initial conversion

This commit is contained in:
Larry Versaw 2020-02-18 08:47:41 -07:00
parent 1b2cf3bd95
commit bcf4e64a71
571 changed files with 5815 additions and 2 deletions

View File

@ -1,3 +1,3 @@
# sw_obs-tn
# Swahili OBS translation notes
Swahili OBS translation notes
STR https://git.door43.org/unfoldingWord/SourceTextRequestForm/issues/173

31
content/01/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,31 @@
# Mwanzo
Huu ni, "mwanzo wa vitu vyote" kabla ya kuwepo kitu chochote isipokuwa Mungu.
# Aliumba
Hapa inatumika kumaanisha kutengeneza kitu pasipokutumia kitu.
# Ulimwengu
Hii inajumuisha kila kitu ambacho Mungu aliumba duniani na mbinguni, vyote vinavyo onekana na visivyo onekana.
# Dunia
Neno "Dunia" linamaanisha ulimwengu wote ambao watu wanaishi.
# Giza
Giza maana yake kutokuwepo na mwanga kabisa, kwasababu Mungu alikuwa bado hajaumba mwanga.
# Utupu
Mungu bado hajaumba kitu chochote isipokuwa Dunia iliyofunikwa na maji.
# Hakuna kilichokuwa kimeumbwa
Hapakuwepo na uumbaji wa vitu isipokuwa maji iliyofunika dunia.
# Roho wa Mungu
Roho wa Mungu, wakati mwingine huitwa Roho Mtakatifu, alikuwepo toka mwanzoni, alitembea juu ya dunia ili aumbe vyote alivyo kusudia.

19
content/01/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# Mungu akasema
Mungu aliumba mwanga kwa kutamka neno.
# Na iwe
Hii ni amri iliyotokea mara moja kwasababu ilinenwa na Mungu. Inaweza kutafsiriwa kwa njia ya kawaida kuwa ni neno lenye uhakika wa kutokea. Kwa mfano, unaweza kutafsiri kama, "Mungu akasema, 'Pawepo na Mwanga.'"
# Mwanga
Huu ni mwanga maalum ambao Mungu aliumba-jua halikuumbwa hadi baadaye.
# Ikawa nzuri
Maneno haya yalitumika mara kwa mara katika historia ya uumbaji, na kusisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikuwa ikimpendeza Mugu na kutimiza mipango na kusudi lake.
# Uumbaji
Neno hili limetumika hapa kumaanisha siku sita ambazo Mungu alivifanya vitu vyote vilivyoko.

15
content/01/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Siku ya pili
Kazi za Mungu za uumbaji ulifuata utaratibu, makusudi na mpangilio. Vitu alivyoumba kwa kila siku zilijenga na kutegemea vitu vya siku iliyotangulia.
# Mungu akasema
Mungu aliumba anga kwa kusema neno.
# Kuumba
Mungu aliumba anga pasipokuwepo na kitu.
# Anga
Neno hili linamaanisha sehemu yote ya juu ya Dunia, hii ikiwa ni pamoja na hewa tunayovuta na mbingu.

15
content/01/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Siku ya tatu
Ni siku iliyofuata kwenye mtiririko ambapo Mungu aliandaa Dunia kwa Maisha.
# Mungu akasema
Mungu aliumba nchi kavu kwa kuamuru.
# dunia
neno hili limetumika kumaanisha sehemu vumbi au udongo, ambayo ardhi iliyo kavu imetegenezwa.
# Kuumba
Neno hili linatumika kumaanisha, kutengeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.

19
content/01/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# Mungu akasema
Mungu aliumba mimea yote kwa kuamuru.
# Nchi na izae
Hii ni amri iliyotokea mara moja kwa sababu Mungu alinena.
# Aina zote
Hii ni aina mbali mbali ya mimea na miti.
# Kuumba
Neno hili linatumika kumaanisha, kutengeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.
# Kilikuwa chema
Neno hili limetumika mara nyingi katika historia ya uumbaji, hii ikisisitiza ya kuwa kila hatua ya uumbaji ilimpendeza Mungu na kutimiza lengo na kusudi yake.

19
content/01/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# siku ya nne
Ni siku ilyofuata kwa mpangilio wa uumbaji wa siku ambayo Mungu aliumba.
# Mungu akasema
Mungu aliumba jua, mwezi, na nyota kwa kuamuru.
# mwanga
Ni kitu ambacho kinang'aa angani na kutoa mwanga kwa dunia.
# usiku na mchana, nyakati na miaka
Mungu aliumba mianga tofauti tofauti ili kutofautisha sehemu ya muda kuanzia ndogo hadi kubwa, na kuziweka zijirudia kwa wakati wote hadi mwisho wa wakati.
# Kuumba
neno hili linatumika kumaanisha, kutegeneza kitu pasipo kutumia kitu chochote.

23
content/01/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,23 @@
# siku ya tano
Mungu aliendelea na mpangilio wake wa uumbaji ambayo alianza siku nne zilizopita.
# Mungu akasema
Mungu aliziumba ndege na vitu viishivyo majini kwa kuamuru.
# Kila kiumbe kinacho ishi na kwenda majini
Mungu hakuumba tu samaki, bali kila aina ya viumbe vyenye kuishi na kwenda ndani ya maji. Kila mmoja anaishi kwa sababu Mungu alichagua kuumba.
# ndege wote
Mungu hakuumba tu aina moja ya ndege, lakini aliumba aina mbalimbali za ndege wazuri ajabu wenye kutofautiana maumbo, ukubwa na rangi.
# ni vyema
Neno hili limetumika mara nyingi katika histora ya uumbaji, hii ikisisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikwenda kama ilivyokusudiwa kutokana na mpango wa hekima ya Mungu na kusudi lake.
# aliwabariki
Mungu aliongea nia yake kuwa wangebarikiwa na kwamba mambo yao yote yaengekwenda vema katika dunia aliowaweka.

31
content/01/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,31 @@
# siku ya sita
Jambo lililofuata, mpangilio katika mfuatano wa siku za matendo ya uumbaji.
# Mungu akasema
Neno alilo liongea Mungu ndiyo njia ambayo wanyama waliumbwa.
# aina mbambali
Hii inamaanisha vitu vingi tofauti tofauti, lakini vyenye mpangilio.
# wanyama wa nchi
Ni aina mbalimbali ya wanyama walioishi juu ya aridhi, mbali na ndege, au wanyama walioishi majini.
# wanyama wa shambani
Ni aina ya wanyama wanaishi kwa amani na watu juu ya ardhi, kwa jina lingine ni wale wanyama wa kufugwa.
# wanaotambaa juu ya nchi
Hii inajumisha jamii ya wanyama wote watambaao kama reptilia na wadudu.
# porini
Ni aina ya wanyama ambao mara nyingi hawaishi kwa amani na watu, hii ni kwa sababu wanaogopa watu, au ni hatari kwao.
# ni vyema
Neno hili limetumika mara nyingi katika histora ya uumbaji, hii ikisisitiza kuwa kila hatua ya uumbaji ilikwenda kama ilivyokusudiwa kutokana na mpango wa hekima ya Mungu na kusudi lake.

19
content/01/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# Na tumfanye
Hii inaonyesha makusudi ya Mungu, kufanya maamuzi ya kumtengeneza mtu kwa namna ya aina yake na kwa makusudi fulani. Inawezekana kutafsiriwakama, "Tutafanya."
# Sisi...yetu...sisi
Biblia inafundisha kuwa kuna Mungu mmoja, lakini kwa maneno ya Agano la Kale "Mungu" iko katika neno la wingi. Na Mungu hutumia maneno ya wingi pale anapoongelea juu yake. Wengine wanafahamu hii kama njia maalumu ya kuelezea ukuu wa Mungu, na wengine hufahamu hii kama Mungu Baba akiongea kwa Mwanaye na Roho Mtakatifu, ambao wote ni Mungu.
# kwa mfano wetu
Mfano, ni taswira inayowakilisha sura ya kitu halisi au mtu. Watu walifanywa kwa namna ambayo wanaweza kuonyesha na kuwakilisha baadhi ya tabia na sifa za Mungu.
# kama sisi
Watu wanazishriki baadhi ya tabia za Mungu ila siyo tabia zote. Maneno haya yanaweza kutafsiriwa kuwa mwanadamu anafanana na Mungu, ila hayuko sawa na Mungu na au jinsi alivyo.
# mamlaka
Mungu aliwapa watu uhuru na nguvu ya kutawala, kuongoza na kuamua namna dunia na wanyama watakavyotumika.

31
content/01/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,31 @@
# alichukua vumbi
Mungu alimfanya mwanadamu kwa kutumia mavumbi kutoka ardhini. Neno hili pengine linaweza kuwa tofauti na neno lililotumika mara kwa mara la neno dunia.
# alimfanya
Neno hili linaonyesha kuwa Mungu mwenyewe alimtengeneza mwanadamu. Hii ni sawa na mwanadamu anavyo tengeneza kitu kwa mikono waye mwenyewe. Hakikisha neno lingine tofauti na "uumbaji" linatumika, hii ni tofauti na alivyo umba vitu vingine vyote ambavyo alifanya hivyo kwa kuamuru kwa kutamka tu.
# mtu
Kwa wakati huu aliyetengenezwa ni mwanaume tu, mwanamke alitengenezwa baadaye kwa njia nyingine.
# akampulizia uhai
Neno hili inaonyesha Nafsi ya Mungu, tendo la ukaribu la kuhamisha uhai wake kwenda kwenye mwili wa Adamu, linganisha na namna mtu anavyotoa hewa.
# uhai
Katika tendo hili, Mungu alimpulizia mwanadamu uhai wa mwili na roho ndani ya mtu.
# adamu
Jina la adamu ni sawa na neno katika agano la kale lenye maana ya "mtu" na ni sawa na neno la udongo/mavumbi ambao alifanywa kwayo.
# bustani
Ni eneo la ardhi lililopandwa miti na mimea kwa kusudi-mara nyingi kuzalisha chakula au kufanya sehemu kuwa nzuri.
# aitunze
Kuendeleza bustani kwa kulimia, kupalilia, kunyeeshea, kuvuna, kupanda n.k.

27
content/01/11.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,27 @@
# katikati
Sehemu ya katikati hutia mkazo na umuhimu wa miti hizo miwili.
# bustani
Ni eneo la ardhi lililopandwa miti n amimea kwa kusudi -mara nyingi kuzalisha chakula au kufanya sehemu kuwa nzuri.
# Mti wa uzima
Mtu alaye matunda katika mti huu hatakufa kamwe.
# mti wa ujuzi wa mema na mabaya
Matunda ya mti huu humuwezesha mtu kutambua mema na mabaya.
# ujuzi
Kuelewa au kufahamu kwa kuwa na uzoefu nao.
# mema na mabaya
Mabaya ni kinyume cha mazuri. Kama ambavyo mazuri humaanisha yale mazuri yanayompendeza Mungu, mabaya humaanisha kitu chochote ambacho hakimpendezi Mungu.
# kufa
Katika hali hii, atakufa kimwili na kiroho.

11
content/01/12.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# siyo vema
Hii ni mara ya kwanza katika uumbaji kwa kitu kutokuwa kizuri. Ina maanisha "bado haijawa nzuri" kwa sababu Mungu hajamaliza kazi ya kumuumba mwanadamu.
# peke yake
Adamu alikuwa mwanadamu mwenyewe, pasipo kuwapo na nafasi ya kuwa na uhusiano na mwanadamu mwingine. Na hakuweza kuwazaa watoto na kuongezeka.
# Msaidizi wa Adamu
Hapakuwepo yeyote aliyefanana kiasi cha Adamu kuweza kuungana naye kukamilisha shughuli alizopewa na Mungu. Hakuna mnyama awezaye kufanya havyo.

15
content/01/13.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# usingizi mzito
Huu ulikuwa usingizi usio wa kawaida.
# akatoa ubavu mmoja na kutengeneza
Maneno haya, yanaonyesha kitendo cha Mungu kutoa ubavu wa Adamu na kutengeneza mwanamke.
# mwanamke
Alikuwa mwanamke wa kwanza, mwanadamu mwenye jinsia ya kike ambaye alikuwa hajatengenezwa hadi wakati ule.
# akamleta kwake
Ni Mungu mwenyewe ndiye aliyewatambulisha. Alimleta Mwanamke kwa Adamu, kama kutoa zawadi nzuri kwake.

23
content/01/14.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,23 @@
# Hatimaye!
Adamu alisema hivyo kuonyesha kuwa alikuwa akisubiri kitu kama mwanamke.
# Kama mimi
Mwanamke alikuwa ni mwanadamu kama Adamu, pamoja na kwamba kulikuwepo na tofauti za umuhimu kati yao.
# Mwanamke
Neno hili linamanisha muundo wa kike ambayo siyo mwanaume.
# kutengenezwa kutokana na mwanaume
Mwanamke alitengenezwa kutokana na mwili wa Adamu.
# mwanaume atamuacha
Hii ilitamkwa kwa wakati uliopo ili kuonyesha mwenendo utakao kuwepo katika siku za baadaye. Adamu alikuwa hana mama wala baba, lakini wanaume wengine wote watakuwa nao.
# watakuwa mmoja
Mme na mke watashirikiana katika mahusiano ya karibu na kipekee, katika umoja na kujitoa kwa kila mmoja wao kwa mahusiano yanayozidi mahusiano na watu wengine wote.

15
content/01/15.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Mungu alimtengeneza
Mungu alimtengeneza mwanaume na mwanamke kwa namna ya kipekee.
# kwa sura yake
Taswira au sura ni kiwakilishi halisi cha kitu au mtu. Mungu aliwatengeneza watu ili kuonyena na kuwakilisha baadhi ya tabia na sifa za Mungu, lakini siyo kuwa sawa na yeye.
# chema sana
Hii inaonyesha zaidi ya maneno yaliyotumika hapo nyuma ya kama ni chema, vyema. Chema sana inamaanisha kwa uumbaji wote na siyo to kwa mwanaume na mwanamke. Kila kitu ilikuwa sawasawa na kama Mungu alivyokitaka kiwe.
# Uumbaji
Siku sita ambazo Mungu alitumia kuumba kila kitu.

23
content/01/16.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,23 @@
# siku ya saba
Ni siku iliyofuata baada ya siku ya sita kuisha.
# amemaliza kazi yake
Mungu alimaliza kazi ya uumbaji ila bado anafanya kazi zingine.
# Mungu akapumzika
Mungu "alipumzika" kwa sababu kazi ya uumbaji ulikamilika. Mungu hakuchoka, au si kwamba ameshindwa kuendelea.
# Aliibariki siku ya saba
Mungu alikuwa na mpango nzuri maalum kwa siku ya saba, na kwa kila siku ya saba baadaye.
# akaifanya takatifu
Hii ina maana, "Mungu alitenga" siku hii kama siku maalum. Haitatumika kama siku nyingine za wiki.
# ulimwengu
Hii inajumuisha kila kitu alihoumba Mungu hapa duniani na mbinguni, yale yanayo onekana na yasiyo onekana.

11
content/02/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# bustani
Ni sehemu maalum yenye kila aina ya miti na mimea ambayo Mungu aliandaa kwa Adamu na Hawa kufurahia na kula mahali hapo.
# kuongea na Mungu
Neno "kuongea" ni kama lile la kuongea na mtu. Mungu huenda alivaa sura ya mwanadamu ili aweze kuongea na mwanaume na mwanamke kwani kifunguu hii kilionyesha kuwa waliongea uso kwa uso.
# haya
Ni hisia inayokuja kwa kujua kuwa tumefanya dhambi au tumepungukiwa kwa namna fulani.

15
content/02/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# mwerevu
Mjanja na mwerevu, mwenye nia ya kudanganya.
# nyoka
Ni mnyama wa ardhini mrefu, asiye na miguu anayetembea kwa kutambaa kwa tumbo lake. Hataivyo katika historia hii ilidhihirika kwamba nyoka ni Shetani, hataivyo kwenye kipengele hii haitajulikana hivyo.
# Je, ni kweli Mungu alikuambia
Nyoka alimuuliza mwanamke kama ni kweli Mungu aliwaambia wasile katika mti wowote ndani ya bustani. Lakini alikuwa akijifanya hajui Mungu alisema nini kwa sababu alitaka kujenga shaka kwenye ufahamu wa mwanamke. Alitaka yeye aweke ulizo au shaka juu ya wema wa Mungu.
# matunda ya mti wowote
Aina zote za matunda kutoka kwa kila aina ya mti ndani ya bustani.

11
content/02/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# matunda
Hatufahamu ilikuwa ni aina gani ya matunda. Tunafahamu tu kwamba ni tunda lililokuwa kwenye mti. Kwa hapa yafaa kutumia neno la jumla la tunda na siyo tunda fulani maalum.
# mti wa ujuzi wa mema na mabaya
Mwanamke alijua kwa hakika kuwa hawaruhusiwi kula matunda kutoka katika mti huo ambao utawafanya wajue mema na mabaya.
# mtakufa
Tumia neno lako la kawaida ya kufa, ni hali ya kufikia uko kwa maisha haya ya kimwili. usikwepe neno hili kwa sababu wazo la kifo linatisha.

7
content/02/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# kama Mungu
Mwanaume na mwanamke tayari wamefanywa kwa namna na sura ya Mungu. Nyoka anashauri kuwa mwanamke atakuwa kama Mungu zaidi kama akijua mabaya. Hata hivyo Mungu hakukusudia yeye kuwa na ufahamu huu.
# kujua mema na mabaya
Kujua kwa njia ya uzoefu mambo yaliyo mema na mambo yaliyo mabaya, au kuwa na uwezo wa kujua kuwa jambo ni jema au baya.

7
content/02/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# hekima
Mwanamke alitamani kuwa na uelewa na ufahamu kama nyoka anavyoonekana kuwa nayo, na kama aliyonayo Mungu.
# aliyekuwa pamoja naye
Hii ni habari muhimu kwani inaonyesha kuwa mwanaume alikuwepo wakati hawa anafanya maamuzi ya kula tunda.

11
content/02/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# mara macho yao yakafunguliwa
Hii inaweza kutafsiriwa kuwa "waliona vitu kwa namna ya tofauti." Inaonyesha kuwa walijua kitu kwa mara ya kwanza. Katika lugha yenu unaweza kuwa na namna vyingine ya kuelezea hali hii.
# wakagundua kwamba walikuwa uchi
Baada ya Mwanaume na Mwanamke kutokumtii Mungu, waliona aibu kwa kuwa uchi. Ndiyo maana walijaribu kujifunika miili yao kwa kuvaa majani ya miti.
# kuficha miili yao
Mwanaume na mwanamke walijaribu kujifunika kwa kutumia majani ili kujificha mbele za Mungu.

7
content/02/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Mungu akitembea
Inaonekana kuwa Mungu alikuja mara kwa mara kuwatembelea Mwanaume na Mwanamke bustanini. Hatufahamu hili lilionekanaje. Kama inawezekana ni vizuri kutumia neno linalotumika kuelezea mtu anapotembea.
# Uko wapi?
Mungu tayari alijua majibu ya swali hilo. Kusudi la swali hili ni kumfanya mwanume na mwanamke waeleze kwanini wanajificha.

15
content/02/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Nani aliyekuambia kuwa uko uchi?
Au "Ulijuaje kuwa uko uchi?" Mungu tayari alijua majibu ya maswali yote. Kwa kuuliza maswali na kufuatilia alikuwa anampa Adamu nafasi ya kukiri dhambi yake ya kutokutii. Kuwa uchi siyo dhambi kwani Mungu aliwaumba hivyo. Ufahamu wao juu ya kuwa uchi ndiyo tatizo. Aibu yao ilionyesha kuwa walikuwa wametenda dhambi.
# amenipa tunda
Mwanaume alimlaumu mwanake badala ya kutubu kwa kutokutii na kuwajibika kwa kutokumtii Mungu.
# ulifanya nini?
Au "Kwanini umefanya haya?" Mungu tayari alijua majibu ya swali hilo. Kwa kuuliza swali hili, alikuwa akimpa nafasi mwanamke akubali kosa lake. Pia Mungu alimaanisha kuwa asingefanya kile alichokifanya.
# Nyoka alinidanganya
Nyoka alinidanganya au alinipotosha. Nyoka alimuambia uongo. Usitumie neno linaloonyesha kama vile alimlogo au kuwa alimpa kitu kilichompofusha macho au kumfanya akili yake achanganyikiwe na kuamua bila yeye kujua. Mwanamke alimlaumu nyoka badala ya kutubu kosa lake la kutotii na kukubali kuwajibika kwa kutomtii Mungu.

19
content/02/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# Umelaaniwa
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Nimekulaani wewe" au "Tatizo baya litakujia." Usitumie neno lenye kuashiria uchawi.
# mtakuwa maadui
Mwanamke atamchukia nyoka na nyoka atamchukia mwanamke. Na uzao wa mwanamke utachukia uzao wa nyoka na uzao wa nyoka utachukia uzao wa mwanamke.
# uzao wa mwanamke
Inamaanisha moja wa uzao wake.
# utakuponda kichwa
Uzao wa mwanamke utaharibu (kuuwa) uzao wa nyoka.
# utamgonga kisigino
Uzao wa nyoka utamjeruhi uzao wa mwanamke kwenye kisigino.

3
content/02/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa kwako
Huenda lugha nyingine zinahitaji kueleea hii kama kitenzi. Unaweza kusema, "Nitakufanya usikie uchungu mkubwa wakati wa kujifungua."

19
content/02/11.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# ardhi imelaaniwa
Kama adhabu kwa kutokutii kwa Adamu, ardhi haitatoa tena matunda. Itampasa Adamu kufanya kazi kwa nguvu nyingi ili apate chakula ya kula.
# utakufa
Mwisho wa adhabu yao ni kifo. Kifo cha kiroho ni utengano wa sisi na Mungu. Kifo cha kimwili ni utengano na miili yetu.
# utarudi katika uchafu
Mungu alimtengeneza Adamu katika mavumbi au uchafu na kumpa maisha. Kwa sababu ya dhambi, maisha yake yatachukuliwa kutoka kwake na mwili wake utaoza na kurudia kwenye uchafu tena.
# Hawa, yenye kumaanisha "mtoa maisha"
Mungu alimpa uhai Adamu na Hawa, na uhai huo walipewa vizazi vyote kwa njia ya kuzaliwa (kuzaliwa kwa watoto).
# Mama wawatu wote
Hii inamaana kuwa atakuwa mama wa kwanza kwa vizazi vyote vya watu. Lugha nyingine zinasema "atakuwa bibi" wa watu wote e

11
content/02/12.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# kama sisi kwa kujua mema na mabaya
Maneno haya, yanaonyesha namna mpya ambayo Adamu na Hawa watakuwa kama Mungu. Kwasababu wamefanya dhambi, wanajua mabaya na wanaweza kufanya. Unaweza kusema "kwasababu sasa wanajua mema na mabaya."
# tunda
Ni aina ya tunda ambayo haukujulishwa au kuelezwa, kwa hiyo yafaa itafsiriwe kama tunda.
# mti wa uzima
Huu ni mti halisi wenye matunda.

19
content/03/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# baada ya muda mrefu
Simulizi hii ilitokea baada ya vizazi vingi (mamia ya miaka) baada ya uumbaji.
# walikuwa waovu na katili
Ni rahisi kusema, "walikuwa waovu na walifanya mambo ya ukatili."
# ikawa mbaya
Inaweza kueleweka kwa kusema "Watu walikuwa wakiishi kwa njia ya uovu na ubaya ambazo hazikumpendeza Mungu."
# Mungu aliamua kuwaangamiza
Hii haimaanishi kuwa dunia itaharibiwa kabisa. ila Mungu alikusudia kuwaangamiza watu wote waliomuasi Yeye na walio sababisha maovu na ukatili. Mafuriko pia itauwa wanyama na ndege wote katika nchi.
# Mafuriko makubwa
Maji mengi ambayo yengeifunika dunia, hata sehemu ambazo mara nyingi ardhi i kavu, na hata kufunika vilele vya milima mirefu.

11
content/03/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# akapata kibali
Mungu alipendezwa na Nuhu, kwasababu alimcha na kumtii Mungu. Japokuwa siyo kwamba Nuhu hakuwa na dhambi, Mungu alimhurumia na akaweka mpango wa kumuokoa yeye na familia yake kutoka kwenye mafuriko makubwa. Hakikisha haitaonekana kana kwamba Nuhu alipata bahati, au kwamba ilitokea tu akaponyoka. Bali, ni mpango na chaguo la Mungu.
# Mafuriko
Maji mengi yenye kuleta maafa.
# mpango wa kutuma
Mungu alipanga kuleta mafuriko yatakayo funika dunia mzima kwa kuruhusu mvua nyingi. Hii ni kwamba alipanga kusababisha mafuriko ya mvua nyingi.

3
content/03/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# safina
Safina ni aina ya mashua ambayo ni kubwa kiasi kwamba inaweza kubeba watu wanane, na wanyama wawili wawili kwa kila kundi la wanyama, pamoja na malisho yao kwa kadri ya muda wa mwaka mmoja.

7
content/03/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Nuhu aliwaonya
Nuhu aliwaambia watu wote kuwa Mungu ataiangamiza dunia kwa sababu ya dhambi.
# wamrudie Mungu
Hii ilimaanisha kuacha kufanya dhambi na kuanza kumtii Mungu.

11
content/03/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Mungu akatuma
Muhu alikuwa hana haja ya kuwatafuat wanyama bali Mungu aliwatuma kwake.
# waliotumika kwa sadaka ya kuteketezwa
Kwa lugha nyingie, inaweza kuwa rahisi kusema kuwa "wanyama wale waliokubalika na Mungu kwa sadaka ya kuteketezwa." Mungu aliamua watu wamtolee wanyama kama sadaka ya kuteketezwa, hata hivyo aliwaruhusu tu Kumtolea aina fulani ya wanyama.
# Mungu mwenyewe alifunga mlango
Hii inatia mkazo kuwa ni Mungu mwenyewe ndiye aliyefunga mlango.

11
content/03/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# mvua iakaanza kunyesha, na kunyesha , na kunyesha
Hii inasisitiza kuwa kulikuwa na mvua isyokuwa ya kawaida, mvua kubwa sana. Lugha nyingine huenda zina namna ya kutia mkazo.
# maji pia yalitokea ardhini
Hii iliashiria kulikuwa na maji mengi yaliyotokea ardhini.
# Dunia yote ikafunikwa
Hii ilimaanisha dunia yote ilifunikwa na maji.

15
content/03/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Mvua kukatika
Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "mvua iliacha kunyesha."
# Safina ikatua
Kulikuwepo na maji mengi kutokana na mvua iliyofunika hata milima. Safina ilielea mlimani na maji yalipoanza kwenda chini, safina ilienda chini na maji na safina ikatulia kwenye mlima.
# miezi mitatu baadaye
Maji yaliendelea kupungua kwa muda wa miezi mitatu baadaye.
# milima ilionekana
Njia nyingine za kutafsiri hii ni "vilionekana" "vikatokeza", vilikuwa vimeonekana. "Inaweza ikawa rahisi kusema, "Baada ya miezi mitatu, maji yalishuka kiasi kwamba Nuhu na familia yake walianza kuona vilele vya milima.

3
content/03/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# kunguru
Aina ya ndege mweusi anayeruka na kula aina ya majani na wanyama, ikiwa ni pamoja na nyama zilizooza za wanyama.

11
content/03/11.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# njiwa
Ndege mdogo mweupe na kijivu mwenye kuruka na kula mbegu na matunda.
# tawi la mzabibu
Mti wa mzabibu una mafuta ambayo watu hutumia kupikia na kujipaka. Kama lugha yako haina neno la "tawi la mzabibu" unaweza kutafsiri kama ni tawi linalotokana na mti uitwao "mzabibu" au tawi kutoka kwa "mti wenye mafuta."
# maji yalianza kukauka/kwenda chini
Inaweza ikawa rahisi kwa lugha yako kusema, maji yaliendelea kuisha, au "kiwango cha maji kilipungua au kilishuka."

3
content/03/12.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# alisubiri wiki moja zaidi
Unaweza kusema, alisubiri suku zaidi, Neno "kusubiri" inaonyesha kuwa Nuhu alisubiri ili maji yakauke kabla ya kumtuma njiwa tena.

11
content/03/13.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Miezi miwili baadaye
Hii ina maana miezi miwili baada ya Nuhu kumuachia njiwa kutoka katika safina. Huenda ni muhimu kusema hii kwa lugha rahisi kama haijaeleweka.
# Muwe na watoto wengi
Hakikisha inaeleweka kuwa ni amri na shauku ya Mungu, unaweza kusema "Ni lazima kuwa na watoto wengi" au "Nataka ninyi muwe na watoto wengi."
# Muijaze nchi
Kama haijaeleweka, unaweza ukasema "muijaze dunia na watu" au "ili pawepo na watu wengi waishio duniani."

7
content/03/14.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# aina ya wanyama waliopaswa kutolewa dhabihu
Njia nyingine ya kusema hii ni, "wanyama ambao watu hutumia kumtolea Mungu dhabihu ya kuteketezwa."
# Mungu alifurahishwa
Mungu alipendezwa na Nuhu kwa kumtolea dhabihu ya kuteketezwa kwa wanyama hao.

15
content/03/15.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# kamwe tena
Hii inamaana "hatarudia tena" au "hatarudia tena wakati wowote" mifano: "Sitalaani tena ardhi" au sitalaani tena ardhi kwa wakati wowote au kwa hakika sitalaani tena ardhi.
# kulaani ardhi
Ardhi na viumbe vingine vyote hutaabika kwa sababu ya dhambi za wanadamu.
# Dunia
Hii inamaanisha ardhi na viumbe vingine vyote vinavyoishi duniani.
# watu ni wenye dhambi tangu utotoni mwao
Njia nyingine ya kusema hii ni, "watu hufanya matendo maouvu kwa maisha yao yote."

19
content/03/16.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# upinde wa mvua
Huu ni upinde wa mwanga wenye rangi ambazo mara nyingi hutokea angani pale panapo kuwepo na mvua ya ngurumo.
# ishara
Ishara ni kama kitu au tukio ambayo ina maana fulani au inayoashiria kitu ambacho ni cha kweli au kitatokea.
# ishara ya ahadi yake
Kwa lugha nyingine inaweza ikawa vizuri kusema "kuonyesha kuwa ameahidi."
# kila wakati
Hakikisha inafahamika ya kuwa, ni kila wakati upinde wa mvua inaponekana na kuendelea. Huenda ni Muhimu kuongeza, "Kuanzia sasa na kila wakati."
# alicho ahidi
Hii inarejea, ile hali ambayo Mungu aliahidi kutoangamiza dunia tena kwa kutumia mafuriko.

15
content/04/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Miaka mingi baada ya gharika
Vizazi vingi vimepita baada ya gharika
# tena, watu wengi
Familia ya Noah iliongezeka na kuwa na watu wengi wa kuujaza mji
# lugha inayofanana
Hii inamaanisha kulikuwa na lugha mojja hivyo watu walielewana
# mji
Ni vyema kutumia neno la jumla linalomaanisha mji kwakuwa kifungu hakitaji jina maalumu.

7
content/04/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# mnara mrefu kuifikia mbingu
mnara huo ulikuwa mrefu kiasi kwamba ncha yake ilifika angani.
# Mbingu
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "anga."

19
content/04/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# alibadili lugha yao
Kwa ghafla Mungu aliwapa lugha tofauti tofauti na hivyo hawakuweza kuelewana tena.
# lugha nyingi mbalimbali
Badala ya kundi moja kubwa kuzungumza lugha moja, sasa waligawaanyika katika makundi mengi madogo madogo na kila kundi likawa na lugha yake.
# aliwatawanya watu
Wakati Mungu alipobadilisha lugha zao, alisababisha watu hao kutawanyika na kila kundi lilienda sehemu yake.
# Babeli
Hatujui kwa hakika mahali ambapo mji huu ulikuwa, zaidi ya kwamba ulikuwa mahali fulani huko Mashariki ya kati.
# alichanganya
Hii inaelezea jinsi ambavyo watu walichanganywa wakati ambapo hawakuweza kuelewana baada ya Mungu kubadili lugha yao.

15
content/04/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Mamia ya miaka baadaye
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "vizazi vingi baada ya watu kugawanyika katika lugha mbalimbali."
# Ondoka katika nchi yako
Hii inaelezea eneo ambalo Abramu alizaliwa na kuishi.
# na familia yako
Mungu alikuwa anamwita Abramu na famia yake tu, na kuwaacha ndugu zake wengine.
# kukufanya kuwa taifa kubwa
Mungu angemfanya Abramu kuwa na watoto wengi, na wangekuwa taifa kubwa na la muhimu.

11
content/04/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# alichukua
lugha zingine zinaweza kusema "alileta"
# Mungu alimuonesha
kwa namna fulani Mungu alimudokezea Abramu kuhusu mahali alipopaswa kwenda. Kifungu hiki hakielezi jinsi ambavyo Mungu alimuonesha.
# nchi ya Kanaani
jina la nchi hiyo iliitwa "Kanaani."

11
content/04/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# ardhi yote utakayoiona
Kama Abramu alikuwa amesimama juu mlimani, angeweza kuona eneo kubwa.
# kama urithi
Mungu aliahidi kumpa Abramu na uzao wake ardhi kama vile baba huwa watoto wake ardhi mali.
# Kisha Abramu akakaa katika nchi
Abramu aliishi mahali pale pamoja na wote alioenda nao.

7
content/04/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Melkizedeki
Melikizedeki alikuwa ni mtu mwenye mamlaka ya dini katika Kanaani ambaye alipokea sadaka na kuziwasilisha kwa Mungu.
# Mungu aliye juu
Watu wa Kanaani waliabudu miungu mimgi ya uongo. Jina "Mungu aliye juu" lilimtambulisha Mungu wa kweli ambaye Melkizedeki alimwabudu.

7
content/04/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Miaka mingi
Miaka mingi ilipita tangu Mungu alipomuahidi Abramu mtoto.
# kama nyota angani
msemo huu unamaanisha kuwa uzao wa Abramu utakuwa na watu wengi kiasi kwamba hakuna atakayeweza kuwahesabu.

11
content/04/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# pande mbili
sehemu hizi mbili zinaweza kuwa, watu wawili, makundi mawili ya watu, au mtu mmoja na kundi la watu. Katika hili patano lilikuwa kati ya Mungu na Abramu.
# kutokana na mwili wako
Kwa mwili wake binafsi Abramu angempa mimba mkewe, ili kwa pamoja wapate mtoto wao kwa njia ya asili. Hii ilikuwa ni ahadi ya ajabu sana maana Abramu na sara walikuwa wazee sana.
# Hawakuwa na mtoto wa kiume
Abramu hakuwa na uzao ambao wangeirithi ardhi yake.

11
content/05/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# bado hakuwa na mtoto
bila mtoto, Abramu hakuwa na uzao wa kumfanya yeye kuwa taifa kubwa.
# Amuoe naye pia
Abramu angemchukua Hagai kuwa mke wake wa pili, lakini Hagai asingekuwa mke halali wa Abramu kama alivyokuwa Sarai. Bado alikuwa mtumishi wa Sarai.
# upate mtoto kwa ajili yangu
Kwa kuwa Hagai alikuwa mtumishi wa Sarai, basi Sarai angehesabiwa kuwa ndiye mama wa mtoto ambaye angezaliwa.

7
content/05/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# ameolewa
Hagai akawa suria wa Abramu - mke wa pili kisheria. Lakini Hagai bado alikuwa mtumishi wa Sarai.
# alimuonea Hagai wivu
Sarai alimuonea Hagai wivu kwa sababu alipata mtoto na yeye asingeweza kupata mtoto.

11
content/05/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# baba wa mataifa mengi
Abramu angekuwa na uzao mkubwa na wangekuwa na ardhi yao na kujiongoza wenyewe.
# Nitakuwa Mungu wao
Njia nyngine ya kusema hili ni, "Nitakuwa kwao Mungu watakayemwabudu."
# kila mtu mme katika familia
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kila kijana na mwanaume katika familia yako."

15
content/05/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# mtoto wa ahadi
Isaka alikuwa mtoto ambaye Mungu aliwaahidia Sarai na Abramu. Na pia atakuwa mtoto ambaye Abramu atapata uzao mwingi kwake
# Nitafanya agano langu na yeye
Hili litakuwa agano sawa na lile ambalo Mungu alifanya na Abramu.
# baba wa wengi
Kama Mungu alivyoahidi, Abrahamu atakuwa baba wa watu wengi ambao pia watakuwa mataifa mengi.
# Binti wa mfalme
Majina ya Sarai na Hagai yote yalikuwa na maana sawa yaani "Binti wa mfalme."

3
content/05/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# wanaume wote wa nyumbani kwake
Hii ina maana ya wanaume na wavulana wote ambao Abrahamu aliwatunza pamoja na watumishi wake wote wa kiume, wadogo kwa wakubwa.

11
content/05/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Mungu aliijaribu imani ya Abrahamu
Mungu alitaka Abrahamu aoneshe ya kuwa amejitoa kikamilifu kwa kwake, na kwamba angetii chochote ambacho Mungu angemwambia.
# Muue
Mungu hakutaka sadaka ya kutekezwa ya mtu. Mungu alitaka kuona ya kuwa Abrahamu alimpenda Mungu zaidi kuliko mtoto wake.
# alijiandaa kutoa sadaka ya kuteketezwa
Abrahamu alijiandaa kumtoa mwanae kuwa sadaka ya kuteketezwa. Mungu alimzuia kabla hajamuua kijana wake.

15
content/05/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# alitembea kwenda eneo la kutolea sadaka
Mungu alimwagiza Abrahamu akamtoe Isaka sadaka juu ya mlima maalumu ambao ulikuwa umbali wa mwendo wa siku tatu kutoka alikokuwa anaishi.
# kuni kwa ajili ya sadaka
Kawaida, kondoo aliuawa kwa ajili ya sadaka na kuwekwa juu ya kuni ili kwamba kuni na sadaka viungue pamoja.
# mwanakondoo
mwanakondoo au mbuzi ndiyo walikuwa wanyama wanaostahili kwa sadaka.
# atajipatia
Yawezekana Abrahamu aliamini kuwa Isaka ndiye alikuwa badala ya "mwanakondoo" ambaye Mungu alimpatia. Hata hivyo Mungu alitimiza maneno ya Abrahamu kwa kumpatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka.

15
content/05/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# kumuua kijana wake
Mungu hakutaka sadaka ya binadamu bali alimpima Abrahamu kujua imani yake.
# Acha? usimdhuru kijana!
Mungu alimlinda Isaka na akamkinga Abrahamu asimdhuru.
# unaniogopa
Abrahamu alimwogopa Mungu. Hii ilijumuisha heshima na uchaji wa Mungu. Kwa sababu ya mambo hayo, alimtii Mungu.
# kijana wako wa pekee
Ishimaeli pia alikuwa mtoto wa Abrahamu, lakini Isaka ndiye alikuwa mtoto wa Abrahamu na Sarai. Agano la Mungu na Abrahamu lilikuwa juu ya Isaka.

7
content/05/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Mwanambuzi
Mwanambuzi ni mbuzi dume.
# Mungu alimpatia mwanambuzi
Kwa muda muafaka, Mungu alimleta mwanambuzi aliyenaswa kwenye kichaka.

15
content/05/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Mwanao wa pekee
Isaka ndiye alikuwa mtoto pekee wa Abrahamu na Sarai.
# nyota za angani
uzao wa Abrahamu ungekuwa kama nyota angani, hauhesabiki
# familia zote duniani
neno "familia" hapa linamaanisha kundi fulani la watu duniani, licha ya wazazi na watoto.
# umebarikiwa kupitia familia yako
hapa familia ina maana ya uzao mkubwa ambao Abrahamu angepewa.

11
content/06/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Alimtuma mmoja wa watumishi wake.
Hii inaweza kutafasiriwa kuwa "alimwambia mmoja wa watumishi wake kurudi nyuma." Neno "nyuma" linamaana kuwa mtumishi anatakiwa arudi sehemu ambayo Ibrahamu aliishi miaka mingi iliyopita kabla hajaenda Kaanani. Hakikisha tafsiri ya sehemu hii ina maana kamili.
# Kwenye ardhi.
Ardhi hii ilikua mashariki ambapo Ibrahamu alikuwa akiishi sasa hivi.
# Kumleta mke kwa ajili ya mtoto wake Isaka.
Hii iinaweza kutafasiriwa kama "kumleta mwanamke ambae hajaolewa ili mwanae Isaka amuoe."

3
content/06/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Mjukuu wa kaka yake na Abrahamu.
Alikua binti wa mtoto wa kaka yake na Abrahamu. Babu yake alikuwa kaka yake na Abrahamu.

3
content/06/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Rebeka alikubali
Japokuwa wazazi wa Rebeka walipanga ndoa yake, hawakumlazimisha kwenda kuolewa na Isaka.

7
content/06/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Ahadi.... zilizorithishwa
Ahadi za agano ambalo Mungu aliweka na Abrahamu hazikuwa kwa ajili yake tu, bali kwa ajili ya kizazi chake.
# Isiyohesabika
Hii inaweza kutafasiriwa kama "nyingi sana." Neno "isiyohesabika" ina maana vitakuwepo vizazi vingi ambavyo watu watashindwa kuvihesabu.

3
content/06/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Tumboni mwa Rebeka
Hii ni, "ndani ya tumbo lake."

15
content/06/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Toka wa wanawe wawili
Hii ni, "kutoka kwenye uzao wa watoto wawili."
# Watashindana wenyewe kwa wenyewe
Watoto wote wawili na taifa ambalo litatokana na wao wataendelea kushindana.
# Mtoto mkubwa
Japokua watoto walikua mapacha, mtoto anayezaliwa wa kwanza ndiye anayepewa nafasi kama mtoto wa kwanza.
# Kumtumikia mdogo
Hii inaweza kutafasiriwa kama, "mwana mdogo anatakiwa kufanya yale atakayoambiwa na mkubwa ayafanye."

15
content/06/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Watoto wa Rebeka walizaliwa.
Lugha nyingine zina njia tofauti ya kusema haya kama, "pale Rebeka alipowaona na kuwachukua" au, "pale Rebeka alipowaleta kwenye mwanga."
# Mtoto mkubwa ..... mtoto mdogo
Hii inaweza kutafasiriwa kuwa, "mtoto atakayekuja kwanza ... mtoto wa pili atakayekuja." Hakikisha kuwa namna ambavyo "mkubwa" na "mdogo" inatafsiriwa iendelee kuleta maana kuwa watoto hawa ni mapacha.
# Nyekundu
Hii inaweza kumaanaisha kuwa ngozi yake ilikua nyekundu sana au nywele katika mwili wake zilikua nyekundu.
# Nywele
Esau alikua na nywele nyingi mwilini mwake. Waweza kusema kuwa "mtoto mkubwa alikua mwekundu na mwenye nywele nyingi."

11
content/07/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Alipenda kukaa nyumbani ... alipenda kuwinda
Lugha nyingine hutumia neno "kupenda" ambavyo ni tofauti na ilivyotumika hapa, "Rebeka alimpenda Yakobo." Kwa mfano hii inaweza kutafasiriwa kama "alipenda kukaa nyumbani" ... "alipenda kuwinda" au "alipendelea kukaa nyumbani" ... "alipendelea kuwinda."
# Nyumbani
Maelezo haya yanaelezea ni eneo ambalo familia wanaishi. Yakobo alipenda kukaa karibu na hema sehemu walipoishi. Lugha nyingine zina maelezo ya kipekee juu ya "nyumba."
# Rebeka alimpenda Yakobo, ila Isaka alimpenda Esau.
Hii inaweza kutafasiriwa kama "Rebeka alimpenda sana Yakobo na Isaka alimpenda sana Esau." Hii haimaanishi kuwa Rebeka na Isaka hawakumpenda mtoto mwingine lakini kila mzazi alikua naupendeleo wake.

7
content/07/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Nipe mimi sehemu ya chakula ... nipe mimi haki zako
lugha nyingine zingependelea kutumia maneno mawili tofauti kwenye neno "nipe." Hii pia hutumika kama "Esau alimpa ... Yakobo alimpa" kwenye sentensi mbili za mwisho.
# Haki kama mtoto mkubwa
Kutokana na desturi, kwa kuwa Esau alikua mtoto mkubwa, alipaswa kupokea mara mbili ya utajiri wa baba yake endapo baba yao atafariki. Ykobo alitafta njia ya kuchukua haki za mtoto wa kwanza toka kwa Esau.

15
content/07/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Akampa baraka zake
Ilikua desturi kwa baba kuelezea shauku zao juu ya mambo mema yatakayotokea kwa watoto wao. Kwa kawaida mtoto mkubwa anapokea ahadi nzuri. Isaka alitaka baraka zaidi zitokee kwa Esau.
# Alimdanganya kwa hila
Neno "hila" inamaanisha kufanya jambo kwa ajili ya kumdanganya mtu. Rebeka alikuja na mpango wa kumlaghai Isaka ampe Yakobo baraka ya pekee badala ya Esau.
# Kuigiza
Neno "kuigiza" linaonesha namna ambavyo Yakobo alimdanganya baba yake (aliyekua na uwezo mdogo wa kuona kutokana na umri wake kuwa mkubwa).
# Ngozi ya mbuzi
Manyoya yaliyopo katika ngozi ya mbuzi yalingemfanya Yakobo aonekane kama Esau.

7
content/07/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Yakobo akaja kwa Isaka
Kwenye lugha zingine inaweza kuwa na uhalisia zaidi kwa kusema "Jakobo alikwenda kwa Isaka."
# Alidhani kuwa ni Esau.
Alidhani kuwa mtu aliyemshika na kusikia harufu yake alikua Esau.

7
content/07/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Haki kama mtoto wa kwanza
Yakobo alitafta namna ya kupata sehemu kubwa ya mali ya baba yake iliyotakiwa kwenda kwa Esau kama mtoto wa kwanza.
# Baraka yake.
Yakobo pia alimlaghai baba yao katika kumpa yeye ahadi ya utajiri wa baraka ya kipekee ambayo Isaka alikusudia kumpa Esau.

15
content/07/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Mpango ya Esau
Mpango wa Esau ulikua ni kumuua Yakobo baada ya kifo cha baba yake.
# Rebeka na Isaka wakamtuma Yakobo.
Rebeka alitaka kumlinda Yakobo toka kwa Esau hivyo akaongea na Isaka juu ya kumtuma yakobo aende zake.
# kwenda mbali kuishi na ndugu zake
Hii ilikua sehemu ile ile ambayo Rebeka aliishi kipindi ambacho mtumwa wa Ibrahamu alimchukua kuwa mke wa Isaka. Kuliweka hili wazi unaweza kuongeza kuwa "ndugu wa ardhi ile ile alipokua akiishi." Arhi ile ilikua mashariki, umbali wa maili mamia.
# Ndugu zake
hii inaweza kutafsairikwa kama "ndugu zao" Kwa kuwa kaka yake na Abraham alikua babu yake na Rebeka, ndugu zake na Rebeka pia walikua ndugu wa Isaka.

3
content/07/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Utajiri
Hii inajumuisha pesa, kundi kubwa ya wanyama na vyote alivyomiliki.

3
content/07/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Baada ya miaka ishirini.
Yakobo aliishi miaka ishirini kwenye nchi aliyotoka mama yake. Kama hiyo haijaeleweka unaweza kusema "Baada ya miaka ishirini akiishi katika nchi ambayo ndugu zake waliishi pia."

3
content/07/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Mtumishi wako Yakobo
Yakobo hakika hakua mtumishi wa Esau. lakini alimwambia watumishi wake kusema hivi kwa sababu alitaka kumuonyesha Esau kuwa alimwendea kwa unyenyekevu na heshima ili Esau asiendelee kua na hasira juu yake.

15
content/07/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Waliishi kwa amani
Hii inaelezea kuwa Esau na Yakobo hawakukasirikiana na kugombana wao kwa wao.
# Wakamzika
Hii inaweza kumaanisha kuwa walichimba shimo kwenye ardhi wakauweka mwili wa Isaka na kufunika shimo hilo kwa kutumia udongo au jiwe. au inaweza kumaanisha kuwa waliuweka mwili wa Isaka kwenye pango na kufunika sehemu ya wazi.
# Agano la ahadi
Hizi ni ahadi alizozifanya Mungu kwenye agano lake na Ibrahamu.
# Ikapita toka kwa Isaka kwenda kwa Yakobo
Ahadi zilizotoka kwa Ibrahamu kwenda kwa mwanawe Isaka na sasa twenda kwa Yakobo mtoto wa Isaka. Esau hakuzipokea ahadi.

19
content/08/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,19 @@
# Alimtuma
Neno hili linamaanisha Yakobo alimwambia Yusufu aende na Yusufu akaenda.
# Mtoto aliyependwa
Hii inaweza kutafasiriwa kama "mtoto aliyempendwa zaidi kuliko watoto wengine."
# Kukagua
Hii inamaanisha Yusufu alienda na kuangalia kama kila kitu kipo sawa kwa ndugu zake. Lugha nyingine zinaweza kusema "kuangalia hali ya kaka zake."
# Kaka
Hawa walikua kaka zake wakubwa na Yusufu.
# Kuangalia kundi la mifugo
Kwa kuwa ilikuwa safari ya siku kadhaa, unaweza kusema "waliokuwa mbali wakichunga mifugo."

11
content/08/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Alikwenda kwa kaka zake
Njia nyingine ya kutafasiri hili ni "akafika eneo ambalo kaka zake walikuwepo."
# Kutekwa
Walimchukua kinyume na matakwa yake. Haikua sahihi kwa wao kufanya hivi.
# Wafanya biashara ya utumwa
Walikua watu waliofanya biashara ya kununua watu toka kwa mmiliki mmoja na kuwauza kama watumwa kwa mmiliki mwingine.

3
content/08/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Damu ya mbuzi
Kaka zake na Yusufu walitaka Yakobo afikiri kuwa damu iliyokuwa katika nguo ni damu ya Yusufu.

3
content/08/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Kiongozi wa serikali
Mtu huyu alikua sehemu ya serikali ya Misri. Njia nyingine ya kusema hivi ni "kiongozi katika serikali ya Misri."

11
content/08/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Akajaribu kulala na Yusufu
Njia nyingine ya kusema hivi ni "alijaribu kumshawishi Yusufu awe naye kimwili." "Kulala na" ni njia ya kuelezea ili kuepuka kuwa neno la kuchukwaza.
# Kumtenda Mungu dhambi
Ni kinyume na amri za Mungu kwa watu kulala pamoja kabla hawajaoana. Yusufu hakutaka kufanya dhambi kwa kutokutii amri za Mungu.
# Kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu
Njia nyingine ya kusema haya yaweza kuwa "kuendelea kumtii Mungu."

11
content/08/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Ilimsumbua sana
Hii inamaanisha kuwa Mfalme aliogopa na kuchanganyikiwa (kwa sababu ya alichokuwa amekiona kwenye ndoto).
# Washauri wake
Walikua wanaume wenye uwezo na maarifa ya pekee wenye uwezo wa kueleza maana ya ndoto. Tafsiri nyingine zinawaelezea kama "wazee wenye hekima."
# Maana ya ndoto
Watu wa Misri waliamini kuwa ndoto zilikua na ujumbe toka kwa miungu ikiwaambia kitakachotokea baadaye. Mungu alitumia ndoto za Farao kumwambia kitakachotokea.

15
content/08/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Kutafsiri ndoto
"Kutafsiri" ni kusema maana ya kitu fulani. Hivyo Yusufu alikua na uwezo wa kuwaambia watu maana ya ndoto zao.
# Yusufu aletwe kwake
Njia nyingine ya kusema hivi inaweza kuwa "aliwaamuru watumishi wake wampeleke Yusufu kwake."
# Mungu atatuma
Mungu atasababisha mazao yakue vizuri kwa miaka saba na baada ya hapo atasababisha wazalishe chakula kidogo sana ili watu na wanyama wasiwe na chakula cha kutosha.
# Njaa
Bustani na mashamba yatazalisha chakula kidogo sana hivyo watu na wanyama hawatakua na chakula cha kutosha.

7
content/08/08.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Alishawishiwa na
Farao alishangazwa na hekima za Yusufu na akampa heshima. Alimuamini Yusufu afanye maamuzi yenye hekima ambayo yatawafaidisha watu. Ingekua sahihi kusema "alishawishiwa na hekima za Yusufu."
# Mtu wa pili mwenye mamlaka makubwa
Farao alimfanya Yusufu kuwa mwenye nguvu na kiongozi wa muhimu sana katika Misri. Farao tuu ndiye aliyekua mwenye nguvu na muhimu kuliko Yusufu.

3
content/08/09.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Kuhifadhi vyakula vingi.
Walichukua vyakula toka kwenye mavuno mengi na kupeleka mijini na kuvihifadhi huko. Hivyo vyakula vikawa vya Farao.

7
content/08/10.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Misri lakini pia Kaanani
Kwenye lugha nyingine inaweza kueleweka vizuri au kua na uhalisia zaidi ukisema "nchi ya Misri, lakini pia nchi ya Kaanani."
# Njaa ilikua kali
Njaa ilikua mbaya sana. Kulikua na chakula kidogo sana na watu wengi nje ya Misri walikua na njaa kali.

7
content/08/11.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Watoto wake wakubwa
Hawa walikua kaka zake wakubwa na Yusufu waliomuuza utumwani.
# Hawakumtambua Yusufu
Hawakujua kama yule mtu ni Yusufu, kwa kuwa sasa Yusufu alikua na umri mkubwa tofauti na mara ya mwisho walipomuona na alikua amevaa kama kiongozi wa Wamisri.

15
content/08/12.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,15 @@
# Aliwajaribu kaka zake
Yusufu aliwaweka kaka zake wakubwa kwenye wakati mgumu kuona kama watamlinda mdogo wao au watamtendea mabaya kama walivyomtendea Yusufu. Walipomlinda mdogo wao Yusufu akajua kuwa wamebadilika.
# Kama wamebadilika
Njia nyingine ya kusema hivi ni, "kama wamekua tofauti na walivyokua." Miaka iliyopita kaka zake na Yusufu walimuuza utumwani. Yusufu alitaka kujua kama sasa wapo tayari kufanya yaliyo mema.
# Msiogope
Njia nyingine ya kusema hivi ni, "Hampaswi kuogopa adhabu yoyote toka kwangu." Kaka zake Yusufu waliogopa kwa sababu walimkosea sana Yusufu na sasa kama kiongozi mkubwa ana mamlaka ya kuwaadhibu. Yusufu angekataa kuwauzia chakula, au hata kuwaweka gerezani au kuwaua.
# Ubaya kwa wema
Kaka zake Yusufu wakafanya yaliyo mabaya kwa kumuuza Yusufu kama mtumwa na akapelekwa Misri. Lakini Mungu aliliruhusu hilo ili Yusufu awahudumie maelfu ya watu toka katika njaa ikiwemo familia yake yenyewe. Hili lilikuwa jambo zuri sana.

7
content/08/14.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Japokuwa Yakobo alikua mzee alienda Misri
Kulikua na umbali toka Kaanani kwenda Misri na ilikua vigumu kwa mzee kutembea au kuendesha mkokoteni kwa umbali huo.
# Kabla Yakobo hajafa
Yakobo alifia Misri. Hakuweza kurudi Kaanani nchi ambayo Mungu alimuahidi kumpa yeye pamoja na uzao wake.

11
content/08/15.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,11 @@
# Agano la ahadi
Muda mrefu uliopita Mungu aliweka makubaliano na Ibrahamu kuwa atampa uzao mwingi, wataimiliki ardhi ya Kaanani na kuwa taifa kubwa. Mungu pia aliahidi kua watu wote watabarikiwa kupitia uzao cha Ibrahimu.
# Kurithisha kwa
Njia nyingine ya kusema hivi yaweza kuwa "kurithisha kwa" au "kumpa" au "kutumika kwa." Ahadi za Mungu kwa Ibrahimu pia zilikua kwa watoto wake na wajukuu na kwa uzao wake wote. Tazama pia maelezo katika OBS 6-4.
# Makabila kumi na mbili ya Israeli
Mungu alimuahidi Ibrahimu, Isaka na Yakobo kuwa uzao wao utakua taifa kubwa. Baadae Mungu alibadili jina la Yakobo kuwa Israeli. Kuzao wa watoto 12 wa Yakobo ukawa makabila makubwa 12. Makabila haya 12 yalitengeneza taifa lililoitwa Israeli ambalo liliitwa kwa jina jipya la Yakobo.

3
content/09/01.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Waliitwa waisraeli
Kundi la uzao wa Yakobo uliitwa "Israeli" ambalo ni jina alilopewa Yakobo na Mungu. Watu wa kundi lile waliitwa "Waisraeli."

7
content/09/02.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Farao
"Farao" ni neno la kimisri linalomaanisha kuwa mfalme wao. Yawezekana Farao huyu alikua ni mtoto wa Farao aliyekufa, ambaye ni uzao wa Farao aliyefahamika na Yusufu.
# Kuwafanya wana wa Israeli watumwa
Hiyo ni "kuwalazimisha waisraeli kufanya kazi ngumu kinyume na matakwa yao na kuwatumikisha kwa ukatili mbaya."

7
content/09/03.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Mateso
Hii inamaanisha waliteseka sana kwa sababu ya namna walivyotumikishwa na kulazimishwa kufanya kazi. Walikatishwa tamaa.
# Mungu aliwabariki
Mungu aliwajali na kuwawezesha kuvumilia mateso na pia kuwawezesha kuwa wengi kwa kuwapa watoto.

3
content/09/04.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Kuona
Njia nyingine ya kusema neno hili ni "aligundua" au "alijua."

3
content/09/05.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,3 @@
# Kwa kwadri walivyoweza.
Walimficha mtoto toka kwa waisraeli mpaka ilipokua ngumu kumuweka mtoto katika hali ya usalama nyumbani kwao.

7
content/09/06.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Mto Nile
Ukweli
Nile ni mto uliopo kaskazini mashariki mwa Afrika
>Mto Nile unapita Misri na kumwaga maji yake bahari ya Mediteranian.
>Mazao yalikua vizuri kwenye bonde lenye rutuba
>wamisri wengi waliishi karibu na Mto Nile kwa kuwa ilikua ni chanzo muhimu cha maji na mazao ya chakula.

7
content/09/07.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,7 @@
# Alimchukua kama mtoto wake
Alikuwa mtoto wa kike wa mfalme. Alipomfanya musakuwa mwanawe, Musa akawa mtoto wa kiume wa mfalme Misri.
# Kumlea
Njia nyingine ya kusema hivi ni "kumyonyesha yule mtoto Musa."

Some files were not shown because too many files have changed in this diff Show More