba tuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa kwake ninyi mmepona.
\v 25 Wote mliokuwa mkitangatanga kama kondoo aliyepotea, lakini sasa mmerudi kwa mchungaji na mlinzi wa roho zenu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa njia hii, ninyi ambao ni wake mnapaswa kujitoa kwa waume zenu wenyewe, ili, hata kama baadhi yao hawajalitii neno, kupitia tabia za wake zao wanaweza kuvutwa pasipo neno,
\v 2 kwa sababu wao wenyewe watakuwa wameiona tabia yenu njema pamoja na heshima.
\s5
\v 3 Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.
\v 4 Lakini badala yake ifanyike kwa utu wa ndani wa moyo, na kuzidi katika uzuri wa unyenyekevu na utulivu wa moyo, ambao ni wa thamani mbele za Mungu.
\s5
\v 5 Kwa kuwa wanawake watakatifu walijipamba wenyewe kwa njia hii. Walikuwa na imani katika Mungu na waliwatii waume zao wenyewe.
\v 6 Kwa njia hii Sara alimtii Ibrahamu na kumwita yeye "bwana" wake. Ninyi sasa ni watoto wake kama mtafanya yaliyo mazuri na kama hamwogopi mabaya.
\s5
\v 7 Kwa njia hiyo hiyo, ninyi wanaume mnapaswa kuishi na wake zenu mkijua kuwa wao ni wenzi wa kike dhaifu, mkiwatambua wao kama wapokeaji wenzenu wa zawadi ya uzima. Fanyeni hivi ili kwamba maombi yenu yasizuiliwe.
\s5
\v 8 Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.
\v 9 Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.
\s5
\v 10 "Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.
\v 11 Na ageuke na kuacha mabaya na kufanya yaliyo mazuri. Atafute amani na kuifuata.
\v 12 Macho ya Bwana humwona mwenye haki na masikio yake husikia maombi yake. Lakini uso wa Bwana uko kinyume cha wale watendao uovu."
\s5
\v 13 Ni nani atakayewadhuru ninyi, ikiwa mwatamani lililo zuri?
\v 14 Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.
\s5
\v 15 Badala yake, mmuweke Kristo Bwana katika mioyo yenu kama mtakatifu. Kila mara muwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza ninyi kwa nini mna tumaini katika Mungu. Fanyeni hivi kwa upole na heshima.
\v 16 Muwe na dhamiri njema ili kwamba watu wanaotukana maisha yenu mema katika Kristo waweze kuaibika kwa sababu wanaongea kinyume dhidi yenu kama kwamba mlikuwa watenda maovu.
\v 17 Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.
\s5
\v 18 Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi. Yeye ambaye ni mwenye haki aliteseka kwa ajili yetu, ambao hatukuwa wenye haki, ili kwamba atulete sisi kwa Mungu. Alikufa katika mwili, lakini alifanywa mzima katika roho.
\v 19 Katika roho, alikwenda na kuzihubiri roho ambazo sasa ziko kifungoni.
\v 20 Hazikuwa tiifu wakati uvumilivu wa Mungu ulipokuwa unasubiri wakati wa Nuhu, siku za ujenzi wa safina, na Mungu aliokoa watu wachache—nafsi nane—kutoka katika maji.
\s5
\v 21 Hii ni alama ya ubatizo unaowaokoa ninyi sasa, siyo kama kuosha uchafu kutoka mwilini, lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo.
\v 22 Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu. Alikwenda mbinguni. Malaika, mamlaka, na nguvu lazima vimtii yeye.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni silaha za nia ile ile. Yeye aliyeteseka katika mwili ameondokana na dhambi.
\v 2 Mtu huyu haendelei tena kuishi katika tamaa za mwili, bali kwa mapenzi ya Mungu, kwa maisha yake yaliyosalia.
\s5
\v 3 Kwa kuwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo.
\v 4 Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu.
\v 5 Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu.
\v 6 Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho.
\s5
\v 7 Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu.
\v 8 Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.
\v 9 Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika.
\s5
\v 10 Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu.
\v 11 Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina.
\s5
\v 12 Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu.
\v 13 Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.
\v 14 Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.
\s5
\v 15 Lakini asiwepo yeyote mwenye kuteswa kama muuaji, mwizi, mtenda maovu, au ajishughulishaye na mambo ya wengine.
\v 16 Lakini ikiwa mtu anateswa kama Mkristo, asione aibu, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
\s5
\v 17 Kwa kuwa wakati umefika kwa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Na kama inaanzia kwetu, itakuwaje kwa wale wasioitii injili ya Mungu?
\v 18 Na kama "mwenye haki anaokolewa kupitia magumu, itakuwaje kwa mtu asiyehaki na mwenye dhambi?"
\v 19 Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, mimi, niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso ya Kristo, na ambaye vile vile ni mshirika katika utukufu utakaodhihirika.
\v 2 Kwa hiyo, ninawatia moyo ninyi wazee, lichungeni kundi la Mungu lililo miongoni mwenu. Liangalieni, sio kwa sababu mnapaswa, lakini kwa sababu mnatamani hivyo, kulingana na Mungu. Liaangalieni, sio kwa kupenda pesa za aibu, lakini kwa kupenda.
\v 3 Msijifanye mabwana juu ya watu waliyochini ya uangalizi wenu, lakini iweni mfano katika kundi.
\v 4 Pale Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu isiyopoteza uthamani wake.
\s5
\v 5 Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.
\v 6 Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.
\v 7 Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.
\s5
\v 8 Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.
\v 9 Simameni kinyume chake. Kuweni na nguvu katika imani yenu. Mkijua kwamba ndugu zenu walioko ulimwenguni wanapitia mateso kama hayo.
\s5
\v 10 Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.
\v 11 Enzi iwe kwake milele na milele. Amina.
\s5
\v 12 Namthamini Silwano kama ndugu mwaminifu, na nimewaandikia ninyi kwa ufupi kupitia kwake. Ninawatia moyo na ninashuhudia kwamba nilichokiandika ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni ndani yake.
\v 13 Waamini waliloko Babeli, waliochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu, na Marko mwanangu, anawasalimu.
\v 14 Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.

122
62-2PE.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,122 @@
\id 2PE
\ide UTF-8
\h 2 Petro
\toc1 2 Petro
\toc2 2 Petro
\toc3 2pe
\mt 2 Petro
\s5
\c 1
\p
\v 1 Simon Petro, Mtumwa na Mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale walioipokea imani ile ile ya thamani kama tulivyoipokea sisi, imani iliyo ndani ya haki ya Mungu na mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 2 Neema iwe kwenu; amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Bwana wetu Yesu.
\s5
\v 3 Kupitia maarifa ya Mungu tumepata mambo yake yote kwa ajili ya uchaji wamaisha, Toka kwa Mungu aliyetuita kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake.
\v 4 Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warith wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii.
\s5
\v 5 Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri kwa njia ya imani yenu, kwa sababu ya uzuri, maarifa.
\v 6 Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa.
\v 7 Kupitia utauwa upendo wa ndugu na kupitia upendo wa ndugu, upendo.
\s5
\v 8 Kama mambo haya yamo ndani yenu, yakiendelea kukua ndani yenu, basi ninyi hamtakuwa tasa au watu msiozaa matunda katika maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 9 Lakini yeyote asiyekuwa na mambo haya, huyaona mambo ya karibu tu; yeye ni kipofu. amesahau utakaso wa dhambi zake za kale.
\s5
\v 10 Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu. Kama mtayafanya haya, hamtajikwaa.
\v 11 Hivyo mtajipatia wingi wa lango la kuingilia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo.
\s5
\v 12 Kwa hiyo mimi nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya kila mara, hata kama mnayafahamu, na sasa mmekuwa imara katika kweli.
\v 13 Nafikiria kuwa niko sahihi kuwaamsha na kuwakumbusha juu ya mambo haya, ningali nimo katika hema hii.
\v 14 Kwa maana najua kuwa si muda mrefu nitaiondoa hema yangu, kama Bwana Yesu Kristo alivyonionyesha.
\v 15 Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya baada ya mimi kuondoka.
\s5
\v 16 Kwa kuwa sisi hatukufuata hadthi zilizoingizwa kwa ustadi pale tulipowaeleza juu ya nguvu na kujidhihirisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, bali sisi tulikuwa mashahidi wa utukufu wake.
\v 17 Yeye alipokea Utukufu na heshima toka kwa Mungu baba pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu ikisema, "Huyu ndiye mwanangu, mpendwa wangu ambaye nimependezwa naye."
\v 18 Tuliisikia sauti hii ikitokea mbinguni pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.
\s5
\v 19 Tunalo hili neno la unabii lililothibitika, ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza. Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kuchapo na nyota za mawio zionekanazo katika mioyo yenu.
\v 20 Tambueni haya ya kwamba, hakuna unabii unaoandikwa kwa sababu ya kujifikirisha kwa nabii mwenyewe.
\v 21 Kwa kuwa hakuna unabii uliokuja kwa mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.
\v 2 Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.
\v 3 Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
\s5
\v 4 Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia.
\v 5 Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.
\v 6 Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni
\s5
\v 7 Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.
\v 8 Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona.
\v 9 Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.
\s5
\v 10 Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, Hawaogopi kuwakufuru watukufu.
\v 11 Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana
\s5
\v 12 Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa.
\v 13 Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe.
\v 14 Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa.
\s5
\v 15 Wameiacha njia ya kweli. wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu.
\v 16 Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosai wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii..
\s5
\v 17 Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao.
\v 18 Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji.
\v 19 Huwaahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala.
\s5
\v 20 Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo.
\v 21 Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa.
\v 22 Mithali hii huwa na ukweli kwao. "mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope."
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ssa, ninakuandikia wewe, mpendwa hii barua ya pili ili kukuamsha katika akili,
\v 2 ili kwamba uweze kukumbuka maneno yaliyosemwa kabla na manabii watakatifu na kuhusu amri ya Bwana wetu na mwokozi kwa kutumia mitume.
\s5
\v 3 Ujue ili kwanza, kwamba wasaliti watakuja katika siku za mwisho kuwasaliti ninyi, wakienenda sawasawa na matakwa yao.
\v 4 Na wakisema "Iko wapi ahadi ya kurudi? Baba zetu walikufa, Lakini vitu vyote vilikuwa hivyo tangu mwanzo wa uumbaji.
\s5
\v 5 Wakajifanya kusahau kwamba nchi na mbingu vilianza kutokana na maji na kupitia maji zamani za kale, kwa neno la Mungu,
\v 6 na kwamba kupitia neno lake na maji yakawa ulimwengu kwa kipindi hicho, ikiwa imejaa maji, iliharibiwa.
\v 7 Lakini sasa mbingu na dunia zimetunzwa kwa neno hilo hilo kwa ajili ya moto. Vimehifadhiwa kwa ajili ya siku ya hukumu na maangamizi ya watu wasio wa Mungu
\s5
\v 8 Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako, wapendwa, kwamba siku moja kwa bwana ni kama miaka elfu moja. Na miaka elfu moja ni kama siku moja.
\v 9 Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi, kama inavyofikiriwa kuwa, Lakini yeye ni mvumilivu kwa ajili yenu, yeye hatamani hata mmoja aangamie, Lakini hutamani kutoa muda ili wote wapate kutubu.
\s5
\v 10 Ingawa, siku ya Bwana itakuja kama mwizi, mbingu itapita kwa kupaza kelele. Vitu vitateketezwa kwa moto. Nchi na vitu vyote vilivyomo vitafunuliwa wazi.
\s5
\v 11 Kwa kuwa vitu vyote vutateketezwa kwa njia hii. Je utakuwa mtu wa aina gani? Uishi kitakatifu na maisha ya kimungu.
\v 12 Inakupasa kujua na kutambua haraka ujio wa siku ya Mungu. Siku hiyo mbingu itateketezwa kwa moto. Na vitu vitayeyushwa katika joto kali.
\v 13 Lakini kutokana na ahadi yake, tunasubiri mbingu mpya na nchi mpya, ambapo wenye haki wataishi
\s5
\v 14 Hivyo wapendwa kwa kuwa tunatarajia vitu hivi, jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye.
\v 15 Na zingatia uvumilivu wa Bwana wetu katika wokovu, kama mpendwa kaka yetu Paulo, alivyowaandikia ninyi, kutokana na hekima ambayo alipewa.
\v 16 Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake, kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa. Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo, Na kama wanavyofanya kwa maandiko. Kuelekea maangamizi yao.
\s5
\v 17 Hivyo, wapendwa kwa kuwa mnayafahamu hayo. Jilindeni wenyewe ili kwamba msipotoshwe na udanganyifu wa walaghai na kupoteza uaminifu.
\v 18 Lakini mkue katika neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo. Na sasa utukufu una yeye sasa na milele. Amina.

204
63-1JN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,204 @@
\id 1JN
\ide UTF-8
\h 1Yohana 1
\toc1 1Yohana 1
\toc2 1Yohana 1
\toc3 1jn
\mt 1Yohana 1
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kile kilichokuwapo tangu mwanzo-kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika-kuhusu Neno la uzima.
\v 2 Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi, na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu.
\s5
\v 3 Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu pia, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
\v 4 Na tunawandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.
\s5
\v 5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia: Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo.
\v 6 Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli.
\v 7 Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambi zote.
\s5
\v 8 Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu.
\v 9 Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
\v 10 Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki.
\v 2 Yeye ni mpatanishi kwa dhambi zetu, na si kwa dhambi zetu pekee, lakini pia kwa ulimwengu mzima.
\v 3 Kwa hili twajua kwamba twamjua yeye, kama tukizitunza amri zake.
\s5
\v 4 Yeye asemaye, "Namjua Mungu," lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.
\v 5 Lakini yeyote ashikaye neno lake, kweli katika mtu yule upendo wa Mungu umekamilishwa. Katika hili twajua kwamba tuko ndani yake.
\v 6 Yeye asemaye anaishi ndani ya Mungu anapaswa mwenyewe pia kuenenda kama vile Yesu Kristo alivyoenenda.
\s5
\v 7 Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani ambayo mmekwisha kuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno ambalo mlilolisikia.
\v 8 Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya, ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu, kwa sababu giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza
\s5
\v 9 Yeye asemeye yuko kwenye nuru na amchukia ndugu yake yuko katika giza hata sasa.
\v 10 Yeye ampendaye ndugu yake anaishi katika nuru na hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza.
\v 11 Lakini yeye amchukiaye ndugu yake yuko gizani na anatembea gizani; Yeye hajui wapi aendako, kwa sababu giza limeyapofusha macho yake.
\s5
\v 12 Nawaandikia ninyi, watoto wapendwa, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake.
\v 13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mnamjua Baba.
\v 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mko imara, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.
\s5
\v 15 Msiipende dunia wala mambo ambayo yaliyo katika dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upendo wa kumpenda Baba haumo ndani yake.
\v 16 Kwani kila kitu kilichomo katika dunia- tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima- havitokani na Baba lakini vinatokana na dunia.
\v 17 Dunia na tamaa zake zinapita. Bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu huyo adumu milele.
\s5
\v 18 Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho. Kama ambavyo mmesikia kwamba mpinga kristo anakuja, hata sasa wapinga kristo wamekuja, kwa hali hii tunajua kwamba ni wakati wa mwisho.
\v 19 Walikwenda zao kutoka kwetu, kwani hawakuwa wa kwetu. Kama vile wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi. Lakini wakati walipo kwenda zao, hicho kilionyesha hawakuwa wa kwetu.
\s5
\v 20 Lakini mumetiwa mafuta na yule Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli.
\v 21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua na kwa sababu hakuna uongo wa ile kweli
\s5
\v 22 Nani ni mwongo bali ni yeye anayepinga kwamba Yesu ni Kristo? Huyu mtu ni mpinga kristo, pale anapo mpinga Baba na Mwana.
\v 23 Hakuna anaye mpinga Mwana akawa na Baba. Yeyote anaye mkiri Mwana anaye Baba pia.
\s5
\v 24 Kama kwa ajili yenu, kile mlichosikia toka mwanzo acha kiendelee kuwa ndani yenu. Kama kile mlichosikia toka mwanzo kitakaa ndani yenu, pia, mtakaa ndani ya Mwana na Baba.
\v 25 Na hii ni ahadi aliyotupatia sisi: uzima wa milele.
\v 26 Nimewaandikia haya ninyi kuhusu wale ambao wangewaongoza ninyi katika upotevu.
\s5
\v 27 Na kwa ajili yenu, yale mafuta mliyoyapokea kutoka kwake yanakaa ndani yenu, na hamtahitaji mtu yeyote kuwafundisha. bali kama mafuta yake yanawafundisha kuhusu mambo yote na ni kweli na siyo uongo, na hata kama yameshawafundisha, kaeni ndani yake.
\v 28 Na sasa, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili wakati atakapotokea, tuweze kuwa na ujasiri na siyo kujisikia aibu mbele yake katika kuja kwake.
\v 29 Kama mnajua kuwa yeye ni mwenye haki, mnajua kwamba kila mmoja atendaye haki amezaliwa na yeye.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Oneni ni pendo la namna gani ametupatia Baba, kwamba tunaitwa watoto wa Mungu, na hivi ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa haukumtambua yeye.
\v 2 Wapendwa sisi sasa ni watoto wa Mungu, na haijadhihirika bado jinsi tutakavyokuwa. Twajua kwamba Kristo atakapoonekana, tutafanana naye, kwani tutamuona kama alivyo.
\v 3 Na kila mmoja ambaye ana ujasiri huu kuhusu wakati ujao ulioelekezwa kwake, hujitakasa mwenyewe kama yeye alivyo mtakatifu.
\s5
\v 4 Kila mtu anayeendelea kutenda dhambi huvunja sheria. Kwa sababu dhambi ni uvunjaji sheria.
\v 5 Mnajua Kristo alidhihilishwa ili kuziondoa dhambi kabisa. Na ndani yake hamna dhambi.
\v 6 Hakuna hata mmoja adumue ndani yake na kuendelea kutenda dhambi. Hakuna mtu hata mmoja adumuye katika dhambi ikiwa amemuona au kumfahamu yeye.
\s5
\v 7 Watoto wapendwa, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Atendaye haki ni mwenye haki, kama vile Kristo naye alivyo mwenye haki.
\v 8 Atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi ni mtenda dhambi tangu mwanzo. Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihilishwa ili aweze kuziharibu kazi za ibilisi.
\s5
\v 9 Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu mbegu ya Mungu hukaa ndani yake. Hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
\v 10 Katika hili watoto wa Mungu na watoto wa ibilisi wanafahamika. Yeyote asiyetenda kilicho cha haki, siyo wa Mungu, wala yule ambaye hawezi kumpenda ndugu yake.
\s5
\v 11 Kwani huu ndio ujumbe mliousikia kutoka mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi,
\v 12 siyo kama Kaini ambaye alikuwa wa mwovu na alimuua ndugu yake. Na kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, na yale ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
\s5
\v 13 Ndugu zangu, msishangae, endapo ulimwengu utawachukia.
\v 14 Twajua tumekwisha toka mautini na kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Yeyote ambaye hana upendo hudumu katika mauti.
\v 15 Mtu yeyote anaye mchukia ndugu yake ni muuaji. Na mnajua kuwa uzima wa milele haukai ndani ya muuaji.
\s5
\v 16 Katika hili tunalijua pendo, kwa sababu kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi yatupasa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu.
\v 17 Lakini yeyote aliye na vitu, na anamuona ndugu yake mwenye uhitaji, lakini huuzuia moyo wake wa huruma kwa ajili yake; je, upendo wa Mungu unakaaje ndani yake?
\v 18 Watoto wangu wapenzi, tusipende kwa midomo wala kwa maneno matupu bali katika vitendo na kweli.
\s5
\v 19 Katika hili tunajua kwamba sisi tuko katika kweli, na mioyo yetu inathibitika katika yeye.
\v 20 Ikiwa kama mioyo yetu yatuhukumu, Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, na yeye hujua mambo yote.
\v 21 Wapenzi, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri kwa Mungu.
\v 22 Na chochote tuombacho tutakipokea kutoka kwake, kwa sababu tunazishika amri zake na tunafanya mambo yanayopendeza mbele zake.
\s5
\v 23 Na hii ndiyo amri yake- ya kwamba yatupasa kuamini katika jina la Mwanaye Yesu Kristo na kupendana sisi kwa sisi-kama alivyotupatia amri yake.
\v 24 Anayezitii amri zake hudumu ndani yake, na Mungu hukaa ndani yake. Na kwa sababu hii twajua kuwa hukaa ndani yetu, Kwa yule Roho aliyetupa.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Wapendwa, msiiamini kila roho, lakini zijaribuni roho muone kama zinatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.
\v 2 Kwa hili mtamjua Roho wa Mungu - kila roho itakayokiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili ni ya Mungu,
\v 3 na kila roho isiyomkiri Yesu si ya Mungu. Hii ni roho ya mpinga kristo, ambayo mliyoisikia kuwa inakuja, na sasa tayari iko duniani.
\s5
\v 4 Ninyi ni wa Mungu, watoto wapendwa, na mmekwisha washinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.
\v 5 Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanachokisema ni cha ulimwengu, na ulimwengu unawasikiliza.
\v 6 Sisi ni wa Mungu. Yeye amjuaye Mungu hutusikiliza sisi. Yeye asiye wa Mungu hawezi kutusikiliza. Katika hili tunajua roho wa kweli na roho wa uongo.
\s5
\v 7 Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo ni wa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu.
\v 8 Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.
\s5
\v 9 Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye.
\v 10 Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia ya dhambi zetu.
\s5
\v 11 Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.
\v 12 Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu.
\v 13 Katika hili tunajua kuwa tunakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa Roho wake.
\v 14 Na tumeona na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.
\s5
\v 15 Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu.
\v 16 Na tunajua na kuamini upendo alio nao Mungu ndani yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
\s5
\v 17 Katika pendo hili limekwisha kamilishwa kati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu.
\v 18 Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.
\s5
\v 19 Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
\v 20 Ikiwa mmoja atasema, "Nampenda Mungu" lakini anamchukia ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona.
\v 21 Na hii ndiyo amri tuliyo nayo kutoka kwake: Yeyote ampendaye Mungu, anapaswa kumpenda ndugu yake pia.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake.
\v 2 Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu -- tunapompenda Mungu na kutekeleza amri zake.
\v 3 Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazishika amri zake. Na amri zake ni nyepesi.
\s5
\v 4 Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, imani yetu.
\v 5 Ni nani aliyeushinda ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
\s5
\v 6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.
\v 7 Kwa kuwa kuna watatu washuhudiao:
\v 8 Roho, maji na damu. Hawa watatu hukubaliana. (Zingatia: Maneno haya "Baba, Neno, na Roho Mtakatifu" hayaonekani katika nakala bora za kale).
\s5
\v 9 Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu kuliko huo. Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu ni huu- kwamba anao ushuhuda kuhusiana na Mwanawe.
\v 10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake mwenyewe. Na yeyote asiye mwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.
\s5
\v 11 Na ushuhuda ndio huu -- kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo ndani ya Mwanawe.
\v 12 Aliye naye Mwana ana uzima. Asiyekuwa naye Mwana wa Mungu hana uzima.
\s5
\v 13 Nimewaandikia haya mweze kujua kwamba mnao uzima wa milele -- ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu.
\v 14 Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia.
\v 15 Na kama tunajua kwamba hutusikia -- chochote tumwombacho tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.
\s5
\v 16 Kama mtu amwonaye ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo, yampasa kuomba na Mungu atampa uzima. Ninasema kwa wale ambao dhambi yao ni ile isiyopelekea kifo -- Kuna dhambi ipelekeayo kifo -- sisemi kwamba anapaswa kuomba kwa ajilli ya dhambi hiyo.
\v 17 Uasi wote ni dhambi -- lakini kuna dhambi isiyopelekea kifo.
\s5
\v 18 Tunajua ya kuwa aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi. Bali aliyezaliwa na Mungu hutunzwa naye salama daima, na yule mwovu hawezi kumdhuru.
\v 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na tunajua kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.
\s5
\v 20 Lakini twajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupatia ujuzi, kwamba tunamjua yeye aliye kweli na kwamba tumo ndani yake yeye aliye kweli, hata katika Mwanawe Yesu Kristo. Ni Mungu wa kweli na uzima wa milele.
\v 21 Watoto wapenzi, jiepusheni na sanamu.

32
64-2JN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,32 @@
\id 2JN
\ide UTF-8
\h 2 Yohana
\toc1 2 Yohana
\toc2 2 Yohana
\toc3 2jn
\mt 2 Yohana
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake, ambao niwapendao katika kweli na si mimi tu, bali na wote wale wanao ifahamu kweli,
\v 2 kwa sababu ya kweli iliyomo ndani yetu na itakayodumu pamoja nasi milele.
\v 3 Neema, rehema, amani zitakuwa nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, katika kweli na pendo.
\s5
\v 4 Ninafurahi sana kwamba nimegundua baadhi ya watoto wanaenenda katika kweli, kama vile tu tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba.
\v 5 Na sasa nakusihi wewe, mwanamke, siyo kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. Na huu ndiyo upendo, tunaopaswa kuenenda, kulingana na amri yake.
\v 6 Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo.
\s5
\v 7 Kwa kuwa wadanganyifu wengi wamesambaa katika ulimwengu, na hawakiri kwamba Yesu Kristo alikuja katika mwili. Huyu ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo.
\v 8 Jiangalieni wenyewe kwamba hampotezi mambo yale tuliyokwisha fanyia kazi, lakini ili kwamba mweze kuipokea tuzo kamili.
\s5
\v 9 Yeyote aendeleae mbele na hadumu katika fundisho la Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana pia.
\v 10 Kama mtu anakuja kwenu na haleti fundisho hili, msimkaribishe katika nyumba zenu na msimsalimie.
\v 11 Kwa kuwa amsalimuye hushiriki katika matendo yake maovu.
\s5
\v 12 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, na sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino. Lakini natumaini kuja kwenu na kuongea uso kwa uso, kwamba furaha yetu ipate kufanywa kamili.
\v 13 Watoto wa dada yenu mteule wanawasalimia.

34
65-3JN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,34 @@
\id 3JN
\ide UTF-8
\h 3 Yohana
\toc1 3 Yohana
\toc2 3 Yohana
\toc3 3jn
\mt 3 Yohana
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.
\v 2 Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
\v 3 Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na ndugu waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.
\v 4 Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli.
\s5
\v 5 Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni,
\v 6 ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu.
\v 7 Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa.
\v 8 Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli.
\s5
\v 9 Nililiandikia kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao, hakubaliani na sisi.
\v 10 Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe hawapokei ndugu. Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao ndugu na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.
\s5
\v 11 Mpenzi, usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwona Mungu.
\v 12 Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli.
\s5
\v 13 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino.
\v 14 Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana.
\v 15 Amani iwe pamoja nawe. Marafiki wanakusalimu. Wasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.

56
66-JUD.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,56 @@
\id JUD
\ide UTF-8
\h Yuda
\toc1 Yuda
\toc2 Yuda
\toc3 jud
\mt Yuda
\s5
\c 1
\p
\v 1 Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo, kwa wale ambao wameitwa, wapendwao katika Mungu Baba, na waliotunzwa kwa ajili ya Yesu Kristo:
\v 2 rehema na amani na upendo viongezwe kwenu.
\s5
\v 3 Wapenzi, wakati nilipokuwa nikifanya kila juhudi kuwaandikia ninyi kuhusu wokovu wetu sote, ilinilazimu kuwaandikia kwa ajili ya kuwashauri ili mshindanie kwa uaminifu imani ambayo ilikuwa imekabidhiwa mara moja tu kwa waamini.
\v 4 Kwa sababu watu fulani wamejiingiza kwa siri kati yenu - watu ambao walitiwa alama kwa ajili ya hukumu - watu wasio wataua ambao hubadili neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, na kumkana Bwana wetu pekee na Bwana Yesu Kristo.
\s5
\v 5 Sasa napenda kuwakumbusha ninyi ingawa kuna wakati mlijua kwa ukamilifu kwamba Bwana aliwaokoa watu kutoka nchi ya Misri, lakini baadaye kuwaangamiza wale ambao hawakuamini.
\v 6 Na malaika ambao hawakuilinda enzi yao wenyewe lakini wakaacha makao yao maalum Mungu amewaweka katika minyororo ya milele, ndani ya giza, kwa ajili ya hukumu ya siku ile kuu.
\s5
\v 7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka, ambayo pia ilijiingiza yenyewe katika uasherati na wakafuata tamaa isiyo ya asili. Walioneshwa kama mifano ya wale ambao huteseka katika hukumu ya moto wa milele.
\v 8 Hali kadhalika, kwa njia ile ile waota ndoto hawa pia huchafua miili yao, na hukataa mamlaka, na wananena uongo dhidi ya mtukufu.
\s5
\v 9 Lakini hata Mikaeli malaika mkuu, wakati alipokuwa akishindana na ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kuleta hukumu ya uongo dhidi yake, lakini badala yake alisema, "Bwana akukemee!"
\v 10 Lakini watu hawa huleta uongo dhidi ya chochote wasicho kifahamu. Na kile wasicho kifahamu- kile ambacho wanyama wasio na akili hujua kwa silika- haya ndiyo yaliyo waharibu.
\v 11 Ole wao! Kwa kuwa wametembea katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu. Wameangamia katika uasi wa Kora.
\s5
\v 12 Hawa ni miamba katika sherehe zenu za upendo, wakisherehekea bila aibu, wakijilisha tu wenyewe. Ni mawingu yasiyo na maji, yanayobebwa na upepo, ni miti iliyopukutika isiyo na matunda iliyo kufa mara mbili, iliyong'olewa mizizi
\v 13 Ni mawimbi ya bahari yenye kelele yakitoa aibu yao wenyewe, Ni nyota zinazorandaranda ambazo weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele.
\s5
\v 14 Enoko, wa saba katika orodha ya Adamu, alitabiri kuhusu wao, akisema, "Tazama! Bwana anakuja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,
\v 15 ili afanye hukumu juu ya kila mtu, na kutia hatia wote wasiomcha Mungu juu ya matendo yao yote waliyokwishafanya katika njia zisizo za kitauwa, na kwa maneno yote ya ukali ambayo wasio watauwa wameyanena dhidi yake."
\v 16 Hawa ni wale wanung'unikao, walalamikao ambao hufuata tamaa zao za uovu, wajivunao mno, ambao kwa faida yao hudanganya wengine.
\s5
\v 17 Lakini ninyi, wapenzi, kumbukeni maneno ambayo yalinenwa zamani na mitume wa Bwana Yesu Kristo.
\v 18 Walisema kwenu, "Katika wakati wa mwisho kutakuwa na watu wanaodhihaki ambao hufuata tamaa zao zisizo za kitauwa."
\v 19 Watu hawa ni watenganishaji, wanatawaliwa na tamaa za asili, na hawana Roho.
\s5
\v 20 Lakini ninyi, wapenzi, kama mjijengavyo katika imani yenu takatifu sana, na kama muombavyo katika Roho Mtakatifu,
\v 21 jitunzeni katika upendo wa Mungu, na msubiri rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo huwapatia uzima wa milele.
\s5
\v 22 Onesheni rehema kwa wale walio na shaka.
\v 23 Waokoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka katika moto. Kwa wengine onesheni huruma kwa hofu, mkichukia hata vazi lililotiwa doa na mwili.
\s5
\v 24 Sasa kwake awezaye kuwalinda msijikwae, na kuwasababisha msimame mbele ya utukufu wake, bila mawaa na kuwa na furaha kuu,
\v 25 kwake Mungu pekee mwokozi kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu uwe kwake, ukuu, uwezo na nguvu kabla ya nyakati zote, na sasa na hata milele. Amina.

838
67-REV.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,838 @@
\id REV
\ide UTF-8
\h Ufunuo
\toc1 Ufunuo
\toc2 Ufunuo
\toc3 rev
\mt Ufunuo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana.
\v 2 Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo.
\v 3 Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia.
\s5
\v 4 Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
\v 5 na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mtawala wa wafalme wa dunia hii. Kwake yeye atupendaye na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake,
\v 6 ametufanya kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba yake - kwake kuwa utukufu na nguvu milele daima. Amina.
\s5
\v 7 Tazama, anakuja na mawingu; kila jicho litamwona, pamoja na wote waliomchoma. Na kabila zote za dunia wataomboleza kwake. Ndiyo, Amina.
\v 8 "Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu, "Yeye aliyepo, na aliyekuwepo, na ambaye anakuja, Mwenye nguvu."
\s5
\v 9 Mimi, Yohana - ndugu yenu na mmoja anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu; nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patimo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda kuhusu Yesu.
\v 10 Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana. Nilisikia nyuma yangu sauti ya juu kama ya tarumbeta,
\v 11 ikisema, "andika katika kitabu unayo yaona, na uyatume kwa makanisa saba, kwenda Efeso, kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia."
\s5
\v 12 Nikageuka kuona ni sauti ya nani aliyekuwa akiongea nami, na nilipogeuka niliona kinara cha dhahabu cha taa saba.
\v 13 Katikati ya kinara cha taa alikuwemo mmoja kama Mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu iliyofika chini ya miguu yake, na mkanda wa dhababu kuzunguka kifua chake.
\s5
\v 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji, na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto.
\v 15 Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi.
\v 16 Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kutoka kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa uking'aa kama mwanga mkali wa jua.
\s5
\v 17 Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, "Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho,
\v 18 na ambaye ninaishi. Nalikuwa nimekufa, lakini tazama, ninaishi milele! Na ninazo funguo za mauti na kuzimu.
\s5
\v 19 Kwa hiyo, yaandike uliyoyaona, yaliyopo sasa, na yale yatakayotokea baada ya haya.
\v 20 Kwa maana iliyojificha kuhusu nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na kile kinara cha dhahabu cha taa saba: nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na kinara cha taa saba ni yale makanisa saba."
\s5
\c 2
\p
\v 1 "Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, "
\v 2 '"Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.
\s5
\v 3 Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado.
\v 4 Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza.
\v 5 Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.
\s5
\v 6 Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia.
\v 7 Kama una sikio, sikiliza yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.'
\s5
\v 8 "Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: 'Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena:
\v 9 '"Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).
\s5
\v 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima.
\v 11 Kama una sikio, sikiliza Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.'
\s5
\v 12 "Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: 'Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
\v 13 '"Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.
\s5
\v 14 Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu na kuzini.
\v 15 Katika hali iyo hiyo, hata wewe unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.
\s5
\v 16 Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu.
\v 17 Kama una sikio, sikiliza Roho anachowaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu ya jiwe, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.'
\s5
\v 18 "Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: "Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana:
\v 19 '"Najua ambacho umefanya - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.
\s5
\v 20 Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita mwenyewe nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.
\v 21 Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.
\s5
\v 22 Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu kwa alichofanya.
\v 23 Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na tamaa. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.
\s5
\v 24 Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, 'sitaweka juu yenu mzigo wowote.'
\v 25 Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.
\s5
\v 26 Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa.
\v 27 'Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.'
\v 28 Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi.
\v 29 Ukiwa na sikio, sikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.'
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa malaika wa kanisa la Sardi andika: 'Maneno ya yule anayeshikilia zile roho saba za Mungu na nyota saba. "Najua ambacho umefanya. Una sifa ya kuwa hai, lakini u-mfu.
\v 2 Amka na kuimarisha yaliyosalia, lakini yako karibu kufa, kwa sababu sikuyaona matendo yako yamekamilika machoni pa Mungu wangu.
\s5
\v 3 Kwa hiyo, kumbuka, yale uliyoyapokea na kusikia. Yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwivi, na hutajua saa ipi nitakayokuja juu yako.
\v 4 Lakini kuna majina machache ya watu katika Sardi ambao hawakuchafua nguo zao. Watatembea pamoja nami, wamevaa nguo nyeupe, kwa sababu wanastahili.
\s5
\v 5 Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe, na kamwe sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, na nitalitaja jina lake mbele ya Baba yangu, na mbele ya malaika.
\v 6 Ukiwa na sikio, sikiliza Roho ayaambiavyo makanisa."
\s5
\v 7 "Kwa malaika wa kanisa la Philadefia andika: Maneno ya aliye mtakatifu na kweli - aliye na funguo za Daudi, hufungua na hakuna afungaye, hufunga na hakuna awezaye kufungua.
\v 8 Najua ambacho umetenda. Tazama, nimekuwekea mbele yako mlango uliofunguliwa ambao hakuna awezaye kuufunga. Najua unazo nguvu kidogo, lakini umelitii neno langu na hujalikana jina langu.
\s5
\v 9 Angalia! Wote walio wa sinagogi la shetani, wale wasemao wao ni Wayahudi na kumbe siyo, badala yake wanadanganya. Nitawafanya waje na kusujudu mbele ya miguu yako, na watajua ya kuwa nilikupenda.
\v 10 Kwa kuwa umetunza amri yangu kwa uvumilivu wa uthabiti, nitakulinda pia katika saa yako ya kujaribiwa ambayo inakuja katika ulimwengu wote, kuwajaribu wale wote wanaoishi katika nchi.
\v 11 Naja upesi. Shikilia sana kile ulichonacho ili asiwepo mtu wa kuitwaa taji yako.
\s5
\v 12 Nitamfanya yeye ashindaye kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka nje kamwe. Nitaliandika kwake jina la Mungu wangu, jina la mji wa Mungu wangu (Yerusalemu mpya, ushukao chini toka mbinguni kwa Mungu wangu), na jina langu jipya.
\v 13 Yeye aliye na sikio, na asikie ambacho Roho anasema kwa makanisa.'
\s5
\v 14 "Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika: 'Maneno yake aliye Amina, wakutegemewa na shahidi mwaminifu, mtawala juu ya uumbaji wa Mungu.
\v 15 Najua ambacho umefanya, na kwamba wewe si baridi wala moto, natamani kwamba ungekuwa wa baridi au moto!
\v 16 Hivyo, kwa sababu wewe ni vuguvugu, si moto wala baridi, nitakutapika utoke kinywani mwangu.
\s5
\v 17 Kwa kuwa unasema, "Mimi ni tajiri, nimekuwa na mali nyingi, na sihitaji chochote." Lakini hujui kwamba wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi.
\v 18 Sikiliza ushauri kwangu: Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri, na nguo nyeupe za kumetameta ili ujivike mwenyewe na usioneshe aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka katika macho yako upate kuona.
\s5
\v 19 Kila nimpendaye, namwelekeza na kuwafundisha namna iwapasavyo kuishi; kwa hiyo, kuwa mkweli na kutubu.
\v 20 Tazama nasimama katika mlango na kubisha. Yeyote asikiaye sauti yangu na kufungua mlango, nitakuja na kuingia nyumbani kwake, na kula chakula naye na yeye pamoja nami.
\s5
\v 21 Yeye ashindaye, nitampa haki ya kukaa chini pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na kukaa chini pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi.
\v 22 Yeye aliye na sikio, na asikilize ambacho Roho ayaambia makanisa."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Baada ya mambo haya nilitazama, nikaona kuwa mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni. Ile sauti ya kwanza, ikizungumza nami kama tarumbeta, ikisema, "Njoo hapa, nitakuonesha yatakayotokea baada ya mambo haya."
\v 2 Mara moja nilikuwa katika Roho, niliona kulikuwa na kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mtu amekikalia.
\v 3 Mmoja aliyekuwa amekikalia alionekana kama jiwe la yaspi na akiki. Kulikuwa na upinde wa mvua umekizunguka kiti cha enzi. Upinde wa mvua ulionekana kama zumaridi.
\s5
\v 4 Kukizunguka kiti cha enzi kulikuwa na viti vya enzi vingine ishirini na vinne, na waliokaa kwenye viti vya enzi walikuwa wazee ishirini na wanne, wamevikwa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao.
\v 5 Kutoka katika kiti cha enzi kulitoka miale ya radi, muungurumo na radi. Taa saba zilikuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi, taa ambazo ni roho saba za Mungu.
\s5
\v 6 Tena mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na bahari, iliyowazi kama kioo. Wote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa na wenye uhai wanne, waliojaa macho mbele na nyuma.
\s5
\v 7 Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, kiumbe wa pili mwenye uhai alikuwa kama ndama, kiumbe wa tatu mwenye uhai alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na yule mwenye uhai wa nne alikuwa kama tai apaaye.
\v 8 Viumbe wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita, wamejaa macho juu na chini yake. Usiku na mchana hawakomi kusema, "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, mtawala juu ya wote, aliyekuwepo, na aliyepo na atakayekuja."
\s5
\v 9 Kila wakati viumbe wenye uhai walipotoa utukufu, heshima, na kushukuru mbele za aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele na daima,
\v 10 wazee ishirini na wanne walisujudu wenyewe mbele yake aliyekikalia kiti cha enzi. Waliinama chini kwake aishiye milele na daima na kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema,
\v 11 "Wastahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Kwa kuwa uliviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako, vilikuwepo na viliumbwa."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyekuwa amekaa katika kiti cha enzi, gombo lililoandikwa mbele na nyuma, na lilikuwa limetiwa mihuri saba.
\v 2 Nilimwona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kubwa, "Nani astahiliye kulifungua gombo na kuzivunja mihuri yake?"
\s5
\v 3 Hakuna mtu mbinguni au duniani au chini ya dunia aliyeweza kulifungua gombo au kulisoma.
\v 4 Nililia kwa uchungu kwa kuwa hakupatikana yeyote aliyestahili kulifungua gombo au kulisoma.
\v 5 Lakini mmoja wa wazee akaniambia, "Usilie. Tazama! Simba wa kabila ya Yuda, shina la Daudi, ameshinda, na anaweza kulifungua gombo na mihuri yake saba."
\s5
\v 6 Kati ya kiti cha enzi na wenye uhai wanne na miongoni mwa wazee, niliona mwanakondoo amesimama, akionekana kama aliye uawa. Alikuwa na pembe saba na macho saba - hizi ni roho saba za Mungu zilizotumwa duniani kote.
\v 7 Akaenda akalichukua gombo kutoka katika mkono wa kuume wa yule aliye kaa katika kiti cha enzi.
\s5
\v 8 Alipolichukua gombo, wenye uhai wanne na wazee ishirini na wanne wakainama hadi nchi mbele ya mwanakondoo. Kila mmoja alikuwa na kinubi na bakuli ya dhahabu iliyojaa uvumba ambayo ni maombi ya waamini.
\s5
\v 9 Waliimba wimbo mpya: "Unastahili kulitwaa gombo na kuzifungua muhuri zake. Kwa kuwa ulichinjwa, na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu wa kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
\v 10 Ukawafanya ufalme na makuhani kwa ajili ya kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala juu ya nchi."
\s5
\v 11 Kisha nilitazama na nikasikia sauti ya malaika wengi kuzunguka kiti cha enzi - idadi yao ilikuwa 200, 000, 000 na wenye uhai na wazee.
\v 12 Wakasema kwa sauti kuu, "Astahili mwanakondoo ambaye amechinjwa kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na sifa."
\s5
\v 13 Nikasikia kila kilichoumbwa kilichokuwa mbinguni na duniani na chini ya nchi na juu ya bahari, kila kitu ndani yake kikisema, "Kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na kwa mwanakondoo, kuwe sifa, heshima, utukufu na nguvu ya kutawala milele na milele."
\v 14 Wenye uhai wanne wakasema, "Amina!" na wazee wakainama chini na kuabudu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Nikatazama wakati mwanakondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema kwa sauti iliyofanana na radi, "Njoo!"
\v 2 Nikatazama na palikuwa na farasi mweupe! Aliyempanda alikuwa na bakuli, na akapewa taji. Alitokea kama mshindi ashindaye ili ashinde.
\s5
\v 3 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri wa pili, nikasikia mwenye uhai wa pili akisema, "Njoo!"
\v 4 Kisha farasi mwingine akatokea - mwekundu kama moto. Aliye mpanda alipewa ruhusa ya kuondoa amani duniani, ili kwamba watu wachinjane. Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa.
\s5
\v 5 Wakati mwanakondoo alipofungua ule muhuri wa tatu, nikasikia mwenye uhai wa tatu akisema, "Njoo!" Nikaona farasi mweusi, na aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
\v 6 Nikasikia sauti iliyoonekana kuwa ya mmoja wa wale wenye uhai ikisema, "kibaba cha ngano kwa dinari moja na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiyadhuru mafuta na divai."
\s5
\v 7 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya nne, nilisikia sauti ya mwenye uhai wa nne ikisema, "Njoo!"
\v 8 Kisha nikaona farasi wa kijivu. Aliye mpanda aliitwa jina lake mauti, na kuzimu ilikuwa ikimfuata. Walipewa mamlaka juu ya robo ya nchi, kuua kwa upanga, kwa njaa na kwa ugonjwa, na kwa wanyama wa mwitu katika nchi.
\s5
\v 9 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya tano, niliona chini ya madhabahu roho za wale waliokuwa wameuawa kwa sababu ya neno la Mungu na kutokana na ushuhuda walioushika kwa uthabiti.
\v 10 Wakalia kwa sauti kuu, "mpaka lini, Mtawala wa vyote, mtakatifu na mkweli, utahukumu wakaao juu ya nchi, na kulipiza kisasi damu yetu?"
\v 11 Kisha kila mmoja alipewa kanzu nyeupe na wakaambiwa kuwa wanapaswa kusubiri kidogo hata itakapotimia hesabu kamili ya watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume itakapotimia ambao watauawa, kama vile ambavyo wao waliuawa.
\s5
\v 12 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya sita, nilitazama na palikuwa na tetemeko kuu. Jua likawa jeusi kama gunia la singa, na mwezi mzima ukawa kama damu.
\v 13 Nyota za mbinguni zikaanguka katika nchi, kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga.
\v 14 Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa. Kila mlima na kisiwa vilihamishwa mahali pake.
\s5
\v 15 Kisha wafalme wa nchi na watu maarufu na majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mmoja aliye mtumwa na huru, wakajificha katika mapango na katika miamba ya milima.
\v 16 Wakaiambia milima na miamba, "Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo.
\v 17 Kwa kuwa siku kuu ya gadhabu yao imewadia, na ni nani awezaye kusimama?"
\s5
\c 7
\p
\v 1 Baada ya haya niliona malaika wanne wamesimama kwenye kona nne za dunia, wamezuia pepo nne za nchi kwa nguvu ili kwamba pasiwe na upepo unaovuma katika nchi, juu ya bahari au dhidi ya mti wowote.
\v 2 Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari:
\v 3 "Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu."
\s5
\v 4 Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144, 000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel:
\v 5 12, 000 kutoka katika kabila ya Yuda walitiwa muhuri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Rubeni, 12, 000 kutoka katika kabila ya Gadi.
\v 6 12, 000 kutoka katika kabila ya Asheri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Naftali, 12, 000 kutoka katika kabila ya Manase.
\s5
\v 7 12, 000 kutoka kabila ya Simioni, 12, 000 kutoka kabila ya Lawi, 12, 000 kutoka kabila ya Isakari,
\v 8 12, 000 kutoka kabila ya Zebuloni, 12, 000 kutoka kabila ya Yusufu, na 12, 000 kutoka kabila ya Benyamini walitiwa muhuri.
\s5
\v 9 Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao,
\v 10 na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: "Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!"
\s5
\v 11 Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu,
\v 12 wakisema, "Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!"
\s5
\v 13 Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, "hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi?
\v 14 Nikamwambia, "Bwana mkubwa, unajua wewe," na akaniambia, "Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.
\s5
\v 15 Kwa sababu hii, wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanamwabudu yeye usiku na mchana katika hekalu lake. Yeye aliye keti juu ya kiti cha enzi atasambaza hema yake juu yao.
\v 16 Hawataona njaa tena, wala kiu tena. Jua halitawachoma, wala joto la kuunguza.
\v 17 Kwa kuwa Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, na atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima, na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati Mwanakondoo alipofungua muhuri ya saba, kukawa na ukimya mbinguni takribani nusu saa.
\v 2 Kisha nikaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, na wakapewa tarumbeta saba.
\s5
\v 3 Malaika mwingine akaja, ameshikilia bakuli ya dhahabu yenye uvumba, amesimama madhabahuni. Akapewa uvumba mwingi ili kwamba autoe pamoja na maombi ya waamini wote katika madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi.
\v 4 Moshi wa ule uvumba, pamoja na maombi ya waamini, ukapanda juu mbele za Mungu kutoka mkononi mwa malaika.
\v 5 Malaika akatwaa bakuli la uvumba na akalijaza moto kutoka kwenye madhabahu. Kisha akalitupa chini juu ya nchi, na kukatokea sauti za radi, miale ya radi na tetemeko la nchi.
\s5
\v 6 Wale malaika saba ambao walikuwa na tarumbeta saba wakawa tayari kuzipiga.
\v 7 Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, na kukatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyikana na damu. Vikatupwa chini katika nchi ili kwamba theluthi yake iungue, theluthi ya miti ikaungua na nyasi zote za kijani zikaungua.
\s5
\v 8 Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake, na kitu kama mlima mkubwa uliokuwa unaungua kwa moto ukatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu,
\v 9 theluthi ya viumbe hai katika bahari vikafa, na theluthi ya meli zikaharibiwa.
\s5
\v 10 Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ikimulika kama kurunzi, juu ya theluthi ya mito na chemichemi za maji.
\v 11 Jina la nyota ni pakanga. Theluthi ya maji ikawa pakanga, na watu wengi wakafa kutokana na maji yaliyokuwa machungu.
\s5
\v 12 Malaika wa nne alipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua ikapigwa, pamoja na theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota. Kwa hiyo theluthi ya vyote ikageuka kuwa giza; theluthi ya mchana na theluthi ya usiku havikuwa na mwanga.
\s5
\v 13 Nilitazama, na nikasikia tai aliye kuwa anaruka katikati ya anga, akiita kwa sauti kuu, "Ole, ole, ole, kwa wale wakaao katika nchi, kwa sababu ya mlipuko wa tarumbeta iliyosalia ambayo imekaribia kupigwa na malaika watatu."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha malaika wa tano alipiga tarumbeta yake. Niliona nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka kwenye dunia. Nyota ilipewa ufunguo wa shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho.
\v 2 Alifungua shimo lisilo na kikomo, na moshi ukapanda juu kwa safu kutoka ndani ya shimo kama moshi kutoka katika tanuru kubwa. Jua na anga vilibadilika vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka shimoni.
\s5
\v 3 Ndani ya moshi nzige walitoka kuja juu ya dunia, nao walipewa nguvu kama ile ya nge juu ya dunia.
\v 4 Waliambiwa kutokudhuru majani katika nchi au mmea wowote wa kijani au mti, isipokuwa tu watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu katika paji za nyuso zao.
\s5
\v 5 Hawakupewa ruhusa ya kuwaua hao watu, bali kuwatesa tu kwa miezi mitano. Uchungu wao ulikuwa kama ule wa kuumwa na nge amwumapo mtu.
\v 6 Katika siku hizo watu watatafuta kifo, lakini hawatakipata. Watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.
\s5
\v 7 Nzige walifanana na farasi walioandaliwa kwa vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji ya dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
\v 8 Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba.
\v 9 Walikuwa na vifua kama vifua vya chuma na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari mengi ya vita na farasi wakimbiao kwenda vitani.
\s5
\v 10 Walikuwa na mikia inayouma kama nge; katika mikia yao walikuwa na nguvu ya kudhuru watu kwa miezi mitano.
\v 11 Walikuwa naye kama mfalme juu yao malaika wa shimo lisilokuwa na mwisho. Jina lake katika Kiebrania ni Abadoni, na katika Kiyunani ana jina Apolioni.
\v 12 Ole ya kwanza imepita. Angalia! Baada ya hili kuna maafa mawili yaja.
\s5
\v 13 Malaika wa sita alipiga tarumbeta yake, na nikasikia sauti ikitoka katika pembe ya madhabahu ya dhahabu ambayo iko mbele za Mungu.
\v 14 Sauti ilimwambia malaika wa sita aliyekuwa na tarumbeta, "Waachie malaika wanne ambao wamefungwa katika mto mkubwa Efrata."
\v 15 Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa kwa saa hiyo maalumu, siku hiyo, mwezi huo, na mwaka huo, waliachiwa wawaue theluthi ya wanadamu.
\s5
\v 16 Idadi ya maaskari waliokuwa juu ya farasi ilikuwa 200, 000, 000. Nilisikia idadi yao.
\v 17 Hivi ndivyo nilivyoona farasi katika maono yangu na wale waliopanda juu yao: Vifua vyao vilikuwa vyekundu kama moto, bluu iliyoiva na njano isiyoiva. Vichwa vya farasi vilifanana na vichwa vya simba, na midomoni mwao ulitoka moto, moshi na salfa.
\s5
\v 18 Theluthi ya wanadamu waliuawa na haya mapigo matatu: moto, moshi, na salfa iliyotoka katika midomo yao.
\v 19 Kwa kuwa nguvu ya farasi ilikuwa katika midomo yao na katika mikia yao—kwa kuwa mikia yao ilikuwa kama nyoka, na walikuwa na vichwa ambavyo walitumia kuwatia majeraha wanadamu.
\s5
\v 20 Watu waliobaki, wale ambao walikuwa hawajauawa na mapigo haya, hawakutubia matendo yao waliyokuwa wamefanya, wala hawakuacha kuabudu mapepo na miungu ya dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti—vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia au kutembea.
\v 21 Wala hawakutubia uuaji wao, uchawi wao, uasherati wao au njia zao za wizi.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kisha nikaona malaika mwingine mkuu akishuka chini kutoka mbinguni. Alikuwa amefungwa katika wingu, na kulikuwa na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake ulikuwa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto.
\v 2 Alishikilia gombo dogo katika mkono wake lililokuwa limefunuliwa, naye aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari na mguu wake wa kushoto juu ya nchi kavu.
\s5
\v 3 Kisha alipaza sauti ya juu kama simba aungurumapo, na wakati alipopaza sauti radi saba ziliunguruma.
\v 4 Wakati radi saba zilipounguruma, nilikuwa nakaribia kuandika, lakini nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Tunza iwe siri kile ambacho radi saba zimesema. Usiiandike."
\s5
\v 5 Kisha malaika niliyemwona amesimama juu ya bahari na nchi kavu, aliinua mkono wake juu mbinguni
\v 6 na kuapa kwa yule aishiye milele na milele —aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo, na bahari na vyote vilivyomo: "Hakutakuwepo kuchelewa tena.
\v 7 Lakini katika siku ile, wakati malaika wa saba atakapokaribia kupiga tarumbeta yake, ndipo siri ya Mungu itakuwa imetimizwa, kama alivyotangaza kwa watumishi wake manabii."
\s5
\v 8 Sauti niliyosikia kutoka mbinguni iliniambia tena: "Nenda, chukua gombo dogo lililofunuliwa ambalo kiko katika mkono wa malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu."
\v 9 Kisha nilikwenda kwa malaika na kumwambia anipe gombo dogo. Aliniambia, "Chukua gombo na ule. Litalifanya tumbo lako liwe na uchungu, lakini katika mdomo wako litakuwa tamu kama asali."
\s5
\v 10 Nilichukua gombo dogo kutoka mkononi mwa malaika na kulila. Lilikuwa kitamu kama asali katika mdomo wangu, lakini baada ya kula, tumbo langu lilikuwa na uchungu.
\v 11 Kisha baadhi ya sauti ziliniambia, "Unapaswa kutabiri tena kuhusu watu wengi, mataifa, lugha, na wafalme."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Nilipewa mwanzi wa kutumia kama fimbo ya kupimia. Niliambiwa, "Ondoka na ukapime hekalu la Mungu na madhabahu, na wale wanaoabudu ndani yake.
\v 2 Lakini usipime eneo la ua wa nje ya hekalu, kwa kuwa wamepewa watu wa Mataifa. Wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
\s5
\v 3 Nitawapa mashahidi wangu wawili mamlaka ya kutabiri kwa muda wa siku 1, 260, wakiwa wamevaa magunia."
\v 4 Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili ambavyo vimesimama mbele ya Bwana wa dunia.
\v 5 Kama mtu yeyote ataamua kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao. Yeyote anayetaka kuwadhuru lazima auawe kwa njia hii.
\s5
\v 6 Hawa mashahidi wana uwezo wa kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe wakati wanatabiri. Wana nguvu ya kubadili maji kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo wakati wowote wakitaka.
\v 7 Wakati watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama anayetoka kwenye shimo lisilo na mwisho atafanya vita dhidi yao. Atawashinda na kuwaua.
\s5
\v 8 Miili yao italala katika mtaa wa mji mkuu (ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri) ambapo Bwana wao alisulubiwa.
\v 9 Kwa siku tatu na nusu baadhi kutoka katika jamaa za watu, kabila, lugha na kila taifa watatazama miili yao na hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi.
\s5
\v 10 Wale wanaoishi katika nchi watafurahi kwa ajili yao na kushangilia, hata kutumiana zawadi kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nchi.
\v 11 Lakini baada ya siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia nao watasimama kwa miguu yao. Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona.
\v 12 Kisha watasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, "Njoni huku!" Nao watakwenda juu mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakitazama.
\s5
\v 13 Katika saa hiyo kutakuwepo na tetemeko kuu la ardhi na moja ya kumi ya mji itaanguka. Watu elfu saba watauawa katika tetemeko na watakaobaki hai wataogopeshwa na kumpa utukufu Mungu wa mbinguni.
\v 14 Ole ya pili imepita. Angalia! Ole ya tatu inakuja upesi.
\s5
\v 15 Kisha malaika wa saba alipiga tarumbeta yake, na sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema, "Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake. Atatawala milele na milele."
\s5
\v 16 Kisha wazee ishirini na wanne waliokuwa wameketi kwenye viti vya enzi mbele ya Mungu walianguka wenyewe chini kwenye ardhi, nyuso zao zimeinama chini, nao walimwabudu Mungu.
\v 17 Walisema, "Twatoa shukrani zetu kwako, Bwana Mungu, mtawala juu ya vyote, ambaye upo na ambaye ulikuwepo, kwa sababu umetwaa nguvu yako kuu na kuanza kutawala.
\s5
\v 18 Mataifa walikasirika, lakini gadhabu yako imekuja. Wakati umefika kwa wafu kuhukumiwa na wewe kuwazawadia watumishi wako manabii, waamini na wale walio na hofu ya jina lako, wote wawili wasiofaa kitu na wenye nguvu. Na wakati wako umefika wa kuwaharibu wale ambao wamekuwa wakiiharibu dunia."
\s5
\v 19 Kisha hekalu la Mungu mbinguni lilifunuliwa na sanduku la agano lake lilionekana ndani ya hekalu lake. Kulikuwa na miali ya mwanga, kelele, ngurumo za radi, tetemeko la ardhi na mawe ya mvua.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ishara kuu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyefunikwa na jua, na akiwa na mwezi chini ya miguu yake; na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa juu ya kichwa chake.
\v 2 Alikuwa na mimba na alikuwa analia kwa ajili ya maumivu ya kuzaa—katika uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 3 Na ishara nyingine ilionekana mbinguni: Tazama! Kulikuwa na joka mwekundu mkubwa ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kulikuwa na taji saba kwenye vichwa vyake.
\v 4 Mkia wake ulikokota theluthi moja ya nyota mbinguni na kuzitupa chini duniani. Joka alisimama mbele ya mwanamke aliyekuwa anakaribia kuzaa, ili kwamba wakati anazaa, apate kummeza mtoto wake.
\s5
\v 5 Alimzaa mwana, mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Mtoto wake alinyakuliwa juu kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi,
\v 6 na mwanamke alikimbilia nyikani, mahali ambapo Mungu alikuwa ameandaa eneo kwa ajili yake, ili aweze kuhudumiwa kwa siku 1, 260.
\s5
\v 7 Sasa kulikuwa na vita mbinguni. Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka; naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana nao.
\v 8 Lakini joka hakuwa na nguvu za kutosha kushinda. Kwa hiyo haikuwepo tena nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika zake.
\v 9 Joka mkubwa—yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani ambaye hudanganya - dunia nzima akatupwa chini katika dunia, na malaika zake wakatupwa chini pamoja naye.
\s5
\v 10 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni: "Sasa wokovu umekuja, nguvu—na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini—ambaye aliwashitaki mbele za Mungu wetu mchana na usiku.
\s5
\v 11 Walimshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao, kwa maana hawakupenda sana maisha yao, hata kufa.
\v 12 Kwa hiyo, shangilieni, ninyi mbingu, na wote mnaokaa ndani yake. Lakini ole wa nchi na bahari kwa sababu mwovu ameshuka kwenu. Amejawa na hasira kali, kwa sababu anajua kwamba ana muda mchache tu.
\s5
\v 13 Wakati joka alipotambua kuwa ametupwa chini kwenye nchi, alimfuata mwanamke ambaye alikuwa amezaa mtoto wa kiume.
\v 14 Lakini mwanamke alipewa mabawa mawili ya tai mkubwa, ili kwamba aweze kuruka hadi kwenye eneo lililoandaliwa kwa ajili yake kule jangwani, eneo ambalo angeweza kutunzwa, kwa wakati, nyakati na nusu wakati-mahali asipoweza kupafikia huyo nyoka.
\s5
\v 15 Nyoka alimwaga maji kutoka mdomoni mwake kama mto, ili afanye gharika ya kumgharikisha.
\v 16 Lakini ardhi ilimsaidia mwanamke. Ilifunua kinywa chake na kuumeza mto alioutema joka kutoka kinywani mwake.
\v 17 Kisha joka akamkasirikia mwanamke naye aliondoka na kufanya vita na uzao wake wote—wale wanaotii amri za Mungu na kushikilia ushuhuda kuhusu Yesu.
\v 18 Kisha joka alisimama juu ya mchanga ufukwe wa bahari.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu.
\v 2 Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, na katika kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.
\s5
\v 3 Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama.
\v 4 Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, "Nani kama mnyama? na "Nani atapigana naye?"
\s5
\v 5 Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili.
\v 6 Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.
\s5
\v 7 Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa.
\v 8 Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.
\s5
\v 9 Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize.
\v 10 Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.
\s5
\v 11 Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka.
\v 12 Alionyesha mamlaka yote katika mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wakimuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.
\s5
\v 13 Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu,
\v 14 na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.
\s5
\v 15 Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe.
\v 16 Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso.
\v 17 Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.
\s5
\v 18 Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Nilitazama na nikaona Mwana Kondoo amesimama mbele yangu juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa 144, 000 wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
\v 2 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisikika kama ngurumo za maji mengi na sauti kubwa ya radi. Sauti niliyoisikia ni kama wapiga vinubi wapigao vinubi vyao.
\s5
\v 3 Wakiimba wimbo mpya mbele za kiti cha enzi na mbele za wenye uhai wanne na wazee. Hakuna hata mwenye uwezo wa kujifunza huo wimbo isipokuwa kwa 144, 000 ambao wamekombolewa kutoka duniani.
\v 4 Hawa ni wale ambao hawakujichafua wenyewe kwa wanawake, maana walijitunza wenyewe dhidi ya matendo ya zinaa. Ni hawa ambao walimfuata Mwana Kondoo popote alipoenda. Hawa walikombolewa kutoka kwa wanadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo.
\v 5 Hakuna uongo uliopatikana katika vinywa vyao; hawalaumiwi.
\s5
\v 6 Nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, ambaye mwenye ujumbe wa mbinguni wa habari njema kwa kuwatangazia wenye kuishi duniani kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu.
\v 7 Akawaita kwa sauti kuu, "Mwogopeni Mungu na mpeni utukufu. Kwa maana muda wa hukumu umekaribia. Mwabuduni yeye, yeye aliyeumba mbingu, na dunia, na bahari, na chemchemi za maji."
\s5
\v 8 Malaika mwingine - malaika wa pili - akafuata akisema, "Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu, ambaye uliwanywesha mataifa divai ya ukahaba, divai ambayo ilileta ghadhabu juu yake."
\s5
\v 9 Malaika mwingine - malaika wa tatu - aliwafuata, akasema kwa sauti kuu, "Yeyote atakayemwabudu huyo mnyama na sanamu yake, na kupokea alama katika paji lake la uso au mkononi,
\v 10 yeye pia atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu, divai ambayo imeandaliwa na kumwagwa bila kuchanganywa katika kikombe cha hasira yake. Mtu atakayekunywa atateswa kwa moto na moto wa kiberiti mbele za malaika zake watakatifu na mbele za Mwana Kondoo.
\s5
\v 11 Na moshi wa maumivu yao ukaenda milele na milele, na hawakuwa na mapumziko mchana au usiku - hao waabuduo mnyama na sanamu yake, na kila mtu aliyepokea alama ya jina lake.
\v 12 Huu ni wito wa subira na uvumilivu kwa waamini, wale ambao hutii amri za Mungu na imani katika Yesu."
\s5
\v 13 Nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Andika haya: Heri wafu wafao katika Bwana." "Ndiyo," asema Roho, "ili waweze kupumzika kutoka kwenye kazi zao, maana matendo yao yatawafuata."
\s5
\v 14 Nilitazama na nikaona kulikuwa na wingu jeupe, na aliyeketi kwenye wingu ni mmoja aliyekuwa na mfano wa Mwana wa Mtu. Alikuwa na taji ya dhahabu katika kichwa chake na mundu mkali katika mkono wake.
\v 15 Malaika mwingine tena alikuja kutoka kwenye hekalu na aliita kwa sauti kuu kwenda kwa yule aliyekaa katika wingu: "Chukua mundu wako na uanze kuvuna. Kwa kuwa muda wa mavuno umeshawadia, maana mavuno yaliyo katika dunia yameshaiva."
\v 16 Tena yule aliyekuwa kwenye wingu aliupitisha mundu wake juu ya dunia, na dunia ikavunwa.
\s5
\v 17 Na malaika mwingine akaja kutoka kwenye hekalu la mbinguni; naye alikuwa na mundu mkali.
\v 18 Na bado malaika mwingine akaja kutoka kwenye madhabahu, na malaika aliyekuwa na mamlaka juu ya moto. Akamwita kwa sauti kuu malaika ambaye alikuwa na mundu mkali, "Chukua mundu mkali na uyakusanye matawi ya mzabibu kutoka kwenye mzabibu wa nchi, kwa kuwa zabibu sasa zimeiva."
\s5
\v 19 Malaika alipeleka mundu wake katika dunia na alikusanya mavuno ya zabibu ya dunia na alirusha katika pipa kubwa la divai ya ghadhabu ya Mungu.
\v 20 Chujio la divai lilipondwapondwa nje ya mji na damu ikamwagika kutoka katika hicho kimo cha hatamu ya farasi, kwa stadia 1, 600.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Tena nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na yenye kushangaza; Kulikuwa na malaika saba wenye mapigo saba, ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho (katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika).
\s5
\v 2 Niliona kile kilichotokea kuwa bahari ya bilauri iliyochanganywa na moto, na ikasimama pembeni mwa bahari ambapo wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake, na juu ya namba inayowakilisha jina lake. Walikuwa wameshikilia vinubi walivyopewa na Mungu.
\s5
\v 3 Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo: "Kazi zako ni kubwa na zenye kushangaza, Bwana Mungu, utawalaye vyote. Mwaminifu na njia zako ni za kweli, Mfalme wa mataifa.
\v 4 Nani atashindwa kukuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu mbele zako kwa sababu u mwema na matendo yako yamejulikana."
\s5
\v 5 Baada ya mambo hayo nilitazama, na sehemu takatifu sana, ambapo palikuwa na hema ya ushuhuda, iliyofungukia mbinguni.
\v 6 Kutoka mahali patakatifu sana wakaja malaika saba wenye mapigo saba, wamevaa mavazi safi, kitani yenye kung'aa na mshipi wa dhahabu kuzunguka vifua vyao.
\s5
\v 7 Mmoja wa wale wenye uhai wanne akatoa kwa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu mwenye kuishi milele na milele.
\v 8 Mahali patakatifu sana kulijawa moshi kutoka kwenye utukufu wa Mungu na kutoka kwenye uwezo wake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nikasikia sauti kubwa ikiita kutoka kwenye sehemu ya patakatifu na ikasema kwa wale malaika saba, "Nenda na ukamwage juu ya dunia mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu."
\s5
\v 2 Malaika wa kwanza alienda na kumwaga bakuli lake katika dunia; majeraha mabaya na yenye maumivu makali yalikuja kwa watu wenye alama ya mnyama, kwa wale ambao waliabudu sanamu yake.
\s5
\v 3 Malaika wa pili alimwaga bakuli lake katika bahari; ikawa kama damu ya mtu aliyekufa, na kila kiumbe hai katika bahari kilikufa.
\s5
\v 4 Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na katika chemichemi za maji; zikawa damu.
\v 5 Nikasikia malaika wa maji akisema, "Wewe ni mwaminifu - mmoja uliyepo na uliyekuwako, Mtakatifu - kwa sababu umezileta hukumu hizi.
\v 6 Kwa sababu walimwaga damu za waamini na manabii, umewapa wao kunywa damu; ndicho wanachostahili."
\v 7 Nikasikia madhabahu ikijibu, "Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki."
\s5
\v 8 Malaika wa nne akamwaga kutoka kwenye bakuli lake juu ya jua, na likapewa ruhusa kuunguza watu kwa moto.
\v 9 Waliunguzwa kwa joto lenye kutisha, na wakalikufuru neno la Mungu, mwenye nguvu juu ya mapigo yote. Hawakutubu wala kumpa yeye utukufu.
\s5
\v 10 Malaika wa tano akamwaga kutoka kwenye bakuli lake katika kiti cha enzi cha mnyama, na giza likaufunika ufalme wake. Walisaga meno katika maumivu makali.
\v 11 Wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na majeraha yao, na bado waliendelea kutokutubu kwa kile walichotenda.
\s5
\v 12 Malaika wa sita alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika mto mkubwa, Frati, na maji yake yakakauka ili kuweza kuandaa njia kwa wafalme watakaokuja kutoka mashariki.
\v 13 Nikaona roho tatu chafu zilizoonekana kama chura watokao nje ya mdomo wa yule joka, yule mnyama, na yule nabii wa uongo.
\v 14 Ni roho za pepo zitendazo ishara na miujiza. Walikuwa wakienda kwa wafalme wa dunia yote ili kuweza kuwakusanya pamoja kwa vita katika siku kuu ya Mungu, mwenye kutawala juu ya vyote.
\s5
\v 15 ("Tazama! Ninakuja kama mwizi! Heri yule adumuye katika kukesha, atunzaye mavazi yake ili asiweze kwenda nje uchi na kuiona aibu yake.")
\v 16 Waliwaleta pamoja katika sehemu iliyoitwa katika kiebrania Amagedoni.
\s5
\v 17 Malaika wa saba alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika anga. Kisha sauti kuu ikasikika kutoka pakatifu na kutoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, "Imekwisha!"
\v 18 Kulikuwa na miale ya mwanga wa radi, ngurumo, vishindo vya radi, na tetemeko la kutisha - tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea duniani tangu wanadamu wamekuwepo duniani, hivyo ni tetemeko kubwa zaidi.
\v 19 Mji mkuu uligawanyika katika sehemu tatu, na miji ya mataifa ikaanguka. Kisha Mungu akamkumbusha Babeli mkuu, na akaupa mji huo kikombe kilichokuwa kimejaa divai kutoka kwenye ghadhabu yake iliyo kali.
\s5
\v 20 Kila kisiwa kikapotea na milima haikuonekana tena.
\v 21 Mvua kubwa ya mawe, ikiwa na uzito wa talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya watu, na wakamlaani Mungu kwa mapigo ya mvua ya mawe kwa sababu lile pigo lilikuwa baya sana.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, "Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi,
\v 2 ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa."
\s5
\v 3 Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
\v 4 Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake.
\v 5 Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: "BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI."
\s5
\v 6 Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu.
\v 7 Lakini malaika akaniambia, "Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).
\s5
\v 8 Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja.
\s5
\v 9 Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake.
\v 10 Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.
\s5
\v 11 Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na anaenda kwenye uharibifu.
\s5
\v 12 Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama.
\v 13 Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama.
\v 14 Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na katika yeye tuliitwa, tulichaguliwa, waaminifu."
\s5
\v 15 Malaika akaniambia, "Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.
\s5
\v 16 Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto.
\v 17 Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.
\s5
\v 18 Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya vitu hivi nilimwona malaika mwingine akishuka chini kutoka mbinguni. Yeye alikuwa na mamlaka kuu, na nchi iliangazwa kwa utukufu wake.
\v 2 Alilia kwa sauti kuu, akisema, "Umeanguka, umeanguka, ule mji mkuu Babeli! Umekuwa sehemu yakaapo mapepo, na sehemu ikaapo kila roho chafu, na sehemu akaapo kila mchafu na ndege achukizaye.
\v 3 Kwa kuwa mataifa yote yamekunywa mvinyo ya tamaa ya uasherati wake ambayo humletea ghadhabu. Wafalme wa nchi wamezini naye. Wafanyabiashara wa nchi wamekuwa matajiri kwa nguvu ya maisha yake ya anasa."
\s5
\v 4 Kisha nilisikia sauti nyingine kutoka mbinguni iikisema, "Tokeni kwake watu wangu, ili msije mkashiriki katika dhambi zake, na ili msije mkapokea mapigo yake yoyote.
\v 5 Dhambi zake zimerundikana juu kama mbingu, na Mungu ameyakumbuka matendo yake maovu.
\v 6 Mlipeni kama alivyowalipa wengine, na mkamlipe mara mbili kwa jinsi alivyotenda; katika kikombe alichokichanganya, mchanganyishieni mara mbili kwa ajili yake.
\s5
\v 7 Kama alivyojitukuza yeye mwenyewe, na aliishi kwa anasa, mpeni mateso mengi na huzuni. Kwa kuwa husema moyoni mwake, 'Nimekaa kama malkia; wala siyo mjane, na wala sitaona maombolezo.'
\v 8 Kwa hiyo ndani ya siku moja mapigo yake yatamlemea: kifo, maombolezo, na njaa. Atateketezwa kwa moto, kwa kuwa Bwana Mungu ni mwenye nguvu, na ni mhukumu wake."
\s5
\v 9 Wafalme wa nchi waliozini na kuchanganyikiwa pamoja naye watalia na kumwombolezea watakapouona moshi wa kuungua kwake.
\v 10 Watasimama mbali naye, kwa hofu ya maumivu yake wakisema, "Ole, ole kwa mji mkuu, Babeli, mji wenye nguvu! Kwa saa moja hukumu yako imekuja."
\s5
\v 11 Wafanyabiashara wa nchi lieni na kuomboleza kwa ajili yake, kwa kuwa hakuna hata mmoja anunuaye bidhaa zake tena -
\v 12 bidhaa za dhahabu, fedha, mawe ya thamani, lulu, kitani nzuri, zambarau, hariri, nyekundu, aina zote za miti ya harufu nzuri, kila chombo cha pembe za ndovu, kila chombo kilichotengenezwa kwa miti ya thamani, shaba, chuma, jiwe,
\v 13 mdalasini, viungo, uvumba, manemane, ubani, mvinyo, mafuta, unga mzuri, ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na watumwa, na roho za watu.
\s5
\v 14 Matunda uliyoyatamani kwa nguvu zako yameondoka kutoka kwako. Anasa zako zote na mapambo yametoweka, hayatapatikana tena.
\s5
\v 15 Wafanyabiashara wa vitu hivi waliopata utajiri kwa mapenzi yake watasimama mbali kutoka kwake kwa sababu ya hofu ya maumivu yake, wakilia na sauti ya maombolezo.
\v 16 Wakisema, "Ole, ole mji ule mkuu uliovikwa kitani nzuri, zambarau, na nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani na lulu!"
\v 17 Ndani ya saa moja utajiri wote huo ulitoweka. Kila nahodha wa meli, kila baharia, na wote wanamaji, na wote wafanyao kazi baharini, walisimama mbali.
\s5
\v 18 Walilia walipouona moshi wa kuungua kwake. Walisema, "Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa?"
\v 19 Walitupa mavumbi juu ya vichwa vyao, na walilia, wakitokwa machozi na kuomboleza, "Ole, ole mji mkubwa mahali wote waliokuwa na meli zao baharini walikuwa matajiri kutokana na mali zake. Ndani ya saa moja umeangamizwa."
\v 20 "Furahini juu yake, mbingu, ninyi waumini, mitume, na manabii, kwa maana Mungu ameleta hukumu yenu juu yake!"
\s5
\v 21 Malaika mwenye nguvu aliinua jiwe kama jiwe kuu la kusagia na alilitupa baharini, akisema, "Kwa njia hii, Babeli, ule mji mkuu, utatupwa chini kwa ukatili na hautaonekana tena.
\v 22 Sauti ya vinanda, wanamuziki, wacheza filimbi, na tarumbeta hawatasikika tena kwenu. Wala fundi wa aina yoyote hataonekana kwenu. Wala sauti ya kinu haitasikika tena kwenu.
\s5
\v 23 Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako. Sauti ya bwana harusi na bibi harusi hazitasikiwa tena ndani yako, maana wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, na wa mataifa, wamedanganywa kwa uchawi wako.
\v 24 Ndani yake damu ya manabii na waamini ilionekana, na damu ya wote waliouawa juu ya nchi."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Baada ya mambo haya nilisikia sauti kama ya mlio mkubwa wa kundi kubwa la watu mbinguni ikisema, "Haleluya. Wokovu, utukufu, na nguvu ni vya Mungu wetu.
\v 2 Hukumu zake ni kweli na za haki, kwa kuwa amemhukumu kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uzinzi wake. Amefanya kisasi kwa damu ya watumishi wake, ambayo aliimwaga yeye mwenyewe."
\s5
\v 3 Kwa mara ya pili walisema, "Haleluya! Moshi hutoka kwake milele na milele."
\v 4 Wale wazee ishirini na wanne na viumbe hai wanne wakasujudu na kumwabudu Mungu akaaye kwenye kiti cha enzi. Walikuwa wakisema, "Amina. Haleluya!"
\s5
\v 5 Ndipo sauti ilitoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, "Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha yeye, wote wasio na umuhimu na wenye nguvu."
\s5
\v 6 Ndipo nilisikia sauti kama sauti ya kundi kubwa la watu, kama sauti ya ngurumo ya maji mengi, na kama ngurumo ya radi, ikisema, "Haleluya! Bwana ni Mungu wetu, mtawala juu ya wote, hutawala.
\s5
\v 7 Na tushangilie na kufurahi na kumpa utukufu kwa sababu harusi na sherehe ya Mwana Kondoo imekuja, na bibi harusi yuko tayari."
\v 8 Aliruhusiwa kuvalishwa kitani safi na yenye kung'aa (kitani safi ni matendo ya haki ya waumini).
\s5
\v 9 Malaika akasema nami, "Yaandike haya: Wamebarikiwa walioalikwa kwenye sherehe ya harusi ya Mwana kondoo." Vilevile akaniambia, "Haya ni maneno ya kweli ya Mungu."
\v 10 Nilisujudu mbele ya miguu yake nikamwabudu, lakini akaniambia, "Usifanye hivi! Mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako mwenye kuushika ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu, kwa kuwa ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii."
\s5
\v 11 Kisha niliona mbingu zimefunguka, na tazama kulikuwa na farasi mweupe! Na yule aliyekuwa amempanda anaitwa Mwaminifu na wa Kweli. Huhukumu kwa haki na kufanya vita.
\v 12 Macho yake ni kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake ana taji nyingi. Ana jina lililoandikwa juu yake asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe.
\v 13 Amevaa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aliitwa Neno la Mungu.
\s5
\v 14 Majeshi ya mbinguni yalikuwa yakimfuata juu ya farasi weupe, walivalishwa kitani nzuri, nyeupe na safi.
\v 15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao huyaangamiza mataifa, naye atawatawala kwa fimbo ya chuma. Naye hukanyaga vyombo vya mvinyo kwa hasira kali ya Mungu, hutawala juu ya wote.
\v 16 Naye ameandikwa juu ya vazi lake na katika paja lake jina, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
\s5
\v 17 Niliona malaika amesimama katika jua. Aliwaita kwa sauti kuu ndege wote warukao juu, "Njoni, kusanyikeni pamoja kwenye chakula kikuu cha Mungu.
\v 18 Njoni mle nyama ya wafalme, nyama ya majemedari, nyama ya watu wakubwa, nyama ya farasi na wapanda farasi, na nyama ya watu wote, walio huru na watumwa, wasio na umuhimu na wenye nguvu."
\s5
\v 19 Nilimwona mnyama na wafalme wa nchi pamoja na majeshi yao. Walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kufanya vita na mmoja aliyepanda farasi na jeshi lake.
\v 20 Mnyama alikamatwa na nabii wake wa uongo aliyezifanya ishara katika uwepo wake. Kwa ishara hizi aliwadanganya wale walioipokea chapa ya mnyama na walioisujudia sanamu yake. Wote wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.
\s5
\v 21 Wale waliobaki waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa mmoja aliyepanda juu ya farasi. Ndege wote walikula mizoga ya miili yao.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kisha niliona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
\v 2 Alimshika yule joka, nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi au Shetani, na kumfunga miaka elfu.
\v 3 Alimtupa kwenye shimo lisilo na mwisho, akalifunga na kulitia mhuri juu yake. Hii ilikuwa hivyo ili kwamba asiwadanganye mataifa tena mpaka miaka elfu itakapoisha. Baada ya hapo, ataachiwa huru kwa muda mchache.
\s5
\v 4 Kisha niliona viti vya enzi. Waliokuwa wamevikalia ni wale ambao walikuwa wamepewa mamlaka ya kuhukumu. Vilevile niliona nafsi za wale ambao walikuwa wamekatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda kuhusu Yesu na kwa neno la Mungu. Walikuwa hawajamwabudu mnyama au sanamu yake, na walikataa kupokea alama juu ya paji za nyuso zao au mkono. Walikuja uzimani, na wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu.
\s5
\v 5 Wafu waliobaki hawakuja uzimani mpaka miaka elfu ilipokuwa imeisha. Huu ndio ufufuo wa kwanza.
\v 6 Mbarikiwa na mtakatifu ni mtu yeyote ambaye achukua nafasi katika ufufuo wa kwanza! Mauti ya pili haina nguvu juu ya watu kama hawa. Patakuwa na makuhani wa Mungu na wa Kristo na watatawala na yeye kwa miaka elfu.
\s5
\v 7 Wakati miaka elfu itakapofikia mwisho, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
\v 8 Atakwenda nje kuwadanganya mataifa katika kona nne za dunia -Gogu na Magogu - kuwaleta pamoja kwa ajili ya vita. Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari.
\s5
\v 9 Walikwenda juu kwenye tambarare ya nchi nao walizunguka kambi ya waumini, mji upendwao. Lakini moto ulikuja kutoka mbinguni na kuwaangamiza.
\v 10 Shetani, ambaye aliwadanganya, alitupwa ndani ya ziwa liwakalo kiberiti, ambamo mnyama na nabii wa uongo walikuwa wameshatupwa. Watateswa mchana na usiku milele na milele.
\s5
\v 11 Kisha niliona kiti cha enzi kikubwa cheupe na yule ambaye alikaa juu yake. Dunia na mbingu zilikimbia mbali kutoka katika uwepo wake, lakini hapakuwako nafasi ya wao kwenda.
\v 12 Niliwaona waliokufa - hodari na wasio wa muhimu wamesimama katika kiti cha enzi, na vitabu vilifunuliwa. Kisha kitabu kingine kilifunguliwa - Kitabu cha Uzima. Wafu walihukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya vitabu, matokeo ya kile walichokifanya.
\s5
\v 13 Bahari iliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake. Kifo na kuzimu viliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake, na wafu walihukumiwa kulingana na walichofanya.
\v 14 Kifo na kuzimu zilitupwa ndani ya ziwa la moto. Hii ni mauti ya pili - ziwa la moto.
\v 15 Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa ndani ya Kitabu cha Uzima, alitupwa ndani ya ziwa la moto.*
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimekwishapita, na bahari haikuwepo tena.
\v 2 Niliona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ambao ulikuja chini kutoka mbinguni kwa Mungu, ulioandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
\s5
\v 3 Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, "Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao.
\v 4 Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
\s5
\v 5 Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, "Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya." Alisema, "Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli."
\v 6 Aliniambia, "Mambo haya yalikwisha kupita! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aonaye kiu nitampatia kinywaji bila gharama kutoka katika chemchemi za maji ya uzima.
\s5
\v 7 Yeye ashindaye atayarithi mambo haya, na nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
\v 8 Lakini kama ilivyo kwa waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao itakuwa katika ziwa la moto wa kiberiti uunguzao. Hiyo ndiyo mauti ya pili."
\s5
\v 9 Mmoja wa malaika saba alikuja kwangu, mmoja ambaye alikuwa na mabakuli saba yaliyojaa mapigo saba ya mwisho na alisema, "Njoo hapa. Nitakuonesha bibi harusi, mke wa mwana kondoo."
\v 10 Kisha alinichukua mbali katika Roho kwenye mlima mkubwa na mrefu na alinionesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu.
\s5
\v 11 Yerusalemu ulikuwa na utukufu wa Mungu, na uzuri wake ulikuwa kama kito cha thamani, kama jiwe la kioo safi la yaspi.
\v 12 Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na miwili, pamoja na malaika kumi na wawili milangoni. Juu ya milango palikuwa pameandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli.
\v 13 Upande wa mashariki palikuwa na milango mitatu, upande wa kusini milango mitatu, upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa magharibi milango mitatu.
\s5
\v 14 Kuta za mji zilikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake palikuwa na majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo.
\v 15 Mmoja aliyeongea nami alikuwa na kipimo cha fimbo iliyotengenezwa kwa dhahabu kwa ajili ya kupima mji, milango yake na kuta zake.
\s5
\v 16 Mji uliwekwa ndani ya mraba; urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Alipima mji kwa kipimio cha fimbo, stadia 12, 000 kwa urefu (urefu wake, upana, na kimo vilifanana).
\v 17 Vilevile alipima ukuta wake, unene wake ulikuwa dhiraa 144 kwa vipimo vya kibinadamu (ambavyo pia ni vipimo vya malaika).
\s5
\v 18 Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi na mji wenye dhahabu safi, kama kioo safi.
\v 19 Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa na kila aina ya jiwe la thamani. La kwanza lilikuwa yaspi, la pili lilikuwa yakuti samawi, la tatu lilikuwa kalkedon, la nne zumaridi,
\v 20 la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolitho, la nane zabarajadi, la tisa yakuti ya manjano, la kumi krisopraso, la kumi na moja hiakintho, la kumi na mbili amethisto.
\s5
\v 21 Milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili, kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja. Mitaa ya mji ilikuwa dhahabu safi, ikionekana kama kioo safi.
\v 22 Sikuona hekalu lolote ndani ya mji, kwa kuwa Bwana Mungu, ambaye anatawala juu ya vyote, na Mwana Kondoo ni hekalu lake.
\s5
\v 23 Mji haukuhitaji jua au mwezi ili kungaza juu yake kwa sababu utukufu wa Mungu uliangaza juu yake, na taa yake ni Mwana Kondoo.
\v 24 Mataifa watatembea kwa mwanga wa mji huo. Wafalme wa dunia wataleta fahari zao ndani yake.
\v 25 Milango yake haitafungwa wakati wa mchana, na hapatakuwa na usiku pale.
\s5
\v 26 Wataleta fahari na heshima ya mataifa ndani yake,
\v 27 na hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake. Wala yeyote ambaye afanyaye jambo lolote la aibu au udanganyifu hataingia, bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uzima, maji yalikuwa ya mng'ao kama wa bilauri. Yalikuwa yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo
\v 2 Kupitia katikati ya mtaa wa mji. Katika kila pembe ya mto palikuwa na mti wa uzima, unaozaa aina kumi na mbili za matunda, na huzaa matunda kila mwezi. Majani ya mti ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
\s5
\v 3 Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwemo ndani ya mji, na watumishi wake watamtumikia.
\v 4 Watamuona uso wake, na jina lake litakuwa juu ya vipaji vya nyuso zao.
\v 5 Hapatakuwa na usiku tena; wala hapatakuwa na hitaji la mwanga wa taa au jua kwa sababu Bwana Mungu ataangaza juu yao. Nao watatawala milele na milele.
\s5
\v 6 Malaika akaniambia, "Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana Mungu wa roho za manabii alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake kitakachotokea hivi karibuni."
\v 7 "Tazama! Ninakuja upesi! Amebarikiwa yeye anayeyatii maneno ya unabii wa kitabu hiki."
\s5
\v 8 Mimi, Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Nilipoyasikia na kuyaona, nilianguka chini mwenyewe mbele ya miguu ya malaika kumwabudu, malaika aliyenionesha mambo haya.
\v 9 Akaniambia, "Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi mwenzako, pamoja na ndugu zako manabii, pamoja na wale wanaotii maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!"
\s5
\v 10 Akaniambia, "Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, maana wakati umekaribia.
\v 11 Asiye mwenye haki, aendelee kutokuwa mwenye haki. Ambaye ni mchafu kimaadili, na aendelee kuwa mchafu kimaadili. Mwenye haki, na aendelee kuwa mwenye haki. Aliye mtakatifu, na aendelee kuwa mtakatifu."
\s5
\v 12 "Tazama! Naja upesi. Ujira wangu uko pamoja nami, kumlipa kila mmoja kulingana na alichokifanya.
\v 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
\s5
\v 14 Wamebarikiwa wale waoshao mavazi yao ili kwamba wapate haki ya kula kutoka katika mti wa uzima na kuuingia mji kupitia malangoni.
\v 15 Nje kuna mbwa, wachawi, wazinzi, wauwaji, waabudu sanamu, na kila apendaye na ashuhudiaye ushahidi wa uongo.
\s5
\v 16 Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia kuhusu mambo haya kwa makanisa. Mimi ni mzizi wa uzao wa Daudi, Nyota ya Asubuhi ing'aayo."
\s5
\v 17 Roho na Bibi harusi asema, "Njoo!" Na yeye asikiaye aseme, "Njoo!" Yeyote aliye na kiu, na aje, na yeyote anayetamani, na apate maji ya uzima bure.
\s5
\v 18 Namshuhudia kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Kama yeyote ataongeza katika hayo, Mungu atamuongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
\v 19 Kama mtu yeyote atayaondoa maneno ya kitabu hiki cha unabii, Mungu ataondoa sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo habari zake zimeandikwa ndani ya kitabu hiki.
\s5
\v 20 Yeye ashuhudiaye mambo haya asema, "Ndiyo! Naja upesi." Amina! Njoo, Bwana Yesu!
\v 21 Neema ya Bwana Yesu iwe na kila mtu. Amina.

286
manifest.yaml Normal file
View File

@ -0,0 +1,286 @@
---
dublin_core:
conformsto: 'rc0.2'
contributor:
- "Christina Abraham Kileo"
- "Cloud Roman"
- "Compiler"
- "Daniel Marura Chacha"
- "Danjuma_alfred_h"
- "Dina Roman"
- "Emmanuel Masanja Mbaaga"
- "Emmanuel Nyamalya"
- "Erasmus Peter Malelo"
- "Ezekiel Manala"
- "Fred"
- "Gabriel Gidale"
- "Gabriel Gidale Merus"
- "Gabriel Lwitakubi Mazige"
- "James Semnkai"
- "Jeremiah Masasi"
- "Jesse Katabi Masolwa"
- "John Ojasi"
- "Joyce Gilbert Masasi"
- "Karen Riecks"
- "Ker"
- "Lameck Yakobo Tobotobo"
- "Ev. Lazaro Chalomhola"
- "Laurent Petro Malelo"
- "Lazarus David Chalomhola"
- "Majama, Musa Isaya"
- "Makene Mafwele"
- "Marco Luma Mahushi"
- "Musa Luzali"
- "Pastor John Kerim"
- "Pastor Jordan"
- "Philipo Mussa Kanwelle"
- "Raphael Musa"
- "Rev. Charles Mabisa"
- "Rev. Yohana Batano"
- "Robert Ndalahwa"
- "Sadiki Kulwa"
- "Samson Nungwana"
- "Thobias Kazwanomo"
- "Zelote Loilang'akaki Lukumay"
creator: 'Door43 World Missions Community'
description: 'An unrestricted literal Bible'
format: 'text/usfm'
identifier: 'ulb'
issued: '2017-11-08'
language:
direction: 'ltr'
identifier: 'sw'
title: 'Swahili'
modified: '2017-11-08'
publisher: 'unfoldingWord'
relation:
- 'sw/tn'
- 'sw/tq'
- 'sw/udb'
rights: 'CC BY-SA 4.0'
source:
-
identifier: 'ulb'
language: 'en'
version: '7'
subject: 'Bible'
title: 'Swahili Unlocked Literal Bible'
type: 'bundle'
version: '7.1'
checking:
checking_entity:
- "Rev. Erasmus Peter Malelo"
- "Ev . Mathew Kazimoto"
- "Rev. Dr. David Magoke"
- "Rev. Elias Ndema"
- "Rev. Alex Nyuri"
- "Rev. Gungutu Elias"
- "Rev. Lameck Tobotobo"
- "Rev. Catherin D. Matia"
- "Rev. Yohana S Dutuyi"
- "Rev. Donald Dutuyi"
- "GS. Andrew Gewe"
- "Ev. Ezekiel Daudi"
- "Rev. John Ndaluka"
- "Ev. Moses Malugu"
- "Rev. Moses Eliakim Ndege"
- "Past. Isack A. Gomugo"
- "Past. Mathias William"
- "Rev. Yekonia M. Koko"
- "Rev. Elisande Mhanga"
- "Ev. James A. Makula"
checking_level: '3'
projects:
-
title: 'Mathayo '
versification: 'ufw'
identifier: 'mat'
sort: 40
path: './41-MAT.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Marko '
versification: 'ufw'
identifier: 'mrk'
sort: 41
path: './42-MRK.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Luka '
versification: 'ufw'
identifier: 'luk'
sort: 42
path: './43-LUK.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Yohana '
versification: 'ufw'
identifier: 'jhn'
sort: 43
path: './44-JHN.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Matendo ya Mitume '
versification: 'ufw'
identifier: 'act'
sort: 44
path: './45-ACT.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Warumi '
versification: 'ufw'
identifier: 'rom'
sort: 45
path: './46-ROM.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '1 Wakorintho '
versification: 'ufw'
identifier: '1co'
sort: 46
path: './47-1CO.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '2 Wakorintho '
versification: 'ufw'
identifier: '2co'
sort: 47
path: './48-2CO.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Wagalatia '
versification: 'ufw'
identifier: 'gal'
sort: 48
path: './49-GAL.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Waefeso '
versification: 'ufw'
identifier: 'eph'
sort: 49
path: './50-EPH.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Wafilipi '
versification: 'ufw'
identifier: 'php'
sort: 50
path: './51-PHP.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Wakolosai '
versification: 'ufw'
identifier: 'col'
sort: 51
path: './52-COL.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '1 Wathesalonike '
versification: 'ufw'
identifier: '1th'
sort: 52
path: './53-1TH.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '2 Wathesalonike '
versification: 'ufw'
identifier: '2th'
sort: 53
path: './54-2TH.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '1Timotheo '
versification: 'ufw'
identifier: '1ti'
sort: 54
path: './55-1TI.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '2 Timotheo '
versification: 'ufw'
identifier: '2ti'
sort: 55
path: './56-2TI.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Tito '
versification: 'ufw'
identifier: 'tit'
sort: 56
path: './57-TIT.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Filemoni '
versification: 'ufw'
identifier: 'phm'
sort: 57
path: './58-PHM.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Wahebrania '
versification: 'ufw'
identifier: 'heb'
sort: 58
path: './59-HEB.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Waraka wa Yakobo '
versification: 'ufw'
identifier: 'jas'
sort: 59
path: './60-JAS.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '1 Petro '
versification: 'ufw'
identifier: '1pe'
sort: 60
path: './61-1PE.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '2 Petro '
versification: 'ufw'
identifier: '2pe'
sort: 61
path: './62-2PE.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '1Yohana 1 '
versification: 'ufw'
identifier: '1jn'
sort: 62
path: './63-1JN.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '2 Yohana '
versification: 'ufw'
identifier: '2jn'
sort: 63
path: './64-2JN.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: '3 Yohana '
versification: 'ufw'
identifier: '3jn'
sort: 64
path: './65-3JN.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Yuda '
versification: 'ufw'
identifier: 'jud'
sort: 65
path: './66-JUD.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]
-
title: 'Ufunuo '
versification: 'ufw'
identifier: 'rev'
sort: 66
path: './67-REV.usfm'
categories: [ 'bible-nt' ]